Riwaya: Siri

SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 23
Helkopta mbili zikitokea
katika operesheni ya
kuwakomboa Coletha na
Olivia zilitua katika kambi
ya kijeshi ya kikosi cha
operesheni maalum.Austin
alikuwa wa kwanza kushuka
ndani ya helkopta kisha
majeruhi wakashushwa na
kusaidiwa na mwisho
ikashushwa miili ya
waliouawa
“Mheshimiwa Rais”
akasema Austin
“Poleni sana Austin.”
Akasema Dr Evans na mara
akasikia sauti ikimuita
“Dady ! alikuwa ni
Coletha akiwa amevalishwa
blanketi kumkinga
baridi.Nyuma yake
alikuwepo Olivia Themba.
“Coletha my princess”
akasema Dr Evans na
kukumbatiana na mwanae
“Ahsante sana baba kwa
kufanya juhudi za
kutukomboa”
“Anything for you my
daughter.Sijui nimshukuruje
Mungu kwa kuonana nawe
tena” akasema Dr Evans na
kumkumbatia tena mwanae
“Vipi hali yako?
Hawajakuumuza wale
mashetani?
“Kwa sasa ninajisikia
vyema.Olivia alinitibu na
hali yangu kwa sasa ni nzuri
kabisa” akasema Coletha na
Dr Evans akamtazama
Olivia aliyekuwa amesimama
pembeni yao
“Olivia.Come here my
daughter” akasema Dr Evans
na kukumbatiana na Olivia.
“Umeyaokoa maisha ya
mwanangu.Thank you”
akasema Dr Evans
“Ahsante nawe
mheshimiwa Rais kwa
kufanya kila juhudi kuja
kutuokoa.Mheshimiwa Rais
ninahitaji kuzungumza
nawe”
“Not now Olivia”
“Mheshimiwa Rais ni
muhimu sana.We have to
talk tonight” akasema Olivia
Dr Evans akawapa pole
makamanda wote
walioshiriki katika
operesheni ile kisha
akazungumza na Austin
halafu akaondoka kuelekea
ikulu akiwa garini na Olivia
na Coletha
Baada ya kufika ikulu Dr
Evans akawa na
mazungumzo ya faragha na
Olivia
“Olivia nimekwisha
kushukuru kwa kuokoa
maisha ya mwanangu pili
nakupa pole sana kwa yote
mliyoyapitia lakini kubwa
nataka kutumia nafasi hii
kuzungumza kuhusu wewe
na hatima yako.Umekuwa na
mashirikiano na magaidi
ambao wamemwaga damu
nyingi ya watanzania wasio
na hatia yoyote.Tumekwisha
wakamata watu kadhaa
wanaohusika katika
mtandao huu na wengine
wameuawa.Uchunguzi mkali
sana utaanza kuanzia kesho
kuwatafuta wale wote ambao
wanajihusisha na IS na
nimekula kiapo kwamba
hakuna hata mmoja ambaye
ana mahusiano na IS atabaki
salama.Lazima tuwatafute
kokote waliko hapa
nchini.Olivia wewe ni kama
mwanangu,mimi na baba
yako ni kama ndugu hivyo
nataka kukupa nafasi
nyingine sitaki upotee.Kabla
sijakueleza zaidi nataka
kusikia kutoka kwako kile
ambacho umesisitiza
kwamba unataka kuniambia”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa Rais na
mimi ninakushukuru tena
kwa kufanya juhudi za
kutukomboa lakini nimeumia
sana kumuacha Mathew
Mulumbi.Alipigwa risasi
wakati akituokoa mimi na
Coletha.Yawezekana
walimuua lakini
hatukupaswa kumuacha
nyuma.Imeniumiza
sana”akasema Olivia na
kufuta machozi
“Olivia mahala
mlipokuwa hapakuwa
sehemu salama hata
kidogo.Watu wale
waliowavamia wangeweza
kurejea tena na kuwamaliza
wote.Operesheni ile ilikuwa
ni kwa ajili ya kuwakomboa
wewe na Coletha na kwa
kuwa tayari mlikwisha
kombolewa hakukuwa tena
na sababu ya kuendelea
kuwaweka katika hatari
ndiyo maana nikaamuru
muondoke haraka
sana.Usihofu kuhusu
Mathew he’ll be
fine.Nitatuma timu ya
kwenda kumtafuta kama
alijeruhiwa au ameuawa
atapatikana” akasema Dr
Evans
“Sijapendezwa na hilo
lakini tuliweke pembeni
kwanza.Mheshimiwa Rais
nataka kufahamu hali ya
baba yangu ikoje?
“Anaendelea vyema”
“Mambo tayari
yamemalizika.Lini ataachiwa
huru?
“Olivia maswali kama
hayo si ya kunipotezea muda
wangu.Nina mambo mengi
ya kushughulikia
yanayohusu usalama wa nchi
na si kupoteza muda kujibu
maswali kama hayo.Kama
hauna kitu cha kunieleza
tuendelee kujadili suala lako
la kushirikiana na magaidi
wa IS” akasema Dr Evans
kwa sauti kali kidogo
“Mheshimiwa Rais
kwanza kabisa mimi si gaidi
naomba ulifahamu hilo”
“But you are working
with them so you are one of
them” akasema Dr Evans
“Hufahamu chochote
kuhusu mimi mheshimiwa
Rais na sikutaka kuweka
wazi kitu chochote nikisubiri
wakati kama huu.Leo
nitakueleza kila kitu”
“Nieleze nielewe kwa nini
unakana wewe si gaidi
wakati unashirikiana nao”
“Mheshimiwa Rais jambo
hili linaanzia katika ugonjwa
wa Edger Kaka”akasema
Olivia na kumsimulia Rais
namna alivyopambana hadi
kumpeleka Edger Kaka
Israel na kilichotokea kule
hadi waliporejea nyumbani.
“Niliagana na Edger
uwanja wa ndege kwa miadi
ya kuonana naye kesho ili
tukatoe pole kwa familia ya
yule msichana aliyeuwa
nchini Israel lakini
hatukuonana tena kwani
ilitokea ajali ambayo
ilihusisha msafara wa Edger
na ikadaiwa kwamba
amefariki dunia.Ni mimi
ndiye niliyeutambua mwili
wake na kilichonifanya
niutambue mwili ule ni
mkufu aliouvaa na
pete.Tulimzika na
tukasahau”akanyamaza kwa
muda halafu akaendelea
“Miaka mitatu baadae
nikiwa kazini nilifuatwa na
meneja wa hoteli Fulani
kubwa hapa jijini akanieleza
kwamba kuna mgeni wangu
ambaye natakiwa kuonana
naye ambaye anazo taarifa
kuhusiana na Edger
Kaka.Nilikwenda kuonana
naye na akajitambulisha
kwangu anaitwa Abu
Dahir.Alidai yeye ni kaka wa
Edger Kaka na akanipa
maelezo kuwa yeye na Edger
mama yao ni mmoja ambaye
ni Habiba Jawad.” Olivia
akanyamza kidogo baada ya
Dr Evans kuonyesha
mshangao
“Habiba Jawad ni mama
wa Edger Kaka?
“Ndiyo mheshimiwa
Rais.Habiba Jawad ni
mzaliwa wa Kenya lakini ana
asili ya Somalia aliolewa na
Nasser Jawad mfanya
biashara tajiri na wakamzaa
mtoto aitwaye Seif Jawad
ambaye ndiye huyu Edger
Kaka.Jina Edger alipewa
baada ya kuhamishiwa
Tanzania.Wazazi wake
walimuhamishia Tanzania
akiwa chini ya uangalizi wa
walezi wa kitanzania
waliolipwa fedha nyingi na
Habiba na ndipo akapewa
jina la Edger Kaka lakini
jina lake halisi ni Seif
Jawad”
“My God ! haya mambo
ni mageni kabisa.Kumbe
Edger Kaka si mtanzania?
Akauliza Dr Evans
“Edger Kaka si
mtanzania”akajibu Olivia
“Baada ya mumewe
kufariki dunia,Habiba
aliolewa na mwanaume
mwingine tajiri mwenye asili
ya Palestina na wakazaa
mtoto ambaye ndiye huyo
Abu Dahir ambaye alinifuata
hapa Tanzania.Abu dahir
alinieleza kwamba Edger
Kaka hajafariki dunia na
akaniomba kwa kuwa
nilikuwa na ukaribu na
Edger basi tushirikiane
kuutafuta ukweli na
kumsaidia Edger.Alinitaka
niachane na kazi yangu ya
udaktari na badala yake
atanipa fedha ambazo
nitajenga kituo cha utafiti wa
magonjwa mbali mbali ya
binadamu na wanyama na
ndicho kituo kile
nilichokijenga.Hiyo ilikuwa
hatua ya kwanza.Baada ya
kituo kukamilika Abu Dahir
akaniita nchini Saudi Arabia
kwa ajili ya hatua ya pili na
kwa mara ya kwanza
nikakutana na mama yake
Edger ambaye ni Habiba
Jawad.Nilizungumza naye
akanieleza mengi historia
yake na yote anayoyafanya
na alikiri kwangu kwamba
anafadhili kikundi cha IS na
vikundi vingine vidogo dogo
vya kigaidi.Alinitaka tuingie
katika hatua ya pili nayo ni
kuufanyia uchunguzi mwili
ule ambao wote tuliamini ni
wa Edger kaka.Nilichukua
sampuli za masalia ya mwili
ule mimi mwenyewe na
kuzifanyia uchunguzi
nikabaini kweli mwili ule
haukuwa wa Edger Kaka na
hapo ndipo tulipoingia katika
hatua ya tatu ambayo ni
kumtafuta Edger Kaka
mahala alipo.IS waliamini
kwamba waliohusika katika
kutengeneza ajali ile ya
Edger ni serikali ya Tanzania
hivyo wakanitaka niandae
kirusi ambacho tutakitumia
kumuambukiza mwanao ili
kukushinikiza uweze
kumuachia Edger.Hilo
likafanyika na nilikwenda
Congo kukutana na Seif
Almuhsin ili kupata matokeo
ya kirusi nilichokitengeneza
na niliporejea hapa ndipo
nikatekwa.Mheshimiwa Rais
IS walinitaka niwafanyie kila
wanachokitaka na kama
nikikataa basi watawaua
familia yangu ndiyo maana
nikakubali kufanya nao
kazi.Mheshimiwa Rais
historia nzima ya mimi na IS
ni hiyo.Mimi si gaidi na wala
si mmoja wao na siwezi kuwa
mmoja wao japo nimeshiriki
katika baadhi ya mipango
yao”akasema Olivia na
kunyamaza
“Olivia maelezo hayo
yamenitoa jasho.Kwa nini
hukunieleza haya yote
nilipokuja kuonana nawe
pale katika idara ya siri ya
mambo ya ndani?
“Lengo langu lilikuwa
kumpata Edger kaka ili
niweze kumalizana na IS
ndiyo maana sikutaka
kukueleza kitu
chochote.Mheshimiwa Rais
narudia tena kusisitiza
kwamba mimi si gaidi na
hata nilipomuambukiza
Coletha kile kirusi nilikuwa
na uhakika hatakufa kwa
kuwa nilikuwa na dawa ya
kumtibu”
“Sasa nimekuelewa
Olivia.Kila mtu alikuwa
anajiuliza maswali mengi
sababu ya wewe kujiunga na
IS na sasa nimepata
jibu.Pole sana kwa yote
uliyopitia” akasema DrEvans
“Ahsante sana
mheshimiwa Rais lakini
nataka nikueleze kwamba
hukupaswa kumuacha Edger
kaka.Yule ndiye gaidi na
alikuwa hapa nchini kwa
malengo maalum.Kwanza si
mtanzania lakini ameishi
hapa nchini kama Mtanzania
na hadi akapata uongozi.IS
walikuwa wanamuandaa
Edger kuwa Rais wa
Tanzania”
“Kuwa Rais? Dr Evans
akashangaa
“Ndiyo.Alikuwa
anaandaliwa kuwa Rais na
wametumia gharama kubwa
kumtengeneza hadi pale
alipofika”
“Kwa hilo nakubaliana
nawe Olivia.Baada ya
kushindwa kwa mpango wao
kwa Edger Kaka walianza
kumuandaa waziri mkuu wa
sasa kwa ajili ya nafasi hiyo”
“Waziri mkuu?
“Ndiyo.He was one of
them” akasem Dr Evans na
kumueleza Olivia kile
kilichotokea mchana wa siku
iliyopita hadi waziri mkuu
alivyokamatwa.
“Mheshimiwa Rais
mmefanya mambo makubwa
sana siku ya leo lakini kuna
makosa pia
yamefanyika.Kwanza mtu
aliyeyafanikisha haya yote
ambaye ni Mathew Mulumbi
hakupaswa kuachwa porini
afe mwenyewe.Pili Edger
Kaka hakupaswa kabisa
kutoka mikononi
mwetu.Alipaswa kuendelea
kushikiliwa hapa hapa
nchini” akasema Olivia
“Nakubaliana nawe
Olivia kwamba hayo ni
makosa yamefanyika lakini
mafaniko pia ni
makubwa.Watoto waliotekwa
nyara
wamepatikana,magaidi
wamekamatwa na wengine
kuuawa na kubwa zaidi
wewe na Coletha mmrejea
nyumbani.Plani yetu
iilikuwa ni kumuua baada ya
mabadilishano lakini mambo
hayakwenda kama
tulivyotaka na wakafanikiwa
kumtorosha Edger
Kaka.Hata hivyo pamoja na
kukimbia lakini hatarejea
tena Tanzania.Umenifumbua
macho Olivia na sasa
tunakwenda kufanya uhakiki
upya wa nani ni mtanzania
na nani siye tukianza na
viongozi.Kuna mengi
yanakwenda kufanyika nchi
itatikisika kwa muda lakini
itakaa sawa.Kilichotokea
kimenipa funzo kubwa.Hata
hivyo kuna jambo ambalo
nataka msaada wako”
“Jambo gani mheshimiwa
Rais?
“Nimeikosea sana familia
yako hasa baba yako.Agrey si
rafiki bali ni zaidi ya
ndugu.Mimi na yeye tuna
historia ndefu.Najua
akifahamu hiki kilichotokea
urafiki wetu utafika mwisho
jambo ambalo sitaki
litokee.What can I
do?akauliza DrEvans
“Ni kweli mheshimiwa
Rais umetokea mvurugano
mkubwa lakini nataka nikiri
kwamba aliyesababisha haya
yote ni mimi.Mimi na wewe
sote tunatakiwa kuwaeleza
wazazi wangu ukweli wote
wa kile
kilichotokea.Itachukua muda
urafiki wenu kurejea kama
zamani lakini nina uhakika
mkubwa mambo haya
yatamalizika” akasema
Olivia
“Tutamaliza mambo haya
kesho lakini kwa sasa
utakwenda kupumzika
umeandaliwa chumba hapa
hapa.Please don’t call anyone
hadi pale muda utakapofika”
akasema Dr Evans
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 24
Saa nne na nusu za
asubuhi msafara wa Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania uliwasili katika
kambi ya jeshi ya kikosi cha
operesheni maalum.Alishuka
garini na kupokewa na
waziri wa ulinzi na
kusalimiana na mku wa
majeshi na makamanda
wengine wakubwa wa jeshi
akiwamo Austin January
mkuu wa kikosi kile cha
operesheni maalum.Baada ya
Rais kuwasili ratiba
iliyopangwa kwa ajili ya
kuiaga miili ya wanajeshi
waliopoteza maisha katika
operesheni ya kuwakomboa
Coletha na Olivia
ikaanza.Viongozi wa dini
walianza kwa dua na sala
mbali mbali za kuwaombea
marehemu wale na ratiba
ikaendelea.Miili ya
wanajeshi wale ikaagwa na
Rais akaondoka kurejea
ikulu ambako alitarajiwa
kulihutubia taifa
“Ndugu watanzania
wenzangu ni siku nyingine
tena nimekuja mbele yenu
kuzungumza nanyi.Awali ya
yote narudia tena kuwapeni
pole wale wote mliofiwa na
wapendwa wenu katika
matukio ya kigaidi
yaliyotokea hapa
nchini.Tunawaombea
marehemu wote wapumzike
kwa amani Amina.
“Ndugu watanzania,nchi
yetu ambayo amani
imetamalaki,ilipatwa na
majanga ya mashambulio
mawili ya kigaidi,moja ni
bomu lililolipuliwa katika
hospitali ya Mtodora na
shambulio lingine ni
kutekwa kwa wanafunzi
sitini na sita katika shule ya
sekondari ya St
Getrude.Katika shambulio la
hospitali ya Mtodora
walifariki watu ishirini na
moja na wengine wengi
kujeruhiwa wengine vibaya
sana na katika wanafunzi
waliotekwa wameuawa
watoto wanne na
tukafanikiwa kuwakomboa
wanafunzi sitini na mbili na
walimu wao
watatu.Wanafunzi wote
waliokombolewa
watakabidhiwa kwa wazazi
wao kwa sasa wanaendelea
kupatiwa msaada wa
kisaikolojia ili kuwaweka
vizuri kwani kitendo
kilichowatokea
kimewasababishia mstuko
mkubwa.Kwa wale
waliouawa taratibu
zinafanywa ili miili yao
ikabidhiwe kwa familia zao
kwa ajili ya mazishi ambayo
yatagharamiwa na
serikali.Tunawapa pole sana
wote mliofiwa na watoto na
ndugu zenu katika
mashambulio haya
tunawaombea uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu.
“Ndugu watanzania
wenzangu magaidi
wanapofanya shambulio
mahali Fulani huwa na
sababu zao aidha kulipiza
kisasi au kulazimisha
wapewe au kutimiziwa
mambo Fulani yenye
manufaa kwao.Hapa kwetu
walifanya hivyo kuna mambo
walikuwa wanayahitaji na
wakafanya mashambulio
yale ili kushinikiza serikali
iwatimizie madai
yao.Serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania
haijawahi na haitafanya
makubaliano yoyote na
magaidi.Jukumu letu ni
kuhakikisha tunawafyekelea
mbali kila pale wanapojaribu
kujipenyeza nchini kwetu na
ndivyo tulivyofanya.Alasiri
ya jana majasusi wetu
wakishirikiana na kikosi cha
jeshi cha operesheni maalum
walifanikiwa kugundua
maficho ya magaidi hao
wakavamia na kuwakomboa
watoto sitini na mbili na
walimu wao watatu.Magaidi
wote waliokuwamo katika
nyumba hiyo
waliuawa.Hatuna huruma na
gaidi yeyote.Msako mkali
ulianza jana hiyo hiyo na
tayari tumefanikiwa
kuwakamata watu kadhaa
ambao wana mahusiano na
kikundi cha kigaidi cha IS na
tunaendelea kukamata
wengine hadi
tutakapohakikisha magaidi
wote wametiwa
mikononi.Nawaahidi
kwamba hakuna gaidi
atakayebaki,tutawakamata
wote na kuufyekelea mbali
mtandao wao wote hapa
nchini.
Usiku wa jana pia
kumetokea mapigano
makubwa kati ya kikosi
chetu cha operesheni
maalum na magaidi katika
mpaka wa Tanzania na
Kenya na katika mapigano
hayo makali tumewapoteza
vijana wetu kumi na tatu na
kuwasambaratisha magaidi
wote.Tunawaombea vijana
wetu hao mashujaa
wapumzike kwa amani
kwani wamemwaga damu
yao kwa kulipigania taifa lao
Ndugu watanzania
katika watu tuliowakamata
wakihusiana na mtandao wa
kigaidi wamo pia viongozi wa
serikali.Wapo baadhi ambao
tunawashikilia tunaendelea
kuwachunguza na pale
uchunguzi utakapokamilika
tutawafikisha
mahakamani.Katika sakata
hili pia tumegundua kwamba
kuna watu ambao si raia wa
nchi hii lakini wanaishi hapa
nchini na tayari wamekwisha
ingia hadi katika ngazi za
uongozi.Tunaanza kufanya
uhakiki wa viongozi wote wa
serikali kujiridhisha kama
kweli ni raia wa
Tanzania.Tumebaini mchezo
unaofanywa na watu
wasiotutakia mema wa
kupandikiza watu wao hapa
nchini toka wakiwa wadogo
kwa malengo ya kuwatumia
katika mipango yao na watu
hao wanaopandikizwa
wamediriki kushika hadi
nafasi za uongozi.Tutakuwa
makini katika mipaka yetu
kudhibiti wahamiaji haramu
ninatoa rai kwenu
watanzania wenzangu kama
unamfahamu mtu yeyote
ambaye si raia wa nchi hii
lakini anaishi hapa nchini
toa taarifa katika vyombo
husika ili aweze
kushughulikiwa haraka sana
kwani wengiwa magaidi
hawa ni wageni ambao
wamekuwa wakiishi hapa
nchini wakifadhiliwa na
wenyeji
Ndugu watanzania
matukio haya
yametufundisha kwamba upo
ulazima wa kuviongezea
nguvu kubwa vyombo vyetu
vinavyohusika katika
mapambano na ugaidi ili
viwe na uwezo mkubwa wa
kubaini matukio ya kigaidi
kabla hayajatokea na
kuyadhibiti.Hilo tutalifanya
haraka sana.Mwisho kabisa
nataka kuwajulisha kwamba
kuanzia leo hii nimelivunja
baraza langu la mawaziri
nitateua baraza jipya hapo
baadae.
Narudia tena wito wangu
wa kuwataka watanzania
tuwe wavumlivu na tuviache
vyombo vya ulinzi na
usalama vifanye kazi yake
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza
BAADA YA MWEZI MMOJA
Tayari umekwisha pita
mwezi mmoja toka
yalipofanyika mashambulio
ya kigaidi.Nchi imetulia na
wananchi wanaendelea na
maisha yao kama
kawaida.Rais Dr Evans
ameunda baraza jipya la
mawaziri.Baada ya uchuguzi
kukamilika aliyekuwa waziri
mkuu wa jamhuri ya
munganowa Tanzania na
wenzake sitini na saba
walifikishwa mahakamani
wakituhumiwa kwa makosa
ya ugaidi.Dr Olivia Themba
alikikabidhi serikalini kituo
cha utafiti wa magonjwa ya
binadamu na wanyama
ambacho alikijenga kwa
fedha kutoka kwa watu wa
IS na yeye akaanza ujenzi wa
hospitali kubwa ya
magonjwa ya moyo pembeni
kidogo ya kituo kile.
Mathew Mulumbi
alitafutwa bila mafanikio na
hakuna aliyefahamu yuko
wapi.Timu iliyotumwa
kumtafuta ilirejea bila ya
Mathew Mulumbi na kutoa
ripoti yake kwamba kuna
uwezekano mkubwa alifariki
na kuliwa na fisi kwani eneo
lilipotokea shambulio lile
kuna fisi wengi.Rais Dr
Evans alituma ujumbe
maalum kwenda Paris
Ufaransa kwa Peniela mke
wa Mathew kupeleka salamu
za pole kufuatia kifo cha
Mathew.Ujumbe ule
uliongozwa na Austin
January ambaye alikuwa na
Mathew eneo la tukio.Ruby
aliondoka nchini kwenda
kuendelea na shughuli zake
lakini Gosu Gosu aliombwa
na Peniela kubaki nchini
kuendelea kusimamia miradi
yote ya Mathew ombi ambalo
Gosu Gosu alilipokea kwa
mikono miwili.
Mahusiano kati ya Dr
Evans na Agrey Themba
yaliendelea baada ya Dr
Evans kueleza ukweli wa kile
kilichotokea na kumuomba
rafiki yake yule mkubwa
msamaha wakasameheana
na maisha yakaendelea
kama ilivyokuwa awali lakini
kilichotokea kilibaki kuwa
siri kati yao
Siku tatu baada ya
shambulio la mpakani
kutokea Devotha aliondoka
nchini kwa ndege akielekea
Dubai na hakuna mwenye
mawasiliano naye tena wala
kufahamu mahala alipo.
Idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi
iliimarishwa zaidi na Rais
aliamua kuitambulisha
rasmi idara hii kwa viongozi
wa juu wa serikali na ulinzi
ili wafahamu uwepo
wake.Kaiza alipewa
ukurugenzi wa idara hii.
TAMATI
MPENZI MSOMAJI HAPA
NI TAMATI YA SIMULZI
YA SIRI PART 1.USIKOSE
KUSOMA SIRI PART 2
YENYE KICHWA
MAISHA NA KIFO CHA
MELANIE CHUMA
 
SIRI
MTUNZI : PATRICK CK
SEASON 9: EPISODE 24
Saa nne na nusu za
asubuhi msafara wa Rais wa
jamhuri ya muungano wa
Tanzania uliwasili katika
kambi ya jeshi ya kikosi cha
operesheni maalum.Alishuka
garini na kupokewa na
waziri wa ulinzi na
kusalimiana na mku wa
majeshi na makamanda
wengine wakubwa wa jeshi
akiwamo Austin January
mkuu wa kikosi kile cha
operesheni maalum.Baada ya
Rais kuwasili ratiba
iliyopangwa kwa ajili ya
kuiaga miili ya wanajeshi
waliopoteza maisha katika
operesheni ya kuwakomboa
Coletha na Olivia
ikaanza.Viongozi wa dini
walianza kwa dua na sala
mbali mbali za kuwaombea
marehemu wale na ratiba
ikaendelea.Miili ya
wanajeshi wale ikaagwa na
Rais akaondoka kurejea
ikulu ambako alitarajiwa
kulihutubia taifa
“Ndugu watanzania
wenzangu ni siku nyingine
tena nimekuja mbele yenu
kuzungumza nanyi.Awali ya
yote narudia tena kuwapeni
pole wale wote mliofiwa na
wapendwa wenu katika
matukio ya kigaidi
yaliyotokea hapa
nchini.Tunawaombea
marehemu wote wapumzike
kwa amani Amina.
“Ndugu watanzania,nchi
yetu ambayo amani
imetamalaki,ilipatwa na
majanga ya mashambulio
mawili ya kigaidi,moja ni
bomu lililolipuliwa katika
hospitali ya Mtodora na
shambulio lingine ni
kutekwa kwa wanafunzi
sitini na sita katika shule ya
sekondari ya St
Getrude.Katika shambulio la
hospitali ya Mtodora
walifariki watu ishirini na
moja na wengine wengi
kujeruhiwa wengine vibaya
sana na katika wanafunzi
waliotekwa wameuawa
watoto wanne na
tukafanikiwa kuwakomboa
wanafunzi sitini na mbili na
walimu wao
watatu.Wanafunzi wote
waliokombolewa
watakabidhiwa kwa wazazi
wao kwa sasa wanaendelea
kupatiwa msaada wa
kisaikolojia ili kuwaweka
vizuri kwani kitendo
kilichowatokea
kimewasababishia mstuko
mkubwa.Kwa wale
waliouawa taratibu
zinafanywa ili miili yao
ikabidhiwe kwa familia zao
kwa ajili ya mazishi ambayo
yatagharamiwa na
serikali.Tunawapa pole sana
wote mliofiwa na watoto na
ndugu zenu katika
mashambulio haya
tunawaombea uvumilivu
katika kipindi hiki kigumu.
“Ndugu watanzania
wenzangu magaidi
wanapofanya shambulio
mahali Fulani huwa na
sababu zao aidha kulipiza
kisasi au kulazimisha
wapewe au kutimiziwa
mambo Fulani yenye
manufaa kwao.Hapa kwetu
walifanya hivyo kuna mambo
walikuwa wanayahitaji na
wakafanya mashambulio
yale ili kushinikiza serikali
iwatimizie madai
yao.Serikali ya jamhuri ya
muungano wa Tanzania
haijawahi na haitafanya
makubaliano yoyote na
magaidi.Jukumu letu ni
kuhakikisha tunawafyekelea
mbali kila pale wanapojaribu
kujipenyeza nchini kwetu na
ndivyo tulivyofanya.Alasiri
ya jana majasusi wetu
wakishirikiana na kikosi cha
jeshi cha operesheni maalum
walifanikiwa kugundua
maficho ya magaidi hao
wakavamia na kuwakomboa
watoto sitini na mbili na
walimu wao watatu.Magaidi
wote waliokuwamo katika
nyumba hiyo
waliuawa.Hatuna huruma na
gaidi yeyote.Msako mkali
ulianza jana hiyo hiyo na
tayari tumefanikiwa
kuwakamata watu kadhaa
ambao wana mahusiano na
kikundi cha kigaidi cha IS na
tunaendelea kukamata
wengine hadi
tutakapohakikisha magaidi
wote wametiwa
mikononi.Nawaahidi
kwamba hakuna gaidi
atakayebaki,tutawakamata
wote na kuufyekelea mbali
mtandao wao wote hapa
nchini.
Usiku wa jana pia
kumetokea mapigano
makubwa kati ya kikosi
chetu cha operesheni
maalum na magaidi katika
mpaka wa Tanzania na
Kenya na katika mapigano
hayo makali tumewapoteza
vijana wetu kumi na tatu na
kuwasambaratisha magaidi
wote.Tunawaombea vijana
wetu hao mashujaa
wapumzike kwa amani
kwani wamemwaga damu
yao kwa kulipigania taifa lao
Ndugu watanzania
katika watu tuliowakamata
wakihusiana na mtandao wa
kigaidi wamo pia viongozi wa
serikali.Wapo baadhi ambao
tunawashikilia tunaendelea
kuwachunguza na pale
uchunguzi utakapokamilika
tutawafikisha
mahakamani.Katika sakata
hili pia tumegundua kwamba
kuna watu ambao si raia wa
nchi hii lakini wanaishi hapa
nchini na tayari wamekwisha
ingia hadi katika ngazi za
uongozi.Tunaanza kufanya
uhakiki wa viongozi wote wa
serikali kujiridhisha kama
kweli ni raia wa
Tanzania.Tumebaini mchezo
unaofanywa na watu
wasiotutakia mema wa
kupandikiza watu wao hapa
nchini toka wakiwa wadogo
kwa malengo ya kuwatumia
katika mipango yao na watu
hao wanaopandikizwa
wamediriki kushika hadi
nafasi za uongozi.Tutakuwa
makini katika mipaka yetu
kudhibiti wahamiaji haramu
ninatoa rai kwenu
watanzania wenzangu kama
unamfahamu mtu yeyote
ambaye si raia wa nchi hii
lakini anaishi hapa nchini
toa taarifa katika vyombo
husika ili aweze
kushughulikiwa haraka sana
kwani wengiwa magaidi
hawa ni wageni ambao
wamekuwa wakiishi hapa
nchini wakifadhiliwa na
wenyeji
Ndugu watanzania
matukio haya
yametufundisha kwamba upo
ulazima wa kuviongezea
nguvu kubwa vyombo vyetu
vinavyohusika katika
mapambano na ugaidi ili
viwe na uwezo mkubwa wa
kubaini matukio ya kigaidi
kabla hayajatokea na
kuyadhibiti.Hilo tutalifanya
haraka sana.Mwisho kabisa
nataka kuwajulisha kwamba
kuanzia leo hii nimelivunja
baraza langu la mawaziri
nitateua baraza jipya hapo
baadae.
Narudia tena wito wangu
wa kuwataka watanzania
tuwe wavumlivu na tuviache
vyombo vya ulinzi na
usalama vifanye kazi yake
Mungu ibariki Tanzania
Ahsanteni kwa kunisikiliza
BAADA YA MWEZI MMOJA
Tayari umekwisha pita
mwezi mmoja toka
yalipofanyika mashambulio
ya kigaidi.Nchi imetulia na
wananchi wanaendelea na
maisha yao kama
kawaida.Rais Dr Evans
ameunda baraza jipya la
mawaziri.Baada ya uchuguzi
kukamilika aliyekuwa waziri
mkuu wa jamhuri ya
munganowa Tanzania na
wenzake sitini na saba
walifikishwa mahakamani
wakituhumiwa kwa makosa
ya ugaidi.Dr Olivia Themba
alikikabidhi serikalini kituo
cha utafiti wa magonjwa ya
binadamu na wanyama
ambacho alikijenga kwa
fedha kutoka kwa watu wa
IS na yeye akaanza ujenzi wa
hospitali kubwa ya
magonjwa ya moyo pembeni
kidogo ya kituo kile.
Mathew Mulumbi
alitafutwa bila mafanikio na
hakuna aliyefahamu yuko
wapi.Timu iliyotumwa
kumtafuta ilirejea bila ya
Mathew Mulumbi na kutoa
ripoti yake kwamba kuna
uwezekano mkubwa alifariki
na kuliwa na fisi kwani eneo
lilipotokea shambulio lile
kuna fisi wengi.Rais Dr
Evans alituma ujumbe
maalum kwenda Paris
Ufaransa kwa Peniela mke
wa Mathew kupeleka salamu
za pole kufuatia kifo cha
Mathew.Ujumbe ule
uliongozwa na Austin
January ambaye alikuwa na
Mathew eneo la tukio.Ruby
aliondoka nchini kwenda
kuendelea na shughuli zake
lakini Gosu Gosu aliombwa
na Peniela kubaki nchini
kuendelea kusimamia miradi
yote ya Mathew ombi ambalo
Gosu Gosu alilipokea kwa
mikono miwili.
Mahusiano kati ya Dr
Evans na Agrey Themba
yaliendelea baada ya Dr
Evans kueleza ukweli wa kile
kilichotokea na kumuomba
rafiki yake yule mkubwa
msamaha wakasameheana
na maisha yakaendelea
kama ilivyokuwa awali lakini
kilichotokea kilibaki kuwa
siri kati yao
Siku tatu baada ya
shambulio la mpakani
kutokea Devotha aliondoka
nchini kwa ndege akielekea
Dubai na hakuna mwenye
mawasiliano naye tena wala
kufahamu mahala alipo.
Idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi
iliimarishwa zaidi na Rais
aliamua kuitambulisha
rasmi idara hii kwa viongozi
wa juu wa serikali na ulinzi
ili wafahamu uwepo
wake.Kaiza alipewa
ukurugenzi wa idara hii.
TAMATI
MPENZI MSOMAJI HAPA
NI TAMATI YA SIMULZI
YA SIRI PART 1.USIKOSE
KUSOMA SIRI PART 2
YENYE KICHWA
MAISHA NA KIFO CHA
MELANIE CHUMA

Hadithi Nzuri sana. Nimesoma yote. Na huwa ninanunua Hadithi hapa. Ushauri Wangu Mdogo bila kutaka kuonekana mbaya ni: kama tukio limeshasimuliwa inakuwa kama Cinema wasomaji tumesoma. Sasa ikija tokea baadaye mhusika Ndani ya Hadithi yenyewe anasimuliwa au kupewa taarifa ambayo kwa wasomaji wanaijua ni vizuri kutoirudia as if simulizi linamuhusu mhusika Ndani ya hadithi. Mfano. Mathew akamsimulia Rais yote yaliyotokea nyuma. Sio tena. Mathews akamsimulia Rais ... moja. Mbili. Tatu. ( vitu ambavyo wasomaji wameshasoma Mfano chapter ya nne, na Rais anasimuliwa chapter ya 10. Asante.
 
Mimi natabiri part two kwamba Mathew hatauliwa na mossad ila wanaweza wakampa kazi kutokana na uwezo mkubwa alionao huwezi kuua asset Kama ilee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom