Riwaya: Siri

Dah leo ucngizi haukupatikana kabisa maana kila nikisoma episode moja damu inazidi kuchemka Big up poti
 
Hapo mwanzo wakati naanza kusoma hii riwaya, nilikuwa sielewi Kwa nn watu wanakuwa na arosto.....
...sasa nimeeelewa baada ya kumaliza chapter zote......

Mkuu tupia mzigo tuendelee na burudani tafadhali
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 2 : EPISODE 1
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Mataifa mbali mbali
duniani yaliendelea kutoa wito
kwa makundi ya kidini
yanayopigana kuacha mara
moja na kuitaka jumuiya ya
kimataifa kuchukua hatua za
haraka za kuzuia umwagikaji
mkubwa wa damu
unaoendelea katika eneo la
Afrika Mashariki .Vikosi vya
majeshi ya ulinzi vya nchi za
Afrika mashariki vikisaidiana
na vikosi vya jeshi la Marekani
viliendelea na juhudi za
kudhibiti mapigano yale
makubwa lakini pamoja na
juhudi zao bado hali iliendelea
kuwa mbaya.Mapigano
yaliendelea kushika kasi kila
uchao.Majengo mengi ya ibada
na yale ya serikali pamoja na
magari vilichomwa moto na
makundi ya watu
wanaopigana.
Nchini Tanzania
mawasiliano ya simu na
inteneti vilizimwa ili kuzuia
watu kuwasiliana na
kuhamasishana kushiriki
katika vurugu.Ni taasisi
muhimu tu za serikali ndizo
zilizoendelea kuwa na
mawasiliano.Licha ya
kutokuwepo kwa mawasiliano
ya simu,bado vurugu
ziliendelea na kuilazimu
serikali kuongeza ulinzi zaidi
katika sehemu muhimu kama
vile mahospitali,mitambo ya
kuzalisha umeme,mitambo ya
kusukuma na kusambaza
maji,mabenki na vituo vya
polisi ambako makundi ya
watu walikuwa wakivamia na
kupora silaha ambazo
walizitumia katika mapigano.
Saa tano na dakika kumi
za usiku,Rais Dr Fabian
alimaliza kikao na wakuu wa
vyombo vya usalama kikao
kilichoanza saa kumi na mbili
za jioni.Kwa muda wa siku
nzima Dr Fabian amekuwa
akifanya kikao baada ya
kingine katika kujaribu
kutafuta suluhu ya machafuko
yale.Baada ya kumaliza kikao
na wakuu wale wa vyombo vya
ulinzi na usalama akawa na
mazungumo ya faragha na
mkuu wa majeshi kwa
takribani dakika arobaini na
walipomaliza akataarifiwa
kwamba wakuu wa idara ya
SNSA walikuwa wanamsubiri
kwa ajili ya kuzungumza
naye.Rais akaelekeza
wapelekwe nyumbani kwake
ataenda kukutana nao huko
kwani bado alikuwa na
mazungumzo ya faragha na
mkuu wa idara ya usalama wa
taifa.
Saa saba kasoro dakika
tisa Rais akaingia sebuleni
kwake ambako aliwakuta Ruby
na Gosu Gosu wakimsubiri.
“Samahani sana vijana
wangu kwa kusubiri muda
mrefu” akasema Dr Fabian
“Usijali mheshimiwa
Rais,tunaelewa uzito wa
majukumu uliyonayo”
akasema Ruby
“Sikuwajumuisha katika
kikao cha wakuu wa vyombo
vya ulinzi na usalama kwa
kuwa idara yenu ni ya siri na
kazi zake zinafanywa kwa usiri
mkubwa hivyo msijisikie
kutengwa” akasema Dr Fabian
huku akilegeza tai yake
“Tunaelewa mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby
“Kama hamtajali naomba
tukapate chakula kwani hivi
mnionavyo sijala chakula toka
nilipokunywa chai asubuhi”
akasema Dr Fabian na
kuongozana na akina Ruby
katika chumba cha chakula.
“Vijana wangu urais ni
mgumu sana.Nawashangaa
wale wanaong’ang’ania
madarakani.Sijamaliza hata
kipindi changu kimoja cha
urais lakini tayari nimeanza
kufikiria kutowania kuteuliwa
tena kipindi cha pili.Urais ni
mzigo mzito.Tazama hivi sasa
nchi imeingia katika
machafuko na watu wote
wananitazama
mimi.Nimeubeba mzigo mzito
mabegani mwangu kana
kwamba mimi ndiye
niliyeanzisha hizi vurugu.Toka
asubuhi sijapata hata nafasi ya
kupumzika ni kikao baada ya
kikao” akasema Dr Fabian
“Pole sana mheshimiwa
Rais.Ni kweli umebeba mzigo
mzito sana” akasema Ruby
“Tuachane na
hayo.Mnaendeleaje upande
wenu? Akauliza Dr Fabian
“Tunashukuru Mungu
tuko salama na tunashukuru
pia miundo mbinu yetu pia iko
salama.Jengo letu kuwa karibu
na ikulu imesaidia sana kwa
machafuko kutofika huku”
akasema Ruby
“Wafanyakazi wenu wote
wako salama? Akauliza Rais
“Ndiyo mheshmiwa Rais
wote wako salama.Tumeweka
kambi pale pale katika jengo
letu na sote tuko hapo hadi
pale hali ya amani
itakapokuwa nzuri” akasema
Ruby na ukimya mfupi ukapita
“Jioni ya leo
nimezungumza na Rais wa
Marekani akanitaka tusitumie
nguvu kubwa katika
kutawanya makundi ya
wanaopigana.Anadai idadi ya
watu wanaouawa na vikosi vya
ulinzi imekuwa kubwa hivyo
kuchochea machafuko zaidi.Si
yeye tu bali hata umoja wa
ulaya umetaka hivyo” akasema
Dr Fabian na kunyamaza
akaendelea kula halafu
akasema
“Nawashangaa sana hawa
viongozi wanaodai tusitumie
nguvu kubwa.Yawezekana
hawajawahi kukutana na
machafuko kama haya ya
kidini katika nchi zao ndiyo
maana inakuwa rahisi kudai
isitumike nguvu.Watu
wanavamia majengo ya
serikali,wanachoma majengo
ya
ibada,wanapora,wanaharibu
magari,wanachoma makazi ya
watu,wanaharibu miundo
mbinu halafu tusitume nguvu
kuwazuia?? Akauliza kwa ukali
“Huu ni upuuzi mkubwa
sana.Lazima tutumie nguvu
kuzuia machafuko haya
yasiendelee.Wanauawa watu
wasio na hatia.Wanawake na
watoto ndio wanaopata taabu
kubwa katika machafuko
haya.Tanzania tumezoea
kupokea wakimbizi kutoka
nchi nyingine lakini na sisi
yametukuta,hatuna kwa
kukimbilia.Tumeichezea
amani yetu na sasa tunayaona
madhara yake ! Naapa
kuendelea kutumia nguvu
kubwa kuhakikisha haya
makundi yanayochafua amani
yetu yanafutiliwa mbali !
akasema Dr Fabian na kuweka
kijiko chini hakuwa tena na
hamu ya kula chakula.Alizama
katika mawazo
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby
“Suala hili linanikosesha
amani kabisa.Malizeni kula
twende katika mazungumzo”
akasema Dr Fabian.Ruby na
Gosu Gosu walimaliza kula Dr
Fabian akawachukua
wakaenda katika chumba cha
mapumziko
“Ni saa tisa sasa
mapambazuko
yanakaribia.Toka
mapambazuko ya jana
sijafumba jicho na ninawataka
ninyi wasaidizi wangu nanyi
pia msifumbe macho yenu
hadi pale tutakapohakikisha
balaa hili limepita” akasema
Dr Fabian halafu ukapita
ukimya
“Vijana wangu nimefurahi
kuwaoneni tena mkiwa
salama.Nataka kufahamu kile
kinachoendelea ndani ya SNSA
kwani toka zilipoanza vurugu
sijapata wasaa wa kukaa nanyi
tukazungumza yale
yanayoendelea katika idara
yenu.Vyombo vyote vya ulinzi
na usalama kuanzia jeshi
polisi,jeshi la
wananchi,zimamoto na
vingine vyote mnavyovifahamu
wamejielekeza katika kudhibiti
vurugu lakini mpaka sasa
hakujakuwa na mafanikio
yoyote vurugu bado zimeshika
kasi” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais idara
yetu kama ilivyo jina lake
haijihusishi sana na masuala
ya udhibiti wa vurugu kwani
hiyo ni kazi ya jeshi la polisi
lakini katika suala hili sisi
tumejikita zaidi katika
kufahamu chanzo cha hizi
vurugu ni nini au ni nani?
Japo vurugu hizi zinatufanya
tushindwe kufanikisha jukumu
letu ipasavyo lakini kuna
mambo kadhaa
tumeyabaini.Katika uchunguzi
wetu wa awali tumebaini
kwamba vurugu hizi zinaweza
kuwa ni zaidi ya
tunavyofikiri.Yawezekana
ikawa ni zaidi ya chuki za
kidini”
“Kwa nini unasema
hivyo?Kuna kitu
mmekigundua? Akauliza Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais,kuna
chembe chembe za siasa ndani
ya vurugu hizi” akasema Ruby
halafu akanyamaza kidogo
“Muda mfupi baada ya
mkuu wa jeshi la polisi kutoa
tamko akiwa jijini Tanga
kuwataka watu waendelee
kuwa wavumilivu na kwamba
serikali inayafanyia uchunguzi
matukio yale ya mauaji ya
viongozi wa dini yaliyokuwa
yanaendelea jijini Tanga,katika
ukurasa wake wa twitter Karim
Abdallah ambaye anaongoza
chama cha siasa cha TPD
aliandika ujumbe akiwahimiza
waumini wa dini ya kiislamu
jijini Tanga kwenda
kuwatafuta wale ambao anadai
walimuua Sheikh mkuu wa
mkoa wa Tanga.Ujumbe huo
wa kichochezi haukukaa sana
akaufuta lakini tayari watu
wengi walikwisha usoma
kwani Karim ana watu wengi
wanaomfuatilia katika
mitandao ya kijamii.Kwa
mwanasiasa kama huyu
kuandika ujumbe kama ule
ambao una mlengo wa
uchochezi inatupa wasiwasi na
kutufanya tulione suala hili
kama lina chembe chembe za
siasa ndani yake.Ukichunguza
katika vurugu hizi utaona kuna
makundi yameibuka ambayo
yanalenga katika kuharibu
miundo mbinu muhimu vile
vile kuvamia na kuharibu
majengo ya taasisi za
serikali”akasema Ruby na Dr
Fabian akapandwa na hasira
“Namfahamu Yule kijana
ni mwanasiasa mchonganishi
na amekuwa akiandika mara
kadhaa jumbe za uongo na
uchonganishi kati ya wananchi
na serikali. Ruby kuna picha
nimeanza kuipata kufuatia
maelezo yako.Sikuwahi
kuusoma huo ujumbe wa
twitter aliouandika lakini
naamini kabisa lazima Karim
atakuwa na mahusiano na
vurugu hizi.Kijana mshenzi
sana Yule ! akasema kwa ukali
Dr Fabian
“Aliufuta ujumbe huo
ndani ya muda mfupi tu lakini
wengi tayari walikwisha
usoma” akasema Ruby
“Mmekwisha anza
kumfanyia uchunguzi huyu
jamaa??akauliza Dr Fabian
akionekana kuwa na hasira
kali
“Mheshimiwa Rais kuna
ugumu kidogo katika
kulitekeleza hilo.Kwanza
tumeshindwa kufuatilia
mawasiliano yake yote kwani
hakuna mawasiliano ya simu
wala intaneti.Pili ni ugumu wa
kumfuatilia nyendo zake kwani
huko mitaani kumetapakaa
vurugu na magari
yanachomwa.Barabara nyingi
zina vizuizi vya kuzuia magari
hivyo tumepata ugumu katika
kuifanya kazi yetu” akasema
Ruby
“Mngenieleza mapema ili
niangalie namna ya
kuwawezesha kutekeleza
majukumu yenu” akasema Dr
Fabian
“Ndiyo maana tuko hapa
mheshimiwa Rais kuleta
maombi yetu kwako”
“Nini mnakihitaji
Ruby?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais kwa
hivi sasa hakuna mawasiliano
ya simu hapa nchini isipokuwa
kwa ofisi nyeti za
serikali.Pamoja na kuzima
mawasiliano ya simu kwa
lengo la kuzuia watu
kuhamasishana kushiriki
katika vurugu,lakini bado
haijasaidia sana kwani bado
vurugu
zinaendelea.Tunashauri
mawasiliano ya simu
yarejeshwe kama kawaida”
akasema Ruby na Dr Fabian
akaonyesha mstuko kidogo
“Turejeshe tena
mawasiliano ya simu? Hali
itakuwa mbaya zaidi kwani
watu wanatumia simu
kuwasiliana na kuhamasishana
kushiriki katika vurugu na hili
ndilo lilipelekea tukaamua
kuzima mawasiliano yote ya
simu na intaneti na hii
itaendelea hivi hivi hadi pale
vurugu zitakapokoma kwani
tukirejesha mawasiliano
tutaendelea kuongeza chuki na
vurugu zitapamba moto !
Akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais pamoja
na nia njema ya jambo hilo
lakini kuna athari zake vile
vile.Siku hizi watu
wanategemea sana simu zao
katika shughuli mbali mbali
hivyo mkiwanyima fursa ya
kutumia simu zao ni
kuwafanya maisha yao yawe
magumu zaidi hata hivyo
sababu kubwa ambayo
tunashauri mawasiliano ya
simu yarejeshwe kama
kawaida ni ili kuwafanya watu
waone maisha yamerejea
kawaida wataamini kwamba
hali ya amani imeanza
kuboreka.Jambo lingine ni
kwamba mamilioni ya
watanzania sasa wanamiliki
simu janja.Tutazitumia simu
hizo kufikisha ujumbe kwa
wananchi kuhusu umuhimu
wa amani na kuepuka
kushiriki katika vurugu
zinazoendelea hivi
sasa.Mheshimiwa Rais
utalihutubia taifa na ili ujumbe
wako uweze kuwafikia watu
wengi zaidi na kwa haraka
tutatumia teknolojia ili hotuba
yako iweze kutazamwa na watu
wote wenye simu janja zao kwa
mara moja”akasema Ruby
“Inawezekana? akauliza Dr
Fabian
“Ndiyo mheshimiwa Rais
inawezekana.Simu janja zote
ambazo zitakuwa zimewashwa
muda huo zitapokea hotuba
yako moja kwa moja bila
mmiliki kujiunga sehemu
yoyote.Kwa mfano waweza
kuwa unawasiliana na mtu
Fulani au unafanya chochote
katika simu basi kila kitu
kitasimama kwa muda na
mtumiaji ataunganishwa moja
kwa moja na hotuba ya
Rais.Pale hotuba itakapokuwa
imemalizika basi mawasiliano
yao yataendelea kama kawaida
na ujumbe utakuwa
umewafikia karibu nusu ya
nchi na hii inaweza ikasaidia
sana kuwafanya watu
wakatafakari kuhusu hizi
vurugu na inaweza ikasaidia
zikapungua kama si
kumalizika kabisa” akasema
Ruby
“Hilo ni wazo zuri
Ruby.Sikuwa nimelifikiria
kabisa” akasema Dr Fabian
“Hilo linawezekana
mheshimiwa Rais na
itatusaidia hata sisi kupata
nafasi nzuri ya kumfuatilia
Karim kujua mienendo yake na
kufahamu mahala alipona
tutamchukua ili atueleze
alichomaanisha katika ule
ujumbe wake wa uchochezi”
akasema Ruby
“Nimekuelewa Ruby na
ahsante sana kwa wazo hili
nitalifanyia kazi.Hilo jambo
litatekelezwa kesho.” akasema
Dr Fabian
“Baada ya hotuba yako
hiyo unaweza ukawatafuta
viongozi wa dini mkakaa meza
moja kulijadili suala hili na
mnaweza kujikuta mmepata
muafaka kwani chanzo cha
vurugu zote ni masuala ya
kiimani” akasema Ruby
“Kuhusu hilo la kukutana
na viongozi wa dini nilikuwa
nafikiria kuwakamata viongozi
wote wakuu wa dini na
kuwafungia sehemu moja
niwaache wazungumze hadi
muafaka upatikane.Tukifaulu
kudhibiti makundi ya dini
tutakuwa tumelimaliza suala
hili kwani hayo makundi
mengine ya waporaji
yanajikinga na mwavuli wa
machafuko ya kidini” akasema
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais sidhani
kama hiyo ni njia nzuri kwa
sasa.Kuwakamata viongozi hao
wa dini kwa sasa itakuwa ni
kuongeza mafuta kwenye moto
kwani chanzo cha vurugu hizo
ni kuuawa kwa viongozi wa
kidini hivyo viongozi wengine
wakikamatwa hata kama ni
kwa nia njema basi vurugu hizi
zitaongezeka mara mbili”
akasema Ruby
“Ruby hawa viongozi
wanaweza wakawa na
mchango mkubwa sana katika
kutafuta suluhu ya vurugu
hizi.Umekuwa ni utamaduni
wetu kukaa mezani
kuzungumza kila pale
kunapokuwa na tofauti zozote
za kiimani naamini hata sasa
kama wakikaa pamoja basi
wanaweza wakazungumza
wanaweza wakafikia
makubaliano na
wakazungumza na waumini
wao kuwasihi waache vurugu”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais,nasema
haitakuwa rahisi kwa viongozi
hao wa dini kuwa na
maelewano hasa ukiangalia
chanzo cha vurugu
hizi.Ukiangalia namna vurugu
hizi zilivyoanza hapa kwetu
Tanzania ,aliuawa kiongozi
mmoja wa kanisa na waumini
wake kadhaa,usiku wa siku
hiyo hiyo akauawa sheikh
mkuu wa mkoa wa Tanga na
hii ilipeleka kila upande
kulaumu watu wa imani
nyingine kuhusika katika
mauaji yale ya viongozi na
vurugu zikaanzia hapo.Mbegu
mbaya ya chuki tayari
imekwisha pandwa miongoni
mwa waumini na viongozi wao
wa dini,kila upande
ukiwachukia wengine.Hata
ukiwaweka pamoja kila
upande utalaumu upande
mwingine kwamba ndio
chanzo cha vurugu.Njia pekee
ya kulitatua suala hili ni
kutafuta chanzo cha vurugu ni
nini au ni nani? Tunatakiwa
kufahamu nani waliomuua
yule kiongozi wa kanisa na
waliomuua Sheikh mkuu wa
Tanga? Tukifanikiwa
kuwafahamu watu hao basi
tunaweza kupata mwanga wa
vurugu hizi na hata
ukiwakutanisha viongozi wa
dini na ukawaeleza kuhusiana
na hiki tunachokifanya
wanaweza wakaelewa”
akasema Ruby
“Papo hapo tusisahau
kwamba vurugu hizi zilianza
Uganda na kuenea Tanzania
hadi Kenya.Tukitaka kupata
kiini cha vurugu hizi tuanze
kuchunguza namna
zilivyoanza nchini
Uganda.Huu ni kama ugonjwa
ambao umeibuka Uganda
ukaingia Tanzania na Kenya na
kama hakutakuwa na tiba ya
haraka basi ugonjwa huu
unaweza ukasambaa Afrika
nzima” akasema Gosu Gosu
“Uko sahihi Gosu
Gosu.Hali hii lazima idhibitiwe
kwa gharama zozote.Hatuwezi
kuacha hali hii
ikaendelea.Nchi imesimama
kutokana na vurugu hizi
ambazo ni kubwa hadi
kushindwa kudhibitiwa na
vikosi vyetu vya
ulinzi.Wamekuja wanajeshi wa
Marekani lakini bado
hawatoshi.Vurugu ni kubwa”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa rais kwa
nini Marekani imetuma
wanajeshi wake Afrika
mashariki? Uliomba msaada
kwao? akauliza Ruby
“Sikuomba msaada
wowote kutoka Marekani.Rais
wa Marekani alilazimika
kutuma wanajeshi kwa ajili ya
kusaidia kuimarisha hali ya
amani vile vile kulinda raia wa
Marekani na wa nchi nyingine
za kigeni waliokwama Afrika
mashariki vile vile kulinda
balozi zake.Kama mnavyojua
ubalozi wa Marekani nchini
Uganda ulichomwa moto na
watu katika vurugu hizi
zinazoendelea hivyo
wamechukua tahadhari katika
balozi zao nyingine za Dar es
salaam na Nairobi.Vile vile
wanatusaidia katika ulinzi wa
miundo mbinu muhimu kama
vile bandari.Wameleta meli za
kijeshi katika bandari za Dar
es salaam na Tanga ambazo
zinasaidia katika ulinzi wa
bandari hizo.Huu ni msaada
mkubwa wametupa” akasema
Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais,kubwa
lililotuleta kwako ni hilo
tulilokueleza kwamba
mawasiliano ya simu yarejee
kama kawaida ili kutuwezesha
kufanya shughuli zetu kwa
wepesi zaidi” akasema Ruby
“Hilo litafanyiwa kazi
kesho msihofu lakini
hakikisheni huyu kijana Karim
anapatikana tena ikiwezekana
achukuliwe ahifadhiwe katika
moja ya nyumba zetu ateswe
sana hadi aeleze alimaanisha
nini kuhusiana na ujumbe huo
wa kichochezi aliouandika
katika ukurasa wake wa
twitter.Nataka huu uwe ni
mwisho wa Karim ! akafoka
DrFabian
“Tunalifanyia kazi hilo
mheshimiwa Rais na
tutafahamu kila kitu” akasema
Ruby na kumtazama Gosu
Gosu
“Mheshimiwa Rais
umechoka sana naomba
tukuache upumzike hata
kidogo kwani inakaribia saa
kumi na moja za alfajiri sasa”
akasema Ruby
“Nitawezaje kulala wakati
wananchi wangu hawajalala
wanakesha kwa hofu na
wengine wakiishi katika
makambi kama wakimbizi
ndani ya nchi yao kwa hofu ya
usalama wao?Nitalala pale
ambapo vurugu zitakoma.Kwa
hivi sasa ninakwenda
kuzungumza na Rais wa China
katika simu.Nawashukuruni
sana kwa mawazo mazuri
mliyonipa.Nadhani hata
wasaidizi wangu nao pia
wamechanganyikiwa na haya
yanayoendelea ndiyo maana
hakuna hata mmoja wao
aliyenipa ushauri kama huu
mlionipa ninyi.Nendeni
mkaendelee na kazi
muhakikishe watu wenu wote
wanakuwa salama na vile vile
muhakikishe mnawapata
walioanzisha vurugu hizi”
akasema Dr Fabian akaagana
na akina Ruby wakaondoka
kurejea katika jengo la ofisi
yao ambalo halikuwa mbali na
Ikulu.Toka vurugu
zilipoanza,karibu wafanyakazi
wote wa SNSA waliweka kambi
hapo katika jengo la ofisi yao
kwa ajili ya usalama wao.
“Gosu Gosu tuna kazi
kubwa ya kufanya kuhakikisha
tunapata kiini cha vurugu
hizi.Naamini hazikuibuka hivi
hivi lazima wapo
waliozianzisha.Ni akina nani
na nini lengo lao? Hayo ndiyo
maswali ambayo tunahitaji
kuyatafutia majawabu”
akasema Ruby
“Nyakati kama hizi ndipo
humkumbuka sana Mathew
Mulumbi.Naamini huko aliko
anaona kile kinachoendelea
hapa nchini.I miss him so
much” akasema Gosu Gosu.
“Are you scared
Papii?akauliza Ruby
“I’m not scared.Mimi ni
mwanajeshi toka nikiwa
mdogo nimeishi katikati ya
mapigano makubwa hivyo
sijawahi ogopa hata mara moja
na sintoogopa kamwe”
akasema Gosu Gosu
“Good.Mathew hayupo na
jukumu hili ni
letu.Tutamshirikisha pia
Austin pale
itakapolazimu.Tuna kazi
kubwa ya kuhakikisha
tunauchimba mzizi wa
machafuko haya” akasema
Ruby na ukimya mfupi ukapita
halafu Gosu Gosu akasema
“Ruby kuna kitu nataka
kuuliza naomba tafadhali uwe
mkweli” akasema Gosu Gosu
“Siku zote nimekuwa
mkweli kwako.Uliza
nitakujibu”
“Ni kuhusu Mathew.Wewe
ndiye ulikuwa mtu wa mwisho
kuonana naye.Unafahamu
mahala alipo? akauliza Gosu
Gosu.Ruby hakujibu
akaendelea kuendesha
gari.Usiku huu hakuwa na
dereva yeye ndiye aliyeshika
usukani.
“Nijibu Ruby.Unafahamu
mahala alipo?
“Kwa nini unahitaji kujua
Gosu Gosu?
“Mathew ni kaka yangu,ni
mtu wangu wa
karibu.Nilipofumbua macho
na kumuona sikuamini macho
yangu kama kweli ni
yeye.Nilidhani labda ni mzimu
ninauona.Kumbe siku zote
hisia zangu kwamba hakuwa
amefariki ni za kweli.Kwa
bahati mbaya nilipata muda
mfupi sana wa kuwa naye
kisha akatoweka tena na
sijafahamu alikuwa wapi,nini
kilimtokea na amekwenda
wapi.Nahitaji kufahamu kama
kuna chochote alikwambia”
akasema Gosu Gosu.Zikapita
dakika mbili Ruby akasema
“Alinieleza kwa ufupi sana
kuhusiana na mambo
aliyoyapitia.Aliniambia
kwamba alitekwa na Mossad
na amepitia mateso mengi
sana.Ukimtazama mgongo
wake wote umejaa makovu
mengi ukionyesha namna
alivyopitia mateso
makali.Alikuwa makini sana
katika kueleza mahala
alipokuwa.Kuhusu mahala
alipo sasa sifahamu na
alinitaka atakapoondoka
nisimtafute ila aliweka ahadi
kwamba atarejea
tena”akasema Ruby
“Hakukueleza anakwenda
wapi? Akauliza Gosu Gosu
“Hapana hakunieleza na
alinitaka nisijaribu kumtafuta
lakini…….” Akasema Ruby na
kunyamaza kidogo
“Kuna nini Ruby?
“Kuna kitu nilikigundua”
akasema Ruby na kunyamaza
tena.
“Katika kipindi chote
alichorejea nilikuwa naye na
niligundua kuna mtu alikuwa
anawasiliana naye na kumpa
taarifa mbali mbali kuhusiana
na operesheni ile iliyomalizika
ya kumuua James Kasai”
“Alikuwa akiwasiliana na
mtu? akauliza Gosu Gosu.
“Ndiyo kuna mtu alikuwa
anawasiliana naye”
“Hukufanya uchunguzi
kujua alikuwa anawasiliana
nani?akauliza Gosu Gosu
“Hapana
sikuchunguza.Mathew hapendi
kuchunguzwa.Mtu huyo
alikuwa anawasiliana naye
usiku tu na alikuwa
anawasiliana naye akiwa
amejifungia ofisini kwake hii
ina maana kwamba hakutaka
mimi au mtu yeyote kufahamu
kuhusu mawasiliano yao na
mimi sikutaka
kuchunguza.Kila alipotoka
kuwasiliana na mtu huyo
alikuwa anakuja na taarifa
mpya.Mathew ana siri kubwa
sana anatembea nayo.Tufuate
vile alivyoelekeza na muda
utakapofika atarejea na
atatuweka wazi nini
kinaendelea katika maisha
yake.Sisi ni ndugu zake na
hataweza kutuficha kitu”
akasema Ruby
“Sawa Ruby
nimekuelewa.Ahsante sana
kwa kuwa muwazi” akasema
Gosu Gosu
“Naamini umeridhika kwa
haya niliyokueleza.Tunalifunga
suala la Mathew hadi pale
tutakaposikia chochote kutoka
kwake kwa sasa tujielekeze
katika kuuchimba mzizi wa
hizi vurugu zinazoendelea”
akasema Ruby.
Walifika katika jengo la
ofisi yao kuu.Ni watu
wachache tu waliokuwa ofisini
alfajiri hiyo wengi walikuwa
katika mahema
yaliyotengenezwa kwa ajili yao
pembeni ya jengo la ofisi.
“Gosu Gosu tutumie muda
huu mfupi uliosalia kabla ya
mapambazuko tupumzike
kwani tutakuwa na ratiba
ndefu sana siku ya leo”
akasema Ruby na kila mmoja
akaelekea katika sehemu yake
ya kulala
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Ni saa tatu za usiku jijni
Washington DC
Marekani.Katika ikulu ya
Marekani Rais William
Washington na makamu wake
Mark Piller walimaliza
kutazama hotuba ya Rais
Armen Hijazi wa Iran.Ni
hotuba iliyosubiriwa kwa
hamu duniani,wengi wakitaka
kusikia msimamo wa Iran
kuhusiana na matamshi ya rais
wa Marekani William
Washington kwamba atalifuta
taifa la Iran.Katika hotuba
yake hiyo ya kumjibu William
Washington,Rais Armen Hijazi
aliionya vikali Marekani
kutothubutu kwa namna
yoyote ile kuvamia ardhi ya
Iran kwani watakachokipata
kitaingia katika historia ya
dunia.Kama haitoshi Rais
Armen alimtaka Rais wa
Marekani kufuta kauli yake
kwamba atalifuta taifa la Iran
kwani kauli yake hiyo
ingeweza kumrudia yeye na
taifa lake.Ilikuwa ni moja ya
hotuba iliyoleta hofu kubwa
kwa Marekani na dunia
wakihofia kuzuka kwa vita
kubwa kwani Rais Armen
aliweka wazi kwamba nchi
yake iko tayari kwa vita na
Marekani na alisistiza kwamba
wataishambulia Marekani
pamoja na washirika wake
watakaoisaidia na alitishia
kwamba baada ya vita hiyo
Marekani haitakuwa sawa tena
na itachukua zaidi ya miaka
hamsini kuijenga tena
Marekani.Katika kumalizia
hotuba yake Rais Armen
aliweka wazi mipango ya Iran
ya kuendelea na urutubishaji
wa madini ya Urani.
“Huu ni upuuzi mkubwa
sana ! akafoka Rais William
baada ya hotuba ile kumalizika
“Siwezi kuvumilia upuuzi
kama huu.Armen hawezi
kututamkia maneno kama
haya sisi ! akaendelea kufoka
William.
“Mheshimiwa Rais haya
maneno yote aliyoyazungumza
Armen ni upuuzi na ni maneno
ya mtu aliyeshindwa.Iran
haina uwezo wowote wa
kuipiga Marekani”akasema
Mark Piller
“Siwezi kuvumilia ujinga
wa namna hii.Marekani ni
taifa kubwa na hatuwezi
kukubali taifa kama Iran
kututolea vitisho vya namna
hii.Ninaapa lazima niishikishe
adabu Iran ! akaendelea
kufoka William ambaye ni
mwepesi sana wa kupandwa
na hasira
“Mheshimiwa Rais hiki
alichokisema Armen
kisikukoseshe amani.Hakuna
anachoweza kufanya
kwetu.Haya matamshi yake
aliyoyatoa leo dhidi yetu
hayatabadili mipango yetu
dhidi ya taifa hilo lakini
nashauri mheshimiwa Rais
huyu mtu tumuendee taratibu”
akasema Mark Piller
“Kiburi alichokionyesha
Armen hakiwezi
kuvumilika.Ameongea kwa
kujitapa kabisa kwamba nchi
yake itaendelea na
urutubishaji wa madini ya
Urani.Hatuwezi kuiacha Iran
ikaendelea na zoezi hili la
urutubishaji wa madini ya
Urani.Lazima tuchukue hatua
kali sana dhidi ya taifa hilo !
akaendelea kufoka William
Washington
“Mheshimiwa Rais suala
hili si jepesi na tunahitaji
umakini mkubwa sana katika
kulishughulikia.Armen ni Rais
mjanja sana.Ametoa matamshi
yale akitegemea kwamba
Marekani lazima itahamaki na
kuanza haraka kuchukua
hatua.Lazima tuwe makini
naye sana.Tumuonyeshe
Arman kwamba sisi ni taifa
kubwa na
hatukurupuki”akaksema Mark
Piller
“Mark hatuna muda wa
kumbembeleza huyu
mtu.Uvumilivu wangu umefika
ukomo.Kinachofuata ni
kumtandika vikali,kuharibu
vinu vyake vya nyuklia na
kumuondoa madarakani rais
Armen ! akasema William
“Mheshimiwa Rais,ni
mapema sana kufikia hatua
hiyo” akasema Mark lakini
William aliyekuwa amewaka
hasira akamgeukia
akamtazama kwa macho
makali na kusema
“Unataka huyu mtu
aendelee kutoa vitsho kwa
Marekani? Unadhani ni hofu
ya namnagani wameipata watu
wetu kufuatia matamshi yake
ya kuivuruga Marekani? Katu
hatuwezi kuwaacha wananchi
wetu waendelee kuishi kwa
hofu ya vitisho vya
Iran.Hawatatuelewa
tutakaposhindwa kuchukua
hatua zozote za
kuwalinda.Msuguano huu na
Iran umechukua muda mrefu
na sasa umefika wakati wa
kuumaliza.Niamini Mark
ninakwenda kulimaliza suala
hili .Siwezi kuipa nafasi Iran ya
kuendelea kuruubisha madini
ya Uran.Iran ikifanikiwa
kutengeneza bomu la nyuklia
hatutaweza kumdhibii tena na
eneo lote la Mashariki ya kati
litaingia katika hofu
kubwa.Lazima tuwahi angali
mapema na njia pekee ni
kuitandika kijeshi” akasema
William
“Mheshimiwa Rais
msuguano huu wa Marekani
na Iran umechukua muda
mrefu kwa sababu mpaka sasa
hatufahamu Iran anamiliki
silaha za namna gani.Mpaka
sasa hatufahamu kwa nini Iran
inakuwa na kiburi cha
kutunishiana misuli ya kijeshi
na Marekani.Hakuna taifa
katika zama hizi ambalo
limewahi kutamka
kuishambulia Marekani zaidi
ya Iran.Lazima kuna kitu
kinaipa kiburi Iran cha kuwa
tayari kuingia vitani na
Marekani hata
kesho.Nimekuwa katika
shirika la ujasusi CIA kwa
muda mrefu na tumekuwa
tukihangaika kujua Iran ina
silaha gani kali lakini mpaka
leo hatujafanikiwa kujua Iran
anamiliki silaha gani.Iran
wamekuwa wakidai kwamba
wana makombora ya masafa
marefu na wametishia
kushambulia nchi zote
washirika wa Marekani katika
Mashariki ya kati ikiwemo
Israel.Mpaka sasa hatuna
uhakika kama hiki
wanachokisema ni cha kweli
ndiyo maana nasema kwamba
hatuwezi kukurupka katika
suala hili.Tunao uwezo wa
kumtandika Iran lakini ni vipi
kama madai yake ya umiiki wa
silaha kali ni ya kweli.Vile vile
tukiivamia Iran kijeshi
tutakuwa tumeanzisha
mgogoro mwingine kwani Iran
na Urusi wana urafiki mkubwa
na wamekuwa wakisaidiana
kijeshi.Hatutapigana vita na
Iran pekee bali tutakuwa vitani
na Urusi pia.Usisahau vile vile
kwamba hivi karibuni Rais wa
Iran alifanya ziara nchini
China na mahusiano ya Iran
na China yameanza kuboreka
hivyo nchi hizi lazima
zitamuunga mkono Iran kama
tutaishambulia kijeshi.Tazama
namna Iran na Urusi
walivyoshirikiana kuiunga
mkono serikali ya Syria hadi
kuiwezesha kukomboa asilimia
zaidi ya tisini ya maeneo
yaliyokuwa yanashikiliwa na
waasi ambao tulikuwa
tunawaunga mkono.Suala hili
ni pana sana mheshimiwa Rais
na inahitaji busara kubwa na
mikakati mizito katika
kulishughulikia” akasema
Mark Piller
“Mark kauli yako ni
uoga.Siogopi kuipeleka nchi
vitani ili kuisambaratisha
Iran.Marekani si taifa la
kutolewa vitisho na taifa dogo
na dhaifu kama Iran !
“Mheshimiwa Rais
ninazungumza kama kachero
mbobezi.Kabla ya kufanya
maamuzi yoyote tunahitaji
kwanza kujiridhisha kuhusu
uwezo wa Iran kijeshi na aina
ya silaha ilizonazo.Tunahitaji
kujiridhisha kuhusu madai
hayo ya Iran kuwa na
makombora ya masafa
marefu.Tunahitaji kujiridhisha
kuhusu uwezo wake wa
kutengeneza bomu la
nyuklia.Tunahit………”
“Mark Piller ! akasema
Rais William na kumkatisha
Mark
“Umefanya kazi CIA
karibu nusu ya umri wako na
kwa muda huo wote mmekuwa
mkihangaika kupata taarifa
kuhusu mfumo wa
makombora na silaha za Iran
bila mafanikio.Itapita miaka
mingapi ili tuweze kupata
taarifa hizo za silaha za Iran?
Kama marais waliopita
walivumilia mimi sina
uvumilivu huo.Nataka
nilimalize suala hili.Iran awe
na makombora makubwa au
madogo lazima atandikwe !
akaendelea kusisitiza William
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo muhimu naomba
nikueleze” akasema Mark
Piller
“Mark tunazungumzia
suala la Iran na
tutakapomaliza ndipo
utanieleza hilo unalotaka
kunieleza.Nataka mimi na
wewe tufike muafaka kwanza
kuhusu suala hili la Iran kabla
sijaomba ridhaa ya bunge !
“Mheshimiwa Rais
ninachotaka kukwambia ni
kuhusiana na suala hilo hilo la
Iran” akasema Mark na Rais
William aliyekuwa amesimama
akaketi
“Nini unataka kunieleza?
“Nimekuwa nikiandaa
mpango wa siri wa namna
tutakavyoweza kulishughulikia
suala hili la Iran” akasema
Mark
“Unaandaa mpango wa siri
? Akauliza William akionekana
kushangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Sikuwahi kukwambia
suala hilo kwani maandalizi
yake hayakuwa yamekamilika
lakini kwa hapa tulipofika
inabidi nikueleze ukweli ili
mimi nawe tuwe katika
ukurasa mmoja.”
“Nakusikiliza Mark”
akasema William
“Kabla ya kukueleza
kuhusu mpango huo kuna
jambo ambalo nataka
ulifahamu ambalo naamini
hulijui ila halitakufurahisha”
“Nini unataka kunieleza
Mark? Akauliza
William.Ukapita ukimya mfupi
Mark akitafakari namna ya
kuanza kumweleza Rais kisha
akasema
“Kwa muda mrefu
Marekani tumekuwa
tunashirikiana na makundi
kadhaa ya kigaidi katika
mipango mbali mbali yenye
maslahi kwa
Marekani.Tumefanya hivyo
katika nchi mbali mbali kama
vile..” Mark akanyamaza baada
ya Rais William kuhamaki
“Kushirikiana na makundi
ya kigaidi?akauliza William
kwa mshangao
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
akajibu Mark
“Marekani haiwezi
kushirikiana na magaidi hata
siku moja.Tumekuwa vinara
katika kupiga vita ugaidi
duniani.Ni kwa juhudi hizo za
kupamba na ugaidi
tulifanikiwa kumuua Osama
bin Laden kiongozi mkuu wa
Alqaeda kundi la kigaidi
lililokuwa hatari
duniani.Tumeendelea pia
kuvisambaratisha vikundi
mbali mbali vya kigaidi
sehemu mbali mbali
duniani.Nashangaa
unaponiambia kwamba
Marekani tunashirikiana na
magaidi !
“Mheshimiwa Rais, ni
kweli tunashirikiana na
makundi ya kigaidi lakini hili
ni suala la ndani mno na la siri
kubwa.Hata marais waliopo
madarakani huwa
hawafahamishwi jambo hili na
hawapaswi kulifahamu.Kwa
ufupi tu ni kwamba kuna
kitengo maalum cha siri ndani
ya CIA ambacho
kinashughulikia mahusiano na
mashirikiano na makundi ya
kigaidi kwa maslahi ya
Marekani.Kwa muda mrefu
sasa Marekani tumekuwa
tukivifadhili kwa pesa na
silaha vikundi mbali mbali vya
kigaidi ambavyo vimekuwa
vikitekeleza mashambulio ya
kigaidi sehemu mbali mbali
duniani kwa maslahi ya
Marekani”
“Mungu wangu ! akasema
William akimtazama Mark
Piller kwa macho ya woga
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokueleza kwamba jambo
hili ni la siri kubwa.Labda kwa
kukupa mfano ni kwamba
tumekuwa tukifadhili
operesheni mbali mbali za
kundi la kigaidi la IS sehemu
mbali mbali duniani na moja
kati ya operesheni ambazo
tumetumia kundi la IS ni
katika machafuko
yanayoendelea Afrika
Mashariki hivi sasa” akasema
Mark na Rais William
akasimama
“Machafuko ya Afrika
mashariki yameratibiwa na
Marekani kwa kuwatumia IS?!
Rais William akashangaa
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Ni mipango ya Marekani”
akasema Mark na Rais William
akasimama akamtazama Mark
kwa mshangao mkubwa
“Mark naomba uniambie
hiki unachonieleza si cha
kweli” akasema William
“Mheshimiwa Rais
ninachokueleza ni ukweli
mtupu na jambo hili lina
maslahi makubwa kwa
Marekani” akasema Mark
“Mark watu wanakufa
kama kuku Afrika Mashariki
hadi tumelazimika kutuma
vikosi vyetu kwenda kusaidia
kurejesha amani.Dunia
inashuhudia machafuko
makubwa kabisa ya kidini
kuwahi kutokea halafu
unaniambia kwamba ni kwa
maslahi ya Marekan…...”
“Mheshimiwa Rais !
akasema Mark na kumkatisha
Rais William.
“Kinachoendelea hivi sasa
Afrika Mashariki kina maslahi
makubwa kwa
Marekani.Tazama bei ya
mafuta ilivyopanda katika soko
la dunia baada ya nchi
wazalishaji wa mafuta kuweka
mgomo baridi na kuzalisha
kiwango kidogo cha mafuta
kuliko mahitaji ya dunia.Hii
imepelekea akiba yetu ya
mafuta kuanza kupungua na
wakati huo huo tuna migogoro
na nchi nyingi ambazo ni
wazalishaji wakubwa wa
mafuta duniani.Hatuna
mahusiano mazuri na
Venezuela,Mashirikiano yetu
na Saudi Arabia yametetereka
pia,Iran ambao nao ni
wazalishaji wakubwa wa
mafuta ni maadui zetu,Iraq
pia hatupati mafuta ya kutosha
kwani serikali iliyoko
madarakani hivi sasa haitaki
mashirikiano na
Marekani.Nchi nyingine kama
Urusi ambayo unafahamu
mahusiano yetu nao.Nchi
kamaLibya ambao wanashika
nafasi ya tisa kwa akiba kubwa
ya mafuta nako
kumechafuka.Kwa ujumla
mahusiano yetu na nchi
wazalishaji wa mafuta duniani
si mazuri na mafuta yetu hapa
nchini hayatutoshi hivyo kwa
namna yoyote ile tunahitaji
kuongeza akiba yetu ya mafuta
na Afrika Mashariki kuna kiasi
kikubwa cha mafuta.Nchi ya
Uganda inakadiriwa kuwa na
mafuta mengi zaidi kuliko nchi
zote katika bara la Afrika hivyo
mipango yetu kuhakikisha
tunapata mafuta kutoka
Uganda” akasema Mark Piller
“Mafuta? ! akauliza
William kwa hasira
“Mafuta yana thamani
kuliko uhai wa watu ?
Sikutegemea kabisa kama
Mark unaweza ukashiriki
katika jambo hili ovu !
akasikitika Rais William
“Mheshimiwa Rais mafuta
ni uchumi.Kuna mgomo baridi
kwa wazalishaji wa mafuta
duniani.Hizi ni njama za
wapinzani wetu dhidi ya
uchumi wetu.Lazima tutumie
kila njia kupata mafuta ndiyo
maana tumeyafuata Afrika
Mashariki.Mheshimiwa Rais
yawezekana haya
tunayoyafanya yasionekana
sawa lakini ni kwa ajili ya nchi
yetu.Marekani lazima iendelee
kuwa taifa kubwa lenye
uchumi mkubwa kuzidi yote
duniani hivyo kila aina ya
mbinu lazima itumike katika
kuhakikisha hilo linatimia”
akasema Mark
“Siamini kama ni wewe
kweli Mark unayezungumza
haya” akasema Rais William
“Mheshimiwa Rais,haya
yote yanafanyika kwa maslahi
ya Marek…….”
“Hata kama ni kwa
maslahi ya Marekani
hatukupaswa kusababisha
machafuko yale yanayoendelea
Afrika mashariki.Ule ni
unyama uliovuka mipaka ya
ubinadamu.Maiti za watu
zimesambaa mitaani huku sisi
tukifaidika kwa mafuta
ambayo Mungu amewajalia
wenzetu.Hili haliwezekani na
siwezi kulifumbia
macho.Lazima nichukue hatua
kalisana kwako na kwa
wenzako wote mlioshirikiana
kuandaa unyama wa namna
hii Afrika Mashariki na
kwingineko duniani ambako
mmekwisha fanya !! akafoka
William
“Mheshimiwa Rais
usithubutu kufanya chochote
kuhusiana na jambo
hili.Hukupaswa kulifahamu
suala hili lakini kwa kuwa u
mtu wangu wa karibu
nimeamua kukueleza kile
kinachoendelea lakini kwa
kwaida Rais hapaswi kabisa
kufahamu chochote kuhusiana
na mambo haya nyeti mno kwa
nchi” akasema Mark
“Mark huwezi ukanipangia
nini cha kufanya.Mimi ni Rais
wa Marekani na nitafanya kila
niwezalo kuhakikisha
ninakisambaratisha kikundi
hicho cha wauaji ndani ya
CIA.Siwezi kukubali
wakaendelea na haya
wanayoyafanya !
“Mheshimiwa Rais
narudia tena kukuonya
usithubutu kufanya
chochote.Utaendelea kuufunga
mdomo wako kama vile
hufahamu chochote
kinachoendelea !
“Mtanifanya nini wewe na
wenzako? Akauliza Rais
William
“Utauawa ! akasema Mark
na ukimya ukapita.William
Washington alionyesha woga
kwa kauli ile ya makamu wake
Mark Piller
“Mheshimiwa Rais
nakushauri fuata kile
ninachokuelekeza.Ukienda
kinyume chake basi sote
maisha yetu yatakuwa
hatarini”
“Kwa nini umenieleza
jambo hili Mark wakati
ukifahamu kuwa sipaswi kujua
chochote? Akauliza Rais
William
“Ni kwa sababu kuna
mpango mkubwa unaoendelea
kuhusu Iran ambao nataka
uufahamu ili usiendelee na
mipango yako ya kuivamia
kijeshi Iran hadi mpango huo
utakapokuwa umekamilika”
“Mpango gani
Mark?akauliza Rais William
akionekana kuanza kupunguza
hasira alizokuwa nazo
“Nitakurejesha kwanza
Afrika Mashariki.Mapinduzi
yale yaliyofanywa na jeshi la
Uganda yaliyomuondoa
madarakani Rais Jenerali
Akiki Rwamirama tuliyapanga
sisi tukishirikiana na Rais wa
Tanzania”
“Tanzania pia walishiriki
katika mapinduzi yale?!
Akauliza Rais William
“Kutokana na
mashirikiano yetu na IS
tuliweza kupata taarifa
kuhusiana na mpango
ulioshindwa kufanikiwa wa
kuwaua marais wa Tanzania
na jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo kwa bomu la kujitoa
muhanga.Katika mpango huo
Jenerali Akiki pia
alishiriki.Baada ya kupata
taarifa hizo nilimtuma
mjumbe maalum kwa Rais wa
Tanzania akazungumza naye
kuhusu kumuondoa
madarakani Rais Akiki kwani
tuliamini lazima atakuwa na
hasira naye na ndipo
ukaandaliwa mpango wa
mapinduzi” akasema Mark
“Rais wa Tanzania naye
alikubali yatokee haya
yanaoendelea katika nchi
yake? Ni rais wa namna gani
huyu ambaye anakubali kuona
raia wake wakiuana namna
ile? Akauliza Rais William kwa
ukali
“Mpango wetu na
Tanzania ulikuwa ni
kumuondoa Jenerali Akiki
madarakani na kuuweka
utawala mpya.Baada ya
mpango huo kukamilika ndipo
tuliandaa haya machafuko
yanayoendelea hivi
sasa.Tulipanga kuanzisha
vurugu nchini Uganda ili
kuilazimisha serikali mpya ya
kijeshi kutumia nguvu kubwa
kuzima vurugu hizo na
kusababisha umwagikaji
mkubwa wa damu hali ambayo
ingepelekea kujengwa kwa
chuki kubwa kati ya serikali na
wananchi.Vurugu hizo
zingekuwa kubwa na hivyo
kuilazimisha Marekani
kupeleka vikosi vyake Uganda
na hapo ndipo tungepata
nafasi ya kudhibiti visima vya
mafuta na kuchukua kiasi cha
mafuta tunachokihitaji.Ili
kulifanikisha hilo tulihitaji
msaada wa Jenerali
Akiki.Haikuwa rahis kumfanya
jenerali Akiki akubali
kushirikiana nasi hadi
tulipotengeneza ajali ambayo
iliripotiwa kwamba familia
nzima ya Jenerali Akiki
waliokuwa wanaelekea Dar es
salaam walikoomba hifadhi
baada ya kupinduliwa na jeshi
walifariki”
“Subiri kidogo
Mark.Umesema mlitengeneza
ajali ambayo ilisadikisha watu
kuwa familia yote ya Akiki
walifariki katika ajali hiyo.Nini
unakimaanisha? akauliza
William
“Mheshimiwa Rais,familia
ya Jenerali Akiki iko salama na
hawakufariki katika ile ajali
kama ilivyodaiwa.Ajali ile
ulikuwa ni mchezo ili kumpa
hasira jenerali Akiki na
kumfanya akubaliane na
mpango wetu kwa nia ya
kulipiza kisasi kwa wale
walioua familia yake” akasema
Mark Piller na Willim
akaendelea kumtazama kwa
macho ya mshangao
“Mark siamini kama haya
maneno yanatoka katika
kinywa chako.Iko wapi familia
ya Akiki hivi sasa? Miili ile
iliyosafirishwa katika
majeneza kwenda Uganda ni
miili ya nani? Akauliza Rais
William
“Mheshimiwa Rais familia
ya Akiki kwa sasa iko sehemu
salama katika nchi Fulani
wakiishi kwa amani wakiwa
chini ya uangalizi wa
CIA.Wako salama kabisa
wanatunzwa vizuri na
wanapata kila
wanachokihitaji.Katika yale
masanduku kulikuwa na miili
lakini haikuwa ya familia ya
Akiki.Mheshimiwa Rais jambo
hili limefanywa kitaalamu sana
kiasi cha kutoweza kufahamika
hadi leo hii ninapokueleza”
“Dah ! akasema Rais
William halafu akainamisha
kichwa akafikiri kwa muda
kisha akamtazama Mark Piller
na kusema
“Mark ninajaribu
kuiaminisha akili yangu
kwamba ni wewe ninaye
kufahamu ndiye unanieleza
haya au ni Mark mwingine”
“Ni mimi mheshimiwa
Rais.Najua haya niliyokueleza
yamekustua sana lakini
naomba usistuke kwani yote ni
mipango kwa ajili ya nchi yetu”
akasema Mark na kunyamaza
kidogo
“Baada ya kumleta Akiki
hapa Marekani nilizungumza
naye akakubali kushirikiana
nasi kuanzisha vurugu Uganda
na akashauri njia pekee ya
kuweza kuleta machafuko
nchini Uganda ni kwa kutumia
dini.Alishauri kama tukiweza
kuwafarakanisha waumini wa
dini ya kikristu na kiislamu
lazima machafuko makubwa
yatatokea.Akiki alikwenda
mbali zaidi akashauri kwamba
kama tunataka kuchukua
mafuta basi machafuko ya
Uganda pekee hayataweza
kutusaidia bali tunahitaji
kueneza machafuko hayo hadi
nchini Tanzania kwani bomba
la mafuta linatoka Uganda
hadi Tanga nchini Tanzania
ambako ndiko meli zetu
zingeweza kupakia
mafuta.Tuliuchukua ushauri
huo na kuanzia hapo
tuliwahitaji IS ili waweze
kuanzisha choko choko za
kidini nchini Uganda na
Tanzania.Vile vile kwa msaada
wa Akiki tuliweza kuwapata
mwanasiasa mmoja wa
Uganda na mwingine wa
Tanzania ambao wangeweza
kuchochea vurugu hizo katika
nchi zao na wanasiasa hao
pamoja na wale viongozi wa
dini kwa sasa wako hapa
Marekani.Tulikubaliana baada
ya vurugu hizo kuanza
watakuwa wameimaliza kazi
yao na watakuja kuishi
Marekani.IS walifanya mauaji
ya viongozi wa dini na
kusababisha hasira na chuki
kubwa miongoni mwa
waumini wa dini hizo na Yule
mwanasiasa wa Uganda
akawachochea viongozi wa
dini ya kikristu kuanzisha
mashambulizi dhidi ya
nyumba za ibada za waislamu
na hapo ndipo machafuko
yalipoanzia.Vurugu zilipoenea
Uganda tulihamia pia Tanga
Tanzania ambako nako vurugu
zikaenea na kusambaa katika
sehemu mbali mbali za
Tanzania.Mheshimiwa Rais
hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi
tukafanikiwa kupeleka vikosi
vyetu Afrika Mashariki na sasa
meli zetu zimepanga foleni
katika bandari ya Tanga nchini
Tanzania zinapakia mafuta na
hifadhi yetu ya mafuta
inaongezeka.Hatuna tena
sababu ya kusumbuka na
mafuta ya kutoka Mashariki ya
kati.Hadi vurug hizi
zitakjapomalizika tutakuwa na
akiba kubwa sana ya
mafuta.Pima mwenyewe
mheshimiwa Rais je hiki
kilichofanyika kina maslahi
kwa nchi yetu au hakina?
Akauliza Mark Piller na Rais
Wiliam akavuta pumzi ndefu
“Mark mlichokifanya kweli
kina maslahi makubwa kwa
nchi yetu kwani tunahitaji
sana mafuta lakini tatizo ni
njia mliyotumia.Tumemwaga
damu za watu kwa ajili ya
kujipatia mafuta.Machoni pa
Mungu hii si sawa hata
kidogo” akasema William
“Nakubali mheshimiwa
Rais lakini tumekuwa
tukifanya hivi kila mara na
hakukuwa na namna nyingine
ya kufanya kuweza kujipatia
mafuta zaidi ya kutumia njia
hii” akasema Mark Piller
“Kwa nini mkaniweka
kando kuhusiana na masuala
haya?Kama si wewe kuamua
kunieleza leo hii
nisingefahamu chochote
kuhusu kile
kinachoendelea.Niliposhauriw
a tupeleke vikosi vyetu Afrika
mashariki niliamini ni kwa nia
njema ya kuzuia mauji
kuendelea kumbe ni mpango
umetengenzwa ili tukachukue
mafuta”
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokueleza awali kwamba
mambo haya yanafanywa kwa
siri kubwa sana na Rais wa
nchi hatakiwi kabisa
kufahamu kitu chochote na
hata mimi kukueleza
nimevunja kanuni zetu kwani
iwapo nitagundulika nitauawa
hivyo ni jukumu lako kuufunga
mdomo wako ili mimi na wewe
tuendelee kuwa salama”
akasema Mark Piller na
ukimya ukatawala.
“Mheshimiwa Rais !
akasema Mark Piller na Rais
William aliyekuwa
ameinamisha kichwa akainua
kichwa akamtazama
“Katika mpango huu
unaoendelea Afrika Mashariki
kuna mpango mwingine
umezaliwa ndani yake ambao
nao una manufaa makubwa
sana ambao unahusiana na
Iran”
“Una mpango gani kuhusu
Iran?akauliza William
“Nilikueleza awali kwamba
kwa muda mrefu tumekuwa
tukiichunguza Iran kufahamu
silaha zake bila
mafanikio.Nimekuja na
mpango mpya ambao unaweza
ukatusaidia kufahamu kuhusu
silaha za Iran na vile vile
kulipua kinu kikubwa
ambacho Iran inakitegemea
katika kurutubisha madini ya
Urani” akasema Mark Piller na
ile mikunjo katika sura ya Rais
William Washington
ikatoweka
“Nieleze kuhusu mpango
huo.Nini umekibuni? Akauliza
Rais William
“Kuna mtu ambaye
tumekuwa tukimtumia katika
mipango yote ya kufadhili
vikundi vya kigaidi ambavyo
tuna mashirikiano navyo.Mtu
huyo ni mwanamama anaitwa
Habiba Jawad.Huyu ni raia wa
Saudi Arabia.Mume wake
ndiye tuliyekuwa tukimtumia
katika kazi hiyo lakini baadae
alionyesha mabadiliko na
tukalazimika kumuua.Baada
ya kuuawa mkewe akarithi
utajiri wote na akaendelea
kuifanya ile kazi aliyokuwa
anaifanya mumewe yaani
kufadhili makundi ya
kigaidi.Tulimuwezesha kimtaji
na utajiri wake ni mkubwa
sana.Ni mmoja kati ya
mabilionea wa Saudi Arabia na
mwanamama mwenye
heshima kubwa.Toka
alipochukua jukumu hili
amelifanya kwa ufanisi
mkubwa.Mpaka sasa yeye
ndiye anayetambulika kama
mfadhili mkuu wa kundi la IS
na makundi mengine madogo
madogo ya kipalestina
yanayopigana na serikali ya
Israel.Ni kwa sababu yake hadi
leo dunia haifahamu kama
Marekani ndio wafadhili
wakuu wa kundi la IS na
itabaki hivyo.Hata ndani ya IS
ni watu wachache tu
wanaolifahamu hilo”
“Sifahamu hayo yote
unayonieleza Mark”akasema
Rais William
“Hupaswi kuyafahamu
mheshimiwa Rais.Si wewe tu
bali rais yeyote wa Marekani
hapaswi kuyafahamu
haya”akasema Mark Piller
“Mheshimiwa Rais,Habiba
Jawad anakuja
Marekani.Ananiletea mtu
mmoja ambaye amekubuhu
katika masuala ya ugaidi.Mtu
huyo tutamtuma Iran”
“Sijakuelewa
Mark.Tutamtumaje gaidi
kwenda Iran?Tunamtuma
akafanye nini?
“Gaidi huyo ambaye
Habiba anakuja naye ndiye
atakayekwenda Iran
kuchunguza kuhusu silaha za
Iran na mfumo wake wa
makombora na vile vile
kuharibu kinu kikubwa
ambacho Iran inakitegemea
katika urutubishaji wa madini
ya Urani” akasema Mark na
Rais William akajikuta akitoa
kicheko
“Sikupaswa kucheka lakini
Mark umenifanya nicheke.Kwa
nini umtume gaidi Iran badala
ya majasusi wetu? Magaidi
hawana mafunzo yoyote wao
wanachofahamu ni kuua
tu.Mpango huo ni wa chini
sana kufanywa na taifa kubwa
kama la Marekani lenye
maelfu ya majasusi wenye
ujuzi wa hali ya juu mno.Tuna
shirika kubwa la ujasusi kuliko
yote duniani.Tuwatumie hao
kuliko kumtuma gaidi
akafanye kazi kwa niaba
yetu.Huu ni mpango wa aibu”
akasema Rais William
“Mheshimiwa
Rais,nimekuwa ndani ya CIA
kwa muda mrefu.Hakuna kitu
ambacho kinaumiza vichwa
vya watu wa CIA kama suala la
Iran na Korea
Kaskazini.Pamoja na kuwa na
majasusi wa kiwango cha juu
mno bado mpaka leo
hatujafanikiwa kufahamu
kuhusu mfumo wa
makombora wa Iran au silaha
inazomiliki.Na hili ndilo
ambalo limeleta ugumu mpaka
leo tunasita kuitandika Iran
kijeshi kwani hatuna uhakika
yawezakana akawa kweli
anamiliki silaha za
maangamizi makubwa kama
wanavyodai.Kwa kuwa
majasusi wetu wameshindwa
tunataka kujaribu njia ya pili
ambayo ni kumtumia gaidi”
akasema Mark Piller
“Hiki ni kichekesho
Mark.Gaidi anawezaje
akaingia Iran na kufanya
uchunguzi kuhusu silaha zake?
“Mpango uko hivi
mheshimiwa Rais” akasema
Mark Piller na kunyamaza
akanywa maji kulainisha koo.
“Gaidi huyo tutampeleka
Afrika Mashariki ambako
atalipua ubalozi wetu jijini Dar
es salaam”
“Kulipua ubalozi wa
Marekani ?! William
akahamaki
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Hilo ni jambo
lisilowezekana
kabisa.Hatuwezi kumtuma
mtu akalipue ubalozi wetu na
kuua watu wetu ! akasema kwa
ukali Rais William
“Tayari tumekwisha fanya
hivyo jijini Kampala
mheshimiwa Rais.Ubalozi
wetu kule ulivamiwa na
kuchmwa moto ule ulikuwa ni
mpango maalum umepangwa
ili kuwafanya wamarekani
wakubaliane na hatua ya
kupeleka vikosi vyetu Uganda”
akasema Mark Piller
“Mungu wangu ! akasema
William akimtazama Mark
Piller kana kwamba ni mara ya
kwanza anakutana naye
“Mheshimiwa Rais”
akaendelea Mark
“Tutaulipua ubalozi wetu
jijini Dar es salaam kisha
tutamkamata huyo gaidi na
kumpeleka mafichoni”
akasema Mark na kunyamaza
kidogo
“Miaka sita iliyopita ndege
ya shirika la ndege la Qatar
ikitokea Moscow Urusi
kuelekea Tehran ikiwa na
abiria mia moja ishirini na
saba ndani yake ililazimika
kutua kwa dharura katika
uwanja wa ndege wa Almaty
nchini Kazakhstan kufuatia
hitilafu iliyojitokeza katika
mojawapo ya injini zake.Baada
ya kutua abiria wote
walishushwa ndegeni na
kupelekwa hospitali kwa
uchunguzi wa afya zao kufuatia
wengi wa abiria kupatwa na
mstuko mkubwa kutokana na
tukio lile.Mheshimiwa Rais sisi
ndio tuliotengeneza tukio lile
hadi ndege ikatua nchini
Kazakhstan.Tulikuwa na
sababu maalum” akasema
Mark na kunyamaza kidogo
halafu akaendelea.
“Miongoni mwa abiria wa
ndege ile,walikuwemo
wanasayansi sita wa Iran
wakitokea nchini Urusi
ambako walikwenda kupatiwa
mafunzo ya siri namna ya
kutengeneza bomu la
nyuklia.Tulizipata taarifa hizo
na kutengeneza mpango ule
kisha tutakafanikiwa kuwapata
wanasayansi hao ambao
tunaendelea kuwashikilia hadi
sasa tukiendelea kuwahoji japo
hawajasema chochote”
“Wako wapi hao
wanasayansi?
‘Tunaendelea kuwashikilia
katika mojawapo ya nyumba
salama za CIA” akajibu Mark
“Gaidi tunayekusudia
kumtuma kulipua ubalozi wetu
Dar es salaam atakamatwa
baada ya kutekeleza shambulio
hilo.Kisha kamatwa atakwenda
kuunganishwa na wanasayansi
hao mahala walikofichwa na
kujenga ukaribu nao.Baada ya
kuzoeana nao atasuka mpango
wa kuwatorosha wanasayansi
hao na wakifanikiwa kutoroka
wataelekea moja kwa moja
nchini Iran.Serikali ya Iran
itakuwa na kila sababu za
kumuamini huyo gaidi kwani
kwa wakati huo dunia nzima
itakuwa ikifahamu kitu
alichokifanya yaani kulipua
ubalozi wa Marekani na Iran
watampokea kama
shujaa.Akiingia Iran ndipo
atakapoanza kuifanya kazi yetu
tuliyomtuma” akasema Mark
Piller na ukimya ukatawala
mle ndani halafu Rais William
akasema
“Mark huo unaonekana ni
mpango mzuri sana lakini
tatizo ni huyo jamaa ambaye
unataka kumtumia katika
mpango huo.Hana mafunzo ya
kijasusi na hawezi kutekeleza
vyema kazi aliyotumwa na
nina wasi wasi anaweza
akagundulika kuwa ametumwa
na Marekani na akauawa hivyo
tukakosa kila kitu”Rais
William akaonyesha wasiwasi
mkubwa
“Hata kama akigundulika
kwamba ametumwa na
Marekani tutakana tuhuma
hizo na dunia itatuelewa
kwanza mtu huyo si raia wa
Marekani na kwa wakati huo
atakuwa anajulikana kama
gaidi ambaye anatafutwa na
Marekani kwa kulipua ubalozi
wake jijini Dar es salaam na
vile vile atakuwa anatafutwa
kwa kutoroka kutoka katika
mahala alipokuwa
anashikiliwa.Kwa sababu hizo
mbili tutakuwa tumejitoa
katika jambo hilo lakini kwa
namna mpango ulivyo uhakika
wa mtu huyo kugundulika ni
mdogo sana”
“Yawezekana mkawa
mmejipanga vizuri kabisa
lakini tatizo ni uwezo wa huyo
gaidi kutekeleza mpango
mkubwa kama huu.Jambo
kama hili linahitaji jasusi
mbobezi.Tunao wengi sana
majasusi wa namna hiyo
ambao tunaweza kuwatumia
katika mpango huo.Kwa nini
tusitafute mmoja wao
tukamtumia badala ya huyo
gaidi? Sijaukataa mpango huu
lakini sikubaliani na mtu
mnayetaka kumtumia.Ni
mpango mzuri sana na kama
ungeniambia kwamba
anayekwenda kuutekeleza ni
jasusi nguli wa Marekani basi
ningekubaliana nawe kwa
asilimia mia moja lakini kwa
gaidi kwenda kutekeleza
mpango huo nashindwa
kukubaliana nawe Mark”
“Mheshimiwa
Rais,hatutaki kumtumia raia
wa Marekani katika jambo
hili.Mtu huyo ambaye Habiba
anakuja naye ni raia wa Saudi
Arabia ambao hawana
maelewano mazuri na
Iran.Endapo misheni
itashindwa kufanikiwa na mtu
huyo akakamatwa basi mzozo
utakuwa ni kati ya Iran na
Saudi Arabia sisi
hatutahusika.Kwa mujibu wa
Habiba Jawad mtu huyo
anayemleta ni mtu mahiri na
sahihi kwa kazi
hiyo.Atakapokuja hapa
tutampima na kuona uwezo
wake lakini sina wasiwasi naye
hata kidogo.Ninamuamini
Habiba Jawad.Nina uhakika
mkubwa mtu anayemleta
atakwenda kuitekeleza vyema
kazi tutakayomtuma akaifanye
Iran”
“Mark nina wasi wasi sana
kuhusu jambo hili unalotaka
kulifanya.Sijui kwa nini
ninakuwa na wasiwasi
mkubwa namna hii” akasema
Rais William
“Naomba uniamini
mheshimiwa Rais.Nina
uhakika mkubwa sana na hiki
ninachokwenda
kukifanya.Tumekuwa
tukifanya mambo kama haya
sehemu mbali mbali na
tukafanikiwa.Mheshimiwa
Rais katika haya
yanayoendeleaAfrika
Mashariki tutaua ndege wawili
kwa jiwe moja.Tunaongeza
akiba ya mafuta na vile vile
kwa mara ya kwanza
tutafanikiwa kujua aina ya
silaha ilizo nazo Iran.Haya ni
mafanikio makubwa sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mark Piller
“Mark katika suala la
mafuta japo mmetumia njia
ambayo si ya kibinadamu
lakini nataka
niwapongeze.Tunahitaji sana
mafuta na nchi za Mashariki
ya kati ambazo ni wazalishaji
wakubwa wa mafuta duniani
ziko katika mgomo baridi wa
kuzalisha mafuta kwa lengo la
kutukomoa sisi kutokana na
sera zetu za kuiunga mkono
Israel.Wamesahau kwamba
Marekani wana uwezo wa
kupata mafuta kutoka sehemu
yoyote ile wanayoitaka.Kwa
sasa mafuta kutoka Afrika
yanaendelea kumiminika
katika hifadhi zetu za
mafuta.Hongereni sana
Mark.Japo niliwekwa pembeni
katika jambo hili lakini lazima
niwapongeze.”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Mark Piller
“Kuna kitu nataka
kukiongeza hapo.Eneo hili la
ukanda wa Afrika Mashariki ni
tajiri sana.Lina utajiri mkubwa
wa madini mbali mbali
ambayo tunayahitaji mno.Kwa
mfano nchini Tanzania pekee
yanapatikana madini ya
thamani kubwa yanaitwa
Tanzanite ambayo
hayapatikani sehemu nyingine
yoyote duniani zaidi ya
Tanzania,yapo pia madini
mengine kama
dhahabu,almasi,na zaidi sana
madini ya Urani.Ukienda
Uganda kuna mafuta,ukienda
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo kuna madini mengi pia
ya thamani kubwa.Kwa ujumla
eneo hili lote limejaa
madini.Kwa kuwa tayari
tumekwisha ingia Afrika
Mashariki ni jukumu letu
kuhakikisha tunajiimarisha na
tunakwenda mbali zaidi ya
mafuta.Wekeni mikakati ya
kuhakikisha tunaongeza vikosi
zaidi Afrika Mashariki na
tunakwenda mbali zaidi kwa
kupeleka vikosi vyetu sehemu
zile zenye utajiri lakini jambo
hili lifanyike kwa ustadi na
umakini mkubwa kama
mlivyofanya katika haya
machafuko.Nataka hadi
tutakapoondoa vikosi vyetu
Afrika mashariki tuwe
tumefaidika na akiba kubwa ya
mafuta na madini mengine ya
thamani”akasema Rais
William
“Mheshimiwa Rais
ninashukuru kwa kuanza
kuelewa kile tunachokifanya
kwa ajili ya nchi yetu.Ili
tuendelee kujiimarisha na
kukaa muda mrefu zaidi Afrika
Mashariki inatulazimu
kutafuta namna ya kuongeza
machafuko katika ukanda huo
wa Afrika Mashariki.Nitakaa
na wenzagu tuone namna ya
kufanya lakini kuna kitu
ninakifikiria ambacho
kinaweza kutupa sababu ya
kuongeza vikosi vyetu na
tukaendelea kuchota
Rasilimali” akasema Mark
Piller
“Nini unakifikiria
kuhusiana na hilo wazo langu?
Akauliza William
“Kutoka katika machafuko
haya yanayoendelea Afrika
Mashariki ninafikiria
kuanzisha kikundi cha uasi
ambacho tutakipa nguvu na
kukifadhili silaha kali ambacho
kitasambaa katika nchi za
Tanzania na Uganda.Hatuna
shida sana na nchi ya
Kenya.Shida yetu ni
Tanzania,Uganda na jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo nchi
ambazo zina utajiri
mkubwa.Kikundi hicho
ambacho kitasambaa katika
nchi hizo tatu kitawezeshwa
silaha nzito na kuendelea
kulifanya eneo la Afrika
mashari liwe ni eneo hatari na
sisi tutaongeza vikosi vyetu
Afrika Mashariki kulinda
amani.Nitazungumza na
Jenerali Akiki kuhusiana na
suala hili na tutaona nini
tukifanye lakini
nakuhakikishia mheshimiwa
Rais kwamba haya maelekezo
yako yatafanyiwa
kazi.Ninachokuomba niamini
na kila kinachoendelea
nitakujulisha lakini nakuomba
haya niliyokwambia iwe ni siri
yako asifahamu mtu mwingine
yeyote mambo haya.Narudia
kukupa angalizo mheshimiwa
Rais kwamba endapo haya
niliyokwambia yatavuja
utakuwa ni mwisho wetu.Hii
ni moja kati ya siri kubwa sana
ya nchi ya Marekani” akasema
Mark Piller
Mazungumzo yao
yalidumu kwa saa tatu kisha
wakaagana na Mark Piller
akaondoka zake.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
MAKAO MAKUU YA SNSA
Saa mbili za asubuhi
wafanyakazi wa idara ya siri ya
usalama wa ndani wa nchi
wakiwa katika ofisi yao kuu
wakiendelea na majukumu yao
katika ukumbi mkubwa
waliyaelekeza macho yao
katika runinga kubwa mbili
wakifuatilia picha kutoka
katika drone kubwa zilizokuwa
zinazunguka angani juu ya jiji
la Dar es salaam kufuatilia hali
inavyokwenda.Mitaa mingi
hata ile ambayo ilizoeleka
kuwa na msongamano
mkubwa wa watu ilikuwa
mitupu.Makundi ya watu
yakijiandaa kwa ajili ya
kuendelea na mapambano
yalionekana katika sehemu
mbali mbali za jiji.Vikosi vya
ulinzi viliendelea kufanya
doria katika baadhi ya mitaa
lakini barabara nyingi zilikuwa
zimefungwa kwa kuwekwa
mawe makubwa na kuchomwa
matairi.Katika baadhi ya picha
yalionekana majengo
yakiungua moto.Maiti za watu
zilionekana pia katika baadhi
ya mitaa.
Wakati wafanyakazi wale
wakiendelea kufuatilia picha
zile,katibu muhtasi wa Ruby
akamfuata na kumjulisha
kwamba Rais anataka
kuzungumza naye katika
simu.Haraka haraka Ruby
akaenda ofisini kwake na
kuinua mkono wa simu
“Mheshimiwa Rais
shikamoo” akasema Ruby
“Marahaba Ruby vipi
mnaendeleaje?akauliza Rais
Dr Fabian
“Tunaendelea vizuri
mheshimiwa Rais.Tunafuatilia
picha za drone kuona namna
hali ilivyo katika mitaa mbali
mbai ya jiji lakini hali bado ni
tete.Barabara nyingi
zimefungwa,majengo
yanaungua moto makundi ya
watu wanaendelea kujiandaa
kuingia mitaani katika
vurugu.Huduma hazipatikani
na maisha yanazidi kuwa
magumu” akasema Ruby
“Nimepokea taarifa
asubuhi hii kutoka kwa mkuu
wa jeshi la polisi kwamba bado
hali ni tete huko mitaani.Hata
hivyo nimekupigia kukujulisha
kwamba ndani ya dakika kumi
zijazo mawasiliano ya simu
yatarejeshwa kama ulivyokuwa
umeshauri na baadae
nitalihutubia taifa ili tuone
kama inaweza ikasaidia
kupunguza vurugu hata kwa
kiasi kidogo” akasema Dr
Fabian
“Ahsante sana
mheshimiwa rais kwa
kulifanya kazi suala hili.Nina
uhakika linaweza kuwa na
matokeo mazuri na watu
wakakuelewa” akasema Ruby
“Ruby kubwa ambalo
limenifanya nitake
mawasiliano ya simu
yarejeshwe ni ili kuwawezesha
kumfuatilia Karim.Mliniambia
kwamba kukosekana kwa
mawasiliano kumewafanya
mkashindwa kumfuatilia Yule
jamaa.Mawasiliano yatarejea
muda si mrefu nataka
mumfuatilie Karimu na
kuhakikisha mnafahamu kila
kitu kuhusu yeye na jioni ya
leo nipewe taarifa kama tayari
mmemkamata au vipi”
akasema Dr Fabian
“Mheshimwia Rais
tutalifanyia kazi suala hilo na
jioni ya leo nitakujulisha kile
ambacho tutakuwa tumekipata
katika uchunguzi wetu
kuhusiana na Karim Abdallah”
akasema Ruby na kuagana na
Rais kisha akakaa katika
kompyuta yake kwa dakika
tano akafanya kazi fulani
halafu akarejea katika ule
ukumbi mkubwa ambako
wafanyakazi wa SNSA
walikuwa wanaendelea
kufuatilia picha za Drone
kujua hali ilivyo katika mitaa
mbali mbali ya jiji la Dar es
salaam.
“Naomba tusikilizane
jamani” akasema Ruby na
watu wote wakawa makini
kumsikiliza
“Toka machafuko haya
yalipoanza mawasiliano ya
simu yalikatwa kwa lengo la
kuzuia watu kutumia simu
kuhamasishana kuhusu
vurugu.Pamoja na kukata
mawasiliano ya simu lakini
bado haijasaidia kupunguza
vurugu” akanyamaza kidogo
halafu akaendelea
“Muda mfupi uliopita
nimetoka kuzungumza na
mheshimiwa Rais na
amenieleza kwamba ndani ya
dakika chache zijazo
mawasiliano ya simu
yatarejeshwa” akanyamaza
baada ya watu kushangilia
“Jana usiku tulikuwa na
mazungumzo na Rais
tukamuomba aruhusu
mawasiliano ya simu
yarejeshwe na amekubali ombi
letu hivyo ndani ya muda
mfupi mawasiliano ya simu
yatarejea.Kubwa ambalo
lilinifanya nimuombe Rais
aruhusu mawasiliano ni kwa
ajili ya kumchunguza huyu
mtu” akasema Ruby na
kubonyeza kitanza mbali na
picha ya Karim Abdallah
ikaonekana runingani
“Anaitwa Karim
Abdallah.Ni mwenyekiti wa
chama cha siasa cha TPD.Kwa
nini ameonekana katika
runinga yetu? Huyu jamaa
kabla machafuko hayajaanza
aliandika ujumbe wa
uchochezi katika ukurasa wake
wa twitter akiwataka waislamu
wa mkoa wa Tanga waungane
wakawatafute wale waliomuua
Sheikh mkuu wa mkoa huo
aliyeuawa na watu
wasiojulikana.Ujumbe huo
japo aliufuta haraka lakini
tayari ulikwisha somwa na
watu wengi.Tunajiuliza nini
sababu ya kuandika ujumbe
kama ule? Kuna wasiwasi
machafuko haya
yanayoendelea yakawa na
chembe chembe za kisiasa
ndani yake hivyo nataka
mawasiliano yatakaporejea
tuanze kumfukua huyu jamaa
kufahamu kila taarifa
zake.Tunahitaji kujua mahala
alipo,kufahamu nani
anawasiliana nao na
wanawasiliana nini,marafiki
zake ni akina nani.Kwa ujumla
nataka tufahamu kila kitu
kumuhusu huyu jamaa.Sasa
kila mmoja aende mahala pake
na tuanze kazi mara moja”
akasema Ruby kisha akaelekea
ofisini kwake akaichukua simu
yake akaiwasha tayari
mawasiliano yalikwisha rejea.
“Ahsante Mungu.Sasa kazi
inaanza”akasema Ruby
RIYADH – SAUDI ARABIA
Toka Mathew alipoondoka
na Habiba kuelekea
Marekani,Najma hakutoka
ndani.Alikuwa amejifungia
chumbani kwake akiwa na
mawazo mengi sana.Pembeni
yake kulikuwa na simu ya
Mathew pamoja na kitabu
cheusi.Aliishika simu ile na
kuitazama halafu akairusha
pembeni
“Huyu Ruby ambaye Abu
ameandika namba zake za
simu katika kitabu chake cha
kumbu kumbu ni nani?Kwa
nini nilipomuuliza Ruby ni
nani alibadilika na haraka
haraka akaninyang’anya kile
kitabu? Akawaza Najma.
“Katika simu yake amepiga
namba za Ruby zaidi ya mara
tatu lakini kwa bahati mbaya
simu hiyo haikuwa
ikipatikana.Tatizo langu nina
wivu mbaya mno na hii ndiyo
sababu kubwa iliyonifanya
nikawa sitaki kuingia katika
masuala ya
mahusiano.Ninampenda sana
Abu Zalawi na sitaki awe na
mwanamke mwingine zaidi
yangu” akaendelea kuwaza
Najma
“Najilaumu sana kwa
kuingia katika mahusiano na
Abu Zalawi bila kuifahamu
historia yake ametoka wapi na
maisha yake yalikuwaje huko
alikotoka.Je alikuwa na mke
au na familia?Hata yeye
mwenyewe hajawahi kunieleza
chochote kuhusiana na
historia yake” Najma akainuka
kitandani na kukaa
“Lakini kwa nini niteseke
wakati namba za simu za huyo
Ruby ninazo? Kwa nini
nisimpigie kuufahamu
ukweli?Yawezekana akawa ni
rafiki yake au ni mtu ambaye
waliwahi kuifanya kazi
wote.Nimepata wivu kwa
sababu Abu hajawahi
kuonyesha kumafuta simuni
mwanamke kama alivyofanya
kwa Ruby jana” Najma
akaendelea kutafakari
“Hapana siwezi kuendelea
kuumia.Ngoja nimpigie simu
huyu Ruby nimfahamu vizuri
na nifahamu ana mahusiano
gani na Abu” akawaza Najma
na kubonyeza namba zile za
Ruby akapiga simu ikaanza
kuita akahisi kama mwili
unamtetemeka.
“Simu yake inaita”
akawaza huku akihisi woga
kwa mbali
“Hallow ! ikasema sauti ya
mwanamke upande wa pili wa
simu na Najma akasita kujibu
“Hallow ! ikaita tena sauti
ile
“Hallow ! akasema Najma
kwa lugha ya kiingereza
“Habari yako?akauliza
Yule mwanamke upande wa
pili
“Nzuri habari yako?
“Nzuri.Nazungumza na
nani kutokea wapi?
“Naitwa Najma niko
Riyadh Saudi Arabia”
“Riyadh ! Yule mwanamke
akaonyesha mshangao
“Ndiyo.Wewe uko
wapi?akauliza Najma na Yule
mwanamke akasita kidogo
“Hallow ! Najma akaita
“Najma
umenifahamuje?Umepata
wapi namba zangu za simu?
“Unamfahamu Abu
Zalawi? Akauliza Najma
“Abu Zalawi?yule
mwanamke akashangaa
“Ndiyo unamfahamu?
Najma akauliza
“Hapana simfahamu.Ni
nani huyo mtu?
“Ni mume wangu lakini
ana namba zako katika kitabu
chake cha kumbukumbu za
mawasiliano na jana alikupigia
simu mara tatu lakini simu
yako haikuwa ikipatikana”
akasema Najma
“Utanisamehe dada yangu
lakini simfahamu mtu mwenye
jina hilo na wala sijawahi kuwa
na rafiki mwenye jina hilo la
Abu Zalawi.Ni mara ya kwanza
ninalisikia”
“Abu ameandika namba
zako za simu katika kitabu
chake na alikupigia alionekana
ana jambo la muhimu sana
anataka kukueleza.Kwani
wewe si Ruby?akauliza Najma
na mwanamke wa upande wa
pili akasita
“Hallow? Najma akaita
“Nakuuliza kwani wewe si
Ruby?Najma akauliza tena
“Naweza kuzungumza na
huyo Abu Zalawi ” akauliza
Yule mwanamke
“Abu Zalawi amesafiri
Alfajiri ya leo.Naomba
tafadhali kama akikupigia tena
simu usimwambie chochote
kuhusu mimi kukupigia
simu.Ahsante sana nimefurahi
kuzungumza nawe japo
umekataa kunitajia jina lako”
akasema Najma na kukata
simu akashusha pumzi na
kutazama namba zile halafu
akaigiza namba za mwanzo
katika kompyuta yake ili kujua
namba zile ni za nchi gani na
majibu yakaja kuwa ni
Tanzania.
“Tanzania ! akasema
Najma na kuvuta pumzi ndefu
“Niliona kwa macho yangu
mawili katika kitabu chake
ameandika jina Ruby.Iweje
huyu mwanamke niliyempigia
ambaye japo amekataa
kunitajia jina lake lakini
naamini ni Ruby akane
kumfahamu Abu? Akajiuliza
Najma
“Au Abu ana jina lingine
anatumia tofauti na Abu
Zalawi?Amefahamiana vipi na
uyu mwanamke wa Tanzania?”
akawaza Najma
“Ninahitaji kumfahamu
Abu Zalawi kiundani na mtu
pekee ambaye anaweza
akanieleza kila kitu kuhusiana
na huyu mtu ni
mama.Atakaporejea katika
hiyo safari waliyokwenda
nitamtaka anieleze ukweli
kuhusiana na Abu Zalawi
kwani kuna mambo yameanza
kunipa mashaka sana
kuhusiana na huyu mtu.Mama
amefahamiana vipi na
Abu?Kuna kitu gani
wanakipanga? Nitafahamu kila
kitu watakaporejea” akawaza
Najma
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliendelea kuishikilia
simu yake baada ya
kuzungumza na Najma.
“Abu Zalawi ! akajiuliza
“Ni nani huyo mtu?
Sijawahi kuwa na rafiki yeyote
mwenye jina hilo la Abu Zalawi
wala sina rafiki yeyote Saudi
Arabia sasa huyu mtu
amenifahamuje hadi ana
namba zangu tena
ninazotumia hapa Tanzania ?
Sijawahi kumpa namba za
simu ninazotumia Tanzania
mtu wangu yeyote wa nje ya
nchi,huyu Abu Zalawi
amezpata wapi?” akajiuliza
Ruby
“Au labda Uingereza
wamekwisha gundua kwamba
sikufariki katika ile ajali ya
ndege na sasa wanaanza
kunichunguza ili wapate
uhakika kama ni mimi?
Akaendelea kujiuliza
“Kwa nini nisimpigie simu
Najma na kumtaka anitumie
picha ya huyo Abu Zalawi
nimuone kama ninamfahamu?
Nadhani hilo litakuwa jambo
jema” akawaza na kuchukua
simu akampigia Najma kwa
kutumia zile namba
alizompigia.
“Hallow” akasema Najma
baada ya kupokea
“Najma samahani sana
kwa usumbufu,Unaweza
ukanitumia picha ya Abu
Zalawi nimuone kama ni mtu
ninayemfahamu?akauliza
Ruby
“Sawa ninakutumia muda
si mrefu” akasema Najma na
kupekua simu ya Mathew
lakini hakukuwa na picha hata
moja ya Mathew.Akapekua
katika simu yake lakini
hakukuwa na hata picha moja
ya Mathew akachanganyikiwa
“Haya mbona ni maajabu
makubwa.Picha zote
zimekwenda wapi? Tumepiga
picha nyingi sana tukiwa
katika mapumziko.Ni maelfu
ya picha lakini hakuna hata
picha moja na sielewi
zimekwenda wapi” akawaza na
kuchukua kamera yake
ambayo nayo pia alikuwa
anaitumia wakati wakiwa
mapumzikoni lakini hakukuwa
na picha hata moja.
“Mungu wangu haya
mbona maajabu? Akasema
kwa mshangao na kuchukua
kompyuta yake mpakato na
haraka haraka akafungua
sehemu ya kuhifadhi picha
ambako alikuwa anahifadhi
picha kila pale kadi ya
kuhifadhia kumbu kumbu
ilipojaa lakini akakutana na
kioja kwani zile picha zote
ambazo walipiga katika
mapumziko hazikuwepo.
“Jamani haya ni mambo
gani yanatokea?Tumepiga
maelfu ya picha kwa miezi
mitatu na hata jana nilikuwa
nazitazama nikichagua zile
nzuri kwa ajili ya kuweka
kumbu kumbu lakini ajabu leo
hii hakuna hata picha
moja.Hakuna picha katika
simu yangu,ya Abu,katika
kamera na hata katika
kompyuta.Zimekwenda
wapi?Nani amezifuta na kwa
nini?akajiuliza na mara simu
yake ikaita tena akazitazama
zile namba ni Yule mwanadada
aliyempigia kutoka Tanzania
“Nitamjibuje huyu dada?
Ataniona mwongo” akawaza
Najma halafu akaipokea ile
simu
“Najma samahani
umeipata picha hiyo ya Abu
Zalawi?akauliza
“Hapana
bado.Nitakutumia baadae
kidogo naomba unisubiri”
akasema Najma na kukata
simu.
“Haya ni maajabu ambayo
sijawahi kuyashuhudia”
akawaza na kuendelea
kupekua kompyuta yake kama
angeweza kupata picha zile
akini hakukuwa na picha
yoyote
“Humu ndani hakuna mtu
mwingine yeyote aliyeingia
zaidi yetu mimi na Abu.Kama
angekuwa mtu mwingine
ameingia ningehisi labda ndiye
aliyefuta picha hizo lakini
hakuna tulikuwa humu watu
wawili pekee.Ningeweza
kusema ni kirusi labda
kimefuta picha hizo lakini
picha zilizofutwa ni zile
nilizopiga na Abu pekee
nyingine zote zipo” akawaza na
kushika kidevuni
“Hapa kuna kitu
kinaendelea.Picha zile
hazijajifuta zenyewe bali
zimefutwa kwa sababu
maalum na aliyezifuta lazima
atakuwa ni Abu.Kwa nini
akafanya hivi? Amefuta muda
gani hizo picha? Najma
akapandwa na hasira
“Huyu Abu Zalawi ni nani
hasa?Mbona anaanza kunipa
mashaka? Nadhani nahitaji
kumfahamu kwa undani zaidi
ni mtu wa aina gani
huyu.Yawezekana
ninavyomfahamu sivyo alivyo”
akaendelea kuwaza Najma.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 2 : EPISODE 3
Timu ya watu wa SNSA
walioko jijini Tanga iliwasili
kaika nyumba ambayo kumbu
kumbu zinaonyesha ndiko
alipokuwa Denis Sambale
mara ya mwisho alipotumia
simu yake kwa
mawasiliano.Walipofika
mahala walipoelekezwa
walipatwa na mshangao baada
ya kukuta nyumba hiyo ikiwa
imeteketea kwa moto na
kubaki gofu.Kila
kilichokuwamo ndani ya
nyumba hiyo kiliteketea
Kwa mujibu wa uchunguzi
wa SNSA,ilibainika kwamba
mtu wa mwisho Denis
kuwasiliana naye alikuwa ni
Augustin Kawala ambaye naye
simu yake haikuwa
inapatikana.Timu ya watu wa
SNSA walielekea mahala
alipokuwapo Augustin mara ya
mwisho alipotumia simu
yake.Nyumba ilikuwa na geti
lililofungwa kufuli kwa nje
kuashiria kwamba hakukuwa
na mtu ndani.Wakavunja
kufuli na kuingia ndani ya
nyumba ile.Mara tu
walipouvunja mlango wa
sebuleni walikutana na harufu
kali ya uozo.Kwa tahadhari
kubwa wakafuatilia harufu ile
ilikotoka na kukuta katika
chumba kimoja mwanamke
mmoja akiwa amelala
kitandani akiwa tayari
ameanza kuharibika.Kifuani
alikuwa amechomwa na kisu
kikubwa.Ilionekana kulikuwa
na ugomvi kabla ya
mwanamke Yule kuuawa
kwani vitu vilitawanyika hovyo
mle chumbani.Kwa tahadhari
kubwa kiongozi wa timu ile ya
SNSA akabandika karatasi
Fulani katika mpini wa kisu na
kuibandua kisha akaimulika
kwa tochi na zikaonekana
alama za vidole zilizokuwa
katika mpini ule wa kisu.
Katika uchunguzi wao
walikuta kuna picha kadhaa
zikimuonyesha mtu aliyevaa
mavazi ya kichungaji zikiwa
zimebandika ukutani na katika
picha nyingine alionekana
mwanamke Yule aliyeuawa
akiwa na Yule mchungaji
ilikuwa ni siku ya harusi
yao.Walikusanya kila
walichoona kingeweza kuwafaa
kisha wakaondoka kurejea
katika ofisi yao.Karatasi ile
iliyokuwa na alama za vidole
kutoka katika ule mpini wa
kisu alichochomwa Yule
mwanamke waliyemkuta
katika nyumba ya Augustin
Kawala ikaingizwa katika
kompyuta na alama zile
zikatumwa ofisi kuu ya SNSA
Dar es salaam.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 2 : EPISODE 4
Katika chumba cha
mipango ofisi kuu ya SNSA
Dar es salaam,Ruby akiwa na
Gosu Gosu msaidizi wake
pamoja na viongozi kadhaa wa
idara mbali mbali zilizomo
ndani ya SNSA walikutana
kufuatia ripoti waliyoipata
kutoka kwa watu wao walioko
Tanga.
“Muda mfupi uliopita
nimepokea taarifa kutoka
Tanga.Tuliwaelekeza watu
wetu kule kumfuatilia Denis
Sambale lakini walipofika
katika nyumba ambayo
tunaamini ni makazi yake
walikuta nyumba hiyo ikiwa
imeteketea kwa moto”
akasema Ruby na
kuwaonyesha picha katika
runinga kubwa za namna
nyumba ile ilivyoteketea na
kubaki gofu
“Denis Sambale mara ya
mwisho aliwasiliana na
Augustin Kawala,watu wetu
wakamfuata huyo Augustin
ambaye naye simu yake
haipatikani na walipofika
katika nyumba ambayo
alikuwepo alipowasiliana na
Denis watu wetu wamekuta
nyumba ikiwa imefungwa
wakavunja mlango wakaingia
ndani na hiki ndicho
walichokikuta” akasema Ruby
na kuwaonyesha picha za Yule
mwanamke aliyekutwa
ameuawa kwa kuchomwa na
kisu kifuani
“Watu wetu walichukua
alama za vidole kutoka katika
mpini wa kisu alichochomwa
mwanamke huyo .Watu wa
idara ya alama wamezifanyia
kazi alama hizo na haya ndiyo
majibu waliyoyapata.Katika
alama zilizokutwa kwenye
hicho kisu kuna alama za
vidole za mtu huyu hapa”
akasema na kubonyeza kitanza
mbali na picha ikajitokeza
“Augustin Kawala.Huyu ni
mchungaji anayemiliki kanisa
la ngome ya ushindi.Katika
alama hizo pia zimekutwa
alama za mtu huyu hapa”
akasema na katika runinga
ikatokea picha ya mwanamke
“Anaitwa Paulina
Kawala.Huyu ni mke wa
Augustin Kawala.Katika picha
zilizotumwa na watu wetu wa
Tanga ipo picha inayoonyesha
Augustin na Paulina siku ya
harusi yao.Kufuatia kukutwa
kwa alama za vidole za
Augustin katika mpini wa kisu
alichochomwa Paulina
inaonyesha wazi kwamba huyu
jamaa anahusika katika mauaji
ya mke wake.Hii ndiyo hali
iliyokutwa chumbani” akasema
Ruby na kuonyesha picha za
namna vitu vilivyovurugika
chumbani.
“Inaonekana kulikuwa na
ugomvi chumbani na kisha
Paulina akachomwa kisu.Mtu
wa kwanza ambaye tunamuhisi
kuhusika na mauaji hayo ni
Augustin Kawala.Hatujui
mahala alipo na simu yake
imezimwa.Kuna kitu kimoja
ambacho naamini
mmekigundua katika zoezi hili
tulilolifanya leo.Tukianza kwa
Karim,ametoweka na hatujui
yuko wapi.Mtu wa mwisho
kuwasiliana naye ni Denis
Sambale akiwa jijini
Tanga.Huyu naye hajulikani
alipo na nyumba yake
imeteketea kwa moto.Denis
naye mtu wa mwisho
kuwasiliana naye ni Augustin
Kawala huyu naye ametoweka
hatujui alipo ila tunaamini
huyu alimuua mkewe na
akakimbia.Wote hawa
mawasiliano yao ya mwisho
yamefanywa siku ambayo
machafuko yalianza jijini
Tanga na wote simu zao
hazipatikani.Binafsi
nalazimika kuamini huu ni
mtandao ambao una malengo
Fulani na ninahisi unahusika
kwa namna moja au nyingine
na haya machafuko”
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Nilipewa orodha ya watu
ambao waliwasiliana na Karim
wiki moja kabla ya machafuko
kuanza.Katika orodha hiyo
kuna mwanasiasa mmoja wa
Uganda anaitwa Joshua
Lulangwa.Nitazungumza na
Rais ili aombe msaada kwa
mamlaka za Uganda kuweza
kupata taarifa za kuhusiana na
huyu mtu.Wakati tukisubiri
msaada huo kutoka kwa
wenzetu wa Uganda sisi
tutaendelea kuwafuatilia watu
wote walioko katika orodha hii
ya watu ambao Karim
aliwasiliana nao na
tutamfahamu kila mmoja wao
na kuchunguza kama ana
mahusiano yoyote na vurugu
hizi.Hakuna kufumba jicho
hadi pale tutakapopata chanzo
cha vurugu hizi ambazo binafsi
ninahisi wanasiasa wanaweza
kuhusika” akasema
Ruby.Tayari ni saa kumi na
mbili kasoro za jioni
akampigia simu Rais
akamjulisha kwamba
atakwenda kuonana naye jioni
ile
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Inakaribia saa saba za
mchana wakati ndege
iliyowabeba Habiba Jawad na
Mathew Mulumbi ilipowasili
katika anga la jiji la
Washington DC.Ni safari
iliyowachukua takribani saa
kumi na nne kutoka Riyadh.
“Mathew imekuwa ni
safari ndefu sana na
tunakaribia kutua lakini kuna
kitu kimoja nataka
kukufahamisha kabla ndege
haijagusa ardhi” akasema
Habiba
“Nakusikiliza mama”
“Sikupaswa kukwambia
lakini wewe ni kijana wangu
hivyo lazima nikwambie ili
ujiandae.Hawa watu
hawakuamini”
“Akina nani? akauliza
Mathew
“Hawa tunaokwenda
kuonana nao”akajibu Habiba
“Wana haki ya kuwa na
wasi wasi nami kwani
hawanifahamu na ni mara ya
kwanza tunakutana mimi na
wao hivyo hali kama hiyo
lazima itokee”akasema
Mathew
“Sikiliza
Mathew.Tutakaposhuka
watakuchukua na kwenda
kukupima.Show them who you
are !
“Watanipimaje?akauliza
Mathew
“Sifahamu lakini lazima
upimwe hivyo waonyeshe
wewe ni nani.waonyeshe
uwezo wako wote ! akasema
Habiba lakini Mathew
hakuonekana kumuelewa
“Mama nashindwa
kukuelewa”
“Mathew sina muda wa
kukufafanulia.Sikiliza kile
ninachokwambia na ujiandae
kwani sikupaswa hata
kukueleza chochote kuhusiana
na suala hili.Hakikisha
hawagundui kuwa
umejiandaa” akasema Habiba
“Mama ni ak…………….”
Akataka kusema kitu Mathew
lakini Habiba akamzuia
“Mathew sihitaji
maswali.Tunakaribia kutua
jiandae” akasema Habiba
Ndege ilitua katika uwanja
wa kijeshi wa Bollling Airface
Base.
“Mathew good lucky”
akasema Habiba na kuinuka
Mathew akachukua sanduku
lake akamfuata Habiba
wakaanza kutoka nje.Habiba
Jawad alikuwa wa kwanza
kushuka ndegeni huku
Mathew akimfuaa nyuma yake.
Kulikuwa na watu watano
wakiwa katika mavazi ya suti
na wengine wanne walikuwa
katika mavazi ya
kijeshi.Wanajeshi wawili
wakamsogelea Mathew na
kumtaka asubiri .Habiba
Jawad aliyekuwa ameogozana
na watu wanne akageuka
akamtazama Mathew kisha
akaingia katika mojawapo ya
magari manne yaliyokuwepo
pale uwanjani na magari
mawili yakaondoka yakabaki
mawili.Baada ya Habiba
Jawad kuondoka Mathew
akaelekezwa kushuka ndegeni
akaongozana na wale
wanajeshi wanne ambao
wawili kati yao walikuwa na
silaha wakaelekea katika
gari.Mlango wa pembeni wa
gari lile ukafunguliwa na
Mathew akatakiwa kuingia
kisha magari yakaondoka bila
Mathew kuelezwa chochote
“Mnaweza mkanieleza
tunakoelekea? Akauliza
Mathew lakini hakuna
aliyemjibu
Walikatisha mitaa kadhaa
ya jijila Washington halafu
wakaingia katika nyumba moja
ambayo kuta zake zote
zilikuwa zimeeneza majani
ambayo huota kufuata
ukuta.Nyuma yote ilikuwa ya
kijani kufuatia rangi ya majani
yale isipokuwa bati ambalo
lilikuwa jekundu.Mathew
akatakiwa kushuka garini
akaongozwa na wanajeshi wale
wanne kuingia ndani.Mlangoni
kulikuwa na jamaa mmoja
aliyekuwa ameva suti nzuri ya
rangi ya bluu akafungua
mlango na wanajeshi wawili
wakatangulia ndani Mathew
akafuata nyuma yao kisha
wanajeshi wale wawili
wakafuata nyuma ya Mathew
pamoja na jamaa wengine
watano.
“Hapa ni wapi? Yule mama
niliyekuja naye ndegeni yuko
wapi?akauliza Mathew
akionyesha wasiwasi
“Tulia na fuata kile
utakachoelekezwa” akasema
jamaa mmoja halafu akaenda
chumbani na kurejea na nguo
akamtaka Mathew avue
mavazi yake na avae nguo zile
alizomletea.
“Ninapelekwa
wapi?akauliza Mathew
“Nimekwambia fanya kile
nilichokuelekeza.Vua mavazi
yako na uvae mavazi haya”
Mathew akashika nguo zile
akazikunjua akazitazama
“Sikiliza
Mathew.Tutakaposhuka
watakuchukua na kwenda
kukupima.Show them who
you are !
Mathew akayakumbuka
maneno aliyoambiwa na
Habiba Jawad,akazitupa chini
zile nguo.
“Sivai mavazi hayo hadi
mtakaponieleza wapi mnataka
kunipeleka ! akasema Mathew
na wale jamaa wakatazamana
“Tafadhali ndugu vaa
mavazi hayo
uliyopewa,usijitafutie
matatizo”Mathew akaelekezwa
“Nimesema sivai mavazi
yenu hadi mtakaponieleza
wapi mnanipeleka ! akasema
Mathew
“Hii ni mara ya mwisho
nakuomba ndugu vua hayo
mavazi uliyovaa na vaa mavazi
haya uliyoelekezwa kuvaa !
akafoka mmoja wa wale jamaa
aliyekuwa amevaa suti ya
kijivu
“Hivi ndivyo
mnavyowatendea wageni
wanaokuja kutembelea nchi
yenu?Kwa nini mmenileta
hapa?Nimefanya kosa gani?
Kuna sheria ya Marekani
nimevunja? Akauliza Mathew
kwa ukali na wale jamaa
hawakumjibu
“Hamtaki kunijibu?
Akauliza tena Mathew
“Kama hamna jibu la
kunipa naomba tafadhali
mniache niende zangu kabla
ubalozi wangu haujaanza
kunitafuta ! akasema Mathew
na jamaa aliyevaa suti ya kijivu
akawapa ishara wale wanajeshi
“Hebu mkaribisheni
Marekani ! akasema Yule
jamaa na wanajeshi wawili
ambao walikuwa wamejaza
mikono yao wakamsogelea
Mathew.Mmoja wa wale
wanajeshi akamtandika
kichwa Mathew akaenda chini
akahisi nyota kwa kichwa kile
kizito.
“Waonyeshe wewe ni
nani.Waonyeshe uwezo wako
wote ! Mathew akayakumbuka
tena maneno ya Habiba Jawad
akiwa ameanguka chini
Akiwa pale chini mmoja
wa wale wanajeshi akainua
mguu wake kwa lengo la
kumkanyaga lakini tayari
Mathew alikwisha kiona
kitendo kile akaukwepa mguu
wa Yule mwanajeshi ambao
ulipiga ardhi kwa kishindo na
Mathew akajigeuza na
kumkata mtama Yule
mwanajeshi akaanguka mzima
mzima sakafuni na kutoa
kishindo.Kwa kutumia miguu
yake akaibinua meza ndogo
iliyokuwa karibu yake
akaidaka na kisha akasimama
kwa kasi na kumpiga nayo
mmoja wa wale wanajeshi
ikampeleka chini.Jicho la
Mathew lililogeuka kama
kinyonga lilimuona
mwanajeshi mmoja akimjia
nyuma yake akageuka na
kumtandika teke zito la uso
halafu akapanda juu ya sofa na
kumrukia mwanajeshi wa nne
mateke mawili mfululizo
kifuani akaanguka chini.Yule
mwanajeshi aliyepigwa na
meza ndogo tayari alikwisha
inuka na mkononi alikuwa
ameshika ubao uliotoka katika
ile meza aliyopigwa nayo na
kwa nguvu akaurusha ubao ule
kumuelekea Mathew lakini
tayari alikwisha uona ule ubao
akaukwepa ukampiga jamaa
aliyekuwa amesimama
akishuhudia wanajeshi wao
wakitembezewa kipigo
kikali.Baada ya kumkosa na
ule ubao Yule mwanajeshi
ambaye tayari alikwisha
pandwa na hasira akaruka
mzima mzima kutaka
kumvamia Mathew mahala
alipokuwa amejibanza lakini
Mathew alikuwa mwepesi zaidi
yake akaruka juu na kumuwahi
Yule jamaa akiwa juu na
kumtandika teke zito la kifua
na kumfanya Yule jamaa
aanguke kama furushi.Mathew
akajigeuza na kutua nyuma ya
Yule jamaa aliyepigwa na ubao
ambaye alikuwa amepiga
magoti damu ikimtoka
mdomoni akamkaba kabali
kwa mkono wake wa kushoto
halafu akaiokota bastora ya
Yule jamaa iliyoanguka
pembeni akamuwekea
kichwani.
“Wote inue mikono juu !
Mathew akawaamuru wale
jamaa waliovaa suti ambao
wote walikuwa wameshika
bastora zao wakimuelekezea.
“Namaanisha
ninachokisema wote inueni
mikono juu ! akasema Mathew
kwa ukali lakini wale jamaa
bao waliendelea kumuelekezea
bastora
“Nitahesabu hadi tatu
kama hamtatii nitamtandika
mwenzenu risasi..Moja !
Mathew akaanza kuhesabu
“Mbili ! akaendelea
“Fanyeni anachowaelekeza
! akasema Yule jama
aaliyekabwa kabali ambaye
alikuwa anapata taabu kuvuta
pumzi.
“Wekeni silaha zenu chini
na muinue mikono juu !
akaamuru Mathew na taratibu
wale jamaa wakaziweka chini
bastora zao na kuinua mikono
juu kama walivyokuwa
wameelekezwa
“Wewe inuka ! Mathew
akamuelekezea bastora mmoja
wa wanajeshi akamtaka ainuke
akaziokote zile bastora na
kumsogezea karibu.Yule
mwanajeshi akafanya
alivyoelekezwa akaziokota
bastora na kumsogezea
Mathew halafu akamtaka
kuchukua pingu kutoka katika
suti zao na kuwafunga
mikono.Mwisho akamtaka
Yule mwanajeshi ajifunge
pingu yeye
mwenyewe.Wanajeshi wengine
watatu hali zao hazikuwa nzuri
wawili walikuwa wamepoteza
fahamu na mmoja alikuwa
anatoka damu
mdomoni.Mathew
alipohakikisha wote
wamefungwa pingu akampiga
Yule jamaa pigo kichwani
akaanguka na kupoteza
fahamu akachukua bastora
mbili akazifutika kiunoni
halafu akatoka mle ndani
akaufungua mlango wa
mojawapo ya gari akaingia
ndani akaliwasha.
“Ninaelekea
wapi?akajiuliza
“Nitajua pa kuelekea ngoja
kwanza niondoke mahala
hapa” akawaza Mathew na
kugeuza shingo akatazama
nyuma ili kugeuza gari lakini
akasikia muunguruo wa
helkopta iliyofikan a
kusimama juu ya ile
nyumba.Mara akasikia
mivumo ya risasi na gari
ikabonyea chini matairi yote
yalipigwa risasi.
“Bastard ! akafoka Mathew
huku akiupiga usukani kwa
hasira na kutokea upande wa
pili ikatokea tena helkopta ya
pili ambayo kama ile ya
kwanza mlangoni alikuwepo
jamaa aliyekuwa na bunduki
kubwa.Wakati Mathew
akitafakari geti likafunguliwa
na gari mbili zikaingia.Mathew
akaelekeza macho ukutani na
kuwaona watu wanne wenye
bunduki wakiwa
wamezielekeza kwake.Wale
jamaa walioingia na magari
wakashuka na mmoja wao
akatumia kipaaza sauti
kumtaka Mathew ashuke
garini.
“Sina ujanja,siwezi kutoka
salama mahala hapa.Wako
wengi na wamejizatiti kwa
silaha” akawaza Mathew na
kufungua mlango wa
gari.Bunduki zote
zikaelekezwa katika lie
gari.Akatoa mguu akaushusha
chini taratibu,akatoa na
mwingine halafu akatoa
mkono wa kwanza
akauonyesha ukiwa mtupu
akatoa na mkono wa pili
akauonyesha ukiwa mtupu
halafu akashuka garini na
kuinua mikono juu.Haraka
haraka na kwa tahadhali watu
wanne wakamsogelea na
kuanza kumpeua hakuwa na
bastora zote aliziacha
garini,akafungwa mikono kwa
pingu na kufunikwa mfuko
kichwani akaingizwa garini na
kuondoka eneo lile.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 2 : EPISODE 5
Gari lilisimama mlango
ukafunguliwa na Mathew
akashushwa.Watu wale
walifanya mambo yao kimya
kimya bila maongezi hivyo
hakujua kulikuwa na watu
wangapi eneo lile lililokuwa na
ukimya mkubwa.Aliingizwa
katika jumba lililokuwa na
ubaridi mwingi.Mlango wa
mojawapo ya chumba katika
jumba lile ukafunguliwa na
Mathew akaingizwa ndani ya
chumba hicho akaketishwa
kitini halafu akafunguliwa
pingu alizokuwa amefungwa
mikononi akafungwa katika
pingu nyingine zenye
mnyororo zilizounganishwa na
chuma kilichokuwa juu ya
meza akaachwa hapo na watu
wale wakaondoka.
“Nini wanataka kukihakiki
kwangu hawa jamaa ambao
Habiba amesema
wananifanyia majaribio? Ngoja
nifuate maelekezo ya Habiba
kwamba niwaonyeshe mimi ni
nani” akawaza Mathew
Ndani ya chumba kimoja
kizuri katika jengo moja
lililokuwa kati kati ya jiji la
Washington watu tisa
walikuwa wameyaelekza
macho yao katika runinga
kubwa wakifuatilia kile
kilichokuwa kinaonekana pale
runingani.Katika runinga ile
alionekana Mathew Mulumbi
akiwa ndani ya chumba
alimofungwa akiwa na mfuko
kichwani
Mathew aliinamisha
kichwa upande mmoja na
alionekana kama vile anauma
kitu kwa meno yake.Baada ya
dakika tatu akainamisha
kichwa mezani na kusogeza
kiganja cha mkono karibu na
mdomo akachukua kitu
ambacho hakikuweza
kuonekana vizuri halafu
akaanza kuchokonoa pingu ya
mkono wa kushoto ikafunguka
akavua ule mfuko aliofunikwa
kichwani halafu akaifungua na
ile ya mkono wa kulia akawa
huru.
“Habiba huyu jamaa ni
Gaidi au ni jasusi?akauliza
Edward Murphy
“Huyu ni gaidi” akajibu
Habiba
“Anafanya mambo ya
kushangaza ambayo magaidi
wengi hawawezi
kuyafanya.Umemtoa wapi
huyu?akauliza Robin
Ross.Kabla Habiba hajajibu
Mathew akaelekea mlangoni
wote wakayaelekeza macho
runingani kutazama
anachotaka kukifanya.Mathew
akauchunguza ule mlango
akagundua ni mlango
unaofunguliwa kwa kutumia
kadi ya kielektroniki.Akavua
kiatu chake cha mguu wa kulia
akang’oa kisigino halafu
akang’oa kipande cha chuma
kisha akatoa bisibisi ndogo na
vitu vingine vidogo
vidogo.Wote mle ndani ya
chumba wakabaki
wanashangaa
Mathew akafungua
sehemu ya kupitisha kadi ya
kielektroiki ya kufungulia ule
mlango.Kulikuwa na nyaya
kadhaa katika kiboksi kile
akazichunguza halafu
akakunjua kisu kidogo sana
ambacho alikitoa katika
kisigino cha kiatu akakata
nyaya kadhaa akazichuna na
kuunganisha na mara mlango
ukafunguka
“Yawezekana wakawa
wananitazama muda huu
ninachokifanya.Hizi ni salamu
zao” akawaza Mathew halafu
akatoka ndani ya kile chumba
akafuata varanda hadi
alipokuta mlango uliokuwa
umefungwa kwa nje.Pembeni
yake kulikuwa na chumba
ambacho mlango wake
ulikuwa wazi.Akaingia ndani
ya kile chumba mara mlango
wa kile chumba ukajifunga
halafu akasikia hatua za mtu
akisogelea ule mlango wa kile
chumba alimo akajiandaa
kukabiliana na yeyote
atakayeingia mle na mara
akaona moshi ukipenya chini
ya mlango.Taratibu akaanza
kuhisi macho yanapoteza
nguvu ya kuona akaanguka
chini na kupoteza fahamu
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 2 : EPISODE 6
Mathew alirejewa na
fahamu na kujikuta akiwa
amelazwa kitandani.Ndani ya
chumba kile kizuri kulikuwa
na akina dada wawili warembo
wakiwa wameketi katika sofa
lililokuwamo mle
chumbani.Taratibu akajiinua
na kukaa wale akina dada
wenye tabasamu murua
wakamsogelea na kuketi
kitandani mmoja wao
akamsugua sugua mgongoni
“Pole sana.Unajisikiaje
sasa? Kuna sehemu yoyote
inauma?akauliza Yule
mwanadada kwa sauti nyororo
“Kichwa kinaniuma sana”
akajibu Mathew na Yule
mwanadada akampa vidonge
viwili akameza.
“Naitwa Sophia
mwenzangu anaitwa
Emily.Wewe jina lako nani?
Akauliza Sophia aliyeonekana
mzungumzaji sana
“Abu Zalawi”
“Abu Zalawi karibu sana
Washington DC.Pole kwa yote
yaliyotokea na sasa nakuomba
uingie bafuni ukaoge halafu
tuondoke”
“Mnanipeleka wapi?
“Sikiliza Abu Zalawi
tumepewa maelekezo
utakapozinduka tukupeleke
sehemu hivyo tusipoteze muda
oga vaa mavazi pendeza”
akasema Sophia na Mathew
akaingia bafuni akaoga kisha
akatoka na kukuta kuna suti
nzuri nyeusi kitandani pamoja
na viatu vizuri vyeusi
akavaa.Hakuwa na haja ya
kujitazama katika kioo kwani
suti ile ilimkaa
vyema.Akagonga mlango
Sophia na Emily wakaingia.
“Mbona hujavaa
tai?akauliza Sophia
“Sipendelei kuvaa tai”
“Sogea hapa karibu”
akasema Sophia na kumfungia
Mathew tai kisha akampa
mfuko ili auvae kichwani.Sura
ya Mathew ikabadilika
“Najua hupendi Abu
Zalawi lakini lazima uvae.Hizi
ndizo taratibu” akasema
Sophia
“Tafadhali vaa Abu Zalawi”
akasisitiza Sophia na Mathew
akauvaa mfuko ule
wakamuongoza kutoka ndani
ya ile nyumba hadi katika gari
wakaondoka
Baada ya mwendo wa
dakika zaidi ya thelathini
hatimaye gari ikasimama na
milango ikafunguliwa Mathew
akashushwa na akahisi kuna
mikono mizito ya mwanaume
ikimkamata mkono wake na
kumuongoza kuelekea
ndani.Waliingia katika lifti
kisha wakashuka na kutembea
kidogo akasikia mlango
ukifunguliwa wakaingia ndani
ya chumba na Mathew
akaenda kuketishwa kitini
halafu akatolewa ule mfuko
kichwani.Ndani ya chumba
kile kikubwa na kizuri
kulikuwa na meza kubwa ya
duara na watu wasiopungua
kumi na tano walikuwa
wameizunguka meza ile na
mmoja wao alikuwa ni Habiba
Jawad.Mathew akashusha
pumzi baada ya kumuona
Habiba
“Abu Zalawi napenda
kuchukua nafasi hii
kukukaribisha sana
Washington DC” akasema
mzee mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la David Walker.
“Ahsante” akajibu
Mathew.
“Kuna mambo yametokea
ambayo
yamekushangaza.Ulichukuliwa
uwanja wa ndege na
kupelekwa mahala
usipopafahamu na hukujua
kwa nini.Kilichotokea ni
utaratibu wetu wa kuwapokea
wageni wanaofika kwa mara ya
kwanza na vile vile
tulikupitisha katika mtihani
mdogo kupima uwezo
wako.Kila mtu ambaye huwa
na ana mahusiano na sisi
hupimwa uwezo wake katika
mambo mbali mbali.Wengine
huwapeleka gerezani au katika
nyumba za mateso kuwapima
namna wanavyoweza
kukabiliana na hali
ngumu.Kwako pia ilipangwa
iwe hivyo lakini kwa umahiri
uliouonyesha nina furaha
kukujulisha kwamba umefaulu
jaribio kwa alama za juu
sana.Mambo uliyotuonyesha
hatukuwa tena na ulazima wa
kuendelea na zoezi la
kukupima.Karibu sana
Washington DC” akasema
David Walker na Mathew
akainamisha kichwa
kushukuru
“Namshukuru sana
Habiba kwa kunijulisha
mapema kile walichokipanga
hawa jamaa” akawaza Mathew
“Abu Zalawi kabla ya yote
napenda nimpe nafasi Habiba
Jawad afanye utambulisho
kisha atoe maelezo
machache.Karibu Habiba
Jawad” akasema David Walker
na Habiba jawad akasimama
“Ahsante David” akasema
Habiba na kumtazama
Mathew
“Kwanza kabisa Abu
nataka uwafahamu watu
walioko humu ndani kwa
majina yao.Tukianzia na
mwenyekiti pale anaitwa
David Walker yeye tayari
amekwisha
jitambulisha.Anayefuata
mkono wake wa kulia ni
Richard Smith,anafuata John
Hill,anafuata David
Carter,Robert Baker,James
Campbell,Michael
Torres,Donald Cooper,Brian
Watson.Tukirudi kwa upande
wake wa kushoto tunaanza na
Jason Brooks,Eric
Wood,Jeffery Jenkins,Carl
Henderson,Terry
Hughes,Willie Simmons
,Wayne Sullivan,Edward
Murphy na Robin
Ross”Habiba akanyamaza
“Baada ya kuwatambua
watu hawa walioko mbele yako
sasa nageukia upande wa
pili.Aliyeko mbele yenu
anaitwa Abu Zalawi.Huyu asili
yake ni nchini Misri lakini kwa
sasa ni raia wa Saudi
Arabia.Anatokea katika kundi
la Ammar Nazari brigades
ambalo nimekuwa nikilifadhili
pia.Kutokana na umahiri wake
ninamtumia kama msaidizi
wangu na leo hii nimekuja
kumtambulisha kwenu rasmi
mumfahamu na kumkabidhi
majukumu.Ninamuamini Abu
Zalawi.Ni mtu ambaye ni
mtiifu kwangu na amenisaidia
mambo mengi.Naamini nanyi
pia mtamuamini kama
mnavyoniamini
mimi.Mlichokiona leo hii ni
sehemu ndogo tu ya uwezo
mkubwa alionao Abu
Zalawi.Ni mtu sahihi kwa kazi
ambayo mnataka
kumtuma.Sina mashaka naye
hata kidogo” akasema Habiba
akanyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Abu Zalawi naamini
unajiuliza kwamba hawa
walioko mbele yako ambao
nimewatambulisha kwako ni
akina nani?kwa nini tumekuja
hapa?Sikukueleza chochote
kuhusiana na safari yetu hii
lakini leo ni wakati muafaka
wa kuufahamu ukweli”
akanyamaza halafu akaendelea
“Unanifahamu kama
mfadhili mkubwa wa makundi
mbali mbali ya kigaidi hasa
kundi la IS.Naamini umekuwa
unajiuliza na si wewe peke bali
watu wengi nahata wale ambao
ninawafadhili kwamba
ninafaidika na nini
ninapofadhili ugaidi?Hakuna
chochote ambacho ninakipata
kutoka kwa magaidi lakini
nimekuwa nikitoa mabilioni ya
fedha kwa makundi mbali
mbali na kufadhili operesheni
zao mbali mbali za
kigaidi.Ukweli ambao wewe na
wengine wote hamuufahamu
ni kwamba timu hii unayoiona
ndani ya chumba hiki ndiyo
inayofanikisha kila kitu.Mimi
ninafanya kazi kwa niaba ya
timu hii.Wao ndio
walioniwezesha kiuchumi na
kuwa tajiri mkubwa na utajiri
huo ndio ninaoutumia
kufadhili makundi ya kigaidi”
akasema Habiba na
kumtazama Mathew.
“Nadhani umestuka sana
kusikia kwamba Marekani
wanafadhili kundi la IS na
makundi mengine ya
kigaidi.Kuna chochote unataka
kukisema? Akauliza Habiba
huku akitabasamu.Mathew
akakohoa kidogo halafu
akasema
“Nimestuka sana.Sikuwahi
kufikiri kitu kama
hiki.Sikuwahi kufikiri hata
siku moja kama Marekani
wanaweza wakafadhili
makundi ya kigaidi.IS
wamekuwa wakifanya
mashambulio mbali mbali
duniani na kupelekea vifo vya
watu wengi na Marekani
imekuwa ikitangaza vita dhidi
ya kundi hili na tumeona hatua
ambazo imekuwa ikizichukua
katika kulikabili kundi
hili.Napata kigugumizi kidogo
kulielewa hili
jambo.Inawezekanaje IS
wakafadhiliwa na Marekani
ambao wamekuwa wakipanga
mikakati mizito na kutumia
fedha nyingi kugharamia
operesheni ya kulimaliza kundi
hili la IS.Au ni kundi lipi la IS
linalozungumzwa hapa?
Akauliza Mathew akijifanya
kustuka na kutokujua
chochote.
“David Walker karibu”
akasema Habiba na kukaa
akamuachia nafasi David
Walker ambaye alitaka kutoa
maelezo kumuelewesha
Mathew
“Unalolisema Abu Zalawi
ni kweli kabisa kwamba
Marekani tumekuwa tukitenga
bajeti kubwa kila mwaka kwa
ajili ya operesheni za
kupambana na ugaidi sehemu
mbali mbali duniani na hii
inaifanya Marekani kuwa
kinara wa kupinga ugaidi
duniani.Pamoja na kuwa
kinara katika vita hiyo dhidi ya
ugaidi duniani lakini kuna
upande wa pili wa ambao watu
wengi hawaufahamu ni
kwamba licha ya kuendesha
vita dhidi ya ugaidi lakini
Marekani tunawatumia
magaidi hao hao katika
mipango mbali mbali yenye
maslahi mazito kwa
Marekani.Hilo ni jambo
ambalo hata wamarekani
wenyewe hawalifahamu na si
wamarekani pekee hata Rais
wa Marekani halifahamu.Ni
jambo linalofanywa kwa siri
kubwa na timu hii unayoiona
humu ndani ndio
tunaoshughulika na jambo
hilo.Hiki ni kitengo maalum
cha siri ndani ya idara ya
ujasusi CIA ambacho ni
maalum kabisa kwa ajili ya
kushughulika na masuala haya
ya mashirikiano na makundi
ya kigaidi.Ni kitengo nyeti na
cha siri mno kiasi kwamba
hata wafanyakazi ndani ya CIA
hawafahamu uwepo wake
hivyo basi kwa mtu kama
wewe kufahamu jambo hili ni
kwamba umeaminiwa mno na
tumekuamini kwa kuwa
umeletwa na Habiba Jawad
ambaye ni mwenzetu na
ambaye ndiye anayefanya kazi
kwa niaba yetu.Sisi
hatuwafahamu viongozi wa
makundi ya kigaidi na wao
hawatufahamu sisi lakini
wanamfahamu Habiba Jawad
hivyo basi tunakuamini kama
alivyokuamini Habiba na
ndiyo maana umeifahamu siri
hii na kuanzia leo hii wewe ni
mmoja wetu japo baada ya
kumaliza mazungumzo yetu
utalishwa kiapo.Sasa tugeukie
ni namna gani tunayatumia
makundi haya ya kigaidi na ni
namna gani tunafaidika nayo?
akasema David Walker.
“Marekani ni taifa kubwa
kiuchumi duniani.Kama nchi
tunahitaji malighafi kwa ajili
ya kuendesha viwanda vyetu
na kuufanya uchumi wetu
uzidi kupaa.Malighafi kubwa
ambayo tunaihitaji ni mafuta
ambayo kwa kiasi kikubwa
dunia nzima inategemea
mafuta kutoka nchi za
Mashariki ya kati.Kwa bahati
mbaya Marekani na nchi
azalishaji wakubwa wa mafuta
duniani hatuna mahusiano
mazuri.Ukiangalia nchi
ambayo inatajwa kuwa na
mafuta mengi zaidi duniani ni
nchi ya Venezuela.Unafahamu
mahusiano ya Marekani na
Venezuela si mazuri.Nchi
nyingine ambazo zina akiba
kubwa ya mafuta ni Saudi
Arabia hawa ni washirika
wetu.Nchi ya tatu ni Canada,ya
nne ni Iran.Hawa hatuna
maelewano mazuri nao hata
kidogo.Zipo pia nchi kama
Iraq,Kuwait,UAE,Urusi na
Libya.Kama nilivyosema
kwamba nchi nyingi
wazalishaji wa mafuta ziko
Mashariki ya kati na nyingi
kati ya hizo hazina maelewano
mazuri na Marekani na hii ni
kutokana na kuwaunga mkono
Israel.Kuna chuki kati ya
Marekani na nchi za kiarabu
japo si zote kwani zipo nchi za
kiarabu ambazo ni washirika
wetu.Ili tuweze kupata mafuta
tunawatumia makundi ya
kigaidi katika kuanzisha vita
na sisi tunapata nafasi ya
kupeleka vikosi vyetu kwa
kigezo cha kuwasaka magaidi
na kisha huchukua mafuta na
kuongeza akiba
yetu.Tumekwisha fanya hivyo
katika nchi kadhaa sina sababu
ya kueleza hapa Habiba
atakueleza kila kitu kwa hiyo
sababu ya kwanza ya
kuwatumia magaidi ni ili
kuifanya Marekani kupeleka
vikosi vyake katika nchi husika
kwa ajili ya kuchukua
mafuta.Naomba nisiendelee
zaidi kwa kuwa utaendelea
kufahamu taratibu kila kitu
kuhusiana na sisi” akanyamaza
akanywa maji halafu akasema
“Abu Zalawi baada ya
kukufahamisha kwa ufupi
kuhusu sisi ni akina nani na
majukumu yetu sasa tunaingia
katika kile ambacho
kimetukutanisha hapa sisi na
wewe” David akanyamaza tena
halafu akaendelea.
“Tulimuomba Habiba
atutafutie mtu mahiri kutoka
katika makundi ya kigaidi kwa
ajili ya kazi maalum.Baada ya
kufanya uchunguzi wake
Habiba amekuleta wewe
ambaye ndiye anayeona
unafaa kwa ajili ya kazi hiyo na
tunaamini Habiba hajakosea
kwani ameleta hasa mtu yule
ambaye
tunamuhitaji.Umetuonyesha
uwezo wako tumeridhika na
sasa ni wakati wa
kukufahamisha kazi gani
ambayo tunataka ukaifanye”
akanyamaza tena kisha
akasema
“Kwa muda mrefu sasa
nchi za Iran na Marekani
zimekuwa katika mgogoro
mkubwa ambao unahusiana na
masuala ya silaha.Iran
ikisaidiwa na baadhi ya nchi
kubwa imejenga vinu vya
nyuklia na inadai kuwa ni kwa
ajili ya kuzalisha nishati ya
umeme lakini tunaamini
mpango wa Iran ni
kutengeneza kombora la
nyuklia.Huu umekuwa ni
mzozo wa miaka mingi na
umepelekea nchi ya Iran
kuwekewa vikwazo mbali
mbali vya kiuchumi.Ni
kutokana na mzozo huo
ililazimika kuwekeana
mkataba kati ya Iran na nchi
za ulala na Marekani wa
kutokuendelea na urutubishaji
wa madini ya Urani.Marekani
ilijitoa katika mkataba huo na
Iran imetishia kuendelea na
urutubishaji wa madini ya
urani.Miaka kadhaa iliyopita
tuliwateka wanasayansi wa
Iran waliotoka Urusi kupatiwa
mafunzo ya utengenezaji wa
bomu la nyuklia.Kukamatwa
kwa wanasayansi hao ni
kihibitisho tosha namna Iran
ilivyojiandaa kutengeneza
kombora la nyuklia”
akanyamaza kidogo kisha
akaendelea
“Kwa siku za hivi karibuni
mzozo huu umechukua sura
mpya kwa kila nchi kutishia
kuishambulia nyingine.Rais
wa Marekani alitishia
kuisambaratisha Iran na Iran
imetishia kwanza
kuwashambulia washirika wa
Marekani katika eneo la
Mashariki ya kati na vile vile
imetishia kuishambulia hadi
Marekani.Iran imetoa vitisho
kwamba kama Marekani
itathubutu kuishambulia basi
itakutana na kipigo ambacho
haijawahi kupigwa.Kauli kama
hizi hatuwezi kuzipuuza na
kuna taarifa za chini chini
kwamba Iran ina mfumo wa
kisasa wa makombora ya
masafa marefu.Kwa muda
mrefu sasa Marekani imekuwa
ikijaribu kufanya uchunguzi
kujua kuhusu silaha za Iran
bila mafanikio na hii ndiyo
inayoifanya Marekani kusita
kuishambulia Iran kijeshi kwa
kuhofia kwamba yawezekana
ikawa inamiliki hizo silaha
inayodai kuwa nazo na
tunaweza kuwaweka katika
hatari kubwa washirika wetu
walio karibu na Iran.Kwa ajili
hiyo basi tumeamua
kukutumia wewe katika suala
hili” David akanyamaza
akamtazama Mathew
“Tunataka kukutuma
uende Iran kufanya kazi mbili
kubwa.Kwanza ni kufanya
uchunguzi kuhusiana na silaha
za nchi hiyo na kazi ya pili ni
kuharibu kinu kikubwa cha
kurutubisha madini ya Urani”
akanyamaza tena na
kumtazama Mathew ambaye
alikuwa kimya akimsikiliza
“Kwa nini mimi?akauliza
Mathew
“Kwa nini wewe? David
naye akauliza kisha
akanyamaza kidogo
“Ni kwa sababu mbinu ya
kutumia majasusi kuichunguza
Iran imeshindwa kuzaa
matunda na hadi leo hii
hatujaweza kupata taarifa
zozote za kuhusiana na silaha
za nchi hiyo hivyo tunataka
kubadili mbinu na tunataka
kukupeleka wewe ambaye
utapokelewa kama gaidi na
shujaa bila kujua kuwa uko
pale kwa kazi maalum.Iran
utaingia vipi?Huu hapa
mkakati wa kukuwezesha
kuingiza Iran” akasema David
huku watu wote mle ndani
wakiwa wamemkazia macho
Mathew
“Eneo la Afrika Mashariki
hivi sasa liko katika machafuko
makubwa sana ya
kidini.Kinachoendelea kule ni
moja ya mipango yetu na kwa
kuwatumia IS tumeweza
kufanikisha kuibuka kwa
machafuko makubwa sana ya
kidini ambayo yamepelekea
Marekani kupeleka vikosi
vyake.Hapa unaweza ukaona
ni namna gani Marekani
inafaidika kutokana na
makundi ya
kigaidi.Tumewatumia IS
kutengeneza vurugu zile na
sasa Marekani inafaidika kwa
mafuta mengi kutoka
Uganda.Meli za Marekani
zimepanga foleni zinapishana
kujaza mafuta ,akiba yetu ya
mafuta inaongezeka.Hii yote ni
kazi ya timu hii unayoiona
humu ndani na ni mfano wa
mafanikio makubwa ambayo
yanapatikana kwa kuwatumia
magaidi” akasema David huku
akitabasamu na kumlazimu
Mathew kutabasamu pia
“Kumbe hawa mabazazi
ndio waliotengeneza vurugu
zile Afrika Mashariki kwa ajili
ya kujipatia mafuta ! Hawana
huruma hata kidogo
mashetani hawa.Natamani
niwasambaratishe wote hapa
hapa.Yaani ndugu zangu
wanakufa Afrika Mashariki
wao wanatabasamu kana
kwamba si chochote ! Ahsante
Habiba kwa kunileta hapa
nimeweza kujua chanzo cha
vurugu zile za
nyumbani.Wamekosea sana
kunieleza ukweli ! akawaza
Mathew
“Safari ya kwenda Iran
itaanzia Afrika Mashariki”
akasema David
“Tutakutuma uende Afrika
mashariki nchini Tanzania
kule unakwenda kulipua
ubalozi wa Marekani jijini Dar
es salaam”
“Kulipua ubalozi wa
Marekani? Akauliza Mathew
akionekana kushangaa
“Ndiyo unakwenda
kulipua ubalozi wa Marekani”
“Mnalipua ubalozi wenu
wenyewe? Akauliza Mathew
“Ndiyo unakwenda
kulipua ubalozi wa Marekani
uliopo jjini Dar es
salaam.Baada ya kulipua
ubalozi huo IS watajitokeza na
kudai kwamba wamehusika
katika tukio hilo na
tutalazimika kuongeza vikosi
zaidi Afrika Mashariki kwa
dhumuni la kuwasaka
IS.Baada ya shambulio hilo
tutaanza kukusaka kisha
tutakukamata na kuitangazia
dunia nzima kuwa
tumemkamata mtu aliyelipua
ubalozi wa Marekani jijini Dar
es salaam.Tukisha kukamata
tutakupeleka mahala ambako
wamehifadhiwa wanasayansi
wa Iran waliotekwa wakitokea
Urusi katika mafunzo ya
kutengeneza bomu la
nyuklia.Utakaa na
wanasayansi hao na baada ya
muda utasukwa mpango wa
kutoroka na utawatorosha
wanasayansi hao wa
Iran.Kitendo hicho kitapelekea
nchi ya Iran wakupokee na
kukuamini kwanza watakuona
shujaa kwa kulipua ubalozi wa
Marekani na pili kwa
kuwatorosha wanasayansi wao
ambao hakuna anayefahamu
hadi leo hii wako
wapi.Utaomba kupatiwa
hifadhi nchini Iran na
hawatakuwa na sababu yoyote
ya kukunyima hifadhi na hapo
ndipo utakapoanza kuifanya
kazi iliyokupeleka huko” David
akanyamaza akamtazama
Mathew
“Si jambo jepesi ndiyo
maana tulimuhitaji mtu
maalum na wewe ndiye haswa
unayefaa kwa kazi hii.Usihofu
tutakuwezesha kwa kila kitu
hadi utakapofanikiwa kuingia
nchini Iran hivyo usiwe na
wasi wasi” akasema David
zikapita sekunde kadhaa David
akasema
“Abu Zalawi nimejitahidi
sana kukupa maelezo marefu
ambayo naamini
umenielewa.Kuna swali lolote
unataka kuuliza?
“Hapana sina swali
nimewaelewa vyema” akajibu
Mathew
“Vizuri sana” akasema
David
“Tumejitahidi vya kutosha
kukueleza kuhusu sisi na kile
tunachokihitaji kwako sasa ni
zamu yetu kusikia kutoka
kwako.Je unakubali kuifanya
kazi hii?
Mathew hakujibu alikaa
kimya kwa muda na wote mle
chumbani wakamkazia
macho.Akainamisha kichwa
akafikiri kwa muda na kusema
“Kwanza kabisa nataka
nimshukuru sana Habiba
Jawad kwa kunitoa mahala
nilipokuwa na kuniamini niwe
msaidizi wake.Sikutegemea
kama siku moja ningeweza
kufika sehemu ya juu kama
hii.Sikitegemea kama siku
moja ningeweza kukutana na
timu ya watu wenye nguvu
kubwa duniani” akasema
Mathew na wale watu mle
ndani wakatabasamu
“Sikuwahi kufikiri kama
siku moja ningeweza
kuaminiwa na kupewa jukumu
kubwa kama hili
nililopewa.Sina sababu yoyote
ya kusema hapana.Mmenipa
heshima kubwa sana ya
kunituma nikafanye kazi ya
taifa kubwa
duniani.Ninawaahidi kwamba
nimekubali na nitafanya kila
mlichoniagiza
nikifanye.Ninawaomba msiwe
na hofu ninajiamini ninao
uwezo wa kutekeleza hiki
mnachonituma nikafanye”
akasema Mathew na makofi
yakapigwa
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Saa moja na dakika
ishirini za jioni iliwakuta Ruby
na Gosu Gosu tayari
wamekwisha fika ikulu
kuzungumza na
Rais.Iliwalazimu kusubiri kwa
saa mbili zaidi ndipo
walipoonana na Rais
“Karibuni sana
jamani.Mtaniwia radhi kwa
kipindi hiki mambo ni mengi
mno hivyo msione kama vile
nimewaweka pembeni”
akasema Dr Fabian
“Usijali mheshimiwa rais
tunalielewa hilo” akajibu Ruby
“Nashukuruni sana
mmefika” akasema Dr Fabian
na kuwachukua akina Ruby
wakaelekea katika chumba cha
mazungumzo
“Kwanza kabisa napenda
niwashukuru mno kwa wazo
zuri mlilonipa jana.Nimeona
matokeo yake.Jioni hii
nimepokea simu kutoka kwa
Mufti wa Tanzania akaniomba
tukutane tuzungumze na
akashauri kama ikiwezekana
tukutanishwe viongozi wote wa
kuu wa dini tukae meza moja
tuzungumze tuone namna
tutakavyoweza kutoka katika
janga hili linalotukabili hivi
sasa.Nimekubali wazo lake na
tayari nimewaelekeza
wasaidizi wangu wanisaidie
kuwatafuta viongozi wengine
wa dini upande wa wakristu ili
tuandae mkutano wa pamoja
tuzungumze.Masuala haya
yanayohusiana na imani za
dini hayawezi kumalizwa na
vikosi vya jeshi bali kwa
mazungumzo na viongozi wa
dini ambao wanayo nguvu ya
kuwashawishi waumini wao
kuacha
vurugu.Nashukurusana kwani
ni wazo lenu ndiyo limezaa
haya mazungumzo.Nimepokea
pia taarifa kutoka kwa mkuu
wa jeshi la polisi ameniambia
kwamba kwa siku ya leo
vurugu zimepungua tofauti na
siku ya jana.Wote wanaamini
hotuba ile imesaidia sana kwa
vurugu kupungua.Hapo pia
ninaelekeza shukrani zangu
kwenu kwani sikuwa na wazo
lile la kuhutubia taifa”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais hata
sisi tunashukuru sana kama
wazo lile limezaa
matunda.Tuna imani kikao
hicho cha viongozi wakuu wa
dini mbali mbali kitakuwa na
matunda mazuri” akasema
Ruby
“Naamini hivyo.Tunaweza
kufikia muafaka mzuri.Vipi
kwa upande wenu kuna
chochote mmekipata?
“Mheshimiwa Rais
tumeanza kulifanyia kazi lile
suala la kumchunguza Karim
Abdallah.Tumefika nyumbani
kwake lakini tumemkosa na
inaonekaana aliondoka haraka
haraka yeye na familia
yake.Katika uchunguzi wetu
tulipata orodha ya watu
kadhaa ambao aliwasiliana nao
na mtu wa mwisho
kuwasiliana naye alikuwa jijini
Tanga.Tuliwatumia watu wetu
wa kule Tanga kumfuatilia
huyo mtu lakini walikuta
nyumba yake ikiwa imeteketea
kwa moto.Tulimchunguza tena
huyo jamaa na kumfuatilia
mtu ambaye aliwasiliana naye
mara ya mwisho ambaye naye
alikuwa hapo hapo Tanga na
watu wetu walipoingia katika
hiyo nyumba walikuta kuna
maiti ya mwanamke
amechomwa kisu kifuani”
akasema Ruby na
kumuonyesha Rais picha za
Yule mwanamke
“Huu ni unyama mkubwa
sana” akasema Dr Fabian
“Watu wetu walichukua
alama za vidole katika mpini
wa kisu wakazituma kwetu
kwa ajili ya kuzifanyia kazi na
tukamfahamu mtu aliyefanya
kitendo kile ni mumewe
ambaye ni mchungaji anaitwa
Augustin Kawala.Huyu naye
hajulikani mahala
alipo.Ukifuatilia kuanzia kwa
Karim hadi kwa huyu Augustin
wana mambo
yanayofanana,wote
wamewasiliana ndani ya siku
moja na simu zao zimezimwa
siku moja halafu wote
hawapatikani tena na
hawajulikani wako wapi.Hii
inatufanya tuamini
yawezekana wakawa kitu
kimoja”
“Dah ! akasema Dr Fabian
“Hatukuishia hapo.Baada
ya kuwakosa hao watu
tuliokuwa tunawatafuta
tuliendelea kumchunguza
Karim na tukafuatilia
mawasiliano yake ya wiki moja
kabla ya vurugu kuanza na
tukagundua kwamba
amewasiliana mara ishirini na
tatu na mtu mmoja anaitwa
Joshua Lulangwa ambaye ni
mwanasiasa wa chama cha
upinzani nchini
Uganda.Mheshimiwa Rais
hapo ndipo tulipofikia na
kukwama.Tunataka
kumchunguza huyu
mwanasiasa Joshua Lulangwa
tufahamu mahusiano yake na
Karim
Abdallah.Wamewasiliana mara
nyingi zaidi ndani ya wiki moja
kabla ya vurugu
kuanza.Tumekuja hapa
kuomba msaada wako ili
uweze kuzungumza na rais wa
mpito wa Uganda Jenerali
Paul Mukasa kumuomba
atusaidie tuweze kupata taarifa
za Joshua Lulangwa” akasema
Ruby
“Ruby kwanza kabisa
nataka niwapongeze kwa
namna mnavyojituma katika
kutafuta mzizi wa jambo
hili.Mimi nitawasiliana na
Jenerali Paul kumuomba
atusaidie kupata taarifa za
huyo mtu ambaye amekuwa na
mawasiliano na Karim
Abdallah.Ninaamini hadi
kufika kesho jioni tutakuwa
tumepata taarifa zake”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais”
“Kuna lingine la
kuzungumza?Nina kikao
kingine muda si mrefu”
akasema Dr Fabian
“Ni hilo tu mheshimiwa
rais lililotuleta hapa kwako
jioni ya leo”
“Basi
nawashukuruni.Endeleeni na
jitihada za kuhakikisha
tunaupata mzizi wa jambo
hili.Kama kuna chochote
mnakihitaji nijulisheni mara
moja” akasema Dr Fabian na
kuagana na akina Ruby.
Baada ya akina Ruby
kuondoka Dr Fabian akaelekea
chumbani kwake na kuketi
sofani akashusha
pumzi.Akachukua simu na
kuzitafuta namba za simu za
Jenerali Paul Mukasa
akampigia
“Dr Fabian” akasema
Jenerali Mukasa
“Jenerali Mukasa.Habari
za huko?
“Huku bado hali si
shwari.Vurugu zinaendelea
kupamba moto kila
uchao.Kadiri siku zinavyozidi
kwenda upepo wa vurugu hizi
unabadilika na sasa kunaanza
kuibuka makundi yenye silaha
ambayo yanashambuliana na
vikosi vya jeshi.Tunaendelea
kuvichunguza vikundi hivi
vinatoka wapi na silaha
vinatoa wapi.Machafuko haya
yanabadilika kutoka katika
machafuko ya kidini na sasa
yanaelekea kwenye uasi.Hivi
vikundi vilivyoibuka vinazidi
kuifanya hali ya amani kuwa
tete zaidi kwani vina silaha
nzito” akasema Jenerali Paul
Mukasa
“Hilo limeanza kujitokeza
hata huku
Tanzania.Kumeibuka makundi
ambayo siyo ya kidini
yanavunja nyumba,maduka
makubwa na
kupora.Wanaharibu na
kuchoma majengo ya serikali
na wana silaha.Nimeelekeza
tuwachunguze makundi hayo
tujue yametokeaje na nini hasa
malengo yake.Jana
nimeelekeza mawasiliano ya
simu yarejeshwe hapa
Tanzania na nikalihutubia taifa
nikawataka watu watafakari na
kuachana na vurugu hizi
zinazoendelea.Nimefurahi
kumekuwa na maendeleo
mazuri kwani taarifa
niliyoipata jioni hii ni kwamba
machafuko yameanza
kupungua na kesho nitakuwa
na kikao na viongozi wa dini
halafu tutajadili kuhusiana na
vurugu hizi”
“Mheshimiwa Rais hizo ni
dalili nzuri za kuelekea katika
suluhu ya vurugu hizi”
akasema Jenerali Mukasa
“Jenerali Mukasa
nimekupigia kuna jambo
ninataka tulijadili
kidogo.Unahisi nini hasa
chanzo cha vurugu hizi
ambazo zimeanzia Uganda na
kusambaa hadi Tanzania na
Kenya? Akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais,kwa
kweli hata mimi nashindwa
kuelewa namna vurugu hizi
zilivyoanza.Zilianza kiajabu
ajabu sana na kushika kasi
kama moto wa petrol.Mpaka
sasa tumeelekeza nguvu katika
kuzimaliza na hatujajikita
bado kujua chanzo chake”
akasema Jenerali Paul Mukasa
“Ipo timu hapa Tanzania
ambayo nimeipa kazi ya
kuchunguza chanzo cha
vurugu hizi kwa upande wa
Tanzania.Katika uchunguzi
wao wa awali wamebaini kuna
mtu mmoja ni mwanasiasa
ambaye wakati kukiwa na vugu
vugu la machafuko hapa
Tanzania aliandika ujumbe
katika ukurasa wake wa twitter
akiwataka waumini wa dini ya
kiislamu wakawashambulie
watu wa dini
nyingine.Tunahisi huyu
anaweza akawa anahusiana
kwa namna Fulani na
machafuko haya.Tunahisi vile
vile kwamba machafuko haya
yana chembe chembe za
kisiasa ndani
yake.Tumechunguza watu
kadhaa ambao wana
mahusiano na huyo
mwanasisasa lakini wote
wametoweka na simu zao
hazipatikani tena.Inaonekana
huu ni mtandao mmoja.Katika
uchunguzi wao wamegundua
kwamba Karim alikuwa na
mawasiliano na mwanasiasa
mmoja wa Uganda anaitwa
Joshua Lulangwa.Karim na
Joshua wamewasiliana mara
nyingi zaidi katika wiki moja
kabla ya machafuko
kuanza.Tunataka
kumchunguza Joshua
kufahamu mahusiano yake na
Karim na kisha tujue kama
wana mahusiano yoyote na
vurugu hizi
zinazoendelea.Tunaomba
msaada wako kupata taarifa za
huyu mtu” akasema Dr Fabian
“Hakuna tatizo
mheshimiwa Rais
nitawaelekeza watu wangu
wafanye uchunguzi kuhusiana
na huyo mtu kisha
nitakujulisha”
“Nashukuru sana Jenerali
Mukasa” akajibu Dr Fabian na
kukata simu
“Naanza kukubaliana na
Ruby kwamba yawezekana
machafuko haya yana chembe
chembe za kisiasa ndani
yake.Lazima tuhakikishe kwa
gharama zozote wale wote
waliosababisha machafuko
haya wanapatikana ”
akaendelea kuwaza Dr Fabian
WASHINGTON DC –
MAREKANI
“Mama Habiba siamini
kwa hiki ulichonifanyia.Hii
ndiyo misheni kubwa
uliyoniambia kwamba
unaniandalia? Akauliza
Mathew Mulumbi baada ya
kupewa dakika chache
kuagana na Habiba kabla ya
kwenda kujiandaa kutekeleza
jukumu kubwa alilopewa.
“Ndiyo Mathew” akajibu
Habiba Jawad
“Siamini mama kama
umekuja kuniuza kwa hawa
jamaa ambao sasa
wananituma nikafanye kazi
zao za hatari.Kwa nini
umenifanyia hivi mama
Habiba? Akauliza Mathew
“Mathew sikiliza hatuna
muda mrefu wa
kuongea.Nimekuleta hapa kwa
makusudi kabisa.Kama kweli
una nia ya dhati ya kumaliza
ugaidi duniani basi hii ndiyo
nafasi pekee unayopaswa
kuitumia.Hiki kitengo ndicho
kinachoongoza makundi
karibu mengi ya kigaidi
duniani hivyo umefika sehemu
unakotakiwa ufike.Finish
them.Fanya wanachokutuma
ufanye wachunguze vizuri
halafu mwisho wa siku
wamalize.Kikundi hiki ni
hatari sana kwa mustakabali
wa dunia.Hakikisha ……”
akasema Habiba na kugeuka
baada ya kusikia hatua za mtu
akiwafuata ambaye alitumwa
kumchukua Mathew.Habiba
akamtaka mtu Yule kusubiri
dakika mbili
“Mathew hakikisha
unafanikisha malengo
yako.Ifanye dunia ikukumbuke
kwa vizazi na vizazi.Maliza
kundi la kigaidi la IS na
makundi mengine.Kisafishe
kikundi hiki kidogo cha watu
hawa ambacho ndicho
kinachohatarisha amani ya
dunia.Hii ni misheni kubwa na
ya hatari.Lolote linaweza
kutokea katika misheni hii
mimi ninakuombea uimalize
salama na kila pale
nitakapokuwa na uwezo wa
kukusaidia nitafanya
hivyo.Jambo la mwisho baada
ya kumaliza misheni hii kama
utakuwa salama tafadhali
usirejee tena Riyadh.Nenda
nyumbani kaendelee na
maisha yako.Kaungane tena na
familia yako kwani lengo lako
litakuwa limetimia kuhusu
kupambana na ugaidi.Kuhusu
Najma usiwe na hofu
nitazungumza naye na
ataelewa.Narudia tena usirejee
Saudi Arabia kwani hadi
wakati huo sintakuwepo
tena.Ule utajiri wako wote
niliokupa utaendelea kuwa
wako na fedha zote zitawekwa
katika ile akaunti yako
utakapomaliza misheni hii
utatulia na familia yako na
kufurahia utajiri huo.”
akasema Habiba Jawad
ambaye machozi yalikuwa
yanamtiririka
“Mathew hii naamini
itakuwa ni mara ya mwisho
kwa mimi na wewe kuonana
hapa duniani.Kwa sasa nina
amani na ninaamini hata
nikifa leo nimeacha chuma
ambacho hakishiki kutu
ambacho kitamaliza
ugaidi.Nakutakia kila la heri”
akasema Habiba na
kumkumbatia Mathew halafu
akaanza kuondoka huku
Mathew naye akiwa
amesimama akimtazama.
“Ahsante Habiba Jawad
kwa kunifikisha
hapa.Umefanya jambo kubwa
sana kunifikisha hatua hii na
sintakuangusha” akawaza
Mathew akiwa bado
amesimama akimtazama
Habiba akiingia katika lifti na
mlango ukajifunga
Mathew aliongozana na
Yule mtu aliyetumwa
kumchukua hadi katika gari
wakaondoka.Ilikuwa ni safari
ya kimya kimya na Mathew
hakujua alikokuwa
anapelekwa.
Safari yao iliishia katika
nyumba moja ambayo geti lake
lilikuwa wazi wakaingia
ndani.Yule jamaa akashuka
garini na kumtaka Mathew
ashuke kisha wakaingia ndani
ya ile nyumba ambako
walimkuta jamaa mmoja
mnene aliyekuwa sebuleni
akitazama runinga.Alikuwa
kifua wazi na alikuwa amevaa
kaptura ya rangi za
jeshi.Akawakaribisha na Yule
jamaa aliyemleta Mathew
katika nyumba ile akatoka nje
akawaacha Mathew na yule
jamaa
“Jina lako nani? Akauliza
Yule jamaa akiwa
ameyaelekeza macho yake
katika mecho ya mpira wa
kikapu iliyokuwa inaendelea
runingani
“Abu Zalawi” Mathew
akajibu
“Naitwa Peter
Tylor.Karibu” akasema Peter
huku akiinua kikombe cha
kahawa na kunywa
“Ahsante” akajibu
Mathew.Peter akanywa
kahawa halafu akaweka
kikombe mezani akazima
runinga na kumtazama
Mathew
“Umewahi kuishi Afrika?
Akauliza Peter Tylor
“Ndiyo nimewahi kuishi
Nairobi Kenya na Cairo”
akajibu Mathew
“Vizuri.Unakwenda tena
Afrika lakini safari hii
unakwenda
Tanzania.Utaondoka hapa na
ndege ya jesi kuelekea
Tanzania.Utakapofika Dar es
salaam utafikia katika kambi
ya wanajeshi wa Marekani na
atakuja mtu Fulani anaitwa
Assad Ismail
kukuchukua.Huyu tayari ana
maelekezo yote ya kuhusu
wewe na ndiye atakayekusaidia
kufanikisha kazi uliyotumwa
kuifanya hapo Dar es salaam.”
akasema Peter Tylor na
kumchukua Mathew katika
chumba kimoja akaanza
kumpa maelekezo ya kazi
ambayo anatakiwa kwenda
kuifanya Dar es salaam.Baada
ya kupewa maelekezo yote
Mathew na Yule jamaa
wakaingia garini na kuondoka
kuelekea katika uwanja wa
ndege wa kijeshi ambako
kulikuwa na ndege inamsubiri.
“Safari njema” akasema
Peter na Mathew akaingia
katika ndege ile ya jeshi
ambayo haikuchukua muda
ikapaa kuelekea Tanzania.
“Habiba amenifikisha
mahala ambako sikutegemea
kufika.Nimegundua siri kubwa
sana ambayo dunia
haiijui.Nimekutana na kikundi
cha watu wachache wenye
nguvu ambao wanaamua kitu
gani wafanye katika nchi gani
hapa duniani.Machafuko
yanayoendea Afrika mashariki
kumbe ni mipango ya
Marekani kutaka kuchukua
mafuta ya Uganda.Hawajali
mamia ya watu wanaouana
kila uchao wao
wanachokitazama ni maslahi
yao tu.Hawa ni watu wakatili
sana ! akawaza
“Namshukuru sana
Habiba Jawad kwa kunifikisha
hapa.Aliponiambia kwamba
kuna mambo mengi ambayo
siyafahamu bado alikuwa
sahihi.Kuna mambo sikuwa
nikiyafahamu na mojwapo ni
hili la idara maalum ndani ya
shirika la ujasusi la marekani
CIA kushirikiana na makundi
ya kigaidi kwa ajili ya maslahi
ya Marekani” akawaza Mathew
“Ninakwenda kufanya kazi
ya kigaidi.Kutoka ujasusi hadi
ugaidi ! akaendelea kuwaza
Mathew akiwa ameinamisha
kichwa
“Nitafanya wanavyotaka
lakini hawataamini kwa kile
nitakachowafanyia.Ile idara
ndogo katika CIA lazima
niifuilie mbali,lazima dunia
ifahamu kile ambacho watu
hawa wanakifanya.Katika hili
natakiwa kuwa
mvumilivu.Natakiwa kwanza
kujenga imani kwao ili
waniamini na ndipo
nitakapoweza kutekeleza
mipango yangu.Lakini
nasikitika sana pale dunia
nzima watakapojua mimi ni
gaidi na nimelipua ubalozi wa
Marekani jijini Dar es
salaam.Ruby ataumia sana
akisikia jambo kama
hili.Wenzangu akina Gosu
Gosu na Austin hawataamini
macho yao pale watakaposikia
kwamba mimi ndiye
niliyelipua ubalozi wa
Marekani.Watoto wangu
watapatwa na mstuko mkubwa
baada ya picha zangu kutolewa
kwamba ndiye niliyelipua
ubalozi wa Marekani na
nitatajwa kama gaidi.Jina
langu litachafuka.Watu
wanaonifahamu hawataamini
kama kweli nimegeuka kutoka
jasusi hadi gaidi.Lakini baada
ya kuchafuka kwa kujulikana
kama gaidi mwisho wa mchezo
huu dunia nzima itanisifu kwa
kile nitakachokifanya.Halafu !
akawaza Mathew na kuinua
kichwa baada ya mmoja wa
wanajeshi waliokuwamo mle
ndegeni kumgusa na kumpatia
chupa ya bia.
“Ahsante” akasema
Mathew na kunywa funda
moja
“Marekani hawajui kama
mimi ni mtanzania.Hawajui
kama mimi ni jasusi na jina
langu ni Mathew Mulumbi na
si Abu Zalawi kama
walivyoambiwa na Habiba
Jawad.Baada ya picha zangu
kusambaa duniani kwamba
mimi ndiye niliyelipua ubalozi
wa Marekani jijini Dar es
salaam lazima siri itafichuka
kwamba mimi ni mtanzania na
nitakuwa nimejiweka katika
matatizo mimi na hata Habiba
pia ambaye amewahakikishia
wamarekani kuwa mimi ni raia
wa Saudi Arabia.Lakini hii
haiwezi kunizuia kuendelea na
mipango yangu.Dunia
itatikisika.Kila chombo cha
habari duniani lazima
kitaniongelea mimi”
akaendelea kuwaza Mathew
huku ndege ikiendelea
kupasua anga kuelekea
Tanzania
RIYADH – SAUDI ARABIA
Saa nane za mchana
Habiba Jawad aliwasili jijini
Riyad Saudi Arabia akitokea
Washington DC
Marekani.Katika uwanja wa
ndege alipokewa na mwanae
Najma ambaye alistushwa kwa
Habiba kurejea peke yake bila
ya Mathew Mulumbi.
“Mbona umerejea peke
yako mama,Abu yuko
wapi?akauliza Najma
“Tutazungumza tukifika
nyumbani Najma” akasema
Habiba na safari ikaendelea
kimya kimya
Waliwasili nyumbani kwa
Habiba na Najma hakutaka
kupoteza muda akamtaka
mama yake wazungumze.
“Mama nafahamu
umechoka sana kwa safari
ndefu.Takribani saa kumi na
nne umekuwa angani ukisafiri
lakini naomba tafadhali unipe
dakika chache
tuzungumze.Nina jambo
ambalo haliwezi kusubiri na
nilitamani nikufuate huko
huko Marekani tulizungumze”
akasema Najma na Habiba
akamtazama mwanae
akagundua kweli kuna kitu
kinamsumbua
“Kitu gani kinakusumbua
Najma?Ni kuhusu kutokurudi
na Abu Zalawi?akauliza
Habiba
“Hilo ni moja wapo lakini
kuna lingine kubwa zaidi ya
hilo” akajibu Najma
“Nieleze tafadhali”
“Kabla sijakueleza
chochote mama nataka
unihakikishie kwamba
utanieleza ukweli mtupu kwa
kile nitakachokuuliza”
akasema Najma.Habiba
akamtazama halafu akasema
“Nini kinakusumbua
Najma? Niambie kile
kinachokusumbua na mimi
nitakujibu” akasema Habiba
“Mama nataka unieleze
kila kitu kuhusiana na Abu
Zalawi”
“Abu Zalawi ni mume
wako,wewe ndiye uko naye
karibu zaidi na ni wewe
unayetakiwa kumfahamu
vyema.Hukupaswa kuniuliza
mimi kuhusu Abu Zalawi
kwani tayari umekuwa naye
kwa muda wa miezi kadhaa
hivi sasa.Unapaswa tayari uwe
unamfahamu vyema” akasema
Najma
“Mama nakuomba
tafadhali unieleze ukweli
kuhusiana na Abu Zalawi.Ni
nani huyu mtu?
Umemfahamuje? Akauliza
Najma
“Najma nini hasa
kinachokufanya uniulize mimi
habari za Abu Zalawi?
“Mama nakuomba sana
unisaidie kunieleza kuhusiana
na huyu mtu nahitaji sana
kumfahamu.Wewe ndiye
unayemfahamu vyema kuliko
mimi.Naomba tafadhali
unieleze kila kitu
unachokifahamu kuhusu Abu
Zalawi” akasema Najma
“Najma
unanishangaza.Kuna nini kati
yako na Abu Zalawi? Kuna
mgogoro wowote kati yenu?
Niambie tafadhali kama kuna
tatizo lolote” akasema Habiba
“Mama ngoja nikuweke
wazi ili upate picha halisi ya
mzigo ninaoubeba.Ulinitaka
niolewe na Abu Zalawi ambaye
ulidai ni mwanaume ambaye
ananifaa.Nilitokea kumpenda
Abu Zalawi kabla hata sijamtia
machoni kufuatia maelezo
yako na nilipomuona kwa
macho nilimpenda na
nikakubali kuolewa naye na
ninakiri kwako mama kwamba
ninampenda sana Abu Zalawi
lakini kuna mambo
yamejitokeza ambayo
yamenifanya nitake
kumfahamu vyema huyu mtu
ni nani?”
“Nini kimetokea Najma?
Akauliza Habiba
“Kabla ya safari ya kwenda
Marekani ulizungumza na Abu
Zalawi na aliporejea chumbani
alionekana kama vile
amechanganyikiwa.Sifahamu
ni kitu gani ulimweleza lakini
hakuwa Yule
niliyemzoea.Alichukua kitabu
hiki hapa akakifungua
akatafuta namba za simu
ambazo zina jina la Ruby
akapiga zaidi ya mara tatu
lakini simu ya huyo mtu
haikuwa ikipatikana.Wakati
akiendelea kumtafuta huyo
Ruby nilikichukua kitabu hiki
na kuzikuta namba hizo za
Ruby.Nilimuuliza Ruby ni nani
akastuka sana na
kuninyang’anya kile
kitabu.Mama mimi nina wivu
sana na ndiyo maana sikutaka
kujiingiza katika masuala ya
mapenzi kwa kuhofia
kuumizwa. Mlipokwenda
Marekani nilipiga zile namba
za Ruby alizopiga Abu Zalawi
akapokea mwanamke ambaye
yuko Tanzania lakini aligoma
kunitajia jina lake.Nilimuuliza
kama anamfahamu Abu Zalawi
akakana kumfahamu,alikana
kuwa na rafiki au mtu
anayemfahamu mwenye jina la
Abu Zalawi.Baadae akanipigia
simu akanitaka nimtumie
picha ya Abu Zalawi na hapo
ndipo kilipotokea kizaa zaa”
Najma akanyamaza kidogo
halafu akasema
“Kwa muda wa miezi
mitatu tumekuwa tukizunguka
sehemu mbali mbali duniani
tukifanya utalii.Katika safari
yetu hiyo tulipiga picha nyingi
sana lakini kitu cha ajabu ni
kwamba nilipozitafuta picha
tulizopiga mimi na Abu katika
safari yetu sikupata hata picha
moja.Nilihifadhi picha nyingi
katika kompyuta yangu
nyingine zilikuwepo katika
kamera na hata katika simu
yangu lakini huko kote
hakukuwa na picha hata
moja.Hiki kitu
kimenishangaza sana mama
namna picha
zilivyotoweka.Hakuna mtu
yeyote aliyeingia chumbani
kwetu zaidi yetu sisi hivyo
naamini aliyefuta picha hizo
lazima atakuwa Abu
Zalawi.Nimejiuliza maswali
mengi kwa nini akafuta picha
zetu?Nimeshindwa kupata jibu
ndiyo maana nataka unieleze
kuhusiana na huyu mtu ni wa
aina gani? Tafadhali mama”
akasema Najma na Habiba
akavuta pumzi ndefu
“Mambo yamekwisha
haribika.Tayari Najma
amekwisha hisi kitu kuhusu
Abu zalawi.Nadhani ni wakati
wake wa kuufahamu ukweli”
akawaza Habiba
“Najma kuna jambo
ambalo nataka nikueleze
kuhusu Abu Zalawi.Kwanza
kabisa ni kwamba Abu Zalawi
hatarejea tena.Ameondoka”
akasema Habiba na sura ya
Najma ikabadilika
“Unasemaje mama ?!
akauliza Najma
“Najma Abu Zalawi
hatarejea tena.Ameondoka”
“Mama sijakuelewa”
“Najma kuna mambo
mengi ambayo huyafahamu
kuhusu mimi” akasema
Habiba na kumtazama Najma
ambaye alionekana
kuchanganyikiwa
“Maisha yangu yamejaa
siri nyingi ambazo nyingine
nitakueleza lakini nyingine
nitakwenda nazo
kaburini.Nina sababu yangu ya
kufanya hivyo” akasema
Habiba na kunyamaza tena
akamtazama Najma
“Siri ya kwanza ni kuhusu
huu utajiri wangu.Utajiri
wangu huu ambao ninautumia
katika kufadhili makundi
mbali mbali ya kigaidi
niliurithi kwa baba yake Abu
Dahir lakini naye utajiri huu
hakuupata hivi hivi.Leo
nitakupa siri ya huu utajiri
wangu” akasema Habiba na
kunyamaza akamtazama
Najma
“Asili ya utajiri wangu huu
ni Marekani.Wao ndio
waliomuwezesha baba yake
Abu Dahir na alipofariki mimi
ndiye niliyerithi utajiri
huo.Kwa nini Marekani
walimpa utajiri huu mkubwa?
Akauliza Habiba lakini Najma
hakujibu kitu chochote
“Ndani ya shirika la
ujasusi la Marekani CIA kuna
kitengo ambacho
kinajishughulisha na
mashirikiano na makundi ya
magaidi.Kitengo hiki ndicho
kilichotuwezesha kuwa na
utajiri huu mkubwa na lengo
kuu la kutupa utajiri huu ni
kwa ajili ya kuyafadhili
makundi ya kigaidi katika
operesheni zao mbali mbali
zenye maslahi kwa Marekani
hivyo basi kwa muda huu wote
nimekuwa nikifanya kazi na
Marekani.Ufadhili huu ambao
tumekuwa tukiwapa makundi
ya magaidi ni maelekezo ya
Marekani” Sura ya Najma
ilibadilika alifungua mdomo
wake akataka kusema kitu
lakini maneno hayakutoka
“Nimekustua
Najma.Lakini umefika wakati
wa wewe kufahamu kila
kitu.Nimeamua kukushirikisha
siri chache kuhusu mimi”
akasema Habiba
“Nimefanya kazi na
Marekani kwa muda mrefu na
sasa nimechoka.Sitaki
kuendelea tena kuwa mfadhili
wa makundi ya kigaidi ndiyo
maana nikamleta Abu Zalawi
ili aweze kulimaliza jambo
hili.Kuna mambo ambayo
huyafahamu kuhusu Abu
Zalawi na leo
nitakufahamisha”Habiba
akanyamaza kidogo halafu
akasema
“Abu Zalawi jina lake
halisi anaitwa Mathew
Mulumbi ni mtanzania”
“Mungu wangu ! akasema
Najma.Habiba akaendelea
“Abu Zalawi si gaidi kama
nilivyokufahamisha awali bali
ni jasusi”
“Jasusi ? ! Najma
akashangaa
“Ndiyo ni jasusi.Najma
kuna mengi ambayo ningetaka
kukueleza lakini nitazungumza
nawe siku nyingine hayo
machache yanatosha kwa
leo.Kubwa ambalo nataka
ulifahamu ni kwamba Abu
Zalawi au Mathew alikuwa
hapa kwa ajili ya kazi maalum
na sasa wakati wake umefika
wa kwenda kutekeleza
majukumu yake na kazi hiyo
anayokwenda kuifanya ni kwa
ajili ya usalama wenu wewe na
kaka yako.Abu ndie mkombozi
wenu kwani akifanikiwa katika
misheni hiyo itakuwa ni
salama yenu lakini akishindwa
maisha yetu yatakuwa
shakani.Abu Zalawi hatarudi
tena”
“Unamaanisha nini
mama?
“Misheni anayokwenda
kuifanya ni misheni ya hatari
kubwa sana na uhakika wa
kurudi salama katika misheni
hiyo ni mdogo” akasema
Habiba
“Mama kwa nini
ukanifanyia hivi? Kwa nini
ukanitaka niolewe na Abu
Zalawi wakati ukijua ni mtu wa
namna gani?Kwa nini
ukaniacha nikazama
mapenzini na Abu Zalawi
halafu unamuondoa? Akauliza
Najma
“Nilikuwa na sababu
zangu kukutaka uolewe na Abu
Zalawi.Bila kuolewa naye
asingekubali kukaa nasi hapa
kwa ajili ya misheni ambayo
nimemtuma akaifanye.Amekaa
nasi hapa hadi ulipofika muda
wake wa kuondoka kwa sababu
yako”akasema Habiba
“Mama wewe ni
shetani.Una roho ya kishetani !
Huna ubinadamu hata
kidogo.Mama wewe ni
mkatil………….” Akasema
Najma na Habiba akamnasa
kofi
“Haya yote niliyoyafaya ni
kwa sababu yenu.Nafanya kila
hatua kuwalindeni ili muwe
salama vinginevyo ninyi nyote
hivi sasa
mngekwishauawa.Kuanzia
sasa anza kuzoea hali hii.Abu
Zalawi ana mke wake na
watoto hawezi kurudi
tena.Kumpoteza Abu si
mwisho wa mais…”akasema
Habiba na Najma akatoka
mbio huku akilia.
“Nimemuumiza sana
Najma.Sikutaka aufahamu
ukweli hu lakini kwa hatua
aliyokuwa ameifikia ni lazima
aufahamu ukweli.Itamchukua
muda mrefu kukubaliana na
ukweli h….” Habiba akastuka
baada ya mmoja wa walinzi
wake kuingia mle ndani
akikimbia
“Kuna nini ?akauliza
Habiba kwa wasi wasi.
“Mama umesikika mlio wa
risasi katika nyumba ya Abu
Zalawi ! akasema Yule mlinzi
na Habiba akatoka mbio
akiongozana na Yule mlinzi na
kukuta walinzi wengine tayari
wamekwisha fika katika
nyumba ile ya Mathew.Habiba
akiwa na wale walinzi
wakaenda chumbani kwa
Najma walinzi wakavunja
mlango akaingia ndani.Najma
alikuwa amelala katika dimbwi
la damu.Hakuwa na uhai
tena.Alijipiga risasi ya
kichwa.Habiba akaanguka na
kupoteza fahamu.
MPENZI MSOMAJI USIKOSE
SEHEMU IJAYO……
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom