Riwaya fupi zilizokuwa zinatoka katika Gazeti la Heko

nameless girl

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
4,195
2,655
Vipi ndugu zangu? Kumepoa heeee? Kwa kipindi hiki cha hili gonjwa linalotunyima uhuru basi hakuna namna. Inabidi tufanye simulizi fupifupi zailizokuwa zinafanywa kwenye gazeti la Heko.

Nitacopy na kupaste ili tufurahi wote. Lakini kwa wale wanaopenda kununua vitabu vya marehemu Mtobwa, bado unaweza kujipatia kwa kuletewa au kwenda dukani Posta au nipigie kwa namba 0712504985.

Leo tuanze na hiii.

SALMA MTOTO WA WATU….
Ndio kwanza nililkuwa nina miezi mitatu katika mtaa huu wa Vuka ulioko Kirumba mjini, lakini msichana huyu amekuwa akinitesa"kiroho mbaya.” Kusema kwel i, mimi nikuwa mmoja Wa vijana wachache sana hapa Vuka niliyekuwa sihusudu ‘vidosho’ Lakin kutokana na tabia yangu ya upole na utanashati iliwavutia sana wasichana wengi wa hapa Vuka.

Wengi walljigonga kwangu kwa kujipitishapitisha, huku wakitoa salamu ‘lukuki’ na vimaswali vya uongo na kweli lakini mimi sikuwajall ndio Kwanza niliwachunia na kuwapa heshima kama dada zangu. lla kulikuwa na msichana mmoja ambaye macho yangu yanapomuona tu huvutwa sana.

Roho yangu hulipuka paa! Mapigo ya moyo hubadilika na zaidi ya hayo huwa najisikia raha isiyo Kifani. Uso wangu hutanda furaha na kujisikia kama kiumbe kilichopata uhai mpya.

Msichana huyo alikuwa si mwingine zaidi ya Salma. Msichana ambaye ameumbwa akaumbika, ana maumbile yasiyo ya kawaida kwa kiumbe yeyote. Nadhani alipewa upendeleo fulani na Muumba, alipokuwa anamwandaa kumshusha katika anga hili lililojaa kila aina ya raha na karaha.

Kuanzia juu mpaka chini Salma amekamilika vyema. Umbo lake la wastani yaani si mnene wala mwembamba, na pia si rahisi kumwita mrefu au mfupi. Rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde zilizochemshwa. Kichwa chake ni cha wastani kilichobeba nywele lainí mithili ya toto la "uhabesh."

Uso wa kimwana Salma ni wa duara na wa kupendeza wenye macho yaliyojaa huba. Ana midomo ya kumwemwesa na iliyojaa ashki . Pua yake ni ya wastani ambayo imechongoka kiasi cha kutosha.

Salma alijaaliwana manani kwa kupewa mashavu ya "nipe busu". Mashavu hayo yana vijishimo vinavyojitokeza pindi atoapo tabasamu lake laini na maridhawa. Tabasamu ambalo lingemfanya muungwana yeyote achanganyikiwe.

Masikio ya kimwana Salma kiasi yalikuwa makubwa yaliyopendeza kuvikwa hereni za aina yoyote ile. Shingo yake ni laini na iliyojaa kwa jisimu la kike. Kifua chake ni cha upana wa kati kilichobeba taswira ya kupendeza.

Kiuno chake msichana huyu ni chembamba na kilichofanya umbo lake kuwa la namba nane. Tumbo lake ni dogo kiasi kwamba litamchukua muda mrefu mtu kugundua kama mrembo huyo ameshapata "msosi” au bado.

Salma alijaaliwa miguu yenye supu na iliyoumbwa kike. Mwendo wake wa hatua za mahesabu uliojaa maringo na ulimbwende wa kike ulikuwa ni moja ya vitu vyake vinavyotosha kumwacha hoi mwanamume yeyote aliyekamilika kiume.

Nilitamani sana kumueleza Salma kuwa nampenda lakini nilishindwa kumwambia kwa hofu ya kukataliwa, kwani nilijiuliza kama atanitolea nje sijui sura yangu nitaiweka wapi.

Sifa ya msichana huyu niliambiwa ameshawatolea nje wavulana karibu wote wa hapa Vuka na ndio ilikuwa sababu kubwa ya kuogopa "kubonga” naye.

Kama vile alijua nampenda kwani kila alipopita karibu yangu mwili wake aliulegeza na kujitupa huku na kule. Hali hiyo ilininyima raha kabisa.

Jamani ni mengi tu yanayofanya niteseke juu yake kumpenda mtu asiyejua kuwa unampenda ni mateso bila ya chuki.
Juu ya mimi kutokuwa na pesa nyingi hilo nalo lilikuwa tatizo lingine linaloufanya moyo wangu kuwa mzíto kwa msichana huyu.

Niliendelea kumuwaza msichana huyu kwa kipindi kirefu lakini bila ya mafanikio yoyote niliyoyapata zaidi ya kuteseka moyo wangu. Baada ya kumuwaza msichana huyu kwa kipindi kirefu lakini bila ya mafanikio yoyote niliyoyapata zaidi ya kuteseka moyo wangu. Baada ya kuona mambo yanazidi kuniwia magumu niliamua kwenda kwa rafiki yangu Akley ili kupata ushauri utakaonisaidia jinsi ya kumpata msichana huyu nimpendaye.

Kwanza rafiki yangu alinitahadharisha kuwa msichana huyo haingiliki lakini hata hivyo ushaurI alionipa ni kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuonana nae (Salma) ana kwa ana na kumweleza yanayonisibu.

Ushauri huu kusema kweli kwa upande wangu ulikuwa mgumu sana hasa kwa kuzingatia mimi sijawahi hata siku moja kusimama na msichana na kumweleza eti nampenda sababu ni kwamba nilikuwa sijui nashindwa nianzie wapi na nishie wapi.

Baada ya kumweleza rafiki yangu Akley kwamba sitaweza kuutekeleza ushauri wake kwa ugumu uliopo, alijitahidi sana kunitoa wasiwasi na woga niliokuwa nao. Akanitia kila aina ya matumaini mpaka nikakubaliana naye kwamba nitajaribu.
Niliondoka kwa rafiki yangu huyo muda wa saa tatu za usiku na kurudi nyumbani kujipumzisha.

Kutokana na uchovu niliokuwa nao haukupita muda mrefu nikapitiwa na usingizi mzito. Mara nilisikia mlango ukigongwa taratibu. Nikavaa taulo na kutoka kwenda kuufungua. Sikutegemea kumuona kiumbe aliyesimama hapo akinichekea. Salma! Alikuwa akiwaka kama malaika.

"Nimekuja mpenzi” alisema mara aliponiona nikimtazama kwa mshangao "Najua umekuwa ukihangaisha roho yako kwa ajili yangu usiku na mchana. Usiwe na shaka, mie ni wako tangu leo na daima," aliongeza akinisogelea huku akiipanua mikono yake kunikumbatia. Kama mtoto mchanga, nilijikuta nikiingia mikononi mwake na kujilaza juu ya kifua chake laini chenye joto.

Rohoni nilijihisi furaha isiyob kifani. Nilijiona kama maji kwa siku kadhaa. Nilijisikia kama mfalme Wa dunia nzima.
Nikamnong'oneza hivyo Salma na kumsikia akicheka. Lakini kicheko chake kilinitisha. Kilikuwa kama kikohozi cha kiume. Nikafumbua macho ili nimtazame vizuri.

Heko Newspaper

January 26, 1995.
 
Nikafumbua macho ili nimtazame vizuri…

Ndio kwanza nikagunduaa kuwa nilikuwa kitandani peke yangu, nikiwa nimekumbatia mto ambao ulilowa kwa machozi. Nilikuwa nikiota, ndoto za alinacha. Hali ya huzuni ilijirudia tena baada ya kugundua kuwa ilikuwa ndoto tu. Nilijiuliza mimi "Kitoli" ni nini hasa kinachonifanya niogope kumweleza Salma.

Nilijadiliana na nafsi yangu kwa kipindi kirefu na niliamua lolote litokee lakini lazima nimweleze ukweli wangu kuliko kuteseka.

Jumatatu moja muda wa jioni ilinikuta kibarazani nikiwa tayari kabisa kukabiliana naye popote pale atokeapo.

Mara nilimwona Salma kwa mbali akielekea huku nilipo.

Hapo woga ukaanza kuniingia lakini hata hivyo, nilipiga moyo konde kwa sababu roho yangu ilikuwa inawaka juu ya msichana nimpendaye.

Aliponikaribia nikataka kumsalimia lakini nilishindwa kwani midomo yangu ilikuwa mizito ajabu. Basi nilipokuwa nazidi "kuwayawaya" Salma akawa ameshapita, kusema kweli nilijilaumu sana kwa kushindwa hata kumsalimia. Hapo nikajiona mtu nisiyekuwa na moyo wa ujasiri.

Siku zilizidi kupita na Salma kuzidi kupendeza, vijana wa hapa wakaanza tena "kumsalandia" Salma. Hali hiyo ilizidi kunifanya niwe sina raha kabisa kwa kuhofia huenda "wakamwopoa.”

Uchungu ulizidi na hasira kuchukua nafasi ya kuilaumu nafsi yangu kuwa na uoga kupita kiasi akili zangu sasa zikadumaa kwa kulifikiria jambo moja tu. Nikaamua kutolifuatilia kwa kuhofia rmakubwa yatakayonipata, nikajitahidi kusahau lakini wapi uwezo wa kumsahau Salma nikawa sina. kila nilipomuona ukurasa mpya wa mateso ulianza.

Jioni moja nikiwa nimekaa tena kibarazani nikiwa napunga upepo nakutazama wapita njia, nikiwa sina hili wala lile ghafla nikamuona Salma akija huku nilipo. Hapo sasa nikaona ni muda mzuri wa kuondoa "dukuduku” langu. Baada ya kuliingiza wazo la kubonga naye wasiwasi ulianza kuniingia moyoni.

Nikaamua kuutenga moyo wa uoga na kuukaribisha moyo wa ujasiri. Aliponifikia tu nikamsalimia.

“Salma hujambo.” Hatimaye nikafaulu kuushinda movo wangu. Nikamudu kuutungua mdomo wangu na kumsabahi kwa sauti ambayo sikuamini kama ni yangu. Ilikuwa ni sauti iliyojaa kila aina ya dalili za uoga. Sauti ambayo hata Salma alibaini kuwa si ya kawaida.

“Mimi sijambo, sijui wewe.” Aliitikia kwa sauti ya maringo.

“Mimi vile vile sijambo," nilimjibu.

Baada ya kusalimiana kulipita muda kukiwa kimya bila ya mmoja kumsemesha mwenziwe. Jamani nisikuficheni hali yangu ilizidi kuwa mbaya kwa upande wangu kwani sasa nilihema kwa tabu, midomo ilianza Kucheza, uso ukaingiwa na dalili zote za uoga.

Nilitamani nikimbie lakini miguu ilikuwa mizito mno. Nikataka nimweleze aondoke lakini kwa upande mwingine nafsi ilikuwa nzito mno.

Niliwaza kwa sekunde chache nikaona heri nikate "mzizi wa kiherehere kwa kumueleza

ukweli wangu kuliko kuitesa nafsi yangu.

"Unajua Salma leo nimeamua kukupasulla ukweli wangu, Kwa kipindi kirefu nilikuwa nasita kukueleza hasa baada ya kuona nafsi yangu inazidi kuteketea.

Kusema kweli Salma mimi nimetokea kukupenda sana kiasi kwamba sijui nijieleze vipi upate kunielewa, lakini kwa ufupi ni kwamba nakupenda.”

Baada ya kumueleza hayo Salma alinitazama kama vile mtu anayesoma mawazo yangu.

“Nashukuru sana Kitoli kwa kunipenda alisema kwa sauti nyororo huku atiachia tabasamu lake laini. Kusema kweli usemi huo wa Salma Sikuuelewa kabisa. Ilibidi nimuulize.

“Sasa Salma una msimamo gani juu yangu?”

“Sina msimamo wowote juu yako yako.”

"Ndio kusema hunipendi?”

“Ndio.”

Duh! Kijasho sasa kilianza kunitoka. Salma akaanza kunitazama kuanzia juu hadi chini,

kwa jinsi alivyokuwa ananitazama mapigo ya moyo wangu yalizidi, nafsi nikailaumu nikajiona

nimekosea, Nikatamani ardhi ipasuke niingie kwa kuepuka mitazamo iliyojaa kiburi na dharau

ya hali ya juu.

“Hivi kwa nini unanitesa namna hi?” nilimhoji kwa sauti iliyojaa huzuni na masikitiko ya kila aina.

“Kwa vipi nakutesa?” aliuliza.

“Kwa majibu yako ambayo siyaelewi.”

Baada ya hapo alitabasamu kisha akanieleza

“Sikiliza Kitoli, ili usiendelee kuteseka juu yangu ni kwamba, mimi sina muda wa kupendana na wewe na wala sitakujibu lolote unalolitaka, kwani mimi nina mpenzi wangu ambaye tumependana kwa moyo wote na tunatarajia kuoana miezi mitatu ijayo. Kwa hiyo sitapenda unitilie kitumbua changu mchanga na wala kunizungumzia jambo lolote linalohusu mapenzi. Nadhani mpaka hapo umenielewa.”

Nilibaki nikiwa nimeinamisha kichwa chini kwa aibu niliyoiona. Salma akarudia mtazamo wake ule ule. Jicho lake sasa lilikuwa limebeba ujumbe fulani toka leo usinifuatefuate.

Baada ya kuridhika kwa mitazamo yake wa dharau aliondoka kwa mwendo wa pozi na maringo ya aina yake.

"Salma! Salma! Salma! Unanitesa mwenzio.” Nilijitahidi kumweleza kwa sauti ya kilio, lakini wapi, hakunisikiliza wala kugeuka. Ndio kwanza aliongeza mwendo.

Nikawa nimeduwaa nisijue la kufanya. Nikarudi nyumbani nikiwa na uchungu, majonzi na hasira tele moyoni. Nilikwenda moja kwa moja mpaka kitandani.Niligalagalaga kwa yaliyonitokea. Nilingiwa na uchungu kama jeraha lililotiwa chumvi
 
Vipi ndugu zangu? Kumepoa heeee? Kwa kipindi hiki cha hili gonjwa linalotunyima uhuru basi hakuna namna. Inabidi tufanye simulizi fupifupi zailizokuwa zinafanywa kwenye gazeti la Heko.

Nitacopy na kupaste ili tufurahi wote. Lakini kwa wale wanaopenda kununua vitabu vya marehemu Mtobwa, bado unaweza kujipatia kwa kuletewa au kwenda dukani Posta au nipigie kwa namba 0712504985.

Leo tuanze na hiii.

SALMA MTOTO WA WATU….
Ndio kwanza nililkuwa nina miezi mitatu katika mtaa huu wa Vuka ulioko Kirumba mjini, lakini msichana huyu amekuwa akinitesa"kiroho mbaya.” Kusema kwel i, mimi nikuwa mmoja Wa vijana wachache sana hapa Vuka niliyekuwa sihusudu ‘vidosho’ Lakin kutokana na tabia yangu ya upole na utanashati iliwavutia sana wasichana wengi wa hapa Vuka.

Wengi walljigonga kwangu kwa kujipitishapitisha, huku wakitoa salamu ‘lukuki’ na vimaswali vya uongo na kweli lakini mimi sikuwajall ndio Kwanza niliwachunia na kuwapa heshima kama dada zangu. lla kulikuwa na msichana mmoja ambaye macho yangu yanapomuona tu huvutwa sana.

Roho yangu hulipuka paa! Mapigo ya moyo hubadilika na zaidi ya hayo huwa najisikia raha isiyo Kifani. Uso wangu hutanda furaha na kujisikia kama kiumbe kilichopata uhai mpya.

Msichana huyo alikuwa si mwingine zaidi ya Salma. Msichana ambaye ameumbwa akaumbika, ana maumbile yasiyo ya kawaida kwa kiumbe yeyote. Nadhani alipewa upendeleo fulani na Muumba, alipokuwa anamwandaa kumshusha katika anga hili lililojaa kila aina ya raha na karaha.

Kuanzia juu mpaka chini Salma amekamilika vyema. Umbo lake la wastani yaani si mnene wala mwembamba, na pia si rahisi kumwita mrefu au mfupi. Rangi ya ngozi yake ni maji ya kunde zilizochemshwa. Kichwa chake ni cha wastani kilichobeba nywele lainí mithili ya toto la "uhabesh."

Uso wa kimwana Salma ni wa duara na wa kupendeza wenye macho yaliyojaa huba. Ana midomo ya kumwemwesa na iliyojaa ashki . Pua yake ni ya wastani ambayo imechongoka kiasi cha kutosha.

Salma alijaaliwana manani kwa kupewa mashavu ya "nipe busu". Mashavu hayo yana vijishimo vinavyojitokeza pindi atoapo tabasamu lake laini na maridhawa. Tabasamu ambalo lingemfanya muungwana yeyote achanganyikiwe.

Masikio ya kimwana Salma kiasi yalikuwa makubwa yaliyopendeza kuvikwa hereni za aina yoyote ile. Shingo yake ni laini na iliyojaa kwa jisimu la kike. Kifua chake ni cha upana wa kati kilichobeba taswira ya kupendeza.

Kiuno chake msichana huyu ni chembamba na kilichofanya umbo lake kuwa la namba nane. Tumbo lake ni dogo kiasi kwamba litamchukua muda mrefu mtu kugundua kama mrembo huyo ameshapata "msosi” au bado.

Salma alijaaliwa miguu yenye supu na iliyoumbwa kike. Mwendo wake wa hatua za mahesabu uliojaa maringo na ulimbwende wa kike ulikuwa ni moja ya vitu vyake vinavyotosha kumwacha hoi mwanamume yeyote aliyekamilika kiume.

Nilitamani sana kumueleza Salma kuwa nampenda lakini nilishindwa kumwambia kwa hofu ya kukataliwa, kwani nilijiuliza kama atanitolea nje sijui sura yangu nitaiweka wapi.

Sifa ya msichana huyu niliambiwa ameshawatolea nje wavulana karibu wote wa hapa Vuka na ndio ilikuwa sababu kubwa ya kuogopa "kubonga” naye.

Kama vile alijua nampenda kwani kila alipopita karibu yangu mwili wake aliulegeza na kujitupa huku na kule. Hali hiyo ilininyima raha kabisa.

Jamani ni mengi tu yanayofanya niteseke juu yake kumpenda mtu asiyejua kuwa unampenda ni mateso bila ya chuki.
Juu ya mimi kutokuwa na pesa nyingi hilo nalo lilikuwa tatizo lingine linaloufanya moyo wangu kuwa mzíto kwa msichana huyu.

Niliendelea kumuwaza msichana huyu kwa kipindi kirefu lakini bila ya mafanikio yoyote niliyoyapata zaidi ya kuteseka moyo wangu. Baada ya kumuwaza msichana huyu kwa kipindi kirefu lakini bila ya mafanikio yoyote niliyoyapata zaidi ya kuteseka moyo wangu. Baada ya kuona mambo yanazidi kuniwia magumu niliamua kwenda kwa rafiki yangu Akley ili kupata ushauri utakaonisaidia jinsi ya kumpata msichana huyu nimpendaye.

Kwanza rafiki yangu alinitahadharisha kuwa msichana huyo haingiliki lakini hata hivyo ushaurI alionipa ni kwamba hakuna njia nyingine zaidi ya kuonana nae (Salma) ana kwa ana na kumweleza yanayonisibu.

Ushauri huu kusema kweli kwa upande wangu ulikuwa mgumu sana hasa kwa kuzingatia mimi sijawahi hata siku moja kusimama na msichana na kumweleza eti nampenda sababu ni kwamba nilikuwa sijui nashindwa nianzie wapi na nishie wapi.

Baada ya kumweleza rafiki yangu Akley kwamba sitaweza kuutekeleza ushauri wake kwa ugumu uliopo, alijitahidi sana kunitoa wasiwasi na woga niliokuwa nao. Akanitia kila aina ya matumaini mpaka nikakubaliana naye kwamba nitajaribu.
Niliondoka kwa rafiki yangu huyo muda wa saa tatu za usiku na kurudi nyumbani kujipumzisha.

Kutokana na uchovu niliokuwa nao haukupita muda mrefu nikapitiwa na usingizi mzito. Mara nilisikia mlango ukigongwa taratibu. Nikavaa taulo na kutoka kwenda kuufungua. Sikutegemea kumuona kiumbe aliyesimama hapo akinichekea. Salma! Alikuwa akiwaka kama malaika.

"Nimekuja mpenzi” alisema mara aliponiona nikimtazama kwa mshangao "Najua umekuwa ukihangaisha roho yako kwa ajili yangu usiku na mchana. Usiwe na shaka, mie ni wako tangu leo na daima," aliongeza akinisogelea huku akiipanua mikono yake kunikumbatia. Kama mtoto mchanga, nilijikuta nikiingia mikononi mwake na kujilaza juu ya kifua chake laini chenye joto.

Rohoni nilijihisi furaha isiyob kifani. Nilijiona kama maji kwa siku kadhaa. Nilijisikia kama mfalme Wa dunia nzima.
Nikamnong'oneza hivyo Salma na kumsikia akicheka. Lakini kicheko chake kilinitisha. Kilikuwa kama kikohozi cha kiume. Nikafumbua macho ili nimtazame vizuri.

Heko Newspaper

January 26, 1995.
Dah!
nameless girl
Darasa la Mapenzi
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom