FANANI MTENZI
Senior Member
- Jul 4, 2017
- 106
- 95
BONIFACE BIRAGE
Upepo upima mti nguvu na kuuona uhodari wake katika kujishikilia udongoni kwa kuimrisha mizizi iliyojikita.Ndiyo falsafa ya maisha na mikumbo yake hujikita katika kumbeba binadamu.”
Haya Laredo aliyakumbuka kama usiku na mchana unapofuatana au kama pande mbili za kioo.Alikumkbuka falsafa hii nakujiuliza katika maisha yake kuna kitu gani cha muhimu,mambo yalikuwa mengi nakujihifadhi kwenye kumbukumbu zake.Ndiyo ugumu upo na umesimama kama upinde!Lakini haukuwa kikwazo kwake.
Alijiangalia vizuri usiku huo akaridhika na uzuri alionao!Kisha alijirashia marashi ni baada ya kuoga.Akakifuata kiitanda ambapo mumewe alikuwa ameshalala.Alitamani sana kukitumia kitanda kile lakini ubaridi ulishapanda nakupazika.Hakuwa na thamani tena ya kuwepo pale.Na kama akienda kusingekuwa na bendera ya penzi lake ikisimama nakupepea mlingoti mzima.Ilikuwa imeshushwa kabisa nakubaki ukiwa.Akatoka pale nakwenda sebuleni pengine huko angepata lepe la usingizi.Alipofika aliwasha runinga nakuanaglia vipindi viwili vitatu lakini usingizi haukuja kabisa!Kifupi akili haikuwa imetulia na wala hakupata kitulizo cha suluhu ya mambo yake.
Kukumbatia mito ya kwenye makochi ndo faraja yake.Ndo iliyompa ahueni japo kidogo.Alitamani joto la mumewe kwa usiku ule.Halikupatika zaidi ya kufunguliwa kiyoyozi wakati wa baridi kali.Akainuka huku upande wa khanga ukijishika vizuri mwilini.Alitoka nje nakuelekea moja kwa moja hadi mlangoni akaufungua mlango nakutoka nje.Baridi ya nje ilimkumbatia mwili nakubusu ngozi yake!Akachichimkwa!
Giza lilishaikumba nchin nakuipa tuzo ya kuwa usiku.Akaanza kupiga hatua akielekea eneo alilotaka.Ni hatua kama saba hadi anapotaka.Alikuwa na wasiwasi kidogo hasa akikutwa kama alivyo isingekuwa vizuri nakumpa maswali.
Akaufikia mlango wa chumba ambacho alitegemea kufika.Hakubisha kama ilivyotegemewa.Kwa jirani hubishwa.Akashika kitasa na kukizungusha,mlango kikalia kacha!Akausukuma mlango naokasukumika.Alikutana na giza bila shaka aliyekuwemo mtu ndani nakuzima taa.Ilikuwa ni desturi yake kuja pale muda kama ule.Alijua nyumba ile hata kama kuna giza.Akaelekea moja kwa moja hadi kilipo kitanda.Aliyepanga pale ni mpangaji mwenzake.Kapanga chumba kimoja.Ni kijana tu mselamsela hivi.
Laredo alifikia kitanda na hapo wakakutana.Alimkuta ndo kama anapitiwa na usingizi.Akamgusa kifua chake kilichowazi nakumfanya azinduke kwa ghafla sana!Akampokea Laredo.Kwa ghafla miili yao ikapanda joto!Mzunguko wa damu na mapigo ya moyo yakaongezeka nakusababisha uchangamfu uliota kama wasiwasi hasa wakizingitia kwamba wanaiba mkutano huo.
Wakapelekeshana kitandani nakuanza kupapasana huku wakibusiana kwa nguvu kana kwamba walishindana!Walizungushana pale kwa dakika zile za kuiba kwa wingi wa hawaa na msukumo wa tamaa ukichangamana na kuridhiana katika tukio lile!
Purushani zile zilichukua dakika kama kumi zikawa zimepoa huku kila mmoja akihema kwa kasi!Hawakuzungumza kwanza walitulia kimya kwa muda lakini fikra hazikupanda kwanza zilijivuta polepole kama mafuta ya navyopanda kwenye kandili!Dakika zikakatika wakiwa bado bado kimya.Kisha Laredo akainuka nakuchukua upande wa khanga akajifunika nakutumia kingo za khanga kujifuta jasho.
“Unatak kwenda?”aliuliza Masua.
“Naenda ndiyo.”
‘Nafiri ungengoja kwanza.”
“Mzunguko wa pili nadhani ufanyike asubuhi mume wangu akiwa ameenda kazini.”
“Lakini Laredo mbona unanibania?”Masua alilalamika.
“Siyo nakubania hata kama tunaiba lakini siokuvuka mipaka.Yule ni mume wangu kumbuka.”
“Kiberiti kisicho na njiti hakina thamani tena.Kwanini unamng’ang’ania?Wewe unaona ni jinsi gani tunavyopendana mimi na wewe.Tunafurahia mahaba yetu kuliko watu wengi.Hata…”Masua akatishwa na Laredo.
“Naelewa unachotaka kusema.Hata mimi mwenyewe sijawahi kufurahia hivi kwa muda mrefu sana.Unanifikisha ninapotaka.Kuna wakati nakuwa na wakati mgumu,Nafikiria kitu.”akakoma nakuinama chini huku akionesha kutokuwa kawaida.Hatia ilimla.
Akafunga khanga vizuri akiwa tayari amesha vaa.
Masua alimgusa mabega kwa ukarimu na hali ya kujali.
“Unafikiria nini?”
“Kumwacha mume wangu iliniwe na wewe.Nakupunda wewe na nina mpenda mume wangu pia.”
“Kwa hivyo unaamua nini?Wewe bado mbichi unahitaji mapenzi ya dhati na mimi nitakupa.Muache ubaki na mimi?”
Laredo akatabasamu kivivu.
“Unadhani ni rahisi sana kuamua hivyo?”
“Ndiyo.Nichague mimi nikuchague wewe.Yaani tumechaguana.”alisisitiza Masua.Jasho lilikuwa likikaukia mwilini kufuatia baridi iliyoambatana na upepo wa usiku!
“Nakupenda Masua wangu.Nataka niwe na waume wawili!”lilikuwa jambo jipya!