Riwaya JOKA KUU ya mwandishi J S KIDOGO. huenda inapotosha ukweli kuhusu Vita ya Kagera. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Riwaya JOKA KUU ya mwandishi J S KIDOGO. huenda inapotosha ukweli kuhusu Vita ya Kagera.

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Jumakidogo, Jan 19, 2012.

 1. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #1
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ni shabiki wa kusoma riwaya, lakini nimekuwa mvivu siku hizi baada ya uandishi wa riwaya kufifia tofauti na zama za kina Willy Gamba. Juzi nimepata bahati ya kusoma riwaya inayoitwa Joka kuu Kagera mpaka Maputo ambayo nimemkuta nacho kitabu hicho rafiki yangu mmoja akikifanyia tafsiri katika lugha ya kifaransa. Japo yaliyoandikwa humo ni hadithi inayodaiwa kuwa ya kubuni ambayo kwa hakika imeandikwa kwa umahiri mkubwa na mvuto katika kuisoma. Lakini yaliyoandikwa humo huenda yakawa yanapotosha ukweli kuhusu vita ya Kagera, ni vigumu kujua siri hiyo. Ama labda mwandishi ameleta mjadala kutokana na hadithi za mapokeo kutoka upande wa pili wa shilingi. Kama hayo ni kweli, basi kazi ilikuwepo...
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kilikuwa kinasimulia nini hasa?
   
 3. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #3
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe ni mnafiki, Riwaya hiyo imewahi kuchapishwa gazetini. Haina upotoshaji wowote kwani haielezei moja kwa moja vita ya Kagera. Bali ni historia ya maisha ya askari aliyepigana vita hiyo. Hukuwa makini!
   
 4. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwandishi ni jumakidogo wa Jf?
   
 5. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #5
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Wewe kweli hamnazo, tatizo lako nimegundua kuwa ni hilo hapo juu. UVIVU wa kusoma riwaya ndiyo umekupelekea kusoma hadithi hiyo pasipo umakini. Naomba usiwapotoshe watu bila ya sababu. Mimi ndiye niliyeandika kitabu hicho. Hadithi inaitwa JOKA KUU, KAGERA MPAKA MAPUTO. Si kweli kuwa inaelezea vita yote ya Kagera. Inaelezea maisha ya askari aliyepigana vita hiyo kwa upande wake, kisha akajiunga na vikosi vya Tanzania vilivyokuwa Msumbiji baada ya kutoroka kesi ya mauaji ya askari mwenzake baada ya vita. Askari huyo anasimulia sehemu yake ya mapambano tu katika uwanja wa vita na wala siyo eneo lote la vita. Japo mazingira ni ya kweli. Lakini hadithi ni ya kubuni kama ilivyo ZAWADI YA USHINDI ya marehemu BEN R MTOBWA. Usipotoshe watu hapa, leo hii tunaweza kusema Ben Mtobwa aliandika upotoshaji kwa sababu hadithi yake ya kubuni tu?
   
 6. u

  utantambua JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2012
  Joined: Aug 1, 2011
  Messages: 1,373
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ufafanuzi wako umeeleweka
   
 7. Kombo

  Kombo JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2012
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,819
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mkuu jk hongera sana!
   
 8. Jumakidogo

  Jumakidogo R I P

  #8
  Jan 19, 2012
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 1,859
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Ahsante sana kiongozi!
   
 9. Chatumkali

  Chatumkali JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,045
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Nimeipitia yote.Ni riwaya ya kubuni.Kitu cha kubuni hakiwezi kupotosha UKWELI kwa sababu si kisa cha kweli.Jamaa amebuni kisa kinachomhusisha askari aliepigana vita ya Kagera na wala hajasimulia vita kama vita.Nadhani kilichokuchanganya ni matumizi ya meneo ya kweli ambapo vita ilipiganwa.Hakuna upotoshaji wowote pale.Jamaa ni kati ya watunzi bora waliopo kwa sasa.
   
Loading...