Riwaya; Mauaji ya kasisi

MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE

+255 766 974 865
Sehemu ya 19 & 20
“Ooh, karibu sana, tulikuwa tunakusubiri wewe tu, watu wote wako tayari kwenye ndege,” alizungumza Yule mwanadada aliyevalia nadhifu kabisa alimkaribisha Madam S na kuingia nae ndani moja kwa moja kwenye ndege hiyo ya kisasa kabisa, alimuonesha siti yake na Madam akaketi tayari kwa safari, baada tu ya yeye kuwa ameingia, ndege ile ilijitoa katika vizuiz vyake ikisukumwa na gari kubwa kuipeleka barabarni.

§§§§§

NDEGE na Kamanda Amata walikuwa wameegesha gari yao pembezoni mwa jengo la Posta katika mji wa Nairobi, wakijadiliana hili na lile jinsi ya kumnasa Wambugu. Kamanda Amata alichukua simu ya Wambugu, simu ya kisasa kabisa akaigeuzageuza na kumtazama Wambugu, “Unamjua Wambugu kwa sura?” akamuuliza.
“Hapana, sijawahi hata kumuona, hata hilo jina ni geni sana kwangu,” Ndege alijibu. Kamanda Amata akaichukua namba ya Wambugu na kuiingiza katika simu hiyo, akaiunga kwenye mtandao wa internet, kisha akaingiza nambari Fulani Fulani na kufungu mtandao wa usalama wa Tanzania, akaingiza ile namba pamoja na jina Wambugu katika na kujaribu kufananisha vitu hivyo. Haikumchukua muda mrefu simu hiyo ilimpa majibu, namba, jina na picha vyote vitatu vilionekana kwa wakati mmoja na maelezo mengine kedekede.
“Ndege!” Amata aliita na kumpa ile simu, “Unahisi huyu anaweza kuwa ndiye?” akamuuliza, Nege akaitazama ile picha kwa makini sana akatikisa kichwa.
“Naijua sura hii vizuri, ni moja kati ya wahalifu wanaoisumbua serikali,” Ndege alijibu huku akiirudhisha ile simu kwa Kamanda, kamanda Amata akaihifadhi ile picha katika sehemu maalumu kwa kazi hiyo ndani ya simu ile. Kisha akafunga ule mtandao na kurudisha simu katika hali ya kawaida, hakuishia hapo, “Ndege, piga simu kwa jamaa yako wa kampuni ya simu, atuambie simu tatu za mwisho za Wambugu zinasemaje tunaweza kupata majibu ya shaka letu.” Ndege akaichukua ile simu na kufanya hivyo kisha wakasubiri jibu watakaloletewa. Haikuchukua muda ukatumwa ujumbe wa sauti katika simu hiyo, Ndege akaufungua na kusikiliza, hawakukosea, ilikuwa sauti ya Bill ikimtaka Wambugu aende Iryamurahi akajifiche huko.

“… najua kuwa una mahangaiko makuu, najua kuwa Mellina amekamatwa, sasa sikiliza, na husijibu simu hii bali tekeleza unaloambiwa, ondoka haraka Nairobi kwa njia za siri unazozijua wewe, njoo Iryamurahi utanikuta hapa, kisha tupange mpango kabambe wa kuondoka katika nchi hii, nakusubiri, ukifika hapa mjini nitakupigia…”

Ilikuwa ni mwisho wa ujumbe ule wa sauti.
“Ina maana Bill yupo Iryamurahi?” Ndge aliuliza kwa mashaka, huku akiwasha gari na kuliingiza barabarani kuchukua barabar ya kueleka Embu.
“Ndege, Bill ni jasusi la kimataifa, hawezi kukaa nchini kwako wakati kazi aliyopewa imekwisha,” Amata alimjibu Ndege, akaichukua tena simu ya Ndege nakuanza kufanya utundu mwingine wa kupata uelekeo ambao Wambugu atakuwepo kwa wakati huo.
“Unafanya nini?” Ndege akauliza.
“Natafuta uelekeo wa Wambugu atakuwa wapi, kama katoka Nairobi au bado hajatoka tusije tukapoteza muda,” Kamanda Amata alijibu.
“Hiyo kazi ndogo Kamanda, piga simu kwa huyo jamaa atatuambia point gani alipigia simu mara ya mwisho na sasa atakuwa maeneo gani kadiri ya signal inavoonesha,” Ndege alimuelekeza Kamanda.
“Ndege acha kutumia njia za kianalogia hizo, sasa hivi namtafuta kwa GPS na nitakwambia alipo,” Kamanda Amata akaiweka simu katika program ya GPS akajaribu kuingiza namba za Wambugu na kuitafuta simu anayoitumia, jibu likaja, ikatumwa namba ya IMEI ya simu ambayo kwa wakati ule ilikuwa imebeba sim card ile, akaendelea na utundu wake mpaka akaweza kuunganisha mtandao huo, taraytibu ramani ya Nairobi na vitongoji vyake ikaonekana katika kioo cha simu hiyo, kidoti chekundu kikatua katika maeneo ya Juja. Kamanda Amata alicheka kwa ushindi huo.
“Wambugu hayupo mbali sana,” Amata alimwambia Ndege, akamtajia na vpimo vya ardhini kabla hajamaliza Ndege akamwambia hilo ni eneo gani. Gari ikaongeza moto kuelekea barabar ya Embu kumuwahi Wambugu, “Tusifanye lolote, twende nae mpaka Iryamurai tukaone kuna nini,” Kamanda Amata alimwambia Ndege aliyekuwa katika usukani akiendesha gari hiyo kwa kasi ya ajabu.
“Kamanda, kimpata Bill utamfanyan nini?” Ndge aliuliza swali la kizushi.
“Sijui, ila shetani anajua maana nina hasira nae, na nitamfuata popote alipo katika dunia hii, mpaka nimtie mkononi,” Amata alijibu. Wakati huo walipita maeneo ya Kasarani na kuendelea kuikanyaga lami kusonga mbele.

§§§§§

Saa sita usiku, ndege ya Swiss ilikanyaga ardhi ya Nairobi katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta. Madam S alikuwa ni mtu pekee aliyeshuka katika ndege hiyo, aliwashukuru wafanyakazi kwa ukarimu wao na kuzishuka ngazi hizo kwa fujo. Alipomaliza itifaki zote, alitoka nje lutafuta usafiri wa kwenda mjini.
“Karibu Madam, karibu sana Nairobi,” ilikuwa ni sauti ya kiume iliyotokea kwa nyuma yake, madam alisita kwa kuwa hakutegemea kupata ukaribisho wa aina yoyote hapo Nairobi, mkono mmoja ukiwa ndani ya jacket aliloliva muda mfupi uliopita katika kukabiliana na baridi ya Nairobi, aligeuka nyuma na kumuona kijana huyo mwembamba mrefu, sura yake haikuwa ngeni sana machoni, alimtazama tena na tena kisha akamkubuka, “Mashaka?” alimuuliza.
“Ndiyo, Mashaka, kutoka ubalozi wa Tanzania,” alijibu Yule kijana ambaye jina lake ni Mashaka, alietumwa miaka kadhaa nyuma kufanya kazi za idara ya usalama katika ofisi za ubalozi wa Tanzania huko Kenya.
“Kwangu?” Madam aliuliza.
“Ndiyo,” Yule kijana akajibu, kisha madam akaondoka eneo lile na kuelekea kunakoegeshwa tax, akaingia na kuketi ndani, Yule kijana akarudi na kuingia kwenye gari binafsi nyingine. Dereva wa tax hiyo akageuka nyuma na kumtazama Madam S, kabla hajaongea chochote Madam S alimwambia, “Safari Park Hotel,” kisha akampa noti tatu za shilingi elfu moja moja za Kenya, safari ikaanza.
Kwa kuwa ni usiku haikuwa tabu na wala haikuchukua muda kwao kufika katika hotel hiyo. Akiwa ameketi katika gari hiyo mara alihisi mfinyo katika mkono wake wa kushoto, akauinua na kuitazama saa yake kisha akabofya kitufe Fulani, mara mkanda mwembamba ukatoka kwa chini ukiwa na maadishi Fulani, akausoma na kuukata kisha akautia kwenye mfuko wa suruali.

‘…Kamanda Amata yupo Nairobi, kwa sasa yupo barabara iendayo Embu akielekea upande wa kaskazini, nimemnasa pindi alipotumia mtandao wetu wa usalama kwa kupitia nywila yako. Chiba…’

Ulikuwa ni ujumbe uliokuwa katika kijimkanda hicho. Madam S alikunja sura, ‘mshenzi kabisa Amata, kaipata wapi password yangu?’ alijiuliza.
Ilimbidi Kamanda Amata kutumia password ya Madam S baada ya kugundua kuwa ile yak wake ilikuwa imefungwa hivyo hakuweza kuingia kwenye mtandao wa usalama wa Tanzania, alijaribu kuibuni password ya Madam S mara mbili, mara mbili ya tatu akaipata na kuingia kwa kutumia jina hilo, baada ya kumaliza kazi hiyo ndipo Chiba alipojua kuwa kamanda Amata yupo Nairobi kwa jinsi alivyokuwa akichukua data ambazo zinaendana na kazi aliyotumwa tangu mwanzo huko Nairobi. Ubalozi wa Tanzania huko Kenya kupitia mtaalamu wa mawasiliano aliyepelekwa kwa ajili ya kublock password zilizoibwa na Bill, Frank Masai aligundua kuwa muingiliano huo uliotokea Nairobi kwa vyovyote madam S alikuwapo hapo, alipowapa taarifa hiyo wengine wakafanya uchunguzi wa haraka na kugundua kuwa Madam S yupo njiani kuja hapo Nairobi, hivyo wakamtuma Mashaka kumuwekea ulinzi kutokana na hali halisi ilivyo katika jiji hilo.

Madam S aliweka kambi katika hotel ya Safari park, alihakikisha kila kitu kipo salama, na kupanga jinsi ya kumsaka Kamanda Amata kwa udi na uvumba. Aliifungua laptop yake ndogo na kuingia kwenye mtandao wa idara ya usalama, kwanza akaangalia ni nini Kamanda Amata alikuwa akifanya katika mtandao huo, akasoma maelezo ya Wambugu na kuitazama picha yake, akaangalia na maelekezo mengine mengi, akaichukua namba ya simu iliyojitokeza hapo ambayo Amata aliitumia kuchukua maelezo hayo, akatabasamu na kumsifu Amata kimoyomoyo kwa jinsi alivyokuwa mtundu wa kufikiri pindi anapohitaji maelezo Fulani. Alikumbuka jinsi anavyoweza kuiga sauti na saini za watu pindi anapohitaji kufanya hivyo, hakushangaa kusikia kuwa ameweza kupenya mtandaoni kwa kutumia password yake. Alijiuliza mwenyewe, nani anaweza kukaa katika cheo cha Kamanda Amata na akatosha katika kila idara, mapambano ya mikono, utumiaji wa silaha za aina na aina, lugha za kutumia, utundu wa kuendesha vyombo vya ardhini, majini na angani, utundu wa kuiga sauti za watu, saini za watu, vyote hivi nani angeweza, kama isingehitajika watu wawili au zidi kufanya kazi ya mtu mmoja. Jambo moja tu lililomuuzi ni wanawake, Kamanda Amata alikuwa mdhaifu sana mbele ya mwanamke, na adui zake wengi walimuweza kwa hilo tu, walimkamata kwa hilo tu. Lakini bado walipokuja kuona jinsi na njia aliyotumia kutoroka walibaki hoi. ‘Kamanda atabaki kuwa Kamanda tu,’ Madam S alijisemea huku akiifunga laptop ile ndogo na kuirudisha mahala pake.

EMBU – KENYA
EMBU, mji uliopo kilomita takribani 120 kutoka Nairobi, upande wa Kaskazini mashariki kuelekea mlima Kenya. Ukifika miezi ya kumi na kumi na moja utafurahi kuona barabara na viunga vyake vilivyopambwa kwa maua ya rangi ya zambarau kutoka katika miti ya Jacaranda.

SAA 4:15 USIKU
MAINA HIGHWAY HOTEL
KWA KUTUMIA mwendo wa miguu, Wambugu alivuta hatu kuelekea katika hoteli hiyo iliyopo katikati ya mji katika mtaa ya Haille Selasie, moyoni mwake alikuwa na amani sana kuwa sasa kafanikiwa kulitoka jiji la Nairobi. Akitegemea kukutana na mtu wake, Bill siku inayofuata huko Iryamurai, kabla hajaifikia kaunta ya hotel hiyo simu yake ikatikisika mfukoni mwake, akaitoa na kuitazama, private call, ilijiandika, hakuipokea akaenda kaunta na kuchukua chumba.
Akiwa ndani ya chumba chake Wambugu aliiona tena simu yake ikiita, akainyakua na kupoke,

“Wambugu, nikipiga simu upokee mara moja, unafuatwa, hapo mahali si salama, ondoka mara moja, nenda utafute sehemu salama,”

Ile simu ikakatika, Wambugu akabaki ameduwaa, hajui la kuamua, ‘Nani ananifuata?’ alijiuliza, ‘Bill amejuaje?’, ulikuwa ni wakati mgumu sana kwa Wambugu kufanya uamuzi, kwa kuwa alikuwa akijiandaa kuoga, ilibidi aahirishe zoezi hilo na kujipanga kutoka katika hoteli hiyo, alirudi kaunta akiwa kaweka mkono wake mfukoni, kashikilia bastola tayari kwa lolote ambalo litatokea. Alikabidha funguo na kuaga kuwa atarudi muda si mrefu. Alitoka na kuzishuka ngazi kadhaa za mlango huo na kupotelea kwenye kichochoro Fulani ambacho kilimleta katika maduka na mchanganyiko wa watu, ‘niende wapi?’ akajiuliza, hakupata jibu, usiku ulizidi kuwa mnene, kichwa kikimuuma, mawazo yake yakivurugika, mipango ikigoma kupangika, ulikuwa wakati mgumu. Wambugu alivuta hatua ndogo ndogo kuelekea kituo cha tax, pale alizikuta tax chache zinazongoja abiria wa usiku, akiwa kutahamaki hivyo mara gari moja aina ya Jeep Cherokee ilisimama ghafla miguuni mwake, mlango ukafunguliwa kwa haraka na Kamanda Amata akatoka bastola mkononi, Wambugu akajua hapo kazi nzito, alipiga risasi moja kwenye kioo cha dereva, wakati Kamanda Amata anazunguka gari kiufundi ili kumfiikia Wambugu, kumbe mwenzake alishaliona hilo, akalala chini na kupita uvungu wa gari akatokea upande wa pili kisha risasi mbili zilifumua matairi nay a tatu ikalenga tank la mafuta. Kamanda Amata alipogeuka nyuma alishuhudia ile gari ikipaishwa juu kwa mlipuko huo, akajishika kichwa kwa sekunde kadhaa kisha akaikimbilia ile gari na bila kujali, alifungua kwa taabu mlango wa dereva, na kumtoa Ndege ambaye alipigwa risasi begani na Wambugu, akamvuta na kumtoa nje, hali ya Ndege haikuwa nzuri kwani jeraha la risasi na ule moto almanusura vimmalize. Haikuwa na aja ya kumtafuta Wambugu aliomba msaada wa wananchi na kumkimbiza hospitali ya Agha Khan.

Wambugu baada ya kuona kafanikisha hilo, alikimbilia kwenye viunga vya mji na kutokomea mbali kidogo na mji. Alitembea polepole na kutafuta mahali pa kujihifadhi usiku huo maana aliona sasa hakuna sehemu yanye usalama kwake.

Polisi wa Embu, walifika katika hospitali hiyo na kukutana na Kamanda Amata aliyekuwa pembeni mwa kitanda cha Ndege wakati mwenyewe akiwa katika chumba cha upasuaji.
“Tunataka tujue ni nani jambazi na nina mwanausalama?” askari mmoja alieonekana kuwa ndio mwenye sauti aliuliza. Kamanda Amata alimtazama kwa tuo askari huyu aliyeonekana anajua sana kuongea. Akamuonesha kitambulisho chake, lo, Yule askari alilowa ghafla na kutoa salamu ya kiaskari kwa ukakamavu wa hali ya juu.
“Sasa sikia, kuna jambazi hili hapa,” akachukua simu ya Ndege na kumuonesha ile picha, Yule polisi akashtuka kidogo na kushangaa akiwa kakunja ndita si kitoto, “Huyu, kafika hapa, ni mtu hatari sana tunamtafuta nchi nzima mpaka nje ya mipaka, ok sasa kama unaruhusu nianze doria usiku huu,” Yule polisi alimueleza Kamanda Amata, baada ya kufikiri kidogo, akaona hiyo ni njia nzuri ya kujua ni wapi huyo mtu anaweza kuwapo. “Ok, hakikisheni mnampata akiwa hai maana kuna maelezo nayataka kutoka kwake,” Yule askari alipopokea hiyo amri, akapiga saluti na kuondoka.
Usiku huo mchakamchaka ulianza, kila kona kila mtaa ni gari za polisi kumsaka Wambugu. Kila nyumba ya wageni ilipekuliwa usiku huo na akila aliyefanana alibebwa na kupekwa kituoni.

Melchior Ndege alirudishwa wodini baada ya lisaa limoja kwa oparesheni iliyofanikiwa sana ya kuitoa risasi iliyokwama katika mifupa ya bega lake la kulia, majeraha ya moto hayakuwa mabaya sana, aliweza kuongea kama kawaida japo chupa ya damu ilikuwa ikiendelea kuingia mwilini mwake.
“Kamanda! Siwezi tena,” alimwambia kamanda Amata kwa sauti ya chini kidogo, wakati huo Kamanda Amata alikuwa ameketi kwenye kiti jirani kabisa ya kitanda kile, “Kwa nini kaka? Tupo pamoja usijali,” Amata alijibu. “Sikia, nina hasira sana na Wambugu kama wewe ulivyo na hasira na Bill, nenda kamsake popote alipo, nitapona tu nikisikia kuwa umempata na umemtoa roho, nenda Kamanda kamalize kazi kabla hawajajua kuwa tuko pamoja,” Ndege alimueleza maneno hayo Amata. Wakapeana mikono, Kamanda Amata akatoka pale hospitali na mlangoni wakakutana na Yule polisi, “Vipi?” alimuuliza, lakini Yule polisi hakujibu kitu, nyuma yake kulikuwa na polisi wengine watatu, “Kamanda Amata, upo chini ya ulinzi kwa kuwa unaifanya kazi hii kinyume cha sheria,” Yule polisi mkubwa akasema hayo, “Nani aliyekwambia?” Kamanda Amata akauliza, “Tumepata taarifa kutoka makao makuu ya polisi Nairobi kwa uthibitisho kutoka katika ofisi yako huko Tanzania, twende kituoni,” Yule askari alimuamuru Kamanda. Kamanda Amata hakuwa na ubishi, alitii sheria bila shuruti, akapakiwa katika gari na kuondolea hospitalini hapo.

Wambugu alipoona hali si nzuri, polisi kila upande alijua kuwa sasa mambo yameharibika, alichomoka kutoka maficho yake na kutega barabara kuu kuona kama kuna gari litakalotokea. Mara akaona pikipiki ikija upande wa kulia kwake akaokota jiwe na kumpiga nalo Yule mwendesha pikipiki, kisha akajitokeza barabarani na kuokota ile pikipiki, akakaa juu yake na kuitia moto, akaondoka kwa kasi kubwa. Gari iliyokuwa imemchukua Kamanda Amata ilikuwa ikipita barabara hiyo na mara wakaiona ile pikipiki ikija kwa kasi sana, dereva akapunguza mwendo kuona ni nani huyo, “Msimamishe tafadhali,” Yule mkuu akamwambia polisi mwingine, ambaye kwa haraka aliruka chini na kutua barabarni kisha akasimama katikati ya barabar kumsimamisha jamaa huyo, lakini akiwa katika hali hiyo, mlio wa risasi ukasikika na mara Yule polisi akawa chali barabarani, Kamanda Amata akatzama huku na huku akishuhudia Yule dereva akishuka kumsaidia mwenzake, akaruka upande wa mbele kwa dereva na kuigeuza gari kwa fujo kuifuata ile pikipiki, mwendo uliokuwa ikiendeshwa hiyo land cruiser haikuwa ya kitoto, Kamanda Amata alikanyaga mafuta kwa ustadi wa hali ya juu, akaiona ile pikipiki ikikata kushoto na kuingia barabara nyingine nae alipofika pale vivyo hivyo akakunja kuelekea kushoto akiendelea kuifuata ile pikipiki.

§§§§§

Usiku wa manane, Madam S alipata taarifa ya kukamatwa kwa Kamanda Amata, taarifa zilitoka katika ofisi za ubalozi usiku huo, likaandaliwa gari kwa ajili ya kwenda Embu kutoka ubalozini kwa minajiri ya kumchukua Kamanda na kumrudisha Tanzania. Aliamka kwa kusuasua, na kujiandaa, alipokuwa tayari aliteremka kwa lifti mpaka chini ambako aliikuta gari hiyo ikimsubiri, akaketi kiti cha mbele na kuanza safari na watu wengine wawiliyaani dereva na Mashaka, Yule kijana waliekutana pale uwanja wa ndege.
Upande mwingine bwana Shikuku alishtushwa na taarifa za kijana wake Ndege kupigwa risasi na Wambugu pia kupata ajali ya moto uliosababishwa na mtu huyo huyo, moyo ulimchafuka na usiku huo akapanga safari yake ya kwenda Embu kujua nini kinaendelea. Akiwa njiani alikuwa akijaribu kuwasiliana na watu wa usalama upande huo kujua hali kwa ujumla ikoje, na kama ni chuki basi hakuna mtu aliyemchukia wakati huo kama Wambugu, aliapa moyoni lazima amtie nguvuni na atumikie kifungo chake kwa mateso makali.
Kwa ujumla usiku huo kila mtu alikuwa akiwaza yake juu ya Wambugu. Madam S alikuwa ametulia kitini haongei chochote, aliwaacha dereva na Mashaka waongee.
Haikuwachukua muda mrefu usiku huo, masaa mawili na nusu tu tayari walikuwa Embu na moja kwa moja walienda katika kituo kikuu cha polisi na kukutana na mkuu wa polisi wa kituo hicho. Madam S alijitambulisha kwao na kuonesha kitambulisho chake.
“Tunasikitika kuwa kijana wako ametoroka,” ilikuwa kauli ya mkuu Yule. Mashaka akamtazama Madam S ambaye alikuwa ameketi bila kuongea neno lolote, “Na isitoshe ametoroka na gari ya polisi,” akaongeza tena Yule mkuu wa polisi. Madam S alikuwa akitikisa kichwa tu kuashiria kuwa ameelewa anachoambiwa.
“Atarudi tu, msiwe na shaka,” madam S akajibu kwa kifupi, kisha akanyanyuka na kumuamuru dereva waelekee hospitali ya Agha Khan ili akamuone bwana Ndege aliyejeruhiwa katika sakata hilo. Alipofika tu pale hospitali alikutana na Bwana Shikuku, kila mmoja alimkumbuka mwenzie, waksalimiana kwa bashasha kwa kuwa ni miaka mingi hawajaonana. Baada ya hapo wote wawili wakaelekea ndani ya hospitali hiyo kumuona Ndege aliyekuwa amelala usingizi.
“Kwa nini usimrudishe Nairobi kwa matibabu?” Madam S akauliza.
“Amesema hatotoka hapa mpaka amuone Kamanda Amata,” Shikuku alijibu.
“Ok, wameivana hawa. Ulikuwa unajua kama AmaTa yuko hapa?” madam S aliuliza tena.
“Ndio kwanza nafahamu sasa kuwa yuko hapa siku nzote sikuwa najua,” Shikuku alidanganya, wakati Ndege alishamwambia kuwa kamanda Amata yupo Nairobi kwa shughuli hiyo ila si kiofisi.
Madam S alitulia kimya akitafakari jambo Fulani, alionekana wazi kukosa raha usiku huo, aliitazama saa yake ilikuwa tayari ni saa kumi alfajiri.

§§§§§

Kamanda Amata alikunja kona kali kuingia ile barabara ambayo ile pikipiki iliingia, alipoenda kama mwendo wa mita mia hivi hakuiona ile pikipiki wala dalili zake, akajua kwa vyovyote huyu jamaa atakuwa mitaa, akasimamisha gari na kushuka bastola yake mkononi, akawa anashangaa akitafuta huku na kule akizungukazunguka kwa hadhari kubwa sana, alipokuwa tayari kukata tama alisikia mnguruno wa pikipiki kwenye vichaka, akawahi na kuiona ikitokomea porini, akainu bastola yake na kufyatua risasi ya kwanza haikua na shabaha ila ya pili alipiga tairi na kulitoa upepo, ile pikipiki ikaanguka, na Wambugu akawa chini, Kamanda Amata akafika eneo lile na kumkuta Wambugu amekwishasimama na amejiandaa kwa mapigano, Kamanda Amata alitaka kufyatua risasi lakini akakuta zimemuishia, aliirusha ile bastola kumpiga nayo Wambugu, Wambugu aliruka hewani kama ninja na kuipiga tik tak ile bastola ikapotelea kwenye vichaka, wakati huo tayari Amata alifika pale kabla hajajiweka sawa, mguu wa nguvu ulimshukia Amata begani, akayumba upande na Wambugu akasimama kwa mguu mmoja kisha akaushusha ule mwingine taratibu kwa madaha, “Siku zote mnajua kuwa kila mtu ni bwege, kama ulikuwa hujui basi mimi ni Sempai,” Wambugu alijisifu huku akisimama katika pozi la kungfu, Kamanda Amata akaona hapo ndo penyewe, “Huwa sijibishani na wahalifu kabla sijawafundisha adabu,” Kamanda Amata alizungumza kwa gadhabu, akaruka hewani kiufundi na kuimshia mapigo makali Wambugu, lakini mapigo yote aliyapangua vizuri sana, kisha akaanza yeye kupeleka mashambulizi ya mikono kwa Kamanda Amata, ambaye naye alikuwa akiyapangua kiufundi sana mpaka Wambugu akamaliza mapigo yote, Kamanda Amata alipomuona sasa hana ujanja mwingine ndipo alipombadilishia staili kutoka kungfu kwenda kick boxing. Teke la kwanza lilitua mbavuni kabla hajakaa sawa lapili likatu shingoni kisha zikafuata ngumi mfululiozo kama ishirini na tano zilizomuacha Wambugu hoi akigalagala, “Nyanyuka juu Sempai, upambane na mwanaume wa shoka, hayo mapigo niliyokupa niliagizwa na Melchior Ndege sasa naanza ya kwangu,” Kamanda Amata alipomaliza maneno hayo, alijivuta kwa hatua ndefu amgfikie Wambugu, lo, Wambugu akamzidi ujanja, alijirusha kutoka pale alipolala akasimama kisha akajibinua na miguu yake yote miwili ikatua tumboni mwa Amata na kumfanya ateme damu, hasira za Amata zikawaka ghafla, aligeuka nyuma kwa kasi na kumchota ngwala Wambugu lakini jamaa akaruka na ule mguu ukapita chini kisha Wambugu akashusha pigo moja la karate lililotua sawia kwenya shingo ya Amata na kumpeleka chini mzima mzima. Kamanda Amata alitambaa kama motto, damu zikimvuja puani na mdomoni, akaona wazi asipofanya makeke anaweza akazimishwa na watu wasiione maiti yake.
“Ha ha ha ha Tanzania Secret Agency namba 1 ndio wewe!!? Unatambaa kama motto, nyanyuka upambane na jabali la chuma linalotisha kama kifo, Kenya yote wananijua na hapa kila goti linapigwa,” Wambugu akasema hayo kwa kujitamba akijipigapiga kifuani. Maneno hayo yalimuuma sana Amata, akanyanyuka kwa kasi na kugeuka akitazamana na Wambugu ambaye mkononi mwake alikuwa ameokota gongo, akaliinu na kumpiga nalo Kamanda lakini Kamanda akalidaka kwa mkono mmoja, akatazamana na macho mabaya ya Wambugu.
Taswira za mauaji ya kikatili ya kahaba Rose ikamjia na kumtia hasira, taswira ya Ndege akiungua moto ikamjia na kumuongezea hasira, kauli ya kushushwa cheo ikamaliza kila kitu akilini mwake.
Kamanda Amata akiwa kalishika lile gongo kwa mkono mmoja alinyanyua mguu wake na kulikanyaga kwa juu akalivunja kwa mtindo huo kisha akabaki na kipande, kwa hasira na visasi akamchoma nacho Wambugu tumboni, yowe la uchungu lilimtoka akaanguka chini, Amata akamuendea palepale alipo na kumvua kibegi chake kisha akakivaa yeye mgongoni, akamnyang’anya simu yake na kuitia mfukoni kisha akamkamata ukosi wa jacket lake na kumburuza mpaka kwenye kibarabara, akampigiza sura yake chini kwa nguvu, “Bill yuko wapi?” akamuuliza kabla hajajibu akampigiza tena kwa nguvu na kuvunja mfupa wa pua. “Sasa ukiniua ndio ntasema?” Wambugu alijibu kwa uchungu. “Nambie haraka, Bill yuko wapi?” Kamanda aliuliza kwa kelele maana hasira ilikuwa bado imetawala kichwa chake. Wambugu alinyanyua uso wake na kutema mabonge ya damu, “Kuna binadamu ambao hamtakiwi kuzaliwa kabisa, kama wewe na Bill, nakuuliza mara ya mwisho kabla sijakutenganisha na roho yako, Bill yuko wapi?” Kamanda aliendelea kuhoji, “Mi si si si sssjui,” Wambugu alijibu kwa tabu sana. Kamanda Amata akamburuza mpaka aliposimamisha gari na kumuinua akamsimamisha wima akimuegemezea katika bodi la gari. “Wambugu! Nakuua,” Amata alimwambia, “Niue braza, kwa maana ukiniacha hai nitateseka sana na mkono wa sheria,” Wambugu akajibu. “Niambie Bill yuko wapi?” akauliza tena, “Braza utanitesa utaniua lakini mimi sijui Bill yuko wapi alishatoroka hapa muda mrefu,” kamanda Amata alishikwa na hasira akampiga kichwa kimoja maridadi na kumuachia akianguka chini kama mzigo.
Mara taa za gari mbili zikawamulika kutoka barabara kuu, na zile gari zikaja mpaka pale, walikuwa ni polisi, wakateremka haraka na kumuweka Kamanda Amata chini ya ulinzi. Kamanda Amata akanyosha mikono juu, wale polisi wakaja na kumtia pingu, nyuma yao akaja mtu mnene kiasi aliyeonekana kuwa na sura ya kikatili isiyo na chembe ya huruma, akamuendea Kamanda Amata, akamtazama usoni, juu mpaka chini, “Hey, askari!” akaita, “Mfungue pingu Kamanda, mpe na begi lake,” wale askari wakafanya hivyo, kamanda Amata akapokea lile begin a kulitupia mgongoni. “Mzima au amekufa?” Yule bwana akamuuliza Kamanda. “Mzima huyo hawezi kufa kirahisi,” Amata akajibu. Yule bwana akatoa amri ya kupakiwa Wambugu garini kisha yeye na Kamanda Amata wakaingia katika gari ndogo ya polisi na kurudi mjini.
“Kamanda Amata, umetusaidia kazi moja ngumu sana ambayo jeshi la polisi la Kenya na vyombo vingine vya usalama imetusumbua kwa miaka takribani kumi kumpata huyu mtu, asante sana kijana” akamshukuru Kamanda na safari ikaendelea mpaka kituo cha polisi cha Embu.

Madam S na Mashaka walikuwa hapo kituoni pia wakimsubiri Kamanda Amata, walimuona alipokuwa akishuka katika ile gari na waziwazi alikuwa ameumia sana kwa jinsi alivyokuwa akitembea, wakakutana uso kwa uso na Amata, wakatazamana. “Madam, kijana wako huyo wapo, sisi hatuna deni nae!” alisema Yule bwana mwenye mwili mnene, kisha akapita kwenda ndani ya kituo hicho, ijapokuwa ilikuwa alfajiri lakini watu walijazana kutaka kuhakikisha kama kweli jambazi sugu Wambugu limekamatwa, jambazi lililowanyima usingizi Wakenya wengi kwa miaka mingi.
Kamanda Amata, Madam S na Mashaka waliingia kwenye gari yao na kuondopka eneo lile, moja kwa moja mpaka hospitali ya Agha Khan ili kwanza apate huduma ya kwanza. Ndani ya nusu saa alikuwa tayari amefanyiwa check up ya nguvu na kutibiwa palipohusika, Mashaka akamuendea Amata katika chumba alichokuwapo kisha akamkabidhi begi jeusi mpano wa briefcase, alkipofungua ndani akakuta suti mpya, saa ya kisasa kwa kazi yake na bastola ndogo.
“Umerudi katika hali yako Kamanda,” Madam S alimwambia walipokutana mara tu Kamanda alipotoka kule ndani, “Yeah, lakini bado kitu kimoja,” kamanda alisema, “Nini?”
“Nataka kumuona Ndege,” akajibu. Wote watatu wakaingia wodini alikolazwa Ndege na kumkuta tayari amewekwa katika kitanda cha magurudumu, amefungwa mikanda sawia na chupa ya majiiliyowekwa baada ya ile ya damu ikiendelea kwenda, “Melchior Ndege,” Kamanda alimwita huku akwa amemuinamia pale kitandani, “Amekufa au amekimbia?” Ndege aliuliza kwa shauku, “Hali yake ilivyo hawezi kuiona jioni, yuko katika mikono ya polisi,” Amata alimwambia Ndege ambaye alionekana wazi kuifurahia habari hiyo. “Asante Kamanda,” Ndege alishukuru, “Asante na wewe” Kamanda akamalizia.

§§§§§

Kama kuna habari iliyomfurahisha Sargeant Maria, basi ni hii ya kupatikana kwa Wambugu, kwa sababu baada ya kumbana sana Mellina kwa kipigo na mateso makali alitaja washirika wote akiwamo Wambugu. Sargeant Maria na wenzake waliishiwa nguvu kusikia kuwa Wambugu anahusika na mauaji ya Kasisi, swali lilikuwa, tutampataje? Lakini ghafla alfajiri hiyo wanaambiwa kuwa Wambugu kapatikana huko Embu karibu na msitu wa Njukiri baada ya vyombo vya usalama kupambana nae vilivyo, baada ya kutaka kujua zaidi ndipo Sargeant Maria aliposikia juu ya Kamanda Amata ambaye yeye siku zote alijua ni mtu wa kwenye riwaya tu, hakujua kuwa ni burudani ya waandishi kuandika visa vyake kila amalizapo kimoja na kuanza kingine. Ulikuwa ni ushindi mkubwa, mkubwa sana, Maria alijiuliza, Mellina tumemkamata, Cheetah, kauawa, Wambui kauawa, Wambugu ndio huyu hapa, sasa ile Mostrance ambayo ndicho chanzi cha kazi nzima haijapatikana, bado kuna kazi mbele.

ITAENDELEA....
 
MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE

Ulikuwa ni ushindi mkubwa, mkubwa sana, Maria alijiuliza, Mellina tumemkamata, Cheetah, kauawa, Wambui kauawa, Wambugu ndio huyu hapa, sasa ile Mostrance ambayo ndicho chanzi cha kazi nzima haijapatikana, bado kuna kazi mbele.

SEHEMU YA 20 & 21


SIKU MOJA BAADAE - DAR ES SALAAM

KAMANDA AMATA na Madam S walikuwa wakitembea kwenye korido ya jengo la ukumbi wa jiji, wakiwa wanatoka kupata kahawa katika kamgahawa kadogo ndani ya ukumbi huo, walikuwa wakizungumza mawili matatu, wakibadilishana mawazo ya hili na lile.
“Sasa Kamanda, kama uliovyoambiwa, umeshuswa cheo na umebadilishiwa idara, idara gani mi na wewe hatujui, lakini nataka uniambie jambo moja tu, baada ya kumkamata Wambugu, umepata chochote juu ya jasusi Bill Van Getgand?” Madam S akauliza. Wakasimama na kugeukiana, “Yeah, Bill yupo German, alishaondoka kitambo sana, na habari hizi nimezifanyia uchunguzi wa kina sana kutoka katika tafutishi zangu kupitia simu na maelezo ya Wambugu,” Kamanda Amata akajibu.
“Ok, Una akili sana Kamanda, siwezi kupata mtu kama wewe tena katika ofisi yangu. Sikiliza, baadae nitakupigia simu tuonane.” Baada ya mazungumzo machache kati yao waliagana na kuondoka kila mtu na hamsini zake.

Ndani ya ofisi za AGI Int’, Gina alikuwa ameandaa bonge la keki na mvinyo wa kutosha kusherehekea kurudi salama kwa boss wake Kamanda Amata. Walipongezana wakiwa wawili tu, wakikata keki na kunywa mvinyo kwa fujo kiasi. Wakiwa katika hali hiyo ndipo simu ya Kamanda iliita kwa fujo, “Aaaaaaa nani tena huyo?” Gina aliuliza kwa sauti ya kilevi. “Madam S” Kamanda Amata akajibu na kuiweka ile simu sikioni.
“Unikute hapa katika ofisini kwangu mara moja,” na ile simu ikakatika, Kamanda Amata akashusha ile simu na kuitia mfukoni, mara Gina akamvamia na kumkubatia kwa nguvu, “Kamanda, sikjawahi kukwambia jamani, mi nakupenda, unioe, uwe mume wangu,” Gina alilalama akiwa kalewa chakari, chezea Dompo wewe! “Hebu toa ulevi wako Gina,” Amata aling’aka lakini Gina bado alikuwa kamng’ang’ania sasa akitaka kumpa ulimi, Amata akamuweka kwenye kiti. “Wewe, uwe na akili, umelewa wewe, mi naenda kwa Madam S kaniita,” Amata alimwambia Gina,

“Tunaenda wote,” Gina nae akaliunga. Dakika chache tu ziliwachukua kuwasili katika ofisi ya Madam S iliyopo mkabala na jengo la hazina, akaingia getini na kuegesha gari panapotakiwa, aliteremka na kumuacha Gina akiwa anakoroma garini, tayari alibebwa na usingizi mzito. Akajiweka tai yake vizuri kisha akajitupia koti lake na kuziendea ngazi zinazoingia katika ofisi hiyo, akiwa mlango wa kwanza alikutana na mtua mmoja ambaye alimjua vilivyo ni mwenzake wa idara ya usalama wa taifa lakini vitengo tofauti akiwa kakunja sura hata hakumsalimu, Kamanda aliponyosha mkono kumsalimi hakupokelewa, akaona isiwe shida alimpita na kuingia ofisini kwa Madam S.

“Karibu Kamanda,” Madam S alimkaribisha huku amesimama badala ya kukaa.
“Asante Madam kwa kunikaribisha katika ofisi yako tukufu ambayo sikutegemea kuiona tena,” Kamanda Amata alizungumza akiwa siriasi kabisa.
“Kamanda Amata, kutokana na mchango wako mkubwa katika kuliokoa Taifa, na kutatua migogoro mizito na mikubwa ambayo ama ingelipoteza Taifa au maisha ya wananchi, maamuzi ya kikao cha watu wa idara ya usalama kimeamua kikushushe cheo kutokana na kutoitilia umakini nafasi uliyopewa na kudharau amri au maamuzi ya wakubwa wako, hivyo umeshushwa cheo na kubadilishiwa kitengo, kutokana na hilo kuanzia sasa ofisi yako ya kazi itakuwa Ikulu, kuratibu na kuhakikisha usalama wa msafar wa Mheshimiwa Rais pindi awapo nje ya jengo la Ikulu.” Madam S alimtazama Kamanda Amata usoni hakuona dalili ya tabasamu wala chuki kutoka kwa mpiganaji huyo.

Kwa kuwa yeye kupata nafasi hiyo alikuwa ametokea katika jeshi la polisi kitengo cha CID alitoa heshima ya kijeshi kwa Madam S ya kuonesha amekubaliana na uamuzi huo bila ubishi. Madam S akamkabidhi barua maalu yenye mhuri wa serikali kuthibitisha hilo pamoja na muhtasari wa kikao, akavipokea na kuvibana kati mkono wake wa kulia. Madam S akamtazama tena Amata, “ Kamanda Amata, kutokana na kuwa idara ya usalama imekosa mtu wa kuishika nafasi yako mithili ileile ya jinsi ulivyokuwa ukifanya kazi kwa makini na akili nyingi, ukiwa tayari kufa kwa ajili ya Taifa lako au kwa ajili ya wanyonge, imeonelewa tukurudishie cheo chako cha Tanzania Secret Agency namba 1 kwa muda usiojulikana mpaka itakavyoamriwa vinginevyo,” Madam S alimtazama tena Kamanda usoni akakutana na sura ileile ya ukakamavu.

Akachukua beji maalum ya utambulisho kwa watu wote wa usalama wa Taifa na kuipachika katika upande wa kushoto wa ukosi wa koti lake, beji ambayo ilichukuliwa wakatia alipofikishwa hospitali Muhimbili akitokea Kenya. Madam S akamkabidhi kikasha kimoja kilichofungwa kwa utepe mwekundu. Akakipokea akaukata utepe na kukifungua ndani, bastola aina ya Walther PPK (PPK ni Polizei Pistole Kriminal-The Criminal Police Pistol), pembeni ya bastola hiyo kulikuwa na kiwambo chake cha sauti. Chini ya hicho kikasha kulikuwa na bahasha ndogo, akaichana na kuifungua, ilikuwa tiketi ya ndege kwenda Ujerumani, alipochambua vizuri akakutana na picha ya Bill Van Getgand, juu yake imeandikwa ‘WANTED’ yaani ‘ANATAFUTWA’ halafu chini yake wameorodhesha mashirika mbalimbali ya kijasusi ambayo yanamtafuta jasusi mwenzao aliyehasi huko KGB na kuingia kwenye mikono ya uhalifu wa kimataifa.

“Kamanda Amata, sasa unaenda kufanya kazi ngumu ambayo shirika la letu la ujasusi japo halitambuliki hivyo kimataifa linakutuma, Safari njema.” Madam S alimaliza na kuketi tena katika kiti chake. Akili ya Kamanda Amata ilianza kufanya kazi ndani ya muda mdogo akiikabili kazi hiyo ngumu na ya hatari ambayo hakujua wapi itaishia. Alimtazama madam S kwa tuo. “Keti chini kamanda,” Madam S alimwambia Kamanda Amata wakati mlango ukifunguliwa na jamaa mmoja akiingia na sanduku moja dogo la chuma, akakaribishwa na kuketi katika kiti kingine pembeni ya kamanda Amata. Kamanda Amata alielewa kinachotakiwa kufanyika, walihitaji kuiridisha ile microchip ya GPS ambayo huweza kumfanya aonekane popote alipo.

Yule daktari akatoa mashine Fulani na kumfanyia vipimo vichache ikiwamo presha ya damu na vitu vingine, kisha akachukua kitu kama sindano iliyounganishwa na bomba kabisa ambapo ndani yake kuna hiyo microchip, akamdunga sehemu Fulani ya msuli wake wa mkono juu ya kiwiko na chini ya bega akasukuma kama anavyosukuma dawa katika sindano ya kawaida, ile microchip ikasafiri katik ule msuli na kujikita ndani kabisa, baada ya hapo akafungwa bandeji na kupewa dawa Fulani za vidonge za kutumia.
Wakati huohuo mlango ukafunguliwa na Chiba akaingia ndani akiwa na begi lake ambalo daima hupenda kutembea nalo, akatoa kompyuta yake ndogo lakini yenye kazi nyingi za kijasusi, akaiweka mezani na kuiwasha kisha akaanza kuingiza namba Fulani Fulani, waya mmoja akaupachika katika sehemu ile aliyohisi ile chip imetuama, ikashikiwa kwa ile bandeji na waya mwingine wenye kitu kama kibanio mwishoni ukabanwa katika kidole gumba cha mkono mwingine, kisha Chiba akawa akifanya kazi katika kompyuta yake.

“Ok, kila kitu tayari,” akasema huku akimtoa zile nyaya zote. Kisha akaingiza mkono katika upande mwingine wa lile begi lake, “Hii hapa saa ya kutumia Kamanda, saa hii ina uwezo wa kukata chuma cha aina yoyite kwa kutumia nishati ya infrared ambayo imekwishawekwa ndani yake, ina uwezo wa kutuma fax fupi na pia inatambua hatari ya mlipuko mahala popote ambapo umetegwa. Uwe mwangalifu kijana,” Chiba alimaliza maneno yake huku akimpigapiga mgongoni.
“Kamanda!” Madam S aliita, “Nimekupigania sana mwanangu, nenda kafanye kazi, nakuomba usichezecheze na wasichana hawa huko, ujue kwamba Bill ni jasusi, si ajabu akawa anajua safari yako yote hata sasa, nimemaliza kwa heri,” Madam S alimaliza na kuagana na Kamanda Amata akabaki na Chiba ofisini. Kamanda Amata akashuka ngazi na kuiendea gari yake ambako alimkuta Gina bado kalala akikoroma.

Akaingia na kuwasha gari akaondoka zake mpaka nyumbani kwake Kinondoni, hakuwa na muda wa kutosha alipanga vitu vyake vichache, akakusanya silaha zake zote za siri na kuzificha panapostahili katika kijibegi chake cha mgongoni ambacho ni yeye tu aliweza kujua kipi kiko wapi na wapi kiko kipi, wakati lile sanduku lilikuwa na nguo na zana ndogondogo. Alijiangalia kwenye kioo cha chumbani mwake na kujiuliza aingie vipi Ujerumani, mkimbizi? Mfanyabiashara, mtalii, muandishi wa habari au vipi, akapata jibu, akafungua kabati na kuchukua bunduki yake ya kisasa kabisa, iliyotengenezwa kwa mfano wa camera kubwa ya picha mnato lakini ndani yake ilikuwa na uwezo wa kubeba risasi ishirini na nane za bastola aina ya Smith and Wesson.

Alipohakikisha kila kitu kipo sawa, akatulia juu ya kitanda huku mawazo yote yakiwa juu ya Bill, kila akikumbuka kitendo alichofanyiwa na Bill alijikuta hasira zikimpanda maradufu, aliamua kumfungia kazi kikweli, ‘ulimwengu utatambua kuwa Bill kauawa na mkono wa Amata, sitaiacha roho yake ipotelee jela wala kwenye mikono ya nani, mi sijui nitakapomuona tu uso kwa uso ama zake ama zangu’ yalikuwa ni mawazo yaliyopita katika kichwa cha Kamanda Amata muda huo. Usingizi ulimpitia na ndoto mbaya zikamuandama, mara anakabwa mara anakimbizwa mara anatumbukia kwenye shimo, basi shida tu.

Kengele ya saa ya mezani ilimuamsha ilikuwa yapata saa nne usiku, alikurupuka na kuingia bafuni akaoga harakaharaka na kujiandaa, alipoenda mutazama Gina, alimkuta bado yuko hoi kwa usingizi akamuandikia ujumbe na kuufutika mahali alipolala kisha ye akachukua gari yake na kuondoka zake kuelekea JNIA tayari kwa safari.

Majira ya saa saba usiku, ndege kubwa ya sirika la Qatar Airways au kama wanavyoliita dege lenye hadhi ya nyota tano liliiacha ardhi ya Dar es salaam na kukata anga kuelekea Doha ambako abiria wangebadilisha ndege ili kuendelea na safari zao. Kamanda Amata alitulia kitini katika behewa hiyo ya VIP akiwa kanyoosha miguu kwa raha zote akipata raha kwa kuwatazama warembo wa Qatar waliokuwa wakijipitisha pitisha na kuumuuliza hili au lile. Akili na mawazo yake tayari yalikuwa yamejipanga kimchezo huo wa hatari ambao unamkabili mbele yake ambao alipenda aufanye kwa siri na kwa muda mfupi.

§§§§§

ACHEN – UJERUMANI

ANDREAS Schurmann alimtazama Bill Van Getgand, hakummaliza, mtu huyo mnene, mwili jumba lakini mwepesi kwenye mapambano alikuwa ameketi mbele ya tajiri huyo, tajiri anayejulikana sana katika mji wa Achen na pembezoni. Ilkuwa ni siku moja tu baada ya Bill kuwasili katika jumba hilo la kifahari lililojengwa katika eneo la Mausbach. Jumba la bei mbaya ambalo hakuna asiyelijua katika mji huo.
“Nini kilikuwa kinakushinda siku zote kupata kitu kidogo kama hiki Bill?” Don Andreas alimuuliza Bill huku akimmiminia bia aina ya Pilsner, bia bora Ujerumani.

“Hata huko nilikoipata usifikiri kazi ilikuwa rahisi, imebidi kumwaga damu,” Bill alijibu huku akiinua glass yake na kuiweka mdomoni kabla hajamiminia kinywaji kilichomo ndani yake, akabeu kidogo, “Imebidi tumwage damu, hakukuwa na jinsi,” alimalizia kusema. “Usijali, maadam tumepata tunachotaka basi,” Don Andreas akamtia nguvu kwa maneno hayo.
“Hii mali yetu kaka, aliwekeza baba wa babu yetu, alikuwa na makusudi mazima juu yake,” Andreas aliendelea kuongea huku akiigeuzageuza ile monstrance mikononi mwake, “Pure Gold!” alitamka maneno hayo huku akiibusu. Akairudisha katika begi lake na kuketi tena kochini. “Ndio Bwana Bill, kazi yangu mi na wewe imekwisha, au kuna linguine la kuniambia? Maana malipo yako tayari yapo benki haijapungua hata senti moja nyekundu,” Andreas alimwambia Bill. Tabasamu pana likamjia Bill usoni, likachanua kama ua la yugiyugi, akainua glass yake na kugonga cheers na Andreas, wakati glass hizo zikagongana simu ya Bill ikaita kwa fujo katika mfuko wake wa shati, akaitoa na kukutana na ujumbe mfupi wa maandishi,

“…Wambugu amekufa mikononi mwa polisi, kazi ya Kamanda Amata,”

Meseji hiyo ilimshtua sana Bill. “Vipi? Mbona unashtuka?” Andreas akauliza. Bill akashusha glass yake na kuiweka mezani. “Mmoja wa vijana wangu ambaye nilimpanga wa mwisho kufa, ameuawa,” Bill alijibu.
“Sasa wewe kinakushtua nyingi, si ndio amekufa!” Andreas akamwambia.
“Tatizo sio kufa, ila nani kamuua” Bill akamwambia Andreas.
Andreas akatikisa kichwa kuashiria kuwa amemuelewa Bill, “Ok, nani amemuua?” akauliza.
“Amekufa mikononi mwa polisi, na ni kazi ya Kamanda Amata, Jasusi la kiafrika kutoka Tanzania, TSA,” Bill akajibu.

“Unasema! Africa kuna majasusi? Tangu lini? Tena Tanzania?” Andreas alionekana kushangazwa na taarifa hiyo.
“Don Andreas, hata kama ASfrica hakuna majasusi, lakini huyu Amata ni zaidi ya Jasusi,” Bill alieleza huku mikono yake ikiwa kiunoni.
“Acha uwoga wewe, wao wapo Africa wewe upo Ulaya, waache wauane tu, hiyo ndiyo sera yetu mataifa makubwa, tunawachonganisha wanauana sisi tunakula maisha,” Andreas akajibu huku akijimiminia kinywaji chake kama kawaida lakini Bill hali haikuwa sawa kama mwanzo, Lijitupa kochini na kuweka mikono yake huku na huko kisha akashusha pumzi ya kina.

“Andreas, ili tuwe na amani katika hili lazima Amata auawe kwa njia yoyote ile,” Bill aliongea kwa jazba.
“Kama wewe umesema kuwa ni mtu hatari basi fanya kazi ili asiharibu mambo yetu, nakuaminia wewe ni jasusi wa KGB hata kama uliwasaliti na kuwakimbia,” Andreas alimwambia Bill huku akimpigapiga mgongoni.
Bill Van Getgand aliingiwa ganzi mwili mzima baada ya kusikia Wambugu kafia katika mikono ya polisi na ni kazi ya Kamanda Amata, hiyo ilikuwa ni salamu tu ambayo alijikuta anashindwa kuijibu. Alikumbuka sumu kali aliyompatia akijua kwa vyovyote asingeamka kwa muda mfupi kama ule, japokuwa hakusikia habari za kifo chake redioni, bado Bill aliamini kabisa kuwa Kamanda Amata mpaka dakika hiyo ni marehemu. Ukimya uliendelea akitafakari jinsi gani swahiba wake Wambugu atakuwa ametoa siri za mpango wao na labda hatari kubwa itakuwa ikiwanyemelea.

Bia iligoma kupita kooni, akili yake bado ilikuwa inazunguka huku na huko akifikiri la kuifanya, alipopata jibu akainua glass yake na kujitupia kinywaji kama kawaida, huku laptop yake ndogo ikiwa mezani tayari kwa kazi Fulani. Aliifungua na kutaka kuingia mtandaoni, Bill nalikuwa na uwezo wa kuingia mtandao wowote anaoutaka kwa kutumia nywila za bandia ambazo huzibuni kiufundi sana yeye mwenyewe na kufungua faili au mtandao wowote anaoutaka ili kujipatia taarifa kwa ajili ya mambo yake ya kijasusi, aliingiza nyila zake ili kuifungua kompyuta hiyo, ilipofunguka kioo chote kilikuwa cha blue, “Shiit!!!” akang’aka, akajaribu tena, hali ilikuwa ileile, akabaki mdomo wazi, kijasho chembamba kikamtiririka kutoka kwapani mpaka maeneo ya kiuno, Bill alihangaika kutumia njia zake zote lakini hakufanikiwa. Ilikuwa ni kazi ya kijana Frank Masai aliyekuwa akishirikiana na Chiba katika kuunda kirusi kibaya kabisa maalumu kwa kuiua kompyuta ya Bill kusudi asiweze kuingia katika mtandao wa siri za usalama wa Taifa la Tanzania, walifanikiwa, Bill Van Getgand alibaki teee, hana la kufanya,

“Wameniweza,” akajisemea kwa sauti ya chini. Bill alikurupuka kitini na kumuaga Andreas kuwa atarudi jioni ya siku ya hiyo, alitoka nje ya hekalu hilo la kifahari na kuingia kwenye gari yake aina ya Jaguar na kuondoka zake. Akiwa na mawazo mengi kichwani alielekea moja kwa moja katika hotel aliyofikia ili akajaribu mbinu nyingine kupata taarifa za watu mbalimbali na mienendo yao kwa siku hiyo.

BERLIN-SCHONEFELD AIRPORT
Saa 10:30 jioni

QATAR AIRWAYS ilikanyaga ardhi ya Ujerumani jioni hiyo ikiwa tayari imemaliza safari yake iliyoanzia Doha na kupita miji kadhaa kabla ya kufika Berlin. Katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Schonefeld, watu walikuwa wengi wakija kuwapokea na kuwalaki ndugu zao waliokuwa wakitoka pande mbalimbali za dunia kuja ama kusalimia jamaa au ndio wanarudi nyumbani, ilimradi tu maisha ya binadamu ni ya kuhamahama. Miongoni mwa waliokuja kupokea ndugu zao alionekana mtu mmoja mwenye ndevu nyingi, aliyevaa vazi la kikasisi lililomkaa sawia, kanzu ndefu nyeusi na kofia kubwa ya rangi hiyo hiyo, alisimama karibu na nguzo Fulani akiwa hana papara ya lolote, alionekana kumfahamu vyema Yule anayekuja kumpokea na si vinginevyo.

Baada ya Kamanda Amata kukamilisha itifaki za uhamiaji ambapo aliingia Ujerumani kama mwandishi wa habari, aliiweka kamera yake vizuri kifuani mwake, kizibao cha khaki kilichomkaa vyema na jeans yake nyeusi, vilimuonesha wazi kuwa ni mwanahabari halisi, usoni mwake aliipachika miwani safi nyeusi, miwani ambayo inaweza kuvuta vitu vya mbele pindi unapojitikisa kichwa kichwa chako, miwani hiyo ina uwezo wa kukuonesha vitu vya nyuma yako kwa kutumia vioo vidogo vilivyowekwa kwenye miimo yake, ina uwezo wa kurekodi picha mjongeo na sauti kwa wakati mmoja. Mkononi mwake alivaa saa kubwa ya kisasa ‘Casio’ yenye uwezo wa kutuma na kupokea fax fupi, inayoweza kukata chuma chenye ugumu wowote kwa kutumia miali mikali ya laser CO2 iliyowekwa ndani yake, kiatu chake cha mpira kisichoathirika kwa mafuta yoyote wala kuungua kwa moto kirahisi kilikuwa mguuni mwake.

Taratibu alitoka katika mlango wa kutokea wasafiri, akiangaza huku na huko na kwa kufanya hivyo miwani yake iliweza kumsogezea watu wote karibu na kuweza kuwachambua kwa harakaharaka, kwa mbali alimuona Yule kasisi aliyekuwa kwenye kiti cha chuma akiwa anasubiri mgeni wake, Kamanda Amata akasita kidogo, mara mkono wake ukafinywa na kitu kama sindano ndogo sana, akainua saa yake na kuiangalia, ilikuwa ikiwaka taa ndogo sana nykundu katikati ya mishale yake, akabofya kitu Fulani na ikaonesha maandishi katika kioo, ‘A priest’ yaani ikimaanisha Kasisi. Hakusita alimuendea kasisi huyo na wakakutana uso kwa uso kila mmoja akimwangalia mwenzake kwa umakini wa hali ya juu. “Karibu Berlin,” Yule Kasisi alimkaribisha Kamanda wakakumbatiana kusalimiana kisha lile sanduku lake likachukuliwa na Yule Kasisi nay eye akafuata kwa nyuma, muda wote alikuwa akitembea huku akitazama kila amuonaye kuona kama kuna hatari yoyote. Moja kwa moja wakaiendea gari moja ya kisasa sana VolksWagen (VW) modeli mpya wakaingia na kuketi ndani yake.

“Naitwa Fr Frank, raia wa Austria, nafanya kazi katika kanisa kuu la Achen,” alijitambulisha Yule Kasisi, Kamanda Amata akatikisa kichwa kuashiri kuwa ameelewa alichoambiwa.
“Yeah, kamanda Amata,” kisha wakacheka pamoja na kugonganisha viganja vya mikono yao. Kwa jinsi walivyokuwa wakipanga waliona haitakuwa vyema Kamanda asishukie moja kwa moja Aachen, ila ashukie Berlin kisha aende Aachen kwa usafiri wa gari, hii ilikuwa ni mbinu ya kuwapoteza malengo kama wapo wanaomsubiri. Mazungumzo yaliendelea kati ya wawili hao huku wakijaribu kupanga mkakati wa kumaliza kazi yao. “Kilichonileta Fr Frank, sio Bill tu, ila nahitaji kuipata ile Monstrance pia,” Kamanda Amata alimwambia yule Kasisi.
“Unajua, Bill baada ya kumchunguza sana, nimegundua kuwa anafanya kazi na tajiri mmoja anaitwa Andreas Schurmann au ‘Don’ kama wengi walivyozoea kumwita, na mimi tangu nimekuja hapa najua kwa vyovyote vile monstrance ile ipo kwake,” Fr Frank alimueleza Kamanda Amata, “Andreas anafanya nini zaidi?” Kamanda kauliza.
“Yeye ni mfanyabiashara mkubwa, ana viwanda na mahoteli makubwa, nyumba tu anayoishi inaizidi ikulu ya Ujerumani,” Fr Frank alimjibu Kamanda.

“Safi nahitaji kuiona nyumba yake na ikiwezekana pia kujua baadhi ya makampuni yake ili nijue nafanya nini,” kamanda Amata alieleza. “Ila ni kibarua kigumu sana Kamanda, “Yule jamaa ana ulinzi kama Rais wa nchi” Fr Frank aliendelea kumueleza Kamanda hali halisi ya kitu alichokuja kukifuata. Kamanda Amata alijaribu kuangalia uzito na kubwa wa kazi yenyewe.

Masaa matano yaliwatosha kufika mji wa Achen ulio kilomita 538.8 kutoka Berlin, kamanda Amata alitulia tuli kama maji ya mtungini, akiwa amechoka na safari kwa namna moja au nyingine. Saa tatu usiku, walifika katika kanisa kuu la Aachen ‘Aachener Dom’ kama linavyoitwa. “Utakaa hapa na sisi, pana usalama zaidi kuliko hotelini, katika mahotel, huku kwenye nchi zetu, huwa wanatoa siri za wageni wanaofika kwa watu wa usalama na wengine kwa wenye nia mbaya. Usijali Kamanda, hapa pako sawa na hii oda tumepewa kutoka kwa watu wako wa ubalozi,” Fr Frank akiwa katika kusema hayo alikuwa tayari akiegesha gari katika maegesho ya ndani ya jengo kubwa kabisa lililojengwa kiustadi nyuma ya kanisa hilo.

Hakuwa na la kusema, zaidi ya kufuata kila anachoambiwa. Mhudumu aliyepokea mizigo ya Amata alimkaribisha katika chumba maalum kilichokuwa ghorofa ya tatu upande wa kaskazini wa kanisa hilo kubwa. Alikikagua kwa jinsi anavyojua yeye lakini hakuona chochote kilichowekwa kwa nia mbaya kwa ajili yake, aliliendea dirisha dogo lililokuwa hapo, akavuta pazia na kuangalia nje huku akiwa amezima taa ya ndani, hakuna kitu alichokiona zaidi ya jengo kubwa umbali kama wa kilomita moja hivi, likipendezeshwa kwa taa nyingi na nzuri. Akiwa bado akiliangalia jengo hilo mlango ukafunguliwa na Fr Frank akaingia, sasa akiwa katika mavazi ya kawaida kabisa, lakini cha kushangaza hakuwa na ndevu tena,

“Kamanda Amata, hilo jengo unaloliangalia ndio jumba la Don Andreas,” Fr Frank alimwambia Kamanda Amata, “Nimekupa chumba hiki kwa makusudi mazima ili uweze kuliona jumba hilo, sasa sisi tunakuacha ratiba zako utapanga wewe, kama utahitaji msaada kutoka kwetu basi usisite kunijulisha,” Fr Frank akondoka zake.
Kamanda Amata alifunga vifaa vyake ikiwemo camera kubwa moja na darubini yenye nguvu kabisa ambayo inaweza kuona umbali wa kilomita kadhaa pia yenye madini ya kukuwezesha kukuonesha gizani, akaiweka pale dirishani pamoja na kamera ndogo ambayo ingeweza kupata picha nzuri za mnato na mjongeo kupitia darubini hiyo. Alipohakikisha vyote viko sawa, alijaribu kuangalia kwa kupitia darubini ile, aliweza kuona walinzi waliokuwa wakizunguka huku na kule wakiwa na mambwa mwakubwa ya kutisha, ndani ya jumba hilo hakukuwa na chochote kinachoendelea, inaonekana ama watu walikuwa wamelala au walikuwa mahali pengine, lakini yeye alikuwa akifanya majaribio tu, hivyo hakujali kama wapo au la.

§§§§§
BILL VAN GETGAND alikuwa mezani akijaribu kuangalia mtandao huu na ule, alipitia mitandao yote ya mashirika ya ndege zinazoingia na zilizoingia siku tatu nyuma lakini hakuona dalili ya mtu anayemuhisi kufika au kuja. Akafanya mawasiliano na watu wake katika mahoteli lakini haikuonekana kabisa kama kuna mtu kutoka upande anaoufikiria. Bill hata kama alihakikishiwa usalama kuwa hakuna anayemdhania kuwepo nchini humo, bado moyo wake ulihangaika maana alijua wazi kuwa Kamanda Amat anweza kuharibu mambo yote na anaweza kuingia Ujerumani hata kwa kuogelea endapo anabaini kuwa anawindwa.

Usingizi haukua na nafasi kwake siku hiyo, alijaribu kuwapanga vijana wake jinsi anavyoweza ili kuhakikisha anapata habari juu ya ujio anaoutarajia. Bill bila kujua kinachoendelea alifumbua macho na kukuta jua tamu linalopenya katika dirisha lake likimmulika usoni, akajiziba macho kwa kiganja chake cha mkono, hakuelewa saa ngapi alilala ila alijua tu muda ailoamka. Aliketi kitandani alipokumbuka juu ya Kamanda Amata moyo wake ulianza kumuenda mbio na akakosa raha.

Katika maisha ya Bill, maisha yake ya kazi yake ya kijasusi tangu akiwa KGB kule Urusi hakuna siku aliishi kwa hofu kama siku hii ambayo alimuhofia sana Kamanda Amata. Japokuwa alishapambana na majabari katika kazi yake, majitu yenye mbinu na uafanisi mkubwa katika mauaji ya kila aina lakini kwa Kamanda Amata alikuwa anajikuta hana kitu, hasa akifikiria jinsi alivyomuwekea sumu na amepona, kwake aliona Amata anatisha zaidi ya kifo. Alijaribu kutuliza mawazo na alipoona yuko sawa, alitoka katika nyumba yake na kuliendea gari lake aina ya Mercedes Benz na kutokomea mjini. Huku akiwa amejiimarisha kwa kila hali siku hiyo maana alijua lolote linaweza kutokea kwa kuwa alama zake za hatari zilikwishamuonesha hilo. Safari hiyo ilikuwa ni katika moja ya makampuni ya Adreas kama walivyopatana jana yake.

§§§§§
AKIWA ndani ya kanzu nyeusi ya kikasisi huku kichwani akiwa na kofia yake nyeusi aina ya barret, Kamanda Amata alikuwa akitembea tembea katika uwanja wa kanisa hilo kubwa kabisa katika mji huo wa Aachen. Kila aliyemuona alimsalimi kwa lugha ya Kijerumani ambayo alikuwa akiifahamu vema. Alipohakikisha ameyachoka mazingira hayo, akaliendea gari moja jeusi lililokuwa limeegeshwa hapo pembeni kwenye maegesho ya magari. Akaingia na kuketi nyuma ya usukani, ilikuwa ni Land Rover County short Chassis, aliiwasha na kuitoa taratibu katika maegesho yake, kishs akaliendea geti kubwa na kufuata ujia mrefu uliokuwa ukiiendea barabara kubwa ya kuelekea katikati ya mji, Kamanda Amata aliendesha gari hiyo kwa mwendo wa wastani akielekea njia ile ambayo ilikuwa ikipita katika jumba la bwana Andreas. Njiani gari nyingi zilimpita nay eye akazipita zingine ilimradi kufanya barabara ipendeze. Baada ya mwendo kama wa dakika kumi hivi aliichepuka na kukunja kushoto kisha akaingia kama shimoni na kupita uvunguni mwa hiyo barabara akatoke upande wa pili.

‘AACHEN COMMONWEALTH GRAVE YARD’ (Uwanja wa makaburi ya jumuia ya madola ya Aachen), lilikuwa ni bango kubwa la kijani lililoandikwa kwa maandishi meupe likionesha mshale kuelekea upande wa kushoto, Kamanda Amata akawasha indiketa kueleka upande huo, akapinda na kulielekea geti kubwa upande huo, ambalo lilifunguka lenyewe bila kufunguliwa na mtu. Akaingiza gari na kushuka, mkononi akiwa na ua moja zuri na kitabu kidogo cha sala. Moja kwa moja akaliendea moja ya makaburi lililokuwa nyuma ya yote, kaburi hilo lilionekana kuwa ni la siku hizi tu kwa uwanja ule ulikuwa umeungana na uwanja wa kuzikia mapadre, akaenda na kulifikia lile kaburi akasimama na kuinua uso wake, mbele yake aliliona jumba kubwa la Don Andreas likiwa limetulia kabisa. Akainama na kuweka lile ua juu ya kaburi hilo, akatulia kimya akiwa amezama katika sala lakini muda wote akiwa analiangalia lile jumba, kwa kutumia miwani yake aliweza kupiga picha kadhaa lile jumba huku akingalia jinsi ulinzi mkali ulivyo, askari waliokaa juu kaabisa ya jengo walionekana kwa uzuri wakiwa na bunduki zao za kawaida tu wakiimarisha doria.

Alipohakikisha ameridhika na utafiti wake, aliinuka na kulielekea gari lake, mara akasimama ghafla, baada ya kukuta watu wawili waliosimama katika gari yake mmoja upande huu na mwingine upande ule. Kamanda Amata aliwatazama harakaharaka watu wale waliovaalia suti nyeusi wakiwa na vipara vichwani mwao, kila mmoja alionekana kutafuna jojo ikiwa ni moja ya kupambana na baridi ya mji huo. Kamanda Amata akaendelea kuifuata gari yake, hakutaka wajue kama ameshtuka kuwaona pale, akafika na kuwasalimu, lakini hakuna aliyejibu, akauendea mlango wa gari yake na kutaka kuufungua, Yule jamaa akamshika mkono kumzuia asiufungue ule mlango, kamanda Amata aligeuka na kumtazama,

“Mnataka nini?” aliwauliza kwa lugha ya Kijerumani isiyo na kovu lolote, “Tunakutaka wewe!” mmoja alijibu, wakati huo Yule mwingine alikuwa akizunguka kuja upande ule, alipomfikia Amata akamshika ukosi wa kanzu yake na kumvutia upande ule wa pili alikokuwa wakati huo Yule mwingine alikuwa ameingia katika usukani akisubiri mateka wao apandishwe garini. Kamanda Amata alikuwa mpole kupita maelezo, alipofikisha kwenye mlango wa upande wa pili ndipo alipowaonesha kuwa yeye ni nani, liwiko kilichotua katika kidevu cha yule jamaa kiliangusha jino moja, kabla hajakaa sawa alimpa konde la kwanza na la pili ambayo yalimpeleka chini. Yule wa ndani akaona mwenzake anazidiwa, akachomoa bastola aanze mashsmbulizi, akachelewa, Kamanda Amata hakuwepo mahali pale, alikuwa ametoweka kama mzuka, akiwa katika kushangaa hilo aliguswa mgongoni na Kamanda ambaye alikuwa nyuma yake upande ambao hakutarajia, alipogeuka alikutana na konde moja lililoshiba kisawasawa ambalo lilimpotezea mtandao kwa sekunde kadhaa, alivutwa chini na Amata na kupewa kichapo cha mbwa mwizi ambacho kilimuacha hoi, akamshika mkono wake huku akimshikisha bastola ileile akamgeukia yule mwingine aliyekuwa akijivutavua pale chini, kwa kupitia uvungu wa gari, alivyatua risasi moja ilifumua vyema goti lake kisha akamgeuzia huyu aliyekuwa naye na kumfanya kitu kilekile.

“Mpeni ujumbe Bill, mwambieni kifo chake kimekuja mlangoni mwake,” Kamanda Amata aliwaambia kwa lugha ya Kijerumani na kuingia kwenya gari yake na kutokomea. Yule mwenye bastola akaona asipoteze nafasi, akacheza na bastola yake kulenga tairi la gari ya Amata lakini alishangaa vyuma vikigongana tu, alipotazama ile bastola haiukua na magazine, alibaki kuduwaa maana hakujua ni wakati gani imeondolewa.
Kamanda Amata aliendesha gari kwa kasi sana mara hii kuelekea misheni alikofikia, aliingia getini na kukuta misa ya maazishi ikiendelea, akaegesha gari na kuteremka harakaharaka, akauendea mlango mkubwa na kupanda kuelekea katika chumba chake, akafika na kujifungia chumbani, akaenda katika ule mtambo wake alioufunga pale dirishani na kuanza kuchunguza nyumba ile, hakujua ni jinsi gani wamejua kama yupo katika mji huo au wameotea kwa kuwa yeye ni mweusi. ‘Mara hii sipotezi nafasi,’ alijiwazia, akchungulia vyema kupitia ile darubini yake, akaangalia vizuri jumba lile tena kwa dirisha moja baada ya jingine, alipofika dirisha la ghorofa ya pili ndipo aliweka tuo kuangalia kinachoendelea.

Hakuweza kusikia lakini aliweza kuona matendo ya watu wawili waliokuwa wakibishana kitu, alijaribu kuziangalia sura zao lakini hakufanikiwa kuzipata, akageuza darubini yake na kuangalia upande mwingine wa jengo lile. Gari moja nyeusi aina ya BMW ya kisasa kabisa ilikuwa ikiegeshwa polepole kabisa mbele ya jumba lile huku ikifuatwa na gari nyingine mbili za mtindo ule. Mtu mmoja mnene, aliyevalia nadhifu kabisa alishuka ngazi akifuatwa na wanadada wawili na vijana wengine wawili waliokuwa kwenye suti nadhifu.

Kamanda Amata aliendelea kuwachunguza na kuwaona wakiwa kamili na vyombo vya mawasiliano masikioni mwao, wote wakaingia katika magari na kisha ule msafara ukaondoka, na kuchukua barabara kuu kuelkea upande wa pili wa mji. Kamanda Amata akashusha pumzi, lengo lake yeye ajue kama Bill huwa anapatikana katika jumba lile au la. Alichomoa memorycard kutoka katika ile darubini akaipachika katika kompyuta yake kisha akatuma zile picha kwa Chiba Tanzania, acheki kama zina lolote. ‘Nimuueje Bill?’ alijiuliza, ‘Uso kwa uso au nimdungue kwa mbali?’ bado alikuwa akishindana na nafsi yake katika kuamua juu ya hilo, ‘Kumdungua ni kumuogopa, nitapambana nae,’ alikata shauri.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
SEHEMU YA 22
Alichomoa memorycard kutoka katika ile darubini akaipachika katika kompyuta yake kisha akatuma zile picha kwa Chiba Tanzania, acheki kama zina lolote. ‘Nimuueje Bill?’ alijiuliza, ‘Uso kwa uso au nimdungue kwa mbali?’ bado alikuwa akishindana na nafsi yake katika kuamua juu ya hilo, ‘Kumdungua ni kumuogopa, nitapambana nae,’ alikata shauri.
§§§§§
BILL hakuamini anchosikia kutoka kwa mmoja wafuasi wake, kuwa Kamanda Amata yupo Aachen na tayari ameshawajeruhi vibaya walinzi wa nje wa Andreas waliokuwa wakimfuatilia kule makaburini. “Nani aliwaambia yule mtu anafuatwa namna hiyo mliyofanya nyie?” Bill aliwauliza wale vibaraka wake. Baada ya kumaliza mazungumzo yake na watu wake, hakuna kilichokuja akilini mwake zaidi ya kukimbia mji huo na kujificha sehemu nyingine, ‘Lakini nitaonekana nimemuogopa, nitapambana nae hapahapa. Bill alitoka mchana huo na kuelekea mjini ambako baada ya pitapita zake akaingia katika kanisa kuu la mji huo, akiwa sasa medhamiria na ameamua kumsaka Amata kwa njia yoyote ile. Alikuta watoto wakicheza cheza katika ngazi za kanisa hilo, mara mbele yake gari oja ilikuwa ikija pale aliposimama, Bill akaisimamisha, alikuwa ni Fr Frank, akitoka kwenda mjini kutafuta mahitaji, Bill aliiendea ile gari na kufungua mlango akaingia na kuketi kiti cha pembeni bastola mkononi, “Unahifadhi wanausalama sio?”
Alimuuliza Fr Frank ambaye alionekana kutetemeka mwili mzima. “Hapana, hapana,” akamjibu. “Huyo kasisi wenu mweusi ni nani? Si Kamanda Amata?” swali lingine lilitua sikioni mwa Fr Frank. Kisha Bill akamuamuru Fr Frank kuendesha gari mpaka maeneo anayoyajua yeye. Lilikuwa ni shamba kubwa ambalo lilikuwa na aina mbalimbali ya miti na mazao, Bill alimshusha Fr Frank na kumuongoza katika banda Fulani, akaingia, alichokifanya ni kumfunga kamba kisha kuanza kumpa mateso makali ili amueleze kama ni kweli wamemficha Kamanda Amata ndani ya nyumba yao, Fr Frank hakujibu kabisa swala hilo.
“Unajifanya jeuri siyo, basi yatakupata yaliyompata Fr Gichuru kule Nairobi,” Bill alimwambia Fr Frank huku akimpa kipigo kikali kwa kutumia mkanda wa kijeshi.
Kisha akamuacha ndani ya banda hilo nay eye akaondoka kurudi mjini. Breki yake ilikuwa moja kwa moja ofisini kwa Andreas, kumpa habari hiyo nyeti. Andreas hakuonekana kuumiza kichwa kwa swala hilo. “Bill, nimeshakwambia fanya nunaloweza umuue bas, sitaki habari nyingine,” Andreas alisisitiza. Kabla hajajibu kitu, Andreas akamwambia Bill, “Ila leo jioni tukutane pale nyumbani kuna tafrija fupi kwa ajili ya kijupongeza kwa kukamilisha hili swala, na Fr Gustav atakuwepo maana tayari yuko njiani.” Bill aliupokea mualiko huo na akawa tayari kujumuika na wageni watakaokuwepo siku hiyo.
Fr Frank alibaki kule bandani peke yake, mwili wake ukiwa hoi kwa maumivu makali ya kipigo alichokipata kwa Bill, kwa kutumia ujanja alionao alijua jinsi ya kujinasua katika kifungio hicho,
Akafanya makeke yake na baada ya dakika kumi na tano alikuwa huru, sasa kilichomsumbua ni kupata funguo ya kutokea nje. Fr Frank alitafuta mahali pazuri kwa kujificha ndani ya banda lile akapapata, akajificha na kutulia tuli akisubiri yeyote atakayekuja aelewane nae. Fr Frank hakuwa mjinga katika mapigano iwe ya mikono au ya silaha, alikumbuka sana alipokuwa jeshini mara baada ya kuhitimu masomo yake huko Austria, alipokuwa akijifunza karate na kungfu akiwa seminari, alimstahi Bill kwa kuwa alihisi labda kuna kitu atakachokigundua mahali hapo. Fr Frank aliajiriwa na FBI kisirisiri na alikuwa hapoa Aachen kwa kazi moja tu ya kumnasa Bill na kupeleka taarifa zote huko Marekani ili wajue jinsi ya kumnasa na kumuweka chini ya ulinzi. Hakutaka kujionesha juu ya hilo hivo alikuwa makini sana katika kulifanya. Ni miezi mitatu sasa tangu ahamishiwe katika kanisa hilo kuendelea na uchunguzi wake, na alikuwa akiju kila ktu kilichotokea kule Nairobi. Akiwa katika mawazo kule katika maficho yake alisikia mlio wa gari ikija maeneo yale akatulia na kusubiria watu hao ambao walikuwa wakizungumza wao kwa wao, harakaharaka alielewa kuwa watu hao wa[po watatu. Mara mlango ulifunguliwa na wale jamaa wakaingia ndani wakashangaa kukuta kiti wazi, hayupo Fr Frank.
Mmoja wao akainua redio yake na kutoa taarifa kwa waliowatuma kuwa mtu wao katoroka, akiwa tayari kamaliza kuongea na simu hiyo, aliirudisha mahala pake na kwaamuru wake wenzake kumfuata, lakini kabla hajafika mbaliki lilikuwa ni t eke zito lililotua nyuma ya sjingo yake, kisha akajiviringa na kusimama upande wa pili, wale wawili nao wakaja kwa pamoja Fr Frank akaruka juu nakuitawanya miguu yake na kumpiga kila mmoja kwa mguu wake, mmoja alijibamiza vibaya katika nguzo iliyokuwa katika banda hilo na kupasuka sehemu ya nyuma ya kichwa chake. Akajibwaga chini akiwa tayari hana uhai, wakati mmoja akiwa tayari katoka nje mwingine aliendelea kumkabili Fr Frank, alirusha ngumi ikakwepwa, akarusha nyingine ikakwepwa tena kwa mtindo uleule, kabla hajakaa sawa Yule jamaa akapigwa teke hafifi katika kanyagio la mguu wake, aliposhusha sura kuangali chini, alijikuta anachezea makonde yasiyo na idadi ambayo yalimpeleka chini sakafuni akiwa hajiwezi, akiwa anatambaa alipigwa teke moja la nguvu mbavuni na akalala chini bila kipingamizi.
Fr Frank alimwangalia Yule jamaa akigalagala pale chini, mara akakumbuka kuwa kuna aliyetoka nje, akaichomoa bastola katika mfuko wake na kuvuta hatua chache kuuelekea mlango, mara akasikia nyuma yake mlio wa kiondoa usalama cha bastola, kwa kazi ya ajabu aligeuka na tayari kidole kilikuwa kwenye trigger, aligeuka huku akiwa anaenda chini kupiga goti moja akachezesha kidole na risasi mbili zikamtwanga Yule jamaa kifuani, akatoa yowe la maumivu nay eye akajiunga na wenzake pale sakafuni.
“Mwambe Bill, sina shida nae, na hsinifuate fuate,” alimwambia Yule aliyekuwa hai bado lakini hali yake ilikuwa mbaya kwani alimvunja mbavu mbili.
Akatoka nje ya ile nyumba na kuingia katika gari yake iliyotumika kumleta pale akapotelea mjini kama kawaida, akarudi mpaka misheni, akaegesha gari palepale, na kuingia ndani.
§§§§§
KAMANDA Amata hakuamini anachokiona katika darubini yake, mmoja wa wahudumu wa misheni, aliyempokea siku alipofika alikuwa akiongea na watu Fulani katika jumba la Don Andreas, Kamanda Amata akagundua hapo kuwa kumbe siri zingine za yeye kufika pale ijapokuwa ilikuwa kwa njia ya siri ni yeye aliyeipeleka kwa watu hao, akatoka na kuelekea jikoni, pale aliwakuta wafanyakazi wengine wakiandaa chakula cha jioni, hakuongea na mtu, akakiendea kibao kinachoonesha zamu za wafanyakazi, kweli siku hiyo Yule mfanyakazi alikuwa off, akaondoka akarudi ndani kila mtu mle jikoni alikuwa akimwangalia mtu huyu mweusi, walimdharau kwa rangi yake lakini yeye hakujali. Alirudi tena chumbani kwake mara hii hakumuona Yule mtumishi pale alipokuwa mwanzo.
Akatembeza tena darubini yake na kunasa dirisha linguine lakini hakuwaona wale watu waliokuwa wakiongea na Yule mhudumu. ‘Msaliti’ alijisemea, na mara mlango wake ukagongwa, akauendea na kuufungua taratibu, alikuwa Fr Frank, akaingia na moja kwa moja akasimama mbele ya Kamanda, “Bill ameshajua kama tuko hapa?” Frank alisema, Kamanda Amata akatulia kumwangalia, hakuielewa kauli yake, “Uko hapa na nani?” akauliza. Fr Frank akagundua kuwa ametereza katika maongezi yake, akamtazama Amata, akakutana na sura ilijikunja kuwa sasa haina utani hata kama na askofu, Kamanda Amata akatoa bastola yake na kumnyooshea Fr Frank, “Niko na nani?” akauliza tena, “Mmeamua kunicheza shere sio? Mpishi wenu anatoa siri za mimi kuwapo kwa Bill sivyo, kumbe mnajua kila kitu, niambie niko na nani?” akazidi kuuliza.
Fr Frank hakuwa na la kujibu, “Usihofu Kamanda, mimi si mbaya kwako,” akasema huku akitetemeka.
“Ninyi wote ni wasaliti humu ndani,” Kamanda Amata bhakuonesha kabisa masihara katika hilo, uso wake uliloa jasho la hasira. Fr Frank akamtazama tena Kamanda,
“Mimi niko upande wako Kamanda,” akamwambia.
“Naitwa Frank Edson, kutoka FBI, idara ya upelelezi ya Marekani, nipo hapa kwa kazi maalumu lakini hakuna anayejua,” akajieleza.
“Lete kitambulisho,” kamanda akaomba, Fr Frank aktoa kitambulisho katika mfuko wake wa ndani na kumpa Amata akakisoma, ni sahihi kabisa.
§§§§§
Frank Edson, mpelelezi kutoka shirika la kipelelezi la Marekani FBI, alikuwa amepewa kazi maalum na ofisi yake, kazi ya kumfuatili Bill ili amtie mkononi na kumpeleka Marekani akajibu mashitaka yake. Frank kama alivyo alikuwa kasisi katika kanisa la Katoliki huko Texas Marekani, ijapokuwa alikuwa akifanya kazi hiyo kwa siri kubwa sana lakini viongozi wake wa juu walilifahamu hilo.
Katika harakati za kumsaka Bill kama jasusi linaloendesha shughuli zake kwa kukodiwa kwa nia mbaya na matajiri mbalimbali duniani, Marekani ilianza kumsaka tangu pale alipotekeleza mauaji ya balozi wao kule Iraq miaka kadhaa nyuma. Walimsaka kila kona bila mafanikio. Bill akaibuka tena katika sakata hilo la Nairobi, kwa kuwa wale waliokuwa wametumwa Kenya walishindwa kumnasa Bill, Frank alitumwa muda mrefu huko Ujerumani kabla Bill hajaenda Nairobi, hivyo akapewa kazi ya kuhakikisha anamtia mkononi hukohuko.
Frank alifika Aachen kama kasisi aliyekuja kwa kazi maalum na kufikia katika kanisa kuu la Aachen. Hivyo alijua kila kitu kinachoendelea juu ya Bill, hata Kamanda ASmata alipokuwa anakuja, Frank alikuwa akimfuatilia tangu akiwa Nairobi hivyo alijuwa wazi kuwa lazima atafika kwa kazi hiyo. Ili asilete Madhara, kwa kuwa yeye alitakiwa ampfikishe Bill akiwa hai huko Marekani, alijua kuwa Kamanda Amata kaja kwa mawili kummaliza. Hivyo alimpokea Amata kwa maelekzo toka ubalozi wa Tanzania, wakijifanya kuwa kanisa linataka kushirikiana na Tanzania katika sakata hilo hasa kwa kuwa walikuwa wanaitaka monstrance yao kumbe sivyo.
Bill alimjua vyema Frank Edson, na alipewa taarifa kuwa yuko hapo kitambo na mmoja wa mashushushu wake ambaye ni mfanyakazi wa misheni hiyo. Frank Edson, siku zote hakugundua kuwa ndani ya misheni hiyo kuna mamluki mpaka alipokuja kupewa siri hiyo na Kamanda Amata.
ITAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
SEHEMU YA 23
ILIPOISHIA
Bill alimjua vyema Frank Edson, na alipewa taarifa kuwa yuko hapo kitambo na mmoja wa mashushushu wake ambaye ni mfanyakazi wa misheni hiyo. Frank Edson, siku zote hakugundua kuwa ndani ya misheni hiyo kuna mamluki mpaka alipokuja kupewa siri hiyo na Kamanda Amata.
§§§§§
Fr Frank akamuonesha Kamanda Amata beji yake maalum ya FBI iliyobanwa vizuri katika loop ya suruali yake. Kamanda Amata akashusha bastola yake na kuirudisha kiunoni. “Samahani, si unajua hizi kazi zetu hakuna kuaminiana,” akamwambia Frank, “Hamna shida hata ningekuwa mimi ingekuwa hivyohivyo,” akajibu Frank, kisha wote wakasogea pale dirishani.
“Sikiliza, unamjua huyu?” kamanda akamuuliza na kumuonesha baadhi ya picha zilizopigwa na ile camera yake aliyoiunganisha na ile darubini pale dirishani, Frank alipigwa na bumbuwazi akabaki midomo ikimchezacheza, “Kaka ungeshakufa muda mrefu sema tu huo ukasisi wako umekulinda, la tayrai mauaji ya kasisi yangeshafanyika hapa Aachen,” Kamanda alimwambia Frank huku akimpigapiga kifuani kwa ngumi yake.
“Sasa Kamanda, hapa mambo yameshaharibika inaonekana huyu mpishi anajua na ameshawapa kila habari zetu, ndo maana walikufuata kule makaburini. Bill huwa hatoki ovyo lakini alinifuata leo hapa,” Frank akmwambia Kamanda. Habari hiyo ilimfanya Kamanda kushtuka, “Unasema Bill alikuja hapa?!” kamanda akauliza.
“Ndiyo, Bill kaja akaniteka hapa leo asubuhi na kunipeleka huko kwenye maficho yao,” Frank akaeleza. “Sasa nani kakuokoa?” lilikuwa swali la Kamanda.
“Si nimekwambia mi ni FBI yaani Federal Beureau of Investigation, sishindwi kujiokoa kwa watu dhaifu kama hawa,” Frank alitamba, sasa akiwa amevua ile kanzu ya kikasisi. “Laiti ningepata hiyo nafasi ningemmaliza huyo mtu palepale, maana sihitaji mahojiano naye, nimetumwa kuirudisha roho yake kwa muumba wake, bas,” Kamanda akamwambia Frank. “No Kamanda, sikiliza, unatakiwa unisaidie tumpate Bill akiwa hai, serikali ya Washington inamtaka akiwa hai ili akaungane na wenzake kule Guantanamo bay,” Frank akamwambia Amata.
“Hamna shida, mimi serikali ya Dodoma imenituma niitenganishe roho na mwili wake, so tutagawana, wewe utamchukua akiwa hai na mi nitamtoa roho yake,” Kamanda Amata alimwambia Frank, kisha wakatazamana si kirafiki tena sasa kiadui zaidi. “Na hapa siwezi kuishi, hapanifai, kwa heri ya kuonana,” Amata akamalizia, kisha akamuacha Frank bado amesimama akitweta kwa hasira wakati yeye anaifungua ile darubini yake pale dirishani.
Saa moja baadae, Kamanda Amata alikuwa nje ya uwanja wa misheni hiyo, hakuna aliyejua kuondoka kwake, akiwa kava kofia kubwa aina ya pama na miwani myeusi akasimamisha tax iliyokuwa ikipita mbele yake, “Novotel tafadhali,” Kamanda alimwambia Yule dereva, naye bila kushangaa alipiga gia na kusonga mbele, dakika chache walikuwa mbele ya hotel hiyo, “Deutsche Mark 75 tafadhali,” Yule dereva alimwambia Amata, “Bado unatumia hiyo pesa ya kizamani? Hapa nina Euro na Dollar,” Kamanda akmwambia yule dereva, “Ok, US Dolar 65” akabadilisha, Kamanda Amata akampatia pesa yake kisha akaiendea kaunta ya bhotel ile.
“Nikusaidie boss,” mmoja wa wahudumu alichukua suitcase ya Amata na kutangulia Kaunta kisha akasubiri pembeni.
“Jina tafadhali,” sauti ya mhudumu mrembo kama Malaika ikamuuliza Kamanda Amata. Kama unavyojua ugonjwa wa kamanda Amata, warembo, akatabasamu, “Fransisco Kintu,” akajitambulisha kwa jina bandia. Yule mhudumu akaandika kwenye kompyuta yake, “Passport yako au kitambulisho tafadhali,” Yule mhudumu akaomba vitu hivyo kimojawapo. Kwa kuwa Kamanda daima alikuwa habahatishi, alivuta wallet yake na kuchomoa moja ya kitambulisho akampa, ‘Fransisco C. Kintu – Utaifa: Uganda – Kazi: Muandishi wa habari UBC.’ Maelezo hayo yalionekana juu ya kitambulisho. Baada ya kuingiza maelezo hayo katika kompyuta yake, akamrudishia kile kitambulisho.
Kamanda Amata akauliza bei kwa siku, akatajiwa akahesabu fedha ya siku mbili akampa Yule dada, “Oh samahani bwana Fransisco, tuhitaji Maestro card au Visa card kama hauna basi kadi yoyote ya malipo,” Yule mhudumu alimwambia Amata, akili ya Kamanda ikafanya kazi haraka, “Samahani situmii hivyo vitu, ninalipa cash, kama haiwezekani basi.”
“Ok, nitakusaidia kwa leo, lakini mara nyingine ukija Ulaya hatulipi kwa cash, sawa bwana?” Yule mhudumu akamwambia Kamanda kwa lugha safi ya kiingereza.
“Ich danke Ihnen” (nakushukuru) Kamanda Amata alishukuru kwa Kijerumani msaada huo.
“Danke, gleichfalls!” (nakushukuru pia) Yule mhudumu naye akajibu, huku akisimama na kelekea sehemu Fulani, akaja na kadi mkononi akampatia, Kamanda Amata akaitazama, kisha akatoa kadi yake ya kibiashara na kumuwekea mezani, akaondoka pale kaunta na kuelekea ghorofa ya juu kwa kutumia lift.
175 ilikuwa ni namba iliyosomeka mlangoni mwa chumba hicho, Kamanda Amata kama kawaida yake aliingia ndani na kukikagua chumba hicho kwa staili ileile aliyoizoea kuona kama kuna chochote cha kufanya ajulikane uwepo wake.
9
CHAKULA cha jioni kilikuwa tayari, simu ikapigwa chumbani kwa Amata kutoka pale kwenye chumba cha chakula ambapo Fr Frank na wageni wengine walitumia. Simu iliita kwa muda mrefu haikujibiwa, ikarudiwa na kurudiwa lakini wapi. Ikabidi Fr Frank aende chumbani kwa Kamanda Amata akamwangalie, alipogonga mlango hakuna jibu lililotoka ndani, akanyonga kitasa na mlango ukafunguka, alipoingia ndani hakukuta mtu, chumba kilikuwa tupu, kitanda kilitandikwa vizuri kana kwamba hakukuwa na mtu aliyekuwa akikitumia chumba hicho.
Akili ikamzunguka Fr Frank, akaona sasa kazi yake inakuwa ngumu ya kumpata Bill akiwa hai kutokana na kutoweka kwa Kamanda Amata.
Fr Frank alirudi mezani akiwa na hasira, “Mgeni wetu hayupo, kaondoka bila kuaga,” wale wahudumu wakashangaa kapitia wapi kwa kuwa hawakumuona kupita hata katika mlango wa kutokea nje. Fr Frank ndipo alipoelewa maneno aliyoambiwa tangu mwanzo na wakuu wake wa kazi, ‘Mtazame sana Kamanda Amata, ni mjanja zaidi ya CIA, huyo ni TSA no 1 ana uwezo wa kujigeuza hewa,’ Fr Frank alipokumbuka maneno hayo akaanza kucheka mwenyewe, kisha akaketi na kuendelea kula huku akifikiri zaidi juu ya Amata, kama alitaka kufanya kazi aliyopewa kwa muda mrefu basi sasa ilimlazimu kubadili utaratibu huo kwani Kamanda Amata alitaka kuifanya kwa muda mfupi zaidi, kasheshe.
§§§§§
NOVOTEL AACHEN – CASINO
KAMA ILIKUWA ni siku ya bahati kwa Kamanda Amata basi hiyo ilikuwa mojawapo kati ya chache katika maisha yake. Alipotoka kaunta alipewa kijikaratasi kama brosure ndogo, hakuwa na muda wa kuifungua ndani, baada ya kujiweka sawa, alipomaliza kuoga na kuchagua suti safi kati ya zile alizozikuta ndani ya kabati hilo, akaijonge meza yake na kukinyanyua kile kijikaratasi kilichopambwa kwa rangi za dhahabu za kuvutia, akakifungua na kukisoma, kilikuwa ni juu ya shindano la kamali ambalo lingefanyika siku hiyo saa 3:30 usiku katika casino iliyopo katika hotel hiyo, matajiri wengi walialikwa, hakuamini kabisa kama katika walioalikwa alikuwemo Don Andreas.
Akajua hapo kuwa Don Andreas ni mcheza kamali maarufu sana kwa jinsi alivyoelezewa pale katika hiyo karatasi, pia matajiri wengine wengi walialikwa, hivyo hata yeye alipewa nafasi kama angependa kushiriki, ama kwa kutazama shindano hilo au kwa kushindana kama ana uwezo. Tabasamu pana likaupamba uso wa kijana shababi, Amata. Katika ile karatasi ya mualiko kulikuwa na namba za kupiga kama utahitaji kushiriki kucheza, akavuta simu ya mezani na kupiga hizo namba kisha akaongea na mchezweshaji wa huo mchezo na kusajiliwa. Kamanda Amata akasubiri muda ufike ili aweze kushiriki mchezo huo na pia kuonana na Don Andreas ana kwa ana.
SAA 3:00 USIKU
POKER POINT
WAGENI walianza kuingia katika ukumbi huo mkubwa wenye kila aina ya starehe, huku kukiwa na muziki wa jukwaani ukipigwa na mwanamama mkongwe aliyealikwa siku hiyo Tina Turner kutoka Marekani. Watu walikuwa wengi na kila mmoja alionekana akiwa ametingwa na shughuli zake ama kunywa pombe na wapenzi wao au wakicheza michezo kama roulette, slots machine, lucky wheel na mingineyo mingi.
Ni meza moja kubwa sana ilibaki wazi hakuna mtu aliyeketi kwenye viti vilivyozunguka meza hiyo, viti kumi na nne, saba kwenye mstari wa mbele uliopakana na meza hiyo yan kijani yenye michoro kadhaa na saba vingine vilikuwa nyuma yake, lundo la karata maalum zisizochoka lilikuwa limewekwa hapo juu, taa angavu kabisa isiyokusumbua macho ilikuwa ikiwaka na kumulika eneo lile nyeti kwa watu nyeti. Mmoja baada ya mwingine waliingia eneo lile wakisindikizwa na akina dada warembo kabisa na kuwapanga vitini kwa namba. Baada ya kutimia vilibaki viti viwili, kimoja cha mbele na cha nyuma cha mpambe.
Wote walishangaa kumuona mtu anayeletwa na mwanadada mrembo, kijana mweusi, aliyependeza kwenye suti nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe na tai ndogo ya kubana shingo (neck tie), akakribishwa na kuketi katika kile kiti kimoja, akawatazama mmoja baada ya mwingine kisha mchezo ukafunguliwa na mchezeshaji akiwataka wachezaji kujitambulisha mmoja baada ya mwingine. Kila mmoja alijitambulisha na Kamanda Amata alijitambulisha kwa jina lile la bandia akijisema kuwa yeye ni mwanahabari lakini ni mcheza kamali mzuri sana katika macasino ya Afrika Mashariki. Akakribishwa kwa kupigiwa makofi. Kamanda Amata alijikuta akiwa amekaa uso kwa uso na Don Andreas.
Mtu mmoja mnene, mwenye sura ya tabasamu muda wote, alikuwa akimtazama kijana huyu bila kummaliza. Mchezo ulianzishwa na kila mmoja alitakiwa kuweka dau la kuanzia lisilopungua $ 2500, matajiri hao wakaanza kuweka na kuweka pesa zao kwa kutumia chungu maalumu kilichopitishwa mezani na mmoja wa wachezeshaji. Kila mtu aliweka kiwango anachojua kuwa anaweza kumudu. Zamu ya Kamanda Amata, kila mmoja alimtazama usoni, akaingiza mkono ndani ya koti na kutoa $ 5000 na kuweka katika chungu hicho. Mcehezo ukaanza taratibu kila mtu akiwa na karata zake. Mchezo ulikuwa mgumu kidogo kwa maana kila mmoja alikuwa anatumia akili sana katika kuzifananisha karata hizo na zile zilizofichwa, kila aliyeshindwa alitoka, hivyo wakazidi kupungua, Kamanda Amata alikuwa wa nne kutoka na kuwaacha watatu, Don Andreas, na tajiri kutoka Venezuela pamoja na mwanamama tajiri kutoka Berlini.
Mchezo ukaendelea na mwisho wa mchezo Don Andreas akatoka mshindi na kukusanya maelfu ya dola za Kimarekani.
Makofi ya pongezi yakatawala katika meza ile. Mchezo ule ukaisha, ukatakiwa kuanza mwingine kwa wale wanaohitaji kuendelea. Wote walirudi tena mezani na ‘betting’ zikaanza kwa mara nyingine, chungu kikapita na kila mmoja akatia mkono kuweka chochote lakini wenzako sharti waone kile uwekacho, zamu ya Kamanda Amata, kama kawaida wote walimtolea macho, akaingiza mkono wake tena katika koti na kutoa kitita kama kilekile, $ 5000 zingine akaweka, wengine katika katika mchezo ule wakaguna, kwa jinsi walivyomtazama hakuwa na muonekano wa kuwa na pesa kiasi hicho anachotoa katika kila bett moja.
Yeye mwenyewe hakuwajali, kwa kuwa hakuna aliyejua mpaka hapo kuwa ni nini anachokitafuta, hivyo hakuona tatizo kutumia pesa hizo anazopewa maalum kwa ajili hiyo ili kupata kile anachotaka. Mchezeshaji aliendelea kuchezesha mchezo ule kwa makini na mbwembe za hali ya juu. Mchezo ukaendele, poker, mchezo wa karata ambaon unatakiwa ucheze kwa kupanga kareta zako zifanane na ile iliyofichwa ambayo hakuna anayeijua, mchezo wa matajiri unaochezwa kwa kuwekeza pesa nyingi, wengine huweka magari au majumba. Kamanda Amata mchezo huu aliupanda sana na sehemu yake kubwa ya kucheza ilikuwa pale New Africa casino, Dar es salaam. Wachezaji walianza kupungua katika mchezo kwa kuwa hawakufaulu, walizidiwa maarifa na wengine, mara hii Kamanda Amata alidumu katika mchezo, japokuwa hakushinda lakini alitoka wa pili na mchezo wa mwisho alicheza na Don Andreas, ambapo alizidiwa kwa ujanja mdogo sana.
“Mr Fransisco, unaweza kucheza tena kwa kuwa umeikaribia bahati, umekaribia utajiri, weka dau lingine na ucheze tena. Kamanda Amata alijikuta hana pesa zaidi, alikuwa na kiasi kidogo ambacho hakingefaa sana kununua token. Mchezeshaji akawapa breki ya kujiweka sawa. Kamanda Amata akainuka na kuelekea kaunta ambako aliagiza glass moja ya pombe kali, akinywa taratibu huku akiandika ujumbe kwa kupitia saa yake kwenda kwa Madam S, dakika moja baadae, alipata majibu na akayafanyia kazi. Mara moja akafanya mchakato palepale hotelini kuweza kubadilisha pesa aliyotumiwa na Madam S, $ 1500 si haba kwa mchezo huo wa mwisho kwa mujibu wa Yule mchezeshaji.
Meza ilijaa tena wadau, kabla hawajaanza mchezeshaji akatoa rai yake kama ilivyo sheria ya mchezo.
“Sasa tunaingia raundi ya mwisho, tumeona wote waliofanya vizuri katika raundi zilizopita, tumeona pia uchezaji wa mgeni wetu kutoka Uganda si mbaya sana, sasa angalisho, kila mtu aweke dau ambalo hatoathirika katika akiba yake baada ya kushindwa mchezo huu,” akamaliza kusema kisha akzungusha chungu, wote wakaweka mapesa kibao, mmoja wao, Yule tajiri wa Venezuela alikuwa ameishiwa na kubaki na kiasi kidogo, akaweka dau gari yake ya thamani, Marcedes Benz CLA45 AMG 4MATIC 355-hp. Ilikuwa ni gari mpya kabisa, toleo jipya ambalo thamani yake si ya kitoto. Kamanda Amata akatupia katika chungu kile $ 1500 kama zilivyo, kila mtu akaguna tena, lakini hawakuguna kwa Yule aliyeweka gari kwa sababu walijua kuwa ana uwezo wa kununua nyingine.
Mchezo ulianza na kila mtu alikuwa makini sana mara hii, hakuna aliyetaka kupoteza mchezo huwo wa thamani kwa maana atakayeshinda atakuwa ni milionea wa kutupwa kwa pesa atakazokusanya. Lakini kamali ni kamali tu, mmoja baada ya mwingine walianza kupanguka. Mwisho wa mchezo wakakutana Don Andreas na Kamanda Amata. Ilikuwa ni nafasi nzuri sana kwa Kamanda Amata kutazamana uso kwa uso na tajiri huyo ambaye siri ya safari yake pale Ujerumani iko ndani ya kifua chake. Don Andreas alikuwa haelewi afanye nini, mara ajishike nywele, mara shavu, mara ajikune ilimradi kutaka kushinda mchezo huo wa dhahabu, wakati Kamanda Amata alikuwa katulia kitini akimtazama kwa makini tajiri huyo anavyochachawa. Wakati mchezo huo ukiendelea, kijana mmoja aliyevalia suti safi nyeupe aliingia pale mezani na kuzunguka nyuma ya Don Andreas akamnong’oneza kitu, Don Andreas alipata mshtuko wa mbali kidogo ambao mpaka uwe mzoefu wa mambo ya kiintelijensia ndio waweza kugundua.
Kamanda Amata aliisoma hali hiyo, akapata hisia ya kitu Fulani. Mchezeshaji alimuhamasisha Andreas kucheza. Mwisho wa mchezo, Kamanda Amata akaibuka mshindi, makofi mengi yalitawala wakatia akikusanya kete zote kuwa ni ushindi wake, pamoja na funguo ya gari ile ya kisasa, aliegemea kiti chake na kumtazama Don Andreas aliyeonekana kuchoka ghafla kitini mwake. Wale wengine walianza kuondoka mmoja baada ya mwingine kwa maana mchezo ulikuwa umefikia mwisho. Kamanda Amata aliiegemea tena meza na kumtazama Andreas.
“Sasa tucheze mimi na wewe, wawili tu,” Kamanda alimwambia Andreas. Don Andreas alimtazama Kamanda Amata.
“Sina dau kwa sasa la kupoteza, wewe tumia utajiri uliopata,” Don Andreas akamwambia Amata huku akijiandaa kuondoka, wapambe wake tayari walikuwa wamekwishafika. Kamanda Amata akamzuia Don Andreas kwa kumgusa kiganja cha mkono alichokisahau mezani, akastuka na kumtazama Kamanda,
“Dau unalo, tena la gharama sana,” kamanda Akamwambia Don. Tabasamu la uongo likatoka katika sura ya Andreas.
“Mostrance, weka dau Mostrance,” kamanda Amata alimwambia Don. Neon hilo lilimfanya Don Andreas kukunja sura ghafla na kurudi sawia kwenye kiti chake kama awali,
“Unasemaje Mr…” kabla Andreas hajamaliza kutaja jina, Kamanda Amata akajitambulisha rasmi, “…Kamanda Amata,” akamalizia. Ilikuwa ni kama tetemeko la ardhi ka Don Andreas kujua kuwa yupo na nani mbele yake.
“Hutoliona jua la kesho kijana,” Andreas akamwambia Kamanda Amata.
“Kama wewe ndiwe umeweka jua liangaze mchana, sawa, ila kama si wewe nitaliona, ila wewe na Bill sijui nani ataliona kati yenu,” Kamanda Amata alinyanyuka kitini na kuanza kuondoka huku yule mchezeshaji akikusanya zile kete tayari kuzibadili kuwa pesa ili apatiwe Kamanda Amata. Kamanda Amata alipoanza kuondoka akakutana na binti mmoja mzuri wa sura, mavazi yake yalionesha asilimia 80 ya mwili wake usiokuwa na nguo, wakasimama na kutazamana nyuso zao, Yule binti akatabasamu, tabasamu la wizi, kamanda Amata akamshika kiunoni na kuondoka naye mpaka kaunta ambako aliagiza kinywaji na kuanza kukimiminia kinywani mwake huku cheers nyingi na Yule binti, Kamanda alikuwa millionea ghafla, lakini alijua wazi hatari inayomkabili muda huo.
“Unahitaji cash au tukuwekee katika akaunti yako?” sauti ilitokea kaunta ikimuuliza Kamanda juu ya pesa zake, “Weka kwenye akaunti kisha nipe namba ya muamala wangu kwa ajili ya kuhakikisha,” alimjibu yule mhudumu wa kaunta.
“Beibi, nimekupenda ghafla,” Yule mwanamke alimwambia Amata. “Usijali leo ni mimi na wewe mpaka majogoo yawike,” kamanda Amata aliongea kwa Kijerumani cha kubabaisha, “Mmmm aliyekwambia huku kuna majogoo ni nani?” Yule binti alizidi maneno ya mtego, “Aaaaa jamani majogoo huyajui,” Kamanda Amata akawuliza Yule binti. Alipokabidhiwa kadi maalumu yenye namba za muamala wake, akamshika mkono Yule binti na kutoka nae pale kaunta, hatua mbili, mkono mmoja ukazungushwa kiunoni, wakapotelea nje ya hotel hiyo.
INAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
SEHEMU YA 24
“Mmmm aliyekwambia huku kuna majogoo ni nani?” Yule binti alizidi maneno ya mtego, “Aaaaa jamani majogoo huyajui,” Kamanda Amata akawuliza Yule binti. Alipokabidhiwa kadi maalumu yenye namba za muamala wake, akamshika mkono Yule binti na kutoka nae pale kaunta, hatua mbili, mkono mmoja ukazungushwa kiunoni, wakapotelea nje ya hotel hiyo.
§§§§§
BILL VAN GETGAND alishusha mtemba wake kutoka kinywani, akapuliza moshi mwingi hewani na kusababisha mchafuo wa mazingira kutokana na huo moshi taka, akashusha kioo cha gari iliyombeba mpaka chini kabisa, kisha akatupa kipisi kilichobaki kwa kulenga katika kasha maalum la takataka liliwekwa hapo jirani na maegesho.
Alimtazama Kamanda Amata akitoka na Yule binti wa kizungu, wakiwa wamekumbatian viunoni, walipolifikia lile gari, wakakumbatiana kwa kutazamana, wakapeana mabusu ya kuinyonyana ndimi zao. Kengele za hatari zikagonga katika kichwa cha Amata, akatoa miwani yake na kuivaa, alipotazama kwenye maegesho akashuhudia kioo cha Vogue kikimalizia kupanda juu, akajua kuna kitu.
“Uko peke yako?” Kamanda Amata akamuuliza.
“Yeah, peke yangu,” Yule binti akajibu.
“Huwa unakuja kufanya nini hapa?” swali lingine kutoka kwa Kamanda.
“Mmmmm huwa nakuja kutafuta wanaume wazuri kama wewe,” akajibu Yule binti. Kamanda Amata akaminya kitufe kwenye funguo ya gari aliyopewa na Benz moja nyekundu ikawaka taa zake kuashiria kuwa ndiyo yenyewe, akaiendea na kufungua milango akajitoma nyuma ya usukani, na Yule binti akakaa pembeni.
“Unanipeleka wapi?” akauliza Yule binti.
“Beach,” kamanda akajibu huku akiondoa gari ile katika maegesho. Nyuma yake ile Vogue nayo ikaondoka, lakini haikuwafuata njia waliochukua wao. Kamanda Amata aliendesha gari hiyo taratibu sana akiizunguka mitaa ya mji huo mkongwe kabisa huko Ujerumani, huku akiwa macho yake yakitazama nyuma, mbele kwa umakini mkubwa sana kujua kama kuna anyemfuata au vipi.
Kamanda Amata aliendelea kuzunguka katika mitaa ya mji huo bila kuegesha gari popote huku akiwa hana maongezi yoyote na Yule mwanamke katika gari hiyo.
“Hey beibi, mbona huongei, na wala huniambii unanipeleka wapi? Mi nataka twende kwangu,” Yule mwanamke alimuuliza na kumwambia Amata ambaye alikuwa ametingwa na usukani wa gari hiyo.
“Najaribisha gari yangu mpya, usijali, nikichoka tutakwenda kwako,” Kamanda Amata alimjibu Yule bibie huku akiendelea kuchapa mwendo, akipita barabara hii na kutokea barabara ile. Mara nyuma yake akasikia ving’ora vya polisi vikija upande wake, akaangali kwenye kioo cha kuendeshea gari akaona gari mbili za polisi zikija kwake, akaongeza mwendo na zile gari zikawa zinakuja kwa kasi.
“Polisi,”Yule mwanmke akamwambia Kamanda.
“Usiogope, hao sio polisi, kwa jinsi wanavyoendesha gari,” Kamanda Amata akajibu.
“AA 768 G weka gari pembeni!!” ilikuwa sauti kutoka katika kipaza sauti ambacho polisi wale walitumia kumsimamisha Kamanda Amata, lakini badala ya kusimama aliendelea kutimua mbio na gari lile, sasa alitembea mwendo wa hatari zaidi. Kamanda Amata kwa ujumla alikuwa akijua kuwa Andreas, Bill na vibaraka wao lazima watakuwa wakimnyemelea katika mitaa hiyo hivyo hakutaka kuuacha mji ule mapema wala hakutaka kurudi hotelini mapema ili aone nini mwisho wake, alishajua kuwa kurudi hotelini ni kujiweka kwenye hatari zaidi.
“Unaitwa nani?” ndio kwanza Kamanda Amata anagundua kuwa hakuwa amemjua kwa jina yuel mwanamke.
“Naitwa Hellen,” akajibu huku akijinyoosha kwa kujipindapinda mwili wake klitu ambacho kilimsisimua Kamanda Amata hasa alipokuwa akikiona kile kifua kilichopambwa na matiti mawili mazuri yakiyotuna kwenye kigauni hicho chepesi sana.
“Hellen, unamfahamu Don Andreas?” Kamanda Amata akauliza.
“Ndio, namfahamu sana, kwani kuna mtu ambaye hamfahamu tajiri huyo matata hapa mjini? Kibosile mpenda vimwana, vipi una shida naye?” Hellen akajibu na kurusha swali.
“Hapana siwezi kuwa na shida na mtu masikini kama Yule,” kamanda Amata akajibu huku akimtazama Hellen, wakati huo ile Mercedes Benz ilikuwa inasoma 158 km/h, mwendo mkali kwelikweli. “Mr Francisco, unajua wewe ni mgeni sana hapa Aachen,” akaanza dodoso zake za kike.
“Hapana, huwa nakuja mara nyingi sana hapa ila wewe hujawahi kuniona, kwa nini unauliza?” kamanda Amata aliendeleza mazungumzo kwa kuwa alijua nini kitafuata. “
Usimwite Andreas masikini, ana masikio zaidi ya million hapa Aachen,” Hellen aliongea kwa mapozi.
“Oooh, sikujua huyo atakuwa shetani basi, maana binadamu kawaida ana masikio mawili tu,” Amata akajibu kwa utani, lakini alipomwangalia Hellen akaona hata kutabasamu hakupo usoni mwake, akajuwa kuwa sasa kaanza kumfika moyoni kwa maneno yale. Hellen alimtazama Kamanda Amata hakummaliza, akaingia za mkono wake mkobani na kutoa kitu kama kikebe cha wino wa mhuri, akakifungua, ndani yake mlikuwamo na sigara tano na kiberiti cha gesi, vyote viliweza kutosha ndani ya kikebe kile. Akachomoa sigara moja na kuiweka mdomoni, akamtazama Kamanda Amata, kabla hajafanya lolote Kamanda Amata aliitambua ile sigara, haikuwa sigara bali ni mfano wa sigara ambayo ukiiweka mdomoni na kusukuma pumzi kwa nje, sio kwa ndani kama kawaida ya kuvuta sigara, hutoa vumbi jepesi sana ambalo litakupa usingizi ndani ya sekunde kumi tu. Kamanda Amata alimnyang’anya ile sigara na kuitupa pembeni, Hellen alipiga kelele, na kitendo hicho kilimfanya Kamanda Amata kukanyaga breki za ghafla akiwa katika mwendo mkali. Hellen alikuwa hajafunga mkanda hivyo alichomoka kwenye kioo cha mbele na kutoka mpaka nje akadondokea barabarani.
“Bull shit!” aling’aka Amata, akakanyaga klachi ya gari hiyo na kuweka gia ya kurudi nyuma na gari ile ikatii amei pale alipoachia klachi na kutimba pedeli ya kusukuma mafuta, kona moja kali ikamgeuza kutazama alipotoka na kutupia namba moja, kisha mbili, mara tatu, akawa amemuacha Hellen pale barabarani akiwa hoi na yeye kurudi kwa kasi alikotoka.
‘Mwanamke mpumbavu sana huyu,’ alijisemea moyoni huku akiongeza kasi ya gari lile ambalo injini yake bado ilikuwa ikidai gia ya sita wakati tayari zilikuwa zimekwisha zile zilizopo. Akiwa katikati ya mawazo yale na kumsonya Yule mwanamke huku akimtukana kimoyomoyo, aliona taa kali zikimmulika usoni akashindwa kupambanua njia halisi iko wapi na hicho pele ni kitu gani. Puuuuuuuu!!!!! Kishindo kikubwa kikasikika, gari aliyokuwa akiendesha Kamanda Amata ilikutana uso kwa uso na katapila la kutengeneza barabara, ilijipiga kwenye jembe la chuma cha pua, ikapinda boneti yote kuelekea kwenye kioo cha mbele, kisha lile katapila likainamisha jembe lake na kuiangusha ile gari na kuibonda vibaya,

ITAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
SEHEMU YA 25
ikaibeba tena na kukokota mpaka kwenye jalala la kutupa magari mabovu. Yule operetta wa lile katapila aina CAT aliinua simu yake ya upepo na kuongea na watu walio upande mwingine,
“Kazi tayari boss (…) hawezi kutoka mpaka Yesu arudi amtoe kimiujiza,” kisha akakata ile simu na kuegesha katapila lake pembeni. Range Rover Vogue, lilifika katika jalala lile ambalo halikuwa mbali sana na pale ilipotokea ajali ile ya kutengenezwa, ikasimama na watu wanne wakashuka, Bill akiwa mmoja wao mkononi akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea.
“Mali hiyo hapo boss,” Yule operetta akamwambia Bill huku akimuonesha kwa mkono ile Marcedes ilivyopondwa na kuwa chuma chakavu kwa ghafla namna hiyo.
“Vizuri sana, alikuwa ananiumiza kichwa sana huyu jamaa, akapumzike kwa amani, jivu kwa jivu. Vumbi kwa vumbi,” Bill alipomaliza kusema hayo, akampa Yule jamaa kitita cha noti kama shukrani kwa kazi hiyo ndogo aliyoifanya. Kisha wao wakarudi garini na kuondoka usiku ule, akaigeuza taratibu Yule drva na kuchukua uelekeo ule waliojia, Bill akainua fimbo yake na kuigemeza dirishani, ncha ya kutembelea ikwa imetazama kule aliko Yule operetta, akakifyatua kijichuma kidogo kilichoupande wa mshikio na kukivuta kwake, lo, Yule jamaa alikuwa akishangaa kuiangalia ile Vogue huku akiwa haamini kupata kile kitita cha noti, alijikuta akipenywa na kitu kama msumari kifuani mwake, mara akadondoka na kuanza kuona macho yake yanakuwa mazito kama yaliyojawa na ukungu, tayari kulikuwa ni giza muda huo lakini giza linguine zito lilimfunika, roho yake ikaacha mwili.
Bill alikuwa amemuua operetta Yule kwa risasi kutoka katika hiyo anayoifanya ni fimbo ya kutembelea. Kijana mmoja kati ya wale waliokuwa garini pamoja na Bill akashuka na kwenda mpaka pale kwa Yule operetta marehemu, akachukua ile pesa na kurudi garini, akamkabidhi Bill. “Kazi ngumu lakini imekwisha bila jasho, alale pema peponi Kamanda,” Bill alizungumza na ile gari ikaondoka eneo lile.
§§§§§
DON ANDREAS hakuamini anachoambiwa na Bill kuwa Kamanda Amata hayupo duniani. Akiwa katika sebule yake kubwa pamoja na mgeni wake kutoka Vatican, Fr Gustav Maker wakijivinjari kwa vinywaji vikali, wote waliifurahia taarifa hiyo kutoka kwa Bill. Dakika chache baadae Bill aliungana nao hapo sebuleni na tafrija isiyo rasmi ikaendelea.
“Kazi haikuwa rahisi mjomba,” Andreas alikuwa akimsimulia Fr Gustav juu ya mkakati mzima mpaka kuipata ile Monstrance.
“Pole sana mjomba lakini maadam umeipata basi utajiri wako utakuwa wa milele,” Gustav alimwambia Andreas, akinua glass yake iliyojaa kinywaji na kujimiminia kinywani mwake, kisha akamwangalia Andreas na Bill, “Iko wapi hiyo Monstrance?” akauliza.
“Ipo katika chumba cha siri,” Andreas akajibu, “Unataka kuhakikisha kuwa ipo au la?” akamtupia na swali.
“Yeah, hilo ni la msingi, nipeleke nikaione,” akaomba. Andreas aliinuka pamoja na Bill kisha wakafuatwa na Fr Gustav. Wote watatu wakaingia chumba cha siri ambacho ni mtu mmoja tu mwenye dhamana ya kukifungua, Andreas mwenyewe kwa kuwa mlango wake unahitaji, namba maalumu ya kubonyeza, alama ya kidole gumba na alama za macho, vyote hivyo ni vya Andreas, walipofika pale alifanya hayo yote, kisha wqakafunga kwa ndani na kuingia huko ilikohifadhiwa hiyo monstrance.
Fr Gustav, akaitazama ile monstrance kwa makini sana ikiwa imelazwa juu ya kijisanduku kidogo ambamo ilitosha kabisa, akainyanyua na kuigeuzageuza, ilikuwa iking’aa sana kutokana na taa iliyokuwa ikiwaka ndani ya chumba kile, ilikuwa ni dhahabu safi ambayo haijachakachuliwa bado. “Niliambiwa kuwa monstrance hii ina siri kubwa sana ndani yake, lakini mpaka sasa sijaijua,” Andreas alimwambia Fr Gustav.
“Ni kweli, na nimekuja hapa kwa sababu hiyo tu, hii Monstrance lazima irudi Vatican,” Kwa kauli hiyo, Andreas na Bill walibaki wakitazamana kabla ya wote kumgeukia Fr Gustav.
“We una kichaa ee!” Andreas alimwambia Gustav.
“Hata kama nina kichaa, lakini monstrance hii lazima irudi Vatican, siri iliyomo nitakwambia lakini hiki chombo lazima kirudi”
Gustav akaishika katikati ile monstrance mkono mmoja upande wa kitako na mkono mwingine upande wa juu akainyoga katikati kama anaivunja au anaifungua, ikafunguka, kisha akaweka kitako chini, akabaki na kipande cha juu. Don Andreas alikuwa bado akishangaa hakujua kuna nini kinafanyika.
“Na hii ndiyo siri iliyomo katika chombo hiki,” Gustav akawaambia huku akiinamisha na kikaratasi kirefu kikatoka ndani ya kile kibomba kidogo ambacho hushika kitako na sehemu ya juu ya chombo kile, Gustav akaiweka chini ile monstrance na kuchukua ile karatasi, akaifunjua kunjua kwa uangalifu, ilikuwa ni ramani kubwa sana inayoonesha njia za kupita mpaka kwenye hazina kubwa ya madini ya dhahabu iliyojificha huko kwenye milima ya Peramiho, kusini mwa Tanzania, mawe makubwa amabayo chini yake kulikuwa na kama mapango yenye madini ya thamani.
Andreas ilikuwa nusu azimie kwa kkile anachokiona, alikuwa akisoma maandishi yale ya kijerumani huku akiwa na tabasamu pana kuliko sura yake. Alipomaliza kuitazama ile ramani na kuyasoma kwa ufasaha yale maandishi yaliyoandikwa karne kwa karne lakini hayakuwa yamefutika, bado yalionekana kwa upya wake. Andreas alitingisha kichwa chake kuashiria kweli amekubali maneno ya babu yake. “Gustav, tumekuwa matajiri wa maisha,” Andreas alimwambia Gustav. “Ni kweli, lakini unajua hazina hiyo hiko wapi?” akauliza.
“Tanganyika kwa maelezo haya, ambayo ni Tanzania ya sasa,” Andreas alijibu.
“Na utaendaje huko kufanya hiyo kazi?” lilikuwa swali la Gustav.
“Aaah Gustav, hiyo sio shida, ni kwenda pale na kununua eneo lote lile, pesa ninayo, watanikubalia tu wale masikini kisha tunachimba. Siri ni uwekezaji tu, tukishawapa kishika mkono basi viongozi wataachia njia,” Andreas alisema kwa kujiamini.
“Haya nakutakia kila la kheri, lakini mmefanya kosa kubwa moja ambalo mimi sikulifurahia,” Gustav akaikatisha furaha ya Andreas.
“Kosa gani?” akauliza.
“Kosa ni watu uliowatumia, kumuua Fr Gichuru ni kosa kubwa sana ambalo usipoangalia litakugharimu,” Gustav akamwambia Andreas.
“Kama amekufa amekufa tu,” Bill akashindilia msumari wa mwisho katika hilo. Andreas akaiweka ile ramani juu ya kijimeza kidogo kwa minajiri ya kuja kuisoma vyema baadae, kisha wote watatu wakatoka nje ya chumba hicho na kikafungwa tena kama klilivyokuwa mwanzoni.

ITAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
SEHEMU YA 26
§§§§§
10
KAMANDA AMATA alijikunguta vumbi, alijitazama hapa na pale alikuwa na michubuko michache lakini alisikia maumivu makali sana katika mkono wake wa kulia, akajaribu kuunyoosha na kuufanyisha mazoezi. Kidogo ukakaa sawa. Akajiangalia zile silaha zake nyeti ambazo huzificha ndani ya nguo zake, bastola yake ilikuwepo, camera na vitu vingine vyote vilikuwa vimetimia, kwa hatua za taratibu alijivuta kurudi barabarani.
Ulikuwa ni usilku mnene sana ambapo hakukuwa na magari mengi katika barabara hii ya kutokea nje ya mji wa Aachen, zaidi yalipita malori. Alitembea hatua za taratibu akipandisha kilima kidogo kilichokuwa hapo, alipofika juu, alikuta kuna Motel, taa zilikuwa bado zikiwaka na magari machache yalikuwa yamepaki nje yake. Akaiendea motel hiyo na kuingia ndani, kulikuwa na watu wachache ambao walionekana washari washari hivi, wakiwa wamevaa kiuni, wengine wakilewa [pombe na wengine wakiwa wanacheza kamali.
“Nahitaji msaada,” alimwambia Yule mwanadada wa kaunta.
“Tukusaidie nini?” Yule dada alijibu kwa Kijerumani safi.
“Mna box la huduma ya kwanza?” akauliza Amata.
“Ndiyo; bila shaka,” Yule mhudumu wa kaunta akajibu na kuingia nyuma ya kaunta akatoka na kikasha chenye alama ya msalaba mwekundu akampatia, Kamanda Amata akafungua ndani yake, akatazama akakuta kuna dawa aina ya Iodine akaichuku, bomba moja la sindano na kijichupa kidogo cha dawa aina ya Diclofenac, akavua shati, akaliweka pembeni, katika mkono wake palikuwa na jeraha kubwa kiasi kutokana na mburuzo alioupata alipokuwa akiruka kutoka ndani ya ile gari kabla haijagongana na katapila, akajipaka ile iodine huku akikunja sura kutokana na maumivu ya dawa hiyo, akaijiwekea na pamba kisha akamuomba Yule mhudumu wa kaunta amfunge bandeji naye akatekeleza hilo. Kamanda Amata alipoona kuwa hapo amekamilisha akajidunga sindano ya Diclofenac kutuliza maumivu. Akaismama na kutoa shukrani kwa Yule dada, akavaa shati lake jeupe ambalo sasa lilikuwa halitamaniki kwa vumbi.
Alipokuwa akitoka, mlangoni alikuta kuna majaketi yametundikwa, akajichagulia moja la rangi nyeusi akajitupia juu yake na kutoka nje, hakuwa na usafiri. Akatazama magari yaliyoegeshwa hapo, akaona moja inayomfaa. Ford Cortiner ya rangi ya buluu ilikuwa imeegeshwa pembeni kidogo mwa jengo hilo na mwenyewe alikuwa ameliacha likiunguruma yeye akiwa ndani kunywa kahawa, bila shaka lilikuwa linatoka safari ya mbali, Kamanda Amata aliingia na kukanyaga mafuta akarudi barabarani, muziki mzuri wa You are not alone uliopigwa na Michael Jackson alikuwa ukitumbuiza. Saa katika dashboard ya gari hiyo ilionesha ni saa nane za usiku ikielekea saa tisa.
Mwendo haukuwa wa kawaida barabarani, Kamanda Amata akili yote ilikuwa imehamia kwa Bill, sasa alikuwa anataka kumaliza biashara yake na Bill. Alikata mitaa michache na kushika barabara inayopita mbele ya kanisa kuu, akalitazama kwa mbali na kupitiliza, akalikaribia hekalu la Don Andreas, kwa kujifanya kuwa hana kazi nalo alipitiliza na kwenda kusimama mbali kidogo, akaegesha gari karibu na kituo cha mafuta, akaliacha linanguruma kama alivyolikuta, alipokuwa anatoka akawasha taa ya ndani kuangalia hiki na kile, hakuamini macho yake alipoiona AK 47 double barrel, akaitoa na kuvunja katikati kama kawaida, haikuwa na risasi, akapekua hapa na pale akakutana na kikebe chenye risasi kama kumi hivi akakichukua, akajaza risasi zote katika mashine hiyo na kujivuta kwa mguu kulielekea jumba hilo lenye ulinzi mkali. Haikumchukua muda kuifikia himaya hiyo yenye utulivu wa pekee, kwa nje ya jumba hilo alifanikiwa kuona gari mbili zimeegeshwa, moja ikiwa ni ile Vogue, ‘Hisia zangu zimesema kweli, Bill yupo hapa na atafia hapa, leo sina huruma na kiumbe cha mtu,’ kamanda Amata alijisemea moyoni, hasira ikiwa inamtawala kila baada ya nukta. Alitazama ulinzi ulivyojipanga akaona kuwa juu kuna walinzi lakini hakujua atafanyaje wasimuone. Akachomoa bastola yake yenye kiwambo cha sauti, akamlenga mmoja na kumpata sawia kichwani, bajati nzuri aliangukia juu kulekule.
Akaona sawa, mmoja tayari, alipokaribia ule wigo wa wavu maalum, akasita, kitu kikamwambia geula kulia, alipogeuka akakutana na taa kubwa inayoongozwa na sense, ukiingia umbali Fulani kutoka ule wigo, taa ile inakumulika kwa mwanga mkali na vingola vinaasha walinzi, hakuwa na mda wa kuhangaika na taa ya mtu, akaifumua kwa risasi moja, kisha akarudi nyuma na kutimua mbio kuuelekea ule wigo akapiga samasoti maridadi kabisa akapita juu ya wigo ule bila hata ya kuugusa, alipotua tu tayari AK 47 ilikohoa na kumteremsha mlinzi mwingine mpaka chini, alipogeuka kushoto kuna mwingine, kwa kutumia bastola yake akamfyatulia moja makini sana iliyochana bega upande wa moyo, Kamanda Amata akahama pale alipokuwa kwa maana alijua ataonekana, akapenya katika ya maua na kuifikia maiti ya mlinzi mmoja akaivua shot gun semi automatic, akaibeba mgongoni. Kamanda Amata akaendelea kusafisha nje kote, alihakikisha si mbwa si binadamu habakishi kitu.
Milio ya risasi ilifikisha taarifa ndani kuwa huko nje hakufai, Bill akanyanyuka na kuwaambia vijana wake wawe tayari.
“Bila Shaka, tumevamiwa,” akmwambia Don Andreas ambaye alionekana wazi presha ikipanda. “Nani atuvamie wakati Kamanda amekwishakufa?” Bill akatoka nje ya nyumba hiyo, hakuna mtu, akiwa amefyumu kwa hasira, akiwagombeza vijana wake kwa uzembe wa kushindwa kuimarisha ulinzi. Akarudi ndani, hakumkuta Don Andreas, kaenda wapi, bahati nzuri vyumba vyake vya siri Bill anavijua, akaingia cha kwanza, cha pili akamkuta, “Hapa si pakukaa Andreas, tuondoke,” Bill alimwambia Andreas.
“Ramani ile pamoja na monstrance lazima tuondoke nazo,” Andreas alimsisitizia Bill, “Don, hatuna muda huyu jamaa ni kichaa,” Bill aliendelea kumnong’oneza. Wakatoka pamoja pale mafichoni na kuukimbilia mlango mkubwa lakini Andreas akarudi tena akiuendea ule mlango ambao una zile hazina zake zote. Bill alimtazama Andreas akiwa anahangaika kuufungua ule mlango. Bill akapotelea upande mwingine wa jumba hilo, sasa akiwa na bastola yake mkononi, akimuwinda huyo aliyevamia.
Kamanda Amata alikuwa akinyata kuuelekea mlango wa siri uliokuwa ukitokea upande wanyuma, aliutazama mlango ule ulikuwa wa chuma imara, sio shida, akaizungusha saa yake nayo ikaanza kuzunguka kwa kasi na kutoa mionzi iliyoweza kukata eneo la kitasa la mlango ule, aliporidhika akaizikma ile saa, akaujaribu mlango ukafunguka bila kipingamizi, akajitoma ndani. Akiwa katika kutembea taratibu, akahisi kitu kama kitu chenye ncha kali kikipenya eneo Fulani la shingoakaanguka chini na kupoteza nguvu, alijaribu kupambana na hali hiyo ikawa ngumua sana, akakumbuka vidonge alivyopewa na Madam S, akapenyeza mkono wake kwenye mfuko wa ndani wa suruali akachukua kimoja na kutumia nguvu yake ya mwisho kukimeza, mara akalegea na kujilaza.
“Ha ha ha ha ha ha ndege mjanja hunasa katika tundu bovu,” Kamanda Amata alisikia sauti hiyo kwa mbali sana, akafumba macho. Mara akasikia kitu kama kiatu kikimkanyaga kwa nguvu kichwani mwake. Akaamka l;akinin hakuonesha kukurukakara yoyote, bado alikuwa palepale chini,
“Utafia ughaibuni, Mbwa mweusi wewe, wewe unaweza nkujifanya polisi wa dunia wewe? Wenzako FBI wamefeli, we una nguvu bgani na hiko kishirika chenu cha upelelezi kuvuka mipaka kuja huku, sasa leo ndio mwisho wako, nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,” Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
ITAENDELEA.
 
MAUAJI YA KASISI
MTUNZI: richard MWAMBE
Nitakuua huku nakurekodi kwenye mkanda wa video niwatumie wenziwako huko kwenu Afrika wakaushuhudie mwisho wako ulivyokuwa wa taabu na mateso, mwenzako anaejifanya kasisi kumbe ni jasusi tayari ninae na chamoto ameshakiona japokuwa hajafa, nitaua mmoja baada ya mwingine,” Bill aliwaamuru vijana wake wamburuze Amata kwenda shimoni kwenye mashine ya kifo.
SEHEMU YA 27
§§§§§
FR FRANK Edson, alipojuwa kuwa Kamanda Amata ameingia katika mtanange hivyo anaweza kumuwahi kumpoteza Bill ilhali yeye anatakiwa ampeleke akiwa hai, aliamua kuyavulia maji nguo na kujikita katikati ya hatari hiyo, alilivamia jumba la Don mapema sana hata kabla Bill hajarudi akajificha katika moja ya stoo zilizokuwa ndani ya jumba hilo. Kwa bahati mbaya au nzuri alipoikuwa katika harakati za kutafuata pazuri pa kujificha kamera ndogo sana ya usalama ilimuona na kupeleka taarifa panapohusika ndipo shughuli ilipoibuka humo ndani, kipigo alichokipata kwa mkono wa Iron Man The Killing Machine alibaki hoi hajiwezi na kutupwa huko shimoni ambako hakuna hewa hakuna chochote ni mateso mpaka unakufa.
Fr Frank alishindwa kujitetea kwa jitu hilo la miraba mine baada ya kupata kipigo cha mbwa mwizi. Alikuwa nusu mfu katika chumba kile.
Kamanda Amata alijilegeza huku akiburuzwa mpaka katika lango la chumba hicho ambamo kinachofanyika ni kukutumbukiza, utakaa umo ufe kisha inamwagwa dawa maalum ambayo inakusagasaga na kuwa katika vipande vidogovidogo kisha wanaflash kama chooni na taka hizo zote hupelekwa baharini kupitia mfumo wa maji taka. Walipofika mlangoni, tayari kumtupa mle shimoni, Kamanda Amata alijitikisa kidogo, wale jamaa wakashtuka, mmoja akainama kumwangalia kama ni mzima au la, Amata akamtemea mate, kwa uzembe wa Yule mlinzi akauchia mkono wa Kamanda ili ajifute mate usoni, kosa. Konde moja zito lilitua tumboni kwa jamaa Yule akatema damu, huyu mwingine hajakaa sawa akachezea kipepsi kimoja kilichjomfanya ajisjike tumbo, sasa Kamanda Amata alikuwa huru na nguvu zake zilezile, alijurusha kiufundi na kuwapiga mateke ya migongoni kisha wale wawili wakaingia shimoni. Kamanda akasonya na kurudi kwa njia ileile.
Akapenya hapa na pale na kutokea eneo lenye veranda kubwa, akawa kizungukazunguka ajui nini cha kufanya, akiwa katika hali hiyo alihisi mkono wenye nguvu umekamata bega alipogeuka akakutana uso na jitu la miraba minne, mara akasikia vicheko kutoka sehemu asiyoijua. Lile jitu likamnyanyua na kumbwaga chini, Amata alijitonesha tena katika majeraha yake, akabaki kugugumia maumivu tu. Aliinua kichwa na kumwangalia huyo aliyemfanyia kitendo hicho, lilikuwa ni jitu lenye pande la mwili, lililojaa misuli mikubwa, kamanda Amata akaona wazi kuwa Frank Edson hakuwa na budi kuwa katika hali ile kama alipambana na dubwana hili, akajikokota kunyanyuka ajaribu bahati yake, konde la pili lilimrusha nyuma na kujibamiza vibaya ukutani, Kamanda Amata akatema damu, alipokuwa akijaribu kuinuka akapigwa teke la mbavu, nguvu ya teke lile ilimsukuma mpaka ukuta wa pili, Kamanda alijikuta akiwa na hali mbaya, alijitahidi kuinuka lakini ilikuwa ngumu, alibaki kutambaa. Mara sauti ikasikika kwenye chombo maalumu kilichofungwa darini, ilianza na kicheko;
“Ha ha ha ha ha ha, Kamanda Amata, wewe unajua sana kufuatilia nyendo za watu sio za miungu kama sisi, sasa leo pambana huyo Israel mtoia roho, kama wewe unaweza kukishinda kifo basi leo tutaona ujanja wako uko wapi, ha ha ha ha ha ha hapo ulipo ndio kuzimu ulipokuwa ukikusikia kwenye vitabu vya dini zenu, pambana na mashine ya kifo hiyo, ukiishinda nitakupa utajiri wangu wote,” Maneno yale yaliyokuwa yakisemwa na mtu asiyemuona yalimtia hasira sana Amata, “Utajiri wako baki nao mwenyewe, kwa kuwa sikutaka kukutoa roho sasa umeniladhimisha kufanya hivyo,” ilikuwa sauti ya uchovu kutoka kwa Kamanda Amata.
Vicheko vikaanza tena kwenye kile chombo, sasa vikiwa kwa fujo zaidi, Kamanda Amata alihisi kitu kama upepo kimepita sikioni mwake pindi alipokuwa akigeuka, kumbe guu la lile jitu lilipita akiwa na lengo la kumpiga teke la kichwani pale chini alipojiinamia, Kamanda Amata kwa kasi akaona amepata nafasi nzuri ya kufanya mambo, alipiga ngumi moja iliyotua kwenye korodani za jitu hilo, likaguna kwa maumivu. Akajiinua kwa ustadi na kujisahaulisha maumivu yake, akawa wima, alikusanya nguvu zake zote na kuruka hewani alikoichanua miguu yake na mateke yote mawili yakatua shavuni mwa lile jitu, lakini halikutikisika hata kidogo. Kabla mguu wa Amata haujatua chini, ulidakwa, Kamanda akautumia kama nguzo na kujivuta kuelekea usoni mwa lile jitu, akalipiga kichwa cha jichoni kwa maana alijua kwa vyovyote atalipoteza maboya, kama aliota.
Kile kichwa kilipotua jichoni lile dubwana lika muachia Amata na kujishika jicho, Kamanda Amata akatua sakafuni kwa miguu miwili baada ya kuruka samasoti safi sana, alitahamaki na kuliona lile jitu likimjia kasi kama mbogo, akalikwepa nalo likajibamiza ukutani, Kamanda Amata akatazama huku na kule akaona taa iliyosimamishwa kwenye nguzo ya chuma, akaiwahi na kuichukua akaivunja taa yake nayo ikabaki bila taa, akaiinua na kumpiga nayo mgongoni, lilipoguka kamanda Amata akatumia ule mnara wa taa akamchoma tumboni, lakini hakufanikiwa hata kumtoboa kutokana na ulaini wa chuma kile lakini alimpiga shoti moja mbaya ya umeme kutokana na kwamba alikuwa hajaichomoa kwenye soketi pale ukutani, Amata akatabasamu kwa hilo.
Lile jitu, lilipigwa shoti iliyolisukuma na likajibwaga zimazima pale chini. Vicheko katika kile chombo vikasimama ghafla. Kamanda Amata aligundua kuwa jinsi ya kulishinda lile jitu sio nguvu bali akili, alipi mguu chini na mara kitu chenye ncha kali kikachomoka kwenye sehemu ya mbele ya solo ya kiatu chake, na mguu mwingine vivyo hivyo, Kamanda Amata sasa akaanza kutumia miguu kuilishmbulia lile jitu, mateke ya usoni, mbavuni yalilifanya jitu lile lipoteze nguvu maana kila alipopigwa kwa teke aliachiwa jeraha kubwa kutokana na vile vyuma kenye viatu vya Amata. Zilikuwa dakika tatu za shughuli kubwa ya kulikalisha chini lile dubwana. Kamanda akasimama tayari kwa pambano akiliangalia lile jitu likigalagala sakafuni huku damu zikitapaka kila mahali.
Upande wa pili, Bill na Andreas walikuwa kimya wakitazama pambano hilo kupitia luninga ndogo ndani ya chumba nyeti cha Andreas, hawakuamini kile wanachokiona, kile kinachofanywa na Kamanda Amata, jinsi anavyotumia akili kuliadhibu jabali lile, mashine ya kifo kama wanavyoiita.
Tangu Andreas amnunue binadamu huyo wa ajabu huko Honduras na kumsafirisha kwa siri mpaka Ujerumani na kumuhifadhi katika nyumba yake, alishamtumia kwa kuua watu wengi sana wakiwezmo maafisa wa polisi, wanajeshi na wote wanaofuatilia nyendo zake kwa ukaribu, hakuna aliyewahi kufurukuta, wengi walikata roho kwa pigo moja tu, kisha miili yao aliitupi ‘kuzinu’ katika chumba alichokiandaa kwa kazi hiyo,. Akishakutupa humo hufungulia hewa yenye chemical kali amabayo hukukausha na kukumeng’enya kuanzia nyama yako mpaka mifupa vyote vinakuwa unga, kisha maji mengi huingia katika chumba hicho na kuondoka na mmeng’enyo huo kupitia mabomba yha maji taka, watu wako watakutafuta miaka nenda rudi na hawatakuona, umefutwa katika orodha ya binadamu duniani.
Leo ilikuwa tofauti, alimshuhudia Kamanda Amata akitoa dozi mbaya kwa jitu lake hilo analolitegemea kwa kazi hiyo. Kijasho kilipita kutoka kwapani na kufika mpaka kwenye kiuno kabla hakijaishia katika nguo alizovaa.
Kamanda Amata alipohakikisha dude hilo limezimika alitzama huku na kule ili kuona cha kufanya, sasa akili yake ilirudi kwa Bill na mwenzake Andreas, akiwa katika kutazamatazama mara akasiki kama nyayo za binadamu zikimfuata kwa nyuma, akatazama kwenye kioo kikubwa kilicho mbele yake na kuliona lile dude limesimama likielekea kwake kwa nguvu zote, Kamanda Amata hakuwa na silaha yoyote ya maana, akajua sasa kuwa amekwisha, kabla hajaona la kufanya, lile jitu likamfikia, likiwa na hasira mbaya, lilimpiga kikumbo Amata akapitiliza mpaka kwenye kioo cha mbele yake, alijibamiza na kile kioo kikamwagika pakabaki wazi, Kamanda Amata akadondokea upande wa ndani wa kile chumba kilichotenganishwa na kile kioo. Ilikuwa ni ofisi ndogoi lakini iliyojaa kila aina ya nakshi na samani za gharama, Kamanda Amata akanyanyuka na kuchukua chungu kilichokuwa na ua ndani yake na kukirusha sawia kichwani mwa jitu lile, likapepesuka kidogo, kabala halijatuliya, Amata akajirusha doule kick na kutu kifuani mwa lile jitu, kutyokana na kupoteza nguvu liliyumba na kujibamiza ukutani, ule mtikisiko wa ukuta ulifanya pambo la juu ambalo lilikuwa ni bichwa la Nyati lililotengenezwa kwa chuma.
Lilianguka na kumpiga kichwani, kisha lile bichwa la nyati liakadondoka sakafuni. Lile jitu likajitahidi kusimama lakini ilikuwa ngumu kutokana na kugongwa vibaya na lile bichwa la nyati bandia, ilikuwa ni nafasi ya Amata ya kumaliza mopja kwa moja akaanguka juu ya lile sanamu la kichwa cha Nyati, akachomwa na pembe za nyati zilizojinyomnga vizuri zikitanguliwa na ncha kali, likatoa kelele za
ITAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
SEHEMU YA 28
Uchungu huku macho yakiwa yamemtoka pima, likakata roho. Kamanda Amata akakung’uta mikono yake kwa kuashiria kazi imeisha, hakuamini kiama kalimaliza hayawani hilo.
§§§§§
Bill aliinuka na bastola mkononi, akiuelekea mlango ili atoke nje, mkono mmoja akiwa na ile fimbo yake ya kutembelea.
“Bill, hapa pameshakuwa pabaya, mi nafunga vyangu najificha dhidi ya huyo mtu wako,” Andreas alimwambia Bill, wote wawili walikuwa katika hali ya kuchanganyikiwa, wakivujwa na jasho jingi. Andreas alichukua begi tupu, akainyanyua ile monstrance na kuiti begini kisha ile ramani, akaenda ukutani na kushusha picha moja, nyuma yake nkulikuwa na vibonyezo au vitufe kumi na mbili vikiwa na nmba pamoja na alama chache, akaanza kuvibonyeza ili mlango wa siri ulio kwenye sakafu ya chumba hicho ufunguke, nukawa unagoma kufunguka, alipojaribu mara ya pili nay a tatu mlango ule ukakubali, taratibu ukawa unapanda juu ili kuwezesha mtu kuingia. Bill aliona taanyekundu ikiwaka juu ya dari la chumba hicho, ikiashiri kuna hatari, mara alishuhudia ule mlango mnene wenye ulinzi mkali ambao huwezi kuingi bila kuthibitisha vitu vitatu, namba ya siri, alama za vidole na alama za macho, na hivyo vyote vilikuwa ni Andreas peke yake aliyeunganishwa.
Mlango ule ulionekana kwa ndani ukikatwa duara kutoka nje, Bill akajua sasa hapa Kamanada anaingia, akaiweka sawa bastola yake, hakuwa tayari kufa wakati anayemlinda anatoroka, akainyosha bastola kwa Andreas, Andreas akasikia mlio wa bastola hiyo ikiwekwa sawa kulipua,
“Bill vipi tena?” Andreas akamuuliza Bill. Sikia bwege wewe, yaani huna shukrani, kazi yote niliyokufanyia, sasa hivi unaona mambo yameharibika unakusanya vyako unataka kutoroka na kuniacha mimi hata kunipa chochote sio, sitaki maelezo, nakumaliza mwenyewe,” Bill alimwambia Andreas kwa ukali.
“Sikia Bill, mi naokoa hii mali ya thamani, wewe ukishamuua huyo Kamanda Amata tuonane nitakupa donge nono,” Andreas alijitetea. “Siki, mi si motto, Kamanda Amata keshakufa mara mbili na kafufuka sasa unafikiri hapa atakufa tena?” Bill alimuuliza Andreas, Mara lile pande la chuma linalokatwa kwa saa ya Kamanda Amata, lilikuwa tayari kutoka mahala pake na kuruhusu mtu wa nje kuingia ndani, Bill alipiga risasi moja na kufumua kifua cha Andreas, Andreas akaanguka chini na kutoa yowe la maumivu, Bill akanyanyua tena mkono wake ulioshika ile bastola na kulenga lile tundu ili ampate Kamanda Amata, alipofyataua, viligongana vyuma tupu, hakuna risasi, akaitupa chini bastola na kunyanyua lile begi alilochukua Andreas na kuingia kwenye ule mlango na kuzama ardhini huku mlango ule ukijifunga nyuma yake.
§§§§§
Kama alitegemea kupona basi ilikuwa kwa asilimia ndogo sana, Frank Edson, aliona kile alichofanya Kamanda Amata pale mlangoni alipokuwa ameletwa na wale watu ili kutupwa ndani ya shimo hilo kusubiri kifo chake. Aliona kitu kidogo ambacho Kamanda Amata alikiangusha kwa makusudi wakati alipowaadhibu vikali wale jamaa wawili na kuwatumbukiza mle shimoni.
Ilikuwa ni kitu kama kidonge kidogo, kwa tabu sana Fr Frank Edson alijivuta kwa kutambaa mpaka akakipata kile kidonge alipokitazama alikijua vyema, kidonge kinachotumika kurudisha nguvu kwa haraka kwa mtu aliyekuwa na uchovu mwingi wa kupigwa au wa shuruba yoyote, pia kinaondoa maumivu kwa muda mrefu. Fr Frank Edson alimuona Amata kama Malaika wake, alikiokota na kukitia mdomoni, akakimung’unya, muda kumi na tano tu alipata nguvu taratibu mpaka akawa sawa na maumivu yake yakapotea, akajinyanyua kutoka pale alipo, akasimama wima, akatazama wale jamaa waliolala pale, waliotupwa na kwa kipigo kikali na Kamanda Amata. Akawapekua katika nguo zao na kupata bastola moja iliyobakiwa na risasi mbili tu,
‘Sio mbaya’ akajisemea. Sasa kazi ilikuwa atatokaje kwenye chumba kile kisicho hata na dirisha, aliuangalia mlango ulikuwa juu umbali wa mita kumi na ukuta wote ulikuwa umewekwa kitu kama niru ambayo kamwe huwezi kuzikwea kwa jinsi zinavyoteleza, ulikuwa mtihani mgumu kwake, akakizunguka kile chumba akigusa hapa na pale, baada ya kuchunguza sana ndipo alipogundua ile sehemu ya kuingizi maji ndfani ya chumba kile, haikuwa na bomba bali ni uwazi mwembamba wa futi mbili kwa upana na uwazi wake ulikuwa ni kama milimita tano, palitengenezwa hivyo ili maji yakitoka yatoke kwa mbinyo na kasi kubwa kutokana na msukumo wa pampu. Akapaangalia na kuona kama anaweza kupita katika upenyo huo, lilikuwa ni wazo finyu sana hata kama angekuwa motto mdogo, sehemu ambayo asingeweza kupenya hata mjusi, lakini yeye alidhamiria kupenya hapo, akiwa kama aliyechanganyikiwa ndipo akagundua kuwa haiwezekani kufanya hilo analotaka kufanya, akajicheke mwenyewe hasa alipojua kuwa yale maji kuna yanapokwenda, akaenda kwenye moja ya kona za chumba hicho, alipotazama kwa makini sana akaona kuna kitu kama kimebandikwa katika ukuta huo, lakini kilikuwa kimefanana sana na ule ukuta, akajua kwa vyovyote hapo pana kitu, akaanza kugongagonga ukuta kwa ile bastola aliofika eneo hilo akasiki ule mlio unabadilika na kuwa mkubwa kiasi akagundua kuwa nyuma yake lazima kuna uwazi, hakuwa na budi, kwa kutumia bastola hiyo hiyo alifyatua risasi moja na ikatengeneza tundu zuri ambalo lilimuwezesha kuona mpaka upande wa pili.
Kweli kulikuwa na uwazi mkubwa, Frank alisikia sauti ya maji yanayotembea, lakini alipochungulia kwa jicho lake aliona mwanga hafifu sana, akaanza kubomoa lile eneo kwa kupiga na ile bastola kama nyundo mpaka akafanikiwa kutengeneza tundu la kutosha, akajipenyeza na kudondokea kwa ndani. Lilikuwa ni bomba kubwa la maji taka, aliweza kutembea kwa kuinama kidogo huku akipita kwenye maji hayo na asijue ni wapi anaelekea, harufu iliyokuwa humo haikuwa tatizo kwake, alitembea mwendo mrefu kidogo, kwa mbele akaona kuna pacha ya bomba hilo ikiungana na bomba linguine ambalo nalo lilikuwa likileta maji kuunga na hili nkisha kuelekea yanakokwenda, Frank alipoifikia ile pacha akasikia kelele ya mtu anayekimbia katika maji, akatul.ia kusibri aone mtu huyo ni nani.
§§§§§
KAMANDA Amata alipoona kuwa lile lango la kwenda chini alikoingia Bill limejifunga, akachoka ghafla, akatazama huku na kule, alichokiona akajua tu ni switchi ya mlango huo, akaelekea pale ukutani hakuwa na akaminya namba ya siri ambayo kuna jinsi unavyoipanga inaweza kufungua kila aina ya mlango, akaingiza tarakimu hizo kumi na mbili na alama Fulani kwa mpangilio maalumu, akabonyeza ok, akadaiwa kuweka alama ya kidole gumba, akajua tu lazima ni kidole cha Andreas kinachohatajika, alimtazama akiwa pale chini amelala hana uhai, “Ndiyo shida ya dhukuma, ukidhulumu utadhulumiwa” akaongea mwenyewe huku akiuendea ule mwili, akachukua kipande cha kioo kizito kilichovunjika hapo, akakata kidole gumba cha Andreas na kwenda kukipachika pale kwenye ile sense, taa ya kijani ikawaka, ule mlango ukafunguka, haraka akauendea, alipotazama mezani akagundua kuwa Bill ameisahau ile fimbo yake Amata akaitazama na kuichukua, alipoigeuza geuza akagundua kuwa haikuwa fimbo ya kawaida, akaingia nnayo na ule mlango ukajifunga, alimweza kumuona Bill kwa mbali akiendelea kwenda,
“Billlllllll…..” aliita, lakini Bill hakusimama. Baada ya kumfuata kama dakika moja na nusu hivi, akamuona Bill akisimama na kugeuka alikotoka, akiwa na begi lake mkononi. Bill hakuwa na ujanja, alikuwa katikati, huku Frank Edson FBI huku Kamanda Amata TSA.
“Bill, huna ujanja, mwisho wako umefika,” ilikuwa sauti ya Fr Frank. Amata aliiskia akajua kuwa ni Frank anaye ongea lakini bado alikuwa hajamuona kutokezea. Bill alibaki pale katikati akihema. Mara Frank akatokezea na kugongana macho na Kamanda Amata. “Kamanda Amata, niachie Bill niondoke naye, asante sana kwa kazi kubwa uliyoifanya ya kunirahisishia kumpata Bill Van Getgand, asante sana, huyu inabidi afike hai pale Washington,” Fr Frank alimwambia Kamanda Amata.
“Sikia Frank, unajua kuwa ulikwishakufa wewe? Kwa nini husemi asante kwa kukurudishia uhai wako? Sasa sikiliza Bill utamchukua akiwa hai wala usijali cha muhimu ni kutafuta njia nya kutoka humu ndani, na njia hiyo lazima yeye Bill atuoneshe,” Kamanda Amata akamwambia Frank, Frank akamsogelea Bill na kumnyang’anya lile begi, Bill hakuwa na ubishi, Frank akamrushia begi Amata, nae akalidaka.
“Haya, njia ya kutoka humu ndani iko wapi?” akamuuliza Bill, alipoona ukimya wake unazidi, akaamua kutumia nguvu, alimshika Bill kwenye ukosei wa shati na kumbamiza kwenye kingo za bomba hilo mara kadhaa, Bill alikuwa akitokwa na damu nyingi katika paji lake la uso.
ITAENDELEA
 
MAUAJI YA KASISI
SEHEMU YA 39
“Frank! Mbona huna huruma wakati wewe ni mchungaji wa kanisa?” Kamanda aliuliza,
“Kwa taarifa yako, ukimfanya hivyo hatofika hai Washington, nifuate njia ipo huku,” akaongeza, kisha akatangulia na Frank akamfuata na Bill akiwa katikati mikono akiwa ameshika kichwani. Walikwenda mpaka kwenye ule mlango, akaufungua na wakatoka wote, wakaingia kwenye chumba kile cha siri, kisha wakaelekea katika lile sebule kubwa, Frank alishangaa kulikuta lile jitu lililomtia adabu likiwa marehemu, Frank moyoni mwake alikiri kuwa Kamanda ni kiboko kama amelizimisha jitu hatari kama lile. Jumba la Andreas lilikuwa kimya ni polisi tu waliokuja kutoka mjini walikuwa huku na kule wakifanya upekuzi wa hapa na pale.
“Weka mikono juu!” ilikuwa sauti ya polisi mmoja wa kike akimuamuru kamanda Amata. Amata akanyanyua mikono juu ile fimbo aliyoichukua pale mezani ikaanguka chini, na Yule poilisi akamuamuru mwenza aichukue. Mara Bill akatokea na nyuma akiwamo Fr Frank Edson.
“Frank Edson FBI,” akaonesha na kitambulisho, wale polisi wakaja kumchukua Bill na kumtia pingu. “Na huyu?” waliuliza juu ya Kamanda Amata, “Muacheni aende zake, ni mwenzetu kutoka shirika la upelelezi Tanzania,” Yule askari akamwita na kumuongoza kuelekea kwenye gari ya polisi. Nje ya jumba la Andreas kulitanda gari za polisi zikiwaka vimulimuli vilivyong’aza eneo lote hilo, Kamanda Amata akatazama saa yake, ilikuwa ni saa kumi na mbili alfajiri. Polisi walikuwa wakikusanya miili na kufanya upekuzi wa hali ya juu katika jumba hilo ambalo siku na miaka yote waliliona ni jumba la mtu mwema.
Mlio wa Helkopta ulisikika ukikaribia eneo hilo, Frank akamtazama Amata,
“Kamanda, Bill anaondoka moja kwa moja USA, uje muagane tafadhali,” FranK alimwambia Amata kwa nyodo. Kamanda Amata akavuta hatua na kufika pale aliposimama Bill huku nyuma yake akiwa ameshikwa na polisi wawili wa kijerumani na Frank alikuwa alikuwa nyuma yao.
Bill na Amata wakawa uso kwa uso,
“Bill nilikwambia siku yetu inakuja, na ndiyo leo, nitautwaa uhai wako kwan kisasi cha Fr Gichuru, Kahaba Rose na wengine wote uliowapotezea maisha yao pa sin a hatia. Nakuapia, hautakanyaga gereza la Guantanamo wala wapi sijui,” kamanda Amata aliongea kwa sauti ya chini ni Bill aliyekuwa akisikia na wale polisi wawili, Frank alikuwa akiongea na redio aliyopewa na mmoja makamanda waliokuja na kikosi hicho. Bill alimtazama Kamanda Amata, akamtemea mate usoni, Kamanda Amata akamkazia macho Bill,
“Sintoyafuta mate haya mpaka nihakikishe umekufa na haupo katika dunia hii, kifo chako ulikinunua mwenyewe kwa gharama kubwa sana,” Bill aliposikia maneno hayo aliikumbuka ile fimbo yake na akaitazama ikiwa nikononi mwa Amata, kisha Kamanda akageuka na kuondoka kueleka upande ambao gari za polisi zilegeshwa, waandishi wa habari kama kawaida yao, walichukua picha huku na huku na kutafuta majibu ya maswali yao. Dakika chache helkopta kubwa likakanyaga ardhi yenye nyasi safi na kutulia tuli, wanajeshi wane waliovalia sare ya jeshi yenye nembo ya bendera ya Marekani walishuka na kumchukua Bill tayari kuondoka nae, itifaki za kuondoka na mtuhumiwa huyo zilifanywa haraka sana na pande mbili za mataifa hayo rafiki. Kamanda Amata alikuwa kasimama upande wa pili wa gari moja ya bpolisi akiwa kaegemeza tumbo lake kwenye ubavu wa gari hiyo, begi lake kalitupia ndani ya gari na ile fimbo ya Bill kaiweka juu ya gari, akiangalia kila kinachoendelea.
Aliishika ile fimbo na kuwa kama mtu anayeichunguza pale juu ya gari, bahati ilioje alipogundua kuwa ile haikuwa fimbo bali ni silaha mbaya sana yenye risasi za mtindo wa msumari, silaha ya Kirusi iliyotumiwa sana na wanazi wa KGB ambamo Bill alikuwa mmoja wao nyakati hizo, aliitazama haraka na kuikuta bado nina risasi tatu, akaiweka vizuri juu ya gari na kulenga shabaha, hakuna aliyemwangalia wala kugundua hila yake. Mguu wa Bill ulikuwa ukikanyaga ngazi ya helkopta hiyo huku akisukumiwa ndani na wale wanajeshi, Fr Frank alikuwa akifuata nyuma, lo, mara walishuhudia Bill akijishika kifua, mara kichwa, akalegea na kuanguka chini, tafrani ikazuka, walipomwangalia tayari alikuwa marehemu, lakini hakuonekana tundu lolote la risasi.
Kamanda Amata aliingia kwenye gari mara tu baada ya kumaliza azma yake, alikuwa akisubiri Bill akanyage japo ngazi ya helkopta hiyo, naye palepale akafyatua bunduki hiyo ya siri, bunduki ya kijasusi, akamtoa uhai Bill Van Getgand.
Fr Frank Edson akawaacha wale wanajeshi wakimhudumia Bill ambaye alikuwa tayari marehemu, akamjia Kamanda pale aliposimama, na kamanda akatoka pale alipo kumuendea Frank, akampa mkono, lakini Frank hakuupokea mkono huo.
“Kamanda Amata, umefanya nini sasa?” Frank aliuliza.
“tatizo nini, wewe ulimtaka akiwa hai sivyo, si umemshika akiwa hai, na mimi nilishakwambia serikali ya Dodoma inataka roho yake tu basi. Asante sana Frank, umeifanya kazi yangu kuimaliza kwa wepesi kuliko nilivyofikiria,” kisha Kamanda Amata akageuka na kuingia kwenye gari iliyokuwa imekwishawashwa tayari, Frank alibaki kumtazama hakuwa na la kufanya, aliitazama ile gari ikitoka getini na kutokomea mjini huku na zingine zikiendelea kutoka moja baada ya nyingine.
DAR ES SALAAM
Saa 09:30 usiku
SIMU YA kitandani mwa Madam S iliunguruma kwa fujo usiku huo, alishtuka na kukunja sura kama kawaida yake kwani alikuwa hapendi sana kukatishwa usingizi. Aliinyakua simu hiyo na kuiweka sikioni.
“Madam S!” ilikuwa suti ya Chiba.
“Ee Chiba, niambie, mbona usiku sana,” Madam S aliuliza.
“Fungua, televisheni yako, Deustche Welle,” akamwambia na ile simu ikakatika. Madam S akaiwahi rimoti haraka na kuwasha luninga yake kubwa iliyofungwa ukutani katika chumba chake cha kulala. Habari ya dharula aliyoikuta kwenye kioo hicho ilimfurahisha kuliko habari zote alizowahi kuzisikia. Ilikuwa ni habari ya moja kwa moja iliyobebwa na maadishi ‘Breaking News’ ilikuwa ikieleza juu ya kukamatwa kwa jasusi lililoisumbua dunia, lakini hata hivyo ikasemekana limejiua kabla halijapakiwa katika helkopta tayari kupelekwa Marekani. Habari hiyo ilikuwa ikisifia shirika la nkipelelezi la Marekani kwa kufanikiwa kulinasa jasusi hilo. Akiwa katika kutazama habari hiyo, fax yake ya mezani karibu na kitanda ikaanza kutoa mlio kama wa mdudu, kijikaratsi chepesi kilikuwa kikitoka na maadishi. Akaiendea na kuisoma fax hiyo.
“…kazi uliyonituma nimeimaliza, Bill Van Getgand amekshaisalimisha roho yake… TSA 1” Madam S alijua kuwa ujumbe huo umetoka kwa Kamanda Amata, akatabasamu, akazima luninga yake na kurudi kitandani.
HATIMA
KAMANDA Amata alikuwa kwenye kititanda cha wagonjwa katika kliniki binafsi ndani ya mji huo wa Aachen, akigangwa majeraha na maumivu mengine. Huku akijisomea magazeti nya siku hiyo akipata habari za tukio lililotukia usiku wa siku hiyo na kusoma habari nyingi za kweli na za uongo.
“Kamanda, Sindano!” alishtuliwa na sauti laini ya kike, kamanda Amata akamwangalia Yule muuguzi wa kizungu aliyekuwa na chano yake yenye kila kitu kwa ajili ya tiba hiyo. Kiukweli pamoja na ujasiri wote, kamanda Amata kwenye swala la sindano alisalimu amri, aliogopa sana kitu hicho tangu utoto. Alitamani kulia alivumilia mpaka shughuli hiyo ilipokamilika.
“Asante dada mzuri, hata sikujua kama umenichoma sindano,”Amata alimchokoza muuguzi. “Kwa nini?” Yule muuguzi akauliza. “Kwa jinsi ulivyo na mikono laini, na upendo unaomfanya mgonjwa asihisi hata kama anapasuliwa nini kuchomwa sindano!” Amata aliongea kwa lugha ya uchokozi, “Hallo,” Kamanda aliita tena wakati Yule muuguzi alipokuwa akitoka mle chumbani, “Nini? Unahitaji sindano nyingine?” akauliza huku akirudishia mlango na kurudi kwa Amata, Kamanda Amata akampa ishara ya kuwa asogee amwambie kitu, Yule muuguzi akasoge kumsikiliza, Kamanda akamshika kwa mikono yake kichwani pande za masikio, akamvutia kwake, hakukuwa na ubishi, akambusu na ndimi zao zikabadilishana mawazo. Baada ya dakika kama mbili za mchezo huo ambao uliwafanya wote wasahau majukumu na magonjwa yao, akamtoa na kumtazama usoni. Yule mwanadada alikuwa akihema kwa nguvu, pepo limechukua nafasi, akajichomoa kutoka kwenye mikono ya Kamanda, akavua viatu na kumpandia kitandani, shughuli mpya ikaamka, Kamanda Amata alipogundua kuwa pazia la dirisha liko wazi, akshika kimnyororo kidogo cha kazi hiyo na kukivuta, pazia likarudi mahala pake na kuwaficha wawili hao kati ulimwengu wa peke yao.

MWISHO
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom