GITWA
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 1,489
- 1,686
- Thread starter
- #101
KAZI IENDELEE...
"Okey, nitafanya hivyo." Alisema Patrick.
"Haya kwa heri." Aliongea yule mtu wa kwenye simu na kukata.
Patrick aliendelea kukata makali ya Long John huku akiaangalia runinga na baada ya muda akawa amepitiwa na usingizi. Alikuja kushtuka majira ya saa tisa, kilichomshitua usingizini ni mlio wa simu ambao ulisikika. Aliposhtuka Mr Wanna See na mwenzie wamekaa huku wakinywa ile pombe iliyokuwa imebaki kwenye chupa. Akichukua simu na kuweka sikioni bila hata kuwasemesha akina Wanna See.
"Hallo Patrick hapa." Alisema. Baada ya kuslimiana na huyo mtu wa kwenye simu aliendelea kusikiliza kwa makini huku akikunja na kukunjua uso wake. Mara alisikika akisema; "Kwaheri tutaonana saa tatu, nitakupitia nyumbani." Alimaliza kusema hivyo akarusisha simu mahali pake na kuwageukia wenzake akina Wanna See.
"Hallo naona mmenifaidi sana nikiwa nayoyoma na usingizi" Alisema Patrick.
"Ha! Wapi rafiki yangu sisi tumefika muda mfupi tu, tulijua labda umeegesha tu." Alisema yule mwenzake na Wanna See.
"Boss kuna taarifa nimepokea hapa sasa hivi" alisema Patrick akiwa anamuangalia Wanna See.
"Inasemaje hiyo taarifa?" Wanna See aliuliza kwa shauku.
"Yule mtu tuliyekuwa tumemteka ila atuambie wapi alipo Pheady kusudi tupate ile mali aliyochukua kwa marehemu Catto, inasemekana amelazwa zahanati ya MAGAMBO. Alipelekwa usiku na wenzie wawili ambao walimfikisha akiwa hajitambui kutokana na mateso tuliyompa. Inasemekana sio mtu wa kutoka leo Wala kesho labda wenzake walazimishe kumchukua." Alimaliza maelezo Patrick.
"Kama ni hivyo huyo ngio atakayetueleza alipo Pheady, hiyo zahanati ipo sehemu gani? Je ni nzuri ya kuweza kwenda kuchukua mtu bila matatizo? Alihoji Mr Wanna See.
"Sehemu yenyewe ni nzuri sana tu hata mchana unaweza kutoa mtu kwa mkwala na ukaondoka kabla ya askari kufika." Alieleza Patrick.
"Kwa hiyo wewe unasemaje kuhusiana na mpango wa kumpata huyo mtu? Maana wewe ndie mwenyeji unayeyaelewa mazingira yalivyo. Na inatakiwa apatikane haraka kabla hajapeperuka, kumbuka wale nao ni watu wa machale yanaweza yakawacheza wakabadili mchezo wakati wowote na kutuunguzia picha." Kabla hakamaliza kuongea mlango uligongwa wakaingia vijana watano kwa pamoja na kusalimiana baadae wakakaa kwenye sofa zilizokuwa wazi pembeni.
Baada ya kuwa wamekaa Patrick aliwauliza; vipi kuna mafanikio yoyote huko?
"Hakuna, tumejitahidi kila njia lakini mpaka sasa hatujapata fununu zozote kuwahusu. Inaonekana wamejichimbia mahali na hawataki kufanya makosa yoyote yatakayowafanya waonekane. Alafu mjini kulikuwa na vurugu ambazo zimetupotezea wakati kidogo. Machinga wa mtaa wa Makoroboi walianzisha maandamano yaliyoambatana na fujo mpaka FFU ikainhilia Kati. Walikuwa wanaelekea manispaa. Kutokana na hizo vurugu na tishio la kuchoma moto manispaa FFU wametanda mitaa yote iliyo karibu na manispaa." Alisema Gilly.
"Kutokana na maelezo aliyotoa Gilly, mpango wa kumpata mtu wetu leo utakuwa mgumu kidogo. Kwani zahanati ya Magambo ipo jirani tu na manispaa." Patrick alisema huku akimwangalia Wanna See aliyekuwa akimsikiliza.
"Hata kama utakuwa mgumu lakini ni lazima awepo mtu pale aangalie nyendo za hapo alipo huyo mtu. Huenda tukamnasa tunayemtaka akija kumsalimia na hapo tutakuwa na uwezo wa kumufatilia." Alisema wanna See.
"Kwani Kuna habari zozote mlizonazo kuhusiana nao?" Aliuliza Zuberi, maana wao waliingia muda mfupi uliopita, hawakuwa na habari alizopata Patrick.
Patrick aliwaeleza kwa kifupi wakawa wameelewa na kuendelea na mpango ulio mbele yao.
"Kwa hiyo pale inabidi tuweke doria yetu ya kisiri au mmoja wetu augue apelekwe pale kwa matibabu na kuhakikisha analazwa pale kwa usiku wa leo ili tuwe na uhakika na tunachofanya." Alisema yule mwenzake na Wanna See ambaye mda wote alikuwa kimya. Walichangia hoja kuhusiana na mawazo aliyotoa huyo ndugu ambaye jina lake ni Lung'otha mwenye asili ya kizuru huko Afrika ya Kusini. Baadae waliafikiana kuwa Kabla ya kitendo chochote kile inabidi Patrick kwanza akonane na huyo aliyempa habari hiyo ili amfafanulie kwa undani zaidi. Kwa sababu pale ni kazini kwa mtoa habari anaweza kuwa msaada iwapo atatumika vizuri.
Baada ya maafikiano hayo Patrick alionelea aondoke wakati huo maana jioni ilishaanza kunyemelea. Nao akina Wanna See walitaka kwenda kumuona mwenzao ambaye yuko Mwanza Hotel. Kabla hawajaondoka Wanna See alimuambia Patrick asubiri, akaelekea chumbani na kurudi na mkoba wake.
Alifungua na kutoa redio kumi na mbili ndogo za mkononi akasema hizi ni redio za kawaida lakini zina sehemu zetu za siri za mawasiliano. Aliwaonyesha jinsi ya kutumia kama mwenzako akiwa anakutafuta utaona uzi unaotumika kutafuta mawimbi ya sauti unakuwa mwekundu na redio inakoroma kama vile haijashika mawimbi sawasawa. Hivyo unatakiwa kubonyeza sehemu iliyojitokeza kidogo pembeni ya kifufe cha kuongezea sauti na hapo mnaweza kuwasiliana. Kwa miiaka hiyo ilikuwa ni teknolajia mpya hivyo waliifurahia.
Baada ya kutoa maelekezo mafupi aligawa kwa kila mtu. Wote walipokea na kujaribu alafu wakatunza na kila mtu akaendelea na majukumu yake huku wakiwa wameahidiana kukutana saa nne za usiku pale kwa Patrick.
Patrick yeye alitakiwa akonane na mtu aliyempa habari za Kikakika ambaye ni Norack. Alifanya hivyo, kwa sababu ahadi ya kuonana ilikuwa bado ilibidi atumie akili nyingine ya kumpata Norack kwa haraka. Baada ya kuonana nae waliongea kwa kirefu na kukubaliana kuwa Patrick atapeleka mgonjwa pale usiku ili huyo mgonjwa achukue jukumu la kumchunga Kikakika. Hakumueleza ukweli wa mambo lakini kutokana na jinsi Norack alivyokuwa akimpenda hakuhoji zaidi isipokuwa kuahidi kumsaidia. Patrick. Patrick alimpatia pesa kiasi cha shilingi laki moja na kumuambia hiyo ni kwa ajili ya msaada anaoendelea kutoa na ahadi ya kujengewa nyumba ipo palepale. Norack alifurahi na kuongezea kuwa ingekuwa vizuri kama wangefika pale kuanzia saa nne na nusu kwani atakuwa tayari ameishaingia kazini. Baada ya hapo waliagana na kuahidiana kuonana baadae lakini hawataonyesha kujuana. Wakati huo ilikuwa ni saa moja na nusu jioni.
Pamoja na kuwa ahadi yao ya kukutana ilikuwa ni saa nne, lakini ilipotimia saa tatu na robo karibu wote walishawasili kwa Mr Patrick pamoja na yule mzungu mwenzie na Wanna See ambaye hakuwepo mchana. Ni Gilly pekee ndie alikuwa hajafika. Walikuwa waliendelea na mazungumzo ya kawaida huku wakitazama mkanda mmoja wa video uitwao Black Eagle, ile video ilionekana kewapendeza sana maana walikuwa wakijadili matukio yanayotokea humo kwenye video. Ni wakati alipofika Gilly ndipo walipoanza kujadili utendaji wao wa kazi na hiyo ilikuwa ni saa nne kasoro robo.
Baada ya mjadala mrefu kidogo ilikubalika Gilly ndie apelekwe zahanati kama mgonjwa aliyepata mshtuko wa moyo. Na Gilly atakuwa amechukua vifaa vyake vyote muhimu kama unga wa kunusa na kusinzia, bastola ndogo na redio ataachiwa kama wa kusikiliza. Unga unaweza kusaidia iwapo itapatikana njia ya kumtoa huyo mtu lazima awe hana fahamu ili kuhepusha bugudha. Gilly, Zuberi na Patrick waliondoka kwenda kutekeleza mpango huo. Wakati wanaondoka ilikuwa saa nne na dakika kumi na mbili, walipofika zahanati Gilly alijifanya yuko hoi akipumua kwa namna ya ajabu, Zuberi na Patrick walimsaidia kutembea huku wakiwa wameweka mikono yake juu ya mabega yao na kumuongoza mpaka kwenye mlango wa zahanati. Daktari alinyanyua uso wakati wanaingia na kuwaashiria wapite moja kwa moja katika chumba cha kuhudumia wagonjwa.
"Habari za shughuri?" Aliuliza Zuberi baada ya kuwa wameingia ndani na kukaa.
"Salama tu, sijui mgonjwa wenu ana tatizo gani?" Aliuliza daktari.
"Hata hatujui, ni hali iliyomtokea ghafla tu baada ya kupokea taarifa fulani hivyo tunahitaji msaada wako."
Baada ya daktari kusikia hivyo akichukua vipimo vyake na kuanza kumpima, alimaliza kumpima lakini hakuweza kugundua ugonjwa wowote maana alikuta mapigo ya moyo yakienda sawasawa.
"Haonyeshi tatizo la moyo" alisema daktari. Patrick na Gilly huku wakionyesha sura za mshangao walisema kwa pamoja" lakini hali yake unaiona ilivyo"
"Ndio kwa macho anaonekana ni mgonjwa lakini kwa hivi vipimo haonyeshi." Alisema daktari.
"Sasa bwana daktari unatushauri tufanye nini?" Aliuliza Zuberi. Daktari alifikiri kidogo alafu akasema "Nawashauri mumuache hapa kwa uchunguzi zaidi ndio tutakuwa na majibu sahihi ya kinachomsumbua"
"Sawa tutamuacha, sijui malipo yataghalimu kiasi gani cha fedha?" Aliuliza Patrick.
Kabla daktari hajajibu aliingia mlangoni Norack akiwa katika vazi la uuguzi. Aliwasalimia Patrick na Zuberi kisha akaongea daktari kuhusu aina fulani ya dawa ambapo daktari alifungua kabati pembeni yake na kutoa vipaketi vya dawa na kumpa.
"Siwezi kuwaambia malipo kabla sijampatia matibabu hivyo nyie muacheni na kesho njooni ndipo mtapata kujua gharama zinazohitajika." Aliongea daktari baada ya muuguzi kuwa ameondoka.
"Sawa, kwa hiyo sisi tunaondoka tutaonana kesho." Alisema Patrick.
Waliagana alafu Zuberi na Patrick wakaondoka huku wakiwa wamemuacha Gilly hapo zahanati akiwa na vifaa vyake vyote vya kazi. Zuberi na Patrick waliwasili kwa wenzao bila matatizo na kuwaeleza mambo yalivyokuwa huko zahanati, baada ya hapo wakatawanyika na kwenda kulala huku wakiwa wameahidiana kuonana kesho yake saa tatu asubuhi iwapo hakutakuwa na dharura yoyote.