Riwaya: Genge

winston20

JF-Expert Member
Jun 21, 2020
1,117
2,256
GENGE
EP1

JULAI 15, 1991 DIAMOND JUBILEE

SAUTI KUBWA YA MUZIKI ilisikika kutoka katika ukumbi huo maarufu jijini Dar es salaam, katika kitongoji maarufu cha Upanga. Ni harusi ya kukata na shoka, kati ya Bi. Egra Mwakasimba na Dastani Kihwelo. Mamia, kama si maelfu ya watu waliujaza ukumbi huo. Wakila na kunywa huku wakitunuku zawadi kemkem kwa maharusi hao. Mishale ya saa mikononi mwa waliowengi ilioneshas saa sita kasoro robo usiku. Wenine walisaanza kusimama na kuondoka wakati wimbo huo unaojulikana kama ‘Wifi twende nyumbani’ ukirindima. Maharusi nao walikuwa wima wakitembea kwa mwendo wa maringo na hatua za hesabu kulielekea lango kuu, tayari kwenda kula fungate.
Nje ya ukumbi huo, gari la maharusi lilikwishaandaliwa na kuegeshwa mahala pake. Mercedes Benz E Class,jipya kabisa, toleo la 1990 lilipambwa likapambika. Gari hilo la pesa nyingi lilitolewa zawadi na idara ya Usalama wa Taifa ambapo Dastani Kiwelo alikuwa mwajiriwa mtiifu. Baada ya kuagana na ndugu na marafiki, Dastani, na mkewe Egra wakajitoma ndani ya chombo hicho kipya.
“Ooooh! Gari zuri sana mume wangu!” Egra akasifia mara tu baada ya kupokelewa na kiti cha ngozi laini. Akatazamana na mumewe na kubusiana kisha Dastani akapachika funguo mahala pake na kuliwasha. Ndani ya gari hilo walijiona wao tu, taratibu gari lile likaingia barabarani na kutokomea huku likiwaacha watu wakisindikiza kwa macho. Mazungumzo kati ya mtu na mkewe yalicukua nafasi wakati tairi zikichachafya Barabara ya Ally Hassan Mwinyi mara baada ya kuiacha ile ya Umoja wa Mataifa. Kutoka kwenye redio ya gari hilo, sauti ya mwaDanada Judy Boucher ilikuwa ikisindikiza kwa kibao matata ckinachokwenda kwa jina ‘Mr. Dream Maker’.
“Asante Dastani,” Egra akashukuru.
“Asante nawe pia, umenifanya niwe mwanaume sasa,” Dastani akamjibu mkewe huku akiongeza mwendo kulipita gari la mbele yake.
“Nataka tujenge familia ndogo, yenye upendo na furaha…” Dastani akajibu, alipotaka kulipita gari lingine akasikia honi kali nyuma yake. Akarudisha usukani kushoto na Benzi lile likatii amri. Mazda jekundu likampita kasi. Ndani ya Mazda lile ‘kibanda wazi’ kulikuwa na mwanamke mmoja ambaye ndiye dereva. Mshtuko wa wazi kwa Dastani ukaonekana.
“Vipi honey, mbona umepoa ghafla?” Egra akauliza.
“Hapana, hamna kitu,” akajikaza kiume, Waswahili husema.
“…unanificha, au ndo x wako? Wanaume amna wema!” Egra akalalama na kueukia upande wa pili.
Wanawake bwana! Hapo keshawaza mengine! Dastani akawaza na kupunguza mwendo. Kama mwanausalama, alishajua nini kitatokea kama akiendelea kufuata barabara hiyo. Akili ilimtuma kuchepuka na kuingia kulia kwenye barabara ndogo ya Kaunda, hakufanikiwa.
Kutoka nyuma ya kiti chake aliisi kitu chenye ncha kali kikimchoma pembeni kidogo ya uti wa mgongo. Akatulia huku gari likiendelea kuseleleka taratibu. Egra akaundua hilo, akageuka nyuma na kukutana macho na mtu aliyevaa soksi jeusi kufica uso wake. Alipotaka kupiga kelele akajikuta akipiwa na kiganja kigumu upande wa nyuma wa shingo, akazirai.
“Endelea na barabara hiyo hiyo mpaka nitakapokwambia,” sauti nzito ya mtu huyo ikamwamuru. Dastani akuwa na ujanja, akatenda aliloambiwa na mtu huyo. Kicwani mwake aliendelea kutafakari na kujaribu kukumbuka ni wapi aliisikia sauti hiyo, asipate jibu.
Dakika mbili zilizofuata walifika eneo la Mbuyuni.
“Kunja kushoto!” akaamriwa. Naye akatii na kucuku barabara ya Ruhinde. Mbele kidogo akatakiwa kukunja kulia, akafanya hivyona kuingia Mtaa wa Galu. Mara tu baada ya kukunja ile kona akaliona lile Mazda jekundu limeegeshwa kando.
“Simama hapo!” akaamriwa, naye akatii. Kutoka kwenye vivuli vya miti, wakajitokeza watu wengine watatu, wanaume ambao sura zao alizifahamu vyema. Dastani akateremshwa garini na kusimama chini,
“Umependeza Dastani, suti ya gharama uliyovaa, gari ya kisasa uliyopewa zawadi na wadosi wako… vyote ni kwa sababu ya kutuuza swahiba zako,” mwanaume wa makamo alizunumza huku akiwa kasimama mita chache tu kutoka kwa Dastani.
“Ilikuwaje ukakiuka maagizo Dastani, ata ukasababisha mipango yetu kwenda fyongo? Mpiganaji wetu , komandoo Salimu Manumba akauawa… yote kwa sababu yako. Na wewe mwenyewe kwa mkono wako ukamuua Bambross pale Embassy Hotel, ukachukua nyaraka nyeti na kuwapa mabosi wako. Tulijua u mwema, kumbe fukufuku mchangani. Watu wa aina yako uwa hawastahili kuishi… kwa taarifa yako, ulichokisema kwa mabwana zako ni asilimia kumi tu ya mpango mzima. Usifikiri tulikuwa wajinga kwamba tungeweka kila kitu mbele yako, la hasha! Sasa wewe utakuwa sanduku letu,” yule bwana akamaliza na kuingia kwenye lile Mazda jekundu pamoja na yule mwanamke wa Kizungu. Dastani akarudishwa garini mwake, mara hii, kwenye kiti cha nyuma huku vijana wengine wawili wakikaa upande huu na ule. Egra akiwa bado kwenye mzimio.
Safari yao iliishia Msasani Peninsula, kando kabisa ya Bahari ya Indi kulikuwa na nyumba moja pweke, ya kifahari. Ni katika nyumba hii ndipo, Dastani na mkewe, Egra, walikuwa wakielekea tayari kwa kuuanza usiku wa kwanza kama wanandoa.
“Usiwe na wasiwasi Dastani, fungate mtakula kama kawaida, na mtainjoi harusi yenu ndani ya nyumba ni hii hii,” yule bwana akazungumza. Dastani hakujibu. Yule mwanamke wa Kizungu mwenyue Mazda jekundu akaja na ndoo ya maji mkononi na kummwagia Egra. Egra akakurupuka na kuanza kuhema kwa nguvu na haraka haraka huku akimwita Dastani kwa sauti kali. Makofi mawili aliyozabwa na yule mwanamke yakamnyamazisa na kumwacha akitweta. Dastani, alilishuhudia tukio lile, akauma meno kwa uchungu na hasira.
“Mwacheni mtoto wa watu msimdhuru, haya hayamuhusu…” Dastani akatamka.
“Hatuwezi kumdhuru huyu, hana hatia, ila ataishi na sisi mpaka Munguamchukue mwenyewe, na wewe, malipo ya kazi yako yamefika…” alipomaliza kusema hayo kikafuatia kipigo kikali kutoka kwa wale vijana. Dakika kumi, zilimwachaDastani akiwa chini, hoi bin taabani, kila alipokohoa alitokwa na damu kinywani. Egra alikuwa akilia kwa uchungu kwa kila alipokuwa akitazama kipigo anachoshusiwa mwenza wake. Wale vijana baada ya kumsulubu Dastani, wakamwacha pale chini na kufunua buti la lile Mazda, wakatoa madumu mawili ya petrol na kuinia ndani ya ile nyumba. Dakika tano baadae wakatoka na kumwaga mafuta yaliyobaki kwenye kibaraza na mengine wakalimwagia lile Benz. Haikupita dakika mbili , upande wa baarini ikawasili boti ndogo.
Vijana wawili wakashuka wakiwa wamebeba miili ya watu wawili; mwanamke na mwanaume. Awakuongea na mtu,wakapitiliza ndani ya nyumba ile moja kwa moja. Iliwachukua kama sekunde arobaini hivi, wakatoka.
“Tayari boss,” wakamwambia yule bwana aliyesimama kando ya Dastani. Akawajibu kwa kutikisa kichwa. Akawapa ishara ya kumbeba Dastani na mkewe, wakafanya hivyo na kuwapakia kwenye ile boti. Pamoja nao, wakafuatana na wale vijana wengine.
“Ash to ash!” akatamka yule mwanaume na kuitoa sigara yake kinywani kisha akaitupia pale kibarazani. Moto mkubwa ukalipuka na kuichoma ile nyumba na kuteketeza lile Benzi wakati wawili wale wakipotea mbali ndani ya Mazda lao.
“Mungu amlaze panapomstahili,” yule bwana akatamka.
“Jesca! Moja kwa moja uwanja wa ndege,” akaoneza kusema. Yule mwanamke aliyeitwa kwa jina la Jesca akaitika kwa kichwa.

* * *

2002 Januari

BRUSELS –UBELGIJI

Wingu zito lilitanda katika anga la jiji hilo, barabara zilifunikwa na kwa barafu na kusababisha baridi kali kwa wakaazi wake. Daima kipindi kama hiki cha miezi ya Desemba mpaka Februari, nchi za Ulaya hupitia katika kipindi hiki, winter.
Nje ya jengo refu lenye sakafu thelathini na sita, linalojulikana kama Tour des Finances, gari moja la kisasa aina ya Audi liliingia katika uwanda wa maegesho, chini ya jengo hilo, likiiacha barabara kubwa ya Royale inayokatiza pembezoni mwake.
Kutoka ndani ghorofa ya ishirini na tano, ndani ya ofisi moja nadhifu iliyosheheni vitabu na makabrasha anuai katika rafu zake zinazong’aa kwa polish safi, hatua za mtu anayeujongelea mlango zilisikika pasi na kificho. Zilipofika mlangoni hapo, zikakoma. Sekunde kumi na tano zilizofuata, mlango ukafunguliwa. Kipande cha mwanaume kikaingia ndani. Kabla hajawasha taa kwa minajiri ya kufukuza iza hafifu lililosababishwa na wingu lile; aliona taa ikiwaka yenyewe.akapiwa na mshtuko na kuwai kugeuka upande wa pili ambako kuna swichi nyingine ya kuongoza taa hiyo.
“Usiogope, ni ugeni tu wa kawaida…” sauti ya mwanaume ikasikika upande ule. Yule bwana akashikwa na kigugumizi na kutazamana macho kwa macho na huyo aliyejiita mgeni.
“Wewe ni nani? Na unafanya nini katika ofisi yangu?” kile kipande cha mtu kikauliza uku akivuta kiti na kuketi nyuma ya meza yake kubwa.
“Mimi ni mgeni wako kutoka katika nchi iliyokulea, mpaka ukawa mtu mzima na kuiasi,” yule mgeni akajibu.
“Nani aliyekutuma?”
“Mama yako!” yule mgeni akajibu huku akicezea vidole vyake.
“Hivi ninyi Watanzania mna matatizo gani? Kwa nini ampendi watu wastarehe na maisha yao? Kutwa kucha mnatufuatilia, tuacheni!” akang’aka yule bwana.
“Jiulize! Ni Watanzania wangapi wanaisi Ughaibuni tumekuwa tukiwafuatilia? Kama si wewena washenzi wenzio tu… mngekaa kwa amani kama mngeondoka kwa amani…lakini mlichokifanya mnakijua, na adabu yake mnaijua. Nyote lazima muitumikie adhabu yenu…” yule mgeni akaeleza. Ndani ya mfuko wa ndani ya suti yake akachomoa bahasha ya khaki, juu ilikuwa na mhuri wa serikali.
“Ichane, uisome, nimetumwa na mama yako kukuletea…”
Yule bwana akaichana kwa kitete huku akivuta kamasi jepesi kulirudisa ndani ya pua zake ndogo. Akatulia kuisoma. kijasho chembamba kikamtiririka ilhali ofisi hiyo ilitawaliwa na baridi.
“Wewe ni nani?” akauliza kwa sauti huku akizungusha kiti kumtazama mgeni huyo. Mkono wake wa kuume ukabonyeza kitufe Fulani na kuruusu saraka ya siri kufunuka katika meza hiyo. Akabaki kakodoa macho akiwa haelewi nini cha kufanya.
“Usihangaike Bwana Titus Mwakibinga, bastola yako ninayo, nilikwisaichukua kitambo!”
Yule mgeni akamwambia mwenyeji wake ambaye mara hii alimtaja kwa jina la Titus Mwakibinga. “Umeju-aje ma-ha-li bastola ya-ngu i-li-po?” Titus akauliza kwa kigugumizi uku akipiga ngumi mezani.
“Kwani wewe ulifikiri hapo ni mahala pa siri? Mimi nilisapajua zamani sana, na sikupata tabu kuichukua,” mgeni akajibu.
“Nakuuliza kwa mara ya mwisho… wewe ni nani?” Titus akatupa swali uku akiwa amefura kwa hasira.
“Naitwa Amata Ric, au Kamanda Amata, TSA 1, code 005…” yule mgeni akajitambulisa huku tayari bastola ikiwa mkononi mwake. Titus alipotazamana na bastola ile alijikuta akiisiwa nguvu.
“Mbiyo za panya! Titus, hata kama kosa umelifanya mwaka ’82, hukumu iko palepale. Kama ulifikiri ukitoroka ndiyo utaukwepa mkono wa sheria, basi umeula wa chuya kwa uvivu wa kuchagua. Hukumu ya kesi yenu ilisomwa mwaka 1985, Desemba 28 na Jaji Antoni Mzavas. Wenzi wako walihukumiwa kifungo lakini wewe na wengine wachache mlitoroka nchi. Titus Mwakibinga, umehukumiwa kifo…” Kamanda Amata akamwambia pasi na lepe la tabasamu usoni mwake.
“Mimi sihusiki, serikali imenionea tu,” Titus akalalama.
“Sasa nani anahusika kama si wewe?”.
“Sijui!”
“Hujui? Kama hujui, basi ni mhusika mmoja wapo…” Amata akasema.
“Nooo!” Titus akang’aka mara alipoona bastola ile imeondolewa usalama.
“Kijana, nitakupa pesa nyingi sana,” akasema Titus.

ITAENDELEA
GENGE
EP2

Nooo!” Titus akang’aka mara alipoona bastola ile imeondolewa usalama.
“Kijana, nitakupa pesa nyingi sana,” akasema Titus.
“Sihitaji pesa yako, nimekuja kutekeleza kile nilichotumwa kama ulivyosoma kwenye hiyo hati,” Amata akasema na kumfanya Titus ageuke kutazama mezani. Macho yake yakagonganana neno KIFO, lililoandikwa kwa wino mzito na kupigiwa mstari mwekundu.
“Buriani Titus! Ukishakufa uwatokee wenzio kwenye ndoto uwaambie kuwa nitamuua mmoja baada ya mwingine. Popote watakapokimbilia…” Amata akasema. Kabla Titus hajaongea chochote tayari, risasi moja kutoka kwenye bastola yake mwenyewe, Glock 23, ikatoboa paji la uso. Titus Mwakibinga akajibamiza kitini na kichwa chake kuegemea kushoto. Amata akaipachika bastola ile mkononi mwa marehemu.
Nje ya jengo lile, akatembea taratibu huku mikono ikiwa mfukoninabubblish ikiteketea kinywani mwake, akapita barabara ya Royal kuelekea Best Western Hotel ambako ndiko aliwekeza makazi yake kwa muda akiwa katika operesheni hiyo. Ze Sindiket…

* * *
Ndani ya hoteli ile, Amata alijitupa kitini, akavua glovesna kuziweka juu ya meza ndogo ya kusomea. Akavuta kabrasha lake na kupekua hapa na pale akitazama kinachofuata. Alipojiridhisa na kazi yake akalikunja kabrasha lile na kulitia mkobani.
1981

DAR ES SALAAM

UPEPO MWANANA uliendelea kuvuma. Dirisha kubwa katika moja ya nyumba nyingi katika eneo la Kawe Mzimuni, liliruhusu upepo huo uwafikie wapendanao wawili waliokumbatiana kitandani usiku huo. Muziki laini kutoka katika santuri ya Mbaraka Mwishehe ulikuwa ukiendelea kusikika kwa sauti ya chini. Kelele za mibweko ya mbwa ikamshtua mwanamke aliyelala kitandani hapo. Mwanamke wa Kizigua, mwenye shepu isiyosemeka, akajivuta na kunyoosa mkono wake mpaka sehemu Fulani, uvunguni mwa kitanda hicho. Taa kubwa ya nje ikawaka na kufanya nuru kali ambayo kila kitu kingeonekana.
Mbwa waliendelea kubweka, mwanamama yule akaamka na kukiacha kitanda. Umbo lake la Kitanga likafanya mitetemo ya kuvutia na kuuweka dhahiri shahiri uanamke wake. Akakiacha cumba na kuelekea sebuleni. Wakati mbwa wakiendelea kubweka, mara kelele iliyofanyika kwa mawe matatatu kurushwa batini, ikamshtua mwanaume aliyelala kitandani hapo.
Akaamka na kupapasa upande aliokuwapo mkewe, hayupo. Akajiinua na kuketi kitandani. Nukta hiyo hiyo mkewe akainia chumbani humo na kujitupa kitandani, akavuta suka na kujifunika mwiliwe akikiacha kichwa tu nje.
Yule mwanaume akatoka kitandani na kuchukua shati lake kutoka kwenye henga. Akavuta hatua na kuelekea sebuleni, kasha geti kubwa. Akatoka nje. Nje tu ya geti hilo kuliegeswa Land Rover 109, na vijana wawili walikuwa wameliegemea.
“Vipi kwema?” akawauliza bila kuwasabahi.
“Mr. Chameleon!” mmoja wa wale vijana akatamka, akashusa kiko chake na kukimata vizuri kwa mkono wake wa kulia, “usiku kama huu, hakuwezi kuwa na wema. Twende zetu ofisini, kuna ujumbe wako.
“Oh shit! Hebu niacheni nipumzike na mama yenu kwanza ee!” Chameleon akajibu.
“Ni kweli mzee, ila huna budi kufanya hilo, namba moja anakuhitaji haraka,” yule kijana akamwambia Chameleon. Mzee yule akajishika kiuno, baada ya tafakari ya sekunde kama kumi hivi, akawaaca wale vijana na kuinia ndani. Mkewe alikuwa tayari keshalala fofofo. Dakika kumi zilizofuata, tayari alikuwa ndani ya Kaunda suti. Akamsukasuka mkewe na kumwamsha.
“Aaaa unanikatisha ndoto yangu bwana!” mkewe akasema huku akiamka na kuketi.
“Mi natoka…”
“Unaenda wapi?” akamuuliza mumewe.
“Kazini mara moja!” Chameleon akajibu.
“We na kazi zako, nisakuzowea. Siku hizi hata ndoa hatufaidi, naachwa na kiu tu…” akalalama mwanamke wa Kizigua.
“Usijali mpenzi, ngoja tulitumikie taifa,” akambembeleza.
“Haya nenda kwenye taifa lako unalolipenda ukalitumikie… na taifa hili unaloliacha likivamiwa na waasi usilalamike!” Mkewe akasema. “Aaaaa mama watoto, unafika mbali sasa…”
“Piiiiiiip! Piiiiip!” honi ya gari ikamshtua.
“Haya mammy, tutaonana baadae!”
“Sawa Daddy”.
Wakabusiana, na mzee huyo akaiacha nyumba na kuondoka zake.

* * *
Saa saba usiku, Chameleon alifika Msasani kuliko na makazi ya Rais ambaye wao walimtambua kama ‘namba moja’ kwa kuwa ndioye aliyekuiwa na dhamana ya ulinzi kwa nchi nzima. “Pole!” Rais akamwambia huku akimkaribisa kiti katika ofisi yake ndogo. Ndani ya nyumba hiyo.
“Asante Meshimiwa, nimeitikia wito…” Chameleon akajibu kwa adabu zote.
“Nisichukue muda wako mwingi… kuna taarifa hii hapa ambayo imenifikia jioni ya leo. Sikuifanyia kazi kwanza, kwa sababu nilikuwa naipitia kwa kina,” akamwambia huku akimkabidhi ile karatasi iliyoandikwa pande mbili. Chameleon akaipokea na kuisoma mara kadhaa. Alipomaliza, akaiweka mezani na kumsogezea mkuu wa nchi.
“Kwa hiyo, hata waziri Kibwana Mtokambali anahusika?” Chameleon akauliza.
“Ningekuwa na majibu, nisingekuita. Nataka ufanye uchunguzi… umchunguze waziri
Kibwana na nyendo zake zote. Pia nataka unipe taarifa kamili za hawa maafisa wa jeshi, akiwamo Kepteni Vincent Mwanachia,” Rais akamwambia Chameleon. Naye akajibu kwa kutikisa kichwa juu chini.
“Chameleon, this is confidencial… hakikisha, ndani ya siku mbili, unanipa majibu stahiki,” Rais akasema na kuagana na mwanausalama wake anayemtegemea. Chameleon alitoka ndani ya ile ofisi, akachukua na ile karatasi huku kichwa chake kikiwa kimejaa mawazo ya nini cha kufanya dhidi ya hicho alichoambiwa. Alitazama saa yake, ikamwonesha kuwa ni saa tisa kasoro robo usiku. Akafikiri aende nyumbani kuendelea kuumaliza usiku na mkewe, au aende ofisini kuanza kupana na kupanua juu ya hicho alichoambiwa, akupata jibu. Mawazo yake yakamrudisa kwenye kauli ya mkewe ambayo iliuchoma moja kwa moja moyo wake, ‘…na taifa hili unaloliacha likivamiwa na waasi usilalamike!’
Saa tisa na dakika na dakika tano usiku alikuwa akipita Barabara ya Chole, Masaki akiwa bado ajui sawia ni wapi aelekeako. Katika barabara hii kulikuwa na nyumba kadhaa za vibopa na vigogo wa serikali. Kati ya nyumba hizo, ilikuwamo ya waziri Kibwana Mtokambali. Bwana Chameleone alikuwa na tatizo kubwa moja, akishapewa kazi basi akili yake uwa hailali mpaka kazi ile itimie. Katika barabara ya Chole maeneo ya Oysterbay, Chameleone alikuwa akiendesha moja ya magari yao ya siri katika idara ya Usalama wa Taifa, Volvo. Alipokuwa katika lindi la mawazo, akautuswa na mwanga mkali wa taa za gari lililoingia katika barabara hiyo kutokea ile ya mbele yake. Akapunuza mwendo na kususa ukali wa taa zake, lakini lile ari la mbele yake alikufanya hivyo na kupelekea mwanga ule kumuumiza machoni. Akapunuza mwendo na kueesa kando kidoo akisubiri ari lile lipite. Badala ya kupita, likawasa indiketa ya kulia na kuinia kwenye ujia mfupi ulioishia kwenye lango la nyumba nyumba moja kubwa.
Bahati gani ya mtende kustawi jangwani? Gari lile lilisimama mbele ya nyumba ya mheshimiwa Kibwana Mtokambali. Chameleon akarudisha gari barabarani nakupita pale polepole akiendelea nasafari yake. TB 620, namba za gari zilisomeka namna hiyo. Kwa kamera yake ndogo ya Kirusi aina ya Cimena, akapiga picha lile gari kwa upande wa nyuma likiwa linamalizikia kuingia ndani ya wigo ule. Chameleon, hakuelewa kama gari lile, usiku ule, alikuwa waziri Kibwana mwenyewe akitoka mizunguko au mgeni kaja kumtembelea, hakuna jibu. Akaamua kuegesha gari lake kwenye kona moja mbele yake. Kisha akaamua kurudi kwa miguumpaka usawa wa nyumba ya waziri Kibwana, mwenye dhamana ya ulinzi wa nchi yake.
Ukuta ulioizunguka nyumba hiyo ulikuwa mrefu kiasi, kadiri ya mita tatu hivi na juuye kulikuwa na waya uliozungushwa kwa usatadi mkubwa na kibao kilichosomeka ‘DANGER’ chenye rangi ya njano na maandishi meusi kilining’inia. Akasimama nje ya ukuta huo kwa kuwa mazunumzo ya awali ya maamkiano ya watu hao aliyasikia.
“Hakuna mtu nyuma yako? Maana hii nchi unaijua!” Sauti ya Kibwana ikasikika.
“Aaaa naijua kazi yangu mheshimiwa…”sauti ya pili ikajibu. Chameleone hakuweza kuigundua sauti hiyo kuya ni ya nani. Alichokifanya ni kutega masikio kwa nguvu zote kusikiliza kile kitakachozungumzwa hapo nje.
“Enhe!”Kibwana akaendeleza mazungumzo, ambapo sasa dhahiri shahiri,sauti zao zilikuwa za chini sana.
“Kule kila kitu kipo sawa. Kesho, kijana wetu atafanya maandalizi ya mwisho na wale kuruta wamejiandaa vyema…”
“Mmeshawapa pesa?” Kibwana akauliza kwa kimuhemuhe.
“Tumewapa nusu na nusu nyingine baada ya kazi…”mgeni akajibu.
“Sawa, sasa sikiliza…”
“Enhe!”
“…mpango ubaki vilevile, saa na siku iwe ile ile… Mimi kama nilivyokwambia, kwa kuwa ratiba ya Mzee ninaijua vyema, nitawaambia ni wakati gani mzuri…”Kibwana akasema kwa msisitizo.

“Sawa,we unachotakiwa utuambie masaa sita kabla!” yule mgeni akajibu.
“Sawa, sasa mipango mingine, we pita ofisini kesho kama saa nane hivi!” Ukafuatia ukimya kidogo na baadae milango ya gari ikasikika ikifungwa. Chameleone akajibanza palepale na kulisuudia lile gari likitokomea katika barabara za Masaki.
Hapa kuna jambo kubwa! Akawaza na kujitoa katika ule ukuta. Akaliendea gari lake na kuingia ndani. Mara baada ya kushusha pumzi ndefu, akawasha injini na kuamua kurudi nyumbani kwake kujipanga kwa siku inayofuata.


SIKU ILIYOFUATA

Siku hii haikuanza vizuri kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam.mvua kubwa yenye radi kali ilikuwa ikinyesa. Mzee Chameleon akajikuta anashindwa kubanduka kutoka katika kifua cha mkewe. Joto mujarab la mwanamama huyo lilimfanya alale kama motto kitandani hapo.
“Mwenzetu we huendi kazini?” Mkewe akauliza. Chameleone akainua saa yake mezani na kutazama. Loh! Ilikwishatimu saa tatu za asubuhi. Akakurupuka na kuijiweka tayari. Baada ya chai nzito kutoka kwa mkewe, akaingia katika gari lake na kutia injini moto.
Katika taarifa ya siri aliyopatiwa jana yake na Mkuu wa nchi, kulikuwa na orodha ya majina kadhaa ambayo kwayo ilimpasa kuyafatilia. Akiwa na mawazokichwani mwake, alijitahidi kuendesha gari kwa uangalifu. Akaiacha barabara ya Kawe na kukunja kushoto kuifuata ile ya Bagamoyo kuelekea Mwenge. Mita chache mbele, akakunja kushoto na kutazamana na lango kuu la kuingia katika kambi ya jeshi ya Colito, Lugalo.Askari aliyekuwa lindo akalifuata gari hilo na kuuliza maswali mawili matatu, kasha akaliruhusu kuingia. Chini ya mwembe mkubwa, ndani ya kambi hiyo akaegesa gari lake na kuvuta hatua ndogo ndogo kuelekea katika canteen ya maafisa.
Hakukuwa na watu wengi, lakini pia hakupenda kukaa kiti cha peke yake. Hatua zake, zikamfikisha mbele ya meza moja iliyokaliwa na mwaDanada alievalia sare za jeshi. Cheo chake ca Kepteni kilijionesha pasi na kificho kwa nyota tatu zilizojipanga vyema mabegani mwake.
“Hujambo bibie?” akamsabahi na kumtupia tabasamu lenye bashasha. Yule binti aliinua sura yake na kumtazama Chameleone kuanzia juu mpaka chini.
“Salama, karibu!” akajibu, kasha akaendelea kuburudika kwa supu ya kongolo iliyokuwa mbele yake.
“Karibu baba, nikusaidie nini?” ni sauti ya mhudumu iliyomshitua kutoka katika kumtazama afande yule, kepteni wa kike.
“Nipatie kongolo na Pepsi Cola. Itakuwa shin’ ngapi?” akauliza.
“Shilingi kumi na mbili tu,” mhudumu akjibu.
“Pamoja na hii ya Kepteni Zuhura…” akaongeza kusema. Yule afande aliposikia jina lake likitamkwa, akainua uso na kumwangalia huyo alitajaye kwa mara nyingine.
“Shilingi kumi na sita tu,” akajibu.Chameleone akatoa noti ya shilingi kumi kumi, mbili, na kumpatia.
“Hizo shilingi nne ununue bofulo kwa ajili ya watoto,” akamwambia mhudumu, naye akashukuru huku akitokomea jikoni. Mara baada ya kumalizana na yule mhudumu, akarejesha macho yake kwa afande yule.
“Asante kwa ukarimu wako,” Kepteni Zuhura akamwambia Chameleone.
“Karibu. Hivi ndivyo wanaume tunavyopaswa kuwa, nitapenda kutembelea ofisini kwako kabla sijaondoka kambini hapa leo hii…” Chamelleone akamwambia Zuhura.
“Karibu sana, lakini bahati mbaya, mimi sina ofisi…”
“KIvipi?”
“Ofisi yangu ni uwanjani tu,” Zuhura akajibu.
“Unamaanisha nini, wakati cheo chako kinakutaka kuwa ofisini? Wewe si ni ofisa!” Chameleone akazidi kudadisi.
“Ni kweli, ila mimi ni mkufunzi zaidi kuliko kuwa ofisini,” akamjibu.

ITAENDELEA











GENGE
EP3

Unamaanisha nini, wakati cheo chako kinakutaka kuwa ofisini? Wewe si ni ofisa!” Chameleone akazidi kudadisi.
“Ni kweli, ila mimi ni mkufunzi zaidi kuliko kuwa ofisini,” akamjibu.
“Ooh, safi sana! Je naweza kujua ni mkufunzi wa nini? Kama hutojali,” mtu mzima, Cameleone akauliza.
“Mimi ni mkufunzi katika Sanaa ya mapigano ya ana kwa ana. Huwa nakuja kuendesha mafunzo haya kwa vijana walio katika Special Force,” Zuhura akajikuta anabwabwaja bila simile mbele ya Chameleone. Muda huo huo, staftahi yake ikafika, akaagana na mwanamke huyo kasha yeye akaendelea na kuitupia kinywani supu aliyoagiza. Dakika ishirini baadae, akawa tayari nje ya kantini hiyo ya maafisa, akivuta hatua taratibu kuelekea jengo la utawala.
Hatua zake ndefu ndefu zikamfikisha kwenye jengo hilo, ambalo juu ya ukuta kuliandikwa jina Colito. Akasimama kwa sekunde kadhaa kabla ajaingia katika ofisi hiyo ambayo kwayo, mkuu wa kikosi hicho huwapo.
“Shida!” sauti kutoka nyuma yake ikamgutusha.
Chameleon akageuka taratibu ma kumtazama huyo asemaye. Kijana mmoja, mrefu, aliyependeza katika mavazi yake ya kijeshi, mgongoni mwake alikuwa kabeba bunduki kubwa, AK47. Kijana yule alikuwa kasimama imara, hacheki wala hatikisiki. Chameleon akajua wazi kabisa kuwa anasubiri jibu hata kama hajauliza.
“Aaaann nahitaji kumuona, Kepten Baka Baka,” Chameleone akajibu huku akisimama sawa kutazamana na mwanajeshi huyo.
“Bakabaka ndiyo nani?” yule mwanajeshi mwenye cheo cha Koplo akamtwanga swali Chameleon lakini hakujibiwa.
“Ninyi ndiyo tunaowatafuta, yaani tumewapiga kule kwenu Uganda lakini bado mnaendelea kutufuatafuata, sasa leo umejileta.
“Mimi nina shida zangu za ofisini kijana!” Chameleone akajieleza.
“Hakuna, wewe ni jasusi, umetumwa, sasa nakuweka ndani,” yule askari akasema pasi na mzaha. Sura yake tu haikuwa na chembe ya huruma, macho yake mekundu yalieleza wazi hisia zake za ukatili. Akapuliza filimbi iliyokuwa katika mfuko wake wa shati lile la kijeshi kwa mtindo wa pekee. Sekunde chache tu, wanajesi wenine wawili wakawasili.nao walikuwa katika kombati za jeshi, na mabega yao kuja katika viwiko yalivikwa kitambaa cheupe chenye herufi mbili nyekundu, MP yaani Military Police au kwa lugha nyepesi tungesema, polisi wa jeshi. Walipofika pale, yule bwana akawapa ishara tu, hawakuhoji, wakamchukua na kuondoka naye.
Mzee Chameleone akatupwa rumande maalumu ambayo huwekwa wanajeshi watukutu au wenye makosa mbalimbali. Na huwekwa ndani kwa amri ya wakubwa wao kulinana na kosa lenyewe. Lakini yeye aliwekwa humo kwa kutuhumiwa kuwa ni jasusi. Akaingizwa kwenye jengo moja lililojitenga kando kabisa na mengine. Kabla ya kufika katika jengo hilo walipita jirani kabisa na uwanja wa mazoezi na hapo alishuudia mazoezi makali ya Martial Art yakiendelea chini ya Kepteni Zuhura. Alipotazama upande ule, akagongana macho na mwanamke huyo aliyekuwa amesimama akiwatazama vijana wake.
“Songaaaa! Usiangalie wake wa wakubwa, ala!” Mp mmoja akamkaripia na kumsukuma mbele.
“Vua viatu, saa, mkanda, kofia na kama una pesa zote weka hapo kwenye mess tin,”akaamriwa, naye akatii. Alipomaliza kutekeleza hayo akaingizwa kwenye chumba kimoja ambacho ndani yake alikutana na watu wenine wanne. Watu wale wote aliwatambua kuwa ni wanajeshi kutokana na suruali zao za mabakamabaka. Ni yeye tu aliyekuwa amevaa kiraia, suti ya mtindo wa Kaunda.
“Kaa kwanza huko mpaka tutakapokuchukua kwa mahojiano…” MP mmojawapo akamwambia huku akimsukumia ndani na kuupia kufuli mlango huo wa chuma.
“Mzee, umepotea njia?” mmoja wa wale vijana akamuuliza.
“Nilipotea njia, nikajikuta ndani ya kambi, nikakamatwa na kuletwa huku,” akamjibu.
“Pole sana! Wananchi lazima muhesimu kambi na maeneo ya jeshi, na si kukatizakatiza kama mnaenda chooni,” akasema yule mwanajeshi.
“Sasa mbona aliyekuleta amesema usubiri kuhojiwa?” mwingine akadakiza swali.
“Mi sijui taratibu zenu za kijeshi, mi najua jeshi la wananchi, kwa hiyo sikuona shida kupita kuuliza niendako…” Chamelleone akawajibu na wote wakaanua vicheko.
Sekunde chache baadae, ukimya ukatawala kama mwanzo. Mzee Chameleone akiwa amekaa upande mwingine wa chumba kile, alikuwa kimya kabisa, akiwaza na kuwazua. Kwa namna nyingine alionakama amepewa nafasi ya utulivu ya kufikiri juu ya kile anachokifuatilia tofauti na anekuwa ofisini.
“We! Kwa hiyo… mi siwezi kukaa humu, ngoja nikaungane na wengine…” mmoja wa wale vijana wa jeshi akamwambia mwenzake.
“Unasema nini wewe? Mimi siwezi, kamwe, waje hata wakitaka waniue…” yule mwenzake akajibu.
“Wenzetu washakubali, wako nje saa hii…” akasema mwingine kabisa ambaye daima alikuwa kimya.
“Nimeapa kuilinda nchi yangu, na si vinginevyo!” akasema yule wa kwanza. Mara ukasikika mlango wa chuma ukifunguliwa. Yule mwanajeshi aliyesema hawezi kukaa mule ndani, akasimama haraka na kuuendea mlango wa chumba kile, kwa mikono yake miwili akasika zile nondo.
“Afandeee!” akaita.
“Tulia we muasi, wazalendo tupo kazini, kuilinda na kuipigania nchi yetu,” akajibiwa kutoka katika moja ya vyumba vile ambamo labda askari wale au yule aliingia.
Maneno yale yalimvutia sana Chameleone, akatega sikio kusikiliza kwa maana alishajuakuwa watu hao wanaongea kwa mafumbo. Dakika mbili baadae, akasikia michakacho ya miguu ya mwaDanamu anayetembea kwa hatua za haraka haraka kuelekea mlango ule. Wakati huo huo akamwona yule mwanajeshi pale mlangoni akaisogea nyuma kama sentimeta thelathini hivi. Kufuri likafunguliwa.
“Onana na Chatu haraka sana! Dakika kumi zikipita hujamwona, utarudi humu. Hakuna mwingine aliyechoka kukaa humu?” yule aliyefungua akauliza, huku akiwa anachungulia mule ndani. Macho yake yakagongana na ya Chamelleone. Sekunde mbili kama si tatu, akaingia ndani ya kile chumba.
“We raia vipi? Aliyekwambia hii ni selo ya watu kama wewe nani?” yulemwanajeshi akauliza.
“Selo ya raia iko wapi afande?” Chameleone akauliza.
“Atakujibu aliyekuleta!” akasema na kutoka nje huku akibana kufuli lile.
* * *
Baada ya saa sita kupita, Chameleone akatolewa ndani ya kile chumba na kuongozwa mpaka cumba kingine, akawekwa ndani yake na kutakiwa kusubiri hapo. Nusu saa baadae waliinia wanajeshi wawili. Mmoja alivaa kombati iliyopambwa kwa nyota tatu mabeani mwake na mwingine alivaa vilevile isipokuwa yeye alipambwa na v moja na kitambaa cheupe chenye erufi M na P. Yule kepteni akaketi kwenye kiti cha mbao na yule MP akasimama kando kiukakamavu kabisa.
“Wewe ni nani?” yule Kepteni akauliza. Chameleone akamtazama kwa jicho bay asana, hakujibu.
“Unajua hatupo kwenye utani ee, miaka hii nchi yetu imekuwa na maadui wengi sana. Taarifa niliyoipata ni kuwa wewe ni jasusi mmoja wa nchi hizo...”
“Hujakosea, mimi ni jasusi mmoja wa nchi hizo. Sasa siwezi kuzungumza chochote na wewe, namhitaji mkuu wako wa kikosi…” Chameleone akawaambia. Wale wanajeshi wakatazamana na kuanza kucheka.
“Unafikiri mkuu wa kikosi huwa anawasikiliza watu kama ninyi? Wewe tunakupia risasi kwa sababu umeidharau kambi,” yule kepteni akasema.
Ikawa zamu ya Chameleone kucheka, akacheka kwa sauti kubwa, kisha akanyamaza na kuwatazama.
“Nyie, msinifanye mimi mtoto mwenzenu, wewe mwili wako ushaingia risasi ngapi?” yule Kepteni hakujibu. Na Chemelleone akaendelea kusema.
“Kwa taarifa yako, hapa nilipo nina risasi mbili mwilini, hivyo siogopi risasi hizo unazozisema. Ondokeni hapa, mkamwite mwenye cheo cha juu kuliko ninyi wote…” akang’aka Chameleone. Yule kepten akasimama kutoka pale alipoketi na Chameleone akafanya hivyo.
“Mfundishe adabu!” akamwamuru yule MP, naye akamjia mzee yule akiwa tayari na mkanda wa jeshi mkononi, asijue anayemfuata kipumbavu ni nani katika medani ya upianaji. Hatua moja kabla ya kumfikia, yule MP akauzunusha ule mkanda hewani tayari kushambulia. Chameleone aliruka juu kimo cha ng’ombe, pio moja maridadi likamfanya yule kijana azunuke kama pia na kujibamiza ukutani, kisha akaanguka chini kama mzigo. Kepteni akamtazama yule mzee, kisha akamtazama kijana wake pale chini akiwa hana fahamu. Hakuwa na uamuzi mwingine zaidi ya kutoka nje na kuufunga mlango.
Dakika kama tano hivi wakawasili vijana wengine watano waliojazia miili. Wakafunua mlango wa kile chumba wakiwa na uchu wa kutoa kipigo kwa huyo mzee. Awakukuta mtu zaidi ya yule MPakiwa sakafuni. Hawakuamini, wakatafuta mpaka kwenye droo za kabati, hakuna mtu.
Wakambeba yule mwenzao na kumuwahisha hospitalini. Kishapo taarifa zaikafika kwa yule kepteni, hakuamini anachoambiwa. Akasimama kwa gadhabu na kutoka nje, alipofika mlangoni akakutana uso kwa uso na Chameleone aliyekuwa amesimama mkabala na ngazi za kuingilia katika jengo hilo la utawala. Palepale alipokamatiwa mwanzo. Yule kepteni akapatwa na mshtuko, hakujua nini afanye, arudi ofisini au aende kumkabili mzee huyo? Utata.
“Hivi, we mzee ni mzimu?” akamuuliza.
“Njoo unishike, uone kama mzimu una mifupa!” Chamelleone akajibu na kuanza kupanda ngazi.
“Unaenda wapi?” akaulizwa na yule kepteni.
“Ofisini kwako, tena uje bila kuchelewa!” Chameleone akamjibu na kumpita pale aliposimama, akaongoza na kuingia kwenye mlango wa tatu. Yule kepteni kwa woga akarudi ofisini kwake na kumkuta mtu mzima yule amekwishaketi kitini.
“Keti kijana! Kepteni Mwanachia…” akamwambia, na yule kepteni akaketi huku kicwani mwake kukiwa na mawazo lukuki.
Ni nani mtu huyu? Alibaki kujiuliza.
“Kepteni! Kumbuka kuwa hiki ni chombo cha wananchi, yakupasa kukitii kiapo chako, na si vinginevyo. Mbinu zozote chafuchafu kwa maslahi yako na ya wenzako, zitawagharimu maisha,” Chameleone akasimama na Kepteni Mwanachia naye akafanya vivyo hivyo.
“Wewe ni nani?” Mwanachia akauliza.
“Mzimu! Na usiku huu nitakutokea nyumbani kwako,” Chamelleone akamjibu na kutoka nje. Moja kwa moja akaliendea gari lake na kuondoka eneo lile.
* * *
Dakika thelathini baadae, Chameleone aliegesha gari lake nje ya ofisi yake ya siri, maeneo ya Hospitali ya Ocean Road, jirani kabisa naupande wa nyuma wa Ikulu ya Tanzania. Akaingia ndani na kuketi kitini, akiitazama meza yake iliyokuwa pweke muda wote. Kwanza akatua mezani hapo kabrasha alilotoka nalo garini, kisha akaingiza mkono mfukonina kutoa karatasi ndogo, ya rangi nyeupe iliyofifia, akaiweka kando ya kabrasha lile. Akainuka na kuuendea mtungi wa udongo uliokuwa kwenye kona ya chumba hicho. Ndaniye, akachukua Pepsi Cola moja kati ya sita zilizowekwa majini mtungini humo. Akafungua kwakutumia meno, na kurudi tena kitini.
Kilikuwa ni kibanda tu kikuukuu kilichotelekezwa pembeni kabisa mwa hospitali hiyo maarufu sana. Kama ungejaaliwa kukiona kwa nje basi ungesema ni ‘choo kibovu’. Hakikuwa na paa upande mmoja. Mbao zilizooza, ndizo zilionekana wazi waziwe. Upande mwingine kulikuwa na paa la vigae vikuukuu. Nje, pembezoni kidogo, palikuwa na mti mkubwa wa zambarau. Katika kibanda hicho, ndipo mzee huyu, mwanausalama mwaminifu wa serikali, alikuwa akifanyia mambo yake tofauti na ofisi yake ya kawaida ambayo huwa na wenzi wake wengi.
Akakisoma kile kikaratasi vizuri.

Bayankata itakuwa DDC Kariakoo
Usiku wa leo saa 4:00 usikose.
Mpenzio.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP5

Hapo alikuta askari wa usalama barabarani pamoja na Landrover 109 iliyokuwa ikiifunga ari iliyopata ajali, tayari kuipeleka polisi.
* * *
Usiku huo huo, timu ya watu watano ilikutana katika nyumba moja kubwa huko Mtaa wa
Chole, Oysterbay. Mtaa unaokaliwa na watu wazito, hasa viongozi wa serikali. Ilikuwa huwezi kupita nyumba mbili bila kukutana na geti linalolindwa na polisi.
“Vipi?” Meshimiwa Kibwana Mtokambali akamuuliza Kepteni Mwanachia, aliyekuwa na watu wengine watatu.
“Inaonekana mipango yetu imegundulika,” Mwanachia akasema.
“Kweli kabisa,” akajibu mwanaume mwingine aliyekuwa na mawazo mengi. Waziri Mtokambali, akazunguka sebule huku na kule na aliposimama akawatazama wanaume wale.
“Tulisema mpango huu uwe siri, imekuwaje? Na mmejuaje kama umegundulika?” Kibwana Mtokambali akauliza huku akiketi kitini.
“Kuna mtu tulimkamata siku ya jana pale kambini. Nyendo zake hazikuwa zinaeleweka, tukamweka mahabusu. Baada ya kuhojiana naye, akawa anang’ang’ania kuonana na mkuu wa kikosi,” Mwanachia akaeleza. Macho pima, yakamtoka Waziri, aliyekuwa ndani ya pajama.
“Ukafanyaje?” akauliza.
“Aliondoka! Lakini majigambo yake yalinitia hofu…” Mwanachia akasema huku wenzake wakibaki kimya.Mheshimiwa Kibwana akatulia kimya kwa sekunde chache, kasha akamtazama Mwanachia kwa jicho la woga.
“Mnajua, hili jambo likimfikia Mwalimu, tumeumia. Lakini hapana, halijamfikia, kama ingekuwa limefika, basi mimi ningekuwa mtu wa kwanza kulijua,” akajifariji.
“Huyo mtu inabidi auawe haraka sana kwa kifo chochote kile… ama la, atatuharibia mipango na kitachofuata sote tutachezea kamba,” akaongeza kusema.
“Mkuu, jaribio la kwanza la kumuua limeshafanyika usiku huu…”
“Mmefanikiwa?” akadakiza kwa swali.
“Ametutoroka, gari yake imepondwa vibaya lakini hatujui ametutoroka vipi na wakati gani,” Mwanachia akaelezana kumwacha mheshimiwa Kibwana Mtokambali akiwa kinywa wazi.
“Chatu,” akaita. Mwanachia au kwa jina la kificho ‘Chatu’ akawa makini kusikiliza.
“Nabadili mpango, na naomba iwe hivyo…” akasema.
“Nakusikiliza mkuu,” akawa tayari kusikia.
“Maadam tulibakiwa na siku kidogo, naomba sasa huo mpango ufanyike kesho,” Kibwana akasema. Wageni wakatazamana, kasha wakarudisha macho kwa Kibwana Mtokambali.
“Sijasema hivyo kimakosa, bali kazi yetu iwe kesho kabla Mwalimu hajajipanga zaidi,” Mheshimiwa Kibwana aliongea mengi kwa lugha ya ushawishi na kila mmoja alikubali na kujiweka tayari. Mwingine alikuwa kiandika kila kinachojadiliwa mahala pale kwa ajili ya kumbukumbu za baadae. Walipomaliza wakapeana mikono na wakajiweka tayari kwa kazi. Wakaagana.
* * *
Usiku ule, mara baada ya kuiacha club ya DDC na kupita eneo la ajali, Chameleone alichukua kebu. Safari yake ilikuwa ya dharula kuelekea katika makazi ya Waziri Kibwana Mtokambali. Lengo kubwa lilikuwa ni kwenda kuifanyia upekuzi wa siri nyuma hiyo, usiku huo.
Hapa kuna jambo kubwa kati ya hawa maafisa wa jeshi na huyu waziri, lazima nipate jibu usiku huu! Akawaza akiwa ameketi kiti cha nyuma kwenye kebu hiyo. Akaitazama saa yake, “Ongeza mwendo kijana uniache Hospitali ya Ocean Road,” akamwambia dereva.
Dakika ishirini tu, akawa tayari ndani ya ofisi yake ya siri ambayo hata uingiaji wake hakuna mlinzi wa eneo hilo alikuwa akijua. Ndani ya ofisi hiyo hakutaka kupoteza muda. Alichukua vitu vitatu anavyovihitaji kwa kazi ya usiku huo. Nje tu ya hospitali hiyo alichukua kebu nyingine, moja kwa moja mpaka Mtaa wa Chole akashuka mbali kidogo na kuacha lile gari lipotelee mbali. Hatua zake, zikamfikisha usawa wa lango kuu la kuingilia katika jumba hilo. Asingeweza kupita getini kwa ulinzi ulikuwa hapo. Akazunguka ukuta mpaka pale alipojificha jana yake. Kwa mtindo uleule akaukwea. Kabla hajatimiza azma yake, akiwa tayari keshajitokeza kwa juu, macho yake hayakuamini yanachokiona. Gari lile aliloliona kule DDC, sasa amelikuta hapa pamoja na maari mengine matatu. Hili lilikuwa ni sadfa tu kwake, hakulitarajia. Kwa sekunde chache, ilimbidi kufanya majadiliano nahisia zake. Aingie kama alivyopanga au afanyeje? Hapana, haina haja, akapata jibu. Badala yake akatafuta eneo zuri ambalo linemwezesha kuona kinachoendelea ndani. Akapapata. Usawa wa dirisha la sebuleni. Ijapokuwa kulikuwa na pazia jeupe, zito, kulikuwa na nafasi kati ya pazia na pazia kama sentimita moja hivi, akazitumia. Akachukua darubini yake ya jicho moja na kuiweka tayari. Kupitia jicho lake la kulia akatumia sentimeta ile moja ya pazia kuweza kuona ndani kwa monocular ile ya Kirusia.
Naam, aliweza kumuona vyema Kibwana Mtokambali, waziri mwenye dhamana ya Mambo ya Nje. Hakuweza kusikia nini anaongea lakini alijuwa wazi kuwa kuna jambo muhimu linajadiliwa. Chameleone hakutapa kupoteza hata jambo moja. Amekosa sauti, akose hata picha? Haiwezekani. Alichukua kamera yake ndogo aina ya Cimena na kuiweka lenzi yake katika kifaa hicho. Akaweza kupata picha ya KIbwana Mtokambali. Wengine aliweza kupata picha zao wakiwa wanaagana na mheshimiwa huyo. Japokuwa picha hizo hazikuwa nzuri sana, lakini zilipatikana.Kwa haraka akakunja kionambali chake chenye jicho moja na kukitia mkobani. Tayari alimmaizi yule mmoja aliyeonekana kuwa ni karani wa kundi lile. Akazimezea mate karatasi zile, akiasubiri aone, kama zinahifadhiwa kwa mheshimiwa au zinaondoka na mtu huyo. Wale watu kule ndani wakaagana, karatasi zile, zikaondoka na yuleyule aliyeziandika. Chameleone, akajitoa pale ukutani na kuvuka barabara. Akajificha nyuma ya miti mikubwa huku akitazama magari yale yakitoka. Tayari alikwishajua ni lipi analolihitaji kati ya yale. Hakuwa na haraka, alifanya kazi yake kwa utulivu na kujiamini.
Gari la tatu, Datsun la buluu, ndilo alikuwa akiendesha karani wa kikao kile. Alipotupa jicho ndaniye, akatanabahi kuwa mtu huyo yu peke yake. Jambo jema zaidi ni kuwa, gari lile lilikuwa la mwisho. Akamshukuru Mungu. Kwa hatua za haraka akaingia barabarani na kukamata mlango wa nyuma wa Datsun ile, pick up. Akakwea kwa sekunde tatu tu na kutua ndani ya bodi hilo bila kufanya kishindo huku gari likiongeza mwendo. Safari ya gari lile ilikuwa ndefu, Chameleone aliendelea kuvumilia na kila alipoinua kichwa kutazama nje ya bodi lile, aligundua kuwa hakuna dalili ya kusimama.
Anaenda wapi? Akajiuliza huku akipiga moyo konde kusubiri mwisho wa safari hiyo.
Alipochungulia tena, akagundua kuwa tayari walikuwa wakipita uwanja wa ndege kuelekea Pugu. Akatazama saa yake, ilitimu saa kumi alfajiri. Lile gari likaanza kupunguza mwendo wake. Akajua muda wowote watasimama, akajiandaa kuteremka kwa upole kama alivyopanda. Naam! Mara tu baada ya kupita lango kuu la jeshi, kikosi cha wa wanaanga namba 603, lile gari likaiacha barabara na kusimama kwenye kichaka cha mikorosho. Mzee huyu alikuwa na akili nyingi sana mpaka nyingine zilimzidi. Alikuwa na uwezo wa kukusoma maamuzi yako ya dakika mbili mbele. Wakati Datsun lile likikanyaga udongo na kuingia kando kwenye mikorosho, yeye alikuwa tayari akining’inia katika mlango wa nyuma, akajiachia na kufika mchangani kwa utulivu. Kutokana na giza, hakuweza kuonwa na dereva, ukizingatia ilikuwa usiku. Akajificha nyuma ya moja ya mikorosho ile.
Ikapigwa honi mara tatu, ikatulia. Sekunde moja tu, aliibuka mtu kutoka upande ule wenye mikorosho mingi. Upande ambao kulikuwa na nyumba sita tu za jeshi. Na nyumba hizi ndizo chanzo cha jina Majumba Sita. Mtu yule , mrefu, mwenye mwendo wa kikakamavu, aliyevalia nguo za jeshi, alijitoma ndani ya gari lile. Chameleone akasubiri kuona kama kuna mwingine atajitokeza, hakuwepo. Alipotaka kujitokeza ili akaingie tena kwenye gari kwa mtindo uleule. Mlango ukafunguliwa na yule jamaa akateremka, akaagana na dereva na kupotelea kichakani. Lile gari likarudi barabarani taratibu na Chameleone hakupoteza muda, akadandia kama mwanzo. Safari ikaendelea. Dakika tano baadae, gari ikasimama mbele ya nyumba moja za jeshi, eneo la Banana, PMQ. Chameleone, tayari alikwishashuka na kujipenyeza uvunguni mwa pick up hiyo. Ijapokuwa ilikuwa na nafasi ndogo uvunguni, lakini alijitahidi kujisweka.
Yule bwana akateremka huku akipiga mruzi kufuatisha melodia ya wimbo mmoja wa Kisukuma. Mara baada ya kufunga mlango wa gari, akavuta hatua na kuingia ndani kwake. Chameleone akajito uvunguni na kujibanza kwenye kiambaza cha ukuta wa kuingia jikoni ambapo mtu yule alipita. Akatulia kuona hatua inayofuata. Taa za jikoni zikawashwa na dakika mbili baadae zikazimwa. Akasubiri kuona hatua nyingine ya mtu huyo. Dakika kama tano hivi akasikia maji yakimwagika chooni. Alilitegemea hili, kwa kuwa hakumwona mtu huyu hata nukta moja akienda kujisaidia. Utulivu ukaja, akajua sasa kumekucha. Akaufikia mlango akanyonga kitasa, akausukuma ndani. Upo wazi.
Wanajiamini sana! Akawaza akiwa anamalizia kuingiza kiwiliwili chake ndani, akaurudishia. Akaingiza mkono kwenye mkoba wake alioupachika vyema kiunoni, akachukua barakoa yake ya kuzuia gesi akaivaa. Mkono mwingine tayari ulikuwa umekamata chupa ndogo. Chupa ile ilikuwa na maandishi ya kikemia, CHCL3, basi. Haikuwa na maandishi mengine. Chameleone akaifungua na kuiziba kwa kidole chake. Akavuta hatua mpaka kwenye milango ya vyumbani na kuiruhusu gesi ile ifanye kazi. Akaoneza na kichupa kingine cha mtindo uleule. Watu wote walioivuta gesi ile, wakalala fo fo fo. Alipojiridhisha, akaingia chumba cha yule anayemtaka. Akamkuta tayari anakoroma tu, pembeni akiwa na mkewe aliyelala kihasarahasara, akiwa hana chochote mwilini mwake.
Ama kweli, ukiolewa, sharti ulale bila nguo! Akajisemea moyoni huku hisia za mwili wake zikipigana na dhamira, pepo. Mwanga wa taa za nje, ulimwezesha kuona yote haya. Katika droo kubwa, pembeni mwa kitanda cha yule bwana, palikuwa na zile karatasi, akazitazama zilivyolala, akazichukua na kufungua ndani. Zilikuwa mbili tu, zenye maandishi machache, akazisoma haraka haraka. Moyo ukampasuka kabla hata hajafika mwisho, muda unakwenda, akitweta. Alimtazama yule bwana pale kitandani, akatamani ambebe amtie garini na kumpeleka Ikulu kwa Rais. Haiwezekani, akatafuta karatasi mule ndani na kupata, akanakili yote yaliyoandikwa. Alipomaliza, akazihifadhi mkobani na kuziacha zile halisi. Akachukua kamera yake na kujaribu kuzipiga picha, ikiwa ni moja ya kuhifadhi kumbukumbu. Maana alijuwa akizichukua, atakuwa amewagutusha kwenye mpango wao dhalimu. Alipomaliza, akahakikisha ahachi alama nyuma yake. Akaondoka.

PAMBAZUKO

CHAMELEONE HAKUWA na furaha hata kidogo alfajiri hii. Tayari alikuwa amekwishaweka mipango yake vizuri. Mpaka dakika hiyo ni yeye tu aliyekuwa akijua nini kitatokea pindi pambazuko la siku hiyo likifika. Alitamani asimamishe saa,lakini hakuweza. Aliondoka kutpoka katika ofisi yake ya siri na kuelekea Msasani alfajiri hiyo. Breki zake zilimsimamisha mbele ya geti la makazi binafsi ya Rais ambako ni jana yake tu alikuwa hapa. Akateremka na kujitambulisha kwa walinzi. Wakamkaribisha na kuelekea ndani ya jumba hilo.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP6

Breki zake zilimsimamisha mbele ya geti la makazi binafsi ya Rais ambako ni jana yake tu alikuwa hapa. Akateremka na kujitambulisha kwa walinzi. Wakamkaribisha na kuelekea ndani ya jumba hilo.
“Ila mzee hajaamka,” yule askari aliyekuwa akimsindikiza akamwambia.
“Usijali,” akamjibu huku tayari akiwa kwenye kibaraza, amezungukwa na askari takribani wane wenye silaha nzito. Kengele ya mlango ilimwamsha mfanyakazi wa ndani, akaufikia mlango. Akapewa taarifa hiyo, naye kadiri ya maelekezo yake ya kikazi akamwamsha mheshimiwa. Sebuleni hapo akabaki Chameleone na Rais tu. Saa kumi na mbili kasoro robo asubuhi.
“Mheshimiwa! Twende ofisini, kuna mambo ya kushughulikia haraka kabla ofisi hazijafunguliwa,” akamwambia.
Rais, akiwa ndani ya pajama, alikuwa kama aliyepigwa soti ya umeme.
“Ofisini?” akauliza.
“Ndiyo Mkuu! Tuna dakika tano tu, chukua vitu vya muhimu vya kutumia ofisini.
Ukishakamilisha hilo, utarudi kujiandaa,” Chemeleone akaeleza huku akianalia saa kila wakati.
“Sawa, wasiliana na watu wa itifaki ili taratibu za kawaida zifuatwe,” mkuu wa nchi akasema.
“Samahani kwa usumbufu, ila nipo kazini. Mkuu, unatakiwa kuondoka na mimi tu. Nataka nikakupe majibu ya kazi uliyonipa, haraka iwezekanavyo,” Chameleone akasema, mara hii kwa msisitizo zaidi. Kwa kusikia hili, Rais, hakuwa na ubishi. Kwa kuwa alikuwa akimwamini namba moja wake, akaingia chumbani na kutoka na mkoba mdogo. Dakika hizi chache, alivaa suruali na shati la kawaida tu. Wakachukuzana mpaka kwenye gari alilokuja nalo mwanausalama huyo. Askari walinzi walishtuka na kutaka kujua kulikoni Rais aondoshwe namna hiyo. Lakini yeye mwenyewe akawataka kutulia na kuendelea na ulinzi kama kawaida. Wakaondoka.
“Niambie kijana!” Rais akaanzisha mazungumzo.
“Hali ni mbaya mkuu, hutakiwi kuwa nyumbani wala Ikulu kwa sasa,” Chameleone akamwambia huku akiongeza mwendo.
“Umegundua nini?” akauliza.
“Huu ni mpango kabambe wa kukuondoa madarakani, kushindwa kwao mara mbili, wameona hakutoshi. Safari hii inaonekana wamejipanga kwa nguvu kubwa. Usiwe na wasiwasi hawataweza,” Chameleone akamtoa hofu mkuu wake.
“’Nini kinawasumbua? Umekwishajua?” akauliza maswali mawili kwa mara moja.
“Sababu hasa sijajua, ila nina hakika nitapata jibu tu, kwa kuwaninajua nani wakuanza naye,” Chameleone akamwambia huku akipunguza mwendo. Tayari alikuwa amewasili eneo la Magogoni, akaegesha gari ufukweni. Ilikuwa yapata saa kumi na moja alfajiri. Kutoka kwenye buti la gari, Chameleone akachukua jambakoti na kumvika mlindwa wake. Pamoja nalo, akamvika kofia kubwa, pama, iliyosukwa kwa miaa. Kisha akamwongoza mpaka kwenye mtumbwi mmojawapo kati ya mingiiliyoegeshwa ufukweni hapo.
“Ingia mzee, tunavuka ng’ambo!” akamwambia.
“Tunavuka na mtumbwi? Si tungechukua boti hapo polisi, mbona wako jirani tu!” Rais akamuuliza mwanausalama wake.
“Mzee, nahesimu mawazo yako, ila kwa sasa hayana nafasi.
Katika mtumbwi huu, walikuwa wao wawili tu. Safari ikaanza, Chameleone akapiga kasia kuelekea upande wa pili wa bahari. Mawimbi hayakuwa haba, yaliwasukasuka huku na huko lakini mtu mzima huyu alikuwa hodari katika kazi yake. Ukimya ulitawala, giza likatamalaki. Dakika thelathini na nne hivi, akaegesha mtumbwi huo pembezoni mwa bahari, upande wa pili, Kigamboni. Chameleone akamchukua mlindwa wake na kupita naye kwenye vichaka akikwepa kukutana na wavuvi na wachuuzi wa samaki. Mwendo kama wa dakika ishirini hivi kwenye vichaka vidogovidogo ukawatosha kuibukia katika barabara ya vumbi, mbali kidogo na bahari.
“Tunakwenda wapi hasa?” Rais akauliza.
“Tunakwenda mahali salama,” akamjibu huku akisimama na kumtaka mkuu wake asimame pia. Mbele yao kulikuwa na kitu kama kichaka kikubwa. Akavuta hatua mpaka pale, akapapasapapasa na kutengeneza upenyo mkubwa tu.
“Ingia twende!” akamwambia rais, na kuhakikisha ameinia kasha akarudishgia kama palivokuwa mwanzo. Akazunguka na kuingia upande wa pili. Lilikuwa gari. Gari dogo aina ya Beetle, au wengi waliliita kobe. Akalitia moto, akaliondoa eneo lile kwa kupita porini kwa porini kufuatisha njia nyembamba. Chameleone alipenda kulificha gari hilo mahali hapo kwa ajili ya kazi zake za siri au moja ya kujilinda inapobidi.
Safari yao ikaishia huko Gezaulole, katika nyumba ya ukubwa wa wastani, iliyojenwa kwa udongo na kusakafiwa vyema kwa saruji. Juu ilipauliwa kwa bati na kuzunukwa kwa uwa wa mianzi.
Chameleone akaegesha gari upande wenye korongo na kuifanya nyumba ile ionekane kwa juu. Wakateremka na kuingia ndani ya nyumba hiyo pweke. Haikuwa inakaliwa na mtu, lakini ilikuwa safi kuanzia nje mpaka ndani. Chumba kimoja wapo kiliteuliwa kumhifadhi mheshimiwa kwa muda. Kilikuwa kimetimia, redio ndogo, kitanda cha BANCO, mtungi wa maji baridi pamoja kiti kimoja.
“Karibu mafichoni mzee! Najua umeshtuka kwa yote niliyofanya lakini sikutaka kumhusisha mtu yeyote katika hili kwa sababu ya usalama wako. Kuna baadhi ya wanajeshi katika vikosi vyetu wameunda kikundi cha uasi. Ndani yao kuna makomandoo wawili na maafisa kadhaa ambao wameshiriki kikamilifu katika kumng’oa Amini. Unawafahamu vyema, japokuwa wachache huwajui. Wamepanga mpango kababe ikiwemo kuvamia Ikulu na kukufurusha mbali,” Chameleone akamweleza Rais.
Akampatia ile karatasi aliyonakili, na kumpa kama dakika kumi za kuisoma. Akaisoma na kuirudia mara kadhaa. Alipomaliza akaitua kando na juu yake akaweka bakora yake ambayo daima haiachi.
“Hakuna kingine, ni uroho wa madaraka… Afrika sijui tutaelimika lini! Wanataka kwenda Ikulu. Ikulu kuna nini? Ni matatizo tu na msongo wa mawazo siku zote, labda kama unataka kwenda na kutumia mali za Watanzania kwa manufaa yako…” akazungumza kwa ukali kidogo. Akatulia kimya klwa sekunde kadhaa. Akaomba karatasi na kalamu, akaandika ujumbe fulani wenye maneno machache tu. Akaikunja ile karatasi na kumpatia Chameleone.
“Mkabidhi waziri wa ulinzi,” akamwambia. Chameleone, akaipokea na kuiweka mfukoni.
“Mkuu, mimi ninakwenda kuona hali halisi ilivyo. Hapa ndani pana kila kitu. Nitarudi baada ya saa nne kukuletea taarifa kamili. Unaweza kupata kinachojiri kwa kusikiliza redio hiyo ndogo kwa sasa,” Chameleone akamwambia rais na kasha akatoka ndani ya nyumba ile. Akahakikisha milango yote imefungwa. Kwa kutumia njia zake za siri, akawasili pwani ya Kigamboni na kuvuka mpaka upande wa pili.
Jua la saa kumi na mbili na nusu asubuhi lilikwishaanza kulipendezesha anga kwa miale ya dhahabu. Chameleone alivuta hatua pembezoni mwa ukuta wa Ikulu, kandokando ya bahari kuelekea hospitali ya Ocean Road. Alipoizunguka na kuingilia mlango wa nyuma, akatokea kwenye ofisi yake ya siri, akaingia na kujifungia. Akachukua redio yake ndogo na kuiwasha, akatafuta idhaa ya taifa na kutega sikio kusikia nini kinaendelea. Kipindi cha Majira cha asubuhi kilikuwa kikiendelea.
Hakuna wanachojua hadi sasa! Akawaza. Hakuona haja ya kupoteza muda, akatoka na kupenya ndani kwa ndani mpaka katika jengo la Ikulu. Akawakuta watu wakiendelea na shughuli zao za asubuhi ikiwa na kuweka vizuri mazingira kwa kuwa hiyo ni ofisi ya rais. Akasalimiana na kupita moja kwa moja mpaka katika chumba cha usalama. Humu ndani alimkuta binti mmoja tu aliyekuwa akifuta vioo na kuweka kabrasha vizuri katika rafu zake.
“Selina!” akaita.
“Bee!” akaitika huku akigeuka kumwangalia mtu huyo. Akampa heshima yake na kusubiri kupata maagizo.
“Mwite Simbaulanga na James…” akamwagiza.
“James yupi?” Selina akauliza.
“James Msambamagoya,” akamweleza.
“Msambamagoya hayupo kazini, aliondoka jana usiku wa saa tano na hakurudi mpaka sasa,”
“Alisema anaenda wapi?”
“Alituambia tu kuwa ana dharula,” akajibiwa.
Chameleone akabaki kimya kwa sekunde kadhaa, kichwa chake kikawa kama kimepigwa shoti ya umeme.
“Ok, chukua hii barua, moja kwa moja ifikishe kwa Waziri wa ulinzi, kasha urudi hapa ninakuhitaji,” akamwambia mwaDanada huyo. Selina aliipokea ile bahasha na kuiacha ofisi hiyo.
* * *

BANANA BAR

James Msambamagoya aliegesha gari lake aina ya Ford Hungrier pembezoni kabisa mwa baa maarufu iliyojulikana kwa jina la Banana, karibu na kambi ya jeshi kikosi cha Wanaanga. Ndani ya gari lake alikuwa yeye na mtu mwingine, mwaume, mrefu, mweusi.
“Kama nilivyowaambia, hatutakiwi kukosea hata kidogo,” James akamwambia yule mtu.
“Hatuwezi kukosea hata kama tumefanya kwa uharaka. Simbamwene keshaenda Msasani kama ulivotuambia. Na nyuma yake kafuatiwa na wapiganaji mahiri endapo kutatokea rabsha yoyote,” yule mwanaume mweusi akajibu.
“Safi! Pale hatopata upinzani kwani waliopo ni polisi wa kawaida, hawajui medani za vita,” James akaongeza kusema.
“Halafu, kikosi namba mbili tayari kimeshafika Magogoni, na klila mmoja ameshachukua position yake,” yule mwanaume akaeleza zaidi.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP7

Halafu, kikosi namba mbili tayari kimeshafika Magogoni, na klila mmoja ameshachukua position yake,” yule mwanaume akaeleza zaidi.
“Safi sasa, ngoja niwaone akina Mwanachia nijue nini kinaendelea…” James akamwambia yule mtu. Kisha akateremka garini na kufuatiwa na yule bwana.
Ndani ya baa hiyo kulikuwa na watu wane tu, waliojifungia katiak cumba maalumu. Mazungumzo machache lakini yenye unyeti yalikuwa yakiendelea.
“Mheshimiwa rais yuko tayari kuingia Ikulu, tayari amefika kwa mara ya mwisho katika ofisi yake ya zamani…” Mwanachia akalieleza jopo, “Chatu, kama tulivyopanga, mara tu tukishika hatamu, nafasi yako ni Waziri wa Ulinzi, utahakikisha majesi yote unayatiisha kwa masaa machache. Kumbuka kuwaweka tayari watu wetu katika kila kamandi,” akaongeza kusema.
Mjumbe mwingine akatazama saa yake. Saa moja na dakika sita asubuhi, “Jamani, mbona Tito hafiki?” akauliza.
Swali hili lilimgutua kila mmoja, hakuna aliyemaizi kuhusu mtu huyo kutokuwapo.
“Si kawaida, na kumbuka ni yeye mwenye dondoo za vikao vyetu, ni mtu muhimu, James , kabla hujakaa vizuri naomba umfuatilie huyu bwana ujue nini kimemsibu mpaka sasa hajafika,”
Mwanachia akatoa maagizo. Kwa kuwa kikao kilipokuwa kikifanyika na nyumbani kwa Tito Mwakibinga hakukuwa mbali, haikuwa vigumu kufika. James, mtumishi wa idara ya usalama wa taifa, mlinzi wa karibu wa rais aliondoka. Huyu ndiye aliyekuwa akitoa siri zote za Ikulu na mienendo ya rais ikiwamo ratiba zake za kila siku. Ni yeye aliyewaambia kuwa siku hiyo rais atakuwa nyuimbani kwake Msasani na si Ikulu. Ni yeye aliyewapa mpaka majina ya walinzi wa nyumba siku hiyo. Yeye huyo huyo ndiye alikuwa masterplan wa mchezo huu. Akiwa anajua fika nini kitatukia siku hii, aliiacha ofisi na kuaga kuwa ana dharula, akatoweka usiku.


MAKAZI YA RAIS, MSASANI

Jairosi Simbamwene, komandoo wa Jeshi la wananchi aliwasili eneo yaliyopo makazi binafsi ya rais. Akapita kando kando ya maua marefu kulielekea lango kuu la nyumba hiyo. Alitembea kwa kujiamini, pasi na wasiwasi wowote huku nyuma yake akifuatiwa na Jeep moja jeupe lililokuwa na wanajeshi, waliovaliovalia mavazi yao ya bakabaka. Vijana hao wote walikuwa na bunduki za kivita mikononi mwao. Hakuna aliyewashangaa, kwani eneo hilo kuwa na askari ni kawaida. Lile jeep lilikunja kona kali likitokea upande wa Kawe na kunyoosha kuelekea katikajumba hilo.
Walinzi wa nyumba ya rais, walijitokeza kulitazama gari hilo lililokuwa likija kasi. Mmoja wao akawahi kibandani ili kuweza kupia simu mahali salama. Hakufanikiwa. Komandoo Simbamwene, alitua ardhini kutoka juu ya kibanda kile. Pigo lake likatua kicwani mwa askari yule, akaenda chini. Kabla wenzake hawajafikiri cha kufanya, tayari alivingirika na kumtia nwara mwingine huku bastola yake ikikoroma na kumvunja mguu wa tatu. Lile Jeep likagonga geti na kukunja kona kali upenuni mwa nyumba ile. Vijana wa jeshi tayari walikuwa chini wamekwishawadhibiti walinzi katika kona zote. Wakawakalisha chini huku mitutu ikiwa vichwani mwao.
Komandoo Simbamwene, aliifikia sebule kubwa ya jumba hilo akiwa na vijana wawili wenye bunduki kubwa za AK 47. Moja kwa moja mpaka chumba cha Mkuu wa nchi, hakuna mtu. Wakasaka kila chumba , kila kona, kila banda. Hakuna mtu.
Kipigo kikaanza kwa walinzi kushinikiza waseme, lakini wote walikiri kuwa hawajui. Zaidi waliwaambia kuwa tangu wameingia lindoni hakuwapo nyumbani.
Dakika kumi zilizofuata, magari matatu yakiongozwa na pikipiki kubwa la polisi yalilikaribia lango la jumba hilo. Kwa uharaka wa ajabu, wale wanajeshi wakawaficha walinzi wote. Simbamwene akamchukua mmoja aliyekuwa naye ndani.
“Fungua geti, ole wako ulete hila yoyote nakufumua kichwa chako,” akamwambia. Yule askari akatembea haraka na kufunua geti. Yale magari yakaingia uwanjani na kukuta lile jeep limeegeshwa.
Ndani Benz ambalo daima upanda rais, alikuwa ameketi Simbaulanga na nyuma ya usukani kulikuwa na Chameleone. Magari mengine mawili yalikuwa na askari wenye silaha nzito. Walijua wanaenda kufanya nini, hivyo walikuwa tayari. Msafara uliposimama tu, vioo viliteremshwa na risasi zilianza kurindima. Kwa ustadi wa hali ya juu. zilikuwa dakika tatu za mabishano ya risasi. Vijana waliokuwa wakiongozwa na Simbamwene walidhibitiwa kikamilifu. Chameleone alishuka garini, bastola Smith and Wesson ikiwa imefumbatwa vyema katika kiganja cha kulia. Kwa uharaka na ujuvi mkubwa alijitupa katika maua na kutambaa kuelekea ukuta wa baraza ya nyumba hiyo. Alipoufikia, alisimama na kutembea kwa kunyata. Hatua kama nne hivi zilimfikisha katika mlango wa nyuma.
Akaupiga teke, ukafunguka. Bastola ya Simbamwene ikabanja, lakini shabaa aikuwa makini. Chameleone akajirusha chini kiufundi. Mara tu alipotua sakafuni, bastola yake ikakohoa. Risasi moja iliyoipita mtambaa panya ikakipata sawia kiatu cha Simbamwene. Aliporuka sarakasi akajikuta amechelewa. Maumivu makali yakapita kwenye unyayo wake. Akatoa tusi zito. Kwa kuchechemea, akamwendea Chameleone na kumuwahi kwa teke moja la mkono, bastola ikamtoka. Teke linguine, akalidaka na kumvuta mguu. Simbamwene aliona Chameleone anapigana kwa mbinu za kitoto sana. Akamdarau, akamkamataukosi wa Kaunda suti yake na kumuinua lakini mwanausalama yule hakumuachia mguu; akamng’ata. Simbamwene akapiga unyende na kumwachia Chameleone. Akasimama haraka, akainua kiti na kukirusha, kikatua kichwani mwa Simbamwene. Chameleone akaruka sarakasi na kuikamata tena bastola yake. Alipoinyoosha kupata shabaha, Simbamwene kwa weledi wa kushangaza, alichumpa na kupita kwenye kioo. Akaangukia kwenye maua nje ya nyumba. Risasi nne za Chameleone zikamkosa na kuchimba sentimeta chache kando ya dirisha.
Nje ya nyumba ile, Simbamwene, hakupoteza hata sekunde, aliruka sarakasi na kutua nje kabisa ya wigo huku akikoswakoswa na risasi za wanausalama. Vijana wake wote walikuwa tayari mikononi mwa serikali. Chameleone na vijana wachache wakatoka nje kumtazama komandoo huyo wasimwone.
“Hawezi kucheza na mimi!” Chameleone akamwambia Simbaulanga huku akiiweka vyema bastola yake. Walipotokeza nje kabisa, majirani wakawapa ishara kuwa ‘amekimbilia huku’. Simbaulanga na Chameleone wakachukua Honda kubwa lililokuwa limeegeshwa nje ya nyumba mojawapo. Mwendo wao wa kasi ukawafikisha katika barabara kuu itokayo Kawe kuelekea Kinondoni. Katika barabara hiyo ya vumbi, walimshuhudia Simbamwene, akimtoa kwa nguvu Mwarabu mmoja aliyekuwa na familia yake garini. Alipowaona wabaya wake, akamvuta mama wa Kiarabu na kumweka ngao mbele yake, na domo la bastola lilikuwa limegusa sikiole.
“Mkithubutu namuua!” Simbamwene akawaambia. Tayari Chameleone alikuwa kasimama chini na bastola yake ikimwelekea mtu huyo.
“Mwache huyo mama aende!” akamwamuru.
“Simuachi!” akajibu huku akimvuta kinyumenyume mpaka katika mlango wa gari.
Simbamwene, akapia risasi moja hewani na kumsukuma kwa nguvu yule mwanamke kuelekea kwa Chameleone. Chameleone akamkwepa na klufyatua risasi moja iliyopita kioo cha nyuma, sentimeta moja tu kando ya mwamba wa kushoto wa kioo cha nyuma. Simbamwene, mara baada ya kumsukuma yule mama wa Kiarabu, aliwahi kujitoma ndani ya gari, nyuma ya usukani. Kutokana na akili za mtyu mzima Chameleone alijua wazi nini komandoo huyo atafanya. Risasi yake ilipenya kisogoni na kufumua vibaya paji la uso la Simbamwene na kuchafua kioo chote cha mbele kwa damu na ubongo.
Chameleone bado alikuwa kasimama huku mikono yake ikiwa bado imelenga bastola upande uleule kana kwamba anasubiri mtu huyo ateremke. Akasonya na kushusha bastola yake taratibu.
“Amekwisha!” Simbaulanga akamwambia Chameleone.
“Yes! Nilikwambia hawezi kucheza na Chameleone.

WAKATI HUO HUO

Kambi ya Jeshi ya Twalipo

Waziri wa ulinzi aliwasili na kukaribishwa na mkuu wa kambi hiyo. Hali ya kambi haikuwa shwari. Mapinduzi.
“Nchi imepinduliwa?” yule Mkuu wa kambi akamuuliza waziri.
“Hapana, lakini nimekuja kwa kuwa nahitaji kukutana na vijana wako wanaohamasisha mapinduzi,” waziri akasema.
“Loh! Nahisi tu hawapo. Watu niliokuwa nawahisi, wote sijawaona kambini tangu jana usiku,” Mkuu wa kambi akajibu.
Kikao hiki cha siri kilifanyika ndani ya ofisi ya mkuu huyo. Baada ya mazungumzo mafupi, wakafika watu wengine watatu kutoka idara ya utambuzi ya usalama wa taifa. Tarumbeta la dharula likapigwa, askari wote wa vyeo vyote wakafika na kujipanga katika uwanja mkubwaunaotumika kwa gwaride. Lengo la waride hilo lilikuwa kwamba, yeyote ambaye hangekuwepo basi angehusishwa moja kwa moja na kadhia hiyo. Mtindo huohuo pia ukafanyika katika kikosi cha wanaanga Banana na kile cha Mgulani.
Orodha ya wasiokuwepo na vyeo vyao ikaandikwa, kasha vikapangwa vikosi vya ulinzi katika maeneo nyeti ya serikali. Ikatangazwa, yeyote aliyewekwa katika orodha hiyo, atakapoonekana popote akamatwe, ikiwa pia kuwatafuta popote walipo.
Waziri wa ulinzi akatumia pia muda huo kuitisha kikao na Mkuu wa majeshi na kebineti yake kuzungumza juu ya nini kimesukuma yote haya kutokea.
* * *
ITAENDELEA
 
GENGE
EP8

Waziri wa ulinzi akatumia pia muda huo kuitisha kikao na Mkuu wa majeshi na kebineti yake kuzungumza juu ya nini kimesukuma yote haya kutokea.
* * *
“… Dar es salaam. Komandoo mmoja wa jeshi la Tanzania ameuawa na askari wengine kumi na mbili kukamatwa leo asubuhi baada ya kurushiana risasi na wanausalama, katika jaribio la kutaka kuipindua serikali. Habari kamili juu ya tukio hilo tutawaletea hivi punde.
Wakati huohuo, Makamu wa Rais ametangaza hali ya tahadhari kwa wananchi kutotembea ovyo kama hauna shughuli maalumu…”
Taarifa ya habari kwa ufupi ya saa mbili asubuhi ilitangaza.
Waziri wa mambo ya nje, Meshimiwa Kibwana Mtokambali akainyanyua redio yake na kuirusha ukutani. Redio ile ndogo ikapasuka vipande viwili huku betri zake zikitawanyika huku na huko. Akatoa sonyo refu lililofuatiuwa na ngumi iliyotua juu ya meza na kuacha vitu visivyo na nguvu luparanganyika.
“Wanatuzidi wapi?” akauliza kwa sauti kana kwamba kuna mtu wa pili, kumbe la.
Kuchanganyikiwa. Siku hii ilikuwa ni tofauti kabisa na nyingine. Kwanza waziri huyu alifika mapema kazini kuliko hata katibu wake. Alivaa suti ya gharama sana aliyoinunua huko ughaibuni, maalum kwa siku maalum. Siku hiyo, ilikuwa hii. Kila mara alifanya mazoezi ya kutabasamu kama rais, kuketi na kujaribu kuongea peke yake kama rais. Loh! Asali ikageuka shubiri. Mtokambali hakukubaliana kabisa na kile alichokuwa anakisikia redioni.
“Kikosi changu hakiwezi kushindwa kamwe,” akajiapiza huku akisimama. Dakika hiyo hiyo, simu ya mezani ikaanza kuita kwa fujo.
Nani huyu? Akajiuliza. Akaukamata mkonga wa simu tayari kusikiliza, moyowe ukaanza kudunda bila mpangilio kama saa mbovu. Akasukuti kwa sekunde kadhaa, simu ile ikakatika.dakika moja baadaye ikaanza kuita tena. Kwa mkono ulojaa kitetemeshi, akauweka sikioni mkonga ule.
“Mheshimiwa, mipango imevurugika.
Yatupasa kukutana shimoni haraka iwezekanavyo,”
Sauti ya upande wa pili ikamwambia.
Bila kificho, aliielewa vyema sauti hiyo, Chatu. Akaushusha ule mkonga na kuuweka mahala pake. Akaanza kuchachawa. Hakujua nini anatakiwa kufanya. Alichoamua ni kuacha kila kitu na kuondoka. Alipoufikia mlango tu, simu ile ikaita tena, akasimama huku mkono wake ukiwa kifuani upande wa moyo.
Nani tena? Akajiuliza. Akarudi na kuinyakuwa simu, akaiweka sikioni.
“Unatakiwa kufika Ikulu haraka sana kwa kikao cha dharula…”
Toooba! Moyo wa Mtokambali ukapiga samasoti. Akazidi kuchanganyikiwa. Aende wapi? Shimoni au Ikulu? Utata. Akabaki katika mbutwaiko, katikati ya ofisi, akasimama kimya.
Nisipoenda Ikulu, nitakuwa nimejichongea, na vipi kama nikienda wakati wameshaijua hila zangu? Watanitia mkononi! Akawaza. Hata hivyo akajikuta hana la kufanya. Akatoka ofisini kwa mwendo wa kinyonge na kulifikia gari la ofisi, Land Rover 109.
“Nifikishe Ikulu,” akamwambia dereva na yeye akaketi kiti cha nyuma akiwa na mawazo.
* * *

Shimoni

Katika msitu wa Kazimzumbwi, watu nanne walikuwa wamekutana katika nyumba moja kuu kuu, katikati ya shamba kubwa sana. Sura zenye wasiwasi zilitawala. Hakuna aliyekuwa akiongea kati yao badala yake, kila mmoja alikuwa anaomba ombi lake. Ni mtu mmoja tu alikuwa hajafika bado, Mtokambali, ambaye mchana wa siku hiyo alitegemea kutangazwa ‘Mwenye Nchi’.
“Nini kimetokea? Wapi tumezidiwa?” Chatu akauliza kwa kuvunja ukimya.
“Hata sielewi, yaani sijui… Simbamwene kauawa!” James akasema kwa mshangao. “Najua ni nani aliyetibua mpango huu…” akaongeza kusema. Kwa maneno hayo, kila mmoja akagutuka na kumtazama mwanausalama huyo.
“Yupo kati yetu?” Mwanachia akauliza.
“No! hayupo kwenye cyndicate hii… ninachojiuliza ni wapi siri hii imevuja?” James akasema.
“Kwa sasa hatuna muda wa kujadiliana nani katoa siri au nani kafanya nini, mpango uliopo sasa ni sisi sote kutoroka nchi…” akadakiza mjumbe mwingine, na hapo kila mmoja akaunga mkono hoja kwa kutikisa kichwa.
“Mpaka sasa hatujui Mtokambali yupo wapi! Kapatwa na nini! Tulishakubaliana hili, na tukala yamini, kuwa mambo yakishindikana, kila mtu aitoroke nchi, tukakutane kwenye shimo jingine…” Mwanachia, mwanajeshi mwenye cheo cha kutosha, akawaambia wenzake. Kikao kikafungwa na ajenda iliyohitaji utekelezaji ni moja tu, kutoroka.
“Lakini tumeshindwa wapi?” mjumbe mwingine akauloiza kwa sauti ya chini.
“Hilo halina mjadala, kwa sasa yatupasa kutekeleza kilicho mbele yetu, basi… Siku ya kumi kutoka sasa tukutane pale ambapo mkataba waetu unasema. Asanteni na kwaherini!” Mwanachia akawaambia wajumbe na kikao kikafungwa.
* * *
Nchi ilikuwa kimya. Habari iliyotikisa kila kona ni juu ya kuuawa kwa komando Jairosi Simbamwene. Kila lililonenwa, likanenwa juu yake.
‘Tamaa ya madaraka,’ wakasema.
‘Mshenzi tu yule, alifikiri ataiweza serikali!’ Wengine wakasikika.
‘Nilijua tu, wasingeweza… mbona miaka ile walishindwa? Wangeweza leo!’ Akina mama nawo hawakuwa mbali katika kuchagiza.
‘Nduli Amin mwenyewe katimua mbiyo, mwaka jana tu hapo, seuze wao’. Maneno chungu mbovu yakamwagika kutoka katika vinywa vya Watanzania. Lakini kubwa kuliko yote, mpaka dakika hiyo, wenye busara wa;lisubiri kusikia japo sauti ya mpendwa wao. Aliyewatoa kwenye makucha ya mkoloni akawaweka huru na kuwafanya watembee wakijigambia Utanzania wao. Kifua mbele, macho mita mia moja. Kimya, hakukusikika lolote redioni. Vipindi vya kila siku vilikuwa vikiendelea. Ilipotimu saa nne asubuhi, pindi tu iliposikika ngoma maarufu ya Hayati Morris Nyunyusa, watu wakajazana redioni. Wasio nazo wakagonga hodi kwa jirani. Habari ni ile ile, kilichoongezeka ni, tu, ‘wengine wanatafutwa’.
‘Wanatuficha, anaweza kuwa ameshauawa, mbona hatumsikii na zaidi wanatuasa tu kuwa watulivu?’ wengine wakadukudukisha mara baada ya dakika kumi za habari kukatika na kufuatiwa na matangazo ya vifo. Maadam serikali iliwataka watu wake kuwa watulivu, walitii.
* * *



IKULU KIKAO CHA DHARULA

Saa tano asubuhi ya siku hiyo hiyo, kikao cha dharula kikafanyika katika ukumbi wa Ikulu. Katika kikao hicho mawaziri wote walikuwepo. Wakuu wa majeshi na vitengo nyeti vya usalama, wote walikutana. Mbele yao, katika meza kuu aliketi Makamu wa Rais na Waziri Mkuu.
“Nchi yetu imeingia tena katika matatizo makubwa. Hii ni aibu kwa taifa!” akaongea kwa mamlaka.
“Leo, majira ya saa kumi na mbili asubuhi, waasi kutoka ndani ya jeshi letu tukufu, wamevamia makazi binafsi ya mzee wetu, Rais wa nchi kwa minajiri ya kufanya mapinduzi,” akasoma katika taarifa aliyoandikiwa. Akatulia kwa sekunde chache na kuendelea.
“Wanajeshi hao waasi walikuwa wakiongozwa komando aliyejulikana kwa jina la Jairos Simbamwene. Nasema aliyejulikana kwa kuwa sasa ni marehemu. Ameuawa na wanausalama wetu watiifu alipokuwa akijariobu kutoroka. Wengine waliouawa ni watatu, na waliobaki wanashikiriwa kwa mahojiano. Ndugu mawaziri, na wakuu wa majeshi, mpaka dakika hii uchunguzi unaendelea na tunahakikisha wote wanaohusika watakamtwa na sharia itachukua mkondo wake,” akakohoa kidogo. Baada ya minong’ono kidogo akaendelea kuwahabarisha.
“Najua, nyote mna hamu ya kujua hatma ya mtukufu Rais wetu. Napenda kuwahakikishia kuwa, waasi hawajamgusa kabisa wala kumwona. Anaendelea vyema, mzima bukheri wa afya na muda si mrefu mtamsikia, ila si leo,” aliposema haya minong’ono ikaongezeka maradufu.
Baada ya hapo, ikafuata taarifa kutoka kwa Waziri wa ulinzi juu mambo yalivyo kiusalama. Majukumu yakapewa kwa idara ya usalama wa taifa. Na kila mtu kadiri ya nafasi yake, akapewa maelekezo ya nini cha kufanya.
Ndani ya chumba hicho cha mkutano, Waziri Kibwana Mtokambali alikuwa kimya akifuatilia kila kilichokuwa kikizungumzwa. Mikono yake alikuwa kaifumbata kifuani, si kama anyehisi baridi, la, bali alikuwa akihisi baridi kali. Watu wakaanza kutawanyika, kwenda kwenye majukumu yake.
Mtokambali aliinuka kitini, hakusalimiana na mtu. Moja kwa moja akaliendea gari lake na kujitoma ndani.
“Nipeleke nyumbani mara moja!” akamwamuru dereva, naye akatekeleza aliloambiwa na mkuu wake. Akili ya Mtokambali ilikuwa mbali kama miisho ya jina lake. Moyo na fikra vilitembea safari isiyojulikana.
Ukichelewa hapa saa sita tu, utakuwa mikononi mwa polisi wenye hasira! Sauti ile ya ndani ikamwambia.
“Nishushe hapa mara moja,” akamwamuru dereva. Naye akaegesha Landrover lile pembeni. Mtyokambali akateremka. “Naingia dukani mara moja, nahitaji kununua dawa za maumivu, sijisikii vyema. Nisubiri, usiondoke…!” akamwambia dereva. Hatua kama ishirini hivi zikamfikisha ndani ya duka lile kama alivyoahidi. Dakika kumi, ishirini, thelathini zikapita. Yule dereva aliendelea kupia miyayo akiwa nyuma ya usukani. Alipochoka, akateremka na kumfuata. Ndani ya duka lile alimkuta mzee wa Kihindi. Alimgundua kutokana na tabani lake kichwani.
“Samahani Kanjbahi…”
“Bila samahani kijana …” yule mzee akamjibu.
“Mhesimiwa Mtokambali ameingia hapa, lakini simwoni kurudi wala kutoka…” yule dereva akaeleza.
“Hujamona! Bona ni muda ile ile yeye toka ije? Mwangalie bizuri nje bhana!” akamjibu na yule dereva akatoka nje kumtafuta mkuu wake. Hayupo.


LISBON – URENO

23 Julai, 2003

Kamanda Amata, alitulia kimya kabisa huku akiwa kaliegemea gari alilokuwa akitumia, Audi TT. Gari hii alipewa maalumu kwa kazi yake aliyotuma kuifanya katika jiji la Lisbon. Halikuwa kubwa, liliweza kubeba watu wanne tu. Pembeni yake alisimama mtu mwingine, mwanamke wa makamo, mvi moja moja kichwani mwake zilidhihirisha hilo. Hakuwa mwingine, Madam S.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP9

Pembeni yake alisimama mtu mwingine, mwanamke wa makamo, mvi moja moja kichwani mwake zilidhihirisha hilo. Hakuwa mwingine, Madam S.
“Usirudie kosa la mwaka jana,” Madam S akamwambia Amata.
“Kosa gani?” akamjibu kwa swali huku macho yake akiwa ameyatupa mbali, akitazama machweo ya jiji hilo.
“Ilitakiwa umhoji kwanza kabla ya kuondoa roho yake…” Madam S akamwambia kijana wake huku akijaribu kuweka vyema kitambaa cha kichwa kilichokuwa kikisukwasukwa na upepo.
“Haikuwa na haja ya kumhoji mjinga yule…” kutokea upande aliokuwa anatazama, akaeuka kule aliko Madam S, “Kwani ulinituma kumuua au kumhoji?” akamuuliza.
“Yote mawili; moja kwenye maandishi na jingine akilini mwako. Tumia common sense wakati mwingine,” akamwambia.
“Jeuri yule, ndo maana nikatimiza andiko kama lilivyoandikwa,” Amata akajibu.
“Sawa, ila tunahitaji vitu kidoo ili kuweka kwenye maktaba yetu,”
“Yeah!”
“Usifanye hivyo safari hii… nipo hapa kwa sababu namhitaji mtu huyo. Ana funguo,” Madam S akamwambia Amata.
“Sawa, zitapatikana. Nitakuletea popote ulipo,” Amata akajibu.
“Vyema!” Madam S akamjibu. Dakika hiyo hiyo gari dogo aina ya Ford Escort likawasili na kusimama mbele yao.
“Tutaonana baadae. Kumbuka kufika Casa De Juncal saa mbili usiku huu, meza namba 5,” Madam akamwambia huku akiingia ndani ya gari lile dogo, lakini la kifahari sana. Akatokomea mjini na kumwacha Amata akiwa pale pale. Kijana huyu nadhifu, mwenye tambo la kuvutia warembo, alibaki pale kwa dazeni za dakika akiwa anasubiri asichokijua. Iza likaingia na kumkuta pale pale akiwa amesimama na kuegemea gari lake. Kama aliyegutushwa, akainua mkonowe na kuangalia saa. Saa moja usiku. Akaingia garini na kuketi kwa utulivu nyuma ya usukani.
* * *

Casa De Juncal

Casa De Juncal ilikuwa umabli wa kilomita sitini kutoka pale alipokuwa Amata kwa muda huo. Ingempasa kuendesha gari kwa muda wa wastani wa saa nzima ili kufika. Muda aliotakiwa kufika, na ule aliopo hapo unemtosha kabisa kufika na kusubiri wakati akipata cappuccino. Akatia injini moto na kuingiza gari barabarani, tayari kwa safari. Avenue de Terra Nova, ndiyo barabara aliyoitumia. Kwa kasi aliyokuwa akienda, isingemchukua saa nzima labda apambane na foleni za barabarani katika jiji hilo. Alipofika njia panda, karibu na magahawa wa Ritiro do Volante, akakunja kulia na kuufuata mzunguko wa Igreja Nova. Akachukua barabara ya kushoto iliyomfikisha katika mgahawa uo baada ya dakika arobaini kupita. Kama angekuwa mwenyeji basi angeweza kupita njia za mkato, lakini haikuwa hivyo.
Kamanda Amata akaegesha gari lake nje ya mgahawa huo. Ukiliona kwa nje jengo hilo, utalidharau, kuukuu, limechoka. Lakini kwa ndani lilikuwa maridadi hasa, lilipambwa likapendeza.
Viti vilipangwa kwa mtindo wa kipekee, upande huu vitatu vitatu kila meza, kule viwili viwili nk.
Amata akaangaza macho na kuitafuta meza na tano hasiione.
“Como você está Senhor! Posso te ajudar?” sauti laini ya mwaDanada mhudumu wa mgahawa huo ikamsabahi na kumuuliza kama anahitaji msaada.
“Sim por favor! Estou procurando uma mesa numbe cinco?” Amata akamjibu kwa Kireno cha kubabaisha, akimtaka aoneshwe meza namba tano.
“Está bem! me siga...” yule binti akamjibu kuwa amfuate. Amata akafanya hivyo. Yule binti mhudumu, akatangulia na Amata akafuata nyuma. Ndipo alipogundua kuwa, binti yule alikuwa amevalia sketi fupi iliyoruhusu robo tatu ya mapaja yake kubaki wazi. Akigeuka kwa mbele huwezi kujua hilo kutokana na apron aliyovaa, iliyofunika vizuri upande huo. Alikuwa mwembaba, mrefu kiasi, alimpita Amata kwa takribani sentimeta tatu. Mwendo wake wa ki-paka ndiyo haswa uliokuwa ukimvuatia kijana huyu.
Upande wa nyuma wa jengo hilo kulikuwa na ghorofa moja ndogo. Sakafu yake ilikuwa na viti vichache sana. Viwili, kila meza. Palikuwa tupu, ni mishumaa tu iliyokuwa ikiwaka katika meza hizo. Moja kwa moja akamwongoza mpaka katika meza hiyo.
Alipokuwa akiketi tu, upande wa mlango akainia mwaDanada mwingine, aliyevalia suti ya kijivu ya gharama. Akavuta hatua mpaka kwenye meza ileile na kuvuta kiti. Akaketi kwa mtindo wa kutazamana na kijana huyo.
“Oh!karibu sana Madam...” yule mhudumu akamkaribisha mwaDanada huyo.
“Asante sana, tuletee Gin Tinto Premium, nyekundu,” yule mwaDanada akaagiza huku jicho lake likiwa limeganda kwa Amata.
“Umejuaje kama nilitaka kinywji hicho?” Amata akauliza.
“Najua. Nilikuwa natembea mawazoni mwako kabla... karibu sana Ureno Kamanda, jisikie upo nyumbani...” akampa mkono, wakasalimiana, “Naitwa Dana...” akajitambulisha.
“Amata Ric!”Amata naye akajitambulisha kwa ufupi sana. Dana akamkazia macho Amata na kumtazama kwa makini. Kisha akajitazama kifuani na kugundua kuwa kifungo cha blauzi yake kimefunuka, hivyo kilifanya matiti yake yaonekane kwa ukubwa kiasi. Naam! Yalikuwa matiti yaliyojaa vema katika sidiria ndogo iliyotosha katika kifua chake. Akakifunga kifungo kile na kujiweka sawa.
“Sicho kilichotukutanisha!” Dana akasema huku sura yake ikiwa imebadilika kabisa.
“Najua! Kilichotukutanisha ni Vincent Mwanachia...” Amata akamwambia.
“Right! Huyu bwana siku nzuri ya kumpata ni kesho,” akaanza kueleza kile kilichowakutanishha.
“Kwa nini isiwe leo?” akamsaili.
“Kesho ndo mambo yatakuwa mukashara... kutakuwa na tafrija ya mikate mikavu katika mgahawa wa Casa de Tostas Absurdo…”
“Mikate mikavu?” Amata akamkatisha.
“Ndiyo, mikate iliyochomwa yaani tosti… ila sasa hii inaokwa mpaka inakuwa kama inaunua vile. Ni tafrija inayokutanisha matajiri tu. Na katika pekua pekua zangu nimegundua kuwa ana mwaliko wa kuwa pale,” akamweleza.
“Ulikuwa na black bag job?” Amata akamuuliza kwa vilugha vyao vya vificho akimaanisha kama ilimpasa kuipekua nyumba au ofisi yake.
“Ilibidi, maana jamaa haonekani ovyo, nilichofanikiwa ni hiyo kadi tu ya mwaliko…” akamwelea Amata ambaye alikuwa akiyarekodi kichwani mwake.
“Hongera sana! Unastahili zawadi,” Amata akamtania. Wakati huo huo kile kinywaji kikawasili, bilauri mbili zikifuatana nacho. Dana akalipia kabisa na yule mhudumu akaondoka eneo lile.
“Tafrija inaanza saa kumi na mbili jioni, kesho. Lakini uwe mwangalifu kwa kuwa jamaa ana yaya wengi,” Dana akamhabarisha Kamanda.
“Cheers!” Amata akamwambia Dana huku akiipuna bilauri yake juu na mwanamke huyo naye akafanya vivyo hivyo, wakagonga na kunywa kidogo kabla ya kuzishusha mezani.
“Casa de Tostas Absurdo!” Amata akarudia kulitaja jina lile.
“Haswaaaa!” Dana naye akamhakikishia kuwa ni hapo hapo.
“Asante kwa maelekezo, nitamnyakuwa kama mwewe afanyavyo kwa vifarana vya kuku…” Amata akamwambia Dana huku bilauri yake ikiwa sentimita moja kutoka kinywani mwake.
“Mi nimemaliza… niruhusu niende,” Dana akaaga.
“Mbona mapema? Hebu kumbuka, yanipasa kukaa mpweke mpaka kesho saa kumi na mbili jioni. Muda huo utapitaje kwangu?” Amata akaanza uchokozi. Dana akaingiza mkono katika blauzi yake, akatoa kimkebe kidogo. Ndani kijimkebe hicho akatoa kadi biashara yake na kumuwekea Amata mezani.
“Nipigie kuanzia saa tano usiku,” akamwambia na kuondoka zake. Kamanda Amata akabaki pale mezani, akiitazama chupa ya Gin Tinto Premium, kazi bora kabisa kutoka Ureno.
Casa de Tostas Absurdo! Akawaza na kuchukua simu mara moja. Akapekua upande waramani na kujaribu kuitazama, walau ajue ni upande upi ilipo. Sekunde hamsini tu zikatosha. Kilichomshangaza ni kuona kuwa mahali alipokuwa amesimama na Madam S ni kilomita tatu tu kufika hapo. Akainua bilauri yake kupiga funda moja, akaishusha mezani. Mara baada ya kuitoa kinywani bilauri ile, akaundua kuwa ana meni mezani pake.
“Wewe ni nani, unajikaribisha pasi na karibu?” Amata akamuuliza. Meni huyo alikuwa mwanamke wa Kizungu. Umri wake tunaweza kuukadiria kati ya miaka thelathini na thelathini na tano hivi.
“Eu sou chamado Quinta!” Akajibu mwanamke yule kuwa anaitwa Quinta.
“Nikusaidie nini, aaanh Quinta?”Amata akamuuliza hukiona wazi kuwa pombe ile inataka kumzidi nguvu.
“Mimi ni mfanya biashara, kahaba, je utapenda kuwa nami usiku huu?” Quita akamuuliza Amata. Hii ilimchukua kama sekunde kumi na tano hivi kuitolea majibu.
“Labda!” akajibu.
“Mwanaume hatakiwi kusema labda. Jibu ndio au hapana,” Quinta akamwambia Amata huku akimtazama kwa macho yake ya bluu. Kope zake ndefu na midomo iliyopakwa rani nyekundu, vilimfanya aonekane kama mtu wa kuchora.
“Labda!” Amata akarudia tena jibu lake na kuona jinsi mwanamke huyo alivyokunja sura kama kaona kinyesi. Akainuka tayari kwa kuondoka. Amata akabaki tu kumtazama asimsemeshe kitu. “Nimeshalipwa pesa kwa ajili yako, tutaonana baadae! Ukitaka kuokoa maisha yangu, lala na mimi...” Quinta akamwambia Amata na kuondoka eneo lile. Kengele za hatari zikalia kichwani mwa Amata, akaelewa nini kinachofuata baada ya hapo.
‘Ukitaka kuokoa maisha yangu, lala na mimi’. Kauli hii ikajirudia kichwani mwa Amata.
Imeshajulikana kuwa nipo? Nani aliyemlipa pesa kwa ajili yangu? Nani kamtishia kumuua? Akajiuliza. Kabla ya kusimama akapia tena funda jingine la Gin Tinto, kisha akasimama na kuondoka zake huku akiiacha ile chupa mezani ikiwa robo.
“Simpendi mtu anayetoa uhai wa mwenzake bila sababu ya msingi,” akajikuta akijisemea huku akishuka ngazi kuelekea chini. Moja kwa moja akaingia katika gari lake na kuketi nyuma ya usukani. Akawasha na kuliondoa eneo lile akaanza safari kuelekea hotelini kwake Epic Sana, Barabara ya Engenheiro Duarte Pacheco 15.
Akiwa tayari katika barabara ya De Casai Lage, akasikia ving’ora vya polisi nyuma yake. Akatazama kwenye kioo na kuona gari la polisi nyuma yake likimwashia taa. Amata akawasha indiketa na kutoa gari nje ya barabara, akasimama.
“Ola somos policiais. Precisamos inspecionar seu carro,” askari mmoja akaja dirishani na kumwambia kuwa wanahitaji kukagua gari lake.
“Ok!” akawaruhusu. Wale askari wakazunguka lile gari na kuomba vibali vyote.
Wakavikagua na kukuta vipo sawa kabisa. “Unajua kwa nini tumekusimamisha?” mmoja akamuuliza.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP10


Ok!” akawaruhusu. Wale askari wakazunguka lile gari na kuomba vibali vyote.
Wakavikagua na kukuta vipo sawa kabisa. “Unajua kwa nini tumekusimamisha?” mmoja akamuuliza.
“Sijui,” Amata akajibu.
“Hili gari limehusika kwenye uhalifu jana alfajiri, na tulikuwa tunalitafuta,” akaeleza askari mmoja.
“Mi sijui, mi nimelikodi jana mchana baada ya kuwasili Lisbon na sikuambiwa kama lina rekodi ya uhalifu...” Amata akajibu.
“Fungua buti!” mwingine akasema. Amata akavuta nobu ndogo chini ya kiti na kuruhusu buti la gari hilo kuachana na loki yake.
“Njoo nje ufungue mwenyewe,” akaamriwa.
Amata akashuka na kuliendea buti upande wa nyuma, akafungua na kujikuta akirudi nyuma hatua tatu. Hakukubaliana na nini anakiona ndani yake. Maiti. Maiti ya mwanamke. Alipotaka kugeuka akajikuta akitazamana na mitutu ya bastola.
“Weka mikono kichwani!” akaambiwa. Amata akatii.
“Piga magoti,” mwingine akaamuru. Amata akatii. Akapiga magoti huku mikono ikiwa kichwani. Akajaribu kuvuta kumbukumbu ya mwili aliouana ndani ya buti lile. Ni wa mwanamke. Mwanamke yule aliyemfuata na kumwambia kuwa amelipwa kwa ajili ya kulala naye.
Nani kamuua? Akajiuliza, hasipate jibu.
“Wahalifu kama ninyi ndiyo tunaowatafuta! Umeua huyu mwanamke jana asubuhi na maiti unazunguka nayo. Sasa utawajua Wareno ni akina nani asee...” askari mmoja akasema huku akiongea na radio call yake. Amata akajiuliza, iweje akutane na mwanamke huyo jioni ya siku hiyo na aambiwe ameuawa jana?
Wamemuua! Akawaza. Akili yake ikaanza kufanya kazi haraka, akagundua kuwa hayupo mikononi mwa polisi bali watu tofauti kabisa. Wamejichanganya. Wakati askari yule akiongea na redio yake, huyu mwingine alikuwa bado kamwekea bastola kichwani. Akampigia hesabu kali za kumfanyia shambulio la ghafla, akifikiria tu atumie sekunde tano kumtyoa uhai.
Amata akashusha mikono yake ghafla, akamkamata mikono yule askari kisha akambinua na kiumbwaga mbele yake. Yule jamaa akatua kama mzigo. Haraka, Amata akainuka na kumuwahi akaukamata mkono wenye bastola na kumlenga yule aliyebaki, akammaliza.huyu mwingine alipojaribu kufurukuta, akamkamata kichwa na kuizungusha shingo, akamvunja na kumuua. Akainuka na kujipukuta vumbi. Akatumia dakika chache kuwapekua marehemu wake. Akachukua kila alichoona kinamfaa na kuvitia mfukoni mwake kisha akacukua ile maiti ya yule mwanamke na kuitia kwenye ari lile walilokuwa wakitumia wale askari. Akaingia garini na kutokomea. Yote hayo yakitukia magari yalikuwa yakipita tu bila kusimama.
Nusu saa baadae aliwasili hotelini kwake. Badala ya kuegesha gari katika maegesho ya hoteli hiyo, akatafuta mahali pengine. Mita mia tano kutoka hoteli ya Epic Sana, kisha yeye akarudi kwa miguu. Ndani ya hoteli hiyo kulikuwa na shughuli nyingi kama kawaida. Akapita kaunta na kuchukua kadi-fungushi. Mbele ya mlango wa chumba chake, ghorofa ya nne, akasimama na kusikiliza kwa umakini kama kuna mtu au chochote ndani. Kimya! Akachanja kadi yake na kufungua mlango. Akaingia kwa tahadhari kubwa, akipepesa macho huku na huku. Hakuna mtu wala kitu cha hatari. Akaingia na kujitupa kitini. Akatoa kila alichochukua kwa wale jamaa. Akavitazama haraka haraka, havina maana, akavitupia mezani na kujiandaa kuingia bafuni kuoga. Tayari alikwishajua kuwa uwepo wake ndani ya jiji la Lisbon umejulikana.
* * *

Upande mwingine wa Lisbon

Nje ya jiji la Lisbon, katika nyumba ndogo, kando ya bahari watu wawili walikutana. Vincent Mwanachia, mwanajeshi aliyeshiriki katika jaribio la kuipindua serikali mwaka 1980 na mwanamama Bi. Jesca Tibatulanwa, mwanaharakati aliyekimbilia Ughaibuni miaka mingi. Wote hawa walikuwa mwiba kwa serikali. Mwanachia alikwishahukumiwa kifo pamoja na wenzake watatu. Mwanamke huyu alipewa vitisho kadha wa kadha na serikali kwa sababu ya msimamo wake. Wawili hawa waliungana na kuwa marafiki sana kwa sababu tu ya itikadi zao. Mwanachia, hakuwahi kurudi Tanzania tangu atoroke mwaka 1980. Arudi afanye nini? Auawe? Dakika chache kabla ya kukutana na mwanamama huyu, alikuwa kwenye mkutano kwa njia ya video yaani video conference. Mkutano ulimkutanisha na wengine walio nchi tofauti, ambao kwa pamoja waliunda Cyndicate yenye sera ya kuiangusha serikali madarakani.
“Bado tunaihitaji ile nchi... watu wachache wameiteka na kuifanya yao!”Mwanachia akamwambia Bi Jesca.
“Tupambane tuikomboe... mimi nina ushawishi mwingi kwa Watanzania, na maadam mmekubali kuniweka kwenye timu hii, ambayo tunania mamoja, tutauwasha moto...” Jesca akamwambia Mwanachie, naye akatikisa kichwa juu chini kukubaliana naye.
“Na wewe lazima upambane, kumbuka serikali imesambaratisha familia yenu. Baba yako amenyongwa kwa kosa kama hili... lazima utimize ndoto ya marehemu baba yako,” Mwanachia akamwambia Jesca.
“Haswaaaa!”
“Lakini sasa kuna jambo linafanyika, mwaka jana aliuawa mwenzetu Titus Mwakibinga kule Brussels...” akasema.
“Ina maana mnawindwa?” Jesca akauliza.
“Siyo m’, sema tu’,” Mwanachia akamrekebisha huku akimmiminia kinywaji kwenye bilauri.
Wakiwa bado bustanini wakibadilishana mawazo, simu ya Mwanachia ikaita kwa fujo. Akaikwapua kutoka katika mfuko wa koti la suti aliyovaa. Akaiweka sikioni mara tu alipobonya kitufe cha kuruhusu simu hiyo izungumze.
“Yes...” akaitikia namna hiyo huku akisogea kando kusikiliza ujumbe anaofikishiwa. Kutoka mbali, Jesca alimuona mzee huyo akibadilika sura, akienda huku na huko. Mara akatulia, akakata simu na kuirudisha mfukoni, kisha akavuta hatua mpaka kwa mwanamke yule.
“Tuondoke!” akamwambia. Bila kubisha wala kuuliza, Bi. Jesca akainuka na vijana wanaomloinda mzee huyo wakawafuata nyuma mpaka kwenye gari lake.
“Nini kimetokea?” Jesca akauliza wakati gari lile likiondoka taratibu.
“Bastard!” Badala ya kujibu, akatukana.
“Kuna mwendawazimu ameingia Lisbon!” akaoneza kusema huku akitoa kitambaa chake na kujifuta jasho asilokuwa nalo.
“Kuna mtu katumwa kutoka nyumbani, kuja kiniua...” Mwanachia akamwambia Jesca.
“Nyumbani?”
“Ndiyo! Yaani Tanzania. Mwaka jana mwenzetu mmoja aliuawa Brussels. Tukafanya utaratibu wote ili kumjua, tukafanikiwa. Tukapanga watu ili kujua nyendo zake. Tukapata taarifa kuwa anakuja Lisbon, nikiwa na maana ananifuata mimi ili atimize alilotumwa...”
“...akuue?” Jesca akamkatisha kwa swali.
“Ndiyo. Sasa kuna mtego tulimtegea, ameutegua na ameua vijana wetu wawili ambao tunawatumia sana kwenye genge letu... dah! Mshenzi huyu nitahakikisha kesho haioni,” Mwanachia akajibu na kuongeza maelezo ya ziada. Kutoka ndani ya lile gari, Mwanachia alitoa taarifa kwa wenzi wake juu ya tukio hilo.
* * *
Mara baada ya kuuawa Titus Mwakibinga kule Brussels, Ubelgiji, iliwawia ugumu mkubwa sana TSA kutambua wapi walengwa wengine walipo. Wote wanaounda sindiket hiyo walitoweka ghafla baada kifo kile kwa kuwa walijisahau na kudhani kuwa wamesahaulika.
Timu nzima ya TSA ilifanya kjazi ngumu sana mpaka kuweza kutambua Vincent Mwanachia anaishi kwa kificho huko Lisbon, Ureno. Baada ya Madam S kupeleka tafutishi hiyo kwa Mkuu wa nchi, ikaandikwa hati ya kifo chake kufuatia hukumu ya mwaka 1984.
Ndani ya jiji la Lisbon, mwaka 2003, Kamanda Amata anakuwa kwenye kibarua kilekile kama cha Brussels. Mara alipotoka bafuni kuoga na kujiweka sawa katika mavazi ya kawaida, alitupia tena jicho kwenye vile vikolokolo alivyovipata kwa wale marehemu. Mara hii akaona kitu kisicho cha kawaida katia ya vile pale mezani. Casino Lisboa. Kipande cha karatasi kiliandikwa hivyo. Akakitazama mara kadhaa, akakihukua na kukikunjua vizuri, akakisoma upya.
Kwa nini mwanzo sikuona umuhimu wake? Akajiuliza. Kuna lolote ninalotakiwa kufanya kule? Akajikuta njiapanda. Akiwa katika hali hiyo, akashtushwa na hodi iliyobishwa mlangoni. Amata akakusanya vile vitu na kuvifungia kwenye droo. Akajiweka tayari na kuuendea mlango uliokuwa ukigongwa kwa fujo. Taratibu, Amata akaufungua na kumruhusu agongaye aingie. Dana. Dana aliingia ndani ya chumba hicho akitweta. Akageuka na kumtazama Amata aliyekuwaakikunja mikono ya fulana yake ya pull neck.
“Umefanya nini Amata?” Dana akauliza kwa tashwishwi. Amata akafanya kama hajasikia swali hilo. Alipomaliza kukunja mikono ya fulana, akachukua saa yake na kuivaa. Dana akasimama mbele yake, uso kwa uso.
“Nakuuliza Amata, husikii?” akauliza kwa sauti ya ukali. Amata akamaliza kuvaa saa yake na kuchukua koti la jinzi, akalivaa na kuliweka sawa. Dana akajitupa kitini na kubaki akimtazama kijana huyo. Alipomaliza kujiandaa, akavuta mkoba wake na kutoa bastola yake aina Beretta Pico na kuipachika kwenye mkwiji wa suruali yake. Akamgeukia Dana na kumtazama.
“Mbona unaingia ndani kwa mtu unapia makelele, we una kichaa?” akamtupia swali. Dana akabaki kimya akitazama tambo la kijana huyo shababi, aliyesimama imara pasi na kutetereka.
“Umeua askari mbele ya CCTV camera, umeharibu kila kitu, wanakutafuta kila kona,” Dana akalalama akiwa kaegemea kiti kile na kupumua kwa nguvu.
“Sijaua askari, wamenifananisha!” Amata akajibu.
“Umeua Amata,” akamwambia na kumwekea picha mezani. Amata akazitazama zile picha kutoka mbali. Akajiona katika picha tatu tofauti katika tukio lile.
“Dana!” akaita.
“Unasemaje?” akamuuliza.
“Unapoongea na mwanaume, uwe mtulivu. Sasa sikiliza, kuanzia sasa ninatengua mission ambayo ninyi mliipanga,” aliposema hayo, Dana akabaki katoa macho.
“Hah, unasemaje? Unapaswa kufanya lile tulilolipanga,” Dana akasimama na kuonea kwa mamlaka.
“Sikiliza, narudia, kuanzia sasa ninatengua mission ambayo ninyi mmeipanga...”
“Halafu ufanyeje?” Dana akamkatisha kwa swali.
“Narudi Tanzania, usiku huu...”
“Una kichaa!” Dana akang’aka.
“Kichaa unacho wewe na bosi wako ambao mmevujisha siri hii kwa Mwanachia...” Amata akamwambia.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP11

Narudi Tanzania, usiku huu...”
“Una kichaa!” Dana akang’aka.
“Kichaa unacho wewe na bosi wako ambao mmevujisha siri hii kwa Mwanachia...” Amata akamwambia.
“Unasemaje!” Dana mishipa ikamtoka, “Sisi tunaweza kufanya upuuzi kama huo?” akauliza.
“Sikiliza Dana... hii kazi mimi nimeifanya miaka mingi kuliko wewe, usifikiri kuwekwa mkuu wa usalama katika ubalozi wetu hapa Ureno ndo umefika. Mimi siyo renki yako, sawa?Hebu nambie, hizi picha wewe umezipata wapi? Ina maana ulikuwa unajua mchezo mzima unaotakiwa kutukia kwangu. Pili, safari yangu ya kuja huku hakuna aliyekuwa anaijua zaidi ya ofisi yako tu, Mwanachia na genge lake wamejuaje kama nipo hapa? Mbona Brussels nilifanya kazi peke yangu na sikujulikana?
Mpo matatani! Yaani mpo matatani...” Amata akaonea kwa ukali na kumfanya Dana kunywea kabisa. Maneno yaligonga mfupa.
“Nani aliyekwambia huo uongo wote?” Dana akajikakamua kusema.
“Uongo? Balozi Asantino Mwampamba, yaani bosi wako, alikuwa kikosi kimoja na Vincent Mwanachia. Yeye alimtangulia tu kuingia jeshini, ni marafiki, wanafahamiana, siwezi kushangaa wakilindana. Nimetenua mission narudi Tanzania,” akamwambia Dana huku akitoa tiketi ya ndege na kumtupia mezani. Dana alipoisoma, ni kweli, ilikuwa ya usiku huo huo.
“Nipeleke Uwanja wa ndege...” Amata akamwambia Dana ambaye sasa hakuwa yale maneno. Amata akainua mkoba wake na kumpa ishara ya kutoka.
“Yaani hata sikuelewi we mwanaume!” Dana akasema huku akiinuka.
“Nipeleke, kama hutaki nitakodi taksi. Na ndipo nitapopata uhakika wa maneno yangu,” Amata akamwambia huku tayari wakianza kutoka hotelini hapo. Baada ya kuweka mambo yote ya hotelini hapo, Dana na Amata wakaelekea Uwanja wa ndege.
“Asante sana Dana! Fikisha salamu zangu kwa Mwampamba...” Amata akamwambia Dana wakati wakiagana katika Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Lisbon.
“Sawa!” Dana akajibu, kisha akamsindikiza mpaka ndani ya uwanja huo na kuhakikisha amemaliza hatua zote za safari.
“Waweza kwenda Dana, nisikucheleweshe na shughuli zako,” Amata akamwambia yule mwanamke.
“Usiwe na wasiwasi, kwa kuwa ilikuwa kazi yangu kukuhost sina budi kukuescort pia...” akamjibu.
Nusu saa baadae, sauti ya mwaDanada ikasikika kwenye vifaa maalumu ikiwataka abiria wote wanaoondoka kuelekea Addis Ababa waingie ndegeni. Kamanda Amata, akamkumbatia Dana na kumbusu shingoni kisha akamwacha na kuelekea katika lango ambalo lingemfikisha pale ndege ilipo. Mita chache kabla ya kuufikia mlango wa ndee hiyo, Amata akafungua mlango mdogo na kutoka nje. Akateremka ngazi mpaka eneo ambalo gari za kukokota mizigo zimeegeshwa. Akiwa anaambaaambaa na ukuta huo, akakunja kona na kuingia katika mlango wazi. Moja kwa moja akaibukia katika chumba ambacho inafikia mizigo. Wafanyakazi wa eneo lile wakataka kumzuia, akajitambulisha na kuwaonesha kitambulisho cha kidiplomasia. Wakamwongoza na kumwonesha njia ya kutokea nje kupitia upande huo.
Upande wa nje kulikuwa na watu wengi na wanafika kupokea na kusindikiza wageni. Giza lilikuwa limemezwa na taaza zenye mng’aro wa dhahabu. Amata akapepesa macho kama atamwona Dana. Akasimama palepale alipo akiangaza kwa umakini , kikachero. Haikuchukua muda, macho yake yakamnasa mwanamke huyo.
Dana alikuwa akitembea haraka haraka huku nyuma akifuatiwa na kijana mmoja. Kutokana na wingi wa watu, Dana alipotea katika macho ya Amata. Amata naye akajitoa pale aliposimama na kuvuta hatua mpaka upande wa pili wa maegesho. Akatembea haraka haraka huku akipita viunga vya maua. Katikati ya magari mengi, kulikuwa na Volks Wagen moja likiwasha hazard. Alipolikazia macho zile taa zikazimika kisha zikawaka zile kubwa kwa mtindo wa flash, akaelewa. Akaliendea na kuingia katika kiti cha mbele, pembeni ya dereva. Ndani ya gari hili kulikuwa na mtu mmoja tu, mwanamama.
“Welcome on board sir... I will fly you safely to Addis’”Madam S akamwambia Amata na wote wakaangua kicheko.
“Ni kuwacheza shere tu, na nataka usiku huu huu nifunge kazi,” Amata akamwambia Madam S.
“Utaanzia wapi?” akauliza.
“Casino di Lisboa!” Amata akajibu.
“Kuna chambo?”
“Bila shaka... nahisi mwanzo utakuwa mzuri. Sasa tupo TSA peke yetu kwenye mchezo huu...” Amata akamwambia Madam S.
“Wataiona ngondo...” Madam S akamalizia huku akiliondoa gari lile maegeshoni na kurudi mjini Lisbon.
* * *
. Mtu mzima , Vincent Mwanachia, mpiganaji wa Jeshi la Tanzania aliyeasi, aliwasili katika Casino kubwa na la kisasa jijini Lisbon. Pembeni yake akiwa na Bi. Jesca Tibatulanwa, mwanaharakati mwenye ulimi wa moto. Anayeweza kushawishi na kukubalikana watu wa rika lote.
“Mbona Casino?” Jesca akauliza.
“Kuna wadau wa kuweka nao mambo sawa hapa, kisha mimi na wewe kesho tutasafiri kukutana na wanachama wengine. Kama ulivyoambiwa na mkuu kuwa tuna mkakati wa aina nyingine katika kutimiza azma yetu,” Mwanachia akamwambia Jesca. Muda huo huo, kijana mmoja akajitokeza kuwapokea na kuwaongoza kuingia ndani ya jengo hilo.
Jengo lilipambwa kwa mataa ya kila aina. Watu wengi walikuwamo wakicheza kamari za aina aina. Kila aliyekuwa hapo, alionekana ni mwenye nazo. Kulikuwa na starehe. Wadada waliovaa nusu uchi walikuwapo. Na wale wasiovaa kabisa, nao walikuwapo. Vinywaji vya kila aina vilikuwa vikipitishwa huku na kule kwa walioagiza. Waliohitaji huduma ya makahaba nao walikuwa na nafasi yao, ili mradi ushetani wote ulikuwa ndani ya jumba hilo.
Katikati ya ukumbi huo kulikuwa na meza kubwa ya Poker. Mchezo wa vibopa. Mwanajeshi mstahafu, Vincent Mwanachia, aliongozwa mpaka kwenye meza hiyo ambayo kwa muda huo ilikuwa na watu wengine wanne. Walinzi wake, wakazunguka mita moja nyuma ya meza hiyo wakiungana na wengine waliwakuta hapo.
“Karibu sana Comrade!” sauti nzito, iliyojawa mikwaruzo ikamtoka mmoja wa wazee aliyeketi mkabala na Mwanachia. Mzee yule mwenye kichwa kisicho na nywele,alikuwa mara kwa mara akipachika kinywani kifaa cha kuvutia dawa ya pumu.
“Nimekaribia,” Mwanachia akajibu.
“Pole sana kwa ajili ya vijana wako,” akamwambia huku akitoa ishara aletewe kinywaji maana alikuwa amesawajika uso wote.
“Mwanaharamu yule, ana bahati sana amekimbia,” Mwanachia akasema.
“Una uhakika?” yule bwana akaonesha hali ya mshtuko kidogo.
“Yap! Mtu wangu mmoja amenihakikishia hilo kwa kuwa amempeleka mpaka uwanja wa ndege. Na ameondoka na Ethiopia Airline,” Mwanachia akmweleza yule mzee.
Nje ya ukumbi ule, Kamanda Amata bado alikuwa ndani ya gari pamoja na Madam S.
“Ok, ngoja niingie ndani, nitakujuza nitakachokiona,” Amata akamwambia Madam S.
Alipotaka kufungua mlango ili atoke nje ya gari lile, akasita kidogo na kurudi ndani. Wakati akifanya hilo likapita gari moja kwa kasi mbele yao.
“Dana!” akatamka.
“Dana?” Madam akauliza kwa kutaka uhakika.
“Yes! Dana. Sasa naanza na yeye, lazima nijue anafuata nini huku,” Amata akasema. Alipotaka kutoka, Madam S akamgusa bega, akampa mzula na miwani.
“Chukua hivi, vaa mara moja. Una bastola?”
“Ndiyo ninayo,”
“Ongeza na hii...” Madam S akampa bastola nyingine, Marksman. Bastola toleo jipya wakati huo, yenye uwezo wa kusafirisha risasi kwa futi 250 kwa sekunde.
Amata akateremka, akavaa ule mzula na kuipachika miwani usoni pake. Alipopachika mikono mkifukoni, akavuka barabara na kuelekea upande wa jumba lile huku akiangaza macho kuona ni wapi Dana ameegesha gari lake. Hakuchukua muda, akaliona. Akajibanza kwenye maari mengine ili aone nini kinaendelea. Alichokishuudia, ni Dana akibishana na vijana wawili wa Kizungu. Akasubiri. Dakika mbili baadae, wakaongozana pamoja kuingia ndani ya jengo lile, naye akawafuata kwa kupita upande wa pili. Walipofika mlango mkuu, wakaingia ndani, nao ukajifunga.amata akawahi , akaingia pia. Baada ya mlango wa kwanza , kulikuwa na mwingine. Kilichomshangaza ni kuwa milango yote haikuwa na ulinzi.
Haiwezekani! Akawaza. Amata akajua wazi kuwa kama hakuna walinzi katika milango hiyo, basi kwa vyovyote anepambana nao mahali pengine. Akaingia na kujikuta kwenye ukumbi ule ule ambao Mwanachia alikuwamo. Hatua zake zikamfikisha katika kaunta kubwa ya vinywaji.
“Um copo de vinho tinto,” akaagiza mvinyo nyekundu. Akaletewa chupa ndogo na bilauri.
Pamoja na kunywa huko, macho yake yalikuwa yakiangaza huku na huko. Mara kwa mara yalikatishwa na wasichana warembo waliokuwa wakikatiza mbele yake. Akaanza upya kutazama, huku akihakikisha hagunduliki na mtu. Wakati akiendelea kutazamatazama, akajikuta akiguswa na bomba dogo la baridi ubavuni mwake.
“Termine sua bebida e vá...” akaambiwa amalize kinywaji chake waondoke. Kamanda Amata akajua tayari keshaingia mikononi mwa majahili. Hakutaka iwe hivyo lakini imebidi. Akawa mpole.
“Não se preocupe, apenas fique em paz,” akawajibu, wasiwe na wasiwasi bali wawe na amani tu.
Dakika kumi baadae, akamaliza kinywaji chake, wakamtaka ateremke kwenye kiti alichokikaa. Akafanya hivyo. Wale jamaa wakamwongoza taratibu upande mwingine wa ukumbi ule. Wakaingia naye kwenye lifti. Humo wakawakuta vijana wengine wawili. Kimya, hakuna aliyekuwa akiongea. Lifti ile ikapanda mpaka ghorofa ya tatu, wakatoka na kumwongoza mateka wao mpaka katika chumba kimoja wapo.
Ndani ya chumba hicho walimkuta Vincent Mwanachia, Dana , yule mzee wa kwenye kamari pamoja na vijana wengine wawili. Ukijumlisha na hawa wanne wanakuwa watu tisa. Vincent Mwanachia, akaanza kupiga makofi na wale wengine akiwemo Dana wakafanya vivyo hivyo. Cumba hiki kikubwa kiasi hakikuwa na samani yoyote zaidi ya viti viwili vilivyokuwa vimekaliwa na Mwanachia na yule mzee.
“Karibu sana kijana!” Mwanachia akamwambia Amata. Amata hakujibu, akabaki kumtazama tu.
“Hata usipojibu, umeshaingia kwenye mikono ya shetani, hutatoka humu. Tumekuwa tukikusaka sana tangu ulipomuua Titus Mwakibinga. Na sasa umejileta mwenyewe...” Mwanachia akaongea kwa Kiingereza ambacho wote walielewa vyema.
“Mbona unaongea maneno mengi? Mimi nimekuletea barua yako tu kutoka nyumbani...” Amata akamjibu.
“Barua!” Mwanachia akashangaa. Akawatazama wenzake kisha wakaanza kucheka. “Iko wapi hiyo barua?” akamwuliza.
“Mfukoni, mwambia kijana aje achukue akupatie,” Amata akamwambia. Mwanachia akampa ishara Dana akachukue barua hiyo. Dana alipoanza kuvuta hatua kumwendea Amata, wale vijana sita, wote wakachomoa bastola kumwelekezea Amata. Dana akamfikia Amata na kuingiza mkono mfukoni, akachomoa bahasha na kumpatia Mwanachia. Mzee huyo akaichana na kuitoa karatasi ya ndani, akaifungua na kuanza kuisoma. Chumba kizima kilikuwa kimya, ni bastola tu zilikuwa zikimtazama Amata. Mwanachia alipomaliza kuisoma karatasi ile akaitupa chini kwa hasira. Akavuta kamasi ndani.
“Hamuwezi, na bado tutaikomboa nchi yetu... muda si mrefu mtashuhudia mapinduzi makubwa,” Mwanachia akasema.
“Na mapinduzi hayo hutayashuhudia hata kidogo... kwa kuwa una masaa mawili tu ya kuishi. Hizi bastola zote, zitakugeukia wewe muda si mrefu,” Amata akasema.
“Pumbavu sana wewe!” yule mzee mwingine akasema.
“Hata kama! Ila hukumu ya rafiki yako ni kifo, na siku ya kifo chake ni leo...” Amata akamwambia yule mzee.
Yule mzee kwa hasira, akarusha kile kidubwana anachotumia kuvutia dawa ya pumu, Amata akakidaka na kupiga msamba akakaa chini. Risasi za wale jamaa zikapita hewani na kuchimba ukuta.
Kabla hawajajiweka sawa, tayari kamanda alijizungusha kiufundi na kumchota ngwala mmoja. Akaenda chini mzima mzima, Amata akamdaka na kukikunja kiganja chake. Akaikamata bastola ile kwa ufanisi, risasi ya kwanza ikafumua kifua cha jamaa mwingine aliyekuwa mbioni kufyatua yake. Chumba kilijazwa na taharuki, mtafutano.
“Muueniiiiii” Mwanachia alipiga kelele. Yule mzee mwingine akabaki kukohoa tu na kupumua kwa shida. Pumu ilimkamata. Kamanda Amata, akabingirika na yule jamaa huku akifyatua risasi hovyo. Kwa makusudi alikuwa akipiga juu. Mara vifaa vya zimamoto vikaanza kumwaga maji na ving’ora vya hatari vikaanza kupiga kelele. Balaa. Upinzani ukaanza kuongezeka, amata akaona isiwe shida, akachomoa bastola na kuanza kazi.alikuwa na nafasi nzuri ya kumuua Mwanachia lakini aliaswa na mama yake asifanye hivyo alitii. Beretta pico ikatema risasi na kumwangusha kijana mwingine huku wengine wakiwahi mlango akiwamo Dana.
Amata akajiviringa chini mpaka kwa Mwanachia akainuka na kumkamata ukosi wa shati. Akamuinua.
“Walinzi wako wote wamekuacha!” Amata akamwambia. Mwanachia akabaki akitetemeka. Vishindo kutoka kwenye korido vya watu wanaokimbia vikamgutusha Amata. Akamwinua Mwanachia na kwa nguvu zote akajirusha nae dirishani. Kioo kikatawanyika huku risasi mfululizo zikimkosakosa.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP12

Walinzi wako wote wamekuacha!” Amata akamwambia. Mwanachia akabaki akitetemeka. Vishindo kutoka kwenye korido vya watu wanaokimbia vikamgutusha Amata. Akamwinua Mwanachia na kwa nguvu zote akajirusha nae dirishani. Kioo kikatawanyika huku risasi mfululizo zikimkosakosa.
“Amekimbiaaa, muwahini chiniiii,” mmoja wa wale walinzi akapiga kelele. Wote wakageuza na kuanza kueteremka, kurudi walikotoka.
* * *
Ndani ya jengo hilo kizaazaa hakikuwa cha kawaida, watu walikimbilia nje. Pindi tu Madam S aliposhuhudia mtifuano ule kupitia runinga ndogo ndani ya gari iliyokuwa imeunganishwa na ile miwani aliyompa Amata, akawasha gari na kuondoka zake.
Huku nyuma aliacha tafrani nzito, kila mmoja akipigania uhai wake. Ni muda mfupi sana , lile eneo lote likazingirwa na polisi na zimamoto. Usalama ukazingatiwa.
Upande wa pili wa jengo lile, Kamanda Amata alitua chini akiwa kamkumbatia Mwanachia. Maua marefu ya liyotengenezwa vyema yaliwapokea, ikawa salama yao. Kwa kuwa haikuwa mbinu ambayo Amata aliifikiria kuifanya, lakini kutokana na mazingira ikambidi.
Hakupoteza muda, akavirinika chini na kumkuta mtu wake akihema ovyo. Alipogeuza macho huku na kule hakuona jinsi ya kutoroka eneo lile maana gari lilikuwa upande wa pili. Akajilaumu kwa kosa alilofanya. Akiwa katika kuamua nini afanye, akasikia sauti kali ya matairi ya gari takisuguana na barabara.
“Spaaarrrrkkkk!” sauti ikamwita, alipogeuka barabarani hakuamini anachokiona. Scoba. Kasimama pale na BMW Sports. Kamanda Amata akampa ishara ya kufungua buti. Scoba akafanya hivyo. Kwa nguvu zote akamnyanyua Mwanachi na kuvuka naye bustani ile mpaka barabarani, akamtumbukiza kwenye buti na kulifunga. Akawahi mlango wa abiria na kuingia. Scoba akapia norinda, kabla hajaweka gari sawa, akashuhudia kioo cha nyuma kikimwaika, risasi.
“Twende!Twende!” Amata akamwambia huku akifyatua kiti na kukilaza. Scoba akapita katikati ya maua na kutokea upande wa pili. Kwa kutendo hicho akawapoteza shabaha wajinga wale. Alipokuja kukaa sawa barabarani, akataka kupenya katika ya majengo mawili ili atokee barabara kuu. Akajikuta akikutana na gri jingine uso kwa uso, hakuna pa kupita. Akapiga rivasi lakini badala yake akagonga gari la nyuma. Hakusimama, akakanyaga mafuta kurudi nyuma huku lile gari la mbele yao likizidi kuwakaribia na wale jamaa wakajitokeza nusu madirishani wakiwa na bunduki aina ya Aptus mikononi.
“Kamanda, Ambush!” Scoba akasema.
“Usijali, we fanya hivi hivi mi nitawafanyia kazi!” akamjibu, “Una bunduki?” akamwongezea swali.
“Kuna Wilson Combat, ipo full !” akamjibu.
“Eeeewaaah!” Amata akashukuru na kuichomoa kutoka ilipohifadhiwa. Akashusha kioo aikwa bado amelala na kiti. Scoba alikuwa akichezesha tairi kwa mtindo ambao wale jamaa walijikuta wanashindwa kupata shabaha.
“Shoo inaanza! Moja , mbili, tat...” kabla hajamaliza alishuhudia kioo cha mbele cha gari lao kikitawanyika. Sekunde hiyo hiyo akaitumia, akainuka ghafla na kuchia riosasi moja tu. Aikukosea, ikpenya katikati ya paji la uso wa dereva. Lile gari likayumba mara ya kwanza na lilipoyumba mara ya pili, likajipiga katika ukingo wa barabara na kuinuka upande mmoja. Amata akaweka shabaha nyinine na risasi ya pili ikafumua tanki ya mafuta. Moto mkubwa ukalipuka. Lile gari likpaishwa juu na kuteremka chini kama mzigo.
Scoba akazungusha gari na kuingia barabara ya Oceanos. Kasi aliyokuwa akitembea nayo ilikuwa ya kuogopesha. Hawakufika hata mwendo wa dakika kumi, tayari maari ya polisi yalikuwa nyuma yao. Kutoka katika magari yale, walisikia matangazo ya kuwataka kuweka gari pembeni.
“Oh Shiiit!” Scoba akatamka aliposikia amri hiyo.
“Usisimame, fanya unachoweza, uwapoteze,” Amata akamwambia. Scoba, akaongeza kasi, akaanza kufanya overtaking za hatari. Alipolipita gari la tatu, lile gari likafunga breki na kusimama ghafla. Kishindo kikubwa kikasikika, kikafuatiwa na kingine. Ilikuwa ajali, iliyohusisha magari manne yakiwemo ya polisi.
“Safi sana! Nakuaminia siku zote pilot wangu,” Amata akampongeza Scoba. Akageuka nyuma kutazama kama kuna anayewafuatam, hakuna. Scoba akaiacha barabara kuu na kuingia barabara ndogo.
“Vipi?” Amata akauliza.
“Katika barabara kuu kama ile, kamera za usalama ni nyingi, hatutaweza kufanikisha misheni yetu,” Scoba akajibu huku akipita barabara yenye vumbi jingi, kandokando ya machimbo ya mawe.
“Angalia katapila tu!” Amata akaongea kwa woga baada ya kuona mwendo wa Scoba na jinsi anavyoyapita maskaveta.
“Upo salama braza, shaka ondoa!’ Scoba akajibu huku akikunja kona kali na kuingia kwenye handaki refu na kubwa, lenye uwezo wa kupitisha magari sita kwa wakati mmoja. Nyuma yao wakasikia kishindo kikubwa na vumbi likitimka. Ajali mbaya ilitokea kati ya gari moja dogo lililokuwa likiwafuatilia kugongana uso kwa uso na skaveta la kutengeneza barabara. Ndani ya gari kulitawaliwa na ukimya, Scoba aliendelea kucheza na usukani. Mara baada ya kuliacha handaki hilo, akapita barabara ndogo ndogo za mitaani, na kuibukia pembezoni mwa jiji hilo.
“Hema ya mkutano?” Amata akauliza.
“Ndiyo, Carmo Convent...” Scoba akamjibu huku akiingiza gari kwenye lango dogo la kutosha wao tu. Akaendesha taratibu kuufuata ushoroba huo wenye giza, uliogeuka kuwa makazi ya buibui na popo. Mwisho wakaibukia kwenye veranda ndogo isiyo na kitu chochote. Taa za gari zikammulika Madam S aliyekuwa amesimama kando kidogo. Amata akamtambua Chiba, TSA 2. Naye alikuwa kasimama hapo na ubamba wake mkononi.
“Karibuni katika Convent ya Carmo...!” Madam S akawaambia Scoba na Amata wakati wakiteremka katika gari hilo. Buti likafunguliwa, Mwanachia akaonekana akiwa amejikunyata ndani yake.
“Umejikunja kama ulivyokuwa tumboni mwa mama yako, mwanaharamu mkubwa!” Madam S akamwambia kwa gadhabu akiwa na bastola mkononi. “Mtoeni, mleteni hapa!” akawaamuru.
* * *
Carmo Convent katika jiji la Lisbon ni sehemu ya makumbusho. Gofu hilo la kanisa ni matokeo ya tetemeko kubwa la ardhi lililotikisa jiji hilo mwaka 1755. Tukio hilo la kuogofya lilitokea tarehe 1 ya mwezi Novemba mwaka huo, siku ya jumapili, Wakristu wakiwa wamejaa ndani yake kusherehekea sikukuu ya Watakatifu wote. Pamoja na tetemeko hilo kuwa kubwa, ni paa tu lililoezuka lakini kuta zake zipo hadi leo. Nchi hiyo imelifanya kuwa eneo la makumbusho ya kihistoria.
Ndani ya gofu hili, mengi hutukia, watu hutumia kwa sherehe, mafunzo, mikutano na mambo mengine ya kijamii. Ni sehemu ya chini ya jengo hili ambako daima hakutumiki, na wapo ambao hata hawakujua kama kuna vyumba au nyumba chini ya jengo hilo. Madam S na Chiba, baada ya kutafiti wapi pa kutimizia kazi yao, walipachagua. Ni Chiba aliyeweka vifaa vyake vya kielektroniki kuhakikisha hilo linawezekana. Kumwongoza Scoba mpaka eneo hilo.
Timu yote ya TSA ilikuwa imetimia ndani ya jengo hilo. Gina akavuta kiti kimoja cha chuma, kikuukuu kilichokuwa eneo hilo. Amata akamkalisha juu ya kiti hicho.
“Za mwizi arobaini, hata kama zikija baada ya miaka mia...” Madam S akamwambia Mwanachia, “mvueni nguo zote!” akaamuru.
“Hah!”Mwanachia akatoa sauti na kuinua uso uliojaa damu. Akafumbua macho na kumtazama mwanamama huyo anayeamuru avuliwe nguo.
“Safi, nilitaka tutazamane, nilifikiri umelala au umezimia... Vincent Mwanachia, mpiganaji mahiri ambaye Afrika na Tanzania tunajivunia kuwa naye. Ukaamua kuasi jeshi lako tukufu, ukadiriki kushiriki uasi mwaka 1980 kwa mara ya pili. Nini hasa lilikuwa lengo lenu? Tunajua kuwa mlikuwa mnataka kulikomboa taifa lenu dhidi ya makucha ya siasa za Mashariki za Ujamaa na kujitegemea... kwa nini mlilikimbia taifa lenu baada ya kushindwa?” Madam S akamuuliza mateka wake aliyekuwa akihema kwa shida.
Hakujibu kitu, badala yake alikuwa na kitu kama kwikwi kikimjia mara kwa mara. Macho yake madogo yalimtazama mwanamama huyo aliyekuwa mita mbili kutoka pale.
“Kamwe hamtoweza kufisha juhudi...” akajibu kwa mkato huku akirudisha uso wake chini.
“Nani aliyekwambia? Nataka unambie wako wapi washirika wako waliobaki?” akamtupia swali.
“Aha ha ha ha haaaaa! A ha ha ha haaaaa!” Mwanachia akaanua kicheko kilichofanya mwangwi wa kutisha. Popo wakatoka katika maficho yao na kuruka huku na huko.
“Achana na sisi wewe malaya uliyekosa kizazi...!” Mwanachia akamwambia Madam S.
Kutoka pale aliposimama, Selina alifyatuka mithiri ya Shaolin, teke moja zito likatua shavuni mwa Mwanachia, akaenda chini mzima mzima. Madam S akaanza kumfuata pale chini, Kamanda Amata akamuwahi na kumvuta nyuma.
“Aaaaaakkkkhhhhh, mwanamke mpumbavu, aaaaaaakkkhhhhh!” Mwanachia akaugulia pale chini. Kwa jinsi alivyokuwa akiongea ilikuwa dhahiri shahiri kuwa amepata maumivu makali katika taya lake.
“Rudia tena nikuue mwanaharamu wewe!” Madam S akang’aka kwa hasira. Mwanachia akaketishwa tena kitini.
“Wako wapi washirika wako?” safari hii swali likatoka kwa Kamanda Amata, akiwa na mkasi mkali mkononi aliyouchukua katika mkoba wa daktari Jasmini sekunde chache baada ya kumuacha Madam S.
“Wewe ni nani uniulize swali kama hilo?” Mwanachia akajibu kwa swali tena kijeuri.
“Majibu ya ‘Yesu’ kwangu huwa hayana nafasi!” Amata akamwambia, ma kumkamata kichwa, akaupachika mkasi sikioni, akasukuma vidole vyake na kuanza kulikata sikio. Damu ikaanza kumwagika.
“Aaaaaaiiiiiiyyyyaaa..... nasema nasema nasema!” akapiga kelele. Amata akalegeza mkono, tayari nusu ya sikio ilikuwa ikining’inia.
“Sema, wako wapi?”
“Rua Camarante, lote 25, aaaaaaiiiiii minha orelha minha orelha,” akaeleza kwa taabu huku akigugumia maumivu. Akawataji mtaa na namba ya kitalu. Wakati hayo yakiendelea mara vikasikika vishindo vya watu wakiteremka ngazi kuja chini ya jengo hilo. Amata akawapa ishara wenzake. Sekunde tatu zilikuwa nyingi sana, wakajificha gizani na kumwacha Mwanachia peke yake pale kitini.
Mara watu wanne wakaingia wakiwa na bunduki mikononi mwao. Wakajipanga mduara, wakimweka Mwanachia kati. Watu wale walikuwa wamevalia nuo nyeusi tupu na nyuso zao zilifichwa kwa barakoa.
“Camarada. você está seguro agora…” mmoja wao akamwakikishia usalama.
“Nós não ... estamos seguros,” akawaambia kuwa hawako salama.
Alipomaliza tu kusema hayo, akajishika paji la uso na kukodoa macho, taratibu akaenda chini mpaka sakafuni na kutua kama mzigo. Risasi ndogo ilididimia katika paji lake la uso na kuishia ndani ya kichwa chake. Yule bwana akamuwahi pale chini.
“Camarada! Camaradaaaaa!” akaita. Akamtikisa. Hakutikisika. “Foi morto, aaaaaaaaaah! Watalipa kifo hiki,” akawaambia wenzake kuwa, ameuawa. Shabaha ya Kamanda Amata kutoka mafichoni ilihitimisha maisha ya mpiganaji muasi, Vincent Mwanachia, akiwa wa pili kwenye orodha aliyopewa na bosi wake iliyomtaka kuwaua.
Wale jamaa wakatawanyika ndani ya lile jengo wakitafuta huku na kule, wasione mtu. Madam S na jeshi lake tayari walikuwa nje, ndani ya gari wakielekea katika maficho yao.
* * *
Taarifa za kuuawa kwa Vincent Mwanachia, zilifika haraka katika moja ya visiwa vya kihistoria katika Bahari ya Hindi. Hapa ndipo bwana mkubwa, mkuu wa sindiketi ile aliweka makazi pamoja na mipango mingine mingi ilisukwa katika kisiwa hiki.
Nje ya jumba kubwa ambalo wengi wao walipenda kuliita Camp Site, aliyekuwa waziri wa zamani wa mambo ya nje, Mr. Mc Tee alijikuta akiangukwa na bilauri ya mvinyo iliyokuwa mikononi mwake. Haraka, akaelekea ndani ya nyumba hiyo na kuteremka ngazi mpaka sakafu ya chini. Akafungua moja ya chumba vidogo vilivyojenwa huko na kuingia kwenye boti. Boti hii ndogo iliweza kupita chini kwa chini kama nyambizi za kivita. Akawasha mtambo wake na kuondoka. Daima wafanyakazi wake walijua kuwa akiingia katika chumba hicho huwa ofisini.
Safari yake iliishia katika kisiwa kingine, umbali wa kilomita mbili hivi. Nako, vivyo hivyo, chombo kile kilisimama chini ya bahari, kisha kikapanda juu taratibu na kutokea katika uwa mpana wa nyumba. Kibwana akateremka na kulakiwa na vijana wake kama sita hivi waliokuwa wakiishi humo.
“Andaeni mazingira kesho kikao cha Sindiketi kitakuwa hapa!” akawaambia huku akiingia ndani ya nyumba hivyo.
“Karibu mpenzi!” Akakaribishwa na mwaDanada wa Kihindi, mwenye nywele mpaka kiunoni. Weupe wake haukuwa hata na tone la chunuzi mintarafu kipele. Alikuwa ndani ya vazi mwororo, la hariri, jepesi lililomuonesha wazi maungo yake. Mwanamke huyu alikuwa hapa kwa kazi moja tu, kumfurahisha kimahaba mwanaume huyu.
Kibwana hakujibu neno, aliongoza mpaka chumba kingine, akaingia na kujifungia, akimwacha yule mwanamke katika sebule ndogo. Hassna, msichana wa miaka ishirini na sita tu, mwenye asili ya Kihindi upande wa mama na Mndengereko kwa baba, alijikuta akiwa mfanyakazi wa ndani katika camp hiyo. Akisafisha vyumba vya watalii wajao hapo na wageni wengine. Bosi akampenda kwa ukarimu wake, akataka binti huyo ahamishiwe kwenye nyumba hiyo iliyo mbali kidogo na camp za wageni. Kwa kuahidiwa pesa nzuri ya kila mwezi, akakubali na kujikuta ndani ya kifungo hasichotarajia. Mke bila ndoa, mpenzi pasi na makubaliano, mama bila watoto. Hakuwa na budi kukubali yote haya pale alipotishiwa kuuawa endapo angekataa kuwa kiburudisho. Ukimtazama anavutia, kiuno chembamba, makalio makubwa kiasi, yanashikika. Kifua chenye matiti kama mapapai machanga, na chuchu kali zenye kuchoma kila amkumbatiaye.
Ndani ya chumba hiki, kulikuwa na meza moja, kompyuta kubwa na kitabu cha kumbukumbu juu yake. Hakukuwa na kiti kingine. Akaketi na kuiwasha ile kompyuta mbele yake. Kisha akachukua kifaa cha kusikilizia akakipachika kichwani mwake mpaka masikioni.
“Lisbon is down!” akasikika akisema. Mc Tee akatulia kimya kwa jozi la sekunde akisikiliza ujumbe wa upande wa pili.
“Bado nashindwa kujua hasa ni jinsi gani wanaweza kutembea juu ya nyayo zetu?” akasikika akisema. Kisha akatulia tena kimya akisikiliza mtu wa upande wa pili. Baada ya dakika kama kumi hivi, akavua kile kidubwasha masikioni mwake na kukipachika kwenye kining’inizio chake. Akaegama kitini na kushusha pumzi ndefu. Baada ya kubofya kitufe fulani, mlango ukafunguliwa. Hassna akaingia ndani, manukato yaliyomfuata nyuma yalikijaza chumba kile na kukifanya kuwa kama pepo ndogo.
“Karibu malkia wangu. Moyo wangu umesawajika, wahitaji tulizo...” akamwambia.
“Hapa nipo kwa ajili yako, kama utakavyo bwana wangu!” Sauti nyororo ya msichana huyo ikapenya masikioni mwa Mc Tee, mwaDanamu mwenye moyo wa pekee kwa waliomzunguka.
Misaada aliyokuwa akiitoa kwa mashule, hospitali na jamii kwa ujumla ilimfanya ajulikane, apendwe, atukuzwe. Mwekezaji, aliyepewa ekari za kutosha katika Kisiwa cha Mafia, Mashariki mwa Tanzania. Mc Tee akajenga kambi kubwa ya kitalii, yenye kila aina ya burudani kwa wenye nazo. Mapumziko kwa wapendanao, likizo kwa watokao mbali, picnics na vikao mbalimbali vya serikali na taasisi zake vilifanyika hapo.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP13

aliyepewa ekari za kutosha katika Kisiwa cha Mafia, Mashariki mwa Tanzania. Mc Tee akajenga kambi kubwa ya kitalii, yenye kila aina ya burudani kwa wenye nazo. Mapumziko kwa wapendanao, likizo kwa watokao mbali, picnics na vikao mbalimbali vya serikali na taasisi zake vilifanyika hapo.
Nyumba aliyokuwa akiishi Mc Tee ilikuwa kando kidogo ya ile kambi ya kitalii. Hapo alikuwa akiishi peke yake. Waliokuwa wakiingia na kutoka ndani humo ni wafanyakazi tu. Hakuna aliyewahi kumwona na watoto wala mke. Alikuwa kapela. Lakini umriwe haukuendana na hali hiyo, ilishangaza. Wengine wakasema ‘labda mkewe yuko kwao India’ na waliobaki wakadhani mgonjwa. Ni Hassna tu aliyeujua ukweli wa mambo. Akasimama nyuma ya kiti hicho, akaanza kumkandakanda mabegani.
“Unaonekana hauko sawa boss!” Hassna akasema. Mc Tee akaishika mikono ya msichana huyo na kumvuta chini kidogo. Shingo zao zikakutana, wakatazamana kwa pembe.
“Kuna jambo limenivuruga,” akamjibu.
“Pole, nipo kwa ajili yako kama utakavyo,” Hassna akasema.
“Ndo maana nilikuchagua kuwa mfariji wangu. Unajua wakati gani unifanyie nini...” Mc Tee akamwambia Hassna, akamvuta kwa mbele na ndimi zao zikakutana. Chumba hakikuwa kikubwa wala hakikutosha kwa kilichoendelea kwa kuwa hakikuwa maalumu. Mkutano wa miili ya wawili hawa ukawa wa burudani zote, harufu nzuriilitawanyika kila Hassna alipoongeza manjonjo katika mtanange huo. Dakika arobaini na tano ziliwaacha hoi, kila mmoja akihema kama mbwa, vinywa wazi. Hassna bado alitamani kuendelea lakini Mc Tee alikuwa nyng’anyang’a. Simu ya mezani ikaita kwa fujo, akamwacha mwanamke huyo na kuinyakua.
“Yes Comrade!” akaitikia kwa kuwa alijua ni wapi simu hiyo inatoka.
“...sawa gati namba mbili ni salama!” akajibu na kukata simu. Akamtazama Hassna, kisha akarudisha macho kwenye ile kompyuta.
“Kesho kuna kikao, weka kile chumba tayari na vile vya wageni vyote viwe katika hali ya usafi...” akamwambia.
* * *
Siku hiyo hiyo, ndani ya jumba kubwa lililojengwa pembezoni mwa ufukwe wa Tamariz katika kijiji cha Cascais, Mghalibi mwa jiji la Lisbon, TSA walikutana. Kutokana na usiri wa kazi yao, ni Madam S pekee aliyekuwa akijua kuwa timu hiyo ipo jijini Lisbon. Kila mmoja alitumwa kwa kazi yake na aliifanya kwa weledi wote. Kamanda Amata na Madam S walikuwa wa mwisho kuwasili katika jiji hilo. Mikononi mwa wote, mlikuwa na kazi moja tu iliyofumbwa kwao isipokuwa Amata. Yeye alijuwa wazi kuwa anakwenda kuitoa roho ya Vincent Mwanachia.
Walikuwa ndani ya chumba kidogo, kila mmoja akiwa amemaliza kazi yake kiukamilifu. Ukimya ulitawala, hata sindano ingeanguka, basi ingesikika kiurahisi sana. Gina alikuwa akimtazama Amata kwa jicho pembe, lakini hakusema lolote.
Katika tukio hili mambo yalikuwa tofauti kabisa, ukilinganisha na lile la Ubelgiji. Na hili ndilo lilifanya Madam S awakutanishe wote katika pango lile kongwe la Carmo Convent.
“Sikutaka iwe hivi, lakini kaka yenu amefanya iwe hivyo...” Madam S akawaambia vijana wake, kisha akatulia kwa jozi la sekunde.
“Wakati mwingine inabidi, ili kuhakikisha usalama wa ninyi nyote. Hatuna muda wa kupopteza sasa, tumeshamwondoa ayawani wa pili, hao wengine tutajipanga tufanyeje!” Madam akaeleza, “cha muhimu kwa sasa ni kila mtu kuondoka, tutaonana Dar es salaam,” akaogeza kusema.
Muda wote ambao Madam S alikuwa akiongea, chumba kile kilitawaliwa na ukimya wa kuogofya. Ubongo wa kila mtu ulikuwa ukitafakari tukio lililopita usiku huo.
“Dana na mkuu wake lazima washughulikiwe, walitaka kutuingiza chaka,” Amata akasema.
“Hilo halina shaka,” Madam akamjibu.
Baada ya mazungumzo machache, wakatawanyika, kila mmoja akiwa na jambo moja tu mbele yake, kufika Dar es salaam.
Dakika zilizofuatia, ndani ya chumba kile alibaki Kamanda Amata na Madam S pekee.
“Hongera Kamanda, akili uliyoitumia leo, imeokoa mengi sana katika upande wetu,” Madam S akamwambia Amata.
“Ilibidi nicheze plani B. Na nina uhakika kilichotokea leo, kitawafanya wajifikirie uzembe walifanya wapi,” Amata akajibu.
“Sure! Sure! Sasa kibarua ni hiki kinachotukabili... bado watatu, Marehemu Kibwana Mtokambali... lazima tujue kazikwa wapi. James Msambamagoya na Jesca Tibatulanwa,” akamwambia.
“Kuwapata hawa ni kazi nzito maana hata fununu hatuna,” Amata akasema.
“Watapatikana tu, TSA si idara ya kuchezea ...”
“Hakika...” Amata akamalizia kwa jibu fupi. “Usiku huu, lazima nifike Rua Camarante, lote 25, kama alivyosema mwenyewe Mwanachia,” Amata akaeleza.
“No Kamanda, achana na hilo, huwezi kujua isije kuwa mtego,” Madam S akaingiwa na woa na kumwonya Amata.
“Kumbuka swali tulilomuuliza, kabla hajafa akajibu namna hii... inatubidi twende. Hatari na vifo ndiyo sehemu ya maisha tuliyoichagua, kwa nini tuogope?”Amata akamuuliza bosi wake.
“Ok ninaheshimu mawazo yako. Kumbe Gina angebaki kukusaidia maana najua unaweza jikuta msambweni,” akasema Madam S.
“Ni kweli, ila angenitia uvivu, nitalishughulikia mwenyewe... naamini sintoiacha roho yangu ugenini...” Amata akasema huku tayari akiwa ameinuka. Madam S akamtazama kutokea pale alipoketi, akambania jicho la kulia.
“All te best kijana! Taifa linakutegemea,” Madam akamwambia, kisha akamshuhudia Amata akipotelea nje ya ile nyumba ndogo iliyojengwa kando tu ya ufukwe wa Tamariz.
* * *

Rua Camarante, lote 25

Kamanda Amata alipita kwa mwendo wa taratibu katika barabara hiyo akichunguza vibao vinavyoonesha namba za viwanja. Haikumuwia ngumu kukiona kile anachokihitaji. Kitalu namba 25. Akatikisa kichwa kuwa ndicho haswa. Kwa mwendo uleule, akaendelea kuifuata barabara ile mpaka upande wa pili. Katika barabara ile, kulikuwa na baa mgahawa wa kisasa uliojitambulisha kwa harufuza vyakula.
Amata akaegesha gari katika mgahawa huo, akateremka na kuliacha hapo. Akavuka barabara, na kwa hatua za wastani akatembea kurudi na ile barabara mpaka alipoifikia ile nyumba. Akachukua kama dakika mbili hivi kama si tatu kuchunguza usalama wake. Alipojiridhisha na usalama wa nyumba hiyo, ilimchukua sekunde tatu kuuruka ukuta na kutua ndani bila klufanya kishindo. Sekunde nyingine tano zikamfikisha kwenye mlango wa barazani. Akatembeza macho yake katika maua yaliyopandwa eneo hilo. Japo hakutaona vyema kutokana na giza la usiku huo, kiukweli alikuwa akiangalia kitu kingine kabisa. Hisia zake zilipomruhusu, akapachika ufunguo wake na kufungua mlango huo pasi na kipingamizi. Akakaribishwa na sebule ya wastani yenye viti vinne tu, na juu ya meza ndogo iliyozungukwa na viti hivyo, kulikuwa na klibweta cha jivu la sigara. Yote haya aliyaona kwa miwani yake maalumu yenye uwezo wa kuona gizani. Alipoambaza macho ukutani, alikutana na picha moja ya watu watano. Wawili kati yao walivalia mavazi ya kijeshi. Mmoja wao alikuwa mwanamke. Picha hii ilivutia macho ya Amata, akaisogelea. Hakuiacha. Baada ya kuichukua, akaendelea na safari yake kwa kupita chumba kimoja baada ya kingine. Ni kwenye chumba cha mwisho ndipo alipopata anachofikiri. Kompyuta, laptop, ilikuwa mezani. Pembeni ya meza hiyo kulikuwa na kitanda kilichovurugika kana kwamba kulikuwa na watu waliokuwa wakikitumia. Hilo halikumvuta. Kompyuta, hiyo ndiyo iliufurahisha moyo wake. Hakuibeba, aliigeuza kwa mikono yake yenye glovu nzito za ngozi. Kwa vifaa vyake, akaipachua Hard Disc na kuitia mfukoni.
Alipokuwa akitaka kutoka, akasikia muungurumo wa gari, mara geti likafunguka. Amata akatoka haraka na kujificha kwenye chumba cha pili.mlango wa chumba hicho akauacha wazi kidogo sana ili tu aone nini na nani wapo ndani humo.
“Kama tutaikuta itakuwa heri sana!” sauti ya kiume ilisikika wakati mlango ukifunguliwa.
“Lazima iwepo, tuliiacha baada ya kumaliza kazi yetu, na alisema atakuja aichukue ili aipeleke...” sauti ya kike ikajibu. Wakapita na kufungua kile chumba, wakaingia.
“Oh, Thank God! Hii hapa,” yule jamaa akasema. Amata akawaona wakitoka tena, mkononi mwa yule kijana alikuwa na ile kompyuta.
Nimewawahi! Amata akawaza huku akiwang’ong’a. Akawaacha waende. Aliposikia muungurumo wa gali likiondoka, na yeye akajitokeza na kutembea haraka haraka. Kwa njia ileile aliyoingilia ndipo akatokea na kupotelea gizani.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP14

DAR ES SALAAM

1981

NDANI YA OFISI YAKE YA SIRI, Chameleone, alipokea taarifa za kutoweka kwa Waziri Kibwana Mtokambali. Haikumuingia akilini hata kidogo. Akaona, kuna haja ya kufanya haraka kuwatia mbaroni wote waliohusika na njama hiyo. Akavuta droo ya meza yake na kuchukua ile karatasi, akatazama orodha nzima. Kisha akaangalia na orodha nyingine ambayo aliipata kupitia watu wake wa siri, aliowapa kazi hiyo.
“Swadakta!” Akajisemea.
Kwa kutumia simu yake ya mezani, akatoa amri ya kukamatwa wote ambao wameorodheshwa katika karatasi hizo mbili. Mshike mshike ukaanza, kambi kwa kambi, nyumba kwa nyumba. Wengi wakatiwa mbaroni. Waliohusika kwa namna yoyote ile, walikamatwa.
Kwa saa kadhaa, hakutoka pale ofisini, alikuwa akisubiri apate taarifa ya nani na nani wapo katika mikono ya dola. Kufikia jioni ya siku hiyo, akiwa ameshapanga mipango yake vizuri, simu ya mezani ikaita. Akainyakuwa na kuiweka sikioni.
“Hallo!” Akaita.
“Hallo... pokea taarifa nzito kama ifuatavyo,”sauti ya upande wa pili ikamwambia.
“Mia!” Akajibu, akiwa na maana ya kumruhusu aendelee. Kutoka upande wa pili akapatiwa majina ya watu wote waliotiwa mbaroni katika operesheni ile.
“Katika orodha ya kwanza hatujaweza kuona hata nyanyo...”
“Kati ya zote?”
“Ndiyo!”
Taarifa hii haikumpa furaha Chameleone. Kwa upande wake alipenda hao ‘papa’ wakamatwe kwanza maana ndiyo wasuka mipango. Mara hii akanyanyuka kutoka kitini, akachukua miwani yake na kuipachika usoni. Akatoka katika ofisi hiyo na kuingia katika gari lake, Land Rover 109. Akalitia moto na kuondoka zake.
Haikumchukua muda mrefu, akaingia katika viwanja vya Ikulu, Magogoni. Kila aliyekutana naye alikuwa katika hali isiyo ya kawaida. Zaidi ya kusalimiana kwa kupungiana mikono, hakuna lililoongelewa. Akazikwea ngazi na kupotelea ndani ya jengo hilo jeupe. Breki ya kwanza ikawa katika ofisi ya Makamu wa Rais. Akamkuta. Mzee huyo alitamani kumrukia Chameleone. Alisimama haraka na kukiacha kiti chake, akavuta hatua kama tatu hivi na kumfikia mwanausalama huyo.
“Afadhali umefika. Kuna mambo tata hapa, tumeshindwa kuyapatia ufumbuzi,” akamwambia.
“Usiwe na wasiwasi mkuu, vijana wapo kazini, kila lenye utata litatatuliwa,” Chameleone akajibu huku akivuta kiti kukaa na Makamu wa Rais akafanya vivyo hivyo.
“Nchi imekuwa kimya, napokea simu kutoka kwa majirani wanauliza kuhusu Mheshimiwa Rais, wao wanajua tumepinduliwa,” Makamu akaeleza.
“Ukawajibu nini?”
“Nimewaambia tu watulie, maadam mimi ndiye ninayeongea basi nchi haijapinduliwa”.
“Ni sahihi, nchi ipo salama, na Rais yupo salama kabisa. Naamini jioni ya leo atalihutubia taifa,” Chameleone akasema. Mara hiyo hiyo, mlango ukafunguliwa, msichana mbichi mwenye umbo la kuvutia, akaingia ndani. Nywele zake ndefu zilizochanwa Afro, ziliudhihirisha ulimbwende wake. Sketi yake ya mtindo wa Zembwela ilimkaa vyema mwilini. Akasimama kando, kwa heshima zote, akakabidhi faili moja kwa Chameleone.
“Asante Selina, nipatie taarifa yako kwa kifupi,” akamwambia.
“Operesheni imekamilika kwa asilimia themanini. Tumewatia mbaroni watu wapatao ishirini na tatu. Wote hao wamehifadhiwa katika Gereza la Ukonga kusubiri utaratibu mwingine wa mahojiano. Lakini watu watano, wenye vyeo vya juu, ambao imesadikiwa ndiyo wasuka mipango, wametoweka kabisa. Kwa tafiti zetu mpaka sasa hatujapata fununu yoyote, na upelelezi unaendelea. Hayo tu,” Selina akamaliza kuwasilisha taarifa hiyo.
“Asante kaendelee na kazi,” Chameleone, akamjibu na kumruhusu kuondoka. Akamgeukia tena Makamu wa Rais na kumsukumia kabrasha lile. Alipolipokea akamwambia, “sitaki kuamini kabisa kama Waziri Mtokambali ni mmojawapo”.
“Kikulacho, ki nguoni mwako mheshimiwa. Tegemea kumpokea Rais muda wowote kutoka sasa,” akamwambia na kusimama, wakaagana.


KIGAMBONI

Katika nyumba pweke aliyokuwa amehifadhiwa Mkuu wa nchi, hakukutokea lolote la kuhatarisha maisha yake. Yeye alikuwa akifuatilia kila kitu kupitia redio ndogo aliyokuwa ameachiwa na mlinzi wake. Punde si punde, akasikia muungurumo wa gari likisimama nje ya nyumba hiyo. Akatulia kusubiri kuona nini kitajiri. Haikusikika sauti ya mtu yeyote kuongea isipokuwa hatua tu za mtu anayetembea haraka haraka.
Mlango ukafunguliwa, mtu huyo akaingia ndani mpaka kwenye kile chumba.
“Mkuu, natumaini u mzima!” Akasema Chameleone.
“Bukheri wa afya. Nilikuwa naendelea kufuatilia taarifa mbalimbali hapa za ndani na nje ya nchi kwa redio hii. Dunia inasadiki kuwa tumepinduliwa...”
“Ni kweli, lakini sasa ni wakati wa kuishangaza pia. Nimekufuata, nikurudishe Ikulu, ukaendelee na majukumu yako. Watanzania wanaisubiri sauti yako kwa hamu sana. Wamekuwa kama vifaranga vilivyonyeshewa na havimuoni mama yao,” Chameleone akamkatisha kwa sentensi yake. Baada ya mazungumzo mafupi wakatoka pamoja na kuingia kwenye gari. Tayari ilitimu saa kumi jioni, walipoondoka na kuiacha nyumba hiyo.
Jambo alilolifanya mwanausalama huyu, ni kumfikisha Rais, kwanza katika ofisi yake ya siri. Akampa taarifa yote ya kazi inayoendelea. Pia akamweleza na wale waliotoroka.
“Hata wakitoroka, kesi yao itakuwa palepale na sheria itawashughulikia maadam hawajatorokea sayari nyingine,” Rais akasema. Kishapo, akamchukua na kumpitisha mlango wa nyuma, mjia za siri mpaka katika jengo la Ikulu. Akaingia naye ndani mpaka katika ofisi yake. Wafanyakazi waliokuwa katika mfadhaiko mkubwa, walipomwona, wapo waliotamani kupiga vigeregere, wengine hata kumbeba.
Taarifa ya kurudi kwa Rais Ikulu, ikasambaa kama moshi wa kifuu. Akapokelewa na makamu wake, Waziri wa Ulinzi na wa Mambo ya ndani. Wanausalama nao wakachukua nafasi zao kumuwekea ulinzi mkuu wa nchi.
Ndani ya ofisi ya Rais, ilikuwa ni kupokea taarifa tu za sakati zima. Saa moja usiku ya siku hiyo hiyo, mafundi wa Redio Tanzania walikuwa pale na OB Van lao, tayari kurusha hotuba ya Rais mubashara. Katika chumba maalumu kilichoandaliwa kwa shughuli hiyo, wanahabari, pamoja na wanausalama, walikuwa kimya kusubiri nini kitaendelea. Katika hali ya kushangaza hawakuamini walipomwona Rais yuleyule ambaye alitoweka kwa saa kadhaa na watu kujua kuwa ameuawa. Makofi ya shangwe yakasikika na kukijaza chumba kizima.
Hotuba ya kusisimua ikawafikia Watanzania popote walipo. Hoi hoi na nderemo zikasikika kila kona ya nchi. Akinamama wakaimba, akina baba wakapiga ngoma, ili mradi ni furaha. Waliotaka mapinduzi wakabaki vinywa wazi, hawana la kusema. Aibu ikawapata popote walipo. Nchi ikatulia, maisha yakaendelea.

Majuma matatu baadae...
Katika Mahakama Kuu, kesi ya uhaini ikaunguruma. Nani yumo na nani hayumo, upelelezi ulikuwa ukiendelea. Wengine wakaachwa huru na wengine wakapata kifungo cha maisha jela. Watano kati ya wote waliotajwa katika kesi hiyo hawakuwepo maakamani na wala haikufahamika wapi walipo. Wamekufa au wapo hai. Utata.
Kwa upande wa mahakama hilo halikuzuia kitu. Jaji aliyekuwa anaendesha kesi hiyo alisoma hukumu ya dakika arobaini na tano. Akawahukumu kifo watu hao watano akiwataja kwa majina; aliyekuwa mkuu wa kikosi cha Jeshi la Anga Titus Mwakibinga, aliyekuwa mkuu wa kambi ya Twalipo, Vincent Mwanachia, aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Kibwana Mtokambali na James James Msambamagoya, mwanausalama namba mbili wa Rais. Mahakama ikafungwa.
Mara baada ya sakata hilo, Rais akaifumua idara ya Usalama wa Taifa na kupanga upya safu yake. Pamoja nayo ikaanzishwa falsafa ya ‘kila mwananchi ni mlinzi wa taifa lake’. Hatua nyingine ikachukuliwa, wakatengenezwa mapandikizi na kupandikizwa kila Nyanja iwe ya kiserikali au binafsi. Yote , ili kupata habari yoyote hata iwe ndogo kiasi gani. Ikafanikiwa.
* * *


MAKAO MAKUU YA T.S.A MARCH 1999

Juu ya meza kubwa anayoitumia Madam S, palikuwa na bahasha moja ya khaki iliyopigwa mhuri uliosomeka ‘CONFIDENCIAL’. Asubuhi hii mara tu baada ya kupata kifungua kinywa, aliichukua bahasha hiyo na kuichana ili kupata kujua nini hasa kipo ndani yake.
‘Ionwe na mhusika tu’ ilianza kwa kuandikwa namna hiyo. Baada ya anwani za serikali na protokalizote za uandishi wa barua kukamilika. Iliendelea.
HATI YA KIFO
…watafutwe popote walipo, wauawe.
Chini yake kukawekwa orodha ya majina manne. Moja kwa moja , Madam S aliukumbuka mkasa huu. Akaendelea kusoma maelezo mengine na kisha akakutana na picha nne za watu hao. Lakini mstari wa mwisho ulidhihirisha wazi kuwa hakuna taarifa yoyote ya wapi watu hao wanapatikana. Na waraka huo ukaeleza kinagaubaga kuwa kuna mapandikizi ya watu hao ndani ya Tanzania, wakifuatilia nyendo na kupata habari zote juu yao. Hata mwanausalama aliyeteuliwa na TNS kufuatilia kujua watu hao wako wapi, alipotea katika mazingira ya kutatanisha mwaka 1990.
Madam S, akaikunja ile karatasi na kuitia kwenye droo.
Limenirudia mwenyewe, sikutegemea kama tutafukua makaburi! Akawaza. Akajiegemeza kitini, kimya. Tayari akili na mawazo yake vikatekwa na maandishi hayo. Saini iliyohitimisha waraka huo ikampa kigugumizi cha kuamua. Tangu litokee sakata la kujaribu kupindua serikali ni miaka kumi na nane ilikuwa imepita. Awamu ya tatu ya utawala, ilikuwa inakaribia kuingia kipindi chake cha pili. Akatafakari kwa jozi la dakika. Aanzie wapi, aishie wapi. Akamkumbuka mwanausalama huyo kijana aliyetoweka, kwa jina moja tu la Dastan. Lakini hakuwahi kujua kama mtu huyo alikuwa kwenye kufuatilia sakata hilo hilo.
Serikali na siri zake! Akawaza.
Naanzia wapi? Akajiuliza. Kila alipoitazama karatasi ile, ilikuwa kana kwamba inamwambia ‘anza sasa’. Madam S akasimama akageukia upande wa nyuma. Macho yake yakatazama nembo kubwa ya TSA iliyonakshiwa kwa nyota sita na kuzungukwa na maandishi, ‘For my people. For my nation’, ikiwa ni sehemu ya kiapo chao, ‘Kwa watu wangu. Kwa taifa langu’. Akapiga saluti, akaketi tena kitini. Akainua mkonga wa simu na kukoroga tarakimu kadhaa.

* * *
ITAENDELEA
 
GENGE
EP15

Macho yake yakatazama nembo kubwa ya TSA iliyonakshiwa kwa nyota sita na kuzungukwa na maandishi, ‘For my people. For my nation’, ikiwa ni sehemu ya kiapo chao, ‘Kwa watu wangu. Kwa taifa langu’. Akapiga saluti, akaketi tena kitini. Akainua mkonga wa simu na kukoroga tarakimu kadhaa.

* * *
Upande wa pili, simu ile ilifikia katika kijimeza kidogo kando ya kitanda kikubwa cha futi tano kwa sita. Kwa uchovu aliokuwa nao, Kamanda Amata akaipuuzia. Hakuijali. Dakika mbili baadae, ikaita tena na kukatika, kasha ikaita kwa mara ya tatu. Akageuka haraka, Danani ya shuka na kuinyakua. Kwa kuwa ilikuwa haina waya, akarudi nayo katikati ya kitanda.
“TSA 1,” akaitikia.
“Unakoroma tu mwanaume…”
“Sasa nifanye nini! Na ndiyo kwanza likizo ipo siku ya pili…”
“Hah! Hah! Hah! Hah! Na ndiyo imesitishwa kwa taarifa yako…” Madam S akacheka na kumwambia Amata, “tukutane Saint Albano nusu saa ijayo”.
Amata akakunja sura kwakukatishwa usingizi wake. Akajivuta kivivuvivu na kuketi, kasha akapia mwayo mrefu na kunyoosha mikono yake; huu upande ule na mwingine ule kule.
Hizi kazi zingine hizi majanga tu, sijui kuna nini tena! Akawaza huku akinyanyuka na kuelekea maliwato. Dakika ishirini baadae akawa jikoni akitengeneza staftahi nyepesi kwa ajili yake. Kahawa ya Kiitaliano, slesi nne za mkate uliopakwa jam, siagi na asali kidogo na ndizi mbivu. Alipojiweka sawa akachukua pikipiki yake kubwa ya Kirusi, Cagiva, tayari kwa safari. Katika jiji la Dar es salaam, ili uwahi miadi, tumia aina hii ya usafiri.
* * *
Kanisa la Anglikana, lililojulikana kama Saint Albano, lilikuwa pembezoni tu mwa Barabara ya Azikiwe karibu kabisa na Posta Mpya. Madam S aliwasili mahali hapo dakika nne tu kabla ya muda wa miadi. Moja kwa moja akaingia katika duka la vitabu na kupitia rafu zilizobeba vitabu mbalimbali. Dakika tatu baadae, Kamanda Amata , naye aliingia katika duka lilo hilo. Moja kwa moja akaelekea katika rafu ambayo Madam S alikuwapo.
“Mama!” akaita kwa sauti ya chini. Madam S akageuka, si kwamba hakumuona, la, bali alitaka kuonesha luwa hawajaonana siku nyingi ili kupoteza mitazamo ya waliomo ndani.
“Oooh mwanangu!” akaitika na kumkumbatia. Kasha wakachukua kama dakika mbili za maamkio hayo. Na baada ya hapo wakatoka mpaka nje ya duka hilo na kuingia katika mgahawa mdogo, wakaketi humo.
“Asubuhi sana Madam!” Amata akamwambia.
“Najua, taarifa inayokuja asubuhi ina mambo yake mwanangu. Niliopna nikikwambia wakati ule ungeweza hata kupoteza fahamu. Lakini taarifa iliyonifikia ni kwamba, mama yako ni mgonjwa na anahitaji msaada wa haraka,” Madam S akamwambia.
“Oh! Anaumwa tena?” Amata akauliza.
“Ndiyo, hali yake imerudi tena kama siku zote, wewe kama mwanawe wa kwanza, anakutegemea sana, tena sana aisee,” Madam S akamwambia. Kisha akatia mkono mfukoni na kuchomoa bahasha ndogo, akampatia. Madam S, akainuka kitini na kuondoka bila kuaga. Amata akamsindikiza kwa macho mpaka alipopotelea katika lango kuu. Akarudisha macho yake kwenye ile bahasha, akaifungua taratibu na kutoa karatasi ndogo ndani yake. Haikuwa na maneno mengi. Macho yake yakagongana na kifungu cha Biblia na maneno machachhe.
‘Rafu namba tano, biblia ya sita kutoka kushoto. Soma, Ezekieli 33:8-9’.
Amata akatulia kimya kwa jozi la sekunde. Hakuelewa nini maana ya maneno hayo. Akainuka taratibu na kurudi mpaka katika duka la vitabu. Mara baada ya kuingia, akaifuata rafu hiyo. Akahesabu mpaka ile Biblia aliyoelekezwa na kuichukua.
Moja kwa moja akafungua kitabu cha Ezekieli sura ile ya telathini na tatu, aya ya nane mpaka ile ya tisa. Ikasomeka…

8 Nikimwambia mtu mwovu:
‘Wewe mtu mwovu hakika utakufa’;
lakini wewe husemi chochote ili kumwonya yule mtu mwovu aachane na mwenendo wake; mtu huyo hakika atakufa kwa kosa lake; walakini nitakudai wewe kifo chake. 9Lakini ukimwonya mwovu aachane na mwenendo wake, naye haachani na mwenendo wake mbaya, yeye atakufa kwa kosa lake; lakini wewe utakuwa umeyaokoa maisha yako.
Kifungu hicho cha maandiko kilisomeka namna hiyo. Baadhi ya maneno yake yalikuwa yamepiiwa mstari kwa wino mwekundu. Kamanda Amata akajua wazi kuna ujumbe uliofichwa ndani yake ambao hakutakiwa kuupata moja kwa moja kiurahisi tu.
Nikimwambia mtu mwovu: ‘Wewe mtu mwovu hakika utakufa’; hakika atakufa kwa kosa lake; Lakini ukimwonya mwovu aachane na mwenendo wake, naye haachani na mwenendo wake mbaya, yeye atakufa kwa kosa lake;
Kamanda Amata akaunganisha maneno hayo akilini mwake, kitu pekee alichong’amua ni kuwa kuna mtu anayetakiwa kufa. Akashikwa na kibuhuti, akatulia kimya kuiacha akili yake itafakari jambo.
Nani? Akajiuliza. Akiwa katika hali hiyo, simu yake ikafurukuta mfukoni, akaitoa na kufunua ujumbe uliokuwa umefika, namba ya mtumaji ilifichwa.
‘Maktaba kuu ya taifa, kitengo cha NBA, gazeti la Mfanyakazi la terehe 14 June, 1980 ukurasa wa 3’.
Hakupoteza muda, akaachana na duka hilo, akaiendea pikipiki yake na kuiwasha. Dakika mbili tu alikuwa katika uwanja wa Maktaba Kuu, akaingia mpaka kule alikoelekezwa. Akapata huduma aliyokuwa anaihitaji. Akaketi kwa utulivu na kuisoma habari yote kwa makini. Habari hiyo ilikuwa ikihusu kesi ya uhaini na hukumu yake. Aliisoma kwa kuirudia rudia. Ndani ya habari hiyo mwandishi aliainisha mambo matatu katika hukumu iliyotolewa na jaji huyo. Hukumu ilikuwa ni kwa kundi la watu waliojaribu kuipindua serikali ya wakati huo. Kundi hilo liligawanywa mara tatu; kuna walioachiwa huru, waliofungwa maisha na wengine walihukumiwa kifo.
Kamanda Amata akashusha pumzi, sasa akaiona kazi inayomkabiri baada ya aya ya mwisho ya habari hiyo kumwambia kuwa waliohukumiwa kifo wote hawakuwapo mahakamani wala nchini kwa ujumla. Akasonya.
Habari hii alikwishakusimuliwa mara nyini na baba yake wakati akiwa shule ya msingi.
Alikadharika aliisikia vijiweni kwa wengi wanaojifanya wanajua mambo. Hasa kuuawa kwa yule Komandoo ijapokuwa kulikuwa na chumvi nyingi ndani yake ili inoge. Hakuwahi kufikiri , lakini leo hii gazeti lilikuwa mbele yake, alichokuwa akikisoma ndicho alichosimuliwa miaka mingi. Akagundua kuwa hata wale wa vijiweni walikuwa hawasomia magazeti ila porojo tu.
Mambo haya mawili yalimfanya Amata azame kwenye tafakari. Kipande cha maandiko matakatifu na Gazeti la Mfanyakazi.
Halafu nini kinafuata? Akajiuliza. Akainuka na kuwaaga wenyeji wake, akapotelea nje. Akiwa tayari juu ya pikipiki yake, kabla ya kuiwasha, mbele yake akakutana uso kwa uso na kijana aliyekuwa akiuza urembo kwenye kisanduku kidogo.
“Kaka mpende mkeo…” yule kijana akamwambia Amata huku akifungua kile kisanduku chake.
“Sijaoa bado!” Akamjibu.
“Hata kama, lakini kuna vile vinavyompendeza shemeji yangu. Fahari ya macho haifilisi duka kaka…” yule kijana akazidi kupigia debe biashara yake huku akifunua upande wa chini kabisa. Macho ya Amata yakagongana na bahasha ndogo nyeupe, juu yake ilikuwa imeandikwa, ‘ZE SINDIKET’.
“Kwa ajili yako hiyo kaka, chukua chukua,” yule kijana akamwambia Amata. Naye akaichukua ile bahasha na kuitia mfukoni. Akachomoa noti ya silini elfu tano akampatia, kisha yule kijana akaondoka zake. Amata akawasha pikipiki yake na kuondoka. Akaikamata barabara ya Bibi Titi mpaka makutano yake na ile ya Ally Hassan Mwinyi. Akaendelea nayo mpaka karibu na njia panda ya kuingia Agha Khan. Akakunja kulia na kuegesha pikipiki mbele ya Kanisa la Orthodox.
Akashuka na kurudi nyuma hatua kadhaa, akaingia katika uwanja wa makaburi wa mashujaa wa Jumuia ya Madola.
Madam S, alisimama karibu kabisa na uziowa makaburi hayo, akitazama jengo la Hospitali ya Agha Khan na kuipa mgongo barabara ya Ally Hassan Mwinyi. Kamanda Amata akasimama kando yake na kujikohoza.
“Umepata changamoto ya kutosha leo,” Madam S akamwambia bila kumtazama.
“Ndiyo nini kunizungusha hivyo?” Amata akauliza.
“Kila ulipopita, pana ujumbe wa kukupa.”
Amata akanyamaza kimya. Macho yake yakiwa upande uleule ambao Madam S alikuwa akitazama.
“Sawa, nimekuja!” Amata akamwambia Madam huku akiiweka vyema miwani yake ya jua. Madam S akageuka na kumtazama kijana wake.
“Safari hii una kazi tofauti kidogo,” akamwambia, “ulikuwa unaua kwa sababu za kujilinda. Lakini sasa unatakiwa kuua kwa agizo kutoka juu…” akavuta hatua kuelekea mlango mkuu wa uwanja huo huku Amata naye akimfuata. Mbele kidogo, akasimama na kumtazama kijana wake. Wakatazamana.
“Una watu wanne wa kuua, kama ulivyosoma kwenye lile gazeti. Mpaka sasa ni mmoja tu ambaye tumeanza kupata harufu ya wapi alipo, wengine watatu ni kitendawili,” akamwambia.
“Kwa hiyo…”
“Kwa hiyo nini? Tafutishi ikikamilika inabidi ukaondoa roho ya huyo jamaa. Ni utekelezaji wa hukumu yake,” Madam S akasema.
Kamanda Amata akashusha pumzi ndefu, akaweka mikono yake kiunoni huku jicho lake likiwa kwa bosi wake.
“Katika hili hili, kuna jambo linanitatiza sana, lakini ukija ofisini tutaongea. Kaweke begi lako tayari kwa kazi, muda wowote hata kama si leo utatakiwa kuondoka,” akamwambia na kuanza kuvuta hatua ndefu ndefu kuelekea nje ya ule uwanja.
“Na likizo yangu…”
“Utamalizia ukirudi,” akamjibu na kuingia arini tayari kwa safari.
Kamanda Amata akabaki kimya akilitazama gari la Madam S likipotelea mjini. Akaitazama pikipiki yake, kisha akaifuata na kusimama kando yake. Kichwa chake kikazama kwenye lindi la mawazo. Kazi mpya imemfikia.
“ulikuwa unaua kwa sababu za kujilinda. Lakini sasa unatakiwa kuua kwa agizo kutoka juu…”
Sauti ya Madam S ikamrudia kwa mwangwi katika ubongo wake.
Natakiwa kuwa muuaji. Assassin! Akawaza moyoni. Kamanda Amata hakuwa na jingine, zaidi ni kukubali kazi. Kama aliichagua na kuikubali kazi ya Kijasusi basi hakuwa na budi kukubaliana na yote yaliyo ndani yake, maadam tu yanakuwa ndani ya kiapo chake. Akapanda pikipiki yake na kuondoka.
* * *
Jioni ya siku hiyo hiyo, Madam S alipokea nukushi kutoka nchi ya mbali. Na hakika alikuwa akiisubiri hiyo kwa saa nyingi.
‘Kazi imekamilika kwa aslimia sabini na tano,
Tumefanya kila kitu, kilichobaki nikubeba mzigo we tu.
HIvyo waweza tuma lori limalize kazi hii… Omega!’
Nukushi ile iliishia hapo. Yeye Madam S aliielewa vyema kile ilichokuwa ikimwambia. Akaichukua ile karatasi na kuikunja kisha akaitia kwenye droo yake ya mezani. Akavuta simu yake na kupiga tarakimu kadhaa kisha akasubiri.
“Kumekucha, njoo ofisini ukiwa tayari kwa safari,” Madam S akazunumza sentensi hiyo moja tu na kukata simu. Muda uliombakia alikuwa akipa simu huku na kule akiweka vizuri jambo hili na lile. Nusu saa baadae, mlango wa ofisi ukagongwa, Kamanda Amata akaingia.
“Safi sana, umevaa kama mcheza kamali leo,” akamtania.
“Kawaida yangu,” Amata akajibu huku akijikaribisha kitini. Suti ya gharama iliusitiri mwili wake, na kumfanya aonekane haswa, kibopa. “Na ole wako unipe tiketi ya economy, nitarudia hapa hapakuendelea na likizo yangu,” akamwambia.
“Usijali mwanangu!” akamwambia na kumpatia bahasha nyeupe iliyofungwa barabara. Kamanda Amata akaichana, ndani yake akatoa tiketi ya ndege na kadi janja ya Master itakayomwezesha kutoa pesa popote pale duniani. Alipojiridhisha akaitia ndani ya mfuko wa koti. Madam S akampatia bahasha nyingine. Akaichana, ndani yake ikadondoka picha, akaitazama na kuigeuzageuza kisha akachomoa karatasi iliyokuwa ndani yake. Akaisoma.
“Unasubiriwa Brussels, hakuna anayejua safari yako zaidi ya mimi na wewe mwenyewe. Fika pale, ndani ya saa ishirini uwe umemaliza kazi na kurudi hapa,” Madam S akatoa amri.
“Maelezo zaidi…”
“Utayakuta huko huko… Hii ni kazi isiyo na jasho Amata, au siyo?” Madam akamuuliza.
“Itategemea, kwangu mimi hii ni kazi ngumu zaidi kwa sababu natakiwa kumuua mtu asiyenipa upinzani. Nitajaribu,” akasema na kuiweka vyema tai yake, “tutaonana kesho kutwa,” akaaga.
“Kazi njema!” Madam S akaitikia na kumpa mkono wa heri. Amata akatoka nje na kutafuta usafiri kuelekea uwanja wa ndege wa Mwalimu Nyerere.

COIMBRA – URENO

ALFAJIRI YA SIKU ILIYOFUATA, Madam S na Kamanda Amata waliwasili katika mji wa
Coimbra, kilomita 210 kwa kupitia mji wa Santarem na Fatima. Moja kwa moja walifika katika uwanja mdogo wa ndege. Dakika sitini na sita ziliwatosha kupata ndege ya kukodi ambayo ingewafikisha katika Jiji la Madrid ncini Hispania.
Muda wote walipokuwa safarini kutoka Lisbon mpaka Coimbra, Madam S hakuzungumzia lolote kuhusu nini Amata alikipata katika tafutishi zake usiku ule. Wakiwa wameketi kwa kutazamana huku pombe kali ikiteketea kati yao, ndipo mazungumzo haya ya wawili yalipoanza.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP16

Muda wote walipokuwa safarini kutoka Lisbon mpaka Coimbra, Madam S hakuzungumzia lolote kuhusu nini Amata alikipata katika tafutishi zake usiku ule. Wakiwa wameketi kwa kutazamana huku pombe kali ikiteketea kati yao, ndipo mazungumzo haya ya wawili yalipoanza.
“Kuna lolote?” akauliza. Mtindo huu wa maswali, ulipendwa sana na mama huyu.
“Kubwa kuliko unavyofikiri. Nimekuta nyumba tupu, maskani ya buibui tu, laptopa mpoja katika chumba cha kulala…” akamjibu huku akijimiminia bilauri nyingine na kuijaza pomoni.
“Umeibeba?”
“Ya nini mimi? Nimeng’oa tu hard disc. Lakini kabla sijatoka, Dana akaja na mtu mwingine, wakaichukua ile laptop,” akamweleza.
“Dana!” Madam S akashangaa.
“Ndiyo, Dana, yaani D-A-N-A,” Amata akajibu na kwa kusisitiza akamtaji herufi moja moja ya jina hilo.
Ukimya ukajidai kati yao, wakati mhudumu wa ndege hiyo ndogo ya kifahari akiwapatia vinywaji vingine. Ilikuwa ndege ya kifahari sana, private jet yenye kasi ya hatari. Alipomaliza, akawaacha na kuondoka zake. Madam S akajikohoza baada ya kumwona Amata akiwa bize kumkodolea macho yule mwaDanada.
“Yeyote amtazamaye mwanamke na kumtamani, amekwishazini naye moyoni…” Madam S akamtania Amata kisha wote wakacheka na kugonganisha viganja vyao.
“Maneno ya kale hayo… ukiyaleta sasa basi wote tutaingia motoni,” akamwambia Madam S.
“Ok, tuyaache hayo. Tutakapokuwa Madrid tutaachana na kila mtu atasafiri kwa ndege yake. Tuonane Dar es salaam, Shamba,” akapiga funda moja na kisha kuiteremsha bilauri yake kwa madaha, “by the way, tuna kazi numu sana ya kuwaangusha hawa wawili waliobaki…”
“Nikukatishe Madam, siyo wawili, kuna wengi katika hili, lazima tuhakikishe tumeng’oa mzizi mkuu,” Amata akasema.
Kamanda Amata aliendelea kugida pombe kwa fujo. Madam S alibaki kumtazama tu pasi na kuuliza neno. Mara mlangowa mudumu ukafunguliwa, yule mwaDanada wa awali akaingia tena.
“Tumekaribia kutua, muwe tayari,” akawaambia. Amata na Madam S wakatazamana, wakashanaa kutangaziwa kienyeji namna ile. Dakika thelathini na tano baadae, walikuwa ndani ya Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Madrid au kama unavyojulikana Adolfo Suarez Madrid-Barajas Airport. Kila mtu alikuwa na hamsini zake kana kwamba hawajuani.
* * *

DAR ES SALAAM SHAMBA

Katika ofisi ya siri kabisa, iliyojengwa ndani ya jumba hilo, Madam S alikuwa mbelea ya meza yenye ukubwa wa wastani. Juu ya meza hiyo kulikuwa na kabrasha lililopambwa na jina ‘ZE SINDIKET’. Taratibu, akalifunua mpaka kurasa ya tatu ambapo palikuwa na majina manne. Akacukua kalamu yake nyekundu na kulikata jina la Vincent Mwanachia. Kisha kwenye kompyuta iliyo mbele yake, akaingiza taarifa za kifo hicho na jinsi kilivyotekelezwa. Alipojiridhishana taarifa yake, akaipakia kwenye seva kubwa inayotumika kutunza siri za serikali za usalama wa taifa kwa ujumla.
Mbele yake, sasa palikuwa na majina mengine mawili; Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya. Hapa akili na mawazo yake viliweka nukta. Aanzie wapi? Ilikuwa ngumu kupata jibu la swali hilo. Kazi ya kujua ni wapi maficho ya Titus Mwakibinga yalipo, ilichukua miaka kama mitatu hivi kwa TSA. Kazi ngumu iliyofamnywa na Gina akisaidiana na Chiba. Alkadhalika kugundua maficho ya Vincent mwanachia, nayo ilikuwa kazi yenye utata kutokana na usaliti uliokuwa ukifanywa na watu wachache waliokuwa katika kitengo cha usalama katika Ubalozi wa Tanzania nchini Ureno.
Madam S, kichwa kikamzunguka, uso ukasawajika. Akalitazama jina la aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, miaka ile, Kibwana Mtokambali. Alivyokuwa mtiifu kwa Rais. Alivyokuwa mchapakazi, mwenye kucheka na kila mtu. Hata Rais mwenyewe alikuwa akimtumia kama mfano kwa wengine kwa jinsi alivyokuwa akiwatendea watu wa jimbo lake. Alijenga shule, hospitali na mambo mengine mengi. Hakuna aliyejua, kumbe nyuma yake kuna mambo mengi ya siri. Kibwana Mtokambali.


* * *

1980

Mara tu baada ya kuingia kwenye duka la Kanjibhai, Waziri Kibwana alipitiliza mpaka katika kaunta ya duka hilo. Mhindi yule wala hakuumiza kichwa, alimjua Kibwana vyema, alifahamu nini anafanya. Kwa namna moja au nyingine, alikuwa msiri wake. Kanjibhai, alimtazama Kibwana jinsi alivyosawajika uso. Hakuwa na maswali, alimfunulia moja ya kabati kubwa na mzee huyo aliingia ndani yake. Mlango ukafungwa. Kabati likabaki kama kabati. Kibwana kapotelea ndani yake.
Mlango wa kabati lile, ulimfikisha Kibwana Mtokambali katika sebule ndogo nadhifu. Hakuwa peke yake, pale alikutana na vijana wawili watanashati. Prakesh na Kumeil.
“Mambo yameharibika,” akawaambia huku akivua koti la suti yake na kulitupia kando.
“Kwa hiyo tufanye mpango uliokusudiwa?” Prakesh akauliza.
“Yes! Ofcourse!” akajibu, “yaani kwa sharia za nchi yetu, natakiwa kuhukumiwa kifo. Sitaki hilo litokee kabla sijauona ukweli wa ndoto zangu…”
“Na kwa nini ufe kabla hujatimiza ndoto zako?” Kumeil akaongeza kusema.
Kumeil na Prakesh wakamchukua Kibwana na kuingia naye katika cumba kingine. Ndani ya kile chumba kulikuwa na mitambo tiba michache.
“Keti hapa!” Kumeil akamwambia Kibwana. Naye akafanya hivyo. Kazi ya kumbadilisha sura na umbo lake vikachukua nafasi ndani ya chumba kile. Kibwana hakuwa na ndevu, zikaoteshwa za bandia ndani ya dakika kumi tu. Macho yake yakafanyiwa maarifa madogo tu, yakawa na utofauti na yale ya kwanza.
“Hawataweza kukugundua,” Prakesh akamwambia.
“Kama ni hivyo si nibaki tu!” Kibwana Mtokambali, akawaambia vijana wale wakati akibadilisha mavazi yake. Muonekano wake ulikuwa tayari na utofauti ambao kwa teknolojia ya wakati ule ingewachukua muda kumundua hhasa kwa nchi zetu za Kiafrika ambazo kila kitu tupo nyuma.
“Miaka haisimami mheshimiwa,” Kumeil akamwambia.
“Kadiri dunia inavyozunguka katika mhimili wake na kubadilisha majira ya mwaka. Basiujue kuwa hata teknolojia inabadilika. Tusipokufanyia surgery ya uhakika labda utajificha kwa miaka miwilia tu. Utagundulika,” Prakesh akamwambia kibwana.
Wakati yote hayo yakiendelea, tayari Waziei Kibwana Mtokambali, alikuwa katika mavazi mengine. Suruari moja ya kijivu iliyomwagika upande wa chini, raba moja matata sana kwa kizazi hicho iliyoshonwa kwa litambaa cha Kodroy. Mara baada ya hapo, wakamchukua mpaka uwani kulikokuwa na gari moja aina ya Peugeot 504, wakaingia na kuondoka zao. Walipita pale pale nje na hakuna ambaye alimtambua. Kibwana akatoroshwa namna hiyo.
* * *

KIKAO CHA SIRI

Ndani ya chumba kidogo katika Ikulu ya Dar es salaam, kikao cha siri kilifanyika baina ya watu watatu tu; Mkuu wa Nchi, Makamu wake, Chameleone kama mwanausalama namba moja wa Rais na Mkuu wa kitengo cha Usalama wa Taifa.
“Tunahitaji kuboresha idara yetu ya Usalama wa Taifa,” Chameleone akaliambia jopo.
“Tunakusikiliza…” Rais akamwambia.
“Mpaka haya yote yanatokea, ina maana idara yetu kuna sehemu tunakosea. Kama unakumbuka katika jaribio lililopita miaka ile ya sabini, mheshimiwa ukafanya mabadiliko na kuunda kikosi maalumu cha usalama wa Rais. Lakini katika chunguzi zangu na watu wangu wa karibu,tumekaa na kuona nini cha kufanya katika kuimarisha usalama wa taifa letu…” Chameleone akazungumzakwa hisia iliyoonekana katika macho yake.
“Endelea…” Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa akadakiza.
“Mheshimiwa Rais, yatupasa kuweka mapandikizi katika idara zote za binafsi na serikali, ili tuweze kukusanya taarifa zozote za uovu dhidi ya serikali na watu wake,” akawaambia. Wote wakatikisa vichwa. Yule mkuu wa idara ya usdalama wa taifa akawa anaandika mambo kadhaa katika kijitabu chake.
“Nina maana kwamba,tupenyeze watu wetu wa UT katika hizi idara, mahospitalini, mashuleni, vyuoni wawe kama wanafunzi na wakufunzi au hata wafanya kazi wa kawaida. Lakini pia tuwawekehata katika sekta za kijamii yaani zile binafsi. Hawa wote kai yao iwe ni kutukusanyia taarifa na kutuletea na sisi tutakuwa tukizichambua na kugawanya zipi ni confidencial, secret na top secret,” akazungumza kwa umakini akiweka na misisitizo kadhaa katika hayo.
Kikao kile kilichukua takribani saa tatu. Mipango ikasukwa, ikawekwa sawa, na utekelezaji ukawa ni jambo linalofuata.
“Sitaki kusikia serikali yetu ikinyanyaswa namna hii,” Mkuu wan chi akasema huku akiiweka vyema fimbo yake juu ya meza.
* * *
Akatutoroka namna hii! Madam S akawaza. Akaachana na jina la huyo Kibwana Mtokambali. Moyoni mwake akajiapiza luwa lazima ampate kwa udi na uvumba. Kama ingekuwa ni muvi basi angeiita, ‘Two Down, Two to Go’. Lakini bahati mbaya haikuwa hivyo, tayari kabrasha lilipewa jina, Ze Sindiket.
Wakati jaribio hili likitukia, Madam S au Selina kwa jina lake, alikuwa akihudumu katika Ikulu ya Dar es salaam, kitengo cha itifaki. Mkuu wake katika kitengo hicho alikuwa James
Msambamagoya. Bonge la mtu, kaenda hewani na kupambwa kwa mwili mkubwa kama Goliath. Hakuwa muongeaji, mambo yake mengi yalikuwa ya kimya kimya tu. Selina alimheshimu kwa kile alichokuwa nacho bwana huyu. Yeye na Chameleone walikuwa nafasi za juu sana katika idara hii ya usalama wa Rais. James, aliitumia nafasi hiyo vyema, akadanganywa na kulaghaiwa na wachache wenye kupenda madaraka. Wakamtumia kama mmoja wa vyanzo vya habari. Pamoja na uintelijensia wake, akajikuta ndani ya Ze Sindiket. Akasaliti ofisi.
“James! Mienendo yako siielewi siku hizi, kuna nini?” Chameleone alimtupia swali hilo siku saba tu kabla ya jaribio lile kufanyika.
“Hapana mkuu!” alimjibu, “hali hii hunitokea tu hasa mambo yangu ya kifamilia yapokuwa yanaenda kombo”.
“Pole sana, jitahidi usiwe katika hali hiyo kwa kuwa kazi yako inakuhitaji daima kuwa makini,” akamuasa. James akajibu kwa kutikisa kichwa.
Ndani ya ofisi ya Chameleone, siku hiyo hiyo, alikutana na Selina. Binti huyu, aliyekuwa na umri sawa na bintiye, alimpenda sana. Akiwa katika kitengo cha usalama ngazi ya wilaya huko Maswa, ndipo Chameleone alipomwona. Umakini na uhodari katika kupanga mipango vilimkosha, akakosheka. Ilikuwa ziara ya kikazi ya Mkuu wa nchi wilayani hapo. Ambapo Selina akiwa katika kamati ya itifaki alionesha umakini sana katika kazi yake, mwepesi wa maamuzi na utendaji. Chameleone akavutiwa. Achana na hilo, alikuwa mrembo, uso wa duara, matiti ya wastani na tumbo lililokuwa ndani kidogo. Hipsi zake zilitengeneza mabisto ya kumvutia rijali yoyote yule.ijapokuwa yalikuwa ndani ya sketi, lakini hayakuficha mnyumbuliko wake. Akitembea, kama nguva ndani ya bahari.
“Huyu ni nani?” Chameleone alimuuliza Simbaulanga. Mkufunzi katika chuo cha mafunzo ya askari kanzu, Mbweni. Ilikuwa ni miezi saba kabla ya jaribio lile la mapinduzi.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP17

Huyu ni nani?” Chameleone alimuuliza Simbaulanga. Mkufunzi katika chuo cha mafunzo ya askari kanzu, Mbweni. Ilikuwa ni miezi saba kabla ya jaribio lile la mapinduzi.
“Mmoja wa wahitimu wangu wenye IQ ya juu sana,” akamjibu. Chameleone akatikisa kichwa juu chini kukubaliana naye.
“Vipi? Unataka awe bi mdogo?” akamuongezea swali.
Chameleone akasikitika, akatikisa kichwa kushoto kulia, “siwezi, huyu ni sawa na binti yangu.”
“Hapa ndiyo kituo chake cha kazi?”
“No! niliagiza aletwe hapa kwa kazi maalumu tu. Ataimaliza leo hii na atarudi chuoni…” Simbaulanga akamjibu Chameleone. Mazungumzo juu ya binti huyo yakapamba moto.
Walipokuwa ofisini siku hiyo, Chameleone alimwambia Selina, “sikiliza binti… nakupa kazi ya siri, na uifanye kwa umakini”. Selina alitulia kimya akisikiliza kwa umakini.
“Nahitaji umfuatilie au umchunguze James… ila uwe makini sana asijue hili. Nataka unambie, akimaliza kazi hupendelea kwenda wapi, na nani ikiwezekana nipe hata orodha ya marafiki zake anaokutana nao mara kwa mara,” akamwambia. Selina hakuwa na hiyana katika hilo. Alilipokea na kuahidi kulifanyia kazi kwa kiwango cha hali ya juu.
Siku ambayo Mkuu wa nchi alimwita nyumbani kwake na kumpa ile taarifa ya watu hatari, jina la James halikuwapo. Lakini katika orodha hiyo alikutana na majina mawili ambayo Selina alimletea majibu kuwa ndiyo washirika wake wakubwa. Na ni mara tatu amemwona nao katika baa ya Banana huko Ukonga. Chameleone akaliweka kumbukumbuni.
Katika mshikemshike wa siku ya tukio, wakati ambapo wengi waliotumbukizwa katika jaribio lile kukamatwa. James hakuonekana. Alikwenda wapi? Hakuna anayejua. James alikuwa mlinzi namba mbili wa Rais, chini ya Chameleone, anayejua nyendo na ratiba za mkuu wake.
“Yupo. Katika mpangilio wa ratiba zake, usiku huo ataupitishia nyumbani kwake. Nafikiri eneo zuri la kutekeleza kazi hii ni nyumbani. Ikulu hakuingiliki,” James alivujisha siri wakati Sindiketi ilipokuwa imekutana kwa siri.
“Tunamuua au tunamteka?” aliuliza Vincent Mwanachia kwenye kikao hicho.
“Hatekwi. Mpango ni kumuua kabisa…” akawaambia. Mipango ikasukwa, akatafutwa mtu maalumu wa kudungua, atakayeweza kutumia risasi moja tu kuusimamisha moyo wa kiongozi huyo. Baada ya mpango ule kugundulika na kila kitu kwenda alijojo, kikao cha siri cha Sindiket kikakaliwa na uamuzi ulikuwa ni kila mmoja atafute njia yake.
James alitoka katika chumba cha mkutano akiwa mwenye mawazo mengi. Hakuwa na muda wa kupoteza. Alipoegesha Landrover lake, ndipo alipoliacha. Hatua mia moja na hamsini zikamfikisha katika nyumba moja anayoijua sana. Ya Husna. Husna, mpenziwe za muda mrefu. Siku hii alikwishamwambia atangulie Zanzibar naye angeunana huko kwa mapumziko. Hesabu zake zilikuwa kwamba siku ya kuungana na mpenziwe huyo Zanzibar, tayari anekuwa Waziri mwenye wizara nyeti katika serikali hiyo mpya. Haikuwa hivyo. Moja jumlisha moja alijikuta anapata kumi na moja.
Akaingia katika chumba cha kulala cha mwaDanada huyo. Ndani ya kabati kubwa la mbao za mninga, alivuta shubaka lililokuwa sehemu ya chini. Akalifungua na kutoa vitu kadhaa ndani yake. Baada ya kuhakikisha kila anachokitaka kipo. Akavua nguo alizovaa na kuvaa zingine. Ndevu za bandia na nywele zikatiwa mvi kiasi. Mbele ya kioo alijiona wazi jinsi alivyobadilika, mtu mzima. Kanzu ilimkaa sawasawa, balaghashia iliyotoboka upande mmoja ilikipamba kichwache.
Bila kuogopa, akatoka nadni ya nyumba hiyo na kupanda UDA, tayari kwa safari. Basi zima mazungumzo yalikuwa hayo hayo. Alisikiliza kwa makini sana ili asikie wananchi wanazungumza nini, jaribio la mapinduzi. Mara kwa mara alijikuta akipata ganzi. Basi lile, likamshusha Stesheni. Pale akatembea mpaka bandarini.kwa kuwa alikuwa akijua mpaka ratiba zote za meli, akaabiri kwenye meli ya MS Mtwara iliyokuwa tayari kuondoka kuelekea Lindi mpaka Mtwara.
Siku moja baadaye, James Msambamagoya, alikuwa katika mji wa Mtwara. Hakuthubutu kabisa kuingia mjini kwa maana alijua anaweza kukamatika. Akapita njia za panya mpaka mpakani. Akavuka na kuingia Msumbiji bila kipingamizi, akapotelea huko.
* * *
Ilikuwa ni siku ya pili tu, baada ya Madam S na Amata kufika Dar es salaam. Kazi ilikuwa bado ya moto, jukumu walilopewa, shuruti walimalize. Akafunga kabrasha lile na kulisukumia kando. Akataka kujaribu kulisahau kidogo, haiwezekani. Mlango ukagongwa, akatazama kwenye luninga yake na kumwona agongaye, akabonyeza kitufe na loki ikajiachia, ukafunguka.
“Karibu!” akamkaribisha. Kamanda Amata akaketi kitini akimtazama Madam S, “Upo sawa?” akamtupia swali.
“Ndiyo.”
“Amata, naomba uendelee kushughulika na hili swala mpaka ulifikishe mwisho. Hata kama ikiwa miaka mitano…” akamwambia na kumsogezeas lile kabrasha.
“Haina shaka, kila kitu kitakamilika, promise!” Amata akamjibu na kusimama.
“Unaenda wapi sasa?” Madam akamuuliza.
“Naelekea idara ya utambuzi, nina kazi hapo,” Amata akajibu na kuondoka zake.


HALI YA HEWA siku hii ilikuwa ya mawingu kiasi, bahari ilitulia na kuruhusu mawimbi ya wastani yajidai. Mc Tee alisimama kwenye ukingo wa baraza ndogo ya nyuma yake. Mkononi alikuwa na kitua mfano wa ubamba wa apple. Alikuwa akibofya hapa na pale huku akiongea maneno machache tu kupitia kifaa mmalumu kilichounganishwa na sikio lake.
 
GENGE
EP18

Mkononi alikuwa na kitua mfano wa ubamba wa apple. Alikuwa akibofya hapa na pale huku akiongea maneno machache tu kupitia kifaa mmalumu kilichounganishwa na sikio lake.
Dakika chache baadae, kutoka majini, karibu kabisa na pale aliposimama, kikaibuka chombo ukubwa kama wa Volkswagen Beetle na kutulia juu yake. Upande wa juu ukafunguka, akateremka mwanaume mmoja mwenye tambo kubwa, ndevu zilizojaa kidevuni mwake zilimfanya aonekane kama gaidi Fulani.
“Karibu sana Comrade!” Mac Tee akamkaribisha mgeni wake na kumwongoza mpaka katika sebule ndogo.
“Bi Jesca vipi?” yule bwana akauliza.
“Tumtarajie dakika chache tu zijazo,” Mc Tee akajibu. Katika sebule hiyo kulikuwa na watu wawili tu yaani Mc Tee na huyo mgeni ambaye aliingia muda huo. Hakukuwa na mtu mwingine yeyote. Punde tu upande wa nje, akaibuka mpiga mbizi, akakwea ngazi mpaka kibarazani. Mc Tee akatoka kibarazani hapo na kumshuhudi mwanamke huyo katika mavazi ya kuogelea na mtungi wake mgongoni.
“Karibu sana Jessy! Big J ameshafika, ulikuwa ukisubiriwa wewe tu,” Mc Tee akamwambia yule mama.
“Asante nimekaribia,” Jesca akajibu na kuvuta hatua mpaka ndani ya sebule ile.
Ukimya ukachukua nafasi yake. Mc Tee akasimama na kuwataka wengine nao kufanya vivyo hivyo. Wakasimama kwa nukta kadhaa. Katika meza iliyo katikati yao wakawasha moto kwenye utambi mdogo uliyoloweshwa mafuta mazito ndani ya kibweta maalumu. Wakafunga mikono na kutulia kimya kwa dakika takribani tano hivi, mpaka ule moto ulipozimika wenyewe. Hii ilikuwa kama ibada kwa kila mmoja wa wanasindiket anapopoteza maisha.
“Ni wapi tunakosea?” Mc Tee akauliza.
“Nimetumia taaluma yangu, lakini nimeshindwa kujua ni wapi tumeacha mwanya,” Big J akajibu.
“Hatutakiwi kushindwa na watu hawa, tumewajaribu mara tatu kwa kutaka kumwaga damu, tumeshindwa. Tumewajaribu mara kadhaa kuwaangusha katika sanduku la kura, tumeshindwa. Sasa wanakuja, wameshaangusha ngome yetu ya Brussels na Lisbon. Tunajipanga vipi kuweka kizingiti wasifike upande huu?” Mc Tee akaeleza na kuuliza. Ukimya ukataradadi kati ya watatu hawa.
“Mi nafikiri twende upande wa pili,” Big J akasema, “tuingize vijana wetu mjini ili wakatafiti kujua wapi tunakosea…”
Mc Tee akatikisa kichwa kukubali. Jesca akabaki kimya kabisa, hakusema lolote.
“Jambo la kufanya, kwanza ni kujua nani kakabidhiwa kabrasha huko TNS?” Mc Tee akasema.
“Tuwe makini sana, tusipoangalia, tutatafuta mtu na kusahau kazi yetu, wafadhili watatushangaa,” Jesca akatamka kwa mara ya kwanza.
“Habari mbaya ambayo hainifurahishi ni kuwa ile laptop haina diski ndani…” “Eeen! Ina maana imeibwa?” Bi J akadakiza swali.
“Ndiyo, yaani kuna mtu aliiwahi laptop akachomoa diski yake, au yeye mwenyewe Mwanachia? Sijui… kitendawili,” Mc Tee akasema.
Ukimya ukajidai kati yao, jambo hili liliwafanya wote wawe kimya. Big J akatahayari. Akapatwa na kigagaziko, mwisho hakuwa na budi kufungua kinywa, “ina maana hata hapa alituwahi?”
“Sijui kama alituwahi au imekuwaje,” Mc Tee akajibu, “cha muhimu hapa ni kufanya utafiti wa kumtambua aliyeshika hiyo laptop baada ya Mwanachia,”akaongeza wazo.
“Wazo zuri na makini, tuwasiliane na Zelda, mstaafu wa MOSSAD anaweza kutusaidia. Yule bwana ameanzisha kitengo chake binafsi cha uchambuzi,” Big J akatoa wazo. Hakuna aliyepingana nalo kwani wote waliujua uwezo wa Big J katika mambo ya Intelijensia. Daima walimtegemea kwa mipango kama au inayofanana na hii.
“Sasa sikia Big J… hapa tunachotaka sisi ni kumtambua huyo mtu. Waelekeze jamaa zako watuletee alama za vidole zote zitakazopatikana,” Jesca akatoa maelekezo.
Kikao hiki cha kwanza kufanyika bila uwepo wa Mwanachia na Mwakibinga kilikuwa kizito sana. Moja ya jambo jingine lililojadiliwa ni kuhusu kuongeza nguvu katia sindiket yao.
“Swala la kuongeza watu kuziba mapengo hayo, soliungi mkono. Kwanza itakuwa ni kama kujitokeza hadharani na kumwanikia kifua adui yako,” Big J aliliambia jopo. “Mi nafikiri tubaki kwa idadi yetu kama tops, halafu kazi yetu itakuwa ni kununua vijana na kuwapa kazi ya kufanya”. W.azo likakubalika na kupitishwa haraka.
“Lazima tutimize azma yetu. Kama ni kupindua serikali basi lazima tufanye hivyo kwa hali yoyote,” Mc Tee akawaambia wenzake, “lakini nafikiri yatupasa kutengeneza mamluki ndani yao ili tupate kujua mipango yote ya ndani dhidi ya tufanyayo,” akamalizia kusema.
“Wakati mwingine, mamluki si watu wa kuamini sana. Sisi twaweza kumpa pesa akawa mamluki, sawa, lakini nyuma yake akawa fukufuku, kwa sababu anaweza kuplay kama D.A… Sote tunajua kilichotupata mwaka 1989 kutoka kwa kijana tuliyemwamini…”
“… Dastan Kihwelo!” Mc Tee akamkata kauli Big J, kisha akamalizi na sonyo kali.
“Dastan, tulimwamini sana, ukizingatia ni kijana ambaye nilimjua ndani nje. Lakini tangu mwaka jana baada ya kifo cha Mwakibinga, naihisi athari ya kazi yake kinyume na sisi.je si mono wake katika kifo cha Mwanachia?” Big J akasema.
“Naunga mkono usemalo, alimuua Bambros. Na Bambros ndiye alikuwa na kabrasha za Mwakibinga na Mwanachia mara baada ya kikao chetu cha Sindiket pale Bagamoyo… shenzi kabisa yule!” Bi Jesca aliongea kwa uchungu.
“Na ataendelea kuhifadhi siri zetu mpaka Yesu arudi, shubamit!” Mc Tee akang’aka.
* * *

Bagamoyo 1989, Julai

Mara baada ya kikao kizito kilichokaa katika Hoteli ya Bagamoyo Sun, Babmbros alitere,mka ngazi haraka haraka kuliekea gari lake alilokuwa ameliegesha chini. Hakutaka kuongea na mtu kwa kuwa alijua wazi kuwa ni nini ambacho amekibeba mikononi mwake. Makabrasha. Makabrasha yaliyohifadhi siri nzito za sindiketi hatari kabisa kwa usalama wa nchi.
Kikao hiki kiliwakutanisha watu sita tu, watano waliokuwa upande wa wasikilizaji na mwingine mmoja aliyekuwa upande wa pili, akiwa anaonekana miguu tu na kusikika sauti. “Mwaka 1990, si mwaka wetu, hivyo tuache kila kitu kitawale kadiri ya ilivyopangwa.
mipango yetu tuendelee kuiweka sawa, na kuanzia mwaka 1995 na kuendelea basi iytakuwa ni utekelezaji tu mpaka tufikie azma yetu. Misaada yote mtapata, nguvu yoyote mnayotaka tutawapatia…”
Hili lilikuwa agizo kuu ambalo mtu huyo asiyeonekana alilitoa wakati akifunga kikao kile. Alirithi ufadhili wa babu kwa baba, akaamini naye akishindwa atamrithisha mwanawe.
Bambros, raia wa Ugiriki aliyechanganya damu na Wahehe wa huko Kidamali Iringa, aliketi katika gari lake tayari kwa safari ya Dar es salaam. Aliaminiwa akaaminika. Alikuwa mtunza siri hodari, hata umng’oe macho, kamwe hasingediriki kukwambia kitu.
“Embassy Hotel, bila kusimama mahali…” akamwambia dereva. Dereva wa gari hilo ambalo siku zote lilimbeba Bambros kwenye harakati zake, akajibu kwa kutikisa kichwa. Akawasha injini, ikaitika. Akatumbukiza gia ya kwanza, ikatii. Lile gari likayaacha maegesho taratibu na kuikamata barabara ya kuelekea Dar es salaam kupitia Bunju mpaka Boko. Saa mbili tu, dereva alizitumia kumfikisha hotelini hapo.
“Utanifuata saa nane usiku, utanikuta hapa hapa!” akamwambia huku akiteremka. Yule dereva akaitika kwa kichwa kama mwanzo. Bambros akatilia mashaka tabia hiyo mpya ya dereva wake, lakini hakuifatilia. Akavuta hatua na mkoba wake mkononi, akamezwa ndani ya hoteli hiyo ya kimataifa. Dereva wa gari lililomleta Bambros alirudiwa na fahamu akiwa ndani ya buti la gari mara baada ya kusimama pale Hoteli ya Embassy. Hata alipojitahidi kugonga hakuna aliyemsikia. Nyuma ya usukani wa gari lile, Dastan aliendelea kumtazama Bambros akipotelea hotelini humo.
“Nitakutembelea baadae!” akajisemea kwa sauti ndogo kisha akaliondoa lile gari mpaka kwenye mzunguko wa saa akaliegesha kandokando ya duka la Magereza. Akateremka mara tu baada ya kufyatua kifungulio cha buti hilo na yeye kutoweka. Hatua kama mia mbili hivi baada ya kuuacha Mtaa wa India, akakunja na kuchukua Barabara ya Morogoro. Mbele kidogo kuliegeshwa gari dogo aina ya Toyota Corona. Akaingia na kuketi kwa utulivu. Dakika kama mbili hivi baadae, kioo cha upande wa pili kikagongwa, akafyatua mlango na kuruhusu mtu wan je aingie ndani.
“Umefanikiwa Dastan?” yule bwana akamuuliza.
“Hatua ya kwanza tayari, kazi iliyobaki ni kwenda kuzibeba tu,” Dastan akajibu kwa utulivu, mkono wake ukavuta droo na kuchukua Big G akaimenya na kuitia kinywani.
“Saa ngapi?” yule bwana akauliza.
“Kama saa sita hivi maana saa nane anatoka,” Dastan akajibu.
“Ok, nafasi nzuri, nafikiri subiri anapotoka ndiyo ukachukue…”
“Hapana! Kama unataka kupata unachotaka, pambania kufa na kupona. Ukisubiri wepesi , utapata usichotaka,” akamgeukia yule jamaa, “Namjua Bambros, anajua kutunza na kuficha siri, nikienda muda huo unaosema, nitakuta magazeti ya Mzalendo na Mfanyakazi tu,” akarudisha macho mbele.
“Ok fanya unaloweza, cha muhimu ni kupata tunachotaka,” yule bwana akamwambia Dastan. Mbele ya gari lile, kulikuwa na mwanamke aliyekuwa akija taratibu kwa mwendo wa kudengua. Mavazi yake yalionesha wazi kuwa ni dada poa. Dastan akapiga honi mara tatu.
“Aaaa Dastan vipi? Unajua mwakaniunaoa wewe, sasa hawa malaya wa nini?”yule jamaa akamlaumu Dastan.
“Tupo kwenye biashara kaka, ye anauza, mi nanunua!” Dastan akajibu wakati yule mwaDanada akifungua mlango na kuingia.
“Karibu Aziza!” Dastan akamkaribisha huku akifungua droo ya kwenye gari. Akatoa kitu kama mkebe na kumpatia, “zawadi yako niliyokuahidi ni hii,” akamkabidhi. Aziza akapokea na kuitia mkobani.
“Leo nataka uniue kitandani kwa mapenzi makali, nimejiweka tayari kwa ajili yako,” Aziza akamwambia Dastan huku akifungua mlango na kushuka.
“Bila shaka, niko ngangari… risasi tatu za kichwa zitakuacha hoi kitandani,”
“Mmmm uwe na shabaha tu katoto…” akaubamiza mlango na kupotelea kwenye mataa ya mjini.
“Vijana mna matatizo sana!” yule bwana akasema, “ina maana mpenzi wako hakutoshi mpaka unakuja kubeba vya barabarani?” akamuuliza.
“Haniridhishi hata kidogo. Ngoja nikamchakaze Aziza!” akamwambia yule jamaa na kuagana naye.
* * *
Aziza aliwasili Hoteli ya Embassy usiku huo. Ujio wake katika hoteli hii ilikuwa ni miadi yake na bwana Bambros au Mtupesa kama alivyopenda kumwita. Alipofika wala hakuuliza, akakwea ngazi taratibu kwenda ghorofani huku akivaa heleni zake alizopewa na Dastan kule garini zikiwa ndani ya mkebe. Dakika chache zilizofuata, alikua ndani ya chumba cha Bambros, akapokelewa na mabusu mazito yasiyo na idadi.
Bambros alipenda sana wanawake, hakujali ni kiasi gani cha pesa angetumia kwa ajili hiyo. Akiwa katika jiji la Dar es salaam, jambo lakwanza alilolifanya ni kutafuta mwanamke wa kumburudisha kila usiku anaokuwa kitandani. Akawapata kadha wa kadha. Dastan alipoujua udhaifu huo akapanga kuutumia vyema katika misheni yake mara baada ya kujiuna na kundi hili hatari. Kundi hili liliamini kuwa Dastan atakuwa mtu safi kwa kuwa atawaletea habari nyingi za siri za serikali juu yao na mpango ya kiutawala kwa kuwa alikuwa ni mwanafamilia wa Usalama wa Taifa. Wakati huo huo, familia ya Usalama wa Taifa ilimuuza kwenye kundi hilo ikitegemea kupata siri za mipango na mikakati yao aghalabu kujua wasakwa wao wako wapi, akina Mtokambali na wengine.
Kifaa cha masikioni alichokivaa Dastan, kilimwezesha kusikia mazungumzo ya Aziza na Bambros. Hata heka heka za kutaka kutupana kitandani alizisikia vyema.
Muda umefika! Akawaza akiwa anavaa gloves mikononi mwake. Akaliacha gari lake mtaa wa nyuma wa hoteli hiyo. Kupitia upande huo huo, akakwea ngazi za dharula mpaka skafu aliyoihitaji. “Nitalalaje na wewe wakati hujanilipa?” Sauti ya Aziza iliyatekenya masikio ya Dastan.
“Oh Sweet heart, kila kitu utapata! Kama shida ni pesa tu jichukulie kwenye briefcase hiyo hapo juu,” sauti ya Bambros ilisikika ikimjibu.
Dastan akafungua mlango na kuingia kwenye korido ndefu ya ghorofa hiyo. Viatu vyake vya mpira havikumfanya asikike. Akatembea tarataibu kukifuata chumba alichokikusudia. Alipoufikia mlango akatulia. Kupitia kile kifaa alianza kusikia miguno ya mahaba ya wawili hao ikishika hatamu.
“Mmmm uwe na shabaha tu katoto…” maneno ya Aziza yalimrudia kichwani, akauma meno.
“Darling, fika haraka, darling jamani… fi-fika!” Aziza aliongea kama mwendawazimu akiwa kitandani na Bambros. Kijana huyo alijua mwanamke aliyenaye usiku huo kanogewa na manjonjo yake. Nje tu ya mlango wa kile chumba, Dastani alikuwa keshaikamata sawia bastola yake. Moyo ulimwenda mbiyo, akapumua kwa nguvu. Aliupata vyema ujumbe wa Aziza kuwa afike wakati huo.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP19

Nje tu ya mlango wa kile chumba, Dastani alikuwa keshaikamata sawia bastola yake. Moyo ulimwenda mbiyo, akapumua kwa nguvu. Aliupata vyema ujumbe wa Aziza kuwa afike wakati huo.
“Nimefika Darling, niko mlangoni…” akajibu kana kwamba Aziza anamsikia kumbe la. Pigo moja la nguvu, lakaufungua mlango. Dastan akaruka sarakasi upande wa pili. Aziza akamkumbatia kwa nguvu Bambros na kujigeuza naye ili amweke sawa upande wa Dastan. Haikuwa rahisi. Bambros aliijua vyema michezo hiyo, alimgeuza Aziza kwa mtindo wa ajabu akidhamiria kama ni risasi basi imuue mwanamke huyo. Wakati huo huo, mkono wake mmoja ulipita kama umeme chini yam to na kuinyakua bastola yake. Alimbwaga Aziza chini, lakini kabla hajaifyatua risasi yake kumwelekea Dastani, akajikuta akipaishwa juu na kubwagwa upande wa pili kama mzigo, macho yamemtoka. Dastan hakua na muda wa kupoteza, akainuka na kuytakua ile briefcase, akatumbukiza kila karatasi lililokuwa juu ya meza ndogo bila kusahau kabatini.
“Vaa nguo Aziza tuondoke chap-chap!” akamhimiza.
Sekunde chache zilizofuata, wakawa tayari ngazini wakiteremka chini. Wakaingia garini na kuondoka kwa kasi.
“Mwanaume una shabaha!” Aziza akamwambia Dastan wakati akifunga vifungo vya blauzi yake.
“Ndiyo kazi yangu,” akamjibu huku akibadili gia na kuweka namba tano.
* * *
“Ndivyo alivyotufanya,” Big J akawaambia wenzake. Ukimya ukajidai kati yao kila mmoja akiwa hana la kusema.
“Msiumize kichwa, nani anatufuatilia,tutamjua tu. Na tukimjua hakuna mswalie Mtume… ni risasi ya kichwa!” Mc Tee akawaambia.
“Sitaki kuamini kuwa wanatuzidi nguvu au maarifa. Big J, we unawajua sana wale, hebu tufanyie utafiti tujue nani anayetutikisa ili tumfanyie kazi. Au la wamekodi mtu,” Bi. Jesca akamwambia Big J.
“Huu si muda wa kujitokeza mama, tumeshabaki wawili, cha kufanya… kama Mc Tee alivyosema, tungoje. Ila azma yetu mwaka unaokuja lazima itimie. Tutaichukua nchi, iwe kwa damu au kwa maji,” Big J akajigamba.
Kikao hakikuwa kirefu lakini kilijawa na maamuzi mazito. Mc Tee, Big J pamoja na Bi. Jesca waliamua kuongeza nguvu, kukodi vijana maridadi watakaoweza kupambana na wana usalama wa serikali pindi tu wakiamua kuwafuatilia.
* * *

Dar es salaam – Shamba

Kamanda Amata na Chiba walikuwa ndani ya chumba maalumu cha utambuzi. Karatasi kadhaa zilizoandikwa mambo mengi kwa kalamu nyeusi zilitapakaa mezani. Wakati Chiba akiwa ametingwa, macho kodo kwenye kioo cha kompyuta; Amata alikuwa akipekuwa karatasi hii na ile, akiandika hapa na pale.
“Vipi umegundua kitu?” Amata akamuuliza Chiba bila kumtazama.
“Mambo mengi mazuri. Hawa jamaa wana mpango mbaya sana kwa nchi hii. Na mpango huu kaka, umesukwa kitaalam kweli kweli. Mpaka sasa tumewaangushan Mwakibinga na Mwanachia lakini kuna gepu kubwa kati yao na Mtokambali na Msambamagoya,” Chiba akamwambia Amata.
“Kivipi?” Amata akamuuliza Chiba huku akiacha kile alichokuwa akifanya.
“Maelezo na vielelezo vyote kutoka kwenye hii hard disc uliyopileta vinaishia kwa hao wawili tu. Hakuna kinachomgusa Mtokambali wala Msambamagoya. Zaidi kuna mambo mengi ambayo nashindwa kuyaelewa yanataka kunieleza nini. Inaonekana ndani ya taarifa hizi kuna taarifa za siri ndani yake…”
“Unataka kunambia kuna kitu kimefichwa?” Amata akamkatisha maelezo kwa kumchapa swali.
“Ndiyo!” akamjibu.
Amata akainuka kutoka pale alipoketi, akachukua kiti kingine pamoja na kitabu chake cha kuandikia kumbukumbu, “Enhe!” Akamtaka kuendelea. Wakati Chiba anaendelea kuelezea kile anachokiona kwenye kompyuta yake, Amata alikuwa bize kunakili hiki na kile.
“Sikia Chiba, hawa jamaa wanauelezea mpango wao kwa mafumbo sana. Inabidi tutulie kujua nini kimefichwa,” akamwambia na Chiba akatikisa kichwa kuafiki.
“Kwa haraka haraka, hii taarifa ipo nusu, inabidi tuipate nusu nyingine ili tuikamilisha,” Amata akamwambia Chiba na kutua kalamu yake mezani.
“Kibarua asee, yanarudi yaleeee ya Dassen Keputo,” Chiba akasema na wote wakacheka.
“Taarifa ya mwisho ambayo alikuwa akiiandika Bwana Vincent Mwanachia, inahusu mapokezi ya mzigo…” Chiba akaeleza.
“Mzigo gani?”
“Haijaelezwa ni mzigo gani ila tu imesema ‘mzigo utapokelewa palepale tulipokubaliana muda wa shetani’ basi,” akaeleza.
“Na ukirudi nyuma kuna taarifa gani zaidi?” Amata akataka kujua.
“Hukutakiwa kumwacha Dana aisee, inaonekanaana mengi anayoyajua kwani hapa naona picha ya pamoja,” Chiba akamwambia Amata. Akainakili ile picha, akaiingiza kwenye softiwea yake ya utambuzi na kuanza kufanya kile ambacho kitaalamu kinaitwa foresinc investigation.
Katika picha ile, kulikuwa na watu watano. Ile softiwea ikamtambua haraka Dana, kisha
Mwanachia. Haikuweza kuwatambua watatu waliobakia, ambao kati yao kulikuwa na mzee wa Kizungu aliyevalia suti ya gharama sana na vijana wawili pia Wazungu. Upigwaji wa picha ile ulionesha wazi kuwa ilipigwa baada ya kikao fulani.
“Fanya uwezalo tupate jina la huyo mzungu na mahali walipopiga hiyo picha,” Amata akasema wakatia akiichukua nakala ile kwenye mashine ya kuprinti.
“Nipe dakika kumi tu,”
“Ok!”
Chiba, TSA 2, mshititi katika kile kinachoitwa Cyber intelligence na Foresinc Investiation, aliijua vyema kazi yake. Alikuwa na kila zana ambayo ingemrahisishia uchunuzi wake, iwe kwa kompyuta au kifa kingine chochote kile. Akaiweka kwenye kioo kikubwa picha ile. Kwa kutumia kipanya cha kompyuta hiyo kubwa. Akakata sura ya huyo aliyemtaka kisha akaihamishia katika kiboksi kingine na kukiamuru kifanye kazi yake. Upande wa kushoto wa kidirisha hicho kukatokea majina yanayopita kwa kasi sana. Upande wa kulia, kulionekana usanisishaji wa viungo vya kichwani kama pua, masikio, midomo, macho ili kuona ni kipi kitaweza kuoana na picha ile. Dakika mbili zilipaita na baadaye kila kitu kikasimama lakini bado upande wa kulia haukuleta majibu sawasawa, mambo hayakuwa mukashara.
Macho hayakuoana, lakini kope zake zilienda sawa kabisa na picha hiyo. Masikio hayakuoana sawasawa hasa la upande wa kushoto. Jina lililosimama upande wa kushoto, lililomeka Mr. Sebastiano Moznich, raia wa Italia, Jiji la Toscana. Maelezo yalienda mbali zaidi, ni mfanyabiashara wa magari ya Ferrari.mwenye makazi yake katika jiji hilo hilo.
Kamanda Amata aliitzama ile picha kwa makini sana, wakati huo Chiba alikuwa ametingwa kwenye kompyuta yake.
“Sebastiano Moznich! Ni nani katika mchezo huu?” Amata akauliza.
“Huyu ndiye key point kwa sasa, lazima aje shamba,” Chiba akasema.
“Sawa, kingine…”
“Siri ya wapi Msambamagoya na Mtokambali wamejificha,” Chiba akamjibu. Kamanda Amata akachomoa bahasha moja ndogo na mara baada ya kuifungua ndani yake, akatoa nakala mbili za picha za black and white. Moja ilimwonesha Msambamagoya James na nyingine Mtokambali Kibwana. Picha hizi zote ziliandikwa kwa nyuma; moja 1980 na nyingine 1979.
“Mpaka sasa watakuwa wameshabadilika sana,” Chiba akamwambia Amata wakati akizitazama zile picha.
“Ndiyo, kwa sasa inabidi tuzitengenezee uzee ili tupate taswira ya mwonekano wao kwa sasa,” Amata akasema.
“Nimekupata,” akajibiwa. Muda huo huo Madam S akaingia ndani ya chumba hicho maalum. Akawakuta vijana wake wakiendelea na kazi.
“Huyo ni nani?” akauliza akiwa anaitazama ile picha pale kwenye liuninga.
“Sebastiano Moznich!” Amata akajibu. Madam S akasogelea zaidi kile kioo, akaitazama ile picha, kisha akamgeukia Amata, “Anahusika?”
“Hatuna uhakika ila turufu yetu imeangukia kwake… hatumhukumu ila tunamtuhumu. Uchunguzi unaendelea,” akaeleza, “Ila Dana anahitajika hapa kwa mahojiano”.
“Haina shida, nitawasiliana na bosi wake, atapatikana tu,” Madam akajibu. Alipomaliza kauli yake, akaangalia na zile nyingine kisha akasoma na maelezo kadhaa yaliyo ndani ya luninga ile.
“Naona mmekwama vijana… ushauri wangu ni mmoja tu na ni ambao nimeufikiria sasa hivi…”
“Enhe…” Amata akamkatiza kwa kushadadia.
“Tusiumize kichwa na hawa watu wawili wakati familia zao zipo hapa mjini. Upelelezi wetu uanzie hapo na baadaye tutapata fununu za kujua ni wapi wamejificha,” akawaambia.
Chiba na Amata wakaafiki na kubaki wakitazana. Hawakuwaza!
Yaani tunawaza vitu vikubwa wakati vidogo tunavisahau! Amata akawaza.
“So?” akamuuliza Chiba.
“Bado nahitaji kumchunguza zaidi huyu jamaa…”
“…nani?”
“Sebastiano. Lakini kama tulivyokubaliana, inabidi tuzigeuze hizi picha kuwa za wakati huu,” Chiba akakumbusha.
* * *
Siku hiyo hiyo, wakati TSA wanaendelea na uchunguzi wao huko Shamba, Mc Tee, Big J na Bi Jesca walikuwa wakihitimisha zoezi lao la utambuzi.
“Vipi?” Bi Jesca aliuliza alipowaona wanaume hao wakirejea vitini. Giza lilikwishaanza kuimeza nchi na muda wa kikao chao ulipitiliza kiasi kwamba kila mmoja wao akawa na wasiwasi na usalama wake.
Mc Tee akaiweka kompyuta yake ndogo mezani, “tumepata jibu” akasema.
“Enhe!” Jesca akadakiza kutaka kujua.
“Hizi alama za vidole katika hii kompyuta ni za mtu hatari sana. Serikali ya Tanzani imeanza kukodi wapelelezi hatari dhidi yetu,” Mc Tee akawaambia wenzi wake.
“Inawezekana. Maana kama angekuwa mwanausalama wa kawaida ningemjua tu, au watu wangu wangemjua lakini wamekiri kuwa TNS hawana code 005” Big J akaeleza.
“Code 005! Inamaanisha nini?” Jesca akauliza.
“Katika utambulisho wa namba za kiusalama kwenye mashirika ya kijasusi, hii code humaanisha mtu hatari kuliko hatari yenyewe. Mwenye uwezo mkubwa wa kufikiri na Sanaa ya mapigano ya kiwango cha juu,” Big J akaeleza.
“Mh!” Jesca akaguna, “Nitakwenda Dar es salaam kwa siri nitawapa jibu kuwa ni nani…” akasema.
“Hilo si wazo jema hata kidogo, kumbuka wewe umeshatikisa nchi kwa maneno yako makali.
Wanakufahamu kwa matusi yako, maandamano uliyoyaitisha yakaitikisa serikali hayajasahaulika.
Wanakusaka, usalama wako tuni kwamba serikali ya Marekani inakulinda kwa namna fulani. Usijaribu kuikanyaga ardhi ya Dar es salaam, wakikugundua hawatakuacha na pumzi yako… be carefull mammy,” Big J akamweleza Jesca. Mwanamke, mwanaharakati aliyeweza kuitikisa serikalikwa maneno yake. Mwenye siri nzito nzito za vigogo, kuanzia za chumbani, sebuleni mpaka ofisini. Alitisha.
“Najua nitakachofanya, mimi ni mwanamke, siogopi kitu…” akawaambia akijipigapiga kifua.
“Angalia sana! Serikali ya Tanzaniainakusubiri kwa hamu sana utie mguu wako wakunyakue. Naogopa na usifanye hivyo. Tunaandaa kikao maalumu, safari hii ni kuwaalika viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa ili tuwasikilize mikakati yao kisha tutumie mwanya huo kupenyeza ajenda zetu…” Mc Tee akawaambia Big J na Jesca.
“Lakini, pamoja na hilo, tunafisha juhudi zetu…?” Big J akauliza huku akijikuna kichwa chake.
“No! Hatufishi. Katika mazungumzo na God Father, amahakikisha kutusaidia kila kitu ilimradi tutimize lengo letu. Ndipo nikakaja na wazo jipya ambalo tungeweza kuliunganisha na lile la msingi. Halafu kwa yote pamoja tutapata matokeo mazuri sana, mtafurahi,” akawaeleza.
“Sawa , tutaweka mipango vizuri ili kila kitu kiwe sawa. By the way, taarifa zaidi za huyu bwana 005 tutazijua tu muda si mrefu. Nimeshazituma kwa mtu wetu,” Mc Tee akaeleza.
“Hatuna shaka na hilo, tukishamjua tu, kazi imeisha. Tutamuua kimya kimya na kuuyeyusha mwili wake kwenye tindikali,” Big J akaongeza kusema.
Kikao cha watu hawa watatu kilihitimishwa. Jambo moja tu lililokuwa likisubiriwa ni ufafanuzi zaidi wa code iliyojitokeza, ambayo wao walikosa kuielewa kwa undani kuwa ni nani inamwakilisha kwa jina, cheo na wajihi wake.

KICHWA CHA MADAM S hakikupata wasaa wa kutulia. Jambo gumu na kubwa liliendelea kumsumbua kichwani.
Tunakwama wapi? Akajiuliza. Usiku huo alilala chali kitandani, akiwa na vazi la kulalia tu. Taa yenye mwanga wa rangi ya orange iliyowekwa kwenye meza ndogo ilikijaza chumba hicho kwa uhafifu wake. Ungeweza kumletea usingizi, lakini kwake haikuwa hivyo, tuli, alitulia. Alihakikisha ananyamazisha kelele zote ubongoni mwake ili achambue kimoja baada ya kingine.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom