Riwaya: Siri

SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 1
KAMPALA – UGANDA
Barabara iliyolekea katika
kanisa la utukufu wa Mungu
ilifurika mamia ya waumini
waliokuwa wakielekea katika
kanisa hilo kubwa jijini
Kampala kuhudhuria ibada ya
Jumapili.Ni saa tatu za
asubuhi lakini tayari kanisa
lilikaribia kujaa huku mamia
ya watu bado wakiendelea
kujongea kanisani hapo.Kania
la Utukufu wa Mungu ni moja
ya kanisa lililojizolea umaarufu
mkubwa sana katika jiji la
Kampala na Uganda kwa
ujumla kutokana na miujiza
mikubwa inayotendeka
kanisani hapo chini ya
mtumishi wa Mungu nabii
Yeremia Aganda.Watu wenye
matatizo mbali mbali
wamekuwa wakiombewa na
kufanikiwa kutatua matatizo
yao kama vile
magonjwa,kupata watoto,kazi
n.k.
Saa nne za asubuhi ibada
kuu ya jumapili ilianza
ikiongozwa na nabii mkuu
Yeremia Aganda,akisaidiana
na wachungaji wasaidizi
wake.Ulifika wakati wa kusifu
na wimbo uliopigwa na bendi
maalum ya kanisa uliwafanya
karibu watu wote mle kanisani
kusimama na kushangilia kwa
shangwe wakimsifu
Mungu.Wakati wimbo ule wa
sifa ukiendelea huku watu
wakicheza kwa furaha,mlipuko
mkubwa wa bomu ukatokea na
jengo la kanisa
likatetemeka,sekunde mbili
baadae ukatokea mlipuko
mwingine.Sekunde nne
milipuko mingine miwili
mikubwa zaidi ikasikika na
kulitetemesha kanisa.
Watu waliokuwa nje ya
kanisa wakifuatilia ibada
walianza kukimbia hovyo
kuokoa maisha yao mara
ghafla yakatokea magari
mawili, sehemu za juu za
magari yale zikafunguliwa
wakajitokeza watu waliofunika
nyuso zao wakiwa na bunduki
kubwa kisha wakaanza
kumimina risasi hovyo kwa
watu wale waliokuwa
wakikimbia kunusuru maisha
yao.Eneo la kanisa liligeuka
kama uwanja wa vita kwa
namna watu walivyokuwa
wakianguka kutokana na risasi
zilizotoka kwenye bunduki
nzito za wale jamaa waliokuwa
katika magari.Tukio lile la
kuwashambulia watu kwa
risasi lilidumu kwa takribani
dakika tano kisha magari yale
yakaondoka kwa kasi na
kuacha idadi kubwa ya watu
wakiwa wameanguka chini na
wengi wao wakiwa wamefariki
dunia
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 2
Saa moja za jioni Jenerali
Paul Mukasa Rais wa mpito wa
Uganda alijtokeza katika
televisheni ya taifa akiwa
ameongozana na baadhi ya
viongozi wa jeshi kwa lengo la
kulihutubia taifa
“Ndugu zangu Waganda,
leo Saa nne za asubuhi
wakati ibada ikiendelea
katika kanisa la Utukufu wa
Mungu,mabomu manne
yalilipuka kanisani hapo na
kusababisha vifo vya watu
wengi waliokuwa ndani ya
kanisa hilo wakiadhimisha
ibada ya jumapili.Muda
mfupi baada ya mabomu
hayo kulipuka ndani ya
kanisa,walijitokeza watu
wengine wakiwa ndani ya
magari mawili na kuanza
kuwamiminia risasi waumini
waliokuwa wakikimbia
kuokoa maisha yao na kuua
watu wengi.Taarifa
niliyoipata muda mfupi kabla
ya kuja hapa kuzungumza
nanyi, jumla ya watu mia
mbili ishirini wamepoteza
maisha yao siku ya leo na
wengine mia nne
wamejeruhiwa wengine
vibaya sana.Ninavishukuru
vikosi vyetu vya ulinzi na
uokozi vilivyofika haraka
sana eneo la tukio na kufanya
kazi kubwa ya uokozi na
kuwakimbiza majeruhi
haraka sana hospitali.
Ndugu zangu,uchunguzi
wa haraka uliofanywa
unaonyesha kwamba
kilichotokea leo ni shambulio
la kujitoa mhanga.Bado
hatujafahamu watu
waliofanya tukio hili ni akina
nani na wametoka
wapi.Uchunguzi wa kina
unaendelea na tutawajulisha
matokeo ya uchunguzi huo
pale utakapokuwa
umekamilika.
Walichokifanya hawa
watu wenye roho za
kishetani,hakikubalili na
hakivumiliki.Ni kinyume cha
ubinadamu na ninawaahidi
ndugu zangu waganda
tutawasaka kokote waliko
watu hawa na kuwashikisha
adabu.Hakuna aliyeshiriki
katika mauaji haya ya
kinyama atabaki
salama.Tutahakikisha wote
wanatiwa nguvuni.Hakuna
jiwe litasalia juu ya
jiwe.Hatutamuogopa
mtu,kikundi au taifa.Yeyote
aliyeshiriki katika jambo hili
la kikatili atakutana na
mkono wetu.Ninacho waomba
ndugu zangu waganda muwe
watulivu katika wakati
huu,vyombo vya uchunguzi
viko kazini vikiendelea na
uchunguzi wa kina wa jambo
hili ili kuwabaini mashetani
hawa ni akina nani.Lengo la
watu hawa ni kuvuruga
umoja wetu hivyo nawaomba
ndugu zangu
mshikamane.Tuendelee na
shughuli zetu kama kawaida
na pale kutakapokuwa na
jambo lolote la kuwajulisha
tutafanya hivyo mara moja.
Kwa wale wote
waliopoteza ndugu zao katika
shambulio la leo, tunawapa
pole sana.Serikali iko pamoja
nanyi katika wakati huu
mgumu mnaoupitia na
tunawaahidi kwamba serikali
itagharamia mazishi ya
ndugu zetu wote waliopoteza
maisha yao.Maandalizi
yanaendelea na pale
yatakapokamilika
mtajulishwa
Kwa mara nyingine
narudia tena kuwapeni poleni
sana waganda wote
Mungu ibariki Uganda
Ahsanteni kwa
kunisikiliza
Hii ilikuwa ni hotuba fupi
ya Rais wa mpito wa Uganda
Jenerali Paul Mukasa kwa
wananchi wa Uganda
Mara tu alipomaliza kutoa
hotuba yake kwa taifa,Jenerali
Paul Mukasa akapewa taarifa
kwamba wakati akihutubia
umetokea mlipuko mwingine
wa bomu katika nyumba ya
watawa waliokuwa waliokuwa
wamekusanyika katika kanisa
lao dogo wa ajili ya ibada ya
usiku.Jenerali Paul Mukasa
akazidi
kuchanganyikiwa.Damu
iliendelea kumwagika katika
jiji la Kampala.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 3
Jumatatu asubuhi,Jiji la
Kampala lilikuwa katika
simanzi kubwa kufuatia
mashambulizi makubwa
yaliyofanyika siku
iliyopita.Karibu kila kona ya
jiji la Kampala kulikuwa na
vilio.Tukio la kuuawa kwa
watawa arobaini waliokuwa
katika ibada ya usiku
liliendelea kuwapa hofu kubwa
wakazi wa jiji la Kampala.Bado
haikujulikana ni nani
aliyekuwa anafanya mauaji
yale makubwa bila huruma na
kwa nini.
Wakati wakazi wa jiji la
Kampala wakiwa katika
simanzi na hofu kubwa
kufuatia mashambulio yale ya
mabomu,basi lililobeba
wanafunzi wa shule ya msingi
inayomilikiwa na kanisa
lilipuliwa na bomu wakati
likipeleka wanafunzi
shuleni.Zaidi ya wanafunzi
arobaini walipoteza maisha
katika shambulio hilo.Damu
iliendelea kumwagika katika
jiji la Kampala.
Muda mfupi baada ya gari
la wanafunzi kulipuliwa kwa
bomu,katika mitandao ya
kijamii ilianza kusambaa video
ikimuonyesha mtu mmoja
aliyeficha sura yake
akiwafahamisha wananchi wa
Uganda kwamba matukio yale
ya mashambulio ya mabomu
yaliyotokea ni kulipiza kisasi
kwa mauaji ya kiongozi wao
wa dini aliyeuawa.Mtu Yule
aliendelea kutoa vitisho
kwamba mashambulio yale
yaliyotokea ni mwanzo tu na
wataendelea kufanya
mashambulio kila siku
wakilipiza kisasi.
Wakati video ile ikiendelea
kusambaa na kuzidisha hofu
kwa wakazi wa jiji la
Kampala,katika redio
inayojulikana kama Utukufu
Redio,inayomilikiwa na kanisa
la utukufu wa Mungu aliwasili
askofu Nobert Odongo
anayesimamia redio hiyo.Sura
yake ilionyesha hasira
kali.Alielekea moja kwa moja
katika chumba cha matangazo
na kuamuru muziki wa
maombolezo uliokuwa
unapigwa usimamishwe
akavaa spika za masikioni na
kuanza kutangaza.
“Ndugu wakristu
wenzangu bila kujali dhehebu
unakotoka,wale wote
mnanisikiiza muda huu ambao
mmeumizwa na unyama
unaoendelea hapa nchini
kwetu,nimekuja hapa
kuzungumza nanyi na
ninaomba mnisikilize kwa
makini sana.Acha shughuli
zako zote na sikiliza ujumbe
huu kwa makini.
Kama mnavyofahamu,
jana kumefanyika shambulio la
bomu katika kanisa letu la
Utukufu wa
Mungu.Tumepoteza watu
wengi katika shambulio la jana
na miongoni mwao wako
watumishi wa Mungu
waliokuwa wakihudumu katika
ibada ya jana akiwemo mkuu
wa kanisa letu,Nabii mkuu
Yeremia Aganda ambaye
ameumia vibaya sana.Katika
mwendelezo wa mauaji hayo,
jana usiku limefanyika
shambulio lingine katika
kanisa nyumba ya watawa
waliokuwa wamekusanyika
kwa ibada ya jioni.Watu hawa
wasio na hata chembe ya
huruma hawakuishia hapo
wameendelea na umwagaji wa
damu ambapo asubuhi ya leo
watoto wetu waliokuwa
wakienda shuleni wameuawa
kikatili kabisa baada ya basi
lao kushambuliwa kwa
bomu.Huu ni ukatili mkubwa
uliovuka kiwango cha ukatili
kwa binadamu.
Ndugu zangu
mashambulio haya yote
yaliyotokea yamelenga watu
wa imani moja tu,wakristu.Hii
ni chuki ya wazi kabisa
inayojidhihirisha dhidi
yetu.Waliofanya mauaji haya
wanafahamika ni akina nani
na wanajitapa kuendelea
kufanya mashambulio zaidi na
zaidi dhidi yetu.Wanafahamika
ni akina nani,wako wapi lakini
serikali yetu imeshindwa
kuchukua hatua za dhati za
kuwadhiti wasiendelee na
kumwaga damu yetu.Kwa
kuwa serikali ya kijeshi
imeshindwa kutulinda dhidi ya
hawa wanaotuwinda
watumalize basi umefika
wakati wa sisi wenyewe
kuchukua hatua za kuanza
kujilinda na kupambana
nao.Hatuwezi kuendelea
kuuawa huku tukiona,lazima
tuchukue hatua za haraka sana
kujilinda.Ndugu zangu
waumini wa kanisa la utukufu
wa Mungu na wakristu wa
madhehebu yote kokote mliko
nawaomba inukeni twendeni
tukapambane na wale
wanaotaka kutumaliza.Kokote
ulipo unaponisikiliza acha kila
unachokifanya hivi sasa.Kama
uko nyumbani funga nyumba
yako,kama uko katika biashara
funga biashara yako elekea
katika kanisa la utukufu wa
Mungu tutakusanyika pale
ambapo damu ya wenzetu
imemwagika.Ukisikia tangazo
hili mjulishe na
mwenzako.Mshike mkono
mwenzako muongoze
muelekee kanisa la utukufu wa
Mungu”
Yalikuwa ni maneno
kutoka kwa askofu Nobert
Odongo akiwataka watu wa
dini ya kikristu kukusanyika
katika kanisa la utukufu wa
Mungu ambako jana yake
kulitokea milipuko ya mabomu
na kuua watu wengi waliokuwa
katika ibada.
Baada ya maneno yale,
askofu Nobert akatoka katika
chumba cha matangazo
akaelekea katika gari lake
lakini kabla hajaingia garini
simu yake ikaita akatazama
mpigaji alikuwa ni Joshua
Lulangwa mwenyekiti wa
chama cha siasa cha ukombozi
wa Uganda.
“Nilikuwa nakusikiliza
askofu.Umefanya vizuri
sana.Naamini tayari watu
wameanza kuelekea mahala
ulipowaelekeza
wakutane.Tayari silaha
zimeanza kupakiwa katika
magari tayari kupelekwa
sehemu ya kukutania.Askofu
kumbuka mara tu vurugu
zitakapoanza ondoka haraka
sana,helkpota iko tayari
inatusubiri tuondoke”
akasema Joshua
“Nimekuelewa
Joshua.Tutakutana muda huo”
akasema askofu Nobert
“Kila la heri” akasema
Joshua na kukata simu.Askofu
Nobert akaingia katika gari na
kuondoka kuelekea nyumbani
kwake
Tamko lile la askofu
Nobert lilisambaa kwa kasi
kubwa kwani redio utukufu ni
moja kati ya redio yenye
wasikilizaji wengi sana jijini
Kampala.Kama alivyoelekeza
askofu Nobert,watu walianza
kuhamasishana kuelekea
katika kanisa la utukufu
walikoelekezwa
wakutane.Makundi ya vijana
na waumini wa dini ya kikristu
walielekea huko kwa haraka na
ndani ya saa moja tayari
uwanja mkubwa wa mpira ulio
karibu na kanisa ulijaa watu na
wengine wengi waliendelea
kuelekea hapo.Utepe wa njano
kuzuia watu kuingia kanisani
ulizungushwa kanisa zima ili
kuipa timu ya wachunguzi
nafasi ya kufanya kazi yao.
Askofu Nobert aliwasili
kanisani akapokewa na
wachungaji akapanda juu ya
meza akashika kipaaza sauti na
kuongoza nyimbo kadhaa
halafu akasema
“Ninawashukuru sana
ndugu zangu kwa kuitika wito
kwa haraka.Pamoja na
kufiwa,pamoja na huzuni
kubwa mliyonayo lakini
mmeitika wito na kufika kwa
haraka sana.Kama mlivyosikia
katika maelezo niliyoyatoa
redioni……” kabla hajaendelea
magari matatu ya jeshi yalifika
na watu wote wakageuka
kuyatazama.
“Msiogope ndugu
zangu.Kuweni majasiri.Hao
waliofika hapa
hawatatutafanya chochote.Hao
ni wale walioshindwa
kutulinda na kuacha tukiuawa
kama wadudu.Hata kama
wamekuja na bunduki na
silaha za maangamizi lakini
kuweni majasiri.Daudi
alipambana na Goliath
aliyekuwa amejihami kwa
silaha hali yeye akiwa na mawe
tu na
akashinda.Ninawahakikishia
hata ninyi msitishwe na
magari yao,msitishwe na
silaha zao tunao uwezo wa
kuwashinda kama Daudi
alivyomshinda Goliath !
akasema askofu Nobert na
kuwapandisha hasira waumini
wake
“Nataka hapo mlipo kila
mmoja ainame aokote
kilichopo chini yake.Kama
kuna jiwe okota,kama kuna
tofali okota na kwa pamoja
tuwaelekee wale wanajeshi
tuwaondoe eneo
hili.Nikihesabu mpaka tatu
tunaanza kuwashambulia bila
kukoma ! akasema Nobert na
waumini wake wakaitika kwa
nguvu kisha akahesabu hadi
tatu na mvua ya mawe
ikaanza.Waumini
hawakuogopa walianza
kuvurumisha mawe kwa
wanajeshi wale na kuvunja
vioo vya magari yao na
kuwalazimu wanajeshi wale
kuondoka haraka eneo lile.
“Tumeshinda !
Tumeshinda ! Tumeshinda !
akapaaza sauti askofu Nobert
huku waumini wake ambao
waliendelea kumiminika kwa
wingi wakishangilia
“Bwana aliye hai
ametushindia.Kama tumeweza
kuwashinda wale watu
waliokuwa na silaha nzito
hatuwezi kushindwa kwa hawa
wanaotuua ! akasema na
waumini wakashangilia kwa
nguvu
“Ndugu zangu katika yale
magari matatu pale kuna
silaha.Kila mmoja atapita pale
achukue kile kinachomfaa iwe
panga,kisu,nyundo au
chochote
atakachoona.Tunawafahamu
wanaotuua na tunawafuata
huko huko waliko.Tutabomoa
nyumba zao za kuabudia na
kuwaondoa kabisa katika jiji
hili.Tumeelewana? akauliza na
waumini wale wakaitika kwa
nguvu kisha wakaanza
kuelekea yalipo magari matatu
aina ya fuso na kila mmoja
akapewa silaha
aliyoihitaji.Kulikuwa na zana
mbali mbali kama
visu,mapanga,mashoka.Silaha
zile hazikutosha kwani watu
walikuwa wengi sana na
askofu Nobert akawataka
waumini wake waelekee ulipo
msikiti ambao haukuwa mbali
na pale kanisani.Akiwa na
shoka begani aliwaongoza
waumini wake wakatembea
kwa haraka wakaelekea katika
msikiti ule na kuanza
kuubomoa halafu
wakauchoma moto.Askofu
Nobert akawaelekeza waumini
wake kuelekea katika msikiti
mwingine.
Taarifa za kile
kilichofanywa na waumini wa
kanisa la utukufu wa
Mungu,zilisambaa kwa kasi na
kuwafanya waumini wa dini ya
kiislamu nao kuanza kujipanga
kwa ajili ya kupambana na
kundi hilo kubwa la waumini
wa kanisa la utukufu
waliokuwa wanavamia
kuharibu na kuchoma misikiti.
Hadi jua lilipoanza
kuzama,jiji la Kampala
lilikuwa tayari katika
machafuko makubwa
yakihusisha makundi ya
waumini wa dini za kikristu na
kiislamu.Watu kadhaa tayari
walikwisha poteza maisha
kufuatia vurugu hizo.Jeshi la
Uganda liliingia mtaani
kujaribu kuzima vurugu hizo
za wafuasi wa dini lakini tayari
vurugu hizo zilikwisha kuwa
kubwa na kusambaa katika
sehemu mbali mbali za jiji la
Kampala.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 4
Usiku kucha mapigano
yaliendelea kati ya waumini wa
dini wakishambuliana na kwa
upande wa pili
wakishambuliana na vikosi vya
jeshi vilivyokuwa vikijaribu
kutuliza vurugu hizo.
Kijua kilianza kuchomoza
huku hali ikizidi kuwa tete
katika jiji la Kampala.Vurugu
ziliripotiwa kuendelea katika
sehemu mbali mbali za jiji hilo
na kwa asubuhi hii si Kampala
pekee bali vurugu zilianza
kuripotiwa katika miji mingine
mikubwa.Vikosi vya jeshi
vikisaidiana na vikosi vingine
vya ulinzi vilisambaa mitaani
lakini makundi ya watu
waliokuwa na silaha mbali
mbali za jadi na za moto
yaliendelea kuleta upinzani
mkubwa sana kwa vikosi hivyo
na kulazimisha vikosi hivyo
vya jeshi kutumia silaha za
moto.
Saa mbili za asubuhi
iliripotiwa kundi kubwa la
watu kuvamia kituo cha polisi
wakaua askari na kuiba silaha
ambazo walizitumia katika
mapambano yake na vikosi vya
jeshi.Hadi ilipotimu saa nne za
asubuhi iliripotiwa wanajeshi
ishirini na saba walikuwa
wamepoteza maisha.Kumi na
nne walifariki baada ya gari
lao kushambuliwa kwa bomu
wakati wakielekea katika
viunga vya jiji la Kampala,
wengine kumi na tatu
waliuawa wakati wakikabiliana
na watu waliokuwa na silaha
za moto.Vifo vya wanajeshi
wale vilipelekea kutolewa kwa
amri ya kutumia nguvu zaidi ili
kudhibiti vurugu zile amri
ambayo iliwafanya wanajeshi
kumpiga risasi kila aliyejaribu
kuwashambulia.
Katika mji wa Jinja nako
vile vile kuliripotiwa kuvamiwa
kwa ghala la silaha na silaha
nyingi kuibwa.Kadiri muda
ulivyozidi kusonga ndivyo
machafuko yalivyozidi kuwa
makubwa.Wakati waumini wa
dini wakiendelea
kushambuliana wakiuana na
kuchomeana nyumba za
ibada,liliibuka kundi lingine la
watu waliokuwa na silaha za
moto ambao walikuwa
wanavamia kupora na
kuchoma majengo hasa ya
serikali.Hawa walikuwa
wakitembea na bendera ya
Uganda huku wakiimba
kutoutambua utawala wa
kijeshi.Taratibu kundi hili la
tatu nalo lilianza kuungwa
mkono na watu wengi
Saa sita za mchana ubalozi
wa Marekani jijini Kampala
ulivamiwa na kundi kubwa la
watu wenye silaha hivyo
kuwalazimu wanajeshi
waliokuwa wakilinda jengo la
ubalozi huo kutumia risasi za
moto kutaka kuwatawanya
watu hao lakini watu wale
walikuwa wengi huku
wakirusha mabomu ya
kurusha kwa mkono ndani ya
ubalozi na kuwalazimu
wanajeshi wale kuomba
msaada kutoka kwa jeshi la
Uganda.Wakati wakisubiri
msaada wa jeshi kundi lile la
watu walifanikiwa kuvunja geti
na kuingia ndani ya jengo na
kuua kila waliyemkuta kisha
wakalichoma jengo la ubalozi
huo.Vikosi vya jeshi la Uganda
vilipofika vilikuta jengo la
ubalozi huo likianza
kuungua.Magari ya zimamoto
yalifika haraka sana na
kuuzima moto ule ulioanza
kusambaa katika ghorofa ya
kwanza.Jumla ya maiti kumi
na nne zilitolewa katika jengo
lile.
TANGA – TANZANIA
Katika moja ya bandari
bubu jijini Tanga,jahazi lilitia
nanga,watu sita wakashuka
haraka haraka wakiwa na
mabegi makubwa migongoni
mwao wakaingia katika gari
lililokuwa linawasubiri
wakaondoka.Hakukuwa na
mazungumzo ndani ya lile gari
wakaenda moja kwa moja
katika nyumba Fulani
“Karibuni sana ndugu
zangu”akasema jamaa mmoja
mwembamba aliyekuwa na
ndevu nyingi
“Ahsante sana” akajibu
jamaa mwingine ambaye
alionekana kiongozi wa wale
jamaa waliokuja na jahazi.
“Mambo yanakwendaje
hapa? akauliza
“Kila kitu tayari
kimekamilika.Wawili
watatumia piki piki kwenda
katika shule ya Mt
Bernadetha,wengine tutatumia
gari” akasema Yule jamaa
mwenyeji na kuweka mezani
ramani ya jiji la Tanga
wakaelekezana halafu
wakaingia katika chumba
kimoja wapo wakayafungua
mabegi yao wakaanza
kuunganisha silaha
walizokuwa wamebeba katika
mabegi yao.Kila mmoja
alipohakikisha silaha yake iko
tayari wakaelekea katika gari
moja lililoandaliwa kwa ajili ya
shughuli wanayotaka
kuifanya.Watu watano
wakaingia ndani ya gari lile
zuri aina ya Rav 4 lenye rangi
nyeusi wengine wawili
wakapanda piki piki kisha
wakaondoka.
Nabii Jonathan Mbegela
wa kanisa la Calvary Chapel
alikua ofisini kwake akiendelea
kusikiliza watu mbali mbali
wenye matatizo na kufanya
maombi maalum ya mtu
mmoja mmoja mara ikasikika
milio ya risasi nje ya ofisi
yake.Akamuacha Yule mtu
aliyekuwa akimuhudumia
akafungua mlango akatoka nje
kuchungulia kuna nini.
Alipofungua tu mlango
akapigwa risasi ya kichwa
akaanguka chini.Risasi
zilirindima kanisani pale na
takribani watu arobaini na
mbili waliofika pale kwa ajili
ya huduma ya maombi
wakauawa.Risasi zilirindima
kanisani pale kwa takribani
dakika kumi na wale jamaa
walipomaliza kile walichokuja
kukifanya wakaingia katika
gari lao na kuondoka kwa kasi
kubwa.Gari tatu zilizojaa
askari polisi zilifika haraka
sana baada ya kupata taarifa
ya tukio lile lakini tayari
wavamizi wale
walikwishatoweka.
Wakati vilio vikitanda
katika kanisa la Calvary
Chapel,katika shule ya msingi
ya Mt.Bernadetha kengele ya
dharura iligonga na wanafunzi
wakaanza kutoka madarasani
wakikimbilia sehemu ya
kukuanyikia.Waalimu
walistuka na kutoka
kuchungulia nani aliyegonga
kengele ile na ndipo
wakagundua aliyegonga
kengele hakuwa mtumishi wa
ile shule.Mara ghafla kutoka
katika mti wa maua akatokeza
jamaa mmoja akiwa na
bunduki na kuanza kumwaga
risasi.Yule jamaa aliyegonga
kengele naye akatoa bunduki
kutoka katika begi lake la
mgongoni naye akaanza
kuvurumisha risasi.Wanafunzi
walianza kuanguka kama
kumbi kumbi.Mvua ya risasi
ilidumu kwa dakika tano
halafu watu wale wakaweka
bunduki zao katika mabegi ya
mgongoni na kuondoka
wakitumia piki piki nyeusi .
Baada ya kufanya mauaji
yale watu wale wakarejea
katika ile nyumba
walimofikia.Nusu saa baadae
likafika gari moja zuri
lililokuwa na vioo vyeusi
akashuka jamaa mmoja
aliyevalia suruali ya jeans na
kufunika kichwa chake kwa
kofia.
“Hongereni sana kwa kazi
nzuri mliyoifanya.Imekuwa ni
kazi yenye mafanikio
makubwa.Watanzania
hawajazoea kuyaona mambo
kama haya yaliyotokea leo na
nchi imetikisika.Tumeanza
vizuri lakini bado tuna kazi
kubwa ya kufanya.Si kazi
nyepesi kuwafarakanisha
watanzania kwa kutumia dini
lakini tutajitahidi.Tumeanza
na kanisa,jioni ya leo
tunahamia katika
msikiti.Mpaka sasa wakristu
wanaamini waislamu ndio
waliofanya shambulio katika
kanisa na kuua
waumini.Tayari tumepanda
mbegu ya chuki.Jioni ya leo
tutavamia nyumba ya shehe
mkuu wa mkoa wa
kumuua.Hii itaongeza mafuta
kwenye moto.Waislamu
wataamini ni wakristo
wamefanya mauaji hayo na
watajipanga kulipiza kisasi na
machafuko yataanzia
hapo.Tayari kuna watu
wamekwisha andaliwa kwa
ajili ya kuhamasisha suala
hilo” akasema Yule jamaa
kisha akwaaga na kuondoka.
************
Taarifa kubwa ambayo
ilitawala vyombo vya habari
duniani ni machafuko
yanayoendelea nchini
Uganda.Hali iliendelea kuwa
tete na tayari machafuko
yalisambaa katika miji yote
mikubwa ya nchi hiyo huku
vifo vingi vikiendelea
kuripotiwa.Hali ikiwa hivyo
nchini Uganda,nchini
Tanzania nako mambo
hayakuwa shwari hata
kidogo.Jijini Tanga yalifanyika
mauaji katika kanisa kubwa la
Calvary Chapel ambapo
kiongozi wa kanisa hilo Nabii
Jonathan Mbegela pamoja na
waumini wake thelathini na
mbili waliuawa na watu
waliokuwa na silaha.Shule ya
msingi ya Mt.Bernadetha nayo
ilishambuliwa na watu wenye
silaha na takribani wanafunzi
ishirini na tatu walipoteza
maisha katika shambulio
hilo.Wakazi wa jiji la Tanga na
watanzania kwa ujumla
waliingiwa na hofu kubwa ya
kutokea yale yaliyokuwa
yanaendelea nchini Uganda.Ili
kudhibiti machafuko yoyote
yasitokee serikali ilimwaga
polisi wa kutosha katika jiji la
Tanga.Nyumba zote za ibada
ziliwekewa ulinzi kwa hofu ya
makundi ya waumini kuvamia
kwa lengo la kulipiza kisasi.
Pamoja na ulinzi mkali
uliowekwa katika nyumba zote
za ibada ndani ya jiji la Tanga
lakini asubuhi wakazi wa jiji
hili waliamshwa na taarifa ya
kustusha mno.Sheikh mkuu
wa mkoa wa Tanga na familia
yake waliuawa usiku kwa
kupigwa risasi.Baada ya
mauaji hayo kufanyika
iliachwa barua mezani ambayo
ilieleza kwamba wamefanya
mauaji yale kulipiza kisasi
kufuatia mauaji yaliyofanywa
katika kanisa la Calvary Chapel
na katika shule ya msingi ya
Mt.Bernadetha.Mauaji yale
yalizua taharuki kubwa
miongoni mwa waumini wa
dini ya kiislamu.Shughuli
zilisimama katika jiji la Tanga
watu wakihofia ualama
wao.Mkuu wa jeshi la polisi
nchini Tanzania aliwasili jijini
Tanga kwa helkopta akafika
katika nyumba ya Sheikh
mkuu wa mkoa aliyeuawa kwa
kupigwa rissi na familia yake
yote halafu akaelekea katika
kanisa la Calvary Chapel na
katika shule ambako waliuawa
wanafunzi.Baada ya
kutembelea sehemu hizo zote
mkuu huyo wa jeshi la polisi
akawa na kikao cha ndani na
makamanda wa polisi kikao
kilichochukua saa tatu kisha
akakutana na waandishi wa
habari na kwa kupitia kwao
akawataka watanzania wawe
watulivu kwani jeshi la polisi
lilikuwa kazini kuwasaka watu
au kikundi cha watu
wanaoendesha mauaji yale.
Nusu saa baada ya mkuu
wa jeshi la polisi nchini
Tanzania kutoa tamko,mmoja
wa wanasiasa vijana kabisa
ambaye anatokea mkoa wa
Tanga akaandika katika
ukurasa wake wa mtandao wa
twitter
“Hii haikubaliki na
haivumiliki.Kiongozi wetu
hawezi kuuawa kinyama
namna hii halafu tunaambiwa
tusubiri uchunguzi ufanyike
wakati wauaji
wanafahamika.
Wametuchokoza na hatuwezi
kukaa kimya lazima
tujibu.Twendeni sisi wenyewe
tukawatafute wale wenye nia
ovu dhidi yetu”
Mwanasiasa Yule kijana
hakuishia hapo tu,aliwatumia
jumbe mashehe wa mkoa wa
Tanga ambazo ziliendelea
kuwahamasisha wawashawishi
waumini wao kuanzisha
vurugu dhidi ya wale ambao
wanadaiwa kumuua kiongozi
wao.
Saa nane za mchana jiji la
Tanga lilijikuta katika
machafuko makubwa,waumini
wa dini wakishambuliana
huku wakipambana na vikosi
vya polisi.Kadiri muda
ulivyozidi kwenda ndivyo
vurugu zilivyozidi kushika kasi
na ilipofika saa kumi na mbili
za jioni maiti za watu
zilionekana katika mitaa mbali
mbali ya jiji la Tanga.Saa moja
za jioni ikaripotiwa vurugu
kubwa kuibuka jijini Dar es
laam na watu kushambuliana.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 5
Machafuko ya kidini
yaliyoanzia jijini Kampala
Uganda yalisambaa katika nchi
za Tanzania na Kenya
pia.Waumini wa dini
waliendelea kushambuliana na
kuuana wao kwa wao hivyo
kupelekea vikosi vya ulinzi
kutumia nguvu kubwa
kuwatawanya na kupelekea
vifo vya watu wengi
kutokea.Machafuko haya
yalishika kasi kutoka katika
miji mikubwa na kuingia
katika miji midogo midogo.IIi
kudhibiti watu kutumiana
jumbe za kueneza chuki
mitandao yote ya simu
ililazimwa ili watu
wasiwasiliane lakini bado
haikusaidia vurugu ziliendelea.
WASHINGTON DC -
MAREKANI
Rais William Washington
alijitokeza mbele ya waandishi
wa habari katika ikulu ya
Marekani kabla ya kupanda
helkopta ya Marine one
kuelekea katika uwanja wa
ndege wa jeshi kupanda ndege
“Wamarekani
wenzangu,wengi wenu
mnafuatilia taarifa za habari
za vyombo mbali mbali vya
habari duniani na mnaona
kile kinachoendelea Afrika
mashariki.Watu wanauana
na kuchinjana kwa ajili ya
imani.Hii si sawa hata
kidogo.Binadamu wote ni
sawa na Mungu
tunayemuabudu ni mmoja
hivyo hatupaswi kuuawa kwa
sababu ya dini.Machafuko
haya yaliyoanzia jijini
Kampala Uganda tayari
yamesambaa eneo kubwa la
Afrika Mashariki na damu
inaendelea
kumwagika.Ukitazama maiti
zilivyozagaa mitaani
inasikitisha sana.
Mwaka 1994 dunia
ilishuhudia mauaji makubwa
kuwahi kutokea katika
historia ya dunia pale
yalipofanyika mauaji ya
kimbali nchini Rwanda.Dunia
nzima ilishuhudia mauaji yale
yakifanyika lakini hakuna
walichokifanya zaidi ya
kuacha watu
wakiuana.Mauaji yale
makubwa yalianza hivi hivi
kama yalivyoanza machafuko
ya Uganda kwa kupanda
mbegu za chuki na watu
wakaanza kuuana
hovyo.Hatutaki tena historia
ile ya Rwanda ijirudie hivyo
basi serikali ya Marekani
itatuma wanajeshi wake
kwenda Afrika mashariki
kurejesha amani na
kuhakikisha yale ya mwaka
1994 hayatokei tena.Kuna
tetesi ya kikundi cha kigaidi
cha IS kushiriki katika
machafuko hayo hivyo basi
wanajeshi watakaokwenda
Afrika mashariki watakuwa
na kazi mbili moja ni kudhibiti
machafuko
yanayoendelea.Jukumu la pili
ni kukabiliana na kikundi cha
IS ambacho kimejipenyeza
katika machafuko hayo na
kufanya hali ya amani katika
eneo la Afrika Mashariki
kuzidi kuwa tete.
Wamarekani
wenzangu,katika machafuko
hayo makubwa kuwahi
kutokea katiuka ukanda wa
Afrika mashariki,ubalozi wetu
jijini Kampala umechomwa
moto na makundi ya watu
wenye hasira na tumepoteza
wamarekani wenzetu kumi na
nne.Kikosi cha wanajeshi
wetu wanaokwenda Afrika
Mashariki watakuwa na
jukumu pia la kuwaondoa
raia wa kigeni waliokwama
kufuatia machafuko hayo.
Mungu ibariki Marekani
William Washington Rais
wa Marekani alimaliza kutoa
hotuba yake fupi kwa
wamarekani halafu
akaongozwa na walinzi wake
kuelekea katika helkopta
iliyokuwa inamsubiri.
SIKU NNE BAADAE -
TANZANIA
Siku mbili toka Rais wa
Marekani atoe tamko la
kutuma wanajeshi wa
Marekani katika eneo la Afrika
Mashariki kwa ajili ya kuzuia
mauaji yaliyokuwa
yanaendelea kufuatia vurugu
za kidini,Meli kubwa mbili za
jeshi la Marekani zilitia nanga
katika bandari ya Tanga
zikitokea katika kambi kubwa
ya jeshi la Marekani iliyoko
Djibout.Meli hizo zilisheheni
vifaa mbali mbali ambavyo
wanajeshi wa Marekani
wangevitumia katika jukumu
lao la ulinzi wa amani.Meli
nyingine mbili zilitia nanga
katika bandari ya Dar es
salaam nazo zikiwa
zimesheheni vifaa mbali mbali
vya kijeshi na shughuli ya
kuandaa kambi kwa ajili ya
wanajeshi wa Marekani
ikaendelea katika miji ya Dare
s salaam na Tanga.Meli
nyingine kubwa mbili nazo
ziliwasili katika bandari ya Dar
es salaam zikiwa na vifaa
ambavyo vingetumika na
wanajeshi watakaokwenda
nchini Uganda
Maandalizi ya kambi
yalipokamilika ndege tatu za
jeshi la Marekani zilitua katika
uwanja wa ndege wa Tanga
zikiwa zimesheheni wanajeshi
waliotumwa nchini kulinda
amani.Vikosi vingine vya
wanajeshi vilipelekwa katika
majiji ya Dar es salaam na
Kampala ambako vurugu
zilipamba moto.
MIEZI MITATU ILIYOPITA
KAMPALA – UGANDA
Jumatano asubuhi mvua
kubwa iliyoambatana na radi
iliyoanza kunyesha saa tisa za
usiku bado iliendelea
kunyesha na haikuwa na dalili
za kukatika hivyo kuwatatiza
watu wengi waliohitaji kuwahi
katika shughuli zao mbali
mbali za kila siku.Pamoja na
ukubwa wa mvua iliyokuwa
inaendelea kunyesha lakini
habari kubwa iliyosambaa
jijini Kampala na nchi nzima
ya Uganda ni mauaji ya spika
wa bunge la Uganda profesa
Joseph Muganda ambaye
aliuawa yeye pamoja na
familia yake yote.Ilikuwa ni
taarifa iliyowastua watu wengi
asubuhi hiyo.
Rais wa Uganda Jenereali
Akiki Rwamirama aliandika
katika ukurasa wake wa
mtandao wa twitter
kusikitishwa kwake na mauaji
yale ya spika wa bunge na
kuyaita ni mauaji ya kinyama
na akaahidi kwamba wale wote
waliohusika katika mauaji yale
watasakwa kila kona ya nchi
na kuhakikisha wanapatikana.
Wakati mvua ile kubwa
ikiendelea kunyesha gari moja
liliwasili katika makazi ya Rais
wa Uganda mlango wa mbele
ukafunguliwa akashuka haraka
haraka mtu mmoja aliyekuwa
na mwavuli akaukunjua na
kuufungua mlango wa kati kati
jamaa moja mwembamba
aliyevalia nadhifu akashuka
akasindikizwa kuingia ndani
ya jengo lile la makazi ya Rais
“Karibu sana Nzeza”
akasema Jenerali Akiki baada
ya kusalimiana na mgeni wake.
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Yule jamaa ambaye Rais
alimuita kwa jina moja tu
Nzeza.
“Ahsante sana Nzeza kwa
kazi kubwa na nzuri
mliyoifanya usiku wa
leo.Nimefurahi sana” akasema
Jenerali Akiki.
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu
Nzeza
“Hakukuwa na tatizo lolote
katika utekelezaji wa kazi
ile?akauliza Jenerali Akiki
“Mheshimiwa Rais
hakukuwa na tatizo lolote.Kazi
yetu tumeikamilisha vizuri
kama ulivyotuelekeza na
tumefanikiwa kuipata ile
rekodi” akasema Nzeza na
kuingiza mkono katika koti
lake akatoa kifuko kidogo cha
nailoni ambacho ndani yake
kulikuwa na diski mweko
akasimama kwa adabu na
kumpatia Rais Akiki.Halafu
akatoa tena bahasha ndogo ya
khaki na kumpatia Rais
“Katika hii bahasha kuna
orodha ya watu ambao Spika
alikuwa anawasiliana nao
mara kwa mara utaipitia kisha
utatupa maelekezo nini
kifanyike”
“Ahsante sana
Nzeza.Nifikishie shukrani
zangu kwa vijana na kila kitu
kitakuwa kama
nilivyowaahidi” akasema
Jenerali Akiki
“Usihofu mzee tuko macho
tunafuatilia kwa karibu kila
kinachoendelea na yeyote
ambaye ataonekana kuwa
hatari kwako tutamuondoa”
akasema Nzeza akaagana na
Rais akaondoka.Jenerali Akiki
akavuta pumzi ndefu
akajiegemeza kitini na kuzama
mawazoni
“Profesa Joseph alikuwa ni
rafiki yangu sana lakini
sifahamu kitu gani
kilichombadilisha hadi akawa
adui yangu.Alikosea sana
kutaka kuniondoa madarakani
na hii haitaishia kwa Profesa
Joseph pekee bali itaendelea
kwa yeyote ambaye
ataendeleza hiki alichotaka
kukifanya spika.Hakuna
anayefahamu ni magumu gani
niliyopitia hadi kukalia kiti
hiki cha urais.Anayetaka
kuniondoa madarakani asubiri
kwanza hadi pale muda wangu
utakapomalizika vinginevyo
nitaendelea kuwakata pumzi
za uhai kila uchao ! akawaza
Rais Akiki akainuka na
kuelekea chumbani kwake
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 6
Jenerali Akiki aliingia
ofisini kwake akaelekeza
asiruhusiwe kuingia mtu
yeyote hadi pale
atakaporuhusu.Akajifungia
ofisini akatoa ile diski mweko
aliyopewa na Nzeza
akaichomeka katika kompyuta
yake ikajitokeza video ya
Melanie Davis akahisi mwili
wote ukimsisimka.
“Melanie !! akajikuta
akitamka kwa mstuko
alioupata
“Imekuaje profesa Joseph
akawa na rekodi ya Melanie?
Akajiuliza na kuanza kusikiliza
rekodi ile huku akihisi mwili
kumtetemeka
“Mwanamke huyu ni
shetani kabisa ! akawaza
Jenerali Akiki alipomaliza
kuitazama rekodi ile,akairejea
tena kwa mara ya pili na ya
tatu.Akatoa kitambaa akafuta
jasho.
“Siamini macho
yangu.Huyu kweli ni Melanie
Yule ninayemfahamu mimi au
ni Melanie wa kutengenezwa?
Akajiuliza na kuendelea kufuta
jasho
“Lakini huyu ni Melanie
yule Yule ninayemfahamu.Kwa
nini akafanya hivi?
Sikutegemea kabisa kama siku
moja angeweza kufanya kitu
cha kijinga namna hii !
akawaza Jenerali Akiki
“Baada ya shambulio lile
lililowaua wake za marais
nikaelekezwa tena kuandaa
shambulio lingine ambalo
linalenga kumuua Rais
Patrice Eyenga.Nilimfuata
James Kasai nikaongea naye
suala hili naye akanipeleka
kwa Rais wa Uganda Jenerali
Akiki ambaye alikubali
kushirikiana nasi katika
mpango huo na alitaka baada
ya Patrice kuuawa James
Kasai achukue nchi.Akiki
alinieleza kwamba Majenerali
wa jeshi la Congo walikuwa
wanandaa mpango wa
mapinduzi hivyo akamuita
mkuu wa majeshi wa Congo
akazungumza naye lakini
wakashindwa kuelewana
kuhusu James Kasai
kushirikishwa katika serikali
baada ya mapinduzi ndipo
tulipoamua kuendelea na
mpango wa kumuua James
Kasai bila kushirikiana na
wakuu wa jeshi la
Congo.Tulipanga Jenerali
Akiki aombe kukutana jijini
Dar es salaam na marais wa
Tanzania na Congo
azungumze nao kuhusu
kutafuta muafaka wa amani
kufuatia mashambulizi yale
yaliyofanywa na James Kasai
jijini Dar es salaam”
Kipande hiki Jenerali
Akiki alikirudia kukitazama
zaidi ya mara tano.
“Yule binti amenivua nguo
zote.Kitu gani kilimfanya
aamue kusema ukweli?
Ninajuta kwa nini
nilimfahamu
Melanie.Ameniletea matatizo
makubwa sana.Haya yote
aliyataka James Kasai kwani
ndiye aliyemleta Melanie
kwangu.Sikuwa nikimfahamu
huyu shetani” akawaza
Jenerali Akiki huku sura yake
ikiwa imejikunja kwa hasira
“Ndiyo maana Spika
alikuwa anajiamini sana kwa
kuwa alijua anao ushahidi
mkubwa kama huu.Melanie
ameweka wazi kila
kitu,hajaniacha na nguo hata
moja.Kwa rekodi hii ikisambaa
ka wananchi sijui nini
kitatokea.Lakini je hakuna
mbunge yeyote aliyeiona?
Kama wapo wabunge ambao
wamekwisha iona nikiwabaini
nao poa lazima wataondoka
kama profesa Profesa Joseph.”
Akawaza Jenerali Akiki
“Lakini rekodi hii Spika
ameitoa wapi?Ninapata picha
kwamba mpango wa
kuniondoa madarakani lazima
ni mpango wa serikali ya
Tanzania.Naamini wao ndio
waliompa Spika wa Bunge ile
rekodi naye akataka kulitumia
bunge kupiga kura ya
kutokuwa na imani nami
kuniondoa katika
madaraka.Huyu lazima ni Dr
Fabian anataka kulipiza
kisasi.Dah ! siamini kama
mambo haya yamefika hapa
lakini kikwazo cha kwanza
nimekiondoa ambacho n I
Spika wa bunge.Aliyafanya
maisha yanguyawe magumu
sana ndani ya siku mbili
zilizopita” akawaza Jenerali
Akiki na kuvuta kumbu kumbu
kilichotokea siku mbili
zilizopita
KAMPALA - SIKU 2
ZILIZOPITA
Inakaribia saa kumi na
mbili za jioni mvua za rasha
rasha ziliendelea kunyesha
katika jiji la Kampala.Ikulu
Rais wa Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama alipata ugeni
ambao hakuutarajia.Mgeni
aliyefika jioni hiyo
kumtembelea alikuwa ni Spika
wa bunge la Uganda.
“Mheshimiwa Spika karibu
sana” akasema Jenerali Akiki
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais.Samahani
kwa kukuvamia jioni hii na
kuvuruga ratiba zako lakini
sintachukua muda mrefu”
akasema Profesa Joseph
Muganda spika wa bunge la
Uganda
“Usijali mheshimiwa
spika.Hapa ni nyumbani
unaweza kuja muda wowote
utakao” akasema Jenerali
Akiki
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais” akasema
spika na ukimya mfupi ukapita
kisha akasema
“Mheshimiwa Rais kuna
jambo muhimu limenileta
hapa kwako ambalo ni
kuhusiana na kile kilichotokea
katika eneo letu la Afrika
Mashariki wiki kadhaa
zilizopita” akasema Spika na
kumstua kidogo Jenerali Akiki
“Mambo mengi yalitokea
hapa Afrika Mashariki katika
kipindi hicho.Kitu gani hasa
unataka
kukizungumzia?akauliza
Jenerali Akiki
“Yote yaliyotokea” akajibu
Spika.Jenerali Akiki
akachukua mkebe akatoa
sigara akaiwasha na kuvuta
akapuliza moshi na kusema
“Karibu”
“Mheshimiwa Rais mengi
yametokea katika jumuiya yetu
katika kipindi cha wiki chache
zilizopita na yote
unayafahamu.Mauaji ya
kinyama yamefanyika na hata
jumuiya ya Afrika Mashariki
iliponea chupu chupu
kusambaratika.Tuyaweke yote
pembeni lakini nataka
kuzungmzia mambo mawili
tu.Kwanza mpango wa mauaji
ya marais wa Tanzania na
Congo na pili ni James Kasai”
Spika akanyamaza baada ya
Jenerali Akiki kuonyesha
mstuko mkubwa.Nusura sigara
aliyoishika mkononi
imponyoke.
“Mheshimiwa Rais
ninaoushahidi usio na chembe
ya mashaka kwamba ulishiriki
katika mpango wa kutaka
kuwaua marais wa Tanzania
na jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo” akasema Spika na
Jenerali Akiki akaangua
kicheko
“Huo ni upuuzi mkubwa
sana.Mimi nitawezaje
kushiriki katika njama za
kuwaua marais wenzangu?
Huo ni uzushi na upuuzi
mkubwa mheshimiwa Spika !
akasema Jenerali Akiki
akionekana kuanza
kupandisha jazba.
“Mheshimiwa Rais kama
nilivyokwambia kwamba ninao
ushahidi usio na hata chembe
ya mashaka kwamba ulishiriki
katika mpango huo wa kuwaua
marais hao wawil……” Spika
akanyamaza baada ya Jenerali
Akiki kusimama kwa hasira
“Mheshimiwa Spika
sijawahi kushiriki katika
jambo hilo na kama kuna watu
wamekuletea taarifa kuwa
nimeshiriki katika njama hizo
za mapinduzi ni
wazushi,waongo na
wanastahili adhabu
kali.Profesa Joseph wewe ni
msomi mkubwa hupaswi
kusikiliza uongo kama huo
ambao unatungwa na
wapinzani wangu
kisiasa.Tunakaribia
uchaguzi,lazima vitu kama hivi
vijitokeze ili wanichafue.Naapa
lazima niwapate wale wote
wanaotaka kunipaka matope !
akasema Jenerali Akiki huku
akigonga meza kwa hasira
“Hakuna anayekupaka
matope mheshimiwa Rais kwa
sababu ni kweli umeshiriki na
ushahidi ninao.Kataa mbele
yangu kama humfahamu
Melanie Davis? Akauliza Spika
na midomo ya Jenerali Akiki
ikatetemeka
“Melanie nani? akauliza
“Melanie
Davis.Humfahamu?
“Simfahamu.Ni mara ya
kwanza ninamsikia mtu
huyo.Ni nani?akauliza Jenerali
Akiki
“Mheshimiwa Rais mdomo
wako unakana kumfahamu
Melanie lakini macho yako
yanakubali.Ulishirikiana na
Melanie Davis na James Kasai
katika mpango huo wa
mapinduzi.Taarifa zote
ninazo.Uliomba kukutana na
marais wa Tanzania na Congo
kwa lengo la kukamilisha
mpango wa mauaji yao kwa
bahati nzuri mpango huo
haukufanikiwa”akasema spika
“Mheshimiwa Spika siwezi
kuvumilia uzushi kama
huo.Mimi ni Rais wa Uganda
nitawezaje kushiriki katika
mpango wa kuwaua marais
wenzangu? Jenerali Akiki
akahamaki
“Usihamaki mheshimiwa
Rais wakati unafahamu fika
kwamba haya yote
ninayoyasema hapa ni kweli
tupu”
“Hakuna ukweli wowote
Spika.Huo ni uzushi na uongo
mkubwa ! akafoka Jenerali
Akiki
“Tukiachana na hilo suala
la kushiriki katika mpango wa
mapinduzi kuna suala lingine
la James Kasai.Huyu ni mtu
ambaye alifanya ukatili
mkubwa kwa kuua mamia ya
watu nchini Congo na baada ya
kufurushwa ulimpa hifadhi
Uganda.James amekuwa
mshirika wako wa karibu sana
na tayari imebainika wewe
ndiye uliyekuwa ukimsaidia
kijeshi katika mapambano
yake dhidi ya serikali ya
Congo.Kibaya zaidi ulimpa
hifadhi hapa Kampala akaishi
maisha ya kifahari huku dunia
nzima ikijua James yuko
msituni.Kwa nini mheshimiwa
Rais ukafanya hivi? Akauliza
Spika na Jenerali Akiki
akaendelea kuvuta sigara yake
kwa fujo sura akiwa ameikunja
“Mheshimiwa Rais haya
yote niliyokueleza ni ya kweli
kabisa na ushahidi wa kutosha
ninao kwamba umehusika
katika kupanga njama za
mauaji ya marais wa Tanzania
na Congo na vile vile umekuwa
mshirika wa James Kasai”
akasema Spika na ukimya
ukatawala mle ndani.Baada ya
muda Jenerali Akiki akasema
“Nini unakitaka Spika?
Kwa nini umekuja kunieleza
haya mambo?
“Kuna kitu kimoja tu
ambacho ninakitaka.Jiuzulu”
akasema Spika na Jenerali
Akiki akaitupa sigara katika
chombo cha majivu
akasimama
“Spika siwezi kufanya kitu
kama hicho.Mimi nijiuzulu ?!!
akasema Jenerali Akiki na
kutoa kicheko kidogo
“Hiki ni kichekesho.Siwezi
kujiuzulu kwa kuwa sihusiki na
hizo tuhuma zilizopikwa na
wapinzani wangu wa
kisiasa.Kamwe siwezi.Narudia
tena siwezi !! akasema kwa
ukali huku akigonga meza kwa
nguvu
“Mheshimiwa Rais
nimekufuata mimi mwenyewe
kukutaka uachie ngazi kwa
heshima.Toa sababu yoyote ile
ambayo wananchi wataikubali
uondoke madarakani kwa
heshima na suala hili litakuwa
limezikwa rasmi.Heshima
yako itaendelea kuwepo na
maisha yako yataendelea kuwa
mazuri hakuna atakayefahamu
haya mambo” akasema
Spika.Jenerali Akiki
akamtazama kwa macho
makali na kusema
“Ninarudia tena siwezi !
Nielewe spika siwezi kuachia
ngazi kwa mambo ya kijinga
kama hayo.Nilichaguliwa na
wananchi wa Uganda
niwaongoze hivyo nitaendelea
kuwatumikia hadi pale muda
wangu
utakapokwisha.Umenielewa
Spika?akauliza Jenerali Akiki
kwa sauti ya ukali
“Mheshimiwa Rais kama
ukikaidi hiki ninachokwambia
kuna mambo mawili
yatafanyika.Aidha uondolewe
na bunge au na
wanananchi.Nitawasilisha
ushahidi nilionao
bungeni,wabunge
watajadiliana na kupiga kura
ya kutokuwa na imani nawe na
yawezekana chama chako
kikakunusuru katika kura hiyo
lakini wananchi hawataweza
kukuacha ukaendelea kukalia
kiti cha urais.Mimi binafsi
nitahamasisha maandamano
makubwa ya wananchi ambayo
hayajawahi kushuhudiwa hapa
nchini wakishinikiza uachie
madaraka.Kwa nini tufike
huko mheshimiwa Rais?Kwa
nini tukuondoe kwa fedheha?
Fanya vile ninavyokushauri na
utaendelea kubaki na heshima
yako” akasema Spika
“Joseph wewe si mgeni
kwangu unanifahamu mimi ni
nani.Sipendi kuyumbishwa na
mtu yeyote.Ninakuonya
Joseph achana na hili
jambo.Kama kuna watu
wamekutuma waeleze kwamba
suala hili haliwezekani.!
Akasema Jenerali Akiki
“Mheshimiwa Rais huu si
wakati wa kunitolea
vitisho.Mimi nawe
tunafahamiana vyema ndiyo
maana nimekufuata
kiungwana kukutaka uachie
ngazi kwa heshima.Usitake
suala hili likafika kwa
wananchi itakuwa ni aibu
kubwa kwako ! akasema Spika
“Spika ninarudia tena
kukuonya kwamba achana na
hili jambo litakuingiza katika
matatizo makubwa.Kitu gani
umekikosa Spika? Unataka
urais?
“Sihitaji urais na wala
sihitaji kitu chchote kutoka
kwako nimeridhika na kile
nilichonacho.Umenionya
niachane na hili jambo na
mimi ninakuonya kwamba
usithubutu kufanya kitu
chochote cha kijinga.Naamini
wewe una nguvu kubwa
unaweza ukaninyamazisha
mimi lakini hautaweza
kuwanyamazisha
wananchi.Ukiniondoa mimi
ataibuka mwingine
ataendeleza pale nilipoachia
mimi na hakuna kuchoka hadi
pale utakapoachia
ngazi.Tunataka kuongozwa na
Rais mwadilifu asiye na hata
chembe ya doa sifa ambayo
wewe huna mheshimiwa Rais”
akasema Spika.Jenerali Akiki
akaendelea kumtazama kwa
macho makali
“Mheshimiwa Rais
nakushukuru kwa
kunisikiliza.Mimi ninaondoka
lakini nataka hadi kufika kesho
saa kumi na mbili za jioni
ujitokeze katika televisheni ya
taifa na utangaze kuachia
ngazi.Kama ukipuuza muda
huo niliokupa basi usije
kunilaumu.Kwa heri
mheshimiwa Rais” akasema
spika na kuondoka huku
Jenerali Akiki akimtazama
kwa hasira
Jenerali Akiki
akatabasamu baada ya kumbu
kumbu ile kumjia
“Nilimuonya profesa
Joseph aachane na suala hili
litamletea matatizo hakutaka
kusikia.Nitaendelea
kuwashughulikia wale wote
ambao watavaa viatu vyake na
kutaka kuliendeleza hili
suala.Hakuna atakayeniondoa
madarakani.Nitatawala hadi
pale muda wangu
utakapomalizika” akainuka na
kwenda dirishani
akachungulia nje
“Nimewaogopa sana
wanawake hasa wale wenye
uzuri wa kimalaika.Melanie
alinichanganya kwa uzuri wake
hadi kujikuta nikifanya
mambo ya kijinga ambayo
sikupaswa kuyafanya kama
Rais wa nchi.Kwa sababu ya
tamaa zangu
nimewasababishia vifo wale
majenerali wa jeshi la jamhuri
ya kidemokrasia ya Congo
ambao walikuwa wanapanga
kufanya mapinduzi ambao
Melanie amewataja katika
rekodi hii kwamba walikuwa
wanaandaa mpango wa
mapinduzi.Majenerali saba
waliokuwa wanaandaa
mpango wa mapinduzi
akiwemo mkuu wa majeshi
waliuawa wiki iliyopita kwa
nyakati tofauti.Mpaka leo
haijulikani nani aliwaua
wakuu wale wa jeshi lakini
baada ya kutazama rekodi ile
ya Melanie tayari nimepata
jibu kuwa wameuawa na
serikali yao.Naamini tayari
Rais Patrice Eyenga
amekwisha itazama rekodi ile
na ndiyo maana akaamua
kuchukua hatua za haraka za
kuzima mpango wa mapinduzi
kwa kuwaua kimya kimya wale
waliotaka
kumpindua.Nitaendelea
kumlaumu sana James Kasai
kwa kumleta kwangu Melanie
Davis ambaye amenisabaishia
haya yote” akawaza na kurejea
mezani akaishika karatasi
moja akaipitia kwa makini
“Katika hii orodha ya watu
ambao wamewasiliana na
Spika wa bunge toka juzi
naamini lazima yupo mmoja
wao ambaye anafahamu
kuhusiana na rekodi hii ya
Melanie.Natakiwa kufanya
uchunguzi wa kina kumfuatilia
mmoja baada ya mwingine
kujua ni yupi ambaye
anafahamu kuhusu rekodi
hii.Nitawaondoa wote bila
kujali ni akina nani.Damu
lazima imwagike kama
ninataka kujilinda nibaki
madara……....” Ghafla Jenerali
Akiki akastuka baada ya milio
ya risasi kuanza
kusikika.Haraka haraka
akainuka kwa lengo la kwenda
kuchungulia dirishani kujua
milio ile ya risasi ilisikika wapi
lakini kabla hajalifikia dirisha
mlango wa ofisi yake ukapiga
teke ukafunguka wakaingia
walinzi wake wanne
wakamshika na kuanza kutoka
naye nje
“Kuna nini?akauliza
Jenerali Akiki lakini
hakujibiwa
“Rekodi ! akasema
Jenerali Akiki lakini walinzi
wale hawakumsikia
alichokisema waliendelea
kukimbia naye huku milio ya
risasi na mabomu vikisikika
nje ya jengo la ikulu
“Kuna nini
kimetokea?akauliza Jenerali
Akiki lakini hakujibiwa
Walinzi wake walimpeleka
Rais Akiki katika njia ya siri
ambayo ilitengenezwa maalum
kwa ajili ya kumuondoa Rais
ikulu pale kunapotokea hatari.
“Weka namba za siri mkuu
lango lifunguke” akasema
mmoja wa wale walinzi na Rais
akaelekeza jicho lake katika
mojawapo ya kioo na baada ya
sekunde chache lango
likajifungua wakaingia katika
njia ile ya siri ambako
kulikuwa na gari maalum
ambalo halipenyi
risasi.Wakaingia katika gari
lile na kufuata barabara
iliyokuwa chini ya jengo la
ikulu na walipofika kilometa
kadhaa gari likasimama
wakashuka na Jenerali Akiki
akatamka neno la siri lango
likajifungua wakapanda ngazi
na kutokea katika bustani
moja nzuri.Mlango wa nyumba
iliyokuwepo mahala pale
ukafunguliwa na ndani yake
kulikuwa na magari manne ya
kifahari ambayo ni maalum
kwa ajili ya kumuokoa
Rais.Bila kupoteza muda
wakaingia katika gari ambalo
funguo yake ilikuwa chini ya
zuria upande wa dereva na
kuondoka eneo lile
“Nini kimetokea? Kwa nini
hamtaki kunieleza kumetokea
nini? akauliza Jenerali Akiki
huku akihema kwa kasi
“Ikulu imevamiwa
mheshimiwa Rais ! akajibu
mmoja wa walinzi
“Ikulu imevamiwa? Nani
kavamia?
“Vikosi vya jeshi”
Jenerali Akiki akavuta
pumzi ndefu na kujiegemeza
kitini
“Nimepinduliwa !
akawaza.Baada ya dakika mbili
akauliza
“Mnanipeleka wapi?
“Mheshimiwa Rais
tunaelekea uwanja wa ndege ili
uweze kuondoka nchini haraka
iwezekanavyo”
“Familia yangu iko wapi?
Akauliza Jenerali Akiki
“Mheshimiwa Rais hatujui
mahala walipo lakini jukumu
letu la kwanza ni kuhakikisha
unakuwa salama ndipo tuanze
kuitafuta familia yako.Usihofu
mheshimiwa Rais watakuwa
salama”
Mmoja wa walinzi wale
akapigiwa simu akaipokea na
alipomaliza kuzungumza sura
yake ilibadilika
“Kuna nini?akauliza
Jenerali Akiki
“Nimetaarifiwa kwamba
vimefika vikosi vya jeshi sasa
hivi na kuuzingira uwanja wa
ndege hakuna ndege
inayoruhusiwa kuruka au
kutua.Ndege ya Rais pia
imezingirwa na wanajeshi !
“Mungu wangu ! akasema
Jenerali Akiki na kushika
kichwa
“Tunaelekea wapi?akauliza
mmoja wa walinzi
“Naomba simu” akasema
Jenerali Akiki akapewa simu
akazungumza na balozi wa
Marekani nchini Uganda
akamueleza kilichotokea na
kumuomba hifadhi katika
ubalozi huo akakubaliwa
“Twendeni ubalozi wa
Marekani” akaelekeza Jenerali
Akiki
*************
Televisheni na redio ya
taifa ya Uganda vilikatisha
matangazo ghafla.Jenerali
Paul Mukasa akajitokeza na
kulihutubia taifa.
“Ndugu zangu wananchi
wa Uganda habari za
mchana.Ninaitwa Jenerali
Paul Mukasa mkuu wa majeshi
wa Uganda.Nimejitokeza
mbele yenu mchana huu
kuwapeni taarifa kwamba Rais
Jenerali Akiki Busingye
Rwamirama amepinduliwa na
jeshi limeshika uongozi wa
nchi.Mimi na wenzangu
tumeamua kumuondoa
madarakani Rais Akiki
kutokana na kupoteza sifa za
kiuongozi kama
mtakavyoelezwa hapo baadae.
Ninawahakikishia ndugu
wananchi kwamba mapinduzi
haya yamemalizika na damu
kidogo imemwagika kwa wale
askari wachache watiifu kwa
Jenerali Akiki na nchi iko
salama kabisa.Ninawataka
wananchi wote muendelee na
shughuli zenu bila
wasiwasi.Shughuli za serikali
zitaendelea kama kawaida
chini ya uongozi wa jeshi hadi
pale uchaguzi mkuu
utakapofanyika na Rais mpya
kupatikana.Tunaahidi
kufanyika uchaguzi mkuu
ndani ya miezi sita kutokea
sasa lakini hadi hapo
utakapofanyika uchaguzi huo
mimi Jenerali Paul Mukasa
nitashika nafasi ya Rais
Ninarudia tena
kuwahakikishia wananchi wa
Uganda kwamba nchi iko
salama na ninawaomba
asitokee mtu yeyote
akathubutu kutaka kuleta
vurugu za aina yoyote ile
kwani jeshi liko imara na
litakabiliana na yeyote ambaye
atadiriki kuleta aina yoyote ya
vurugu.Kuanzia sasa hadi wiki
mbili ninatangaza amri ya
kutotembea hovyo kuanzia saa
mbili za usiku.Marufuku
mikusanyiko isiyo na kibali
cha jeshi au maandamano ya
aina yoyote.
Katika kipindi hiki
ambacho jeshi limeshika
madaraka tutakuwa wawazi na
wa kweli.Mtafahamu kila
kinachoendelea katika serikali
ya Uganda,mtafahamishwa
kila senti moja ya serikali
ilivyotumika.Ule mtandao
wote wa kifisadi wa Rais Akiki
tutaufyeka na mali zote
walizoiiba zilizoko ndani na
nje ya nchi zitarejeshwa katika
mikono ya serikali
Narudia tena kuwaomba
utulivu na tuendelee na
shughuli zetu za kujiingizia
kipato kama kawaida.
Mungu ibariki Uganda
Ahsanteni kwa kunisikiliza
Jenerali Paul Mukasa
alimaliza kutoa hotuba yake
fupi kwa taifa kuhusiana na
mapinduzi yale yaliyofanywa
na jeshi la Uganda na
kujtangaza yeye kuwa Rais wa
mpito wa Uganda hadi pale
utakapofanyika uchaguzi
mkuu ndani ya miezi sita
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Akiwa ofisini kwake Rais
wa jamhuri ya muungano wa
Tanzania Dr Fabian Kelelo
alistuka baada ya simu yake
kuita na jina la mpigaji
likajitokeza katika kioo cha
simu.Akakunja sura kwa
hasira
“Dr Natukukunda !
akasema Dr Fabian akiitazama
simu ile ikiita halafu akaipokea
“Hallow Dr Natukunda”
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
samahani sana nimekupigia
kuomba msaada wako”
“Unahitaji msaada gani
nikusaidie?akauliza Dr Fabian
“Jeshi limepindua
nchi.Mume wangu sifahamu
alipo,mimi na watoto
tumefanikiwa kutoroshwa na
walinzi na hivi sasa
ninakaribia kufika mpakani
ninakuja
Tanzania.Mheshimiwa Rais
ninakuomba msaada wako
tupate hifadhi ya muda nchini
Tanzania wakati tukitafuta
namna ya kuweza kuondoka
Afrika Mashariki” akasema Dr
Natukunda Rwamirama mke
wa Jenerali Akiki.Ukapita
ukimya mfupi.
“Mheshimiwa Rais
nakuomba tafadhali tuko
kwenye hatari kubwa na
hatuna sehemu nyingine ya
kukimbilia zaidi ya Tanzania !
akaendelea kuomba Dr
Natukunda
“Mko wangapi?akauliza Dr
Fabian
“Niko na watoto wangu
wawili msaidizi na walinzi
watatu”
“Sawa nitatoa maelekezo
kwa vyombo husika viweze
kuwasaidia mtakapofika
mpakani” akasema Dr Fabian
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akajibu Dr
Natukunda na kukata simu
“Mmejipeleka wenyewe
katika mdomo wa Mamba
mwenye njaa.Bado nina hasira
kubwa na Jenerali Akiki.Kama
isingekuwa kwa msaada wa
Mathew na wenzake hivi sasa
ningekwisha poteza maisha
kwani Akiki na wale magaidi
walikuwa tayari
wamekamilisha mipango yote
ya kutuua mimi na Patrice
Eyenga.Akuanzae
mmalize.Alinianza na mimi
ninammaliza.Nimeanza na
yeye kuondoka madarakani na
sasa naelekea kwa familia
yake.Nataka huko aliko apate
machungu,aumie kama
ninavyoumia mimi kwa kifo
cha mke wangu Millen.Yeye
ndiye aliyemfadhili James
Kasai ambaye ndiye aliyemuua
mke wangu” akawaza Dr
Fabian na kumpigia simu
waziri wa mambo ya ndani ya
nchi akampa maelekezo ili Dr
Natukunda na wote
alioongozana nao waruhusiwe
kuingia nchini na kupewa
hifadhi.
“Sasa ni zamu yako
Jenerali Akiki.Kokote uliko
salamu zangu
utazipata.Utakufa taratibu
sana kwa mateso
utakayoyapata” akaendelea
kuwaza Dr Fabian
MAKAO MAKUU – IDARA YA
SIRI YA USALAMA WA
NDANI WA NCHI (SNSA)
Idara ya siri ya usalama wa
ndani wa nchi, kazi ziliendelea
kama kawaida kwa sasa ikiwa
chini ya uongozi mpya wa
mwanamama Ruby au
Annabel jina ambalo amekuwa
akilitumia toka alipofika
Tanzania akitokea Uingereza.
Baada ya Edwin Mbeko
kuuawa rais alimkabidhi Ruby
idara hii nyeti aiongoze na
toka alipoanza kuiongoza idara
hii mabadiliko mengi
makubwa yamekwisha fanyika
na ufanisi ulikuwa mkubwa
kufuatia mabadiliko makubwa
yaliyofanywa katika idara hii.
Akiwa katika ofisi yake
akiendelea na kazi simu yake
ikaita alikuwa ni Rais Dr
Fabian
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby baada ya
kupokea simu
“Ruby habari za leo?
“Nzuri kabisa mheshimiwa
Rais”
“Tayari umepata taarifa za
kilichotokea Uganda? Akauliza
Dr Fabian
“Ndiyo mheshimiwa rais
tayari tumepata taarifa za
mapinduzi ya kijeshi
yaliyofanyika leo hii”
“Yule shetani
ameondolewa madarakani na
jeshi na mpaka sasa hajulikani
mahala alipo.Ninashukuru
kwa kuwa amepata
alichokistahili” akasema Dr
Fabian huku aitoa kicheko
kidogo
“Mheshimiwa Rais
unahusika kwa namna yoyote
na haya mapinduzi? Akauliza
Ruby
“Kwa nini umeuliza Ruby?
“Nataka nifahamu kama
unahusika kwa namna yoyote
na haya mapinduzi kwani
yametokea ndani ya kipindi
kifupi sana toka kushindwa
kwa jaribio la kutaka kuwaua
wewe na Rais Patrice Eyenga
na hakuna sababu kubwa ya
maana iliyotolewa na jeshi kwa
nini wamefanya mapinduzi
yale” akasema Ruby
“Ruby yule jamaa alistahili
hiki alichokipata tena hata
zaidi ya hapa.Alitakiwa
akamatwe na kupewa mateso
makali sana.Kuhusu mimi
kuhusika na mapinduzi hayo
hapana sijahusika kwa namna
yoyote ile” akasema Dr Fabian
“Sawa mheshimiwa
Rais.Sisi tunaendelea na
majukumu yetu vyema na
hakuna tatizo lolote” akasema
Ruby
“Ruby ninakuhitaji hapa
ikulu sasa hivi nina
mazungumzo muhimu nawe”
akasema Dr Fabian
“Sawa mheshimiwa Rais
ninakuja hapo sasa hivi”
akajibu Ruby na Rais akakata
simu.
Ruby akachukua
kompyuta yake akafunga ofisi
na kuelekea maegesho
akamuelekeza dereva wake
waelekee ikulu.
“Dr Fabian ameonekana
kufurahishwa sana na
mapinduzi yaliyotokea leo
nchini Uganda.Ninapata
mashaka kidogo kuamini hana
mkono wake katika mapinduzi
haya.Wasi wasi wangu ni
kwamba yawezekana
uchunguzi ukafanyika na
ikagundulika kwamba
Tanzania ina mkono wake
katika mapinduzi yale basi
nchi itachafuka sana.Kwa
kuwa amekiri yeye mwenyewe
kwamba hahusiki kwa lolote
katika mapinduzi hayo basi
vizuri.Hata kama kukitokea na
umwagaji damu, Tanzania
hatutalaumiwa.Kwa upande
Fulani hata mimi nimefurahi
kwa Jenerali Akiki kuondolewa
madarakani.Alikosea sana
kushirikiana na magaidi
kutaka kuwaua marais
wenzake” akawaza Ruby akiwa
njiani kuelekea ikulu
Kutoka ofisi kuu za SNSA
hadi ikulu si mbali hivyo
alitumia dakika kumi na tano
kufika ikulu.Walinzi wake
wawili wakawahi kushuka
garini mmoja akamfungulia
mlango akashuka na kuelekea
ndani ya jengo la ikulu
kuonana na Rais
“Karibu sana Ruby”
akasema Dr Fabian baada ya
Ruby kuwasili
“Nashukuru mheshimiwa
Rais”
“Shughuli zinakwendaje
hapo SNSA?
“Kila kitu kinakwenda
vyema hakuna tatizo lolote”
“Nafurahi kusikia
hivyo.Ruby kuna mambo
mawili nimekuitia
hapa.Kwanza ni kuhusu suala
la msaidizi wako.Nina mafaili
ya watu kadhaa ambao
ninafikiria kumteua mmoja
wao kuwa msaidizi wako.Idara
nyeti kama hii lazima uwe na
mtu wa kukusaidia.Nina
majina ya watu nane ambao
nimeletewa na wasaidizi
wangu na wote hao ni watu
wenye ujuzi na uzoefu mkubwa
katika masuala ya
usalama.Ninaendelea
kuyapitia mafaili yao na
nikimaliza nitakushirikisha
nawe pia katika kuamua ni
nani anafaa kuwa msaidizi
wako” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
nimekwisha liweka wazi suala
hili toka awali kwamba mtu
pekee ambaye nataka awe
msaidizi wangu ni Papi Gosu
Gosu sitaki mtu mwingine”
akasema Ruby.Rais
akamtazama na kuuliza
“Kwa nini Papi Gosu Gosu
na si mwingine?
“Nimeshiriki naye katika
operesheni kadhaa
ninamfahamu vizuri na zaidi
ya yote ninamuamini
sana.Ninataka mtu ambaye
atashika nafasi yangu pale
nisipokuwepo awe ni mtu
ninayemuamini na chaguo
langu ni GosuGosu hivyo
mheshimiwa Rais usipoteze
muda kupitia hayo mafaili ya
watu wengine” akasema Ruby
“Lakini huyu jamaa kwa
maelezo niliyoyapata kutoka
kwa Austin si mtanzania wa
kuzaliwa”
“Mheshimiwa Rais
usisahau kuwa hata mimi nina
uraia wa Uingereza japo asili
yangu ni Tanzania” akasema
Ruby na Dr Fabiana akaguna
kidogo
“Vipi kuhusu afya yake?
Akauliza
“Anaendelea
vizuri.Ninawasiliana naye kila
siku na kwenda nyumbani
kwake kujua maendeleo
yake.Anaendelea vizuri na hata
madaktari wanaomuhudumia
wamenihakikishia hilo”
“Kazi hizi hazihitaji mtu
mwenye tatizo lolote la
kiafy….”
“Mheshimiwa Rais Gosu
Gosu yuko vizuri naomba
uniamini mimi.Hata kama leo
na kesho nisipokuwepo yeye
anafaa sana kuongoza idara
kubwa kama hii” akasema
Ruby
“Sawa Ruby nitalifikiria
hilo suala”
“Ahsante mheshimiwa
Rais”
“Umemtaja Gosu Gosu
nimemkumbuka Mathew
Mulumbi.Mnawasiliana?
“Hapana.Baada ya
kumaliza operesheni ile
alitoweka na hakuna anayejua
alikwenda wapi wala hakuna
mwenye mawasiliano naye”
“Yule ni mtu wa ajabu
sana.Sikumfahamu hapo kabla
na hata nilipoelezwa kuhusu
yeye sikuamini hadi pale
alipoonyesha maajabu
makubwa kwa kumuua James
Kasai mtu ambaye tulikuwa
tumeandaaa kikosi cha
kwenda kumsaka.Kingine
ambacho mpake leo hii
kinausisimua mwili ni jinsi
alivyoweza kupambana na mtu
mwenye bomu.Ninajiuliza ni
vipi kama Yule mtu angeamua
kujilipua? Sina cha kusema
kuhusu Mathew.Ningepata
nafasi ya kuzungumza naye
kwa kirefu zaidi ningemuomba
abaki hapa nchini ningempa
kazi nzuri sana katika masuala
ya usalama.Anafaa sana”
akasema Dr Fabian
“Mathew anajitosheleza
kwa kila kitu katika maisha
yake na hahitaji ajira
serikalini” akasema Ruby
“Tuachane na hayo ya
Mathew
Mulumbi.Nilikwambia
nimekuita hapa kwa masuala
mawili” akasema Dr Fabian na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Nimepigiwa simu na Dr
Natukunda Rwamirama mke
wa Rais wa Uganda
aliyepinduliwa.Amefanikiwa
kutoroka na familia
yake.Alinipigia simu akiomba
hifadhi nchini Tanzania”
“Umemkubalia ombi lake?
“Ndiyo nimekubali ombi
lake na tayari nimemuelekeza
waziri wa mambo ya ndani ya
nchi ahakikishe mama huyu na
wote alioongozana nao
wanaingia nchini na kupatiwa
hifadhi” akasema Dr Fabian
“Vizuri sana.Umeonyesha
uungwana mkubwa sana licha
ya mambo ya ajabu aliyotaka
kuyafanya mume wake”
akasema Ruby.Dr Fabian
akavuta pumzi ndefu kisha
akasema
“Ruby kuna jambo nataka
ulifahamu ambalo yawezekana
hautalipenda”
“Jambo gani mheshimiwa
Rais?
“Nina sababu maalum ya
kukubali mke wa Jenerali
Akiki apewe hifadhi Tanzania”
akasema Dr Fabian na
kunyamaza kidogo
“Mke wangu Millen
aliuawa na James Kasai
ambaye alikuwa anafadhiliwa
na Jenerali Akiki.Kama
haitoshi Jenerali Akiki
akashirikiana na James Kasai
na magaidi wa IS kuandaa
mpango wa kuniua.Sikufichi
Ruby bado nina jeraha bichi la
kuondokewa na mke
wangu.Kila usiku
ninapoitazama picha yake
kidonda nilichokipata nahisi
kinavuja damu.Nina hasira na
Jenerali Akiki na ninataka
maumivu haya niyapatao naye
ayapate” akasema Dr Fabian
“Unataka kufanya nini
mheshimiwa Rais? Akauliza
Ruby huku sura yake
ikionyesha wasi wasi.Dr
Fabian akavuta pumzi ndefu
na kusema
“Nataka kuiteketeza
familia yote ya Jenerali Akiki
watakapokuwa hapa Tanzania”
Ruby alipatwa na mstuko
akasimama
“Mheshimiwa Rais hapana
! Aliyeshiriki katika mpango
wa kutaka kukuua ni Jenerali
Akiki na si familia
yake.Hawahusiki na chochote
hivyo hakuna sababu ya
kuwaumiza ! akasema Ruby
“Nalifahamu hilo Ruby
lakini ninataka kumuumiza
Jenerali Akiki kama mimi
ninavyoumia ! akasema Dr
Fabian
“Mr President no !
Hatuwezi kuua familia ambayo
si hatari kwa usalama wa nchi !
“Ruby hili si
ombi.Nimekwisha dhamiria
hivyo na jambo hili lazima
lifanyike.Familia yote
watauawa watakapokuwa hapa
nchini.Nataka uandae watu
mahiri katika idara yako
watakaotekeleza jambo hilo
kwa siri” akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais
utanisamehe kama nitakosa
nidhamu lakini idara
ninayoiongoza
inajishughulisha na kulinda
usalama wa ndani wa nchi na
si idara ya kutumika katika
mauaji binafsi.Familia hii
ambayo unataka iuawe si
hatari kwa usalama wa ndani
wa nchi wanakuja hapa nchini
kwa ajili ya kupata hifadhi
hivyo mimi kama mkuu wa
idara hiyo siwezi kuandaa timu
ya kushiriki katika mauaji
hayo ambayo hayana tija kwa
usalama wa nchi” akasema
Ruby na Dr Fabian
akamtazama kwa macho
makali
“Ruby mimi ndiye mkuu
wa idara hii unayoiongoza na
ndiye mwenye uamuzi wa
mwisho katika kila jambo
hivyo kama kiongozi wako
ninakuamuru nataka uandae
timu itakayotekeleza jambo
hilo na hakuna mjadala katika
hilo suala ! akasema Dr Fabian
kwa sauti kali kidogo
“Nafahamu mheshimiwa
Rais kwamba idara ya SNSA
iko chini yako lakini
umeniteua mimi niwe
mkurugenzi wake na kwa
mamlaka uliyonipa ninao
uwezo wa kukataa kufanya
jambo lolote ambalo
halitakuwa na maslahi kwa
usalama wa nchi.Mauaji ya
famili ya Jenerali Akiki ni ya
kulipiza kisasi na si kwa
sababu za kiusalama” akasema
Ruby na Dr Fabian akasimama
“Ruby nakuonya chunga
sana kauli yako
unapozungumza
nami.Huzungumzi na
mchumba wako,hapa
unazungumza na Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania hivyo kuwa na adabu
! akafoka Dr Fabian
“Ninakuagiza na hili si
ombi bali ni amri.Nataka
uandae timu ya watu mahiri
kwa ajili ya kuimaliza familia
ya jenerali Akiki.Narudia tena
kwamba hili si ombi ni amri
nenda kaitekeleze ! akasema
Dr Fabian kwa sauti kali
“Mheshimiwa Rais ulinitoa
Uingereza ili nije kuongoza
idara ya usalama wa ndani ya
nchi.Hukunileta hapa kuja
kufanya mauaji kwa
kufurahisha nafsi yako.Kama
kuna ulazima wa kuua basi ni
kwa sababu za usalama wa
nchi lakini sioni hatari ya
familia hii kwa usalama wa
nchi yetu.Narudia tena
mheshimiwa Rais utanisamehe
kwa haya maneno yangu lakini
huo ndio msimamo wangu na
endapo utaendelea kusisitiza
suala hilo ni bora ukaniondoa
katika nafasi hii ya ukurugenzi
kisha ukaendelea na mipango
yako ya kuua watu wasio na
hatia ! akasema Ruby na Dr
Fabian akamtazama kwa
hasira
“Ruby nakushangaa
sana.Unafahamu fika
alichonifanyia Jenerali Akiki
na..”
“Ninafahamu mheshimiwa
Rais lakini familia hii
hawahusiki na chochote
alichokifanya Akiki hivyo
hawastahili hicho unachotaka
kuwafanyia.Nakushauri
mheshimiwa Rais sitisha huo
mpango wako.Mambo
yamekwisha tulia hivi
sasa,James Kasai aliyekuwa
tishio hayupo tena,mtandao
wa IS hapa nchini
umeng’olewa,SNSA
imesafishwa na inafanya kazi
vizuri, na nchi iko
salama.Nakushauri
mheshimiwa Rais achana na
hilo suala linaweza kuibua
matatizo mengine kwa wakati
huu ambapo mambo
yametulia” akasema Ruby.Dr
Fabian akafikiri halafu
akasema
“Sawa Ruby
nimekuelewa.Ahsante kwa
ushauri wako”
“Nashukuru mheshimiwa
rais kwa kunielewa”
“Niliyokuitia ni hayo
mawili hivyo tumemaliza
mazungumzo yetu.Kuna lolote
lingine ambalo unataka
kuniambia?akauliza Dr Fabian
“Hakuna mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby wakaagana
akaondoka
“Sikujua kama Ruby ni
mwanamke mwenye msimamo
mkali namna hii.Lakini
alichokisema ni cha
kweli.Idara yake inasimamia
usalama wa ndani wa nchi na
familia ya Jenerali Akiki haina
hatari yoyote kwa usalama wa
nchi.Hata hivyo,nafsi yangu
inakataa kabisa kuwaacha
salama.Nataka nimuumize
Akiki.Nimeanza kwa
kumuondoa madarakani na
ninataka kumuongezea mateso
kwa kuimaliza familia yake
pia.Ninataka aishi maisha
magumu yenye mateso
makali.Nimekwisha
muelekeza Jenerali Mukasa
kuhakikisha wanataifisha mali
zake zote zilizoko ndani na nje
ya nchi,kuzuia akaunti zake
zote za benki ili Jenerali Akiki
aishi maisha ya
taabu.Ningeweza kupanga
mpango wa kumuua lakini
nataka afe taratibu kwa
mateso” akawaza Dr Fabian na
kuchukua simu akampigia mtu
Fulani akamtaka afike ofisini
kwake mara moja.
Baada ya kutoka ikulu
Ruby akaelekea nyumbani kwa
Gosu Gosu kumjulia hali.
“Karibu sana Ruby”
akasema Gosu Gosu aliyekuwa
amekaa pembeni ya bwawa la
kuogelea akisoma kitabu cha
hadithi
“Ahsante Gosu
Gosu.Sikujua kama nawe u
msomaji wa vitabu” akasema
Ruby
“Ni kweli sikuwa msomaji
wa vitabu lakini nimeanza
kuvutiwa na huyu mwandishi
Patrick Ck ninasoma kitabu
chake hapa” akasema Gosu
Gosu na kufunika kitabu
alichokuwa anakisoma.
“Habari za huko
utokako?akauliza
“Huko kwema.Vipi
maendeleo yako?
“Ninaendelea
vizuri.Nimetoka hospitali
wamenipima na kuniambia
ninaendelea vizuri”
“Nafurahi kusikia hivyo”
“Usihofu Ruby muda si
mrefu nitakuwa tayari kuanza
majukumu yangu”akasema
Gosu Gosu
“Nimetoka ikulu kuonana
na Rais nimemkumbusha tena
kwamba ni wewe ndiye
ninayekuhitaji kuwa msaidizi
wangu ndiyo maana
ninakuombea umalize
mapumziko uliyopewa ili uje
kunisaidia katika majukumu
yangu” akasema Ruby na Gosu
Gosu akatabasamu
“Ruby ahsante sana kwa
kunichagua niwe msaidizi
wako.Ninakuahidi pale tu
mapumziko yangu
yatakapomalizikana madaktari
kuniruhusu kuendelea na kazi
basi nitaanza kazi haraka sana
katika idara yako” akasema
Gosu Gosu
“Umesikia kilichotokea
Uganda leo?
“Amenipigia simu Austin
akanijulisha kwamba Rais wa
Uganda amepinduliwa na
jeshi”
“Ni kweli amepinduliwa na
jeshi na mpaka sasa hajulikani
mahala alipo ila familia yake
wameomba hifadhi nchini
Tanzania”
“Rais amekubali kuwapa
hifadhi Tanzania?
“Ndiyo amekubali kuwapa
hifadhi lakini nina hofu”
“Hofu ya nini Ruby?
“Kuhusu usalama wao”
“Rais hakupaswa kuwapa
hifadhi.Jenerali Akiki ni mtu
mbaya sana !” akasema Gosu
Gosu.
“Lakini familia yake
haihusiani na yale aliyoyafanya
Akiki ndiyo maana Rais
ameamua kuwapa hifadhi”
akasema Ruby wakaendelea na
mazungumzo mengine jhalafu
Ruby akaondoka akarejea
ofisini kwake
KAMPALA - UGANDA
Magari ya jeshi yaliendelea
kumwaga wanajeshi katika
mitaa ya jiji la Kampala
kufanya doria kuhakikisha jiji
linakuwa salama.Japo
shughuli ziliendelea kama
kawaida lakini watu walikuwa
na hofu kubwa kwamba
yangeweza kutokea
machafuko.
Katika ubalozi wa
Marekani jijini Kampala
alikokimbilia Jenerali
Akiki,ulinzi
uliimarishwa.Kikosi maalum
cha wanajeshi wa Marekani
kilifika haraka sana katika
ubalozi huo kikitokea katika
kambi ya wanajeshi wa
Marekani waliokuwa katika
program ya mafunzo maalum
kwa wanajeshi wa jeshi la
Uganda na kujiandaa
kukabiliana na hatari yoyote
ambayo ingeweza kutokea
ubalozini hapo.
Saa tatu toka yafanyike
mapinduzi na Jenerali Akiki
kukimbilia katika ubalozi wa
Marekani,helkopta mbili za
jeshi la Marekani kutoka
katika kambo yake iliyoko
nchini Kenya ziliwasili na
kutua katika ubalozi wa
Marekani nchini Uganda.Bila
kupoteza muda Balozi wa
Marekani nchini Uganda
akiwa na familia yake akaingia
katika mojawapo ya helkopta
ikaondoka halafu Jenerali
Akiki akaingizwa katika
helkopta nyingine akaondoka
kuelekea nchini Kenya.
“Ahsante Mungu kwa
kunisaidia nimeweza kutoka
salama Uganda.Waliofanya
mapinduzi walikuwa na lengo
la kuniua.Lakini
imewezekanaje yakapangwa
mapinduzi bila ya watu wangu
wa usalama kufahamu?
Naamini katika mpango huu
wa mapinduzilazima
walifahamu lakini wakakaa
kimya.Kwa sasa
kinachoniumiza kichwa ni
familia yangu.Je
wamefanikiwa kutoka salama
au wanashikiliwa na jeshi?
Akajiuliza Jenerali Akiki akiwa
ndani ya helkopta wakielekea
nchini Kenya
“Watanzania wana methali
isemayo kikulacho ki nguoni
mwako.Leo nimeamini methali
hii ni ya kweli
kabisa.Sikutegemea kama Paul
Mukasa angeweza
kunipindua.Sasa nimeamini
Paul na Profesa Joseph
walikuwa kitu
kimoja.Sikuelewa profesa
Joseph aliposema kwamba
hata kama nikimuondoa yeye
ataibuka mwingine kuendeleza
pale alipoishia sasa
nimefahamu mtu aliyekuwa
anamzungumzia ni Paul
Mukasa ambaye
nimemlea,nimemfundisha
nimempandisha cheo hadi
akawa mkuu wa majeshi lakini
leo hii kwa kufuata ushauri wa
wabaya wangu ameamua
kunisaliti akanipindua.Kweli
katika hii dunia hupaswi
kumuamini mtu yeyote.Wa
kuaminiwa ni Mungu
pekee.Nilimuamini Melanie
mwisho wa siku akanivua nguo
na kuanika mipango
yetu,nilimuamni Mukasa
nikamuweka katika nafasi ya
juu kabisa lakini malipo yake
ni kunipindua tena kama
walinzi wangu wasingewahi
kuniokoa ningeweza hata
kuuawa.Ngoja nikatulize
kwanza akili niitafute familia
yangu na baada ya kuwapata
ninaahidi Uganda
haitakalika.Paul Mukasa
atajuta kile alichokifanya !
akawaza Jenerali Akiki
Iliwachukua saa moja na
dakika arobaini kuwasili
nchini Kenya wakaelekea moja
kwa moja katika kambi ya
kijeshi ya Marekani iliyokuwa
nje ya jiji la Mombasa.Dakika
chache baada ya kuwasili
katika kambi hiyo ya kijeshi ya
vikosi vya Marekani vilivyoko
nchini Kenya katika
operesheni ya
kulisambaratisha kundi la
kigaidi la Alshabaab,Jenerali
Akiki akapelekwa katika
chumba cha mikutano ya moja
kwa moja kwa njia ya video
ambako alikutana na mkuu wa
kambi ile.
“Jenerali Akiki karibu sana
katika kambi yetu.Naitwa
Kanali Robert Darby mkuu wa
kambi hii ya wanajeshi wa
Marekani hapa Mombasa.Pole
sana kwa kilichotokea”
“Ahsante sana Kanali
Robert.Ninashukuru mno kwa
kunitoa Uganda na kunileta
hapa” akasema Jenerali Akiki
“Kabla ya yote kuna mtu
anataka kuzungumza nawe”
akasema Kanali
Robert,akabonyeza kitanza
mbali na katika runinga
akaonekana Rais wa Marekani
William Washington
“Mheshimiwa Rais,
Jenerali Akiki yuko tayari kwa
mazungumzo”akasema Kanali
Robert
“Jenerali Akiki” akasema
Rais William Washington
“Mheshimiwa Rais !
akasema Jenerali Akiki
“Pole sana Jenerali Akiki
kwa yaliyotokea
leo.Sijafurahishwa na huu
mfululizo wa mapinduzi
unaoendelea katika nchi za
Afrika.Kilichotokea leo ni
kama ugonjwa ambao
umeenea kwa kasi barani
Afrika.Kumekuwa na
mapinduzi katika nchi mbali
mbali na wakati mwingine
kupelekea umwagikaji
mkubwa wa
damu.Ninakuhakikishia mimi
na serikali yangu
hatukubaliani na hiki
kilichofanywa na jeshi na
hatuiungi mkono serikali hiyo
inayoongozwa na jeshi.Bado
tunaendelea kukutambua
wewe kama Rais halali wa
Uganda”akasema Rais William
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais kwa maneno
hayo”
“Nini mipango yako baada
ya haya yote kutokea?akauliza
Rais William
“Kwa sasa baada ya kuwa
niko sehemu salama ninataka
kuitafuta familia yangu ambao
mpaka sasa sifahamu mahala
walipo.Sijui kama wako hai au
wanashikiliwa na jeshi”
akasema Jenerali Akiki
“Usihofu Jenerali
Akiki.Nitawaelekeza maafisa
wa ubalozi wetu nchini
Uganda wafuatilie kujua
mahala iliko familia yako kisha
watachukuliwa na kuletwa
hapo Mombasa kisha tutajua
nini cha kufanya.Kwa sasa
endelea kupumzika hapo
wakati taratibu nyingine
zikiwekwa sawa”
“Nashukuru sana
mheshimiwa Rais kwa msaada
huu mkubwa ambao sikuwa
nimeutarajia” akasema
Jenerali Akiki na Rais William
akazima runinga yake
“Rais William yuko
sahihi.Afrika huu ugonjwa wa
mapinduzi tayari umeota
mizizi.Ngoja kwanza niipate
familia yangu halafu
nitajipanga namna ya
kuwafundisha adabu wasaliti
hawa.Ninaapa Uganda na
Afrika Mashariki kwa ujumla
hakutakalika.Wamekosea sana
kunipindua
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 7
Wakati bado tukio la
mapinduzi ya kijeshi nchini
Uganda yaliyomuondoa
madarakani Rais Jenerali
Akiki Rwamirama
halijapoa,Afrika Mashariki
iliamshwa na taarifa nyingine
za kustusha na
kuhuzunisha.Familia ya
Jenerali Akiki ambayo iliomba
kupatiwa hifadhi nchini
Tanzania ilifariki yote katika
ajali ya gari.
Saa moja na dakika ishirini
na mbili za asubuhi baada ya
kumaliza mazoezi ya asubuhi
Ruby alirejea chumbani kwake
kwa ajili ya kuoga ili ajiweke
tayari kuikabili
siku,alipotazama simu yake
akakuta amepigiwa na watu
kadhaa wa idara yake pamoja
na Gosu Gosu
“Kuna nini asubuhi yote
hii wanaanza kunitafuta?
Akajiuliza na kuamua
kumpigia kwanza Gosu Gosu
“Hallo Gosu Gosu.Vipi hali
yako?akauliza Ruby
“Ninaendelea vyema.Vipi
wewe uko salama?
“Salama kabisa”
“Nilikupigia simu ikaita
bila kupokelewa nikapata
wasiwasi” akasema Gosu Gosu
“Nilikuwa mazoezini.Is
everything okay?akauliza Ruby
“Jana tulipokuwa
tunazungumza kuhusiana na
mapinduzi ya kijeshi nchini
Uganda ulinieleza kwamba
familia ya Rais aliyepinduliwa
iliomba hifadhi nchini
Tanzania”
“Ndiyo waliomba hifadhi
nchini Tanzania na rais
akamuelekeza waziri wa
mambo ya ndani ya nchi
ahakikishe familia hiyo
inapewa hifadhi”
“Ulionyesha wasi wasi
kuhusiana na usalama wao
wakiwa hapa nchini.You knew
something was going to
happen to them? Akauliza
Gosu Gosu
“Kwani vipi Gosu Gosu
mbona maswali
mengi?akauliza Ruby
“Taarifa ambazo
zimepatikana asubuhi hii ni
kwamba familia yote
wamefariki katika ajali ya gari
alfajiri ya leo wakati wakija
Dar es salaam”
“Ajali ya gari?! akauliza
Ruby kwa mshangao
“Ndiyo Ruby.Taarifa
zinadai kwamba gari
walilokuwa wamepanda
liligongana na lori kubwa la
mizigo na watu wote
waliokuwa katika gari hilo
dogo wamepoteza maisha”
“Jesus Christ ! akasema
Ruby kwa mstuko.Akabaki
ameduwaa kwa muda hadi
pale Gosu Gosu alipomstua
“Ruby !
“Gosu Gosu taarifa hizi ni
za kweli? Akauliza
“Ni taarifa za kweli
kabisa.Ni taarifa ambayo
imesambaa sana katika
mitandao ya kijamii na hata
katika taarifa ya habari ya
asubuhi leo wametangaza”
“Dah ! akasema Ruby na
kufikiri kidogo halafu akasema
“Gosu Gosu ahsante kwa
kunipa taarifa
hizi.Nitawasiliana nawe tena
baadae” akasema Ruby na
kukata simu
“Aaaaggghh !! akasema
kwa hasira baada ya kumaliza
mazungumzo na Gosu Gosu
“Hii si ajali ya kawaida.He
killed them ! akasema kwa
uchungu
“Tulikubaliana
akanihakikishia kwamba
hatawaua tena kumbe alikuwa
ananidanganya ili
kuniridhisha.Ameniudhi mno
Dr Fabian.Sikutegemea kama
angeweza kufanya kitu kama
hiki cha kukatili uhai wa watu
wasio na hatia yoyote !
akawaza Ruby na kuchukua
simu akampigia Dr Fabian
lakini hakupokea simu.
“Kwa nini viongozi hawa
wanakuwa wakatili kiasi hiki?
Amepata faida gani baada ya
kuwaua familia ile?Mke wake
amerejea baada ya kuua
familia ya Jenerali
Akiki?Badala yake amechuma
dhambi bure kwani watu wale
hawakuwa na tatizo lolote
naye.Hawakuwa na hatari
yoyote kwa nchi” akawaza
Ruby akiwa amekaa kitandani
“Nitawezaje kufanya kazi
na mtu kama huyu ambaye
anatumia madaraka yake kuua
kila amtakaye?Hapana
hatuwezi kwenda namna
hii.Vifo vya familia ya Akiki
vimeniumiza sana” akawaza
Ruby na kumpigia tena simu
Dr Fabian lakini
haikupokelewa.
“Hata kama hapokei simu
nitamfuata huko huko na
kumueleza ukweli” akawaza
Ruby akiwa amefura hasira
MOMBASA – KENYA
Saa tatu za asubuhi balozi
wa Marekani nchini Uganda
ambaye amehamishiwa nchini
Kenya kufuatia mapinduzi ya
kijeshi yaliyomuondoa
madarakani Rais Jenerali
Akiki,aliwasili katika kambi ya
wanajeshi wa Marekani
alikokuwa amehifadhiwa
Jenerali Akiki.Akiongozana na
Kanali Robert Darby
wakaelekea moja kwa moja
katika chumba alimolala
Jenerali Akiki
“Habari za asubuhi
mheshimiwa Rais” akasema
balozi
“Karibuni.Kuna taarifa
zozote kuhusu familia
yangu?Mmekwisha fahamu
mahala walipo? Akauliza
Jenerali Akiki akionekana
kuwa na wasiwasi
“Mheshimiwa
Rais,tumepokea taarifa
asubuhi hii kutoka kwa watu
wetu waliotumwa kufuatilia
mahala ilipo familia yako”
akasema balozi
“Familia yangu iko
salama?akauliza Akiki
“Mheshimiwa Rais kwa
taarifa tulizonazo ni kwamba
baada ya mapinduzi kutokea
familia yako waliokolewa na
walinzi na wakaelekea nchini
Tanzania ambako waliomba
kupewa hifadhi……”
“Subiri kwanza.Unasema
familia yangu waliomba
hifadhi Tanzania? Akauliza
Jenerali Akiki
“Ndiyo,waliomba hifadhi
nchini Tanzania na
wakakubaliwa”
“Mungu wangu ! akasema
Jenerali Akiki akionyesha
wasiwasi mkubwa.
“Wako salama?akauliza
baada ya ukimya wa sekunde
kadhaa
“Mheshimiwa Rais taarifa
zilizopatikana asubuhi ya leo
kutoka Tanzania zinasema
familia yako yote wamefariki
katika ajali ya gari wakati
wakielekea Dar es salaam
usiku wa kuamkia leo”
Jenerali Akiki aliyekuwa
amesimama akahisi miguu
inamuisha nguvu taratibu
akaanza kwenda chini Kanali
Robert akamdaka na
kumketisha sofani.
“Ee Mungu baba kwa nini
umeniadhibu namna hii?
Ungenipa adhabu nyingine
yoyote lakini si kunichukulia
familia yangu.Wanangu
walikuwa kila kitu katika
maisha yangu ! akasema kwa
uchungu Jenerali Akiki akiwa
amefunika uso wake kwa
viganja vya mikono.Kanali
Robert na balozi wakatoka
wakamuacha Jenerali Akiki
peke akiendelea kububujikwa
na machozi
“Dr Fabian ! akasema kwa
hasira
“Naamini hii ni mipango
ya Dr Fabian kulipiza kisasi
kwangu.Hata mpango huu wa
mapinduzi ni yeye
aliyeshirikiana na jeshi
kuuandaa na hakuridhika
kunitoa madarakani akaamua
kuimaliza na familia yangu
pia.Ameniumiza
sana.Nitawaliliaje familia
yangu? Akaendelea kuwaza
Jenerali Akiki akiendelea
kububujikwa machozi
“Ninaapa kama
nitaendelea kuwa hai nitalipiza
kisasi kibaya sana kwa Uganda
na Tanzania.Nchihizi mbili
nitahakikisha hazikaliki !
akawaza
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Katika chumba kimoja
ndani ya ikulu ya Marekani
watu wanne walikutana kwa
ajili kikao cha
dharura.Aliyeitisha kikao
hicho ni Mark Piller makamu
wa rais wa Marekani.
“Ahsanteni sana kwa
kufika katika kikao hiki cha
dharura na nimewaiteni hapa
kwa sababu ninyi ni watu
ninaowaamini.Tumekuwa
tunashirikiana katika mipango
mbali mbali yenye maslahi
kwa Marekani” akafungua
kikao makamu wa Rais
“Kama mlivyosikia kile
kilichotokea nchini
Uganda.Jeshi limempindua
Rais wa nchi hiyo Jenerali
akiki Rwamirama na jenerali
Paul Mukasa aliyekuwa mkuu
wa majeshi amejitangaza kuwa
Rais wa Uganda.Mahusiano
kati ya Uganda na Marekani
kwa siku za hivi karibuni
yameboreka hasa baada ya
kumpeleka balozi mpya
ambaye amefanya kazi kubwa
ya kuimarisha mahusiano ya
nchi hizi mbili.Baada ya
mapinduzi hayo kutokea
Jenerali Akiki aliomba hifadhi
katika ubalozi wetu jijini
Kampala.Kutokana na hali tete
ya usalama ilitulazimu
kumuhamisha na kumpeleka
katika kambi yetu ya kijeshi
iliyoko Mombasa Kenya
ambako yuko hadi sasa na
yuko salama”akasema Mark
Piller
“Huu mchezo wa kupindua
serikali umeanza kuota mizizi
katika bara la afrika hivi
sasa.Ndani ya miezi sita tayari
serikali zaidi ya tano
zimekwisha pinduliwa”
akasema mmoja wa wale watu
walioshiriki kikao kile
“Katika kila mapinduzi
unayoyaona yanatokea barani
Afrika lazima kuna mkono wa
mataifa ya nje hasa mataifa
makubwa” akasema Mark
Piller
“Haya mapinduzi ya
Uganda kuna taifa lolote
linahisiwa limehusika?
“Ni mapema bado kusema
chochote hadi pale uchunguzi
utakapofanyika” akajibu Mark
Piller
“Tumemuhifadhi Rais
huyo wa Uganda katika kambi
yetu nini mipango yake au
mipango yetu? Akauliza
mshiriki mwingine wa kikao
kile
“Ndiyo maana nimewaita
hapa ili tujadiliane kuhusu
suala hili.Mapinduzi haya
yanaweza kuwa na faida
kwetu. Jenerali Akiki anaweza
kuwa muhimu kwetu”
“Faida zipi tunaweza
kuzipata kutokana na
mapinduzi haya? Akauliza
mmoja wa washiriki wa kile
kikao
“Mafuta” akasema Mark
Piller na kuwatazama wenzake
halafu akaendelea
“Kwa taarifa
zilizopatikana,Uganda ina
akiba kubwa sana ya mafuta
kuliko nchi zote kusini mwa
jangwa la Sahara.Utafiti
unaonyesha kuwa inaweza
kuongoza kuwa na kiwango
kikubwa cha mafuta barani
Afrika.Tunaweza kuitumia
fursa hii kujipatia akiba ya
mafuta kutoka Uganda.Kwa
sasa kumekuwa na uhaba
mkubwa wa mafuta duniani
baada ya nchi wazalishaji
wakubwa wa mafuta kuzalisha
kwa kiasi kidogo tofauti na
mahitaji ya dunia ili
kupandisha bei.Tunahitaji
mafuta hivyo hatuwezi
kutegemea mafuta ya nchi za
Mashariki ya kati wakati zipo
nchi zina akiba kubwa ya
mafuta na tunaweza kuyapata
bila gharama kubwa na
mojawapo ikiwa
Uganda”akasema Mark Piller
“Hilo ni wazo zuri sana
mheshimiwa makamu wa
Rais.Bei ya mafuta katika soko
la dunia imepanda mno na
kama nchi ya Uganda ina akiba
kubwa ya mafuta litakuwa
jambo zuri lakini ni namna
gani tutaweza kuyapata hayo
mafuta?
“Wazo langu ni kumleta
Jenerali Akiki hapa Marekani
kisha nitazungumza naye na
kumshawishi kumpatia makazi
hapa Marekani na huo
utakuwa ni mwanzo wa
kuelekea katika mpango wa
kuelekea katika mafuta.Kama
tunakubaliana na mpango huu
basi nataka tufanye maandalizi
ili Jenerali Akiki aweze
kuletwa kwa siri hapa
Marekani” akasema Mark
Piller na mazungumzo
yakaendelea kisha wote
wakafikia makubaliano juu ya
suala lile
BAADA YA SAA MBILI
MOMBASA KENYA
Zilipita saa mbili toka
Jenerali Akiki alipopewa
taarifa za vifo vya familia
yake.Kanali Robert na balozi
wa Marekani nchini Uganda
wakarejea tena katika chumba
kile cha Jenerali Akiki
“Pole sana Jenerali Akiki”
akasema balozi
“Kuna taarifa nyingine
mmezipata kuhusu familia
yangu?
“Taarifa tulizozipata ni
kwamba utaratibu unafanyika
hivi sasa nchini Tanzania kwa
kushirikiana na balozi wa
Uganda nchini Tanzania ili
miili ya marehemu iweze
kurejeshwa Uganda kwa
mazishi.Tutaendelea
kukujulisha kila
kinachoendelea” akasema
balozi
“Ouh jamani ! akasema
Jenerali akiki na kuinamisha
kichwa
“Jenerali Akiki hiki ni
kipindi kigumu sana kwako
lakini unapaswa kuwa
jasiri.Wewe ni mwanajeshi
ukianguka hupaswi kulala
hapo,inuka na usonge
mbele.Mapambano
yanaendelea na ili uweze
kupambana unahitajika uwe
jasiri sana” akasema Kanali
Robert
“Sijawahi kuumia namna
hii katika maisha yangu !
“Pamoja na yote haya
Jenerali Akiki hupaswi kukata
tamaa.Kama alivyosema
Kanali Robert kwamba
mapambano bado
yanaendelea,inuka kamata
silaha songa mbele” akasema
balozi
“Nipambane na nani kwa
nini?Nimekata tamaa kabisa
sioni hata sababu ya kuendelea
kupambana.Nilipambana
kumuondoa dikteta nchini
Uganda ambaye aliiipeleka
nchi shimoni,nimeirudisha
nchi katika ramani ya dunia na
haya ndiyo malipo
yake.Imetosha.Sitaki tena
mapambano sitaki kitu
chochote.Ninachokihitaji hivi
sasa ni kufa nikaungane na
familia yangu ! akasema kwa
uchungu Jenerali Akiki huku
machozi yakiendelea kumtoka
“Jenerali Akiki maneno
kama hayo hayapaswio
kutamkwa na mwanajeshi
kama wewe.Umepitia mambo
mengi hadi kufika hapa
ulipofika na hujawahi
kushindwa na mafanikio yote
uliyoyapata ni kwa sababu ya
kutokata tamaa.Unalopitia
sasa hivi ni kubwa lakini
hupaswi katu kukata
tamaa.Mungu ana sababu zake
kwa nini amekuacha
hai.Ungeweza kuuawa katika
mapinduzi yale lakini walinzi
wako walikuokoa na hivi sasa
uko katika mikono salama.Hii
yote ni mipango ya Mungu”
“Mungu yupi ? akauliza
Jenerali Akiki
“Sidhani kama yupo huyo
Mungu kwani asingekubali
familia yangu yote iteketee !
akasema Jenerali Akiki kwa
hasira
“Jenerali Akiki,nimepewa
maelekezo na makamu wa Rais
wa Marekani kwamba
tukuondoe hapa na
kukupeleka nchini
Marekani.Atakuwa na
mazungumzo nawe marefu
hivyo jiandae ndani ya nusu
saa kutoka sasa utaondoka na
ndege ya jeshi kuelekea
Marekani” akasema Balozi na
Jenerali Akiki hakujibu
kitu.Balozi na Kanali Robert
wakatoka wakimuacha
Jenerali Akiki katika tafakari
nzito.
DAR ES SALAAM –
TANZANIA
Ruby aliwasili ikulu kwa
ajili ya kuonana na Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania.Ni kawaida yake
kufika hapa kila asubuhi ili
kumpa Rais muhtasari wa kile
kinachoendelea ndani ya idara
ya SNSA.Asubuhi hii hakuwa
na faili lolote alilobeba zaidi ya
mkoba wake mdogo.
Akiwa ndani ya ofisi
yake,Dr Fabian alisikia
mabishano nje ya ofisi yake na
mara mlango ukafunguliwa
akaingia Ruby akiwa
ameongozana na katibu
muhtasi wa Rais.
“Mzee nimempa
maelekezo lakini
amenipuuz…..”
“It’s ok Sauda” akasema Dr
Fabian na Sauda akatoka
akamuacha Ruby katika ofisi
ya Rais
“Karibu uketi” akasema Dr
Fabian huku akiendelea na
shughuli zake
“What’s the meaning of
this?akauliza Ruby na Dr
Fabian akalifunika faili
alilokuwa analipitia
“Unamaanisha nini
Ruby?akauliza Dr Fabian
“Hupokei simu yangu,
halafu umetoa maelekezo
hakuna mtu kuingia ofisini
kwako leo.Nini maana yake?
Unanizuia hata mimi? akauliza
Ruby
“Ruby eleza kilichokuleta
uondoke ukaendelee na
shughuli zako.Leo si siku nzuri
kwangu ! akasema Dr
Fabian.Ruby akamtazama
halafu akasema
“Hatimaye umefanikisha
lengo lako”
“Lengo gani Ruby?
“You killed them”
“Akina nani?
“Familia ya Jenerali Akiki !
“Taarifa niliyoipokea ni
kwamba wamefariki katika
ajali ya gari na hakuna mtu
aliyewaua.Sihusiki na chochote
katika vifo hivyo” akasema Dr
Fabian na Ruby akaendelea
kumtazama kwa macho makali
“Nini umekipata baada ya
kuiteketeza familia ambayo
haikuwa na hatari yoyote kwa
nchi? Umepata amani ya
moyo? Mkeo Millen amerejea?
Akauliza Ruby kwa sauti kali
na Dr Fabian akanyanyuka
kwa hasira
“Ruby chunga sana ulimi
wako.Hapa unazungumza na
Rais wa jamhuri ya Muungano
wa Tanzania na si hawara yako
hivyo kuwa na heshima. Wewe
ni nani wa kuja kunipandishia
sauti? Umeanza kupoteza
heshima Ruby kuwa
muangalifu sana ! akafoka Dr
Fabian
“I’m sorry Mr President !
akasema Ruby
“One more thing,usirudie
tena kulitamka jina la mke
wangu kama unataja boga !
akafoka Dr Fabian huku
akimnyooshea Ruby kidole.
“Samahani mheshimiwa
Rais sintarudia tena”akasema
Ruby
“Na iwe hivyo.Heshimu
ofisi hii na usije tena ukaanza
kunifokea ! akasema Dr Fabian
wakatazamana kwa muda
akaketi
“Sit ! akasema Dr Fabian
na Ruby akaketi
“Nina ratiba ndefu siku ya
leo.Tuzungumze masuala ya
kazi na si masuala hayo
mengine yasiyohusiana na kazi
yako”
“Mheshimiwa
Rais,kilichonileta hapa kwako
ni suala hilo la familia ya
Jenerali Akiki”
“Hilo suala nimekwisha
lifunga.Sitaki mjadala wa suala
hilo uendelee.Umenisikia
Ruby?
“Nimekusikia mheshimiwa
Rais” akajibu Ruby
“Good.kama hakuna
lingine nenda kaendelee na
shughuli zako kama ukiwa na
jambo muhimu
tutawasiliana.Suala la hiyo
ajali linashughulikiwa na jeshi
la polisi wao ndio watakaotoa
taarifa nini hasa
kilichosababisha ajali hiyo”
akasema Jenerali Akiki na
Ruby akasimama akachukua
mkoba wake akaanza kupiga
hatua kuelekea
mlangoni.Kabla hajakishika
kitasa cha mlango akasimama
akafikiri kidogo halafu
akageuka akaudi mezani
“Kuna kitu umesahau
Ruby?akauliza Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais”
akasema Ruby na kunyamaza
akamtazama Dr Fabian
“Nini unataka kusema
Ruby?akauliza Dr
Fabian.Ruby akameza mate na
kusema
“Mheshimiwa Rais
utanisamehe kwa hiki
ninachokisema lakini ni lazima
nikiseme.Nina uhakika
mkubwa ajali ile
imetengenezwa ili kuiondoa
familia ile.Lakini fahamu
kwamba umefanya kosa kubwa
na hiki ulichokifanya iko siku
athari zake utaziona” akasema
Ruby kisha wakaangaliana kwa
sekunde kadhaa halafu Dr
Fabian akauliza
“Umemaliza?
“Ndiyo mheshimiwa Rais”
“Good.Go back to work”
akasema Dr Fabian na Ruby
akageuka akaondoka
“Huyu mwanamke
itanilazimu niwe naye makini
sana.Anaonekana si mtu
ambaye anaweza akanisikiliza
kwa kila ninachomuamuru
kukifanya.Hapendi kupindisha
mambo.Nisipokuwa makini
naye iko siku anaweza
akaniingiza katika matatizo”
akawaza Dr Fabian huku
akichezea kalamu yake
“Edwin Mbeko alikuwa
mtiifu sana alifanya kila
nilichomuelekeza lakini kwa
huyu japo anafanya kazi yake
vizuri ila nitapata wakati
mgumu sana kumtumia katika
mambo yangu binafsi.Lakini
watu kama hawa dawa yao ni
ndogo tu.Nitaanza kumuweka
karibu yangu.Yawezekana
labda mimi naye hatujazoeana
sana ndiyo maana anakuwa
mzito kutekeleza majukumu
yangu.Huyu hataweza
kunisumbua dawa yake ni
ndogo tu” akawaza Dr Fabian
huku akitabasamu
Ruby alipotoka kuonana
na Rais hakurejea tena ofisini
kwake akafululiza moja kwa
moja kwa Gosu Gosu
“Ahsante sana Ruby kwa
kuja kunitembelea.Ninapata
faraja kubwa kwa namna
mnavyonijali” akasema Gosu
Gosu
“Usijali Gosu Gosu.Sisi
tayari ni ndugu moja hivyo
lazima kufuatilia maendeleo
yako kwa karibu sana”
akasema Ruby
“Is something wrong
Ruby?akauliza Gosu Gosu
“Nothing wrong Gosu
Gosu”
“Hapana Ruby.Sura yako
inaonyesha wazi kuna kitu
kinakusumbua.Niambie kuna
tatizo gani linakusumbua?
Akauliza Gosu Gosu
“He killed them ! akasema
Ruby kwa hasira
“Nani unamzungumzia?
“Rais Dr Fabian ! akasema
Ruby
“Kafanya nini Rais?
“Naamini ndiye
aliyeelekeza familia ya Jenerali
Akiki wauawe”
“Kwa nini unasema hivyo
Ruby?
“Alinipa maelekezo
kutuma timu ya kuwaua lakini
nilikataa.Idara yetu
inashughulika na usalama wa
nchi na familia ile hawakuwa
na hatari yoyote kwa nchi !
akasema Ruby na kuinamisha
kichwa kwa sekunde chache
halafu akasema
“Imeniumiza
sana.Kulikuwa na watoto
wadogo ambao hawafahamu
hata mambo anayoyafanya
baba yao.Kwa nini wauawe
bila kosa? Hii si sawa hata
kidogo” akasema Ruby
“Uko sahihi Ruby.Kama
familia hiyo hawakuwa na
hatari yoyote kwa nchi
hakukuwa na sababu ya
kuuawa” akasema Gosu Gosu
“Hicho ndicho
kinachoniumiza zaidi !
akasema Ruby
“Lakini isikuumize sana
kwani idara yako haijahusika
katika suala hili.Imekuwa
vizuri umemuweka wazi na
ameufahamu msimamo wako
lakini ………..” Akasema Gosu
Gosu na kunyamaza kidogo
“Lakini nini?
“Kwa hiki ulichokifanya
cha kukataa kuifanya kazi yake
kinavuruga mahusiano mazuri
mliyo nayo na inaweza ikakupa
ugumu kufanya kazi
zako.Idara hii ya usalama wa
ndani inatumiwa sana na
marais katika kufanikisha
baadhi ya masuala yao
binafsi.Viongozi wote wa SNSA
waliopita walikuwa watiifu
kwa marais na walitekeleza
kila walicho watakiwa
wafanye”
“Mimi ni tofauti na hao
waliopita ! akasema Ruby
“Ruby naamini Rais
hajafurahishwa na hiki
ulichokifanya kukataa
kushiriki mauaji ya familia ya
Jenerali Akiki.Nina wasi wasi
sana kama mazingira ya
kufanya kazi yako yatakuwa
rafiki.Rais anaweza akakuona
wewe kama kikwazo katika
kufanikisha mambo yake hivyo
akafikiria hata kukuondoa”
akasema Gosu Gosu
“Unalosema ni kweli lakini
sina hakika kama Dr Fabian
anaweza akafikia hatua hiyo”
akasema Ruby
“Ushauri wangu
mdogo,achana na hiyo kazi
tufanye biashara.Yale
makampuni yote ambayo
Melanie aliyanunua kwa
Peniela yamerudishwa kwa
Mathew na yanahitaji
usimamizi.Achana na hiyo kazi
ambayo tayari imeanza kuleta
mtafaruku.Naamini atakuja
tena na suala lingine
atakuelekeza ulifanye na
ukikataa utakuwa adui
yake.Kwa nini ifike huko?
Angali bado mapema achana
na hiyo kazi na tujikite kwenye
biashara” akasema Gosu
Gosu,Ruby akatabasamu
“Ni mapema mno
kuogopa.Nina muda mfupi
ndani ya SNSA hivyo sipaswi
kuogopa.Ngoja nijipe muda
zaidi na kama kukionekana
kuna hatari yoyote kwa mimi
kuendelea kufanya kazi SNSA
basi nitafuata ushauri wako”
akasema Ruby
“Sawa Ruby uamuzi ni
wako lakini kuwa makini sana”
akasema Gosu Gosu
wakaendelea na mazungumzo
mengine kisha Ruby
akaondoka kuelekea ofisini
kwake
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 8
Imetimu saa mbili za usiku
Ruby akiwa amejipumzisha
nyumbani kwake gari nne
nyeusi zilifika katika geti la
nyumba yake.Akiwa sebuleni
kwake aliona taa ya kijani
ikiwaka katika kisanduku
kilichokuwa ukutani pembeni
ya runinga iliyounganishwa na
kamera za usalama
zilizofungwa kuzunguka
nyumba yake.Taa ile ya kijani
huwaka pale geti kubwa
linapofunguliwa.Alistuka na
haraka haraka akachukua
kitanza mbali akabonyeza
kamera ya getini akaziona gari
nne zikiingia
“Nani hawa? Mbona sina
ratiba ya kuonana na mtu
yeyote usiku huu?Kwa nini
walinzi wameruhusu watu
kuingia bila kunijulisha?
Akajiuliza
Ruby.Aliogopa.Haraka haraka
akacheza na kompyuta yake na
kuifunga milango yote kwa
ndani halafu akaendelea
kuwafuatilia watu wale kujua
ni akina nani.Gari mbili za
mbele wakashuka watu
waliovalia suti nadhifu na
kulizunguka gari la tatu.Macho
yao hayakutulia waliangaza
kila kona kisha wawili kati ya
wale jamaa wakaelekea katika
mlango mkubwa
wakagonga.Ruby
akawachunguza kwa makini
kwa kutumia kamera ya
mlangoni
“Akina nani hawa?Mbona
siwafahamu?Wanataka
nini?akajiuliza Ruby wale
jamaa wakiendelea kugonga
mlango.Akachukua simu na
kuwapigia walinzi wake getini
kuuliza kwa nini wameruhusu
watu kuingia bila ruhusa yake
na akajibiwa kwamba
wamelazimka kufungua kwani
ni msafara wa Rais.Haraka
haraka Ruby akaenda mlango
akafungua.Wale jamaa wawili
wakaingia ndani wakakagua
sebuleni halafu mmoja wao
akausogeza mkono ake aliovaa
saa karibu na mdomoni wake
akasema
“Clear !
Haikupita hata dakika
moja mlango ukafunguliwa
wakaingia watu wanne kisha
akafuata Rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr
Fabian Kelelo
“Hello Ruby” akasema Dr
Fabian akitabasamu
“Mheshimiwa Rais !
akasema Ruby na Rais
akawataka wale walinzi wake
watoke nje
“Umenistua sana
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby
“I’m sorry Ruby.Sikutaka
kukueleza kama ninakuja
kwako nilitaka
nikustukize”akasema Dr
Fabian
“Karibu sana.Utapenda
kunywa nini? Akauliza Ruby
“Chochote
utakachoniandalia
nitashukuru”
Ruby akaenda katika
kabati ambalo huhifadhi
vinywaji vikali akachukua
chupa mbili na kuziweka
mezani,akammiminia Rais
kinywaji katika glasi na yeye
akajimiminia
“Karibu”
“Ahsante Ruby”
“Ungeniambia kama
utakuja ili nikuandalie hata
chakula kidogo” akasema Ruby
“Usijali Ruby.Nilitaka
nikustukize nione namna
unavyoishi hapa.Are you
alone?
“Ndiyo niko peke yangu”
akajibu Ruby
“Kwa nini unaishi
mwenyewe?Huna mtu wa
kuishi naye?
“Nina mfanyakazi wa
ndani ambaye kuanzia jana
amepata dharura amekwenda
kumuuguza mama yake
mgonjwa,vile vile nina walinzi
na kama haitoshi nina mbwa
anaitwa Bravo nilipewa na
Mathew ninampenda sana”
akasema Ruby
“Wewe na Mathew
mnaonekana mna ukaribu
mkubwa”
“Ni kweli mheshimiwa
Rais nina ukaribu na Mathew
Mulumbi”
“Vizuri sana.Lakini
unahitaji kuwa na mwenzi
sasa.Utaishi namna hii hadi
lini? Akauliza Dr Fabian na
Ruby akatoa kicheko kidogo
“Mambo hayo
mheshimiwa Rais hayataki
haraka.Muda utakapofika basi
nitakuwa naye lakini kwa sasa
nimejielekeza katika kazi
yangu”
“Kwa hiyo huna
mchumba? Akauliza Dr Fabian
na Ruby akacheka tena kidogo
“Mchumba ninaye ila yuko
nje ya nchi”
“Hongera.Ana bahati sana
huyo aliyekupata.Siku akija
nchini umlete kwangu
nimfahamu”
“Usijali mheshimiwa Rais
nitamleta” akasema Ruby na
ukimya mfupi ukapita
“Ruby nimekuja hapa bila
taarifa kuna suala ambalo
limenileta usiku huu” akasema
Dr Fabian na kunyamaza
kidogo halafu akaendelea
“Ulipokuja ofisini kwangu
asubuhi ya leo hatukuwa na
mazungumzo
mazuri.Nilikutolea maneno
ambayo si ya
kiungwana.Nafahamu
nilikukera hivyo nimekuja
kukuomba msamaha.Siku ya
leo haikuwa siku nzuri kwangu
ndiyo maana nilikuwa katika
hali ile.Nakuhakikishia it won’t
happen again” akasema Dr
Fabian na Ruby akatabasamu
“Mheshimiwa Rais mambo
kama yale ni ya kawaida
kutokea katika sehemu za kazi
hivyo sikushangaa kwa vile
nimekwisha yazoea.Nimefanya
kazi katika ofisi ambayo
inaweza kumpa mtu shinikizo
la damu lakini nilimudu vyema
na ndiyo maana hawakutaka
niondoke hivyo suala lile
lilimalizika pale pale.Mimi pia
ninaomba samahani sana kwa
tabia yangu asubuhi
ile.Nilikosa heshima kwako
mkuu wa nchi,sikupaswa
kuzungumza nawe namna
ile.Nami pia naomba
unisamehe mheshimiwa Rais
hata kama nitakuwa na jambo
limenikaba kooni nitajitahidi
kutafuta namna nzuri ya
kuliwasilisha” akasema Ruby
“Nimekusamehe Ruby”
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby na Dr Fabian
akanyanyua glasi yake
“Friends again?
Ruby akatabasamu na
kusema
“Friends” kisha
wakagonganisha glasi zao.
“Mheshimiwa Rais
ninataka kuuliza na ninaomba
uwe mkweli na muwazi
kwangu”
“Usijali Ruby uliza”
“You did it? Akauliza Ruby
na Dr Fabian akawa kimya kwa
muda halafu akatingisha
kichwa kukubali
“Yes I did it” akasema na
kunyamaza kidogo
“Naomba niwe muwazi
kwako Ruby.Ajali ile ilikuwa ya
kutengeneza kwa lengo la
kuwamaliza familia ya
Akiki.Nina hasira kubwa na
Jenerali Akiki kwa kitu
alichotaka kunifanyia na
niliapa kumfanyia kitu kibaya
sana na hasira hizo ndizo
ambazo zimenipelekea
kuimaliza familia yake namna
ile.Dr Natukunda alikuwa ni
rafiki wa mke wangu na
sikutegemea kama siku moja
ningeweza kumfanyia ukatili
huu lakini ni mume wake
ndiye aliyenifanya niwe na
roho ya ukatili hata
nikalazimika kuimaliza familia
ile yote.Ninataka nimuumize
Akiki.Kama si kwa jitihada
zenu ninyi kuweza kung’amua
mipango aliyokuwa nayo
Jenerali Akiki, hivi sasa tayari
ningekwisha kuwa marehemu
ndiyo maana wewe na
wenzako akina Mathew mnayo
nafasi kubwa ndani ya moyo
wangu kwani mlipambana
kuokoa maisha yangu.Jasiri
Mathew Mulumbi aliweza
kupambana na mtu mwenye
bomu ambalo lililengwa
kuniua.Mimi na Jenerali Akiki
tulikuwa marafiki na tulikuza
mashirikiano kati ya Uganda
na Tanzania.Kila ninapofirikia
kwa nini Akiki ajiunge katika
mpango wa kuniua ninajikuta
ninapatwa na hasira
kali.Hukupendezwa na kile
nilichokifanya kwa familia ya
Jenerali Akiki I’m so sorry
lakini sikuwa na namna
nyingine ya kufanya,roho ya
kisasi ilikwisha niingia”
akasema Dr Fabian na
kunyamaza akanywa funda
moja kisha akasema
“Kuna jambo lingine
ambalo nataka nikufahamishe
leo ambalo ni la siri
kubwa.Tumeufungua ukurasa
mpya hivyo sitaki kukuficha
jambo” akasema Dr Fabian
akanywa tena funda lingine
akasema
“Mapinduzi yaliyofanyika
jana nchini Uganda
yaliyomuondoa madarakani
Jenerali Akiki mimi pia
nimeshiriki katika kuyapanga”
Ruby aliyekuwa ameshika
glasi akiipeleka mdomoni
akajikuta akiishusha haraka
mezani kwa mshangao
alioupata.
“Nimekustua,samahani
kwa hilo lakini nimelazimika
kukueleza ukweli.Kuna kitu
kimoja ambacho unapaswa
ukifahamu kuhusu mimi.Nina
tatizo la kuamini watu ndiyo
maana jambo kama hili
nimelifanya mwenyewe kwa
siri na wewe ni mtu wa kwanza
unalifahamu kwa hapa
nchini.Nimechagua kukuamini
na kukushirikisha katika
mambo yangu nyeti” akasema
Dr Fabiana akanyamaza
akamtazama Ruby
“Dah ! akasema Ruby
“Kama nilivyokueleza
awali kwamba chuki
niliyokuwa nayo dhidi ya
Jenerali Akiki ni kubwa sana
hivyo nilidhamiria
kumuumiza,kumfanya awe na
maisha magumu.Niliwasiliana
na spika wa bunge la Uganda
nikamtaka aje Tanzania kimya
kimya nikazungumza naye kwa
kirefu kuhusiana na mambo
yote anayoyafanya Rais Akiki
naye alishangaa
sana.Hakufahamu kama
James Kasai alikuwa anaishi
jijini Kampala.Nilimpatia
rekodi ile ya Melanie Davis
tukakubaliana aitumie
kumtaka Akiki aachie ngazi
kwa hiari yake na kama
akigoma basi bunge litumike
kumuondoa.Tulitengeneza
mtandao mkubwa na
kumshirikisha pia mkuu wa
majeshi wa Uganda ili endapo
mpango wa kwanza wa
kumtaka aachie ngazi au
kuondolewa na bunge
kushindwa kufanikiwa basi
jeshi lifanye mapinduzi.Kwa
bahati mbaya katika mchakato
huo spika wa bunge la Uganda
aliuawa yeye na familia yake
na ndipo jeshi lilipochukua
nchi” akasema Dr Fabian na
kuchukua glasi akanywa funda
moja kubwa
“Say something Ruby !
akasema Dr Fabian
“Mheshimiwa Rais sijui
niseme nini.Nakushukuru kwa
kunieleza ukweli” akasema
Ruby
“Baada ya kuufahamu
ukweli nini maoni yako?Ni
wewe pekee ambaye una
uthubutu wa kusimama na
kunieleza ukweli.Usiogope
nieleze ukweli”
“Sina maoni yoyote
mheshimiwa Rais” akasema
Ruby na Dr Fabian akanywa
kinyaji kidogo halafu akasema
“Asubuhi wakati
unaondoka ofisini ukiwa
umekasirika ulinieleza
kwamba kwa hiki
nilichokifanya nitasababisha
matatizo
makubwa.Ulimaanisha nini?
“Zilikuwa ni hasira tu
mheshimiwa Rais lakini
sikumaanisha chochote.By the
way yuko wapi Jenerali Akiki
kwa sasa?
“Hajulikani
alipo.Alifanikiwa kutoroka
mara tu wanajeshi
walipovamia ikulu.Naamini
hata huko aliko salamu zangu
atazipata.Mali zake zote
zitataifishwa na serikali
atabaki hohehahe.Atapata
mateso makali na atakufa
taratibu”
“Kuna uwezekano
amejificha nchini
Uganda?akauliza Ruby
“Bado haijulikani lakini
jeshi linandelea na uchunguzi
kumtafuta mahala alipo”
akasema Dr Fabian na ukimya
ukapita
“Mheshimiwa Rais mimi
bado si mtaalamu sana wa
mambo ya kiusalama lakini
ushauri wangu ni kufanya kila
linalowezekana kuhakikisha
tunafahamu mahala alipo
Jenerali Akiki na
kummaliza.Kama ataendelea
kuwa hai nina uhakika
mkubwa atajipanga kulipiza
kisasi”
“Jeshi la Uganda
linaendelea na msako na
watanijulisha kila
watakachokipata halafu
tutaangalia nini cha
kufanya.Kwa kuwa ameondoka
madarakani Akiki hana nguvu
tena na hawezi kupanga njama
zozote.Mali zake zote ziko
nchini Uganda na zote
zimetaifishwa na jeshi hivyo
basi hana nguvu yoyote ya
kuweza kupanga shambulio la
aina yoyote ile”
Ruby na Dr Fabian
walikuwa na mazungumzo
marefu hadi ilipotimu saa tatu
za usiku ndipo Rais
alipoondoka kurejea ikulu
WASHINGTON DC –
MAREKANI
Jenerali Akiki alifikishwa
Marekani na kupelekwa katika
nyumba aliyoandaliwa jijini
Washington DC.Ilkuwa ni
nyumba nzuri kubwa na yenye
ulinzi wa kutosha.
“Maisha yana maajabu
sana.Yanaweza kubadilika
ndani ya sekunde moja tu.Jana
nilikuwa Rais,jeshi lote likiwa
chini yangu,nilikuwa na ulinzi
mkali na kauli yangu ilikuwa
ya mwisho lakini leo tazama
mahala nilipo.Niko
ugenini,sina kitu chochote
ninalishwa na kuvishwa,sina
msafara tena,sina timu ya
walinzi na zaidi ya yote sina
familia” akawaza na
kuinamisha kichwa chake kwa
mawazo
“Kila ninapoikumbuka
familia yangu ninapatwa na
uchungu mkubwa
mno.Naamini kabisa kwamba
ajali iliyowaua ni mpango wa
serikali ya Tanzania
inayoongozwa na Dr
Fabian.Anataka kulipiza kisasi
baada ya kugundua kwamba
nilishiriki katika kupanga
mauaji dhidi yake na Patrice
Eyenga.Hata mimi
kupinduliwa naamini ana
mkono wake kwani Spika wa
bunge asingeweza kuipata
rekodi ile ya Melanie.Lazima
aliipata kutoka Tanzania na
mtu ambaye naamini aliyempa
rekodi ile ni Rais Dr Fabian”
akavuta pumzi ndefu alihisi
kizungu zungu akajilaza
kitandani
“Yote haya
ameyasababisha James
Kasai.Yeye ndiye aliyemleta
Melanie kwangu nikamtamani
na kujikuta nikikubali kufanya
kila alichotaka nikifanye.Yule
mwanamke nahisi alikuwa
shetani kwani sikujielewa
nilikuwa nakubali tu
kutekeleza kila
alichonielekeza.Ni aibu kwa
Rais kama mimi kuanguka
penzini na binti mwenye umri
sawa na mwanangu.Ni aibu
kubwa hii” akawaza na
kuinuka
“Natamani hata nijipige
vibao kwa ujinga
nilioufanya.Kwa tamaa zangu
nimekosa kila kitu.Nimemkosa
Melanie,nimeikosa familia
yangu na hata urais wangu
nimeupoteza.Hivi sasa
ninaishi kama mkimbizi”
akaendelea kuwaza huku
akibubujikwa na machozi
“Nilikuwa nikisikia tu
marais wakipinduliwa sikujua
kama huwa wanapata taabu za
namna hii.Mbaya zaidi
nilishiriki katika mpango wa
kumpindua Rais Patrice
Eyenga lakini mpango
haukufanikiwa na kibao
kimenigeukia mimi,jeshi
likanipindua.Nimejifunza
mengi kupitia haya
yaliyonikuta.Kuna muda
ninaichukia siasa natamani
ningebaki jeshini lakini tamaa
za madaraka zikanipeleka
kufanya mapinduzi
nikamuondoa Rais
madarakani na nilichokifanya
ndicho kimenitokea mimi”
akaendelea kuwaza Jenerali
Akiki
“Kuna sauti ninaisikia
ndani mwangu ikiniambia
niachane na siasa nianze
maisha mapya.Nina mali
nyingi nimezichuma ninaweza
kuishi maisha mazuri tu bila
matatizo lakini papo hapo
kuna sauti nyingine ninaisikia
inaniambia nisikubali lazima
nilipize kisasi kwa hawa watu
walionifanyia ubaya.Lakini
hata kama nikiamua kujipanga
kulipa kisasi ni kwa ajili ya
nani? Akajiuliza
“Ngoja niachane kwanza
na haya mawazo kwa sasa.Pale
akili yangu itakapokuwa
imetulia nitajua nini cha
kufanya lakini kwa sasa siwezi
kufanya maamuzi yenye kufaa”
akawaza na kujilaza kitandani
Saa mbili za usiku kwa saa
za Marekani watu sita
wakaingia ndani ya nyumba
alimokuamo Jenerali Akiki
aliyekuwa amejikunyata
sebuleni akitazama
runinga.Watu wale
hawakumsemesha kitu
wakafanya ukaguzi katika
nyumba nzima halafu akaingia
Mark Piller makamu wa rais
wa Marekani.Huyu ni mmoja
wa mwanasiasa kijana sana na
anayetajwa kuwa na ushawishi
mkubwa katika siasa za
Marekani.Jenerali Akiki
akasimama
“Mheshimiwa makamu wa
rais ! akasema Jenerali
Akiki.Hakutegemea kama
Mark Piller angekwenda
kumtembelea usiku ule.
“Jenerali Akiki” akasema
Mark wakasalimiana
“Karibu sana mheshimiwa
makamu wa Rais.Sikutegemea
kukuona hapa mida hii”
akasema Jenerali Akiki
“Nimekuja mida hii kwa
kuwa nisingeweza kuja
mchana kwanza kutokana na
kazi nyingi na pili ni kuhusu
uwepo wako hapa Marekani”
William akanyamaza kidogo
halafu akasema
“Naomba ufahamu
Jenerali Akiki kwamba uwepo
wako hapa Marekani
tumeufanya siri.Wanaofahamu
uko hapa ni watu wachache
sana.Sababu kubwa ya kufanya
jambo hili kuwa siri hatutaki
dunia ifahamu kuwa uko hapa
Marekani hivyo usishangae
kwa masharti ya kutowasiliana
na mtu yeyote.Kwa ujumla
naomba usihofu kitu hapa uko
salama kabisa,ulinzi ni mkali”
“Nashukuru sana
mheshimiwa makamu wa
Rais” akasema Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki pole sana
kwa yote yaliyokutokea na
kubwa zaidi tukio la kuipoteza
familia yako” akasema Mark
“Ahsante mheshimiwa
makamu wa Rais.Ninajaribu
kuifanya akili yangu ikubali
kwamba suala hili ni la
kawaida lakini inakuwa
ngumu.Kuondokewa na
familia nzima kwa wakati
mmoja si kitu rahisi hata
kidogo.Itanichukua muda
kulizoea jambo hili na kuliona
la kawaida”
“Pole sana Jenerali
Akiki.Maisha yetu ya kila siku
yamejawa na mitihani mingi
na huu uliokupata ni
mojawapo ya mtihani wa
maisha ambao inakubidi
uushinde.Kwa namna yoyote
ile Jenerali Akiki lazima
ushinde mtihani huu” akasema
Mark
“Ninajitahidi sana
mheshimiwa makamu wa rais
,ninajiahidi lakini ni
ngumu.Itanichukua muda
kulizoea jambo hili.Hata kama
ingekuwa ni wewe ungekuwa
katika hali yangu ungeona
ugumu wa haya
ninayoyaptia.Jana tu nilikuwa
Rais wa nchi nikitembea na
msafara mkubwa,nikitoa amri
na kuheshimiwa na kila mtu
lakini leo hi tazama mahala
nilipo.Hili pekee linatosha
kabisa kukupa ugonjwa wa
moyo lakini kama haitoshi
famili yangu pia
wameuawa.Haya ni mateso
yasiyovumilika hata kidogo
lakini nitajitahidi” akasema
Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki moja ya
kile kilichonileta hapa kwako
usiku huu ni kukuhakikishia
kwamba serikali ya Marekani
bado inasimama
nawe.Hatuitambui serikali ya
kijeshi na kesho Rais atatoa
tamko la kutoitambua serikali
hiyo.Marekani ni taifa kubwa
na tukitoa tamko mataifa
karibu yote makubwa
yataungana nasi kuupinga
utawala huo wa
kijeshi.Tutautaka utawala huo
wa kijeshi kurejesha madaraka
kwa serikali waliyoipindua
haraka sana ama sivyo
watakabiliana na vikwazo
vikubwa vya
kiuchumi.Tutazishawishi nchi
kubwa ambazo ni wanunuzi
wakubwa wa mafuta ya
Uganda wapunguze au kuacha
kabisa kununua mafuta ya
Uganda na kuufanya uchumi
wa nchi hiyo kuporomoka kwa
kasi.Tutaweka vikwazo vya kila
aina kushinikiza serikali hiyo
ya kijeshi kurejesha madaraka
kwa serikali
iliyopinduliwa.Naomba usife
moyo Jenerali Akiki sisi
tunakutambua wewe bado ni
Rais wa Uganda na
tutasimama nawe hadi
tuhakikishe unarejea
madarakani” akasema Mark
Piller
“Ahsante sana
mheshimiwa makamu wa
rais.Nimekosa neno la
kushukuru kwa maneno haya
mazito ambayo yamenifariji
sana”
“Usijali Jenerali
Akiki.Karibu sana Marekani
jisikie nyumbani”
“Mungu akubariki wewe
na serikali yako kwa msaada
huu mkubwa” akasema
Jenerali Akikiakiwa ameikunja
mikono yake kifuani
akishukuru
“Jenerali Paul Mukasa !
akasema Mark na kunyamaza
kidogo akamtazama Akiki
“Huyu alikuwa mkuu wa
majeshi.Lazima ni mtu
uliyemuamini sana.Imekuaje
akaamua kukugeuka?akauliza
Rais William.Jenerali Akiki
akavuta pumzi ndefu na
kusema
“Paul Mukasa alikuwa
mwanafunzi wangu
jeshini.Nilimpenda alikuwa
kijana mtiifu na
mkakamavu.Katika kila hatua
niliyokuwa ninapanda jeshini
sikumuacha nyuma niliendelea
kumpigania ili naye aweze
kupanda cheo.Nilipofanya
mapinduzi mtu pekee ambaye
niliamini angeweza kufaa
kuwa mkuu wa majeshi ni Paul
na bila kupoteza muda
nikamteua akawa mkuu wa
majeshi.Tumefanya kazi kwa
mashirikiano makubwa na
sikuwahi hata kuota kama siku
moja Paul angeweza kufanya
kitu kama hiki
alichokifanya.Nilistuka mno
nilipoambiwa kwamba Paul
amejitangaza ndiye Rais wa
Uganda baada ya mapinduzi”
akasema Jenerali Akiki na
kunyamaza akainamisha
kichwa
“Unadhani nini
kimesababisha akafanya hiki
alichokifanya?akauliza Mark
Piller
“Suala hili lazima lina
mkono kutoka nje ya
Uganda.Paul peke yake
asingeweza kufanya hiki
alichokifanya.Alikuwa mtiifu
mno kwangu”
“Unasema kuna mkono wa
mataifa ya nje?Ni taifa gani
unahisi limehusika katika
mpango huu wa
mapinduzi?akauliza Mark
Piller.Jenerali Akiki akafikiri
kidogo na kusema
“Tanzania”
“Tanzania?!
“Ndiyo” akajibu Jenerali
Akiki
“Tanzania na Uganda ni
nchi marafiki wakubwa.Iweje
Tanzania ishiriki katika
kuipindua serikali ya
Uganda?akauliza Rais William
na Jenerali Akiki akawa kimya
“Jenerali Akiki unadhani
kwa nini Tanzania ikashiriki
katika kuipindua serikali ya
Uganda? Kama unafahamu
chochote nieleze tafadhali”
akasema Mark Piller
“Nitakueleza ukweli Mark
Piller lakini naomba kile
nitakachokuambia kisivuke nje
ya kuta za nyumba hii”
“Niamini tafadhali”
akasema Mark Piller
“Kulikuwa na mpango wa
mapinduzi kuiondoa
madarakani serikali ya
jamhuri ya kidemokrasia ya
Congo na mimi nilishiriki
katika mpango huo”
“Mlitaka kuipindua
serikali ya jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo?Mark
Piller akauliza
“Ndiyo.Nilishiriki katika
mpango huo wa kumuondoa
madarakani Rais Patrice
Eyenga”
“Kwa nini mlitaka
kumuondoa madarakani Rais
Patrice Eyenga? Akauliza Mark
Piller
“Mheshimiwa makamu wa
Rais naamini unajua kwamba
vita iliyokuwa inaendelea
katika jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo ilikuwa
na manufaa makubwa kwa
nchi tajiri”
“Hilo nalifahamu.Nchi
nyingi tajiri zimefaidika sana
kwa vita iliyokuwa inaendelea
nchini Congo” akasema Mark
Piller
“Uganda pia ilifaidika
katika mapigano yale kwani
sisi tulikuwa tunamfadhili
James Kasai.Alipoingia
madarakani Rais Patrice
Eyenga alimaliza machafuko
yaliyodumu kwa miaka mingi
na kukata ile mirija yote
iliyokuwa inazifaidisha nchi
mbalimbali.Majenerali wa
jeshi la Congo
hawakufurahishwa na kile
alichokifanya Patrice Eyenga
kwani walikuwa wakifadikika
kutokana na mapigano yale
hivyo waliandaa mpango wa
mapinduzi kumuondoa
madarakani Patrice
Eyenga.Hilo lilikuwa kundi la
kwanza lakini kulikuwa na
kundi la pili ambalo liliandaa
mpango wa mapinduzi ambalo
ndilo nilishirikiana nalo”
akasema Jenerali Akiki na
kumueleza Mark Piller kila
kitu kuhusiana na mpango ule
wa Melanie Davis wa kuwaua
marais Patrice Eyenga na Dr
Fabian Kelelo.
“Hivyo ndivyo ilivyokuwa
mheshimiwa makamu wa
Rais” akasema Jenerali Akiki
“Nilisikia kuhusu mpango
ule wa kuwaua marais wa
Tanzania na Congo kwa bomu
la kujitoa mhanga lakini
sikujua kama wewe nawe
ulishiriki katika mpango
ule.Ahsante kwa kunieleza
ukweli” akasema Mark Piller
na ukimya ukapita.
“Jenerali Akiki sahau hayo
yote yaliyotokea na hapa
umekuja kuufungua ukurasa
mpya.Kabla sijakueleza
chochote nataka kukuhakisha
kwamba mimi binafsi niko
tayari kukusaidia lakini nataka
kujua tutaanzia wapi
kukusaidia.Nataka kusikia
mipango yako.Je unataka
kurudi tena Uganda? Bado
unataka kukalia kiti cha Urais?
Nieleze mipango yako
tafadhali” akasema Mark Piller
“Mheshimiwa makamu wa
Rais kwa kweli mpaka sasa
sifahamu nini hasa
ninakihitaji.Akili yangu naona
kama imefika mwisho wa
kufikiri” akasema Jenerali
Akiki
“Akiki wewe ni
mwanajeshi usiruhusu akili
yako ikashindwa kujua hatima
yako.Katika maisha kuna
kuanguka lakini ukianguka
simama haraka endelea
mbele.Nawe pia umeanguka
hivyo unapaswa kusimama na
kusonga mbele.Hukufika hapa
ulipofika kwa bahati
mbaya.Ulipambana ukafika
hapa ulipofika hivyo usikubali
kirahisi watu hawa wakaharibu
kila kitu ulichokipigania kwa
muda mrefu.Umeijenga
Uganda usiwape nafasi watu
hawa ya kuiharibu Uganda na
kuvuruga yale yote
uliyoyajenga.Unapaswa
kupambana”
“Mheshimiwa makamu wa
Rais sitaki tena
kupambana.Nataka nibadili
maisha yangu”
“Maisha ya namna gani
unataka kuishi Jenerali Akiki?
“Sitaki tena kurejea
Uganda.Nataka nipate sehemu
niishi maisha yaliyotulia yenye
amani.Ninafahamu mnao
uwezo wa kunirejesha
madarakani lakini sitaki tena
urais.Nimeponea tundu la
sindano sitaki tena kurejea
Uganda.”
“Nimekuelewa jenerali
Akiki na mimi nakuahidi
kukusaidia kwa hilo lakini
naomba ufahamu kwamba
hautakuwa na maisha yenye
furaha na amani unayoyataka
kama wale watu ambao
wamekuondoa madarakani
wataendelea kusalia
madarakani.Kokote
yanakofanyika mapinduzi
kuna mambo mawili tu
ambayo humtokea Rais
anayepinduliwa.Kuuawa au
kufungwa gerezani na mali
zake zote hutaifishwa awe
amezipata kihalali au
kifisadi.Akibahatika kukimbia
Rais huyu hugeuka mkimbizi
na wakati mwingine anaweza
akaishi ugenini kwa maisha
yake yote yaliyobaki.Paul
Mukasa na wenzake
wataendelea kukusaka kujua
mahala ulipo.Hii inakufanya
uwe katika hatari kubwa lakini
nakutoa hofu kwamba hapa
Marekani utakuwa
salama.Utapewa uraia wa
Marekani na utaishi maisha
mazuri yenye hadhi yako”
“Nashukuru sana makamu
wa Rais”
“Jenerali Akiki kama
umechagua kutorejea tena
Uganda hayo ni maamuzi yako
na tunayaheshimu,hata hivyo
kuna jambo ambalo lazima
tulifanye.Wasaliti wale
waliokupindua hatuwezi
kuwaacha hivi hivi lazima
tuwafunze adabu” akasema
Mark
“Nini unakitaka
mheshimiwa makamu wa
Rais?akauliza Jenerali Akiki
“Nataka Uganda
isitawalike.Nataka wananchi
wa Uganda wauchukie utawala
wa kijeshi na wapaaze sauti
kuukataa utawala huo na
kutaka kurejeshwa kwa serikali
ya kiraia.Mambo
yatakapokuwa magumu
wanajeshi watalazimika
kurejesha madaraka kwa
serikali ya kiraia.Unaonaje
wazo hilo? Akauliza Mark
Piller
“Ni mpango mzuri sioni
tatizo lake” akasema Jenerali
Akiki
“Ahsante kwa
kukubali.Kinachotakiwa ni
kuzusha vurugu kubwa nchini
Uganda zitakazolilazimisha
jeshi kutumia nguvu na
kupelekea umwagikaji
mkubwa wa damu na hii
itajenga chuki kubwa kati ya
utawala wa kijeshi na
wananchi.Jumuiya ya
kimataifa haitakaa kimya
itapaaza sauti kuutaka utawala
wa kijeshi kuondoka na
kuachia madaraka kwa serikali
ya kiraia.Jenerali Akiki nataka
unisaidie mawazo ni namna
gani tunaweza kuchafua hali ya
amani nchini Uganda ili
tuweze kuidhoofisha serikali
ya kijeshi iliyokuondoa
madarakani?akauliza Mark
Piller.Jenerali Akiki alichukua
muda kidogo akatafakari na
kusema
“Kikubwa inachotegemea
serikali kwa sasa ni mafuta
ambayo yanaipatia Uganda
fedha nyingi sana.Tunaweza
kuwadhoofisha kwa kuondoa
chanzo hiki kikubwa cha
mapato.Kuna bomba la mafuta
ambalo linatoka Uganda
kwenda Tanga
Tanzania.Bomba hili
likilipuliwa nchi itakosa
mapato na watashindwa
kuendesha serikali.Nashauri
tuwadhibiti katika mafuta
mheshimiwa makamu wa rais”
akasema Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki tukilipua
bomba la mafuta linalokwenda
Tanzania bado hatutakuwa
tumefanya kitu.Ninachotaka
mimi ni kuleta machafuko
nchini Uganda ambayo
yatapelekea vurugu kati ya
jeshi na wananchi.Nataka
damu imwagike” akasema
Mark Piller.Jenerali Akiki
akamtazama Mark kwa muda
halafu akasema
“Mark Piller nimekueleza
ukweli wangu wote kwa nini
nimepinduliwa.Nataka nawe
unieleze ukweli.Kwa nini
unataka itokee vurugu
Uganda? Ni kweli vurugu hizo
unazozizungumzia ni kwa ajili
ya kuidhoofisha serikali ya
kijeshi au ni kwa maslahi
yenu? Akauliza Jenerali Akiki
“Jenerali Akiki
usizungumze kuhusu ninyi bali
sema ni kwa maslahi
yetu.Wewe tayari ni mmoja
wetu na kwa kuwa u mmoja
wetu nitakueleza ukweli” Mark
Piller akanyamaza kidogo
halafu akasema
“Nchi ya Uganda ina
mafuta mengi mno kuliko nchi
nyingine yoyote Afrika.Akiba
ya mafuta ya Uganda
iliyogunduliwa ni kubwa sana
kuzidi hata zile nchi
zinazofahamika kwa uzalishaji
mkubwa wa mafuta.Unaonaje
kama tukichukua kiasi kidogo
cha mafuta ya Uganda na
kuongeza katika akiba yetu ya
mafuta? Akauliza Mark
Piller.Jenerali Akiki akafikiri
kidogo kisha akasema
“Mheshimiwa makamu wa
Rais sasa nimepata picha
nzima kuhusiana na haya
mazungumzo yetu.Kila kitu
tulichokizungumza hapa
msingi wake ni mafuta ya
Uganda”
“Ndiyo Jenerali Akiki”
akajibu Mark Piller na ukimya
ukapita
“Usiogope Jenerali
Akiki,tayari wewe ni mwenzetu
na kiasi kidogo cha mafuta
tutakachokichukua na
kuongeza katika akiba yetu ni
kwa ajili ya ndugu zako
wamarekani.Ukiwa kama mtu
mwenye mchango mkubwa
katika jambo hili utanufaika
sana.Utaishi maisha ya
kifahari sana hapa Marekani
yenye hadhi yako.Umefanya
kazi kubwa sana katika nchi
yako,umeiweka Uganda
ikaonekana katika ramani ya
dunia lakini hakuna thamani
yoyote unayopewa,hata mali
zako zimechukuliwa na lengo
lao ni ili uishi maisha magumu
ya taabu.Hustahili kutendewa
hivyo.Hapa Marekani
tunakuthamini na utaishi
mazuri yaliyojaa amani na
furaha.Hutatamani tena
kurejea Afrika” akasema Mark
“Mheshimiwa makamu wa
Rais hilo unalotaka nilifanye ni
usaliti mkubwa kwa nchi
yangu na bara la afrika.Huo ni
unyonyaji mkubwa” akasema
Jenerali Akiki na maneno yale
Mark Piller hakuonekana
kuyapenda
“Jenerali Akiki,kauli kama
hizo zilizungumzwa miaka
mingi na viongozi wazalendo
kwa bara la Afrika mfano Rais
wa kwanza wa Tanzania Julius
Nyerere na wengineo ambao
walikuwa na uchungu wa kweli
na bara la Afrika lakini kwa
wewe hupaswi kutamka
maneno kama hayo.Hauna sifa
hiyo ya uzalendo kwa nchi au
bara lako.Umemfadhili James
Kasai kiongozi wa waasi
ambaye aliua watu
wengi.Kiongozi mwenye
uzalendo kwa bara lake hawezi
akafanya kitu kama
hicho.Ulishiriki katika mpango
wa mauaji ya maraisi
wenzako,kiongozi mzalendo
huwezi ukafanya jambo kama
hilo.Jenerali Akiki hivi sasa
hauna kitu chochote,hauna
mahala pa kwenda na hakuna
nchi wanayoweza
kukupokea.Serikali ya
marekani imekupokea kwa
mikono miwili na kukupa
makazi ya kama haitoshi
utapata mara mbili ya kile
ulichokipoteza baada ya
mapinduzi.Ni juu yako ukubali
au ukatae.Ukikubali utakuwa
raia wa Marekani na kufaidika
lakini endapo utakataa basi
hatutakuwa na namna
nyingine zaidi ya kukuruhusu
ukatafute hifadhi nchi
nyingine au tutakurejesha
Uganda.Chaguo ni lako
jenerali Akiki.Labda nikuweke
wazi kwamba Marekani
inapokea watu wale ambao
watakuwa na manufaa kwa
nchi.Kama nawe unataka kuwa
raia wa Marekani lazima uwe
na faida kwa nchi hii” akasema
Mark Piller na kumtazama
Jenerali Akiki
“Nini unakitaka Jenerali
Akiki? Unataka kuwa raia wa
Marekani au unataka kurejea
Afrika?akauliza Mark Piller
“Sitaki kurejea
Afrika.Nitaishi hapa
Marekani”
“Kama unakubali kuishi
hapa Marekani huna budi
kukubaliana na haya
niliyokueleza” akasema Mark
Piller
“Kama mpango ni
kuchukua mafuta basi vurugu
ndani ya Uganda pekee
hazitasaida kufanikisha
mpango huo.Bomba la mafuta
linaanzia Uganda na kwenda
katika bandari ya Tanga nchini
Tanzania.Ili mpango huo
ufanikiwe lazima eneo lote la
Afrika Mashariki liingie katika
machafuko ndipo itawezekana
kuchukua mafuta hayo katika
bandari ya Tanga” akasema
Jenerali Akiki
“Hapo sasa
tunazungumza.Ni vipi basi
tunaweza kuliweka eneo la
Afrika Mashariki katika
machafuko ili tuweze
kufanikiwa kudhibiti mafuta?
Akauliza Mark Piller
“Kuna njia moja tu
ambayo inaweza ikatumika
kuleta machafuko makubwa
katika eneo zima la Afrika
Mashariki” akasema Jenerali
Akiki
“Nakusikiliza Jenerali
Akiki.Ni jambo gani hilo?
Akauliza Mark Piller
“Ni kwa kutumia dini”
“Dini?
“Ndiyo.Tukitumia dini
inaweza ikaleta machafuko
makubwa si Uganda peke yake
bali eneo lote la afrika
Mashariki”
“Hebu nifafanulie namna
dini inavyoweza ikaleta
machafuko Uganda na Afrika
mashariki” akasema Mark
Piller
“Kiongozi mkuu wa
waislamu nchini Uganda
atauawa na watu
wasiojulikana.Baada ya mauaji
hayo,tutazungumza na kikundi
cha kigaidi cha IS ambao
watafanya mashambulio ya
mabomu katika makanisa na
mashule yanayomilikiwa na
dini ya kikristu.IS wataeleza
kwamba mashambulio hayo ni
ya kulipiza kisasi kwa mauaji
ya kiongozi mkuu wa waislamu
nchini Uganda” akasema
Jenerali Akiki
“Subiri kidogo Jenerali
umesema kuhusu kushirikiana
na kikundi cha kigaidi cha IS?
Akauliza Mark Piller
“Ndiyo mheshimiwa
makamu wa Rais !
“Hilo
haliwezekani.Marekani katu
haiwezi kushirikiana na
magaidi kwa namna yoyote
ile.Magaidi ni maadui zetu na
tunawasaka kwa udi na
uvumba kila mahala walipo na
kamwe,narudia tena kamwe
hatuwezi kushirikiana nao
katika jambo lolote”
“Kama mnahitaji mafuta
ya Uganda basi mashirikiano
na IS ni kitu cha lazima.Si IS
pekee bali kikundi chochote
cha kigaidi iwe Alshabaab au
Boko Haram” akasema
Jenerali Akiki
“Hebu nieleze namna
unavyotaka kuwatumia IS
katika suala hili”
“Kama nilivyo tangulia
kusema kwamba kikundi ha IS
kitashambulia makanisa na
shule za taasisi za kidini na
kusababisha vifo
vingi.Tutamtafuta mtu ambaye
atatumika kuchochea na
kuwapandisha hasira wakristu
ili wakalipize kisasi kwa
waislamu na hapo tutakuwa
tumepanda mbegu ya chuki
kwa waumini wa dini hizi
mbili.Machafuko ya kidini
yakianza ni kama moto wa
petroli,jeshi halitaweza
kuyazuia.Yatasambaa nchi zote
za Afrika mashariki”akasema
Jenerali Akiki
“Lakini uislamu
haukubaliani na matendo ya
kigaidi.Watakanusha kwamba
waliofanya mashambulio hayo
katika makanisa na misikiti
hawauwakilishi uislamu”
akasema Mark Piller
“Ni kweli. Lakini maelezo
watakayoyatoa baada ya
mashambulio hayo
hawatajitaja kuwa ni kundila
IS bali watasema ni kikundi
cha waislamu”
“Hilo ni wazo zuri pia.Ni
vipi kama akristu
hawatachukuah atua zozote
baada ya mashambulio hayo
kutokea katika nyumba zao za
ibada?akauliza Mark
“Hapa kuna watu ambao
lazima tuwatumie ili kuamsha
hasira kwa waumini wa dini ya
kikristu na kuchochea
machafuko.Kuna mwanasiasa
mmoja anaongoza chama cha
upinzani ambaye
tutazungumza naye na yeye
ndiye atakayewapanga
viongozi wa dini
watakaowachochea waumini
wao kuanzisha mashambulizi
dhidi ya watu wa dini
nyingine.Hawa nao lazima
muwape hifadhi hapa
Marekani.Baada ya machafuko
wataondoka Uganda na kuja
huku kimya kimya huku
wakiacha moto ukiendelea
kuwaka Uganda”
“Hilo halina tatizo.Lazima
wataangaliwa kwa namna ya
kipekee kabisa” akasema Mark
Piller
“Machafuko haya
yatakuwa makubwa
yatasambaa katika miji
mingine ya Uganda na
hatimaye nchi nzima.Uganda
ikiingia katika
machafuko,tutahamia Tanga
Tanzania.Ili kuweza kuchukua
mafuta lazima jiji la Tanga
liingie katika machafuko
pia.Nina uhakika mkubwa
sana kama tukitumia dini
kuwagombanisha wakristu na
waislamu basi machafuko
yatakuwa makubwa na damu
itamwagika.Machafuko
yatakapokuwa makubwa
mtakuwa mmepata kigezo cha
kupeleka majeshi yenu Afrika
Mashariki kwa lengo la
kulinda amani na mtafanikiwa
kuchukua kila mkitakacho
lakini ili mpate sababu ya
kutosha ya kupeleka wanajeshi
Afrika Mashariki kuna jambo
lazima lifanyike ambalo sina
hakika kama mtakubaliana
nalo”
“Jambo gani Jenerali
Akiki? Akauliza Mark Piller
“Ubalozi wa Marekani
ulioko Kampala inabidi
ulipuliwe”
“Kulipua ubalozi wa
Marekani?! Mark Piller
akashagaa
“Ndiyo Mark.Lazima
iwepo sababu ya kupeleka
wanajeshi Uganda na Afrika
mashariki hivyo ili kuongeza
uzito lazima ubalozi wa
Marekani Kampala ulipuliwe
na raia wa Marekani kuuawa”
akasema Jenerali Akiki.Mark
Piller akafikiri kidogo halafu
akasema
“Sawa nitaunda timu
maalum ya kulishughulikia
suala hilo”
“Mtu ambaye
atahamasisha machafuko
kutokea anaitwa Joshua
Lulangwa.Huyu ni
mwanasiasa anayeongoza
chama cha upinzani
kijulikanacho kama chama cha
ukombozi wa Uganda.Huyu
ndiye atakayewaandaa
viongozi wa dini ambao
watahamasisha wafuasi wao
kushambuliana.Ataandaa
kiongozi mmoja mwenye
ushawishi upande wa wakristu
na mwingine upande wa
waislamu.Narudia tena hawa
watakaochochoa machafuko
mnatakiwa muwape hifadhi
Marekani.” akasema Jenerali
Akiki
“Hilo halina tatizo Jenerali
Akiki tutalitekeleza” akasema
Mark Piller.
KISIWA CHA
VITI LEVU – FIJI
Baada ya matembezi
marefu katika msitu mnene
Mathew Mulumbi na Najma
walirejea kupumzika katika
hoteli walikofikia.Mara tu
walipofika mapokezi Mathew
akajulishwa na muhudumu wa
mapokezi kwamba wakati
wamekwenda kutembea
msituni kuna mtu alifika
kumtafuta.Mathew alistushwa
kidogo na taarifa ile hakujua
nani aliyekuwa
anamtafuta.Hakufahamiana
na mtu yeyote katika kile
kisiwa kwani walikuwa na siku
tatu tu toka wamefika katika
kisiwa kile kwa mapumziko.
“Hakutaja jina lake huyo
mtu aliyekuja kunitafuta?
akauliza Mathew
“Hapana hakutaja jina lake
ila alisema atarejea tena
baadae” akasema Yule
muhudumu kisha Mathew
akaelekea chumbani kwake
“Abu kuna nini alikuwa
anakwambia Yule mwanadada
wa mapokezi?akauliza Najma
ambaye alimuacha Mathew
akizungumza na muhudumu
wa mapokezi akaelekea
chumbani.
“Alikuwa ananipa taarifa
kwamba kuna mtu alikuja
kunitafuta” akasema Mathew
“Nani huyo aliyekuja
kukutafuta? Hakutaja jina
lake? Kuna mtu unafahamiana
naye hapa?
“Hakutaja jina
lake.Nashangaa kwa kuwa
hakuna mtu anayetufahamu
huku ugenini.Tutamfahamu
mtu huyo kwani aliahidi
kurudi tena baadae” akasema
Mathew kisha wakaoga na
kwenda kupata chakula cha
mchana.
Kwa muda wa miezi
mitatu Mathew na mpenzi
wake Najma wamekuwa katika
mapumziko wakizunguka
sehemu mbali mbali duniani
kutalii.Baada ya kurejea
kutoka Dar es salaam ambako
alifanikiwa kumuua james
Kasai na Khalid Sultan
Khalid,Habiba Jawad kwa
kufurahishwa na kazi
aliyoifanya Mathew alimtaka
yeye na Najma wakazunguke
sehemu mbali mbali duniani
kwa muda wa miezi minne ili
kuweka akili sawa kabla ya
kuingia katika misheni
nyingine.Kwa kipindi cha
miezi mitatu Mathew na
Najma wamekuwa
wakizunguka sehemu mbali
mbali duniani wakifanya
utalii.Walifika sehemu nyingi
maarufu kwa utalii duniani na
siku tatu zilizopita walifika
katika kisiwa cha Fiji
wakiendelea na mapumziko
yao.Kwa muda huo wa miezi
mitatu Mathew Mulumbi
alijitahidi kujiweka mbali na
runinga au simu.Hakutaka
kutazama au kusikia kitu
ambacho kingeweza kuharibu
mapumziko yao.
Baada ya kupata chakula
walirejea chumbani kwao
kupumzika kabla ya jioni ya
siku ile kwenda katika
matembezi ya miguu
ufukweni.
Saa moja za jioni walirejea
hotelini ndipo walipokutana
na Yule mtu aliyekuwa
akiwatafuta.Ni mmoja kati ya
walinzi wa Habiba Jawad
wakamkaribisha katika
chumba chao kikubwa
“Tulijiuliza sana
tulipoambiwa kuna mtu
amekuja kutuulizia kwani
hatuna mtu tunayefahamiana
naye hapa Fiji” akasema
Mathew
“Hata mimi nilijua
mtastuka na sikutaka kutaja
jina langu makusudi ili
kuwastua” akasema Malik na
wote wakaangua
kicheko.Chakula kikaletwa
wakala na maongezi rasmi
yakaanza
“Abu Zalawi nimetumwa
na mama Habiba anawahitaji
mrejee nyumbani.Amenituma
niwaombe samahani kwa
kukatisha mapumziko yenu”
akasema Malik
“Kuna tatizo
ganinyumbani?akauliza Najma
“Hakuna tatizo lolote
lakini amenituma hivyo”
akasema Malik
“Kama hakuna tatizo kwa
nini mama anatusumbua
katika mapumziko
yetu?akauliza Najma
“Hajatusumbua kwani
tumekuwa na mapumziko
marefu sana.Kwa miezi mitatu
tumekuwa angani na majini
tukistarehe.Ni wakati wa
kurejea nyumbani” akasema
Mathew
“Tunaondoka usiku
huu.Ndege iko tayari uwanja
wa ndege wa Nadi kwa ajili ya
kuelekea Saudi
Arabia”akasema
Malik.Hakukuwa na muda wa
kupoteza Mathew na Najma
wakaanza kujiandaa kwa ajili
ya kurejea Saudi Arabia japo
Najma hakuonekana kufurahia
kuondoka mapema kisiwani
Fiji.
 
SIRI PART3: MTUNZI PATRICK CK
JASUSI/GAIDI
SEASON 1 : EPISODE 9
Saa saba za mchana siku
iliyofuata ndege ya akina
Mathew iliwasili Riyadh Saudi
Arabia.Ilikuwa ni furaha kwa
kila mmoja wao kuwaona tena
Mathew na Najma.Baada ya
kuoga walikwenda kujumuika
katika chakula cha mchana
pamoja na Habiba Jawad kisha
wakaenda kupumzika
kutokana na uchovu wa safari
kwani walitembea angani kwa
takribani saa kumi na sita
kutoka kisiwa cha Fiji hadi
Riyadh
Saa moja za jioni
walikutana nyumbani kwa
Habiba kwa chakula cha jioni
alichokiandaa kwa ajili
yao.Walizungumza mengi
kuhusiana na miezi mitatu ya
kuzunguka sehemu mbali
mbali duniani.Baada ya
kumaliza kula chakula Habiba
akamuomba Najma
akapumzike na amuache
Mathew alikuwa na
mazungumzo naye.Habiba
akamchukua Mathew
wakaelekea katika chumba
chake maalum kwa
mazungumzo
“Mathew mtanisamehe
sana kwa kukatisha
mapumziko yenu” akaanzisha
maongezi Habiba
“Usijali mama
tumepumzika vya kutosha
sana.Vipi maendeleo yako?
Akauliza Mathew
“Hilo ni mojawapo ya
mambo yaliyopelekea
nikawarudisha nyumbani”
akasema Habiba na
kunyamaza kidogo
“Mathew kama
nilivyokueleza wakati ule
nilipokutuma Dar es salaam
kwamba sina muda mrefu sana
wa kuishi na sasa ninazidi
kuelekea ukingoni” akasema
Habiba
“Mama unaniogopesha
ukisema hivyo.Unaonekana
una afya njema
kabisa.Huonekani kama ni
mtu ambaye unahesabu siku”
akasema Mathew na Habiba
akacheka kidogo
“Sitaki kukuogopesha
Mathew Mulumbi lakini
ninaelekea ukingoni.Sina
muda mwingi sana kutoka
sasa”
“Nini kinakusumbua
mama?
“Tuyaweke hayo pembeni
kwa muda lakini narudia tena
kukusisitiza kwamba hii ni siri
kubwa na nimechagua wewe
uifahamu kwa kuwa
ninakuamini” akasema Habiba
“Ahsante sana mama kwa
kuniamini na kunishirikisha
katika jambo hili
kubwa.Ninakuahidi kwamba
sintamweleza mtu mwingine
yeyote” akasema Mathew
“Nafurahi kusikia hivyo”
akasema Habiba na
kunyamaza kwa sekunde
chache halafu akasema
“Mkiwa mapumzikoni
kuna mambo yametokea
ambayo naamini hujayasikia
bado” akasema Habiba
“Ni kweli mama nikiwa
mapumzikoni sikutaka
kutazama runinga au
kuwasiliana kwa
simu.Sikutaka kuvuruga
mapumziko yetu” akasema
Mathew
“Kuna mambo yametokea
Afrika mashariki.Rais wa
Uganda Jenerali Akiki
Rwamirama alipinduliwa na
jeshi”
“Jenerali Akiki
amepinduliwa?! Mathew
akashangaa
“Ndiyo amepinduliwa na
jeshi”
“Anastahili
kupinduliwa.Hafai kuongoza
nchi”akasema Mathew
“Inakaribia miezi mitatu
toka jeshi la Uganda
lilipofanya mapinduzi hayo na
hali ilikuwa shwari kabisa
lakini siku chache zilizopita
yameibuka machafuko
makubwa sana yaliyoanzia
Uganda na kusambaa katika
nchi nyingine za Tanzania na
Kenya.Kumekuwa na
umwagaji mkubwa wa damu
na inahofiwa yanaweza tena
kutokea mauaji mengine kama
yale yaliyotokea Rwanda
mwaka 1994” akasema Habiba.
“Nini kimesababisha
machafuko hayo? Yameibuka
makundi ya waasi? Mathew
akauliza
“Haya ni machafuko ya
kidini.Waumini wa dini za
kikristu na kiislamu
wanashambuliana na kuuana”
akasema Habiba
“Machafuko ya dini
yamefika hadi Tanzania?
Akauliza Mathew
“Ndiyo.Machafuko hayo
yamefika hadi Tanzania”
“Hilo haliwezekani kwa
Tanzania.Kwa miaka mingi
waumini wa dini tofauti
tumeishi kama ndugu.Ukifika
Tanzania hutajua dini ya mtu
kwani wote tu ndugu
moja.Nini kimetokea leo hadi
ndugu wafarakane na kuanza
kuuana? Akauliza Mathew
“Jambo hili lilianza kama
mzaha.Aliuawa kiongozi
mmoja wa dini na upande
ambao kiongozi wao aliuawa
walianza kulipiza kisasi kwa
wenzao na hadi sasa
machafuko hayo yamekuwa
makubwa na vyombo vya
usalama vimeshindwa
kuyadhibiti.Kuna kila dalili
kwamba machafuko haya ya
kidini yanaweza kuenea katika
sehemu nyingine za bara la
Afrika na kama
yasipodhibitiwa mapema
yanaweza yakasambaa dunia
nzima.Tayari Marekani
imekwisha peleka vikosi vya
jeshi Afrika Mashariki katika
jitihada za kujaribu kuzuia
machafuko hayo yasiendelee
kusambaa” akasema Habiba
“Mama Habiba bado
sijapata picha nini sababu ya
machafuko hayo? Kwa
ninavyowafahamu watanzania
ni vigumu mno kuingia katika
vita ya kidini.Tumeishi kwa
miaka mingi kama ndugu moja
na kila pale kunapotokea
mivutano ya kidini humalizwa
kwa mazungumzo kati ya
viongozi wa dini.Nini
kimetokea leo wakaacha
utamaduni ule wa kukaa meza
moja wakazungumza na
kuanza kushambuliana?
Akajiuliza Mathew
“Mathew kinachoendelea
Afrika mashariki ni zaidi ya
mapigano ya kidini.Yalianza
mapigano ya makundi ya
waumini wa dini na sasa
yameibuka tena makundi
mengine ya makabila,makundi
ya kisiasa n.k.Suala hili
limezidi kuwa pana zaidi kila
uchao”
“Serikali za Afrika
Mashariki zimefanya juhudi
gani katika kumaliza vurugu
hizo?akauliza Mathew
“Mathew machafuko ya
kidini ni mabaya sana na kila
siku yanaongezeka ukubwa na
nguvu yake kama
kimbunga.Majeshi
yamelazimika kutumia nguvu
kubwa na kilichotokea ni watu
wengi kuuawa.Kwa ujumla hali
ni mbaya sana Afrika
Mashariki” akasema Habiba
“Ruby,Gosu
Gosu,Austin.Wako salama
kweli?akajiuliza Mathew
“Tuliweke na hilo pembeni
nilitaka tu ufahamu
kinachoendelea
nyumbani.Kubwa zaidi
nililokuitia hapa ni kwamba
kesho alfajiri tunasafiri mimi
na wewe tunakwenda
Marekani”
“Marekani?! Mathew
akashangaa
“Ndiyo.Mbona
umeshangaa?
“Nini tunakwenda kufanya
huko? Akauliza Mathew
“Tunakwenda kuonana na
wakuu wa IS”
“Wakuu wa IS wako
Marekani? Akauliza Mathew
na Habiba akatabasamu
“Mathew niliwahi
kukwambia kwamba kuna
mengi bado huyafahamu
unatakiwa
ujifunze.Nitakueleza kidogo.”
Akasema Habiba na
kunyamaza kidogo halafu
akasema
“Kundi la IS lilianzishwa
na Marekani kama chombo
cha kuwasaidia kuvamia nchi
za kiarabu zenye utajiri wa
mafuta na vile vile kuidhibiti
nchi ya Iran isiweze kuwa taifa
lenye nguvu zaidi katika eneo
la Mashariki ya
kati.Usishangae kusikia
kwamba kundi la IS
limeanzishwa na
Marekani.Yawezekana
hufahamu lakini Mwaka 197o
shirika la ujasusi la marekani
CIA lilikitumia kikundi cha
Muslim Brotherhood cha Misri
katika kuzuia Urusi isieneze
sera zake katika nchi za
kiarabu.Marekani pia waliunga
mkono kundi la Sarekat dhidi
ya Surkano nchini
Indonesia,vile vile waliunga
mkono kikundi cha Jamaat e
Islami dhidi ya Zulfiqar Ali
Bhutto nchini Pakistan.Hii ni
historia fupi nimekupa
utambue kwamba Marekani
wamekuwa wakivisaidia
vikundi vinavyojihusiana na
ugaidi pale inapolazimika kwa
ajili ya maslahi yao.Tukiweka
pembeni makundi hayo
niliyokutajia tuje katika kundi
la IS.Hili kundi ni zao la
Marekani kama nilivyokueleza
ambao wanatumia kundi hili
kuvamia nchi maadui wa
Marekani katika eneo la
Mashariki ya kati,kulitumia
kama kigezo cha kuvamia
kijeshi nchi hasa zile zenye
utajiri mkubwa wa mafuta na
ndani ya Marekani wanatumia
kundi hili kama tishio kwa
usalama wa nchi hivyo
kuhalalisha udukuajiwa taarifa
za wananchi kwa kigezo cha
usalama.
Kwa muda mrefu sasa
nimekuwa nikifahamika kama
mfadhili mkuu wa kundi la IS
na makundi mengine ya
kigaidi lakini ukweli ni
kwamba mimi ni chombo tu
kinachotumika katika ufadhili
huo bali wafadhili wakuu ni
Marekani.Umewahi kujiuliza
kwa nini sikamatwi japo
ninafadhili ugaidi? Ni kwa
sababu mimi ninatumika tu
kama chombo.Mume wangu
alikuwa anafanya hivyo na
alipofariki nilibeba mimi
jukumu hilo.Wanaofahamu
suala hili hata ndani ya
Marekani ni watu wachache
sana.Ninakwenda nawe kesho
Marekani nataka ukajifunze
kwani wewe ndiye
utakayechukua mikoba baada
yangu.Tutakaporejea safari
hiyo nitakupa maelekezo nini
kinafuata.Nadhani
umenielewa Mathew.Ninakupa
maelezo mafupi mafupi
kukupa nafasi ya
kujifunza.Jiandae kwa mambo
makubwa yanayokuja huko
mbeleni” akasema Habiba
Jawad.
Habiba alihitaji
kupumzika hivyo hakutaka
maongezi zaidi akamtaka
Mathew naye akapumzike na
kujiandaa kwa safari yao ya
alfajiri.
Mathew alirejea chumbani
kwake lakini kichwa chake
kilikuwa kimevurugika kabisa
“Nina wasi wasi mkubwa
na usalama wa Ruby kufuatia
machafuko hayo makubwa
yanayoendelea Afrika
Mashariki.Ninatamani
kumpigia simu lakini sitaki
ajue mahala nilipo” akawaza
Mathew
“Abu kuna nini?Mbona
sura yako imerudi tofauti na
ulivyoondoka?Mama
amekwambia nini?akauliza
Najma
“Kesho tuna
safari.Ninasikitika kukuacha
peke yako” Mathew
akadanganya
“Ouh mpenzi wangu
kumbe ni hilo tu.Usipate taabu
kwani mtarejea na utanikuta
hapa ninakusubiri.Mama
kakwambia mnakwenda wapi?
“Tunakwenda
Marekani.Safari ya kibiashara”
“Mama anakuamini sana
Abu Zalawi” akasema Najma
na Mathew akachukua kitabu
katika kabati lake akaitafuta
namba ya simu ya Ruby
akapiga lakini simu
haikupatikana
“Hii inazidi kunipa wasi
wasi kama Ruby ni
mzima.Natamani niondoke
hata sasa hivi niende Tanzania
kujua kama yuko salama.Ruby
ninampenda kwa moyo wangu
wote na nilimuahidi kurudi
nyumbani kwa ajili yak…..”
“Abu,huyu Ruby ni nani?
Akauliza Najma.Mathew
aliyekuwa ameelekeza macho
ukutani akageuka na kustuka
baada ya kumkuta Najma
akiwa na kile kitabu chake
ambacho ameandika
mawasiliano ya watu mbali
mbali
“Ruby ni Rafiki yangu”
akasema Mathew na kuchukua
kile kitabu akakifungia
kabatini.
MPENZI MSOMAJI MAMBO
YAMEANZA..USIACHE
KUENDELEA NA SIMULIZI
HII KATIKA SEHEMU YA
PILI
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom