Riwaya: Mchezo Mchafu

Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
70
235
Riwaya
Kwa usiku ule nyumba aliiona kubwa sana kulala peke yake tena akiwa katika hali ya kuvurugwa kutokana na yote aliyokutana nayo kwa siku ile. Alijiinua kivivu na kuelekea chumbani akajilaza kitandani akijaribu kuubembeleza usingizi ambao hata hivyo ulimkatalia katakata.

Alikata shauri na kuingia bafuni kujimwagia maji walau kuupa mwili wake ahueni ya uchovu, baada ya kuoga walau mwili wake sasa ulipata nguvu mpya ikimpotezea kiasi uchovu aliokuwa nao, lakini kichwa bado kilikuwa kizito kwa mawazo. Ghafla kama aliyezinduka, aliamua kuvaa nguo na kutoka na gari lake akiwa hajui anakoelekea.

Akiwa na gari lake alikatisha maeneo ya Sinza Palestina ambako kwa karibu aliiona Bar ya rafiki yake itwayo ‘Twiga Bar’, eneo la mbele la Bar ile kuna jiko la vyakula mbalimbali vikionekana katika kabati kubwa la vioo vikiwa vimepangwa katika namna inayovutia huku vikimulikwa na taa yenye mwanga mkali, na ndipo alipokumbuka kwamba alikuwa hajala kwa siku nzima tangu alipokunywa chai asubuhi, na ghafla tumbo nalo likajieleza, alianza kuhisi njaa kali na kiu.

Alilisogeza gari lake mbele ya Bar ile na kuegesha vizuri kisha alishuka na kujisogeza mbele ya meza moja wapo iliyo karibu na ‘Counter’ muhudumu mmoja alikuja na kumsikiliza.

Naweza kupata mchemsho wa samaki wa maji baridi?” aliuliza Danny baada ya kukaribishwa.

Mchemsho upo wa samaki sato!

Naomba haraka tafadhari, usisahau ndimu na pilipili!” alijibu Danny huku akigusagusa simu yake kuangalia vitu fulani.

Sawa, nikuletee na kinywaji gani?

Niletee na ‘Castle Lite’ mbili za baridi”

Wastani wa dakika tano akisubiri chakula alichoagiza huku akitafakari masahibu aliyokutana nayo kwa siku ile, punde chakula kilifika na kuanza kula huku akishushia na funda za bia ya baridi aliyoagiza.

Alimaliza chakula na kuendelea kuagiza bia moja baada ya nyingine huku muda ukizidi kuyoyoma na giza la usiku likizidi kukomaa huku wateja wakizidi kupungua katika Bar ile ikielekea saa saba za usiku sasa. Pamoja na kunywa bia nyingi akiagiza kila chupa ilipoisha, lakini hakuonesha dalili za kuzidiwa na ulevi, alionekana kuizoea bia aliyoagiza.

Kwa muda wote aliokaa katika Bar ile, alionana na baadhi ya watu anaojuana nao na baadhi yao aliwaagizi vinywaji kwa kadri walivyohitaji huku yeye akiwa ndiye mlipaji. Hakuwa amejiandaa kwa matumizi hayo makubwa kwa vinywaji, ndani ya pochi yake ya kuwekea pesa kulikuwa na kiasi kidogo cha shilingi elfu tisini tu ambacho chote kiliisha kwa kulipia bili za marafiki na wahudumu ambao nao waliomba kununuliwa vinywaji na vyakula.

Akili yake ilizama zaidi katika kumfikiria Chiku na mambo aliyokutana nayo kwa siku ile, hivyo kila aliyemsalimia na kumuomba kinywaji hakumkatalia.

Wakati muhudumu alipoleta bili ya vinywaji alivyotumia, Danny alijipekuwa katika pochi yake na kujikuta na zile shilingi tisini elfu tu huku akipungukiwa na jumla ya shilingi themanini na tano kutimia shilingi laki moja na elfu sabini na tano alizotumia kwa ujumla.

“ …Brother kama vipi acha funguo ya gari utakuja kuikomboa kesho” meneja wa Bar ile bwana Shirima aling’aka kwa lafudhi ya kichaga baada ya muhudumu kumjuza.

Unasemaje wewe, yaani niache gari langu kwako kwa ajili ya shingi elfu themanini tu?!” Danny naye alijibu kwa jeuri akionesha dharau, kisha maneno mawili matatu yalipita kati yao na kuzua zogo dogo ambalo hata hivyo Danny alilimaliza kwa kugundua kosa alilolifanya na kujionya awe mpole ili kupusha jinamizi la shari ambalo limeonekana kumwandama tangu asubuhi ya siku hiyo.

Siyo kesi, meneja tulia tuyaongee kama vijana tuyamalize kianamume” alisihi Danny.

Sasa hayo ndio ya kuongea lakini sio kuleteana dharau kwenye kazi bhana” Shirima naye alijibu huku akionesha kushusha jazba aliyokuwa nayo huku akionekana kusaidiwa na uzoefu wa kusimamia Baa aliokuwa nao kwa miaka kadhaa.Sasa sikia, hiyo pesa kesho asubuhi nitakuja kuilipa, kwa leo nitakuachia hii simu yangu ya ‘Smart’ ina thamani ya shilingi laki sita za kitanzania” Danny aliongea kwa kujiamini huku akiandaa simu kwa kuikabishi kwa meneja. Kwa ofa ile meneja Shirima hakuwa mkaidi, alikubali na kukabidhiwa simu akiihifadhi mfukoni mwake katika suruali ya ‘Jeans’ aliyovaa.

Danny aliona amefanikiwa kuizima shari nyingine iliyokuwa ikimnyemelea kama mwendelezo wa masahibu yaliyomsibu kwa siku ile, kumbe hakujua kwamba ndiyo alikuwa akisaini mkataba rasmi wa kuingia katika misukosuko ya kidunia iliyobadili maisha yake yote na kumwachia majuto yasiyoelezeka.----​Baada ya Danny kukabidhi simu na kuondoka zake kuna baadhi ya wateja walibaki wakimalizia vinywaji vyao. Mmoja kati ya wateja wale alionekana kuelemewa na pombe kiasi, aliinuka kutoka alipokuwa na kwa mwendo wa kuyumbayumba alienda moja kwa moja mpaka mbele ya ‘Counter’ ya Baa ile na kumkabili meneja Shirima.

We fala, ebu funga Bar yako umruhusu mke wangu niondoke naye, au unataka kwenda kumlala wewe?!

Aliongea katika sauti ya kilevi lakini akionekana kuzoeana na meneja Shirima ambaye hata hivyo hakujibu kitu licha ya kumuona na kumsikia mteja yule, zaidi ngozi yake ya usoni ilijenga mkunjo kuashiria kutofurahia aidha uwepo wa mteja yule pale mbele yake au vile alivyoitwa ‘Fala’ huku akiamuriwa kuifunga Bar yake eti ili mlevi mmoja aweze kuondoka na muhudumu wake.

We bwege, mimi si naongea na wewe, au unaniona mlevi, mimi sijalewa kwa taarifa yako” mteja yule aliongeza kauli nyingine katika namna ileile ya awali ambayo kwa sasa ilifanikiwa kuufungua mdomo wa meneja Shirima.

Dah, nimekusikia Afande ngoja kidogo tunakamilisha masuala ya kiofisi mtaondoka tu usiwe na wasiwasi!” Shirima alijibu kinyonge akionesha wazi kumgwaya yule mteja aliyemwita kwa jina la Afande.

Aaaaah, wee Fidea mimi natangulia kwenye gari utanikuta!” mteja yule aling’aka nakuondoka kwa dharau kuelekea kwenye maegesho ya magari kwa mwendo uleule wa kuyumbayumba kwa kuzidiwa na ulevi.

Alijongea na kufanikiwa kufika katika gari alilokusudia, akajipapasa mfukoni na kuutoa ufunguo alioutumia kuufungua mlango wa lile gari na kujitosa ndani yake na punde akaliwasha na kuliacha likiunguruma akimsubiri Fidea wake waondoke. Wastani wa dakika tatu tu, alipiga honi za fujo kumhimiza Fidea aje waondoke, alirudia kupiga honi za fujo kila baada ya dakika kadhaa.Honi zile zilizidi kumkera Meneja Shirima ambaye alikuwa akiongea na Fidea huku akionekana kukasirishwa na uwepo wa mteja yule na vitendo vyake. Ni wazi Meneja Shirima alijuwa kwamba mteja yule ni aina ile ya wateja ambao hukaa katika Bar mpaka muda wa kufunga akisubiri aondoke na muhudumu, anafahamu wengi wa wahudumu wa Bar hawategemei mshahara mdogo wanaopokea kwa mwezi bali huongeza kipato chao ili kumudu ukali wa maisha kwa kushiriki biashara haramu ya ngono na wateja wakware kama huyo afande anayemsumbua.

Ni wazi, alitamani kumzuia Fidea asiondoke na yule mteja, lakini alionekana kumgwaya kwa kuwa ni askari na alionekana anamjua muda mrefu akija pale Bar kama mteja wa kawaida lakini anamfuata Fidea mpenzi wake.

Yule mteja mkorofi baada ya kuona Fidea anachelewa, aliamua kuiondosha gari kutoka pale eneo la maegesho na kuiweka barabarani kama njia ya kuzidi kumhimiza Fidea.

Sasa ni wakati ule akiirudisha gari yake nyuma bila ya kutazama kwa umakini ndipo aligonga gari dogo lililokuwa likipita nyuma ya gari lake. Alisikia kishindo kile cha kugonga kitu, alipoinua shingo kutazama kupitia kioo cha nyuma aliona aliona gari nyingine ikiwa nyuma yake, kwa akili za kilevi zikamwambia kwamba ni yeye ndiye amegongwa, alishuka kwa hasira huku akitukana matusi mazito kwa dereva wa gari lile jingine.

Kuona vile, dereva wa gari lile jingine naye hakuwa mnyonge, alijibu mitusi ile huku akijiandaa kwa lolote dhidi ya yule mteja wa Fidea, yaani kama ni ngumi basi alikuwa tayari kuzichapa, kwa nini awe mnyonge wakati ni yeye ndiye amegongwa?

Tofauti na dereva yule wa gari jingine alivyotegemea, yule mteja wa Fidea licha ya kuwa sehemu ya akili yake inaongozwa na pombe lakini alikuwa akijitambua, badala ya kuzikunja ngumi kama kasi aliyokuja nayo kushuka kwenye gari lake ilivyoashiria, mikono yake miwili ilenda nyuma ya mgongo wake eneo la kiunoni na kuinua fulana ndefu aliyovaa na kisha kuibuka na bastola akiielekeza moja kwa moja kwa yule dereva wa gari jingine.

Yule dereva anaijua bastola, na hasa alipoona ipo mikononi mwa mtu anayeendeshwa na pombe, alirudi nyuma na kusimama mikono yake ikiwa juu huku mwili wake ukitetema kwa woga.

We K…… ntakumwaga ubongo wako sasa hivi, kwanini umegonga gari langu, unajua thamani yake hili?”

Basi brother, ss….sama…hahani naomba nisamehe ilikuwa ni bahati mbaya tu, nitakutengenezea gari lako kwa gharama zangu”

Bastola inatisha, asikwambie mtu, jamaa ilibidi akubali kosa ambalo hakulitenda ili mradi tu anusuru uhai wake dhidi ya hasira za mlevi.

Nani brother wako hapa, au unadhani ‘Toy’ hili? Mteja yule wa Fidea licha ya kuombwa msamaha hakupoa, alitaka kumthibitishia yule dereva wa gari jingine kwamba aliyoishikilia mkononi ni bastola ya ukweli na wala sio ‘Toy’ la plastiki, alifyatua kitunza usalama na kuielekezea juu na kisha kufyatua risasi moja hewani.

Sauti ya mlipuko wa risasi kwa nyakati zile za saa saba za usiku iliwatisha na kuwavutia watu wachache waliokuwa eneo lile kuangalia upande ule wa maegesho ya magari kutaka kujua kulikoni, wengi kati ya watu wale wachache walidhani ni tukio la ujambazi linafanyika hivyo hakuna aliyethubutu kujisogeza eneo lile mpaka walivyomuona meneja Shirima anaelekea eneo lile na kuanza kumsihi yule mteja wake aliyekuwa bado ameshikilia bastola mkononi.

afande, ebu shusha kwanza hiyo bastola, haya yanazungumzika, gari lako halijaumia, limechubuka tu rangi kidogo” afande yule mteja wa Fidea ni kama aliyekuwa ana subiri wa kuja kumsihi au kumbembeleza, alishusha bastola yake na kuirudisha mafichoni nyuma ya mgongo eneo la kiuno akiipachika kwa msaada wa mkanda wa suruali ya ‘jeans’ aliyokuwa ameivaa.

Meneja Shirima alikagua harakaharaka na kuthibitisha hakuna uharibifu mkubwa katika gari la mteja wake Afande licha ya kuwa ni yeye ndiye aliyemgonga mwenzie, ni gari la yule dereva mwingine ndilo liliharibika kwa kubonyea na kubanduka ‘bampa’ la nyuma lililobaki likining’inia na kuharibu mwonekano mzuri wa gari lile aina ya ‘Nissan Morano’.

Licha ya kujitambua wazi kwamba yeye hakuwa na makosa yoyote katika ajali ile ndogo, yule dereva wa gari jingine alikubaliana na suluhu iliyosimamiwa na meneja Shirima kwa kumtaka alipe kiasi cha shilingi laki tano ambazo kwa bahati nzuri alikuwa nazo ili kumfidia afande ambaye rangi ya gari lake ilionekana kuchubuka baada ya kuikagua kwa kuimulika kwa mwangaza wa tochi ya simu.

Hatma ya dereva yule aliruhusiwa kuondoka zake baada ya kuliegesha ‘bampa’ lililong’ooka.

Sasa walibaki watu wanne tu pale kwenye maegesho, yeye Shirima, Afande, Fidea na mlinzi wa Bar ile ambao kwa pamoja walisogea eneo lile baada ya kuonekana mambo yamedhibitiwa na maneja Shirima.

Fidea ingia kwenye gari twende zetu, hapa pameshaharibika” bila ya kushaurian na yeyote mteja Afande alimuamuru muhudumu Fidea.

Sawa Afande, Fidea utaondoka naye lakini kwa usalama wako haitokuwa hekima wewe kuendesha gari kwa hali uliyokuwa nayo” Meneja Shirima alisihi tena kwa sauti ya ileile ya kichaga iliyojaa unyenyekevu.

Sasa unataka nani aendeshe badala yangu?” Afande akionekana kuafiki ushauri wa Meneja Shirima aliuliza.

Mimi nitakuendesha mpaka nyumbani kwako, nitawaacha hapo kisha nitaondoka na bodaboda kwenda kwangu

Afande kwa mara nyingine aliafikiana na mawazo ya meneje Shirima, sasa alijitosa kiti cha nyuma akiungana na Fidea aliyemfuata huko na meneja Shirima alikaa nyuma ya usukani wa gari lile. Sasa meneja Shirima alionekana kama dereva wa tax aliyeodiwa na wateja wake. Mlinzi wa Bar ile alibaki eneo lake la kazi wakati akiliangalia gari la afande likiondoka eneo lile.

Fidea akiwa pale siti za nyuma na Afande alionekana kama ana jambo lake na meneja Shirima ambaye licha ya kuingilia ule ugonvi na yule dereva na sasa kuamua kuwaendesha Fidea na Afande wake hakuonekana kufurahia yote yaliyokuwa yakifanyika, ilikuwa ni kama anayafanya afanyeje tu.

Nyumba anayoishi Afande mteja wa Fidea ipo maeneo ya Manzese Tiptop nyuma ya hotel maarufu iitwayo Moshi Hotel, kwa usiku ule iliwachukua mwendo wa wastani wa dakika kumi tu kufika nyumbani kwake, lakini baada ya kufika waligundua yule mteja Afande hakuwa na ufunguo wa mlango wa nyumbani kwake, ni aidha alikuwa ameusahau pale Bar alipokuwa akinywa wakati akimsubiri muhudumu Fidea au atakuwa amedondosha mahala asipopajua.

Wakati wakijadili hayo yule mteja Afande alionekana kuzidiwa na kuelemewa na usingizi kiasi hata wazo la kurudi Twiga Bar kuitafuta funguo yake hakuliafiki, aliruhusu mlango wake uvunjwe ili yeye na mpenzi wake Fidea waingie wakalale mengine wangeyarekebisha kesho panapo majaaliwa.

Kazi ya kuuvunja mlango ilifanywa na Shirima wakati yeye Afande aiwa amejilaza ndani ya gari kusubiri afunguliwe mlango akalale. Kwa kuwa hakuwa amejiandaa na dhana yoyote kurahisisha kazi ile, Shirima alichukua takribani dakika kumi kufanikisha zoezi lile akitumia ‘wheel spanner’ aliyoichukua kutoka kwenye buti la gari lile la Afande.

Wakati wakifanikiwa kufungua mlango ule baada ya kuuvunja tayari Afande alikuwa akikoroma ule mkoromo wa kilevi pale kwenye viti vya nyuma vya gari yake ndogo. Kwa meneja Shirima kitendo cha Afande kulala ilikuwa ni kama vile bahati mbaya ambayo aliisubiri baada ya kuitarajia kwa muda mrefu tangu wakiondoka kule Twiga Bar Sinza.

Hakulaza damu, alinong’ona jambo na Fidea ambaye aliafiki japo kwa hali ya kutokujiamini na wanalotaka kulifanya. Shirima kwa kutumia mikono yake alimvuta Afande kutoka kwenye zile siti za nyuma ya gari, na alipokuwa akimvuta ili kuweza kumbeba ndipo alipogundua tayari jamaa alikwishaumwaga ndani ya gari tena wenyewe ule wa mlevi wenye harufu kali ya pombe huku suruali yake ya Jeans ikiwa chapachapa. Lakini Shirima hakujali aliivumilia hali ile na kumbeba mpaka ndani ya chumba chake kimoja cha uani alichokuwa amepanga na kumbwaga juu ya kitanda chake kilichoenea vizuri chumbani pale.

Shirima anawajua vizuri walevi kwa uzoefu aliokuwa nao akihudumia Bar nyingi kama meneja. Baadhi ya wateja wake waliowahi kuzidiwa na pombe na kisha kuchukuliwa na usingizi huchukua muda mrefu kuja kuamka. Na usingizi wa mlevi ni usingizi wa robo tatu ya kifo, akishalala hata umfanyaje hawezi kuamka mpaka pombe itakapomtoka na akili yake kurejea katika hali ya kawaida ndipo huamka.

Aliona hiyo sasa ndiyo fursa ya dhahabu kwa yeye kufanya jambo lake na muhudumu wake Fidea ambaye alikwishapanga naye muda mrefu kwamba leo wangefanya tendo la kustareheshana miili yao lakini mipango hiyo ilikuja kutibuliwa na ujio wa huyu Afande Sadock ambaye alijijengea ufalme wa wazi kummiliki muhudumu Fidea kama mpenzi wake.

Jambo moja ambalo Afande Sadock alikuwa halijui kuhusu Muhudumu Fidea ni kwamba yeye alikuwa ni mpenzi wa muda mrefu wa meneja Shirima ambaye hata hivyo kazi ya uhudumu kwenye Baa ile ya Twiga ni yeye ndiye aliyemsimamia kuhakikisha anaipata na kupokea malipo mazuri tofauti na wahudumu wengine.

Kwa ajili hiyo alijijengea utamaduni wa kwamba kila anapomuhitaji kimapenzi basi bila ya pingamizi huondoka naye baada ya kufunga Baa.

Uhusiano wa Afande Sadock na Fidea uliibika kibabe sana baada ya Afande Sadock na timu yake ya baadhi ya maaskari wa kituo cha polisi Sinza kuwakamata huyo meneja Shirima na wahudumu wake kwa madai ya kufanya biashara nje ya muda unaoruhusiwa kisheria. Salama yao kujiepusha na usumbufu huu ilikuwa ni kutumia pesa kwa kuwapa kila wanapokuja na ndipo Afande Sadock alipotumia mwanya huo kuanzisha mahusiano na Fidea baada ya kuvutiwa naye.

Sasa mahusiano ya Fidea na Afande Sadock ni mahusiano ambayo yanamuumiza meneja Shirima lakini kwa sababu za kibiashara analazimika kuyavumilia na kuyaacha yaendelee huku moyoni akiumia na hasa kila anapomwona Afande Sadock amekuja, jambo ambalo yeye Afande Sadock hakuwahi kulijua.

Hivyo kwa hali aliyokuwa nayo kimwili akiendeshwa na ashki zilizompanda muda mrefu aliamua kuitumia fursa hiyo kwa kufanya mapenzi na Fidea palepale katika kitanda cha Afande Sadock mwenyewe akiwa amelala akikoroma pembeni hoi hajiwezi kwa usingizi wa pombe.

Kwa kutarajia angemaliza tendo lile haraka, meneja Shirima hakuwa na mambo mengi, alishusha nusu mlingoti suruali yake mpaka sehemu ya magoti na kuanza kustarehe na Fidea wake huku akimdhihaki Afande ambaye bado alikuwa akikoroma mithili ya aliyemeza dawa za usingizi.

Starehe ya tendo iliwazidia wote wawili, kiasi cha Fidea kuishia kutoa miguno na kelele za mahaba bila kujijua, kuashiria kufurahia huduma aliyopewa na bosi wake meneja Shirima. Kelele zile zilizidi kuongezeka kadri ya muda ulivyozidi kwenda na hata Shirima kulazimika kutumia mkono wake mmoja kufunika mdomo wa Fidea kuzuia sauti isisambae kuhofia kumuamsha babu Jinga aliye lala pembeni yao.

Katika yale maajabu saba ya dunia pengine ilisahaulika tu, yamkini starehe ya tendo ilipaswa nayo kuingia kuwa ni ajabu mojawapo na kusomeka kama maajabu nane na si saba ya dunia. Ni kwa sababu tu tendo huwa na nguvu mbele ya yeyote mwenye nguvu akaonekana dhaifu, humfanya mwenye akili kuonekana zuzu asiyefaa, humfanya aliye makini kuonekana mzembe, wakali huwa wapole na wapole nao huwa wakali na hata makatili wakubwa.

Lakini pia humfanya mwenye kumbukumbu kuwa msahaulifu kama ilivyomtokea meneja Shirima ambaye sasa alikwishajisahau kwamba sehemu aliyokuwepo akifurahia tendo na Fidea wake haikuwa salama kwake, kwake Fidea ndio kabisaa, kelele za utamu alizokuwa akipiga utadhani alimeza ‘amplifier’ mbili tumboni mwake, akili yake haikuwa na muda wa kufikiri kuhusu Afande Sadock, tangu alivyothibitisha kwamba amelala na jinsi anavyomjua akishalala ni mpaka kesho tena.

Ni bahati mbaya sana siku huwa hazifanani, mseto wa kelele na miguno ya muhudumu Fidea, mtikisiko na kelele za manung’uniko ya kitanda na upepo wa kibaridi cha alfajiri uliokuwa ukipenya kupitia mlango ulioachwa wazi kwa makusudi na meneja Shirima vilimzindua Afande Sadock kutoka usingizini.----​

Ilikuwa mida ya karibia na saa kumi alfajiri alipozindukana, hakuwa ameishiwa na usingizi hasa, akili yake bado ilikuwa na mawenge ya usingizi mzito wa usiku wa manane ambao bado ulikuwa haujamwisha.

Huwa si kawaida yake kuamka muda huo, lakini sababu ya zile pilikapilika za kwenye kitanda chake zilimlazimisha kuamka kujua kulikoni.

Japo chumba chote kilikuwa giza lakini kwa msaada wa mwangaza hafifu kutoka nje kupitia mlango uliokuwa wazi, meneja Shirima aliweza kuona mwili wa Afande Sadock ukijigeuza huku mikono yake ikitumika kufikicha macho ili kuyapa nuru ya kuweza kuona yale yanayotokea ndani ya chumba chake.

Mwanzo hakuiamini akili yake, alihisi kama anaota, na kile anachokisikia ni mapichapicha tu ya ndotoni na hasa akijijua kwamba pombe zilikuwa bado hazijamwisha.

wewe nani?” Afande Sadock huku mdomo ukiwa bado mzito kiasi aliuliza kama anaita ili kuhakiki kama bado yupo ndotoni au lah. Lakini badala ya kujibiwa alistushwa na alichokiona kama taswira ya mtu akichomoka kutoka kitandani pale huku akishikilia suruali yake kujaribu kuifunga akikimbia kupitia ule mlango uliokuwa wazi na kutokomea zake nje.

Nyumba ile ilikuwa imejengwa kwa ule mtindo wa herufi ‘L’ ambapo baada ya kutoka hakupata upinzani wowote zaidi ya kuelekea vichochoro vilivyokuwa karibu na kutokomea zake gizani bila kutazama nyuma.

Afande alitaka kuinuka kutoka pale kitandani lakini hakuweza, alihisi kama amevutwa na mtu ili abakie pale kitandani, bado hakuwa na nguvu ya kushindana na mwili wake mwenyewe uliomkatalia kuinuka, bado mipombe aliyogida pale Twiga Bar ilikuwa ikiuadhibu mwili wake. Aliamua kutulia pale kitandani akijaribu kutafakari kile alichokiona akijiuliza ni mtu, kibwengo au ni taswira tu ya mtu iliyojijenga akilini mwake. Alikuwa ni kama anayebishana na akili yake iliyokuwa ikimuhakikishia kwamba alichokiona ni mtu halisi na wala si kitu kingne.

Akili yake ghafla ikahamia kwenye ule mlango wa chumba chake ambao bado ulikuwa bado uko wazi.

Kama niliyemuona si mtu basi ni nani aliyeufungua mlango huu, ina maana nimelala mlango wazi?

Alianza kuoanisha ile hali ya mlango kuwa wazi na kile alichokiona sehemu kubwa ya akili yake ilizidi kumuhakikishia kwamba aliyemuona ni mtu na ndiye hasa aliyefungua ule mlango.

Sasa iliku ni majira ya saa kumi za alfajiri, kadri muda ulivyozidi kwenda ndipo akili yake ilivyozidi kutengemaa, pombe ikimtoka kichwani na kumbukumbu nazo zikaanza kumrejea, na ndipo alipokumbuka kwamba mara ya mwisho alikuwa na muhudumu Fidea aliyetoka naye Twiga Bar na kuja naye nyumbani akiwa sambamba na meneja Shirima, kila alipoivuta kumbukumbu ni wapi waliachana na meneja Shirima hakuipata.

Hapo akili yake ikamuelekeza kukidadisi kitanda chake na ni hapo ndipo alipomwona muhudumu Fidea akiwa amelala fofofo akigeuka upande mwingine akimpa yeye mgongo.

Kumuona Fidea pale kitandani kulimzidishia kuzipuuza zile hizia zilizokuwa zikimdhihaki akilini mwake kwamba aliona mtu akitoka pale chumbani kwake yalikuwa ni mawenge tu ya usingizi wa pombe, na hata kuhusu mlango alijishawishi kuamini kwamba yawezekana ni kwa sababu ya uchovu wa Fidea kuhudumia siku nzima Bar walijisahahu kuufunga usiku ule walivyorudi.

Alijaribu tena kuinuka pale kitandani, safari hii aliweza, tayari pombe zilizidi kumwachia mwili wake, aliuendea mlango na kuchungulia kwa kutoa kichwa nje kisha akafunga, akajijongeza kwa msaada wa ukuta mpaka ilipokuwa swichi ya taa, akawasha taa na kumwangalia Fidea tena, akamshuhudia akiwa amelijalaza pale kitandani akiwa uchi, akaamini kwamba pengine alijilaza hivyo makusudi kwa ajili yake, kumbe hakujua tu, Fidea tangu alipokatishwa starehe ya tendo na bosi wake Shirima aliyefyatuka kutoka mwilini mwake na kutokomea zake nje, hakupata nafasi ya kujifunika akiigiza kuzama usingizini huku moyo ukimwenda mbio akihofia kama afande Sadock ameshuhudia mchezo wake na Shirima.

Hamu ya tendo ikampanda Afande Sadock, ashki zikamtawala na hasa alipokumbuka tena kwamba jana alilazimika kumsubiri Fidea mpaka usiku wa manane kwa ajili hiyo, akazima taa na kujisogeza kwa Fidea wake ili aanze kuicheza ile ngoma ya kikubwa aliyokusudia kuicheza.

Alimsogelea Fidea na kuanza kumtomasa hapa na pale katika mwili wake ulioumbika vizuri, Fidea naye akazuga kuamka kutoka usingizini na kuanza kutoa ushirikiano na yeye alijibu mapigo kwa kumpapasa Afande Sadock sehemu zile zisizozoea kushikwashikwa, na mara vinywa vyao vilikutana.

Lakini kabla ule mchezo haujakolea zaidi Afande alipitiwa na kumbukumbu ya jambo fulani ambalo ghafla lilimpotezea hisia zote alizokuwa nazo, kisha kwa sekunde mbili au tatu akiwa bado amemkumbata Fidea pale kitandani akaganda bila kufanya lolote kama anayesikiliza jambo au kitu alichokisikia awali, sasa anasubiri kijirudie tena ili akisikie kwa uhakika.

Kuna jambo zito alilolikumbuka lililopiga shoti ubongo wake, ni ile bastola yake. Kisha kama cheche ya moto wa mkaa alilipuka kutoka kwenye mwili wa Fidea bila kujali giza la chumbani pale. Moja kwa moja aliishia katika kupapasa ukuta na hatimaye aliipata tena ile swichi ya taa na kuwasha. Macho yake yaliishia kwenye suruali yake iliyokuwa sakafuni, aliipekua hakuiona bastola yake.

Hakujua ni wakati gani mwili wake ulianza kutoa jasho, aliloa mwili mzima kama aliyemwagiwa maji.

kwani vipi mwenzetu, umepoteza nini? Aliuliza Fidea ambaye muda wote baada ya taa kuwashwa alibaki kitandani akimshangaa aliyepotewa na utulivu aliendelea kutafuta kitu.

Bastola”, afande alijibu kwa ufupi.

bastola imefanya nini” safari hii Fidea alijibu huku akiinuka na kukaa pale kitanzania huku macho yakimtoka kwa mshangao, hakujibiwa, jamaa aliendelea kuitafuta silaha yake, sasa alikuwa ameinamisha mgongo akiangaza sakafuni chini ya kitanda.

Katika hali iliyomshangaza pale chini ya kitanda, zaidi ya chupa za pombe mbalimbali na maji ya kunywa zilizokwishatumika, pia aliona kitu kingine asichokitarajia, Simu Janja aina ya ‘Samsung’ ambayo hakujua ni ya nani.

Hii simu ni ya nani?” aliuliza huku akiwa ameishika mkononi akiikagukagua.

Mh, makubwa leo, we Sadock simu ipo chumbani kwako wewe halafu unaniuliza mimi eti ni ya nani, ntajuaje mie?”

Jibu lile lilimkatisha Afande Sadock hamu ya kuuliza tena, alikwishajua simu si ya Fidea, sasa alibaki na swali akijiuliza ni ya nani?

Swali hili lilimuongezea hofu ya kupoteza silaha yake hasa alipokumbuka lile tukio aliloamini kuliona la mtu kutoka chumbani mwake na baadae kuuona mlango wake ukiwa wazi, kiasi alianza kuunganisha matukio, sasa aliamini yule alikuwa ni mtu kweli, mwizi, na ndiye atakayekuwa amechukua bastola yake na pengine ndiye mwenye simu ile akiiangusha wakati ule alipokuwa akikimbia, kiasi alijilaumu kwa uzembe uliosababishwa na pombe alizokunywa usiku wa jana pale Twiga Bar.

Muda wote akihangaika kuitafuta silaha yake alisumbuliwa na ujinga mwingine, alijitahidi kwa nguvu sana kuificha ile hali ya woga na kukata tamaa aliyokuwa nayo isionekane kwa Fidea, hakuweza, japo nafsi yake ilimdanganya kwamba amefanikiwa, Fidea alishuhudia namna afande alivyonywea kwa woga uso ukimsawijika akionekana kuzidiwa na mambo.

Kiasi alihisi ahueni alipokumbuka kuhusu gari lake lililopo nje, alivaa bukta na kuufungua mlango uliokuwa umefungwa na komeo tu ya kawaida na kisa kutoka nje kuelekea kwenye gari akiamini huenda aliidondosha huko. Ufunguo wa gari yake ulikuwa juu ya stuli yake ndogo iliyokuwepo chumbani pale.

Tayari mwangaza wa asubuhi ulianza kutawala, ukilisukumia mbali lile giza zito la usiku, afande Sadock aliitarajia faraja kwa kukiona kile alichokuwa akikitafuta, lakini haikuwa hivyo, alichokiona kilimuongezea tena pigo kiasi cha kujihisi kama njia zote za haja zikimlegea. Gari lake lilikuwa limevunjwa kioo, hali iliyomtangazia kwamba asitarajie kukuta kitu chochote cha maana ndani ya gari lake, na ndivyo ilivyokuwa.

Alifungua mlango wa mbele na kushuhudia redio, power window, vioo vya pembeni na taa zote zimeng’olewa, huku gari lake ni kama likimdhihaki kwa namna lilivyoonekana.

Mungu wangu, hiki ninini tena?” alimtaja Mungu huku akiendelea kuilaumu nafsi yake kwa uzembe wa kiasi kile uliosababishwa na pombe. Alikuwa na uhakika sababu ya hayo yote ni pombe kwa sababu anachokumbuka kwa uhakika ni vile alivyokuwa pale Twiga Bar alipoenda kwa ajili ya muhudumu Fidea, lakini zaidi ya hapo hana analokumbuka kwa uhakika wa asilimia mia moja, na maana ya hiyo hali ya kutokukumbuka mengine ni kwamba akili yake kwa wakati ule haikuwa na msaada kwake baada ya kuzidiwa na pombe, kwa mara nyingine aliilaani tena pombe.

Hali aliyoikuta pale kwenye gari yale ilimtangazia kuthibitisha kwamba ni kweli ameibiwa na huyo mwizi aliyevunja kioo cha gari lake na mlango wa chumbani wake, na ndiye kwa hakika aliyeichukua silaha yake.----​Koba na mwenzie Dogo Benja ni vijana wa kihuni waishio mitaa ya Manzese, hawana kazi rasmi ya kuwaingizia kipato zaidi wanategea kudokoadokoa vya watu mitaani, iwe kwa kuchukua bila ya mwenye nacho kujua au mara kadhaa kwa kutumia nguvu kwa kukaba na kupora mali za watu, hasa nyakati za usiku………..itaendelea

kitabu cha riwaya MCHEZO MCHAFU kipo mtaani, wasiliana na 0673966615

Cover Mchezo Mchafu.jpg
 
mtu wa vumbi

Member
Jan 9, 2022
9
4

View attachment 2096725
Mkuu hard copy ipo tayari?
 
Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
70
235
Ipo tayari Kaka, tembelea maduka ya vitabu yote katikati ya jiji la Dar es Salaam
 
Makonyeza

Member
Feb 2, 2020
70
235
Yes, nimezingatia hilo, kama hard copy unaona kwako uduanzi basi ingia pale Amazon. Com utapata kitabu hiki katika soft copy na utaenjoy brother, ushindwe wewe tu
 
Similar Discussions

2 Reactions
Reply
Top Bottom