Riwaya Angamizo 14

Feb 5, 2016
16
4
RIWAYA YA KIPELELEZI: ANGAMIZO
MWANDISHI: HALFANI SUDY
SIMU 0674 395733
WHATSAPP 0757 633010

SEHEMU YA KUMI NA NNE

Daniel hakusubiri.
Alichukua lile begi lenye laptop na kutoka nalo nje akiwa anakimbia. Akitafuta hotel salama na kujifungia ndani peke yake.Tayari kuifungua ile laptop yenye siri nzito. Moyo wake ulikuwa unamwenda kasi alipoliona faili lililiandikwa Siri! Akabofyabofya kidogo.
Sasa akatulia na kuanza kulisoma. Ghafla mlango ulifunguka kwa kasi! Ulikuwa umevunjwa kwa teke zito!.
Waliingia wazee wawili wakiwa wamevaa suti nzuri nyeupe.
"Hatujaja kuua. Tumefata laptop tu !" Mzee mmoja alisema.
"Hamuwezi kuipata laptop mpaka mniuwe kwanza" Daniel nae alijibu. Wale wazee walicheka kwa sauti kwa pamoja.
Walijiamini sana!
Wazee wale walitoa bastola .Midomo miwili ya bastola ilikuwa inamuangalia Daniel! Hakuihofia. Yeye alitabasamu tu. Wale wazee wawili Walikuwa wamenuna hasa.Tabasamu lile la Daniel waliliona kama dhihaka toka kwa Daniel. Wakawa wanamsogelea taratibu pale kitandani alipokaa. Daniel aliacha kuwaangaalia. Akawa anaitazama ile laptop. Ikifanya alichoiagiza. Ilikubali! Kichwani alifikiria cha kufanya.
Jamaa walimkaribia sasa. Zilibaki hatua kama tano wamfikie kabisa. walikuwa makini. Walikuwa wanamtambua Daniel. Walijua kosa moja tu lingewagharimu maisha yao yote!
"Simama juu !" Mmoja aliamrisha. Daniel alisimama taratibu.
"Mikono juu!" Yule yule wa mwanzo alitoa amri nyingine Daniel alinyoosha mikono yake juu.
Yule aliyetoa amri alimsogelea huku yule mwengine akiwa amebaki palepale. Akimnyooshea bastola yake. Jamaa alimpekua Daniel harakaharaka. Alipata visu viwili na bastola moja. Hivyo viliwekwa sehemu ya kawaida. Silaha alizoweka sirini hakuzipata. Zilihitaji mtu anayejua kupekua hasa. Akaishika ile laptop. Bila kuitazama akaifunga. Wakawa wanarudi kinyumenyume sasa.
"Naitwa kaspersky " yule aliyempekua Daniel alisema.
"Naitwa Zwangendaba" Na yule aliyekuwa kimya muda wote alisema.
Wakatokomea na laptop mbio!
"Tutakutana tu " Daniel alisema kimoyomoyo, huku akitabasamu.
Akatoka nje taratibu. Kwa utulivu mkubwa. Kama hajatizamwa na midomo miwili ya bastola dakika chache zilizopita. Alitembea kwa madaha. Kwa mwendo wa kujiamini. Huku akijiuliza kwanini wale jamaa walimwacha akipumua. Akawacheka ujinga. Hawakujua kuwa walifanya kosa la karne. Daniel Mwaseba alikuwa zaidi ya wanavyomfahamu!
Akarandaranda mitaa ya Mikocheni bila uelekeo maalumu. Aliranda makusudi. Alikuwa anachunguza kama kuna mtu anamfatilia. Hakumwona mtu. Akaingia kwenye "internet cafe" moja. Akalipia masaa mawili. Akaifungua email yake.
Alikuta akichokitaka.
Daniel aliikuta email iliyotumwa muda mfupi uliopita. Aliwapongeza wamiliki wa hoteli ile aliyokuwa mwanzo kwa kuweka "wireless internet'. Aliikuta email aliyojitumia yeye mwenyewe muda mfupi uliopita alivyokuwa kule hotelini. Kabla ya wale jamaa hawajamvamia. Kichwa cha email kilisomeka "SIRI ". Daniel akatabasamu tena. Sasa alianza kuisoma. Alianza kuisoma ile email yenye siri nzito!
"Hili ni Angamizo !.
Macho yasiyohusika hayapaswi kabisa kuona maandishi haya...."
Ghafla Daniel alihisi anapapaswa bega. Daniel aligeuka. Alikuwa anatazamana uso kwa uso na Zwangendaba!.
" Sasa nimekuja kuichukua roho yako rafiki yangu, unajifanya mjanja? " Alimnong'oneza Kwa sauti ndogo iliyopenya vizuri katika sikio la kushoto la Daniel.
Kwa mara ya kwanza mapigo ya moyo yalimpiga Daniel!. Hakutegemea kabisa watu wale kuwa mahali pale muda ule. Hakutegemea kabisa kukamatwa kirahisi namna ile. Alihisi Kutekenywa na kitu kigumu mbavuni.
Akaelewa.
Alikuwa ameguswa na bastola kwenye mbavu zake.
"Simama juu" Zwangendaba alinong'ona tena.
Daniel alisimama. Watu wote ndani ya 'internet cafe' hawakuelewa nini kinaendelea. Kila mtu alikuwa anatazamana na kompyuta yake. Daniel alikuwa anatekwa kimya kimya. Kaspersky naye aliingia ndani ya internet cafe. Akaisogelea ile kompyuta akiyoitumia Daniel. Akaifuta ile email ya siri. Akarudi nje wakapanda kwenye Noah yao nyeusi. Safari ya kwenda kusikojulikana iliaanza.
Ndani ya gari ilikuwa kimya. Hakuna aliyeongea. Wale majamaa wawili walikuwa wanavuta bangi kwa fujo ndani ya gari. Gari yote ilitapakaa moshi wa bangi. Yalikuwa mateso kwa Daniel. Hakuwa mvutaji hata wa sigara. Lakini hakuruhusu hata kukohoa. Alijua kukohoa tu ataonekana dhaifu mbele ya watu wale.
Safari isiyojulikana ilifika mwisho. Ilikuwa nje kidogo ya Jiji la Dar es salaam. Kulikuwa na kibanda kidogo porini. Kibanda kilichojitenga na nyumba za watu. Walimuweka kwenye kibanda hicho. Daniel alishuhudia migongo ya Kerspersky na Zwangendaba ikitokomea. Daniel walimfungia peke yake kwenye kibanda hicho!
Kilikuwa kibanda kidogo chenye mlango mmoja tu. Hakukuwa na madirisha wala sehemu yoyote ya kutolea au kuingiza hewa. Walimfungia kinje-nje. Alisikia muungurumo wa gari, jamaa walitoweka kwa kasi kwa gari yao. Bila shaka kwenda kumalizia mpango wao hatari wa Angamizo!.
Hawakutaka kumuua Daniel. Nia yao Daniel ashuhudie Angamizo litakaloikumba Serikali yake. Walimuacha hai ili ateseke kwa kuona Angamizo hilo litakuwaje?

DANIEL TUNDUNI, WALE MAJAMAA KWA MARA NYINGINE TENA WAMEIGUNDUA MBINU YA DANIEL...NJOO TENA KESHO KUUFAHIDI UHONDO HUU...MIMI TEAM ZWANGENDABA. WEWE JE?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom