Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,672
- 40,549
Na. M. M. Mwanakijiji
John Maduhu alimshika mkono mchumba wake Alice Rutashobya (alijulikana zaidi kwa jina la Koku) wakitoka nje ya ofisi za Paroko wa kanisa la Mt. Francis Ksaveri la Nyakahoja kuelekea walikoegesha gari lao pembezoni mwa kanisa hilo. Kanisa la Nyakahoja ni moja ya parokia maarufu zaidi mkoani Mwanza na ilijulikana kama parokia ya watu mashuhuri. Mtaani wengine waliita parokia ya mabishoo. Ukienda Nyakahoja siku ya Jumapili usishangae ukipigana vikumbo na Mkuu wa Mkoa, Majaji, Makamanda wa Polisi n.k kwani wakatoliki wengi mashuhuri walikuwa wanasali kanisani hapo. Zaidi ya yote ni parokia pekee iliyokuwa na misa ya kiingereza, na kihindi. Jinsi ilivyo Parokia ya Mt. Petro ya Oysterbay kwa watu wa Dar, ndivyo ilivyo Parokia ya Mt. Francis kwa watu wa Mwanza.
Kanisa hilo lipo pembezoni mwa ziwa Victoria limezungukwa na ukuta uliolitenganisha na ziwa hilo kati yake na ziwa kukiwa na barabara ya kwenda Airport. Upande wa pili wa barabara hiyo kulikuwa kumetanda vibanda kadhaa vya wauza mbao na kwa mbali uliweza kuona eneo la Mwaloni ambako wavuvi na mitumbwi yao walikuwa wakibahatisha bahati zao kwenye hilo ziwa la maji baridi.
Jioni hiyo upepo ulipunga taratibu huku sauti za milio ya gari zikisikika lakini kutokana na ule ukuta basi makali ya sauti hayakuwa makubwa kufika kanisani. Kwenye moja ya vibanda vya kupumzikia vilivyoko nje ya kanisa hilo kulikuwepo na kwaya ya vijana wakifanya mazoezi, huku vijana wengine wakicheza mpira wa nyavu kwenye uwanja ulio upande wa kushoto wa Kanisa hilo.
John na Alice walikuwa ni miongoni mwa wachumba kadhaa waliokuwepo hapo Nyakahoja kwa mafundisho ya ndoa siku hiyo ya Jumamosi. Walitarajia kufunga ndoa mwezi wa nane kwenye Kanisa hilo Katoliki la Kiroma. Kama kawaida baada ya mafundisho wapenzi hao wawili walipata muda wa kukaa na kuzungumza mawili matatu kuhusu maandalizi ya harusi kabla ya kwenda kwenye hoteli ya Victoria katikati ya Jiji kupata chakula cha jioni.
"Baba anataka kuzungumza na wewe" Alice alisema huku akimminya mkono John kwa mapenzi.
Hisia kubwa ya mapenzi ilimuingia John, na dakika ile alijua kuwa uamuzi wa kumuoa Alice ulikuwa ni sahihi na alikuwa tayari kuahidi mbele ya Mungu na wanadamu kufanya lolote kumpa maisha mazuri binti huyo wa watu.
"Kuna tatizo gani?" John aliuliza huku akisimama kwa sekunde chache kumuangalia Koku. Pole pole na kwa mwendo wa kusuasua waliendelea kuelekea walikoegesha gari kwenye ukingo wa ukuta wa barabara, chini ya mti mkubwa. Kulikuwa na magari mengine matatu yameegeshwa eneo hilo. John alikuwa ameshika ufunguo wa gari kwa mkono mwingine huku akiurusha rusha hewani. Ilikuwa ni ajabu kwa Mzee Patrick kutoa mwito wa kumuona John, kwani wakati wowote ule John alikuwa anakaribishwa nyumbani kwa mzee huyo maeneo ya Igoma nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenye barabara ya kwenda Musoma bila kuhitaji mwaliko.
Mzee Patrick Rutashobya, alikuwa ni mkimya na asiyependa sana kufuatilia mambo ya vijana wake na katika uzee wake amejikuta anapenda zaidi kukaa nyumbani na kuangalia wajukuu zake. Katika miaka ya utumishi wake aliwahi kuitumikia Tanzania kama balozi katika nchi kadhaa zikiwemo Zimbabwe, Ufaransa, Ubelgiji na Ujerumani. Mwaka 1997 mke wake aliyedumu naye kwa miaka 32 alifariki dunia kitu kilichomfanya mzee Rutashobya kuamua kustaafu toka katika ajira ya serikali. Hata hivyo, mzee huyo hakujifunga na huzuni au kukubali kugubikwa na majonzi bali aliendelea na shughuli zake binafsi ikiwemo kufungua hoteli mpya na ya kisasa iliyoko pembezoni mwa uwanja wa CCM Kirumba, iliyojulikana kwa jina la Paradiso.
"Hakuna tatizo lolote" Alice alimjibu na kumwambia kuwa wakitoka Kanisani kesho basi aende kumuona mzee nyumbani huko Igoma. Walikubaliana kwa hilo na John alimfungulia Alice mlango na akaingia garini huku sketi yake fupi ya kijivu iliyombana mapajani ikijikunja na kuonyesha mapaja yake yaliyopendeza na kunona. John aliangalia kwa sekunde chache na kuombea ile siku ifike ile ale vya "kwake" pasipo kuiba. John alizunguka mbele ya gari na kuingia upande wa dereva. Harufu ya manukato mazuri ya Paradise ya Chanel aliyekuwa amejipulizia Koku ilijaza gari hilo. John alijihisi yuko karibu na pepo.
"Alice, nakupenda sana" John alisema kabla hajawasha gari huku akimwangalia Alice aliyekuwa akijiweka vizuri kwenye kiti na kujifunga mkanda wa usalama. Koku alichukua mkoba wake na kutafuta rangi yake ya mdomoni. Alice alimgeukia John na kumvuta karibu, alimwangalia machoni na kumuambia kuwa na yeye anampenda zaidi. Wakiwa bado wamekaa ndani ya gari hilo aina ya Toyota Sequoia la rangi nyeusi iliyokuwa na vioo vya giza John alimmwagia busu zito tena la nguvu. Alice naye alirudisha busu hilo na kwa dakika chache walipeana denda huku wakiguna guna. Waliachiana na kuamua kutoka hapo kabla Padre Massawe hajawazukia.
John alirudisha gari nyuma hadi alipopata nafasi ya kuweza kuligeuza kuelekea getini na nje ya eneo la kanisa hilo. Mawazoni alikuwa anamfikiria Alice, mapenzi yake kwake na zaidi ya yote jinsi uhusiano wao ulivyokuwa. Alimshukuru Mungu kuwa amempa mwenzi ambaye atakuwa ni mke mwema na mama wa watoto wake. Kati ya wanawake wote aliowahi kuwa na urafiki nao John hakuwahi kuwa karibu na yeyote kama alivyo kwa Koku. Akiwa na Koku alijihisi yuko huru kusema chochote, na hakuficha hisia zake. Koku alikuwa ni binti anayejua kusikiliza, na ni mcheshi. Wakati mwingie kile kicheko chake tu kilimtuliza John na kumuhakikishia kuwa mambo yatakuwa poa. Alipofika getini akiwa katika dimbwi la mawazo John aliangalia kulia na tena kushoto na kumtazama Koku aliyekuwa anang'aa utadhania malkia. John alisubiri viexpress na magari kadhaa yapite ili apate nafasi ya kuingia barabarani.
"Unakumbuka tulipofanya mapenzi mara ya kwanza" John alimuuliza, huku akiangua kicheko cha kinafiki.
"Nisahau nichekwe!" Alice alijibu. John alijisemea moyoni, "kweli asahau achekwe". Wakiwa bado hapo, akili ya John na mawazo yake yakazima kuikumbuka siku ile waliyokutana kimwili kwa mara ya kwanza. Bila ya shaka Alice naye alikuwa amepotelea kwenye mawazo hayo hayo. Walishikana mikono huku wakisubiri zamu yao kwani magari yalikuwa yakienda kwa kasi kutoka Uwanja wa CCM Kirumba ambako timu ya Simba ilikuwa imecheza na timu ya SC Villa ya Uganda.
* * *
Ilikuwa siku ya Jumapili jioni John na Alice walielekea eneo la Nyegezi nje kidogo ya Jiji la Mwanza kwenda kuangalia kiwanja ambacho mzee Rutashobya amewanunulia ili wajenge nyumba yao. Barabara ya nyegezi ilikuwa ni ya vumbi kubwa na licha ya mvua iliyonyesha jana yake, ardhi ilikuwa kavu utadhani haijawahi kulowa. John alikata kona kwenye makutano ya barabara ya Shinyanga na ile ya kuelekea kwenye Chuo cha Jamii cha Nyegezi na baada ya mwendo kidogo alikata kona kulia tena kueleke kiliko chuo cha Uvuvi Nyegezi. Eneo hilo zaidi lilikuwa na viunga vya mpunga, na upande wa kulia kulikuwa na viwanja ambavyo vingine vilishaanzwa kujengwa. Kiwanja chao kilikuwa kwenye kona ya vilima viwili vya mawe. Waliegesha gari lao kwenye kibanda cha mafundi, na baada ya dakika chache za kuangalia angalia hapo na kumsalimia mlinzi, waliamua kwenda juu ya vilima vile vya mawe kuangalia jua linavyozama.
Walifika kileleni na waliweza kuona vizuri mandhari ya ziwa Victoria likiangazwa kwa mionzi ya dhahabu ya jua linaloanza kuzama. Mawe makubwa yaliyojipanga utadhani matofali yaliwazunguka wapenzi hao wawili na kuwaficha na mtu yeyote yule huku yakiwapa kivuli kizuri na upepo mwanana wenye harufu ya Sangara toka ziwani ukiwapepea. Ndege aina ya mbayuwayu walikuwa wakiruka huku na kule huku kundi la nyangenyange likipepea angani kama herufi ya v. John alikuwa ameketi chini huku miguu yake ikining'inia kwenye jiwe, Alice aliamua kulala chali huku akiwa amekunja miguu yake, kichwa chake akiwa amekiagamia kwenye mapaja ya John.
"Hivi unafikiri watamaliza kujenga kabla ya harusi?" Alice alimuuliza John huku akimuangalia kwa macho yake yenye upole wa njiwa lakini yenye kuashiria ujanja wa sungura.
"Natumaini hivyo, sitaki kuendelea kupanga tukishafunga ndoa" John alijibu. John aliacha kuzichezea nywele za Alice na kuanza kufungua vifungo vya blauzi yake. Kifua cha Alice kilikuwa kimetuna siyo tu kwa kujaliwa maziwa yapendezayo, bali hata sidiria aliyovaa ni ile inayonyanyua matiti na hivyo kuyafanya yaonekane kama maembe dodo yanayoning'inia mtini. Alice alijinyanyua na kuiteremsha sidiria yake hadi tumboni bila kuifungua. Alirudi na kuendelea kuegama kwenye mapaja ya mpenzi wake. John, huku mkono wake wa kushoto ukiwa unampa egemezo kwenye mwamba, mkono wake wa kulia ulinza kuyachezea matiti ya Alice, na kwa upole kama anayegusa almasi alizichezea chuchu za binti huyo wa Kihaya. Alice hakusema kitu bali alifumba macho na kufurahia mikono migumu ya mpenzi wake iliyompa raha isiyo kifani.
Jua lilikaribia kuzama kabisa na rangi ya mionzi yake ilibadilika toka ile ya dhahabu na kuwa nyekundu ya damu. Ndege walianza kutoweka angani na kurudi kwenye viota vyao. Alice alijigeuza na kulalia tumbo, aliifungua zipu ya suruali ya John na kwa taratibu alianza kumwinua mzee aliyekuwa tayari amekuwa mgumu hisia aliyoisikia wakati ameweka kichwa chake mapajani. Bila kufanya ajizi wala kuomba ruhusa alianza kumfyonza kwa taratibu huku akimwangalia yule "mzee" na kumpa sifa John kwa jinsi alivyojaliwa. John nusura apige kelele! Alipohisi kuwa John yuko taabani alimuacha na kumwashiria john ajivute chini kidogo ya jiwe hilo na kulala chali. Alice aliteremsha chupi yake huku akiwa bado amevalia sketi yake, na kumchuchumalia pole pole huku akiushikilia uume wa John na kuongoza kwenye hazina ya maji ya utulivu. Alikuwa amelowa kichizi na michirizi ya majimaji ya uke wake yalimchuruzikia John na kung'arisha ala yake!
Alice alikuwa fundi wa mapenzi. Hakumbakishia wala kumpa kwa kibaba alimpa yote huku John na yeye akijibu mapigo kiufundi. Walikuwa wamelowa jasho walipofika kilele kwenye miamba ya jiji la Mwanza. Kwa karibu dakika chache waliendelea kukumbatiana huku wakitaki muda usiende au kesho isije. Walipomaliza kiza kilikuwa kimeshaingia. Bila ya haraka wakavaa nguo zao, baada ya kujipangusa, na kuanza kuteremka kuelekea walikopaki gari lao. Mlinzi alisema alianza kuingiwa na wasiwasi lakini John alimhakikishia kuwa walitaka tu kuona jua "linavyozama" kando ya "ziwa Victoria". Mzee wa Kimakonde hakujua walimaanisha nini. Waliondoka na kurudi nyumbani.
* * *
"John, angalia gari hilo!" Alice alipiga kelele kumzindua John aliyekuwa bado amezama kwenye dimbwi la kumbukumbu ya tendo la mapenzi siku kule Nyegezi. John alishtuka na kuzinduka. Alikuwa ameishaanza kuingia barabarani na hakupata nafasi ya kuliona lori la Scania lilikokuwa linakuja kwa kazi likitokea Pasiansi. Licha ya jitihada zake za kukata kona na kuongeza kasi kuokoa maisha yake na ya mpenzi wake hakuweza kulizidi mwendo lori hilo.
Sauti ya breki zilisikika huku matairi ya gari yakisugua barabara hiyo ya lami. Wapenzi hao hawakuwa na nafasi! Kwani lori la Scani hilo lililokuwa limesheheni magunia ya dagaa liliwaparamia kwa nguvu zote na kusababisha mlio mkubwa wa mgongano uliosika hadi maeneo ya Hospitali ya Sekou Toure. Lori hilo liliwaburuza kwa karibu mita 100 hadi kwenye lango la shule ya Nyakahoja huku gari lao la Toyota likiwa limekunjwa kunjwa kama karatasi! Magari hayo mawili yalipoweza kusimama, matokeo yalikuwa ni dhahiri. Miili ya wapenzi hao ilikuwa imepondwa pondwa huku baadhi ya viuongo vyao vikiwa vimetupwa kando ya barabara na damu ikiwa imesambaa ndani ya gari lao. Ndoto ya maisha yao baada ya ndoa ilifutiliwa mbali kama jani linavyopeperushwa na upepo. Kwa dakika na muda wa karibu miaka miwili tangu wakutane, wapenzi hao wawili wakawa wameiunganishwa milele kwa damu. Watu walioshuhudia ajali hiyo, na waliokuwepo pale kanisani walisema kuwa angalau John na Alice waliweza kupeana busu kabla ya kifo.