Riwaya: Hekaheka za Komando Zedi Wimba na Jasusi Honda huko Somalia

Whsp haupo online muda! Nimekutext ili nifanye malipo kimyaaa
Mkuu ww fanya malipo, kisha utaona nakuwa online muda huo huo mana Siwezi kukaa online 24hrs ninakuwa online pale tu ninapoona pesa imeingia
 
RIWAYA; URITHI WA GAIDI

NA; BAHATI MWAMBA

SIMU; 0758573660


SEHEMU YA TATU



“It’s showtime baby!!” Kitambi alitamka kwa madaha kama jingo ya radio free Africa mwanza.
Remi aliganda kama sanamu huku akizisikia hatua nzito za bwana Kitambi zikielekea juu alikotokea yeye.

Ebana eeh hili lilikuwa sawa na somo la hisabati gumu kulielewa na linahitaji utulivu na usikivu kulifaulu.

****

MOGADISHU – SOMALIA.

Pembezoni kidogo mwa pwani ya mji wa Mogadishu ndani ya Somalia kulikuwa kuna tukio linaendelea kwa umakini wa hali ya juu bila kuwa na bughudha ama kelele yoyote. Kulikuwa kuna makundi mawili yaliokuwa yanafanya jambo katika barabara ya Old Mogadishu pembeni kidogo mwa fukwe ya Second Lido. Kutoka pahali fulani ndani ya hoteli ya Lugo kulikuwa kuna watu waliokuwa wamevaa kanzu za bei mbaya na vibandiko vya bei mbaya vile vile. Miongoni mwa watu wale kuna wawili waliokuwa wanakazi maalumu ambayo mmoja alikuwa na kiona mbali na kazi yake ilikuwa ni kuona mjongeo wa kile kilichowaweka pale. Lakini pia kulikuwa na mtu mwingine ambae alikuwa na mzigo mkubwa mgongoni ambao ulikuwa na mawimbi maalumu ya kupokelea simu za upepo kutoka kwa watu maalumu waliokuwa wamepandikwa kwenye barabara ile ya old Mogadishu.

Nyuma ya vijana wale kulikuwa kuna walinzi zaidi ya kumi ambao walihakikisha ulinzi eneo lile huku wakionekana kujali zaidi usalama wa watu wawili waliokuwa wamekaa kwenye viti ndani ya chumba kile cha gorofa tatu katika hotel ya Lugo.

Watu wale wawili walionekana kufuatilia kwa makini kila taarifa waliopewa na vijana wao kutokea nje ya eneo lile na kunaswa na mawimbi maalumu yaliokuwa katika mtambo uliokuwa umekaa sawia mwa kijana shababi aliekuwa mle ndani.

“Kabla ya dakika kumi ndege ataangusha YAI kiotani” ilisikika sauti kupitia simu ya upepo mle ndani na hapo mmoja ya watu waliokuwa wamekaa ambae alionekana ni kijana zaidi kuliko mwingine alinyanyuka na kuelekea dirishani kisha akanyoosha mkono na kijana aliekuwa na kiona mbali alimpatia nae akakipachika usoni mwake.

“Wapo ndege watatu, hatujui YAI lipo kwa ndege gani” Alisema yule jamaa kijana aliesimama dirishani na kiona mbali.

Hakuna aliemjibu nae hakujali akaendelea..

“Wamarekani ni wajanja sana,sina hakika kama watatupa YAI kamili”

Kauli ile ilimyanyua bwana aliekuwa amekaa peke yake nae akasogea karibu na dirisha na huku nyuma walinzi nao walisogea eneo lile kuhakikisha usalama zaidi.

“Unahisi wanaweza kutufanyia janja yao?” aliuliza yule mzee.

“Nahisi! Japo sina hakika” alisema yule kijana huku akishusha kiona mbali na kukirudisha mikononi mwa kijana aliekuwa nacho mwanzo.

“Kwani kuna anae mfahamu huyo Ahmed?” aliuliza yule kijana.

“Hapana! Na aliekuwa anamfahamu aliuwawa kwenye mashambulizi yaliotekelezwa na wamarekani mwaka 2006. Hivyo tunacheza pata potea japo ni muhimu sana kwetu huyu jamaa.” Alijibu Mzee wa kisomali.

“Mimi nakumbuka tu nilichokiona kwake wakati anaonana na Baba ila nimemsahau wajihi wake” alisema Kijana na jambo lile likafanya wote mle ndani wamakinike hasa yule Mzee.

“Nadhani ukiwakumbusha vijana ulichokiona itakuwa vyema zaidi ili tusipokee yai viza” alisema Mzee huku akijikuna kidevu chake kilichokuwa na ndevu ndefu wastani kama walivyo mashekhe wengi.

“Bwana alikuwa na kovu baya sijapata ona,Kovu lilianzia kifuani upande wa kushoto kuelekea upande wa mbavu za kulia likiwa limechora michirizi mingi huku lilipoanzia ni kama alijeruhiwa na mnyama mkali; Simba ama Chui” alisema kwa hisia kijana huku akijaribu kurekebisha kanzu yake ili imkae vyema.

Mara ileile taarifa ikatolewa kwa mapandikizi yalioko nje nayo yakaifanyia kazi.
*

Kundi lingine ndilo hasa lilikuwa linalengwa na kundi la kwanza lililoko Lugo Hotel. Kundi hili lenyewe lilijitenga katika viunga viwili. Kiunga cha kwanza kilikuwa upande wa mashariki mwa old Mogadishu na kilikuwa na watu wawili na Kiunga cha pili kilikuwa ndani ya magari matatu yaliokuwa na nembo za kikosi maalumu cha kulinda amani Mogadishu cha AMISOM(Africa Union Mission).
Ndani ya gari lililokuwa mbele kulikuwa kuna askari saba waliokuwa tayari kwa lolote na gari la nyuma pia lilikuwa na askari saba ila gari la katikati lilikuwa na askari komando watatu tu na mtu mwingine mmoja aliekuwa amefungwa minyororo mikono na miguu huku sura yake ikiwa imechakaa na mwili wake ukiwa umedhoofu sana.

Gari ya mbele ilionesha ishara kuwa wanapaswa kusimama eneo husika.

Magari yote yakasimama.

Kwenye gari la katikati, Komando mmoja alitoa kinasa sauti alichokuwa amekipachika sikioni mwake na kukipachika sikioni kwa yule mtu aliekuwa amefungwa kwa minyororo.

“Wanaweza kukujaribu kwa kila namna ili wathibitishe kama kweli wewe ndie Ahmed Twalibu sahihi,usije kutetereka na jukumu lako ni moja tu kuhakikisha tunajua maficho ya FLAMINGO kisha tutakupa utaratibu mwingine” ilisikika sauti kutoka kwa mtu aliekuwa kiunga cha kwanza mashariki mwa eneo lile.

“Nitawasiliana vipi na nyinyi kusubiri maelekezo?” aliuliza mtu aliekuwa amefungwa kwa minyororo.

“Siku mkipokea mzigo wa silaha hakikisha unatafuta risasi moja ambayo ni blanco hiyo itakuwa na ujumbe wako. Lakini kumbuka mwili wako ni mawasiliano na sisi Honda” ilisema sauti kutoka kiunga cha kwanza.

“Goda up kamanda!” ilisema sauti nyingine tofauti na ya awali iliokuwa upande wa kiunga cha kwanza.

“Goda up komredi” alijibu Honda p.a.k Ahmed Twalibu.

Kutokea nje ya gari walilokuwamo kukagongwa mara kadhaa na ikawa ni ishara kwao kushuka ndani ya gari huku Honda au Ahmed wa bandia akiwa amezingirwa na makomando watatu wa kikosi cha AMISOM. Na kutoka eneo lile lote ilikuwa limezingirwa na makomando kumi na saba kiujumla huku madereva wa magari yale wakiwa nao wametulia vyema kwenye gari zao tayari kwa lolote.

Ukimya ulikuwa wa kutisha kwenye barabara ile na makomando nao walikuwa kimya wakiwa makini na hatua zao wenyewe na mbele ya magari yao kulikuwa kuna gari dogo lililokuwa wazi na juu ya gari lile kulikuwa kuna kijana mdogo mwenye kupata umri wa miaka kumi hadi kumi na tano na alikuwa amebeba silaha ya kivita mikononi mwake bila wasiwasi wowote na ile ndio ilikuwa ishara ya kuwa pale ni eneo husika.

Wote wakiwa kimya,mara ukasikika mkoromo kutoka kwenye mifuko ya mmoja wa makomando waliokuwa wamemzunguka Ahmed Twalibu.

Komando yule alitoa simu ya upepo iliotoa mkoromo kuashiria kuna simu nyingine inayoingia.

“Mwacheni asogee mbele peke yake na nyinyi mrudi nyuma” iliunguruma sauti kutokea kwenye simu ile kwa lugha mbovu ya kingereza kwa lafudhi ya kihabeshi.

“Ni jicho kwa jicho komredi,tunaomba tuone upande wenu” Alisema komando wa kikosi kilichompeleka pale gaidi Ahmed.

Ukapita ukimya wa sekunde kadhaa.

“Anzeni nyie kisha tutawapeni wa kwenu” ilisema sauti kutoka upande wa pili.

Komando yule aliwaangalia wenzie ambao nao waliishia kutazama tu bila kusema kitu.

Akili zao zilikuwa zinapiga hesabu kali kukubaliana na jambo lile.

“Ok!!” alijibu kifupi komando yule na hapo komando wengine waligeuka na kutazamana kwa maamuzi yale ya kiongozi wao.

Dakika iliofuata walimpisha Ahmed asogee mbele kama ilivyotakiwa akiwa amefungwa vile vile minyororo mikononi na miguuni.

Honda; p.a.k Ahmed Twalibu alipiga hatua kivivu huku nae akiangaza macho yake kushoto na kulia taratibu bila papara.
Hatimae alifika kati kati ya gari lililokuwa wazi na juu kukiwa na mtoto aliebeba silaha na wale makomando ambao muda wote walikuwa kimya bila hata kupepesa macho yao.

Kutoka kwenye chumba ndani ya hotel ya Lugo; kijana yule aliekuwa na asili ya Saudia,alishusha chini kiona mbali na kuwageukia wenzie waliokuwa na asili ya kisomali.

“Anaweza kuwa ndie,mruhusuni tutamjua akiwa chini yetu” alisema huku akikabidhi tena kiona mbali kile kwa mtu aliekuwa nacho awali.

“Basi itifaki izingatiwe” alisema mzee wa kisomali huku akikuna msitachi wake.

Vijana walijua nini wanapaswa kufanya.

*

Kijana aliekuwa kwenye gari na mtutu wa bunduki,alisikia mlio wa mluzi mara mbili na hivyo alijua ni kipi cha kufanya wakati huo.

Haraka kutoka pale alipokuwa, akashuka kibabe utadhani ni mtu mzima. Akapiga hatua bila wasiwasi wowote na kumfikia Honda p.a.k Ahmed Twalibu.

Hakujishugulisha na pingu alizokuwa amefungwa Ahmed bali alibaki akimtizama usoni bila kupepesa. Honda aliona macho ya yule mtoto yalivyojaa ukatili ingali ni mdogo. Alikakamaa mithili ya wabeba mizigo bandarini.

Hakika ilihuzunisha.

Ila mtoto yule hakuonekana kujali.

Akachomoa kisu na kuiweka pembeni bunduki yake kisha akamfuata Ahmed.

Mtoto yule bila uoga alianza kurarua nguo za Honda p.a.k Ahmed Twalib gaidi aliesakamwa na makundi mbalimbali wakitaka ajiunge nao na sasa Ahmed yupo Somalia mbele ya kikundi cha kiharamia na kigaidi huku yakiwa ni makabidhiano maalumu na serikali ya Marekani.

Mtoto yule alieonekana ni fundi wa kutokea kutumia kisu,hakumaliza dakika moja tayari nguo za Ahmed zilikuwa hazitamaniki na yule mtoto akabaki akilikodolea kovu baya kifuani mwa Ahmed. Yule mtoto alishindwa kuelewa kovu limesababishwa na nini na ni binadamu gani anaweza kuhimili kuishi na kovu kubwa kiasi kile maishani mwake.

Hakika bwana mdogo aligwaya.

Bwana mdogo yule akabeba mtutu wake na kugeuka, lakini kama alisita hivi na kugeuka tena kulitazama kovu lile.

Kuna kitu kilipita akilini mwake.

Kovu gani hili? Mbona kama ni bandia? Aah!!” alijakatalia haiwezi kuwa maigizo katika mwili wa mtu.

Bwana mdogo aligeuka na kumpa ishara Ahmed amfuate. Ahmed akaanza kujivuta kivivu kumfuata huku makomando waliomfikisha pale wakiwa kimya na umakini wa hali ya juu.

Bwana mdogo yule alipiga mbinja kadhaa kisha akajipiga kifuan mara kadhaa. Ilikuwa ni ishara ya kukamilisha kazi yake na sasa wakubwa wake waendelee na utaratibu wao.

Wakati Ahmed anapakizwa kwenye gari na bwana mdogo yule, Makomando walishuhudia watu wengine watatu wakitokea kwenye jengo moja bovu lililokuwa pembezoni mwa barabara. Watu walionekana wakiwa wamedhoofu kupita maelezo na walizeeka kweli.

Walikuwa ni mateka wa kijeshi tangu miaka ya tisini baada ya vita kati ya kikundi cha kigaidi cha AIAI(Al-Itihaad Al-Islamiya).

Komando kiongozi aliona wahusika wa mabadilishano yale, akatoa ishara kwa makomando wale wa AMISOM nao wakaanza kuelekea kuwapokea watu wale walioonekana kudhoofu miili yao.

Lakini gafla ikasikika risasi moja hewani na makomando wote wakakoki silaha zao tayari kwa lolote.

Alikuwa ni bwana mdogo aliepiga risasi juu.

Akashuka kwenye gari na kumwacha Ahmed akiwa na dereva akawafuata wale makomando ambao walikuwa wamesimama bila kujua wafanye nini.

Akawafikia!!

“Oya!! atakaepiga hatua kusogea hapo alipo nitamvua chupi hadharani, nguruwe weupe nyie” alifoka bwana mdogo bila kuogopa macho ya kikazi ya makomando wale ambao mitutu yao ilikuwa sawia kifuani mwa bwana mdogo yule.

Walipigwa mkwara wakatulia.

Bwana mdogo akageuka kibabe na kuwafuata wazee waliokuwa wanakikokota kuwaendea wale makomando.

“Na nyie vibwenzi nitawatoa roho sasa hivi, mtaondokaje bila mi Mzee wenu kutoka hapa.” Bwana mdogo akaachia mkwara mbuzi wazee wale waliokuwa makimando miaka hiyo kabla ya dhahama iliowakumba na kujikuta wakiwa mateka miaka mingi.

Bwana mdogo alianza kuondoka kwa madaha huku akipiga mluzi wa wimbo asioujua,na kabla hajafika kwenye gari akawageukia wale wazee.

“Mnadhani na huo uzee mnaenda kufanya nini. Nendeni mshikishwe tunguli na Wamarekani vibwengo ninyi”

Alah!!!

Mtoto anatema mkwara kwa wakubwa.

Makomando wote walibaki wakiwa wameganda kama sanamu. Mtoto aliwashangaza kwa kujiamini kwake.

Na kweli walitulia hadi bwana mdogo alipoondoka pale ndipo na wao walipowahi kuwapokea wazee wale na kuwaingiza ndani ya magari yao na kuondoka eneo lile la Old Mogadishu.

Wao hesabu zao zilienda sawa siku hiyo na hesabu za kikundi kile ambacho hakikuwa na jina kubwa la ugaidi miaka ya karibuni, nacho kilijua kipo safi katika hisabati yao.

**

Bwana mdogo yule hakwenda mbali na mateka wake Ahmed. Walizunguka kona ya kwanza na ya pili wakaingia kwenye jumba lililoonekana kama ni karakana ya kutengenezea magari.

Humo ndani kulikuwa kuna magari mengi mabovu na mazima yalioonekana kupitia shuruba nyingi sana. Mbali na hayo pia kulikuwa kuna watu wengine wanne.
Kati ya watu hao wawili walikuwa na mitutu ya kivita huku mikanda ya risasi ikiwa imezunguka mabegani mwao, na wawili walikuwa ni wasichana wazuri wa kihabeshi wenye umri si zaidi ya miaka kumi na saba ambao walikuwa wamefungwa mikono kwa nyuma na vitambaa vyeusi machoni pao. Walionekana kupitia mateso mengi mana walidhoofu na miili yao kugandana na makovu mabichi.

Hakika ilitia huzuni.

Honda p.a.k Ahmed alitazama kwa huzuni wasichana wale.

Watekaji hawakujali.

Bwana mdogo yule alibaki akiwa anamtazama Honda kwa dakika kadhaa,kisha akaanza kumzunguka kwa madaha kama anaekagua kitu hivi kisha aliporidhika na tambo zake alisimama mbele ya Honda na kwa gafla akamtandika ngumi kali ya tumbo na kumfanya Honda ainame kwa maumivu makali yaliosambaa tumboni kwake.

Ngumi ya bwana mdogo ilikuwa ni ngumi ya mtu mzima hakika..

“Naitwa Sozi mfalme wa wajane hapa Somalia”alijigamba bwana mdogo huku akirekebisha mtutu wake begani na kuutia mikononi kisha akapiga mluzi na hapo akaja jamaa mwingine aliekuwa na zana za ufundi na alipofika bila kuelekezwa alianza kushugulika na vifyatuo vya minyororo iliokuwa mwilini mwa Honda.

Dakika nne baadae Honda alikuwa huru lakini hakuruhusiwa kupiga hatua hata moja.

“Ahmed; nataka ufanye kazi moja tu hapa” alisema Sozi bwana mdogo mtata au alivyopenda kuitwa mfalme wa wajane. Haijulikani wajane gani aliomaanisha huyu bwana mdogo.

Aliita wale vijana waliokuwa na wale mateka nao wakaanza kuwaburuza mabinti bila huruma na kuwafikisha pale walipokuwa Sozi na Honda au kama walivyomjua kwa jina la Ahmed.

“Hawa ni wahabeshi wa huko Ethiopia; mabwana zao walituchafua ndani ya nchi yetu sasa waliwaacha hapa na kifo kimefika na wewe ndo utawauwa” alisema Sozi huku akiikoki silaha yake na kitendo bila kutegemea akaachia risasi ilioenda kutua kichwani mwa binti mmoja na kumsambaratisha ubongo wake bila huruma.

Hakika Sozi alikuwa katili zaidi ya umri wake.

Akamgeukia Honda.

“wewe ni gaidi Ahmed; hivyo huoni huruma kwa hawa mende,piga risasi tu huyu aliebaki ili tujue kweli sifa unazopewaga ni za kweli.” Alisema Sozi huku akimpa mtutu wa kivita Honda waliemjua kwa jina la Ahmed.

Mmoja wa wasomali wale alimvua kitambaa yule binti. Binti alimlitizama Honda kwa huruma sana.

Honda alibaki akiwa hana la kufanya.

Ukitaka kumuua nyani usimtizame usoni.

Mfalme wa wajane alibaki akimtizama Ahmed na maamuzi yake.

Honda alikuwa katikati ya hisabati za Wasomali.

Hakujua aepuke vipi mtego wa hesabu ile, huruma ilikuwa kubwa karibu ibebe ujasiri wake.

Ataua?

***


Maoni yako ni muhimu sana katika kazi hii.karibuni
Kudo kaja moto chini ila isiwe nguvu ya sada maana alosto inauma sana
 

Similar Discussions

15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom