Riziki Daudi ajifungua watoto wanne

Zamiluni Zamiluni

JF-Expert Member
Feb 11, 2014
13,997
15,103
[h=2]Ajifungua watoto wanne, aomba msaada
[/h]
Riziki-Daudi-May22-2014%281%29.jpg



Mkazi wa Kunduchi Beach Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Riziki Daudi (22), akiwa amewapakata watoto wake wanne aliojifungua kwa upasuaji wiki iliyopita katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). PICHA:OMAR FUNGO.


Mkazi wa Kunduchi Beach Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam, Riziki Daudi (22), amejifungua watoto wanne ambao ni njiti katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) huku akiomba msaada kutokana na ugumu wa maisha.

Akizungumza na NIPASHE hospitalini hapo jijini Dar es Salaam jana, Riziki alisema kuwa alijifungua watoto hao Jumapili iliyopita ambao wawili ni wa kike na wawili wa kiume kwa njia ya upasuaji.

Aliongeza kuwa kutokana na maisha kuwa magumu, anaomba wasamaria wema wamsaidie ili aweze kuwalea watoto hao kwa maelezo kwamba mzazi mwenzake hana shughuli maalumu ya uhakika ya kuingiza kipato cha kuweza kumudu gharama za kuwalea watoto hao.

Riziki alieleza kuwa watoto hao wamezaliwa kabla ya muda na kwamba wana miezi saba.

Alisema kuwa madaktari waliamua kumfanyia upasuaji baada ya kubaini kuwa anasumbuliwa sana na kifafa cha mimba, hali ambayo ingeliweza kuhatarisha maisha yake pamoja na ya watoto hao.

"Huu ni uzazi wangu wa kwanza, lakini tatizo ni kwamba ujauzito huu umekuwa ukinisumbua sana hasa kifafa cha mimba, ambacho kilikuwa kinasababisha nipoteze fahamu mara kwa mara, jambo lililosababisha madaktari waamue kunifanyia upasuaji kabla ya ujauzito kufikisha umri wake wa kawaida yaani miezi 9 ili kuyaokoa maisha yangu pamoja na ya watoto wangu," alisema Rikizi.

Riziki aliyeonekana kuwa na uchovu, alisema kuwa watoto hao wanaendelea vizuri ingawa mmoja ambaye ni wa mwisho hali yake haiko vizuri sana, na kwamba walizaliwa wote wakiwa na uzito sawa wa kilo moja moja.

Akizungumzia hali yake, alisema kuwa bado anaumwa na anasikia maumivu, uchovu, hana nguvu pamoja na kizunguzungu, hivyo bado anahitaji matibabu zaidi ili afya yake irejee katika hali yake ya kawaida.

"Kwa kweli bado ninaumwa, nasikia maumivu makali kwenye mshono, uchovu, sina nguvu na ninasikia kizunguzungu, hivyo bado ninahitaji matibabu zaidi ili niweze kurudia kwenye hali yangu ya kawaida.

Alieleza kuwa kwa sasa anasaidiwa na mama zake wadogo, ambao hata hivyo, hawana uwezo wa kumsaidia kuwatunza watoto hao ambao wanahitaji uangalizi maalum ili waweze kukua wakiwa na afya nzuri kama watoto wengine.

Riziki amewaomba wasamaria wema kumsaidia nepi, nguo, fedha, chakula na misaada mingine kwa ajili ya kuwahudumia watoto hao.

Watoto hao wanatunzwa kwenye wodi maalum iliyopo kwenye jengo la wazazi la MNH, chini ya uangalizi wa wauguzi.

Aliwaomba wasamaria wema ambao watakuwa wameguswa na tatizo lake kuwasiliana naye kwa namba za simu 0783717648 ya Hadija Abeid, au 0717365040 ya Thuwaiba Mohammed au 0788 711458 ya Daudi Haji.





SOURCE: NIPASHE
 
Aisee kweli anahitaji msaada sana watoto 4 kwa mpigo maisha haya.
 
Mungu ni mkubwa watoto wanne kwa mpigo kisha wanaume wawili na wanawake wawili.

Nafikiri kwa maisha yetu ya sasa hapo inatosha haitaji tena watoto kama wanaume unao, kama wanawake unao pia - upewe nini tena.

Na baba wa watoto sijui yuko wapi sasa kwa kweli huyu bibie anahitaji msaada wa hali ya juu, hili nalo linazidi kuwa tatizo sasa hivi linapokuja swala la ulezi kwenye kushika ujauzito wanashirikiana ikitokea ujauzito na baada ya kujifungua wanaume hatuonekani.

Kwa kweli inabidi tujifundishe hapa sio mambo ya kukimbiana baada ya kumpa ujauzito binti wa watu, hili swala wanaume linatuhusu sana.

Namalizia kwa kumpa pole na hongera pia
 
anaomba msaada sawa ila mwenye hao watoto yuko wapi? mbona hajatajwa wala kujitokeza na kwa nn kwenye issue za kina mama kuomba msaada kwa wananchi ni wanawake tu ndo wanaojitokeza!!!
 
anaomba msaada sawa ila mwenye hao watoto yuko wapi? mbona hajatajwa wala kujitokeza na kwa nn kwenye issue za kina mama kuomba msaada kwa wananchi ni wanawake tu ndo wanaojitokeza!!!
Ni kweli mkuu ila kwa case ya huyu mama, hapo ni hospitali pia kilichovuta hisia ni uzazi wa watoto wanne na ndio maana na vyombo vya habari vikasogea eneo la tukio (hospitali) kuchukua tukio na katika kuchukua tukio ndio hivyo tena request ikatolewa. Btw amesema mumewe ana uwezo mdogo hivyo anaomba msaada (tofauti na ambae anasema ametelekezwa).
 
Dah!mungu awasimamie wtt,wawe na afya njema na wakue waweze kua faraja kwa wazazi wao,i wish ningekua mm aisee!
 
Never ask why when persons ask for assistance.
Let us extend hands that giveth and spine in interrogatives.
May Almighty God gives her strength and early recover.
 
Kwa masikitiko makubwa ktk wale watoto wanne mmoja wao amefariki dunia.
Tuombee kwa Mwenyezimungu awape afya njema hao watoto watatu waliobakia.
 
Hili jambo liko wazi kuwa anahitaji msaada wa maafisa ustawi wa jamii na mafungu ya kazi hii yapo.
 
Mungu ni mkubwa saana hongera zake japo nilisikia kwenye radio moja jana mmoja amefariki wanebaki watatu. Mungu akukuzie Inshallah hao waliobaki waje wakufae baadae.
 
Back
Top Bottom