Riwaya: Siri

HaMachiach

JF-Expert Member
Dec 15, 2015
3,394
6,073
Mtunzi.Patrick CK

Season 1.SIRI

Simu.0764294499

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kushuka.

Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa na abiria wakaanza kushuka. Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka”

Ndege ya shirika la ndege la Tanzania ilitua katika uwanja wa ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam ikitokea nchini jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.Ndege ilisimama mlango ukafunguliwa naabiria wakaanza kushuka.

.Mtu mmoja ambaye mavazi yake yalionyesha ni mfanyakazi wa kampuni moja ya upakiaji na upakuzi wa mizigo ndegeni alikuwa amejibanza mahala Fulani akiwa ameyaelekeza macho yake katika ndege ile akatoa simu na kupiga “Mlango umefunguliwa na abiria wameanza kushuka” “Sijakosea ni mwenyewe” akawaza na kupiga simu “Ameshuka ndegeni.

Amevaa suruali ya jeans ya bluu, fulana nyeupe,miwani myeusi ya jua” akasema yule jamaa “Una hakika ni yeye?akauliza jamaa wa upande wa pili wa simu “Ninamuona kwa mbali lakini nina uhakika ni yeye” “C’mon Denis.Get closer to her and confirm it’s her !!

Akasema kwa ukali jamaa aliyekuwa anazungumza na Denis simuni.Haraka haraka Denis akaanza kusogea kuwafuata abiria waliokuwa wanashuka lengo likiwa ni kumkaribia mrembo yule.

Hakuna aliyemtilia shaka kwani alikuwa ni mfanyakazi wa mle uwanjani.Alijitahidi sana na kumsogelea mrembo yule ambayealikuwa amevaa spika za masikioni na hakuonekana kuwa na wasi wasi wowote. “Confirmed.Ni yeye” Denisakatoa taarifa

“Good job Denis.Malipo yako yatakuja baadae” akasema yule jamaa upande wa pili wa simu na kukata simu. Msichana yule mrembo aliingia ndani ya jengo la uwanja na kukamilisha taratibu zote halafu akatoka akiwa na mkoba mweupe na sanduku dogo la chuma alilokuwa analikokota.Katika sehemu ya kusubiria wageni watu watatu walikuwa
wanamsubiri.

Wote walikuwa wamevaa suti nzuri zilizowapendeza,wakasalimiana kisha mmoja wao akalibeba sanduku la yule mrembo wakaelekea garini. “Anaelekea garini,yuko na walinzi wake” jamaa mmoja aliyekuwa katika sehemu ya kupokelea wageni akawasiliana na wenzake

“Wako walinzi wangapi?akaulizwa “Ana walinzi watatu”akajibu "Good.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa” akasema jamaa aliyeonekana ndiye mkubwa wa wale jamaa waliokuwa wakimfuatilia yule mrembo Msichana yule mrembo akaelekea katika gari moja zuri jeusi aina ya Landcruiser V8 akafunguliwa mlango akaingia pamoja na mlinzi mmoja.

Wengine wawili wakaingia katika gari la nyuma yake kisha wakaondoka pale uwanjani. “She’s on move” Jamaa
mwingine aliyekuwa katika gari lililokuwa pale uwanjani akatoa taarifa kisha akawasha gari wakaondoka wakaanza kulifu lile gari alilopanda yule msichana.Jamaa walikuwa wamejipnga kwa kuweka watu katika barabara kadhaa kwa ajili ya kumfuatilia yule msichana lengo kwa kupokezana ili asiweze kugundua kama anafuatiliwa.

Walitumia magari tofauti tofauti ili wasigundulike Gari la yule msichana liliingia barabara ya Msanda ambayo inaelekea pembezoni mwa jiji “Ameingia barabara ya Msanda nadhani anaelekea nyumbani kwake” akasema jamaa aliyekuwa katika gari lililoshika zamu ya kumfuatilia.Wale jamaa walikuwa sahihi kwani msichana yule alikuwa anaeleka nyumbani kwake katika makazi mapya ya Urangi.

Ni eneo tulivu nje kidogo ya jiji ambalo limejengwa majumba ya kifahari sana. Barabara ilikuwa na magari
machache hivyo mwendo wa gari ulikuwa mkali.Gari zile mbili za yule msichana ziliacha barabara kuu na kufuata barabara ya changarawe lakini iliyojengwa vizuri sana, gari zile ambazo zilikuwa zinamfuatilia hazikumfuata tena bali zikaegesha pembeni ya barabara kusubiri maelekezo Mita kama mia tano kabla ya kulifikia jumba lake ikatokea helkopta yenye rangi nyeupe ambayo ilikuwa inapita chini sana.

Helkopta ile ilipofika usawa wa nyumba ya yule mrembo ikageukia barabarani ambako magari mawili ambalo moja wapo amepanda yule msichana yalikuwa yamepunguza mwendo kwani yalikaribia kufika katika jumba kubwa la yule msichana.Kitendo cha helkopta ile kupita chini sana na vile vile kusimama katika jumba lile kiliwashangaza walinzi wa yule mrembo.

“Something is not right.Olivia get down!! Akasema mlinzi aliyekuwa garini na yule msichana kisha akatoa bastora yake.Mlango wa helkopta ukafunguliwa na jamaa mmoja aliyekuwa na bunduki kubwa akajitokeza na kwa kasi ya aina yake akaanza kumimina risasi kuelekea katika yale magari ambayo yalibakiza mita chache sana kufika nyumbani na tayari geti lilikwisha funguliwa.

Dereva wa gari la mbele alilopanda yule msichana mrembo akapigwa risasi ya kichwa na gari lile likapoteza uelekeo na kwenda kugonga ukuta.Mvua ya risasi ikaendelea kunyeshea gari lililokuwa nyuma ambalo lilikwenda kuligonga kwa nyuma gari la mbele alimokuwa amepanda yule msichana mrembo aliyekuwa amelala chini ya kiti.Watu wote waliokuwa katika gari lile la nyuma walikuwa wameuawa na ile mvua ya risasi toka kwa mtu aliyekuwa katika mlango wa helkopta.

Mlinzi mmoja tu aliyebaki alifungua mlango na kutaka kutoka nje ili kukabiliana na watu wale katika helkopta lakini hakufanya chochote kwani alijikuta akichakazwa kwa risasi akaanguka na kufa pale pale. Kwa kasi kubwa zikafika gari mbili ,wakashuka watu sita,waliokuwa na silaha wakiwa wamefunika nyuso zao na kujihami kwa fulana za kujikinga kwa risasi.

Haraka haraka wakaenda katika gari na kumtoa msichana yule mrembo wakamuingiza katika gari lao,likachukuliwa pia sanduku lake pamoja na mkoba mdogo aliokuwa nao kisha magari yale mawili yakaondoka kwa kasi kubwa.Helkopta nayo ambayo bado ilikuwa pale juu ikapaa na kutoweka.

“We have giraffe..I repeat we have giraffe” jamaa mmoja aliyekuwa katika gari moja kati ya zile mbili akawajulisha wenzake “Good job.Kila kitu kiende kama kilivyopangwa” akatoa maelekezo“Sawa mkuu”akajibu yule jamaa. Gari zile zilikwenda kwa mwendo wa kasi na baada ya kufika katika mzunguko wa picha ya kiboko,zikaachana kila moja ikafuata njia yake.

Moja ikafuata barabara ya umoja wa Afrika na nyingine ikafuata barabara ya Kannani.Gari zote mbili zilikuwa na namba zinazofanana ili kuwachanganya wale watakaozifuatilia.Gari ile iliyopita barabara ya Kannani ndiyo ambayo msichana yule mrembo alikuwemo,ilielekea moja kwa moja hadi katika nyuma moja maeneo ya vigenge likafunguliwa geti likaingia ndani.

Haraka haraka msichana yule akashushwa garini akafungwa mikono na miguu akaingizwa katika buti ya gari lingine aina ya mercedece benzi na gari lile likatoka bila kupoteza muda.Lile gari lingine lililokuwa limembeba mwanzo likafunguliwa namba zile za bandia na kufungwa namba zake halisi kisha nalo likatoka.

Gari lile aina ya Mercedece Benz lililokuwa na watu watatu ndani yake,lilikwenda hadi katika jumba moja kubwa likafunguliwa geti na kuingia ndani hadi gereji.Wale jamaa wakashuka garini,buti likafunguliwa yule msichana mrembo akashushwa akaingizwa ndani ya lile jumba akapelekwa katika chumba kimoja akawekwa kitandani.Bado mikono na miguu ilikuwa imefungwa pia usoni alikuwa amefungwa kitambaa hakuweza kuona chochote na mdomoni aliwekewa kitu cha kumzuia kupiga kelele.

Mlango ukafungwa wale jamaa wakatoka. Dakika chache baadae gari mbili zikawasili na kutoka katika gari la nyuma akashuka jamaa mmoja mnene. “Mr Kaiza kazi imemalizika na Dr Olivia yuko ndani tayari”akasema mmoja wa wale jamaa waliofanikisha kumteka Olivia “Kazi nzuri sana Godson” akasema Kaiza

“Huu hapa mkoba wake ndani yake kuna mkufu,simu na vifaa vidogo vidogo” akasema Godson na kumkabidhi Kaiza vile vifaa
******************

Taarifa za tukio la kutekwa kwa Dr Olivia Themba mtoto wa bilionea Agrey Themba zilianza kusambaa kwa kasiya upepo kwani ni mtu ambaye anafahamika sana.Kwanza ni kutokana na shughuli anayoifanya ya udaktari na utafiti wa magonjwa mbali mbali na vile vile kuwa mtoto wa bilionea Agrey Themba. Dr Olivia Themba ni mtoto wa tatu kuzaliwa kati ya watoto watano wa mabilionea Agrey na Lucy Themba.

Baada ya kuhitimu masomo yake ya udaktari alirejea nchini na kufanya kazi katika hospotali kuu ya magonjwa ya moyo kabla ya kuanzisha kituo chake cha utafiti wa magonjwa mbalimbali ya binadamu na wanyama.Kupitia kituo hicho kikubwa cha utafiti katika ukanda wa Afrika mashariki na kati wamefanikiwa kupata tiba ya magonjwa mbali mbali ya wanadamu na wanyama waliyoyafanyia utafiti.

Ni kituo ambacho kimekuwa na mafanikio makubwa na hata seriali wamekuwa wakikitegemea sana
kituo hiki katika tafiti mbali mbali za magonjwa ya binadamu na wanyama. Agrey Themba alipokea taarifa za kutekwa mwanae OIivia akiwa katika kikao muhimu cha kibiashara ikamlazimu kutoka kikaoni haraka sana na kumtaka dereva amuwahishe nyumbani kwa mwanae kujua kilichotokea na kuthibitisha kama taarifa zile ni za kweli.

“Ee Mungu kama kweli mwanangu ametekwa nyara,mlinde dhidi ya mikono ya watu hao waovu ambao hatujui wana lengo gani naye” Agrey akaomba akiwa garini.Alikuwa na wasi wasi mwingi “Nani hawa ambao wamethubutu kumteka mwanangu?Wanataka nini?

Akajiuliza Agrey aliyeonekana kuchanganyikiwa huku simu zake zikiendelea kuita mfululizo lakini alihisi mikono mizito hata kupokea simu “Ninawaza sana lakini mpaka sasa bado sijapata jibu nini hasa ambacho hawa jamaa wanakitaka hadi wamteke mwanangu.Je wamemteka ili wadai malipo ya fedha? Mbona hawajapiga simu kudai chochote mpaka
sasa? Akaendelea kujiuliza Agrey.

Simu aliyoamua kuipokea ni simu ya mke wake Lucy Themba ambaye alitaka kujua kama taarifa zile ni za kweli.Agrey alimueleza kuwa yuko njiani akielekea eneo la tukio kuthibitisha kama ni kweli mwanae ametekwa nyara.Mke wake naye alipanda gari haraka haraka akaanza safari ya kuelekea nyumbani kwa mwanae.

Agrey alifika nyumbani kwa Olivia na kitu cha kwanza kilichomthibitishia kwamba taarifa zile ni za kweli ni uwepo wa magari ya polisi pamoja na askari polisi kadhaa wenye silaha wakilinda eneo lile.Eneo lote la nyumba ya Dr Olivia lilizungushiwa utepe wa njano kulifunga eneo lile na kuzuia watu wasiingie wakati polisi wakiendelea na uchunguzi wao.

Agrey alishuka garini akapokewa na kamanda wa polisi wa wilaya ambaye alikuwa ameambatana na kikosi cha askari waliofika haraka sana eneo la tukio baada tu ya kupewa taarifa za tukio lile.Kamanda Sospeter Mwarabu akamjulisha Agrey kwamba taarifa zile za kutekwa kwa mwanae ni za kweli,akampeleka kumuonyesha gari alimokuwa amepanda Dr Olivia.Miili ya walinzi wa Olivia ilitolewa na kupelekwa hospitali kuhifadhiwa.

Askari polisi walikuwa wamezagaa kila kona ya nyumba ile wengine walikuwa ndani ya nyumba wengine shambani wote wakichunguza tukio lile.Agrey alichanganyikiwa baada ya kuona namna damu ilivyotapakaa ndani ya magari. “Kamanda Mwarabu una uhakika mwanangu ni mzima?akauliza Agrey kwa wasi wasi “Kwa taarifa tulizozipata kutoka kwa mlinzi wa getini ambaye wakati tukio linatokea alikuwa amejificha mwanao alichukuliwa ndani ya gari akiwa mzima na kuingizwa katika gari la watekaji.

Inaonekana hao jamaa lengo lao lilikuwa ni kumpata Olivia ndiyo maana wakawaua walinzi wake wote lakini yeye hawakumgusa.Ni watu wataalamu sana na mpango huu waliupanga kimakini mno” akasema kamanda wa polisi aliyekuwepo eneo la tukio. “My God please help my daughter !! akasema Agrey huku macho yake yakilengwa na machozi.Muda huo huo Lucy Themba mama yake Olivia naye aliwasili eneo la tukio na kushuka garini haraka haraka huku akifuta machozi akamfuata mumewe.

“Agrey tell me it’s not true! Akasema Lucy “Calm down my love.Tum…..” Kabla Agrey hajamaliza mke wake akaangua kilio kikubwa. “Lucy nyamaza kulia.We have to be strong for our daughter” akasema Agrey na kumnyamazisha mke wake. “Agrey please find my daughter!! Fanya kila uwezalo na hakikisha unampata Olivia.Nitakufa kama Olivia hatapatikana!! Akalia Lucy

“Lucy usihofu.Nitafanya kila niwezalo kuhakikisha kwamba Olivia anapatikana.Polisi wanafanya kila wanaloweza kuhakikisha Olivia anapatikana haraka sana”akasema Agrey “Hao watekaji kama wanataka pesa wapatie kiasi chochote cha pesa wakitakacho ili mradi mwanangu awe salama” akasema Lucy kwa sauti ya chini “Ninaamini hao watekaji shida yao ni pesa hivyo lazima watapiga simu na kudai kiasi kikubwa cha fedha ili waweze kumuachia Olivcia.

Ninakuahidi Lucy kama wakipiga simu na kudai pesa nitawapa kiasi chochote wakitakacho ili wamuache huru binti yetu” akasema Agrey na kamanda wa polisi akawasogelea na kumpa pole Lucy “Kamanda kuna chochote mmekipata hadi sasa kinachoweza kupelekea kuwafahamu hao watekaji ni akina nani?akauliza Agrey

“Mpaka sasa bado ila tunaendelea na uchunguzi na kila pale tutakapopata chochote tutakuwa tunawajulisha.Kwa sasa ninawahitaji tuzungumze kidogo” akasema kamanda Mwarabu wakaelekea ndani sebuleni. “Bwana na bi Themba napenda kuwajulisha kwamba jeshi la polisi tulipokea taarifa kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa Dr Olivia aliyetujulishja kuhusu tukio lililotokea na tukafika hapa ndani ya muda mfupi sana lakini tayari watekaji walikwisha mchukua Dr Olivia na kutoweka.

Tumeambiwa kwamba watekaji walikuwa na helkopta na mtu aliyekuwa na bunduki ambaye alikuwa anarusha risasi kutokea ndani ya helkopta na baadae yakatokea magari mawili na watu wakashuka wakiwa na silaha na kumchukua Dr Olivia.Tayari tunawashikilia watumishi wote wa ndani pamoja na mlinzi aliyekuwepo getini kwa mahojiano,tunafuatilia vile vile picha za kamera za ulinzi kwani jumba hili la Dr OIivia kuna kamera nne.

Ninawahakikishia kwamba tunafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba mwanenu anapatikana haraka tena akiwa hai. Ninachoomba ni ushirikiano wenu mkubwa.Bado hatujui lengo la watekaji hawa ni nini, lakini kuna mambo mengi yanayoweza kupelekea wakamteka Dr Olivia.

Yawezekana watekaji wanahitaji fedha,yawezekana ikawa ni visasi,na yawezekana ikawa hata ni wivu wa kimapenzi. Sababu ziko nyingi na tunajaribu kuangalia sababu inayoweza kupelekea Dr Olivia akatekwa.Katika hili tunahitaji sana msaada wenu.Ninyi ni wazazi wake na mwanenu mnamfahamu vyema, nataka kufahamu kutoka kwenu kuhusu maisha yake kwa ujumla”akasema Kamanda Mwarabu Agrey akavuta pumzi ndefu na kusema

“Olivia ni mtu anayependa kuishi maisha ya kawaida sana.Hata baada ya kumaliza masomo yake ya udaktari na kuanza kazi bado tulikuwa tukiishi naye nyumbani kwetu.Ni binti wa pekee kwetu na hatukuwa tayari kumuacha akaishi peke yake lakini alituomba kwamba tayari amekwisha kuwa mtu mzima na anahitaji kuanza maisha yake mwenyewe ndipo tulipomruhusu akaja kuishi hapa katika nyumba hii.

Olivia ni mpole na sina hakika kama ana maadui wowote.Aliamua kusomea udaktari ili awasaidie watu kwani ni kitu alichokipenda toka akiwa mtoto mdogo.Amekuwa anaifanya kazi yake ya udaktari kwa moyo na upendo mkubwa ndiyo maana akawa ni mmoja wa madaktari maarufu hapa nchini”akasema Agrey “Mara ya mwisho kuwasiliana naye ilikuwa lini?akauliza kamanda “Leo asubuhi.Alitupigia simu akiwa Cogo DRC alikoenda kwa shughuli zake za udaktari na akatujulisha kwamba anarejea nchini leo mchana” akajibu Agrey “Dr Olivia yuko kwenye mahusiano? Mnamfahamu mpenzi wake?

“Mpaka sasa Olivia bado hajamuweka wazi mpenzi wake.Kila ninapomuuliza kuhusu suala la mahusiano jibu lake ni kwamba ataweka wazi mambo yote muda ukifika.Amejikita zaidi katika kazi zake ndiyo maana hajaweka wazi mpenzi wake hadi sasa”akajibu Agrey “Bwana na Bi Themba, kama hawa jamaa lengo lao la kumteka Dr Olivia ni kujipatia fedha tuna hakika watawasiliana nanyi na kudai fedha.Kama wakiwapigia simu tafadhali tuwasiliane haraka sana.

Najua wakipiga simu watawatisha msitoe taarifa kwa polisi ama watamuua mtoto wenu lakini nawaomba msiogope,wasilianeni haraka sana na jeshi la polisi na tutafanya kila juhudi za kumkomboa Olivia na kudhibiti matukio kama haya yasiendelee hapa nchini.Endapo pia mtapata taarifa zozote zinazoweza kusaidia kuwafahamu watekaji hawa msisite kutujulisha haraka sana” akasema kamanda wa polisi “Afande tutatoa ushirikiano mkubwa sana kila pale tutakapopata chochote kile kuhusiana na kutekwa kwa binti yetu.

Nakuomba vilevile muwe mnatujulisha kila hatua mnayopiga katika uchunguzi huu” akasema Agrey Themba na kamanda wa polisi akatoka kwenda kuendelea na uchunguzi wao.Agrey akamshika mkono mke wake wakatoka mle ndani hadi katika gari lake wakaondoka eneo la tukio.Bado Lucy alikuwa anaendelea kulia.

KItendo cha binti yake kutekwa nyara kilimuumiza mno.Wakiwa garini Agrey alikuwa na kazi ya kupokea simu zilizokuwa zinaingia mfululizo kutoka kwa watu mbali mbali wakiwapa pole kufuatia kitendo kile cha kutekwa binti yao Dr Olivia.Simu ya Agrey ambayo huitumia kuwasiliana na watu wake wa muhimu ikaita, alikuwa ni rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Evans mwaluba.

Agrey akamuonyesha mke wake “Rais anapiga” akasema Agrey na kupokea ile simu “Dr Evans” akasema Agrey “Agrey nimepata taarifa za tukio la kutekwa Dr Olivia nimestuka sana” akasema Dr Evans Agrey akavuta pumzi ndefu na kusema “Mheshimiwa rais ni kweli tukio hili limetokea na Olivia ametekwa.Lucy na mimi tumetoka eneo la tukio sasa hivi na hali tuliyoikuta pale ni ya kutisha.Walinzi wote wa Olivia wameuawa na yeye kutekwa nyara.

Hatujui ni nani waliomteka nyara na kwa kusudi lipi” akasema Agrey “Poleni sana Agrey.Hizi ni taarifa za kustusha mno.Matokeo kama haya ya utekaji ni mageni sana hapa nchini kwetu.Hatukuzoea mambo ya namna hii”akasema rais “Mheshimiwa rais naomba tafadhali utusaidie binti yetu apatikane na watekaji hawa wajulikane.Kama familia tumeumizwa mno na kitendo hiki” akasema Agrey

“Agrey mimi kama mtu wa karibu na familia yako nimeumizwa pia na jambo hili na ninakuahidi kwamba kwa namna yoyote ile lazima Olivia apatikane akiwa mzima wa afya. Nitatumia kila nguvu niliyonayo kuhakikisha Olivia anapatikana.Tayari nimekwisha toa maelekezo kwa mkuu wa jeshi la polisi nchini kwamba wahakikishe hadi kufika jioni ya leo Olivia awe amepatikana.Nimeelekeza nguvu kubwa iwekwe katika kuwasaka watekaji ambao tunaamini bado wako hapa hapa Dar es salaam.

Tayari njia zote za kuingia na kutoka Dar es salaam zimefungwa na msako mkali umekwisha anza.Nimeelekeza ikiwezekana ufanyike msako wa nyumba kwa nyumba hadi Olivia apatikane.Ninawatoa hofu Agrey na familia yako kwamba kama serikali tunafanya kila tuwezalo kuhakikisha kwamba Dr Olivia anapatikana.Hatuwezi kuwapa nafasi watekaji hawa ya kufanya kila watakacho katika nchi yetu hii iliyotamalaki amani” akasema Dr Evans naye akionekana kuumizwa sana na tukio lile

“Mheshimiwa rais ninakushukuru sana kwa maneno hayo ambayo yametupa faraja kubwa sana na matumaini ya kumpata mwanetu akiwa salama.Kwa niaba ya familia yangu ninasema ahsante sana” akasema Agrey “Nimeagiza kupewa ripoti kila baada ya saa moja kuhusiana na mwenendo mzima wa kuwasaka hao watekaji na kila nitakapokuwa ninapata taarifa nitakuwa ninawajulisha” akasema rais na kuagana na Agrey.

“Mheshimiwa rais naye ameguswa sana na ameahidi kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha Olivia anapatikana.Amekwisha toa maelekezo kwa jeshi la polisi kufanya kila waliwezalo kuhakikisha Olivia anapatikana” Agrey akamwambia mke wake wakiwa garini wakirejea nyumbani kwao Mara tu rais alipomaliza kuzungumza na Agrey
Themba, akazitafuta namba za Devotha Adolph mkurugenzi wa idara maalum ya siri ya usalama wa ndani wa nchi akapiga na simu ikapokelewa.

“Devotha what’s the situation? akauliza Dr Evans “Kila kitu tayari mheshimiwa rais.We have Olivia in our custody”akajibu Devotha “Good.Hakikisha kila kitu kinakwenda vyema.Sitaki tatizo lolote litokee.Hakikisheni mnatumia kila aina ya mbinu kupata taarifa kutoka kwake.Taarifa alizonazo ni muhimu sana kwetu” “Sawa mheshimiwa rais,tayari tumejipanga vyema kwa ajili ya kuhakikisha anatupa taarifa zote” akasema Devotha

SIKU NNE ZILIZOPITA

Saa kumi na mbili za jioni gari moja jeusi liliwasili katika makazi ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania jijini Dar es...
 
SIRI
episode 2
Mtunzi.Patrick CK

SIKU NNE ZILIZOPITA

Saa kumi na mbili za jioni gari
moja jeusi liliwasili katika makazi
ya rais wa jamhuri ya muungano
wa Tanzania jijini Dar essalaam.Mtu mmoja aliyevaa suti
nyeusi akashuka toka ndani ya lile
gari akapokewa na msaidizi wa rais
akamkaribisha ndani ambako
alipokewa na rais
“Mheshimiwa rais
ninashukuru sana kwa makaribisho
mazuri.Ninaitwa Peter seruseko”
akasema yule mgeni akitokea
jamhuri ya kidemokrasia ya Congo
“Karibu sana Peter.Rais wako
alinipigia simu akanieleza kwamba
atamtuma mjumbe aniletee ujumbe
wa muhumu sana ambao hakutaka
kunieleza simuni” akasema rais Dr
Evans na kumtaka yule jamaa
amfuate katika chumba cha
mazungumzo ya faragha “Karibu tena kwa mara
nyingine Peter.Ni ujumbe gani
mheshimiwa rais wa Congo
amekutuma uniletee?akauliza Dr
Evans
“Mheshimiwa rais kama
alivyokueleza rais simuni ni
kwamba kuna jambola muhimu
sana ambalo hakupaswa kukueleza
simuni” akasema Peter na
kunyamaza kidogo halafu akasema
“Mimi ninafanya kazi katika
idara ya usalama wa taifa ya Congo
DRC.Tulipokea taarifa kutoka
vyanzo vyetu kwamba mtu mmoja
anaitwa Seif Almuhsin ambaye
anatajwa kwamba amekuwa kinara
wa kutafuta vijana kutoka ukanda wa Afrika mashariki Katina kusini
kwenda kujiunga na kikundi cha
Islamic state alikuwa anaelekea
nchini Congo.Seif ana wawakilishi
katika nchi mbali mbali na
anafanya shughuli zake kwa usiri
na umakini mkubwa sana.Baada ya
kupewa taarifa hiyo tulianza
maandalizi ya kumfuatilia kujua
anachokwenda kukifanya nchini
Congo.Tulimfuatilia toka
aliposhuka ndegeni hadi katika
hoteli alikofikia.Alifikia katika
hoteli kubwa kuliko zote nchini
Congo na alidai kwamba alikuwa
katika mapumziko.Katika hoteli
hiyo tulifanikiwa kumnasa Seif
akiwa na mtu mmoja katika sehemu ya mapumziko” akasema
Peter na kutoa kompyuta yake
akaiwasha na kumuonyesha rais
video ambayo ilimuonyesha Seif
akiwa amekaa pembeni ya bwawa
la kuogelea akiwa amevaa kaptura
nyeupe akiwa kifua wazi pembeni
yake akiwa na glasi yenye kinywaji
chenye rangi nyekundu,alikuwa
amejilaza katika kiti akisoma
gazeti.Mara akatokea mwanamke
mmoja akiwa amevaa kaptura fupi
sana rangi nyeupe ambayo kifungo
chake kilikuwa kimefunguliwa na
kuifanya nguo ya ndani ya rangi
nyekundu aliyokuwa ameivaa
kuonekana,tumbo lake lilikuwa
wazi na aliyafunika matiti yake kwa kwa sidiria nyekundu.Mkononi
alikuwa ameshika kompyuta
mpakato.Msichana yule
aliyetembea kwa mwendo wa
madaha alikwenda kukaa pembeni
ya kiti alichokaa Seif,walisalimiana
na walionekana kuzungumza na
baadae Seif akahama kutoka katika
kiti chake akaenda kukaa katika kiti
alichokaa mrembo yule akaanza
kumuelekeza kitu katika kompyuta
yake.
Dr Evans alistuka sana baada
ya kuona video ile
“Dr Olivia?! Akasema kwa
mshangao.
“Unamfahamu huyu
mwanamke?akauliza Peter “Ndiyo ninamfahamu.Anaitwa
Dr Olivia Themba.Ni daktari
maarufu sana hapa nchini na ana
kituo chake chake cha utafiti wa
magonjwa mbali mbali”akajibu Dr
Evans
“Huyo ndiye ambaye
ameonekana akiwa na Seif kila
mara.Alifikia katika hoteli aliyofikia
Seif na ni siku ile ile ambayo Seif
alifika ndipo na huyu naye
alifika.Ukaribu wao umetufanya
tuhisi wawili hawa wanafahamiana
na walikuwa na sababu maalum ya
kukutana kule Kinshasa.Rais wa
Congo alifikishiwa taarifa hizi na
akaona ni taarifa za muhimu sana
na akanituma kwako nikuletee taarifa hizi moja kwa moja ili
serikali ya Tanzania muanze
kumfanyia uchunguzi huyu daktari
na kujua mahusiano yake na Seif na
kwa nini wakakutane Kinshasa”
akasema Peter.Dr Evans
akaonekana kuzama katika
mawazo mengi.
“Peter kuna taarifa zozote za
ziada mlizoweza kuzipata kuhusu
watu hawa wawili?akauliza Dr
Evans
“Tulichofanikiwa kukipata ni
hiyo video.Hatukufanikiwa kunasa
maongezi yao lakini nyakati za
usiku muda mwingi walikuwa
wanakuwa pamoja.Kuna nyakati
walikuwa wanajificha mahala na kuzama katika mazungumzo
mazito.Tunalazimika kuamini
kwamba kuna jambo wanalipanga
ndiyo maana rais akanituma nije
nikupe taarifa ili muanze kuchukua
tahadhari” akasema Peter
Baada ya tafakari ya muda Dr
Evans akasema
“Peter ninakushukuru sana
kwa taarifa hii muhimu
sana.Ahsanteni sana kwa
uchunguzi mlioufanya na
nitampigia simu pia rais wako
kumshukuru kwa taarifa hii.Serikali
yangu itaanzia hapa mlipoishia
ninyi na ninakuhakikishia kwamba
lazima tutajua kila kitu kuhusiana
na Seif na Dr Olivia.Tutajua kama kuna jambo wanapanga kulifanya
afrika mashariki” akasema Dr
Evans.Peter hakuwa na la ziada
kwani tayari alikwisha fikisha
ujumbe aliotumwa akaagana na
rais akaondoka zake.
Baada ya Peter kuondoka Dr
Evans akaitazama tena video ile
katika kompyuta yake
“Dr Olivia ametoka wapi na
huyu mtu? Katika video hii
wanaonekana wakiwa katika
mikakati Fulani,je Olivia hafahamu
kama Seif ni mtu muhimu sana
katika kikundi cha IS?Hafahamu
kama huyu ndiye ambaye amekuwa
akiandikisha vijana kutoka ukanda huu wa Afrika kwenda kujiunga na
kikundi cha IS?akajiuliza Dr Evans
“NInamfahamu Dr Olivia toka
akiwa mtoto mdogo,mimi na baba
yake ni marafiki wakubwa toka
tukiwa vijana wadogo na hadi sasa
nimekuwa mtu wa karibu na
familia yao lakini kwa hiki
alichokifanya cha kuwa na ukaribu
na huyu mtu tunalazimika
kumuweka mikononi na
kumchunguza kujua kuhusu
mahusiano yake na Seif na kama
wana mipango yoyote” akawaza Dr
Evans na kumpigia simu
Devotha Adolph na kumtaka afike
ikulu haraka sana. “Mwili wote umenisisimka
baada ya kumuona Dr Olivia akiwa
na huyu mtu hatari.Lazima
tumchunguze tujue wana mipango
gani.Siamini kama Dr Olivia
anaweza akawa na ushirika na
IS.Kama ana mahusiano nao
atakuwa ameyaharibu maisha yake
kabisa kwani hatutakuwa na
namna nyingine yakufanya zaidi ya
kumpoteza.Olivia ni mtoto wa rafiki
yangu mkubwa Agrey Themba
ambaye ni mfadhili mkuu wa
chama chetu na amekuwa akitoa
misaada mingi sana kwa nchi.Ni
mtu mwenye heshima kubwa sana
katika nchi hii lakini kama mwanae
ni mshirika wa IS atanisamehe kwani lazima adhibitiwe haraka
sana” akawaza Dr Evans
Devotha Adolph aliwasili ikulu
haraka sana kama
alivyotakiwa.Rais akampokea
wakaenda katika chumba cha
mazungumzo ya faragha.
“Ahsante sana kwa kufika kwa
haraka Devotha.Nimelazimika
kukuita kuna jambo la dharura
limejitokeza” akasema Dr Evans
“Jambo gani mheshimiwa
rais?akauliza Devotha
“Nimepata mgeni maalum jioni
hii kutoka kwa rais wa jamhuri ya
kidemokrasia ya Congo ambaye
alitumwa kuniletea taarifa muhimu sana”Dr Evans akanyamaza kwa
sekunde kadhaa halafu akaendela
“Idara ya usalama wa taifa ya
Congo ilipata taarifa siku chache
zilizopita kwamba Seif Almuhsin
ambaye ni mtu muhimu sana katika
mtandao wa IS ambaye amekuwa
akikusanya vijana katika ukanda
huu wa afrika mashariki kati na
kusini kujiunga na mtandao wa
IS.Walianza kumfuatilia Seif toka
alipowasili nchini Congo lengo ni
kutaka kujua dhumuni lake la
kwenda huko.Baada ya kuanza
kumfuatilia waligundua kwamba
kuna mtu ambaye amekuwa
akikutana na Seif kwa uficho hapo
hotelini na kila wanapokutana wameonekana wakijadili jambo
Fulani” akasema Dr Evans na
kuicheza ile video ambayo
ilimuonyesha Seif akiwa na Dr
Olivia katika bwawa la
kuogelea.Devotha akaitazama video
ile akairudia tena mara ya pili
“Umegundua nini katika video
hii Devotha?akauliza Dr Evans
“Ukiitazama video hii kwa
makini utagundua kwamba
kukutana kwa watu hawa wawili si
kwa bahati mbaya.Wanaonekana
wazi wanafahamiana.Tizama hata
namna wanavyozungumza ni wazi
ni watu ambao wanajuana kabla ya
kukutana hapa” akasema Devotha “Hata mimi baada ya
kuitazama video hii mara moja
nilihisi hivyo.Kukutana kwa watu
hawa si kwa bahati mbaya.Seif ni
mtu muhimu sana katika mtandao
wa IS na kama amekutana na
kufanya mazungumzo na Dr Olivia
tena nje ya nchi hii inatupa picha
kwamba kuna jambo lipo kati ya
watu hawa wawili.Ninaelekeza
kwamba huyu Dr Olivia awekwe
mikononi na achunguzwe kwa kina
kuhusiana na mahusiano yake na
Seif.Nataka achukuliwe katika
mtindo wa kutekwa ili isijulikane
kama ni sisi ndio
tunaomshikilia.Tukimchukua
katika mtindo huu tutapata nafasi nzuri ya kumuhoji na kufahamu
kwa kina kuhusu mahusiano yake
na mtandao wa IS.Lazima
tujiridhishe kama Dr Olivia naye ni
mshirika wa IS” akasema Dr Evans
“Nimekuelewa mheshimiwa
rais.Nitawaelekeza vijana wangu
haraka sana waanze maandalizi ya
mpango huu wa kumteka Dr Olivia”
“Vizuri.Nataka niwakumbushe
kwamba Dr Olivia ni mtu mwenye
jina kubwa hapa nchini kutokana
na kazi zake anazozifanya.Vile vile
baba yake ni mtu maarufu hapa
nchini,ni rafiki yangu mkubwa
sana,ni mfadhili mkubwa wa
chama,ni mmoja wa walipa kodi
wakubwa ambao nchi inawaheshimu hivyo kutekwa kwa
mwanae ni jambo linalotakiwa
kufanywa kwa umakini mkubwa
mno.Kusiwe na aina yoyote ya
dosari itakayopelekea watekaji
kujulikana.Ninaamini unao vijana
mahiri kabisa wenye uwezo
mkubwa na mpango huu
mtautekeleza vizuri.Uzembe
wowote ule ukifanyika utapelekea
mfahamike na mkijulikana
mtakuwa mmeniangusha mimi
hivyo hakikisha mpango
unaandaliwa vizuri na kusiwe na
aina yoyote ya uzembe”akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais ninakuahdi
kwamba hakutakuwa na uzembe wowote utakaofanyika na
tutahakikisha tunampata Dr Olivia
pamoja na” akasema Devotha
*****************
Mlango wa chumba
alimowekwa Dr Olivia
ukafunguliwa na watu wawili
wakaingia.Dr Olivia hakuweza
kuwaona watu wale kwani alikuwa
amefungwa kitambaa usoni na
kuwekewa kitu mdomoni
kilichomfanya ashindwe
kuzungumza chochote.Mmoja wa
watu wale walioingia mle ndani
alikuwa na mkoba mdogo
akauweka mezani akaufungua na kuchukua sindano akavuta dawa na
kumchoma Dr Olivia shingoni na
taratibu akapoteza fahamu
“Tayari tunaweza kumuondoa”
akasema yule jamaa
“Thanks doctor” akajibu Kaiza
na kuwaita watu wawili
wakamuinua Dr Olivia na
kumuweka katika buti ya gari aina
ya mercedece benzi kisha Kaiza na
wale jamaa wengine watatu
wakaingia katika gari lile na
kuondoka katika ile nyumba.
Walivuka daraja la Nyerere na
kuelekea Kigamboni ambako
walifika hadi katika nyuma moja
yenye rangi nyekundu geti
likafunguliwa wakaingia ndani.Moja kwa moja gari lile
likaingia katika gereji na bila
kupoteza muda buti likafunguliwa
Dr Olivia akashushwa.Bado hakuwa
na fahamu akaingizwa ndani ya ile
nyuma.Chumba kimoja
kikafunguliwa mlango,kulikuwa na
ngazi za kushuka chini ambako
waliukuta mlango ambao Kaiza
aliweka kiganja chake cha mkono
ukafunguka wakaingia ndani ya
chumba kikubwa kilichokuwa na
hewa nzuri iliyotokana na
kiyoyozi,vitanda viwili vikubwa
vyenye mashuka mazuri.Ukutani
kulikuwa na picha nzuri za
wanyama na misitu,luninga
kubwa,pia kulikuwa na kabati ambalo kulikuwa na redio
kubwa,kukawa pia na friji la
vinywaji,kabati la nguo,meza ya
vipodozi bila kusahau choo na bafu
zuri.Kilikuwa ni chumba kizuri sana
kilichosheheni kila kitu.Dr Olivia
akalazwa kitandani na kufunguliwa
mikono na miguu akatolewa
kitambaa usoni pamoja na kile kitu
walichomfunga mdomoni ili
asiweze kupiga ukulele.Yule jamaa
aliyemchoma sindano ya
kumpoteza fahamu akamchoma
tena sindano nyingine shingoni
“Itamchukua muda gani
kuamka?akauliza Kaiza
“Dakika kumi na tano hadi
ishirini” akajibu yule daktari “Ahsante sana” akajibu Kaiza
kisha wakatoka wote na kwenda
katika chumba kingine ambacho
kilikuwa na luninga kubwa
iliyounganishwa na kamera
zilizofungwa ndani ya chumba kile
alimowekwa Dr
Olivia.Walimshuhudia Dr Olivia
akiwa amelala
kitandani.Wakamuacha mtu mmoja
katika kile chumba wengine
wakaenda sebuleni.Kaiza
akachukua simu na kupiga
“Madam Devotha,tayari twiga
yuko kitalu 7” akasema Kaiza
“I’m on the way” akajibu
Devotha “I need a drink” akasema Kaiza
na kufungua friji kubwa
lililosheheni vinywaji akachukua
kinywaji alichohitaji halafu
akaenda katika chumba kimoja
kulimokuwa na watu wanne na
kompyuta kumi na nne.
“Kuna taarifa yoyote
mpya?akauliza Kaiza
“Mpaka sasa hakuna taarifa
yoyote mpya” akajibu mmoja
wao.Kaiza akayaelekeza macho
yake katika luninga kubwa
iliyokuwa ukutani ambako picha
mbali mbali kutoka katika kamera
mbali mbali jijini Dar es salaam
zilikuwa zinaonekana.Ukiwa ndani
ya chumba hiki ndani ya muda mfupi unaweza ukaona kila kona ya
jiji la Dar es salaam.Akiwa ndani ya
kile chumba aliweza kuziona gari
mbili zikivuka geti na kuingia ndani
ya nyumba ile
“Devotha amekuja” akasema
na kutoka haraka mle ndani ya kile
chumba akaenda nje na kumpokea
Devotha kisha akamuongoza
kuelekea ndani
“Good job Kaiza” akasema
Devotha.Kaiza akamkaribisha
Devotha katika sebule kubwa yenye
sofa kubwa la mzunguko.Watu
wote waliokuwemo ndani ya ile
nyumba wakaitwa kuzungumza na
Devotha “Nimekuja kuwashukuru sana
kwa kazi nzuri mliyoifanya leo.Kazi
kubwa ya idara yetu ni kuhakikisha
kwamba nchi inakuwa salama na
ndivyo tulivyofanya.Kwa
ushirikiano wenu tumeweza
kumpata Dr Olivia Themba na
kinachofuata kwa sasa ni
kumchunguza.Kama
mnavyofahamu Dr Olivia ni mtu
maarufu.Ni daktari mwenye jina
kubwa kutokana na kazi
anazozifanya vile vile ni mtoto wa
tajiri mkubwa hapa nchini.Baba
yake ni rafiki mkubwa wa rais ,vile
vile ni mfadhili mkubwa wa chama
kinachotawala,viongozi wengi wa
serikali wanafahamiana naye hivyo basi msako wa kumtafuta Dr Olivia
utakuwa mkubwa.Tuna kazi kubwa
ya kuhakikisha kwamba kwa
namna yoyote ile hakuna
anayegundua nani waliomteka
Olivia wala mahala alipo hadi hapo
tutakapomaliza uchunguzi
wetu.Macho na masikio yenu
yawepo kila mahala kuhakikisha
kwamba hakuna yeyote atakayejua
kama Dr Olivia yuko hapa” akasema
Devotha kisha akawataka wengine
wote wakaendelee na kazi zao
akaongozana na Kaiza na watu
wengine sita wakaenda katika
chumba kimoja chenye meza
kubwa ya mikutano.Bila kupoteza
muda Devotha akafungua kikao “Nawapongeza tena kwa kazi
nzuri ya leo.Naamini zoezi
lilikwenda vyema na hakuna tatizo
lolote ambalo linaweza
kutokea.Nataka kujua maendeleo
ya Dr Olivia”akasema Devotha
“Olivia anaendelea vyema.Kwa
mujibu wa Dr Kalela hana tatizo
lolote.Hakuumizwa sehemu yoyote
ile kama ulivyotoa
maelekezo.Vijana walijitahidi sana
kuhakikisha kwamba Dr Olivia
haumizwi kwa namna yoyote
ile.Hivi sasa tunasubiri aweze
kuzinduka” akajibu Kaiza ambaye
ni msaidizi wa Devotha
“Good.Sasa ni wakati wa
kufahamu lile jambo kubwa lililotufanya tumteke Dr Olivia.Vifaa
vyake vyote mmefanikiwa
kuvipata?akauliza Devotha
“Ndiyo madam.Kama
nilivyokwambia kwamba vijana
walijitahidi sana kuhakikisha
kwamba hakuna uharibifu wowote
unaotokea hivyo kila kitu kiko
salama” akasema Kaiza na kutoa
ishara mtu mmoja akainuka
akatoka na kurejea na sinia ambalo
ndani yake kulikuwa na simu mbili
za Dr Olivia,saa pamoja na mkufu
wenye kidani cha Tanzanite.Vile
vile kulikuwa na mkoba mdogo
uliokuwa na vitu vidogo vidogo
ndani yake kama hereni,rangi za
mdomo na kucha pamoja na dola elfu mbili za Marekani pia kukawa
na kompyuta mpakato
“Peleka kompyuta hii ndogo
kwa vijana waichunguze,nataka
kujua kila alichokihifadhi ndani ya
hii komputa na lengo kubwa ni
kuangalia mahusiano yake na Seif
Almuhsin wa kikundi cha IS”
akasema Devotha na Kaiza
akaichukua ile kompyuta na
kwenda kuikabidhi kwa timu ya
vijaan waliokuwa katika kile
chumba chenye kompyuta nyingi
na kuwapa maelekezo ya kufanya
kuhusiana na ile kompyuta halafu
akarejea tena kundelea na kikao
“Simu zake ni muhimu sana
lakini hatutaweza kuziwasha kwa sasa kwani zitakuwa zinafuatiliwa
na zitaweza kuonyesha mahala
alipo hivyo tuziweke pembeni kwa
muda hadi pale itakapolazimika
kuziwasha.Sanduku lake
mmelipekua?akauliza Devotha
“Hapana bado” akajibu Kaiza
“Open it” akaelekeza Devotha
na mmoja wa wale watu mle ndani
akalifungua lile sanduku
taratibu na kuanza kutoa kitu
kimoja kimoja na kukiweka
pembeni.Ndani ya sanduku lile
kulikuwa na nguo na vitu vichache
ambavyo huvitumia katika kazi
yake ya udaktari.Chini kabisa ka sanduku lile kulikuwa na kasha
ambalo lilikuwa linawaka taa ya
kijani na lilionekana kutumia
betri.Wote wakaingiwa na hofu.
“Hicho ni kitu gani?akauliza
Devotha
“Linaonekana ni kama kasha la
kuhifadhi vitu muhimu.Huyu ni
daktari inawezekana kuna vitu
vyake muhimu amevihifadhi ndani
ya hili kasha” akasema yule jamaa
aliyefungua sanduku la Dr Olivia
“Dr Kalela go check what’s
that” akasema Devotha.
Dr Kalela akakichukua kile
kifaa kilichokuwa kinawaka taa ya
kijani akakichunguza halafu
akakifungua.Akastuka baada ya kuona kilichokuwamo ndani ya lile
kasha
“Kuna nini mbona umestuka
namna hiyo?akauliza Devotha
“Blood samples”
“Blood samples?akauliza
Devotha
“Ndiyo.Kuna sampuli nne za
damu” akasema Dr Kalela.
“Dr Kalela nenda kazihifadhi
hizo sampuli sehemu nzuri
tutazifanyia uchunguzi tujue
sampuli hizo amezitoa wapi na kwa
makusudi yapi?akasema Devotha
na Dr Kalela akaenda kuzihifadhi
sampuli zile za damu katika
chumba maalum.Nyumba ile ilikuwa na chumba maalum cha
tiba.
“Dr Olivia amekwisha
zinduka?akauliza Devotha na wote
wakaenda katika chumba chenye
kompyuta zilizounganishwa na
kamera zilizo katika chumba alimo
Dr Olivia ambaye bado alikuwa
amelala kitandani hakuwa
amezinduka
****************
 
SIRI
Episode 3
Mtunzi. Patrick CK

Msafara wa rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania uliwasili
katika makazi ya bilionea Agrey
Themba.Rais Dr Evans na Agrey ni
marafiki wa muda mrefu na wamekuwa na mazoea ya
kutembeleana kujuliana hali mara
kwa mara.Agrey na mkewe Lucy
Themba wakajulishwa kuhusu
kuwasili kwa rais wa Jamhuri ya
muungano wa Tanzania Dr Evans
ambaye alifika bila kutoa taarifa,
wakatoka kwenda kumpokea.Rais
alishuka garini na kupokewa na
Agrey na mkewe wakamkaribisha
ndani.Wageni waliokuwa wamefika
kuwapa pole akina Agrey na
mkewe wakalazimika kutoka
kumpisha rais
“Karibu sana Evans” akasema
Agrey
“Agrey tayari tulikwisha
zungumza simuni lakini nimeona itakuwa vyema kama nikija
mwenyewe kuwapeni pole kwa hili
lililotokea.Ni jambo la kustusha
sana” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais
tunashukuru sana kwa kuja
kututembelea na kutupa
pole.Tumefarijika mno kwa ujio
wako” akasema Agrey
“Agrey nimeguswa sana na hili
lililotokea.Dr Olivia ni sawa na
mwanangu hivyo ninakuahidi
kwamba nitafanya kila lililo ndani
ya uwezo wangu kuhakikisha
kwamba anapatikana akiwa
mzima.Nimekwisha toa maelekezo
kwa jeshi la polisi kuhakikisha
wanatumia kila uwezo walionao kumsaka Dr Olivia.Ngoja nimuulize
IGP wamefikia wapi hadi sasa
katika msako” akasema Dr Evans
akachukua simu na kumpigia mkuu
wa jeshi la polisi
“Mheshimiwa rais” akasema
mkuu wa jeshi la polisi baada ya
kupokea simu ya Dr Evans
“IGP naomba unieleze
mmefikia wapi katika msako wa Dr
Olivia? Akauliza rais
“Mheshimiwa rais toka
lilipotokea tukio lile jeshi la polisi
liko kazini na tunafanya juhudi
kubwa kuhakikisha kwamba
tunajua mahala aliko Dr Olivia na
kuwakamata watekaji
wote.Mwelekeo si mbaya mheshimiwa rais na kuna hatua
tayari zimekwisha pigwa mpaka
sasa.Tayari tumeipata helkopta
ambayo ilitumika katika tukio lile
ikiwa imetelekezwa nje kidogo ya
mji.Helkopta hiyo inamilikiwa na
kampuni moja ya kukodisha ndege
ndogo na helkopta.Wamiliki wake
wamekiri kwamba helkopta hiyo ni
yao na kwamba asubuhi ya leo
rubani wake aliondoka nayo katika
mazoezi ya kawaida na hakurejea
hadi pale walipopata taarifa
kwamba helkopta yao imetumika
katika tukio la kumteka Dr
Olivia.Polisi wamemfuatilia rubani
wa helkopta huyo nyumbani kwake
na kumkuta yeye,mkewe na watoto wake wawili wote
wameuawa.Tukio hilo la kuuawa
kwa rubani huyo limeturudisha
nyuma sana hata hivyo bado
tunaendelea na uchunguzi kwani
picha za kamera zilizofungwa pale
nyumbani kwa Dr Olivia
zinaonyesha gari mbili zilizofika na
kumchukua Olivia.Watu
walioshuka katika magari yale
walikuwa wamefunika nyuso zao
wasitambulike.Kingine kinachotupa
ugumu zaidi ni kwamba gari zile
zote mbili zilikuwa na namba
zinazofanana.Watekaji hawa
waliamua kuweka namba bandia
zinazofanana katika magari hayo ili
kutuchanganya.Pamoja na hayo yote mheshimiwa rais napenda
kukuhakikishia kwamba jeshi la
polisi tutatumia kila uwezo tulio
nao kuhakikisha Dr Olivia
anapatikana kabla ya giza kuingia”
akasema mkuu wa jeshi la polisi
“Ninashukuru sana IGP kwa
taarifa hiyo yenye kutia
moyo.Ninakuomba uongeze nguvu
zaidi na hakikisha unafanya kila
uwezalo Dr Olivia apatikane”
“Tutafanya kila tuwezalo
mheshimiwa rais na
ninakuhakikishia Dr Olivia
atapatikana”
“Ahsante sana.Kila la heri”
akasema Dr Evans na kukata
simu.Mazungumzo yake na mkuu wa jeshi la polisi yalisikiwa na
Agrey na mkewe kwani alikuwa
ameweka katika sauti kubwa ili
wote wasikie
“Nadhani mmesikia namna
jeshi la polisi wanavyofanya kila
wawezalo kuhakikisha kwamba Dr
Olivia anapatikana.Ninarejea tena
kuwahakikishia kwamba Dr Olivia
atapatikana” akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais
tunakushukuru sana kwa namna
unavyohangaika na suala
hili.Tumefarijika mno kwa juhudi
za jeshi la polisi.Tunaamini
kwamba mwanetu atapatikana
akiwa salama” akasema Agrey “Ninachowaomba kama kuna
chochote mnadhani kinaweza
kusaidia katika uchunguzi
muwasiliane na jeshi la polisi na
kuwaeleza ili wakifanyie kazi hata
kama ni kidogo kiasi
gani.Yawezekana watekaji hawa
lengo lao ni fedha hivyo
watakapowapigia kudai fedha ili
wamuachie mtoto wenu
wasilianeni kwanza na jeshi la
polisi msiogope vitisho
watakavyowapa kwamba
mkiwasiliana na polisi mwanenu
mtamkosa.Tunataka kumuokoa Dr
Olivia vile vile kuwakamata
watekaji” akasema Dr Evans “Tutafanya hivyo mheshimiwa
rais” akajibu Agrey.
Rais Dr Evans hakuchukua
muda mrefu sana pale kwa akina
agrey akawaaga na kuondoka.
********************
Dr Olivia alizinduka kutoka
usingizini na kujikuta akiwa katika
chumba chenye ubaridi mwingi
.Hali ile ya hewa iliyokuwemo mle
chumbani ilikuwa tofauti kidogo na
hali aliyoizoea chumbani
kwake.Akageuza macho kutazama
kila kona na kugundua kwamba
alikuwa katika sehemu tofauti na
ndipo kumbukumbu za kile kilichotokea zilipomrejea.Akainuka
na kwenda katika mlango ambao
ulikuwa unafunguliwa kwa
kutumia kadi maalum akashindwa
kuufungua na kwenda kujikunyata
kitandani akaanza kulia.Aligundua
kwamba tayari amekwisha tekwa
na hakuwa na uwezo wa kutoka
mle ndani.
“It’s time” akasema Devotha
aliyekuwa na timu yake
wakimfuatilia Dr Olivia katika
luninga.Kaiza akarekebisha tai yake
halafu akashuka kuelekea katika
chumba alimo Dr Olivia.
Akiwa bado amejikunyata
kitandani akilia mlango ukafunguka
akayaelekeza macho yake mlangoni na jamaa mmoja mnene akaingia
mle ndani na kuufunga mlango.
“Habari yako Dr Olivia”
akasema Kaiza kwa sauti ya upole
lakini Dr Olivia hakujibu kitu
“Unajisikiaje Dr Olivia?Kuna
sehemu yoyote unahisi
maumivu?Kichwa,miguu..”
“I’m fine.Tell me why I’m
here”akasema Dr Olivia
“Usiogope Dr Olivia.Uko
salama.Can I get you something to
drink? Akasema Kaiza akienda
katika friji kubwa akalifungua na
kuchukua chupa mbili za maji ya
matunda akampatia moja Dr Olivia. “Sihitaji kinywaji chenu nataka
mniambie kwa nini mnaniweka
hapa?akauliza Dr Olivia
“Relax Dr Olivia we’re not bad
people”akajibu Kaiza na kuvuta kiti
akaketi karibu na Dr Olivia
“Mngekuwa watu wazuri
msingethubutu kunivamia mkaua
walinzi wangu na kuniteka.What do
you want from me?You want
money?Semeni ni kiasi gani
mnakihitaji
niwapatie.Hamkupaswa kuua watu
wangu kwa sababu ya fedha”
akasema Dr Olivia na kufuta
machozi
“Dr Olivia hatuhitaji pesa”
akajibu Kaiza “Kama hamuhitaji fedha nini
mnahitaji toka kwangu?Niambieni
basi mnachokitaka niwapatie ili
mniache niende
zangu.Mmewaweka wazazi na
ndugu zangu katika wakati mgumu
sana hawajui mahala
nilipo.Tafadhali niambieni mnataka
kitu gani na mniahidi nikiwapa
mnachokihitaji mtaniacha niende
zangu”akasema Dr Olivia
“Olivia we need to ask you
some questions.There are few
things we want to know from
you.Ukionyesha ushirikiano kwetu
nakuahidi tutakuacha uende zako”
akasema Kaiza “Ni vitu gani mnataka
kuvifahamu kutoka kwangu?Please
tell me.Nitawapa kila
mnachokitaka” akasema Dr
Olivia.Kaiza akakohoa kidogo
kurekebisha koo na kusema
“Dr Olivia hukuwepo nchini
kwa siku kama tano
zilizopita.Ulikwenda wapi?akauliza
Kaiza.Dr Olivia akamtazama kwa
macho makali
“Mmekuwa mnanifuatilia kila
ninachokifanya hadi mkajua
kwamba siko nchini.Who are you
peple?akauliza Dr Olivia
“Please answer the question
Dr Olivia” akasema Kaiza “Kwa nini
mnanifuatilia?akauliza Dr Olivia
“Dr Olivia naomba ujibu swali
nililokuuliza ili tuokoe muda”
“Fine.Nilikuwa nimekwenda
nchini Congo DRC”
“Ulikwenda kufanya nini
nchini Congo DRC?akauliza Kaiza
“Mimi ni daktari nilikwenda
nchini Congo katika shughuli zangu
za utafiti”akajibu Dr Olivia
“Kitu gani ulikwenda kukitafiti
nchini Congo?
“Ninafanya utafiti wa
magonjwa mbali mbali ya
binadamu na hata
wanyama.Nilikwenda nchini Congo kufanya utafiti kuhusiana na
ugonjwa wa Sonzae”
Kaiza akavuta pumzi ndefu na
kuuliza
“Dr Olivia katika sanduku lako
tumekuta sampuli nne za
damu.Unaweza ukatueleza umetoa
wapi sampuli zile na kwa
madhumuni gani?
“What’s your name?akauliza
Dr Olivia
“Naitwa Kaiza”
“Mr Kaiza nadhani unafahamu
kazi yangu ninayofanya.Mimi ni
mtafiti na sampuli zile nimezitoa
nchini Congo ni damu kutoka kwa
nyani ambao wanasemekana ndio chanzo cha ugonjwa wa Sonzae”
akajibu Dr Olivia
“Dr Olivia sampuli hii ya damu
ina virusi vya Sonzae? Akauliza
Kaiza kwa mshangao
“Kwa nini ukaingiza hapa
nchini damu yenye virusi hatari vya
Sonzae? Hujui kama hili ni kosa
kubwa umelifanya ambalo linaweza
kukugharimu? akauliza Kaiza.Kwa
mara ya kwanza Dr Olivia akatoa
kicheko kidogo.
“Mr Kaiza.Nataka nifanye
makubaliano nanyi”akasema Dr
Olivia
“Makubaliano? Unataka
kufanya makubaliano gani nasi?
akauliza Kaiza “Chukueni sampuli zile za
damu mlizozikuta katika sanduku
langu,mzipeleke maabara
mkazifanyie uchunguzi na muone
kama zina virusi vya ugonjwa wa
Sinzae.Kama damu hiyo itakuwa na
virusi vya Sonzae nichukulieni
hatua na niko tayari kupata adhabu
kwa kuingiza nchini damu yenye
virusi vya Sonzae lakini kama damu
hiyo itakutwa ni salama haina
virusi vya Sonzae basi mtaniacha
niende zangu.Do we have a deal?
Akauliza Dr Olivia
“Dr Olivia tutafanya uchunguzi
wetu kuhusu sampuli zile za
damu,mimi na wewe nataka
tuzungumze kuhusu suala lingine la muhimu zaidi” akasema
Kaiza,akatoa picha katika bahasha
na kumuonyesha Dr Olivia
“Unamfahamu huyu mtu
pichani?Umewahi kumuona?
“Ndiyo ninamfahamu.Anaitwa
Alzahwir” akajibu Dr Olivia
“Unafahamiana naye vipi?
“He’s my friend”
“Your friend?Mmefahamiana
lini?
“Nimekutana naye nchini
Congo.Mimi na yeye tulifikia katika
hoteli moja tukakutana na kuwa
marafiki”
“Kabla ya kukutana nchini
Congo hamkuwahi kufahamiana
kabla?akauliza Kaiza “Sikumfahamu Zahwir
kabla.Mara ya kwanza nimekutana
naye Kinshasa”
“Dr Olivia ninakuomba
unieleze ukweli bila kuficha
chochote kwani ni ukweli pekee
ndio utakaokusaidia ukawa huru
lakini kama hautakuwa mkweli
ninasikitika kwamba yawezekana
usitoke humu ndani.Nataka
unieleze ukweli kuhusiana na huyu
mtu unayemfahamu kama Zahwir”
“Nikueleze kitu gani
Kaiza?Nimekwisha kueleza
kwamba mtu huyu nimekutana
naye Kinshasa tukawa marafiki na
sikuwahi kumfahamu hapo kabla”
akasema Dr Olivia.Kaiza akaenda katika luninga akaiwasha na video
ikatokea ikimuonyesha Seif
Almuhsin akiwa amekaa pembeni
ya bwawa la kuogelea na akatokea
Dr Olivia akaketi pembeni yake
akiwa na kompyuta yake wakaanza
kuzungumza.Video ile ilionekana
kumstua Dr Olivia
“You were following me?!
Akauliza Dr Olivia kwa ukali.
“Dr Olivia naomba video hii
ukitazama vizuri utagundua
kwamba wewe na Zahwir
mnafahamiana vyema kabla ya
kukutana hapa.Je unamfahamu
vyema huyu mtu ni nani?akauliza
Kaiza “kwa nini mnanifuatilia?
Akauliza Dr Olivia
“Dr Olivia nataka unijibu swali
nililokuuliza huyu mtu unayedai ni
rafiki yako unamfahamu
vyema?akauliza Kaiza
“Zahwir ni mfanyabiashara”
akajibu Dr Olivia.
“Sikiliza Dr Olivia nimekuuliza
makusudi ili kujua namna
unavyomfahamu huyu mtu na
inaonekana bado humfahamu
vyema.Mtu huyu haitwi Alzahwir
kama alivyokwambia bali anaitwa
Seif Almuhsin.Huyu ni mtu muhimu
sana katika kikundi cha IS na
amekuwa akifanya kazi ya
kukusanya vijana kutoka ukanda huu wa afrika ya mashariki kati na
kusini ambao hujiunga na kikundi
hiki hatari duniani” akasema Kaiza.
“Sifahamu chochote kama Seif
ni mtu hatari,sifahamu kama
anatoka kikundi cha IS” akasema Dr
Olivia
“Are you sure?
“Yes I’m sure.Nimekutana naye
hotelini Congo na sikuwa
nikimfahamu kabla ya hapo”
“Dr Olivia kitendo cha
kuonekana ukiwa karibu na mtu
huyu kinatufanya tuwe na mashaka
nawe sana.Tunataka kufahamu
mipango ya Seif,tunataka kufahamu
nyendo zake ukitusaidiakutueleza
hilo ninakuahidi kwamba tutakuacha huru.Tunaamini wewe
na yeye ni washirika na lazima
unamfahamu vyema” akasema
Kaiza
“Nimekwisha sema kwamba
simfahamu kabisa huyu
mtu,nimekutana naye kwa mara ya
kwanza Congo,kama ningefahamu
jambo lolote kuhusu huyu mtu
ningekueleza” akasema Dr Olivia
“Dr Olivia fikiria kuhusu
hatima ya maisha yako kwani kama
hautatupa ukweli basi hautaweza
kutoka humu ndani.Yawezekana
ukawa ni mwisho wako.Ninakupa
nafasi nyingine ya kutafakari na
nitakaporejea tena humu ndani
nataka nipate maelezo yote kuhusiana na mipango ya Seif
Almuhsin” akasema Kaiza na
kutoka mle ndani akamuacha Dr
Olivia katika mawazo.
“Kaiza sijafurahishwa na kile
ulichokifanya mle ndani!! Akasema
Devotha kwa ukali wakiwa katika
ofisi yao baada ya Kaiza kutoka
kumuhoji Dr Olivia
“Ulitegemea nifanye nini
Devotha? Akauliza Kaiza
“I sent you in there to find
answers.Nilitegemea ungetumia
ujuzi na uzoefu wako katika
kuhakikisha unapata kile
tunachokihitaji.You were too soft.Is
it because she’s so pretty?akauliza
Devotha “Jamani nyote mmefuatilia kile
nilichozungumza na Dr Olivia na
kile alichokisema.This woman is
very smart.Anatakiwa kuhojiwa
taratibu.Tukienda haraka
tutashindwa kupata kile
tunachokihitaji”akasema Kaiza
“C’mon Kaiza we don’t have
much time.Tunatakiwa haraka sana
kutafuta majibu kutoka kwake.Joto
la kupotea kwake linazidi kupanda
huko nje hivyo tujitahidi kwa
haraka tuwezavyo kuhakikisha
tunapata majibu”akasema Devotha
“kwa kumtazama machoni
anaonekana kuna kitu
anakificha.Kuna jambo
analo.alipoiona video ile akiwa na Seif alistuka sana na hakutegemea
kabisa kama alikuwa
anafuatiliwa.Vijana wamefikia wapi
katika kuichunguza kompyuta
yake?Ukitazama katika ile video
Olivia na Seif walikuwa
wanaelekezana kitu katika ile
kompyuta na kwa kuwa Olivia
hakuwa na habai kama anafuatiliwa
naamini hakufuta vitu katika hiyo
kompyuta yake” akasema kaiza na
Devotha akamchukua wakaenda
katika ofisi ambako kompyuta ya
Dr Olivia ilikuwa inafanyiwa
uchunguzi
“Kuna chochote mmekipata
hadi sasa?akauliza Devotha “Tumepata mawasiliano yake
ya barua pepe lakini baada ya
kuyachunguza tumekuta
anawasiliana na mtu ambaye
anaitwa Sayid Omar ambaye
tunaendelea kufuatilia tujue
mahala alipo” akajibu mmoja wa
wale vijana na kumpatia Devotha
karatasi kadhaa.
“Hayo ndiyo mawasiliano yao
lakini wametumia lugha ya
kiarabu”
“Damn! Tutapataje tafsiri ya
mawasiliano yao?Ni Aziz pekee
ambaye alikuwa anafahamu
kiarabu.Kuna ulazima wa kutafuta
mtu anayejua lugha ya kiarabu au
kumpeleka kijana mmoja akajifunze lugha hiyo.Ni muhimu
sana kwa sasa.Yawezekana katika
mawasiliano haya kuna mambo ya
muhimu sana yanayoweza kutupa
mwanga mkubwa lakini hatuwezi
kufahamu chochote kwa kuwa
hatujui kiarabu” akasema Devotha
“Hii pia ni picha ambayo
tumeikuta katika kompyuta yake”
akasema yule kijana na kumpatia
Devotha picha waliyoikuta katika
kompyuta ya Dr Olivia
“Coletha..Huyu ni mtoto wa
rais” akasema Devotha akionekana
kushangaa
“Rais Dr Evans na Agrey baba
yake Olivia ni marafiki wakubwa na
familia zao ni marafiki pia hivyo Olivia kuwa na picha ya Coletha
haileti wasiwasi kwani naamini
wanafahamiana.Kikubwa hapa ni
kuhakikisha tunamfahamu huyu
Sayid Omar ni nani na yuko
wapi.Ingekuwa rahisi sana kwetu
kama tungeweza kujua
kilichoandikwa katika barua pepe
hizi walizokuwa wanatumiana
lakini hatujui kiarabu hivyo kitu
pekee tulichonacho ni kujua mahala
aliko huyo Sayid” akasema Kaiza
“Damn !! akasema mmoja wa
wale vijana mle ndani
“Kuna nini?akauliza Devotha
“Hawa jamaa ni wataalamu
kwani ukijaribu kufuatilia namba
ya kompyuta anayotumia huyo Omar unakuta kuna zaidi ya
kompyuta mia moja ambazo
zinaonekana ziko sehemu mbali
mbali duniani kwa hiyo ni vigumu
kufahamu ni yupi hasa
anayewasiliana na
Olivia.Wamefanya hivi ili
kumchanganya yeyote ambaye
atahitaji kufuatilia kutaka kujua
mahala aliko Sayid”
“Damn !! akasema Devotha
kwa ukali
“Endeleeni kufuatilia kama
kuna chochote tutakipata,Kaiza
tunakwenda tena kwa
Olivia.Lazima atueleze huyu Sayid
Omar ni nani” akasema Devotha.
 
SIRI
Episode 4
Mtunzi. Patrick CK

“Kamera zote ndani ya chumba
kile zizimwe nataka kuzungumza
naye nje ya kamera” akaelekeza
Devotha wakati wakielekea katika
chumba alimo Dr Olivia.Kaiza
Akaufungua mlango na kuingia
ndani.Dr Olivia akastuka baada ya
kumuona Devotha
“You?! Akauliza Dr Olivia na
kusimama
“Sit ! akasema Devotha na Dr
Olivia akaketi kitandani kwake
“I think I know you.Sura hii si
ngeni kwangu”akasema Dr
Olivia.Wakatazamana kwa muda
kisha Dr Olivia akauliza “Tell me why I’m here?What
exactly do you want from
me?akauliza Dr Olivia
“Dr Olivia nimekuja
mwenyewe kuzungumza nawe
hivyo nahitaji unieleze ukweli ama
sivyo mambo yatakuwa mabaya
zaidi kwako.Please be serious !!
akasema Devotha akiwa ameikunja
sura hakuhitaji masihara.Dr Olivia
akamtazama na kuuliza
“Unataka nini kutoka kwangu?
“Ulikuwa Kinshasa siku chache
zilizopita na ukiwa kule
umeonekana ukiwa na Seif
Almuhsin ambaye ni mtu muhimu
sana katika mtandao wa kikundi
cha IS.Ulipohojiwa na Kaiza umekana kumfahamu Seif kabla
lakini baada ya kupekua kompyuta
yako tumekuta mawasiliano yako
na Sayid Omar.Ili kuficha kile
mnachowasiliana mmetumia lugha
ya kiarabu.Tunaendelea kuzifanyia
uchunguzi barua pepe hizo na
kuzifasiri kwa Kiswahili lakini
wakati zoezi hilo linaendelea
nataka uniambie huyu Sayid Omar
ni nani na yuko wapi? Akauliza
Devotha.Dr Olivia akamtazama
hakumjibu kitu.
“Nijibu Olivia nina muda
mchache sana wa kuzungumza
nawe.Nataka kujua Sayid ni nani!!
Akasema Devotha “You’ve been following me
why?akauliza Dr Olivia
“Olivia naomba nikuweke wazi
kwamba mimi ndiye mkuu hapa na
ndiye mwenye uwezo wa kuuliza
swali na wewe kazi yako ni kujibu
kwa ufasaha kile
utakachoulizwa,huna uwezo wa
kuuliza chochote.Nijibu tafadhali
Sayid Omar ni nani na yuko wapi?
“Ninataka kujua mmekuwa
mnanifuatilia kila
ninachokifanya.Nini hasa mnataka
kutoka kwangu?akauliza Dr Olivia
“Dr Olivia mimi nina roho
mbaya kama shetani na huwa
sipendi mzaha.Ninapokuuliza kitu
unapaswa unijibu haraka tena kwa ufasaha.Nataka kujua kuhusu Sayid
Omar ni nani?.Hii ni nafasi ya
mwisho ninakupa” akasema
Devotha.Dr Olivia hakujibu kitu
akainamisha kichwa
“Dr Olivia don’t make this
harder,you wont like it” akasema
Devotha
“Fanyeni mnachotaka kufanya
lakini sintawaeleza chochote!!
Akafoka Dr Olivia
“Dr Olivia tunao uwezo wa
kutumia nguvu lakini
tunakuheshimu sana ndiyo maana
ninakuuliza kistaarabu.Please tell
us who is Sayid Omar? Akauliza
Devotha “Nimekwisha waambia
kwamba fanyeni kile mnachotaka
kukifanya lakini sintawaeleza
chochote.” akasema Dr Olivia
Devotha akamfanyia ishara
Kaiza akatoka mle chumbani na
baada ya muda akarejea akiwa na
watu watatu.
“Guys mpelekeni chumba cha
mahojiano,akikaa humu
anashindwa kufunguka” akasema
Devotha na bila kupoteza muda
jamaa wale wakambeba Dr Olivia
na kumpeleka katika chumba cha
maalum cha mahojiano.Ndani ya
chumba hicho kulikuwa na meza na
viti viwili.Kulikuwa na mitambo
kadhaa maalum kwa ajili ya kutesea.Kuta za chumba zilitapakaa
damu Dr Olivia akapatwa na
woga.Hali ya chumba kile
ilimuogopesha.Mkono wake wa
kushoto ukafungwa pingu
iliyounganishwa na meza,mkono
wa kulia alifungwa kifaa fulani
mkononi mwake
kilichounganishwa na mashine
ambayo iliwashwa.Devotha na
Kaiza walikuwa katika chumba
kingine chenye kompyuta mbili
wakifuatilia kinachoendelea katika
chumba alimowekwa Dr
Olivia.Macho yao yalielekezwa
katika kompyuta moja
iliyounganishwa na ile mashine
iliyomo ndani ya kile chumba alimo Dr Olivia.Walikuwa wanafuatilia
chati iliyokuwa ikipanda na
kushuka
“She’s scared.Tayari
amekwisha ingiwa na woga.Huu ni
wakati mzuri sana wa kuanza
kumuhoji” akasema Devotha kisha
yeye na Kaiza wakaelekea katika
chumba kile cha mahojiano
“Dr Olivia sasa tumefungua
ukurasa mpya.Tulikupa nafasi ya
kutueleza ukweli lakini ukashindwa
kuitumia sasa tumeamua kutafuta
ukweli kwa njia hii.Nilikwambia
kwamba hautaipenda njia hii lakini
hatuna namna nyingine zaidi ya
kuitumia kutafuta ukweli.Hiki ni
chumba cha mateso na ninaomba nikuweke wazi kwamba ukiingizwa
ndani ya chumba hiki hutatoka hadi
pale utakapofunguka.Kuna mateso
makali ndani ya chumba hiki
utatamani roho ikutoke lakini
hautakufa.Utalia hadi machozi
yatakauka,utapata maumivu makali
mno ambayo haujawahi kuyapata
toka uzaliwe,kila mshipa ndani ya
mwili wako utauma lakini hakuna
atakayekuonea huruma.Dr Olivia
bado unaweza kuyaepuka mateso
haya kwa kutueleza Sayid Omar ni
nani na yuko wapi?
“Ukweli upi mnataka
kuufahamu?Nimekwisha waeleza
kila kitu mnataka nini
tena?akauliza Dr Olivia “Tueleze kuhusiana na Sayid
Omar na Seif Almuhsin”akasema
Devotha
“Nimekwisha waeleza kwamba
sikwenda Congo kukutana na huyo
Seif bali nilikwenda kufanya utafiti
kwa wanyama ambao wanatajwa
kuwa chanzo cha maambukizi ya
Sonzae” akasema Dr Olivia
“Last chance Dr Olivia.Tell us
the truth” akasema Devotha
“Kwa nini mnanilazimisha
niwadanganye?Ninawaambia
kwamba sikwenda Kinshasa
kuonana na Seif” akasema Dr Olivia.
“Bado hataki kusema
ukweli,Josh she’ all yours endeleeni
na zoezi”akasema Devotha. Dr Olivia akatolewa pale katika
kiti akalazwa katika meza
akashikwa barabaraba na watu
wale wenye nguvu kisha
akafunikwa kitambaa usoni
akaanza kumwagiwa maji usoni .
“Stop !! akasema Devotha na
kitambaa kile kikaondolewa Dr
Olivia akavuta pumzi ndefu na
kuanza kukohoa mfululizo kisha
akaanza kulia.
“Dr Olivia are you ready to
talk?akauliza Devotha lakini Dr
Olivia bado aliendelea kukohoa
“Do it again” akasema
Devotha,Dr Olivia akashikwa tena
na kufunikwa kitembaa kile usoni akaanza kumwagiwa maji.Baada ya
muda Devotha akawasimamisha
“Are you ready ?!! akamuuliza
Dr Olivia
“ I need…uhh..!! Dr Olivia
akashindwa kuzungumza akitafuta
hewa
“Take a deep breath Olivia”
akasema Devotha
“Unataka nini?akauliza
“I want to make a deal with
you.If I tell you about Sayid will you
let me go?akauliza
“Kama ukitueleza ukweli
kuhusu Sayid Omar na Seif
Almuhsin tunaweza kukuacha
huru” akasema Devotha “Give me your word” akasema
Dr Olivia akiendelea kukohoa
“I give you my word”
“Ili kujua mahala aliko Sayid
nitawapa namba ya kompyuta yake
na mtaifuatilia mtajua mahala
alipo.”
“Wait” akasema Devotha na
kuchukua simu akapiga
“Tino nataka uchukue
maelekezo kutoka kwa Dr Olivia
kuhusu mahala aliko Sayid Omar”
akasema Devotha na kumpa simu
Dr Olivia atoe maelekezo.Dr Olivia
akamtajia yule mtu namba Fulani
akamtaka azitumie kumtafuta Sayid
na Devotha akaichukua simu yake. “Please let me know
wakifanikiwa kumpata Omar”
akasema Dr Olivia.Baada ya
sekunde chache simu ya Devotha
ikaita
“Tino kuna nini?akauliza
Devotha
“Madam tafadhali njoo haraka
sana” akasema Tino.Devotha na
Kaiza wakatoka haraka sana ndani
ya kile chumba na kwenda katika
ofisi ya akina Tino kukuta kukiwa
na taharuki kubwa.Kompyuta zote
ziligoma kufanya kazi
“Nini kimetokea hapa?akauliza
Devotha
“Baada tu ya kuweka zile
namba alizotoa Olivia ndipo mambo haya yalipoanza.Mfumo
mzima umegoma kufanya kazi
hakuna kompyuta hata moja
inayofanya kazi”
“Oh my God Can’t you make it
work?akauliza Devotha
“Tumejaribu madam lakini
imeshindikana.Ametuchezea
mchezo mbaya sana na sasa ni yeye
pekee mwenye uwezo wa
kuzifungua kompyuta zetu”
akasema Tino
“Oh my God !! disconnect
everything !! akasema Devotha na
kwa haraka wakaanza kuchomoa
kompyuta zao zote Devotha alikuwa amesimama
akitetemeka mwili.Wote mle ndani
jasho lilikuwa linawatoka
Devotha akapiga simu katika
vituo vingine na kuwataka wazime
kila kitu.
“Jesus Christ !! akasema
Devotha akiwa amesimama
amechanganyikiwa.Alikuwa na
hasira ziso kifani
“Ni mara ya kwanza kitu kama
hiki kinatokea katika mifumo
yetu.Can anybody fix this?akauliza
Devotha
“Hakuna namna
tutakavyoweza
kufanya.Tumefungwa.Somebody is
in control with our system.Kuna namba ambazo tunatakiwa
kuzipata ili tuweze kufungua
mfumo wetu na kuanza kuutumia
tena” akasema Tino
“Oh my God!! Akasema
Devotha akatoka haraka sana na
kwenda katika chumba cha silaha
akachukua bastora
“Today it’s me or her!!
Akasema Devotha
“Devotha tafadhali jitahidi
kujizuia kwani ukitumia hasira
nyingi hatutaweza
kufanikiwa.Olivia tayari
ametuweka katika kona,anacheza
na akili zetuThat woman is very
dangerous we need to be carefull”
akasema Kaiza “Kaiza hatuwezi kuchezewa na
mtu kama huyu.She must talk !!
akasema Devotha.Waliingia katika
chumba cha mahojiano,Devotha
alikuwa anahema kwa kasi huku
akimtazama Dr Olivia kwa hasira
kali.Akawataka watu wote mle
ndani watoke akabaki yeye na Dr
Olivia mle chumbani
“It’s me and you now!!
Akasema Devotha
“Mmempata Sayid?akauliza Dr
Olivia.Devotha akamrukia na
kuanza kuntandika ngumi
mfululizo
“You devil you need to fix our
system!! Akasema Devotha.Dr Olivia alikuwa anatokwa na damu
mdomoni.
“I cant fix it !! Mfumo wenu
wote tayari ninaushikilia na
mkitaka niufungue mfanya kile
nitakachowaelekeza!” akasema Dr
Olivia na kumpandisha Devotha
hasira akaenda kuchukua mtungi
mdogo wa gesi akauwasha
“Nitakupa mateso makali sana
hadi utakapokuwa tayari
kuufungua mfumo wetu!! Akasema
Devotha
“Nataka kuzungumza na rais !!
Akasema Dr Olivia.Devotha
akaendelea kumtazama kwa hasira
akiwa ameshika ile gesi inayowaka
akiwa tayari kumuunguza Olivia “Unataka nini?akauliza
Devotha
“You want me to fix your
system,get me president.Nataka
kuzungumza naye ana kwa ana na
baada ya kuzungumza naye
nitafungua mfumo wenu” akasema
Dr Olivia
“You are going to talk to me !!
akasema Devotha kwa ukali.
“Ni rais pekee ambaye
ninaweza kuzungumza naye”
akasema Dr Olivia.Devotha
aliendelea kumtazama kwa hasira
kali
“Dr Olivia ngoja nikuweke
sawa kwamba hautaweza kupata
nafasi ya kuzungumza na rais kama kuna kitu unataka kumueleza
utazungumza na mimi.Rais si mtu
ambaye unaweza ukamuita muda
wowote ule unaotaka wewe na
ukampata.Kama liko jambo
muhimu unataka kumueleza rais
nitalipokea badala yake”
“Nimesema namtaka rais
nizungumze naye ana kwa ana”
akasema Dr Olivia
“Dr Olivia talk to me.You won’t
see president” akasema Devotha
“Sitaki kurudia tena
nimekwambia nataka kuonana na
rais pekee.Kama unataka kufungua
mfumo wenu get me president”
akasema Dr Olivia.Devotha
akashusha pumzi.Kwa hasira alizokuwa nazo alitamani hata
kumkata kichwa Olivia
“I’ll get you president but me
and you we’re not over!!
Devotha akamueleza Dr Olivia
halafu akatoka ndani ya kile
chumba akakutana na Kaiza na
moja kwa moja wakaelekea katika
ofisi ndogo ya Devotha na kumpigia
simu rais
“Devotha nipe maendeleo ya
huko”akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais nashindwa
nianzie wapi”akasema Devotha
“Nini kimetokea
Devotha?akauliza Dr
Evans.Devotha akamueleza kila
kitu kilichotokea “My God ! Hili suala mbona
limechukua sura mpya? Huyu
Olivia ni nani hasa? Akauliza Dr
Evans na ukimya ukatawala.Bado
Devotha alikuwa na hasira sana
“Devotha unashauri
nini?akauliza Dr Evans
“She wants to talk to you!!
“Anataka kuonana na mimi? Dr
Evans akastuka
“Ndiyo anahitaji kuzungumza
nawe” akasema Devotha na Dr
Evans akavuta pumzi ndefu
“Kwa nini anataka
kuzungumza nami?Kuna jambo
gani anataka kunieleza?Kwa nini
asizungumze nanyi?akauliza rais “Mheshimiwa rais Olivia tayari
ametubana kwenye kona.Kila kitu
kimesimama na tunamtegemea
yeye pekee aweze kutupa codes za
kuufanya mfumo wetu uweze
kufanya kazi tena hivyo
tunalazimika kufanya anavyotaka
na kitu pekee anachokitaka ni
kuonana nawe” akasema Devotha
Dr Evans akafikiri kidogo na
kusema
“Davotha,unadhani Olivia
anataka kunieleza nini?
“Amesema anataka kuonana
nawe na hajaeleza sababu” akajibu
Devotha
Ukimya mfupi ulitanda na
baada ya muda rais akasema “Devotha unadhani kuna
ulazima wa mimi kuonana naye?
“Ndiyo mheshimiwa rais.Kuna
ulazima wa kuonana
naye.Yawezekana kuna jambo la
muhimu sana anataka kukueleza
vile vile tunahitaji kurudisha
mfumo wetu ambao ni yeye pekee
mwenye uwezo wa kuurejesha”
akasema Devotha.Rais akasikika
akishusha pumzi
“Nitaonana naye
wapi?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais nadhani
ingekuwa vyema kama ungekuja
kuonana naye hapa hapa katika
ofisi yetu ndogo Kigamboni”
akasema Devotha “Devotha siwezi kuja huko
muda huu.Nitakuja usiku baada ya
kiza kuingia”
“Sawa mheshimiwa
rais.Ninakushukuru kwa kukubali
kuja kuonana naye.Tutakusubiri”
akasema Devotha na kukata
simu.Devotha na Kaiza wakarejea
katika chumba alimo Dr Olivia
“Rais amekubali atakuja
kuonana nawe jioni ya leo.Nataka
uufungue mfumo wetu.Tunahitaji
kuendelea kufanya kazi zetu”
akasema Devotha
“Mpaka nitakaponana na rais
ndipo mtakapopata nafasi ya
kuendelea na mambo yenu kwa
sasa siwezi kuwapa chochote na mkijaribu kufanya chochote
mtaharibu kila kitu” akasema Dr
Olivia na kugeuka kitandani
akajilaza.
“C’mon Olivia tuna mambo
mengi makubwa tunafanya.Dakika
moja bila kufanya kazi tunakosa
mambo mengi sana”
“I don’t care.You started this
and you didn’t know who you are
messing with.Sintajali mnafanya
nini ninachotaka ni kuonana na rais
ndipo muendelee na mambo
yenu.Kama hamtajali nataka
mnirejeshe katika chumba
change,nataka kupumzika na vile
vile nahitaji matibabu mmeniumiza
sana” akasema Dr Olivia.Devotha akamtazama kwa hasira kali
akamtaka Kaiza
waondoke,akawaelekeza vijana
wake wamrejeshe Dr Olivia katika
chumba alichokuwa amehifadhiwa.
 
SIRI
Episode 5
Mtunzi. Patrick CK

SAA MBILI ZA USIKU
OFISI NDOGO YA IDARA YA SIRI YA
USALAMA WA NDANI
Gari mbili ziliwasili katika ofisi
ndogo za idara ya siri ya usalama
wa ndani wa nchi zilizoko
Kigamboni.Watu wanne wakashuka
haraka kutoka katika gari la mbele
na kulizunguka gari la nyuma
baada ya sekunde chache mlango
ukafunguliwa akashuka rais wajamhuri ya muungano wa Tanzania
Dr Evans Mwaluba akiwa amevaa
koti jeusi na kofia kufunika kichwa
chake.Hakutaka kujulikana kwani
hata safari hii ilikuwa ya siri
.Alipokewa Devotha Adolph akiwa
na msaidizi wake Kaiza
wakamuongoza rais hadi ndani ya
jengo
“Karibu sana mheshimiwa
rais” akasema Devotha
“Ahsante.Sitaki kuchukua
muda mrefu hapa.Kuna mafanikio
yoyote yamepatikana hadi sasa
katik akuurejesha mfumo wenu
ufanye kazi?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais mpaka sasa
bado hatujaweza kufanikiwa.Kila kitu kimesimama na
tunachposubiri ni wewe
uzungumze na Olivia ili aweze
kutufungulia mfumo wetu kama
alivyoahidi”akajibu Devotha
“Devotha unadhani baada ya
kuzungumza nami atafungua
mfumo wetu?akauliza Dr Evans
“Mheshimiwa rais hatujui kitu
gani anataka kukueleza lakini
ameahidi akizungumza nawe
atatufungulia kila kitu.Tuna
uhakika huo”
“Nimeuliza hivyo kwa sababu
kama ameweza kufanya kila kitu
kimesimama na akafanikiwa
kunileta hapa anaweza akaomba tena kitu kingine au hata kuachiwa
huru”
“Mheshimiwa rais Dr Olivia
tayari amekwisha onyesha kwamba
ni mtu hatari hivyo hatutaweza
kwa namna yoyote ile kumuachia
huru na hatutakubaliana tena na
chochote atakachokitaka” akasema
Devotha.
“Good.Huyu mwanamke kuna
mambo mengi anayafahamu hivyo
anapaswa kuendelea kushikiliwa
hapa kwa muda mrefu hadi tupate
kila tunachokitaka kutoka
kwake.Basi tusipoteze
muda.Nataka nikutane naye”
akasema Dr Evans na kushusha
pumzi.Alionekana kuwa na
hofu.Devotha na Kaiza
wakamuongoza Dr Evans kuelekea
katika chumba ambacho
angezungumza na Dr Olivia.
“No any camera in
here?akauliza Dr Evans
“Hiki ni chumba maalum kwa
ajili ya maongezi ya faragha.Hakuna
kamera wala chochote cha
kurekodi” akasema Devotha.Ndani
ya chumba kile kulikuwa na meza
na viti viwili vile vile kulikuwa na
seti ya sofa.Baada ya dakika tano Dr
Olivia akaletwa ndani ya chumba
kile alimokuwamo rais akiwa
amefungwa pingu
mikononi.Alisimama kwa sekunde
kadhaa baada ya kukutanisha macho na rais aliyekuwa ameketi
sofani.
“Mfungueni pingu” akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais…....”
Devotha akataka kusema kitu lakini
rais akamkatisha
“It’a ok.Mfungueni pingu awe
huru” akasema Dr Evans.Dr Olivia
akafunguliwa pingu .
“Thank you.Give us the room
now” akasema Dr Evans na watu
wote mle chumbani wakatoka
akabaki Rais na Dr Olivia
“Karibu Olivia.Come sit here
beside me” akasema Dr
Evans.Olivia akaenda kuketi katika
sofa lililoelekeana na rais.Dr Olivia
akamtazama rais kwa macho
yaliyojaa hasira
“Rafiki mkubwa wa baba
yangu.Ninakuheshimu kama baba
yangu siamini kama umefikia hatua
kama hii.Baba yangu anajua watu
walioniteka ni akina
nani?Umemjulisha?akauliza Dr
Olivia
“Dr Olivia I have nothing to do
with this.Sihusiki kwa namna
yoyote ile na kitendo hiki cha
kutekwa hadi pale nilipojulishwa
kuwa unashikiliwa na unataka
kuonana nami” akasema Dr
Evans.Bado Dr Olivia aliendelea
kumtazama kwa macho makali
yenye hasira “Wewe ni rais wa jamhuri ya
muungano wa Tanzania una nguvu
na uwezo wa kufanya jambo lolote
lakini kabla ya kuwatuma watu
wako waniteke umejiuliza itakuaje
iwapo baba atagundua kuwa
nimetekwa na serikali?Umetafakari
athari zake? Akauliza Dr Olivia
“Olivia please understand
what I’m saying.I have nothing to
do with this.Waliokuleta hapa
walikuwa na sababu maalum ya
kufanya hivyo,kwa nini
hawajamchukua mtu mwingine ila
wewe?Mahala hapa huwezi
kuletwa bila sababu ya
msingi.Nimeamua kuja mimi
mwenyewe baada ya kusikia kwamba mtu unayeshikiliwa hapa
ni wewe vinginevyo nisingefika
kabisa hapa.Nieleze kile
unachotaka kunieleza ili nione
namna ya kukusaidia uweze kutoka
hapa” akasema Dr Evans
“Nimezoea kukuita baba lakini
leo nitakuita mheshimiwa rais
kukupa heshima unayostahili kama
mkuu wa nchi.Nimekuita hapa nina
jambo la muhimu sana nataka
kukueleza.” Akanyamaza kidogo
akavuta pumzi ndefu na kusema
“Mheshimiwa rais
nimekamatwa na kuletwa hapa
baada ya kuonekana nikiwa na mtu
anayeitwa Seif Almuhsin ambaye
anatajwa kuwa mtu muhimu sana katika kikundi cha IS.Mheshimiwa
rais nataka nikiri kwamba
nilikwenda Kinshasa kukutana na
Seif.” akasema Dr Olivia na sura ya
Dr Evans ikabadilika.Matone
madogo madogo ya jasho
yalionekana usoni pake.Aliingiwa
na hofu kubwa
“Kwa ..kwa..” akataka kusema
kitu akashindwa na kuanza
kukohoa.
“Pole mheshimiwa rais”
akasema Dr Olivia
“Dr Olivia kwa nini ukafanya
hivyo ulivyofanya? Hujui kama Seif
ni mtuhatari sana?
“Ninafahamu hilo mheshimiwa
rais kwamba Seif ni mtu hatari lakini nimelazimika kukutana naye
kwa sababu maalum ambayo
nitakueleza lakini kwanza kuna
kitu nataka nieleze” akasema Dr
Olivia
“Unataka kunieleza nini Olivia?
“Unamkumbuka Edger
Kaka?akauliza Dr Olivia na mstuko
ukaonekana usoni kwa Dr Evans.
“Ed..edger?!! Dr Evans
akastuka sana
“Ndiyo mheshimiwa
rais.Usiniambie tayari umekwisha
msahau” akasema Dr Olivia
“Nimestuka umemuulizia kwa
sababu huyu mtu amekwisha fariki
kitambo.Nini unataka kunieleza
kuhusu Edger?akauliza Dr Evans “Edger alikuwa ni mwanasiasa
kijana ambaye alipendwa na kila
mtu hapa nchini.Alikuwa na
michango mizuri bungeni na
aliwasaidia mno watu wa jimbo
lake.Aliwahi kuibua mambo
makubwa kama vile ufisadi
mkubwa uliokuwa unafanyika
serikalini.Alikuwa jasiri na
hakumuogopa mtu.Alikuwa ni
mbunge kijana ambaye alitarajiwa
kuleta mageuzi makubwa sana
katika siasa za nchi yetu na wengi
walikwisha anza kumtabiria
kwamba alistahili hata kuwa rais
wa nchi.Ni mtu ambaye taifa
haliwezi kumsahau” akasema Dr Evans ambaye alikuwa anafuta jasho
usoni kila mara
“Mr president,I need Edger
kaka back”akasema
Olivia.Kitambaa alichokuwa
amekishika Dr Evans akifuta jasho
usoni kikaanguka.Alipatwa na
mstuko mkubwa.
“You what? akauliza Dr Evans
“Nadhani umenisikia vizuri
mheshimiwa rais.I need Edger
back! Akasema Dr Olivia
akionyesha hana masihara
Dr Evans akavuta pumzi ndefu
halafu akasimama
“Dr Olivia nadhani unahitaji
msaada wa kitabibu.Edger kaka
amekwisha fariki na kuzikwa na kuoza kaburini.Unawezaje
kuniomba nimrudishe mtu ambaye
amekwisha fariki?Am I god? Kama
huo ndio upuuzi ulioniitia hapa I’m
afraid I wont help you and you’ll
die in here.Umeniudhi sana Olivia!!
Akafoka Dr Evans
“Mr President please sit
down.Mimi na wewe bado tuna
mengi ya kuzungumza” akasema Dr
Olivia
“Mengi ya kuzungumza?Kama
hautanieleza kile ulichoniitia hapa
nitaondoka na hawa jamaa
waliokuleta hapa wataendelea
kukukutesa hadi useme
ukweli.Nakupa nafasi ya mwisho ya
kunieleza kile ambacho umeniitia hapa” akasema Dr Evans na kuketi
sofani alikuwa anahema haraka
haraka.Akaokota kitambaa chake
na kufuta jasho usoni
“Please be quick !! akasema Dr
Evans
“Mheshimiwa rais kikubwa
nilichokuitia hapa ni hicho kwamba
namuhitaji Edger Kaka.Bring him
back,I need him,we need
him,Country need him” akasema Dr
Olivia na sura ya Dr Evans ikazidi
kujikunja kwa hasira.Alitamani
amvamie Dr Olivia
“Nashindwa kukuelewa
Olivia.Una akili zako timamu ?
Unawezaje kuniomba nimrejeshe
mtu aliyekufa?Umepatwa na tatizo gani Olivia?Nadhani unahitaji
msaada wa daktari !! akasema Dr
Evans kwa hasira
“Mheshimiwa rais mimi ni
mzima kabisa na sina tatizo lolote
la kiakili.Ninafahamu
ninachokiongea na
ninakimaanisha”akasema Dr Olivia
“Si bure una tatizo
Olivia.Umepata matatizo ya kiakili
unahitaji msaada.Let me help
you.Nitakutafutia daktari mzuri
sana ambaye atakusaidia katika
tatizo hili ulilo nalo” akasema Dr
Evans
“Mheshimwia rais nimekwisha
kwambia kwamba mimi sina tatizo
lolote la kiakili.Nina akili zangu timamu ninakifahamu kile
ninachokisema” akasema Dr Olivia
“Hapana Olivia una matatizo”
“Mheshimiwa rais ninaongea
kitu ambacho nina uhakika nacho
na wewe unafahamu kabisa
kwamba ninachokiongea ni cha
kweli.We both know that Edger
Kaka is not dead.Edger is still alive.I
need him back ! Country need him
back !.Muda wa kuogopa umepita
sasa ni wakati wa vita na vita hivi
havitamalizika hadi pale Edger
Kaka atakaporejea” Akasema Dr
Olivia.Fundo lilimkaba Dr Evans
akamfuata Dr Olivia akamkaba
shingo “I warn you little rat don’t play
with me,I can kill you right now !!
akasema Dr Evans akiwa
amemkaba Dr Olivia shingoni kwa
mikono yake miwili.Akamuachia na
kumsukuma kwa hasira Dr Olivia
akaanguka chini akaanza kukohoa
mfululizo.
“Unajua unazungumza na nani
wewe mtoto?Ninakuonya usicheze
na mimi kabisa ninaweza
kukupoteza !! akasema Dr Evans
kwa hasira
“Kama ulivyompoteza Edger !!
akasema Dr Olivia akiwa amekaa
chini.Dr Evans akazidi kukasirika
na kumsogelea Dr Olivia pale chini “Olivia nani amekuharibu
kichwa chako namna hii? Nani
amekueleza upuuzi huu mkubwa?
Edger kaka amefariki kitambo sana
na amekwisha oza kaburini,nani
amekupandikiza ujinga kwamba
hajafa?
“Edger hajafa mheshimiwa rais
na wewe unalifahamu hilo !!
Akasema Dr Olivia,akainuka na
kukaa.Dr Evans akamtazama Olivia
kwa hasira midomo ilikuwa
inamtetemeka kwa hasira
“Mheshimiwa rais ninafahamu
ninachokiongea na hata wewe
unajua ni kweli ila ni ngumu
kukubali lakini nakuhakikishia
kwamba nina taarifa zote na nimekwisha fanya uchunguzi wa
kina hadi kubaini kwamba Edger
hajafa.Nimeufanyia uchunguzi
mwili ule ambao unasemwa ni wa
Edger na nina uhakika mwili ule si
wa Edger.Hii ina maana kwamba
Edger hajafa na unafahamu mahala
aliko.I need him back.!!akasema Dr
Olivia.Dr Evans hakujibu
kitu,aliwaka hasira.
“Mheshimiwa rais najua suala
hili si rahisi kwako lakini
n……………..”
“Listen to me carefully!!
Akasema Dr Evans na kumkatisha
Olivia
“Sijajua nani amekutuma
kwangu unichafue lakini yeyote aliyekutuma amekosea
sana.Umefanya kosa kubwa
kukubali kutumika Dr Olivia.Huyu
aliyekutuma kwangu amekuharibia
maisha yako na ninasikitika
kukwambia kwamba huu utakuwa
ni mwisho wako,you’ll never see
the sun again.Aliyekutumia katika
jambo hili amekudanganya na
amekuharibia maisha yako”
Akasema Dr Evans kwa ukali.
“Nini hasa lengo lenu la
kunitengenezea kashfa kubwa kiasi
hiki? Lengo ni
kunichafua?Kuniharibia nafasi
yangu ya urais?Nini hasa
mnakitaka wewe na wenzako
ambao mmeamua kutunga uongo huu mkubwa?Dr Olivia umekosea
sana kuamua kujiunga na hao watu
ambao nawaita ni maadui zangu
ambao lengo lao ni kunichafua
mimi.Ninaapa kwamba lazima
niwatafute wote na kuhakikisha
wote wanashughulikiwa
kikamilifu.Dr Olivia ninakufahamu
toka ukiwa mdogo,wewe ni kama
mwanangu,mimi na baba yako
tumekuwa marafiki wakubwa toka
enzi za ujana wetu lakini kwa hili
uliloamua kulifanya sintakusamehe
hata kidogo.Nitakushughulikia
kama ninavyowashughulikia
maadui zangu wengine.I’ll destroy
you Olivia!! Akasema Dr Evans na kugeuka ili aondoke Dr Olivia
akamuita
“Before you go Mr President”
akasema Dr Olivia na Dr Evans
akageuka
“Naomba ufahamu kwamba hii
ni vita.Hata kama ukinipoteza mimi
lakini vita hii itaendelea hadi Edger
apatikane.Mheshimiwa rais ninajua
sintapata nafasi ya kuonana nawe
tena kwani umekwisha nihakikishia
kwamba sintaliona tena jua,kabla
hujafungua huo mlango na kutoka
kwa nini usimpigie simu Coletha na
kujua maendeleo yake? akasema Dr
Olivia.Dr Evans akastuka na
kumfuata Dr Olivia akamkusanya na kumuinua akamgandamiza
ukutani
“Olivia ninaapa kama kuna
jambo lolote litamtokea Coletha
nitakukata kichwa chako!! Akasema
Dr Evans
“J..j..jus call her “ akasema Dr
Olivia.Dr Evans akamuachia Dr
Olivia na kutoa simu yake haraka
haraka akampigia mwanae Coletha
“Dady” akasema Coletha baada
ya kupokea simu ya baba yake
“Coletha nataka uniambie
unaendeleaje?
“I’m not feeling well dady”
akasema Coletha na Dr Evans
akageuka akamtazama Dr Olivia “You are not feeling well?Nini
tatizo?akauliza
“Kulitokea tukio dogo hapa
chuoni,bweni letu lilitaka kuwaka
moto lakini kwa kuwa kuna mifumo
ya kisasa ya utambuzi wa moto
kengele ya dharura ililia haraka
sana na kutuamsha tukakimbia
nje.Kulikuwa na mkanyagano
wakati wa kutoka ndani ya bweni
na mimi nilijikuta nikianguka na
kupoteza fahamu.Kwa bahati nzuri
moto ule uliwahi kudhibitiwa na
haukuleta madhara yoyote”
“Oh thank you Lord.Kwa nini
hukunijulisha Coletha kama kuna
tukio kama hilo? Akauliza Dr Evans “Halikuwa tukio kubwa dady
na lilidhibitiwa haraka sana,chuo
hiki kina mitambo ya kisasa kabsia
ya utambuzi na udhibiti wa
moto”akajibu Coletha
“Coletha naomba kuanzia sasa
kila kitu ambacho kitatokea na
utakachoona si cha kawaida
tafadhali usisite kunijulisha.Vile
vile nitakuongezea ulinzi zaidi,pia
nitamleta daktari maalum wa
kukuhudumia”
“Kwa nini dady unataka
kuniongeza ulinzi? Hawa nilionao
hawatoshi?Kuna tishio lolote la
usalama?Coletha akauliza
“Ninataka kuhakikisha
unakuwa salama Coletha.Usichangamane na watu
usiowajua,usile wala kunywa
chochote hadi daktari wako
athibitishe ni salama”
“Dady mbona maisha yangu
yatakuwa magumu sana?Kwa nini
unafanya hivyo? akauliza Coletha
“Coletha hali ya usalama si
nzuri ndiyo maana ninataka
kuhakikisha unakuwa salama”
“Usihofu baba.Niko salama”
akasema Coletha
“Nataka vile vile kufahamu
katika siku mbili tatu zilizopita
haujakutana na mtu yeyote ambaye
humfahamu akakupa kitu
chochote? Haujakutana na kitu chochote ambacho si cha
kawaida?akauliza Dr Evans
“Hapana dady sijakutana na
tatizo lolote zaidi ya hilo la la tishio
la moto lililotokea”
“Sawa Coletha zingatia hayo
niliyokueleza.Nini
kinachokusumbua kwa sasa?
Akauliza Dr Evans
“Toka lilipotokea tukio lile
mwili wangu hauko sawa ila
nimepatiwa dawa na nimepewa pia
mapumziko” akasema Coletha
“Sawa Coletha kama ukiona
kuna tatizo lolote nijulishe haraka
sana” akasema Dr Evans na kukata
simu
“Is she okay?akauliza Dr Olivia “She’s fine”
“No she isn’t!! She’s
sick”akasema Dr Olivia
“Umejuaje kama anaumwa?
“Sikiliza mheshimiwa
rais,mwanao Coletha amechomwa
sindano yenye virusi ambavyo
nimevitengeneza mimi”
“What?!! Akauliza Dr Evans
kwa mstuko na kumsogelea
“Mwanao Coletha amechomwa
sindano yenye virusi ambavyo
nimevitengeneza mimi na tayari ni
mgonjwa.Dalili za ugonjwa
zimeanza kujitokeza kwa mwili
kukosa nguvu ndani ya siku kumi
na mbili kama hajapatiwa matibabu
atafariki.Virusi hivi ni vipya na vinaua na hakuna bado mwenye
dawa yake zaidi yangu.Ukithubutu
kumpeleka hospitali utamuua
kwani watampa dawa ambayo si
maalum kwa kuwaua virusi
hao.Nilikwambai mheshimiwa rais
kwamba hii ni vita,nimeanza na
Coletha nitaendelea na jamaa
wengine wa familia yako kama
hautakuwa tayari kukubaliana na
ombi langu la kumrejesha Edger
Kaka” akasema Dr
“Aaaghh!! Akapiga ukulele wa
hasira Dr Evans na kumvaa Olivia
akamuangusha chini na kuanza
kumtandika ngumi mfululizo
“How could you…oh God…!! Dr
Evans alichanganyikiwa “No ! That’s not true” akasema
Dr Evans
“It’s true.Binti yako Coletha
amechomwa sindano yenye virusi
na atakuwa mgonjwa wa kwanza
kupata virusi hivi hatari ambavyo
vinaua ndani ya siku chache.I’m the
only one who can save her na
siwezi kumuokoa hadi pale
utakapomrejesha Edger kaka!!
Akasema Olivia.Dr Evans
akamuinua
“Mheshimiwa rais nataka
tufanye makubaliano.Bring back
Edger and I’ll save your daughter”
akasema Dr Olivia.Dr Evans
alimtazama Olivia kwa dakika moja huku akihema haraka haraka
akasema
“Olivia umekosea sana kucheza
na mimi.Binti yangu akifariki dunia
ninaapa nitausafisha ukoo
wako.Nitawaua kuanzia baba
yako,ndugu zako wote huku
ukishuhudia.Kifo cha mwanangu
kitasababisha damu nyingi
kumwagika.Usiku huu Coletha
anapelekwa hospitali kwa ajili ya
uchunguzi na kama akikutwa na
ugonjwa usiku huu huu moto
utaanza kuwaka!! Akasema Dr
Evans
“You take her to hospital you
kill her !! akasema Dr Olivia “Huwezi kunizuia kumtibu
mwanangu.Nitampeleka hospitali
na kubaini virusi unavyodai
kumuambukiza.Nitatumia uwezo
wangu wote kuhakikisha anapona
na njama zako wewe na wenzako
hazitafanikiwa.Olivia I’m sorry this
is the end of the road for
you.Hakuna namna utatoka salama
ndani ya jengo hili.Waliokutumia
hawatakupa msaada wowote”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais unao uwezo
mkubwa wa kumpeleka mwanao
sehemu yoyote kwenda kutibiwa
lakini nakuhakishia kwamba
kamwe hataweza kupata tiba ya
virusi alivyopandikizwa.Nmevitengeneza
mimi mwenyewe na dawa yake
ninayo mimi mwenyewe.Please
don’t kill me because you’ll need
me” akasema Dr Olivia.
Rais Dr Evans alitoka ndani ya
kile chumba akiwa anatiririkwa na
jasho na alionekana
kuchanganyikiwa.
“Mheshimiwa rais” akasema
Devotha
“Devotha I’m going to kill that
woman.Fanya maandalizi na pale
nitakapokupa ruhusa basi auawe
mara moja” akasema Dr Evans
“Nini kimetokea mheshimiwa
rais? Akauliza Devotha lakini Dr
Evans hakujibu kitu “Samahani kwa kuuliza
mheshimiwa rais lakini Happy ni
mtu muhimu sana kwetu kwani ana
mahusiano na Seif Almuhsin wa
kikundi cha IS na vile vile
tunamtegemea aweze kutufungulia
mfumo wetu.Kuna sababu yoyote
kwa nini tumuue?akauliza Devotha
“Devotha utafuata maelekezo
yangu.Nimesema kwamba yaanze
haraka sana maandalizi ya kumuua
Olivia and wait for my call”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais vipi kuhusu
mfumo wetu?Vipi kuhusu
uchunguzi tunaoendelea nao
kuhusu IS?Kuna kila dalili kwamba
Olivia ana mahusiano nao,tukimuua tutashindwa kupata chochote”
akasema Devotha
“Tafuteni namna nyingine ya
kuweza kurejesha mfumo wenu au
wekeni mfumo mpya,Olivia is going
to die !!Mmenielewa? akauliza Dr
Evans na Devotha akaitika kwa
kichwa kisha rais akatoka kwa
haraka kuelekea katika gari lake
akaingia na kuondoka.Kila mtu
alibaki anashangaa kwa
kilichotokea.Hali aliyokuwa nayo
rais baada ya kutoka kuzungumza
na Dr Olivia haikuwa ya kawaida.
Dr Evans akiwa garini baada
ya kutoka katika ofisi ile ya akina
Devotha akampigia simu mwanae
Coletha “Dady” akasema Coletha
“My princess jiandae ninakuja
kukuchukua kukupeleka hospitali”
akasema Dr Evans
“Hospitali?!
“Ndiyo dear.Nataka
kukupeleka hospitali kwa ajili ya
uchunguzi”
“Dady I’m fine.Siumwi sana ni
mwili tu unakosa nguvu lakini
tayari nimekwisha pata dawa”
akasema Coletha
“Coletha tafadhali usinywe
tena hizo dawa.Ninakuja
kukuchukua sasa hivi kukupeleka
hospitali” “Dady you sound strange,is
there any problem?akauliza
Coletha
“Jiandae Coletha ninakuja hapo
sasa hivi” akasema Dr Evans na
kukata simu.jasho liliendelea
kumtoka.
“Michael give me my pills” Dr
Evans akamwambia mlinzi wake
ambaye alimpa dawa katika
kichupa.Haraka haraka Dr Evans
akatoa vidonge viwili akatafuna.
“Are you ok mr
President?akauliza Michael
“I’m fine.Tunakwenda chuoni
kwa Coletha” akasema Dr Evans
halafu akachukua simu na kumpigia
daktari “Mheshimiwa rais” akasema
Dr Stanslaus Mbeula
“Dr Mbeula ninakuja hapo
hospitali na mwanangu ninaomba
nikukute hapo tafadhali,nina tatizo
kubwa nahitaji mno msaada wako”
akasema Dr Evans
“Mheshimiwa rais tayari
nimekwisha toka lakini ninarejea
huko sasa hivi”
“Ahsante sana,tunakuja huko
muda si mrefu” akasema Dr Evans
Devotha na Kaiza wakaenda
katika chumba alichokuwamo rais
na Dr Olivia na kumkuta Olivia
anatokwa na damu mdomoni
“Nini kimetokea
humu?akauliza Devotha “Tafadhali naomba mnirejeshe
katika chumba change nahitaji
kupumzika” akasema Olivia
“Olivia tueleze tafadhali nini
kimetokea humu?Hali aliyotoka
nayo rais si ya kawaida kabisa na
wewe unatokwa na damu nini
kimetokea humu?akauliza tena
Devotha
“Nothing happened.Nipelekeni
katika chumba changu” akasema Dr
Olivia
“Olivia ulitaka kuzungumza na
rais na tukafanya kila tuwezalo
kuhakikisha rais anakuja hapa
ukjaonana naye.Ni wakati wako
sasa wa kutimiza ahadi yako.Please give us back our system” akasema
Devotha
“Nimesema nirejesheni katika
chumba changu.Kila kitu kuhusu
mfumo wenu anacho rais so go ask
him” akasema Dr Olivia
“You gave him the codes?
“Nimewaambia kila kitu
anacho rais.Muulizeni yeye
atawapa maelekezo” akasema Dr
Olivia.Kila mtu alichanganyikiwa
hakuna aliyejua kilichotokea kati ya
Dr Olivia na rais.
“Olivia tafadhali tuweke wazi
kilichitokea humu kwani lengo letu
ni zuri kukusaidia.Maelekezo
aliyotupa rais si mazuri hata
kidogo” akasema Devotha “Najua ameelekeza niuawe
lakini hatathubutu kufanya
hivyo.He needs me so much”
akasema Dr Olivia.Devotha
akaelekeza arejeshwe katika
chumba kilicho chini ya lile jengo
“Mambo ndiyo
yameanza.Sintaogopa kuyatoa
maisha yangu kumpigania Edger
ambaye kitendo alichotendewa ni
cha ukatili mkubwa.Hii haitakuwa
vita rahisi ninapambana na watu
wenye nguvu na uwezo
mkubwa,watu makatili yawezekana
sintaweza kufika mwisho wa
mapambano haya lakini silaha
yangu kuu ni kujiamini na kwenda
na mipango yangu kama ilivyopangwa” akawaza Dr Olivia
akaingia bafuni kuoga halafu
akajilaza kitandani.
“Niliihofia sana siku ya leo,siku
mapambano ya kupigania haki
yatakapoanza.Ninashukuru
nilijiandaa vyema kabla ya
kuanzisha harakati hizi za
kumrejesha Edger.NImeanza
vyema,rais ametoka jasho lakini
naamini haitakuwa rahisi
kwangu,damu itamwagika nyingi
lakini mwisho wa siku lazima
ushindi upatikane.Hapa tayari
nimefika nusu ya safari yangu
nilikotoka si kugumu sana kama
huko ninakoelekea hata hivyo
nitajitahidi kupambana” akawaza Dr Olivia na kuanza kukumbuka
safari yake hadi hapa alipofika.
 

Similar Discussions

13 Reactions
Reply
Back
Top Bottom