Duh, hii kali, moto, hatari.RIWAYA; MTOTO WA RAIS
Imeandikwa na HalfaniSudy
Simu 0652 212391
Sehemu ya Kumi na Moja
Donald Tengo akahema kwa nguvu, akajaribu kuipiga tena ile namba lakini ilikuwa haipatikami.
"Kuna nini Mheshimiwa Donald?" Balozi Rwekaza aliuliza.
"Wanangu wametekwa!" Donald alisema kwa kulalama.
"Wametekwa? Na nani?"
"Sijajua bado ni kina nani wamewateka. Ila mtekaji amesema nimpigie baada ya nusu saa aniambie nini anataka kutoka kwangu?"
"Safi, tutumie nafasi hii kumnasa mtekaji"
"Kivipi mzee Rwekaza?"
"Tumwite Amanda atusaidie kunasa mahali alipo mtekaji wakati ukimpigia simu. Tukishalijua eneo tunaandaa shambulio la kwenda kuwaokoa watoto wako" Mzee Rwekaza alisema.
"Good Mzee Rwekaza, umewaza vizuri sana. Unajua uwezo wangu wa kufikiri umepungua sana baada ya tukio hili. Mpigie Amanda"
Baada ya dakika kumi Amanda alifika pale sebuleni. Mzee Rwekaza alimuelekeza jambo la kufanya. Amanda alitoa tarakilishi mpakato yake na kuunganisha na simu ya Donald Tengo. Wakati akishughulika akauliza.
"Vipi John alikupigia?" Amanda aliuliza.
"Daah hili tukio limeharibu kabisa uwezo wangu wa kufikiri. Sijawaza kumpigia dereva wala mlinzi wangu. Sijui akili zangu zimeenda wapi? Sijamwambia hata mama yao"
"Usihofu Mheshimiwa Donald. Tulimalize hili kwanza, kisha tuone ilikuwaje watoto wakatekwa"
Baada ya nusu saa kupita, Donald akaipiga ile namba ya mtekaji. Sasa simu ilipatikana.
"Hallo" Donald aliita simuni.
"Habari za sahivi mheshimiwa Donald Tengo" Sauti ya mtekaji ilisema.
"Nzuri kijana, vipi wanang..." Donald Tengo akataka kupoteza muda ili Amanda afanye kazi ya kunasa eneo inapotokea simu ile.
"Najua unachojaribu kufanya mheshimiwa Donald. Na hii inaonesha kwa namna gani usivyowependa wanao"
"Sijakuelewa kijana.."
"Najua unajaribu kuidukua simu hii lakini tambua kuwa hatopata kitu huyo mtu wako" Mtekaji alitoa kauli iliyomchanganya kila mmoja.
Donald Tengo alihamanika. Alichanganywa sana na maneno ya mtekaji.
"Unayafanya yote hayo kwakuwa hujui wanayoyapitia wanao. Nitakapokutumia maiti za wanao ndio utanielewa! Naitwa Daniel Mwaseba!"
Simu ikakatwa.
Mheshimiwa Donald Tengo jasho lilimtoka. Moyo ulimwenda mbio, hakuweza kuvumilia, chozi lilimdondoka.
"Pole sana Mheshimiwa Donald" Mzee Rwekaza alisema.
Donald alimwangalia tu, macho yake yakijitahidi kuzuia machozi.
"Umegundua lolote Amanda?" Mzee Rwekaza akamgeukia Amanda.
"Maajabu, maajabu makubwa sana, mfumo unaonesha mahali ilipopigwa simu hiyo ni hapahapa nyumbani kwako" Amanda alisema akiwa amechoka.
"Tunafanyaje sasa?" Mzee Rwekaza aliuliza.
"Tushamjua mtekaji wa watoto wa Mheshimiwa Donald, tushamjua mtu aliyesababisha ajari ya Alexander na kumteka. Sasa ni kuingia mtaani na kumsaka huyo Daniel Mwaseba. Na tutampata, tutampata tu!!" Amanda alisema kwa hasira.
"Watoto wangu!" Donald Tengo alisema kwa hasira.
"Tutawapata mkuu. Tukimpata Daniel Mwaseba tumewapata watoto wako. Lakini kwanini mlinzi na dereva wako hawajakwambia kitu mpaka sasa?" Amanda aliuliza swali kwa uwoga.
"Wote wamekufa!" Sauti ngeni ilisikika mle ndani. Ulikuwa ugeni wasioutegemea. Alikuwa ni Daniel Mwaseba amesimama katikati ya mlango wa kuingilia sebuleni.
"Nimekufata nyumbani kwako, nimekufata Donald Tengo. Nimeona kwenye simu hatuwezi kuelewana. Nimeona nikufate hapa. Ni kweli nimewashikilia watoto wako wawili, hivyo usijidanganye kufanya ujanja wowote ule. Watauwawa!
Nikwambie tu wakati ninyi mkijaribu kuidukua simu yangu mimi nilikuwa katika harakati za kuingia hapa. Wakati mkiwa katika mchakato wa kuidukua simu iliyounganishwa na mtandao mimi nilikuwa ninamuua mlinzi wako wa mwisho. Sasa ni mimi na nyinyi baada ya kuwauwa walinzi wako nane huko nje.." Daniel alisema kwa kujiamini.
"Unataka nini hasa wewe?" Donald Tengo aliuliza kwa sauti dhaifu.
"Unataka kujua ninataka nini? Ninataka kujua kiongozi wenu wa mpango wa kumuondoa rais Profesa Mark madarakani!!"
Mstuko ulitokea katika sura zote tatu. Hawakutegemea, katu hawakutegemea mipango yao kustukiwa mapema kabisa.
"Nani kiongozi wenu?"
Ukumbi ulikuwa kimya.
"Donald, upo tayari kushuhudia watoto wako wakiuwawa kwa kumficha mkuu wa huu mpango haramu? Sio mwanaume wewe, sio baba, sikuzote baba yupo tayari kufanya lolote lile ilimradi kuiokoa familia yake, laki.." Daniel hakumaliza kuongea. Mdomo wa baridi kutoka katika bastola ya Kizito ulikuwa umemgusa shingoni.
"Mwisho wako! Huu ni mwisho wako Daniel Mwaseba!" Kizito alisema akiwa nyuma ya Daniel.
"Kizito, Daniel kashikilia watoto wangu.."
"Nasi tunamshikilia yeye. Wakiuwawa watoto wako naye tunampeleka kuzimu!" Kizito alisema.
"Amanda njoo umpekue huyu mwanaharam!" Kizito alisema. Amanda alimsogelea Daniel kwa tahadhari kubwa sana. Alimpekua kila sehemu ambayo alihisi kutakuwa na silaha. Akapata bastola tatu, mabomu matatu ya mikono na visu vinne.
"Mpeleke chumba cha mateso tukamuoneshe dunia!"
***
Kule katika nyumba ya Daniel, wakina Martin walikuwa wanashuhudia kila kitu kupitia kamera ndogo aliyoibandika katika kifungo chake cha shati.
"Wanaenda kumtesa Daniel" Hannan alisema kwa majonzi.
"Ndivyo alivyotaka Daniel, kujikamatisha kwa Donald Tengo ili apate nafasi ya kuipata kasiki ya siri. Daniel anajua hawezi kuuliwa kwakuwa bado tunawashikilia wanawe" Martin alisema.
"Atateswa lakini.." Hannan alilalama.
"Ndio maana kavaa ile kamera, akiteswa tutaona kila kitu nasi tutawatesa watoto wake, kisha tutamtumia video ya mateso Donald Tengo. Hawawezi kuendelea kumtesa Daniel" Martin alisema.
"Daniel mbishi sana. Nilimwambia aache huu mpango sio nzuri lakini hakutaka kunisikia. Ona sasa yupo majaribuni. Ule mpango wa awali wa kuwatumia watoto wa Donald Tengo ulikuwa bora sana. Donald angefunguka tu. Asingevumilia kuona watoto wake wanateseka" Hannan alilalama.
"Huu sio muda wa kulalamika Hannan, ni muda wa kuona mipango yetu inaendaje. Ni muda wa kuona tunamuokoaje Daniel endapo mpango wetu wa awali ukifeli. Daniel anatutegemea sana sisi, tukifeli sisi tumemfelisha na yeye. Lazima tuwe imara katika wakati huu kuliko wakati wowote" Martin alisema.
Hannan alivuta pumzi kubwa. Aliuona ukweli katika maneno ya Martin.
"Kuna kitu nilikiona wakati napekua taarifa za Donald Tengo lakini sikuwaambia" Hannan alibadilisha mada.
"Kitu gani hicho uliona Hannan?"
"Ni taarifa niliyoikuta katika mtandao wa siri sana wa majasusi. Na niliamua kuzipeleleza zaidi mwenyewe baada ya kudukua simu ya Magdalena Lema"
"Magdalena Lema? Mke wa rais?" Martin alishangaa.
"Ndio Martin"
"Niambie taarifa gani hizo ulizozipata?"
"Donald Tengo ana uhusiano wa siri wa kimapenzi na mke wa rais!!"
"Unasemaje Hannan?" Martin alishangaa.
"Donald Tengo anatembea n
mke wa rais!" Hannan alirudia.
"Kwanini hukutuambia wakati tupo na Daniel?"
"Niliamua kuthibitisha kwanza taarifa hizi ndipo niwaambie. Lakini kwa bahati mbaya kabla sijawaambia Daniel aliamua mpango mwengine. Mpango wa kujitekesha kwa makusudi ili apate nafasi ya kuipata Kasiki ya siri ya Donald Tengo.."
"Daah hiyo ni siri nzito sana umegundua Hannan. Mke wa Rais kutembea na waziri wa fedha katika Serikali ya mumewe ni bonge la kashfa. Natamani Daniel angekuwepo hapa tuone angekuwa na mawazo gani juu jambo hili" Martin alisema.
"Hapa hayupo Daniel, tupo sisi, tunaweza kufanya kitu ambacho akija Daniel tunaweza kuendelea nacho" Hannan alisema.
"Umewaza kufanya nini Hannan katika suala hilo?"
"Mimi ninaona tumchimbe zaidi Magdalena Lema, huenda tukapata kitu zaidi"
"Sawa Hannan" Martin alikubali.
Hannan alianza kubofya tarakilishi yake, wakati Martin alikuwa makini na picha za kamera ya siri ikiyoonesha chumba cha mateso alicholazwa Daniel Mwaseba.
"Ona, ona Martin.." Martin aliacha kuangalia picha za kamera na kwenda kwa Hannan.
"Umeiona hii picha" Hannan aliuliza.
Martin aliingalia ile picha. Mstuko ulionekana usoni mwake.
"Umeitoa wapi hii picha?" Martin aliuliza.
"Nimempekua mke wa rais katika ukuta wake wa mtandao wa facebook. Hakukuwa na lolote la kumtilia shaka. Nilianza kuangalia picha zake mbalimbali. Ndipo nikaiona picha moja amepiga na mwanamke mmoja. Juu ya picha aliandika
'Rafiki yangu wa siku zote'
Katika picha hiyo alikuwa amemshirikisha huyo mwanamke. Huyu mwanamke kwa majina anaitwa Salma Lungu. Niliamua kumpekua huyu Salma Lungu hukohuko facebook. Baada kuangalia picha kadhaa za Salma ndipo nikaikuta picha hii" Hannan alisema.
Martin aliiangalia kwa umakini ile picha "Bila shaka huyu wa kushoto ni Salma Lungu, anayefatia ni Magdalena Lema, huyu mwengine ni Donald Tengo. Ili kuujua vizuri uhusiano wa Donald na Magdalena lazima tumsake huyu Salma Lungu. Ni nani huyo Salma?" Martin aliuliza.
"Cha kushangaza, nimejaribu kumpekua Salma kwa namna nyingine. Lakini hakuna taarifa zozote zile kuhusu yeye, sehemu yoyote ile"
"Inawezekana vipi kusiwe na taarifa zake mtandaoni. Ila hii sura sio ngeni kwangu, ni kama nimewahi kumuona mahali fulani. Tunafanyaje sasa kumpata?"
"Ngoja niangalie vizuri ukuta wa Facebook wa Salma nione anatuma sana picha akiwa maeneo gani? Huo utakuwa ni mwanzo nzuri wa kumjua zaidi"
"Sawa"
Hannan akapekua kama dakika kumi hivi, kisha akasema
"Njoo uone hii picha Martin"
Martin akasogea katika tarakilishi ya Hannan
"Kuna nini Hannan?"
"Angalia hii sebule, hujawahi kuiona?"
"Aaah hi ni sebule ya ya Donald Tengo, kama tulivyoiona leo katika kamera ya siri aliyoivaa Daniel Mwaseba"
"Naam. Inavyoonesha Salma Lungu na Donald Tengo ni wapenzi pia! Hii aliyoivaa Salma ni gauni ya kulalia, bila shaka siku hii alilala nyumbani kwa Donald Tengo!" Hannan alisema.
"Salma Lungu ni nani haswa?" Hannan alijiuliza kwa sauti ndogo. "Mbona hakuna taarifa yoyote mtandaoni kuhusu Salma Lungu? Nimeangalia hadi katika kanzidata ya vitambulisho vya Taifa, vitambulisho vya kura, hadi RITA katika vyeti vya kuzaliwa. Hakuna taarifa kuhusu Salma Lungu. Ananiumiza sana kichwa. Inamaana hakuzaliwa Tanzania? Hakusoma Tanzania? Ni nani Salma Lungu?" Hannan alisema huku akiipiga kofi tarakilishi yake.
Mara, mwanga ukatokea katika video iliyokuwa inaonesha katika chumba cha mateso alichokuwemo Daniel Mwaseba. Hannan na Martin macho yao yalielekezwa huko.
Video ilionesha mlango ukifunguliwa. Akaingia Amanda akiwa na Kizito.
"Tumekuja kaka. Safari hii tumekuja kivingine, tumekuja kuuliza maswali, nawe utupe majibu. Majibu sahihi ya kila tutakachokuuliza" Kizito alisema.
Daniel aliwaangalia tu huku akiiruhusu kamera yake ikiwamulika wale watu wawili usoni. Alifanya vile makusudi.
"Umemficha wapi Alexander Helb?" Amanda aliuliza.
Daniel alikaa kimya.
Kizito alienda kwenye kabati dogo lililokuwemo mle ndani. Kilikuwa ni chumba kidogo chenye dirisha moja dogo lililokuwa juu kabisa ya kile chumba. Dirisha lisiloruhusu mwanga, hivyo mwanga ulisubiri na mlango ufunguliwe ili mwanga upate kupita.
Ndani ya kabati alitoa waya mdogo ulioambatana na mashine ndogo.
"Kinaitwa kibano hiki, utasema tu wapi ulipomweka Alexander!" Kizito alisema wakati akiunganisha ule waya katika umeme ukutani. Akatoa vyuma viwili virefu, akamvua shati Daniel ili amgusishe vile vyuma. Hapo ndipo wakina Martin walipoteza picha. Kamera ilifunikwa vibaya na lile shati walilomvua.
"Wameitoa kamera?" Hannan aliuliza.
"Hatuwezi kuona kwasasa. Wamemvua shati ili wamtese" Martin alisema.
"Tufanye kama Daniel alivyotuagiza"
***
Kule katika chumba cha mateso wakati wakijiandaa kumtesa Daniel na kibano, ghafla aliingia Donald Tengo.
"Mwacheni, mwacheni, msimfanye kitu" Donald Tengo alisema.
"Kuna nini mkuu?" Amanda aliuliza.
"Angalia" Donald Tengo alimpa simu yake Amanda. Kulikuwa na video fupi, Amanda akaicheza.
"Mimi ni mzalendo kwa Taifa langu. Ujumbe wangu kwako Mheshimiwa Donald ni sasahivi watu wako wako katika harakati za kumtesa Daniel. Nakushauri kawaambie waache mara moja, la sivyo utapokea kichwa cha mwanao mmoja. Nitaanza na Candy!! Naitwa Hannan" Video iliishia hapo.
Wote watatu walitoka nje ya chumba cha mateso jasho likiwatiririka.
Amanda, nini kimetokea?" Donald aliuliza walipofika sebuleni.
"Sijaelewa kwa namna gani watu wake wamegundua kwamba tunataka kumtesa muda huu. Ni mambo ya kushangaza sana" Amanda alishangaa.
"Kuna mambo mawili tu, kati ya hayo moja limefanyika. Aidha Daniel ana kamera ya siri ama ana kinasa sauti!" Kizito alisema.
Donald Tengo alitingisha kichwa kukubaliana nae.
"Mhamisheni katika kile chumba, mpelekeni baharini!!"
Amanda na Kizito walienda katika chumba alichowekwa Daniel, walimfungua kamba na kumpeleka katika chumba kingine. Kilikuwa ni chumba kidogo zaidi, kikiwa hakina dirisha, wala kitu chochote kile ndani yake. Cha kushangaza katikati ya chumba kulikuwa na bomba la maji. Akiwa anatazamwa na midomo miwili ya bastola Daniel alisukwasukwa mle ndani. Kwa umakini mkubwa huku akimwelekezea bastola Daniel alienda katikati ya chumba. Akafungulia lile bomba la maji. Maji mengi yalianza kumwagika mle ndani. Jamaa walifunga mlango na kutoka nje, wakiacha chumba kikianza kujaa maji!
"Mshampeleka baharini?" Donald aliuliza.
"Ndio mkuu" Kizito na Amanda walijibu kwa pamoja.
"Safi, sasa tunaenda kuwasaka wanangu popote pale walipo. Hawa watu wanamtegemea sana Daniel katika mipango yao. Hivyo kumuacha akifa baharini itaturahisishia sisi. Na kama hao wenzake walikuwa wanapata mawasiliano nae kwa kamera au kifaa chochote kile imekula kwao, maana kitakuwa kimesharibiwa na maji" Donald Tengo alisema.
"Ni kweli mkuu. Misheni ya kuwasaka watoto itakuwaje?"
"Ita vijana wa bahari nyekundu kumi. Nitamtumia Dick, yule kijana wetu wa usalama wa Taifa atuambie mahali anapoishi Daniel. Tukishapapata tu tumemaliza mchezo. Watoto wangu lazima watakuwa nyumbani kwa Daniel Mwaseba"
"Hata Alexander atakuwa hapohapo" Kizito alisema.
"Ndio, nilishasahau kuhusu Alexander, kupotea kwa watoto wangu kumeharibu sana uwezo wangu wa kufikiri. Naahidi naenda kuwateketeza vibaya sana hao watu waliowateka wanangu. Watamjua Donald Tengo ni nani! Nahisi hawaujui vizuri upande wangu wa pili. Mimi ni mnyama!" Donald Tengo alisema kwa ghadhabu.
Wote watatu wakajipanga vizuri. Amanda akawapigia simu vijana wa bahari nyekundu, ndani ya robo saa vijana kumi waliwasili wakiwa katika magari mawili. Donald Tengo akampigia simu Dick, mtu wao wanaomtumia katika idara ya usalama wa Taifa kuwapa taarifa. Akawaelekeza nyumbani anapoishi Daniel, wakaelekea huko.
Hannan na Martin walikuwa wamepoteza kabisa mawasiliano na Daniel Mwaseba. Hii iliwapa hofu sana juu ya usalama wa Daniel.
"Tunafanyaje sasa Martin? Daniel hapatikani kwa namna yoyote" Hannan aliuliza.
"Itabidi nimfuate Daniel nyumbani kwa Donald Tengo. Inaonesha Daniel yupo katika hatari" Martin alisema.
"Ni hatari sana kwa wewe kwenda huko. Sitaki kukupoteza na wewe Martin kama nilivyompoteza Daniel. Hawa watoto waliopo hapa hawana thamani yenu nyinyi. Hawana thamani kwangu na hata kwa taifa"
"Hannan, kwenda nyumbani kwa Donald Tengo ni njia pekee ya kumpata Daniel. Pale ni mahali ambapo alipotelea. Na bila shaka ndipo mahali alipo mpaka sasa. Siwezi kumuacha Daniel akiteketea kirahisi kwa namna hii. Licha ya kufanya kazi pamoja kwa muda mrefu lakini Daniel kwangu amekuwa ni kama ndugu. Siwezi kumwacha ndugu yangu akifa kifo cha namna hii, wakati nina uwezo wa kumwokoa. Sitoweza kujisamehe kamwe. Nitaenda kupambana kama ni kufa ni bora na mimi nikafie humo."
"Sawa Martin, mimi nitabaki hapa kuwalinda hawa watoto. Ila usiende hivihivi. Chukua kifaa hiki kitatusaidia katika mawasiliano. Kama utapata tatizo lolote niambie, nitakuwa njiani kuja kukusaidia. Na mimi nife pamoja na ninyi" Hannan alisema kwa hisia.
***
Maji ya baridi yakiyotoka katika bomba, katika chumba alichowekwa Daniel yalikuwa yanamfika katika mabega sasa. Mwanzoni alijaribu kuufungua mlango, lakini utundu wake wa kucheza na milango mbalimbali hapa ulikwama. Mlango wa chuma haukukubali utundu wowote ule. Giza la chumbani, ukichanganya na ubadili mkali wa maji yale yalimtesa sana. Kama wakina Donald Tengo wangerejea na kumuuliza chochote kile, pasi na shaka safari hii angewajibu.
"Mbinu zangu zote hapa zimefika mwisho. Maji haya ya baridi yamezimaliza nguvu zangu. Ninakufa, ninakufa kifo kibaya sana. Ni kweli ninakufa lakini ninaamini wakina Hannan watalimaliza jambo hili, kuhakikisha uhaini huu haufanikiwi, na yoyote yule aliyehusika katika uhaini huu akipelekwa katika vyombo vya dola" Daniel aliwaza wakati maji yakimfikia shingoni.
Wakati huo, Martin Hisia alikuwa anaendesha gari kwa kasi sana. Akielekea katika nyumba ya Donald Tengo. Nusu saa tu ilimfikisha katika nyumba ile ambayo aliamini Daniel alikuwemo. Bila wasiwasi akaenda getini. Akagonga. Akasubiri kama dakika mbili hivi, geti dogo lilifunguliwa, alitoka njemba moja akiwa na bunduki mkononi.
"Wenyewe hawapo.." Njemba ilisema kwa sauti ya kibabe kabla hata hajaulizwa kitu.
"Samahani kaka.." Martin alisema lakini alikatishwa.
"Nimekwambia wenyewe hawapo!" Njemba safari hii alisema kwa ubabe. Na hiyo ndio nafasi aliyokuwa anaisubiri Martin.
Ghafla!
Alimsukumia ndani kwa kutumia kifua chake. Kilikuwa ni kitendo cha ghafla ambacho kilimwacha Njemba akidondoka chini, bunduki yake ikiwa mkononi. Kabla Njemba hajapata nafasi ya kutafakari, Martin alimrukia na kumchoma kisu cha kifua mara mbili. Njemba alitaka kupiga ukelele lakini Martin alimuwahi kwa kumziba mdomo. Sauti yake ikapotelea humo.
Njemba alikata roho.
Martin alienda upande wa kulia wa ile nyumba. Nako kulikuwa na mlinzi aliyekuwa anavuta sigara, bunduki yake ikiwa kaisimamisha ukutani. Kwa haraka akamuwahi risasi moja ya paji la uso kwa bastola yenye kiwambo cha kuzuia sauti. Jamaa akadondoka chini. Martin alizunguka ile nyumba hakuwakuwa na mlinzi mwingine.
Akaingia ndani.
Wakati huo, Donald Tengo akiwa na vijana wa bahari nyekundu walikuwa wanakaribia nyumbani kwa Daniel Mwaseba huko Mikocheni.
"Humu ndani ninaamini ndimo walimo watoto wangu. Kuweni makini kuhakikisha watoto wangu hawapati madhara yoyote yale." Donald Tengo alisema huku wengine wakimsikia kupitia vifaa walivyovaa masikioni mwao.
Na misheni hii ndogo ilianza.
Vijana wa bahari nyekundu walijipanga katika makundi mawili ya watu watano watano. Kundi la kwanza lilipita upande wa mashariki huku wengine wakielekea upande wa magharibi. Donald Tengo, Amanda na Kizito walibaki ndani ya gari huku wakifatilia kwa umakini mkubwa sana kila kitu kinachoendelea.
Baada ya kuhakikisha eneo la nje liko salama, vijana walizama ndani. Silaha zao zikiwa zimetangulizwa mbele. Kwa umakini mkubwa sana walisonga mbele kuifata nyumba ya Daniel Mwaseba. Kwa kutumia funguo maalum walifungua mlango na kuingia ndani. Baada ya dakika tano kifaa cha sikioni cha Donald Tengo kilipata uhai.
"Mkuu tumefanikiwa kuingia ndani lakini hakuna mtu humu ndani?"
"Unasemaje bahari nyekundu?" Donald Tengo aliuliza kwa hamaki.
"Hakuna mtu ndani, tumepekua kila mahali lakini hatujaona mtu. Kuna chumba kimoja tumepekua tumekuta vitu kadhaa vinavyoonesha ni vya Daniel Mwaseba"
"Mmekuta kama kitu gani?"
"Tumekuta nguo na albam ya picha, bila shaka ni za Daniel"
"Ok njoo na hiyo albam ya picha, inaweza kutusaidia. Waweke na zawadi wakutane nayo watakaporudi" Donald Tengo alisema.
Kijana alimwelewa.
Baada ya kuthibitisha kwamba watu wa Daniel hawakuwemo mle ndani walirejea nyumbani.
"Hakuko sawa nyumbani!" Kizito alisema kwa ghadhabu wakiwa kama mita mia moja kufika nyumbani kwa Donald Tengo.
Macho ya Donald nayo yalielekea getini. Aliona geti la nyumba yake likiwa wazi. Ilimpata hofu kuu. Hakutaka kumpoteza Daniel kabla hajawapata wanawe. Walishukia nje, wakatembea kwa tahadhari kubwa wakielekea ndani. Kila mmoja bastola yake ikiwa mkononi. Waliingia mpaka ndani, baada ya kuacha maiti ya mlinzi wake nyuma. Baada ya wale wa awali kuuwawa. Walizunguka nyuma na kukuta maiti ya mlinzi mwengine.
"Adui katoka nje" Kijana mmoja wa bahari nyekundu alisema.
"Kwanini?" Amanda alisema.
"Unaona hizi alama za viatu. Hivi ni viatu vya mvamizi, inaonesha wakati akiondoka" Yule kijana wa bahari nyekundu alisema.
"Twendeni ndani, bado hatujajua uharibifu alioufanya Daniel Mwaseba" Donald Tengo alisema.
Wakaingia ndani, walichokutana nacho huko, wote walibaki midomo wazi.
Sebuleni kulikuwa kumetawanywa vibaya sana. Kila kitu kikiwa hakipo katika mpangilio waliouacha. Friji liligeukia kule, kabati liligeuzwa huku, runinga ilikuwa chini huku makaratasi kadhaa yakiwa yamemwagwa pembeni ya meza ndogo.
Donald Tengo alikimbilia katika chumba ambacho walikiita baharini, alipigwa na butwaa, mlango aliouamini kuliko kitu chochote kile ulikuwa chini. Mlango imara, wa chuma ambao fundi wake alimwaminisha kwamba hakuna atakayeweza kuufungua hapa duniani ulikuwa umefunguliwa. Na ndani ya chumba hiko Daniel Mwaseba hakuwemo. Donald Tengo alichanganyikiwa sana. Kwa kasi alienda chumbani kwake, akachukua rimoti iliyokuwa juu ya feni. Akabonyaza kuelekea ukutani. Ukuta ulisogea, lakini macho yake hayakuamini.
"Wamechukua kasiki yangu ya siri! Oooh tumekwishaaa" Donald Tengo alipiga ukelele mkubwa.
Kwa hakika alikuwa amepatikana!
"Sasa kila kitu kipo mikononi mwake, ushahidi wote anao, huu sio wakati wa vita vya siri tena, ooooh no, Daniel safari hii nikikupata nitakuua mwenyewe, sitojari tena maisha ya watoto wangu!! Lakini amepajuaje mahali hapa nilipoificha kasiki yangu ya siri, amejuaje kama huu ukuta unafunguka? Ni mtu mmoja tu niliyewahi kumwambiai siri hii. Mmoja tu, mpenzi wangu wa maisha Salma Lungu! Je ni yeye ndiye aliyeivujisha siri hii? Haiwezekani, haiwezekani!" Donald Tengo alichukua simu yake na kumpigia Salma Lungu. Simu ilikuwa haipatikani. Na hii ilikuwa ni kwa mara ya kwanza simu ya Salma Lungu isipatikane tangu walipoingia katika mahusiano. Akazidi kuchanganyikiwa.
Akapiga simu kwa Balozi Rwekaza.
"Mzee Rwekaza itisha kikao cha dharura sasahivi" Donald Tengo alisema kwa sauti iliyoambatana na hofu.
"Kuna tatizo gani Donald?" Mzee Rwekaza aliuliza.
"Utajua kwenye kikao.." Donald Tengo alisema na kukata simu.
Itaendelea..
Kali sana, Tengo anashikwa mchana kweupeRIWAYA; MTOTO WA RAIS

Riwaya; Mtoto wa Raid
Imeandikwa na Halfani Sudy
0652 212391
Sehemu ya Saba
Masaki; Dar es Salaam.
Katika nyumba moja ya thamani kubwa kulikuwa na kikao cha watu kumi. Waziri wa fedha, mheshimiwa Donald Tengo alikuwa mbele ya watu tisa waliokuwa wamevalia suti za thamani, zenye rangi nyeusi. Kulikuwa na utulivu mkubwa, watu wote wakitega masikio yao kumsikiliza Donald Tengo.
"Karibuni sana wajumbe, hatukuwa na ratiba ya kukutana hapa kwa siku ya leo. Tulikubaliana tutakutana hapa mwisho wa mwezi huu tukiwa tumeimaliza hii kazi, lakini tumekutana hapa kwa dharura. Kuna tatizo kidogo limetokea.
Katika kikao chetu cha mwisho nakumbuka niliwaambia wajumbe juu ya ujio wa Alexander Helb. Jasusi hatari sana kutoka Uholanzi. Ilifanyika kama ilivyopangwa, tulimshawishi Alexander na alikubali kuacha kazi zake huko Uholanzi na kuja kushirikiana na sisi. Tulimuingizia bilioni moja kama malipo ya awali, na tulimwahidi bilioni mbili baada ya kumaliza kazi yetu" Donald akanyamaza kidogo kuacha maneno yake yaingie ubongoni mwa wajumbe.
Baada ya sekunde kadhaa akaendelea,
"Leo asubuhi Alexander aliwasili hapa lakini lilitokea jambo la kushangaza sana pale uwanja wa ndege.
Ni hivi, gari waliyopanda Alexander na Joyce ilipata ajari!" Donald Tengo alinyamaza, akachukua chupa ya maji na kuimiminia mdomoni. Kisha akasema "Mwanzoni tulidhani ni ajari ya kawaida tu, lakini baada ya kufanya uchunguzi wetu tuligundua kwamba ilikuwa ni ajari ya kupangwa, na Alexander alichukuliwa na watu wasiojulikana baada tu ya kutokea ajari!. Na tangu hapo hatujajua mahali alipopelekwa Alexander na watekaji" Donald alimaliza.
"Daah ni habari mbaya sana hiyo kwetu. Alexander alikuwa na umuhimu mkubwa sana kwa hapa tulipofikia. Bila ya Alexander hata kazi ya ZAK ni bure tu. Je, mmejaribu kuisachi simu ya Alexander kujua mahali alipopelekwa?" Mjumbe mmoja aliuliza.
"Tulijaribu kumtafuta mjumbe, Amanda aliifanya hiyo kazi, lakini aligundua kitu cha ajabu sana. Simu ya Alexander ilionekana bado ipo Uholanzi. Hii ilitushangaza sana!" Donald Tengo alisema.
"Hujuma, bila shaka kuna hujuma. Bahati mbaya sana hujuma zimeanza wakati tukiwa ukingoni mwa mpango wetu wa kumuondoa rais Mark madarakani. Sasa, lazima tuhakikishe tunazizima hujuma hizi. Lazima tuhakikishe tunajua wapi alipopelekwa Alexander na kina nani waliomteka? Wote tulikuwepo hapa wakati ukimueleza Alexander juu ya kazi hii. Ulimueleza kuhusu mpango wetu, hivyo kukamatwa kwake ni kuweka rehani siri zetu. Hivyo kuna umuhimu mkubwa sana wa kuhakikisha Alexander anapatikana. Tuwatumie vijana wa bahari nyekundu kumsaka Alexander popote pale alipo!" Mjumbe mwengine alisema.
"Upo sawa Mjumbe, Bahari nyekundu wakiongozwa na Amanda nitahakikisha hawalali hadi watuambie wapi alipopelekwa Alexander, na ni kina nani waliomteka. Kuhusu Alexander kutoa siri hilo hatuna shaka nao. Alexander ni jasusi, sio rahisi kutoa siri kirahisi hivyo." Donald Tengo alisema.
Kikao kiliendelea kwa muda wa saa tatu. Wakapanga. Wakakubaliana. Sasa walianza msako maalum wa kumsaka Alexander Helb, iwe mvua, iwe jua. Awe mashariki, awe magharibi. Awe kusini, awe kaskazini, jasusi Alexander Helb lazima apatikane!!!
***
Ulikuwa ni wakati wa jioni. Jua lililokuwa likiwasulubu wana Sinza mchana nd'o lilikuwa linazama. Sasa Sinza nd'o ilikuwa imechangamka. Baa mbalimbali zilikuwa zimejaa wateja wakiimaliza siku kwa kusindikiza na bia. Makelele ya muziki yalikuwa yanasikika katika baa hizo.
Daniel na Martin walikuwa wamepaki gari yao katika kituo cha mafuta kilichopo Sinza Afrika sana. Macho yao yalikuwa yameelekezwa katika geti la shule ya sekondari ya Kenton. Ulikuwa ni muda ambao walikuwa wanausubiri kwa hamu.
Na dakika waliyokuwa wakiisubiri ikafika. Waliliona gari jeusi likitoka getini.
"Gari tunayoisubiri ni ile pale. Kazi ianze.." Daniel alisema.
"Ndio Daniel, na misheni ianze" Martin alisema huku akishuka katika gari. Akafungua buti la gari na kuitoa pikipiki. Akaiwasha na kuanza kuifuata ile gari, wakati Daniel nae akifata kwa nyuma kwa gari.
Ile gari nyeusi ilifika katika makutano ya Bamaga iliyotoka katika geti la shule ya sekondari Kenton. Gari lilikuwa katika foleni ili waelekee Masaki, nyumbani kwa Donald Tengo. Ghafla, dereva bodaboda mmoja aliikwaruza ile gari karibu na mlango. Ilikuwa ajari ndogo lakini dereva wa gari nyeusi hakuweza kuivumilia.
Pengine kuonesha umwamba wake. Si ni dereva wa waziri!!
Kwa kasi akafungua mlango na kuanza kumfata yule dereva bodaboda. Alipofika alitulizwa, alikutana na hasira ya dereva bodaboda, akala kibao. Mlinzi akiwa ndani ya gari alishuhudia tukio lile. Naye alitoka kwa kasi kwenda kumsaidia dereva.
Lilikuwa kosa,
Kwa kasi Daniel alienda kwenye ile gari nyeusi, bastola ikiwa mbele aliwanyooshea watoto waliokuwa wamekaa katika siti za kati. Kwa ulaini, aliwachukua wote na kuwapeleka katika gari yake wakati wenye gari wakigombana na Martin Hisia. Daniel akaondoka na Candy na Cindy.
Kule ugomvi uliisha baada ya watu kuanza kukusanyika. Dereva wa gari nyeusi akaona isiwe tabu. Yeye na mlinzi wake wakarudi katika gari yao huku wakimruhusu dereva bodaboda aondoke. Walipofika katika gari watoto hawakuwepo!!
Ilikuwa tafrani!!
***
Wakati hayo yakifanyika katika makutano ya Bamaga Sinza. Vijana wa bahari nyekundu, Amanda George akiwa na Kizito Kizito walikuwa katika viunga vya uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Kizito aliyekuwa dereva alipaki gari nje uwanja. Wakaingia ndani kuanza kupeleleza chanzo cha ajari iliyotokea asubuhi. Kizito akamwita dereva teksi mmoja, alimtambua kwa sare alizovaa, kitambulisho chake kilionesha kwamba anaitwa David.
"Habari kaka, ninaitwa Musa ni Mwandishi wa habari wa gazeti la uchunguzi la Dukua. Najua unalifahamu gazeti hilo, hutoa habari za kina za kichunguzi kuliko gazeti lolote lile hapa nchini. Huyu ni mwenzangu anaitwa Feriha" Kizito alidanganya.
"Sawa ndugu mwandishi, naitwa David Msomi ni dereva teksi hapa uwanja wa ndege, nina miaka mitano sasa" David alisema.
"David tunahitaji kitu kimoja tu kutoka kwako, kimoja tu na bila shaka tutakulipa vizuri. Kwako tunataka taarifa ili kwetu zikawe habari. Tupo tayari kununua taarifa kwa gharama yoyote ile ili gazeti letu la Dukuo lizidi kuwa juu katika habari za uchunguzi" Kizito alisema.
"Taarifa gani mnataka kaka?" David aliuliza.
"Tunahitaji taarifa kuhusu ajari ya leo asubuhi"
"Ile ya Range rover nyeusi na gari la maji taka?" David aliuliza.
"Naam" Kizito aliitikia.
David aliangalia juu. Alikumbuka vizuri sana ajari iliyotokea asubuhi.
"Kuna kitu gani unakijua juu ya ajari ile ambayo vyombo vingine vya habari hawawezi kukipata?" Kizito aliuliza.
"Mtanilipa sh ngapi nikiwapa taarifa?" David aliuliza.
"Inategemea na uzito wa taarifa yako. Lakini sio chini ya laki moja" Amanda alisema.
David aliwaza sana, kisha akasema " Majuto".
"Unajuta nini David?" Amanda aliuliza.
"Kitu ambacho watu hawakijui ni Majuto, Majuto ndiye aliyesababisha ile ajari ya asubuhi!" David alisema.
"Kivipi?" Kizito aliuliza huku akijifanya kuandika katika karatasi aliyoishika.
"Pesa, nipeni pesa yangu kabisa. Namjua Majuto lazima ataniua! Nipeni pesa ile niondoke kabisa hapa ndipo nitawaambia" David alisema.
Amanda alitoa simu yake. Akapiga sehemu. Akaongea kama dakika tano, kisha akamuuliza David wakati simu ikiwa hewani.
"Una akaunti benki?"
David aliitikia kwa kichwa.
"Niandikie namba ya akaunti yako na jina la benki kwenye simu yako" David akaandika. Akampa Amanda. Amanda akaisoma ile namba kwa aliyekuwa anaongea nae kwenye simu. Akakata simu. Baada ya kama dakika tano simu ya David ikaingia meseji.
'Milioni moja ilikuwa imeingia katika akaunti yake'
"Bila shaka pesa zimeingia, Eeeh tuendelee. Ilikuwaje kuhusu Majuto na ile ajari ya Range rover nyeusi?" Kizito aliuliza.
"Majuto alikata breki ya ile range rover kabla haijatoka. Na hiyo ndio sababu ya ajari ya asubuhi!"
"We ulijuaje?" Kizito aliuliza.
"Nilimwona, nilimwona kwa macho yangu akikata breki za ile gari"
"Umemwambia yeyote yule taarifa hiyo?" Amanda aliuliza.
"Hapana ninyi ni wa kwanza kuwaambia. Hata Majuto mwenyewe hajui kama nilimwona" David alisema.
"Ok tunashukuru sana kwa taarifa yako. Andika namba yako hapa tutakutafuta tukihitaji ufafanuzi zaidi" Amanda alisema.
Kisha wakaagana.
"Kifuatacho?" Kizito aliuliza.
"Msako wa Majuto popote pale alipo!" Amanda alisema.
"Amanda, umemuingizia kweli milioni moja yule kisebengo hahahaha" Kizito alisema huku akicheka.
"Mambo ya mtandao yale. Mwache aende benki ataenda kukutana na salio zero katika akaunti yake hahaha" Amanda alisema huku akicheka.
Majuto! Kijana aliyetumiwa na Daniel Mwaseba anasakwa na vijana wa bahari nyekundu..
Wakati kule, watoto wa Donald Tengo wako mikononi mwa Daniel. Hatua gani itafuata baada ya kuwapata?
Lako Jicho!
Wazee wenzangu mwenzenu arosto imenishinda, nimeamua kununua, now nipo season 6.
Story nzuri sana.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobileappNn
Wazee wenzangu mwenzenu arosto imenishinda, nimeamua kununua, now nipo season 6.
Story nzuri sana.
Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile