Naomba kueleweshwa kuhusu msemo wa 'riziki mafungu saba'

Ngai Moko

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
1,238
1,616
Ni msemo maarufu sana katka jamii zetu, katika kufkria kwangu kote bado sijaweza kujua undani wa msemo huu au maana kamili.

- Je ni mafungu kwa maana kuna fungu la kwanza mtu hultumia tangu kuzaliwa kwake mpaka fungu la saba kufa kwake!!

- Je ni mafungu saba kwa maana Jumamos - Ijumaa?

- Je ni mafungu saba kwa maana njia za utafutaj? Na je hapa wizi unaingia katka moja ya hayo mafungu??

Au msemo huu ukoje kwenu wadau, naomben kueleweshwa.
 
Kimsingi, "Riziki Mafungu Saba" maana yake ni kwamba hupaswi kuchoka wala kukata tamaa kutafuta riziki yako kwasababu ukikosa leo hilo ni fungu moja tu, bado una nafasi (mafungu) nyingi ambazo ukizitumia vema unaweza kujipatia riziki yako. Kwahiyo neno Mafungu katika muktadha huu linatumika kumaanisha 'NAFASI za kutafuta riziki', wakati neno Saba limetumika kumaanisha 'NYINGI', kwa maana ya nafasi nyingi, na sio saba kama idadi yenye ukomo! Sijui kama nimewasaidia wakuu..
 
Lete mafuta itaingia tu...

Ubarikiwe ndugu kwa maelezo yako
 
Kuongezea tu ni kuwa kila mmoja ana fungu lake,usihangaike sana kuwa kama fulani kwani ukimfikia naye keshasogea mbele,hivyo kila mmoja hupata majaliwa yake na kamwe fungu langu halitakuwa lako. Msemo unatuasa kutokuwa na roho mbaya kwani kila aliye hai analo fungu lake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom