Riwaya : Kichaa

inabidi uchonge na mods
Yaan jana ndio nimeona hili tatizo jamani mpaka nirudi kwenye thread tuliyokutana ndio najua umeniquote kama hapa nimerudi huku nimejua mpo nisingerudi nisingejua chochote
 
Yaan mm humu jf kuna watu kama 5 hivi na Madame s naona kaongezeka sipati notification zao kabisa kuna hearly Bujibuji Palantir sijui ndio hivyo Archduke yaan nisiporudi kwenye thread niliyokutana nao sitajua kama wameniquote
tatizo n nn sjui maybe kuna hitilaf za kiufundi mana jf app inazingua natumia browser nayo pia inaleta shida tutakimbilia wapi
 
Daah ni simulizi moja nzuri sana...

Inafurahisha kama mambo ya Musa...

Inahuzunisha kama mambo ya Aisha, mama Neema...

Inachekesha kama mambo ya Mavugo...

Inafikirisha kama mambo ya Devi...

Inasononesha sana...

Cc: mahondaw
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 30.

ENDELEA.

''Mchukueni haraka na tumuwahishe hospitali tafadhali kuweni makini na mfanye haraka.'' Aliongea Peta Mwambe baada ya kumuona Mavugo ameanguka chini ghafla. Pita mwambe alikuwa na furaha sana huku woga ukimjaa hapo hapo kwani alihofia hali ya Mavugo kutokana na kuanguka kwake. Lakini alifurahi kumuona tena kwa mara nyingine Mavugo ilhali ameishi akimtafuta katika maisha yake yote.
Devi, Neema,kibakuli,Endrew,Aisha, pamoja na Pita Mwambe huku wakifuatiwa na walinzi, wote waliweza kupanda kwenye magari ya msafara wa waziri yule na moja kwa moja waka wahi, Hospitali kwa ajili ya kuwahi kuokoa maisha ya Mavugo.

Walienda hatimae walifika hospitali ya Bugando walipofika walimchukua Mavugo huku wakisaidizana na manesi hatimae mgonjwa alifikishwa na kuanzishiwa matibabu. Peta Mwambe alisahau kuwa kilichomleta si kusaidia wagonjwa wa ghafla bali ni kumuomba Neema iliaka msomeshe kama alivyotoa ahadi.
Aisha, Neema, Devi, Kibakuli, wote walikuwa wamekaa kwenye viti wakitulia huku wakijiuliza ni yapi yaliyopelekea Mavugo kuzimia ghafla na mbona alipomuona tu Waziri akaonesha kumjua? walitamani sana wamuulize waziri maswali yale kwani waliamini kabisa yeye ndie atakuwa na majibu yao lakini walijihisi hawajahitimu mpaka kufikia kiwango cha kumuuliza Waziri maswali kama yale. Walikaa sana pale huku muda wote huo Waziri akitembea tembea nje ya mlango utadhani mlinzi, alivyoonekana nikama alikuwa akimuomba Mungu muda wote. Naam, ingetosha tu akachukua ndege na kurejea kwake, au angetoa amri hata apelekwe hotelini kwa ajili ya yeye kupata chakula na kupumzika huku akisubiria hali ya mgonjwa hata kama mgonjwa anamuhusu, lakini yeye hakuthubutu kufanya jambo hilo katu na hiyo ilikuwa niishara ya kuwa huenda Waziri huyo akawa anaukaribu flani na Mavugo, Walinzi wa Mwili wa Waziri walianza kuhisi kama wana saidiwa kazi yao walimsihi atulie lakini hakutulia wala kuwajibu chochote.
''Do... do..docta, vipi hali ya mgonjwa?'' Alihoji Waziri baada tu yakumuona daktari akitoka kwenye chumba kile alichokuwemo Mavugo. Dokta yule alimuomba Waziri Pita Mwambe awe mpole huku akimuomba Mungu iliwao wafanye kazi yao vyema na kumsihi Waziri yule aketi angalau kitini kwani zoezi lile linaweza kuchukuwa muda kidogo hivyo waliomba wamsubiri mgonjwa wao mpaka hapo atapo amka.
.................................... .......................................................

Mama Musa alimaliza kufanyiwa oparesheni vyema na madaktari wale waliyo kuwa na ujuzi wa hali yajuu. Aliruhusiwa moja kwa moja akaanza kuondoka yeye na Musa pamoja na binti yule kisura ambae ni mtoto wa Waziri. Ile wanatoka kwenye chumba kile na kukatiza kidogo tu, macho ya Musa yaliweza kuya tazama machoya Neem huku machoya Neema yakiwatazama wote watatu, mapigo ya mioyo yao yaliwaenda kasi sana wote wawili. Walikaribiana na kupeana salamu kisha waliulizana juu ya ujio wa kila mmoja maeneo yale. ule haukuwa muda tena wa kuongelea maswala ya mapenzi, kudharauliana au kuheshimiana bali ulikuwa muda wa kila mmoja wao kuswali kwa lugha yake na Mungu wake ilikuokoa uhai wa mgonjwa tu. Mama Neema na Mama Musa wanatambuana vizuri tu hivyo nao pia wali salimiana huku Waziri mwambe yeye akiwa amesimama na macho yake ameyaelekeza kwenye mlango wa chumba alichomo Mavugo.
Waziri yule alihisi kama kuna watu tofauti na kina mama neema walikuwa pale ndipo alipogeuza macho yake kule walipo watu wale, alishangaa sana baada ya kumuona mwanae kipenzi akiwa pale. Alihisi mauza uza kwani muda si mwingi sana alikuwa nae huko Dar-es-salaam. Hasira za ghafla zilimuijia huku akitamani angalau amshambulie mwanae huyo, aliamua kumfuata huku akimuita na alipofika tu bila kuuliza alimchapa kofi la shavu mwanae.
''Shemeji??????'' Aliita Mama Musa, Mama alijawa na umasikini kwanzia tumboni mpaka kwenye mavazi yake. Sauti ile haikuzilenga ngoma za masikio ya wengine bali zilililenga skio la Waziri na Waziri alisikia sauti ile lakini ni kama hakuijali kwani alijua wazi kuwa wenye uwezo wa kumuita yeye Shemeji hawawezi kuwa kwenye hospitali kama ile bali kwenye mahospital makubwa tena ya binafsi.
Mama Musa alionekana kam amelukwa na akili kutokana na kuwa makini katika kumuita Waziri utadhani anaita mtu wa nasaba yake.
''shemeji???????'' Aliita tena kwa mara ya pili baada ya kuona muito wake wa mara ya kwanza haukuitikiwa, ndipo Waziri yule akageuka ilikuangalia ninani huyo asiye na heshima kiasi hicho. Inamaana yeye hana televisheni kwao ilikugundua kuwa aliyekuwa mbele yake ni Waziri wa michezo na utamaduni, au amekosa majina kama vile Muheshimiwa na mengineyo mpaka afikie kumuita kiongozi yule namna hiyo?? Bila shaka segerea ilikuwa ikimuita.
''Haaaaaaaaaaa!!!!!!!! Kumbe ni shemeji??'' Alijibu Waziri na kumuendea Mama yule kwa furaha ambayo kama wale waliyokuwa karibu wangeambiwa watoe mfano wa furaha ile aliyokuwa nayo Waziri basi wasingeweza kupata mfano huo.
Palepale, chemchem ya machzi ikaanza kutuka kwenye mboni za Mama Musa kisha Waziri na Mama Musa wakakumbatiana huku wakileta mshangao wa hali ya juu si kwa Neema, si kwa Devi, Aisha, Kibakuli, Musa, kisura,wala Dokta Endrew, hata wale walinzi wa Waziri, wote walishangaa kumuona waziri nadhifu kama yule akikumbatiana na Masikini. Laiti kama kungekuwa na mpiga picha bila shaka angeuza sana kwenye magazeti.
''Shem, kipi hasa kilicho kupata? mbona upo katika hali hii? vipi na mbona uliacha kazi kwenye Hospitali ya Muhimbili? shem, niambie ninini hasa maana nimeishi kuwatafuta bila mafanikio yoyote.
Kila Waziri yule alivyozidi kuongea ni kama alizidi kuyaita machozi ya Mama Musa tu. Lakini maswali ya Waziri yaliwashangaza sana waliyokuwa pale hata mtoto wa Mama Musa ambae ndo Musa mwenyewe nae alishangaa sana kusikia vile. Alihisi huenda wawili wale wakawa wamefananishana tu kwani katika maisha yake yote hakuwahi kusikia kuwa Mama yake alishafika Dar-es-salaam kwani hospitali ya Muhimbili ipo huko Dar-salaam. Kingine ni pale aliposikia juu ya kazi ya Muhimbili wa kati yeyeanajua waajiliwa halali wa kule ni wale wataalamu wa masuala ya udaktari, ina maana Mama yake ni Daktari? alijikejeli kwa kusema kuwa haiwezekani.
'' Shem, yaliyonipata anajua Mungu tu maana hata mii binafsi sielewi. Naikumbuka sana siku hiyo, Siku ambayo ilinitenganisha mimi mwanangu mfanya kazi wangu pamoja na Mume wangu kipenzi. Siku hiyo ilikuwa ni moja tu lakini ilitoshazaidi kunifanya hadi leo hii niishi maisha ambayo sikuwahi kuyawaza katika Maisha yangu, hakika ilikuwa ni pigo kubwa ambalo kamwe sitolisahau katika maisha yangu, huku kipindi hicho nikiwa na mimba ya Mwezi mmoja tu.'' Mama Neema alijitoa katika kumbato lile kisha akainamisha kichwa chini na kuanza kusimulia kwa umakini.
************************** **************

Ilikuwa ni majira ya saa nane usiku kama ilivyokuwa ikisema saa ya ukutani ndani ya nyumba ya Muandishi mmoja wa habari hapa Tanzania.

Nyumba hiyo ilikuwa tulivu sana kutokana na wahusika kufakamia mashuka na vitanda tu.

Si.. Baba mwenye nyumba, mama mwenye nyumba mtoto wala mfanyakazi. Wote walikuwa katika usingizi mzito.

Muda huo huo, waliingia watu wabaya kuanzia sura hadi mavazi.

Haikujulikana funguo za nyumba hiyo walizipatia wapi, lakini tayari walikuwa ndani.

Walikuwa takribani saba, huku miili yao wakiwa wameivika makoti yakazi. Watatu kati yao walikuwa wameshikilia marungu mikononi mwao huku wakiwa wamehifadhi silaha aina ya pisto ubavuni mwa mikanda ya suruali zao. Wale wengine ambao wao hawakuwa na marungu mikononi. Wenyewe walishikilia mapanga . Hakuna hata mmoja kati yao aliefunika wala kuweka alama yeyote ya uficho kwenye sura yake. Kila mmoja alijulikana.

Sasa, walijitawanya. Wawili walienda kwenye chumba cha mtoto na wawili walienda kwenye chumba cha mfanyakazi, huku watatu wengine wakipitiliza moja wa moja hadi kwenye chumba cha baba na mama wa familia hiyo. Hawakuenda kutoa salamu, bali kuwachukua wale waliokuwamo ndani ya vyumba vile na kuwapeleka moja kwa moja hadi sebureni.
Naam.. Walifanikiwa kwa jambo hilo, na sasa waliwakutanisha wanafamilia hao sebureni.

"Tumewakosea nini? Mbona mmekuja na mapanga pamoja na marungu huku mmehifadhi pisto utadhani mnaenda kwa wahalifu wa kimataifa." Aliongea Baba wa familia ile baada ya kusukumwa chini na kumsababishia ajibamize.

Hakuna majibu yoyote aliyoyapata kutoka kwa wanamume wale bali aliishia kuziona sura zilizojikunja na kuashiria kwamba hazipo hapo kwa ajili ya kucheka, bali kwa kazi fulani.

Mtoto baada ya kuona Baba yake amesukumwa. Hakutaka kuvumilia, palepale alijitoa mikononi mwamabwana wale waliokuwa wamemshika bila hata kumkaza, na kwenda moja kwa moja hadi alipoangukia baba yake. Huku mama pamoja na mfanyakazi wakiendelea kutoa kilio cha chinichini kutokana na mkwara waliochimbwa wa kutokupiga kelele.

Mmoja kati ya mabwana waliokuwa wamemshika mtoto yule, alimfuata kwa mara ya pili kwa niaba ya kumtoa pale chini. Lakini mtoto yule alikaidi na kumng'ata bwana yule mwenye sura mbaya iliyomkaa vyema usoni mwake.

Pale,pale kitendo bila kupoteza muda jamaa yule alitoa pisto iliyokuwa imefungwa kifaa cha kuzuwia sauti na moja kwa moja akamtwanga mtoto yule kichwani.

Mtoto yule palepale alianguka kifudifudi na kupoteza maisha. Mama wa mtoto hakuweza kuvumilia badala yake alitoa maneno ya kashfa na kutamani kumfuata mwanae angalau amshike lakini nafasi ile aliikosa kutokana na kukabiliwa na mabwana wenye misuli migumu.

Badala yake alianza kufyatua matusi, ambayo yalimpelekea awashwe kofi moja na kutulia kimya utadhani hayupo. Mume wake alijitahidi kujitoa maungoni mwa wanaume wale waliokuwa wamemdhibiti vilivyo kuanzia mikono, shingo na hata miguu. Hakuweza kufurukuta hata kidogo. Kila alipojaribu, alikutana na upinzani wa misuli migumu.

"ha,ha,ha,ha,ha.. Unajifanya unajua sana kuandika sindio?, leo tuna kuvunja vidole vyako ilituone utakuwa ukiandika huo ushenzi wako kwa kutumia nini." Aliongea mmoja kati ya watu hao saba na alikuwa ni mmoja kati ya waliokuwa wameshikiria marungu.

Wale walomshikiria bwana yule waliweka kijisturi cha mbao mbele ya bwana yule kisha wakaiweka mikono ya bwana yule kwenye kisturi kile na kuilaza vyema. Ni vidole vipatavyo kumi ambavyo vyote kwa pamoja vilikuwa vimewekwa juu ya situri hiyo.

"Aaaaahhhh!!" Ni sauti ya maumivu iliyotoka kwa bwana yule, na hiyo ni baada ya kupigwa rungu moja kwenye sturi na kumsababishia aumie vidole. Aliendelea kupiga mayowe ya maumivu lakini hakuna hata mmoja aliemsaidia.

Hawakuishia hapo watu wale.

"Hatuhitaji mashahidi." Ni kauli kutoka kwa mmoja kati ya watu wale wa kazi.

"Kwahiyo mkubwa, huyu binti tumfanye nini?" Aliuliza mmoja kati ya watu wale wa kazi.

"kata kichwa"

Mungu wangu! Kichwa cha binti yule kilitengana palepale na kiwiliwili chake. Masikini binti wa watu alikufa kifo cha kikatili sana, ni zaidi ya kuku au ng'ombe kwa sababu wao huchinjwa kwa heshma na kusomewa dua kabla.

Hawakuishia hapo watu wale wenye roho ngumu utadhani paka. Sasa walimshika mke wa bwana yule, huku kwa wakati huo bwana yule akiendelea kugugumia maumivu ya vidole vyake ambavyo kwa muda huo hakuwa na uhakika kama vingekuwa vizima au la.

ITAENDELEA.
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 31.

ENDELEA.

"Aaaaahhhh!!" Ni sauti ya maumivu iliyotoka kwa bwana yule, na hiyo ni baada ya kupigwa rungu moja kwenye sturi na kumsababishia aumie vidole. Aliendelea kupiga mayowe ya maumivu lakini hakuna hata mmoja aliemsaidia.

Hawakuishia hapo watu wale.

"Hatuhitaji mashahidi." Ni kauli kutoka kwa mmoja kati ya watu wale wa kazi.

"Kwahiyo mkubwa, huyu binti tumfanye nini?" Aliuliza mmoja kati ya watu wale wa kazi.

"kata kichwa"

Mungu wangu! Kichwa cha binti yule kilitengana palepale na kiwiliwili chake. Masikini binti wa watu alikufa kifo cha kikatili sana, ni zaidi ya kuku au ng'ombe kwa sababu wao huchinjwa kwa heshma na kusomewa dua kabla.

Hawakuishia hapo watu wale wenye roho ngumu utadhani paka. Sasa walimshika mke wa bwana yule, huku kwa wakati huo bwana yule akiendelea kugugumia maumivu ya vidole vyake ambavyo kwa muda huo hakuwa na uhakika kama vingekuwa vizima au la.

Mbele ya macho ya bwana yule. Alitazama mke wake kipenzi, mama wa mtoto wake, na mlezi wa familia yake. Akichojolewa nguo, moja baada ya nyingine. Kisha kuingiliwa bila ridhaa yake tena mbele ya macho ya mme wake.

Hapo sasa wakamfuata bwana yule na kumpiga rungu moja la kichwa, na kumpelekea apoteze akili zake kabisa na asijielewe. Palepale alipoteza fahamu na watu wale walimchukua na kwenda kumtupa yeye pamoja na familia yake, kwa kudhani kwamba atakuwa amekufa.
Lakini kutupwa kwao walitupwa tofautitofauti, mke wa bwana ylu aliyepigwa rungu la kichwa alikuja kushtuka yupo kwenye nyumba moja ambayo ilikuwa ikifuka moshi mkali sana kuhamaki alijikuta yupo uchi wa mnyama huku akiwa amezungukwa na wanawae watatu ambao walitoka kumkanda muda si mrefu. Hakuwa, ameumizwa sana kiasi cha kuharibu mimba yake ile ya mwezi mmoja tu ambayo hata kuonekana ilikuwa bado. Alihudumiwa na watu wale asio wafahamu na ndani ya miezi mitatu alirudi mjini huku akiamini kuwa, mme wake pamoja na mtoto wake watakuwa tayari wamesha fariki, akiwa katika hali ya uoga wa kuwaogopa wauaji aliamua asirejee nyumbani kwake kwa kujua kuwa kule pasingekuwa salama kwake kwa muda ule hivyo aliamua kwenda hotelini huku akizitegemea pesa alizokuwa nazo.
Siku moja akiwa hotelini pale mara alishangaa baada ya kuijiwa na mpita njia mmoja ambae nae kama yeye alikuwa amejihifadhi hotelini pale. Yule mpita njia akamuhoji kwani alikuwa akimfahamu. Alimuhoji kuhusu mume wake tu, baada ya kukumbushwa vile alibaki analia tu na kumuhadithia mkasa mzima ndipo yule mpita njia alipomwambia kuwa yeye katika mambo yake ya biashara huko Mwanza aliweza kukutana na mumewe lakini alimkuta yupo katika hali tofauti kabisa. Alikuwa amechakaa, huku akiwa hajielewi kabisa, pia mpita njia yule aliongeza kwakusema kuwa aliwahi kujifanya Mpelelezi baada ya kupata taarifa kuwa yule Mwehu alikamatwa baada ya kufanya mauaji. Alijipeleka gerezani baada ya kuhonga na alikutananae tena mwehu yule kisha akamsaidia na kujifanya yeye ni mpelelezi lakini mwehu yule alimkejeli na kumtaja hadi jina kisha akaondoka. Mpita njia yule hakuwa na namna zaidi aliamua kurejea Dar-es-salaam na kwa bahati hotel aliyofikia ndiyo aliyo kuwemo, mke wa mwehu yule na ndio maana akaona amuhadithie. Mwanamke yule aliamua kwenda kuchukuwa pesa benki na moja kwa moja akaianza safari ya kwenda mwanza, hata alipofika alivamiwa na wizi waliyomkwapua kila kitu alichokuwa nacho na kumfanya aanze kuishi maisha ambayo hakuwahi kuyaishi. Aliombaomba hatimae akapata mtaji wa karanga, hivyihivyo na mimba yake alianza kuuza karanga huku akisahau jukumu lililompeleka kule kutokana na umasikini uliomuingia ghafla. Na hayo ndio yakawa maisha yake.
********************** ********************************

Mama Musa aliimaliza historia ile ambayo ilimfanya kila mmoja ashangae, ilikuwa ni kama filamu nzuri. Dokta Endrew hakuwa mbali katika historia hiyo na hapo ndipo akapata fursa ya kumuelewa Mavugo vizuri. Waziri yule alimpa pole Maqma Neema na kumlalamikia kwa kukaa kimya muda wote ule kisha akamshangaza sana Mama Neema baada ya kumwambia kuwa mume wake yupo kwenye chumba cha matibabu na wote waliopo pale wapo kwa ajili yake.

''Unasemaaa????'' Alihoji Mama Musa baada ya kupata taarifa ile mpya kabisa kichwani mwake.

''Ndo hivyo shemeji. Mumeo yupo hapa na ameshtuka ghafla baada tu ya kuniona.'' Aliongea Waziri yule. Chizi la tofauti na mwanzo lilimtoka tena Mama Musa chozi lile halikuwa na maana yakilio bali lilikuwa likimaanisha furaha isiyo kifani.
Kwa jinsi Mama Musa alivyokuwa akimpenda mume wake alitamani sana aende kumuona mume wake yule, lakini ilibidi asubiri tu maana mgonjwa wao alikuwa bado hajazinduka.
''Na huyu amefika vipi hapa?'' Alihoji Waziri huku akimsonteshea kidole mwanae Kisura wa Musa.
''Huyu ndie aliyenisaidia kwani bila yeye hakika nisingekuwepo duniani mpaka muda huu. Huyu ndie msaada wangu, ndie alitoa pesa na mimi nimetibiwa. Kwani vipi, unamjua?'' Alijieleza Mama Musa kisha akahoji.
''Usinambie...!!!'' Aliongea kwa mshtuko Waziri, kisha akasema,''Shemeji, huyu ni mwanetu kabisa.'' Alijibu Waziri na hapo kila mtu aliyekuwapo pale akashtuka sana hata Musa nae hakuamini kila kilichokuwa kikitendeka maeneo yale. Kila kilichokuwa kikiendelea kwake alikuwa akiona kama ni filamu ya maigizo tu.
''Ndo hivyo shemeji, Umesaidiwa na mwanao nasi mtu baki.'' Hata kama wangeendelea kushangaana basi wange maliza hata mwaka mzima likini yanini waendelee kutengeneza maswali ilhali majibu yote yapo palepale, wote kwa pamoja walimshukuru Mungu kwa kuwa kutanisha pale ilhali hawakuwahi kuwaza kukutana tena kwa mara nyingine.
Labda kwa ufupi, Musa Waziri Mwambe ni rafiki wa Mavugo na waliishi pamoja tangu utotoni na hata kusoma walisoma pamoja katika shule moja huko Dar-es-salam kwanzia Elimu ya msingi hadi o-level. Baada ya hapo walitengana kutokana na kuchaguliwa shule tofauti kulingana na michepuo yao. Walikuja kukutana tena huku kila mmoja akiwa na kazi yake, wakati huo wote walikuwa wameshaoa, Mavugo yeye alikuwa na mtoto mmoja huku maisha yake ya kiwa mazuri kabisa pia Mwambe alikuwa hivyohivyo, tofauti yao Mwambe kabla ya kuingia kwenye maswala ya Siasa alikuwa ni Muhasibu katika moja kati ya mabenki makubwa huko Dar-es-salaam huku Mavugo yeye akiwa na kazi njema aliyoisomea ya uandishi wa habari. Naam, alipendwa sana kwani kila chapisho lake lilikuwa na ukweli, aliyaongelea matatizo ya jamii yake na hata hakusita kuwa anika watu ambao walikuwa wakienda kinyume na matakwa ya taifa lao jambo ambalo lilimpelekea kupata maadui wengi wenye vyeo na wenye pesa nyingi au vizito kwa jina jepesi. Mwambe yeye aliamua kujiingiza kwenye siasa kwani ndio ilikuwa ndoto yake toka alipokuwa na umri mdogo. Bila kusahau wawili hao, walilelewa na kusomeshwa kwa ufadhili wa taasisi moja isiyokuwa ya kiserikali ambayo ilijitolea kusomesha watoto wa mitaani ambao hawa kuwa na msaada. Natumai mpaka hapo utakuwa umemfahamu Waziri Mwambe Historia yake japo kiufupi.

''Docta, anaendeleaje mgonjwa wetu?'' Alizungumza Docta Endrew baada tu ya kumuona mmoja kati ya madaktari waliyokuwa wakimshughulikia Mavugo.
''Nafikiri mnaweza kwenda kumuona kwani tayari ameshaamka.'' Furaha iliwajaa baada yakusikia kauli ile na wote wakaupigania mlango wa kuingia kwenye chumba alichokuwemo Mavugo. Peta, Mwambe nikama aliisahau heshima ya suti yake kwani jinnsi alivyo ipelekesha mlangoni, haikuwa kawaida.
''Haaaa!!!! Mke wangu'' Aliita Mavugo kwa mshangao baada tu ya kumuona Mama Musa. Palepale Mavugo akayasahau maumivu ya kichwa na kujiinua kitandani kwa upesi wa ajabu na moja kwa moja akaenda kumkumbata mkewake.
''Mke wangu, kumbe bado upo hai???'' Aliuliza Mavugo huku amemkumbata mke wake kwa majonzi, Swali la Mavugo halikuweza kujibiwa hiyo ilitokana na hali ya Mama Musa kwa mda huo kwani alikuwa amejaza furaha iliyoziba maneno yote mdomoni na kumfanya ashindwe kuongea lolote. Docta Endrew aliangalia juu na kunyoosha mikono yake yote miwili na kumshukuru Mwenyezi Mungu kani hakutegemea kabisa kumpatanisha Mavugo na ndugu zake kiurahisi namna hiyo.
Wote kwa pamoja walishukuriana huku kila mmoja akimuona mwenzake mwenye umuhimu katika jambo lile, si, Neema, Aisha,Devi, Kibakuli, Endrew wala wengine.
Naam, pasina Endrew basi Mavugo asingeonana na Mkewe, pia pasina Neema basi Pita mwambe asingeonana na Mavugo. Hakika kila mmoja alikuwa na haki ya kushukuriwa.
Hapo, Mavugo akarejea katika hali yake ya kawaida.
''Hebu tuelezee, labda unaweza ukawa unawafahamu wale watu waliyokuvamia na kukuharibia kabisa mfumo wa maisha yako?'' Alihoji Mwambe .
''Bila shaka, naziona sura zao ndani ya ubongo wangu, huku unyama wao ukiendelea kufanyika kiifikra. Hakika hawana haki katika hii dunia zaidi ya kutiwa kitanzi tu. Hakika na jaribu kufumba macho ilinitengeneze ndoto ya kufikirika, lakini naishia kuliona tendo la kweli lililofanywa na mtu niliyemuamini na kumpatia nafasi kubwa katika maisha yangu. Sito sahau, hatakama jicho langu litaingiwa mchanga lakini nitaishia kuuona ukatili huo, ndani ya macho ya fikra zangu. Naam, mimi ni muandishi wa habari, kazi yangu nikuandika habari, wale nilowaandika kwene habari ndio waliyoni haribia mfumo mzima wa maisha yangu, wamenifanya nidharaulike, nipoteze heshma. Niishi kama kichaa, niijutie mpaka elimu yangu ya Habari, labda kiufupi ilikuwa hivi...........................

Baada ya mimi na wewe kuachana, wewe ukaenda shule, kwa mara ya kwanza huko ndiko nilipokutana na rafiki yangu mmoja ambae alikuwa mchangamfu, lakini asipende makuu na mtu. Nakumbuka, mara ya kwanza kukutana nae baada ya mimi kuripoti shule na kupangwa chumba kimoja nayeye. Tulianzisha urafiki baada ya mwanafuzi mwenzetu tuliyekuwa tunalalanae kuleta mambo ya dharau, hakuwa anafanya usafi kitendo kilichopelekea sisi tumtenge na ndipo tukajikuta ghafla tumekuwa marafiki. Mwenzangu alikuwa akipenda sana maswala ya sheria na kutokana na upendo huo alijikuta akiathirika hata kwenye maisha yake ya kawaida.
''Oy, We mwanasheria amka tupige pindi.'' Nilizoea kumuamsha hivyo kila ilipofika mida yetu ya kujisomea, sikwamba hakuwa na jina anaitwa Maganga Mazezere Maluvya yeye alipenda kujiita Trriple M, tofauti na mimi ambae nilipenda sana kumuita mwanasheria.
'' Aisee, Mavugo, nitakufunga mimi. Hujui una muamsha jaji wa baadae, sasa unapaswa uwe makini sana sio ukijiskia tu kunisukumasukuma basi unafanya.'' Nikawaida yake kabisa kunijibu hivyo, kwahiyo sikuwa nikipatwa na mshangao wa aina yoyote kwani nillisha mzoea kabisa. ''Acha zako, inamaana hata hao majaji ndo huwa wanaamshwa kama mayai!!!Hebu nawa huko tupige pindi.''
 
RIWAYA: KICHAA.

Na: ZUBER R. MAVUGO.

N0. 32.

ENDELEA.

''Oy, We mwanasheria amka tupige pindi.'' Nilizoea kumuamsha hivyo kila ilipofika mida yetu ya kujisomea, sikwamba hakuwa na jina anaitwa Maganga Mazezere Maluvya yeye alipenda kujiita Trriple M, tofauti na mimi ambae nilipenda sana kumuita mwanasheria.
'' Aisee, Mavugo, nitakufunga mimi. Hujui una muamsha jaji wa baadae, sasa unapaswa uwe makini sana sio ukijiskia tu kunisukumasukuma basi unafanya.'' Nikawaida yake kabisa kunijibu hivyo, kwahiyo sikuwa nikipatwa na mshangao wa aina yoyote kwani nillisha mzoea kabisa. ''Acha zako, inamaana hata hao majaji ndo huwa wanaamshwa kama mayai!!!Hebu nawa huko tupige pindi.''

''Takufunga? Sipendi dharau, hata kidogo. Wewe ni muandishi halafu mimi ni jaji hivi unadhani utaniweza wewe???? Kwanza hebu leta hilo daftari la Histori hapa nianze kwanza mimi kusoma lasivyo, Ibara ya hamsini na mbili kifungu namba moja hadi mbili kitatumika hapa.'' Alikuwa akipenda kunionea kwa vifungu vyake nisivyovielewa, lakini yote kwa yote tulikuwa tukichukulia kila maneno tuliyo kuwa tukiyaongea kama sehemu yetu ya utani tu. Baada ya maneno yetu basi wote hukaza msuli kwani tulikuwa tukisoma mchepuo wa aina moja.
Yeye ndie aliye nifunza kuuheshimu muda kwani hapo kabla sikuwahi kuuheshimu muda hata kidogo. Nilikuwa radhi muda unipite nami nikajiona niko sawa tu.
'' We Mavugo, ngoja nikwambie kitu, hivi unajua kila kitu kifanywacho na binadamu kwa siku, hutegemea muda.'' Kwakuwa nilipenda ubishi basi sikuwa nikisita kumbishia,''Umeanza uanasheria sasa, naona unaniona mwehu, ina maana hata kuongea tunategemea muda!!! aaaaah!!! hahahaha we jamaa wewe muongo kinoma.'' Nilimjibu vile huku tukielekea kwenye kijimgahawa kilichopo shuleni kwetu, kwakuwa anaujua ubishi nilobarikiwa basi alikuwa akiniacha na kuanzisha mada nyingine tofauti na ile kisha baadae hunielewesha.
Shule yetu ilikuwa ni mchanganyiko hivyo hatukuwa na uwezo wa kuepuka mabinti ambao tulishindanao darasani kutwa nzima tofauti ni kwamba hatukupewa uhuru wa kulala pamoja nao kwani shule yetu ilikuwa na mabweni yawasichana na yale ya wavulana.
Mimi katika maisha yangu sikuwahi kujua wala kutegemea kujua kitu kinachoitwa Mapenzi, nilikuwa nikishuhudia tu toka nipo mdogo watu wakipendana na hata kwa macho ya barehe yangu changa niliweza kutamani tu wasichana lakini sikuwakaribia kutokana na aibu niliyokuwa nayo, nadhani hata wewe ni shahidi Mwambe kwani o-level tulisoma wote. Nilikuwa sipendi kumuongelea msichana na hata nilipo muona mtu akilia kwa ajili ya sichana nilikuwa sisiti kuangua kicheko cha dharau mbele yake hadi hapo atakapo nichukia. Bila shaka niliwaona wote waliyokuwa wakiumia kwa ajili ya mapenzi ni kama mapunguwani, nilikuwa nikijisemea, ''Mwanamume huwa analililia daftari lake bwana nasi kumlilia mwanamke ambae haleti hata maarifa.'' Rafiki zangu walikuwa wakinicheka ukiwemo na wewe Mwambe, na kuniambia kwamba , ''Mavugo unaongea tu, huyajui mapenzi wewe.'' Nadhani nawe nishahidi kwa jinsi nilivyokuwa nikiwaangulia kicheko kilichokuwa kikiwafanya muendelee na shughuli zenu na kuniacha mimi kivyangu.

Ilikuwa mara ya kwanza katika maisha yangu kuona msichana aliyeridhiwa na moyo pamoja na nafsi yangu kwa ujumla. Siku hiyo ilikuwa ni jumapili au siku ya wali kama tulivyoipachika jina. Muda huo nilikuwa nimekaa mazingira ya uwanjani kama ilivyokuwa kawaida yangu toka shule ya awali. Hapo ndipo alipopita mrembo yule ambae macho yangu yalimpatia vigezo vyote vya urembo wa dunia na kumpa kura ya ushindi wa urembo huo endapo kama angeshiriki. Katika maisha yangu sijawahi kuklubali niyakodoe macho yangu kwa ajili ya kumuangalia msichana lakini siku hiyo ndio mara yangu ya kwanza, nilimuangalia sana binti yule kisha nikaanza kupekuwa ndani ya kichwa changu huku nikijaribu kuufananisha urembo wake na urembo wowote ambao nilishawahi kuuona lakini sikupata, nilifikiria mara ya pili ndpo nilipoamua kumfananisha urembo wake na urembo wa wale wanaosifiwa kwenye vitabu vya dini kuwa huwa ni wazuri, watiifu, na hufuata amri za Mungu tu. Hawajawahi kumkosea wala kukaribia kufanya hivyo. ''Ewaaa!!!! Huyu ni maraika kweli.'' kupitia mapigo ya moyo wangu, chapisho la maneno hayo liliweza kuonekana kifira huku sjui nimuite, sjui niacha zikiendelea kunisumbua akilini mwangu. Nafsi ilitamani kumshika binti yule walau hata mkono tu, lakini kila ilipoiamrisha miguu kitete kilinijaa na kushindwa kumsogelea. Nilisahau kabisa kama binti yule aliye nishugulisha mwili mzima kasoro kivuri ndani ya dakika moja tu, alikuwa akiondoka na kuniacha nikipata fursa ya kumuangalia maungo yake ya nyuma, sikuwa na dini wala sikupenda mambo ya dini lakini nilijikuta nikiropoka ''Astaghafirullah'' Labda pengine kwa kuwa malaika yule alikuwa amevaa mavazi ya kiisilamu tu. Hapo hapo fikra zina nichukuwa na kujikuta nawaza nipo katika ndoa huku shekh akifungisha ndoa.
''Hivi!!! Mavugo, sikuhizi unavuta bangi???'' Alinihoji Maganga baada ya kunikuta nipo nikichekacheka peke yangu. Hakika hakujua mwenzie nilipokuwa kifikra. Nilikasirika sana baada yakukatishwa mawazo yangu kwani nilijua kabisa tayari nimeshaoa, nilijaribu kufumba macho na kukumbuka mawazo yale, lakini malaika wanguu hakuja tena.
Kwakuwa ni raiki yangu mkubwa basi siku sita kumwambia jambo lile.
''Sheria ya Mapenzi kifungu namba tatu kilichoandikwa na wapendanao wa kwanza walisema kuwa, Mapenzi huanza kama chemchem ndogo ndani ya moyo lakini chemchem hiyo huzaa bahari kubwa na kuujaa moyo kadri mpendaji anavyo zidi kujiathiri kimawazo kwa kumuwazia yule aaehisi kuwa anampenda. Ikumbukwe kwenye tahadhari ya wapendanao wa awamu ya pili wao waliwahi kusema kuwa ile ladha ya uchungu ambayo hupelekea mapigo ya moyo na baada ya hapo kuhisi raha, ndio hiyohiyo ambayo hupelekea maumivu pindi yule unaehisi unampenda atakapo kuacha na makovu. Kwahiyo sasa tuna pata jibu kuwa asilimia za upendo ndani ya mapenzi ndizo hugeuka kuwa za maumivu baada ya kutendwa. Karibu sana kwenye uwanja wa dhambi kwani huku kwetu kulizana ni sunna kabisa.'' Huweziamini moyo ulikuwa ukikimbia kadri Maganga alipokuwa akiongea maneno yake, nami nilikuwa niki yanukuu kwenye kidaftari changu kidogo kwani nilipenda sana kukusanya habari na sikuwa mtu wa kurdhika habari inipite kwakuwa nilipenda sana uandishi wa habari.
''Kwahiyo nipe anuani nikusaidie kukuunganishia.'' Aliongea, Maganga huku akitazama na kulichanua lile tabasamu lake la kuoneshea ushirikiano.
'' Wewe, kwani ukimpenda mtu hadi ajue bwana... Achana nae, mistaki'' Nilikaidi kinamna ile.
''Acha mambo yako wewe, muandishi gani anaekub ali kupitwa na habari?''
''Habari??? Ipi hiyo nikaandike.''
''Jione ulivyo bwege,'' Huku akiigiza maneno yangu kwa kubana pua na kunifanya nijionee aibu, '' Eti, Habari, ipi hiyo nikaandike,'' Kisha akaendelea, '' Ujuwe, juha si yule mfalme tu wa kwenye vitabu, bali hata kuwa mtu wa aina yako ni ujuha tosha.'' Hapo aliniacha hoi kwa hasira za ghafla kwani kila nilipokuwa nikilifikiria lile neno Juha nilikuwa nikichukia sana. Kwa hasira nikamvagaa kimaneno, ''Usiniletee, umeona nani juha hapa. alafu usidhani kukaa kimya muda wote ndio nakuogopa, sasa umependa wewe au mimi!!! Mbona unataka kuniwekea masharti kwenye moyo wangu? Kwani we hauna limoyo? Sasa siuliite juha lakwako nasi kuniita mimi, tena kwa taarifa yako juha mwenyewe.'' Nilimjibu huku kwa akili yangu nikijua ataniacha kumbe nitofauti na nilivyodhania.
Huku akicheka, ''Aisee!!! sijawahi kuona muoga kama wewe, huo ni uoga tu unakusumbua. Eti unajiita muandishi!! Muandishi gani unaogopa hadi madem, natuone sjui utafika wapi boya wewe.'' Labda niseme tu ukweli kuwa maneno yake yali ni choma sana, ni dhahiri kabisa alikuwa amenipatia kwani nilikuwa nikiogopa wasichana na sikuwa na lakuongea mbele yao. Nikaanza kusaka jibu kichwani mwangu la kuifanya kauli yake ione kane ya uongo....

Sikila anaechanua tabasamu anamaanisha kudhihirisha furaha, wengine hutumia njia hiyo kuyafuta yale yawaumizayo. Hakika uso umehifadhi mengi sana ya siri kutoka moyoni na kamwe hauwezi kuyaelezea pasina vigezo muafaka. Ndivyo ilivyokuwa kwangu, nilipokosa jibu la kumjibu rafiki yangu Maganga nilijifanya ninafuraha ilhali moyo wangu una aibu isiyo mithilika. Hakika aliniweza, nilitamani iwepo jokofu iliangalau nikapoze joto la aibu ile lakini hapakuwa na kitu hicho. Nilitamani sana kumwambia rafiki yangu angalau akanisaidie kuongea na mrembo yule lakini nafsi ilikataa huku ikinisihi kuwa niende mwenyewe kwani si adabu mwanamume kuzielezea hisia zake mbele ya mwanamume mwenzake ilhali anakila kitu cha kumfuata mwenyewe ampendae ''Staki kutongozewa.'' Nikauli iliyotoka moja kwa moja moyoni, baada ya kuisikiliza kauli ile palepale ni kamwambia Maganga kuwa lazma nimtafute mrembo yule na niyaelezee ya moyoni mwangu.
Kama wafanyavyo vijana walika letu, tulijipongeza huku Maganga akiniambia kuwa huo ndio uanaume nami nikafurahia huku nikimpiga ngumi za begani. Tulichukuana na kuelekea, bwenini kwa ajili ya kujadili jinsi gani nitaweza kuongeanae.
''Sio, hivyo. Tatizo lako wewe bado mshamba sana, mrembo huwa hafatwi kwa style hiyo.'' Alinikosoa Maganga kipindi tupo bwenini tukifanya majaribio mbalimbali ya jinsi nitakavyomfuata mrembo yule kwani kiukweli sikuwa nikifahamu chochote kuhusu msichana.
''Kumbe vipi?'' Nilimuhoji huku nikisogea karibu na sanduku la nguo na kumuacha yeye ilianielekeze.
''Kwanza unapomfuata unatakiwa uhakikishe kuwa uko safi, usikubali kabisa akusome hata kidogo kwani akikusoma tu, tayari ataanza kukudharau.......'' Aliendelea kunielezea mambo kadha wa kadha huku nami nikiandika baadhi japo si yote.
''......aisha yangu yapo mikononi mwako, uzuri wako haunitoki machoni mwangu, kwamara yakwanza tu kukuona nilihisi moyo wangu ukikufuata, nilijitahidi kuuzuia lakini katu haukukubali, sikuwa najua kilicho nipata lakini baada ya kuitazama sura yako kwa umakini ndipo nilipogundua kuwa nusu ya moyo wangu ipo kwako na hicho ndicho chanzo cha kugundua kuwa nakupenda. Kila jina ninalojaribu kukupatia nahisi halito sadifu uzuri wako mrembo, kabla ya kuja hapa nimejaribu kupekuwa majina mazuri mazuri ni yajuayo lakini hakuna hata moja ambalo linawianna na uzuri wako, kama mimi tu nimepata shida kukutungia jina basi sipati picha hao waliyokuzaa sijui walikupa jina gani? Acha niseme tu ukweli, sina uhakika kama wewe ni mtanzania halisi, nahisi utakuwa chotara tena chotara wa huko umalaikani......'' Hiyo ni baadhi tu ya mistari aliyokuwa akinipatia Maganga huku nami nikiinukuu kwenye daftari langu ilinisisahau. Maganga alikuwa anakipaji cha saikolojia ingawa saikolojia si kipaji, hakika sikuwa nikimuelewa rafiki yangu yule kwani mambo yake niliyafananisha kabisa na yale ya watu waliyobarikiwa.
 
KICHAAA

ZUBERY R. MAVUGO.

[MR...FEELLING]

NO: 33

ENDELEA.

''......aisha yangu yapo mikononi mwako, uzuri wako haunitoki machoni mwangu, kwamara yakwanza tu kukuona nilihisi moyo wangu ukikufuata, nilijitahidi kuuzuia lakini katu haukukubali, sikuwa najua kilicho nipata lakini baada ya kuitazama sura yako kwa umakini ndipo nilipogundua kuwa nusu ya moyo wangu ipo kwako na hicho ndicho chanzo cha kugundua kuwa nakupenda. Kila jina ninalojaribu kukupatia nahisi halito sadifu uzuri wako mrembo, kabla ya kuja hapa nimejaribu kupekuwa majina mazuri mazuri ni yajuayo lakini hakuna hata moja ambalo linawianna na uzuri wako, kama mimi tu nimepata shida kukutungia jina basi sipati picha hao waliyokuzaa sijui walikupa jina gani? Acha niseme tu ukweli, sina uhakika kama wewe ni mtanzania halisi, nahisi utakuwa chotara tena chotara wa huko umalaikani......'' Hiyo ni baadhi tu ya mistari aliyokuwa akinipatia Maganga huku nami nikiinukuu kwenye daftari langu ilinisisahau. Maganga alikuwa anakipaji cha saikolojia ingawa saikolojia si kipaji, hakika sikuwa nikimuelewa rafiki yangu yule kwani mambo yake niliyafananisha kabisa na yale ya watu waliyobarikiwa.

''Hapa sasa acha nijisomee mapema kishanianze kuhifadhi mistari, siunajua tena haya mambo ili yakae kichwani yanahitaji kuhifadhiwa.'' Nilimwambia rafiki yangu yule, nae akaniacha nifanye nilichotaka kisha akatoka na kwenda kupiga soga na marafiki.
Mimi nilidurusu mistari ile mpaka hapo nilipo hakikisha kuwa imeingia yote kichwani, baada ya hapo nikaingia kwenye zoezi la kuongea sasa, hapo nilikuwa nikijiumauma mwenyewe ndipo nilipoamini kumbe kutongoza ni interview ngumu kuliko zote ambazo nimepata kuziona toka nifike katika hii dunia, Kichwa kiliniuma kwa kuwaza majibu atakayo nipatia baada ya kila msitari.

''Nakupenda sana.....'' Nilijisemea ndani ya mchezo ule wa maigizo ambao niliamua kuutunga mwenyewe.

''Kilichokufanya unipende, nikipi hasa?'' Nilijiuliza mwenyewe maswali yale magumu iliniweze kuyatatua kwa ajili ya kujihami, sio aje aniulize nami nikoswe jibu.

''Kilichonifanya nikupende ni uwiano wa kiajabu, kutoka katika hisia zangu hadi kwenye kila kiungo ulicho nacho.'' Nilijijibu kisha nikajipatia vema kuwa akiniuliza hivyo nami nikamjibu vile basi itakuwa safi.

''Kwani nini hasa kilichokuvutia kutok kwang?'' Nilijihoji swali lile huku nikilitafutia ufumbuzi. Swali lilikuwa gumu sana katika kichwa changu, nilipekuwa kamusi yangu ya maneno, nikakosa maneno ya kutengeneza sentensi kamili, hapo nikajikuna sana kichwa.

''kila ulichobarikiwa na Mungu, nilichokiona na ambacho sijakiona, mfano umbo lako lenye ghadhabu na macho yangu, tabia yako ambayo unanionesh, maneno yako yakutokavyo mdomoni utadhani maneno matakatifu yaliyoandikwa na mtu asiye julikana, una sura ya kipekee na unafaa kuishi nami katika sayari yangu ya mapenzi, tafadhali elewa kila ni kwambiacho kwani kwani unapoonesha kutokuelewa mimi najihisi mwenye dhambi na kuzimu ya mapenzi inaniita. Nakuomba, nikubalie ombi langu.''

Hapo, niliyaandika na maneno yale kisha nikaenda kumpelekea na Maganga nashukuru alinipongeza na kuniambia nimejitahidi sana.
Safari ikaanza ya mimi kumfuatilia mrembo yule aliye hitimu mafuno ya uzuri ndani ya moyo wangu. Naam, ilituchukua muda sana kumpata kwani shule yetu inawanafunzi wengi sana halafu nilikuwa simjui hata jina lake, niliutegemea sana uzuri wake kumtafutia, hatimae tulibahatisha kumuona. Alaaa sikujua kama anapenda sana big ji, nilimuona akiwa ameshikiria big ji mkononi huku nyingine akiendelea kuitafuna.
Moyo niliuhisi kama unanitoka kwa hamu uliyokuwa nayo nikamuomba Maganga anisubiri baada ya kumsikia mwenyewe akikili kupitia mshangao wake wa ghafla kuwa yule binti ni zaidi ya wale wanaoandikwa vitabuni. Nilimsogelea kwa kujiamini kupitiliza kwakuwa nilikuwa nimekariri mistari ya kuongea nae, kwa mara ya kwanza nikamfikia mremnbo yule, nikampa salamu nae akaitikia.

Labda, nikili tu wazi kuwa tokea nianze kusikiliza nyimbo, sijawahi sikia msanii yeyote wa kike mwenye sauti ile, nikaamua kuifananisha sauti yake na sauti ya ndege mzuri anaejifunza kubembeleza watoto wake katika kiota, lakini hakuna nilichoambulia kwani sauti ile ilikuwa nzuri, hapo sasa nikajihisi kwa maa yakwanza ninakutanza na moja kati ya maajabu saba ya dunia.

''Sema kaka mbona unashangaa?'' Aliniambia mrembo yule, naam nikweli nilikuwa nikishangaa jinsi Mwenyezi Mungu alivyompendelea binti yule.

''Kaka?'' Aliniita tena baada ya kuniona sishtuki, kwa muda huo nikama aliniua kabisa kwani ndio mara ya kwanza kushikwa bega na mrembo kama yeye. Mwili ulinifa ganzi, taraibu bila kujitambua nilijikuta nikienda chini huku mawazo yangu yakiwa katika urembo wake. Nikama uchawi, lakini ndio ilikuwa kweli kabisa, nilidindoka chini na kutojielewa kabisa. Nilipokuja kushtuka, nilishangaa ushungi wenye harufu ya manukato mazuri ambayo sijawahi kuyanusa, ukinipepelea, nilinusa harufu ile kwa nguvu huku nilijikuta naushikiria ushungi ule, nilipotupa macho kumuangalia aliye kuwa akipepea, alikuwa ni yule mrembo ambae ameniweza moyoni mwangu, nilisisimka baada ya kumuona katabasamu kisa mimi nimeanguka.

Alinipa pole na kunisindikiza hadi nilipomuacha rafiki yangu Maganga. Kiukweli sikuweza hata kumwambia chochote binti yule hadi pale alipoondoka na kufika mbali ndipo moyo wangu ukaanza kuhitaji tena awepo karibu ilimdomo uyaelezee yaliyomo ndani ya Moyo.

Kwenye kutambulishana majina hapo ndipo nilipo pata fursa ya kulijua jina lake hakika lilinichukuwa muda sana kunikaa kichwani.

'' acha uboya wewe......... mtoto, amesema anaitwa Faraithati na si Karaishati shauri yako,'' Aliongea Maganga huku akiongeza,'' Sikia mshkaji wangu. Unajua wewe ndie unatakiwa ulitaje jina la huyo shemeji yangu kiufasaha kuliko mtu yeyote yule. Ukijifanya kushindwa watakupiku wale wanayojua nini maana ya jina'' Ah! Mimi kusikia maneno yale nikaliandika lile jina pembeni haraka na kuanza kulihifadhi mwisho wa siku nikajikuta nimeliweka kichwani.

Siku ile ya jumapili ilipita hatimae juma jipya tulilianza, huko shuleni. Mimi sikuwa nikipenda kuonewa hata siku moja, walikuwa wakipata sana kazi wale wanaojiita viongozi kwani walinyanyasa wanafunzi wote lakini watu kama mimi hatukuwa tukiguswa kabisa. Usimamiaji wangu wa maamuzi ulipelekea viongozi waniundie makosa iliniptiwe adhabu. Nilijitahidi kumtafuta sana yule malaika lakini sikufanikiwa kumpata, nilijitega eneo lile nililo kutana nae kwa mara ya kwanza lakini sikufanikiwa kumuona kwa shule yetu ilikuwa inawanafunzi wengi sana. Kuanzia o-level hadi high-level. Sikujua alisma kidato cha tano ama cha sita kutokana na kujaa kwa mikondo na madarasa pale shuleni.

Nilimaliza hadi wiki nzima pasina kumuona, nilihisi labda atakuwa kahama shule, wiki iliyofuata niliweza kubambikiziwa kosa la na kupewa adhabu ya kuhamisha ardhi iliyokuwa imeinika na kuisogeza pembeni. Kwa vile adhabu zile nilishazizoea, skuwa na jinsi zaidi ya kuzifanya tu.

''Haaa!!!! Wewe tena'' Nisauti ile iliyowahikuniangusha chini wiki moja nyuma, sauti ambayo ilishanishinda kabisa kuifananisha na chochote kile. Nikageuka nyuma, macho yangu yakakutana na macho ya Faraithati, msichana ambae hakuna kama yeye. Kuhamaki nikamuna na tai nilishangaa sana kwani najua kuwa wote wenye ruhusa ya kuvaa tai ni viongozi tu.

Aliponiona hata yeye alishangaa sana kunikuta katika adhabu kama ile. Nilimueleza tu ukweli kwamba nimemtafuta takribani wiki nzima bila kumpata, aliniambia kuwa mara nyingi huwa anakuwa bize sana na masomo kitendo kinachompelekea asionekane sana. Maongezi yetu hayakuweza kuathiri adhabu yangu kwani yeye aliwekwa pale akiwa kama msimamizi kwakuwa alikuwa ni kiranja wa nidhamu.

Nilifanya adhabu ile mpaka ikaisha ndipo tulipo pata muda mzuri zaidi wa kuongea, nilijitahidi kuongelea stori za mapenzi ilinimshawishi lakini alionekana kutokupenda stori za namna hiyo, nilijipanga kimaneno na kuanza kuongea yale ya kwenye daftari lakini majibu niliyo jibiwa yalikuwa tofauti na yale niliyo ya dhania. Alinambia kuwa hana shida ya mwanamume kwa muda ule nilipomuuliza juu ya sababu alisema kuwa endapo atayaruhusu mapenzi kuingilia masomo yake basi atashuka kimasomo jambo ambalo hakuhtaji litokee kabisa kwakuwa mimi ni king'ang'anizi nilijitahidi kung'ang'aniza lakini alikataa tu. Mtoto wa kiume nilimwaga chozi kwa ajili ya kumlilia yeye lakini hakulielewa chozi langu. Skuwa na jinsi niliondoka pale nikiwa nimepewa adhabu mbili, ya moyo na ile ya kuhamisha ardhi. Huku nalia nilienda bwenini na kulala. Nilijifikiria mara mbilimbili lakini jibu nililopata ni kwamba siwezi ishi bila Faraythati. Nikamtafta mara nyingine kwenye simu lakini hakunielewa tu, uamuzi wa mwisho nilioufikiria ulikuwa ni ule wa kuchukuwa kamba na kujifunga katika kichwa changu kwa kuizungusha ilinijiue mwenyewe kuliko kuteswa na mapenzi, nimengisana yaliyonipata hadi nikaamua vile.

Majibu aliyokuwa akinijibu, na alisha wahi kuniambia kuwa nijiue pale nilipomuuliza nifanyenini ili aridhike.
Kwakuwa alikipenda kifo changu kuliko uhai wangu hapo nami nikaona bora nimridhishe, kamba ikakaa shigoni vyema kabisa nikaanza kuhesabu hatua za kuliendea kaburi, ile nakisukuma kiti tu hivi kwa ajili ya zoezi lile lakumridhisha

Faraythati mara mlango ukafunguliwa na sikumjua aliyeingia lakini nilikuja kumjua baada ya kujikuta hospitali, kumbe nilikuwa nimezimia.
Nilikasirika sana baada ya kukatishwa zoezi lile la kifo na rafiki yangu Maganga aliyenipenda sana kiasi cha kutotaka kuuonma uhai wangu ukichomoka hivihivi. Nasaha pamoja naushauri wa kina kutoka kwake ndivyo vilivyonijenga na kuniahidi kuwa lazma niwe na Faraythati kwa hali yoyote ile.

ITAENDELEA
 
KICHAAA

ZUBERY R. MAVUGO.

[MR...FEELLING]

NO: 34

ENDELEA.

Majibu aliyokuwa akinijibu, na alisha wahi kuniambia kuwa nijiue pale nilipomuuliza nifanyenini ili aridhike.
Kwakuwa alikipenda kifo changu kuliko uhai wangu hapo nami nikaona bora nimridhishe, kamba ikakaa shigoni vyema kabisa nikaanza kuhesabu hatua za kuliendea kaburi, ile nakisukuma kiti tu hivi kwa ajili ya zoezi lile lakumridhisha

Faraythati mara mlango ukafunguliwa na sikumjua aliyeingia lakini nilikuja kumjua baada ya kujikuta hospitali, kumbe nilikuwa nimezimia.
Nilikasirika sana baada ya kukatishwa zoezi lile la kifo na rafiki yangu Maganga aliyenipenda sana kiasi cha kutotaka kuuonma uhai wangu ukichomoka hivihivi. Nasaha pamoja naushauri wa kina kutoka kwake ndivyo vilivyonijenga na kuniahidi kuwa lazma niwe na Faraythati kwa hali yoyote ile.

Kama utani niishangaa baada ya mrembo yule kunifuata na kunipa pole kisha mwenyewe tu akasema kuwa amekubali kuwa na mimi kwakuwa amegundua kuwa ninampenda sana na huo ndio mwanzo wa mimi kujihusisha kwenye mapenzi. Nilikaa kwenye penzi lile tamu ambalo halikuathiri masomo yetu. Tulipendana sana zaidi hata ya mapenzi yalivyo. Kila alichokuwa nacho niliona kuwa ndio uzuri wa kike huku moyo wangu ukiendelea sana kumshukuru rafiki yangu wapekee ambae bila yeye bila shaka nisingempata mrembo yule mzuri badaa yake ningekuwa kuzimu huku nikiendelea kutumikia kosa lile lajinai katika makosa makubwa yaliyomo ndani ya vitabu vya dini, kujiua. Tulimaliza masomo yetu ya A-level hatimae wote kwa pamoja tulichaguliwa kujiunga katika chuo kimoja. Naam, kila mtu alikuwa akisoma alichopenda. Faraythati alienda kusomea Sarufi huku Maganga yeye akisomea sheria bora alivyokuwa kuliko alivyoenda kuwa. Huko muda wote alitembea na vitabu vya wanasheria wakubwa hapa duniani huku yeye maisha yake yakibadilika na kuwa mkali kwa yeyote anayeivunja.

Alikuwa hata hatakikniona nimevaa suruali na tishheti, muda wote yeye alitaka anikute nimevaa suti huku akinambia kuwa mtu mwenye heshma zake huwa hava kihuni. Kwakiasi kikubwa nilimshukuru sana kwani yeye ndie aliye nisihi toka A-level kwamba natakiwa nisome ninachokipenda nasi kumuiga mtu, japo niliikatia tamaa fani yangu kutokana na kero nilizokumbana nazo eti nasoma masomo ya wasichana maana mie nilikuwa nikisoma Historia, kiswahili pamoja na kiingereza nilitaka kusomea linguistics kama alivyo fanya mpenzi wangu lakini Maganga alinikarisha na kunisihi kwamba sitakiwi kuishi maisha ya kuiga hivyo nikafanya nilichopendam huko ndiko nilipoigundua hazina ya kipaji kingine cha ziada ambacho nilikuwa nacho lakini sikuwa nikikifahamu. Udodosaji, hicho ni kipaji kilichonipelekea ni pate mafanikio sana pindi nilipokuwa nikisoma, nilikuwa nikifanya vizuri sana katika masomo yangu hayo na hata tulipochukuliwa na kupelekwa katika magazeti mbalimbali kuandika habari tulizo kusanya wakurugenzi wa makampuni walipenda sana habari zangu kwani nilikuwa nikifuatilia tukio basi nitalielezea kiundani zaidi ya tukio lenyewe lilivyo.
Nilijituma sana kila siku nilikuwa nikifatilia habari mbalimbali ambazo hata hazikunihusu.

Mimi kamera pamoja na kalamu tu. Rafki yangu alinipongeza sana kwa juhudi zile huku akiniambia kuwa nifanye zaidi ya vile, nilipiga picha sehemu wanapo fanya biashara haramu kisha nikaandika habari, nilifanya yote hayo huku bado nikiwa nasoma, hata nilipomaliza Masomo yangu kwa kupatiwa shahada, nilipata kazi katika moja kati ya makampuni makubwa ya magazet i ambayo yalitoa oda kwa wanafunzi watano watakao fanya vizuri basi wangeajiriwa bure.

Huko nika fanya kazi kwa bidii huku rafiki yangu yeye akipata kaz i serikalini, naam, alitimiza ndoto zake za uana sheria. Mpenzi wangu yeye alipata kazi katika moja ya shule za serikali na sitoisahau ile siku aliyoniaga. Tuliagana vizuri sana nikamsindikiza hadi kwenye gari tena nikiwa mimi na mwana sheria Maganga. Tulivyoachana, baada ya muda kidogo nilipewa taarifa juu ya ufatiliaji wa ajali iliyojitokeza punde tu. Kwakuwa ile ndio kazi yangu basi nilipanda gari na kuelekea huko ambako kunasadikika kutokea ajali huku kwa muda huo nikiwa tayari nimeachana na rafiki yangu muda si mwingi.

Haikuwa mbali sana mpaka kufika maeneo ya karibu kabisa na morogoro, nilishuhudia gari lililokua lime lala chali, mataili juu,juu.
Niliijua gari ile nikakumbuka kuwa mimi ndie niliyemlipia mpenzi wangu apande kwenye gari ile. Hapo sikuyaamini macho yangu baada ya kusogea vyema eneo lile la tukio na kukuta miili ya watu ikitolewa nje na raia wema. Ingawa niliagizwa kupiga picha lakini sikuweza kupiga kutokana na hali niliyokuwa nayo kwa muda ule. Kila mwili uliyotoka ndani ya gari lile ulikuwa hautamaniki hata kidogo. Nilianza kumsaka mpenzi wangu ambae muda simrefu ningeweza kufunga nae pingu za maisha mbele ya shekh kwani nilimuahidi nipo radhi kuwa muislamu kwa ajili yake.

Mwili ulinisisimka baada ya kuziona nguo nilizozinunua mimi kwa pesa yangu zikiwa zimetapa kaa damu huku aliyezivaa akiwa amelazwa kwenye ile miili ambayo haikuhitaji utafti wa kitaalamu ilikugundua kuwa haikuwa ikipumua tena. Nililia sana baada ya kumuangalia vizuri usoni mwake na kuviona vile vioo vilivyokuwa vimeujaa usowake na kumpatia sura ya kuogofya zaidi. Mtoto wa kiume nilishindwa kuyazuia machozi yangu.

Kamera ilinitoka mkononi na kuanguka chini huku mimi nikijitembeza taratibu kuufuata ule mwili wa Faraythati uliyokuwa ukitisha sana. Sikuweza kuuogopa hata kidogo kwakuwa niliupenda sana, nilipoufikia niliupigia magoti na kuanza kutka kilio cha maneno. Nitalia hadi lini? Nitaumia hadi lini? Hayo ni baadhi ya maswali niliyojiuliza huku nikiutafakari ushauri wa rafiki yangu Maganga ambae aliishi kunishauri na kuyafuta machozi yangu kila alipo yaona yakinitoka.
Wazo jingine ambalo lilikuwa halina msalie mtume liliweza kuniijia moja kwa moja na nikawaza kuwa kuliko kuteseka na kulia kila siku ni bora nimfuate mpenzi wangu kule alipoelekea kwani sikuona umuhimu wa mimi kuishi bila yeye. Kwa miguu yangu nilienda dukani kununua sumu ya panya na kwenda kuinywa ilinipoteze maisha yangu.

Nilifanikisha kuinywa na kuanza kusikia maumivu ya tumbo ambayo yalinipelekea kujitupa huku na kule bila kujali ninapojitupia ni salama au la. Kwa mar a nyingine tena, rafiki yangu alinikuta chumbani kwangu nikiwa nimelalachini huku povu likinitoka. Rafiki yangu Maganga alishughulika mwenyewe kuuokoa uhai wangu kwa kunipeleka moja kwa moja hadi hospitali ya Muhimbili ambayo ilikuwa karibu zaidi na nilipokuwa nikiishi.

Nilipatiwa tiba huko, mpaka hapo nilipoweza kufumbua macho yangu tena. Nilipoyafungua macho ndipo nilipo kutana na mwwanamke mrembo ambae alikuwa kama pacha wa yule alyeondoka duniani. Kwa haraka haraka nilihisi labda niko peponi kufuatia kifo nilichojipatia lakini nilipatwa na mshangao zaidi baada ya kumuona
Maganga akiwa amejiinamia huku akimuomba Mungu mimi niamke. Naam, ni Daktari yule wakike ambae alikuwa wa kwanza kugundua kuwa nilikuwa tayari nimesha ya fumbua macho yangu. nae kwa sauti ya upole akamwambia Maganga anitazame. Ile sauti ya daktari yule ilinifanya nijihisi mjinga kwa kutaka kujiua kwani ningekosa bahati ya kumuona msichana mrembo kama yule.

Niliuhisi uzuri wa daktari yule ukiukuna moyo wangu palepale nikajisikia kupona ghafla, daktari pamoja na Maganga wote kwa pamoja walifurahi sana lakini mimi furaha yangu haikuwa kupona bali kumuangalia daktari yule aliyewafanana kabisa wale wanawake wa peponi. Alinipa ushauri na kunisihi ni punguze sana mawazo baada ya kuruhusiwa sikukubali kabisa niondoke bila namba zake za simu. Nilipofika nyumbani huku nikijutia maamuzi ya kijinga ambayo huwa nina yapata. Nilitumia muda wangu mwingi sana kujishauri huku ule uliyobaki nikifanya kazi kivivu. Kwa mara yakwanza nilianza kusoma vitabu vingi na hiyo ni baada ya kuzidisha mazoea sana na daktari yule. Naam, mazoea furaha ilizaa amani kati ya mimi na yeye kisha amani ikazaa pendo ladhati ambalo lilitokea lenyewe tu. Hapo nilipata ushauri mzuri sana uliyonipelekea nikabadilika kuliko nilivyokuwa hapo awali sasa nikawa nipo bize na kazi tu na kiukweli siku muogopa yeyote.

Niliandika makala mbalimbali za ubepari huku zikilenga zaidi kuwakataa wawekezaji wanje, pia sikuwa mnafki katika kuikosoa serikali nadhani hata wewe ni shahidi na swala hilo lilinifanya zaidi nipendwe na wananchi wanao vuja jasho. Kama vitisho nilikutana navyo vingi sana kutoka kwa baadhi ya wale ambao wamepewa nyadhifa mbalimbali katika nchi hii. Makala zangu zilikuwa zikiwagusa sana na hata kupelekea kunifunga kwa mwaka mzima jela kwakunisingizia kuwa nilikuwa na hamasisha ugaidi. Kwa kipindi hicho na kumbuka ndio kwanza nilikuwa nimeoa n mke wangu alikuwa na ujauzito. Mke wangu alipata tabu sana kukaa mbali namimi lakini nikiwa hukohuko niliweza kumuandikia mke wangu makala moja niliyoipa jina la 'I will back' makala ile ilikuwa ni kama fumbo lakini iliongelea vilivyo maswala ya nchi hii, niliuongelea utumbili na unyani huku nikikusanya baadhi ya ushahidi japo kwa kifupi wa namna watu wanavyo hangaika kummfunga paka kengele. Si hiyo tu, vilevile niliandika makala kama, Yupi ananifaa?,
Sijisemei mimi namsemea mwanangu nakadhalika. Makala zile japo zilikuwa katika kalamu tena ya mkaa lakini mke wangu alizitunza na niliporejea kutoka jela nilihakikisha nazituma kwenye magazeti.

Nilifuhi na mwanangu pamoja na familia yangu, nikiwa kama muandishi niliweza kubaini kumbe rafiki yamgu Maganga alikuwa akishirikiana na wauaji pamoja na wafanya biashara haramu katika utetezi wake aliwatetea mahakamani watu wale. Nilipogundua hilo ilibidi ni muonye lakini katu hakukubali onyo langu na hata nilipomwambia kuw nitamshitaki alinicheka na kunisihi kuwa nisijifanye najua kuandika kila jambo kwani mambo mengine yanaweza kunigharimu. Kwakuwa sikupenda haki iende hivi hivi ndipo nilipoanza kumfuatilia na kumuandika badala yake nilizuiwa hata kutuma habari nilizoziandika kuhusu yeye, nilipouliza sababu sikupewa.
 
KICHAAA

ZUBERY R. MAVUGO.

[MR...FEELLING]

NO: 35

ENDELEA.

Sijisemei mimi namsemea mwanangu nakadhalika. Makala zile japo zilikuwa katika kalamu tena ya mkaa lakini mke wangu alizitunza na niliporejea kutoka jela nilihakikisha nazituma kwenye magazeti.

Nilifuhi na mwanangu pamoja na familia yangu, nikiwa kama muandishi niliweza kubaini kumbe rafiki yamgu Maganga alikuwa akishirikiana na wauaji pamoja na wafanya biashara haramu katika utetezi wake aliwatetea mahakamani watu wale. Nilipogundua hilo ilibidi ni muonye lakini katu hakukubali onyo langu na hata nilipomwambia kuw nitamshitaki alinicheka na kunisihi kuwa nisijifanye najua kuandika kila jambo kwani mambo mengine yanaweza kunigharimu. Kwakuwa sikupenda haki iende hivi hivi ndipo nilipoanza kumfuatilia na kumuandika badala yake nilizuiwa hata kutuma habari nilizoziandika kuhusu yeye, nilipouliza sababu sikupewa. Nilipojifanya king'ang'anizi nilifukuzwa kazi kwa kosa lakujitia kiherehere, nilikaa bila kazi na Maganga aliendelea kufanya ujinga wake, kwakuwa nilikuwa muandishi ambae kwa wakati huo jamii ilinihitaji sana na baadhi ya makampuni walikuwa wakisoma kazi zangu.

Ndipo nilipoletewa mkataba wa kuandika makala mbalimbali huko ndiko nilipojaribu kufichua uovu wa rafiki yangu yule, lakini nako pia nilitiomuliwa utadhani nilikuwa mkosaji kumbe mfumbuaji macho wa wananchi. Niliamua kwenda polisi huko nako sikupata msaada zaidi ya mimi mwenyewe kuteswa kwa kuwekwa ndani. Nilikuwa nikiifahamu sheria vizuri hivyo niliona jambo lile lakuwekwa ndani bila kosa ni uonevu wa maaskali, nilipotoka kwa dhamana nikapitiliza mahakamani na kwenda kumshtaki rafiki yangu Maganga ambae alikuwa akipokea rushwa kutoka kwa watu haramu na kuwatetea.

Kuna wengi walikamatwa na madawa ya kulevya lakini yeye aliwatetea kupitia hongo aliyopatiwa, alipokea rushwa hata kwa wauaji kitu ambacho kilinifanya nimuone mnyama. Nilipoenda mahakamani nilionekana kuwa sina ushahidi wa kutosha ingawa nilikuwa hadi na uthibitisho wa picha mbalimbali nilizompiga kipindi akipokea rushwa. Zaidi nilishauriwa kuwa niachane na mambo hayo kwani kazi yangu nikupiga picha pindi raisi au kiongozi wa serikali anapo toa ahadi kwa wananchi lakini sikupiga picha mambo kama yale. Pia waliniambia kuwa nisipede kujiingiza katika mambo yasiyo nifaa kwani itakuja kupelekea nijiingize matatizoni, mimi muandishi wa habari hivyo sina mamlaka ya kuingilia masuala ya polisi na mahakama.

Hapo niliamini kweli Maganga alikuwa akishirikiana na watu wenye mtandao mkubwa sana. Nilijisemea kuwa sikati tamaa mpaka nimuweke ndani, hapo nilimfuatilia na kumpiga picha tena akiwa anawasaidia walanguzi wa madawa ya kulevya, pia nika mpiga picha kipindi anapokea rushwa kisha nikajisemea kuwa swala hili lazma niliweke wazi kwa wananchi iliwatambue kabisa mambo yaliyokuwa yakifanywa na wale ambao wao wamewapa kipaumbele na kuaamini kuwa wanaweza kuwa saidia. Niliiweka habari ile gazetini na ikasambaa mtaani, watu wakajionea lakini chakushangaza baada ya siku mbili nilishangaa chapisho lililofuata kutoka gazeti hilohilo nililotumia likiwa lime kanusha habari yangu huku likinichafua vilivyo kwakusema kuwa huo nimpango wngu wa kumuharibia sifa mwanasheria mchapa kazi. Mchana wa siku hiyo mke wangu aliniita nakuniambia kuwa ni bora nitafute kazi nyingine kuliko hiyo ya uandishi kwani alihisi inapoenda kunipeleka ni kubaya sana.

''Hebu angalia, mtoto wetu ndio kwanza hata miaka kumi na oja hajatimiza istoshe mie mkeo ni mjamzito kwasasa we unadhani kwa kazi hiyo ya kutengeneza mabifu na wenye pesa tunaweza kufika?, najua unapenda haki na niwajibu wako kufichua maovu yatendwayo na watu pasina kujali. Lakini unadhani kwa hali hii tutafika?'' Alongea mengi sana mke wangu siku hiyo huku akinionesha gazeti lile lililotumika kunichafua na kumsafisha maganga.

Nilichukuwa muda wangu kufikiria ndipo nilipokumbuka kuwa ni heri ningesoma Linguistics niliyo shauriwa na marehemu Faraythati kuliko fani ile ya uandishi wa habari ambayo nilikazaniwa na Maganga niisome. Niliona, Faraythat alikuwa ana macho ya kuona mbali kwani kazi ile ndio iliyopelekea mimmi na rafiki yangu kukosana.

Ningekuwa mwalimu, ningewafundisha wanafunzi lugha na wakaelewa kisha nikachukuwa mshahara na nisikosane na Maganga zaidi tungesaidiana na kila mmoja angekuwa na maisha yake kuliko muda huo ambao nilikuwa nikiishi kwa bifu. Naam, niliona kazi ya uandishi hainifai, ndipo usiku wa siku ile nikiwa na mkewangu huku nikimuuliza juu ya biashara ambayo angependa nifanye kwani nilikuwa nina pesa katika akaunti yangu ambayo ingeweza nisaidia kufanya mambo yangu vizui tu. Mpka kwenye majira ya saa saba usiku tayari tulikuwa tumepata jibu, usiku huohuo ndipo walipoingia watu ambao mwanzo sikuwafahamu, watuwale walinipiga na kuniulia mwanangu pamoja na mfanyakazi wangu huku nikishuhudia kwa macho yangu mawili wakimbaka mke wangu.

Sikuwa na lakufanya zaidi ya kulia tu kwa uchun gu, mke wangu alianguka chini nami nikajua moja kwa moja atakuwa amepoteza maisha, watu wale walinmifuata pale na ndepo walipo nidokeza kuwa kazi ile walitumwa na Maganga kwani alishanionya sana lakini siku taka kusikia hivyo siku ile nio ilikuwa siku yangu ya kupoteza maisha iliniende nikafanye kazi yangu ya uandishi huko ahera. Mmoja wao alinyanyua rungu na kunipiga nalo. Na hapo ndipo mwanzo wa mimi kusahau kila kitu.

Nakumbuka nilitoka ubungo hadi hapa Mwanza kwa ajili ya kuja kutafuta maisha yangu. Sikuwa na kumbuka kama niliacha mke huko wala chochote lakini nilikuwa nina picha moja tu ambayo ndio ilikuwa ikinikumbusha mambo fulani niliyowahi kuyafanya maishani mwangu lakini kiukweli sikuwa nikiweza kuyaelezea kwani yalikuwa yakija na kupotea tu. Nilipoanza kuishi maisha yangu nililichagua jalala na kuhisi huko ndiko kunaweza kunisaidia mimi nisiyekuwa na makazi ya kuishi na hivyo ndivyo ilivyokuwa hadi leo hii nadhani ndio nimejitambua kwani sikuwanikijielewa kabisa kwa lolote lile.
*****

Mavugo alimaliza kuhadithia kumbukumbu ile hospitali na kuwaacha wote wakiwa na majonzi mengi, yote kwa yote walifurahi na kumshukuru Mungu kwa kuwapa ambacho hawakuwahi kukiomba.

Bila dokta Endrew kumuta Mavugo , na bila Mwambe kumuhitaji Neema, pia bila Mama Musa kuugua basi watu wale ilikuwa ni vigumu sana kukutana. Hakika Mungu hashindwi na chochote, kiwe kigumu ama chepesi. Mungu, hufanya vitu vya kushangaza sana ambavyo huleta mazingatio ya hali ya juu sana. Anaweza kukupa mtihani iliatoe fundisho au onyo kwa binadamu ambao mioyo yao imesha kata tamaa na kuamini kuwa Mungu hayupo. Ewe ndugu yangu, kaka, dada uliye hospitali ukilia kwa kukosa matibabu usimlaumu Mungu kwa kudhani kuwa hayupo na wewe au amekutenga sana. Mungu hufanya yote hayo kwa sababu zake, kama aliweza kumuokoa Mavugo ambae hakuwa na anachokikumbuka katika maisha yake basi hashindwi kukuokoa wewe ambae una ikumbuka familia yako kwa kuhangaika na kuhakikisha nyumbani hawashindi njaa. Jina la Mungu lihimidiwe.

Naam, wote kwa pamoja walitoka na kwenda hadi nyumbani kwa Devi hata walipofika huko, walipanga jinsi ya kuwakamata wale wote waliyosababisha Mavugo kuwa katika hali ile. Hilo halikuwa Tatizo kwa Waziri Mwambe ambae alifanya kazi hiyo nndani ya siku tatu tu na wote waliyompelekea Mavugo, kupoteza mwanae pamoja na kunajisiwa kwa mke wake yule ambae ilikuwa bado kidogo tu ampoteze mwanae aliyekuwa tumboni.

Maganga pamoja na wapuuzi wenzake walipatiwa hukumu ya kunyongwa hadi kufa kwani hawakufaa kabisa kuonekana katika uso wa dunia hii. miasha kati ya Mavugo na mkewe yaliendelea vizuri kama yalivyokuwa zamani huku akiwa chini ya usimamizi wa waziri Mwambe.

MWEZI MMOJA BAADAE.

'' Musa kwasasa sina hata chembe ya hisia nawewe. Kwa mambo yote yaliyotokea nimejikuta nikikuona kuwa wewe ni zaidi ya kaka kwa upande wangu tafadhali niruhusu nikuite Kaka na mapenzi yetu yasibaki hata kwa historia kwani mimi nawewe ni zaidi ya ndugu sasa.'' Aliongea Kisura huku akiwa amekaa kwenye moja kati ya makochi makubwa yanayo patikana sebuleni mwa kina Musa.

'' Usijali hata mimi nakuchukulia kama Dada yangu kufuatia ukaribu wa wazazi wetu. Tafadhali naomba unisamehe kwa kukufanya mpenzi ilhali wewe ni dada yangu. Labda zaidi tumshukuru Muumba kwani hakuruhusu tufanye chochote ambacho kinge tupelekea kujutia katika maisha yetu. Nakupenda sana dada yangu.'' Alijibu Musa, pia hakusita kumueleza kisura kuwa yule Neema ndio mpenzi wake wa halali. Wote kwa pamoja walifurahi sana na kutaniana, huku kwa wakati ule Neema akiwa Dar-es-salaam huko kwa waziri ambako ndiko alipokuwa akilelewa kwa muda huo.
............................ .................................

'' Mavugo, hakika wewe ni mwanamume wa kweli. Nimejaribu kupitia historia yako ya maisha na misimamo yako mbalimbali nimeamini hilo. Kumbe wewe hukuwa kichaa bali mwalimu uliye letwa na Mungu kwa ajili ya kuja kunifundisha mimi Endrew kuwa kusoma sana si kujua kila kitu. Umenifanya niuone uwezo wa Mungu mbele ya macho yangu, nashukuru sana kwa hilo. Ama kukutana kwetu kulikuwa na maana kubwa sana.'' Aliongea Docta Endrew pindi alipokuwa ametembelewa na Mavugo pamoja na mke wake MRS. Mavugo ama Mama Musa kama alivyojulikana. Mama yule ni daktari mkubwa sana lakini aliamua kuiacha shughuli ile kufuatia m,atatizo yaliyompata katika maisha yake. Aliirejesha furaha yake baada ya kuungana na familia yake tena kwa namna ya tofauti zaidi.

''Dokta Endrew. Nadhani unakumbuka kuwa niliwahi kukuambia hakuna binadamu asiye kachaa. Utakuwa umeamini kupitia maajabu haya ambayo kiukweli Mungu ameyatenda mahala pake. Waingereza huwa wanatabia ya kufanya uchunguzi huku wakijipatia ma vyeo ya sayansi lakini kamwe muafrika hana tabia hiyo na ndio maana huwa na imani kuwa kila kilichopo ni kwa ajili ya uthibitisho wa kuwa Mungu yupo. Uwepo wa mashariki na magharibi ndio chanzo cha kukuaminisha wewe kuwa jua huzama na kuchmoza, ilhali wana sayansi husema kuwa juwa huwa palepale isipokuwa dunia ndio huzunguka. Hakika uongo umekuwa ukweli, macho ya binadamu yameparazwa na misemo ya kisasa, huku masikio yao yakisikiliza kile kinachoitwa utandawazi na kusahau kuwa upo tangu dunia kuwekwa katika hii anga.

Kama wewe huamini, hebu nenda katizame milima jinsi ilivyo simamihwa utabaini kuwa hakuna isubiricho bali ni kiama. Ingetosha kabisa mbingu ikaoza na kuanguka kama ifanyavyo miti lakini Mungi kutimiza ubora wa utofautishaji ameipa miti majani na kuni nyima mimi binadamu yote hayo ni kutufanya tuamini kuwa hana ashindwalo. Kabla sijanyanyua mguu wangu na kurejea kulitumikia kampuni langu la magazeti ambalo nimepatiwa na ndugu yangu bwana Mwambe nataka nikupe kauli yangu ya hitma isemayo kuwa;

Binadamu yeyote ana maana yake kuwepo katika hii dunia na anamsaada mkubwa kwa binadamu mwenzake iwe kifikra au kifedha. Hivyo usimdharau yatima kwa kupungkiwa wazazi, usimdharau, kichaa kwa kupungukiwa ufikiri, usimkebehi masikini kwa kukosa chakula, usimuogope tajili kwa kuwa na mali. Hakuna mbora kati ya binadanu mwenzake zaidi ya mchaMungu pekee.'' Aliongea Mavugo kisha akachukuwana na mkewe hadi kwenye gali lao na baada ya kulipanda moja kwa moja wakaelekea nyumbani kwao.

Maisha ya Mavugo yakawa mazuri huku akipendwa na kuheshimiwa na wananchi wote wachukia uovu. Magazeti yake yaliuzika sana nchini kutokana na ubora wa waandishi aliyo waajili wakiwemo waandishi wa Hadithi za masimulizi ambao wao aliwalipa kwa kiwango cha juu sana kwani wao ndio walikuwa wakifanya magazeti yake ya uzike na kwa kasi sana. Wote kwa pamoja wakaishi maisha ya raha mustarehe huku shida wakiisikia na kuitatua kwa baadhi ya watu. Alifungua kituo cha kulelea watoto yatima na kujitolea magari katika hospitali mbalimbali za serikali hapa nchini. Na hivyo ndivyo alivyoendelea kuishi katika maisha yake yote.

MWISHO.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom