Riwaya ya Halfani Sudy

Six Man

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
254
892
Simulizi kutoka kwa Halfani sudy
Inaitwa; Red Butterfly
Mawasiliano; 0652212391

Sehemu ya kwanza

Ulikuwa ni usiku wa saa nane kamili. Usiku tulivu huku kelele za miti na ndege ndizo zikizosikika nje ya nyumba aliyolala mpelelezi Daniel Mwaseba maeneo ya Masaki.

Mara simu maalum ya Daniel Mwaseba ilianza kuita kwa nguvu, mlio wake maalum alioutega kwa sababu maalum. Mlio ambao haukuwa ule wa mtu kupiga. Sekunde hiyohiyo harakaharaka Daniel aliamka toka usingizini na kuitoa simu yake iliyokuwa chini ya mto. Simu ilikuwa inaita kwa nguvu na kuwaka taa nyekundu na kuzimika karibu na sehemu ilipo spika, inawaka na kuzimika.

"Ina maana ameua tena?" Daniel Mwaseba alisema huku akiangalia saa katika simu yake. Simu maalum ya Daniel ilikuwa imeunganishwa moja kwa moja na geti lake. Ilikuwa mtu yoyote akigusa geti lazima taarifa zipelekwe katika simu yake. Na alitega hivyo baada ya visa vya Red butterfly.

Harakaharaka Daniel aliinuka kitandani. Alitoka na kwenda katika chumba chake maalum. Alikuta kompyuta zake zote nne zikiwa zinawaka. Kompyuta moja iliyokuwa karibu na dirisha ndiyo iliyokuwa inaonesha picha za geti la nyumba yake. Daniel aliisogelea ile kompyuta na kuanza kuiangalia kwa umakini.

Kompyuta ilionesha nje ya geti kulikuwa na mwanamke mmoja mtu nzima akiwa na mkongojo. Mwanamke alikuwa anatumia mkongojo wake kugonga geti la Daniel Mwaseba kidogokidogo. Daniel alimwangalia kwa makini yule mwanamke mtu mzima.

"Red Butterfly umenifata tena nyumbani kwangu kama kawaida yako? Inamaana umeua tena?Safari hii nitakuonesha mimi ni nani?" Daniel alisema huku akichukua bastola iliyokuwa juu ya meza na kutoka nje harakaharaka.

"Red Butterfly ama zangu ama zako" Daniel aliwaza akiwa katika uwanja mpana sasa wa uwa wake, alikuwa anakimbilia nje kwa tahadhari kubwa sana. Bastola yake ikiwa mkononi, kidole chake cha shahada kikiwa katika triga tayari kumlipua Red Butterfly au yeyote yule atakayejipendekeza mbele yake. Daniel alipania kumaliza michezo ya kijinga anayoicheza Red butterfly kila anapofanya mauaji.

Alipolikaribia geti alipunguza mwendo. Sasa alikuwa anakwenda kwa tahadhari kubwa zaidi ili kumstukiza Red Butterfly. Kwa mkono wa kushoto alikuwa anafungua geti taratibu huku mkono wake wa kulia akiwa kaishika imara bastola fupi nyeusi huku kidole cha shahada kikiwa palepale kwenye triga. Taratibu geti lilifunguka. Daniel aliruka samasoti huku bastola yake akiielekeza pale alipokuwa Red Butterfly. Daniel alibaki mdomo wazi, hakukuwa na Red Butterfly. Alikuwa kalionesha bastola geti lake. Red Butterfly alikuwa ameruka tena kama kawaida yake.

"Kwa mara nyingine tena nimemkosa Red butterfly. Bila shaka na leo nitasikia taarifa za mtu kuuwawa na kubandikwa stika ya kipepeo mwekundu katika paji lake la uso ama tumboni. Huyu kibibi kizee mwenye mkongojo ni nani haswa? kila anapokuja kugonga hapa lazima auwe mtu na kumbandika stika ya kipepeo mwekundu" Daniel alijiuliza huku akiangaza huku na kule kwa kasi na umakini. Ilikuwa vilevile alibaki peke yake na bastola yake mkononi.
Red Butterfly hakuwepo.

Daniel alirudi sebuleni kwake. Alikaa juu ya sofa huku akiwa na mawazo lukuki.

"Huyu mwanamke ambaye nimepachika jina la Red Butterfly kutokana na kuja kugonga geti langu kisha yanatokea mauaji ya mtu aliyebandikwa stika ya kipepeo mwekundu usoni kwake ama tumboni ananiumiza sana kichwa changu. Hii ni mara ya sita anakuja kugonga katika geti langu na nikienda tu getini anayeyuka. Nini lengo la kuja kunigongea geti baada tu ya kufanya mauaji yake ya kinyama. Nusu saa mfululizo Daniel aliwaza na kuwazua. Afanye nini ili kumdhibiti mwanamke yule mwenye umbo la kizee. Anaua, anakuja kugonga kwangu na kuyeyuka. She is a red butterfly, tutaonana laki..."

Wakati Daniel akiwa katikati ya mawazo alisikia mlio wa simu yake ikiita. Alinyanyuka pale katika sofa na kuelekea chumbani kwake. Alijua tu ni nani aliyekuwa anampigia, pia alijua kwa vyovyote vile Red butterfly tayari kashafanya mauaji.

Aliichukua simu yake Kitandani ili kujua tu safari hii kamuua nani?. Hisia zake zilikuwa sahihi. Simu ilikuwa imepigwa na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP John Rondo. Akaipokea na kusikiliza Red butterfly itakuwa kamuua nani?

" Hallo Daniel?" IGP Rondo aliita simuni.

"Habari afande?" Daniel aliita kwa sauti ya uwoga.

"Kuna mauaji yametokea..." IGP John Rondo alisema.

"Nani kauwawa?" Daniel alimkatisha IGP John Rondo kwa swali.

"Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Elisha Ngwena ameuwawa usiku wa saa saba. Amepigwa risasi ya tumbo na mtu asiyejulikana. Nakuomba uende sasahivi kujua nini chanzo cha kifo chake. Ukitoka hapo njoo moja kwa moja ofisini kwangu nitakuwa na kikao na wewe" IGP John Rondo alisema.

"Sawa mkuu. Nitakuwa nyumbani kwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi tu na nikimaliza mahojiano yangu nitakuwa ofisini kwako" Daniel alisema.
Simu ilikatwa.

Itaendelea kesho Mungu akipenda..


Inaitwa Red butterfly, kutoka kwa mwandishi Halfani Sudy..
 
Maandishi ya Halfani Sudy
Anatusimulia Red Butterfly
Mawasiliano 0652212391

Hii ni sehemu ya Pili

Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Elisha Ngwena ameuwawa usiku wa saa saba. Amepigwa risasi ya tumbo na mtu asiyejulikana. Nakuomba uende sasahivi kujua nini chanzo cha kifo chake. Ukitoka hapo njoo moja kwa moja ofisini kwangu nitakuwa na kikao na wewe" IGP John Rondo alisema.

"Sawa mkuu. Nitakuwa nyumbani kwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi tu na nikimaliza mahojiano yangu nitakuwa ofisini kwako" Daniel alisema.
Simu ilikatwa

Daniel alikaa kitandani. Alishika tama, mawazo yalikuwa kwa yule mwanamke bibi kizee, Red Butterfly.

"Red Butterfly kaweza kumuua Mheshimiwa Elisha Ngwena. Kapitaje getini kwa Mheshimiwa waziri kwenye ulinzi mkali na kwenda kumuua? Ngoja niende nikapate majibu" Daniel alinyanyuka na kwenda bafuni kuoga. Alipomaliza kuoga alivaa nguo. Akachukua bastola na zana zake za kazi. Alielekea Mikocheni nyumbani kwa Mheshimiwa Elisha Ngwena, ambaye sasa alikuwa ni marehemu.

Alitoka nje, aliingia katika gari lake na kuelekea Mikocheni.

"Red Butterfly, iwe isiwe lazima anahusika na kifo cha waziri wa mambo ya ndani. Haya yatakuwa mauaji yake ya mwisho, nitahakikisha haui tena" Daniel alikuwa anawaza akiwa ndani ya gari yake.

Daniel Mwaseba alifika Mikocheni saa moja kasoro dakika ishirini na tano asubuhi. Alikuta ummati wa watu umejaa. Viongozi mbalimbali wa serikali walikuwepo, wabunge na mawaziri na viongozi kadhaa wa dini. Daniel alipaki gari yake 'parking' ambapo kulikuwa kumejaa magari mengi sana. Alishuka na kuelekea sehemu ambapo kulikuwa na waombelezaji wengi, wengine walikuwa wakilia na wengine wakiwa katika majonzi makuu.

"Red Butterfly rafiki yangu bila shaka popote ulipo umefurahi sana. Najua furaha yako ni kuwaona watu wakiwa katika majonzi namna hii. Lakini, sasa zamu yako ya kulia wewe imefika" Daniel Mwaseba alikuwa anawaza wakati akielekea kwa wale waombolezaji. Aliwasalimia mmojammoja kwa kuwapa mkono. Alikuwa akitoa pole. Kisha akaingia ndani.

Sebuleni alikutana na watu kumi, miongoni mwao kulikuwa na mjane wa marehemu na ndugu zake wengine. Mke wa marehemu alikuwa ni msichana mdogo sana kiumri. Daniel alijitambulisha na kuomba nafasi ya kuongea faragha na mjane wa marehemu. Watu wengine waliokuwa pale sebuleni walitoka nje huku wakilia kwa maumivu makali sana. Hali iliyosababisha mjane wa marehemu nae kuwapokea kwa kilio. Daniel alipata kazi ya kumbembeleza mjane wa marehemu, kazi iliyodumu kwa dakika tano.

"Naitwa Daniel Mwaseba. Ni mpelelezi wa siri wa kifo cha marehemu Mme wako. Watakuja pia Polisi kukuhoji, wape pia ushirikiano nao watafanya upelelezi wao, lakini mimi ni mpelelezi maalum kutoka ikulu" Daniel alisema.

Mjane wa marehemu aliitikia kwa kichwa huku akifuta mafua kwa kanga.

"Kwanza pole sana kwa msiba, la msingi naomba unijibu maswali yangu ili yatusaidie kumjua muuaji wa mume wako ni nani?" Daniel Mwaseba alisema.

"Sawa kaka" Daniel kwa mara ya kwanza aliisikia sauti ya mjane wa marehemu.

"Unaitwa nani?" Daniel aliuliza.

"Naitwa Ilham Mshana. Mke wa marehemu Elisha Ngwena aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani"

"Mliooana lini na marehemu, na mna watoto wangapi?" Daniel aliuliza tena.

"Tuna mwaka mmoja katika ndoa, bado hatujajaaliwa kupata watoto" Ilham alijibu.

"Pole sana kwa msiba wa mumeo Ilham. Najua jinsi inavyoumiza pale unapoondokewa na mtu wa karibu. Nishawahi kupitia mazingira kama haya" Daniel alimpa pole mjane wa marehemu.

"Ahsante sana kaka. Ingawa naumia sana na hiki kifo cha mume wangu. Yeye ndio alikuwa tegemeo letu katika kila kitu. Lakini leo kazimika kama mshumaaa" Ilham akaanza kulia tena.

"Yalikuwaje mazingira ya kifo chake?" Daniel aliuliza bila kujali kama Ilham alikuwa analia.

Ilham alijitahidi kufuta machozi huku akiongea "Hakuna anayejua muuaji aliingia vipi na saa ngapi? Hakuna anayeelewa alipita vipi kule getini ambako kuna walinzi wanne wakiolinda nyumba hii. Muuaji alipita mote huko na kuja kugonga mlango wa chumba chetu. Kwa jinsi sauti ikivyosikika bila shaka hakuwa anagonga na mkono, ulikuwa ni mti au bastola. Mume wangu aliamka na kwenda kufungua akijua labda ni ndugu zetu tunaoishi nao humu. Alikuwa anajiamini kwakuwa haikuwa rahisi kwa mtu mwengine kuweza kuingia humu ndani kwakuwa kuna walinzi kule getini. Alipofungua tu, muuaji hakusema kitu alifyatua bastola yake na kudumbukia katika tumbo la mume wanguuu, nimekuwaaaa mjanee mimi Ilhaaaaam" Baada ya maelezo ilikuwa tafrani. Ilham hakuongea tena, alilia mfululizo akimlilia marehemu mumewe. Daniel akaona pale hatapata la maana. Aliwaita ndugu wa marehemu na kuwahoji, wote walikuwa na maelezo sawa na ya Ilham.

Baadae akaenda chumbani kuuona mwili wa marehemu. Aliufunua, ilikuwa mithili ya miili saba aliyokutana nayo katika kadhia hii. Na mwili wa marehemu Elisha Ngwena ulikuwa na stika ndogo sana ya kipepeo mwekundu tumboni mwake. Daniel aliibandua ile stika na kuiweka mfukoni mwake.

Saa kumi na mbili asubuhi Daniel alitoka Mikocheni nyumbani kwa Mheshimiwa Elisha Ngwena na kuelekea makao makuu ya Polisi Posta kuitikia wito wa IGP John Rondo. Huku kichwani akiwa na mawazo lukuki kuhusu Red Butterfly.

Alipofika kwa katibu mahsusi wa IGP John Rondo moja kwa moja aliruhusiwa aingie. Daniel aliingia ofisini, alipofungua tu mlango alisita.

"Karibu Daniel..." IGP John Rondo alisema.

Daniel alisogea taratibu. Mle ndani kulikuwa na viti sita. Viti vitano vilikaliwa kasoro kimoja tu, akajua kile kimeachwa kwa ajili yake. Alienda kwenye kile kiti na kukaa.

"Karibu sana Daniel. Najua umestuka baada ya kuwakuta watu usiowategemea katika ofisi yangu. Tangu saa tisa usiku tupo hapa baada tu ya kusikia kifo cha Mheshimiwa Elisha Ngwena"
Daniel aliitikia kwa kutingisha kichwa chini juu.

"Mheshimiwa Rais, naona kijana tayari kashafika. Tunaweza kuendelea na kikao chetu" IGP John Rondo alisema.

Je kitaongelewa nini katika kikao hiko? Je Red Butterfly ni nani? Nini lengo haswa hadi anafanya mauaji?
 
Maandishi ya Halfani Sudy
Hii ni Red butterfly
Mawasiliano 0652 212391

Na hii ni sehemu ya nne.

Daniel aliwaeleza kila kitu kuhusu ile stika yenye kipepeo mwekundu kukutwa katika miili ya marehemu yote. Baada ya maongezi yaliyodumu kwa muda wa saa zima kikao kifungwa huku wakiwa wamekubaliana namna ya kumkamata Red butterfly. Kila mmoja aliondoka akiwa na matumaini tele. Kwamba ule ulikuwa mwisho wa Red butterfly...

***

Wiki ya pili sasa, nyumba ya Daniel Mwaseba ilikuwa inalindwa na wanajeshi watano toka jeshi la Wananchi wa Tanzania. Pikipiki tano zilifichwa mahali huku wanajeshi wakipewa ruhusa kuomba helicopter ya jeshi muda wowote ule watakaohitaji.

Ndani ya wiki hizo mbili Red butterfly hakufika katika nyumba ya Daniel Mwaseba, na mauaji hayakutokea pia. Hii iliwapa imani kubwa sana Red butterfly ndiye alikuwa muuaji mwenyewe. Pamoja na kutotokea kwa Red butterfly hakukuwafanya wanajeshi kusahau kazi yao. Walikuwa wanailinda kwa zamu nyumba ya Daniel usiku na mchana.
Waliilinda, na kulinda, mpaka ikaja ile siku ambayo Red butterfly alienda kugonga katika geti la nyumba ya Daniel Mwaseba.

Ilikuwa usiku wa saa sita usiku. Wanajeshi wawili walikuwa macho lindoni huku watatu wakiwa wamelala. Ilikuwa ni kawaida yao kupeana zamu muda wa kulala wakati wengine wakiendelea kulinda. Kipindi hiko Daniel Mwaseba alikuwa ndani ya nyumba yake akiwa amelala ndipo aliposikia mlio wa simu yake. Daniel alikurupuka na kuelekea nje, hakwenda kuangalia kwenye kompyuta kama alikuwa Red butterfly mwenyewe, kwa mlio aliutega katika simu alikuwa na asilimia zote kuwa Red butterfly alikuwa anagonga geti lake nje.

Kule nje mwanajeshi akiyeitwa Mosha ndiye aliyemuona Red butterfly pale getini. Alimstua mwanajeshi mwenzake kisha wakawaamsha wale wengine watatu. Wanajeshi wote watano wakawa macho na silaha zao mkononi tayari kumkamata Red butterfly. Walikumbuka maneno ya mkuu wa jeshi.

"Itakuwa vyema zaidi mkimkamata akiwa hai, ila hata mkimuua sio mbaya sana"

Wanajeshi walikuwa wanataka kufanya vyema zaidi, wamkamate Red butterfly akiwa hai.

Mosha ambaye ndiye alikuwa kiongozi wa wale wanajeshi watano aliwapanga vizuri wenzake. Wakaweka vizuri 'earphone' zao kwa ajili ya mawasiliano. Mosha mwenyewe alikuwa anashambulia kutokea kati, Idd alikuwa anashambulia kutoka upande wa kulia, Haji alikuwa anashambulia kutokea kushoto. Imma na Adrian walipanda katika pikipiki zao endapo Red butterfly akikimbia tu waanze kumfukuza. Kumbuka Daniel Mwaseba nae alikuwa anakuja wakawaka akitokea kwa ndani. Red butterfly aligonga mlango kwa mara ya pili kisha akaanza kuondoka.

"Wee bibi simama hapohapoooo!!" Mosha alisema kwa ukali.

Nukta ileile Red butterfly aligeuka mithili ya mzimu na risasi moja iliingia katika bega la Mosha. Ilikuwa ni shabaha kali sana gizani, cha kushangaza risasi ilitoka katika mkongojo wa Red butterfly!!

Sekunde ileile Idd na Haji walianza kumshambulia Red butterfly. Red butterfly alilala chini huku naye akijibu mashambulio yale kwa ule mkongojo wake. Risasi yake ya pili iliingia katika paja la kulia la Haji. Yowe la nguvu lilimtoka Haji huku akianguka chini kama mzigo akiiacha silaha yake mita kadhaa mbele.

Sekunde tatu baada ya kupigwa risasi Haji, Daniel Mwaseba nae alitokea kule getini.
Alikutana nayo!
Mkongojo wa Red butterfly ulifanya kazi yake, mguu wa Daniel ulikuwa unavuja damu! Risasi kutoka kwa Red butterfly ilipenya chini kidogo ya goti. Daniel alianguka palepale getini huku akipiga kelele za maumivu.

Idd alikuwa anapiga risasi hovyo wakati Red butterfly akikimbia zigzag na zile risasi kumkosa gizani. Aliingia katika uchochoro pembeni ya nyumba ya Daniel, alirukia katika pikipiki alilolihifadhi pale na kuondoka kwa kasi.

Imma na Seif walikuwa nyuma yake na pikipiki za jeshi. Red butterfly akiwa katika mwendokasi mkali aligeuka hivyohivyo. Mkongojo wake ulikohoa mara mbili gizani, kikohozi kilichowafanya Imma na Seif wapate ajari mbaya sana, tairi za mbele za pikipiki zao zilikuwa hazina hewa. Mkongojo wa Red butterfly ulizipasua.
Red butterfly aliongeza mwendokasi wa pikipiki yake na kutokomea.
Kibibi kizee kilitumia risasi sita huku risasi zote sita zikifanya alichozituma.
Ilikuwa shabaha kali sana gizani!!

Idd ndiye aliyepiga simu kuomba msaada. Dakika kumi baadae Ambulance ya hospitali ya Hurbert Kairuki ilifika na kuwabeba majeruhi watano, huku Idd akiwa haamini uwezo wa bibi kizee yule. Alikuwa na shabaha ya uhakika, sio ya kubahatisha. Alikuwa na wepesi wa ajabu sana. Uwepesi wa Red butterfly...

"Yule bibi kizee ni nani? Shabaha yake akilenga ni nadra sana kukosa. Ana wepesi wa ajabu sana, niliona jinsi alivyogeuka kwa kasi na kumshambulia Mosha kwa risasi. Ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua na risasi yake ilimpata Mosha pajani na kumsukumia mtaroni. Yule bibi kizee ni nani? Nimemwona vizuri taa za pikipiki za kina Adrian zilivyommulika wakati anakimbia, ni kizee haswa akiwa amevaa joho jeupe lenye picha ya kipepeo mwekundu kwa nyuma. Hakika yule ni Red butterfly kama alivyosema Daniel Mwaseba" Idd alikuwa anawaza wakati gari la wagonjwa la hospitali ya Kairuki likikimbia kwa kasi kuelekea hospitali.

Walifika hospitali na moja kwa moja wagonjwa waliingizwa katika chumba kilichoandikwa 'emergency'. Idd alibaki nje ya chumba kile akizungukazunguka huku mawazo tele kichwani.

"Hapa yapaswa nimpigie IGP John Rondo nimfahamishe kuhusu hili shambulio la Red butterfly na jinsi lilivyoleta madhara" Idd aliwaza huku akitoa simu yake mfukoni, alimpigia IGP John Rondo.

"Haloo Mkuu" Idd alisema baada ya IGP John Rondo kupokea simu.

"Eeeh nambie Idd mbona usiku sana" IGP John Rondo alisema kwa sauti ikiyoonesha alikuwa anatoka usingizini.

"Kuna tatizo mkuu. Tupo hospitali ya Kairuki hapa Mikocheni, wakina Daniel wameshambuliwa usiku huu na Red butterfly.... " Idd alisema.

"Eeeh unasema? Nakuja hapo Kairuki sasa hivi" Sauti ya John Rondo ilijaa fadhaha.

Simu ikakatwa.

Nusu saa ilitosha kumfikisha IGP John Rondo katika hospitali ya Hurbert Kairuki. Alikutana na Idd na kusimuliwa kila kitu kilivyotokea kule nyumbani kwa Daniel. Ilikuwa ngumu sana kuamini kitu alichokifanya Red butterfly kwa maana John Rondo alikuwa anamuamini sana mpelelezi Daniel Mwaseba. Kupigwa risasi kwa Daniel kulimtambulisha John kwamba huyo Red butterfly alikuwa mtu wa kuotea mbali.

Je nini kitatokea? Tukutane hapahapa kesho kuisoma riwaya hii ya aina yake..
 
RIWAYA; RED BUTTERFLY
MWANDISHI; HALFANI SUDY
SIMU 0652 212391

SEHEMU YA TANO

Kuna tatizo mkuu. Tupo hospitali ya Kairuki hapa Mikocheni, wakina Daniel wameshambuliwa usiku huu na Red butterfly.... " Idd alisema.

"Eeeh unasema? Nakuja hapo Kairuki sasa hivi" Sauti ya John Rondo ilijaa fadhaha.

Simu ikakatwa.

Nusu saa ilitosha kumfikisha IGP John Rondo katika hospitali ya Hurbert Kairuki. Alikutana na Idd na kusimuliwa kila kitu kilivyotokea kule nyumbani kwa Daniel. Ilikuwa ngumu sana kuamini kitu alichokifanya Red butterfly kwa maana John Rondo alikuwa anamuamini sana mpelelezi Daniel Mwaseba. Kupigwa risasi kwa Daniel kulimtambulisha John kwamba huyo Red butterfly alikuwa mtu wa kuotea mbali.

IGP John Rondo alienda kukutana na daktari mkuu wa hospitali ya Hurbert Kairuki. Alimwelezea kila kitu kuhusu umuhimu wa watu waliolazwa katika chumba cha 'emergency'. Daktari mkuu alimwabarisha kwamba wagonjwa walikuwa wanafanyiwa upasuaji wa dharura wa kutolewa risasi ndani ya miili yao. Na watakuwa sawa baada ya muda mfupi tu.

Baada ya saa moja ndipo upasuaji wa dharura ulimalizika. Walifanikiwa kutoa risasi katika miili ya wale askari watatu, lakini wale askari waendesha pikipiki ilishindikana kuokoa maisha yao. Wote walifariki katikati ya matibabu.

Hali ya Daniel na Haji zilikuwa afadhali, lakini hali ya Mosha ikiwa ni ya hatari sana na kupelekwa katika chumba cha wagonjwa mahututi. Risasi walizopigwa Daniel na Haji zilipita kwenye nyama tu, huku risasi aliyopigwa Mosha ilipasua mfupa. Ripoti hiyo ilikiwa mbaya sana kwa IGP John Rondo hasa akifikiria Daniel yupo kitandani wakati muuaji yupo mtaani. Alijua lazima ataendelea kuuwa!!

"Pole sana soldier" IGP John Rondo alimwambia Haji baada ya kufika kitandani kwake.

"Ahsante sana mkuu" Haji alisema kwa sauti ya maumivu.

"Pole na tunakuombea upone haraka" IGP John Rondo alisema.

"Nashukuru sana mkuu" Haji alijibu.

Alipotoka katika kitanda cha Haji alienda kitanda alicholazwa Daniel Mwaseba.

"Karibu sana mkuu" Daniel alisema alipoona tu sura ya IGP John Rondo.

"Pole sana Daniel" IGP John Rondo alisema.

"Ahsante mkuu, ndio kazi zetu zilivyo, waweza kupoteza maisha wakati wowote ule" Daniel alisema.

"Pole tena, Idd amenieleza kila kilivyotokea usiku nyumbani kwako. Nimeustaajabu sana uwezo wa Red butterfly. Uharaka wake katika kuamua na kutenda ni sio wa kawaida. Shabaha yake ni ya hatari sana" IGP John Rondo alisema.

"Ni kweli, Red butterfly ni mzimu ule. Anafanya mambo kwa uwezo wa ajabu sana. Nashindwa kuelewa yule mwanamke kizee katoka wapi na nini dhumuni lake la kufanya maajabu. Yaani alipiga bastola sekunde ileile nilivyoweka mguu wangu nje ya geti. Sikuwa hata nimeona risasi imetokea upande gari. Nilisikia maumivu makali sana na kuanguka chini huku nikilia. Nilimshuhudia wakati Red butterfly akirukia pikipiki isiyo na mlio. Nilielewa kwanini nilikuwa namkosa siku zote. Alikuwa anagonga na kwenda kwa kasi ya ajabu kule nyuma ambapo hakukuwa na kamera na kudanda katika pikipiki yake. Nilimwona jinsi alivyogeuka kimaajabu akiwa juu ya pikipiki na kuachia risasi mbili kwa kutumia mkongojo wake wa ajabu. Taa za kina Adrian zilimmulika kwa nyuma, alikuwa amevaa joho jeupe lenye nembo ya kipepeo mwekundu. Alitokomea wakati mimi nikiugulia maumivu ya miguu" Daniel alimwelezea IGP John Rondo.

"Pole kwa mara nyingine tena. Bila shaka aligundua u hatari kiasi gani ndomana aliwahi kukushambulia kabla hujaamua cha kufanya. Pamoja na uhodari wake lakini najua Red butterfly anakuogopa sana" IGP John Rondo alisema.

"Sidhani kama ananiogopa. Ninachohisi mimi anakuja kunigongea kila anapofaanya mauaji kwakuwa kuna ujumbe fulani ananiletea. Swali la kujiuliza ni ujumbe gani huo? Nina dhima ya kwenda kuutafuta huo ujumbe" Daniel alisema kwa hisia.

"Ni kweli tupu usemayo Daniel. Lakini wewe sasa u majeruhi. Kwa mujibu wa daktari itachukua zaidi ya wiki tatu kupona kabisa, na wiki moja ya mapumziko. Hizo ni wiki nne. Je Red butterfly hatofanya tena mauaji? Je atamuua nani safari hii? Ni ngumu sana kumruhusu Red butterfly kufanya mauaji mwezi nzima. Hatujui atauuwa wangapi? Lazima tufanye kitu Daniel kitachomzuia Red butterfly kufanya mauaji na hatimaye kumkamata" IGP John Rondo alisema.

Daniel alitulia akitafakari. Aliungalia mguu wake uliokuwa umefungwa kwa bendeji kubwa nyeupe. Mawazo yake hayakuwa kwenye mguu lakini. Alikuwa anamuwaza Red butterfly. Afanye nini kumzuia yule mwanamke wa ajabu kufanya mauaji tena? Lilikuwa swali gumu sana kwake kupata jibu la haraka. Baada ya dakika moja na sekunde arobaini, kichwani kwake lilipita jina moja tu, Elizabeth Neville. Ndio Elizabeth Neville anaweza kufanya kitu kwa kipindi ambacho yeye atakuwa anauguza jeraha lake la risasi.

"Mkuu, najua ukubwa na weledi wa majeshi yetu. Lakini mimi naamini majeshi yetu yanatumia nguvu zaidi ya weledi, utafiti na busara. Mtu atakayeweza kumfatilia Red butterfly anatakiwa awe na vitu hivyo, na mtu huyo ni mmoja tu kwasasa" Daniel Mwaseba alisema.

Je ni nani atakayepokea kijiti hiki?
 
Maandishi ya Halfani Sudy
Katika Red butterly
Simu 0652 212391

Hii ni sehemu ya sita

Daniel alitulia akitafakari. Aliungalia mguu wake uliokuwa umefungwa kwa bendeji kubwa nyeupe. Mawazo yake hayakuwa kwenye mguu lakini. Alikuwa anamuwaza Red butterfly. Afanye nini kumzuia yule mwanamke wa ajabu kufanya mauaji tena? Lilikuwa swali gumu sana kwake kupata jibu la haraka. Baada ya dakika moja na sekunde arobaini, kichwani kwake lilipita jina moja tu, Elizabeth Neville. Ndio Elizabeth Neville anaweza kufanya kitu kwa kipindi ambacho yeye atakuwa anauguza jeraha lake la risasi.

"Mkuu, najua ukubwa na weledi wa majeshi yetu. Lakini mimi naamini majeshi yetu yanatumia nguvu zaidi ya weledi, utafiti na busara. Mtu atakayeweza kumfatilia Red butterfly anatakiwa awe na vitu hivyo, na mtu huyo ni mmoja tu kwasasa" Daniel Mwaseba alisema.

"Ni nani huyo Daniel?" IGP John Rondo aliuliza kwa wahka.

"Ni Elizabeth Neville" Daniel alijibu kwa kujiamini.

"Unamaanisha mke wako Daniel?" IGP John Rondo aliuliza.

"Ndio, mke wangu ana uwezo mkubwa sana wa kupeleleza kisa hiki cha Red butterfly na kukifikisha mwisho. Zaidi ya kuwa mke wangu, Elizabeth Neville ni jasusi hatari sana. Najua unajua mkuu. Ukimpa kazi ya kumsaka Red butterfly atakuletea yule mwanamke. La msingi we mtafute, muelezee na umuamini tu" Daniel Mwaseba alisema.

"Kwani kwa sasa yupo wapi mkeo?" IGP John Rondo.

"Alisafiri kwenda China kufatilia mambo ya biashara zake. Anarudi leo jioni. Akifika hapa na kuambiwa kilichotokea atakuwa tayari kumsaka aliyenifanya hivi. Hapo nitakukutanisha nae na uumpe ABC amini Utakuwa mwisho wa mauaji ya Red butterfly" Daniel Mwaseba alisema.

"Nitafanya hivyo, nitaenda kuonana na mkeo airport jioni" IGP John Rondo alisema.
Baada ya mahojiano yaliyodumu takribani dakika kumi mkuu wa Polisi wa Tanzania aliondoka. Baada ya kupanga mipango na Daniel Mwaseba na mipango kupangika.

***SURA YA PILI***

Saa kumi na moja jioni IGP John Rondo alikuwa katika uwanja wa Julius Nyerere. Ndege moja tu kutoka China ilikuwa inawasili muda huo. Na ndani ya ndege hiyo iliaminika kwamba mke wa Daniel Mwaseba, Elizabeth Neville alikuwemo humo.

IGP John Rondo akiwa na askari sita nyuma yake walikuwa mahali pa kusubiria wageni waliokuwa wanawasili. Walishuka abiria sitini na tano, macho kumi na nne ya askari yaliyoenda uwanja wa ndege kumpokea Elizabeth Neville hayakumuona. Wote walishikwa na mfadhahiko, Elizabeth alikuwa wapi wakati waliambiwa na Daniel kuwa anarudi na ndege ile na kwa muda ule. Iweje wafike muda uleule na Elizabeth Neville asiwepo, cha kushangaza zaidi katika mfumo wa abiria waliotakiwa wawemo katika ndege hiyo jina la Elizabeth Neville lilikuwepo. Yalikuwa maajabu ambayo hayakuingia kabisa katika kichwa cha IGP John Rondo.

"Atakuwa wapi huyu mwanamke?" IGP John Rondo aliuliza.

"Kuna utata juu ya ujio wa Elizabeth Neville, rekodi zote zinaonesha alitakiwa kuwepo kwenye hii ndege. Jina lake lipo sasa sijui kimetokea nini mpaka mwenyewe hayupo." Inspekta Adrian alisema.

"Cha kufanya hapa ni kwenda kumueleza Daniel kilichotokea. Daniel ni mtu mwenye kutafakari sana, atajua tu kitu gani kimetokea" John Rondo alisema.

Walikubaliana. Kutoka Uwanja wa ndege moja kwa moja walienda Mikocheni ilipo hospitali ya Hurbert Kairuki. IGP John Rondo mwenyewe ndiye aliyemueleza Daniel kila kitu kilichotokea kule uwanja wa ndege. Daniel akiwa kitandani aliwaza sana, kisha akauliza.

"Mnadhani mke wangu atakuwa wapi?"

"Kusema kweli hatuelewi kabisa. Tumeona tuje kukwambia wewe kilichotokea kule uwanja wa ndege labda utakuwa na mawazo yoyote" IGP John Rondo alisema.

Baada ya kufikiria kidogo Daniel alisema "Hapo cha kufanya ni kuwasiliana na watu wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China watueleza je Elizabeth Neville alipanda katika hiyo ndege?" Daniel alisema.

"Wazo zuri sana Daniel. Tutafanya hivyo sasahivi tujue kama Elizabeth Neville alipanda ile ndege" IGP John Rondo alisema.

"Na endapo kama hakupanda basi kuna mchezo fulani umechezwa. Kama alikuwepo basi utakuwa ni mtihani wa mwaka, iweje Elizabeth apotelee hewani?" Daniel alisema.

"Ngoja tufatilie hilo tujue. Nitakuja tena hapa kukwambia majibu ya huko China" IGP John Rondo alisema.
IGP John Rondo aliaga kwa miadi ya kurudi baada tu ya kupata majibu.

Nusu saa baadae IGP John Rondo alirudi wodini kwa Daniel Mwaseba. Sura yake ikiwa yenye wingi wa mawazo. Daniel aliiona sura ya IGP John Rondo tangu kule mlangoni. Sura yake ilimwambia kuna kitu.
Baada ya salamu John Rondo alisema.

"Tumewasiliana na watu wa uwanja wa ndege kule China. Hata wao wameoneshwa kushangazwa sana na tukio hili. Hata huko China jina la Elizabeth Neville limeonekana katika orodha ya watu waliotakiwa kuondoka kutoka leo kule China kuja Dar es salaam, lakini Elizabeth Neville mwenyewe hakuwepo, nao bado wanafanya uchunguzi kimetokea nini.." Wakati anaongea mara siku yake iliita.

"Kuna taarifa mpaya tumeipata mkuu" Simu kutoka China ilisema "Ndege yetu ilitakiwa kuondoka na watu sitini na nne, na kweli iliondoka na watu sitini na nne, lakini cha kushangaza katika orodha yetu ina watu sitini na tano. Kwa mantiki hiyo inaonesha kuna mfanyakazi wetu aliongeza jina la mtu ambaye hajasafiri, na huku akiirudia namba ishirini mbili mara mbili katika orodha, na bila shaka mtu huyo ni Elizabeth Neville. Bado tunafanya uchunguzi ni nani kafanya hivyo na kwa malengo gani?" Yule mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China alisema.

"Nimekuelewa Maxi Lee. Fanyeni uchunguzi, nasi twachunguza huku tujue kitu gani kimetokea. Ukipata lolote usisite kuwasiliana na mimi" IGP John Rondo alisema.

"Sawa mkuu" Maxi Lee alijibu na siku ikakatwa.

"Daniel haya mambo yanazidi kuwa na utata. Yule mtu wetu anayetupa taarifa kutoka kule anasema ndege ilitakiwa kuondoka na abiria sitini na nne. Lakini katika orodha kulikuwa na abiria sitini na tano ila kuna namba moja ilirudiwa mara mbili. Hivyo kwa mwonekano wa kawaida inaonekana kama orodha ni ileile sitini nne kumbe wamezidi. Kwahiyo ndege ilikuja na abiria sitini na nne ila mkeo aliyekuwa anatengeneza idadi ya watu sitini na tano hakuwepo ndani ya ndege. Swali la kujiuliza ni, Yuko wapi?" IGP John Rondo alisema.

Wakati Daniel Mwaseba yupo kitandani, mkewe Elizabeth Neville hajulikaki alipo...Je Elizabeth Neville yupo wapi? Inaitwa Red butterfly na msimuliaji wako ni Halfani Sudy?
 
Maandishi ya Halfani Sudy
Red butterfly (7)
Simu 0652 212391

"Kuna utata juu ya ujio wa Elizabeth Neville, rekodi zote zinaonesha alitakiwa kuwepo kwenye hii ndege. Jina lake lipo sasa sijui kimetokea nini mpaka mwenyewe hayupo." Inspekta Adrian alisema.

"Cha kufanya hapa ni kwenda kumueleza Daniel kilichotokea. Daniel ni mtu mwenye kutafakari sana, atajua tu kitu gani kimetokea" John Rondo alisema.

Walikubaliana. Kutoka Uwanja wa ndege moja kwa moja walienda Mikocheni ilipo hospitali ya Hurbert Kairuki. IGP John Rondo mwenyewe ndiye aliyemueleza Daniel kila kitu kilichotokea kule uwanja wa ndege. Daniel akiwa kitandani aliwaza sana, kisha akauliza.

"Mnadhani mke wangu atakuwa wapi?"

"Kusema kweli hatuelewi kabisa. Tumeona tuje kukwambia wewe kilichotokea kule uwanja wa ndege labda utakuwa na mawazo yoyote" IGP John Rondo alisema.

Baada ya kufikiria kidogo Daniel alisema "Hapo cha kufanya ni kuwasiliana na watu wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China watueleza je Elizabeth Neville alipanda katika hiyo ndege?" Daniel alisema.

"Wazo zuri sana Daniel. Tutafanya hivyo sasahivi tujue kama Elizabeth Neville alipanda ile ndege" IGP John Rondo alisema.

"Na endapo kama hakupanda basi kuna mchezo fulani umechezwa. Kama alikuwepo basi utakuwa ni mtihani wa mwaka, iweje Elizabeth apotelee hewani?" Daniel alisema.

"Ngoja tufatilie hilo tujue. Nitakuja tena hapa kukwambia majibu ya huko China" IGP John Rondo alisema.
IGP John Rondo aliaga kwa miadi ya kurudi baada tu ya kupata majibu.

Nusu saa baadae IGP John Rondo alirudi wodini kwa Daniel Mwaseba. Sura yake ikiwa yenye wingi wa mawazo. Daniel aliiona sura ya IGP John Rondo tangu kule mlangoni. Sura yake ilimwambia kuna kitu.
Baada ya salamu John Rondo alisema.

"Tumewasiliana na watu wa uwanja wa ndege kule China. Hata wao wameoneshwa kushangazwa sana na tukio hili. Hata huko China jina la Elizabeth Neville limeonekana katika orodha ya watu waliotakiwa kuondoka kutoka leo kule China kuja Dar es salaam, lakini Elizabeth Neville mwenyewe hakuwepo, nao bado wanafanya uchunguzi kimetokea nini.." Wakati anaongea mara siku yake iliita.

"Kuna taarifa mpaya tumeipata mkuu" Simu kutoka China ilisema "Ndege yetu ilitakiwa kuondoka na watu sitini na nne, na kweli iliondoka na watu sitini na nne, lakini cha kushangaza katika orodha yetu ina watu sitini na tano. Kwa mantiki hiyo inaonesha kuna mfanyakazi wetu aliongeza jina la mtu ambaye hajasafiri, na huku akiirudia namba ishirini mbili mara mbili katika orodha, na bila shaka mtu huyo ni Elizabeth Neville. Bado tunafanya uchunguzi ni nani kafanya hivyo na kwa malengo gani?" Yule mfanyakazi wa uwanja wa ndege wa kule Beijing China alisema.

"Nimekuelewa Maxi Lee. Fanyeni uchunguzi, nasi twachunguza huku tujue kitu gani kimetokea. Ukipata lolote usisite kuwasiliana na mimi" IGP John Rondo alisema.

"Sawa mkuu" Maxi Lee alijibu na siku ikakatwa.

"Daniel haya mambo yanazidi kuwa na utata. Yule mtu wetu anayetupa taarifa kutoka kule anasema ndege ilitakiwa kuondoka na abiria sitini na nne. Lakini katika orodha kulikuwa na abiria sitini na tano ila kuna namba moja ilirudiwa mara mbili. Hivyo kwa mwonekano wa kawaida inaonekana kama orodha ni ileile sitini nne kumbe wamezidi. Kwahiyo ndege ilikuja na abiria sitini na nne ila mkeo aliyekuwa anatengeneza idadi ya watu sitini na tano hakuwepo ndani ya ndege. Swali la kujiuliza ni, Yuko wapi?" IGP John Rondo alisema.

"Natamani ningekuwa mzima nitegue hiko kitendawili. Huwa naburudika sana kufumbua mafumbo ya utata kama hayo" Daniel Mwaseba alisema kwa majonzi.

"Ni kweli Daniel. Lakini safari hii yametokea hayo pengine kuwapa nafasi wengine waoneshe uwezo wao. Usisikitike sana, kuna kijana mmoja anaitwa Adrian namuona anakuja vizuri sana. Mwanzoni alikuwa kule Mkuranga kabla ya kuhamishwa na kuletwa makao makuu. Naona tumpe nafasi ya kufumbua fumbo hili, hata siku Daniel usipokuwepo tutajua tuna Adrian" IGP John Rondo alisema.

"Adriiiian" Daniel alisema akikuna kichwa. "Si ni yule aliyefanya kazi ya kufumbua fumbo la Briefcase akiwa na Inspekta Jasmin?" Daniel aliuliza.

"Ndo huyohuyo, Adrian Kaanan, yupo vizuri sana kijana. Na nilikuwa nae kule uwanja wa ndege hivyo anafahamu kidogo nini tunafatilia. Kwakuwa Elizabeth Neville hayupo tumpe Adrian kazi ya kumtafuta Elizabeth Neville pamoja na Red butterfly" IGP John Rondo alisema.

"Kwakuwa ni askari siwezi kumkatalia kwakuwa ni moja ya majukumu yake. Lakini kiukweli hii kazi ni ngumu sana na ni hatari pia. Yupo wapi huyo Adrian?"

IGP John Rondo alitoka nje, akimwita Adrian na kuingia naye ndani. Wakaongea wakiwa watatu na Adrian kupewa kazi mbili, moja kumsaka Red Butterfly pia kumtafuta Elizabeth Neville yupo wapi. IGP alimwambia Adrian kuwa miongozo yote itatoka kwake na kwa Daniel Mwaseba. Adrian alipokea kazi hiyo kwa mikono miwili. Ilikuwa ndio kazi yake kubwa baada ile ya Briefcase ambayo akiifanya akiwa chini ya Inspekta Jasmin.


Mfupa huu mgumu unaelekea kwa Adrian Kaanan..je atauweza? Itaendelea kesho Mungu akipenda...
 
MAANDISHI YA HALFANI SUDY
RED BUTTERFLY 8
SIMU 0652 212391

Ilikuwa siku ya tatu tangu wakina Daniel washambuliwe. Hayakutokea mauaji yoyote kutoka kwa Red butterfly wala Elizabeth Neville hakujulikana alipo. Adrian Kaanan alikuwa anaendeleza upelelezi wake kwa umakini mkubwa sana. Alikuwa ameshapita katika familia za marehemu wote saba na kugundua mambo kadhaa ambayo alikuwa anaamini yatamsaidia katika upelelezi wake. Siku hiyo asubuhi na mapema alienda wodini kwa Daniel Mwaseba kumueleza wapi uchunguzi wake ulipofikia.

"Habari yako kaka Daniel?" Adrian alimsalimu Daniel.

"Nzuri aisee. Ninaendelea poa. Kidonda kinaendelea kukauka na maumivu yamepungua sana. Daktari amenambia kinapona haraka tofauti kabisa na matarajio yao" Daniel Mwaseba alisema.

"Tunakuombea sana Daniel upone haraka. Taifa linakusubiri katika harakati za kulijenga" Adrian alisema.

"Eeeh vipi ishu ya kumtafuta mke wangu imeishia wapi?" Daniel aliuliza.

"Bado naendelea kuchunguza mahali alipo shemeji. Nawasiliana mara kwa mara na watu wa kule China, kwa sasa wamemtambua na kumkamata mtu aliyeliingiza jina la Elizabeth Neville katika orodha ya watu walioondoka na ndege ile juzi. Bado wanamfanyia mahojiano. Maxi Lee amesema jioni atanipigia anipe nini amejibu katika hayo mahojiano. Tukipata sababu ya kuongezwa jina la Elizabeth Neville katika orodha ya abiria waliokuja juzi ndipo tunaweza kupata kiini cha mahali alipo. Kwa vyovyote vile huyo mtu aliyeliongeza jina la mkeo kule China anajua mahali mkeo alipo" Adrian alijibu.

"Umepiga hatua nzuri sana Adrian. Nashukuru umeenda vizuri sana kuhakikisha mke wangu anapatikana. Na vipi kuhusu suala la Red butterfly? Umefikia wapi?" Daniel aliuliza tena.

"Hapo ndipo kwenye utata kaka. Suala la Red butterfly ni suala tata sana. Baada ya kupewa kazi hii ya kuchunguza kuhusu Red butterfly nilienda katika familia zote za wafiwa. Nilianza katika familia ya kwanza ya Mzee Matojo. Nilifanya mahojiano na mjane wa marehemu. Hakuwa na mengi ya kusaidia katika kumpata Red butterfly, kikubwa kilichoganda kichwani kwangu kwamba mzee Matojo alikuwa anafanya kazi katika kiwanda cha Urafiki kabla ya kazi yake ya sasa. Nilipotoka pale nikaenda katika familia ya mzee Mahenge, kule niliongea na mdogo wa marehemu, naye alinisimulia mengi ingawa hayakunisaidia sana katika msako wa Red butterfly, lakini kubwa nililoondoka nalo pale mzee Mahenge naye ashawahi kufanya kazi katika kiwanda cha nguo cha urafiki. Nikahoji familia zingine nne, majibu yalifanana. Wote walifanya kazi kabla katika kiwanda cha urafiki. Mwishowe nikaenda kwa mjane wa mheshimiwa Elisha Ngwena..."

"Najua mzee Ngwena ashawahi kuwa meneja pale kiwanda cha urafiki" Daniel Mwaseba akadakia.

"Na hilo ndilo lilinivuruga kaka Daniel, kwanini marehemu wote saba wawe wamewahi kufanya kazi katika kiwanda cha Urafiki?"

"Uliyonieleza hapa yote nayafaham Adrian. Upelelezi wangu ulinifikisha hapo ulipofika wewe. Na nilikomea hapo kabla ya kupigwa hii risasi ya mguuni. Nafurahi sana kwakuwa umegundua kitu ambacho niligundua mimi awali. Sikutaka kukwambia kuhusu kiwanda cha urafiki kwakuwa nilitaka kujua kama nawe utafika hapo? Sasa hapo ndio mwanzo wa upelelezi wako Adrian. Hadi hapo ulipofikia nimeweka imani kubwa sana kwako kama utafumbua fumbo hilo" Daniel Mwaseba alisema.

"Usiwe na shaka na mimi kaka Daniel, nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kuhakikisha nayafumbua mafumbo haya mawili" Adrian alisema.

Waliongea kama nusu saa huku Daniel akimpa maelekezo Adrian. Walielewana, walikubaliana. Na Adrian alienda kuyafanyia kazi.

***

Saa nne kamili asubuhi ilimkuta Adrian Kaanan nje ya kiwanda cha nguo cha Urafiki. Alipaki gari yake na kuingia kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki.

"Kwa majina ninaitwa Adrian Kaanan. Ni askari Polisi ambaye nachunguza vifo vya watu saba akiwemo mheshimiwa Elisha Ngwena. Nimeamua kuja hapa ofisini kwako kutokana na utata wa vifo vya watu hao. Katika uchunguzi wangu nimegundua kuwa watu wote saba waliouwawa wamewahi kufanya kazi hapa. Na hiyo ndio sababu ya mimi kuwa hapa" Adrian alisema.

"Karibu sana Adrian. Mimi ndiye meneja wa kiwanda hiki. Ninaitwa Christopher Mbulu. Umeongea jambo ambalo hata hapa tulikuwa hatujaligundua bado juu ya marehemu wote saba kuwahi kufanya kazi katika kiwanda chetu" Christopher alisema.

"Ndio hivyo meneja. Marehemu wote waliwahi kufanya kazi hapa kwenu. Sasa hapo ndipo tunapopata mashaka na kuhisi labda kuna kitu kilitokea hapa miaka hiyo ambacho kinaweza kuwa pengine ndio sababu ya vifo vya watu hao?" Adrian alisema na kuuliza swali.

"Nimekuelewa vizuri sana Adrian. Sasa nini msaada wetu hapa. Mana mauaji haya yanatishia sana usalama wa nchi yetu" Meneja Christopher alisema.

"Hapa nimekuja kufata kitu kidogo sana. Najua huwa mnatunza rekodi muhimu hapa. Sasa nilikuwa ninataka safu ya uongozi wa kiwanda hiki wa mwaka 1954 hadi 1957. Watu waliofariki inaonesha wamefanya kazi hapa miaka hiyo" Adrian akasema.

"Hizo rekodi lazima zitakuwepo. Ngoja nimwite mtu wa records atutafutie" Meneja alisema na kutoka nje. Baada ya kama dakika kumi alirudi na karatasi nne mkononi.

"Nimezipata Adrian. Hii hapa ni safu ya uongozi ya mwaka 1954, hii ni ya 55, hii ni ya 56 na hii ndio ya 57" Meneja alisema huku akimkabidhi Adrian karatasi moja moja.

"Nashukuru sana meneja. Bila shaka katika karatasi hizi ninaweza kugundua jambo la kunisaidia katika uchunguzi wangu. Mimi ninaenda..nitakapohitaji chochote tunawasiliana" Adrian alisema na kupeana mkono na meneja. Akaondoka.

Ni dakika kumi na tatu tu tangu Adrian aondoke mle ofisini aliingia mgeni mwengine ofisini kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki. Mgeni huyo alikuwa mwanamke mrembo sana. Aliingia ofisini kwa madaha. Harufu ya marashi yake yaliimeza ile ofisi ya meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.

Baada ya salamu na kukaribishwa kitini mwanamke aliuliza swali.

"Yule Kijana aliyetoka hapa dakika kumi na nne zilizopita alikuwa amefata nini?"

Je huyu mwanamke ni nani? Na anataka nini? Sehemu ijayo sio ya kukosa.
 
MAANDISHI YA HALFANI SUDY
RED BUTTERFLY (9)
SIMU 0652 212391

Ni dakika kumi na tatu tu tangu Adrian aondoke mle ofisini aliingia mgeni mwengine ofisini kwa meneja wa kiwanda cha Urafiki. Mgeni huyo alikuwa mwanamke mrembo sana. Aliingia ofisini kwa madaha. Harufu ya marashi yake yaliimeza ile ofisi ya meneja wa kiwanda cha nguo cha Urafiki.

Baada ya salamu na kukaribishwa kitini mwanamke aliuliza swali.

"Yule Kijana aliyetoka hapa dakika kumi na nne zilizopita alikuwa amefata nini?"

Meneja alibaki na mshangao maana halikuwa swali alilolitarajia hata kidogo kutoka kwa mwanamke yule mrembo sana. Kilichomshangaza zaidi ni hali ya kujiamini ya mrembo yule.

"Nina mambo mengi ya kufanya Christopher, naomba nijibu swali langu niondoke" Mwanamke alisema huku akiuweka mkongojo wake juu ya meza alipoona meneja Christopher akichelewa kujibu.

"Huyu ni Red butterfly anayetafutwa. Na huu ndio mkongojo ambao niliusoma katika gazeti akitumia kuwashambulia wakina Daniel Mwaseba..." Meneja alikuwa akiwaza huku hofu dhahiri akijijenga usoni mwake.

"Alifa..." Kabla meneja hajaongea, mlango wa ofisi ulifunguliwa kwa pupa, alitokea Adrian akiwa kashika bastola imara mkononi mwake, bastola ilikuwa imeelekea katika kichwa cha yule mwanamke.

Yule mwanamke alistuka sana. Hakuutegemea ujio wa yule kijana aliyekuwa anamfatilia tangu alivyotoka katika hospitali ya Kairuki alipolazwa Daniel Mwaseba.

"Nyoosha mikono juu kabla sijapasua kichwa chako!!" Adrian alisema kwa ukali.

Siwezi kukamatwa na kitoto kama hiki, lazima nifanye kitu hapa. Iam a butterfly" Yule mwanamke aliwaza.

Sekunde ileile aliruka juu ya meza kimaajabu na kusimama nyuma ya mgongo meneja wa kiwanda. Mkongojo wake ulikuwa mkononi Iakini sasa ulikuwa mfupi mithili ya bastola. Mdomo wa bastola ulikuwa umegusana na shingo ya Meneja Christopher. Yule mwanamke alifanya kitendo kile kwa kasi ya ajabu. Kasi ambayo haijawahi hata kufikiriwa hata siku moja na Adrian Kaanan.

"Ni Red butterfly mwenyewe. Kasi yake ni ileile" Adrian alisema kwa sauti ndogo.

"Ukifanya ujanja wowote Adrian namuua huyu meneja!" Yule mwanamke alisema kwa sauti kubwa.

Meneja alikuwa anatetemeka sana. Ubaridi wa mdomo wa bastola ulimwogopesha sana. Ilikuwa mara yake ya kwanza kukaribiana na kifo katika maisha yake.

"Umekwisha Red butterfly, leo ni mwisho wako ..." Adrian alijisemea kimoyomoyo.

"R.B on target" Adrian alisema kwa sauti ndogo. Sekunde ileile waliingia wanajeshi watano wakiongozwa na Idd. Wanajeshi walikuwa katika gwanda za jeshi la Wananchi wa Tanzania. Na silaha zao mkononi.

Yule mwanamke hakuamini macho yake. Alihisi kuwa amekamatwa kirahisi sana.

"Wameniweza hawa wajinga. Sikuliwaza hili hata kidogo. Bila shaka hii itakuwa ni mipango ya Daniel Mwaseba tu. Hakika yule mwanaume sio binadamu wa kawaida. Sasa nitajiokoaje hapa?"

"Weka bastola yako chini!!" Idd alisema kwa ukali.


"Nikiweka bastola chini hapa nitakuwa nimejikamatisha mwenyewe. Siweki" Yule mwanamke aliwaza.

"Bastola sita za wanaume wenye mafunzo ya kijeshi umeelekezwa wewe. Huna ujanja wa kutoka hapa tena Red butterfly. Hapo ni kutii amri tu. Weka silaha yako chini" Adrian alisema akimrai yule mwanamke wa ajabu.

"Hamuwezi kunikamata mimi nyinyi. Na mkifanya ujanja wowote nitaondoka na roho ya huyu meneja!!" Yule mwanamke alisema kwa ukali.

Yule mwanamke akauangalia ule mkongojo wake. Akatabssamu. Wakati huo risasi alikuwa ameshaisogeza katika chemba kwa maana akitomasa kidogo tu triga ya mkongojo ule wa ajabu ilikuwa risasi inadidimia shingoni mwa meneja kiwanda cha urafiki. Christopher alikuwa anatetemeka huku akiamini ni miujiza tu ya Mungu ndiyo itakayomuacha salama.

Yule mwanamke akamnyanyua kwa nguvu Christopher kwa kutumia mkono wa kulia, sasa walikuwa wamesimama sambamba. Meneja Christopher mbele, yule Mwanamke wa mwenye kasi ya ajabu na shabsha ambaye walikuwa wanamtambua kwa jina la Red butterfly alikuwa nyuma.

"Niseme tena tu uhai wa huyu fala ninao mimi. Hata mkinipiga risasi roho yangu haitoenda motoni kabla sijaichakaza vibaya san shingo ya huyu mjinga. Sasa ombi ni moja tu kwenu, wekeni silaha chini na mnipishe hapo mlangoni. La sivyo nitakufa lakini nitakuwa nimeuwa..." Yule mwanamke alisema kwa kujiamini na woga wote uliomvaa awali ulikuwa umemtoka. Alijua ile ni karata yake pekee ambayo ilimpasa kuitumia vizuri kujiokoa. Maneno aliyoyasema yaliingia vizuri kwa wale askari. Na walijua kwamba mwanamke alikuwa anasema kweli. Alikuwa na uwezo wa kuuwa kabla hajafa. Na dhamira yao kama askari ilikuwa kumlinda meneja Christopher na sio kusababisha kifo chake. Ilikuwa dhima kuu ya askari, kulinda raia.

"Nakuuwaaa mwanaume.." Yule mwanamke alisema kwa sauti ndogo sikioni mwa meneja Christopher.

Leo kuna shughuli hapa, je Red butterfly atatoka salama?, ngoja nikupe ofa leo, kwa 2000 tu unaipata riwaya hii yote, ni whatsapp 0652 212391.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom