Riwaya ya rais yaeleza uzinzi wake na Diana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Riwaya ya rais yaeleza uzinzi wake na Diana

Discussion in 'Celebrities Forum' started by KiuyaJibu, Sep 23, 2009.

 1. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Kutoka Paris,Ufaransa
  Rais wa zamani wa Ufaransa Valery Giscard d'Estaing (83),ameandika kitabu cha riwaya chenye hisia za kuwepo uhusiano wa kimapenzi kati yake na marehemu Princess Diana.
  Waigizaji ndani ya kitabu hicho wanaeleza uhusiano wa kimapenzi,kati ya mwanasiasa mwandamizi wa Ufaransa na Princess Patricia,binti mfalme wa Cardiff.
  Kitabu hicho kinaeleza matukio yanayoshabiana na yale yaliyomtokea Princess Diana (wakati wa uhai wake) baada ya kuachana na mume wake Prince Charles.
  Ndani ya kitabu hicho Princess Patricia (ambaye kwa hisia za wengi ni Princess Diana) alielezwa kuwa na urafiki na mwanasiasa aliyejitambulisha ni rais Jacques-Henri Lambertye wa Ufaransa(ambaye ni Valery Giscard d'Estaing).
  Patricia na Lambertye walikutana kwenye chakula cha usiku kilichoandaliwa kwenye kasri ya Buckingham,London,Uingereza ambapo Patricia alimuelezea kiongozi huyo matatizo ya ndoa yake.
  Kwa mujibu wa kitabu hicho,Patricia alimueleza kiongozi huyo kwamba,ndoa yake ilikuwa na matatizo kutokana na kitendo cha mumewe(Charles),kuendeleza vitendo vya uzinzi na mwanamke mwingine wa pembeni,hawara.
  Maelezo hayo yanafanana na vitendo vya Prince Charles ,ambaye aliwahi kumueleza bayana Princess Diana kwamba ana hawara aitwaye Camilla Parker Bowles,na lazima aendeleze mahusiano naye.
  Patricia au "Diana"baada ya kuzidiwa na vituko vya mumewe aliamua kuanza kujirusha na wanaume wengine akiwemo rais huyo,kipindi hicho akiwa kwenye kampeni ya kupambana na ukimwi na mabomu ya ardhini duniani.
  Kitabu hicho kilieleza kuwa Patricia na Lambertye walifikia kilele cha uhusiano wao,waliposafiri pamoja kwenye treni kwenda Ufaransa kuhudhuria sherehe ya kiserikali.
  "Nilimbusu mkono wake na akanitazama kwa mshangao,macho yake yenye rangi ya kijivu yalikuwa yakipepesa huku akitikisa kichwa taratibu",aliandika Giscard ndani ya kitabu hicho.
  Maelezo ndani ya kitabu hicho yamezua kioja kwamba kiongozi huyo wa zamani wa Ufaransa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na Princess Diana.Kwa wakati huo kiongozi huyo alikuwa amemzidi umri Princess Diana kwa miaka 35.
   
 2. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2009
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Thanks for the details. Ndiyo mambo ya wakubwa hayo. Yapo duniani kote.

  Leka
   
 3. KiuyaJibu

  KiuyaJibu JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2009
  Joined: Aug 29, 2007
  Messages: 769
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 45
  Dah!Hata hivyo jamaa alifaidi na ndiyo maana ameshindwa kuvumilia akaona bora aweke mambo hadharani.
   
Loading...