Madame S
JF-Expert Member
- Mar 4, 2015
- 17,172
- 34,277
RIWAYA: KICHAA.
Na: ZUBER R. MAVUGO.
N0. 01.
Njaa, iliendelea kulisumbua tumbo lake na kumpelekea kuanza kujipitisha maeneo ya ma'ntilie, huku akiamini kuwa shibe yake ipo mikononi mwao.
"mmh, mmh, mmh, puu. Lalalalala. Toka! Hebu tutolee kichefu chefu hapa," Ni baada ya mtu huyo kufika kwenye moja kati ya migahawa ipatikanayo maeneo ya Igoma ndani ya jiji la Mwanza, sauti moja ya mwanamama muuza mgahawa ndio iliyatoa maneno hayo yenye kuonesha kukereka kwa uwepo wa mtu fulani maeneo yale.
"Bado hunisikii. Eti, eee," Alibwata tena, huku mate yake yakishindwa kujizuia kubakia mdomoni na kujikuta yaki mwaga cheche zilizokuwa zikimfuata kijana ambae maneno hayo yalimuhusu yeye. Kijana yule ni kama hakuwa mwenye kusikia maneno yale, si.. Kwamba hana masikio. Laa! Hasha, bali pindi yalipomfikia yalipita sikio moja na kuelekea jingine.
"We.. Kichaa, unajifanya hausikii, si,ndio? Mnatoka huko makwenu mmefanya uchawi au kuiba mmelogwa halafu mnakuja mjini kuwa kero kwetu. Hebu toka, kabla sijakufanyia kitu kibaya." Mama yule aliendelea kumfukuza yule kijana kwa maneno lakini ndio kwanza kijana yule aliendelea kutabasamu huku meno yake machafu yakipata ruksa ya kuonekana maeneo yale.
"Anhaa! Kumbe unanicheka eti ee! Kwahiyo hapa nafanya upuuzi. Ngoja nikuoneshe," Aliongea mama yule huku miko yake akiwa ameiweka kwenye kiuno chake ambacho amekipiga kanga nzuri yenye maandishi ya bezo.
"Asia?," Aliita mama yule na baada ya yule muitwaji kuitika. Akasema, "Niletee hilo sufuria lenye maji ya moto hapa. Nataka ni muoneshe huyu mbwa," Asia, alitii amri na kuleta sufuria hilo. Kwa kuwa lilikuwa la moto, alishindwa kulibeba bila kuweka kitu cha kuzuia hali ile. Aliamua kuchana boksi na kulitengeneza vizuri kisha akalishikamanisha na sufuria lile, baada ya hapo akaliinua na kumpelekea Mama yule.
"Mwanaharamu mkubwa wewe. Unataka kuleta gundu mida hii.. Mbwa wewe." Alitamka maneno yale, kisha akayasindikiza maneno yake na maji ya moto yaliyompata vilivyo kijana yule.
Masikini, kijana yule, aliangua kilio kama cha mbwa mwizi. Sasa alishindwa kustahimili maumivu aliyonayo na kujikuta akikimbia hovyo mfano wa mbwa aliepigwa jiwe la kichwa.
"Hicho ndicho chakula chako. Mbwa mkubwa we... Na bado, allaaa!! Ukichaa peleka milembe, mjini kila mtu yupo timamu bwana." Maneno yale ya bila huruma ya ubinadamu yaliendelea kutoka mdomoni kwa mama yule bila hata haya. Aliendelea kujisifu kwa kuhisi amemkomesha binadamu mwenzake na kusema.
"Hatorudia tena. Wewe mbwa mwenyewe ukimwagia maji kiasi hicho, harudi tena. Ije yeye binadamu? Na akirudi basi atakuwa na roho ya paka. Halo, halo. Analeta ujiwe mbele ya nyundo. He,he,he,he. Ndo.. Basi tena." Baada ya kutamba kwa maneno yake pamoja na vidole vyake alivyovichezesha huku mkono mmoja akiwa kauweka kiunoni. Alirudi na sufuria lake ndani ya mgahawa huo, kisha akateka maji ya mengine na kuyachemsha.
"Mamaaa! Mammaaa! Nakufa! Nakufaaa. Yalaaaa!" Kijana yule alipiga kelele za uchungu wa maumivu huku akiendelea kukimbia hovyo bila kujielewa. Ingawa alikuwa na minywele mingi iliyochakaa, ngozi yenye ukurutu uliokomaa nakuwa kama machacha, ngozi hiyo ilifunikwa na madaso ambayo zamani yalikuwa nguo. Madaso hayo, yalichanika kila mahali, kwa harakaharaka usingeshindwa kumuita kichaa mtu yule, maana hata usowake, ulipambwa na poda ya jalala aina ya majivu, pamoja na mafuta ya oil.
Naam, alikuwa ni kichaa. Nadhani hata mama yule aliempa adhabu hiyo ya maji ya moto. Alimpa kwa sababu alijua kijana yule ni kichaa. Akashtaki wapi wakati Mahakama yake ni jalala? Akamlilie nani wakati wazazi wake ni mbwa wapatikanao mtaani? Nani wakumsaidia kijana huyo ambae hata hatathamani.
Ni njaa pekee ndiyo iliyompelekea kufanyiwa hivyo. Wakati wewe ukisikia njaa unakimbia mapema nyumbani kwako na kupata chakula, au unaenda mgahawani. Kumbe kuna wengine wanapata adhabu ya kuunguzwa na kutengenezewa majiraha kisa njaa zao.
Masikini, kijana yule aliendelea kukimbia huku maji yale yakiwa yameachia hatamu ya umoto na kusababisha maumivu yasiyo mithilika. Hapohapo jiraha kubwa lililoambatana na uvimbe kutokana na kuunguzwa kwa maji lilijijenga kuanzia, mkono wakushoto, ubavuni hadi mguuni. Aliendelea kukimbia hivyohivyo huku akiita neno 'MAMAA' na wala mama yake asije.
Wengi waliomuöna barabarani walimzomea wengine wa kimcheka na kumthihaki, huku wachache wakimtumia kwenye mada zao. Hakuna hata mmoja aliemsaidia kichaa yule japokuwa alikuwa akiomba msaada.
Alikimbia na kwenda kujitupa jalalani. Hakuwa na mahala pengine pakujisitili zaidi ya jalalani. Huko akakutana na watoto ambao nao walivalia madaso kama yeye huku wakiokota vyuma chakavu, pamoja na kina mama waliochafuka kwa kutafuta chakula ambacho hutupwa jalalani hapo. Watu wale masikini ndio walikuwa msaada wake, walimfuata na kumbeba, ingawa kila walipomvuta nguo, waliishia kubakiwa na kipande cha nguo hiyo kutokana na kuisha kwake. Lakini hilo halikuwafanya waache kumbeba na kumsogeza pembezoni mwa jalala lile.
Walipomsogeza pembeni, mapema tu wakaanza kumpatia huduma ya kwanza ya kishamba. Bora wangekuwa na asali ilikumpaka huenda ingesaidia, hawakuwa na dawa yeyote zaidi ya mchanga uliopatikana maeneo yale ya jalala. Walimpakaa mchanga ule wenye chembechembe za uchafu kisha wakamuhitaji apumzike iliasiendelee kuyahisi zaidi maumivu.
"Mpumzishe kwa lazima." Aliongea mama mmoja aliekuwa amesimama huku akiendelea kukiadhibu kichwa chake kwa kukikuta kutokana na muwasho aliokuwa akiupata;muwasho wa mmba pamoja na chawa katili.
"Sawa, maana inabidi apumzike tu." Alijibu mama mwingine ambae yeye alikuwa bize na kufukuza inzi maeneo ya kidonda. Kisha mama yule akaiacha kazi ile kwa nukta, na kupeleka mkono wake hadi kwa maeneo ya shingoni mwa kichaa yule ambae sasa alikuwa akipiga mikono yake chini pamoja na paji lake ilikupolea maumivu kama alivyodhani. Mama yule, aliigusa gusu shingo ya kichaa yule iliyojaaliwa ukurutu mgumu, na nikama alikuwa akitafuta mshipa fulani. Hata alipoupata aliuzimisha kiustadi wa hali ya juu na palepale kichaa yule alipoteza fahamu.
Ingawa njia ile ina madhara, lakini ndio njia pekee iliyopatikana kwao. Hawakuweza kumpeleka mgonjwa hosipitali akachomwe sindano ya ganzi iliasihisi uchungu au sindano ya usingizi kutokana na kutokuwa na pesa. Walilitambua hilo na walijua wazi hata kama wangempeleka hospitali, asingepata msaada wa aina yoyote ile zaidi ya kuangaliwa kwenye benchi kwa kebehi kama inzi mla mavi. Kwao, waliona njia pekee ya kutuliza maumivu ni kumfanya mgonjwa azimie kwa muda. Kumbe wakati wewe unapopata jiraha na kupigwa ganzi, au sindano ya usingizi. Kuna wengine ambao hata hiyo sindano hawaipati badala yake wanapata nyenzo za hatari.
"...we mama, leta hiyo siso kabla sijakuharibia hapa." Ni sauti ya ukali iliyotoka kinywani mwa mtoto mwenye umri wa miaka kumi na nne, maeneo ya jalala hilo. Sauti hiyo isiyojali utofauti wa miaka iliendelea kukoroma. Mama alieambiwa atoe chuma chakavu, alionesha kama kutosikia sauti ile ya dharau tena ukizingatia mtoaji wa sauti ile ni mtoto ambae anauwezo mkubwa sana wa kumzaa. Alifikiria endapo atampa chuma kile chakavu basi ataikosa pesa il-hali nae anashida chungu nzima, hivyo aliona uamuzi wa yeye kuwa nunda ndio pekee utamsaidia mbele ya mtoto yule.
"..we maza nunda sio? Nakwambia leta hapa hiyo siso." Aliendelea kutoa amri mtoto yule utadhani anaongea na mtoto mwenzake kumbe ni mama mzima. Mtoto yule alikuwa ana ngozi chafu iliyojaa ukurutu;ngozi ambayo hakuivika shati kutokana na ukosekanaji wa mashati juu ya hali duni aliyonayo. Huku chini akiwa amevaa kaptula iliyotoboka na kupelekea makalio yake yaliyopauka na kupata sugu kutokana na kukaliwa bila heshima yaonekane vilivyo pasina uficho.
"We... Mtoto wa mbwa, hebu kuwa na adabu pamoja na heshma. Wakubwa husalimiwa mjinga wewe, na sio kutolewa amri za siso tu." Aliongea mama yule kauli iliyohifadhi hasira za wazi juu ya kuchukia amri za mtoto yule mdogo ambae kwa kumuangalia tu. Anashindwa hata kumfananisha na watoto wake kutokana na umri mdogo alionao.
"Afu.. We, maza takuharibia sasa hivi. We sema kama hutaki kunipa hiyo siso uone kama siichukui kwa nguvu. Heshima unaijua wewe? Kama ungekuwa na heshima ungekuja huku jalalani? Acha ujinga. Wenye heshima na adabu wapo majumbani kwao wakipikia waume zao na kuosha watoto wao. Wewe upo huku jalalani halafu unaitaji heshima, sijui adabu. Hebu lete hiyo siso, mpuuzi mkubwa."
Mtoto yule alimkwapua mama kile chuma chakavu, kwa kuwa mama yule hakukubaliana na ile hali ya kunyakuliwa kirahisi chuma ambacho angekiuza na kupata pesa. Ndipo alipoamua kumvaa mtoto yule na kumng'ata vilivyo maeneo ya tumboni kwa kutumia meno yake yasioujua mswaki badala yake yanakijua chakula chajalala. Chakula ambacho kina bakteria waliojificha na wanaoonekana bila hata hadubini.
"Unaning'ata. Ayaah! Niachie mbwa wewe." Alibwata mtoto yule baada ya meno ya mama kuzama vilivyo kwenye ngozi yatumbo lake. Mama yule alisikia kilio cha mtoto yule, lakini hakini hakuhtaji kumuachia mpaka hapo atakapo hakikisha karejeshewa chuma chake iliakauze na kupata pesa.
Hapo mtoto yule akajihami kwa kumpiga mama yule na kile chuma kichwani. Kitendo kile kilimpelekea yule mama kuanguka chini huku damu nyingi zikimtoka na palepale alipoteza maisha.
Hakuna aliebaki maeneo ya jalala lile. Si, wakinamama waliokuwa wakimsaidia kichaa pembezoni mwa jalala, wala machokoraa waliokuwa wakijitafutia riziki. Wote walikimbia ilikuepuka kubambikiziwa kesi na maafande. Hata yule mtoto nae alitimka. Hapo ulibaki mwili wa mama yule. Pamoja na kichaa aliekuwa pembezoni.
Masaa kadhaa yalipita, hatimae yule kichaa alizinduka, kumbe muda huo ndio maafande walikuwa wanafika kwenye eneo la tukio. Walimbeba mama yule na kumbwaga kwenye gari kisha wakamchukua yule kichaa yule na kumsukumia ndani ya gari bila kujali jeraha lake.
"Afande, huyu mjinga ndio tuna mbebesha kesi ya mauaji." Aliongea afande mmoja.
"Huyu lazma itaijibu serikali, kwanini ameua." Alipokeza afande mwingine. Kisha maafande hao wakaingia wote kwa pamoja ndani ya gari.
Yule kichaa alisikilizia maumivu maradufu ya alivyo yapata kabla, kusukumwa na maafande wale kulimpelekea yeye kutonesha jeraha lake na kuyahisi maumivu makali yasiyo na ganzi. Alipiga ukelele kila maumivu yalivyozidi kuongezeka.