Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,809
- 6,081
RIWAYA; NGOMA NGUMU
NA: BAHATI K MWAMBA
SIMU: 0758573660/0624155629
NAIROBI, KENYA…
Kulikuwa na mabishano makubwa ndani ya nyumba moja ya kifahari, katikati ya jiji la Nairobi. Kulikuwa na familia inayoongozwa kwa misingi ya kihuni na ukorofi uliyotukuka. Familia ambayo iliamua kuliteka jiji la Nairobi na kuliweka chini ya himaya yake; rushwa ikiwa ni silaha yao kubwa, pale ambapo vyombo vya usalama huonekana kuingilia mipango yao.
Familia hiyo ilikuwa inaongozwa na vijana watano waliorithi mikoba ya mzee wao, ambae alikuwa anasota gerezani. Vijana nao waliamua kujigawa kiuongozi, kulingana na umri wao; yaani mwenye uongozi wa juu alikuwa ni yule wa kwanza kuzaliwa, kisha uongozi ulifuata kwa waliofuatia.
Wakati wote huwa wanashauriana, lakini mwenye maamuzi ya mwisho ni kaka yao, ambae walipenda kumuita ‘MHISANI’ yaani mwenye nguvu ya kutenda.
Tofauti na siku zote ambapo maamuzi hutolewa kulingana na daraja la umri na, maamuzi ya mwisho hayapingwi, lakini siku hii maelewano yalikosekana ndani ya nyumba. Maelewano ambayo yalitibuliwa na kijana mmoja tu, huku wengine wanne wakiwa wamekubaliana cha kufanya. Wenzake walipojaribu kumsihi asiwe mbishi, alitishia kujiondoa kwenye hilo kundi la kihuni(genge), huku akiwaahidi kuwa, ataitawala Nairobi peke yake na wasije kujaribu kuingia kwenye mgogoro nae, watajuta.
Nyumba ilizizima, ubaridi ukawaingia wenzake. Walimfahamu vema mdogo wao wa mwisho, alikuwa ni mtu wa mipango isiyoshindwa, lakini waliogopa zaidi kwa sababu, ni yeye ndiye aliyekuwa kiongozi wa vijana wote waliokuwa wanawafanyia kazi. Hiyo ilimaanisha, wahuni wote wa Nairobi, walimsikiliza yeye tu na, hata makundi mengine ambayo yaliutaka utawala wa Nairobi, walishindwa kutawala kwa sababu yake. Vijana walimtii na walimheshimu, pia alikuwa amepandikiza vijana wake wengi kwenye makundi mengine na kila kilichopangwa huko, yeye alikijua na kukifanyia kazi kabla, hakijaleta madhara.
Hilo liliwatisha ndugu zake ambao wao walikuwa wanaongoza vitengo vingine kama vile; kukusanya madeni na kukopesha watu, kuingiza na kutoa mizigo ya magendo, kusimamia pesa inayoingizwa na kutolewa kwenye kundi na vitengo vingine vilivyotosha kuongozwa na watu watano.
Iliwatisha zaidi kwa sababu jambo walilokuwa wanabishania, walikuwa wamelipanga na kulifuatilia zaidi ya miaka sita, hivyo mmoja kutaka kujiondoa ilimaanisha, watarudi nyuma tena kwenye utekelezaji.
“Ok! Ugomvi uishe bwana mdogo, hatuna haja ya kugombana huku tukiwa na lengo moja sote. Kaka zako tunakusikiliza, lakini leo ni mara ya mwisho kukubali kukusikiliza, siku nyingine inabidi usikilize amri ya waliokutangulia. Hii si familia ya kambare eti kila mmoja anandevu.” Kiongozi wa familia aliongea kwa mamlaka, huku akiwatupia macho wenzake ambao nao walikuwa wanamtazama mdogo wao kwa hila. Haijawahi kutokea amri ya mdogo ikafuatwa na wakubwa, lakini siku hiyo ilibidi iwe.
“Sina kingine ninachoweza kusema zaidi ya kile ninachokisimamia..” Alinyamaza kidogo na kuwatazama ndugu zake ambao walikuwa kimya wakimsikiliza.
“Vijana wangu hawataweza kuifanya kazi yenu.” Alinyamaza tena na alipotaka kuendelea kuzungumza, alikatishwa na kaka yake mkubwa kabisa, waliemwita Mhisani.
“Kwa nini unasema hawawezi wakati mna kila kitu? Mnasilaha, pesa na ushawishi! Sasa kwa nini kazi hii kwenu ionekane ngumu wakati hadi ramani imepatikana na imebaki kufanyiwa kazi tu?”
“Silaha, pesa na nguvu si mafanikio. Ili tufanikiwe katika hili, tunahitaji kutumia akili nyingi sana wakati wa utekelezaji, pia usiri ikiwa ni nguzo muhimu sana kwenye suala hili”
“Kwa hiyo una maaanisha, kundi lako lote halina watu wenye akili? Litakuwa ni kundi ambalo halina siri?”
“Akili ni jambo moja, usiri ni jambo lingine. Kumbukeni tunawatu wetu na maadaui tunaohumohumo.”
“Kwa hiyo unataka tufanye nini?”
“Hii kazi apewe mtu mwingine kabisa, sisi tubaki wafuatiliaji na watoa msaada kila inapohitajika!” Bwana mdogo alizungumza, lakini wenzake walibaki kumshangaa na wasielewe. Aliendelea kuongea.
“Kwa jinsi jengo lilivyo, inahitaji itumike nguvu kubwa sana ili kufanikisha tunachokitaka, pia itatuchukua muda mrefu sana kupata tunachokitaka na inawezekana kabisa tusikipate kirahisi na tukaishia kurushiana risasi na maofisa wa jeshi. Tusipokuwa makini, tutamfuata Baba Gerezani.”
Ukimya ukapita, kisha mmoja aliyeitwa Amolo aliuliza…
“Kwa hiyo tufanye nini? Kwa maana naona unazunguka tu!”
Mdogo wao aliyeitwa Kamonga, alitoa picha tatu na kuzirusha kwenye meza, kisha alikaa kimya bila kusema kitu, wenzake walibaki wamezubaa na wasijue alimaanisha nini.
Alipoona hawamuelewi, aliwambia..
“Tizameni hizo picha kisha tujadili kinachotakiwa kufanywa kwenye mpango wetu.”
Walizichukua zile picha na kuzitizama kwa umakini mkubwa, kila picha ikiwa imeandikwa jina la mhusika na nchi anayopatikana.
“Una maana gani kutupa picha hizi?” Mhisani alimuuliza.
“Nina maanisha mmoja kati ya hao jamaa anaweza kuifanya hiyo kazi vizuri bila kelele na ikafanikiwa, hivyo tuanze kuchagua na sifa zao nadhani mnazifahamu, maana si wageni kwetu” Kamonga alifafanua.
“Una maanisha kazi hiyo ifanywe na mtu mmoja!?” Mhisani aliuliza kwa mshangao.
“Ili ikamilike ni lazima ifanywe na kichwa chenye kuwaza vema, lakini tukiifanya kwa kutumia nguvu, hakuna tutakachoambulia kabisa!”
“Duh! Ni vema tuachane na hili jambo!”
“Kama mnataka kuachana nalo, mimi nitalifanya peke yangu na nisiulizwe lolote.”
“Bwana mdogo acha jeuri! Hii ni kwa masilahi yetu wote na kiburi si uungwana hata chembe!” Mhisani alionya.
“Let’s make it brothers!” Amolo aliingilia kati huku akijiweka vema kwenye kiti, kisha aliwatizama wenzake wote ambao walimpa usikivu.
“Hili jambo tulifanye kwa misingi ya sheria zetu!” Alinyamaza kidogo huku akimtupia jicho la husda mdogo wake, Kamonga. Kisha aliendelea.
“Sheria zipo wazi kabisa; endapo jambo litafanywa kwa kulazimishwa na mmoja miongoni mwetu, adhabu yake huwa ni kifo mbele ya jopo letu.” Alinyamaza baada ya kuona Kamonga alitaka kukatisha maelezo yake, alimruhusu.
“Lakini kanuni hiyo inaruhusu jambo hilo kufanyika endapo lililolazimishwa, halitofanikiwa.” Kamonga alifafanua kanuni hiyo.
“Upo sahihi kabisa!” Amolo aliafiki.
“Basi tukubaliane kuteua mmoja kati ya hao jamaa, aweze kutufanyia kazi yetu kwa ufanisi unaohitajika.”
“Basi sawa! Mimi nampendekeza huyo jamaa mwenye sare ya jeshi la polisi.” Amolo alisema huku akiitupa mezani picha aliyokuwa ameshika. Wenzake waliichukua na kuipitisha machoni mwao kwa mtindo wa kupokezana.
“Mh! Sajenti Nyau!?” Tindo ambaye alikuwa kimya muda mrefu, aliuliza kwa mshangao huku akiwatizama ndugu zake, ambao na wao walikuwa wanamtupia jicho la kulikoni. Tindo aliendelea kuzungumza, baada ya wenzake kukaa kimya.
“Huyu jamaa ni ofisa wa jeshi la polisi hapa Kenya, japo hutusaidia kazi zetu kwa ufasaha, lakini sina hakika kama tunahitaji kumkabidhi kazi kubwa namna hii.”
“Kwa nini?” Mhisani aliuliza.
“Kwa sababu ni mtu anaeongozwa na tamaa ya pesa. Anaweza kuuza hata huu mpango kwa wabaya wetu” Tindo alijibu swali aliloulizwa.
“Kwa hiyo unamaanisha tuachane nae?” Amolo aliuliza.
“Kama mtaniunga mkono, tuachane nae!”
“Mimi sikuungi mkono!” Mhisani aliingilia kati. Wenzake walibaki kumtazama, wakingoja maelekezo zaidi.
“Sajenti Nyau ni fundi haswaa! Pia ni mkenya mwenzetu na anatufahamu vema kabisa na hajawahi kutuchoma serikalini. Nikimsifia, sifa zake zitajaa hapa na itoshe kusema tu, Sajenti Nyau anatosha kabisa. Hao mamluki wa nchi za nje, hawatufai kwa sasa!” Alifafanua.
“Hata Mimi naona Sajenti Nyau hatoshi kufanya kazi hii. Hana sifa. Naomba ikipendeza, apewe Gomba, huyo jamaa wa Uganda. Ni profesheno. Anaweza kutuletea hiyo plate.” Atumba, ambae alikuwa ni mkubwa akimfuata Mhisani, alisema huku akiitupa picha ya Gomba mezani. Wenzake walimtazama, walihitaji kumsikiliza zaidi. Aliendelea kusema.
“Kumbukeni tunaenda kuiba Benki. Na hatuibi pesa, tunaiba plate namba tano. Na kila mtu anajua hiyo plate ilivyo na umuhimu na namna inavyolindwa. Sasa mtu kama Nyau, ataharibu kabisa, matokeo yake tutaikosa na mipango yetu ya muda mrefu, itakuwa kazi bure.”
“Kwa hiyo unataka kusema Gomba anazosifa za kuweza kuiba hiyo plate?” Mhisani alimuuliza.
“Hakika anaweza, anazosifa zote. Akili,nguvu, ufundi ni miongoni mwa sifa kubwa za Gomba.”
“Vipi kuhusu tamaa, hawezi kutudabo kurosi kweli?”
“Sijawahi kusikia akituhumiwa kwa hilo jambo.”
“Kwa hiyo huna hakika?”
“Hapo kweli sina hakika!”
“Basi tupige kura!”
Wote wanne walikubaliana kupiga kura, lakini wa tano ambae ndiye wa mwisho, alikuwa kimya akiwatizama. Walipiga kura na matokeo yakawa; Nyau kura mbili na Gomba kura mbili, huku Kamonga akiwa hajashiriki kupiga kura, ikatakiwa apige kura, ili kuamua kati ya Gomba au Nyau, ni yupi ambae angelipewa kazi ya kuiba plate namba tano, kwenye Benki ya Umoja.
“Tunaingoja kura yako bwana mdogo!” Mhisani alifoka, huku akimtizama Kamonga kwa macho makali.
“Hao mliowachagua si chaguo langu, bali chaguo langu ni huyu hapa!” Alisema huku akiitupa picha mezani, wenzake waliitupia macho, kisha walimtizama.
“Zuki Gadu!?” Amolo aliuliza kwa mshangao.
“Yes, huyohuyo. Huyo ndiye anaeweza kuifanya kazi hii. Mwenyewe hupenda kuijiita Miguu ya kuku, akipita haachi nyayo, wala sauti ya vishindo vyake, haisikiki” Kamonga alisema huku akisimama na kuzungusha shingo yake, mbele ya kaka zake.
“Wewe ulomjuaje huyu jamaa?” Atumba alimuuliza.
“Miguu ya kuku aliwahi kuwa mlinzi wa Baba, hivyo anatufahamu vema, pia anauwezo mkubwa sana wa kufanikisha mambo yake. Anafaa kwa kazi hii” Kamonga alijibu kwa uhakika.
“Sasa mlinzi binafsi ataweza kweli kashikashi za serikali? Unatushangaza bwana mdogo” Mhisani aliongea bila kuficha wasiwasi wake.
Ulikuwa mtihani mkubwa, majina matatu mezani, lakini lilihitajika jina moja tu ili kazi ifanyike. Kazi nzito na ya hatari. Ilihitajika plate namba tano kutoka Benki ya Umoja, Benki yenye ulinzi kuliko Benki zote ndani ya jiji la Nairobi.
Hakika ilikuwa ngoma ngumu
...
Mwandishi; Bahati Mwamba.
Simu; 0656741439/0758573660/0624155629.
ENDELEA KUWA NAMI