Six Man
JF-Expert Member
- Dec 19, 2017
- 254
- 892
Simulizi kutoka kwa Halfani sudy
Inaitwa; Red Butterfly
Mawasiliano; 0652212391
Sehemu ya kwanza
Ulikuwa ni usiku wa saa nane kamili. Usiku tulivu huku kelele za miti na ndege ndizo zikizosikika nje ya nyumba aliyolala mpelelezi Daniel Mwaseba maeneo ya Masaki.
Mara simu maalum ya Daniel Mwaseba ilianza kuita kwa nguvu, mlio wake maalum alioutega kwa sababu maalum. Mlio ambao haukuwa ule wa mtu kupiga. Sekunde hiyohiyo harakaharaka Daniel aliamka toka usingizini na kuitoa simu yake iliyokuwa chini ya mto. Simu ilikuwa inaita kwa nguvu na kuwaka taa nyekundu na kuzimika karibu na sehemu ilipo spika, inawaka na kuzimika.
"Ina maana ameua tena?" Daniel Mwaseba alisema huku akiangalia saa katika simu yake. Simu maalum ya Daniel ilikuwa imeunganishwa moja kwa moja na geti lake. Ilikuwa mtu yoyote akigusa geti lazima taarifa zipelekwe katika simu yake. Na alitega hivyo baada ya visa vya Red butterfly.
Harakaharaka Daniel aliinuka kitandani. Alitoka na kwenda katika chumba chake maalum. Alikuta kompyuta zake zote nne zikiwa zinawaka. Kompyuta moja iliyokuwa karibu na dirisha ndiyo iliyokuwa inaonesha picha za geti la nyumba yake. Daniel aliisogelea ile kompyuta na kuanza kuiangalia kwa umakini.
Kompyuta ilionesha nje ya geti kulikuwa na mwanamke mmoja mtu nzima akiwa na mkongojo. Mwanamke alikuwa anatumia mkongojo wake kugonga geti la Daniel Mwaseba kidogokidogo. Daniel alimwangalia kwa makini yule mwanamke mtu mzima.
"Red Butterfly umenifata tena nyumbani kwangu kama kawaida yako? Inamaana umeua tena?Safari hii nitakuonesha mimi ni nani?" Daniel alisema huku akichukua bastola iliyokuwa juu ya meza na kutoka nje harakaharaka.
"Red Butterfly ama zangu ama zako" Daniel aliwaza akiwa katika uwanja mpana sasa wa uwa wake, alikuwa anakimbilia nje kwa tahadhari kubwa sana. Bastola yake ikiwa mkononi, kidole chake cha shahada kikiwa katika triga tayari kumlipua Red Butterfly au yeyote yule atakayejipendekeza mbele yake. Daniel alipania kumaliza michezo ya kijinga anayoicheza Red butterfly kila anapofanya mauaji.
Alipolikaribia geti alipunguza mwendo. Sasa alikuwa anakwenda kwa tahadhari kubwa zaidi ili kumstukiza Red Butterfly. Kwa mkono wa kushoto alikuwa anafungua geti taratibu huku mkono wake wa kulia akiwa kaishika imara bastola fupi nyeusi huku kidole cha shahada kikiwa palepale kwenye triga. Taratibu geti lilifunguka. Daniel aliruka samasoti huku bastola yake akiielekeza pale alipokuwa Red Butterfly. Daniel alibaki mdomo wazi, hakukuwa na Red Butterfly. Alikuwa kalionesha bastola geti lake. Red Butterfly alikuwa ameruka tena kama kawaida yake.
"Kwa mara nyingine tena nimemkosa Red butterfly. Bila shaka na leo nitasikia taarifa za mtu kuuwawa na kubandikwa stika ya kipepeo mwekundu katika paji lake la uso ama tumboni. Huyu kibibi kizee mwenye mkongojo ni nani haswa? kila anapokuja kugonga hapa lazima auwe mtu na kumbandika stika ya kipepeo mwekundu" Daniel alijiuliza huku akiangaza huku na kule kwa kasi na umakini. Ilikuwa vilevile alibaki peke yake na bastola yake mkononi.
Red Butterfly hakuwepo.
Daniel alirudi sebuleni kwake. Alikaa juu ya sofa huku akiwa na mawazo lukuki.
"Huyu mwanamke ambaye nimepachika jina la Red Butterfly kutokana na kuja kugonga geti langu kisha yanatokea mauaji ya mtu aliyebandikwa stika ya kipepeo mwekundu usoni kwake ama tumboni ananiumiza sana kichwa changu. Hii ni mara ya sita anakuja kugonga katika geti langu na nikienda tu getini anayeyuka. Nini lengo la kuja kunigongea geti baada tu ya kufanya mauaji yake ya kinyama. Nusu saa mfululizo Daniel aliwaza na kuwazua. Afanye nini ili kumdhibiti mwanamke yule mwenye umbo la kizee. Anaua, anakuja kugonga kwangu na kuyeyuka. She is a red butterfly, tutaonana laki..."
Wakati Daniel akiwa katikati ya mawazo alisikia mlio wa simu yake ikiita. Alinyanyuka pale katika sofa na kuelekea chumbani kwake. Alijua tu ni nani aliyekuwa anampigia, pia alijua kwa vyovyote vile Red butterfly tayari kashafanya mauaji.
Aliichukua simu yake Kitandani ili kujua tu safari hii kamuua nani?. Hisia zake zilikuwa sahihi. Simu ilikuwa imepigwa na mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP John Rondo. Akaipokea na kusikiliza Red butterfly itakuwa kamuua nani?
" Hallo Daniel?" IGP Rondo aliita simuni.
"Habari afande?" Daniel aliita kwa sauti ya uwoga.
"Kuna mauaji yametokea..." IGP John Rondo alisema.
"Nani kauwawa?" Daniel alimkatisha IGP John Rondo kwa swali.
"Waziri wa mambo ya ndani Mheshimiwa Elisha Ngwena ameuwawa usiku wa saa saba. Amepigwa risasi ya tumbo na mtu asiyejulikana. Nakuomba uende sasahivi kujua nini chanzo cha kifo chake. Ukitoka hapo njoo moja kwa moja ofisini kwangu nitakuwa na kikao na wewe" IGP John Rondo alisema.
"Sawa mkuu. Nitakuwa nyumbani kwa waziri wa mambo ya ndani muda mfupi tu na nikimaliza mahojiano yangu nitakuwa ofisini kwako" Daniel alisema.
Simu ilikatwa.
Itaendelea kesho Mungu akipenda..
Inaitwa Red butterfly, kutoka kwa mwandishi Halfani Sudy..