Riwaya: Siri

Aise hii simulizi ili nipita vipi? ?... naona taswira ya Jiwe katika hii simulizi

Kikulacho kinguoni mwako
 
SIRI

Episode 11
Mtunzi. Patrick CK

mia moja kuwa mtaiweza kazi
hii.Kazi yetu kubwa ni kuwamaliza
kisiasa wale wote wanaoonekana
kuwa na nguvu kubwa ndani na nje
ya chama na ambao wanaonekana
kuwa tishio kwa mheshimiwa rais
kama watachukua fomu za
kugombea .Kuna watu wawili hapa
ambao tutaanza nao.Wa kwanza ni
mheshimiwa Damiani
Mwamba.Yeye huyu kwa mujibu
wa taarifa tulizozipata ni kwamba
tayari amekwisha tengeneza timu
yake ya kuhakikisha anapata
ridhaa ya chama ya kugombea
urais.Mbio zake za chini chini
zinaonekana kushika kasi na
anapata uungwaji mkono mkubwa kila siku.Huyu ni tishio kubwa kwa
meshimiwa rais.Wa pili ni huyu
kijana mbunge Edger ambaye kwa
sasa yuko katika matibabu nchini
Israel.Huyu naye ni kijana hatari
sana.Uungwaji wake mkono katika
jamii hususani vijana ni wa
kiwango cha kushangaza.Japokuwa
hajatangaza nia yake ya kugombea
urais lakini akitangaza kuwania
urais atakuwa na nafasi kubwa ya
kushinda.Hatuwezi katu kumpa
nafasi hiyo.Kwa sasa tumemtuma
Judy amfuate huko huko Israel
katika hospitali anayotibiwa . Kazi
atakayoifanya kule ni kuchunguza
nyendo za Edger na kila
anachokifanya.Kwa huyu Edger tayari tumemailza hatua za
awali.Shughuli inabaki kwa
Damiani Mwamba.kama
tunavyomjua Damiani mwamba ni
mtu mwenye mtandao mkubwa wa
watu kwa hiyo tunatakiwa tuwe
naye makini mno.Kazi ya kwanza
tunayotakiwa kufanya ni
kumchunguza kwa undani nyendo
zake.Tunatakiwa tujue anapendelea
nini,rafiki zake ni nani,anapendelea
kwenda kupumzika baa gani kama
anatumia kilevi, kwa ufupi
tunatakiwa tuifahamu tabia yake
kwa ujumla.Tukishamsoma na
kumfahamu
kiundani,kitakachofuata ni
kumuwekea microchip katika simu yake.Microchip hiyo ambayo sisi
tutakuwa tukiifuatilia kwa kutumia
satellite,ndiyo itakayokuwa
ikituonyesha Damiani yuko wapi,na
tutaweza hata kuyapata maongezi
anayoongea.Baada ya hapo tutajua
wapi pa kuanzia kazi yetu.Sitaki
kazi hi ichukue muda mrefu.Ndani
ya wiki mbili zijazo ni lazima tuwe
tumekwisha anza utekelezaji wa
mpango wetu.Kwa sasa mnatakiwa
muanze kujipanga kwa utekelezaji
wa kazi hii.Kumbukeni kuwa
hakuna kushindwa katika
hili.Kushindwa kokote kule
kutamuweka mheshimiwa rais
sehemu mbaya zaidi.Tuliepuke hilo
lisitokee na kuliepuka hilo ni kwa kuwaangusha hawa jamaa
mapema.Tukimaliza ndani ya
chama tutahamia katika vyama
pinzani.Paul nataka mpaka jioni ya
leo niwe nimepata mchanganuo
mzima wa shughuli nzima
itakavyokwenda ikiwa ni pamoja
na gharama zote ili niwasilishe kwa
mheshimiwa rais haraka
iwezekanavyo.Mpaka hapo kuna
tatizo lolote?
Donald akawaangalia vijana
wale ambao wote wamewahi
kufanya kazi katika mashirika
mbali mbali ya kiusalama duniani
na kwa sasa walikuwa na kampuni
yao wenyewe ya kukodiwa kufanya
kazi binafsi.Donald amekuwa akiwatumia sana vijana hawa
kumfanyia kazi zake chafu.Kikundi
hiki cha watu watano kilikuwa na
utaalamu wa hali ya juu katika kila
nyanja ,kuanzia utaalamu wa
kompyuta,mawasialiano,silaha nk.
*****************
Dickson Kipuma mlinzi wa siri
wa waziri mkuu alikuwa
anatazamana na mkuu wake
aliyemuita ofisini kwake kwa
dharura
“Dick nimekuita kwa
dharura,kuna kazi imejitokeza
ambayo hakuna anayeweza
kuifanya kikamilifu zaidi yako.Kazi hii inakwenda kufanyika nje ya
nchi” akasema waziri mkuu na
kunyamaza kidogo halafu
akaendelea
“Nadhani umeshasikia kuhusu
ugonjwa wa ghafla uliompata
mbunge Edger kaka siku chache
zilizopita.Alipatwa na ugonjwa wa
ghafla akiwa bungeni na kutokana
na hali yake kuwa mbaya
akapelekwa nchini Israel na kwa
sasa hali yake inaendelea
vizuri.Taarifa kutoka kwa
madaktari nchini Israel inaonesha
kuwa Edger aliwekewa sumu kwa
lengo la kumuua.Ninahisi kuwa
watu waliofanya mpango ule wa
kumuua Edger ni baadhi ya viongozi wa serikali na wafanya
biashara wakubwa.Kuna mambo
Edger ameyagundua kuhusiana na
ufisadi mkubwa uliofanywa na
mtandao wa vigogo wa serikali
wakishirikiana na wafanya
biashara ndiyo maana
wakataka.Mpango wao
umeshindwa kufanikiwa naamini
lazima watabuni tena mpango
mwingine wa kummaliza”
akanyamaza tena kwa sekunde
kadhaa halafu akaendelea
“Edger anao ushahidi
unaoweza kuwatia hatiani watu
hao.Tunatakiwa tuulinde ushahidi
huo ili wasiweze kuunyakua na
kuuharibu.Ninakutuma uende Israel na kufanya kazi ya kumlinda
Edger na kila jambo baya hadi hapo
atakapokuwa amepona kabisa na
kurejea nyumbani.Edger amelazwa
katika hospitali ya Rambam mjini
Haifa.Kazi unayotakiwa kuifanya ni
kumlinda kwa siri kama
unavyonilinda mimi.Hatakiwi mtu
yeyote afahamu kuwa unamlinda
hata Edger mwenyewe hatakiwi
kujua kama analindwa.Mipango ya
safari yako inaandaliwa na kila kitu
kitakamilika jioni ya leo.Nataka
kesho uondoke nchini na kwenda
huko Israel.Kwa taarifa tu ni
kwamba utalazwa hapo hapo
Rambam medical center alikolazwa
Edger ukiwa kama mgonjwa toka nchini Zimbabwe na unayekwenda
kutibiwa maradhi ya
moyo.Maandalizi yote kuhusu suala
hilo yameshafanyika.Yair ambaye
ni jasusi katika shirika la Mosad
ndiye niliyemuomba aandae
mipango yote na ndiye
atakayekuwa msaada mkubwa
kwako.Atakupokea katika uwanja
wa ndege wa Haifa.Ninamwamini
sana Yair kwa sababu miaka mitatu
iliyopita nilimsaidia hifadhi nchini
Tanzania wakati alipokuwa
akitafutwa auawe na majasusi wa
Kirusi.Hali ilipokuwa shwari
aliondoka na kurudi nchini
kwao.Amekubali kushirikiana nawe
kwa moyo mmoja ukiwa kule Israel.Dickson narudia tena kuwa
kwa gharama yoyote ile yatubidi
kumlinda Edger pamoja na
ushahidi alionao utakaotusaidia
kuwafikisha mbele ya sheria
mafisadi wote wanaolihujumu
taifa” akasema waziri mkuu.
HAIFA - ISRAEL
“Karibu sana
Juddy.Nimefarijika mno kwa kuja
kwako.Nimekuwa mpweke sana
huku,niko peke yangu na baada ya
kutoka hospitali kumtazama Edger
ninakuwa peke yangu hotelini
ninaboreka mno kwa kukosa hata
mtu wa kuongea naye.Watu wengi huku wanazungumza lugha ya
kiyahudi na mimi siijui lugha
yao.Nafurahi umekuja nimepata
mtu wa kunisaidia” akasema Dr
Olivia akimkaribisha Judy
Amos,msichana aliyetumwa na rais
kwenda Israel kumsaidia Olivia
kumuuguza Edger.Judy aliwasili
mjini Haifa jioni hiyo na kufikia
katika hoteli aliyokuwa amefikia Dr
Olivia
“Hata mimi nashukuru sana
kupata nafasi hii ya kuja huku
Israel kukusaidia kumuuguza
mheshimiwa mbunge.Rais Dr Evans
alinisisitiza mara mbili mbili kuwa
nihakikishe nakusaidia kazi zote ili
upate muda wa kupumzika” Judy akasema na kumfanya Olivia
atabasamu.
“Ahsante sana Judy.Kazi
kubwa iliyoko huku ni kwenda
hospitali kumtazama mgonjwa na
kuhakikisha Edger anapona
haraka.Kwa upande Fulani
ninafurahi kuwepo huku kwani
nimepata walau wasaa wa
kupumzika.Nikiwa nyumbani
ninafanya kazi mwaka mzima bila
mapumziko”akasema Dr Olivia
“Nadhani rais ameliona hilo
ndiyo maan akanituma
nijenikusaidie ili uweze kupata
mapumziko mazuri.Usijali dada
Olivia nitakusaidia kazi zote ili nawe uweze kupata muda wa
kupumzika”akasema Judy
Dr Olivia akatabasamu
tena.Waliongea mengi usiku
ule,wakikumbushana mambo
mengi nyumbani na baadae
wakaachana kila mmoja akaenda
kulala katika chumba
chake.Alipofika chumbani kwake
Judy akafungua begi lake dogo
akatoa kompyuta yake ndogo
akaiwasha na kwa kutumia
mtandao wa Skype akawapigia
simu wenzake nchini Tanzania.
“Hello Paul” Judy akamsalimu
Paul kiongozi wa kundi lao baada
ya kufanikiwa kumpata simuni. “Hello Judy.Nipe
habari,umeshafika? Paul akauliza
“Ndiyo
nimeshafika.Nimeshaonana na Dr
Olivia na hajaonesha wasi wasi
wowote.Kesho tunakwenda wote
hospitali na huko ndiko
nitakapoianza kazi yangu.”
“vizuri sana.Jitahidi kuwa
makini katika kila unalolifanya”
Paul akamsisitiza.
“Usijali Paul.Niko makini sana
katika kila jambo.Tutawasiliana
kesho saa sita mchana ambako kwa
huko nyumbani Tanzania itakuwa
ni saa tano subuhi.” “Okay Judy usiku
mwema”akasema Paul na kuagana
na Judy
Judy akapanga vifaa vyake
tayari kwa kazi halafu akalala.
Saa nne za asubuhi juu ya
alama siku iliyofuata iliwakuta Dr
Olivia na Judy wakiwa
hospitalini.Edger alikuwa amekaa
kitandani akiwa na tabasamu usoni
mara alipomwona Dr Olivia
“Unaendeleaje Edger ? Dr
Olivia akauliza.
“Namshukuru Mungu
naendelea vizuri sana.Vipi wewe
unaendeleaje?
“Mimi naendelea vizuri
pia”akasema Edger “Edger tumepata mgeni.”
Akasema Dr Olivia
“Mgeni wetu anaitwa
Judy,ametumwa na rais kutoka
Tanzania kuja kunisaidia kazi ya
kukuuguza.Amefika jana jioni na
tuko wote hoteli moja”akasema Dr
Olivia
Edger akatabasamu na
kusema.
“Judy karibu sana.Habari za
nyumbani Tanzania? Sisi
tumeshakuwa wenyeji huku
tayari”akasema Edger
“Nashukuru sana mheshimiwa
Edger,nimeshakaribia”akajibu Judy.
“Vipi nyumbani wanasemaje?
Edger akauliza “Nyumbani kuko shwari
hakuna tatizo lolote”
“Vipi vuguvugu za siasa
zinakwendaje? Edger akauliza tena
“Edger please !
nimeshakuambia kila siku kuwa
kwa sasa hebu acha kabisa kufikiria
masuala ya siasa hadi hapo
utakapokuwa umepona na kuwa na
nguvu za kuhimili mikiki mikiki ya
siasa.” Dr Olivia akasema na
kumfanya Edger atabasamu.
“Sawa daktari wangu
nimekuelewa.Leo nataka unipeleke
bustanini nikaone jua” Edger
akasema.
“Usijali Edger”akajibu Dr Olivia
huku akifungua mlango akatoka na kurudi na kiti cha magurudumu
ambacho Edger hukitumia.
Taratibu huku akisaidiwa na
Dr Olivia Edger akainuka na
kwenda kukaa katika kiti kile.
“Dr Olivia,wakati mheshimiwa
mbunge akienda kupunga hewa safi
nje,mimi ngoja niendelee kupanga
panga vitu vizuri.Nikimaliza
nitawafuata huko chini.”Judy
akasema
“Sawa usijali Judy.”akasema Dr
Olivia
Dr Olivia akajibu halafu
akaanza kukisukuma kiti kuelekea
katika lifti.
Judy akabaki akitabasamu kwa
nafasi ile nzuri aliyoipata.Akaufungua mkoba wake
na kutoa kidude kidogo sana
kinacholingana na laini ya
simu.Kidude hiki kilichojulikana
kama micro transmitter akakiweka
chini ya kitanda upande wa
kichwani mahala ambako haikuwa
rahisi kuonekana.Alipohakikisha
kidude kile kimeshika sawa
sawa,akachukua tena chombo
kingine chenye ukubwa wa saa ya
mkononi,akakiwasha,halafu
akaandika namba Fulani,kikatoa
mlio akatabasamu halafu akaenda
chini ya kabati akakinasisha
chombo kile.Kwa kutumia vyombo
vile viwili tayari alikwisha
unganisha chumba cha Edger na kompyuta iliyoko chumbani kwake
na hivyo kuweza kusikia chochote
kile ambacho Edger alikuwa
akiongea.Akatabasamu na kukaa
kitandani.
“Kazi imeanza” akasema kwa
sauti ndogo halafu akatoka na
kuwafuata akina Olivia
“Dr Olivia,sijui nikushukuruje
kwa jinsi ulivyojitoa
kunihudumia.Sioni nikulipe kitu
gani.Umeacha kazi zako nyingi
Tanzania,wagonjwa wengi
wanakukosa kwa ajili ya
kunihudumia mimi.Kwa kuwa Judy
amekuja nadhani ni wakati
muafaka wa wewe kurudi
nyumbani ili ukawashughulikie na watu wengine” Akasema Edger
wakiwa wamekaa katika bustani
nzuri wakipata upepo.Dr Olivia
akacheka kidogo halafu akajibu.
“Edger wewe ni mgonjwa
wangu pia.Ni lazima nihakikishe
kuwa umerudi katika hali yako ya
kawaida ndipo nikuache.lakini kwa
sasa sintaweza kuondoka na
kukuacha huku peke yako.”
Huku akitabasamu Edger
akasema.
“Nashukuru kwa uamuzi wako
huo,lakini vipi kuhusu mumeo na
familia yako? Huoni kuwa
hauwatendei haki kwa kuwa mbali
nao? watu wengine” Akasema Edger
wakiwa wamekaa katika bustani
nzuri wakipata upepo.Dr Olivia
akacheka kidogo halafu akajibu.
“Edger wewe ni mgonjwa
wangu pia.Ni lazima nihakikishe
kuwa umerudi katika hali yako ya
kawaida ndipo nikuache.lakini kwa
sasa sintaweza kuondoka na
kukuacha huku peke yako.”
Huku akitabasamu Edger
akasema.
“Nashukuru kwa uamuzi wako
huo,lakini vipi kuhusu mumeo na
familia yako? Huoni kuwa
hauwatendei haki kwa kuwa mbali
nao? Dr Olivia akatoa kicheko
kikubwa.Edger akamtazama kisha
naye akatabasamu na kusema
“Mbona unacheka hivyo Dr
Olivia?akauliza Edger
“Nacheka kwa swali hilo
uliloniuliza” Dr Olivia akajibu
“Nini kimekufurahisha kwa
swali hilo? Akauliza tena Edger
“Unavyonitazama,ninaonekana
nina mume? Dr Olivia akauliza
“Malaika kama
wewe,msomi,daktari bingwa,mtoto
wa tajiri mkubwa ni lazima uwe na
mume tena mwenye hadhi
kubwa”akasema Edger na
kumfanya Dr Olivia aangue tena
kicheko kikubwa na kujibu. “Sina mume bado na wala
sifikirii kwa sasa kuwa na
mume.Bado nina mambo mengi ya
kufanya kabla ya kufikiria kuwa na
familia”
Jibu lile linamshangaza Edger
na kumfanya aulize.
“Hapana haiwezekani Dr
Olivia.Niambie ukweli.”
“Huo ndio ukweli Edger.Sina
mume na wala sifikirii kwa sasa
kuwa na mume”
“Mpaka lini? Edger akauliza
“Hahahaa Edger,nimeshasema
ni mpaka hapo moyo wangu
utakapoamua,lakini kwa sasa bado
nina mambo mengi ya kufanya” “Mambo gani hayo
yanayokufanya usifikirie kuwa na
familia kwa umri ulionao?
Dr Olivia akanyamaza kimya
kwa muda halafu akasema
“Edger it’s personal.Naomba
tusiendelee na masuala
hayo.Yananikumbusha mbali sana”
Edger akahisi lazima kuna kitu
kinachomfanya Dr Olivia atamke
vile.Hakutaka tena kuendelea
kumuuliza swali lolote kuhusiana
na maisha binafsi.Baada ya kimya
cha muda Dr Olivia akauliza.
“Edger umeniuliza mimi
kuhusu familia,toka tumefika hapa
sijasikia hata siku moja hata salamu
toka kwa mkeo au familia zaidi ya wazazi wako? Ina maana huna mke
na watoto?Ndugu zako wako wapi?
Edger akatabasamu,akatamani
kucheka lakini hakuwa bado na
nguvu za kufanya hivyo.
“Dr Olivia mimi ni kama
wewe.Sina mke wala mtoto”
Olivia akacheka kidogo na kuuliza.
“Mtu maarufu kama wewe
huna mke wala mtoto?akauliza Dr
Olivia
“Kweli Dr Olivia.Siku zote
sipendi kusema uongo.Ukweli ni
kwamba nilikuwa na rafiki yangu
wa kike ambaye nilipendana naye
mno na niliamini yeye ndiye
angekuwa mke wangu kwa siku za
mbele,lakini kitu alichonifanyia,ikanibidi nijiulize
mara mbili kuhusu kuingia katika
mahusiano kwa mara nyingine
tena”
Dr Olivia akamkazia macho
Edger na kuuliza.
“Alikufanyia kitu gani huyo
rafiki yako kiasi cha kukufanya
usitake tena kuingia katika
mahusiano?
Edger akafikiri kwa muda
halafu akasema.
“Kwa kuwa ni muda sasa
umeshapita sioni sababu ya
kutokwambia.Kwa ufupi ni
kwamba dada yule hakuwa
mwaminifu katika uhusiano
wetu.Wakati akiniambia kuwa ananipenda na yuko tayari kuwa na
mimi katika shida na raha,alikuwa
na uhusiano wa kimapenzi na
kigogo mmoja serikalini.Nilipokuja
kugundua hilo nilihuzunika
mno.Kitu cha ajabu ni kwamba
baada tu ya mimi kugundua uchafu
huo aliokuwa akiufanya na kuamua
kuachana naye,kigogo huyo naye
aliachana naye.Nilikuja kugundua
baadae kuwa hii ilikuwa ni moja ya
njama za vigogo
kuniumiza.Nadhani walifanikiwa
kwa sababu ni wazi niliumia
mno.Toka wakati huo nikaamua
kujiweka mbali kabisa na masuala
ya mahusiano hadi hapo moyo wangu utakapopona na kuamua
kupenda tena”
Dr Olivia akamtazama Edger
kwa sekunde kadhaa halafu
akasema.
“Pole sana Edger kwa
yaliyokukuta.Mapenzi ndivyo
yalivyo.Baada ya kugundua kuwa
ulikuwa ni mpango wa vigogo
kukufanyia vile,unafikiria nini
kumsamehe huyo dada? Kwa
sababu alikuwa anatumika tu
kukuumiza”akasema Dr Olivia
“Hapana Dr Olivia sintaweza
kufanya hivyo kwa sasa kwa
sababu nilikwisha mtoa kabisa
moyoni mwangu.Ingawa ameomba
msamaha mara nyingi na kutaka turudiane lakini moyo wangu
hauko tayari kumpokea tena kama
mpenzi wangu ataendelea kuwa
rafiki yangu na sehemu ya historia
yangu”
Wote wakakaa kimya halafu Dr
Olivia akasema
“Edger inaonekana kazi hii ya
siasa inakufanya uwe na maadui
wengi”
Edger akatabasamu na kujibu
“Dr Olivia kazi ya siasa kweli ni
ngumu hasa pale unapofanya kazi
zako za siasa kwa maslahi ya
taifa.Unajua watu wengi
wamejiingiza katika siasa hivi sasa
kwa maslahi yao binafsi.Watu
kama hawa wamejenga mitandao mikubwa ya kutafuna rasilimali za
nchi na kujifaidisha wao na familia
zao.Ukitaka kupambana nao
unakuwa adui yao mkubwa,na
kupambana na watu kama hawa
kwa maslahi ya wanyonge walio
wengi inakubidi uwe na moyo
mgumu sana kwa sababu watu
hawa hawasiti kukutoa roho kwa
kuogopa kuwekwa wazi”
Huku akiwa na sura yenye
kuonesha huzuni na wasi wasi Dr
Olivia akasema
“Kwa nini susiachane na
mambo hayo ya siasa kama hali
yenyewe iko hivyo?
“Siwezi kuacha siasa Dr
Olivia.Nina deni la kuwatetea watanzania wanyonge ambao haki
yao inadhulumiwa na wajanja
wachache.Niko tayari kuutoa uhai
wangu kwa ajili ya kuwatetea
masikini hawa.Napata uchungu
moyoni nionapo kigogo anajenga
nyumba ya millioni mia mbili
wakati kuna watu wengi hawana
nyumba za kuishi.Dr Olivia siwezi
kuacha siasa.Nitapambana hadi
mwisho”
“Maneno yako Edger
yamenichoma hata mimi.Umasikini
walio nao watu wetu ndio
unaonipelekea hata mimi kufanya
kazi usiku na mchana ili
kuwasaidia.Ukiangalia gharama za
matibabu ya moyo ziko juu mno kiasi kwamba si watanzania wote
wenye uwezo wa kumudu gharama
hizi.Umasikini wa mtu si sababu ya
kumfanya akose tiba.Najitahidi kwa
kadiri niwezavyo kuokoa maisha ya
kila mgonjwa anayekuja kutibiwa
katika hospitali yetu.Watu hawa
wasiokuwa na huruma kwa
wananchi masikini wamenipa
hasira mno.Niko tayari kuungana
nawe Edger ili kupambana na watu
hawa na kuwasaidia walio wengi.”
Edger akatabasamu
akamtazama Dr Olivia usoni halafu
akasema
“Dr Olivia nafurahi kusikia
kuwa uko tayari kupambana na
hatimaye kuwasaida wanyonge wengi.Pamoja na moyo huo wa
kizalendo lakini nakusihi usijiingize
katika masuala ya siasa.Ukiingia
huko utahatarisha maisha yako”
“Edger ninawachukia mno
mafisadi hawa wanaolirudisha
nyuma taifa letu na kusababisha
umasikini kwa watanzania.
Nakubaliana na wewe kuwa watu
hawa ni hatari na wana nguvu ya
kufanya lolote walitakalo.Ugonjwa
wako umenifundisha mengi.Edger
umeponea tundu la
sindano.Ulipaswa ufe lakini
niliamua kupambana kufa na
kupona mpaka leo hii uko hapa na
unaendelea vizuri.Kama
nisingekuwa na moyo mgumu wa kijasiri,ni wazi hivi sasa ungekuwa
marehemu.Kitendo hiki peke yake
tayari kimenifanya niingie katika
mapambano ya kisiasa kwa sababu
tayari nimeshakuwa na
maadui”akasema Dr Olivia
Edger akastuka kwa maneno
yale ya Dr Olivia,akajiweka vizuri
kitini na kuuliza.
“Dr Olivia umenistua kwa kauli
yako kwamba nilipaswa nife
nimeponea tundu la sindano.Nini
hasa kilitokea? Nimekuwa
nikijiuliza maswali mengi kila siku
juu ya ugonjwa wangu. I’m sure you
know something.Please tell me
Olivia” Edger akasema. Dr Olivia akamtazama usoni
huku akijishauri kama amwambie
ukweli au asimwambie chochote
“Edger natamani sana
kukueleza kilichotokea lakini
ninashindwa nianzie wapi kwani ni
mambo ya ajabu sana yaliyotokea
lakini nitakueleza bila kukuficha”
akasema Dr Olivia “Nieleze
tafadhali nini kilitokea Dr Olivia?
Edger akasema
Dr Olivia akamtazama Edger
kwa sekunde kadhaa halafu
akasema
“Tulipata taarifa toka ofisi za
bunge kuwa unaletwa katika
hospitali yetu kutokea Dodoma na
ulipoletwa tukaanza kukushughulikia mara moja.tatizo
kubwa lilikuwa shinikizo la
damu.Tulijaribu kadiri tuwezavyo
lakini hali yako ilikuwa inabadilika
badilika kila wakati.Mimi na
madaktari wenzangu tulishindwa
kuelewa ninihasa kilichokuwa
kinakusumbua na kusababisha hali
yako kubadilika namna ile ndipo
tulipofanya maamuzi kwamba
upelekwe nje ya nchi.Nilimuita
mama spika na kuongea
naye.Nikamueleza ukweli kuwa
unatakiwa uhamishiwe nje ya nchi
haraka iwezekanavyo.Nilifahamu
wewe ni mbunge na suala la
kupelekwa nje ya nchi lingepewa
uzito mkubwa lakini zilitokea sarakasi ambazo nashindwa hata
kuzielezea”
“Niambie kila kitu Dr Olivia”
akasema Edger
“Badala ya pendekezo la
kusafirishwa nje ya nchi kufanyiwa
kazi,iliamriwa kwamba uhamishwe
kutoka katika hospitali kuu ya
moyo na upelekwe katika hospitali
ya muhimbili kwa madai kwamba
ugonjwa unaoumwa unaweza
ukatibiwa pale pale nchini.Nilistuka
sana nilipopata taarifa
zile.Sikuelewa nini dhana ya
kufanya vile.Edger mimi ni daktari
na siku zote hakuna kitu
ninachokiogopa kama mgonjwa
ninayemtibu kufa kwa uzembe.Sikutaka hilo litokee
,ikanilazimu kuongea na baba
yangu nikamuomba azungumze na
rais amuombe msaada kwani wao
ni marafiki wakubwa
sana.Nashukuru rais alimuelewa
baba na akatoa ndege yake ambayo
ndiyo iliyokuleta huku.Bila yeye
hivi sasa ungekwisha kufa”akasema
Dr Olivia akatulia kidogo,akavuta
pumzi ,halafu akaendelea.
“Nawashukuru madaktari na
uongozi wa hospitali hii kwa jinsi
walivyolishughulika na ugonjwa
wako.Muda mfupi baada ya kuanza
kutibiwa wakapata majibu ya
vipimo vyao nikaitwa na kuambiwa
kilichokutokea.” “Nini kilinitokea? akauliza
Edger baada ya kuona Dr Olivia
amekaa kimya ghafla
“Madaktari walithibitisha
kwamba uliwekewa sumu”
Kimya kikatanda na baada ya
dakika mbili Dr Olivia akasema
“Kwa mujibu wa madaktari
sumu hiyo iliingia mwili kupitia
ngozi.wanahisi aidha ulipuliziwa au
uliogea sabuni iliyopakwa sumu
hiyo.Ni moja kati ya sumu hatari na
yenye kuua kwa muda wa masaa
machache.Hii ni sumu inayotumika
katika mauaji ya kimya
kimya.Niliogopa sana nilipopewa
taarifa hiyo.Nikajaribu kuunganisha
taarifa hii na matukio yaliotokea Dar es salaam nikagundua huu
ulikuwa mpango kabambe wa
kukuua.Dana dana zilizokuwa
zikipigwa zilikuwa na lengo la
kuvuta muda ili uweze kufariki
kabla ya kufika asubuhi.Baada ya
taarifa hiyo,niliomba uongozi wa
hospitali uimarishe ulinzi katika
chumba chako na asiruhusiwe mtu
yeyote kuingia chumbani kwako
bila ruhusa yangu.Nashukuru hilo
limefanyika na hakuna mtu yeyote
anayeruhusiwa kukuona bila
kupitia kwangu.Kwa ufupi hiyo
ndiyo taarifa ambayo sikutaka
kukwambia mapema nikisubiri
hadi hapo utakapokuwa na nguvu
za kutosha.” Dr Olivia akakaa kimya.Edger
akamtazama kwa dakika kama
mbili hivi halafu akatabasamu na
kusema kwa sauti ndogo
“Hii ndiyo siasa”
Dr Olivia hakujibu kitu
akaendelea kumtazama Edger
“Olivia ahsante sana kwa
kuyaokoa maisha yangu lakini
sishangazwi na jaribio hili la kutaka
kuniua lakini Mungu yuko upande
wangu.Sijui hata nianzie wapi
kukushukuru Dr Olivia kwa sababu
bila wewe leo hii tayari
ningekwisha zikwa na kusahaulika”
Edger akasema huku machozi
yakimtoka.
 
SIRI

episode 12

mtunzi. Patrick CK

“Edger please don’t cry,be
strong”Akasema Dr Olivia
“Nimeshindwa kujizuia
Olivia.Inaniuma mno.Nakumbuka
siku ile nilipopatwa na tatizo hili
nilikuwa niwasilishe muswada
binafsi kuliomba bunge liunde
kamati teule kuchunguza kufilisika
kwa benki ya taifa ya
vijana.Nakumbuka asubuhi ile
niliamka mzima na mwenye afya na
sikuwa na tatizo lolote
lile.Nakumbuka wakati kipindi cha
maswali na majibu kinakaribia
kumalizika nilianza kuona macho
mazito nikahisi kusinzia.Ghafla
nikaanza kuona giza,nguvu
zikapotea na sikujua tena nini kilitokea hadi nilipokuja kupata
fahamu na kujikuta hapa hospitali
Israel”
Edger akatulia akameza mate
na kusema
“Katika utafiti wangu
niligundua kuwa kuna baadhi ya
vigogo serikalini wakishirikiana na
baadhi ya wafanya biashara
wakubwa walichota matrilioni ya
fedha katika benki ya taifa ya vijana
na kuifanya ifilisike.Nilijitahidi
kujiridhisha vya kutosha na
ushahidi nilioupata na ndipo
nilipomuandikia spika nikimuomba
kuwasilisha muswaada binafsi ili
niliombe bunge liunde kamati teule
ichunguze jambo hilo.Jambo hili si dogo na wahusika wake si watu
wadogo pia ndio maana nilitaka
kulishirikisha bunge kama mhimili
ili baada ya kuchunguza na kupata
ukweli basi serikali ichukue hatua
stahili.Nafikiri watu hawa walipata
taarifa kuwa nimekusudia
kulipeleka bungeni suala hili na
ndiyo maana wakajipanga na
kuniua.Mpango huu ulipangwa
kitaalamu mno na ndiyo maana
hata ulipotoa pendekezo la
kunisafirisha nje ya nchi kwa
matibabu lilipangwa vikali.Lengo
lilikuwa moja tu ,mimi nife” Edger
akatulia ,akainamisha kichwa chini
na kufikiri kwa sekunde chache
halafu akainua kichwa na kusema “Wanataka kuniua kwa sababu
ya kupigania masikini walio wengi
!! Is that fair? Edger akauliza kwa
hisia kali.
“Ni bora wangefanikiwa katika
mpango wao huu,lakini kwa kuwa
wameshindwa kufanikiwa
kuniua,inafuata zamu
yao.Nitawaandama usiku na
mchana,sintawapa nafasi ya
kupumua!! Edger akasema huku
akigonganisha mikono yake kwa
hasira.
“Edger tafadhali achana na
mawazo hayo kwa sasa.Kikubwa
kwa sasa ni kujitahidi upone kabisa
halafu ndipo utafikiria nini cha
kufanya.Nadhani suala pekee ni kuhakikisha watu hao
wanafikishwa mbele ya sheria”
“Nashukuru sana Dr Olivia kwa
kutambua thamani yangu na
kunijali,lakini kwa hili sintakuwa
na muda wa kupumzika.Watu hawa
wana nguvu,wana uwezo wa
kusimama hata juu ya sheria.They
are powerfull Dr Olivia ndiyo
maana nilitaka suala hili likaanzie
bungeni ili lipate nguvu kubwa ya
mhimili” akasema Edger
Dr Olivia hakujibu kitu akaendelea
kumuangalia Edger kwa macho ya
huruma
“Pamoja na nguvu na uwezo
walio nao sintawaogopa hata
kidogo.Nitapambana nao kwa maslahi ya Taifa.Nitapambana kwa
maslahi ya vijana wale
wanaosumbuka kwa kukosa mitaji
iliyochotwa na mafisadi
hawa.”akasema Edger
“Edger,kama una mipango ya
kuendelea kupambana na hao watu
itakulazimu upate uungwaji mkono
kutok akwa baadhi ya viongozi
waadilifu ndani ya serikali ili uwe
na nguvu vinginevyo hutafika
kokote.Rais Dr Evans ni rafiki
mkubwa wa baba ninaweza
kuzungumza naye ukamueleza
kuhusu suala hili na akakusaidia
kwani yeye ana nguvu kubwa”
akasema Dr Olivia “Hapana Dr Olivia usimweleze
kitu chochote mtu yeyote yule.This
must remain between us” Edger
akasema
“Tayari nimekwisha mueleza
spika wa bunge na baba
yangu.Those are two people I trust”
Edger akashika kichwa
akafikiri na kusema
“You did a mistake Dr
Olivia.No body should be trusted
these days”
“But I trust my own father
Edger”akasema Dr Olivia
Kimya kikapita tena hakuna
aliyeongea kwa muda wa sekunde
kadhaa.Dr Olivia akasema “Edger ,usipowashirikisha
watu kama hawa ambao wana
nguvu na msaada mambo
yanaweza kuwa magumu sana
kwako”
“Olivia si kwamba sitaki
kushirikisha mtu ,ukweli ni
kwamba watu hawa wana mtandao
mpana sana na huwezi kujua yupi
yumo na yupi
hayumo.Nitashirikiana na watu
lakini wale tu
ninaowaamini”akasema Edger
“Mimi nitakuwa wa kwanza
kushirikiana nawe” akasema Dr
Olivia
Edger akatabasamu akamshika
mkono Dr Olivia “Dr Olivia I trust you very
much ,but I don’t think it’s a good
Idea to involve you in this.Its too
dangerous”
“Edger kama ni kwa maslahi ya
taifa na watanzania masikini
sintaogopa chochote”
Edger akatabasamu huku
akiwa ameushika mkono wa Dr
Olivia
“Okay you are in”
Huku akitabasamu Dr Olivia
akasema
“Nini sasa tutafanya baada ya
kuujua ukweli.Tutawaanika vipi
watu hawa kwa jamii ya
watanzania iwafahamu? Edger akafikiri kwa dakika
moja,akainua kichwa na kusema
“Kuna kitu kimoja ambacho
sikuwa nimekifikiria hapo
kabla,lakini baada ya kunipa ukweli
wote nimefanya maamuzi”
“Ni kitu gani hicho Edger” Dr
Olivia akauliza kwa shauku
“Sintakwambia kwa
sasa.Naomba nitafakari kwa kina
hiki ninachotaka kukifanya halafu
nitakujulisha”akasema Edger
Dr Olivia akamtazama Edger
kwa uso wa kuonyesha
kutoridhishwa na jibu lile la Edger .
“Olivia nahitaji unitafutie
kompyuta mpakato
iliyounganishwa na mtandao wa Intaneti.Kuna watu nahitaji
kuwasiliana nao usiku wa
leo.Unaweza kunisaidia kwa hilo?
“Ndiyo Edger hakuna
tatizo,nitaongea na uongozi wa
hospitali ili watafute kompyuta
hiyo unayoihitaji”
“Nashukuru sana Dr Olivia”
Edger akasema na kukaa kimya huu
akiendelea kumtazama Olivia.
******************
Saa sita za mchana kwa saa za
Israel,Dickson Kipuma mlinzi wa
siri wa waziri mkuu aliyetumwa
kufanya kazi ya kumlinda
mheshimiwa mbunge Edger Kaka,aliwasili Rambam medical
center,akiwa ameongozana na
mwenyeji wake jasusi toka shirika
la ujasusi Israel aitwaye Yair huku
akionekana ni mgonjwa sana.Dick
ambaye aliingia nchini Israel
akijulikana kama Christopher
Nkosizwe raia wa
Zimbabwe,alipokelewa na
kupelekwa moja kwa moja katika
chumba maalum alichokuwa
ameandaliwa.Tayari Yair alikwisha
fanya mipango yote na uongozi wa
hospitali ile ulifahamu nini sababu
ya Dick kuwapo pale hospitalini.
“Nadhani kwa sasa unaweza
ukapumzika.Kwa kuwa kila kitu
kimekwenda kama tulivyokuwa tumepanga endelea kupumzika
kwa uchovu wa safari.Mimi
naelekea Tel aviv kuna kazi
natakiwa kuifanya kule Baada ya
siku mbili nitarudi.”Akasema
Yair,akatoka na kumuacha Dick
mle chumbani.Dick akafungua
dirisha na kuifurahia mandhari ya
kuvutia ya mji wa Haifa.Chumba
alichopangiwa kulala kilikuwa
karibu na chumba alimolazwa
Edger.
Wakati akiwa katika tafakari
mlango unafunguliwa na akaingia
muuguzi akiwa na sinia la
dawa.Muuguzi yule akajitambulisha
kwa Dick kuwa anaitwa
Salome.Alikuwa ni mama wa makamo.Salome akampatia Dick
dawa za kumeza na kumuomba
apumzike hadi hapo baadae
atakapokuja daktari kumtembelea.
“Salome samahani,hivi hapa
katika hospitali yenu mgonjwa toka
afrika ni mimi peke yangu? Dick
akauliza kabla muuguzi Salome
hajatoka mle chumbani
“Hapana hauko peke
yako.Kuna mgonjwa mwingine
naye ametoka Tanzania kwa hiyo
wagonjwa toka afrika mko wawili
tu hapa hospitalini kwetu” Salome
akajibu.
“Nashukuru kwa kulifahamu
hilo.Ningefurahi sana kama
ningeweza kufahamiana na mwafrika mwenzangu kwa sababu
najiona mpweke sana
hapa”akasema Dickson
“Usijali Christopher,utaonana
naye tu kwa sababu hali yake kwa
sasa ni nzuri na anaweza hata
kutembea.Kwa hivi sasa yuko
bustanini akipumzika.Kama
unahitaji kuonana naye kwa sasa
nikupeleke”
“Hapana Salome kwa sasa
nahitaji kupumzika ,nadhani
nitaonana naye baadae”
Muuguzi yule akatoka bila
kufahamu kuwa Dick ambaye kwa
sasa alijulikana kama Christopher
hakuwa mgonjwa. ***************
Saa nne za usiku saa za
Israel,mlio ulisikika toka katika
kompyuta ya Judy.Kwa haraka
akakurupuka toka kitandani
akaenda kutazama.Mitambo yake
ilikuwa imenasa kitu toka katika
chumba cha Edger.Mlio ule ulikuwa
ni ishara kuwa Edger alikuwa
akitaka kuwasiliana na mtu kwa
njia ya simu.Mchana wa siku hiyo
Edger alimuomba Dr Olivia
amtafutie kompyuta
iliyounganishwa na mtandao wa
Intanet.Vifaa vile alivyovitega Judy
katika chumba cha Edger vilikuwa
na nguvu ya kunasa kila aina ya mawasiliano ya kielektroniki
yanayofanywa toka ndani ya
chumba kile.
“Hallow Sayid” Akasema Edger
akizungumza na mtu kupitia
mtandao wa skype wakizungumza
kwa lugha ya kiingereza
“Edger,Nafurahi sana kuisikia
sauti yako.Sikuamini uliponitumia
ujumbe kuwa utazungumza nami
muda huu.Nilihisi labda ni mtu
mwingine anajifanya ni wewe
lakini baada ya kukuona sasa roho
yangu imetulia.Vipi maendeleo
yako? Akauliza mtu yule aliyekuwa
anazungumza na Edger
“Namshukuru Mungu kwa sasa
hali yangu inaendelea vizuri sana.Sina mawasiliano ya simu
hapa ndiyo maana nikaamua
nikupigie kwa kutumia simu ya
intanet.” Akasema Edger
“Ashukuriwe Mungu
sana.Nilistuka mno baada ya
kupata taarifa za
kilichokutokea”akasema Sayid
“Nawashukuru pia Sayid kwa
dua na sala zenu” Edger akasema
“Edger nini hasa kilitokea?
Akauliza Sayid na Edger
akamueleza kila kitu kilichotokea
kuhusiana na ugonjwa wake.Sayid
akasema
“Edger nadhani wakati
umefika na hakuna muda wa
kusubiri zaidi.Ni wakati sasa wa kugombea urais katika uchaguzi
mkuu ujao.Tumetumia muda mrefu
kukujenga na kutengeneza jina lako
na tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa
sana na sasa muda umefika wa
wewe kutwaa nchi” akasema Sayid
na ukimya ukatawala
“Sayid nafahamu hilo ndilo
hasa lengo letu lakini nadhani
muda wangu wa kuwa rais bado
haujafika.NInataka niendelee
kujijenga zaidi kisiasa na
kuifahamu vyema nchi.Nataka niwe
na uzoefu mkubwa wa uongozi
kabla ya kufikiria kuingia katika
nafasi hiyo kubwa zaidi”
“Edger hatuna tena muda wa
kusubiri.Watu hawa watakuandama usiku na mchana na
hawasita hata kukuua hadharani na
juhudi zote tulizofanya za
kukujenga zitakuwa bure.Njia
tayari imekwisha
safishwa,wananchi wanakuamini
na una mtaji mkubwa wa wafuasi
hivyo itakuwa rahisi kwako
kuchukua nchi katika uchaguzi
mkuu ujao.Usipochukua nchi katika
wakati huu hautachukua muda
mrefu utauawa.Edger sema ndiyo
na mimi nitafanya kila kitu na
kuhakikisha unakuwa rais wa
Tanzania.Lengo la kukufadhili
katika harakati zako za siasa ni
kuhakikisha kwamba siku moja
unafikia nafasi ile kubwa kabisa ya kisiasa yaani kuwa rais wa
Tanzania na muda wa kuifikia
nafasi hiyo ni huu
umewadia.Sitegemei jibu la hapana
katika suala hili.Usihofu kuhusu
gharama kila kitu kitakuwa juu
yangu” akasema Sayid
Edger akafikiri kwa muda
halafu akasema
“Sayid naomba unipe muda
kidogo wa kulitafakari hili suala
halafu nitakupa majibu”
“Hakuna tatizo katika suala
hilo Edger.Unao muda mwingi wa
kutafakari lakini nategemea jibu
zuri kutoka kwako.Jambo lingine
nitaandaa walinzi ambao
watakulinda ukiwa hapo hospitali na hadi utakapotoka hospitali.Hawa
waliotaka kukuua wataendelea na
njama zao hadi mipango yao
itakapofanikiwa”akasema
Sayid.Walizungumza mambo mengi
na Edger na baada ya takribani
dakika arobaini za mazungumzo
yao wakaagana.
Mara tu baada ya Edger na
Sayid kukata simu,Judy akawapigia
simu watu wake Tanzania,simu
ilipokelewa na Paul
“Judy mambo yanakwendaje
huko?Tumekuwa tunaisubiri kwa
hamu kubwa sana simu yako”
akasema Paul
“Paul tayari kuna jambo
nimelinasa.Kwa kutumia mtandao wa Skype Edger ametoka
kuwasiliana na mtu anaitwa Sayid
Omar ambaye nilipomchunguza
kumfahamu ni nani nikagundua ni
tajiri mkubwa sana anaishi nchini
Saudi Arabia na anamiliki visima
vya mafuta katika nchi kadhaa za
kiarabu.Kikubwa kuhusu Sayid
nikwamba ni mmoja wa watu
wanaotajwa kufadhili kikundi cha
kigaidi cha IS.Kwa mazungumzo
yao inaonekana Edger amekuwa
akipokea ufadhili mkubwa kutoka
kwa Sayid Omar na lengo kubwa ni
kumuandaa awe rais wa
Tanzania.Nitakubaliana na hilo
kwani Edger amekuwa ni mbunge
asiyeogopa kitu, kumbe kuna watu nyuma yake wanaompa ujasiri huo
mkubwa.NItawatumia
mazungumzo yao muyasikie”
akasema Judy
“Nimekosa neno la kusema
lakini good job Judy.Jambo hili
ulilolipata ni kubwa sana.Umekuwa
ni mwanzo mzuri sana na nina
imani tutapata mambo mengi zaidi
yaliyojificha kuhusiana na huyu
mbunge ambaye anajipambanua
kuwa ni mpigania wanyonge
kumbe nyuma ya pazia ana siri
kubwa.Good job Judy” akasema
Paul.
MPENZI MSOMAJI USIKOSE
SEHEMU YA PILI YA SIMULIZI HII.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom