Riwaya: Dhahama

Hassan Mambosasa

JF-Expert Member
Aug 2, 2014
3,350
4,485
RIWAYA: DHAHAMA

SURA YA KWANZA

Hali ya simanzi ilikuwa imetawala katika eneo zima la kasri la kupendeza la kifalme katika himaya ya Majichungu inayopatikana katika bahari ya hindi, himaya hii ya kijini iliingia katika huzuni baada ya mfalme wao kuwa katika harakati za mwisho za maisha yake. Mfalm huyu aitwaye Zulain mwenye miaka yapata elfu tatu alikuwa katika ugonjwa kwa muda wa miaka kumi sasa leo ndiyo dalili za kufikia mwisho wa uhai wake zilionekana dhahiri kwa majini wote wa hapo kwenye kasri hilo. Akiwa kalala kwenye kitanda chake cha thamani kwa muda wa miaka kumi kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua ambao haujulikani, kwa mara ya kwanza aliinuka kitandani ghafla akakaa kitako kisha akasimama akaelekea kwenye kiti chake cha enzi akiwaacha watumishi wake wakiwa na simanzi sana. Kuugua mfalme kwa muda mrefu kisha kuinuka ghafla ni dalili tosha ya kuwa siku za mwisho za miaka yake zimekaribia, hivyo hata watumishi wa ndani ya kasri hili walitambua kuwa siku za mwisho za uhai wa mfalme wao zimekaribia.

Hata mfalme mwenyewe alitambua kuwa ana masaa ya kuishi duniani au siku ya kuishi duniani hivyo alitaka kuongea maneno ya mwisho kabla roho yake haijaachana na mwili wake, alipokaa kwenye kiti chake jambo la kwanza kulitamka ilikuwa ni kuitiwa mawaziri wake wote pamoja na viongozi wengine waliopo chini ya utawala wake ili awaambie jambo la muhimu pamoja na kuacha kauli ya mwisho katika himaya yake. Amri ya kuitwa mawaziri na viongozi wa juu katika himaya yake ilitekelezwa mara moja na baragumu maalum likapulizwa kwa haraka sana na mpulizaji wake anayetoka katika himaya hiyo, ndani ya sekunde kadhaa chumba cha mkutano kilijaa mawaziri na viongozi wenye nyadhifa kubwa katika himaya hii ya kijini ambao walikuwa ni majini wa aina mbalimbali.

"Himaya ya Majichungu inaelekea kukumbwa na simanzi kubwa kwani kiongozi wake niliyetawala kwa muda wa miaka 2500 nakaribia kufa na dalili kuu ya kufa kwangu nadhani imeonekana kabisa dhahiri kwenu na kwa watumishi wangu, sasa basi suala la kutafutwa mrithi wa taji langu na kiti changu cha enzi nawapa nyinyi. Nahitaji mjukuu wangu Zalabain ambaye ndiye mrithi wa kiti changu cha enzi na taji langu apatikane haraka iwezekanavyo kwa namna yoyote na afutwe popote alipo aletwe huku akabidhiwe jukumu lake la ufalme kwani mwanangu Zaif ambaye ndiye baba mzazi wa Zalabain hatunaye na wote mnatambua ni jinsi alivyougua hadi akata roho katika himaya hii. Sasa basi Zaif kabla hajafa alisema duniani yupo mjukuu wangu aitwae Zalabain, sasa inabidi huyo mjukuu wangu atafutwe.kwa hali yoyote hadi apatikane ili aje kuchukua wadhifa wangu kama mrithi pekee aliyebakia. Pia nahitaji mila na desturi za himaya hii zibaki kama nilivyozikuta na zisibadilishwe kwa namna yoyote na wala asitokee kiumbe akabadilisha au akamshawishi kiumbe yoyote abadilishe.

Mwisho kabisa nahitaji Sadik bin Zultash baba wa mapacha Saliim na Salmin aachiwe huru kuanzia sasa kwani uzao wake kwa faida moja umetusaidia kwa kutuletea jini mwenye nguvu kuliko wote na anayeifanya himaya yetu isidhuriwe na kiumbe wa aina yoyote, sina la ziada ni hayo tu" Mfalme Zulain alihitimisha na kikao kikamalizika mara moja karibia viongozi wote wakatawanyika wakiwa na simanzi juu ya mfalme wao. Siku iliyofuata ilikuwa ya simanzi zaidi kwa himaya nzima ya Majichungu kutokana na kifo kilichomkumba mfalme wao, himaya nzima iliomboleza kifo hicho kwa muda wa wiki saba na baada ya hapo jeshi la majini watatu ambao ni makomandoo likaundwa kwenda kumtafuta Zalabain popote alipo ili aje kurithishwa ufalme wa babu yake.

****

WIKI MOJA BAADAYE
USIKU WA MANANE
AMBONI
TANGA
Eneo la miamba yenye mapango ya kihistoria jijini Tanga jirani kabisa na mto mkubwa Tanga nzima uitwao mto Sigi kulikuwa kuna kundi la vijana kumi waliokuwa wameuzunguka mti mmoja wa mkoko ambao unasadikika kuwa mti wa ajabu kutokana na kuota eneo ambalo lipo mbali na ufukwe wa bahari. Vijana hao walikuwa wameuzunguka mkoko huo ambao ulikuwa umening'inizwa chupa ya ukubwa wa lita moja ambayo ilikuwa ikijibadili rangi kila kukicha, walikuwa wamejifunga kaniki nyeusi kiunoni na vitambaa vyekundu kichwani na kwenye mikono yao. Muda wote walikuwa wapo makini kuitazama chupa hiyo pamoja na mazingira ysnayozunguka mto Sigi pamoja na upande wa mapango ya Amboni, walikuwa wapo kimya sana na umakini wao katika kuangalia mazingira ya hapo ndiyo ulizidi kwani walikuwa wanapambana na wachawi wa kila namna ili kuilinda chupa iliyopo hapo mtini ambayo huonekana usiku kwa wenye uwezo kuiona na mchana haikuonekana kabisa.

Siku hiyo majira ya saa nane usiku vijana hao walimshuhudia Mamba mmoja mkubwa akitoka ndani ya mto Sigi na akakaka pembezoni mwa mto huo mita chache kutoka pale walipo, wote walimpuuzia mamba huyo kutokana na dawa zao wanazotumia hawezi kuwaona. Walibaki wakimtazama yule Mamba kwa jinsi alivyo mkubwa huku kuliko hata Mamba wote waliowahi kuwashudia katika mto Sigi tangu wakiwa watoto, mmoja kati ya wale vijana alishikwa na shauku ya kwenda kumtazama yule Mamba na akasogea karibu zaidi kwani dawa zao zilikuwa zinawazuia wasionwe na wanyama wakali. Alisogea akamtazama zaidi na akabaini ni mamba wa ajabu mwenye rangi tofauti na Mamba wa pale mtoni, akiwa anashangaa uajabu wa yule mamba ghafla alijikuta akipigwa mkia akatumbukia mtoni na mamba huyo naye akazama mtoni akiwaacha wale vijana waliobakia wakikimbia hadi pembezoni mwa mto wakiacha kuilinda ile chupa. Hilo lilikuwa kosa jingine kwao na hawakupata hata nafasi ya kulirekebisha kwa balaa lililotokea, kimbunga kikali kilivuma kuuzunguka ule kwa muda wa dakika kadhaa na kilipoacha ile chupa wanayoilinda ilikuwa imepasuliwa tayari.

Kabla hata hawajatafakari kitu cha kufanya maji ya mto Sigi nayo yalianza kuzunguka kisha yakanyanyuka juu urefu wa mlima huku yakizunguka na yakatengeneza umbo la jitu kubwa ambalo mkono mmoja lilikuwa limemshikilia kijana yule aliyepigwa mkia na Mamba akaingia mtoni. Vijana walipoona hivyo wakajua wameingiliwa na kazi yao imeshaharibika hivyo walitaka kukimbia ili kujiepusha na hatari kwani viumbe waliowavamia sio wa kawaida, walikimbilia upande lilipo pango wakijua ni salama kwao ili wapate sehemu ya kutorokea. Walipokaribia kuingia pangoni walikutana uso kwa uso na nyoka mwenye vichwa kumi na ikawabidi wakimbilie mtoni kwa upande mwingine bila ya kutambua wanajipeleka kwenye eneo la kifo, vijana hao walijitupa mtoni kwenye maji wakiwa wanataka kuokoa maisha yao tu na wala hakukumbuka kuwa dawa waliyojipaka ya kuzuia wasidhuriwe na wanyama wakali inatoka mwilini ikiwa utaingia kwenye maji. Walipokuja kukumbuka tayari walikuwa wamezungukwa na mamba zaidi ya kumi wa mto huo, walikuwa wamejirusha sehemu yenye maskani ya Mamba bila ya kujijua na wakawa kitoweo cha Mamba.

****

Sherehe kubwa ilifanyika katika kasri la kifalme la Majichungu katika kusherekea kupatikana kwa mjukuu anayepaswa kurithi kiti na taji la ufalme wa babu yake, ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mjukuu huyo mwenye mchanganyiko wa binadamu na jini kufika katika himaya tangu azaliwe. Sherehe ilipoisha ndipo taratibu zote za kimila na desturi za kumpatia ufalme Zalabain zikaandaliwa kama ilivyofanyika kwa wafalme waliopita.

Siku iliyofuata sherehe nyingine ya kuvikwa taji la ufalme ilifanyika katika uwanja mkubwa uliopo nje ya kasri la kifalme ambayo ilihudhuriwa na wanahimaya hiyo karibia wote, kiti cha kifalme kilitolewa kikawekwa sehemu yenye jukwaa lililopambwa kwa busati lenye rangi nyeupe. Muda wa kuvikwa taji Zalabain ulipowadia Mkuu wa baraza la sheria la himaya hiyo aliingia akiwa amebeba taji la kifalme liliwekwa kwenye kasha lililopambwa na fito zenye rangi nyekundu, Zalabain akiwa nyuma ya Mkuu huyo wa baraza la sheria pembeni yake akiwa na walinzi wenye miili mikubwa pamoja na sura za ajabu. Zalabain na mkuu huyo walipanda katika jukwaa lenye kiti cha kifalme huku mamia ya wanahimaya ya Majichungu wakishangilia kwa nguvu, aliamriwa aketi kwenye kiti cha ufalme naye akatii akaketi na Mkuu wa baraza la sheria akashika kasha lenye taji la kifalme akasogea kisha akawageukia Wanahimaya ambao wapo hapo kushuhudia tukio hilo.

"Leo ni siku maalum na ya kihistoria ya kumpata kiongozi wetu aitwae Zalabain bin Zaif atakayeiongoza himaya yetu akirithi utawala wa Babu yake Zulaif, akiwa na miaka 26 tu atakuwa kiongozi mdogo kuwahi kutokea katika Himaya yetu hii hivyo naomba mumpokee" Mkuu wa baraza la sheria aliongea kisha akamgeukia Zalabain ambaye tayari ameshavaa mavazi ya kifalme akawa anatazama nae.

"Kwa mamlaka niliyokabidhiwa ninakukabidhi na kukuvisha taji hili la Kifalme litakalokufanya uwe mfalme, miongoni mwa wafalme, wa ukoo wa kifalme, waliowahi kuwa wafalme, uwe kiongozi wa kasri la kifalme. Zalabain sasa wewe ni mfalme wa himaya ya Majichungu" Mkuu wa baraza la sheria alipomaliza kusema maneno hayo aliliweka taji kichwani mwa Zalabain huku halaiki ya wanahimaya wakishangilia, kushangalia huko kulizimika ghafla mithili ya umeme unavyozimika eneo lenye giza. Wote walibaki wameduwaa baada ya taji la kifalme lililowekwa kichwani mwa Zalabain kuruka kando likaanguka kwenye busati lililotandazwa hapo jukwaani. Mkuu wa baraza la sheria aliona ni jambo la kawaida sana na aliinama akalishika ili alinyanyue lakini taji halikuinuka na lilikuwa zito sana na ikambidi alishike kwa mikono miwili na akashindwa kuliinua vilevile. Aliamua awaite wale walinzi walioingia na Zalabain walinyanyue nao wakashindwa pia kulinyanyua eneo hilo. Wanajeshi wanaoaminika wana nguvu sana nao walishindwa kulinyanyua taji hilo, Zalabain mwenyewe alibaki akiwa anashangaa kwa tukio hilo ambalo hakulielewa limetokana na nini.

Mnajimu mkuu wa Himaya hiyo aliitwa mara moja na akapewa kazi ya kulitatua tatizo hilo kwani yeye ndiye anayeaminika katika himaya hiyo, mnajimu huyo wa kijini alianza kulizunguka taji hilo la kifalme kisha akajaribu kuliinua lakini alishindwa kabisa na akaanza kubadilisha macho yake yakawa kama ya paka akamtazama Zalabain.

"Siyo uzawa wa ukoo wa mfalme huyu ndiyo maana taji limemkataa na wala siye mtoto halisi wa Zaif, taji hili linahitaji abadilishwe kiongozi kwani kizazi cha ukoo wa mfalme alibaki Mfalme Zulain tu ambaye amefariki tayari. Ufalme unatakiwa uhamishwe katika koo nyingi.." Mnajimu alishindwa kumalizia kauli yake na akajikuta amepigwa kofi zito hadi akaanguka chini, akiwa hajajua nani aliyempiga akahisi anakabwa shingoni huku akinyanyuliwa juu. Walinzi walipoona hali hiyo walitaka kusogea ili wamdhibiti kiumbe anayemkaba Mnajimu mkuu lakini walisita baadaya kiumbe mwenyewe kujitokeza hadharini, Salmin ambaye anajulikana na wanajamii hiyo kama jini mwenye nguvu kuliko wote ndiye aliyeonekana akimkaba Mnajimu huyo shingo.
"Kwanini unasema uongo ilihali wewe ni Mnajimu unayeheshimiwa na kuaminiwa katika himaya hii" Salmin alimuuliza Mnajimu huku akizidi kumkaba, Mnajimu aliomba aachiwe ili aongee na alipoachiwa ndipo akamwaga uhalisia wa jambo lenyewe.

"Wanahimaya na wakuu wote naomba mnisamehe sana kwa kusema uongo juu ya mjukuu wa mfalme, tamaa ya madaraka ndiyo imesababisha niseme uongo. Niliahidiwa kupewa nafasi ya mkuu wa baraza la sheria ikiwa tu nitafanya hila ufalme uhamishiwe katika ukoo wa waziri mkuu ili waziri mkuu awe mfalme wa Himaya hii, narudia tena viongozi wangu na wanahimaya wenzangu naomba mnisamehe kwani mimi nina nafsi na tamaa ni kitu cha kawaida kwa mwenye nafsi" Mnajimu alitoa maelezo hayo akiwa na aibu usoni kutokana na jambo alilolifanya, kuomba kwake msamaha hakukusaidia kitu kwani alikamatwa yeye na Waziri mkuu baada ya mkuu wa baraza la sheria kutoa amri hiyo. Baada ya kukamatwa kwa Waziri mkuu na Mnajimu mkuu Salmin alilitazama taji la kifalme kisha akamtazama Zalabain kwa umakini, macho yake yalianza kutoa nuru mithili ya almasi iliyomulikwa na mwanga mkali.

"Zalabain.......Zalabain mrithi wa kiti cha mfalme aliyestahiki kuvishwa taji la ufalme wa himaya hii lakini taji limemkataa kutokana na jambo moja tu ambalo mrithi wa kiti hiki hatakiwi kuwa nalo kabisa ambalo wewe unalo, udhaifu.....udhaifu wako ndiyo chanzo cha taji hili kukukataa. Ikiwa unatakiwa kuwa mrithi wa taji hil na kuna ubaya ambao umetendewa unatakiwa ulipe kisasi kwanza na si kusamehe ili upate taji hili, baba yako Zaif ameangamizwa na wanadamu akiwa na miaka 1500 na wanadamu hao ndiyo chanzo cha taji hili kukukataa na pia kuwa zito kuinuka kwa yoyote mwenye wazo la kuliweka kichwani mwako. Kisasi cha ubaya uliofanyiwa ndiyo kinahitajika ili hili taji likae kichwani mwako na hakuna mwingine atakayelivaa isipokuwa wewe, unapaswa utambue kwamba himaya hii yote inahitaji kiongozi na haiwezi kuendelea bila kiongozi na pia kiongozi ni wewe unatakiwa ulipe kisasi ili watu wako uwaongoze na si usamehe wapotee. Je upo tayari kuongoza himaya hii?" Salmin alifafanua chanzo cha kutokea jambo lililotokea kisha akamuuliza Zalabain.

"Nipo tayari kuongoza, nipo tayari kisasi cha kuuawa kwa baba yangu na nipo tayari kulipa kisasi cha ubaya uliotendwa kwangu" Zalabain aliongea huku macho yakibadilika na kuwa mekundu kabisa na yenye kung'aa, Salmin alimsogelea akamshika mkono kwa sekunde kadhaa kisha akamuachia halafu akamuambua "kazi njema". Salmin aliliokota taji la kifalme akamkabidhi Mkuu wa baraza la sheria kisha akaondoka, sherehe hizo ilivunjwa hapohapo na Zalabain akahitajika atimize kile alichoahidi mbele ya majini wote wa himaya hiyo.

****
Asubuhi ya siku iliyofuata tangu litokee tukio la kutoveshwa Zalabain taji, wafanyakazi wa kampuni ya upangishaji nyumba iitwayo Extoplus walikuwa wanasafiri kuelekea katika kijiji cha Duga Maforoni kwenda kuhudhuria sherehe ya uzinduzi wa nyumba mpya za kupangishwa za ksmpuni hiyo. Siku hiyo wafanyakazi wote waliotakiwa kwenda kwenye sherehe hiyo walijawa na hofu, karibu kila mfanyakazi alikuwa anasita kwenda anasita kwenda kwenye sherehe lakini hawakuwa na uwezo wa kukataa kwani ni idara nzima imeteuliwa kuhudhuria sherehe hiyo. Saa mbili kamili wote walikuwa kwenye basi wakielekea Duga kuhudhuria sherehe hizo, ndani ya basi kimya kilitawala kuanzia mwanzo wa safari na kilikuja kuvunjwa baada ya gari aina ya toyota coaster waliyokuwa wanaitumua kuvuka daraja la Utomfu. Mwanamke mmoja wa makamo alivunja ukimya uliopo ndani ya gari kwa kusema, " jamani mimi jana usiku nimeota ndoto ya ajabu sana".

"mmh! Hebu tueleze ni ndoto gani hiyo" Mwenzake aliyekuwa pembeni naye alidakia.
"nimeota nashuka kwenye gari natoka kazini nikakutana na mtoto wa miaka sita hizi akaniamkia kwa uchangamfu na mimi nikaitikia, yule mtoto kaniuliza unaujua mtego wa panya mimi nikamjibu ndiyo. Akaniuliza je kiumbe chochote kikiugusa unamnasa au unanasa panya tu, nikamjibu yoyote akiugusa ananaswa haijalishi kama Panya au siyo panya. Nilipomjibu akatabasamu nikamuuliza mbona umeniambia hivyo, akanijibu safari yako ya kesho Duga ni mtego wa panya ukienda utanasa ingawa wewe sio panya. Nimeshtuka usingizini hapohapo nikawa najiuliza kuhusu ndoto hiyo jamani ina maana gani" Yule mwanamke alieleza ndoto yake na alipomaliza wafanyakazi wote walikuwa wameingiwa na woga hapohapo.

"jamani hata mimi hii ndoto nimeiota" Mwanamke mwingine akadakia huku akionesha kuogopa.
"hata mimi" Mwanaume wa makamo ambaye ni mmoja wa wafanyakazi hao naye akadakia na mwishowe wote kwa pamoja wakatamka kwamba wameiota ndoto hiyo na hofu ikawa imetawala nafasi zao huku wengine wakimsihi dereva ageuze gari wasiende. Walikuwa wameshafika Amboni na sasa wapo kwenye daraja la kulia la mto Sigi hivyo dereva alikuwa yupo makini kulimaliza daraja hilo na hakuwasikiliza kabisa, baada ya kulipita daraja ndipo dereva akasema "jamani hata mimi nimeota ndoto ya namna hiyo lakini nimeipuuzia kwani si kila ndoto ni ya kweli".

"unasemaje wewe hebu simamisha nishuke nipande mabasi yanayotoka Horohoro nirudi mjini" Mwanamke yule aliyeeleza kuhusu ndoto alikuja juu.
"sawa ngoja tufike Mpirani kwenye kituo ili upate hilo gari" Dereva akimwambia yule mwanamke lakini hakutaka kumuelewa.

"simamishe gari nakuambia!" Yule mwanamke alizidi kufoka, dereva hakuwa na jinsi ilimbidi akanyage breki lakini gari ilikataa na ndiyo mwendo ulikuwa unazidi na usukani ikawa unajiongoza wenyewe.

"we mwanaharamu wewe simamisha gari nishuke sio kuongeza mwendo" Yule mwanamke alizidi kufoka baada ya kuona mwendo wa gari unazidi kuwa mkali, dereva hakumjibu yule yeye alitoka kwenye usukani akasimama kisha akawaangalia wafanyakazi wa idara nzima akiwa na hofu.

"si mimi ninayeendesha jamani gari linaenda lenyewe hili hebu oneni" Dereva aliongea huku akiwaonesha wafanyakazi wote jinsi usukani ulivyokuwa unajiongoza wenyewe, wafanyakazi wote walipoona hicho kioja walijikuta wakijaribu kutoka nje lakini walishindwa kwani milango haikufunguka na vioo vyote vilijifunga ghafla hata vile vilivyokuwa wazi vyote vilijifunga. Wafanyakazi wote walijaribu kupiga vioo ili wavunje lakini walishindwa kwani vioo vilikuwa vigumu sana, gari nayo ilizidi kuongezeka mwendo hadi ikawa kama ipo kwenye mashindano.

Makelele ya woga ndiyo yalitawala kwa watu wote kasoro kijana mmoja ambaye ni mmoja kati ya wafanyakazi wa idara hiyo ya kampuni ya Extoplus, yeye alikuwa kauchapa usingizi na wala hakunekana kama anatambua kuna tatizo, mwendo wa gari ulivyozidi kuwa mkali ilibidi wamuamshe huku wakimpigia kelele hadi akaamka. Kijana huyo alipoamka alionekana kukerwa na sauti za watu waliokuwa wanampigia kelele, kisha akalala tena akionekana kazidiwa na usingizi.

"We Saleh hebu amka si tupo kwenye hatari we unalala,.amka tusaidiane kutoka ndani ya gari hili tutakufa wote" Yule mwanamke aliyekuwa aking'ang'ania kushushwa alipaza sauti kumuambia yule kijana aamke aache kulala wapo hatarini, yule kijana aliinua kichwa mara ya pili akiwa anaonekana kama mtu ambaye alikuwa hajalala na hana dalili ya kusinzia. Saleh alikuwa amejawa na tabasamu alipoinua uso wake hadi wenzake wote wakawa wanamshangaa sana, wenzake walipozidi kumtazama kwa hofu yeye aliangua kicheko kabisa akionekana kufurahishwa na hofu ambayo imevamia nyuso za wenzake. Alipoona wamezidi kumshangaa aliamua kuwaambia, "mtakufa nyinyi ila sio nitakufa mimi". Kauli hiyo ilizidi kuwashangaza sana wenzake waliokuwa wana hofu na kifo, wote walimuona kama mtu aliyechanganyikiwa kwani si jambo la kawaida kwa mtu mwenye akili timamu kutamka maneno hayo katika eneo la kuelekea kwenye mlango wa kifo.

"We Saleh ni wewe kweli tunaokujua ni muoga au umechanganyikiwa tayari?" Mwanamke mwingine aliyekaa pembeni yake alimuuliza akionekana kuchanganywa na kauli ya Saleh.

"ushasema Saleh ni muoga sasa, utaulizaje ni Saleh au siyo wakati unaona kabisa mimi siyo muoga, labda jibu la kukusaidia ni kwamba Saleh yupo nyumbani kwake Mikanjuni amepumzika baada ya kuota ndoto iliyokuwa na onyo juu ya safari hii aliyoizingatia lakini nyinyi mnaojifsnya wapuuzaji wa mambo kisa elimu zenu leo utakuwa mwisho wenu" Yule kijana aliyesadikika kuwa ni Saleh alianza maneno yaliyozidi kuwashangaza wafanyakazi wote pamoja na dereva wa gari. Mwanamke mmoja aliyekaa pembeni yake yule kijana akiwa upande wa dirishani aliamua kumtandika makofi mawili mazito ya mashavu huku akisema, " hebu amke Saleh nahisi umelala bado".

"Nishaamka tayari ngoja nikulaze wewe sasa ulale milele" Yule kijana aliongea kisha akampiga yule mwanamke ngumi moja ya kichwani juu kidogo ya sikio, ngumi hiyo ilitoboa kichwa cha huyo Mwanamke na ubongo wake uliochanganyika na damu ukaruka hadi kioo cha dirishani na kuibadilisha taswira ya eneo la karibu na hapo kuwa damu na madonge ya ubongo yakiwa yameruka hadi kwa wengine waliopo jirani na endo hilo. Mayowe ya uoga yalizidi ndani ya gari hilo huku watu karibia wote wakitamka majina ya mama zao kutokana na tukio waliloliona, Yule kijana alipoona makelele yamezidi aliamua kunyanyuka akawatazama wafanyakazi huku macho yake yaking'aa kama macho ya paka. Mikono yake ilianza kutoa kucha ndefu kama za Simba na sura yake ikabadilika ikawa ya kutisha, mabegsni alitoa mabawa kama ya popo na kinywaji akawa anatoa cheche za moti pamoja na mngurumo unaoashirua hasira.

"Kwa jina la yesu pepo mchafu usiyehitajika tokaaaaa!" Mwanaume mmoja ambaye alikaa kiti cha nyuma kabisa alipaza sauti huku akimnyooshea mkono yule kijana ambaye muda huo alikuwa amegeuka kiumbe wa ajabu, Yule kiumbe aliangua kicheko huku akimtazama yule Mwanaume kwa jinsi anavyobabaika kukemea kama Mlokole.

"Ha! Ha! Ha! Ha! Yaani kila siku unashinda bar ukinywa pombe na unamuasi Mungu kwa kila unachokifanya na Kanisani kwako ni kama kituo cha polisi kwa teja ndiyo utegemee ukikemea nitaondoka. Mungu hasaidii watu kama nyinyi ambao mmeshindwa hata kumtaja mkiwa na tatizo . Mnashuhudia huyu mwenzenu nikimuua na mmekimbilia kuwataja mama zenu kama ndiyo mnaowaabudu. Sasa naanza na wewe unaejifanya kimbelembele sana" Yule kiumbe aliongea kisha akamnyooshea mkono yule Mwanaume aliyekuwa anakemea, yule mwanaume alijikuta akivutwa kuufuata ule mkono kwa kasi ya ajabu na alipoukaribia mkono wa yule kiumbe aliachiwa pigo moja takatifu lililomgawanya vipande viwili mithili ya papai linalotayarishwa kwa ajili ya kutolewa mbegu ili liliwe.

Tukio hilo lilishuhudiwa na kila mmoja humo ndani na hadi wanashuhudia vipande vya mwili vya yule mwanaume vikianguka chini tayari mwanamke aliyekaa kitu kilicho jirani na yule kiumbe alikuwa ameshapoteza fahamu papo hapo kutokana na mshtuko wa moyo na akaanguka jirani na miguu ya yule kiumbe akiwa hajitambui, yule kiumbe alimtazama yule mwanamke kisha akaachia pigo la kutumia mguu wake lililoshuka kwemye shingo ya yule mwanamke hadi kichwa kikaruka na damu zikaanza kusambaa ndani ya gari ikiweka taswira isiyopendeza.

"huyu peke yake ndiyo kafa kifo cha kistarabu akiwa hana fahamu ila nyinyi mtakiona cha mtema kuni" Yule kiumbe aliongea kisha akanyanyua mikono yake juu, watu wote nao walienda juu wakajipigiza kwenye paa la gari hiyo. Yule kiumbe alipoirudisha mikono yake chini watu nao walirudi chini wakijipigiza kwenye sehemu za juu viti ambazo hutengenezwa kwa chuma kilichovikwa godoro gumu. Sauti za kuvunjika kwa viungo vya ilisikika walipojipigiza kwenye viti huku mayowe ya maumivu yskitawala ndani ya gari ambayo yalimfanya yule kiumbe apeleke mikono yake juu na chini kwa haraka na watu walizidi kujibamiza kwenye paa na kwenye viti.

Waliendelea kubamizwa hivyo kwa mara nyingi hadi wakawa wamevunjika kila viungo vya miili yao na wakawa hawawezi hata kunyanyuka, baadhi ya wafanyakazi walikuwa kwenye hali mbaya kwani mifupa yao mingine iliyovunjika ilikuwa imetoka nje ya miili iliyowaletea maumivu makali yaliyowafanya walie kama watoto wadogo.

"Sasa nyinyi wa kupuuzia mambo nataka mfe huku mjiona kwa kuungua moto" Yule Kiumbe alisema huku akiwasha moto kwenye kiti cha mbele pembeni ya dereva halafu akatoweka huku gari likizidi mwendo kuliko uwezo wa mwendo wake.

Gari hiyo aina ya toyota coastar ilikuwa imeshafika maeneo ya Bwaga Macho ambapo mbele kulikuwa na gari kubwa la mafuta likitembea kwa mwendo wa tararibu sana kutokana na uzito uliolielemea, gari iliyobeba wafanyakazi ilienda kugonga gari la mafuta kwa nyuma na kupelekea gari tanki la mafuta litoboke na mafuta yavujie ndani ya gari lililobeba wafanyakazi ambalo tayari moto ulikuwa unaunguza kiti cha mbele.

Kilichofuata hapo ulikuwa ni mlipuko mkubwa hadi gari zote mbili zikarushwa juu huku zikiteketea, zilipotua chini ziliteketea zote hadi zikabaki mabati tu kutokana na kikosi cha zima moto kuchelewa kufika eneo hilo vikitokea Chumbageni wilaya ya Tanga.

Ilikuwa kizaazaa kilichozaa vizaazaa vingine kwani wakati tukio hilo linatokea hilo linakaribia kutokea tayari waganga wa jadi wa eneo lote la Bwaga Macho walishaona kwamba kuna kiumbe wa ajabu aliyekuwa anawatesa wanadamu ndani ya gari, walihitaji kuwakomboa wanadamu waliopo ndani ya gari hiyo kwa kupambana na kiumbe hicho. Wakati yule kiumbe anaweka moto kwenye kiti cha ndani ya basi la wafanyakazi halafu anapotea ndani ya gari lile ili aondoke, alikutana na makombora kumi ya kwa pamoja kutoka kwa waganga kumi tofauti ambayo yalimrudisha nyuma hatua kadhaa lakini hayakumdhuru.

Alipoangaza vizuri aliona kundi la waganga wapatao kumi wakiwa wanaelea hewani wakiwa waejifunga kaniki nyekundu viunoni na vilembe vyeusi, waganga hao tayari walikuwa wamemzunguka tayari wakitaka kummaliza kwa pamoja. Waganga hawa hawakutambua kuja kwao hapo ni kujiingiza katika vita isiyowahusu, wao walichojali ni kupambana na kiumbe aliyesababisha kuteseka kwa wanadamu wasiowajua. Wakiwa wanapanga kuachia makombora mengine yule kiumbe alijizungusha kama pia na kikatokea kimbunga kikali kilichowazoa wote kwa pamoja, uzito wa kimbuka hicho ukisababisha hata viti vilivyokuwa jirani na hapo kupeperushwa huku waganga wakitoa mayowe ya maumivu wakiwa wapo ndani ya kimbunga hicho. Hadi magari yanalipuka kimbunga hicho bado kilikuwa kipo angani na hadi yanateketea yanaisha bado kilikuwa angani kikizunguka huku sauti za watu wakilia kwa maumivu zikisikika, tukio hilo lilishuhudiwa na kila mtu aliyekuwa eneo hilo ingawa hawakujua hizo kelele ni za kina nani.

Kimbunga hicho kilipoanza kupungua ndiyo wakashuhudia lita nyingi za damu iliyokuwa ina vipande vya nyama pamoja na mifupa ya binadamu ikidondoka barabarani na kulifanya eneo zima liwe kama machinjioni na kupelekea baadhi ya watu wasio na uatahimilivu wa kushuhudia vitu kama hivyo kukimbia huku wengine wakuzirai hapohapo baada ya kuona mafuvu ya binadamu yakiwa yametapakaa damu katika hali ambayo si rahisi kutazamika.

****
Jirani na uwanja wa mpira wa miguu uliopo jirani na njia ziendazo katika bwawa maarufu la Duga maforoni linalotumiwa na wananchi wa eneo lote la Maforoni kulikuwa na nyumba za kisasa kama ishirini zilizojengwa na kampuni ya Extoplus ambazo zilikuwa zinazinduliwa katika siku hiyo ambapo sherehe ya uzinduzi ilikuwa inasubiri wafanyakazi kutoka makao makuu wafike ili sherehe hizo zianze. Wageni na waandaaji wa sherehe hiyo walisubiri hadi ilipotimu saa sita adhuhuri lakini hawakuona dalili za kufika wafanyakazi hao, ilipopigwa simu makao makuu ya kampuni ya Extoplus walipewa taarifa ya wafanyakazi hao kuondoka ofisini tangu saa mbili asubuhi.

Hali hiyo ilizidi kuwachanganya sana waandalizi wa sherehe hiyo na ikawabidi watume kikosi cha watu kumi wakiwa ndani ya gari kwenda kufuatilia kilichowapata wafanyakazi hao, gari ya kampuni ya Extoplus nyingine aina ya landcruiser prado iliondoka Duga maforoni kwenda kufuatilia gari ya kampuni iliyokuwa imebeba wafanyakazi wa kampuni yao. Watu waliotumwa kwenda kufuatilia wenzao nao hawakufika mbali kwani walivaana foleni kubwa ya barabarani walipokuwa wapo katika daraja liliopo katika barabara hiyo ya Mombasa ambalo linajulikana kwa vibweka vyake ambavyo vilitokea mwaka 2003 katika ujenzi wa madaraja na uboreshwaji wa madaraja, moja ya vibweka vyake ambavyo vinasemwa na wakazi wa jiji la Tanga vilivyowahi kutokea ni mashine za kupimia wakati wa ujenzi kutofanya kazi na ikapelekea mwaka huo ujenzi wa madaraja ufanyike na daraja hilo kushindikanika kujengwa.

Kikosi cha wafanyakazi kumi kilichotumwa kuangalia wenzao kiliishia hapo darajani ambako kuna lami baada ujenzi wa mara ya pili kufanikiwa kujenga, magari ya hapo darajani yalikuwa hayaendi kabisa.na ikawalazimu washuke waulize kujua kipi kilichosababisha magari hayo yakwame, walipoambiwa chanzo cha kukwama kwa magari hayo walijikuta wakikodi pikipiki kila mmoja wakienda kushuhudia wenyewe kilichotokea huku gari wakimuachia mmoja aliyekuwa dereva ambaye aligeuza akarudi.

SURA YA PILI

Utepe mwekundu tayari ulikuwa umezungushwa katika eneo la barabarani lenye damu pamoja na mifupa ya binadamu na barabara yote ilikuwa imefungwa , askari wa jeshi la polisi vikosi vitatu tofauti walikuwa wamefika hapo wakiwa wanafanya kazi yao katika eneo la tukio. Kulikuwa kuna askari wa usalama barabarani ambao walikuwa wakipima kwani inasadikika kuwa chanzo cha tukio hil ni ajali, kulikuwa kuna askari kanzu kutoka kitengo cha CID (criminal investigation department) ambao walikuja kuchunguza juu ya tukio hilo ambalo pia lilihusisha mauaji kutokana na uwepo wa mabaki ya miili ya binadamu. Kikosi cha mwisho cha jeshi la polisi tayari kilikuwa kimechelewa kufanya kazi yao kwani magari yote yalikuwa yameshateketea kwa moto kabisa, kikosi hichi cha jeshi la polisi cha zima moto kilifanya kazi tu ya kutoa miili ya watu waliokutwa katika magari hayo ambayo haikutambulika na kuipakiza kwenye magari ya wagonjwa ya hospitali kuu ya Bombo ambayo tayari yalikuwa yameshafika eneo la tukio. Askari wa CID waliochukua maelezo kwa mashuhuda wa tukio hilo walijikuta wakiwa na walakini mkubwa juu ya maelezo hayo kwani yalikuwa yametawaliwa na imani za kishirikina hasa baada ya kusikia juu ya kimbunga kilichodondosha damu nyingi iliyochanganyika na vipande vya nyama pamoja na mifupa, mashuhuda wengi wa tukio hilo walisema watu waliouliwa katika tukio hilo la kimbunga ni waganga kwasababu ya kuonekana kwa mavazi kiganga kuonekana pamoja na vitu kadhaa vya kiganga. Mashuhuda wengine wa tukio hilo walikuwa ni wasaidizi wa waganga ambao walithibitisha waliokuwa kwenye tukio hilo ni waganga waliokuwa wakiwaokoa watu waliokuwa wapo ndani ya gari iliyoungua moto. Maelezo yao yalionekana kuwa hayana maana mbele ya jeshi la polisi kwani polisi na serikali nzima ilikuwa haiamini uwepo wa wachawi au uchawi hivyo waliyapuuzia maelezo yao.

****

Kundi la vijana kumi ambao sasa wamebaki tisa baada ya mmoja wao kugeuza na kurudi na gari lilifika Bwaga Macho kwa msaada wa pikipiki tisa walizozikodi, kitendo cha kushuka kwenye pikipiki zao mmojawapo aliona kibao cha namba za gari kilichokuwa kipo kwenye majani na ikamlazimu akiokote akiangalie. Alijikuta akishtuka sana baada ya kubaini ni namba ya gari la kubeba wafanyakazi la makao makuu, yule mtu aliwaonesha wenzake akionesha haamini kama ni namba za gari la kampuni au siyo.

"hizi namba za usajili za staff bus namba 5?" Aliwauliza wenzake huku akionekana kutoamini.
"eeh! Ndiyo zenyewe kabisa, hebu chekini hii picha niliyopiga mbele ya staff bus namba 5" Mwingine alikiri kuwa namba ya basi hilo kisha akatoa simu yake akawaonesha picha ya mbele ya aliyoiseti kwenye simu yake ambayo hujulikana kama wallpaper kwa lugha ya kigeni, walipoiona hiyo picha waliamua kukimbia kuelekea enro lilipotokea tukio.

Waliyaona magari mawili yaliyoungua yakiwa yapo jirani na dimbwi kubwa la damu lililokuwa limeanza kukauka tayari. Dimbwi hilo pamoja na magari yaliyoungua yalikuwa yamezungushiwa utepe ili kuzuia watu wasiingie. Vijana hawa walijikuta wakitaka kuingia katika eneo liloozungushiwa utepe lakini askari hao waliwazuia na kuwaelewesha wapo kazini lakini vijana hawa hawakutaka kabisa tena mmoja wao ndiyo alionekana kutaka kufanya fujo na mwisho wake wote wakawekwa chini ya ulinzi. Walipelekwa hadi upande wenye askari wengi wakawekwa chini ya uangalizi wa askari na mmoja kati ya wale vijana alikuwa muda wote alikuwa akilia huku akiiangalia gari ya abiria ambayo ilikuwa imebeba wale wafanyakazi kutoka idara moja ya makao makuu ya kampuni ya Extoplus.

"Hebu nyamaza mtoto wa kiume wewe unalialia nini" Mmoja wa maaskari ambao alikuwa akiwangalia hawa vijana wa kampuni ya Extoplus alimwambia yule kijana aliyekuwa analia.

"mama yangu yupo ndani ya gari lililoungua sasa wewe ulitaka nicheke" Kijana alimjia juu yule askari aliyekuwa anamwambia hivyo.
"kijana una uhakika gani kama gari lile ndiyo mama yako alikuwemo?" Yule askari aliuliza.
"uhakika ninao kibao cha namba za gari hiki hapa tumekiokota kule kwenye majani" Aliongea yule kijana kisha akampatia askari kibao chenye namba za usajili wa gari.

"tena askari gari yenyewe ni hii hapa niliwahi kupiga nayo picha" Kijana yule aliyeiweka picha ya gari la wafanyakazi kwenye simu yake akiwa amepiga nalo picha naye aliongea huku akimuonesha askari picha aliyoipiga na ile gari yenye namba sawa na namba zilizokuwa kibao cha namba za usajili walichokiota. Yule askari aliziangalia kwa umakini kisha akaangalia muundo wa mabaki ya gari la abiria lililoungua halafu akawaambia, "hebu nifuateni mara moja"

Yule askari aliondoka mara moja akaelekea mahali pengine kwenye kundi kubwa la maaskari waliovaa kiraia na waliovaa sare za polisi, alimfuata askari mmoja aliyevaa kiraia akatoa heshima kisha akamuuma sikio huku akiwaonesha kidole wale vijana. Yule askari aliyevaa kiraia aliwasogelea wale vijana akiwa na yule askari aliyewaleta kisha akawaashiria wamfuate, alielekea kwenye gari ya polisi aina ya toyota land cruiser yenye viti katika sehemu ya kuwekea mizigo kisha akapanda akawamuru nao wapande.

"naitwa ASP John Faustin natokea kito cha polisi Mkwakwani, wenzangu mnaitwa nani majina yenu" Asp John alijitambulisha kwa wale vijana huku akionesha kitambulisho chake cha kazi kisha akawauliza majina yao, wale vijana walitaja majina yao wote.

"ok James naomba naomba uache kulia unieleze kila kitu" Asp John alimuambia yule kijana aliyekuwa analia baada ya kuona gari lile lililoungua.
"afande sisi wote ni wafanyakazi wa kampuni ya Extoplus na tulikuwa tupo Duga kwenye sherehe za uzinduzi wa nyumba mpya za kupangishwa za kampuni yetu, tulikuwa tukitarajia ujio wa staff wa idara ya uhasibu kuiwakilisha ofisi ya makao makuu tangu asubuhi lakini hadi inafika saa sita hawakuwa wamefika. Sisi tulitumwa kuwafuatilia na tulifuatilia ndipo tulipokuta hali hii tena tulianza kuanza kuona kibao cha namba za usajili za gari ya kampuni, na tuliifananisha na picha ya gari la kampuni tukaona linafanana kila kitu" James aliongea huku akiwa na uchungu.

Asp John aliyanakili maelezo ya James kisha akajiandaa kuuliza swali jingine lakini king'ora cha gari la zima moto kilimkatisha na akajikuta akiangalia lilipo gari la zima moto. Wale vijana nao waliliona lile gari la zimamoto likipita pembezoni mwa eneo la tukio kwa tabu kisha likaingia barabarani kisha likaingia barabarani likawa linaelekea Duga Maforoni kwa mwendo wa kasi sana huku milio ya ving'ora vyake ikiwa imetawala njia nzima. Asp John alipoona hali hiyo alihisi kuna jambo na akawa anataka kujua kuna nini kilichotokea, alinyanyua simu ya upepo akaongea kwa muda kisha akatulia akasikiliza upande wa pili na akajikuta amegwaya.

"nyumba za kampuni yenu zilizokuwa zinazinduliwa zote zimeungua kwa moto wa hitilafu ya umeme" Asp John aliwaambia wale vijana.
"eti nini?" James alisema kwa mshangao.

"Ndiyo maana yake hizo nyumba mlizotakiwa kuzizindua leo zote zinateketea kwa moto" Asp John alimuambia James ambaye alionekana kutoamini kwa alichomuambia, vijana wote wa kampuni ya Extoplus walichoka kuliko walivyochoka baada ya kusikia mali ya kampuni ikiwa inaungua.

Taarifa hizo zilikuwa ni kama kupigilia msumari wa moto kwenye kidonda ambacho hakijapona kwa James, kilio chake kilichoanza kunyauka usoni mwake mithili ya mche usiopata matunzo kilianza kuchipua tena kwa taratibu mithili ya mti wa muhogo unavyoota majani baada ya kuwa umechimbiwa chini kwa muda wa siku kadhaa. Kilio hicho kilikolea baada muda wa dakika mbili tu mithili ya garimoshi la makaa ya mawe lililosaza mabeleshi kadhaa ya makaa ya mawe, Asp John ilimbidi asitishe kufanya mahojiana na akawa ana kazi ya kumbembeleza James akishirikiana na wenzake ili waendelee na mahojiano. Ilikuwa ni kazi ngumu sana kumtuliza James ambaye alionekana kuna jambo jingine linamuuma ambalo halikujulikana kwa wenzake wala kwa Asp John.

"nina mkosi gani mimi?" James aliongea akiwa yupo katikati ya kilio chake.
"ya nini useme hivyo wakati huna dalili ya kuonekana na mkosi katika maisha yako" Asp John alimfariji.
"we afande hujui hulisemalo na mimi ninajua nilisemalo" James aliongea huku akipangusa michirizi ya machozi iliyokuwa inatiririka mashavuni mwake.
"James unaongea nini mbona hatukuelewi?" Kijana mmojawapo aliyefika na James aliyefika eneo hilo alimuuliza akionekana kutatizwa sana na kauli zake.

"Gasper yaani ungejua nilichokutana nacho juzi" James alisema huku akimtazama yule kijana aliyesema hawamwelewi.
"hebu wengine nyamazeni kwanza, James hebu eleza vizuri nikuelewe" Asp John aliongea akiwa amemahika bega James.
"Afande juzi nikiwa natoka kazini niliamua kuelekea Makorora jirani na kituo kikubwa cha mabasi yaendayo mikoani, niliamua kwenda kwa mguu kutokana na eneo lenyewe kutokuwa mbali na ofisi yetu. Wakati navuka reli zilizopo njiani kuelekea kwenye kituo cha basi nilikutana na mwanamke wa kiarabu ambaye alinichangamkia kwa kunisalimia ingawa hatufahamiani. Yule msichana aliniambia kuwa anafikiri kuwa mimi nimepotea njia na alitaka anielekeze njia iliyosahihi kuifuata, nilimwambia mbona sikuelewi na yeye akaniambia hivi punde utanielewa wala usijali. Aliniambia nyenzo yangu kuu ya maisha imegharamiwa kwa kitu kilicholetwa baada ya kuondoka maisha ya mwingine, mzazi wako wa kiume anatambua hili ingawa analificha ndiyo maana ana maslahi mazuri kutokana na kusitiri kisichostahiki kusitiriwa.

Sasa basi tambua na wewe unafuata njia ambayo baba yako ndiyo maana nikakuambia umepotea njia sasa basi unatakiwa ubadili muelekeo uende njia nyingine la si hivyo utakuja kuzama shimo moja ukiteketea ambalo wazazi wako watazama wakitekea siku ya sherehe ya nje ya mji. Kusema kweli nilimuona yule msichana ni kachangayikiwa na nilibaki nikiwa nashindwa hata kumuuliza swali, msichana yule nilimuona akivuka barabara kisha akawa anafuata uelekeo wa reli zinazopita pembeni ya shule ya sekondari ya Usagara . Nilibaki namtazama hadi pale lilipopita basi kubwa la abiria ambalo llinikinga nisimuone na basi hilo lilipopita sikumuona tena yule msichana na sikuelewa ameondoka vipi.

Nilibaki nilishangaa kwa muda wa dakika kadhaa hadi pale nilipohisi kushikwa bega na nilipogeuka nilimuona mwanamke ambaye kiumri anafaa kunizaa akiniuliza nina tatizo gani, nilipomjibu sina akaniuliza kwanini nilikuwa naongea mwenyewe kwa muda mrefu. Nikamwambia nilikuwa naongea na mtu ambaye tayari ameshavuka barabara ameelekea njia iliyopo relini inayoelekea katika shule ya Usagara, nilpomuambia maneno hayo aliniambia nina matatizo maana yeye alikuwa akinitazama kwa muda mrefu na ameniona nikiongea peke yangu. Niliona huyo mwanamke ananichanganya tu kama alivyonichanganya yule msichana kwa kauli zake" James alieleza akiwa amepunguza kulia kwa muda na alipomaliza aliendelea kulia, maelezo yake yaliwashangaza sana wwnzake hadi ingawa hayakuwa wazi kwao kuelewa kinamchomliza James. Imaniza kishirikina pamoja na uchawi ndiyo uliyotawala maelezo ya James, wenzake wote walimshangaa sana.

"James unajua maelezo yako hayana tija yoyote katika ushahidi wa kiserikali kwani hakuna kipengele chochote cha sheria za serikali inayosema uchawi unahusika katika ushahidi pia katika maelezo yako hayajaonsha kiini cha wewe kulia uliposikia kuhusu kuungua kwa hizo nyumba" Asp John aliongea kwa upole huku akimtazama James usoni.

"Afande nimeambiwa wazazi wataketea katika shimo moja siku ya sherehe ya nje ya mji, huoni kama siku ya sherehe yenyewe ndiyo leo na mzazi wangu mmoja ameshateketea kwenye huu mlipuko wa basi la kampuni. Unafikiri moto wa pili atakuwa salama huko hebu jaribu kufikiri, tena ngoja niende hukohuko" James aliongea akionekana amechanganyikiwa kabisa kwa matukio yaliyomtokea hadi muda huo, aliamua kunyanyuka ili aondoke lakini Asp John akamzuia na kupelekea aanze kizazaa kutokana na fujo alizozianzisha James. Wenzake nao walijaribu kumtuliza lakini ilishindikana kabisa na hata walipomzuia alipiga makelele kama kichaa akiwasihi wamuachie.

"James hebu tulia kwanza huna uhakika wa kifo cha baba yako sasa fujo za nini?" Asp John alimuambia
"unasemaje wewe? Hivi ingekuwa ndiyo wewe unakutana na mtu anakupa habari za namna hii na siku himi uliyoambiwa unakutana na mabalaa kama hili utakuwa katika hali gani? Hebu fikiri ingekuwa ndiyo mzazi wako na si kufikiri imemtokea mwenzako" James aliendelea kulalamika huku akizidi kuleta utata kwa Asp John na wenzake waliombana ili asiondoke.

"subiri basi nimalize kukuhoji ndiyo uende James" Asp John alimsihi.
"hapa hahojiwi mtu ikiwa sijaenda Duga kumuona kama baba yangu yupo hai au la, ukitaka mahojiano nami basi uniache niende na nikitoka huko ndiyo unihoji" James alizidi kuwela utata.

"ok haina shida ngoja twende wote huko kwa gari....Kostebo ondoa gari usawa wa Duga Maforoni" Asp John alimuambia James kisha akapaza sauti kumuambia askari aliyekuwa amekaa kwenye usukani.

"afande" Aliitikia yule askari kidha akawasha gari na akaweka gia akaanza kulipitisha gari pembeni ya barabara kuvuka eneo lenye utepe halafu akaongeza mwendo kuelekea Duga maforoni.

****

Muda ambao ajali ya pili ya moto inatokea kwa upande mwingine mkoa wa Tanga katika sehemu ya jiji kulikuwa kuna kikao kizito cha viongozi waiuu wa kampuni ya Extoplus wakiongozwa na mwenyekiti mtendaji na mmiliki wa kampuni hiyo bwana Hamid Buruhan, kikao hicho kilikuwa kinajadili mambo mbalimbali kwa ajili ya kukuza kampuni hiyo. Mambo mbalimbali ya kimaendeleo yalikuwa yakijadiliwa kuhusu kukuza kampuni ikiwemo suala la kuongeza nyumba za kupangisha katika sehemu zote zenye maendeleo duni ambazo watumishi wa umma hupelekwa ili wapate makazi bora kama waliyoyaacha mjini. Mojawapo ya kutekezwa mpango huo ulikuwa umeshaanza katika kijiji cha Duga na ulitegemea kuendelezwa katika sehemu zingine za Tanga nzima, mameneja hawa wakuu walikuwa, mkurugenzi, pamoja na mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo walionekana wana ari ya kuwa na kampuni kubwa yenye maendeleo katika kila kona ya nchi na hata nchi nyingine.

"Hadi kufikia mwaka 2020 mpango wetu huu utatufikisha mahala tulipojiwekea kufika katika nyanja za kimaendeleo. Extoplus kwa maendeleo" Hamid alihitisha kisha kikao hicho na hapo kikao kikawa kimefikia mwisho kwa siku hiyo, alipeana mikono na wafanyakazi wake wakuu huku akibadilishana nao mawazo kwani walikuwa pia ni marafiki zake. Walionekana na furaha sana wala hawakutambua kama kuna kuzungumkuti kimetokea kinachohusu kampuni yao, walikuwa na furaha sana kutokana na kiasi kikubwa cha fedha wanachokiingiza kutokana miradi yao na hata uzuri wa maisha wanayoishi.
"GRIIIIII! GRIIIIIIII!" Mlio wa simu ya mezani isiyo na waya ulisikika ukilia ambayo ilikatisha maongezi na Hamid akaipokea kisha akasema, "halloo!".

"kuna tatizo gani wewe Gasper hebu eleza vizuri nikuelewe" Hamid aliongea
"etii! Unase.."Hamid alisema kwa mshangao sana akionekana ameshtushwa sana na taarifa aliyopewa na hata maneno aliyoyataka kuyasema hakuyasema kabisa kwani nguvu zote zilimuishia kutokana na taarifa hiyo na akaanguka kama gunia la chumvi akiwa tayari ameiachia simu. Wenzake walipomfikia na kumtazama mapigo yake ya moyo walikuta yanapiga kwa mbali na ikawalazimu wote kwa pamoja wambebe kumuwahisha katika zahanati ya kampuni hiyo iliyopo ghorofa ya pili ya kampuni hiyo, walifanikiwa kufika salama na wakamuingiza kwenye wodi akaanza kuhudumiwa kwa haraka sana.

Mameneja wakuu wote walikaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa ili wasubiri majibu ya daktari pamoja na wauguzi ambao walikuwa wanashughulika katika kumtibu mkuu wao wa Kampuni, baada ya kupita dakika kumi na tano tangu waanze kusubiri kaimu mwenyekiti mtendaji wa kampuni na hiyo na rafiki wa karibu wa Hamid anayeitwa Hisan Shelukindo alinyanyuka kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akasema, "jamani mimi nimesahau simu katika chumba cha mkutano floor ya nane wacha niifuate nitarejea maana ni muhimu kuwa nayo kwa ajili ya kupokea taarifa muhimu".

Hisan aliposema hivyo wenzake waliitikia kwa kutikisa vichwa kisha akaondoka hadi nje ya mlango wa kuingilia katika zahanati, akitokea kwenye korido kisha akatembea hadi zilipo lifti za jengo la kampuni yao. Alibonyeza kitufe kilichokuwa kipo jirani na lifti kisha akasubiri kwa muda mfupi ambapo lifti ilifunguka akaingia akabonyeza kitufe namba nane, milango ya lifti ilijifunga na lifti ikaanza kupanda kuelekea juu hadi ghorofa ya nane, lifti ilifunguka kisha Hisan akashuka akatembea hadi kwenye mlango wa chumba cha mkutano akaufungua. Alikutana na giza kutokana na taa ya humo kuzimwa na chumba chenyewe huwa hakipitishi mwanga hata mchana kutokana kuwa na vioo visivyoruhusu mwanga kupita.

"Mmh! Hizi taa za humu kazizima nani tena" Hisan ajisemea huku akiwasha taa na ilipowaka alirudishia mlango wa chumba hicho cha mkutano kisha akatembea kuelekea mezani alipoiacha simu yake, akiwa yupo katikati ya umbali uliopo kati ya meza na mlango taa za humo ndani zilizima tena na giza likarudi kama ilivyokuwa awali kabla hajawasha taa.

"Shit! Hawa vijana wa chumba cha kuongozea umeme wanafanya upuuzi gani, inamaana wameachia umeme wa Tanesko ndiyo ufanye kazi" Hisan alijisemea kisha akageuka ili aende kufungua mlango ili hata mwangaza wa madirisha yaliyopo kwenye ngazi yamuongoze kuifuata simu yake, alipopiga hatua moja taa zikawaka ten akaghairi kwenda kufungua mlango akarudi kuchukua simu yake. Alianza kutembea kuelekea kwenye meza na alipofika akaichukua simu yake halafu akaanza kuelekea mlango ili atoke nje, alitembea kwa hatua kubwa hadi mlangoni akanyonga kitasa kuufungua lakini haukufunguka na ilionekana ulikuwa umefungwa kwa nje. Hisan alijikuta akiachia tusi zito sana kutokana na kitendo hicho, aligeuka nyuma akaangalia chini akaiona simu iliyoangangushwa na Hamid alipopoteza fahamu.

Wazo la kuiokota ndiyo lilimjia kichwani mwake na akalitaka kulitekeleza tu kwani hakukuwa na njia nyingine itakayomuwezesha yeye kupata msaada kutoka nje, alipoanza kupiga hatua ili aifuate taa zilizimika tena kisha kofi zito lilitua shavuni mwake lililompeleka hadi chini. Taa zilipowaka hakuona mtu yoyote ndani ya chumba hicho ingawa maumivu ya kofi alilopigwa alikuwa anayasikia, aliposimama miguu yake yote ilizolewa yote kama anapigwa mtama na akajikuta ameenda kusalimiana na sakafu yenye marumaru katika chumba hicho. Taa za chumba hicho zilizima tena safari kipigo kizito kikawa kinamshukia Hisan bila hata kumuona huyo anayempiga, taa zilipowaka tena Hisan hakuwa anaweza hata kuinuka na alikuwa akitokwa na damu usoni sehemu nyingine za mwili wake na mbele yake kulikuwa kuna mtoto wa miaka takribani saba akiwa amekasirika san ambaye sura yake haikuwa ngeni sana kwa Hisan.

"Jamadin" Hisan aliita kwa uoga na macho yake yakawa yakimtazama yule mtoto.
"nipe" Yule mtoto alisema kwa sauti nzito iliyojaa kitetemeshi.
"nikupe nini?!" Hisan aliuliza kwa uoga.

"narudia kwa mara ya mwisho nimesema nipe" Yule mtoto aliongea kwa hasira akaanza kumfuata Hisan
"nikupe nini?!" Hisan aliongea akiwa anatetemeka akijiburuta kusogea nyuma kwa makalio yake, Yule mtoto alizidi kumsogelea na alipomkaribia alipotea kimaajabu akamuacha Hisan akiwa anashangaa lakini mshangao wake haukudumu kwani alijikuta akishikwa kichwa chake kwa nguvu kutokea upande wa nyuma. Kichwa chake kiliminywa kwa nguvu hadi kikapasuka na akawa ameingia katika orodha ya wasio na uhai waliowahi kuwa hai.

****
Gari ya waliyopanda James na wenzake pamoja na Asp John ilikuwa ilienda kilomita kadhaa kutoka pale bwaga macho kwenye ajali wakaikuta ile gari aina ya Landcruiser prado iliyotumiwa na wakina James kuja nayo ikiwa ipo pembeni na mwenzao akiwa yupo pembeni akiwa ameegemea. Gari ya polisi waliyopanda kina James ilienda kuegeshwa mbele ya gari hiyo na kisha wote kwa pamoja wakashuka wakamfuata mwenzao wakiwa na Asp John.
"Vipi Tom gari mbovu nini?" Gasper alimuuliza yule mwenzao waliyemuachia gari arudi nalo kule Duga kwenye sherehe ya kampuni.

"aisee hii gari kuiendesha ni kujitakia kifo bora mlivyokuja tuondoke wote mimi siigusi tena na kazi kwenye hii kampuni naacha" Tom aliongea huku akiwafuata.

"kuna nini kijana?" Asp John alimuuliza.
" jamani baada ya kuniachia hii gari nimeendesha vizuri ila nilipo fika hapo nyuma nikiwa kwenye mwendo mkali naanza kusikia sauti ya bosi mkuu ikivuma kama mwangwi masikioni mwangu ikisema nataka damu ya vijana wangu kumi. Nikiwa najifikiria juu ya eneo inapotoka sauti hiyo si ndiyo nikashudia kioo cha mbele chote kikiwa kimejaa damu hadi nikawa sioni kabisa ingawa nilijitahidi kusimamisha gari nikafanikiwa na hapo damu hizo zikawa zimetoweka mara moja na kioo kikawa kawaida kama ilivyokuwa awali.

Nimeshuka ndani ya gari na sina hamu nalo tena" Tom aliongea akiwa anahema sana kwa uoga, wenzake wote waliposikia kilichomkuta ndiyo walizidi kuingiwa na hofu kasoro tu Asp John alionekana yupo kawaida tu.

"nyie hebu wacheni uoga wenu, wewe hebu nipe hizo funguo za gari hiyo niendeshe mimi na nyinyi pandeni hiyo ya polisi tuondoke" Asp John aliwaambia akionekana hana hofu kabisa.
"Afande utakufa usipande" James aliongea.

"kwani wewe ndiyo utakuwa hufi, kama leo ndiyo nitatakiwa nife nitakufa tu hata nisipoendesha hili gari, hebu nipe ufunguo sasa"Asp John aliongea na Tom akampatia ufunguo wa gari.

"mambo si hayo bwana sio kuleta uoga wa kike wakati nyinyi ni wanaume" Asp John aliongea akiwa anaelekea kwenye gari ya kampuni ya Extoplus baada ya kukabidhiwa ufunguo na Tom, aliufikia mlango wa gari hiyo akaufungua akawa anaingia ndani ya gari.

"leo sihitaji damu ya askari jasusi nataka ya hawa hapo mbele sasa ukijipendekeza tu katika jambo lisilo kuhusu utasalimiana na kaburi" Sauti ya mwangwi ilivuma kwenye masikio ya Asp John lakini akaipuuzia na kuamua kuingia ndani ya gari kisha akaiwasha gari hiyo, alinyonga ufunguo na gari ikawaka kisha ikazima. Alinyonga tena ufunguo safari hii gari ikatikisika sehemu ya injini kisha moto mkubwa ukawaka ukawa unakuja kwa kasi mithili ya moto wa nyikani kwenye katika upande aliopo Asp John.

"Ha! Ha! Ha! Ha! Si mbishi wewe ngoja nikuchome kama kuni" Sauti yenye kuvuma iliendelea kusikika masikioni mwa Asp John na hapo akaona hatar ipo mbele yake na akaamua kujirusha nje akaangukia upande wa pili barabara sehemu yenye majani, moto uliokuwa unawaka ndani ya gari haukuonekana na wala gari halikuonesha kama linalipuka. Asp John alijinyanyua kutoka pale alipojirusha akaenda hadi pale alipowaacha vijana wa kampuni ya Extoplus akawaambia, "pandeni kwenye gari tuondoke".

"Afande kulikoni mbona umejirusha nje baada ya gari kuwaka si ulisema unaliendesha" Tom alimuambia Asp John kwa kejeli kutokana na tabia yake ya kudharau mambo anayoambiwa.

"kaa kimya na upande kwenye gari na mwenzako tuondoke" Asp John aliongea huku akipanda kwenye gari la polisi aliyokuja nayo, vijana wa Extoplus nao wakapanda na safari ikaendelea na muda huo ndiyo Gasper alimpigia simu msichana wa mapokezi makao makuu aliyemuunganisha simu na mkuu wao Hamid akamueleza tukio zima. Baada ya dakika kumi na tano walikuwa tayari wameshafika Duga maforoni na wakielekea moja kwa moja hadi kwenye soko kuu la Duga maforoni wakashukia upande huo kutokana na upande wa pili kwenye eneo la tukio kutokuwa na nafasi, walivuka barabara wote kwa pamoja wakaupita uwanja wa mpira wakakuta umati wa watu ukiwa umezunguka nyumba hizo bado zilikuwa zinateketea na moto huo ulishindikana kuzimwa na kikosi cha zima moto kilichofika hapo kwani magari yao yalitumia maji hadi yakaisha lakini moto haukuzimika hata kidogo. Asp John pamoja na wale vijana waliwafuata wale askari wa jeshi la polisi kikosi cha zimamoto ambao walionekana kukata tamaa kabisa katika uzimaji moto, maaskari hao walitoa saluti kwake huku wakisema, "jambo afande".

"jamboo, nipeni taarifa mmefikia wapi katika kazi yenu kwani naona bado moto unawaka" Asp John aliwaambia.
"Afande tumefanya juhudi za kuuzima huu moto kwa kutumia kila njia ila imeshindikana hadi maji yanaisha hatukuweza kuuzima na ikatubidi tutumie gesi lakini bado tumeshindwa kuuzima na inasadikika Mkuu wa idara ya sheria makao makuu ya kampuni hizi yupo ndani ya nyumba ya tatu na hajatoka hadi muda huu na hata tulipofika tulikuwa tukisikia kelele za mtu akiomba msaada lakini sasa hazisikiki" Mmoja wa maaskari wa zimamoto aliongea kwa ufupi juu ya tukio hilo la kuungua kwa nyumba hizo, James aliposikia maelezo hayo alipiga kelele huku akiita, "Babaa!". Aliwapita askari wa kikosi cha zimamoto akakimbia kuelekea ulipo moto katika nyumba ya tatu ya kampuni, maaskari wote walianza kumkimbiza ili wamuwahi asiingie ndani ya moto huo kutokana na ukali wake.

Mbio za watu wote waliokuwa wakijaribu kumzuia James asiingie ndani ya nyumba hazikuzaa matunda yoyote katika kumzuia kwani James aliingia ndani ya nyumba hiyo kabla hawajamzuia, wenzake pamoja na maaskari wote walipojaribu kuikaribia mlango wa nyumba aliyoingia James walijikuta wakitupwa nyuma wote baada ya mlipuko mzito kutokea katika nyumba hiyo kisha nyumba nyingine zilizosalia nazo zikapata mlipuko wa aina hiyo hiyo. Asp John, maaskari wa zimamoto pamoja na wenzake James wote walisikitika kwa kitendo cha James kuingia katika nyumba hiyo inayoungua ambayo tayari imeshatoa mlipuko mzito wa moto, bado walikuwa wamelala chini baada ya kutupwa na mlipuko mzito waliposogelea nyumba aliyoingia James ili wamuokoe. Ajabu ya mlipuko huo uliowatupa haukuwaunguza hata kidogo wala hata kunuka harufu ya moshi, walikuwa wameumia tu baadhi ya sehemu za miili yao baada ya kuanguka chini.

Wakiwa hawana hata akili ya kunyanyuka pale chini tayari jambo jingine la kustajaabisha lilianza kutokea ambalo liliwafanya wakimbie kuelekea ulipo uwanja wa mpira ili wakae mbali na ardhi ambayo imebeba nyumba hizo, lilikuwa ni tetemeko la ardhi lililoikumba ardhi iliyobeba nyumba hizo huku eneo la jirani na hapo likiwa limetulia bila kupatwa na tetemeko hilo. Matofali ya nyumba hizo ambazo bado zilikuwa zinawaka yaliporomoka katika mpangilio wake uliounda ukuta na yakajazana kama tanuli katika kila nyumba iliyokuwa imejengwa, tukio hilo lilishuhudiwa na halaiki ya watu ambayo tayari ilikuwa imeshajikusanya katika uwanja wa mpira kuangalia maajabu hayo. Waandishi wa habari kituo cha televisheni cha Tanga nao walikuwa wakilirusha tukio hewani, hata waandishi wa habari waliopo mkoa wa Tanga kuwakilisha vituo vyao wakikuwa wameshawasili pia walikuwa kazini.

Tetemeko hilo la ardhi la maajabu liliendelea kutikisa ardhi hiyo inayomilikiwa na kampuni ya Extoplus hadi hata matofali yalijijaza vifusi katika kila eneo lililokuwa limejengwa nyumba yakasagika yakawa mchanga mtupu, baada ya tetemeko kutulia ndipo askari wa zimamoto na uokoaji walipopata ujasiri wa kusogelea katika kifusi cha mchanga uliosagika ambao ulikuwa ni wa matofali wa nyumba ile waliyoingia James na Baba yake kwa nyakati tofauti. Walikifukua kifusi hicho kwa kutumia vifaa vyao na kukagua kila sehemu ili waweze kuitoa miili ya baba na mwana lakini hawakuambulia hata kiungo kimoja cha miili ya James na baba yake, askari walizidi kupigwa na mshangao watu tukio hilo kwani ilikuwa ni jambo la ajabu sana.

"mmh! Sijawahi kukutana na tukio kama hili tangu nianze kufanya kazi katika kikosi cha zimamoto na uokoaji katika jeshi la polisi" Kiongozi wa askari wa zimamoto na uokoaji alimuambia Asp John.

"hivi jambo kama hili linawezekanaje?" Asp John alijikuta akiuliza swali ambalo halina maana yoyote kwa mkuu wa kikosi cha zimamoto na uokoaji.
"hilo swali hata sijui nikujibu vipi unaona kabisa imezekana katika namna isiyokuwa rahisi, mtu aingie ndani ya nyumba halafu ilipuke tu kisha tetemeko liloikumba ardhi ya ukubwa wa ekari kumi na tano litokee liangushe matofali yasagike halafu moto uzime tusipate hata baki la mwili wa binadamu katika sehemu waliyoingia" Yule mkuu wa kikosi cha zimamoto aliongea.

"ama kweli hii ni dunia ina mambo ambayo usiyoweza kuyadhania" Asp John aliongea huku akisikitika.
"ndiyo hivyo afande" Mkuu wa kikosi cha zimamoto aliongea.

"hapa hamna la ziada ngoja nirudi nikaendelee na tukio la kule la Bwaga macho, vijana nina shida na nyinyi hebu nifuateni" Asp John aliongea huku akiondoka na wale marafiki zake James wakamfuata.

SURA YA TATU

Hadi jioni inaingia tayari tukio lile la ajabu lilikuwa lishaenea jiji zima la Tanga na kwingineko ndani ya nchi ya Tanzania na hata Afrika ya mashariki, ilitokea kuwa habari iliyoteka vyombo vyote vya habari katika ukanda huu na hata katika kituo BBC idhaa ya Kiswahili ilitangazwa na kupelekea kuwa habari iliyosikika karibia dunia nzima kwa watu wanaongea kiswahili. Taarifa za vibweka vilivyotokea huko Duga zilimfikia mmiliki wa kampuni ya Extoplus Hamid akiwa yupo kitandani katika wodi ya zahanati ya kampuni yake tangu alipoanguka kwenye chumba cha mkutano, aliipata taarifa hiyo kupitia luninga iliyopo katika wodi aliyolazwa akawa amebaki na masikitiko tu kutokana na hasara aliyoipata kuungua kwa nyumba hizo ambazo zilimgharimu pesa nyingi hadi kukamilika kwake. Hadi saa nne usiku anaruhusiwa alikuwa na majonzi kutokana na jambo hilo, alirudi nyumbani kwake kwa msaada wa dereva wake.

Asubuhi ya siku iliyofuata alitoka mapema nyumbani akaenda ofisini akiwa na mawazo lukuki kichwani mwake, siku hiyo ilikuwa mbaya kwa Hamid kuliko siku zote za maisha yake kwani alipifika ofisini kwake tu akakumbana na kisanga kingine baada ya mwili wa kaimu mwenyekiti mtendaji wa kampuni yake Hisan kukutwa ukiwa chumba cha mkutano alichokuwemo siku iliyopita akiwa na wafanyakazi wake wakuu wakiongea. Mwili wa Hisan ulikutwa na mfanya usafi wa kampuni hiyo ambaye alichanganyikiwa baada ya kuuona ukiwa hauna uhai upo sakafuni. Tukio hilo lilikuwa ni tukio jingine la aina yake ambalo ilionekana ni kama mkosi umeingia kwenye kampuni hiyo kutokana na kuzaliwa kwa jambo jingine lililozidi kumchanganya Hamid, baada ya polisi kuchukua vipimo vyote pamoja na kuondoka na mwili wa Hisan afisa ajira wa kampuni hiyo aliingia katika ofisi ya Hamid akiwa na faili kubwa aliloweka mezani kisha akaweka barua juu yake.

"Msuya ndiyo nini hii unaniletea" Hamid aliuliza.
"Bosi hiyo ni barua ya kuacha kazi katika kampuni hii ili niwe salama na maisha yangu" Msuya ambaye ni afisa ajira katika kampuni hiyo aliongea.
"unasema nini wewe?!" Hamid aliuliza kwa mshangao.

"ndiyo hivyo bosi kutokana na ndoto niliyoiota usiku wa leo iliyonipa onyo juu ya maisha nikiendelea kufanya kazi hapa sina budi kuacha kazi, uamuzi huu si wangu peke yangu bali ni wa mameneja wote pamoja na wakuu wa idara wote na barua zao zipo kwenye faili nililokuletea" Msuya aliongea maneno yaliyozidi kumchanganya Hamid.

"yaani Msuya pamoja na kuwa ni msomi mwenye elimu kubwa bado unaamini ndoto" Hamid aliongea kwa masikitiko.

"Sina budi kufanya hivyo kwani kila mtu aliyeandika barua hii ameota ndoto kama hii tena ameonywa kuhusu kifo kilichotokana na ubishi wa staff wa idara ya uhasibu waliokufa jana ikiwa atabisha. Nimeamua kuacha kazi mimi na wenzangu na kila mmoja hahitaji marupurupu yoyote tunaondoka kama tulivyokuja" Msuya aliongea kisha akatoka ndani ya ofisi hiyo akimuacha Hamid akiwa amechanganyika akiwa anakaribia hata kulia, alitulia ofisini kwake kwa muda mfupi kisha akaamua kutoka kupitia idara zote kuangalia kama kile alichoambiwa na Msuya ni kweli au ilikuwa ni utani. Huko ndipo aliposadikisha maneno ya Msuya baada ya kukuta ofisi zote zikiwa zipo tupu hakuna hata mfanyakazi, Hamid alijikuta akianza kulia mwenyewe na akaona hali aliyoikimbia kabla hajawa na familia sasa inaanza kumrudia. Yeye hakutaka hali hiyo imtokee tena na alikuwa yupo tayari kuizuia kwa namna yoyote ile na hapo ndipo alipopata ufumbuzi wa matatizo yake kwa mtaalamu wake maalum.

"Dokta Bundi atanisaidia niepukane na adha hii ngoja niwahi kwenda kwenda kwake Mwamboni" Hamid alijisemea mwenyewe kisha akaanza kutoka mbio kuelekea nje ya ofisi ambapo alipanda gari yake akaiondoa kwa mwendo wa kasi akiwa na haraka ya kuwahi safari yake. Aliendesha gari kwa mwendo wa kasi akiwa na ari ya kuwahi kufika Mwamboni kwa mganga wake ambaye huwa anamsaidia katika matatizo mbalimbali, akiwa yupo ndani ya gari akiwa anakatiza katika barabara ipitayo Chumbageni alisikia sauti ikimuambia "aisee nishushe hapohapo chumbageni police station nataka kuongea na jamaa yangu".

Hamid alishtuka sana akatizama nyuma kwa uoga na akijikuta anatamani hata apotee kimiujiza humo ndani ya gari, laiti kama moyo wake ungekuwa na nguvu kama ya vijiko vinavyojenga barabara ya kugusa ukuta tu na kuuangusha basi ungekuwa ushapasua kifua chake kwa jinsi ulivyokuwa unadunda kwa nguvu baada ya kumuona Hisan aliyekutwa akiwa amekufa katika chumba cha mkutano asubuhi ya siku hiyo.

"unashangaa nini Hamid hebu simamisha gari hapo Chumbageni polics station nikaangalie ripoti ya kifo changu kilichonipata jana kama polisi wamechunguza kiusahihi" Hisan aliongea huku akionekana yupo katika hali ya kawaida tu, Hamid alikuwa tayari ameshaachia mkojo ulimtoka bila hata kujijua.

"Ona sasa dume zima una miaka arobaini na nane unajikojolea kisa kumuona mtu aliyekufa akiwa anatembea, hebu simamisha gari nishuke wewe nishafika tayari nataka nikaangalie ripoti ya kifo changu nasikia anayo Inspekta Ismail Mdoe. Au hii sura inakuchanganya ngoja niibadilishe basi uoga ukupungue" Hisan aliongea kisha akabadilika kuanzia sura hadi mwili ukawa wa mtoto aliyemtokea Hisan kabla hajafa.

"Hapo vipi utaniogopa tena?" Aliuliza huku akimtazama Hamid ambaye alizidi kuogopa na akawa anahangaika kufungua mlango ili ajitupe nje kuikimbia sura aliyoiona sasa hivi ikiwa ina macho mekundu, milango ya gari ilikuwa haifunguki na hata alipotoa kifunga mlango bado haikufunguka hata kidogo. Hamid aliendelea kuhangaika na kukivuta kitasa cha ndani cha mlango akiwa haamini kama mlango umejifunga, alibaki akihangaika kuchezea kitasa kutokana na kuchanganywa na tukio hilo.

"ukimaliza uniambie" Yule mtoto alimuambia huku akikunja miguu yake ikatengeneza umbo la nne akimtazama akiwa na tabasamu lisiloashria furaha hata kidogo.

Hamid alikuwa ameshasahau kama alikuwa anaendesha gari na alipokuja kukumbuka aliona gari linaenda lenyewe kwa mwendo wa taratibu sana na lilikuwa likipitwa na magari yanayowahi. Alibaki akimtazama yule mtoto huku akitetemeka kiuoga na mikono akiwa ameweka ishara ya kuomba msamaha.
"halafu unataka kuruka nje huku umejifunga mkanda sasa ndiyo unafanya ujinga gani?" Yule mtoto alimuambia Hamid ambaye hakuwa anatambua hakuwa amefungua mkanda katika harakati za kutaka kuoko nafsi yake, alipotaka kuufungua mkanda yule Mtoto alinyoosha mkono wake na mkanda wa gari ukamzunguka Hamid shingoni mwake kama nyoka na ukaanza kumkaba kwa nguvu hadi mishipa ya damu ya kichwani ikawa inaonekana.
"Nipe" Yule mtoto alimuambia Hamid huku akimtazama kwa hasira.

"siii....sinaa" Hamid aliongea kwa tabu kutokana na jinsi mkanda ulivyomkaba.
"kimoja umenipatia, nataka unipe kilichobakia. Sasa nipe!" Yule mtoto aliongea kwa hasira huku akitokwa na cheche za moto mdomoni.
"sinaa!" Hamid aliongea kwa tabu huku macho yake yakibadilika rangi kutokana na kukabwa, mishipa ya kichwani ilikuwa imemtoka hasa.

"Ok haya fungua mlango ukimbie" Yule mtoto aliongea na muda huo mkanda ukaacha kumkaba Hamid na mlango ikawa ipo kawaida, Hamid alifungua mkanda akafungua mlango akajitupa nje bila hata kuangalia barabarani. Kitendo cha Hamid kujitupa nje ilsikika
honi ya gari ya mizigo iliyolia kwa nguvu pamoja na vyuma vya breki kutoa mlio mkali, vishindo viwili vizito vikafuata kwa kupishana sekunde mbili na hapo kila aliyekuwa yupo karibu na eneo hilo akashika kichwa kwa mshangao.

Gari aina ya Scania ya mizigo ndiyo ilikumbana na kishindo cha kwanza baada ya kumgonga Hamid na kupelekea kichwa chake kupasuka na kutengeneza taswira isiyofaa barabarani kuangaliwa na binadamu wa kawaida kwani haifai binadamu kuona kichwa cha binadamu mwenzako kikiwa kimepasuliwa kama puto liliingia katika kichaka chenye miiba. Kishindo kingine kilikuwa ni cha gari la Hamid baada ya kugonga mti wa mwembe uliopo katika makutano ya barabara inayotoka Kwa minchi, inayoelekea Amboni na hiyi inayopita Chumbageni. Ndani dakika zisizopungua tatu tayari maaskari walishajaa kutokana na kituo cha polisi kutokuwa mbali na hapo ilipotokea tukio hilo, askari hao walikuwa mchanganyiko kati ya askari wa usalama barabarani na wa kawaida ambao walishiriakiana na kuifanya kazi hiyo kwa haraka.

Uchunguzi wa magari yote yalipokaguliwa yalizidi kushangaza watu kwani katika gari aina ya Scania hakukuwa na dereva ingawa mashuhuda walisema dereva hakushuka na katika gari aina ya range rover sport aliyokuwa anaitumia Hamid hakukuwa na dereva vilevile. Maaskari wakiwa bado hata hawajasahau tukio la siku iliyopita tayari wanakutana na tukio jingine la kushangaza kama hilo.

"sasa haya magari yatajiendeshaje yenyewe hebu nyinyi kachunguze vizuri mazingira ya jirani na ule mwembe ilipogonga ile Range tena someni na stika zake tumjue mmiliki nilitaka kusahau hilo" Askari mwenye nyota tatu mabegani mwake aliongea, maaskari walipiga saluti kisha wakaenda kuchunguza walichoambiwa na mkubwa wao kwa haraka. Baada ya dakika moja tu tangu wale askari waondoka simu ya upepo ya yule Inspekta ambaye ndiye mwenye nyota tatu ikakoroma kisha ikasikika sauti ya yule askari mwingine ikimuita kule kwenye gari aina ya Range rover iliyogonga mti wa Mwembe, Inspekta huyu alienda haraka hadi pale kwenye kwenda kuona alichoitiwa. Alipofika alipigiwa saluti kisha akaongozwa na askari mwingine hadi kwenye kioo cha gari hiyo, yule askari aliyemuongoza alimuonesha yule Inspekta stika za gari ile ambazo ziliandikwa jina la mwenye gari.
"Hamid Buruhan, si mmiliki wa kampuni iliyokumbwa na kadhia isiyoeleweka jana" Inspekta aliongea
"ndiyo afande" Yule askari aliyemuita aliitikia.

"Sajenti Shehoza hebu licheki hili gari halafu..." Yule Inspekta aliongea lakinj akasitisha maneno yake baada ya kuona alama za kung'oka majani yaliyoonekana yametokana na kuburuzwa kitu kuelekea katika majani marefu yaliyopo jirani na Mwembe, aliamua kufuatilia alama hizo kuelekea kwenye majani marefu akiwa anatazama chini kwa umakini sana ambapo aliona vitu mbalimbali vya uganga vikiwa vimeanguka njiani kama vile hirizi na vibuyu pamoja na kitambaa chekundu cha kaniki. Inspekta huyo aliendelea kufuatilia hadi mwisho wake ambapo alikutana na mwili wa mzee wa makamo ukiwa umelazwa kwenye majani yaliyoonekana kupunguzwa kwa kitu chenye kali katika sehemu ulipolazwa mwili huo. Mavazi yaliyokuwa yamevaliwa na maiti hiyo ambayo yalionakana aliyavaa mwenyewe kabla hajakumbwa na umauti yalikuwa ni ya kiganga kabisa, kaniki nyekundu aliyojifunga ilitosha kumtambulisha kama mganga ukiachilia mbali hirizi iliyopo begani kwake.

Inspekta yule aliwaamrisha maaskari wale wachukua vipimo vyote juu ya mwili kisha wawaite wauguzi maaskari waliofika hapo baada ya kupigiwa simu waje wauchukue mwili ukahifadhiwe, Inspekta huyo aliondoka akarudi alipokuwa awali ambapo barabara ilikuwa inasafishwa baada ya uchukuaji wa vipimo kukamilika alisimamia taratibu zingine. Gari la kuvuta magari mabovu maarufu kama Break down nalo liliitwa likaondoa magari yote yakaenda kuhifadhiwa katika kituo cha polisi cha Chumbageni. Maaskari waliokuwa kule kwenye majani marefu walirejea wakiwa na wauguzi maalum wa jeshi la polisi waliobeba machela yenye mwili wa yule mzee aliyekutwa kwenye majani, wakiwa wanaelekea kwenye gari la wagonjwa la hospitali kuu ya Tanga yaani Bombo. Mwanamke mmoja asiyejulikana ametokea wapi alikimbia hadi pale walipokuwa wale maaskari na wauguzi akaufungua ule mwili kisha akaanza kulia kwa uchungu huku akipiga kelele kwa uchungu.

"Jamani mume wangu mimi!" Aliropoka yule mwanamke huku akiishika machela iliyobeba mwili.
"we mama hebu tulia tufanye kazi yetu" Sajenti Shehoza aliongea huku akimzuia yule mwanamke na wale wauguzi wakaendelea na safari.
"Baba Hadija nilikumbia usisaidie usiowajua umeona sasa, Mayoooo mayooo" Yule mwanamke alizidi kuongea kwa nguvu huku akilia kama mtoto mdogo.

****

Wakati askari wakishughulika katika ajali ya kutatanisha iliyotokea Chumbageni, upende mwingine wa jiji la Tanga katika maeneo ya Raskazone hali ilikuwa shwari kuliko kawaida katika kampuni ya mafuta ya Matro inayosifika kwa kutoa huduma bora za mafuta jijini Tanga na kwingineko. Ndani ya makao makuu ya kampuni hii wafanyakazi walikuwa wakiendelea na kazi kama kawaida ili kuinua kampuni na pia kuendesha maisha yao. Siku hiyo mmiliki wa kampuni hiyo Hussein Buruhan ambaye ni mmojawapo wa matajiri wakubwa nchini alikuwa yupo ofisini kwake ghorofa ya kumi na mbili ya jengo la kampuni hiyo akiendelea na kazi kama kawaida.

Baada ya nusu saa za uchapaji kazi alianza kuhisi kubanwa na haja ndogo na ikambidi aende msalani kutokana na kushindwa kuvumilia kukaa katika hali hiyo, alifunga ofisi kisha akaingia katika maliwato ambayo ipo jirani na ofisi yako. Aliingia moja kwa moja msalani akajisaidia kisha akatoka akiwa anapiga uruzi wa nyimbo anayoipenda akiwa na tabasamu pana usoni mwake, kama ilivyo kawaida yake huwa akitoka maliwatoni lazima aende kwenye kioo kipana chenye masinki yenye koki kadhaa za maji kwa chini yake ili anawe mikono. Alienda kwenye sinki hilo akafungua maji akanawa mikono kisha akanawa uso akiwa anapiga uruzi wa wimbo anaupenda unaoitwa this i promise you ulioimbwa na kundi la wanamuziki wa kimarekani liitwalo N-sync, akiendelea kupiga uruzi huo ghafla taa za huko kwenye maliwato zikazima na kukawa giza kutokana na madirisha madogo yaliyomo humo kutopitisha mwanga vizuri.

Baada ya nusu saa za uchapaji kazi alianza kuhisi kubanwa na haja ndogo na ikambidi aende msalani kutokana na kushindwa kuvumilia kukaa katika hali hiyo, alifunga ofisi kisha akaingia katika maliwato ambayo ipo jirani na ofisi yako. Aliingia moja kwa moja msalani akajisaidia kisha akatoka akiwa anapiga uruzi wa nyimbo anayoipenda akiwa na tabasamu pana usoni mwake, kama ilivyo kawaida yake huwa akitoka maliwatoni lazima aende kwenye kioo kipana chenye masinki yenye koki kadhaa za maji kwa chini yake ili anawe mikono. Alienda kwenye sinki hilo akafungua maji akanawa mikono kisha akanawa uso akiwa anapiga uruzi wa wimbo anaupenda unaoitwa this i promise you ulioimbwa na kundi la wanamuziki wa kimarekani liitwalo N-sync, akiendelea kupiga uruzi huo ghafla taa za huko kwenye maliwato zikazima na kukawa giza kutokana na madirisha madogo yaliyomo humo kutopitisha mwanga vizuri.

*****

"shit! Yaani hawa Tanesco wanakera sana" Hussein alisema kutokana na umeme kuzimika humo maliwatoni, lawama zake zote alizielekeza kwenye kampuni ya usambazaji umeme nchini kutokana na kuzimika kwa taa ya humo ndani. Hakuwa ametambua kama alikuwa anawabebesha lawama kwa wasiohusika na tatizo hilo, hakika hakujua kama kuna ugeni uliokuwa umemfikia na dalili yake ndiyo hiyo ya kuzimika kwa taa humo maliwatoni. Akiwa na uso ulionekana kukerwa kabisa na tatizo hilo taa ziliwaka tena akajikuta akitukana tusi zito halafu akainama ili anawe uso ingawa alisita baada ya kuhisi hayupo peke yake blali kuna mtu mwingine, aligeuza uso pembeni akamuona kijana mwenye asili ys uchotara wa kiarabu na mbantu akiwa ananawa uso wake tararibu bila hata kushughulika kumuangalia Hussein na wala haikujikana aliingia muda gani hapo.

"wewe umeingia saa ngapi hapa?" Hussein alimuuliza yule kijana, yule kijana aliposikia swali la Hussein aliacha kunawa kisha akajifuta uso wake halafu akamtazama kwa sekunde kadhaa.

"nimeingia muda si mrefu" Yule kijana alijibu kisha akafungua tena koki ya maji akaendelea kunawa, jibu hilo lilimchanganya zaidi Hussein na akajikuta akimshangaa sana yule kijana hadi akaanza kumuogopa kwani mlango haukuwa umefunguliwa kuashiria kama kuna mtu aliingia.
"Kwanza wewe ni nani mpaka uingie kwenye sehemu ambayo staff wa kawaida hawafiki?" Hussein alimuuliza yule kijana.

"mimi ni Zalabain ndiyo maana nimeingia humu na cheo changu ni prince ndiyo maana nipo humu" Yule kijana aliongea huku akitabasamu.
"unasemaje mbona sikuelewi na sikujui?" Hussein aliongea kutokana na kuchanganywa na maelezo ya yule kijana.

"utanielewa na utanijua" Yule kijana aliongea na hapo ndani taa zikazimika tena na zikawaka, yule kijana sehemu aliyokuwepo awali hakuonekana kabisa na hapo ndipo Hussein alizidi kuingiwa na uoga. Alipoangalia kwenye kioo ambacho kilimuonesha upande wa nyuma yake ndiyo alizidi kuchanganyikiwa kwa alichokiona, alitaka kusoma dua ya kujikinga na viumbe waovu lakini mdomo wake ulikuwa mziti na haukufunguka kabisa kama amelishwa mawe. Alipogeuka ili aone vizuri kwa kudhani labda anaona maruweruwe tu ndipo akajikuta akipokea kofi zito lililompeleka hadi chini, alipoinua uso wake alikutana uso kwa uso na yule mtoto ambaye aliwatokea Hisan na Hamid muda mfupi kabla hawajaiaga dunia.

"Huna akili kweli yaani unataka kusoma dua chooni kisa umeniona mimi, toka lini jina la Muumba likatajwa chooni wewe na hata ungesoma unafikiri angekusaidia wakati muda unaingia chooni hukumkumbuka hata kidogo kwa kumuomba akulinde ukiwa humu" Yule mtoto aliongea huku akisikitika.
"sio mimi nisamehe" Hussein aliongea huku akitetemeka akiwa amekaa kitako kwenye sakafu ya maliwatoni hapo.

"Heh! Kwanini siyo wewe, inamaana huitwi Hussein Buruhan mtoto wa tano wa mzee Buruhan" Yule mtoto alimuambia Hussein huku akionekana kushangaa kwa jinsi anavyoongea.

"ndiyo mimi Hussein" Hussein alijibu huku akitetemeka kwa uoga.
"basi kama wewe ndiyo Hussein basi ndiyo wewe" Yule Mtoto aliongea kwa hasira kisha akamsogelea Hussein kwa kasi sana na alipomfikia alimkaba kooni hadi akawa hawezi kupumua vizuri, alimnyanyua juu akambamiza kwenye kioo kikubwa kilichokuwa kipo humo ndani juu ya masinki ya kunawia. Hussein alikatwa na vipande vya vioo na akajikuta akipiga kelele za kuomba msaada huku akimtaja mama yake kama ilivyo watu wengi wakiwa katika matatizo, kelele hizo hazikusaidia chochote kwani kipigo kiliendelea kama kawaida na alizidi kumtaja mama yake.

"Watu kama nyinyi ndiyo mungu hawasaidii hata kidogo, yaani unamkumbuka mama yako kwenye shida halafu unamsahau Mungu wako anayekupa pumzi hizo zinazokutia jeuri. Haya nipe upesi" Yule mtoto alimuambia Hussein.

"si.....sina" Hussein aliongea kwa tabu kutokana maumivu ya kipigo alichokipata.
"ohoo! Huna, basi utaenda kuonana na kaka yako Hamid huko roho yake ilipo" Yule mtoto aliongea kisha akajizungusha kama pia hadi kikatokea kimbunga kilichomzoa Hussein akawa yupo katikati, milio ya makofi ndiyo ilifuatia akiwa yupo humo ndani ya kimbunga hicho na makelele ya maumivu yakawa yanasikika. Kimbunga hicho kilipokuja kuisha Hussen alitupwa chini akiwa amevunjika sehemu mbalimbali za mwili wake, Yule mtoto bado alikuwepo na safari hii alikuwa yupo karibu yake zaidi na mkono wake wa kushoto ukiwa umekamata koo la Hussein.

"salamu zao kwa waliotangulia kabla yako" Yule mtoto aliongea kisha akalivuta koromeo la Hussein hadi akalitoa nje kiaha akalivunja akautoa mfupa wake akauweka pembeni, Hussein tayari alikuwa amekwisha maliza mkataba wake wa kuishi duniani hadi muda huo akiwa miongoni waaiokuwepo duniani kimwili.

****
KITUO CHA POLISI CHUMBAGENI
TANGA

Baada ya yule mama kuvamia mwili wa yule mwanaume aliyekutwa kwenye majani amekufa katika ajali ya gari ya Hamid, yule Inspekta aliamuru yule mama awekwe chini ya ulinzi kwa mahojiano zaidi na alipelekwa kituo cha polisi Chumbageni kusubiri Inspekta arudi ili afanye mahojiano naye. Inspekta yule aliporudi kituoni baada ya kumaliza kusimamia kazi kule barabarani yule mwanamke aliingiza kwenye chumba cha mahojiano, yule inspekta aliingia katika chumba cha mahojiano akiwa na maaskari waliokuwa wadogo kivyeo.

Naitwa Inspekta Ismail Mdoe, kulia kwangu yupo Sajenti Juma Shehoza na kushoto kwangu kuna Staff sajenti Dickson Mushi, sijui mama unaitwa nani?" Yule Inspekta ambaye ndiye Inspekta Mdoe aliongea huku akitoa utambulisho kwa wenzake.

"naitwa Mwanamkuu Jumanne" Yule mwanamke alijibu kwa unyonge.
"Ok Bi Mwanamkuu una umri gani, unafanya kazi gani na unaishi wapi?" Inspekta Mdoe alimuuliza.
"nina miaka 48 nafanya biashara ndogondogo, ninaishi hapahapa Chumbageni" Bi Mwanamkuu alijibu kwa unyonge, muda huo Sajenti Shehoza alikuwa akiandika kila kilichokuwa kinafanyika kwenye mahojiano hayo.

"wewe na marehemu mna uhusiano gani?" Inspekta Mdoe aliuliza.
"Marehemu ni mume wangu" Bi Mwanamkuu alijibu.

"ok, unaweza ukatuambia kilichokufanya utamke yale maneno kwenye eneo la ajali?" Inspekta Mdoe alimuuliza.
"afande chanzo cha kutamka maneno yale ni kutokana na mume wangu kuingilia mambo yasiyomuhusu na hatimaye akauawa" Bi Mwanamkuu alizidi kuongea na safari machozi yalikuwa yakimtoka.

"una uhakika gani na hayo unayoyasema? Hebu fafanua kauli yako" Staff sajenti Mushi alimuuliza kwa mara ya kwanza.
"muda mfupi kabla mume wangu alikuwa akiendelea na kazi zake za uganga, alipandisha maruhani yake akasema kuna mtu yupo hatarini kuuawa hivyo anahitaji kumsaidia. Akichukua vifaa vyake vya uganga akaenda huko, na sikumuona tena hadi niliona mnambeba" Bi Mwanamkuu aliongea huku akilia, maelezo hayo yaliwafanya maaskari hao waliokuwa wanamuhoji watazamane kwa muda wa sekunde kadhaa.

"Mama usituletee maelezo yasiyokuwa na uthibitisho wowote" Inspekta Mdoe aliongea akionesha kuchanganywa na maelezo aliyoambiwa.
"Afande hii siyo kiwango chenu naomba muiache na huyu mbaya wangu aliyeniulia mume wangu nitamkomesha" Bi Mwanamkuu aliongea kwa hasira kisha akaanza kuangaza pande zote za humo, alianza kunguruma kama simba akiashiria mashetani yamempanda. Maaskari waliokuwa wanaomuhoji walibaki wakimtazama tu wakionekana kuwa hofu nae, Bi Mwanamkuu aliposimama akionekana ana hasira kimbunga kizito kiliibuka humo ofisini kikamzoa na kilipotoweka naye alitoweka papo hapo.

****

Mfanyakazi wa kampuni ya Matro anayehusika na usafishaji vyoo na korido katika ghorofa la kampuni hiyo alianza kufanya kazi kama ilivyokuwa kawaida yake, alianza kufanyakazi katika ghorofa tofauti na mwishowe akamalizia katika ghorofa ya mwisho ambayo ndiyo inapatikana ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Kijana huyo anayeitwa Niko alianza kusafisha korido mbalimbali za ghorofa hiyo na hatimaye zamu ya kusafisha maliwato za ghorofa hiyo ya mwisho ikaanza, alianza kwa kusafisha maliwato ndogo na hatimaye akahamia kwenye maliwato kubwa ambayo ipo jirani na ofisi ya mmiliki wa kampuni hiyo. Akiwa na kotoroli chenye vifaa ambacho alikiburuza hadi katika mlango wa maliwato hiyo kisha akaupa mlango mgongo akawa anakiburuza kitoroli ili aingie nacho ndani akiwa ameufungua mlango kwa kuusukuma na mgongo wake.

Alifanikiwa kuingiza kitoroli hadi ndani akiwa anaimba kwa kuchangamka akiwa ameungalia mlango na ameipa mgongo sehemu ya ndani ya maliwato hiyo, akichukua fagio lenye nyuzi maalum kwa kufanyia usafi akaanza kufanya usafi kuanzia mlangoni na sehemu za pembeni ya mlango. Baada ya kumaliza kufanya usafi maeneo hayo ndipo alipogeuka nyuma ili aendelee na usafi akakutana na hali isiyopendeza kutazamwa. aliuona mwili wa bosi wake mkuu ukiwa upo chini na koromeo lipo pembeni ya mwili huo. Niko alijikuta akitoa ukelelewa uoga kisha akakimbia kuelekea mlangoni, aliponyeza kitufe cha kengele ya hatari ya ghorofa kisha akakaa kitako akawa kama mtu asiyejielewa kabisa.

Mlio wa kengele ya hatari katika jengo lote ulisikika na kupelekea kundi kubwa la wafanyakazi litoke nje ili kuchukua tahadhari kama kuna uwepo wa jambo la hatari, walinzi wa kampuni wenye silaha wakaanza kupandisha wakiwa na tahadhari kubwa kwani kengele hiyo ilimaanisha jambo la hatari. Walinzi hao walipita kwenye ghorofa mbalimbali kwa tahadhari na hatimaye wakafika ghorofa ya mwisho, walitembea kwa tahadhari katika ghorofa hiyo hadi walipomuona Niko wakamfuata huku wengine wakiwa wanaangalia usalama. Walipomfikia Niko aliishia kuonesha kidole ndani ya maliwato ndipo maaskari hao walipoingia huku wengine wakimuuliza maswali ambayo hakuyajibu zaidi ya kutetemeka. Walinzi walioingia waliwaita wenzao wakajionea kilichotokea humo ndani ya maliwato, simu ilipigwa haraka kituo cha polisi ambapo polisi walifika ndani ya muda mfupi tu wakajionea hali halisi na wakachukua vipimo mbalimbali pamoja na kuuchukua mwili wa Hussein.

****

Maeneo hayohayo ya Raskazoni kwa upande mwingine kulikuwa kuna mzee wa makamo aliyekuwa akiangalia luninga sebuleni, alikuwa ni mzee wa miaka takribani hamsini na ushee ingawa alionekana kutozeeka sana. Wakati mwili wa Hussein ukiwa umeondolewa kule kazini na ukiwa tayari umeshafikiishwa hospitali ili kuhifadhiwa, mzee huyu aitwae Shafii Buruhan alipigiwa simu na alipoipokea na akasikia alichokisikia alizidi kuchanganyikiwa na akabaki akilia kwa sauti kama mtoto mdogo hadi mkewe akaja sebuleni akamuona mume wake akiwa katika hali hiyo.
"Baba Zayina kuna nini?" Mke wake aliimuuliza baada ya kumkuta akiwa analia kama mtoto.

"wadogo zangu Hamid na Hussein mama Zayina" Shafiu alijibu huku akilia kwa kushindwa kustahimili jambo aliloambiwa.
"wamefanyaje tena?" Mke wake aliuliza akionekana kutoelewa.

"hatunao tena duniani, wadogo zangu mimi jamaniii" Shafii alijibu huku akilakamika na mke wake akaanza kumbembeleza huku yeye mwenyewe akilia baada ya kusikia mashemeji zake wamefariki. Shafii alilia sana kama mtoto mdogo kutokana na vifo hivyo, mkewe naye alikuwa ana kazi ya kumbembeleza ingawa hata yeye alikuwa akitokwa na machozi.

"Baba Zayina jikaze wewe ni mwanaume" Mke wake alimwambia huku akimfuta machozi, muda huo mlango wa hapo sebuleni ukafunguliwa na akaingia mwaume alivaa kinadhifu.

"Ally mdogo wangu" Shafii akimuita yule mwanaume kwa jina lake halisi.
"Kaka kuna nini mbona unalia" Allu alimuuliza kaka yake.

"kaka zako Hamid na Hussein hatunao" Shafii aliongea kwa huzuni huku akitokwa na machozi, Ally aliposikia taarifa hiyo alijikuta akikaa chini kisha machozi yakaanza kumtoka ingawa hakutoa sauti kuashiria analia.

"Ally jikaze twende hospitali tunahitajika" Shafii aliongea akinyanyuka macho yakiwa mekundu kwa kulia, aliingia ndani halafu akarejea akiwa amevaa viatu na miwani ya jua ili kuficha macho yake.

"Farida sisi tunatoka, wewe baki. Ally twende" Shafii alisema huku akimnyanyua, kisha wakaondoka hadi nje.

***-

Taarifa ya kifo cha mmiliki wa kampuni ya Matro tayari zilishawafikia waandidhi wa habari na hadi anafikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti tayari waandishi wa habari walikuwa wamejaa nje ya chumba hicho wakisubiri kupata habari kamili. Hadi gari aina ya Cadillac la milango sita linawasili jirani na mlango wa chumba cha kuhifadhia maiti bado waandishi wa habari walikuwa wamejazana eneo hilo, dereva wa cadillac hilo aliposhuka kwenda kufungua mlango waandishi wa habari walikuwa wapo makini kujua anayeshuka katika gari hilo la gharama ni nani. Shafii alipotangulia kushuka kamera mbalimbali za waandishi wa habari zilikuwa zikifanya kazi ya kumpiga picha tu, waandishi wa habari walikimbilia kumuuliza maswali mbalimbali lakini hawakupata ushirikiano.

Shafii aliingia ndani ya sehemu ya kuhifadhia maiti akiwa na Ally na alipita hadi ofisini ndani ya ofisi hiyo ya chumba cha kuhifadhia maiti alimkuta msimamizi wake akiwa amekaa kwenye kiti akipitia mafaili mbalimbali.

"karibu mzee" Msimamizi wa hicho chumba alimkaribisha.
"Asante" Shafii aliitikia huku akivua miwani ya jua akafuta machozi.
"pole sana mzee wangu kwa masaibu haya" Msimamizi alimpa pole.
"asante sana, nakusikiliza" Shafii alisema.

"Ok nifuateni" Msimamizi aliongea kisha akainuka akaingia ndani ya chumba cha kuhifadhia maiti, Shafii na Ally nao walimfuata kwa nyuma. Yule msimamizi alielekea sehemu yenye mitoto mingi kama ya meza au kabati akiwa anatafuta namba maalum hadi akazifikia namba za mitoto ya makabati ya jokofu ya kuhifadhia maiti yanayofuatana, alifungua mojawapo kisha akafungua lailoni lenye zipu akamuonesha Shafii ambapo aliuona mwili wa mdogo Hussein ukiwa hauna koo. Shafii aliutazama mwili ule kwa umakini huku machozi yakimtoka kisha akamuamuru yule msimamizi afungue jingine, jingine lilipofunguliwa aliuona mwili wa mdogo wake Hamid ukiwa umeharibika kutokana na ajali aliyoipata.
"hapa kuna mkono wa mtu nasema sikubali" Shafii aliongea kwa hasira.

"ndiyo maana mzee nikakuita uje kujionea mwenyewe ili uwahi kwa babu kule" Msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti alimuambia.
"ok nashukuru ngoja niende kwa babu yako kabla mambo hayajawa mabaya" Shafii aliongea huku akimpa burunguru la pesa yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti halafu akaondoka huku Ally akiwa anamfuata, walipotoka nje Shafii alimuambia mdogo wake "Ally wewe nenda ukampe taarifa shemeji Hamisi na wengine juu ya vifo hivi, mimi naenda kwa Mtaalamu Sauti ya radi kule Amboni".
Shafii aliingia ndani ya gari na dereva akaondoa gari, Ally alichukua teksi naye akaondoka.

****

Safari ya Shafii iliishia Amboni kwa mganga wake ambaye ndiye babu yake yule msimamizi wa chumba cha kuhifadhia maiti Bombo, gari yake ilisimama kwenye umbali mrefu kutoka pale yalipo makazi ya mganga huyo kwenye pori dogo lililopo karibu sana na mto Zigi. Shafii alishuka akatembea kwa mguu hadi kwenye kibanda cha mganga Sauti ya Radi kisha akabisha hodi huku akivua viatu vyake, alipopewa ukaribisho aliingia ndani akaketi kwenye jamvi kuukuu mbele ya vibuyu vya mganga.

"Karibu Shafii mwana Buruhan" Mganga Sauti ya radi alimkaribisha Shafii kwa mara ya pili, Shafii aliitikia ukaribisho huo kisha akaeleza kila kitu kwa mganga.

"hakuna kinachoshindikana hapa mbele ya sauti ya radi nikinguruma natoa miale maadui wanashindwa wenyewe, kuna kiumbe anakuandama na leo ndiyo kiama chake" Mganga Sauti ya radi aliongea kwa msjigambo kisha akanyanyuka akatoka nje, alirejea akiwa na moto kidogo kwenye chombo kinachotumika kuwekea ubani. Alikiweka kile chombo mbele ya Shafii kisha akamwaga dawa zake kwenye moto uliomo kwenye chombo hicho, moshi mzito ulitanda humo ndani na mzee Sauti ya radi akawa anaimba nyimbo zisizoeleweka huku akimzunguka Shafii akicheza kama anacheza ngoma ya kikabila. Moshi huo ulipokuja kupungua Mganga akiendelea kucheza alihisi anashikwa kiuno wakati akicheza, moshi ulipoisha alihisi anashikwa makalio kwa kutomaswa. Alipogeula nyuma kumuangalia anayemshika alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa anatabasamu.

"Yaani ungekuwa mwanamke ungefaa kucheza Baikoko kwa jinsi inavyojua kukata kiuno" Zalabain aliongea akiwa bado hajatoa mikono kwenye makalio ya Mganga Sauti ya radi.

Zalabain alizidi kuonesha uso wa dharau kwa kuyaminya makalio ya mganga Sauti ya Radi na kusanabisha mganga huyo apandwe na hasira sana, Mzee Sauti ya Radi alinguruma kwa nguvu kama simba dume aliyejeruhiwa akiashiria mashetani yamempanda tayari kwa ajili ya kukabiliana na kiumbe aliyejitokeza muda huo ambaye hakuonekana na nia nzuri kwake wala kwa Shafii. Alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain aliambulia patupu kwani hakuonekana kabisa, Mganga alipoona anachezewa akili alizidi kupandwa na hasira mara dufu. Aligeuka kila pande za eneo alilopo lakini hakumuona Zalabain na alimuona Shafii akiwa amekaa pale alipokuwepo akionekana hajui chochote kinachoendelea, Mganga hapo alishusha pumzi kisha akasema "ana bahati sana yule".

"Nina bahati sana kwa kuweza kushika makalio yako sio, sasa nimeyashika tena ili nikujulishe kwamba bahati hiyo ni yangu tu" Sauti ya Zalabain ilisikika kwa mara ya pili na Mganga akahisi kushikwa makalio kwa mara nyingine tena safari hii alijiona kaingia katika mikono ya basha kwa jinsi alivyokuwa anatomaswa, mara hii hata Shafii alimshuhudia Zalabain akiwa yupo nyuma ya Mganga Sauti ya Radi akifanya udhalilishaji wake. Mganga alipogeuka nyuma akabiliane na Zalabain alipigwa kofi moja lenye uzito wa aina yake hadi shavu lake likachanika kabisa, Zalabain alipotea kwa mara ya pili na moshi mzito ukatanda kama ukungu ikifuatiwa na sauti ya Mganga akilia kama mtoto mdogo. Sauti ya mtu akipigwa vibao ndiyo iliyokuwa imetawala ndani ya nyumba hiyo ya Mganga kwa muda wa dakika kadhaa, ilipokuja kuisha moshi uliotanda ghafla uliondoka papo hapo na Zalabain akaonekana amesimama akiwa ameukanyaga mwili ya Mganga ambao haukuwa hata na dalili ya kuwa na uhai.

Alama za mikono zilionekana katika mwili wa Mganga zilizoweka kama mhuri karibu kila sehemu katika mwili wa Mganga huyo, Zalabain alikuwa kasimama akiwa na hasira tena akiwa anamtazama Shafii huku akihema kwa nguvu sana.

Shafii naye alijikuta akitokwa na upepo bila hata kutarajia na jasho lilikuwa likimvuja kama alikuwa amekaa jirani na moto mkali kwa muda mrefu, kila akitazama macho ya Zalabain yalivyo na hasira ndiyo alizidi kusota kwa kurudi nyuma hadi akafika ukutani kabisa akawa pa kwenda hana akabaki akimtazama Zalabain kwa uoga sana.

"Unafikiri unaweza kunizuia mimi kwa kutumia nguvu za huyu mzee?" Zalabain alimwambia Shafii huku akiukanyaga mwili wa Mganga Sauti ya Radi kwa nguvu hadi viungo vikawa vinavunjika na kuzidi kumtia uoga Shafii.

"Ujue kila mwizi na arobaini yake na siku ya arobaini yake ndiyo hukamatwa au kuuliwa, sasa wewe utabaki unapumua kwakuwa arobaini yako bado ila ikifika utakufa kifo cha huzuni kuliko hata hiki cha huyu" Zalabain aliongea huku akimtazama Shafii na akamaliza kauli kwa kuikanyaga shingo ya mganga hadi kichwa chake kikaruka upande aliopo Shafii na kupelekea yowe la uoga limtoke kwa uoga kutokana na kuogopa kichwa hicho kikiwa hakina uhai. Zalabain alipotea papo hapo baada ya kichwa kuruka upande aliopo Shafii na hapo ndipo akili ya kukimbia ilipomjia Shafii na akasimama na kuanza kukimbia bila hata kuangalia wala kuangalia mlango upo wapi, alijikuta akipigiza uso ukutani katika ukuta wa nyumba ya mganga baada ya kukimbilia ukutani akijua ni mlango ulipo kutokana na kuchanganyikiwa na balaa aliloliona.

"Oooow!" Aliachia ukelele wa maumivu kutokana na kuumia pua yake alipojibamiza ukutani hapo, Shafii alinyanyuka akawa anaona mawenge tu na asijue wapi mlango ulipo. Alipoamua kutimua tena mbio alikutana tena na ukuta ulimbamiza puani kisawasawa hadi zikaanza kumchuruzika damu puani, aliumia sana lakini alinyanyuka na kuanza kukimbia tena mbio akiwa amefumba macho kwa maumivu ya puani aliyonayo. Alifanikiwa kutoka nje na akatimua mbio moja kwa moja bila hata kuangalia mbele tena akiwa na mbio kuliko kawaida, laiti angeshindanishwa na mwanariadha Usain Bolt mwenye uwezo wa kukimbia mita 100 kwa sekunde tisa angekuwa mshindi yeye kwa jinsi alivyokuwa ana kasi ya ajabu kukimbia eneo ambalo alishuhudia mauzauza ya kifo cha Mganga wake wa toka siku nyingi.

Mbio za Shafii zote hakuwa ameangalia mbele na alikuja kufumbua macho na kurudiwa na akili zake za kawaida baada ya kuhisi amekumbwa kikumbo kikubwa na mtu mwenye mwili wenye ubavu kuliko yeye, alianguka chini moja kwa moja lakini alijiinua akiwa na wasiwasi sana moyoni mwake baada ya kumshuhudia mtu aliyechafuka kwa mchanga mweupe akiwa ameshika gunia.
"hivi we mzed una akili timamu kweli? Huoni kama ulikuwa unakimbilia mtoni tena kwenye Korongo ambalo chini kuna mamba wengi sana?" Yule mtu alimuuliza Shafii huku akimshangaa sana.

"hapa ni wapi?" Shafii naye alijikuta anamuuliza yule mtu.
"We mzee umechanganyikiwa nini hebu angalia kushoto kwako" Yule mtu alimuambia Shafii huku akimuonesha upande wa kushoto, Shafii alipogeuza macho upande wa kushoto aliona yupo mita takribani mbili kutoka mwisho wa Korongo refu ambalo chini yake mto Zigi unapita tena sehemu hiyo ya mto huo mkubwa Tanga nzima ulikuwa umejitanua sana na chini mamba walikuwa wanaonekana bila hata kificho wakiwa wapo pembeni.
"Hiii!" Shafii alisema kwa uoga akaanza kukimbia upande mwingine ili akae mbali na eneo hilo la korongo.

"Mzee wangu una matatizo sana, yaani isingekuwa mimi kukuona wakati naenda kuchimba mchanga mtoni basi ungekuwa kitoweo cha Mamba sasa hivi" Yule mtu alimuambia Shafii ambaye alikuwa ametulia tayari na akawa anamsikiliza.

"asante kijana, sasa utaendaje kuchimba mchanga mtoni wakati kuna mamba?" Shafii alimuuliza yule mtu kutokana na kushangazwa na mtu kwenda kuchimba kwenye mto huo wenye mamba wengi sana, yule mtu aliposikia swali la Shafii alimuonesha kamba nyeusi iliyofungwa begani mwake yenye hirizi pamoja na simbi kadhaa.

"hii ndiyo kinga yangu Mamba hanishiki ila kwa mgeni ukisogea hata pembeni umeisha, mzee umekumbwa na nini mbona una damu puani na usoni umechanika?" Yule mtu alimueleza Shafii kisha akamtazama kwa udadisi na akagundua ameumia, alimuuliza juu ya kilichomuumiza kwani alikuwa anavuja damu nyingi sana.

"Kijana ni habari nyingine kabisa usijali sana....asante sana hii ni zawadi yako ya kukomboa maisha yangu" Shafii aliongea kisha akatoa pochi yake mfukoni akamkabidhi noti kadhaa yule mtu halafu akamuaga akaondoka. Ilikuwa bahati kwa yule mtu kupata kitita kikubwa cha pesa kama hicho kwa kumuokoa mtu asiyemjua asiingie katika maskani ya mamba wengi wa mto Zigi ingawa kwa Shafii ilikuwa ni jambo dogo sana kutoa kitita kama hicho cha fedha kwani alikuwa ni tajiri sana. Shafii alirudi hadi alipoacha gari lake akaingia akamuamuru dereva aondoe gari kuelekea hospitali.

****

Muda ambao Shafii alikuwa anaona vibweka vya kuuliwa mganga wake aliyeanza kumtumia miaka mingi iliyopita, ndiyo muda huohuo mdogo wake aliwasili nyumbani kwa shemeji yake Shafii yaani kaka wa Bi Farida mke wa Shafii anayeitwa Hamis. Ally aliingia nyumbani kwa Hamis akiwa na huzuni kwa kuwapoteza kaka zake tena machozi yalikuwa yakitaka kumtoka kila akiwakumbuka kaka zake hao, alipokelewa na mfanyakazi wa ndani wa nyumba ya Hamis na akapelekwa hadi ukumbini ambapo alimkuta Hamis akiwa amekaa kwenye jamvi akinywa shurubati ya maembe.
"Ally vipi kwema?" Hamis alimuuliza Ally kutokana na hali ya huzuni aliyomuona nayo.

"si kwema shemeji" Ally alijibu na machozi yalianza kumtoka hapo hapo.
"heeh! Kunani hebu nieleze?" Hamis alimuuliza Ally.

"Kaka Hamid na Hussein hatunao" Ally akiongea na hapo machozi yakaanza kumtoka kama chemchem.
"Eti nini?" Hamis aliuliza kwa hasira na hapo akaanza kunguruma na mwili wake ukaanza kutetemeka kama kamwagiwa maji ya baridi, Ally alipoona hali hiyo aliacha kulia hapohapo akatoka mbio kufuata ukumbi mwembamba uliopo katika nyumba hiyo na alirejea akiwa ameshika udi unaowaka akamuwekea Hamis mbele yake jirani na pua zake.

"Kuna dhahama, kuna dhahama! Linataka kuikumba familia zetu nasema sikubali lazima nililizuie......nasema sikubali! Nasema sikubali! Nasema sikub...Aaaasrgh!" Hamis aliongea akionekana tayari ameshapandisha mashetani kichwani lakini alijikuta akikabwa shingoni hadi akashindwa kuongea akabaki akitoa ukelele wa maumivu huku akishika shingo yake hadi Ally akaanza kuogopa. Hamis alianza kukoroma huku macho yakiwa yamemtoka kwa namna ya kutisha, Ally alipoona hivyo alinyanyuka akataka kukimbia lakini mtama mzito ulimkuta na yeye akaanguka chini huku mpigaji akiwa hamuoni. Alipoanguka alipigwa kofi la nguvu la kwenye shavu akatulia chini kama maji mtungini, baada ya Ally kuanguka ndipo Hamis alipohisi kuachiwa tangu aanze kukabwa. Alikohoa mfululizo akamkimbilia Ally akamtikisa Ally lakini hakuonesha dalili ya kuamka, Hamis alipagawa kabisa hasa alimpotazama Ally aliyetulia tu.

"Sijatumwa kuua bali nimetumwa kuzuia, Hamis umerithi majini kutoka kwa babu yako lakini ukataka kuyatumia kupambana na usichokiweza sasa nimeyakaba nikayaua na wewe utakiona. Huyo mwenzako pia kapata aliyostahiki kwa kiherehere chake" Sauti ilisikika ikitokea juu ya dari ikawa inavuma kama mwangwi ikapotea.

"Hamidaa!" Hamis aliita kwa nguvu huku akimnyanyua Ally.
"Abee Baba!" Sauti ya kike iliitika ikitokea chumbani.
"leta funguo za gari upesi" Hamis aliongea akielekea mlangoni, binti wa miaka takribani kumi na nane alimfuata kwa nyuma akiwa na ufunguo wa gari. Hamis alienda kwenye gari lake na yule binti akafungua mlango wa gari Ally akawekwa, geti kubwa lilifumguliwa na Hamis akaingia ndani akawasha akaliondoa kwa kasi.

SURA YA NNE

Hali ya jiji la Dar es salaam ilikuwa tulivu na muda huo sehemu mbalimbali za jiji kulikuwa kuna watu wakiendelea na pilikapilika zao za kila siku, upande wa chuo kikuu cha Dates salaam wanafunzi walikuwa wakiendelea na masomo yao kama kawaida yao. Ilikuwa ni vipindi vya pili vya masomo baada ya vile vya asubuhi na wanafunzi wote wenye vipindi muda huo walikuwa wapo madarasani wakifundishwa.

Darasa la wanafunzi wanaosoma shahada ya sheria masomo yaliendelea kama kawaida na muda huo Professa wa chuo hicho alikuwa akifundisha darasani na wanafunzi walikuwa wapo makini sana kumsikiliza, katikati ya kipindi aliingia kaimu mkuu wa chuo darasani akiwa na mgeni ambaye hakufahamika ni nani hadi muda huo. Kaimu mkuu alimfuata Professa aliyekuwa anafundisha akamuuma sikio kwa sekunde kadhaa, Professa alimsikiliza kaimu mkuu wa chuo kisha akaafiki kwa kutikisa kichwa.

"Zaina Buruhan you are needed (Zaina Buruhan unahitajika)" Professa aliongea na wanafunzi wote wa humo darasani wakamtazama binti aliyenyanyuka katika viti vya katikati ya darasa.

"Take your things you are not return today, there is an emergence(Chukua vitu vyako hutarudi leo, kuna dharura)" Kaimu mkuu wa chuo aliongea na Zaina akachukua vitabu vyake akamfuata Kaimu mkuu wa chuo akiwa na yule mgeni kisha wakatoka nje.

Walipofika nje kaimu mkuu wa chuo alimtambulisha yule mgeni kwa Zaina na mgeni akaonesha kitambulisho chake akajieleza kwa Zaina dhumuni lake la kuja hapo chuoni.

"kuna dharura gani huko nyumbani?" Zaina alimuuliza yule mgeni
"nimetumwa tu kuja kukufuata mengine utayajulia huko huko nyumbani, Baba yako na mama yako wameniambia nisikueleze chochote" Yule mgeni alijibu, kwakuwa alikuwa ameshakamilisha taratibu zote za hapo chuoni Zaina na yule mgeni waliondoka kwa pamoja hadi kwenye gari la kifahari alilofika nalo yule mgeni wakaingia kwa pamoja na safari ikaaza, baada ya dakika thelathini walifika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere wakashuka wakaingia ndani ya majengo ya ndani ya uwanja sehemu ya ndege binafsi. Walipanda kwenye ndege ndogo ya kisasa ambayo ilikuwa ikiwasubiri wao na wakafunga mikanda, milango ya ndege ilipofungwa ndege ilianza kutembea taratibu ikielekea kwenye njia za kurukia na hatimaye ikaiacha ardhi ya jiji la Dar es salaam.

Baada ya dakika ishirini ndege hiyo ilianza kuinama kwa mbele kisha ikashuka chini taratibu, baada ya muda ndege hiyo iligusa ardhi kisha ikasimama papo bila kutembea ardhini kama ilivyozoeleka ndege ikigusa ardhi lazima itembee mitaa kadhaa ndiyo isimame.

"mbona ikitua hii ndege haitembei kama ndege zingine" Zaina alimuuliza yule mfanyakazi wa baba yake aliyemfuata chuoni.
"hii ni tofauti na ndege unazozijua, unaweza ukashuka sasa" Yule mgeni aliongea, Zaina alisogea mlangoni akafunguliwa na akakutana na ngazi ya kushuka kwenye ndege zenye rangi ya dhahabu tofauti na zile alizotumia kupanda. Aliposhuka chini kabisa alikutana na mandhari tofauti na ya uwanja wa ndege wa Majani mapana wa jijini Tanga, anga la eneo hilo lilikuwa jekundu kupitiliza na lisilo na wingu hata. Mbele yake kulikuwa kuna kasri kubwa la kifahari lililotandazwa zulia jekundu kuanzia mlangoni hadi pale aliposimama, alipogeuka nyuma kuangalia ndege aliyoitumia ndipo aliposhtuka zaidi baada ya kubaini hakuwa amepanda ndege bali alikuwa yupo kwenye joka kubwa lenye miguu na masharubu kwenye mdomo na mgongoni alikuwa na kitu kama behewa la treni lilipambwa kwa vito mbalimbali na lilikuwa na ngazi ya dhahabu ambayo ndiyo ile aliyoshuka wakati anatoka. Hadi kufika eneo hilo kumbe alikuwa amempanda mnyama anayejulikana kama dragon bila kutambua akijua ni ndege, alipoona yupo katika mazingira asiyoyaelewa aliachia ukelele wa uoga na kupelekea eneo zima pembeni ya zulia kuanzia kwenye ngazi alizoshukia hadi kwenye mlango wa kaari kuonekane kuna viumbe wenye sura za binadamu wakiwa wamekaa mstari mmoja.

"We mwanadamu hebu wacha kelele" Sauti ya yule mtu aliyemchukua chuoni ndiyo ilisikika ikitokea kisha yule aliyemdhania ametumwa na baba yake akatoka ndani ya behewa lililopo mgongoni mwa dragon akiwa ana mavazi sawa na viumbe waliojipakaza mstari.
"hapa ni wapi na wewe ni nani?" Zaina aliuliza kwa uoga.

"sina mamlaka ya kujibu maswali yako msubiri mwenye mamlaka akujibu maswali yako" Aliongea kisha akashuka akapiga hatua kumsogelea Zaina halafu akamwambia "angalia kule mlangoni kama ukijijua wewe ni mgeni, mkuu wa eneo hili mjukuu wa mfalme anaingia".

Alipomuambia hivyo alipiga goti la kiheshima na viumbe wote nao walipiga goti na mlio kama wa tarumbeta ulisikika na milango ya kwenye kasri ikafunguka, Zalabain alionekana akija hadi pale alipo Zaina huku akitabasamu akiwa na umbile lake la kibinadamu.
"Karibu sana Zaina nadhani majibu ya maswali yako yote utayapata" Zalabain aliongea akitabasamu.
"Wewe ni nani na hapa ni wapi?" Zaina aliuliza akiwa na hofu.

"Naitwa Zalabain mjukuu wa mfalme na hapa ni ndani ya makao ya himaya ya Majichungu" Zalabain alieleza
"Majichungu?! Ni wapi?" Zaina aliuliza kwa wasiwasi ingawa tabasamu la Zalabain lilimuonesha kwamba hakuna hofu yoyote.
"chini ya bahari" Zalabain alijibu.

"unasema?" Zain aliuliza akiwa na mshtuko kisha akaanza kurudi nyima kwa uoga. "Haina haja ya kurudia mara mbili Zaina utanijua zaidi ila inabidi ukae huku kwa ajili ya usalama wako tu na pia kwa ajili ya tahadhari, hutakiwi kuingizwa kwenye mtego wa panya bila kujijua wakati huna hatia, Hallain!" Zalabain alimueleza Zaina kisha akaita kwa sauti na kupelekea viumbe wengine wenye sura za wanawake warembo wenye asili ya bara la Asia wajitokeze mbele ya Zalabain.

"Kiongozi wetu tumeitika wito wako" Viumbe hao waliongea kwa utiifu wakiwa wamepiga goti moja kiheshima.
"Mchukueni huyu mmoja wa wanadamu wenye heshima huku kwetu.......Zayina utakaa hapa na usijaribu kuleta ubishi upate matatizo huku binadamu wanachukiwa kwani wao ndiyo chanzo cha kuwa na wingu jekundu kila muda humu kwenye himaya na mwanga wenye nuru haufiki kutokana na kuibiwa kito Dainun cha baba yangu Zaif" Zalabain aliongea na wale viumbe wakamchukua Zaina wakatoweka naye. Baada ya Zaina kuchukuliwa Zalabain aliingia ndani ya kasri akiwa ameongozana na yule kiumbe aliyemleta Zaina hadi katika chumba cha siri cha ndani ya Kasri hilo, huko ndani ya chumba hicho walikutana na Salmin akiwa amekaa kwenye kiti kimojawapo kilichonakshiwa na mapambo ya lulu. Zalabain na yule kiumbe waliketi kwenye viti vya aina hiyohiyo wakawa wanamtazama Salmin.

"je mmefanikiwa kuipata Dainun?" Salmin alimuuliza Zalabain
"hapana bado sijafanikiwa kuipata kwani kila anayetakiwa aende na maji nikimuuliza anasema hana" Zalabain alimueleza.
"Inabidi uipate hiyo ndiyo taji la kifalme litakaa kichwani mwako hata kama ukilipa visasi hadi ukamaliza bila ile hutakuwa mfalme na hata ukiipata hujalipa kisasi bado taji litakukataa vilevile" Salmin alimuambia Zalabain.

"Sawa nimekuelewa, enhe wewe Kainun niambie kazi niliyokuagiza imeendaje" Zalabain alimuuliza yule kiumbe aliyemchukua Zaina.
"Mtukufu mjukuu wa mfalme na mfalme wetu mtarajiwa kazi imeenda kama ulivyoniagiza kwa kumzuia yule mwanadamu anayeitwa Hamisi aliyepandisha vijini vyake akataka kuingilia kazi yako ya kurudisha nuru iliyopetea katika himaya yetu" Kainun alitoa maelezo kwa Zalabain.
"Vizuri kama umemzuia, je niambie ulimzuia vipi?" Zalabain alimpongeza kisha akahitaji kujua aliyoitumia kumzuia Hamisi asiingilie kazi yake.
"Baada ya yeye kuwapandisha majini wake kwenye kichwa chake niliamua kumkaba shingo yake hadi yakafa yote kisha nikampiga kofi moja yule mwenzake aliyetaka kuchochea kuharibika kwa kazi yako kwa kuleta udi unaowaka" Kainun alieleza kila kitu alichokifanya hadi Zalabain akatabasamu huku akitikisa kichwa kuashiria amependezwa na kazi yake.

"Vizuri sana kwa kumtandika kibao huyo Ally Buruhan maana anafuata mkumbo tu" Zalabain aliongea.
"Kainun napenda asipewe kazi nyingine hadi hali itulie maana majini aliowanyonga ni watoto wa mganga Sharkar aliyeuawa na kaka yangu Saliim miaka mia moja na ushee kupita baada ya kristo kuondoka, kwa mujibu wa maono yangu hao vifo hivyo tayari vishagundulika kwa ukoo wa Sharkar sasa huyu kumuachia kazi nyingine itakayomlazimu kutoka nje ya himaya hii ni sawa na kumkaribisha na vita na kifo chake" Salmin aliongea baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu tena macho yake yakibadilika rangi yakawa yanawaka kama ya paka, Zalabain aliposikia maelezo hayo akatulia akajifikiria kwani hakuwa na mwingine mwenye kuaminika na kutumwa katika kazi zake miongoni mwa majini wote wa himaya hiyo isipokuwa Kainun na ndiyo huyu ameambiwa asimtumie na jini mwenye nguvu zaidi na mwenye kuona yajayo. Himaya hiyo kuna baadhi ya watumishi walikuwa sio wa kuaminika kutokana na kuwa miongoni mwa wafuasi wa waziri kkuu aliyetaka kupata ufalme kwa hila sana, alipoambiwa asimtumie Kainun kwake lilikuwa ni jambo jingine gumu kwake.

"Hapo unanipa wakati mgumu sasa, watumishi hawa sio wa kuaminika huenda kuna wengine ni wafuasi wa aliyekuwa waziri mkuu aliyefungwa katika gereza la giza. Sina wa kuaminika atakayekuwa akisaidia kuzuia kazi yangu isiharibike zaidi ya huyu tu" Zalabain aliongea.
"Usisononeke Zalabain nadhani yupo jini mwingine mwenye msaada mkubwa kwako kama Kainun na naamini atakufaa kuzuia watu na viumbe wasiohusika wasiharibu kazi yako" Salmin alimuambia Zalabain kwa utulivu.

"unafikiri nani atakayeweza kuwa mbadala wa Kainun?" Zalabain aliuliza.
"Baada ya mimi na pacha wangu Saluim kuzaliwa katika kasri la mfalme Mukhatar wa bara Arabu kuna jini mmoja alinieleza kuhusu asili na chanzo cha kufanya mambo yasiyofanywa na binadamu wa kawaida. Jini huyu alinieleza kuhusu asili yangu mimi ni jini na niliyezaliwa na mwanamke wa kibinadamu ila baba yangu ni jini huyu Ibin Zultash na sio mfalme Mukhtar kama nilivyoelezwa wakati nikiwa mdogo na mama yangu ambaye alikuwa Malkia wa himaya baada kifo cha mfalme Mukhtar. Jini huyu ndiye aliyemuelekeza kaka yangu akaenda kwa mganga wa kijini Sharkar akaongezewe nguvu, baada ya kaka yangu kuongezewa nguvu alikosea sharti akanywa damu aliyoambiwa asinywe na hapo akawa muangamizi akaangamiza himaya ya mama yetu na akataka kumuangamiza huyu jini ambaye aliamua kujisalimisha nyumbani kwao ambapo ndiyo hapa Majichungu.

Nilipopambana na kaka yangu kwa msaada ya mganga Zaid wa bara Arabu nilifanikiwa kumshinda kaka yangu na nikamfungia kwenye sanduku nikaja kulifukia h Afrika kipindi hicho ni pori tu kwani ilikuwa imepita miaka 100 tu tangu Kristo aondoke duniani, baada ya kazi hiyo niliwachukua Zaid na mama yangu tukaja kuishi huku na tukapokelewa na babu yako kipindi hicho bado ni kjana mdogo wa miaka arobaini hivi. Jini huyo alipokuja huku akifungiwa katika gereza la giza na hakuwahi kutoka hadi leo hii ninavyokusimulia habari hii, huyo ndiyo jini pekee kwa mujibu wa maono yangu anaweza akakaimu nafasi ya Kainun" Salmin alisimulia kisa cha MUANGAMIZI kisha akamtajia jini mwingine mwenye kuaminika.


"je naweza kulijua jina lake huyo kiumbe?" Zalabain aliuliza.
"usiseme unaweza bali ni wajibu wako kumjua anaitwa Maalun nadhani ukimpa uhuru atakaimu nafasi ya Kainun... Kainun utaendelea kuwa mkuu wa majeshi ya angani kama ilivyokuwa awali" Salmin aliongea kisha akamtazama Zalabain usoni, Zalabain alipotazamwa hivyo alipiga kofi mara na viumbe wa ajabu wakatokea mbele yake wakiwa na mavazi yanayofanana.

"Ndiyo mtukufu tumeitikia wito wako" Wale viumbe waliongea kwa utiifu wakipiga goti moja mbele ya Zalabain.
"nahitaji nimuone Maalun hapa akiwa ametolewa gereza la giza ndani ya sekunde tatu tu" Zalabain aliongea na wale viumbe walipotea kisha wakarejea wakiwa wamemkamata Maalun aliyeonekana kuwa mnyonge sana.

"muwekeni kwenye kiti na nyinyi muondoke haraka sana" Zalabain na wake viumbe wakakuweka Maalun kwenye kiti wakapotea.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Maalun kuwa huru baada ya kufungea gerezani kwa muda wa miaka takribani 2000 kutokana kuisaliti himaya hiyo na kwenda kuishi kwenye ardhi ya wanadamu, alipoona wale majini waliomleta wamepotea alianza kuwatazama wote waliobaki ambapo hakumtambua Zalabain wala Kainun. Yeye alimtambua Salmin tu na hapo akamuangukia miguuni akaanza kuonesha kuomba msamaha.
"Maalun yaliyopita na pia kuongelewa kwake kumepita, kosa ulilotenda milenia mbili zilizopita nishakusamehe cha msingi inabidi tuangalie liliopo hapa" Salmin aliongea na wote wakaafiki kwa kichwa, kauli hiyo ilimfanya Maalun atabasamu na apotee ghafla alipokuwa ameamuangukia na akatokea kwenye kiti kimojawapo kilichopo hapo walipo wenzake.

"Oooh! Namshukuru mungu kumbe nguvu bado zipo, haya nawasikiliza" Maalun aliongea huku akiwatazama wenzake kwa zamu kisha macho yake yakaweka kituo kwa Zalabain halafu akamwambia " nakusikiliza ewe mtukufu"
Zalabain alianza kumueleza Maalun kila kitu hadi majukumu aliyotakiwa kuyafanya, maelezo yalipofikia mwisho wote walimtazama Maalun wakisubiri kusikia uamuzi wake.

"Kwa ajili ya kuokoa himaya hii isiteketee kwa kukosa mfalme anayestahiki nipo tayari kwa kazi yako ewe mtukufu na hata ungeniambia nikusaidie kuwaangamiza nipo tayari" Maalun alikubali na wote wakatabasamu.
"vizuri Maalun na anza kazi yako kuanzia sasa, yeyote atakayeingilia kazi ya mfalme mtarajiwa wewe mzuie ashindwe kuendelea kabisa na si kuua maana utamuharibia kazi Mfalme wetu mtarajiwa" Salmin aliongezea kisha akasimama akapotea na wote waliosalia wakatoka ndani ya chumba cha siri.

****

Upande wa ardhi ya binadamu kwa muda huo ndiyo muda ambao Shafii alifanikiwa kufika katika hospitali yake akapewa tiba ya majeraha yaliyompata na kushonwa usoni alipopasuka kutokana na kujigonga alipoona tukio la Mganga Sauti ya Radi akiuawa na Zalabain, alipomaliza kutibiwa ndipo alipopokea taarifa ya kulazwa kwa mdogo wake katika hospitali hiyohiyo upande wa wagonjwa mahututi. Taarifa hiyo ilimfanya atoke sehemu aliyokuwa anatibiwa baada ya kumaliza tu kushonwa vidonda vyake akaelekea mahali zilipo wodi za wagonjwa mahututi wa hospitali hiyo iliyopo chini ya kampuni yake, alipokaribia katika mlango wa chumba cha wagonjwa mahututi alimuona Hamisi akiwa amekaa kwenye dawati la kusubiria wagonjwa akiwa amejiinamia. Shafii alimfuata upesi kisha akamuuliza. "Shemeji kuna nini kimemkuta Ally" Shafuu aliuliza huku akimtazama Hamisi ambaye naye aliishia kumshangaa kutokana na plasta alizonazo usoni pamoja na michubuko kadhaa.

"Aisee! Shemeji we acha tu. Hii ni vita kali na Ally amekumbwa na kadhia ya kupigwa na kiumbe kisichoonekana na mimi majini yangu yote yameuawa " Hamisi aliongea kwa masononeko.

"Vipi hali yake ipoje huko wodini?% Shafii aliuliza.
"bado madakatari wanafanya kazi yao, na wewe vipi mbona maplasta mengi usoni? Umepata ajali? Hamisi alimuekeza Shafii kisha akamuuliza kilichomsibu hadi akawa na plasta nyingi usoni.

"Yaani shemeji ni bora ingekuwa ajali ingekuwa afadhali kuhusu kisanga kilichonikuta huko kwa Sauti ya Radi, yeye mwenyewe ni mfu hadi muda huu" Shafii aliongea akioneksna anakaribia kukata tamaa kabisa
"hivi huyu anayeiangamiza familia yangu nimemfanya nini? Au uadui wa kibiashara, yaani Ally mdogo wangu hata kuoa hajaoa ndiyo kwanza anajijenga kimaisha yeye aje kumfanyia hivi kweli. Sikubali hata kidogo nitapambana kulipa kisasi cha hawa wadogo zangu" Shafii aliongea huku machozi yakimtoka kwa uchungu alionao.

"Shemeji nafikiri hii vita tutakuwa wote katika kukomboa familia zetu, waite Hassan, Yusuf na Halid waje watuongezee nguvu" Hamisi alimuambia Shafii, muda huohuo mlango wa wodi ulifunguliwa na daktari akatoka akiwa anaelekea ofisini kwake. Wote walipomuona walimkimbilia wakawa wanamuuliza ju ya hali ya Ally lakini dakari aliwasihi waende naye ofisi, wote walitii wakaelekea hadi katika ofisi ya Daktari huyo na walipofika wakaribishwa katika viti. Shafii na Hamis walikaa wakawa wanaamuangalia Daktari ili wapewe raarifa za Ally kimatibabu.

"Mgonjwa anaendelea vizuri kwa sasa ingawa bado hajarejewa na fahamu, tatizo kubwa alilolipata mgonjwa wenu ni kuvunjika kwa taya yake kwani inanekana alipigwa na kitu kizito shavuni na kupelekea damu zivuje sikioni pia ikionekana hata sikio lake limepatwa ingawa bado haijathibishwa na E.N.T surgery wa hapa hospitali. Kwa sasa tumempatia matibabu kwa ajili ya taya lake na baadaye mtaalam wa E.N.T atakuja kucheki sikio lake. Ni hayo tu bosi" Daktari aliongea kwa kirefu juu ya tatizo lililomkuta Ally, maelezo hayo yalimsikitisha sana Shafii na akajikuta anapandwa na hasira zaidi hadi machozi yakawa na yanamtoka.

"Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Na bado tu huo ni mwanzo tu ila kwa sasa naomba utambue binti yako wa pekee yupo katika himaya yangu" Mwangwi wa sauti ya Zalabain ulivuma katika masikio ya Shafii na kumfanya ashtuke sana hadi Hamisi na Daktari wakamshangaa.

"shemeji kuna nini?" Hamisi alimuuliza Shafii baada ya kumuona alivyoshtuka na sasa alikuwa anaangalia dari la ofisi hiyo ya Daktari kama ndiyo kwanza analiona kutokana na sauti hiyo iliyomjia masikioni mwake ikitokea huko darini.

"Ohoo! Zaina, Zaina mwanangu" Shafii aliropoka kisha akatoka mbio huko ofisini kwa daktari hadi Hamisi naye ustahimilivu ukamshinda ikabidi amkimbize shemeji yake, Daktari naye alijitahidi kukimbia kwa uwezo wake wote ili amuwahi Shafii. Wote kwa pamoja mbio zao hazikuzaa matunda katika kumkamata Shafii aliyeonekana amechanganyikiwa kwani aliingia kwenye gari yake aina ya Cadillac akaiwasha bila hata kumuambia dereva wake aliyekuwa yupo pembeni katika mti akiwa amepumzika, Shafii aliwaachia vumbi tu kwa mwendo bao aliondoka nao kama jambazi anayefukuzwa na polisi baada ya kupora benki.

"Beka daka ufunguo huo tumuwahi huyo asipatwe na matatizo" Hamisi alimwambia dereva wa Shafii kisha akamrushia funguo za gari halafu akakimbia kuelekea lilipo gari lake, Beka naye alimfuata akaingia upande wa dereva akawasha gari, Hamisi naye alishaingia kiti cha pembeni ya derwva akafunga mkanda.

Gari ya Hamisi nayo iliondoka kwa mwendo uleule alioondoka nao Shafii kuingia barabarani, baada ya kukimbiza gari sana waliona moshi mwingi ukiwa umetanda katika reli zilizopo katika njia iendayo Makorora tena kichwa cha treni kikiwa kimesimama mita kadhaa kutoka eneo la lenye moshi mzito. Barabara nzima ilikuwa imefungwa na kundi hilo na ikawalizimu Hamisi na Beka wasimamishe gari lao wafunge milango vizuri waende kuangalja kuna nini kimetokea, waliposogea karibu zaidi ndipo walipoliona Cadillac la Shafii likiwa lipo matairi na wananchi walikuwa wakimtoa Shafii ndani ya gari hiyo baada ya kufanikiwa kuvunja kioo. Hawakutaka kupoteza muda nao walijichanganya katika kundi hilo la watu wakafanikiwa kufika mbele wakamtoa Shafii ndani ya gari hilo ambaye alikuwa hajitambui, walimpakiza kwenye gari wakishirikiana na wasamaria wema wakampeleka wakamkimbiza hospitali kwani alionekana bado anapumua.

****

Zaina alipelekwa kwenye chumba ambacho kilikuwa kina hadhi kubwa kuliko hata chumba alichokuwa akikitumia kule nyumbani kwao, alikuwa akipewa kila huduma aliyokuwa ya muhimu kwa wanadamu kutoka kwa vijakazi wa kasri la kifalme hadi akajihisi yupo ndani ya sehemu salama. Zilipita siku mbili akiwa ni mtu wa kukaa ndani na hana popote pa kwenda zaidi ya kukaa humo, hali hio ilianza kumchosha tu ndani ya siku hizo mbili tu kutokana na mazoea kutokaa ndani aliyokuwa nayo. Siku ya tatu ilipoingia alianza kulalamika kwa kufanywa mateka kwa watumishi hao waliomletea chakula, onyo alilopewa na Zalabain alilipuuzia na akawa anawatolea maneno mabovu vijakazi hao.

"Kelele wewe mwanadamu la sihivyo nitakiponda kichwa chako kwa ngumi moja tu ukasalimiane mababu zako waliotangulia" Sauti ya ukali ilisikika na kisha Kainun akatokea akiwa na hasira baada ya kusikia maneno ya Zaina.

"nirudisheni kwetu hamtaki!" Zain alizidi kuongea kwa ukali kama anaongea na binadamu wa kawaida.
"unasemaje wewe sasa nakutoa utumbo huku unajiona maana nyinyi wanadamu ndiyo chanzo cha matatizo kwenye himaya hii yote yaani nuru hatuijui tangu Mfalme wetu alipokufa kwa ajili ya ubaya wenu mlioufanya" Kainun aliongea kwa hasira akawa anamfuara Zaina kama Mbogo aliyejeruhiwa na sasa hivi akageuka na kuwa umbo la kutisha. Kuonekana kwa Kainun akiwa na umbile lake la kijini kulimfanya Zaina apatwe na mshtuko na azirai hapohapo, Zalabain naye alitokea hapohapo akiwa na hasira kupitiliza hadi macho yakawa mekundu. Alimpiga pigo la nguvu Kainun hadi akaenda chini kama gunia la udongo ulaya, alimuinua Kainun akamkunja akamuinua akamtazama usoni kwa hasira sana.
"unataka kufanya nini wewe?!" Zalabain alimuuliza halafu akampiga kichwa kizito.

"Ewe mtukufu hakika unatambua sisi tunavyowachukia binadamu kwa kutusababisha tusiwe na nuru, binti huyu wa kibinadamu ameanza kutoa maneno machafu katika kasri hili takatifu" Kainun aliongea kwa ghadhabu zaidi.

"hata kama afanye hivi unamjua ni nani huyu na kwanini nimempa hadhi sawa na familia ya kifalme?" Zalabain aliongea kwa hasira hadi mdomo wake ukawa unatoa cheche akamsukuma Kainun akaanguka chini.

"Mtukufu huyu si binti wa yule mmoja wa wabaya wako tu" Kainun aliongea akiwa amekaa kitako chini.
"Hata kama ni mtoto mtoto wa mbaya wangu lakini elewa mama yake ni mama yangu ila baba yake si baba yangu, huyu ni dada yangu mdogo Kainun. Unafikiri ukimuua nitakuacha wewe ukiwa hai" Zalabain aliongea kwa hasira zaidi hadi akawa anatetemeka, Kainun aliposikia hivyo alibaini kama ametenda kosa akaomba radhi hapohapo akiwa amepiga magoti.
"Inuka uende na usitie mguu chumba hichi ushamtisha Zaina" Zalabain alimuambia Kainun ambaye aliinuka na kuondoka.

***

SIKU ILIYOFUATA

Ndani ya nyumba mbovu yenye vumbi pamoja na samani za kizamani katikati ya jiji la Tanga, ndani ya nyumba hiyo Shafii alionekana akiwa amezungukwa na mke wake, mtoto wake na baba yake mzazi wakiwa wanamtazama kwa chuki huku yeye akionesha uso wa majuto akiwa amesimamia magongo mafupi kutokana na kushindwa kutembea.

"naomba kuanzia leo usiniite baba yako na mimi nasema sikuwahi na mtoto kama wewe!" Mzee Buruhan aliongea kwa hasira huku akimtazama Shafii ambaye alikuwa analia kama mtoto akiomba msamaha.
"Mke wangu, mwanangu nisameheni ili baba naye anisamehe" Shafii alipiga hadi magoti ingawa alikuwa anasikia maumivu kutokana na kutopona vizuri mguu.

"Baba yangu aliyepelekea uzao wangu hawezi akafanya hivi, nina wasiwasi nilikuwa nakuita baba kimakosa tu. Sina baba mshirikina na katili kama wewe" Zaina naye alitia msumari wa moto kwenye kidonda cha Shafii kwa maneno aliyoyaongea.

"We! We! We! Tena komaeh! Usiniite mkeo mimi, nafikiri nilioana na wewe kwasababu uliniloga lakini sikuridhia hivyo mimi siyo mkeo" Bi Farida aliongea kisha akamsindikiza na singi Shafii hadi akadondoka.

"Tena umuombe msamaha huyo hapo na siyo sisi" Mzee Buruhan aliongea huku akioneaha kidole kwenye mlango mkubwa wa kuingia ndani ya nyumba hiyo mbovu ya kizamani, Mtu mwenye joho jeusi alionekana akiingia akjwa ameahika sururu lenye mpini mweupe. Mtu huyo alipomkaribia Shafii, Mzee Buruhan, Bi Farida na Zaina walitoka nje wakimuacha Shafii na huyo mti aliyeingia.

"We shetani unakufa" Yule mtu alimuambia Shafii halaf akampiga sururu la kichwa kwa nguvu.
"Aaaaaaaaaaaargh!" Shafii aliachia ukelele wa maumivu lakini alipoangaza macho yake alijikuta yupo sehemu yenye kitanda cheupe na shuka jeupe, alipoona mazingira hayo alizidi kupiga kelele kwa nguvu akidhani labda yupo kuzimu.
"jamani atajitoa dripu yule, muwahini na sindano ya usingizi kabla hajajitonesha na ile shingo yake iliyovunjika" Ilisikika sauti ya kike ikitokea kushoto kwake.

Ilikuwa ni sauti ya muuguzi wa kike baada ya kuona dalili za purukushani anayotaka kuileta Shafii baada ya kuzinduka kutokana na ndoto mbaya aliyokuwa anaiota, mandhari ya eneo alilokuwepo ndiyo ilizidi kumchanganya kabisa akajiona ndiyo kama anaandaliwa kwa ajili ya kupigwa sururu na yule mtu aliyemuota ndotoni. Wauguzi waliokuwa wapo ndani ya wodi aliyolazwa walimuwahi kwa sindano ya usingizi ili asije kusababisha madhara mengine zaidi kwa mwili wake. Hadi muda huo tayari mwili wake ulishapata madhara mengi kutokana na ajali ya gari na laiti kama angecheleweshwa basi ingekuwa ni mengine, Shafii tayari alikuwa kashavunjika shingo.na kiuno katika ajali ya gari aliyoipata kutokana na kuchanganyikiwa baada ya sauti kusikika akilini mwake ikimwambia mwanae kipenzi tayari yupo ndani ya mikono ya mtu asiyemjua tena mwenye nia mbaya na yeye.

****

RASKAZONE
TANGA

Siku iliyofuata katika jiji la Tanga ilikuwa ni siku nyingine iliyobeba tukio la ajabu jingine ambalo lilistahiki kuingia katika matukio ya ajabu yaliyowahi kutokea nchini Tanzania, ilikuwa ni siku ya pili imepita baada ya kutokea tukio la kuungua zile nyumba za kampuni Hamid kule Duga maforoni. Majira ya saa nne asubuhi wafanyakazi wa kampuni ya mafuta ya Matro ambao hawakumalizia kazi zao kutokana na tukio lililotokea hapo ofisini kwao la kuuawa kwa mmiliki wa kampuni hiyo walihitajika kufika mapema kumalizia viporo vya kazi yao ili waweze kwenda mapumzikoni kutokana na kifo cha mmiliki wa kampuni hiyo, ilipotimu saa tano asubuhi wafanyakazi wote walikuwa kwenye ukumbi wa mkutano wakimsikiliza msemaji wa kampuni hiyo baada ya kumaliza viporo vya kazi vilivyosalia siku iliyopita.

"Natumai wote ni wazima wa afya na mpo hapa kusikiliza jambo nililowaitia, kikubwa kilichonifanya niwaite hapa ni juu ya kutokea kwa msiba wa bosi wetu kipenzi na wote mnalitambua hili. Sasa basi kwa taarifa zilizonifikia ni kwamba kumetokea vifo viwili ndani ya siku moja ambacho kimoja ni cha bosi wetu kipenzi na kingine ni cha kaka yake mmiliki wa kampuni ya Extoplus nadhani wote mnamfahamu. Hivyo misiba hii yote miwili itafanyika nyumbani kwa baba yao mzazi mzee Buruhan maeneo ya Sahare jijini hapahapa, ikiwa sisi ni miongoni mwa wafanyakazi wake tuliyempenda inabidi wote twende tukamfariji mjane wa marehemu pamoja na familia nzima ya mzee Buruhan. Hakika sisi ni wa....."

Msemaji mkuu wa kampuni ya Matro alitoa maelezo kwa wafanyakazi wa kampuni aliyoyapata ambayo hayakuwa yamefika kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo, alipokuwa anataka kuhitisha maelezo hayo alisikia mlango mmojawapo wa chumba cha mkutano ambao hautumiki ukifunguliwa kwa nguvu na ikaonekana aliyefungua ni mtu mwenye ubavu mkubwa kwa jinsi ulivyotoa kishindo hadi kitasa chake kikaanguka papo hapo. Macho ya kila mmoja aliyepo eneo hilo yalielekea kwenye mlango huo na hapo ndipo wakapigwa na butwa baada ya kumuona mtoto mdogo wa kike mwenye takribani miaka sita akiingia huku kabeba mdoli mdogo mwenye umbo la dubu mweupe, macho ya baadhi ya wafanyakazi yalionesha kumtambua huyo mtoto ila baadhi hawakumtambua hata kidogo. Mtoto huyo wa kike mzuri alizidi kumfanya Msemaji mkuu wa kampuni hiyo apagawe zaidi, mtoto huyo alipiga hatua hadi alipo Msemaji mkuu wa kampuni hiyo kisha akamuangalia usoni huku akitabasamu.

"Annet mwanangu umekuja na nani?" Msemaji mkuu alijikuta akiuliza huku akiwa ameduwaa na hata wengine waliduwa kwa jinsi mlango aliopitia huyo mtoto ulipotoa kishindo kizito sana hadi kitasa chake kikaanguka.

"nimekuja mwenyewe baba" Mtoto huyo anayeitwa Annet alijibu kwa lafudhi ya kitoto ambayo ilisikika na kila mmoja humo katika chumba cha mkutano.
Msemaji wa kampuni aliposikia hilo jibu la mtoto wake alichuchumaa chini akamshika mashavu huku akitabasamu kwa ishara ya upendo wote anaotakiwa kuuonesha baba kwa mtoto wake kisha akamuuliza, "ni nani aliyeufungua mlango kwa nguvu hadi kitasa kikaharibika?"
"Mimi hapa nimeugusa tu kwa mkono mmoja nikausukuma ukafunguka" Annet alijibu na akazidi kuwashangaza watu waliomo humo ndani hadi Msemaji mkuu wa kampuni naye akazidi kushangaa majibu anayoyatoa binti yake huyo mdogo.

"Samahani kwa kuwavamia mkutano wenu na kuwakatisha, nimetumwa tu kuwaeleza ujumbe niliopewa ambao unawahusu nyinyi na ujumbe hamtakaa kuusambaza wala kusimulia kwa wengine kwani mlipewa nafasi mkaichezea. Ni hivi siku iliyopita baada ya kufa kwa bosi wenu nyinyi mlipoondoka hapa kwenye kampuni hii ilikuwa ndiyo salama yenu ila kwakuwa mmerudi, nimeambiwa niwaambie kuwa hili ndiyo kaburi lenu" Annet aliongea kwa sauti nzito tofauti na ile ya kitoto aliyokuwa anaongea tena akatoa maneno yaliyozidi kuwachanganya.

"We Annet unasemaj..?" Msemaji wa kampuni hiyo alishindwa kumalizia kauli yake baada ya Annet kupotea katika mazingira yasiyo ya kawaida, jengo zima lilianza kutingishika kama limekumbwa na tetemeko la ardhi vioo vya madirisha vikaanza kuvunjika na kuzidi kuwatia wafanyakazi wote hofu. Wafanyakazi walipojaribu kukimbilia mlangoni ili watoke walikuta milango ikiwa imejifunga, mtetemeko wa jengo hili ulizidi kuwatia hofu na wakajikuta wakitaja jina la muumba kwa mara ya kwanza baada ya kutaja majina ya mama zao kwa muda mrefu.

****

LAS VEGAS
MAREKANI

Wakati wafanyakazi wa kampuni ya Matro wakikumbana na janga lililotokea hapo kwenye makao makuu ya kampuni hiyo, upande mwingine wa bara la Amerika ya kaskazini katika mji wa Las Vegas nchini Marekani majira ya saa nne usiku kwa masaa ya huko ambapo yapo masaa kumi nyuma ya Tanzania. Kijana mwenye mavazi ya anasa zaidi alionekana akiingia ndani ya klabu maarufu ya usiku ya jijini humo, Falzal ndiyo jina lake huyu kijana mwenye kila aina ya majigambo na mwenye jeuri ya kuchezea pesa katika starehe. Ingawa bado ni kijana msomi na aliyekuja nchini humo kwa ajili ya masomo, aliishi mithili ya mtu maarufu wa jijini humo.

Alipoingia ndani ya klabu hiyo ilikuwa kama kawaida yake lazima aende kwenye meza ya wacheza kamari kama kawaida, hiyo ndiyo ilikuwa starehe yake nyingine ambayo ilimuingizia pesa nyingi na kumfanya aishi maisha ya kifahari sana jijini humo. Aliwasalimu watu anaocheza naoo kamari kila siku akiwemo Miliver mcheza kamari maarufu hapo La vegas kisha akaketi, alimuangalia Miliver akatabasamu kisha akasema, " naona leo umekuja kunikuzia mtaji kama kawaida yako"

"Ha! Ha! Ha! Leo unaliwa wewe ngoja utaona tu"Miliver aliongea huku akicheka.
Faiz alipotaka kuchukua kete alishtushwa na mlio wa simu kutoka kwenye suruali yake na ikamlazimu awaombe radhi wachezaji kamari wenzake halafu akasogea pembeni sehemu isiyo na sauti nyingi na akaipokea simu.

"Baba vipi mbona usiku hivi?" Falzal aliongea baada tu ya kumsalima aliyekuwa anaongea naye kwenye simu.
"kuna tatizo gani baba mpaka nirudi nyumbani si uniambie tu nielewe hapahapa"Falzal alizidi kulalamika akiona anaharibiwa starehe zake.
"Sawa baba nakuja kesho asubuhi" Falzal alikata simu kisha akionekana ni mwenye uso wa masononeko kisha akaondoka humo kwenye klabu ya usiku pasipo kumsemesha yeyote na uso wake ulikuwa unalengwa machozi, aliingia ndani ya gari na akaondoka hapo akionekana ni mwenye kuchanganyikiwa sana baada ya kupokea simu kutoka kwa baba yake.

****
RASKAZONE
TANGA

Wakati Faizal akiondoka kwenye klabu ya usiku majira ya saa nne usiku kwa saa za Marekani, huku Tanzania majira kama hayo ya saa nne ila asubuhi kuna kitu kingine kabisa kigeni ndani ya nchi hii kilikuwa kinaanza kutokea. Tukio la aina yake ndiyo lilianza kuonekana kwa watu waliopo karibu na jengo lenye ofisi za makao makuu ya kampuni ya mafuta ya Matro, jengo hilo lilianza kutetemeka na taratibu likaanza kuporomoka kuelekea chini likivunjika vioo pamoja na kuta zake zikiporomoka. Lilikuwa ni tukio la kustajaabisha sana kwani eneo la chini ya ardhi lenye msingi wa jengo hilo lilipasuka kisha likafunguka na jengo zima likaingia chini ya ardhi huku eneo zima linalomilikiwa na kampuni ya Matro likiwa lunatetemeka kama kuna tetemeko la ardhi, tetemeko hilo lilipokuja kutulia eneo lenye msingi wa jengo la Matro lilibaki kama urefu wa kaburi lililojengewa. Jambo la namna hiyo halikuwahi kutokea nchini Tanzania ingawa huwa inakumbwa na matukio makubwa, tetemeko la ardhi lililoikumba eneo lenye ukubwa wa ekari moja ambalo ndani yake ndiyo zilipo ofisi kuu za kampuni ya Matro halijawahi kutokea hata katika nchi nyingine ndani ya dunia hii.

Baada ya muda mfupi kikosi cha uokoaji kilikuwa kimeshafika katika eneo hilo ambapo walibaki wakishangaa tu kwani hawakuwa na kifaa chenye uwezo wa kuchimba chini lilipodidimia ghorofa hilo wakati linavunjika, kikosi hicho kilichokuja kwa ajili ya uokoaji na chenye ari ya kufanya uokoaji kilijikuta kikishindwa kufanya uokoaji kutokana na ugumu walioukuta eneo hilo lililohitajika kufanyiwa uokoaji.

Wakiwa wamesimama hapo mlio wa mkoromo wa simu ys upepo ya kiongozi wao ilisikika na ikamlazimu kiongozi huyo atoe simu hiyo ya upepo na kuiweka mdomoni kisha akazungumza kwa kutaja eneo alipo halafu akajitambulisha, sauti yenye kukoroma ilisikika ikiongea ambapo ilisikika vyema kwa kiongozi ambaye alibaki akiwa amepigwa na butwa halafu akawaangalia wenzake huku akihema kwa kasi.

"Jamani sheli zote za Matro zinaungua sasa inahitajika timu kubwa ya msaada ya kusaidia uokoaji, sasa hatuwezi kukaa hapa mpaka mashine ya uokoaji kutoka Dar es salaam iletwe. Team twendeni tukasaidiane na wenzetu kwenye uwezekano wa kutoa msaada na sio kubaki" Kiongozi huyo aliongea kisha akaanza kukimbia yalipo magari yao na wenzake wakawa wanafuata nyuma, magari ya kikosi cha uokoaji yaliondoka eneo hilo la Raskazone kwa kasi yakiacha mamia ya raia kutojua sababu ya wao kuondoka eneo hilo.

SURA YA TANO

Siku iliyofuata nyumbani kwa Mzee Buruhan tayari turubai kubwa lilikuwa limeshafungwa katika eneo la wazi la nyumba hiyo pamoja na maeneo jirani na eneo hilo, hadi muda huo tayari watu walishajaa nyumbani hapo kutokana na umaarufu wa watoto wa mzee Buruhan waliofariki katika vifo vya kutatanisha. Upande wa kinamama kulisikika vilio kutoka kwa watu wa karibu ambao walikuwa na uchungu wq kuondokewa watu hao, ilikuwa ni siku ya kuhuzunisha kwa familia nzima ya Mzee Buruhan kutokana simanzi iliyowakumba.

Watoto wa mzee Buruhan waliosalia ambao ni ,Ally,Hassan na Falzal tayari walikuwa wapo msibani wakiwa na huzuni sana huku kaka yao mkubwa Shafii akiwa yupo hospitali kutokana na ajali aliyopata. Taratibu zote za mazishi ziliendelea kama zilivyopangwa na baada ya adhuhuri ndugu wawili wa damu walizikwa kwa wakati mmoja, baada ya mazishi watu walitawanyika na kuwaacha watu wa karibu wa marehemu wakiwa hapo msibani kuendelea na taratibu zingine zilizokuwa zimewekwa hapo awali katika ratiba ya msiba huo uliowagusa wengi kutokana na vifo vilivyowapata ndugu hao wawili wa damu.

****

HIMAYA YA MAJINI YA MAJI CHUNGU

Wakati mazishi ya Hamid na Hussein yakiwa yanaendelea yalikuwa yakishuhudiwa kwenye kioo kikubwa mithili ya sinema kilichopo katika chumba maalum ndani ya kasri la himaya ya Majichungu, Zalabain na Salmin walikuwa wakishuhudia kila kitu hadi maziko yanakamilika, baada ya kumaliza kuangalia tukio hilo waliangalia pia tukio la kuanguka kwa ghorofa la kampuni ya Matro na kuungua kwa sheli zote za kampuni hiyo.

"kazi nzuri ewe mjukuu wa mfalme nadhani bado magugu makuu manne ili kazi yetu ikamilike na hakikisha kila mmoja anaondolewa kwenye ardhi waliyokufanyia ubaya yaani Tanga na ukimmaliza yeyote nje ya Tanga utakuwa umefanya kazi bure tu" Salmin aliongea
"Nashukuru kwa kunifahamisha ewe jini mwenye nguvu uliyezaliwa milenia moja na robo tatu iliyopita, naishukuru sana nafsi yangu iliyonizuia kumuua yule mmoja wao anayesoma Marekani. Usiku kwa masaa ya Marekani tayari nilikuwa nimeshafika kwenye eneo maarufu analochezea kamari yule binadamu kwa lengo moja tu la kummaliza.

Nilitumia njia ya kujigeuza Miliver ambaye ni mchezaji kamari maarufu jijini Las Vegas ambaye nilimlaza usingizi ili asije kucheza kamari siku hiyo. Nilikuwa na kila njia ya kumuangamiza lakini nafsi ilinizuia kufanya hivyo na mimi nikaacha, nafikiri nisingeisikiliza nafsi ningekuwa nimejipa hasara" Zalabain aliongea
"ungejipa hasara haswa kwani ufalme ungeupata kwa njia ya kafara ya ndugu yako wa damu kama ungefanya uzembe huo" Salmin alisisitiza kisha akaendelea kusema, "hakikisha yule binadamu harudi tena Marekani yaani kwa lugha rahisi ni kwamba anahitajika awafuate ndugu zake"
"Hilo ondoa shaka nitalifanyia kazi haraka iwezekanavyo na inabi......." Zalabain alimuambia Salmin na alipotaka kuendelea kuongea Salmin alimzuia huku macho yake yakibadilika rangi na kuwa mekundu yaliyokuwa yanawaka kisha yakarudi katika hali ya kawaida.

"vizuizi vya kuingia vya kuingia kwenye himaya hii vinavyozuia tusivamiwe vipo wazi" Salmin aliongea huku akisimama kwa haraka.
"Ndiyo ni kweli vimefunguliwa maana kuna mfalme wa himaya ya jirani ana ziara hapa kwenye himaya yetu" Zalabain aliongea
"Ni mtego huo hao ni watu wa jamii ya kishetani ya KAKIN wametuma majini yao kulipa kisasi, wale wabaya wako mmoja wao ni mwanachama wa jamii hiyo na hao majini wameshaingia inabidi tuwazuia kabla hawajaleta madhara sasa hivi" Salmin aliongea kisha akapotea hapohapo na Zalabain naye akapotea akatokea nje ya Kasri akamkuta Salmin akiangalia juu ya anga la himaya yao ambalo limebadilika rangi kutoka ile rangi nyekundu hadi nyeusi isiyopendeza kiasi cha kuleta giza.

"tangu Dainun iibiwe hatujawahi kupata giza sasa jiulize giza hili linatokana na nini kama sio kuvamiwa huku, agiza askari wa baragumu apulize baragumu la hatari ili raia wote waingie majumbani mwao na hii vita ni yetu wasihusike" Salmin aliongea huku akimtazama Zalabain ambaye alipiga kofi moja akatokea kiumbe wa ajabu mbele yake.

"Ndiyo mtukufu mfalme mtarajiwa" Yule kiumbe aliongea kwa utiifu.
"puliza baragumu la hatari haraka iwezekanavyo raia wote waingie majumbani mwao" Zalabain alitoaamri kwa kiumbe huyo, kiumbe huyo aliitikia kwa ishara kisha akapotea papo hapo na baragumu la hatari muda huo huo likaanza kulia.

Salmin na Zalabain walipaa juu huku macho yao yakiwaka kama nuru ya nyota angani, walipofika juu walitanua midomo yao wakapuliza na ukatoka upepo mzito sana ambao uliliondoa giza lote kama unavyoondoka ukungu na mwanga ukarudi. Mbele yao walikuwa wakitazamana na viumbe wenye sura za ajabu tena wenye rangi nyeusi, miili ya viumbe hao haikuwa ikieleweka ilivyo ilikuwa na umbile kama tambara bovu jeusi. Viumbe hao walikuwa wamebeba silaha za aina mbalimbali za kijini wakiwa na hasira za dhahiri, viumbe hao wakihema walikuwa wanatoa moto mdomoni kwa jinsi hasira zilivyokuwa zimewazidi.

"Jisalimisheni kwa usalama wa jamii yenu yote hii" Mmoja wa wale viumbe aliongea.
"Ondokeni kwa amani kwa usalama wenu na si mpaka tutumie nguvu" Salmin aliongea kwa upole sana
"Naona jeuri sasa ngoja tuanze na wewe" Yule kiumbe alisema kisha akamnyooshea silaha yake Salmin iliamuangamize lakini alijikuta anaangamia yeye baada ya shoti kali zilizotoka kwenye macho ya Salmin kutua mwili mwake.

Wenzake waliosalia walijiandaa kuwashambulia Salmin na Zalabain lakini walichelewa kwani walijikuta wakizungushwa na upepo wa ghafla uliotengenezwa na Zalabain ambao uliwafunga kama wamefungwa na kamba ngumu kisha waliangamizwa wote kwa pamoja kwa kuunguzwa na moto uliotoka mdomoni kwa Salmin uliowaunguza wote wakawa majivu.

"Habari yao imekwisha funga kizuizi" Salmin aliongea kisha akashuka chini taratibu na Zalabain akaenda juu zaidi akanyoosha mkono mmoja uliotoa mwanga wa ajabu ulioelekea juu halafu akashuka chini taratibu baada ya kumaliza kazi yake.
"hakuna atakayeweza kuivamia himaya ya majichungu nikiwa mimi nipo na himaya hii itadumu mpaka mwisho" Salmin aliongea kumuambia Zalabain kisha akainama chini kiutiifu akapotea mbele ya macho ya Zalabain.

Baragumu la kuashiria hakuna hatari tena katika himaya hiyo lilipulizwa na raia wa himaya hiyo wakatoka majumbani mwao kuendelea na shughuli nyingine za kawaida na Zalabain akarudi ndani ya Kasri la ufalme.

****

Wakati majini waliotumwa kuleta maafa wanauawa upande mwingine kwenye chumba chenye watu waliovalia majoho meusi ambacho kilionekana kwa muonekano kilikuwa kipi chini ya ardhi. Kilikuwa kimetawaliwa na jazba miongoni mwa watu waliomo humo ndani, kiongozi wa watu ndiyo alionekana kuwa na jazba za wazi hadi akavua kofia ya joho lake akasema kwa hasira, "Haiwezekani! Haiwezekani! Hussein wamuue na majini yetu wayaue, lazima! Lazima! Tulipe kisasi kwa ajili ya Hussein mwanachama wetu".

Sauti ya kiongozi huyo ilisikika kwa nguvu na kusababisha tetemeko zito litokee kwa sekunde kadhaa na lilipotulia ilisikika sauti ikisema, "Dalipso Londo usiingie kwenye vita isiyokuhusu hata kidogo, Hussein alikuwa ana janga lake tofauti alilolichuma kabla hajaungana nanyi,nimetumwa na mkuu wa wakuu nikuonye ukae mbali na tukio hilo na uhakikishe unamtia nguvuni Qwanta Alfred Lumaki aliyetutia hasara".
Wote walikuwa wameinama kiutiufu na waliinua vichwa vyao baada ya sauti hiyo kuacha kuzungumza.
"ndiyo mkuu" Dalipsol Londo alitii

"kazi ianze sasa hivi ili dunia iwe chini yetu tukiipata damu ya Alfred Lumaki na Qwanta wenzake,ndiyo furaha ya mkuu wa wakuu ni ushindi kuwa upande wetu na si vinginevyo" Sauti ile iliendelea kusikika kama mwangwi kisha ikapotea haraka sana, Dalipsol Londo aliwageukia wenzake akawaambia, "vita ya mamba kiboko haimtii wahka kwani amani hutawala hata bila kuingilia hiyo vita hivyo haina haja ya yeye kuingilia, ndiyo hivyohivyo vita ya Hussein na familia yake haitufai sisi kuingilia ile inawahusu yeye na familia yake na wala haivurugi hata kipengele cha kazi yetu".

Baada ya Dalipsol Londo kusema maneno hayo alipiga kofi mara moja na mlango wa eneo walilopo ukafunguliwa, aliingia mtu aliyevaa joho jeusi akiwa anavuta kitoroli kidogo kilichofungiwa kondoo mweusi na pembeni kulikuwa kuna kifaa chenye ncha kali. Toroli hilo lilivutwa hadi mbele ya Dalipsol Londo kisha yule mtu akamkabidhi kifaa chenye ncha kali huku akiwa ameinamisha kichwa kwa heshima, Dalipsol Londi alikipokea kifaa hicho kisha akasema, "ni muda kuanza ibada kuu zaidi ya zote kwa mkuu ambaye ndiye mungu yetu mkuu, hatuna Mungu mkuu zaidi yake mkuu wa wakuu".

Alipomaliza kutamka maneno hayo alimtoboa yule kondoo shingoni kisha chombo kikubwa kikakingwa chini, damu ya yule Kondoo iliingia ndani ya chombo hicho hadi kikajaa na Kondoo aliondolewa na yule mtu aliyemleta akiwa bado anatapatapa kutokana na jeraha lililotobolewa na Dalipsol Londo. Damu ile ya Kondoo ilitiwa kwenye kwenye bilauri zilizotengenezwa na madini ya fedha na zikasambazwa kwa watu waliokuwa wapo humo ndani, kila mmoja alikamata bilauri yake na wakazinyanyua juu kwa pamoja huku vichwa wakiviinamisha.

"Kwa jina la mkuu wa wakuu mwenye mamlaka kuu ya kutupa nguvu pamoja na pumzi kuu" Dalipsol alitamka maneno hayo huku bilauri akiwa ameinua juu kama wengine, alipomaliza kutamka maneno hayo aliinywa damu ile huku wenzake wakifanya hivyo hivyo.

Kakin ni jamii ya watu wanaoabudu nguvu za giza ambayo ilianzishwa miaka mingi iliyopita huko mashariki ya mbali na iliingia Afrika miaka mingi iliyopita kupitia waziri mkuu wa utawala wa Roma aliyetoroka katika himaya ya Roma kuepuka kuuawa na mtawala wa himaya hiyo aliyekuwa anaitwa Miltonus baada ya kubainika ni mwanajamii wa Kakin. Bwana huyu aliitwa Hilainus aliingia barani Afrika na akapokelewa kwa ukarimu sana kama ilivyo kawaida ya Waafrika kupokea wageni kwa ukarimu, aliingiza falsafa za jamii ya Kakin kwa siri sana hadi akajipatia wafuasi kutoka pande mbalimbali za Afrika. Hadi anafariki tayari alikuwa na familia yake na jamii hiyo ya siri ilikuwa imeshasambaa mhalimbali na ilikuwa inaendeshwa kwa siri mno kwani habari za uovu wa jamii zilikuwa zishasambaa barani kote ingawa haikujulikana ni nani aliyeileta Afrika.

Usiri wa ibada za jamii hii ulizidi sana pale mtawala wa himaya ya Soghai Sunni Ali alipowaua kwa kuwakata vichwa watu waliobainika ni watumishi wa jamii hiyo, asilimia kubwa ya himaya za kiafrika tayari zilikuwa zimeufuata uislamu baada ya kufanya biashara na waarabu kwa muda mrefu kipindi ambacho himaya ya roma bado inanyanyasa watumwa. Hadi imani za Kakin zinaingizwa barani hapa tayari Uislamu ulikuwa umeshasambaa sana, juhudi za upambanaji dhidi ya jamii haramu ziliwahusisha wanajamii wote wa Afrika bila kujali tofauti ya kiimani iliyokuwa ipo kati ya waislamu na ambao walikuwa wana imani za kizamani za kuabudu miti na mapango ambao walitofautiana sana kiimani na Kakin ingawa walitegemea majini walioiita mizimu. Wote kwa pamoja walipambana sana na udhalimu na Kakin na baadaye hatimaye waislamu walijitoa baada ya kuzaliwa mtoto aliye na mchanganyiko wa mashariki ya mbali na Habaishi waliokuwa wafuasi wa Waothodoksi, mtoto huyu alipewa jina cheo cha Qwanta ambaye katika uzao wake walishirikishwa majini weupe wanaojulikana kwa jina la majini wa nuru. Majini hao walikuwa wametengana na wale wa giza waliokuwa wako pamoja na Kakin, majini hawa walikuwa wapo tayari kuona jamii nzima ya Kakin inaangamia ili dunia iwe huru na walimpatia nguvu za ajabu mtoto huyo ili alete mapinduzi katika, kisa hicho kilichoelezewa na mwandishi wa mkasa huo aitwae Hassan Omar Mambosasa alichokipa jina la KUANGUKA KWA KAKIN kuanzia kitabu cha kwanza na hadi cha mwisho ndiyo kinaelezea kinagaubaga juu ya jamii hii na kuanguka kwake.

****

Baada ya siku kadhaa tangu mazishi ya Hamid na Hussein yafanyike Falzal alipanga arudi Marekani na alienda kukata tiketi katika ofisi za shirika la ndege la Ermirates za jijini Tanga lakini alijikuta akishindwa kuondoka baada ya kuambia kuwa hakuna ndege hata moja iliyokuwa ikiingia Marekani kutokana na hali ya ukungu iliyokuwa imetanda katika bahari ya Antalantiki, habari hiyo ilimnyong'onyesha sana na akajikuta akibakia kwenye jiji la Tanga na hata alipojaribu kwenda jiji la Dar es salaam ili akaendelee na starehe napo alijikuta akishindwa kutokana na kukosa gari linaloenda huko. Alipouliza juu ya chanzo cha kuvunjika kwa safari hiyo alijibiwa kuwa daraja la mto Wami lilikuwa limevunjika na hata alipojaribu kwenda uwanja wa ndege wa Majani mapana wa jijini Tanga kukata tikeri ya ndege alikosa vilevile akaambiwa ndege za mashirika mbalimbali zilizokuwa zinarusha ndege zake kuja Tanga zimevunja safari zao.

Hali hiyo ilimfanya Falzal ajihisi ana mkosi baada tu ya kurejea nyumbani akiwa ili ahudhurie msiba wa kaka zake, maisha ya anasa aliyoyazoea kuishi kule marekani ndiyo yalimfanya ashindwe kukaa jijini Tanga kwani akiishi maisha hayo alikuwa anamtia aibu baba yake mzazi.

Heshima ya mzee Buruhan ndani ya jiji la Tanga kutokana na busara alizonazo kwa kuwaongoza wanae zilimfanya aheshimike kwani wanae ni watu maarufu sana ndani ya jiji hilo, hivyo laiti Falzal angeishi hivyo hapo Tanga angetia doa heshima ya baba yake. Falzal alijiona ni kama yu kifungpni kwa kukosa maisha anayoyapenda na aliyoyazoea, alivumilia kukaa hivyo kwa muda wa takribani siku mbili na hatimaye siku ya tatu akachukua mizigo yake akaiweka kwenye gari na akaazimia kuondoka mbali na jiji la Tanga ili akaishi atakavyo hadi pale atakapoondoka tena Marekani. Eneo alilofikiria kwenda ni Arusha tu kwani ndiyo ambapo hapakuwa na kikwazo chochote, aliamua kutumia usafiri binafsi ili awe huru zaidi.

Hakika hakutambua kama alikuwa anajaribu kukwepa jambo lisilokwepeka labda akukwepeshe muumba ndiyo linaweza kukwepeka lakini si kwa nguvu za kawaida kuweza kulikwepa, hakujua na alikuwa ameshasahau juu ya janga walilolifukia ambalo limejifukua bila ya wao kujijua. Hakutambua kama vikwazo vya safari vinatokana na jambo ambalo lisilokuwa na la kawaida.

Falzal aliwaaga ndugu zake pamoja na mzazi wake kisha akaingia kwenye gari binafsi anayoitumia aina ya toyota landcruiser, alianza safari vizuri huku akiwa na shauku kuu ya kuliacha jiji la Tanga ili aende kuendelea na maisha yake ya anasa aliyoyaacha hapo awali.

Aliendesha gari kwa mwendo wa wastani hadi alipoanza kukaribia Majani mapana ndipo alipozidi kuongeza mwendo wa gari ili aendane na mwendo unaotakiwa katika barabara aliyopo, alipokaribia eneo ambalo kuna njia iendayo kwenye mzani wa magari makubwa wa Majani mapana aliona mzee mwenye mizigo akumpungia mkono njiani ili amsimamishe lakini alimpita kwa mwendo mkali sana huku akisonya.

"Vizee vingine bhana vinadhani kila gari ni ya kubeba watu masikini kama wao, akapande basi huko asinisumbue mimi" Falzal aliongea kwa dharau kisha akaongeza mwendo zaidi.

"vijana wengine bhana wanadhani kila mali inaweza ikadumu bila kujali imepatikana kwa njia gani, wakatafute kupitia jasho lao wenyewe" Ilisikika sautu ikitoka kwenye kiti cha nyuma cha gari hilo na ikamfanya Falzal ageuke nyuma huku akiwa ameachia usukani, loh! Sallaleh alimuona yule mzee aliyempita pale barabarani akiwa amekaa kwenye kiti cha nyuma akiwa amekunja nne akiwa na mavazi yake machakavu aliyomuona nayo pale njiani wakati anampita. Falzal alizidi kupatwa na uoga sana kwani haiwezekani mtu akiyempita njiani tena kwa mwendo wa kasi amkute ndani ya gari yake, alibaki akimtazama huku akitetemeka kwa uoga hasa alipoona tabasamu la yule mzee.

"Kijana kamata usukani utagonga huoni kama tupo kwa Minchi tunaelekea kwenye ule mzunguko tena kuna tuta mbele, dereva gani usiyekuwa na umakini uwapo barabaranu wewe tena punguza mwendo maana tunaingia katikati ya jiji magari ni mengi" Yule mzee alimwambia Falzal huku akutabasamu na mahali alipomtajia Falzal palikuwa ni mahali ambapo ni mwanzo kabisa alipapita hata kabla hajafika Majani mapana, Falzal alipoangalia mbele kweli aliona anakaribia kwenye tura na alipunguza mwendo haraka sana na akalipita tuta kisha akashika usukani vizuri akawa anaingia kwenye mzunguko wa kwa Minchi. Falzal alilizungusha gari kwenye mzunguko huo ili arudi alipotokea katika barabara kuu iendayo Segera, alipotaka kunyoosha tairi kisha akate kidogo aingie barabara ya hiyo ambayo alitokea kuingia mzunguko huo wa kwa Minchi alijikuta akishindwa baada ya usukani kugoma na hivyo akazunguka tena ule mzunguko na gari ikaingia katika barabara kuu iendayo Mombasa.

" Huwezi ukatoka nje ya Tanga hata kwa namna gani , ulidhani ukimaliza hiyo roundabout ya Kwa Minchi utaweza kurudi kule ulipokuwa unaelekea. Sasa umeula wa chuya kijana" Yule mzee aliongea huku akitabasamu.

"we...we.....wewe ni nani?" Falzal aliuliza huku akitetemeka na alikuwa akimuangalia huyo mzee pamoja na kuangalia mbele ili asipate ajali, uoga uliokuwa umeibugika nafsi yake ulimfanya ashindwe kutambua kama gari hiyo ilikuwa inaenda yenyewe kwa mazingira ya ajabu pasipo yeye kuiendesha.

"Achia usukani kijana maana unajisumbua gari hiyo inaenda yenye na si wewe unaiendesha na si unataka kunijua mimi ni nani sio?" Yule mzee aliongea kisha akaongea akajibadilisha akawa na sura ile ya mtoto ambayo iiliwatokea kaka zake muda mfupi kabla hawapoteza maisha katika mazingira ya kutatanisha.

"Jamadin! Ha..pana siyo we..we" Falzal aliongea huku akitetemeka kwa uoga kwani hakutarajia kumuona aliyemuona hapo.
"Unashangaa kuniona mimi? Ha! Ha! Ha! Kwanini usijishangae kwa kuhusika kufanya maisha ya mwenzako aliyeumbwa kama wewe kuwa duni" Yule mtoto aliongea kwa sauti yenye kukwaruza tena alicheka kicheko kisichokuwa kinaashiria furaha kwani machoni alishaanza kutoa damu.

"Kutumia nguvu za wenzenu kujitajirisha mliona raha sana sasa leo ni zamu yako Falzal ambaye hupaswi kuitwa baba mdogo kwa mabaya uliyonifanyia" Yule mtoto aliongea huku akilia kwa machozi ya damu
"Si.....siyo mimi Jamadin ni kaka ndiyo aliyekukosea na ndiyo aliyepanga kila kitu" Falzal aliongea kwa uoga.

"Huna cha kujitetea kwa sasa kitachoweza kufanya nikusamehe wewe mwanaharamu, kwanza nipe ukitaka ufe kistarabu la si hivyo nakurarua kama Simba anavyorarua nyama ya swala" Yule mtoto aliongea kwa hasira hadi miale ya moto ikawa inamtoka mdomoni mwake.
"Ni...nikupe nini Jamadin?" Falzal aliuluza huku akiwa anazungusha macho yake kuangalia kama anaweza kupata upenyo wa kukimbia lakini hakukuwa na upenyo wa kutokea kwani milango ilikuwa imefungwa na vioo vimebanwa hadi mwisho.

"Mmmhu! Yaani hilo suala la kunitoroka usifikirie kabisa, nimesema nipe kile kinachowafanya muwe matajiri kila kukicha na kile kinakufanya uwe na bahati kila ukicheza kamari" Yule mtoto aliongea kwa hasira sana.

"sinacho mimi Jamadin anacho..." Falzak alijitetea na alipotaka kumtaka mwenye kitu kinachotafutwa na huyo mtoto lakini alijikuta akikabwa kooni baada ya huyo mtoto huyo kumnyooshea kidole.

"sijakuambia umtaje huyo aliyenacho, sasa nilikuambia nakurarua ukiwa huna na sitengui kauli yangu" Yule mtoto aliongea kisha akatoa makucha mikononi akaanza kumrarua hadi mwili wa Falzal ukawa ni damu tupu tu na vidonda kila sehemu ingawa roho yake haikuachana na mwili na maumivu ndiyo yalitawala mwili wake wote, alipiga makelele akilia kama mtoto mdogo lakini hakukuwa na mtu aliyesikia kulio chake kwa muda huo.

"Sasa wasalimie ndugu zako waliokuwa wametangulia kaburini nadhani watakuwa wanakungoja huko walipo" Yule mtoto aliongea kisha akatoa moto mkubwa wenye mlipuko mithili wa bomu ambao ulisambaa gari zima
Hadi muda huo tayari gari la Falzal lilikuwa limeshafika maeneo ya Kisosora kwenye matanki ya mafuta ya kampuni ya BP iliyopo jirani na bahari ya hindi, yule mtoto alipopuliza ule moto gari lote lilipuka na likarushwa juu hadi ndani ya maji na hu ndiyp ukawa mwisho wa maisha ya Falzal ndani ya dunia na ukawa mwanzo wa maisha mengine nje ya dunia hii katika ulimwengu usionekana kwa macho ya kawaida.

****
Hali ya Shafii kiafya iliendelea kuwa nzuri na hadi muda huo alikuwa tayari amesharuhusiwa na yupo nyumbani akiuguzwa na mke wake, huzuni kubwa ilkuwa ni sehemu iliyoutawala moyo wake hasa akikumbuka vifo vya wadogo zake. Hakuwa na la kufanya kwa muda huo kwani yeye alikuwa ni mtu wa kutembea na baiskeli ya walemavu kwani kiuno kilikuwa ni sehemu iliyopatwa na kadhia katika ajali ile iliyomkuta na ingemchukua muda mrefu mpaka kutengemaa na kuwa na hali ya kawaida kama ilivyokuwa hapo awali. Hadi muda huo si yeye wala familia yake waliokuwa na habari na jambo lililomkuta Falzal tangu alipowaaga anasafiri kuelekea Arusha akitumia gari binafsi, hawakujua akama falzal ni mmoja wa marehemu kwa muda huo.

Kusononeka, kuhuzunika na kuumia moyo ndiyo jambo ambalo lilikuwa likimsumbua Shafii kila siku hasa alipowakumbuka ndugu zake na jambo lile aliloambiwa na sauti asiyoitambua kuhusu mwanae wa pekee Zayina kuwa ametekwa na yupo chini ya adui yake ambaye hamtambui hadi muda huo aliwahi kumfanyia ubaya upi kwani hakuna dui yake mwenye ubavu wa kumfanyia mambo hayo kwa mujibu wa mganga wake marehemu Sauti ya radi kama alivyomuambia. Alikuwa akimiliki cheni yenye kidani chenye kito kisichofahamika hapa duniani ambayo ndiyo ilifanya awe na nguvu miongoni mwa maadui zake na pia kidani hicho kilikuwa na uwezo wa kuwalainisha mioyo wanadamu wenzake ambao walitaka kufanya jambo baya kwake au kwa jamaa zake. Fikra zilizokuwa zipo kichwani ni kuwa adui aliyekuwa anamfanyia ubaya alikuwa ni mwanadamu wa kawaida na hakuwahi kuwaza kama kuna jini anayeweza kumfanyia hivyo kwani fikra zake zilimpa asilimia mia moja kuwa hajawahi kumfanyia ubaya jini katika maisha yake zaidi ya kuwafanyia ubaya wanadamu wenzake tu.

"ni nani huyu na ana shida gani na mimi kwani hata cheni niliyokuwa nayo inashindwa kumtambua hata kidogo.Jamadin,gasper,Hilson na wengine wengi niliowahi kuwafanyi ubaya tayari wametangulia mbele za haki" Shafii alijiuliza katika nafsi juu ya utata wa tatizo linalomsumbua la kuondokewa na watu anaowapenda.

"Eeeh! Mungu nimekosa nini mja wako nipo njia panda mja wako" Kwa mara ya kwanza Shafii alijikuta alijikuta akimtaja muumba baada ya kukaa kwa kipindi kirefu akimuasi mwenyezimungu kwa kumtegemea mwingine tofauti na yeye, maneno yake yalisikiwa nyema na mke wake ambaye alikuwa yupo nyuma yake akimtazama mumewe wake kwa masikitiko makuu jinsi anavyolalalmika kwa Mwenyezi mungu. Bi Farida muda wote huo akimtazama mumewe kwa jinsi anavyolalamika alijua ni kutokana na vifo walivyokufa wadogo zake, wala hakutambua kama mumewe alikuwa akiteswa na sauti ya mbaya wake ambaye alikuwa hamtambui. Machozi yalipoanza kutiririka katika macho ya Shafii. Hali ya Shafii ilimfanya Bi Farida amkumbtie kwa nyuma kisha akambusu shavuni kwa upendo halafu akamwambia,"Baba Zayina kazi ya Mungu haina makosa yapasa kumshukuru katika kila hali kwani amekujalia uzima katika ajali mbaya uliyoipata, haipaswi kumlaumu kwakuwa ndugu zako wamepoteza maisha mpenzi wangu"
"Mke wangu inauma sana nahisi dunia yote nimeangushiwa mimi inauma.....inauma sana" Shafii aliongea huku machozi yakimtiririka machoni mwake.

"Ha! Ha! Ha! Ha! Nadhani unatambua ule msemo wa waswahili waliosema kwamba jeraha la kujitakia halihitaji pole, sasa usitegee pole kwa mtu ambye baadaye akija kukujua upande wa pili wa maisha atakuacha na janga lako mwenyewe. Ha! Ha! Ha! Ha! Ha! Mwanao Zayina najiandaa kuwapikia supu mbwa wangu wamle nikishamchinja" Sauti ileile iliyompa taarifa ya kuwa kuna jambo baya lnalotaka kutokea kwa mtoto wake ndiyo ilimpa taarifa iliyomfanya ashtuke

"He! Baba Zayina kuna nini mbona unashtuka hivyo hadi unanitisha mume wangu" Bi Farida aliuliza
"Nimejitonesha sehemu ya mgonogni mke wangu kutokana na kusononeka huku" Shafii aliamua kudanganya huku akiuma meno kwa maumivu kana kwamba alijitonesha kweli kumbe alishtushwa na sauti ya adui yake mkuu ambaye aliyewahi kumlea mwenyewe kwa mikono yake bila kujua ambye alimwambia jambo baya ambayo ameazimia kwenda kulifanya kwa binti yake kipenzi aliyempenda. Laiti kama wanadamu tungalipewa uwezo wa kuona yaliyojificha katika mioyo ya wenzetu basi Bi Farida angeliomba talaka mapema sana lakini Mungu muumba hakutupa uwezo huo wa kuona yaliyo katika mioyo ya wenzetu ndiyo maana Bi Farida hakutambua jambo linalimtatiza. Ama kweli moyo wa mtu ni kiza nene zaidi hata ya giza nene lililotanda kwenye pori nene katika usiku mnene, mungu muumba alikuwa na maana yake sana kutuumba wanadamu kwa kuficha yaliyopo mioyoni kwani hadi muda huo tayari wanadamu tungekuwa tushafarakana kama tungebaini yaliyopo kwenye mioyo ya wenzetu.

"ngoja nikuwahishe ndani mume wangu ukanywe zile dawa na upumzike" Bi Farida aliongea huku akianza kuburuza kiti cha matairi cha mumewe huku akiita, "Jamali! Jsmali!".

"naam!" Sauti kutoka ndani ya chumba kimojawapo ilisikika ikiitika.
"njoo unisaidie kumuweka kitandani mjomba wako" Bi Farida alimuambia yule mtu aliyemuita huku akikisukuma kiti cha matairi kuelekea chumbani kwake, muda huo Shafii alikuwa bado ameuma akiweka maumivu yake ya kuigiza ili azidi kumchota mke wake akili ajue ni kweli ameumia.

"Sawa shangazi nakuja sasa hivi" Sauti ya Jamal ilisikika kisha mlango wa chumba kimojawapo ukafunguka na akatoka kijana aliyefanana sana sura na Hamis kaka yake Bi Farida na shemeji yake Shafii, Jamal alitembea upesi akamfikia shangazi yake akachukua kiti alichokalia Shafii akaanza kukiburuza yeye kukiingiza katika mlango wa chumba kimojawapo ambacho kimejitenga sana na vyumba vingine ndani ya nyumba hiyo, alipoingia ndani alikiburuza kiti hadi mahali kilipo kitanda cha kisasa kilichotengenezwa kwa mtindo wa kipekee na kunakshiwa kwa mapambo mbalimbali. Jamali alipofika hapo alimbeba mjomba wake kwa uangalifu akamlaza kitandani halafu akatoka chumbani kwa mjomba wake upesi kutokana na heshima aliyonayo kwao ambayo haimpasi kukaa humo ndani muda mrefu kama alikuwa tayari amemaliza kile kilichomfanya aitwe.

Bi Farida alichukua dawa za kutuliza maumivu akampatia mumewe pamoja na maji, Shafii alizinywa hizo dawa kisha akajilaza huku akiuma meno vilevile na baada ya muda alijifanya kapitiwa na usingizi ili kutuliza wahka aliyokuwa nao mkewe juu yake kwani wasiwasi ulikuwa mkubwa sana kila akimuangalia anavyouma meno kwa hasira. Bi Farida baada ya kumuona Shafii kalala alimfunika na shuka vizuri halafu akambusu usoni, alitoka chumbani akaelekea sebuleni akamkuta Jamali anaongea na simu ya mezani ambapo alipofika tu mpwa wake huyo alisema, "eeh huyu hapa ongea naye".

Jamal alimkabidhi mkonga wa simu shangazi yake kisha akaenda kukae sebuleni kwenye kochi, Bi Farida alichukua mkonga wa simu akauweka sikioni na kuongea " ndiyo ni mama yake hapa.......hapana hajarudi nyumbani tangu muhula wa masomo ulipoanza.......nyinyi mnasema tulimtuma mtu aje kumfuata sisi hatukutuma ingawa ni kweli kulikuwa na matatizo huku nyumbani.....sawa toa taarifa ya kutoonekana kwake nyumbani wala chuoni".
Baada ya kuongea hayo maneno kwa njia ya simu aliikata simu kisha akaanza kulia kwa sauti ya chini kutokana na taarifa aliyopewa, Jamali aliinuka akaenda kumbembeleza shangazi huku akimuuliza jambo lililomfanya alie.

"Jamal binamu yako hajaonekana chuo tangu siku ile ya msiba wa wajomba zako na huko chuoni kwao walikuja watu wakasema wametumwa na baba Zayina kumfuata arudi kwa ajili ya msiba jambo ambalo siyo la kweli kabisa" Bi Farida alieleza huku akilia kwa uchungu sana.

"Shangazi usilie sasa inabidi wewe ndiyo upange mkakati wa kumtafuta kwani mjomba hali yake ndiyo hiyo unaiona na hii taarifa akipewa itamletea matatizo zaidi, naamini Zayina yupo salama tu na hajadhurika hivyo tuanze kumtafuta haraka iwezekanavyo bila hata kumuhusisha mjomba"Jamal alimuambia shangazi yake.

"Jamali mwanangu mimi jamani, sijui wamemkosea nini mpaka wamafanyie hivyo. Oooh! Yarrabi nisaidie mimi" Bi Farida alizidi kulalamika kwa sauti tofauti na awali.

"Shangazi sauti hiyo mjomba ataamka na asikie iwe mengine nafikiri unajua jinsi anavyompenda sana Zayina, hebu fikiria akiamka utamuweka katika hali gani kama akijua. Inabidi tutoe taatifa kwa wajomba wengine na baba ila yeye tu asiambiwe ili wasaidie katika hili" Jamali aliongea kwa upole tena kwa kusihi hadi Bi Farida akatulia akawa anafuta machozi hadi aliponyamaza.

"Sawa nimekuelewa anko, ngoja nimpikie baba yako na shemeji Hassani ili tuje tujadili hili suala" Bi Farida alimuambia Jamali halafu akanyanyuka akaenda mezani alipoiacha simu yake ya mkononi akawapigia wahusika aliowahitaji katika kujadili hilo suala.

Baada ya nusu saa Hamis na Hasaani walikuwa tayari wameshawasili nyumbani kwa Shafii na kikao cha watu wanne kikawekwa eneo la bustanini na wahusika wa kikao hicho wakawa ni Bi Farida, Hamis, Hassani na Jamali. Kikao kilianza kwa Bi Farida alifungua kikao kwa kueleza kils kitu juu ya taarifa aliyoipata kutoka kwa uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kisha akaeleza ushauri alioupata kutoka kwa Jamali wa kuwaita wao ili waweze kulitatua tatizo hilo.

"Umefanya vizuri sana mwanangu kwa kumshauri shangazi juu ya hili suala" Hamis alimpongeza Jamali kisha akaendelea, "dada hili suala kwa jinsi unavyolieleza ni zito sana na linahitaji tufikirie kwa kina haswa maana huyo mtu aliyemfuata Zayina akamwambia mnamuita nyumbani anajua nini anafanya na ametumia taarifa ya msiba huu kuwa ni njia ya kumnasa".

"Shemeji Hamis naungana na wewe katika suala hili itakuwa huyu mtu ni adui namba moja wa kaka sasa inabidi huu msako tutume watu wenyewe wauendeshe kwani tukitumia vyombo vya dola itakuwa tunaharibu tu maana hatuwezi jua huyu mtu ana nguvu gani katika serikali. Kumbuka Zayina kusoma chuo kile tulifanya siri kwa wanafamilia tu kwani tunatambua mtu maarufu ana maadui sana ndiyo maana tukawaambia watu wengine kwamba Zayina anasoma Ulaya ili tuwapoteze njia ya kumtafuta, sasa tujiulize huyu mtu ana ni nani na ana lengo gani mpaka amejua Zayina alipo na akafanya hilo alilolifanya" Hassani naye aliongea kwa mara ya kwanza katika kikao hicho.

"Shemeji tayari mimi nishawaambia uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam watoe taarifa juu ya suala hilo hivyo tayari lipo kwenye vyombo vya dola, sasa tufanyeje?" Bi Farida aliongea
"Aaaah! Shemeji umekosea sana kufanya hivyo huoni huyo aliyemshikilia Zayina atazidi kuwa makini ili tusimjue" Hassani alimlaumu shemeji yake kwa kuwaambia uongozi wa chuo kutoa taarifa.

"Dada hapo umekosea sana kufanya hivyo kwani alichokuwa anaongea Shemeji hapa ni sahihi kabisa kukifanya katika suala hili kwani haitakiwi kuwashirikisha wanausalama inatakiwa tutumie pesa yetu mtoto apatikane" Hamis naye alimlaumu dada yake.
"Jamani nilikuwa nimechanganyikiwa haswa kutokana na kupokea taarifa hiyi, sasa tutafanyaje?" Bi Farida aliongea akionekana kutambua alichokifanya sicho katika kutoa taarifa ya kuwaambia uongozi wa chuo.

"Hukutakiwa kufanya hivyo dada" Hamis alimlaumu dada yake.
"Baba na mjomba hili suala limeshatokea na haliwezi kuwa halijatokea yaani tukubali Shangazi alikosea kuwaambia uongozi wa chuo kuto taarifa polisi lakini tusimlaumu kwa kufanya hivyo maana huo muda wa kulaumiana hamna, cha msingi ni kukaa na kujadili hilo tufanye nini ili Zayina apatikane jamani" Jamali kwa mara ya kwanza aliongea baada ya kuwasikiliza wakubaa zake, maneno yake yalionekana kuwaingia mjomba wake na baba yake hadi wakakaa kimya kwa muda wakijifikiria halafu wakatazamana na wakapeana ishara ambayo hakuna yoyote aliyeiona.

"Sawa mwanangu nimekusikia tuachienu hili suala tulishughulikie naamini Zayina atapatikana ndani ya muda mfupi tu" Hamis huku baada ya kushusha pumzi, Hassan naye alikubaliana na maneno naye.

"nafikiri hili suala lipo kwetu na tutalifanyia kazi sasa naomba Kaka asijue juu ya hili" Hassani naye aliongea kisha akasimama pamoja na Hamis.
"Shemeji yupo wapi tukamjulie hali kidogo kwani kuja huku bila kumjulia hali si jambo jema" Hamis aliuliza
"Yupo chumbani kapumzika baada ya mgongo kushtuka, nafikiri atakuwa kashaamka twendeni mkamuone" Bi Farida aliwaambia huku akinyanyuka kwenye akaelekea ndani, Hamis na Hassani walikuwa nyuma wakimfuata.

Wote kwa pamoja walielekea chumbani kwa Shafii ambapo walimkuta akiwa tayari ameamka.
"Karibuni jamani" Shafii aliwakaribisha
"Asante Chumbio" Hamis aliitikia ukaribisho huku akikumbushia jina la utani la Shafii, Hassani na Bi Farida wacheke.
"hilo jina husahau tu Bonoeza" Shafii naye aliongea huku akitia jina la utani la Hamisi nakupelekea wote wacheke humo ndani.
"Bonoeza siku hizi umelizoea si ulikuwa ukiitwa unarusha mawe kaka" Bi Farida naye aliongea huku akicheka na kupelekea wote humo ndani wacheke sana.

"Ila hilo jina umenikumbusha mbali sana niliwahi kumpiga mwenzangu tukichunga mbuzi kisa hilo jina, ila toka naingia kwenye ujana hadi utuzima naona kawaida tu" Hamis aliongea huku akicheka.
"Haya jamani ngoja niwaache na soga lenu la kiutuzima" Bi Farida aliongea kisha akatoka humo chumbani akiwaacha Kaka yake, mume wake na shemeji yake.

Alipofunga mlango wa chumbani mwake mada ikabadilika papo hapo na ikaongelewa mada inayowahusu hao wanaume watatu waliokuwa na ukaribu tangu utotoni, mambo yao mengi ya siri walikuwa wakiambizana na hata mengine mazito walishirikiana.
" kajua Zayina anashikiliwa na mbaya wetu ambaye bado hatujamtambua" Hamis alimuambia Shafii
"Natambua sana kama anajua hilo kwani wakati anaongea na simu sikuwa nimelala kama anavyofikiri na hata alipolia kwa sauti na kulalamika nikawa namsikia" Shafii aliwaambia.

"Hiii ni balaaa haswa inabidi tumtafute mtaalamu mwenye uwezo wa kudhibiti majini maana anayefanya haya si mwanadamu wa kawaida" Hassani aliongea.

"Hilo ndiyo la kufanya inabidi atafutwe mtaalam ila asiwe mzee Mahmud maana yule mzee atatuvua nguo tuaibike kwanza halafu ndiyo atusaidie maana tiba zake hufanya kazi ukiongea ukweli tu, sasa sisi hatuko tayari kuvuliwa nguo" Shafii aliongea
"Kweli kabisa bwana Shemeji ni bora kufa na matatizo yetu shingoni kuliko kukubali kuvuliwa nguo" Hamis alidakia baada tu ya Shafii kumaliza kauli yake.
"Jamani hili suala tupiganeni hadi kufa maana wataalamu ni wengi hapa Tanga tena leo hii nimepata taarifa kuna mtaalam mwingine anaitwa Mafindo yupo Pangani nasikia huyo ni kiboko ninahisi ndiyo itakuwa mwisho wa matatizo" Hassani aliongea
"Enhee Hassani umenena haswa naona mkitoka hapa muanze huko au mnasemaje jamani na ningekuwa mzima ningeungana nanyi" Shafii aliafikiana na Hassani.

"Sawa naona tusipoteze muda bali twende huko ili mambo yasiwe mabaya" Hamis alisema kisha akanyanyuka akampa mkono Shafii na Hassani naye akafanya hivyo hivyo.

"Kila la heri jamani" Shafii aliwaambia kuwatakia heri katika mpango huo wanaoenda kuufanya, Hamis na Hassani waliondoka upesi ili wawahi kurudi kwani Pangani kulikuwa mbali na muda ulikuwa umeenda sana.

SURA YA SITA

Hali ya hewa ilikuwa ni tulivu sana na mawingu ng'amba yalikuwa yamepamba anga zima na kulifanya jua lisionekane kabisa na kuweka hali ya kivuli na kuwafanya wakazi wa jiji la Tanga kuwa na ahueni ya joto haswa kwa wale wanaotembea kwa miguu pembeni mwa barabara. Hamis na Hassani walikuwa wapo ndani ya gari binafsi wakielekea Pangani na muda huo tayari walikuwa wanaimaliza barabata ya Taifa wakiingia katika mzunguko wa magari unaounganisha barabara nne zikiwemo barabara ya Taifa, barabara ya Pangani, barabara ya jamhuri na barabara iendayo kukutana na barabara ya Chuda. Waliuzunguka mzunguko huo wa unaounganisha barabara hizo na wakafuata barabara ya pangani kwa mwendo wa wastani kutokana na uwepo wa baiskeli nyingi zikiwa zimebeba wasafiri, walitembea kwa mwendo huo hadi walipofika jirani na duka la dawa la Mang'ombe.

Hapo walijikuta wakiingiwa na moyo wa huruma na kusimamisha gari baada ya kijana mwenye asili ya kisomali aliyekuwa amevalia kinadhifu alipowapungia mkono kuwasimamisha, waliegesha gari pembeni na kijana huyo aliwaomba wamsaidie afike Pangani kwani alikuwa ameibiwa pesa yake yote ambayo ingemtosha kuifanya nauli ya kuelekea huko. Kijana huyo alikubaliwa kwa moyo mkunjufu kupanda gari hilo kutokana na moyo wa kusaidia watu alionao Hamis, alipanda kwenye gari akakaa kiti cha nyuma na safari ikaendelea kama kawaida. Njiani maongezi yalitawala kwenye gari hilo kutokana na ucheshi mkubwa aliokuwa nao huyo kijana ambao uliwavutia sana kwani alitokea kuchangamsha safari yao isionekane imepooza, Hamis ndiye alikuwa dereva wa gari hilo na alionekeana kutendea gia za gari hiyo kwa kubadilisha gia moja na kwenda nyingine na mwendo wa gari aliuzidisha kutokana na uchache wa magari.

Baada ya mwendo takribani saa moja wakiwa njiani mvua kubwa ilianza kunyesha na ikamlazimu Hamis apunguze mwendo ili kuepuka ajali kwani mvua hiyo ilifanya kioo cha gari kiweke ukungu kwa ndani na kusababisha iwe tabu kuona mbele, ukungu ulipozidi Hassani aliufuta kwa kitambaa kilichopo ndani ya gari.

"Dah hili eneo kila nikipita huwa nakuta mvua" Yule kijana aliongea
"Labda ulipita kipindi cha mvua tu ila si kila muda tu linakuwa na mvua, hivi unaelekea Pangani sehemu gani?" Haasani aliongea kisha akamuuliza swali huyo kijana.

"ninaelekea Kuani kumuona babu yangu maana ni muda sijamtembelea" Yule kijana alimjibu.
"Imekuwa kama bahati na sisi tunaelekea hukohuko sasa nafikiri utafika moja kwa moja hadi huko, si tunaenda kumuona mzee Mafindo nafikiri unamfahamu" Hamis naye aliongea huku akibadilisha gia ya gari.

"Said Humud au ukipenda gaza wa mafindofindo, ndiye babu yangu ninayeenda kumtembelea imekuwa kama bahati yaani ila bahati hii imeingia dosari" Kijana huyo alianza kuongea kwa uchangamfu hayo maneno yake lakini mwishowe akamaliza akiwa amekunja sura na macho yakawa mekundu.
"Kijana unamaanisha nini?" Hassani aliuliuza huku akimtazama yule kijana lakini alijikuta na hofu zaidi baada yakuona sura ya yule kijana imebadilika na kuwa ya hasira"
"Unataka kuelewa siyo? Haya ngoja nikueleweshe" Yule kijana alisema kisha akajibadilisha sura na kuwa ya mtoto yule aliyewatokea watoto wa mzee Buruhan muda mfupi tu kabla hawajafa kwa kuuawa na mikono yake.

"Ushaelewa au bado unataka uelewe zaidi" Yule mtoto alimuambia Hassan ambaye alipatwa na mshtuko sana baada ya kuiona sura ya yule mtoto.
"Jamadin! Hapana siyo wewe" Hassan alisema na kupelekea Hamis naye ageuke aangalie kwani aliona kama ameangalia vibaya alipotumia kioo cha kati, Hamis alijikuta akikanyaga breki ya gari lakini gari halikusimama bali ndiyo lilizidi mwendo.
"Hamuwezi kunikimbia nyinyi wanaharamu na huu ndiyo mwisho wenu" Yule mtoto wanayemtambbua kwa jina la Jamadin aliongea kwa hasira kisha akamuangalia Hassani akamuambia, "nipe kile ".

"Si....sina"Hassani aliongea kwa uoga huku akiweka mikono ishara ya kuomba msamaha lakini alijikuta akipigwa shingoni na mkono wa yule mtoto hadi kichwa chake kikakatika na kuruka kwenye mapaja ya Hamis na damu zikawa zinatoka kwa wingi, Hamis alijikuta anatoa yowe la woga baada ya kichwa cha Hassani kutua kwenye mapaja yake hadi akajikojolea papo hapo.

"Mjomba leo ndiyo unakuwa na uoga siyo wakati mlipokuwa mkifanya yenu wala hakuwa unaogopa, nadhani umetambua kuwa ubaya huzikwi nao bali unalipwa hapahapa na leo ndiyo hukumu yako" Yule mtoto aliongea kisha akampiga Hamisi ngumi ya kichwa iliyotoboa kichwa chake hadi ubongo na mabonde ya damu yakaruka kwenye kioo cha mbele.

Huo ndiyo ukawa mwisho wa Hamis na Hassan katika dunia hii baada ya kupatiwa malipo kwa kila walichokitenda kwani ndiyo mwisho wa yoyote afanyaye balaa kana walilolifanya wao, hakika mshahara wadhambi ni mauti kama wahenga walivyonena tangu zamani na ndiyo kilichowapata Hassani na Hamis.

Siku zote mchimba kaburi huingia mwenyewe ndiyo atafanikiwa kulichimba haitotokea mchimbaji wa kaburi akachimba kaburi na kulimaliza pasipo kuingia yeye mwenyewe, Hamis na Hassani hivyo hivyo ni wachimba kaburi waliochimba kaburi na wakaingia ndani yake na matokeo yake wakakutwa na kisanga kizito kilichosababishwa na uchimbaji wao wenyewe. Walichimba kaburi pasipo kujua kama kaburi hilo litakuja kuwazika wenyewe na wamekuja kujua kuwa kaburi hilo ni kaburi lao wenyewe na wamekuja kujua tayari wameshachelewa, laiti wasingefanya hivyo tangu awali wangekuwa ni miongoni mwa waliosalimika hadi muda huo.

****
Baada ya dakika takribani kumi tangu Hassani na Hamisi waiage dunia, hali ilikuwa shwari katika jiji la Tanga na hakuna aliyekuwa na habari ya kutokea kwa tukio la kinyama katika barabara ya Pangani likiwahusisha watu maarufu waliouawa kinyama kutokana na kisasi kizito cha mabaya waliyoyafanya kipindi cha nyuma. Nyumbani kwa mzee Buruhan muda huo alitembelewa na rafiki yake kipenzi aitwae Mahmud ambaye anafahamika sana huko Mkinga kama mganga maarufu sana na aliyetatua matatizo mengi yaliyowakumba watu na familia zao na hata yenye utata. Mzee huyu alikuja kwa lengo la kumpa pole rafiki yake kipenzi kutokana na vifo hivyo kwani hakuwepo ndani ya Tanga kipindi msiba unatokea na ndiyo amerejea na ameamua kupitiliza nyumbani kwa rafiki yake moja kwa moja baada tu ya kupumzika nyumbani kwake. Mzee Mahmud alikaribishwa kwa utiifu na rafiki yakr kipenzi na akapatiwa kinywaji anachokipendelea kila awapo nyumbani kwake, alikaribishwa kahawa na rafiki yake huyo kisha wakachukua bao wakaenda kwenye kibaraza cha nyumba ya mzer Buruhan wakakaa na wakaanza kucheza kama ilivyo kawaida yao.

"Mzee mwenzangu unajua kazi zetu hizi za kuagua zilinitoa huku Tanga nilipozaliwa na kukulia hadi Mombasa nikaenda kumuagua bwana mmoja aliyetupiwa jini zito, basi hiyo shughuli ilinichukua mwezi na nusu na hadi namaliza huku mshazika ndiyo maana hukuniona" Mzee Mahmud aliongea huku akiwa na kikombe cha kahawa mkononi.

"pole na majukumu mzee mwenzangu ndiyo kama nilivyokueleza yaliyonifika na hata sijui chanzo chake nini?" Mzee Buruhan aliongea kwa unyonge.
"haina haja ya kuhuzunika mzee mwenzangu bali inabidi uwalaumu wanao na janga hili mzee mwenzangu limeanzwa na wao na sasa mwenzao wanalimaliza" Mzee Mahmud aliongea kisha akanywa kahawa funda moja bila hata kumtilia maanani Mzee Burhan aliyeonekana kutoielewa kauli hiyo.
"Mzee mwenzangu mimi ni rafiki yako wa muda mrefu sana na kuhusu hili suala jua mwanao mkubwa analielewa fikra, na kama yupo tayari kuliweka bayana utabaki na nguzo tu lakini kama hataki kuliweka bayana hutabaki na nguzo hata moja" Mzee Mahmud alizidi kuongea maneno yaliyomfanya Mzee Buruhan abaki akimtazama kwani anamtambua fika ni mganga mwenye uwezo mkubwa wa kujua yaliyojificha.

"Sijakuelewa mzee mwenzangu" Mzee Buruhan alisema huku akimtazama Mzee Mahmud kwa umakini, Mzee Mahmud alipotazamwa alitoa tabasamu tu kisha akasema, " zamu yako kucheza mimi nishalala mzee mwenzangu".

Mzee Buruhan aliacha kumtazama akaliangalia bao kisha akachukua kete akaanza kucheza huku akiwa njia panda kutokana na kauli ya Mzee Mahmud ambaye huwa hafafanui akishaeleza mambo kama hayo halafu akabadili mada ghafla.

Maneno ya mzee Mahmud bado yalibaki ndani ya kichwa chake ingawa yalikosa ufafanuzi wa kutoka kwa mzee huyo aliyebobea katika uganga, Mzee Buruhan aliendelea kucheza bao huku akiwa na mawazo sana juu ya maswali ya maneno ya utata aliyoambiwa na mzee Mahmud. Hadi alipolala katika mchezo huo wa bao bado mawazo lilikuwa juu ya maneno hayo, mzee Mahmud alipoanza tena kucheza bao huku ameinamisha kichwa chake akitazama kwenye bao kwa umakini hakujua kama mzee mwenzie alikuwa akimtazama sana kichwani mwake na alitamani hata akione ndani hicho kichwa chake ili atambue ni nini anachowaza lakini suala hilo lilishindikana kabisa kwani yaliyomo katika ubongo wa mtu huwezi kuyaona hata ukipasua kichwa chake na kuangalia ndani.

"Kuna kisa cha zamani sana mzee mwenzangu nakikumbuka hadi leo hii katika kichwa changu, hakika wahenga hawakukosea kukitunga kwani ni kisa kinachohusu vijana wawili waliompenda msichana mmoja kigori huko mashariki ya mbali" Mzee Mahmud alianzisha mada nyingine huku akiendelea kucheza bao na safari hii alikuwa anamtazama mzee Buruhan usoni mwake akiwa na tabasamu hafifu.

"Mzee mwenzangu kama kawaida hukaukiwi visa vyenye mafunzo na kuburudisha, hebu nipe habari bwana" Mzee Buruhan alimuambia mzee mwenzie ili apate kusikiliza kisa kutoka kwake kwani mzee Mahmud alikuwa akijulikana kwa jinsi alivyokuwa hodari kwa kusimulia visa na hadithi zenye kufundisha, hakika taaluma ya fasihi simulizi ya wakati wa zamani bado ilikuwa ipo ndani ya halmashauri ya ubongo wake ingawa alionekana kuzeeka sana.
"Katika kijiji kimoja cha jamii ya wastarabu alizaliwa binti mmoja mrembo sana aliyeitwa Giguna katika familia yenye hadhi duni sana katika Jamii ya Watarabu, binti huyo alianza kuwa gumzo kijijini happ tangu akiwa mdogo kutokana na uzuri aliokuwa nao uliokuwa wa ajabu sana. Hadi anavunja ungo ilikuwa ni habari nyingine katika kijiji hicho kwani vijana wa rika lake walikuwa wakimtamani kila kukicha kutokana na umbo maridadi alilokuwa nalo, haikuwahi kutokea binti mwenye umbo kama lake ambalo lilijaa utata mtupu tena alijaliwa kuwa na kiuno kilichojitenga kama mdudu Mavu.

Usoni alikuwa na sura yenye mvuto wa ajabu sana na jicho lenye umbo la nusu mwezi, Giguna alikuwa ni binti mrembo haswa na kila alipokuwa akiwatazama wavulana wa rika lake walidhani kuwa wanaitwa lakini haikuwa hivyo bali asili ya jicho lake ndiyo lilimchengua sana kila mvulana. Ilipotimia majira manne ya mwaka katika kijiji hicho walihamia familia ya wasafiri kutoka mbali ambao walipenda sana kuweka makazi katika kijiji hicho na walipewa ukaribisho mkubwa kutoka kwa kiongozi wa kijiji hicho, familia hiyo nayo ilikuwa gumzo kijiji hapo kutokana na kuwa na kijana aliyekuwa na mvuto wa ajabu na usafi uliopitiliza kuliko hata vijana wengine wa kijiji hicho. Kijana huyo alijulikana kama Mufedi ambaye alikuwa na asili mchanganyiko iliyomfanya awe na nywele za kipekee sana ambazo hata angeishi bila chanuo basi zingeonekana ni nzuri sana na zipo kama zimechanwa.

Mufedi alikuwa ni mtu wa kukaa na vijana wenzie wa rika lake hadi wakamzoea kutokana na ucheshi wake alionao ambao uliwafanya vijana wenzake wafurahi kila kukicha, ndani ya muda mfupu tu katika kijiji hicho tayari Mufedi alikuwa yupo midomoni mwa mabinti wa kijiji hicho kama ilivyo kwa Giguna alivyokuwa yupo katika midomo ya wavulana wa kijiji hicho. Ilifika kipindi hata wasichana wa kijiji hicho wakawa wanakuja nyumbani kwao Mufedi na kumsaidia mama yake Mufedi kazi mbalimbali wakiwa na lengo tu la kuiona sura ya Mufedi jinsi ilivyokuwa ni nzuri na yenye kuvutia, baadhi ya wasichana waliokuja hapo nyumbani kwao Mufedi na kumuona akiwa sehemu kubwa ya kifuani mwake haijastiriwa walikiri kwamba alikuwa ni mvulana mwenye uzuri wa ajabu. Maneno ya chini kwa chini juu ya uzuri wa ajabu alionao kijana huyo yalienea hapo kijijini kama ilivyokuwa akisemwa Giguna na wavulana wa kijiji hicho, muda wote huo si Giguna wala Mufedi aliyewahi kumuona mwenzake kwa macho na kila mmoja alisikia sifa za mwenzake kupitia marafiki zake. Siku moja ambayo ndiyo ilikuwa chanzo cha kuanzishwa kitu ambacho hakikutarajiwa kuanzishwa ndiyo siku ambayo wawili hawa kwa mara ya kwanza walionana, siku hiyo Mufedi alikuwa akiongea na marafiki zake vipenzi walioitwa Nikeze na Nunele.

Giguna siku hiyo aliagizwa kupeleka mzigo nyumbani kwao Mufedi baada ya wazazi wake na mufedi kufanya biashara ya kubadilisha mali kwa mali kwani kipindi hicho bado fedha zilikuwa hazijaanza kutumika. Ilikuwa ni muda mrefu Giguna alikuwa hajaonekana kutokana na kuwasaidia sana wazazi wake na bibi yake kazi za hapo nyumbani kwao, eneo alilopita ndiyo walikuwa wamekaa Mufedi, Nikeze na Nunele wakipiga soga na kuchia vicheko. Giguna alipokaribia Nikeze alimuita lakini hakuitikiwa ndipo Nunele alipomuita akasimama kutokana na heshima aliyokuwa nayo, Nunele na Giguna walikuwa ni ndugu wa damu na Nunele ndiyo mkubwa kwa Giguna. Hivyo Giguna alijongea hadi walipo akiwa amejitwisha furushi kichwani lililokuwa na mzigo aliotumwa kuupeleka, hapo ndipo kwa mara ya kwanza Giguna alimuona Mufedi na Mufedi alimuona Giguna na wakaongea kwa lugha ya macho na nyoyo pasipo wengine kutambua wanachozungumza.

"Giguna u waitwa wanyamaza si vizuri hivyo" Nunele alimuambia Giguna baada ya kunyamazia salamu ya Nikeze.
"Kaka nataka wahi nilipotumwa niweze wahi rejea" Giguna aliongea kwa sauti nyororo huku akimtazama Mufedi kwa jicho la kuibia.
"hapana dada sifanye hivyo muache wslau akusindikize kidogo tu hutachelewa kurudi" Nunele alimuambia kisha akampa ishara Nukeze amfuate Giguna, Nukeze hakufanya ajizi alimfuata Giguna na taratibu akaanza kwenda huku akiongea kwa maneno ambayo hayakusikiwa na yoyote zaidi yao wenyewe. Huo ndiyo mwanzo uliozua safari nyingine kabisa isiyosafiriwa kwa umbali mrefu, ilikuwa kama ukurasa ila haukuwa na karatasi. Siku na siku zilisogea na hatimaye dalili za dhahiri kabisa zikachipuka na kuonesha kila mmoja alikuwa akimuhitaji mwenzake, katika msogezo huo wa siku ndipo ikafika siku ambayo haitasahaulika kwenye ukurasa mpya wa upendo ulioanza kuchipuka katika mioyo yao" Mzee Mahmud aliweka kituo hapo katika kusimulia na kumuangalia Mzee Buruhan ambaye alionekana kuwa na hamu ya kuendelea kuisikiliza hicho kisa anachosimuliwa.
"Aaaah! Mzee mwenzangu wakatisha pasipo stahiki kukatishwa" Mzee Buruhan alimlaumu mzee Mahmud kwa kukatishiwa uhondo mwanana uliokuwa unapita kwenye masikio yake na kujenga taswira kwenye ubongo wake kama vile alikuwa anaangalia sinema ya kile anachosimuliwa na kusikiliza simulizi tu.

"Weka mafuta kwanza tuendelee na safari huoni kikombe kitupu hicho na birika lina mafuta tele ya kunifanya niendelee kutoa burudani" Mzee Mahmud alimuambia mzee Buruhan huku akimpa kikombe chake cha kahawa ili aongezewe kahawa aweze kuendelea kusimulia.
"simulia walau kidogo basi mzee mwenzangu huku nakuongezea kahawa" Mzee Buruhan alimuambia Mzee Mahmud akiwa amenyanyua birika la kahawa ili amuongezee kahawa.

"Basi bwana siku hiyo si wakaombana namba za simu ili waweze kuongea vizuri maana ya vijana unayajua" Mzee Mahmud aliamua kusimulia kitu kingine kabisa tofauti kabisa na kufanya Mzee Buruhan amtazame kwa mshangao.
"Ushaanza visa vyako tayari mzee mwenzangu, sasa umesema zamani na hizo namba za simu zimeingia vipi" Mzee Buruhan alimuambia Mzee Mahmud huku akianza kucheka.

"Sasa si wewe unalazimisha gari kwenda wakati mafuta yamekwisha, umeona wapi likatembea huku likisubiri mafuta" Mzee Mahmud aliongea huku akicheka kidogo na kusababisha Mzee Buruhan acheke kwa nguvu kutokana na vituko vya mzee mwenzake.
"Yaani mzee mwenzangu hubadiliki kabisa tangu upo kijana tabia ni zile zile tu" Mzee Buruhan aliongea huku akimtilia kahawa mwenzake.
"ewaaa! Mambo si hayo sasa twende kazi" Mzee Mahmud aliongea huku kisha akinywa kahawa kidogo.
"sasa endelea mzee mwenzangu usikatishe habari" Mzee Buruhan alimuambia.

"Siku hiyo ilikuwa ni majira ya jioni baads ya jua kuzama, Giguna alicheleewa kuchota maji mtoni na ikambidi akimbie mara moja mtoni ili walau apate maji ya kuoga kwa usiku wa siku hiyo kwani ilikuwa ni kawaida kulala akiwa nadhifu usiku. Alipofika mtoni ndipo akakutana na Mufedi akiwa na kabeba vazi lake la juu lilionekana kuloa na alibakiwa na shuka kubwa aliyojifunga kiunoni iliyofika juu ya kitovu, kitendo cha wao kuonana tu walibaki wakitazamana tu kwa muda mrefu bila hata kusema chochote. Walikuwa wapo kwenye njia nyembamba iliyochongwa baada ya miguu ya watu kukanyaga nyasi hizo kwa muda mrefu hatimaye baadhi zikakauka na kufanya njia, ilikuwa lazima mmoja ampishe mwenzake kwenye hiyo njia ili apite kwani haikuwa inatosha kupishana. Kwa ufinyu wa njia hiyo hakuna aliyefanya hivyo wote walisimama tu wakizamana tu hatimaye Mufedi akajikaza akamshika Giguna bega, walisogeleana karibu zaidi na muda huo hakuna yoyote aliyetambua nini wanafanya kwani walijikuta wamefikwa na hisia za ajabu kila mmoja kutokana upendo walionao kwa mwenzake.

Ule usemi aliousema nabii wa Mungu kwamba kwenye watu wawili wa jinsia tofauti basi watatu wao atakuwa ni ibilisi ndiyo ulijidhihirisha hapo na wakajikuta wameingia sehemu isiyotakiwa kuingilika, tangu siku hiyo ndiyo ukurasa haswa wa mapenzi ya dhati baina yao ukafunguliwa na mapenzi ya siri baina yao yakawa yanaendelea. Katika kipindi hicho ndipo Mufedi alipokuja kubaini kwamba Nukeze alikuwa akimtaka Giguna kwa muda mrefu lakini hakukubaliwa kabisa ndiyo maana hata siku ile alipomuita hakuitika kutokana na kuchoka usumbufu wake, mapenzi baina yao yaliendeshwa kwa usiri mkubwa na hawakumueleza yoyote hadi pale siku moja mmoja wa watu hapo kijijini alipokuja kubaini uhusiano huo. Ginota rafiki kipenzi wa Giguna ndiye mtu aliyekuja kufahamu uhusiano huo baada ya kuwakuta wakitoka kuvuja ile amri sijui ya ngapi ya imani ya wenzetu hao, siku hiyo ilibidi Giguna amuambie ukweli juu ya uhusiano wao na akamuapiza kumtunzia hiyo siri pasipo kujua anamuaminisha nyoka.

Giguna jambo ambalo hakuwa analijua ni kwamba Ginota ni mmoja kati ya wasichana waliokuwa wamezama kabisa katika kumpenda Mufesi lakini hakuwahi kumuambia Giguna kwasababu ana mahusiano na Nunele na laiti angemwambia ungekuwa ugomvi kati yao kwani Giguna asingekuwa tayari kuona kaka yake Nunele anasalitiwa. Pia katika jambo ambalo Giguna hakulitambua ni kwamba Nukeze alikuwa akimtumia sana Ginota katika kumshawishi Giguna amkubali lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwani macho ya Giguna hayukutamani hivyo moyo wake haukuhitaji, kumbuka macho yasipotamani moyo hauwezi kuhitaji. Ginota hakuweza kustahimili kuona rafiki yake kampata mwanaume aliyekuwa anagombewa hapo kijijini na wasichana wote kama vile ni lulu yenye thamani, Ginota aliifikisha habari hiyo kwa mpenzi wake Nunele na kupelekea taarifa hiyo ifike kwa Nukeze.

Hapo ndipo vita mpya ya mapenzi ilipoanza chini kwa chini, Nunele na Nukele walikuwa wanacheka na Mufedi kwa jino pembe tu lakini walikuwa wakipanga kumuua Mufedi kila muda lakini ilishindikana na kila walipoenda kwa waganga ili wamuue kazi yao ilikataliwa na mwisho wake wakafanya kitu ambacho kilimuumiza sana Mufedi na ikawa ndiyo mwisho wa mapenzi ya Giguna na Mufedi. Waliamua kwenda kwa mganga wakafanya dawa ili ambayo walimtilia Giguna kwenye maji ambayo alikuwa anakunywa na alipoyanywa ndiyo ikawa mwanzo wa Giguna kumpenda Nukeze na Mufedi kukosa penzi lake baada ya kukataliwa wazi na kutolewa maneno yasiyofaa na Giguna. Mufedi alidhani utani lakini alikuja kujua ni kweli baada ya kutaka penzi mtoni wakati Giguna alipoenda kuchota maji, Giguna alipiga kelele ya kuwa anavakwa na kusababisha watu wajae na Mufedi aliambulia kipigo nusura afe. Tangu siku hiyo Mufedi hakumgusa tena Giguna na alipopona tu aliondoka kijijini hapo akiiacha familia yake baada ya wanakijiji kutomuhitaji, huo ndiyo mwisho wa kwanza wa simulizi hii na muendelezo utaujua mzee mwenzangu tuombeane uzima tu" Mzee Maud aliishia hapo kuelezea simulizi hiyo.

"Mzee mwenzangu unajua ninamuonea huruma sana huyo kijana yaani naona kama nimefanyiwa mimi hivyo" Mzee Buruhan aliongea baada ya kuisikiliza hiyo simulizi kwa umakini.
"Fahari yetu waswahili kujaliwa sanaa inayokuteka akili zako ukaona kama tukio ni la kweli" Mzee Mahmud aliongea huku akimalizia kikombe cha kahawa.

"Yaani hata bao nimesahau kulicheza" Mzee Buruhan aliongea huku akitabasamu.
"Mzee mwenzangu huku leo silali naondoka maana narudi Mkinga leo leo nimekuja kukupa pole tu ujue sijakutupa rafiki yako wa toka utotoni" Mzee Mahmud alisema huku akinyanyuka kivivu.
"Haya mzee mwenzangu ngoja nikuitie kijana akutoe na usafiri hadi Makorora ukapate gari ya kurudi nyumbani" Mzee Buruhan alimuambia mzee Mahmud.

"Hasbuk mzee mwenzangu shukran sana muache kijana apumzike mimi nitatumia sehewa hapo tu niende chapuchapu haina haja ya gari" Mzee Mahmud aliongea huku akitembea na Mzee Buruhan akawa anamsindikiza, walitoka hadi nje ya nyumba eneo linaloegeshwa baiskeli nyingi za kukodisha. Mzee Mahmud alikodi moja na dereva wake akamuaga Mzee Buruhan akaondoka.

****

Majira ya jioni kwa huku duniani upande mwingine wa himaya isiyokuwepo juu ya ardhi ya wanadami tayari kikao kilikuwa kimeshawekwa ndani ya chumba maalum cha mkutano, ilikuwa ni ndani ya himaya ya Majichungu katika ya bahari ambapo ndiyo makazi ya majini wasiyohusika na utumikishwaji katika nguvu za giza. Ndani ya chumba hiki cha mkutano walikutana viongozi mbalimbali wa himaya hiyo baada ya mkutano wa dharura kufanywa ghafla kutokana na hali inayokuja mwezi mmoja baadaye iliyoonwa na jicho la Salmin ambaye naye alikuwa ni mmoja kati ya waliohudhuria mkutano huo akiwa pamoja na baba yake mzazi. Hali iliyokuwa inatarajia kuingia hapo mwezi mmoja baadaye ilikuwa ni hali ya kutishia usalama wa viumbe wote waliokuwa majini kwa asili zote kasoro wale wa mchanganyiko ndiyo pekee wangeweza kusalimika na mkasa huo na si vinginevyo, ilikuwa ni lazima hali hiyo idhibitiwe haraka iwezekanavyo lasi hivyo himaya hiyo itakumbwa na na balaa kubwa sana.

"Jamani hali ni tete katika himaya yetu na tusipofanyia ufumbuzi suala hili basi tujue himaya yetu itakubwa na balaa kubwa, hebu tumsikilize Salmin atuambie ni nini alichokiona katika maono yake ya kuona mambo yajayo" Zalabain alifungua mkutano huo kwa maelezo hayo.

"Asante sana kiongozi wetu na mfalme mtarajiwa wa himaya hii kwa kunipa nafasi hii, hali halisi inayokaribia kutufikia ni ujio wa wadudu kutoka himaya ya giza baada ya wao kubaini kuna ukosefu wa giza kwa muda mrefu katika himaya hii baada ya kufariki kwa mtukufu mfalme. Viongozi wa himaya ile ambao ni maadui wakubwa wa himaya hii wameona ndiyo njia pekee ya kuidunisha himaya yetu kwa kutuma wadudu watakaoachia vimelea ambavyo vikimpata jini yoyote ambaye hana damu ya binadamu yaani ambaye hajachanganyika au hajatokana na uzao wa binadamu na jini itakuwa ndiyo mwisho wa maisha baada ya vimelea hivyo kumtesa kwa muda mfupi tena kwa maumivu. Balaa hili namaanisha tutakaopona ni mimi na mfalme mtarajiwa tu ikiwa halitozuiwa ila kama likizuiwa ni himaya nzima itasalimika, hivyo mchango wenu ndiyo unahitajika katika kusaidia kulitatua hili janga" Salmin alitoa maelezo yake.

"wote tumemsikia Salmin mwenye nguvu kuliko sisi sote akitueleza juu ya kinachokuja kutokea ikiwa tu hatutalichukulia hatua hili suala. Sasa basi nimewaita hapa ili tujadiliane kwa pamoja kama ilivyo kawaida yakitokea matatizo kama haya huwa lazima viongozi wa himaya hii wahusishwe, nitasikiliza maoni yenu kila mmoja kuhusu hili suala" Zalabain aliongea, halafu akawatazama wote waliomo humo ndani mmoja baada ya mmoja na macho yake yalitua kwa mkuu wa majeshi wa himaya ambaye macho yake yaliwaka kama taa kuashiria ana jambo anataka kulisema.

"Ndiyo Jenerali" Zalabain alimuambia mkuu huyo wa majeshi wa himaya hiyo huku akimuashiria asimame, mkuu wa majeshi alisimama kisha akatoa heshima kwa Zalabain na wengine waliopo hapo ndani kisha akasema, "Kiongozi wetu mkuu na viongozi wengine napendekeza tuwawahi hao wanamajini wa himaya ya giza kabla hata hawajawaachia hao wadudu kuja huku, najua wadudu wote wanaotaka kuwaachia bado watakuwa wanawaunda kwani wangekuwa tayari wangeachiwa muda wowote. Hivyo mimi napendekeza tutume jeshi liende kwa siri likaharibu huo utengenezaji wa hao wadudu itakuwa tumeiokoa himaya nzima kuliko njia nyingine yoyote".

Mkuu wa majeshi alipomaliza kutoa kauli hiyo alikaa chini na viongozi kadhaa wakanyoosha mkono kuashiria wamekubaliana na hilo wazo la mkuu wa majeshi, upande wa mawaziri wa himaya hiyo mmojawapo macho yake yaliwaka kuashiria anataka kuongea.

"Ndiyo waziri tunakusikiliza" Zalabain alimuambia waziri huyo ambaye alisimama akatoa heshima zote halafu akasema, "Kiongozi wetu mtukufu nimekaa katika himaya hii kwa muda wa miaka 4000 hadi inatimu siku hii ya leo ninapopokea taarifa hii, katika miaka hiyo yote nimeshuhudia balaa kama hili liliwahi kutaka kutokea kwa kutengenezwa viumbe wenye sumu na himaya hiyo hiyo ya nguvu za giza lakini kwa masaada wa Dainun ya kale ambayo muda wake uliishia siku ile alipotawafu babu yako. Hivyo basi kinga mpya ya balaa hili ni kupatikana kwa dainun mpya ambayo ilikuwa ipo mikononi mwa hayati baba yako ndiyo itasaidia kuzuia haya mabalaa milele mpaka utakapoiacha dunia hii"
"Asante kwa maoni yako waziri, mzee Zultash ongea" Zalabain aliongea kisha akamruhusu baba yake Salmin aongee baada ya macho yake kuwaka. Mzee Zultash alisimama akatoa salamu kwa wote waliomo humo ndani pamoja na kuonesha heshima kwa viongozi wakubwa.

"Asante kiongozi wetu, mimi hapa
naungana na wazo alilolitoa mkuu wa majeshi la kwenda kuharibu utengenezwaji wa hao wadudu kwani sote tunatambua kwamba Dainun mpya imeibiwa na mpaka ije kupatikana hatujui itatuchukua muda gani kwani hao viumbe wataingia ndani ya himaya hii mwezi ujao. Kumbukeni mwezi kwetu tunauona kama juma moja analoliona mwanadamu wa kawaida, sasa hamuoni hapo tutakuwa tumechelewa na maafa yatakuwa yameshatufikia jamani" Mzee Zultash aliongea na viongozi wote wakamuunga mkono hata yule waziri aliyetoa hoja ya kutafutwa Dainun naye alimuunga mkono.
"Kama ilivyo sheria yetu inavyosema, hoja ikiungwa mkono zaidi imepita. Basi jeshi la makomandoo litumwe kwenda kuharibu utengenezaji wa wadudu hao huku nikiwa naisaka Dainun kwani mwenye kuimiliki kashajulikana" Zalabain aliongea.

Kikao kilikwisha muda huo huo na maandalizi ya kikosi cha kuokoa himaya ya Majichungu yalianza mara moja, Kikosi kilichokuwa chini ya Salmin na mkuu wa majeshi ndicho kilichopewa jukumu zima la kuiokoa himaya hiyo. Vizuizi vya himaya hiyo vilifunguliwa na kikosi hicho kilitoka haraka sana na kisha vizuizi vikafungwa tena ili kuzuia himaya hiyo isivamiwe na maadui kwa ghafla, kikosi hicho kilitumia nguvu zao za ajabu za kijini kusafiri pasipo hata kutumia usafiri wa aina yoyote kama ilivyozoeleka kwa wanadamu wanapotaka kwenda mahali.

Majini haya yalikuwa yakielea katika anga la chini ya bahari kwa kasi sana yakielekea upande wa kusini wa himaya yao ambapo ni katika eneo lenye giza kubwa sana kiasi ambacho ingemlazimu mwanadamu wa kawaida kutumia mwanga wa aina yoyote kulivuka eneo hilo, lakini kwa hawa majini ilikuwa kawaida kwao kupita eneo kama hili bila kutumia nuru ya aina yoyote ile. Walipita eneo hilo lenye giza kwa mwendo wa kasi sana hadi walipokaribia eneo lenye miti mirefu ambayo ilienda juu pasipo kuonekana mwisho wake ilibidi wasimame baada ya kupokea amri kutoka kwa Salmin baada ya macho yake kuwaka kwa nguvu halafu yakazima.

"sasa tunaingia pori la giza linapakana na mapango ya Zabakut ambayo ndiyo hutumiwa na majini wataalam wa himaya ya giza kutengeneza viumbe mbalimbali kwa ajili ya kuangamiza himaya zingine, sasa basi katika pori hili kuna ulinzi mkali sana wa viumbe maalim waliotengenezwa mithilli ya miti ili kuwahadaa maadui wao wajue ni miti yote hii halafu wawaue kabla hata hawajalivuka hili pori. Umakini wenu unahitajika kwani hakuna njia nyingine ya kufika kwenye mapango ya Zabakut zaidi ya hii kwani hii miti haina mwisho urefu wake hivyo hatuwezi kupita kwa juu, nadhani tumeelewana sasa tuingie tukiwa pamoja na si kugawanyika makundi" Salmin alihitimisha hapo akatoa ishara na kikosi chote kikaanza kuingia katika msitu huo kwa pamoja, walipoingia ndani ya pori hilo walipokelewa na giza nene zaidi hata ya lile walilolipita mwanzo na ukimya mkubwa sana ambao unatisha sana na laiti angehema mtu basi ungemsikia papo hapo. Walipita kwa umakini sana na kutembea kwao kulikuwa kwa umakini sana ili wasije wakaingia katika mikono ya maadui zao, walipofika katikati ya msitu mmoja wa wanajeshi wa kikosi chao aliyekuwa nyuma alitoa ukelele wa maumivu uliovuma pori zima na kuwafanya wenzake wageuke kwa haraka

****

Upande wa nyumbani kwa Shafii ilikuwa tayari usiku umeshaingia na Bi Farida alikuwa yupo sebuleni akiongea na Jamal, Shafii alikuwa yupo chumbani kapumzika muda huo kutokana na kunywa dawa kali sana ambazo zilimlazimu kulala usingizi mzito. Muda huo ndiyo ulikuwa muda ambao kidonda kingine kikubwa zaidi ya kile cha awali katika moyo wa Shafii kilijitokeza kwa namna isiyotarajiwa kabisa kama ingeweza kutokea, muda huo tayari watumishi wa nyumba hiyo walikuwa wamelala kutokana na kuwa ni usiku sana. Mtumishi peke wa nyumba hiyo aliyekuwa macho ni mlinzi tu ambaye alikuwa bado alikuwa na kibarua cha kuilinda nyumba hiyo kwa muda wa usiku. Bi Farida akiwa anaendelea na mazungumzo na mpwa wake sauti ya maji yakimwagika katika matanki yaliyopo nje ya nyumba hiyo kwa upande wa uani ilisikika, Jamali aliponyanyuka kwenda kufunga maji hayo Bi Farida alimuambia aache akafunge yeye kisha akainuka akaelekea ulipo mlango wa uani.

Bi Farida alifungua mlango na akatoka nje akakutana na mazingira tofauti na ya nyumbani hapo, aliona nje ya nyumba yake kulikuwa kuna giza lakini alipotoka nje katika baraza la uani aliona wingu jekundu limetanda juu angani na kufanya eneo lote liwe jekundu kama vile muda wa machweo ya jua. Alipoangalia katika ngazi za kushuka chini aliona rundo la viumbe waliovalia mavazi ya maaskari wa zamani katika vita vya mapanga huko katika himaya roma wakiwa wamejipanga mstari na ngazi zilionekana na ndefu mno tofauti na zilivyo ngazi za baraza nyumbani kwake, hali hiyo ilimshtua sana na na akaamua ageuze ili arejee ndani alipotoka akiwa anapiga makelele ya uoga akimuita Jamali lakini alijikuta akikaa kimya baada ya kuona mazingira ya mlango huo ni tofauti na mazingira ya mlango wa nyumbani kwake. Mlango huu ulikuwa wa dhshabu wenye mapambo mbalimbali ya kupendeza na mlangoni kulikuwana walinzi waliovaa makofia ya chuma wenye kimo kirefu tofauti na Binadamu wa kawaida, Bi Farida alijikuta anapiga kelele lakini mmoja wa walinzi alimnyooshea kidole na sauti yake ikakatika hapohapo ikawa haisikiki.

"Huyu mwanadamu anataka kutuzibua masikio sasa, yaani hajui kama sauti yake ni kubwa mno akiwa huku ndani ya himaya hii. Mchukueni nyinyi masikio yanatuuma sasa hivi" Mmoja wa walinzi aliongea kwa sauti nzito huku akiwa ameshika masikio kama ambavyo wenzake wote walivyokuwa wameshika masikio kutokana na kuumizwa na makelele ya Bi Farida, kauli ya yule mlinzi aliposema mchukueni hakuelewa anamaanisha nini na alikuja kuelewa baada ya kujikuta amezungukwa na wasichana watatu wenye urembo wa hali ya juu ambao haikujulikana walifika vipi hapo hadi muda huo.
Akiwa anajiuliza swali hilo wale wasichana walimshika mkono na akajikuta akitokea katika mazingira mengine akiwa pamoja nao hao wasichana, alijikuta akiwa yupo ndani ya chumba chenye mapambo ya kila aina ambacho ukubwa wake kilizidi kumshangaza na kumfanya azubae akishangaa hadi pale alipoondolewa mshangao wake kwa kusikia sauti ya isiyokuwa ngeni masikioni mwake.

"Mama" Ndiyo sauti ya kike aliyousikia ikitokea nyuma yake ambayo ilimfanya ageuke atazame alipoitwa.
"Zayinaa!" Bi Farida alitamka akiwa anaonekana kutoamini macho yake kwa kumkuta Zayina eneo hilo akiwa amevaa mavazi ya kifahari na vito vya thamani na alikuwa akipepewa na wanawake wawili wenye uzuri ambao haukuwahi kuonekana duniani na walikuwa na nywele ndefu na nyeusi kupitiliza.

****

Yule mwanajeshi mmoja aliyetoa ukelele katika kikosi cha kilichotumwa na himaya ya Majichungu alikuwa amezungukwa na mzizi mmoja wa mti ambao ulikuwa ulikuwa unatambaa kama nyoka na kitendo cha kupiga kelele ndiyo ikawa amechokoza nyuki waliofiwa na malkia wao na sasa hasira zote za nyuki zimehamia kwake. Mizizi ya ule mti ilianza kubadilika rangi na kuwa ua rangi sawa na uji wa volkano unaotoka baada ya mlima wa volkano kulipuka, mwanajeshi huyo wa kijini alijikuta akiteketea hadi akawa majivu.

Kelele za yule mwanajeshi kabla hajafa zilifanya eneo hilo la msitu lenye giza kuonekane macho yanayong'aa kama ya macho ya simba yakimulikwa na tochi gizani, macho hayo yalionekana kuwa mengi kila sehemu kuashiria kuna viumbe wengi ndani ya pori hilo walikuwa wamewaona na macho hayo yalizidi kusogea karibu kuashiria kuwa viumbe hao wanasogea karibu.

"Zaghari bekatu mudyosiye jikiteee, zaghari bekatu mudyosiye jikitee. Halkumisate fadyozile gaitak( Washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu, washeni nuru za macho yenu muda wa mapambano huu. Hakikisheni tunawamaliza tutizimize kazi)" Salmin alitumia lugha inayotumiwa na wanajeshi wa Majichungu pekee ikitokea dharura kama hiyo, lugha hiyo haikuwa inafahamika na kiumbe mwingine yoyote isipokuwa wanajeshi hao.

Wote kwa pamoja waliwasha nuru ya macho yao na kuwafanya waone pori zima kama mchana ingawa ilikuwa ni giza nene lipo porini hapo, hapo waliwashuhudia viumbe wenye maumbo kama miti wakiwa na wanawaangalia na wengine tayari wakiwa wamewazunguka wakiwa na macho yaliyojaa hasira. Viumbe hao walianza kuwashambulia kina Salmin na kupelekea utokee mpambano mkali kwani hadi muda huo tayari kikosi cha Salmin kilikuwa kimeshajianda, viumbe waliopo msituni hapo walijikuta wakipigwa vibaya na kikosi cha kina Salmin kwani nguvu zao ambazo waliamini wanazo wao peke yao walishangaa Salmin akiwa anazitumia baada ya kumgusa jini mojawapo wa himaya ya giza na kuzinyonya nguvu zake.

Mpambano ulipowazidia majini wa himaya ya giza mmojawapo alianza kukimbia ili akatoe taarifa ya uvamizi, jini huyo alikuwa ameshaonekana na Salmin ambaye alisoma mawazo yake akamjua lengo lake
Salmin alijigeuza mti kama viumbe wengine kisha akatoa mzizi mmoja mtefu ulioenda kumfunga yule jini halafu akamuunguza kama alivyowaunguzwa yule mwanajeshi aliyekuwa yupo upande wao, alirudi katika hali ya kawaida akaendelea kupambana hadi walipowamaliza majini wote wa himaya ya giza ambao walilala chini kama miti iliyoangushwa katika ukataji miti.

Salmin alianza kuwapiga miale ya radi majini hao mmoja baada ya mmoja na wakabadilika wakawa na maumbo ya majini wa kawaida ambao walikuwa wamevaa sare moja, alimvua mmojawapo sare akavaa yeye mwenyewe kisha akawaamuru wenzake wafanye hivyo. Baada ya muda mfupi wote walikuwa na sare zinazofanana kisha wakasonga mbele kuuvuka msitu huo.

****

Bi Farida alienda kumkumbatia mtoto wake kwa nguvu huku machozi ya furaha yakimtoka akiwa haamini kama angemkuta hapo, alijisahau kabisa kama yupo ugenini katika eneo asilolijua na akajikuta akiwa na furaha ya kumuona aliyesadikika ametekwa.
"Nani kakuleta huku mama?" Zayina alimuuliza mama yake baada ya kuachiana tangu walipokumbatiana.

"mimi ndiyo nimemleta huku" Sauti ya Zalabain ilisikika kisha akajitokeza akiwa ameongozana na mwanamke wa makamo aliyebeba chupa na beseni lenye rangi ya fedha, Bi Farida aliposikia sauti hiyo akageuka nyuma akakutana uso kwa uso na sura ambayo alihisi aliwahi kuiona mahali.
" we ni nani?" Bi Farida aliuliza huku akimkazia macho Zalabain.

"Kaka Jamadin huyo" Zayina alidakia kujibu na kumfanya mama yake ashangae kwani anatambua mwanae huyo alishafariki.
"Fanya kazi yako" Zalabain alimuambia yule mwanamke aliyekuja naye huku akiupuuzia mshtuko wa mama yake, yule mwanamke alimsogelea Bi Farida akampatia chupa aliyokuja bila hata kujali kama itapokelewa au haitapokelewa. Bi Farida aliipokea chupa hiyo akaifungua na akanywa kimiminika kilichokuwa kipo ndani yake hadi akamaliza, alimrudishia kile kichupa yule mwanamke na yule mwanamke akampatia beseni la rangi ya fedha alilokuja nalo.

Bi Farida alipolipokea hilo beseni tu alijikuta akibanwa na kichefuchefu cha ajabu na akainamisha kichwa humo ndani ya beseni akaanza kutapika vitu ambavyo vilimshangaza sana Zayina hadi akageuza shingo pembeni huku akiwa kaziba mdomo, mwisho wa kutapika alitapika kitu cha duara chenye mizizi ambayo ilikuwa inachezacheza kuashiria kina uhai. Baada ya kutapika hicho kitu Bi Farida alizirai papo hapo halafu akazinduka baada ya sekunde kadhaa huku akihema kwa nguvu, alipoinua macho yake akamuona Zalabain na akajikuta akimuita, "Faimu".
"Hapana mama ni Jamadin mwanao" Zalabain alimuambia Bi Farida.

"Mwanangu Jamadin" Bi Farida aliongea huku akiinuka akaenda kumkumbatia Jamadin hadi Zayina akatokwa na machozi.
"Nafurahi mama umetoka katika kifungo kizito ulichokuwa umefungiwa, Zayina njoo na wewe" Zalabain alimuambia mama yake kisha akamgeukia Zayina aliyekuwa akiwatazama, Zayina alisogea akaungana nao katika kukumbatiana.

****

Baada ya kuwamaliza majini wa himaya ya giza waliowekwa kulinda katika eneo la pori hatimaye walilivuka pori hilo na wakatokea katika eneo la mbele la mapango ya Zabakut, walikuta lango la kuingilia katika mapango hayo likiwa limefungwa na pembeni kukiwa na walinzi waliovalia sare kama walizovalia wao. Walitembea hadi kwenye lango hilo ambapo Salmin alitoa salamu ambayo hutumika na himaya hii na wenzake pia wakafanya hivyo, walinzi waliitikia salamu hiyo kisha wakafungua mlango bila kujua wamewaingiza maadui zao ndani ya sehemu yao ambayo hutumika haswa kutengenezea silaha zao hatari na za maangamizi.

Salmin akiwa mbele aliwaongoza wenzake kuingia ndani ya mapango ya Zabakut, waliingia mpaka ndani na wakafuata njia iliyochongwa vizuri kama ukumbi mwembamba wa nyumba unaotengenisha ambao hujulikana korido na waswahili wazungu katika nchi ya waswahili.

Pembezoni ya ukumbi huo katika ukuta kulikuwa kuna mafuvu ya binadamu yaliyokuwa yamepangwa safu moja na yalikuwa yakitoa moto ambao ndiyo ulitumika kama muangaza wa humo ndani ya pango, walitembea hadi sehemu yenye makelele mengi wakakuta lango kubwa sana lililokuwa na mlinzi mwenye kichwa cha nyoka na mwili wa kawaida. Waliposogelea mlango huo yule mlinzi anyoosha mkono na ardhi ya mbele yao kina Salmin ikapasuka na kuacha bonde kubwa na uji wa volcano ukaonekana ndani ya bonde hilo, Salmin aliliruka bonde hilo hadi upande wa pili akamfikia yule mlinzi na kumgusa begani halafu akasogea pembeni.

"Toa utambulisho wako" Yule kiumbe alimuambia Salmin huku akijiweka tayari kupambana.
"Mikaf kama wewe" Salmin alimuambia yule.

"mikaf huwa tunauwezo wa kugeuza ardhi vyovyote, mbona nimepasua hiyo hukuiunga upite" Yule kiumbe alimuuliza Salmin swali ambalo hakulijibu na alijigeuza akawa na kichwa cha nyoka kama yule kiumbe halafu akaiunga njia ile na kupelekea kiumbe yule atabasamu, wenzake walipita wakaja hadi pale alipo.

"Wafanyakazi wapya wa hazina hii, ni wataalam wamekuja kumalizia uundwaji wa silaha zetu" Salmin alimuambia yule kiumbe ambaye alifungua mlango akamruhusu aingie na wenzake akijua ni Mikaf kama yeye mwenye kugawa majukumu.

Mikaf ni majini wa himaya ya giza wenye uwezo wa kuongoza ardhi na udongo na kuupinda au kuufanya watakavyo, majini hawa katika himaya hiyo hufanya kazi ya usimamizi na ulinzi wa sehemu muhimu za himaya ya giza na hutambuana kwa kuoneshana nguvu zao tu. Salmin alivyofika jirani na yule Mukaf anayelinda tayari alikuwa ameshaijua hulka yake kwa kutumia uwezo wa ajabu alionao, pale alipovunja njia aliruka juu na kumgusa begani ambapo alichukua nguvu zake kutokana na uwezo wake alionao na alipoambiwa ajitambulishe ndiyo akaiunga njia akiwa tayari ameuchukua uwezo wa yule Mukaf.

Baada ya kuingia ndani ya eneo hilo kikosi cha Majichungu kiliona chupa mbalimbali zikiwa zimehifadhiwa wadudu wa ajabu wenye mabawa ambao walikuwa wakipiga kelele na kurukaruka, kila chupa ilikuwa imeungamishwa na fito za shaba maalum ambazo ziliingia kwenye mtungi mkubwa wenye kimiminika cha njano.

"wapo kwenye hatua ya mwisho ya ukuaji hawa, walikuwa wakitunzwa kwenye hizi chupa tangu watengenezwe sasa inabidi tumalize kazi yetu tuiokoe himaya yetu. Fanyeni kama nitakavyofanya" Salmin aliwambia wenzake kisha akaenda hadi kwenye mtungi mkubwa akaushika na wenzake nao wakamfuata wakafanya hivyo hivyo, alitoa miale ya radi mikononi iliyoingia humo na wengine nao wakatoa miale hiyo. Mitungi yote iliyowekwa wadudu hao ilipigwa na miale ya radi hadi wadudu hao wakafa wote na makelele ya wadudu hao yakaisha papo hapo kukawa kimya, baada ya kumaliza kazi hiyo Salmin alitumia nguvu za mukaf akakanyaga ardhi ikafunguka akaingia na wenzake wakaingia na kutoroka eneo hilo baada ya kazi yao kukamilika.

SURA YA SABA

Mlio wa maji kumwagika katika nyumba ya Shadii uliisha kuashiria kuwa koki ya maji ishafungwa na maji hayaingii kwenye matanki yaliyojaa, Jamali aliendelea kumsubiri shangazi yake atarudi kwa muda wa saa zima hakurejea na hapo ikamlazimu aende uani kuangalia huenda amekumbwa na tatizo kwani alikuwa hajamaliza kuzungumza naye na hakurejea ndani. Alifika hadi sehemu iliyokuwa na matanki ya maji ambapo kama maji yakijaa na kumwagika basi hujulikana wa eneo hilo kulowana hasa bustani ya maua ambayo imezunguka eneo lenye matanki ya maji, cha ajabu eneo hili lilikuwa kavu kabisa hakuna dalili ya kumwagika maji. Akiwa anashangaa hali hiyo alisikia sauti ya mjomba wake akipiga yowe la maumivu huko ndani na ikamlazimu kukimbia kuelekea chumbani kwa mjomba wake (muda huo Shafii anapiga yowe la maumivu ndiyo muda ambao Bi Farida alizirai kule kwemye himaya ya majini baada ya kutapika vitu visivyoeleweka).

Jamali alipofika chumbani kwa mjomba wake alimkuta akiwa ameanguka chini akiwa amekaukiwa na sauti, alimuinua na kumuweka kitandani ambapo Shafii alionesha ishara ya kutaka maji kwenye bilauri yaliyppo humo chumbani mwake mezani na ikamlazimu Jamali amletee maji upesi. Shafii alikunywa maji yote kwenye bilauri ndiyo akaweka kuongea na neno la kwanza kulitamka ni jina la mkewe, alipoona hamuoni mkewe alimuuliza Jamali mahali alipo shangazi yake. Jamali alimueleza kila kitu juu ya kutoonekana kwa shangazi na maajabu aliyoyaona, hali hiyo ilimshtua sana Shafii akabaki amechanganyikiwa.

"mpigie baba yako muambie aje hapa sasa hivi" Shafii alimuambia Jamali huku akimuonesha simu ilipo, Jamali alienda kupiga namba ya baba yake lakini haikuwa inapatikana na alijaribu zaidi ya mara nne lakini jibu ni lilelile.
"Haipatikani"Alimuambia mjomba wake

"He...hebu mpigie na Hassan usipompata piga nyumbani kwenu umuulizie baba yako" Shafii aliongea akionekana amepagawa kabisa, Jamali alupiga namba ya Hassani ila matokeo yalikuwa yaleyale na ikamlazimu apige nyumbani kwao amuulizie baba yake.
"Anko nyumbani wanasema hajarudi tangu alipoondoka na anko Hassani"Jamali alimuambia Shafii huku akionekana kuchanganywa na haliya mjomba wake.

"Etii?!" Shafii aliuliza kwa nguvu halafu akazirai papo hapo kutokana na taarifa anazoambiwa, hali hiyo ilimchanganya Jamali na ikambidi awaamshe wafanyakazi wote wa nyumba hiyo na jitihada za kumuwahisha hospitali zikafanywa mara moja.

****

Shafii alikuja kuzinduka siku iliyofuata akajikuta akiwa yupo hospitalini amelazwa akiwa ametundikiwa dripu ambayo ilikuwa inakaribia kuisha, alipoangaza pembeni aliwakuta Mzee Buruhan, Mzee Mahmud na Mama Jamali mke wa Hamis wakiwa wamezunguka kitanda chake.
"Faridaaa!" Shafii aliita jina la mke wake kwa nguvu huku akijaribu kuinuka kitandani
"Shafii hebu tulia kwanza utasababisha matatizo mengine tu" Mzee Buruhan alimuambia huku akimzuia asifanye fujo.
"Mama Zayina, Zayina mpo wapi?" Shafii alipiga kelele zaidi na ikabidi daktari aitwe mara moja ili kumtuliza, Mzee Buruhan na Mzee Mahmuf walimshikilia Shafii hadi daktari alipokuja akamchoma sindano ya usingizi ndiyo ikawa ahueni.

Baada ya Shafii kulala mzee Buruhan na mzee Mahmud walitoka pamoja na mke wa Hamis wakaenda kuka kwenye madawati ya kusubiria wagonjwa, baada ya muda mke wa Hamis aliondoka kwenda kufuata chakula kwa ajili ya mgonjwa akawaacha wazee hao peke yako.
"Kama nilivyokuambia mzee mwenzangu kuhusu huyu mwanao, awe mkweli ujue tatizo alilonalo ndiyo nitakubali kumsaidia" Mzee Mahmud aliongea.


"Mzee mwenzangu tatizo kila kukicha una misemo ambayo imejaa vitendawili vitupu hebu niweke wazi walau kidogo nipate fununu ya jambo linalomsumbua mwanangu" Mzee Buruhan alimlalamikia rafiki yake kutokana na kauli zake zilizo jaa mafumbo.

"mzee mwenzangu hiyo kinyume na utaratibu wa taaluma yangu siwezi kusema hata kama nalitambua tatizo hili, huwa sina tabia ya kukuficha kitu ila kwa hili wacha nikuambie ukweli tu nitakuwa nimekiuka masharti ya utalaamu wangu wa uganga ikiwa nitalisema suala hili pasipo muhusika mwenyewe kufungua kinywa chake na kuliongelea. Utanisamehe kwa hilo" Mzee Mahmud aliongea huku akimshika bega mzee Buruhan ambaye alionekana kuwa njia panda kutokana na matatizo yaliyomkumba mwanae
"mzee mwenzangu hakuna hata njia nyingine ya kunisaidia niweze pata fununu kidogo ya hili suala?" Mzee Buruhan aliuliza huku akiwa ameinamisha uso wake chini akionekana amekata tamaa kabisa ya suala hilo.

"Siku zote mwanamke atakaye mtoto lazima akubali kuvua nguo ya ndani ili alichokificha kionekane na hawezi kupata mtoto ikiwa atakataa kuivua hiyo nguo. Ndiyo hivyo hivyo mwanao akubali alilolificha moyoni mwake lifumbuke la si hivyo hataweza kupata msaada katika hilo, cha kukusaidia akiamka muambie umebaki peke yako ukitaka usipoteze vyote awe muwazi kwangu na kwako. Naenda msalani mara moja mzee mwenzangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akajiinua kivivu kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akawa anaelekea chooni, mzee Buruhan alimtazama tu akiwa anatamani sana ajue jambo lililopo ndani ya kichwa chake lakini hakuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Mzee Mahmud aliipopotea katika upeo wa macho yake aliinua kichwa juu akiweka ishara ya kuomba dua halafu akatikisa kichwa kuonesha anasikitishwa, hakuwa na jambo jingine alilomuomba Mungu zaidi ya kumshtakia tu juu ya balaa lililomkuta mwanae na kumfanya awe na matatizo tu katika mwaka huo ambapo miaka mingine yote aliishi kwa amani na furaha pamoja na familia yake lakini sasa furaha hiyo imetoweka katika maisha yake. Laiti angelijua kwamba alikuwa anashtaki mtuhumiwa kuwa ameonewa wala asingelifanya hivyo lakini kwakuwa hakujaliwa uwezo wa kulibaini kwani alikuwa ni mwanadamu wa kawaida tu, hakutambua kama jereha la mwanae ni la kujitakia hivyo halihitaji pole hata kidogo.

Mzee Mahmud alipofika kwenye mlango wa msalani baada ya kuondoka pale kwenye dawati alihisi hali isiyokuwa ya kawaida katika mwili wake lakini aliipuzia na kuingia humo msalani, alipoingia ndani alipitiliza sehemu za kujisaidia haja ndogo akawa anaelekea sehemu maalum ya yenye vyoo ndani ambayo hutumiwa na wale wanaohitaji kumaliza haja zao kwa siri tu. Alipofika hilo eneo alifuata mlango wa moja wa vyoo akashika kitasa ili aufungue lakini alisita baada ya kusikia upepo mzito ukivuma kwa ghafla ambao ulitaka hata kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni lakini aliuzuia, upepo huo ulipotulia Mzee Mahmud alionekana kukerwa nao kwa kitendo cha kutaka kumuadhiri ambapo aligeuka nyuma akionekana kuwa na hasira za waziwazi juui ya tukio hilo.

"Adabu gani hizo ewe mwanajini wataka kuniadhiri kwa hizo nguvu zako ulizojaliwa?" Mzee Buruhan alilalamika baada ya kumuona yule aliyetaka kumuadhiri kwa kutaka kuupeperusha msuli aliojifunga kiunoni alikuwa yupo mbele yake baada ya kugeuka nyuma, alikutana uso kwa uso na Zalabain akiwa amefumbata mikono kifuani mwake.

"Samahani mzee wangu kwa hilo" Zalabain aliomba radhi.
"sema una shida gani" Mzee Buruhan aliongea huku akiuweka msuli aliojifunga kiunoni vizuri.
"nimekuja kukuambia tu mimi ndiye ninayemtesa Shafii na huwezi kuharibu kazi yangu kwa kujaribu kumsaidia" Zalabain aliongea kwa msisitizo.

"Ndiyo nimeshakutambua tangu unajitokeza pia sipo kwa ajili ya kumsaidia dhalim kama yule bali nipo kwa ajili ya kumsaidia Buruhan ili asiondokewe na nguzo zake zote, kiufupi ni hivi nazuia usimuue yule mziwanda wake asiye na hatia" Mzee Mahmud alimuambia huku akijiamini halafu akameza mate kidogo kisha akaendelea, "Shafii ni haki yake kwa alichokifanya ila Ally hana hatia yoyote na usimuingize katika orodha hiyo, pia ningependa mumponyeshe sikio lske na taya lake ambayo mumjeruhi kutokana na kujaribu kuleta kile kitakachoyafanya majini ya marehemu Hamis yafanye kazi. Ukumbuke pia yeye anachukia ulilofanyiwa ila mali yako anayoimiliki Shafii ndiyo inamfanya ashindwe kufanya jambo lolote, usihukumu yule asiye na hatia kama ni ufalme utapewa pasipo yeye kupoteza uhai wake".

"unasema nini wewe?" Zalabain alimuuliza Mzee Mahmud
"kama ulivyosikia ewe mwana wa jini, ukumbuke mimi nilikataa kutengeneza uchawi kama uliomtapisha mama yako jana kwasababu najua siyo haki kufanya hivyo, pia niligoma kufanya dawa ya kumuua baba yako ili mama yako awe chini ya mwingine kwasababu najua haikuwa haki. Pia utambue nakuambia usimuue Ally kwasababu najua utakuwa hutendi haki ewe mwanajini kamuuulize ibin Zultash atakueleza, mwisho kabisa nakuambia hivi upotee sasa hivi kuna mtu anaingia humu msalani sasa hivi asije akaniona naongea peke yangu kama kichaa wakati nina akili zangu timamu" Mzee Buruhan aliongea kisha akageuka nyuma akaingia chooni bila kujali kama Zalabain ameondoka au yupo, baada ya kumaliza haja zake alitoka hakumkuta Zalabain na akarudi kule alipokuwa yupo awali. Alimkuta mzee Buruhan yupo na Ally wakiongea na iilonekana Ally alikuwa kapona kabisa tatizo la kuvunjika taya na sikio kwani hakuwa mwenye kuweza kuzungumza wala kusikia, lakini hapo alikuwa akizungumza na kusikia vizuri kabisa.
Mzee Mahmud alimuonesha ishara ya kumsalimia Ally kama ilivyokuwa akifanyiwa kwa kutoweza kusikia vizuri lakini.

"Mzee mwenzangu anaongea huyu na kusikia sasa hivi usimsabahi kama vile unamsabahi bubu" Mzee Buruhan alimuambia rafiki yake.
"Yapaswa tumshukuru Mungu basi mzee wangu maana huu muujiza tosha" Mzee Mahmud aliongea akionekana kufurahishwa na suala hilo.
"Alhamdililah" Ally na baba yake waliitikia kwa pamoja.

Mzee Mahmud alibaki kutabasamu tu kila alipomuangalia Ally kwa kufurahishwa na usikivu alionao Zalabain baada ya kufanya kile alichomuambia, tabasamu lake lilifanya Mzee Buruhan na Ally nao watabasamu wakijua kafurahishwa na hali ya Ally kutengemaa.
"Ally hebu sogea karibu" Mzee Mahmud alimuambia Ally huku akimtazama kwa umakini, Ally alimsogelea Mzee Mahmud pasipo kujua ni kipi alichokuwa anataka kufanyiwa kwani alimzoea sana mzee Mahmud na alimchukulia kama baba yake tu. Alipomsogelea Mzee Mahmud aliambiwa achuchumae mbele yake naye akatii amri kama alivyoambiwa, mzee Mahmud alimshika kichwani na akamtamka maneno yasiyoeleweka na kusababisha Ally ashtuke halafu aangalie mazingira ya hapo yalivyo halafu akaenda kukaa kwenye dawati pembeni ya baba yake alipokaa awali.

"Baba hivi hapa tupo kwa ajili gani?" Ally aliuliza tu baada ya kukaa pembeni ya baba yake akionekana kutotambua yupo hapo kwa ajili gani.
"Kha! We Ally maswali gani hayo hutambui kama tupo hapa kumuangalia kaka yako kalazwa tangu jana" Mzee Buruhan alimuambia Ally akionekana kutoelewa kitu alichofanyiwa na mzee Mahmud hadi akasahau yupo pale kwa lengo gani wakati alipoingia tu aliulizia hali ya kaka yake.
"Khaa! Kumbe tupo hapa kwa ajili ya kumuangalia firauni huyo, sina muda huo muache afe maana huyo ni zaidi ya shetani" Ally aliongea maneno ambayo yalizidi kumshangaza sana Mzee Buruhan na akajikuta akimtazama mzee Mahmud akionekana kutoelewa kafanya nini, Ally alinyanyuka ili aondoke lakini mzee Mahmud alimuita akamuomba aketi akakaa chini.

"Ally tambua undugu ni kovu na halifutiki usifanye hivyo, najua unaumia kwa kile alichokifanya kaka yako lakini kumbuka ndugu ni ndugu tu" Mzee Mahmud aliongea kwa ustarabu wa hali ya juu akitegemea ataeleweka na Ally lakini haikuwa hivyo.
"Baba zangu mngejua alichokifanya huyo firauni mnayekuja kumuangalua wala msingethubutu kukaa hapa, na sijui hata ni kwasababu gani nilikuwa nikimpenda kwa kipindi chote hicho nahisi aliniroga yule maana miale ya mkufu wake sielewi hata imemifanyaje wakati nilikuwa nikimchukia" Ally aliongea huku akionesha kumchukia kaka yake.

"Ally unaongea nini wewe?" Mzee Buruhan aliuliza akionekana kushangaza na maneno anayoyaongea mwanae.
"Mzee mwenzangu kama nilivyokuambia hili tatizo linajulikana ila huyu hatakiwi kulisema na akilisema atakuwa kiziwi kama mwanzo muache huyo Shafii aeleze kila kitu. Unajua..." Mzee Mahmud aliongea maneno yaliyomfanya Mzee Mahmud atulie kimya na alishindwa kumalizia kauli yake baada ya mke wa Hamis kurudi akiwa amebeba chombo cha chakula kwenye mfuko wake.

"Vipi mgonjwa jamani tayari ameshaamka?" Mke wa Hamis aliongea baada tu ya kuwasili na alimuonesha Ally tabasamu kisha akampa mkono akampa mkono ili amsalimie akijua kuwa Ally hawezi kuongea.

Ally hakuupokea mkono wa Mke wa Hamis zaidi ya kusonya kwa nguvu kisha akanyanyuka akasema, "shetani jike mkubwa wewe".
Ally alinyanyuka kwenye dawati la kusubiri wagonjwa akaelekea mahali akimuacha wazee wake na mke wa Hamis wakimshangaa sana, mke wa Hamis alipotaka kumfuata nje Mzee Buruhan alimshika akamzuia.

"Salma mama naomba unisikilize kwa umakini, achana na Ally kwa sasa kaa hapo usubiri muda wa kumuona mgoniwa akizinduka tukamuone" Mzew Buruhan alimuambia Salma mke wa Hamis.

"Lakini Ally kapatwa na nini wazee wangu kwani alikuwa hawezi kuongea na kusikia ila sasa hivi anaongea na kusikia ila amekuwa kama akili haziko sawa hadi ananisonya mimi" Salma aliongea huku akishangazwa na hali ya Ally yule aliyekuwa anamsikiliza na kumtii na kumuheshimu ameamua kuonesha dharau.

"Hebu mama kuwa muelewa achana na habari za Ally sasa hivi, tufikirie kuhusu mgonjwa tu" Mzee Mahmud aliongea kwa msisitizo huku akionekana kutopendezwa na maneno ya Salma.

"Sawa baba zangu nimewaelewa" Salma alijibu kwa shingo upande ili tu asiwaudhi wazee ambao anawaheshimu.

****
Wakati Ally akifunguliwa na kuanza kumuoneshea dharau upande wa himaya ya Majichungu Zalabain ndiyo alikuwa amerejea muda huo na aliamua kupitia chumbani walipo mama yake na dada yake ili awaone kutokana na upendo alionao kwao, alibisha hodi kwa adabu ingawa alitambua hata akiingia muda huo asingewakuta wakiwa bila stara. Alipokaribishwa aliingia kwa adabu na akaenda hadi walipokuwa wamekaa kitandani na akawasalimia, halafu naye akaketi kitandani jirani yao.

"Mwanangu kila nikikutazama namuona baba yako kwa jinsi wote mlivyokuwa na sura zilizofanana, haya niambie unatoka wapi?" Bi Farida aliongea kisha akamuuliza Zalabain.

"Nilikuwa Tanga kwenye hospitali ya SBN nilienda kuongea na mzee Mahmud" Zalabain alimuambia mama yake.
"Mh! Huyo mzee huko hospitalini anafanya nini?" Bi Farida aliuliza.
"Amekuja kumuangalia mumeo amelazwa" Zalabain alimuambia mama yake.

"Jamadin sina mume kama huyo mimi tena sitaki kumsikia ukimtaja, mume aliyetakiwa kunioa mimi ni Faimu tu na sijui ilitokea nini mpaka nikamkana na nikamsababishia matatizo makubwa sana akahama kijijini akiwaacha jamaa zake. Nampenda Faimu na natamani nimuone hata leo ili nimuombe msamaha maana yeye ndiyo kila kitu kwangu" Bibi Farida aliongea na mwishowe akalia kutokana na kujutia aliyoyafanya ya hapa zamani, Zalabain ilimbidi amkumbatie mama yake ambembeleze kutokana na upendo alionao kwake.
"Samahani mama kwa kukupa taarifa smbayo hutaki kuisikia, sipendi uhuzunike nakupenda sana" Zalabain alimuambia mama yake baada ya kunyamaza.

"Nakupenda pia mwanangu" Bi Farida alisema huku akitabasamu kwa mbali, waliendelea kuongea maongezi mengine kwa furaha wakiachana na suala ambalo lilionekana kutomfurahisha kabisa Bi Farida.

****

Baada ya masaa mawili Shafii aliamka kutoka usingizini akiwa yupo vizuri kiafya kuliko awali, hali yake iliendelea kutengemaa na ilipofika muda wa alasiri aliruhusiwa na daktari na alirudi nyumbani akiwa ameongozana ns wote waliokuja kumuona hospitali kasoro Ally tu ambaye hakurudi tangu aondoke pale hospitali. Shafii alipelekwa moja kwa moja chumbani kwake na akaachwa apumzike na kisha wazee wake wakakaa sebuleni hadi ilipoingia jioni ndiyo mzee Buruhan na mzee Mahmud waliingia chumbani kwa Shafii wakamkuta akiwa ameamka ameegemea mito kitandani kwake, Shafii alipoona ujio wa wazee wale alihisi kuna jambo ila alikaa kimya ili apate uhakika wa wasiwasi wake.

"Shafii" Mzee Buruhan alimuita
"Naam Baba" Shafii aliitikia
"unajua kama wewe ndiyo nguzo kuu kati ya nguzo zangu nne zilizobakia?" Mzee Buruhan alimuuliza
"nafahamu hilo baba" Shafii alijibu.

"Hussein hatunaye, Hamid hatunaye, Hassan ni mdogo kwako, Falzal ni mdogo kwako na Ally pia ni mdogo kwako. Wewe pekee ndiyo mkubwa ndiyo kiongozi wao ingawa wote wana maisha yao na hata wanajisomesha wakitaka kujiendeleza kielimu. Nadhani unatambua hilo" Mzee Buruhan alisema.
"Ndiyo baba natambua hilo" Shafii alijibu.
"Sasa basi inapotokea tatizo lenye kuhitaji kuelezewa ili lisizidi zaidi inabidi lielezewe mwanangu ikiwa utakaa kimya haitasaidia chochote" Mzee Buruhan aliongea.

"Baba sijakuelewa unachomaanisha" Shafii aliongea.
"Shafii najua unatambua suala la upotevu wa mke wako na hata mwanao linalokufanya uwe na matatizo kila kukicha, sasa mwanangu ukilificha itakusaidia nini ikiwa unalifahamu chanzo chake. Kumbuka mficha maradhi kifo humuumbua mwanangu, mwanangu ni bora uitoe aibu mbele ya daktari ili utibiwe kuliko kuficha tatizo halafu ufe na ugonjwa. Ongea chanzo cha haya ni nini?" Mzee Buruhan alimsihi mwanae.
"Baba kusema ukweli sijui wala sitambui suala hili linasababishwa na nini?" Shafii alikataa.
"Shafii vuta kumbukumbu zako vizuri umefanya nini mpaka yote haya yatokee au hutaki familia yako uione tena ikiwa na upendo" Mzee Buruhan alizidi kumsihi.

"Baba napenda sana familia niione tena ikiwa ina upendo lakini sikukumbuki chochote kilichosababisha haya ninayofanyiwa" Shafii alikana kabisa juu ya suala hilo.

"Jirani na mashine ya kusaga unga kule Mpirani miaka ishirini na moja iliyopita unakumbuka kilitokea nini pale kwenye nyumba yako uliyokuwa unaishi baada ya wewe kuhama tena ilikuwa majira ya saa sita usiku?" Mzee Mahmud aliongea kwa mara ya kwanza na kumfanya Shafii ashtuke kwa jambo alilotajiwa, lilikuwa ni jambo ambalo alishalisahau kabisa katika ubongo wake na sasa alikumbushwa na mzee huyu ambaye ni mganga mtaalam.
"Shafiii unakumbuka nini hiyo siku" Mzee Buruhan naye aliunganisha maelezo ya rafiki yake ingawa hakuyaelewa kabisa, maneno ya mzee Mahmud yalimfanya anyamaze ghafla huku akiwa ameinamisha kichwa chake chini.

"Shafii si nakuuliza" Mzes Buruhan aliongea huku akimtikisa bega baada ya kuona yupo kimya, Shafii alikurupuka baada ya kutikiswa bega kama alikuwa yupo katika usingizi mzito.

"Ha..hapana si....sikumbuki chochote" Shafii aliongea kwa kubabaika baada ya kuhisi moja ya jambo baya alilolifanya linakaribia kugundulika.
"Una uhakika?" Mzee Mahmud aliuliza.
"ndiyo baba zangu nina uhakika wa kile ninachokiongea" Shafii alijikaza akajibu kwa kujiamini.

"mzee mwenzangu sisi twende tukanywe kahawa si unaona muda huu na kiubaridi cha kipupwe kimeanza, Shafii kama hujui juu ya hilo basi inakupasa utambue kuwa maisha ya mkeo na binti yako yapo kwenye kinywa chako kueleza unachojua na ukikaa kimya jua kinachofuata ni kama kilichowapata wadogo zako ia utambue umebaki peke yako" Mzee Mahmud huku akiwa tayari amesimama na Mzee Buruhan naye akasimama, wote kwa pamoja walianza kutembea kuelekea ulipo mlango ili waondoke lakini sauti ya Shafii ikiwaita iliwafanya wasimame na kugeuka wakamtazama.

"Nipo tayari kuwaambia kilichotokea wazee wangu naomba mnisaidie" Shafii aliongea baada ya kuona maji yamemfika shingoni na maneno ya mzee Mahmud ndiyo kabisa yalimfanya akubali. Mzee Mahmud alimtazama Shafii kwa tabasamu hafifu halafu akamuambia, "kesho muda kama huu pale ulipokuwa unaishi kule mpirani ndiyo kutakupa ahueni ya tatizo lakokwa familia yako"
Mzee Mahmud aliposema maneno hayo alitoka humo ndani bila hata kumuangalia Shafii kwa mara nyingine, Mzee Buruhan naye alifuata akiwa nyuma yake.

****

Maneno ya Ally baada tu ya kupewa mkono na Salma yalimfanya Salma karibia siku nzima akiwa anajifikiria kwani Ally alikuwa amepatwa na nini mpaka awe vile, ilipofika jioni aliamua kutoka na kwenda kumtafuta Ally bila ya kumueleza mtu ili aongee naye tu kwani Ally alikuwa ni mmoja kati ya wanaume aliokuwa anawapenda na kipindi cha nyuma alipokuwa msichana alishajaribu kujivika ujasiri na kumueleza Ally yaliyo moyoni mwake lakini aliishia kukataliwa baada ya Ally kuwa anamuheshimu sana Hamis ambaye alikuwa na mahusiano na Salma kabla hajamuoa. Baada ya mpango ambao ndiyo chanzo cha balaa lote lililowakumba watoto wa mzee Buruhan, Ally alifungwa akili na akawa anasikiliza wote waliofanya mpango ule bila hata kuwapinga na alifungwa akili baada ya kuujua mpango huo akawa amekasirishwa nao. Baada ya kufungwa akili ndipo Salma alipompata Ally kutokana na yeye pia ni mmoja kati ya watu walioshiriki huo mpango, alimtumia Ally vyovyote atakavyo baada ya Ally kutopinga kauli yake. Sasa akili ya Ally ilipofunguliwa na Mzee Mahmud na Salma kujibiwa vile alijikuta roho ikimuuma akijua Ally amepatwa na tatizo hivyo aliamua kumtafuta. Hakukujua kama Ally wa leo siyo wa jana alichokuwa anakijali yeye ni penzi lake haramu alilolianzisha kwa Ally hata alipokuwa yupo ndani ya ndoa.

Tamaa za kutamani kingine wakati akiwa tayari ana kingine mkononi ndiyo zilimfanya Salma afanye jambo hilo ambalo lilipelekea afiche siri nzito sana ambayo laiti ingaligundulika mapema basi angekuwa ameleta matatizo makubwa sana kwa Hamis na Ally.

Juhudi za Salma kumtafuta Ally ziliendelea kwa usiku huo akiwa yupo ndani ya gari yake na hatimaye alimkuta akiwa amekaa kwenye matairi yaliyochimbiwa katika uwanja wa mpira uliopo mkabala na shule ya sekondari ya Usagara, Salma alimfuata hadi hapo akaegesha gari pembeni kisha akashuka akaenda kumkumbatia Ally akitegemea atapokelewa lakini alijikuta akisukumwa hadi akaanguka chini akaumia.
"Kaa mbali na mimi malaya wewe!" Ally alimuambia kwa ukali.

"Lakini Ally mpenzi wangu nimefanyaje?" Salma aliuliza kwa masikitiko makubwa huku akionekana kuumia baada ya kusukumwa.
"Unajifanya hujui siyo tena usiniite mpenzi wako kuanzia hivi sasa, we wa kunifanya mimi mtumwa wa ngono hadi umesababisha nisioe wakati natakiwa kuwa na familia sasa hivi" Ally alifoka.

"Ally nakupenda ndiyo maana nimefanya hivyo hadi nikazaa na wewe" Salma akaongea huku akilia.
"Weee tena ishia hapo hapo" Ally alimkaripia huku akimuongeza teke la mguu Salma.
"Ally nikatae ila ukae ukijua Hamida siyo mtoto wa mume wangu bali ni damu yako, ndiyo maana hata alipozaliwa kaka yako alikutania umefanana naye miguu ila ukweli ile ni damu yako kabisa" Salma aliongea huku akilia, Ally alipuuza maneno ya Salma akaondoka eneo akimuacha akilia ingawa kuna jambo lilikuwa likiisumbua akili baada ya kusikia maneno hayo.

" "Ally huyu mtoto kafanana na wewe hiyo miguu balaa ingawa ana sura ya mama yake na baba yake" Shafii aliongea huku akicheka.
"Haaaa! Shemeji nawe waanza kwahiyo waataka sema kafanana na babaye na Ally pamoja nami" Salma alisema huku akimtazama Shafii.
"Ndiyo hivyo ahemeji" Shafii alisema.

"Wewe Chumbio waleta zako sasa huoni kama hiyo miguu ni ya mama yake kabisa, wamefanana tazama kucha hizo uache msifia mdogo wako" Hamis aliongea na kusababisha wati wote wacheke humo ndani.

"Bonoeza usichukie basi masihara ni jadi yetu tangu twacheza michezo ya kitoto, hongera bwana kwa kupata binti mrembo huyo na urembo wake unaonekana tangu akiwa mtoto" Shafiu aliongea huku akimpa mkono wa pongezi rafiki yake kipenzi.
"shukrani Chumbio rafiki wa tangu utotoni" Hamis aliitikia huku akicheka
"sasa Bonoeza hapo inabidi ufuge mbwa na bunduki ununue mapema maana wajanja wataanza kuja kutoa salamu sana kumbe wataka wampate malkia hapa" Shafii alisema na wote waliopo nyumbani kwa Hamisi wakacheka " Maneno aliyoambiwa na Salma ndiyo yalivuta kumbukumbu yakamkumbusha siku hiyo ambayo Hamida alikuwa ndiyo kaletwa nyumbani baada ya kuzaliwa katika hospitali ya Ngamiani, alizidi kukumbuka zaidi na hapo akakumbuka tukio jingine kabisa baada ya kumuona Hamida akiwa na miaka mitano tu tangu azaliwe na siku hiyo alikuwa akibadilishwa nguo na mama yake Salma, siku hiyo alimuona Hamida akiwa ana mwili unaofanana wake sana. Ally alikumbuka zaidi juu ya siku hiyo na akawa anajifikiria kwa umakini haswa ndipo akajikuta anaamini lakini siyo kwa asilimiia zote yale maneno aliyoambiwa na Salma.

"Dah nimefanyishwa dhambi mbaya ya kuzini na mke wa mtu bila kujijua" Alky aliongea huku akikata mitaa na alionekana ni mwenye majuto makuu juu ya jambo hilo ingawa hakutegemea kama atalifanya, alitembea huku uelekeo wake maalum ukiwa haujulikani kwani alikuwa anazurura mitaani tu.
"ni bora nilale nje kuliko kulala kwenye mali haramu niliyokuwa nimekabidhiwa na nikajikuta nimeipokea bila kujijua, ni bora nisifanye kazi niwe masikini kuliko kuitumia hii elimu niliyosomeshwa kwa kutumia fedha haramu zilizosababisha mwanadamu mwenzangu amwage damu kwa manufaa ya wengine. Shahada nimeipata kwa pesa zilizotokana na damu ya mwenzangu kumwagika, nawachukia Shafii, Hamid, Hassan, Hussein, Falzal, Hamisi pamoja mke wako Salma aliyetoa kitu kichafu ili aangamizwe kiumbe asiye na hatia.

Hisan Shelukindo pia mwanaharamu mkubwa wewe umekuwa na maisha mazuri kwa ukatili wenu huo" Ally aliongea kwa hasira akiwa tayari ameshafika Sahare kwa kutembea tu bila hata mpangilio; alihisi uchovu kwa kutembea siku hiyo nzima na akakaa katika baraza la maduka ambayo yalikuwa ndiyo yamekamilika ujenzi wake lakini bado hayajafunguliwa. Alijiona ni mmoja wa wenye makosa kwa kutumia sehemu ya mali iliyotokana na njia haramu ingawa hakujijua, alijikuta hata akilengwa na machozi na hatimaye alianza kulia kimya kimya hadi pale alipochoka akainuka kwenye baraza hiyo.

"Bora uwe masikini utaabike kuliko uwe tajiri kwa njia isiyo ya halali bila kujijua, inauma sana" Ally alisema kwa uchungu huku akinyanyuka tena barazani hapo na kuanza kutembea kama ilivyokuwa awali, alitembea akawa anafuata uelekeo wa nyumbani kwa baba yake hadi alipofika akaingia ndani na moja kwa moja akaenda kujitupa sebuleni akalala usingizi mzito bila hata kuwa amekula kitu chochote siku hiyo.

Asubuhi ya siku iliyofuata aliamka akajisafisha mwili wake akatoka hadi nje, akamuona dereva wa gari za baba yake akiwa yupo barazani akipata kifungua kinywa akamsabahi kisha akawa anaelekea getini.

"Kaka unaelekea wapi nikutoe maana gari zipo hapa" Dereva wa baba yake alimuambia.
"unaweza ukapumzika kaka mkubwa" Ally alimuambia dereva wa gari ya baba yake kisha akatoka nje akawa anaelekea ilipo barabara ya Mombasa, alitembea hadi akipoifikia hiyo barabara akamuita dereva wa pikipiki akaja mara moja.

"Mpirani kaka" Ally alimuambia dereva wa pikipiki ambaye alimchangamkia akamuambia apande tu bila hata kutaja bei, Ally alipanda hiyo pikipiki na safari ikaanza ambapo ilichukua dakika kumi na tano kwa mwendo wa pikipiki akawa ameshafika Mpirani akampa dereva yule pesa yake kisha akaingia mtaani na akatembea hadi mahali ambapo nyumba zipo moja moja na hatimaye akaifikia nyumba kubwa ambayo ipo kama gofu tu ikiwa ipo katikati ya shamba kubwa ikionekana kuwa ipo peke yake mbali na makazi ya watu wengine. Nyumba hiyo ilionekana kutolewa milango na baadhi ya madirisha baada ya kukaa siku nyingi bila kutumiwa kama makazi ya watu na eneo zima lenye kuizunguka nyumba hiyo lilikuwa na majani mengi yaliyoonekana hayaku punguzwa kwa muda mrefu.

Ally aliingia ndani ya nyumba hiyo iliyoezekwa kwa bati lililochakaa na sakafu ya chini ilionesha kuwa ni ya udongo mwekundu ambao hutumiwa kukandika kuta za nyumba za udongo, ilikuwa ni nyumba kubwa yenye vyumba takribani vinne na sebule ambayo ndani ina kuta za udongo zilizowekwa plasta kwa nje. Sebule kubwa ya nyumba hiyo ilikuwa na usafi mkubwa kupitiliza ambao ulimshangaza sana Ally na vyumbani kulikuwa kuna nyuzi nyingi za buibui kiasi kwamba haiwezekani hata kidogo mtu wa kawaida kuingia humo ndani bila hata kusafisha hizo nyuzi za buibui, Ally aliangalia kila chumba akawa anakumbuka matukio tofauti ambayo yalikuwa yakifanyika hasa kipindi ambacho anaishi katika nyumba hiyo ambayo kwa sasa imetekelezwa na mwenyewe.

"Ni historia nisiyoweza kuisahau na ni mazingira yasiyoweza kusahaulikavkwa mtu kama mimi na natamani niyarudie niishi kama nilivyokuwa awali huenda amani ya moyo wangu itarejea kama ilivyokuwa awali" Ally aliongea akiwa amesimama katika mlango wa chumba ambacho ndiyo alikuwa akikitumia kipindi akiishi katika nyumba hiyo.

Akiwa amesimama hapo alisikia sauti ya mtu akipiga uruzi kutoka nje ya nyumba hiyo na ikamlazimu atoke aende kutazama ni nani huyo, alipokuwa akikaribia mlango wa kutokea mlango wa nyumba hiyo alikutana na kijana wa kisomali aliyekuwa akifanana sana na mtu ambaye alikuwa anamjua ila jina lilikuwa limemshamtoka kichwani mwake. Kijana huyo alikuwa amevaa kanzu nyekundu iliyomka vyema na kofia ya rangi ya kahawia, Ally alipomuona huyo kijana alizidi kuvuta kumbukumbu juu ya alipomuona lakini hakukumbuka chochote.
"habari yako kijana" Ally alimsabahi yule kijana.

"salama tu, shikamoo" Yule kijana aliitikia.
"Marhaba sijui ni nani mwenzangu" Alky aliitikia kisha akamuiliza swali yule kijana.
"naitwa Fahmi ni mjukuu wa mzee mmoja maarufu wa kiarabu anayeitwa Muburaka" Yule kijana alieleza.
"Mzee Mubaraka huyuhuyu baba yake Faimu waliyehamia kijiji cha Bwagamacho" Ally alisema.
"Ndiyo huyo huyo na mimi ni mtoto wa Faimu" Fahmi alieleza.

"ok ok karibu bwana leo nimekuja kuzuru makazi yetu ya zamani" Ally alieleza.
"Asante sana, mimi huwa ni sehemu yangu ambayo napenda kukaa huwa inanikumbusha mengi sana hii na nikiwa na huzuni basi huwa nakuja kukaa hapa ndiyo maana unapaona pasafi sana hasa upande wa sebule hii" Fahmi alieleza.
"Ok kijana ndiyo maana nilitaka nishangae imekuwaje mpaka pawe hivi, karibu tukae sote na mimi leo nimependelea sana kukaa humu" Ally alimuambia huku akimpa mkono Fahmi ambaye aliupokea akiwa na tabasamu pana usoni.
"umefanana sana na baba yako hadi mkitabamu mpo hivyohivyo, hakika mungu kawajalia tabasamu pana kijana" Ally alimwambia Fahmy na kusababisha Fahmy atabasamu.

"asante anko, napenda nikuite anko kama hutajali" Fahmi alimuambia Ally.
"si vibaya waweza kuniita hivyo tu kwani umeonesha heshima kubwa sana kwangu kijana" Ally alisema.
"asante sana nafurahi kuongea na wewe" Fahmi alisema.
"hata mimi pia, vipi baba yako hajambo?" Ally aliongea huku akitabasamu kisha akamuuliza juu ya hali ya baba yake, swali hilo lilimfanya Fahmi aondokwe na uso wa tabasamu usoni mwake ingawa alilazimisha tabasamu hilo lirudi katika uso wake.
"Baba yupo uarabuni kwa sasa na huko ndipo alipojenga maisha yake" Fahmi alijibu huku akilazimisha tabasamu usoni mwake.
"ohoooo! Mpe hongera sana rafiki yangu aliyenijali sana yule" Ally aliongea huku akitabasamu.

Maongezi yao yaliendelea hadi ilipotimu adhuhuri Fahmi akaaga akaondoka na akamuahidi Ally angerejea akiwa na ugeni mkubwa sana kama angekuwepo hapo. Alky alimpa ahadi ya kuwepo eneo kwa siku nzima hivyo angemkuta, hakuutambua ugeni huo ulikuwa ni ugeni gani na laiti angeutambua angetamani hata auone muda huo lakini haikuwezekana. Ally aliendea kukaa hapo hadi ilipofika muda wa alasiri akaja kijana mwingine akiwa na chombo cha chakula akampatia, yule kijana alimuambia chakula hicho kilikuwa kimeagizwa aletewe na Fahmi. Ally alishukuru sana akakila chakula chote kutokana na njaa ambayo tayari ilishaanza kushambulia tumbo lake, baada ya kumaliza kula alitoa shukrani kwa ubinadamu aliofanyiwa na yule kijana
aliyetumwa pia akamwambia apeleke shukrani za dhati kwa Fahmi kwa kumjali namna hiyo.

Baada ya kijana yule kuondoka Ally aliendelea kukaa hapo akikumbuka mambo mbalimbali kipindi akiishi ndani ya nyumba hiyo kabla hajahama, mambo mengine ya furaha na upendo na alivyokuwa akiishi na shemeji yake ambaye alimjali yalimpa tabasamu kila akiyakumbuka ila alipokumbuka wema aliofanyiwa na kaka yake alijikuta anasonya tu kwani hakuupenda hata kidogo huo wema wake na wala hadi muda hakuona umuhimu wake.
"Shetani katumia ushetani kunifanikishia malengo yangu, hadi sasa sioni umuhimu wa mimi kufikia haya malengo ikiwa kuna mwenzangu kateseka kwasababu ya huyo shetani. Kakimbia kwao kwasababu ya huyo shetani. Shetani huyu kanisaidia ili na mimi anitumbukize katika ushetani"Ally aliongea kwa hasira kisha akanyanyuka akasema, "namchukia maana bila yeye mimi nisingetumiwa kama mtumwa wa ngono na yule malaya aliyekubuhu kwa umalaya tangu yupo kigori. aaargh! Nawachukiaaa!" Ally aliongea kwa hasira kisha akapiga ngumi ukutani na kupelekea sehemu ya plasta iliyowekwa juu ya ukuta wa udongo wa nyumba hiyo uanguke.

Chuki za waziwazi kwa kaka yake ndiyo zilikuwa zimeutawala moyo wake na hakumpenda kama ilivyokuwa akimpenda hapo awali, hakuona umuhimu wa yeye kumuita kaka wakati kafanya mambo yasiyopendeza kwa mwanadamu yoyote mwenye moyo wa kibinadamu na siyo wa kama aliokuwa nao kaka yake. Alitokea kuwachukia ndugu zake wote walioshiriki mpango ule hakuona faida ya kuwa na ndugu kama wao katika dunia hii, aliona ni bora angekuwa na undugu na jiwe kuliko kuwa na undugu na hao aliowaheshu kama kaka zake lakini hakuona ustahiki wao wa heshima hiyo aliyowapa.

SURA YA NANE.

Majira ya magharibi katika eneo hilo alilokuwepo Ally paliiingia ugeni mwingine ambao haukutia mguu katika eneo hilo kwa miaka kadhaa tangu walipoondoka, ugeni huo ulikuwa ni msafara wa magari mawili ya kifahari yenye thamani kubwa sana nchini Tanzania kwa kipindi chote. Magari hayo yalikatisha katika majani baada ya barabara ya kuingia eneo hilo kuwa imeota majani kila sehemu. Ally aliposikia mingurumo ya gari hiyo wala hakujishughulisha kwenda kuangalia zaidi ya kutulia vilevile sehemu ya dirishani ya sebule hiyo alipokaa katika eneo ambalo dirisha limetolewa, aliposikia hatua za mtu akiingia hapo ndani yeye alielekeza machp mlangoni tu na hadi mtu huyo anaingia tayari alikuwa ameshamuona na ni mtu kati ya watu anaowaheshimu akiwa amebeba mikeka inayotengenezwa kwa ukindu maarufu kama majamvi kwa wakazi wa jiji la Tanga
"Ally kumbe huku" Sauti ya mtu huyo ilimsemesha na hapo Ally akainuka akamfuata.

"ndiyo baba nipo huku, shikamoo" Ally alimuamkia baba yake baada tu ya kumjibu swali alilouliza.
"marhaba tumekutafuta sana mchana wa leo ili uje huku maana kuna jambo muhimu sana" Mzee Buruhan alisema.
"sawa baba nipo tayari hakuna kilichoharibika" Ally aliongea huku akimpokea baba yake majamvi.
"yatandike hapo chini kwa ajili ya wageni watakaokuja maana mzee Mahmud kasema kuna ugeni utafika hapa kwa ajili ya jambo hili tuliloitiwa hapa.
"sawa baba" Ally alitii amri akaanza kuyatandika majamvi chini kama alivyoambiwa na baada ya muda akawa amemaliza.
"vizuri sasa tumsubiri mzee mwenzangu anakuja sasa hivi na nimeambiwa nisiwaruhusu ndugu zako kuingia mpaka yeye afike" Msee Buruhan aliongea huku akienda kuketi dirishani alipokuwa ameketi Ally awali, Ally naye aliungana naye kwenda kukaa alipokuwa awali.
Baada ya dakika tano mlio wa pikipiki ulisikika nje ya nyumba hiyo ikija na kisha baada ya dakika moja ikaondoka, muda huo huo mzee Mahmud alionekana akiingia mlangoni akiwa amebeba taa nne kubwa za kuchaji baada ya pikipiki hiyo kuondoka.
"vipi kila kitu tayari?" Mzee Mahmud aliuliza.

"ndiyo kila kitu tayari mzee mwenzangu" Mzee Mahmud alijibu.
"vizuri basi, Ally hujambo mwanangu" Mzee Buruhan alipongeza kisha akamjulia hali Ally.
"Sijambo baba shikamoo" Ally alijibu kisha akamsalimia.
"Marhaba mwanangu vizuri kwa kuwepo hapa, ngoja nianze kazi" Mzee Buruhan aliongea kisha akaanza kutamka maneno yasiyoeleweka akawa anazunguka eneo zima lenye mikeka halafu akafanya hivyo kwenye kila pembe ya ukuta hadi akamaliza sehemu zote na alipomaliza kufanya hivyo aliwasha taa alizokuja nazo akazitundika ukutani kwenye kila kona.

"Sasa hao wanaweza kuingia wakae upande wa kushoto na uwaambie wasiongee mpaka niwaambie mimi, Ally kaa pembeni yangu" Mzee Mahmud aliongea kisha akakaa chini, mzee Buruhan alitoka nje na baada ya muda akarejea akiwa pamoja na Shafii,Salma, Hamida na Jamal.
Shafii aliongozwa na Jamal hadi eneo wanalotakiwa wakae na alishushwa kwenye kiti akakalishwa kitako, baada ya wote kukaa chini kwenye jamvi waligeuka wakawa wanamtazama mzee Mahmud kujua kinachofuata.

"Bado ugeni mmoja uingie, wageni karibuni" Mzee Mahmud aliongea huku akitazama mlangoni na kupelekea watu wote watazame mlangoni, ugeni ulioingia hapo ulikuwa ni watu wanaowajua ambapo wengine walishtuka baada ya kuuona ugeni huo ambao haukueleweka umefika hapo kwa usafiri gani kwani walionekana tu wapo mlangoni.

Wa kwanza kuonekana mbele ya macho yao alikuwa ni Zalabain akiwa amevaa joho jeusi na kofia nyupe ambaye alitambulika kwa Ally na Shafii pamoja na mzee Mahmud, Ally alimtambua Zalabain kama Fahmi aliyekuwa naye hapo hadi muda wa adhuhuri na hakumfahamu kwa vingine kabisa. Shafii alimtambua huyo mtu kama mbaya wake baada ya kuiona sura yake siku aliyokufa mganga Sauti ya radi na alimkimbia, alipomuona alishtuka sana alitamani hata ardhi ipasuke atumbukie asionekane eneo hilo kwani alishuhudia ukatili wa Zalabain hivyo alimuogopa. Wageni wengine walioingia eneo hilo walikuwa ni Bi Farida na Zayina wakiwa wamevaa nguo za thamani kubwa walizopata wakiwa katika ulimwengu wa majini, Shafii alipowaona alijikuta akijawa na furaha akataka kutamka neno ila ishara ya baba yake ikimkataza kutozungumza ikamfanya atulie.

"Karibu Zalabain mwana Zaif mjukuu wa Zulain mfalme wa himaya ya majini ya Majichungu, karibu uketi upande ule wa pili ukiwa na wageni wenzako" Mzee Mahmud alisema huku akitabasamu na kusababisha Zalabain atabasamu pia, Zalabain na mama yake pamoja na dada yake walienda kukaa mwingine kabisa pembeni ya upande aliopo Shafii.

"Sasa basi nimewaita hapa ili tuweze kutatua tatizo ambalo lingemsababishia mzee mwenzangu hapa asibakiwe na hata muhomili mmoja ndani ya dunia hii, utatuzi wa tatizo hilo utaanza kuonekana tu ikiwa ukweli wote utakuwa utakuwa hadharani" Mzee Mahmud alisema kisha akamwangalia Shafii akamwambia, "Shafii napenda uanze kuongea ukweli kuanzia unaanza kumpenda Bi Farida na ulivyompata hadi ukamuoa, tafadhali narudia tena tafadhali ukweli ni muhimu katika kila kitu".

Baada ya mzee Mahmud kumaliza kuongea alimpisha Shafii ili aeleze ukweli wake wote, Shafii naye hakuwa na jinsi zaidi ya kueleza ukweli wote juu ya suala hilo ili apate nafuu ya matatizo yake kwa jinsi anavyoamini na kwa jinsi alivyoambiwa na mzee Mahmud. Shafii alianza kwa kusafisha koo lake kisha akasimulia, "Kwanza napenda nitangulize msamaha kwa hichi nitakachokusimulia ikiwa kitakuwa kimemkwaza yoyote kwani si kizuri, nilikuwa ni mtoto mtiifu sana kwa wazazi wangu kwa kipindi ambacho bado sikuwa nimepevuka kutokana na malezi ya kimaadili aliyonilea baba yangu kwa kipindi hicho. Ndiyo muda huo huo mke wangu mama Zayina alikuwa angali binti mdogo hata kuvunja ungo bado ingawa alikuwa akitajwa ni mmoja kati ya mabinti wenye uzuri ambao haukuwahi kutokea katika kijiji chetu cha Bwagamacho Baada ya Farida kuanza kupevuka ndipo uzuri huo wa umbo na kila kitu ulianza kuonekana na kipindi hicho na ndiyo wavulana wa rika langu wakaanza kumfuata lakini waliambulia kukataliwa na binti huyo na hata wengine walishtakiwa kwa wazazi wao baada kumtongoza, jambo hilo lilinitisha na kunifanya nishindwe kwenda kumuambia kwa kuhofia ukali wa baba yangu kama akijua. Nilimpenda sana tena sana lakini nilihofia kupigwa sana na baba yangu kama nilivyoshuhudia wenzangu wakifanyiwa hivyo na baba zao baada tu ya mashtaka kuletwa nyumbani juu ya kumtongoza Farida. Baada ya miaka miwili kupita ndipo nilipoanza kupata ujasiri wa kumtongoza ingawa nilikuwa nina uoga kwa mbali, kutongoza kwangu kuligonga mwamba na hata nilipomueleza rafiki yangu kipenzi Hamis ambaye ni kaka yake juu ya suala hilo aliniambia yupo tayari kumsaidia ikiwa tu na yeye nitamsaidia kufanikisha jambo analolitaka.

"Jambo gani wataka nikusaidie Bonoeza" Nilimuuliza Hamis.kwa kutia jina la utani ambalo hakuwa analipenda kabisa kwa kipindi hicho.
"Shafii waanza sasa nimesema hilo jina silitaki nitaacha kusaidia nikamjaze sumu dada yangu umkose" Hamis alinijia juu baada ya kumtajia hilo jina.
"Hamis nisamehe rafiki yangu niambie shida yako sasa" Nilimuomba radhi na nikawa tayari kuisikiliza hiyo shida yake kwani ndiye rafiki yangu wa shida na raha.

"rafiki yangu hii ni aibu sana hasa kwa vijana wa rika langu na nimeificha ila kwakuwa wewe ni rafiki yangu wa muda mrefu nimeamua nikueleze ili unisaidie na wewe nikusaidie, kiufupi nampenda sana Salma yule mtoto mzee Rajabu ila mdomo wangu ni mzito kutamka neno hili kwake na ninabaki nikiungua ndani kwa ndani tu" Hamis alinieleza tatizo lake ambalo nilikuwa nipo tayari kumsaidia tu ili nipate moyo wa dada yake kipenzi, tatizo lake lilikuwa ni dogo tu kwani hata Salma alikuwa akimpenda vilevile na ishara zote niliziona ila tu wote hawakuwa na ujasiri huo. Nilimsaidia hadi akampata Salma na mimi akaanza harakati za kunisaidia lakini hazikuzaa matunda kabisa kwani msimamo wa Farida bado ulikuwa ni uleule na hata alipomtumia Salma katika suala hilo ilikuwa vilevile na yeye alizidi kunipa moyo kuwa nitampata ingawa nilianza kukata tamaa juu ya suala hilo.

Niliendelea kumbembeleza Farida lakini sikuchoka kwani niliamini yeye alikuwa akinipenda mimi pia na kama angekuwa hanipendi basi angelikuwa amenishitaki siku nyingi nyumbani kwetu juu ya kumsumbua kwangu lakini hakufanya hivyo, hakika sikutambua kama kaanza kukomaa kiakili na jambo kama hilo hakuwa na haja tena kulisema kwani ingeonekana ni akili za kitoto. Niliendelea kujipa moyo nikijua ipo siku nitampata na sikutambua kama mawazo yangu ni sawa na kuchemsha mawe nikitegemea yatachemke kutokana na upendo mzito nilionao kwake, sikutambua kama najipa matumaini hayawezekani kutokea hivihivi kama kubadilika kwa majira ya mwaka kutoka kiangazi hadi vuli. Nilichojali ni kupata jibu sikujali itachukua muda gani hadi niwe naye, niliendelea kusumbuka katika kumueleza kila siku lakini niliambulia patupu na nikawa natembea na matumaini ya kumpata tu kichwani mwangu. Matumaini yangu yaliishi katika moyo wangu lakini baadaye yalikufa baada ya muda wa miezi kadhaa tu na nikajikuta nikiumia moyoni, kufa kwa matumaini yangu kulikuwa ni baada ya kuingia kikwazo katika kumpata Farida.

Nakumbuka vizuri kijijini kwetu waliingia wageni ambao walipatiwa eneo ambalo baadaye walilinunua wakajenga makazi yao ya kudumu, wageni hao walikuwa ni wenye asili ya tofauti na watu walioko kijijini kwetu kwani wao walikuwa na asili ya uarabu lakini siyo wang'avu kabisa na ninaweza kuwaita wasomali pia. Walikuwa ni mke na mume pamoja na kijana wao mmoja ambaye ni makamo yetu, wageni wenyewe walioingia katika kijiji chetu walikuwa ni Mzee Mubaraka mkewe pamoja na mtoto wao wa pekee Faimu. Kuja kwa huu ugeni ndiyo kikwazo kikuu cha kumpata Farida kilichokuwa kinaniumiza akili, kikwazo hiki sikuweza kukibaini hapo awali kwani Faimu hakuonekana kama atakuja kuwa kikwazo katika kumpata Farida.

Ndani ya mwezi mmoja wa kwanza tangu Faimu awasili pale kijijini kweti tayari wavulana wa rika letu walishaanza kumchukia kwani alikuwa kikwazo kwao kikubwa cha kuwapata wasichana hao, uzuri wa sura, umbo na hata muonekano mwingine alionao Faimu ulifanya awe midomoni mwa wasichana wa karibia kijiji kizima na kila msichana alikuwa na ndoto za kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Faimu na kupelekea kuwa na ushindani mkubwa katika kumpata.

Mabinti hawa walibuni mbinu mbadala ya kufanya waweze kuwa chaguo la wazazi wa Faimu kwani kipindi hicho mzazi akimpenda binti basi hufanya mipango ili aweze kuwa mkwewe, sasa basi ili waweze kuwavutia wazazi wa Faimu walikuwa wakienda mara kwa mara nyumbani kwa mzee Mubaraka wakitumia njia ya kumsaidia kazi mke wa mzee Mubaraka ili waonekane ni mabinti watiifu. Mbinu hiyo ya mabinti wa kijijini kwetu haikujulikana na mzazi yoyote zaidi ya kuona ni tabia njema tu ya mabinti zao katika kuwakirimu wageni ili tu nao wakipata mabinti waje kuwakirimu, hakika ukarimu ndiyo ulikipamba kijiji chetu na ndiyo maana hila hiyo haikugundulika kwa wazazi zaidi ya kubainika na wavulana tu wa kawaida waliozidisha chuki sana kwa Faimu.

Ulipotimia mwaka mmoja tangu Faimu ahamie hapo tayari alikuwa anachukiwa na robo tatu ya wavulana wa kijiji hicho na marafiki zake wakuu tulikuwa ni mimi na Hamis tu, sisi pekee tulikuwa ni marafiki zake wakubwa kutokana na kuwa mcheshi sana kwetu. Katika kipindi hicho hakuwahi kumtambua Farida kwani tangu ahamie alisikia habari za Farida ila hakupata bahati ya kukutana naye ana kwa ana kutokana na kazi mbalimbali zinazomkabili Farida, hata Farida naye kwa mujibu wa Hamisi alithibitisha kuwa hakuwa kumuona Faimu zaidi ya kusikia kuna mgeni kahamia ana urafiki na sisi.
Kusema uongo dhambi na pia kumsifia uzuri mwanaume mwenzio siyo vizuri ila ukweli Faimu alikuwa mzuri sana hadi akafikia hatua baadhi ya kina mama wa kijijini wakaanza kumtaka huku mabinti wengine walidiriki kupigana kisa yeye tu, ilifika kipindi wasichana uvumilivu ukawashinda wakamuambia ukweli na hadi wengine walitoroka majumbani mwao kipindi cha usiku wakaenda kuvamia chumbani kwake ili walale naye lakini bado alikuwa na msimamo wake kama mtu anayejitambua.

Siku moja tukiwa kwenye kijiwe chetu tukiongea nikiwepo mimi, Hamis na Faimu mcheshi wetu aliyetufanya tucheke kila kukicha. Siku hiyo Farida alipita mbele ya macho yetu na ndiyo hapo nikamuonesha Faimu nikamtambulisha ni shemeji yake ili tu amuheshimu na asije akampenda kwani nilishabaini mwenzangu wasichana kwake ni kama mbwa na yeye ni chatu wanamfuata wenyewe, nilipomuita Farida siku hiyo alikataa kuitika akaendelea kwani alikuwa ametumwa na baba yake.

Niliponyamaziwa mimi niliumia sana na ndipo Hamis akamuita akaitika na akajongea pale tulipo kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwake kama kaka yake, Farida alipofika macho yake yalikuwa hayotoki usoni kwa Faimu hadi nikaanza kujisikia wivu ingawa nilijipa moyo baada ya Faimu kumtazama mara moja kisha akainamisha macho yake chini asimtazame tena.
"Farida mdogo wangu heshima wafunzwa nyumbani ila hutaki itumia ukiwa upo nje ya nyumbani, Shafii si akuita mbona wamfanyia hivyo au hapaswi kukuita" Hamis alimuambua Farida ambaye alikuwa ameinamisha macho chini kwa aibu.

"apaswa niita kaka ila ntachelewa, baba kaniagiza kwa mzee Mubaraka nipeleke huu mzigo niwahi rudi" Farida aliongea huku akiangalia chini.
"Si vibaya akikusindikiza basi hebu nenda najua hutochelewa" Hamis alimuambia Farida ambaye alikubali kutokana na heshima aliyokuwa nayo kwa kaka yake, nilimsindikiza Farida huku nikimchombeza kuhusu ombi langu kwake na hata nilipozidi aliiua mada yangu na akawa ananiuliza juu ya Faimu na ikanibidi nimueleze kila kitu na kisha nikaendelea kumchombeza Hadi namsindikiza na kurudi kwa wenzangu sikuwa nimeambulia jibu la kuniridhisha moyo wangu ingawa niliporejea Faimu aliniuliza juu ya Farida niliamua kumdanganya.

"Kila kitu kipo kizuri rafiki na hapa alishindwa itika sababu aona haya yupo kakaye" Nilimdanganya Faimu huku nilichojibiwa kikibaki kuwa siri moyoni mwangu na kwa Hamisi ambaye anajua kila kitu juu ya kukataliwa kwangu.
"Shafii nipe mkono" Faimu aliniambia huku akitabasamu na mimi nilimpatia bila hata hiyana, Faimu alinipa mkono kwa ishara ya kutoleana pongezi halafu akaniambia, "hongera sana Shafii wajua kuchagua haswa rafiki nikupe hongera".

Maneno ya Faimu yalinifanya nitabasamu ingawa moyoni nilijiona ni mjinga kwa kupewa sifa nisizostahiki kupewa na nilipata ahueni sana na nikawa na uhakika Farida ni wangu tu kwani niliyemuhofia hakuonekana kuwa na muda nae hivyo sikuwa na mpinzani kwani kijiji kizima nilishawapa vitisho vijana wenzangu kumfuata Farida nikiwaambia ni mali yangu. Baada ya siku hiyo urafiki wetu ulidumu kama kawaida ingawa ulikuja kuingia dosari miezi mitatu mbele kutokana na taarifa aliyotuletea Salma ambaye alikuwa ni shemeji yangu kwa Hamis, siku hiyo nilijikuta nikipandwa na ghdhabu sana kutokana na taarifa hiyo kwani iliniuma mno tena iliniuma sana.

Salma alituletea taarifa ya kuwaona Faimu na Farida wakifanya jimai katika kichaka kilichopo kando ya mto ambao tunautumia kuchota maji ya matumizi ya nyumbani, Salma alieleza kuwa wote walikiri kuwa wanapendana na ndiyo chaguo la kila mmoja.
Iliniuma, iliniuma tena sana kupata taarifa hiyo kutokana na kumpenda sana Farida aliyekuwa hana upendo na mimi Nilitamani kumfanyia jambo la kwenda kumpiga Faimu na nimuonye juu ya kuachana na Farida lakini Hamisi alinizuia akiniambia sina mahusiano na Farida na ningefanya hivyo na Farida akatangaza ningeumbuka sana. Maneno ya Hamis niliyaafiki na hapo ndipo tukaanza mikakati ya kumfanyia kitu kibaya Faimu, niliwashirikiaha wadogo zangu wote katika mpango huo kasoro Ally ambaye sikumuamini kutokana na urafiki wake na Faimu ambao nilikuwa siuelewi. Hamid ,Haasan, Hussein na Falzal wote walikubali kumfanyia njama Faimu kwani wasichana waliokuwa na mahusiano nao walikuwa wakimpenda Faimu hivyo jambo hilo liliwakera sana, tulianza kusuka mpango wa kumkamata Faimu akipita kuelekea kuchunga mbuzi wa kwao ili tumuue lakini mpango huo ulishindikana kwa namna ambayo haikueleweka.

Mara ya kwanza tulipanga tumuue akiwa machungani akichunga mbuzi lakini tulipoenda tulimkosa kwa siku mbili tofauti ambapo tulimuona ni yeye alikuwa amepeleka mbuzi machungani lakini tulipoenda tulikuta anayechunga mbuzi ni mzee ambaye hatumjui, mpango huo ulishindikana kwa mara nne mfululizo na hata yule mzee tunayemkuta tukimuuliza anasema ameondoka baada ya kuleta mbuzi huku machungani. Muda wa kurudisha mbuzi alikuwa akionekana ni yeye anarudisha hao mbuzi, tulipomfuata kwa urafiki wetu wa kinafiki na kumuuliza juu ya alipokuwa alituambia huwa anatoka kidogo tu akimuachia yule mzee ila anarudi. baadaye.

Mipango ya kumuua ilipokosa mafanikio ndipo tukatumia mbinu nyingine tofauti ya awali ingawa nayo haikufanikiwa, tuliamua kwenda waganga wa kijijini kwetu ili tumuue kwa njia ya uchawi lakini cha ajabu waganga wote walisema hilo suala haliwezekani, mwishowe tukaamua kumuhadaa rafiki wa baba yetu kipenzi mzee Mahmud ili amuue kwani tuliamini yeye ndiyo mganga mwenye nguvu peke yake kijijini kwetu lakini baba yetu naye alikataa katakata akisema siyo kazi yake kufanya ubaya.
"wanangu mnalolitafuta nj kubwa sana tofauti mnavyofikiria, Faimu ni mwenye nyota kali sana hakuna mganga yeyote awezaye kuizima na yasimkute matatizo labda Muumba amnusuru. Pia siui bali naagua" Nayakumbuka maneno ya baba yetu ambaye ni sawa na baba yetu aliyepelekea uzao wetu alivyotuambia
"Kaka twafanyaje sasa maana yule simpendi sana" Hamid aliongea tukiwa tunajadiliana nyumbani kwetu baada ya kutoka tu nyumbani kwako Baba yetu Mzee Mahumd.

"jamani sikilizeni, yabidi twende kwa baba yake Sauti ya radi wa pale Maforoni nafikiri tutaweza" Hussein alitoa wazo ambalo nililiafiki na nilipanga kwenda mwenyewe huko Maforoni, siku iliyofuata asubuhi na mapema nikaenda maforoni kwa kupitia njia ya mkato na nilitumia muda mfupi tu nikawa nimeshafika kutokana na kutumia baiskeli yenye uwezo mzuri. Nilifika nikapokelewa vizuri na yule mganga na nikamueleza tatizo langu lote, mganga huyo aliongea na walimu wake kwa muda mfupi kisha akaniambia "Kijana huyo mpinzani wako ana nyota kali sana na kumuua haiwezekani sema nakupa dawa moja utaenda mchanganyia huyo binti kwenye maji ya kunywa na akinywa yeye atakupenda wewe milele tu, huyo mbaya wako atakuwa hana nafasi tena".

Mganga alinipatia dawa hiyo ya unga na nilirejea kijijini haraka sana nikawaambia ndugu zangu nilipofikia kisha tukamuita Hamis na tukamuambia kila kitu, Hamis akasema tumuachie hiyo kazi ataimaliza na kweli tulimuachia hiyo akaifanya na matokeo yakaja mazuri sana.
Farida alianza kunipenda mimi akawa hamtaki Faimu jambo ambalo lilikuwa ni ajabu kwa Faimu ambaye alizidi kumfuata Farida na hatimaye alitukanwa sana mbele za vijana wengine na kusababisha vijana wazidi kumcheka. Faimu hakukoma alizidi kumfuatilia Farida na majibu yakawa ni yaleyale, na huo ndiyo ukawa mwisho wa penzi lao.

Nakumbuka mara mwisho Faiz alimfuata Farida kisimani akalazimisha penzi na matokeo yake yalikuwa ni mabaya, kwani Farida alipiga kelele za kuwa anabakwa na sisi tuliokuwa karibu tukamvamia na kuanza kumpiga na baadaye watu waliongezeka hasa vijana wanaomchukia ambayo walimpiga sana kisha akapelekwa kwa kiongozi wa kijiji. Wazazi wake waliitwa wakaelezwa juu ya hilo ambalo lilikuwa ni aibu kwao na jambo llililowakera, baada ya siku kadhaa kiongozi wa kijiji alimfukuza Faiz katika kijiji na ikawa ni furaha kwa vijana wa kijiji hicho pia huzuni kwa wasichana waliompenda kwani hakuwahi kuonekana hadi leo hii".

Hadi anafikia kituo kueleza juu ya hilo tayari Bi Farida alikuwa analia kwa kwikwi baada ya kubaini jambo alilofanyiwa na Shafii, Zayina naye alisikitishwa sana uovu alioufanya baba yake. Zalabain hasira zilimpanda zaidi hadi macho yakawa mekundu lakini hakufanya lolote juu ya hilo kutokana na kuzuiwa na mzee Mahmud, hasira zilipomzidi Zalabaun machozi yalimtoka na akawa anatetemeka hadi midomo ikawa inacheza.

Upande wa mzee Buruhan hasira zilimpanda kwa ujinga wa mwanae lakini alipotaka kuongea Mzee Mahmud alimzuia kutokana na masharti aliyowapa, mzee Mahmud alitazama hali za watu waliomo humo ndani na mwisho wake akayatuliza macho yake yaliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kutokana na uzee kwenye uso wa mzee Buruhan. Alimtazama mzee mwenzake halafu akasema, "mzee mwenzangu nadhani unakumbuka zaidi kile kisa nilichokusimulia nikitumia mafumbo pia nikiongeza chumvi ili usijue na nilikuambia muendelezo wake utaujua sasa usikilize huo muendelezo wake leo. Nilitia chumvi kukuambia hakuna aliyejua usiri wa penzi la Giguna ambaye ndiye huyu Farida na Mufeji ambaye ni Faimu ila ukweli ni kwamba kuna mtu mwingine ambaye alikuwa anajua ambaye ninampa Nikuza ambaye ni mdogo wa mwisho wa Nukeze au Shafii mdogo huyo ukipenda muite Ally. Haya Ally tusimuulie kile unachojua katika uhusiano wa Farida na Faimu".

Ally aliposikia maneno hayo alimtazama sana kaka yake kwa chuki kisha akamtazama Bi Farida kwa huruma sana halafu akafunguka kile anachokijua, "Baada ya mimi kuanza kupevuka tu tayari Faimu alikuwa ni mwenyeji ndani ya kijiji chetu na alikuwa ni rafiki wa huyo firauni wa kizazi hiki, Faimu namkumbuka kama mtu aliyenizidi umri ambaye alikuwa anapenda kukaa na mimi na hakutumia udogo wangu kwake kuwa sababu ya kunitenga kama ilivyo hao ndugu zangu. Nilimpenda kutokana na uchangamfu wake na hata kunishauri mambo mengine katika umri huu wa upevukaji tofauti na wengine walioniacha nikacheze na watoto wadogo walionizidi umri kwa kisingizio kuwa sijakua, katika kipindi hicho niliomba ushauri kwake pia baada ya huyu Salma niliyemuheshimu kuanza kunitaka kimapenzi na alinishauri vizuri nimkatae.

Siku moja nakumbuka niliwakuta Farida na Faimu wakiwa wamekaa kihasara sana niliyeambiwa ni shemeji yangu, iliniuma sana ila nilikuwa kawaida baada ya kujua juu ya uhusiano wao na nilipotambua kuwa hakuwa shemeji yangu kama nilivyoambiwa. Niliukubali uhusiano wao kwa mikono miwili na niliufanya siri yangu kutokana na kaka zangu kutonihusisha katika yao, hata Salma alipokuja kuniambia juu ya kubaini hilo nilimuambia wamependana hivyo uwaache ingawa yeye alisema anaenda kumuambia mchumba wake na mimi nilipuuzia tu kwani namjua huyo ni mmoja kati ya wasichana walioenda nyumbani kwa mzee Mubaraka ili tu aonekane na Faimu kwakuwa anamtaka. Siku moja ndipo huyuhuyu Salma aliyekuwa ananitaka aliniletea taarifa ya uhusiano mpya wa Farida na Shafii ambao umeanza , nilienda kumuuliza Faimu juu ya hilo na akanibainishia kuwa Farida hamtaki. Sikutaka kuamini moja kwa moja nikamfuata Farida mwenyewe kwani alikuwa ananiheshimu na mimi namuheshimu, sikujali ndugu yangu kumpata ila niliangalia yule aliyenijali zaidi hata ya ndugu anavyonijali akiumia mimi iliniuma pia kwani nilimuheshimu sana.

"Farida umekuwa vipi? Si uliniambia wampemda Faimu wewe ni nini kimekupata?" Nilimuuliza Farida.
"Sikumpenda Faimu ila nilipotea njia ila sasa simronda(simtaki)" Farida aliniambia tena mwishoni akazidi kuniwekea msamiati wa kidigo akiniambia hamtaki.

"Farida kumbuka ulisema Faimu ndiyo chaguo lako leo umehamia kwa kaka yangu tena" Nilimuambia Farida nikiwa hata simuelewi.
"haaaa! Ally aaambiwa mimi huyo Farida mchetu(binti) wa Jumanne nimesema hivyo? Ally nampenda Shafii na sikumbuki Faimu nilimpenda vipi, niheshimu kama shemejio kwa kaka yako kama ninavyokuheshimu" Farida aliniambia neno hilo ambalo lilinichanganya na nikampelekea taarifa Faimu ambaye pia alionekana kuchanganywa ila zaidi yangu. Baada ya muda zilinijia taarifa za kutaka kumbaka Farida na nilienda kumshuhudia hiyo siku anayopigwa na roho iliniuma kutokana na jinsi alivyonipenda, baada ya kupona majeraha yake Faimu alikuja kuniaga akahama kijiji na sikumuona tena hadi leo hii na niliendelea kumuheshimu Farida kama alivyoniambia nimuheshimu. Baada ya...."

"Basi Ally ishia hapohapo kwa kusimulia unachojua juu ya kaka yako......Mzee mwenzangu umesikia hayo yanayosemwa nataka uujue muendelezo wa kisa chetu hadi mwisho. Salma wewe ueleze ukweli wote siku ya kwanza kumuona Faimu jua ukidanganya yatakayokupata shauri yako kuna nguvu kubwa hapa" Mzee Mahmud alimkatisha Ally kisha akamgeukia Mzee Buruhan akamuambua maneno machache, alipomaliz alimgeukia Salma akuambia asimulie na akamuonya juu ya usemaji uongo.

Salma aliposikia hayo maneno alijifikiria kwa muda mfupi kisha akaanza kusema, "Baada ya Faimu kuwasili kijijini kwetu nilimuona ni mstarabu kumbe ni mshenzi kupi...". Salma alishindwa kumalizia kauli yake baada ya eneo alilokaa kutokeza shimo kubwa kwa nyuma na nguvu kubwa ya upepo ikawa inamsukuma kuangukia kwenye hilo, alipiga kelele akijua wenzake wameona kule alichokiona kumbe alikuwa amekiona yeye, Mzee Mahmud na Zalabain tu. Kelele zake ziliwashangaza wengine wote waliomo humo kasoro waliiona kilichomtokea, Zalabain naye aliposikia kauli ya Salma hasirs zikampanda ila alishindwa kunyanyuka baada ya nguvu kubwa iliyopo hapo kumzuia. Mzee Mahmud alinyoosha mkono akatamka maneno yasiyoeleweka na lile shimo likapotea, hali ya kawaida ikarudi kama awali huku Salma akawa anahema kwa uoga.

"Kwanini unakuwa mbishi binti si nimekuambia uache kusema uongo unadhani hii ni sehemu ya kudanganya, nimekuambia kuna nguvu nzito hapa au huelewi? Sasa rudia tena iwe mwisho wa maisha yako" Mzee Mahmud aliongea kwa hasira halafu akamgeukia Zalabain akamwambia, "Huna nguvu ya kufanya hivyo bila nguvu zilizopo hapa kukuruhusu kufanya unachotaka kufanya hivyo tulia kwanza usiendekeze hasira mbele ya nguvu kubwa".
"Haya endelea kusimulia na uwe mkweli" Mzee Mahmud alisema.

Salma aliposikia kauli ya mzee Mahmud hakuwa na ujanja zaidi ya kusimulia yaliyompata akiogopa kufa na aliongea, "Urafiki wangu na Farida ni wa siku nyingi sana na yeye alinijua kama wifi yake mapema kabla ya waru wote kujua, hata shemeji Shafii alipoanza kumpenda alinisihi nimbembeleze ili akubali na mimi nilifanya hivyo lakini aliendelea kushikilia msimamo wake uleule wa kutokibali kuwa na Shafii. Nilijitahidi sana mwisho nikachoka nikaamua kuacha na nikawa namuonea huruma sana shemeji yangu kwa jinsi anavyoumia, baada ya muda kidogo kupita ndipo familia ya Faimu ilipoingia hapo kijijini kwetu na nilipomuona Faimu kwa mara ya kwanza nilijikuta nampenda na nilitaka kuwa naye kwani nilishazoea kukaa na kutembea na wanaume mbalimbali na nilianza haya hata kabla sijampata Hamis na nilipokuja kumpata nilitulia ila nilijikuta nikiirudia tabia yangu hiyo kwa mara nyingine tena niliifanya kwa mara mbili tofauti.

Mara ya kwanza nilianza kwa Faimu nikawa najipitisha sana kwao ili anuone nikijua nitamnasa tu kama nilivyonasa vijana wa hapo kijijini kumbe Faimu hakuwa kijana wa hivyo, uvumilivu uliponishinda niliamua kumuambia ukweli lakini pia nilimkosa baada ya kukataliwa na akanitishia kumuambia Hamis. Mara ya pili niliirudia tabia yangu kwa kumtaka Ally baada ua uzuri wake kuonekana alipofikia kwenye balehe lakini pia alinikataa nikajikuta nazidi kumsumbua nikijua nitampata tu kwani ni mtoto yule bado akili haijapevuka zaidi ya kupevuka mwili tu, nilipoona nakataliwa sikuchoka na niliamua kuanzisha mazoea ya kawaida naye. Siku nilipokuja kuwafuma Farida na Faimu na wote wakakiri kuwa wana uhusiano ndiyo siku niliyoona ya kutumia sababu hiyo kwa njia mbili, kwanza ni kulipa kisasi cha kukataliwa na Faimu na pili ni kumteka Ally kiakili. Nilijua Ally ni bado ana akili za kitoto hivyo nilipanga nimuambie hii habari ili ajue ni jinsi gani nampenda hadi nikaamua kumuambia hiyo habari ili aamini moyo wangu upo kwake, pia nilitaka nimuambie mpenzi wangu juu ya usaliti wa rafiki yao kwao waweze kumfanyia kitu kibaya ili nimcheke na hata amkose Farida.

Sikutaka kurudi nyuma katika azma hii ambayo niliiweka na hapo ndipo nilipoona ni nafasi nzuri ya kuweza kujipa furaha niliyokuwa naitaka, nilianza kutimiza azma hii kwa kumuambia Ally juu ya uhusiano wa Farida na Faimu nikijua na yeye ataumia akisikia kaka yake ameporwa tunda alilokuwa akilitaka kila siku ili aweze kulimiliki katika mkono wake. Tena nilijifanya naongea kwa hisia zaidi ili nimteke akili zaidi kwa kuamini huyu bado ni mtoto, nilimuambia lengo la kumuambia hiyo habari ni kutokana na jinsi gani nampenda na sipendi aumie akisikia kaka yake ameumia kwani na mimi nitaumia pia kutokana na jinsi ninavyompenda yeye. Nilizidi kuongea kihisia kwa kumuekeza ni jinsi gani namuamini mpaka ikafikia kumuambia hayo mambo kwani nilihisi ndiyo mahali salama ya moyo wangu, nilijivika ujasiri tofauti na watoto wengine wa kike nikiwa naeleza hayo maneno ambayo nilijua kabisa kwa mtu kama Ally mwenye kusumbuliwa na mihemko ya upevukaji basi nitaweza kumpata kirahisi jambo ambalo lilikuwa kinyume na nilivyotarajia.
Baada ya kutua maneno yangu yote niliyokuwa nimeyapanga kinywani mwangu Ally alinitazama sana kisha akaniuliza, "hivi watu wakipendana na wenyewe wakiridhiana kuna haja ya kuwafuatilia?"
Nilimjibu, "hakuna haja ya kuwafuatilia".

Jibu langu hilo nilimjibu kirahisi tu kwani bado nilimuona mtoto na ana itikadi za kitoto hivyo sikuhofia kabisa kama ataongea neno jingine kwa jinsi anavyompenda kaka yake, nikiwa nasubiri ni nini atasema kifua chake kilipanda na kushuka kuashiria anashusha pumzi ili aongee kitu ambacho niliamini kabisa atakuwa ameguswa na maneno yangu.

"Sasa kama hakuna haja ya wafuatilia basi Farida na Faimu nao wamependana haina haja ya wafuatilia waache na mapenzi yao na pia usitegemee nitaumia kwa jinsi kaka yangu anavyolazimisha kupenda kwa Farida ikiwa hatakiwi. Tena ukirudia tena nitongoza kwa njia hii nitakushtaki kwa kaka ili amuambie Hamis wakujue tabia yako ambayo waifanya kwangu" Ndiyo maneno yaliyotoka kinywani kwa Ally baada tu ya kumuambia kuhusu hiyo habari hadi nikawa najiona kama nimepungua umri na umbo kutokana na maneno yake jinsi alivyoniumbua.

Nilikubali kwa Ally nimeshindwa kwa siku hiyo labda nijaribu kwa mbinu nyingine kabisa tofauti na ile ili niweze kumpata kwani alinivutia sana, niliamua sasa kwenda kuifanya njia yangu ya pili ya kwenda kumuambia Hamis ambayo ilifanikiwa kwa kiasi kikubwa sana kwani alichukizwa sana na kusikia Faimu ana mahusiano na dada yake na taarifa hiyo ilifikishwa kwa Shafii na mipango hiyo ya kwenda kwa mganga ili kumkomoa Faimu ndipo ilipoanza".
Salma aliweka kituo kikuu katika kusimulia kwake na hadi muda huo mzee Buruhan alikuwa akimtazama kwa hasira sana kutokana na kuujua ukweli wa tabia yake, watoto wake nao walioneshwa kuwa na mshangao hasa wa tabia aliyokuwa anafanya mama yao kwani hawakutegemea kama ataweza mambo kama yale.

Upande wa Bi Farida baada ya Salma kumaliza kusimulia kilichompata tayari hasira dhidi ya shoga yake kipenzi zilikuwa zipo juu na mawazo ya urafiki nae yalikuwa yameshatoka kichwani mwake, alimtazama wazi kwa macho yaliyojaa chuki kuu iliyoongezewa na machozi yenye uchungu kutokana na masikio yake kupata hiyo habari ya kuwa rafiki yake aliyempenda na kumuamini amekuwa akimzunguka kwa miaka mingi bila ya yeye mwenyewe ingawa alimuamini sana na kumthamini.

Ama kweli kikulacho kinguoni mwake kama waliozaliwa toka awali walivyonena na rafiki yako ndiye adui yako kama ambavyo waliozaliwa toka walivyotoa maana ya msemo wao huo waliounena, ama kweli rafiki anaweza akawa siyo rafiki kama ambavyo Salma alivyokuwa akifanya kwa Farida haikustahiki aitwe rafiki kwani kafanya yasiyostahiki kufanywa na anayeitwa rafiki kwani ni usaliti mkubwa sana alioufanya.
Baada ya kisa hicho mhusika wa aliyeita hapo familia zote ambaye ni mzee Mahmud alikuwa akimtazama kila mtu aliyepo eneo hilo katika uso wake ili kujua hali zao zipo vipi waliposikia simulizi hiyo, alizungusha shingo yake iliyozungukwa na ngozi iliyofunyaa kwa kila mmoja aliyepo eneo hilo huku akiwa mithili ya mtu anayechambua fikira za mtu zilizomo ndani ya ubongo wake na mwishowe akayatuliza macho kwa rafiki yake kipenzi wa tangu, ujana na hadi wanazeeka pamoja. Mzee Mahmud alimtazama rafiki yake hadi alipobaini katambua kama anamtazama ndipo akafungua kinywa chake, "mzee mwenzangu umesikia mambo ya watoto wetu hayo? Je una lolote la kusema kabla sijaendelea na kinachofuata?"

Mzee Buruhan alipoulizwa hilo swali alimtazama Shafii kwa umakini kisha akamuuliza, "Shafii hivi Farida ni nani yako?"
"ni mke wangu baba" Shafii alijibu akiwa ameinamisha uso wake chini kutokana na aibu aliyonayo kwa baba yake baada ya mabaya yake kubainika.
"Kwa kigezo kipi Farida mkeo we mwana? Aliridhia kwa moyo wake wakati unaenda kutoa posa au kizizi chako ulichokichukua huko Maforoni ndiyo kilimfanya aridhie?" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali wa wastani na kusababisha Shafii atazame chini kwa aibu kutokana na kitendo alichokifanya kwani kilikuwa cha aibu sana tena amekieleza mbele ya watoto.

"Wajukuu samahanini sana kama nitakuwa nimekosea na pia nitakuwa sijaongea kauli nzuri kwa mujibu wa maadili yetu mbele yenu nyinyi. Ila lazima niseme ukweli juu ya hili, alichokifanya huyu ambaye ni mjomba kwa wengine na pia ni baba kwa mwingine ambaye yupo hapahapa ni sawa na kumuingilia mwanamke akiwa amelewa hivyo ninaona alikuwa anabaka na hayupo katika ndoa. Sina la ziada mzee mwenzangu" Mzee Buruhan aliongea maneno yaliyozidi kumuumiza Shafii na pia kumtia sibu mbele ya mtoto wake pamoja na wapwa zake, maneno hayo yalimfanya Zalabain azidi kuwa na hasira na mama azidi kulia kwani alikuwa amekosewa haswa na kosa kubwa lenye kujaza maudhi tele kwa kiumbe yoyote mwenye uhai na aliyejaliwa akili na matamanio.

SURA YA TISA

Mzee Mahmud naye alisikitika sana hulu akimtazama Shafii na Salma kwani alijua fika wamefanya ujinga mkubwa sana ambayo utawafanya waumie na wajute kwa muda mfupi tu na hawatapata bahati ya kuusafisha ujinga huo tena katika dunia hii kwani wakati wake ulipita wakati jambo hilo wanalifanya. Walikuwa wamepoteza muda wao mwingi katika matumizi mabaya yasiyofaa na walifanya kosa pasipo kusahau kubwa hawataweza kulisahihisha tena hilo kosa, kwani muda wake ulishapita tayari hivyo matumizi yao mabaya ya muda wao kipindi cha nyuma ndiyo yalimfanya mzee Mahmud awasikitie kila akiwaangalia.

Giza nje ya eneo hilo lilikuwa tayari lishaumeza mwangaza mdogo wa muda wa magharibi ambao waliukuta kipindi wanaingia eneo hilo, nuru yote ilishapotea tayari na kiza kizito kikawa kimelimeza eneo lote kwa nje kutokana na uwepo wa miti na mapori katika eneo la jirani na hiyo nyumba. Majira hayo yalimfanya mzee Mahmud aendelee na utaratibu aliouweka kwa haraka ili usiku mnene usiwakute wakiwa eneo hilo, na kutokana na msjira hayo ilimbidi aseme "Shafii sasa endelea kusimulia ulipoanza mahusiano yako na Farida hadi mnaishi kwa pamoja".

Sauti ya mzee Buruhan ilifika mapema zaidi hata ya robo sekunde tu tangu azungumze katika masikio ya Shafii ambaye naye alinyanyua kinywa chake na kusimulia, "Baada ya Farida kuwepo katika mikono yangu na kuwa msichana nilikuwa nikikutana naye kimwili kupunguza mihemko ya ujana na pia nilifanya hivyo ili tu nikija kumkosa niwe tayari nimeshatumia mwili wake kwani hilo ni jambo la fahari sana kwa kijana kama mimi, sikuwa na imani na dawa hizo na niliamini dawa niliyomfanya anipende itaisha tu kutokana na kiwewe cha kupendwa ghafla na sikuwa ninaamini kabisa kama nitakuja kuendelea kukaa naye. Nilianza kuingiwa na imani ya kuendelea kukaa naye baada ya Hamis kunishauri nipeleke posa nyumbani kwao nimuoe moja kwa moja kuliko kusababisha mimba mapema, jambo hilo nililikubali kwa mikono miwili na nikaona hiyo ndiyo njia inayofaa ili kumfanya Farida awe wangu kabisa na hata kama Faimu akija kujua ajue tayari amemkosa Farida na si mali yake tena. Kwa mara ya kwanza katika ujana wangu nilijivika ujasiri na kumueleza baba yangu juu ya suala hili na yeye alifurahishwa na uamuzi wangu wa kwenda kuposa akiniambia tayari nilishakuwa mkubwa na hilo ndiyo jambo la maana nimeamua kama kijana anayejitambua, baba yangu alienda kumueleza mzee Jumanne ambaye ndiye baba mzazi wa Farida ambaye aliridhia kwa mikono miwil hilo suala kutokana na utiifu nilionao kwake hapo kijijini. Taarifa hiyo ilipelekwa kwa Farida ambaye alikubali na furaha yangu ikazidi na hapo ndipo nikazidi kuamini ile dawa ya mganga ambaye ni baba mzazi wa mzee Sauti ya radi ilifanya kazi na inaendelea kufanya kazi na wasiwasi wa kumoksa Farida sikuwa nao kabisa, baada ya muda mfupi baba yangu aliweka kila kitu sawa ndos ikafungwa na tukayaanza maisha yetu katika nyumba ya baba yangu iliyokuwa ipo shambani kwake huku wazazi wa pande zote mbili wakituahidi kututafutia makazi yaliyobora kwa ajili yetu.

Maisha yetu na ndoa na Farida yalikuwa ya furaha kwa kipindi cha mwaka wa kwanza na katika kipindi hicho nilikuwa tayari nishaanza kufanya shughuli ili nipate kipato kwa ajili ya familia yangu na mke wangu maisha yetu yaende mbele, mwaka wa pili wa ndoa yetu ulipoingia Farida alianza kuweweseka usiku na alipoamka asubuhi alikuwa mchovu sana hali iloyozidi kunipa wasiwasi sana na ikanilazimu niende kwa baba mzee Mahmud akanipa dawa ambaye nilimpatia dawa ambayo ilimsaidia Farida sana akawa hapatwi tena na hali hiyo, baada ya Farida kupona hilo tatizo haikupita hata muda mrefu akashika ujauzito ambayo ulinifanya niwe na furaha sana na hata wazazi wa pande mbili walijawa na furaha baada ya kuwapa taarifa hiyo. Furaha ya wazazi baada ya Farida kupata ijauzito ilionekana wazi baada ya kutupatia zawadi iliyotufurahisha zaidi, wazazi wa pande zote mbili walijenga nyumba kubwa hadi ikaisha bila sisi kutambua na walikuja kutukabidhi baada ya kuwapelekea taarifa ujauzito na wakatuambia ndiyo sehemu ya pekee itayotufaa kuanzisha familia yetu. Nyumba yenyewe ndiyo nyumba hii ambayo tumo wote hivi sasa ambayo ilitufanya mimi na mke wangu kuhama kule kijijini na kuja kuishi hapa Mpirani nikiwa na mdogo wangu Ally, tuliyaanza maisha mapya kwa furaha sana na mdogo wangu Ally tayari alikuwa yupo shule ya msingi akiwa yupo ukingoni kumalizia elimu hiyo.

Miezi tisa ilipitimia Farida alijifungua mtoto wa kiume mwenye afya nzuri ambaye alizidi kuongeza furaha ya ndoa pamoja na furaha ya wazazi wetu ambao walikuja kututembelea na wakapata bahati ya kumuona huyo mtoto aliyelepekea furaha yetu izidi, mtoto huyo tulimpa jina la Jamadin ambalo ni jina la babu yangu mzaa mama ili jina hilo zuri lisiweze kupotea bila kupatikana mrithi wake ndani ya dunia hii kama ilivyo kawaida ya jamii zetu kurithisha watoto wao majina ili tu jina liwepo na liendelee kuwepo. Jamadin alikuwa ni mtoto mchangamfu sana na aliyefanya familia yetu iwe na furaha kuputiliza, matendo yake ya tangu utoto yalikuwa ni yenye kufurahisha na ndiyo maana familia yetu ilizidi kuwa na furaha. Kipindi hicho tayari Ally alikuwa ameshamaliza elimu ya msingi na alikuwa anasubiri majibu ili aweze kuendelea na elimu ya sekondari ambayo ilikuwa ikionekana na hadhi kubwa kama mtu akiisoma, muda huo wa kusubiri majibu ndiyo muda ambao Ally alikuwa akiutumia kucheza na Jamadin hadi akawa amemzoea sana kuliko hata mimi niliyekuwa nashinda kwenye mihangaiko Makorora na kurejea nyumbani jioni sana. Baada ya mwaka mmoja kupita tayari Ally alikuwa sekondari na ndugu zangu wengine wote walikuwa wapo Tanga mjini tukifanya shughuli pamoja baada ya kuoa kila mmoja, furaha ya kuwa karibu na ndugu zangu ndiyo ilizidi maradufu kwani kazi tuliifanya kwa umoja na kuzidi kujiingizia kipato kwa ajili ya familia zetu ambazo zilitegemea sana uchapaji kazi wetu ili ziweze kujipatia chakula na mahitaji mengine muhimu.

Kipindi hichi ndiyo Hamis naye alikuja kuungana nasi baada ya kumuoa Salma na alipata nyumba ya kukodisha Usagara akakaa huko na tukawa tukifanya kazi pamoja, miaka miwili baadaye Ally akiwa kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Usagara ilibidi tumuhamishie nyumbani kwa Hamis ili awe karibu na shule asome vizuri. Tuliendelea kuchapa kazi kwa kipindi hicho hadi tukawa na mafanikio kidogo yaliyoniwezesha kuhama Mpirani nikaja kuishi Chumbageni baada ya kuweza kukodi nyumba nzuri iliyoniwezesha kukaa vizuri na familia yangu. Ally alimaliza kidato cha nne alikuja kuungana na sisi Chumbageni na kuifanya familia yetu iwe na furaha zaidi kwani Jamadin alikuwa amekaa karibu na Ally mtu anayeelewana naye sana. Mwaka huo aliomaliza Ally kidato cha nne ndiyo mwaka ambao mambo yalibadilika kwa nna ya kustajabisha sana, vitega uchumi vyetu vilianza kuyumba na kupungua katika namna ya kustajabisha sana hadi ikafikia tukawa na kitega uchumi kimoja tu ambacho nacho kilitekea na moto katika mazingira ya kutatanisha. Hali hiyo ilitufanya tuanze kufanya kazi kama waajiriwa ili tuokoe familia zetu na tuweze kusogea hatua kadhaa kimaendeleo, tulifanya kazi na kulisha familia zetu pamoja na kulipa pango la nyumba na hakukuwa na pesa nyingine yoyote iliyobaki tuseme tutatumia kuanzisha shughuli nyingine.

Mambo yalipoanza kuzidi kuwa mabaya wote kwa pamoja tuliweka kikao nyumbani kwa Hamis na tukashauriana tuende kumuona mtaalam aliyetusaidia kumuondoa Faimu kijijini huenda akatusaidia cha kufanya ili tuweze kukomboka katika balaa hili, siku iliyofuata wote kwa pamoja tulienda Duga maforoni kwenda kuonana na mganga wetu aliyetufanyia dawa miaka kadhaa iliyopita. Safari hiyo ya kwa mganga ndiyo iliweza kubainisha tatizo la kukwama kwa mambo yetu, tulimkuta mtoto wake yule mganga ambaye ni Sauti ya radi ambaye alitutajia tatizo kubwa la kuharibika kwa shughuli zetu niliambiwa lipo kwangu na tulihitaji utatuzi basi nikubaliane na sharti la kutoa kile kinachofanya kuwe na kssumba katika mipango yetu. Nakumbuka vizuri maneno ya mganga Sauti ya radi aliniambia, "mtoto unayelea ndiyo kikwazo cha kukwama kwa matatizo yenu na kama mkitaka mfanikiwe basi yule mtoto anatakiwa atolewe sadaka katika eneo alilozaliwa na baadaye utakuja kupata mtoto wa pili wa kike ndiye akikua utajri utazidi na hata wenzako watatajirika pia".
Kweli ilikuwa ngumu sana kukubali lakini nilipoelezwa juu ya nguvu kubwa za maajabu alizonazo yule mtoto kiasi kwamba ameweza kutambua uchawi nilimuwekea mama yake hadi nikampata. Mganga alienda mbali akanitajia uajabu wa huyo kama siamini niende nikamkate kidogo mkononi mwake nijifanya ni bahati mbaya halafu niangalie kitakachotokea, siku hiyo nilirudi nyumbani nikiwa nimechanganywa na masharti ya mganga na nikaagana na wenzangu nikawaambia kesho tutajua cha kufanya kingine.

Sikutaka kuamini mambo ya yule mganga nimtoe kafara mtoto wa pekee niliyekuwa naye wakati hata wa pili bado sijajaliwa, nilipingana na suala hilo lakini nilitaka nijaribu vile alivyoniambia mganga ili nione itatokea vipi. Majira ya alasiri siku hiyo nilikuja na mpira wa upepo wa ndani ya baiskeli nikawa na panda kipende cha mti kinatumika kutengeneza manati, nilimuita Jamadin nikamuambia anishikie miandae mipira kwa ajili ya manati nataka kuipeleka shamba itumiwe na banu yake. Jamadin alinielewa mapema ingawa ndiyo kwanza alikuwa ana miaka mnne, alishika nilivyomuelekeza na nilianza kukata ule mpira wa baiskeli na nikajifanya nimekosea nikamkata na kiwembe na damu ilimtoka lakini alitulia kimya tu. Kitendo hicho kilinichanganua na nikajikuta naangalia pembeni nitafute walau kitambaa nizuie damu isitoke, niliangaza macho pembeni nikakosa kitambaa na niliporudisha macho sehemu niliyomkata Jamadin nilijikuta nikishtuka hadi nikarudi nyuma kwa uoga. Jeraha lile nililomkata na kiwembe sikuliona na niliona hakukuwa na jeraha sehemu yoyote katika mkono wake, Jamadin yeye alikuwa ananitazama kwa dharau tu nilivyokuwa natetemeka baada ya kutoona jeraha nililomkata na kiwembe.

"Uahajua ulichotaka jua?" Aliniuliza hivyo na nilipokaa kimya aliondoka bila kunisemesha chochote na hapo ndiyo ukawa mwanzo wa mimi kuanza kumuogopa yeye na pia nikajikuta nipo tayari kwa sharti alilonipa mganga Sauti ya radi. Siku iliyofuata nilienda kuonana na wenzangu mapema iwezekanavyo na nikawaeleza juu ya kila kitu nilichokishuhudia na nilikuwa tayari kumtoa Jamadin kwani siyo mtoto wa kawaida, siku hiyo tulienda kwa sauti ya radi na tukaambiwa vitu vilivyokuwa vinahitajika kwa ajili ya kafara ya Jamadin. Ilihitajika jeneza dogo jeusi linalolingana na urefu wa Jamadin, damu ya mwisho wa mwezi wa mwanamke, chupa ya ujazo wa nusu lita yenye mfuniko na kaniki nyekundu mita moja na visu saba. Vitu vingine tuliambiwa vitapatikana hapo kwa mganga na kafara hiyo ambayo ilipangwa kufanyika usiku wa kuamkia siku ya ijumaa ambayo ni keshokutwa yake na mikakati ya kumnasa Jamadin tuliambiwa ianze. Mganga Sauti ya radi alisema atatusaidia katika kumfunga Jamadin asibaini kitakachokuja kutokea. Baada ya kupewa hayo mahitaji wote tulienda kuyatafuta siku hiyohiyo ya jumatano na ilipofika jioni tulikuwa tumeshapata kila kitu, siku iliyofuata tulipanga mikakati ya kumnasa Jamadin katika mikono yetu bila yeyote kutambua ili twende tukamtoe kafara mipango yrtu ifanikiwe.

Ili kutimiza azma yetu ya mtoa kafara Jamadin tuliamua tumtumie Ally kwani ndiyo njia rahisi ya kumnasa Jamadin, siku hiyoida ya alasiri nilimuagiza Ally Makoroea kwa makusudi na Jamadin aliomba kwenda na nikamruhusu kwani hiyo ndiyo njia ya kumnasa. Huko Makorora tulikuwa tumeandaa vijana wa kukodi waliokuwa wanatumia gari aina ya volkswagen tuliyomuazima tajiri mmoja wa jijini Tanga enzi hizo aliyeitwa Brown ambaye ni chotara kwa sasa ni Marehemu, tajiri huyu mwanae wa kiume ndiye alikufa kule Duga Maforoni wakati nyumba za kampuni ya Hamid zilipoungua na pia mjukuu wake smbaye namtambua kwa jina la James alikufa mulemule. Vijana hao walifaniliwa kuwateka Ally na Jamadin na kuondoka nao ambapo njiani Ally alipigwa kisogoni akazirai akatupwa kando ya reli mita chache kutoka katika mzunguko wa Kwa Minchi majira ya usiku, kupotea kwa Jamadin na Ally nyumbani kwangu ilikuwa ni huzuni sana kwa mke wangu lakini kwangu mimi ilikuwa ni kawaida kwani nilikuwa najua kila kitu. Tulikusanyika nyumbani wanaume wote huku mimi nikionekana kulia sana na nilibembelezwa hadi nikanyamza ndipo tulipoanza kujadiliana kimaigizo nini cha kufanya, baada ya mjadala wanaume wote sita tulikubaliana tuongie mtaani kumtafuta Jamadin na Ally na wake wote wakakaa nyumbani kwangu wakimbembeleza Farida.


Tuliwaacha wake zetu na matumaini hewa ya kurudi wakiamini tulikwenda kumtafuta kumbe tulikwenda kufanya kitu kingine tofauti na kumtafuta mtoto huyo, haikuwa safari ya kwenda kumtafuta Jamadin kama walivyokuwa wakifikiria bali tulikuwa tunaenda kumalizia shughuli yetu tuliyoambizana na mganga Sauti ya Radi ikamilike siku hiyo. Sehemu ya kwanza baada ya kutoka nyumbani kwangu ilikiwa ni Kisosora upande wa ufukweni mwa bahari ya Hindi jirani na kichaka kimoja, hapo tuliwakuta wale vijana wakiwa na Jamadin waliyemfunga kamba ngumu pamoja na kitambaa mdomoni ili asipige kelele. Walitukabidhi Jamadin kwani tulikuwa tushamalizana nao kila kitu na ilikuwa ni kuagana baada ya kukabidhiana tu, hicho ndicho kilifanyika hapo na sisi tukaianza safari ya kuekea mpirani ambapo tulifika majira ya saa ya tano usiku tukiwa na asusa yetu. Ilipokaribia saa sita mganga alianza kuandaa mazingira ya kuanza ikiwa ni pamoja na shimo kubwa kuchimbwa katika eneo la sebule ambalo ndiyo hapa tumekaa, baada ya kazi hiyo kukamilika alituambia tulizunguke shimo hilo tukiwa na kisu mkononi kila mmoja ambavyo vilikuwa vimefungwa vipande vya kaniki nyekundu upande wa kwenye mpini wa kushikia. Mganga alianza kazi yake kwa kupiga manyanga huku akiimba nyimbo alizozitambua yeye na baada ya muda upepo mkali sana ulisikika ulivuma kama kimbunga kuizunguka nyumba tuliyomo, upepo huo uliendelea kuvuma hadi mlango mkubwa wa kuingilia sebuleni hapo uliokuwa umefungwa ulifunguka kwa nguvu sana.

Ulikuwa ni upepo wenye kuogopesha lakini mganga alituambia tusitetereke na lile duara letu kulizinguka shimo tulilolichimba tuache uwazi upande unaotazamana na mlango, Hamis na Falzal ambao walikuwepo katika upande huo walijisogeza pembeni kwa kutusukuma sisi na sisi tulisogea ili waweze kutimiza maelekezo ya mganga ya kupisha njia. Upepo ule mkali uliendelea kuvuma na ulizidi kutuogopesha sana lakini tulijikaza kisabuni kama watoto wa kime, ulizidi kuvuma na hatimaye ukaingia ndani ukapita pale kwenye upenyo wa duara letu ukaingia hadi kati ya shimo tulilochimba ukajenga sura ya mtu kwa kutumia vumbi la kimbunga ambalo ndilo liliingia nalo. Kitendo cha kuona umbile la mtu katika upepo huo tulijikuta tukitamani kukimbia ilikuwa inaogopesha sana sana lakini mganga alitusihi tusikimbie na tufanye kile atakachotuambia, mganga kwa kitendo cha upesi alimwaga ile damu ya mwezini ya mwanamke kulizunguka shimo hilo na ule upepp ukawa unajaribu kutoka ndani ya eneo lililozunguahiwa damu lakini ulishindwa kwani ulipokaribia mpaka wa ile damu ambayo ni ya Shemeji Salma ulirudi huku sauti isiyoeleweka kama ya popo aliyejeruhiwa ndiyo ikawa inasikika kutoka kwenye ule upepo. Mganga baada ya kuhakikisha ule upepo umeshindwa kuivuka ile damu ya Mwezini alituamrisha tuchome visu vyetu kwa pamoja katika sehemu ya kifua na ya mgongo ya umbo la mtu lililotengeneza na upepo huo kwa kutumia vumbi jingi lililosababishwa na huo upepo, wote kwa pamoja tulichoma visu vyetu kwemye huo upepo ambavyo vilitupa hisia ya kwamba tumetoboa kitu hadi makelele ya popo aliyejeruhiwa yakssikikakwa nguvu kwenye ule upepo kisha ukazama ndani ya shimo kwa mara moja.

Hapo ndipo mganga akambeba Jamadin aliyekuwa kafungwa kamba akiwa anafurukuta aweze kutoka lakini alishindwa kutokana na kamba ngumu alizokuwa amefungwa, alimuingiza ndani ya shimo hilo kisha akaliingiza lile jeneza tulilolileta ndani ya shimo pamoja na chupa. Alimlaza Jamadin juu ya jeneza kisha akatuamuru kila mmoja amchanje mara sita kwa kutumia kisu alichonacho mkononi, sote tulifanya ambapo Jamadin alitoa ukelele wa maumivu lakini hatukumjali hata kidogo mpaka tulipomaliza kumchanja ndipo tulipoanza kuona ajabu jingine lilitokea katika mwili wa Jamadin baada ya yeye kutanua mdomo apige kelele tulipomaliza kumchanja lakini kelele hazikutoka zaidi ya kutoka mwanga mweupe ulioingia ndani ya chupa. Mganga aliifunga ile chupa kwa kukaza sana kifuniko halafu akaiweka ile chupa pembeni, alipomtazama Jamadin nasi tulimtazama ndipo tukaona ajabu jingine lililopo kwemye mwili wake ambalo awali hatukuliona. Shingoni mwa Jamadin tuliona amevaa mkufu wenye vito vyenye kuvutia ambavyo hatujawahi kuviona duniani na mpaka hii leo havijawahi kuonekana sehemu yoyote. Mganga aliniamuru niuvue ule mkufu shingoni mwa Jamadin niuvae mimi nami nikafanya hivyohivyo ambapo nilishuhudia maajabu mengine ambayo sikuwahi kuyashuhudia kwani ule mkufu nilipouvaa haukuonekana kifuani mwangu, kitendo cha kuvaa mkufu tu wenzangu wote vifuani mwao kulitokea mwangaza wa kung'aa kisha ukafifia papo hapo tukabaki tukishangaa lakini mganga aliishia kutabasamu tu kisha akatueleza sasa tupo miongoni mwa watu matajiri duniani kutokana na nguvu ya mkufu huo hivyo tujipongeze kwa hilo. Kauli hiyo ulitufanya wote tufurahi sana kwani ndiyo ulikuwa mwisho wa kuteseka na kasumba iliyotukumba ghafla katika maisha yetu na sasa ni muda wa kufurahia maisha, baada ya hapo ule mwili wa Jamadin tuliuweka ndani ya lile jeneza jeusi na tuliliinfiza shimoni halafu zoezi la kufukia ndiyo lilifuata hadi likaisha. Mganga naye alifanya maajabu yake eneo lile likawa kama halijachimbwa awali wala halikuwa na muonekano wa eneo lililochimbuliwa, baada ya zoezi hilo ndipo tulirudi mjini haraka sana na tulienda hadi kwa minchi tukamuokota Ally kwanj tulijua ni eneo gani ametupwa.

Tulirudi naye nyumbani tukiwa hatuna Jamadin katika mikono yetu na hiyo ndiyo ilikuwa siku ya huzuni kwa Farida kwani alilia sana kutokana na hilo, kazi ya kumbembeleza ikawa kwetu sisi pamoja huku mioyoni mwetu tukitambua wazi tunafanya unafiki kwani tunatambua ni kila kitu. Siku iliyofuata wasamaria wema walileta mwili wa Jamadin uliokotwa Kisosora na walikuwa na asilimia mia kuwa yule ni Jamadin lakini hakuna aliyekuwa anatambua kuwa Jamadin tulishampoteza na tukamzika mpirani, mazishi ya mwili wa ulioletwa yalifanywa huku Farida akiwa na uchungu mwingi sana hadi nikawa namuonea huruma lakini ilishatokea. Baada ya muda taarifa hiyo ilishasahaulika kidogo ndipo siku moja tukiwa tushaanza kuingia katika mafanikio Ally kwa bahati mbaya alitusikia tukizungumza kuhusu hilo suala tulilolifanya tukiwa na Salma, siku hiyo Ally alitufokea sana lakini niliweza kumdhibiti baada ya ule mkufu kutokea kimaajabu kifuani mwangu kisha ukaachia mionzi yake iliyoenda kumuingia na kuanzia hapo akawa anatusikiliza sisi tu na si mwingine".

Simulizi ya Shafii iliishia ambapo ndiyo simulizi iliyokuwa imemvua nguo zote mbele ya kila mtu hapo ndani kwani ubaya waliouficha sasa uliluwa umeshagundulika, Bi Farida alimtazama Shafii kwa chuki za wazi baada ya kubaini upande wake wa pili wa maisha yake aliouficha kwa kipindi. Hakuna mwingine ambaye aliyekuwa ametarajia kama Shafii angeweza kufanya vile kwa mtoto asiye na hatia kama Jamadin, ilikuwa ni huzuni iliyojaa chuki za wazi baada ya kila mmoja kubaini uovu uliokuwa ukifanywa na Shafii kwa takribani miaka ishirini na sita iliyopita. Baada ya simulizi hiyo hata Mzee Mahmud aliyekuwa akiitambua simulizi hiyo alisikitika pia kila akimtazama Shafii kwani alijua alikuwa amefanya janga kubwa tofauti na yeye alivyokuwa anadhani, alibaki akimuangalia kwa sekunde kadhaa kisha akajikohoza ili kusafisha koo lake apate kuongea bila sauti yake kukwaruza.

"Shafii hivi unajua ni kitu ulichokifanya mpaka dhahama hii inawakumba wenzako na hadi sasa mliousuka mpango huo mmebaki wewe na Salma tu kwani mliyemkosea tayari ameshawapoteza Falzal, Hassan na Hamis. Kwanini lakini unafanya mashindano na kiumbe usiyemjua Shafii?" Mzee Mahmud alilalamika kisha akamtupia jicho Zalabain halsfu akamnyooshea kidole akasema, "umemuona huyu aliyeingia na Farida na Zayina? Ulijua utamuua siyo mlipouchimbia mwili wake hapa tulipokaa? Huyo ndiye Jamadin mwenyewe na hakufa kama mnavyofikiria, na ile chupa iliyofungiwa kitu kilichokuwa kinatoka mdomoni mwake ilifunguliwa na huu mwili mliofukia ukatolewa akarudi kama awali. Hivi we mtoto unamjua ni nani huyu uliyekuwa unamfanyia ubaya huo? Loh! Nakuonea huruma sana kwa ujinga wako ulioufanya mwanangu.... Jamani ngoja nimkaribishe mgeni mwingine ambaye sikuwaambia kama atakuwepo katika eneo hili aje awaeleze kuhusu asili ya Jamadin. Mzee Mubaraka karibu tafadhali" Mzee Mahmud alimlaumu sana Shafii kwa kitu alichokifanya na alitumia muda huo kumtambulisha Jamadin ambaye anajulikana alikufa mbele ya wote hapo ambapo wengine walishtuka sana walipolijua hilo, alitumia fursa hiyo kumkaribisha mgeni mwingine ambaye anajulikana hapo kama baba yake Faimu aliyekuwa lulu kwa warembo wa miaka mingi iliyopita ambao sasa hivi warembo hao walikuwa kina mama wanaoukimbilia uzee.

Ukaribisho wa Mzee Mahmud ulifafanya watu waangalie mlangoni ambapo walimuona mzee wa kiarabu mwenye ndevu nyingi aliyevalia kanzu safi ya rangi nyekundu na kofia akiingia ndani humo, alionekana ni mzee hasa lakini hapo alikuwa alitembea vizuri kama kijana wa kawaida tofauti na watu wengine waliomzoea. Mzee huyu hakuwa mwingine bali ni mzee Mubaraka ambaye baada tu ya kuingia alitoa salamu kwa wote na kupelekea kidevu chake kilichobeba ndevu nyrupe zilizosimama kama mwiba kicheze baada ya kinywa chake kufunguka. Salamu yake iliitikiwana watu wote na mzee huyu alienda moja kwa moja hadi kwa Zalabain akatoa salamu ya heshima kama wafanyavyo vijakazi wakifika kwa watukufu wa familia ya kifalme, salamu hiyo iliwashangaza sana watu wote kwani hawakuelewa kwanini mzee huyo alisalimia kwa salamu hiyo.

Iloonekana ni babu na mjukuu wake kwa jinsi walivyofanana lakini kusalimia kwa namna ile ndiyo kuliwapa swali jingine lisilo na libu katika vichwa vya watu wote waliopo eneo hilo, Mzee Mubaraka hakujali mishangao iliyowapata waliomo humo ndani yeye alienda kuketi jirani na mzee Mahmud.
"Naam mzee Mubaraka najua watambua suala lote uliloitiwa hapa sasa naomba ueleze asili yake jina lako na asili ya Faimu pamoja na Jamadin na vingine vyote" Mzee Mahmud aliongea huku akimtazama Mzee Mubaraka usoni ambaye alitikisa kichwa kuashiria amekubaliana naye.
Mzee Mubaraka alipopewa ruhusa hiyo aliwatazama wote waliopo humo ndani kisha akasema, "kwa jina naitwa Mubaraka bin Yaktwash ni jini niliyezaliwa katika himaya ya majini ya Majichungu". Alikatisha kidogo kusimulia kisha akawatazama waliopo mule ndani ambapo wengine walionesha kushtuka kusikia taarifa hiyo, hakuwajali mshtuko wao na aliendelea, "Nimezaliwa miaka elfu mbili iliyopita katika himaya hiyo na nilipoanza kuwa kijana nilianza kufanya kazi nikiwa kama mtumishi wa ndani ya kasri la mfalme Zulain, nikiwa nina miaka mia tano tangu nizaliwe katika alizaliwa mtoto wa pekee wa mfalme wetu mtukufu aliyeitwa Zaif. Mtoto huyo nilikabidhiwa kuwa msaidizi wake hadi anakua mkubwa na alikuwa ni mtoto mwenye kupendwa sana na wanamajini wote wa himaya hiyo kwani alionekana aliwa mwerevu tangu yupo mdogo, Nilikuwa mlezi na msaidizi wake kwa muda wa miaka mingi sana hadi alipotimiza miaka elfu na mia tano mimi nikiwa nina miaka elfu mbili. Zaif kwa kipindi hicho alimuaga baba yake anakuja kufanya matembezi duniani na kukaa kwa muda kidogo ili aweze kuyaona maisha ya wanadamu yalivyo, alikubaliwa na baba yake kwa mikono miwili na akapewa angalizo la kuwa makini na wanadamu kwani siyo viumbe wazuri. Alikabidhiwa watumishi wawili na mmojawapo akiwa ni mimi na mwingine ni jini wa kike mwenye taaluma ya upishi katika kasri la mfalme, wote kwa pamoja tuliingia duniani kama wasafiri na tulifikia kijiji cha Bwagamacho ambapo nilijitambulisha kama Mubaraka na yule jini wa kike nilimtambulisha kama mke wangu na mtoto wa mfalme wetu mtakatifu nilimtambulisha kwa jina la Faimu nikimtaja ni mtoto wangu wa kumzaa.

Tuliyaanza maisha yetu ya happ kijijini karibu kila mwanakijiji akidhani sisi ni wanadamu tena wa familia moja kasoro Mzee Mahmud hapa ndiye aliyeweza kubaini sisi ni majini ila hakuwa na neno na sisi baada ya kutubaini hatukuja kwa nia mbaya eneo hilo, maisha yetu yaliendele kwa amani hapo kijijini ambapo Faimu akiwa nje ya nyumba alikuwa akitupa heshima kama wazazi wake ila tulipokuwa ndani mbali na upeo wa mwanadamu yeyote tulikuwa tulimpa heshima kama mwana wa mfalme wetu mtukufu. Hadi Faimu anaanza kupendwa na wasichana hapo kijijini tayari tulikuwa tumeshabaini hilo suala na walipokuja kujitolea kufanya kazi tulikuwa tukiwacheka sana wanadamu kwa jinsi walivyo na papara ya kupenda tu, kwa Faimu ilikuwa ni burudani tu kwani alikuwa anajifunza mengi jinsi binadamu alivyo ambavyo yeye alikuwa hawajui zaidi ya kuwasikia. Aliishi maisha ya kibinadamu tu na alikuwa akiona fahari sana kubadilishana mawazo na wanadamu ingawa wa rika lake wengi walikuwa wanamchukia, hata alipokuwa na urafiki wa pamoja kati yake na wanawadamu ambao ni Shafii na Hamis alikuwa akifurahi sana hata siri walizokuwa wakizificha aliluwa akizijua sana. Kipindi hicho alishajua uwepo wa Farida kwa kutumia nguvu zake za kijini na alimpenda sana ingawa alitaka ajithibitishie kama anapendwa na hakuwa tayari kutumia uwezo wake kumuingilia na kumshawishi, alikuwa akitusimulia sisi watumishi wake ambao alitufanya kama washauri wake wakuu.

Nasi tulimshauri asitumie nguvu bali ahakikishe anapendwa naye na kama hapendwi aache, ushauri huo alioufuata na akasubiria ziku ya kuonanana na Farida hadi ilipowadia. Hakumlazimisha Farida kuwa na mapenzi bali alikubali kwa hiyari na uhusiano ukaanza, huku huyu Ally akiwa mtu wa kwanza kubaini kwani ndiye aliyekuwa akipendwa hasa na Faimu kati ya wanadamu wote hapo kijijini. Uhusiano wake ulipovurugwa alionekana ni jinsi gani ameuzwa lakini hakutaka kutumia nguvu zake kabisa na aliishia kumuomba penzi Farida kisimani akaambiwa anataka kubaka akapigwa sana akionekana hafai mwishowe akaondoka hapo kijijini baada ya kufukuzwa na hakuwa tayari kutumia nguvu zake na hata mtukufu mfalme aliposikia alitaka kuwaangamiza wanadamu hao lakini kwa huruma ya mwanae akawaacha. Jambo ambalo wanadamu hawa hawakulitambua ni kwamba dawa waliyompa Farida kila siku usiku ilikuwa inapunguzwa na Faimu na hapo Farida hurudi katika akili na hukutana kimwili na Faimu kwa kipindi hicho chote huwa alikuwa anamjia kwa njia ya ndoto, hadi huyu bwana hapa anamposa Farida baada ya kumuweka chini yake kwa kutumia nguvu za kichawi tayari huo mchezo Faimu alikuwa anaendelea na ndiyo katika kipindi hicho akawa anamuona anaweweseka na hata alipokuja kuacha tayari Farida alikuwa ana ujauzito wa Faimu huyu bwana akidhani ni wake.

Jamadin alipozaliwa Faimu alikuwa yupo makini sana katika kumlinda mwanae kuliko kitu kingine chochote pia alimpatia mkufu wenye kidani kinachoitwa Dainun ili umlinde na hadi hawa mabwana wanataka kumtoa kafara Jamadin kipindi hicho akiwa na miaka mitano hapa duniani na mmoja kwamujibu wa mila za kijini ambazo miaka mitano ya kwanza ya mtoto huhesabiwa ni mwaka mmoja . Faimu alishajua hilo na alifika eneo hili akiwa na jazba sana. Alifanya hila ya kutengeneza upepo nje ili aharibu kazi yao kisha aliingia ndani akiwa yupo kama kimbunga ndipo alipojikuta amenasa kwa kuzungushiwa damu ya hedhi ya mwanamke akawa hawezi kutoka kwani ina madhara sana kwake kama akiisogelea, hapo ndipo mabwana hawa wakamchoma kwa pamoja visu vilivyochovya kwenye damu ya hedhi katika mwili wake na kumfanya apate jeraha kubwa. Faimu aliishiwa nguvu na alizama chini ya ardhi mimi nikaja kumtoa nikampeleka kwa mtukufu mfalme ili apatiwe matibabu kwa jereha hilo, kuanzia siku hiyo Faimu alikuwa mtu wa kukaa kitandani kwani mkufu wenye Dainun ambao ni mali yake ndiyo ungeweza kumponya tu. Baada ya mwaka mmoja Faimu alifariki akitoa tamko mwanae ndiye aje kukaimu nafasi yake ya ufalme atapofariki baba yake, agizo jingine alilotoa ni kisasi chote kilipwe na mwanae tu. Kiongozi Zalabain au Faimu alipokuja kupatikana taji lilimkataa mpaka upatikane huu mkufu na kisasi kulipwe kwani hawa ndugu ndiyo chanzo kuzaliwa watoto waliodumaa katika himaya yetu kutokana na kutoonekana kwa usiku kwa muda mrefu".

Mzee Mubarak alimaliza simulizi yake iliyomliza sana Bi Farida baada ya kusikia kuwa Faimu kwa muda huo ni marehemu, mzee Buruhan aliposikia hiyo habari hasira zilimzidi maradufu na akasimama wima huku akihema kwa nguvu.
"Mzee mwenzangu tulia basi walsu kidogo tumalizie" Mzee Mahmud alimsihi rafiki yake.
"Sihitaji hata kuendelea kumuangalia huyu mwanaharamu na sina mtoto kama yeye ngoja niondoke nje mkimaliza mtanikuta" Mzee Buruhan alisema kwa jazna kisha akaanza kutembea kuelekea nje.

"Baba usifanye hivyo" Shafii alilalamika kumsihi baba yake.
"kelele wee! Shaytwani mkubwa usiniite baba yako na sina mtoto kama wewe mtoto wangu ni Ally tu" Mzee Buruhan aliongea kwa ukali kisha akatoka nje akamuacha Shafii akilia kwa uchungu, muda huo huo Ally naye akainuka akamtazama Shafii kisha akamtazama na Salma halafu akamtazama Hamida kwa huruma sana.

"Salma naomba unipatie mwanangu niondoke naye" Ally aliongwa kwa ustarabu halafu akamuangalia Mzee Mahmud akamuambia, "Baba huyu mwanamke ni zaidi ya shetani yaani kanitumikisha kama mtumwa wa ngono kwa miaka mingi baada ya ule mkufu kunifanya niwapende na ushenzi wao, sijaoa wala kuwa na mke na umri huu matokeo yake napata mtoto kupitia huyu malaya tena mke wa mtu. Hebu muulizeni Hamida ni mtoto wa nani".
Ally alipoongea maneno hayo hadi Shafii aliweka mkono kinywani kwa ujinga alioufanya Salma ambaye aliishia kuona aibu tu, aliinamisha kichwa chini kutokana na fedheha iliyomkuta hadi wanae wakawa wanamuona ni binadamu wa ajabu.
"Salma huyo Hamida ni mtoto wa nani?" Mzee Mahmud aliuliza taratibu huku akimuangalia Salma kwa Macho ya ukali sana, Salma alishindwa kujibu na akakaa kimya akiwa ameinamisha macho chini hadi alipokaripiwa.

"wa A....A..Ally" Salma alijibu huku akitazama chini kwa aibu na kupelekea mwanae mkubwa Jamal asimame akawa anaenda alipo Ally ambapo ni jirani na mlango wa kutoka mje ili aondoke, Salma alimshikilia miguu mwanae lakini alijikuta akisukumwa kwa nguvu.
"Bora ningezaliwa na shetani kuliko wewe" Jamal aliongea kwa hasira halafu akatoka nje huku akilia kwa uchungu, Hamida naye alinyanyuka kisha akaanza kumtazama mama yake huku machozi yakimtoka kwa uchungu. Salma alipotaka kumkumbatia miguuni alimsukuma kwa nguvu halafu akaenda halipo Ally akawa anamtazama huku machozi yakimtoka, Hamida alimkumbatia baba yake kwa mara ya kwanza huku akilia na Ally naye alimpokea mwanae huku machozi yakimtoka kwa alichofanyiwa.

"Baba samahani naondoka humu nikiwa nina mwanangu, sina kaka humo" Ally alizungumza kwa hasira halafu akatoka nje akiwa na Hamida, Salma alipotaka kuwafuata alijikuta hawezi kuinuka kabisa.
"Shafii nadhani unakumbuka jana jioni nilikuambia leo ndiyo utapata nafuu ya tatizo lako, sasa basi napenda utambue kuwa sikumaanisha litatuliwa basi nafuu yenyewe ndiyo hii ya kuwaona Bi Farida na Zayina ila si kukusaidia zaidi kutokana na udhalimu mlioufanya. Niliwaonya msifanye hivyo tangu mnaenda kumuwekea dawa Farida lakini hukusikia kwa ubishi wako, sasa mwanangu donda la kujitakia halihitaji pole uguza bila msaada wala pole. Nadhani Zalabain Jamadin ana mengi ya kuongea na wewe mkiwa wewe na Salma sasa mtazungumza naye wawili, mimi sisaidii madhalimu kama nyinyi" Mzee Mahmud naye aliongea kisha akanyuka akasema, "lengo langu ilikuwa kumnasua Ally maana naye angekumbwa na balaa lisilomuhusu na nimefanikiwa sasa nawatakia mazungumzo mema na Zalabain".

Mzee Mahmud alitoka nje akazidisha machungu sana kwa Shafii ambaye alilia sana pia Salma naye alijuta kwa yote aliyokuwa akiyafanya kwani hakuwa na muda wa kurekebisha tayati alishachelewa kabisa.
Mzee Mubaraka, Bi Farida pamoja na Zayina nao walinyanyuka wakabakisha watu watatu tu waliobaki humo ndani na walianza kutembea kwataratibu kuufuata mlango ulipo.

"Mke wangu, mwanangu" Shafii aliita huku akinyoosha akiwa anazidi kulia sana kwani hakuwa anaweza hata kunyanyuka, maneno yake yalimfanya Bi Farida asimame kisha akamsonya kwa nguvu halafu akasema, "mkeo nani kwa ndoa ipi? Sina mume kama wewe".
Bi Farida alipimaliza kuongea hayo maneno alitoka nje kwa hasira akiwa amemshikilia Zayina aliyekuwa analia tu kutokana na kilio cha baba yake lakini alimuacha apate adhabu kwa uovu wake
Zalabain alipohakikisha mtumishi wake,mama na dada yake wametoka nje alimama wima akiwa na macho yaliyojaa ghadhabu sana akawasogelea Shafii na Salma, alimuangalia Salma kwa macho makali halafu akamsogelea karibu zaidi na kusababisha Salma atokwe na haja ndogo papo hapo.

"Wakati unatoa damu yako ya hedhi iliyosababisha baba yangu afe mbona hukujikojolea, ulijua na mimi itaniua wakati mnanichanja na visu vyenu nilikuwa nina Dainun shingoni mwangu. Sasa leo zamu yako" Zalabain aliongea kisha akaushika shingo ya Salma akaiminya kwa nguvu hadi mishipa ikapasuka damu zikaanza kuvuja, alishika na kichwa akakivuta akakichomoa kabisa halafu akamgeukia Shafii akamwambia "nipe".
Shafii kwa uoga aliokuwa nao aliposhuhudia Salma alivyouawa aliweka mkono kifuani mwanga ukatokea na hapo mkufu ukaonekana ukiwaka halafu ukazimika ghafla, kuzimika kwa mkufu kulimfanya Shafii ashangae sana akabaki akimuangalia Zalabain huku akitetemeka.

"He! Ulijua hiyo Dainun itatoa mwanga uniue nayo, kwa taarifa yako nguvu kubwa ya Mzee Mahmud inaizuia hiyo isifanye kazi. Nipe!" Zalabain aliongea huku akimsogelea Shafii akiwa na jazba, Shafii hakuwa na ujanja aliivua Dainun akampatia Zalabain huku akitetemeka.
Zalabain aliichukua Dainun akaivaa shingoni mwake na kusababisha Dainun ipige mwanga mkali ulioenda juu kisha ikaanza kung'aa, alitoa tabasamu kisha akanyooshea Shafii kidole akamuambia, "umenipatia kimoja bado kingine tumalizane kabisa".

"Kipi?" Shafii aliuliza huku akitetemeka
"roho yako" Zalabain alijibu na macho yake yakaanza kutoa machozi ya damu tabasamu likawa limefutika usoni
"hapana" Shafii alisema huku aliweka mikono ishara ya kuomba msamaha lakini haikusaidia kitu kwani Zalabain alijigeuza kimbunga kikali kikamvaa Shafii kikawa kinamzungusha na kupelekea Shafii atoe mayowe ya maumivu yaliyosikika hadi nje, taswira mbaya ya kuruka kwa damu pembeni wakati akizungushwa ndiyo ilionekana na kisha vipande vya mifupa vvikaruka pembeni vikiwa na damu tupu. Muda huo tayari Shafii alikuwa ameaga dunia kutokana kupata mshahara kwa kile alichokifanya miaka mingi iliyopita.

****

Watu wote waliokuwa nje walisikia kelele za Shafii lakini hakuna hata oja aliyethubutu kumsaidia na makelele yalipotulia haukupita muda mrefu nyumba yote ikaanza kuporomoka yote kisha ardhi yake ikafunguka kifusi chote kikazama na huo ndiyo ukawa mwisho wa Shafii, watu waliona kitendo hicho walisikitika sana wengine walitokwa na machozi kwani ingawa kafanya mabaya bado alikuwa na nafasi kwa baba yake na mtoto wake.
Kulipotulia kabisa Zalabain alitokea akiwa ana Dainun shingoni mwake akamchukua mama yake na dada yake pamoja na mtumishi wake wakaondoka, waliobaki walitafita nyumba za kulala hapo Mpirani usiku huo baada ya kushuhudia mwisho wa dhahama ya kujitakia


****

Miale ya Dainun iliyopiga angani ilisababisha mwangaza wa kawaida kurejea katika himaya ya Majichungu, ndelemo na vifijo kutoka kwa majini wa aina mbalimbali ndiyo zilisikika na siku iliyofuata sherehe ilifanywa katika viwanja vya kasri la kifalme. Zalabain alivikwa rasmi taji la ufalme ambalo halikumkataa lilikaa kwenye kichwa chake vizuri kabisa, sherehe kubwa ilifanywa ilishuhudiwa na dada yake pamoja na mama yake wakiwa na furaha kama alivyokuwa yeye ana furaha.

MWISHO!!


MTUNZI: HASSAN O MAMBOSASA

SIMU:+255713776843
+255762219759

WHATSAPP:+255713776843


SHUKRANI ZOTE ANASTAHIKI MWENYEZIMUNGU
MUUMBA WA DUNIA NA VILIVYOMO KWA KUNIPATIA
AFYA NJEMA ILIYONIWEZESHA KUANDIKA RIWAYA
HII KWA MARA NYINGINE
 
Duh! Hii simulizi noma sana. Hongera kwa mtunzi na asante sana kwa kutuletea burudani nyingine.
 
Wapuuzi hawa jf ungewaletea nunu nusu kama punje za kuku..ili wakuthamini na kukuandama kutwa kucha kumalizia hii riwaya.......
Hapo ungekuwa JF Celebrity..................
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom