Riwaya: Barua Kutoka Jela

RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA


SEHEMU YA KUMI NA TATU

Inspekta Jamila alitaka kujua kuhusu yule jambazi aliyepinduka na gari baada ya yeye kupiga mipira yote miwili ya nyuma ya gari ile kwa risasi na kupelekea kupinduka kwa gari ile.
"Yule nae alifariki saa mbili baadae tangu alipofikishwa hapa. Yule alikuwa na tatizo la kukosa hewa kwani mbavu zake sita zilivunjika, tatu kila upande na hata kama angepona asingefanya kazi yoyote yule!"
Hiyo ilikuwa ni ripoti ya Daktari aliekuwa akiwahudumia wagonjwa wale toka walipofikishwa Hospitalini pale jana yake.
Inspekta Jamila alipelekwa hadi katika chumba cha kuhifadhia maiti pale Muhimbili na kuonyeshwa maiti zile, na akawatambua na akawapiga picha katika nyuso zao!
Kiasi Roho ya Inspekta Jamila iliingia simanzi kidogo alipoiona ile maiti ya yule jamaa aliemwambia "UHAI WAKO NIMEUSHIKA UPO MKONONI MWANGU"
Inspekta Jamila alitoka katika wodi ya Kibasila na kuelekea Moi, ofisini kwa Dokta Masawe, alisubiri sana, sasa akiwa yupo katika benchi walilokalia wagonjwa waliokuwa wanasubiri huduma ya Dokta Masawe, lakini hadi inatimu saa nne kulikuwa hakuna dalili za Dokta Masawe bali daktari mwingine aliingia kwa dharula na kuwahudumia wagonjwa!
Inspekta Jamila akakata shauri kuwa, kwa kuwa waliahidiana wakutane pale Amana Ilala, basi akaandae mtego wake. Alitoka nakuiendea gari yake akiwa yupo katika mawazo tele na mwendo wa haraka mara, simu yake ya mkononi ilikuwa inaita. Ilikuwa ni namba iliyopigwa katika mfumo wa Private namba!
Inspekta Jamila akasita pale alipo, kisha kabla hajapokea simu ile aligeuka na kuangalia sehemu yote ile ili kuangalia kama kuna mtu yoyote anaepiga simu, akaona patupu!
Akaendelea kuifata gari yake huku simu ile ikiendelea kuita, akafungua mlango wa gari na kuingia ndani!
Na ile simu ikakatika wala na yeye asihangaike tena na simu ile,kwani alikumbuka yeye alivyomcheza shere Dokta Masawe, akachelea na yeye asije fanywa hivyo!
Inspekta Jamila alikuwa akiendesha gari yake kuelekea ofisini kwake walipokubaliana na Afande Kubuta wakutane ili ikiwezekana leo wafunge kazi, kwa kuwakamata wahalifu wale wanaotoa roho za watu kwa sababu ya mali ambayo hawakuitolea hata jasho katika kuichuma. Kwani mwenye mali masikini ya mungu huangaika kwa miaka na miaka, kisha hawa madhalimu wanakuja kuchukua kwa siku moja, lakini pia wanakutoa na roho yako au wakuache majeruhi! Udhalimu wa hali ya juu kabisa huu.
Inspekta Jamila aliendesha gari yake akitokea Muhimbili, akaingia Mtaa wa Malik, alipofika Makutano ya Malik na Umoja wa Mataifa, aliacha barabara ya Mtaa wa Malik na kupinda kushoto kuchukua barabara ya Umoja wa Mataifa. Asubuhi ile kulikuwa na foleni kidogo hivyo alitembea na gari taratibu kiasi, hadi akafika Makutano ya Barabara ya Ally Hassan Mwinyi na Umoja wa Mataifa, akakata kulia kushika njia ya Ally Hassan Mwinyi akaendesha gari yake kwa kasi kidogo kwa kuwa askari aliyesimama pale kwenye taa za Makutano ya barabara inayokwenda AGA KHAN HOSPITAL na ALLY KHAN ROAD, alikuwa anazivuta sana, gari zinazotoka daraja la Salender katika barabara ile ya Ally Hassani Mwinyi.
Katika makutano ya barabara ya Ohio na Ally Hassan Mwinyi , alichepuka kushoto kuelekea Mtaa wa Ohio na kabla hajafika Jengo la PPF akakata kulia kuingia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, akapitiliza hadi nyuma katika ofisi za mbao ambapo ndipo ofisi yake ilipo, akaiegesha gari yake katika maegesho, na kushuka kuelekea ofisini kwake ambapo baada ya kuingia tu alimkuta Afande Kubuta ameshajaa tele kama pishi ya mchele akimsubiri!
Baada ya salaam za utii za itifaki walikaa kujadili namna ya kuendelea na upelelezi kutoka pale walipofikia.
Afande Kubuta alitoa taarifa kwa kirefu namna walivyokwenda kwa Dokta Masawe kwani alishampa ripoti ya jambo hili, ila alimpa kwa muhtasari tu, sasa akamweleza A – Z.
"Hadi ninakuja hapa askari tuliembakiza kuangalia kila anayeingia na kutoka kwa Dokta Masawe bila yeye kujulikana amenipigia simu muda si mrefu kuwa Dokta Masawe hajarudi nyumbani kwake!"
Afande Kubuta alikuwa anampa ripoti yake Inspekta Jamila.
"Sawa Afande kazi nzuri, sasa mimi nina simu ambayo jana niliongea na Dokta Masawe baada ile ya Voda kumkosa, hivyo nataka tumpigie kutumia simu namba ile."
Inspekta Jamila alimwambia Afande Kubuta, na Afande Kubuta akashangaa aliposikia neno hilo, akashindwa kujizuia na akasema.
"Afande tunachelewa tumpigie sasa hivi." Alisema Afande Kubuta!
"Hapana Afande Kubuta, huyu tunatakiwa tumpigie simu tukiwa Computer Room, na kama atapokea simu wakati huo, basi atakuwa anatusogeza hatua thelathini mbele."
Inspekta Jamila alimwambia Afande Kubuta, na hata alipokwisha kusema maneno yale, Afande Kubuta alikuwa anatabasamu huku akimpa tano Inspekta Jamila.
Wote kwa pamoja Inspekta Jamila na Afande Kubuta walinyanyuka vitini wakaelekea katika chumba cha mawasiliano kilichosheheni Computer, wakaeleza shida yao kwa mtu wa mawasiliano anaeitwa Dihenga ambaye pia ni askari.
baada ya kuweka mambo sawa Inspekta Jamila akampigia simu Dokta Masawe huku akiomba mungu simu ile isiwe imezimwa.
Na baada ya sekunde kadhaa simu ya Dokta Masawe ikawa inaita.
"Hollow nani mwenzangu?!"
Dokta Masawe alipokea simu huku akiwa anahema ile mbaya.
Wakati huohuo Dihenga bila kufanya ajizi akafanya vitu vyake!
"Jenifa hapa Dokta nilikuwa nakukumbusha kuhusu ahadi yetu."
Inspekta Jamila alianzisha mazungumzo mara moja.
"Dah! Afadhali nimekuona, Aha Samahani afadhali nimekusikia, kwani nilikuwa natafuta namna ya kukupata nikawa nashindwa kwani namba yako ya simu hukunipa. Nimepatwa na dharura nimesafiri toka jana usiku hapa nipo Moshi. Sasa ile kazi yako sitoweza kuifanya kwa kweli. Kwani sitarajii kurudi siku za hivi karibuni. Hivyo tafuta Daktari mwingine."
Dokta Masawe huku akibabaika kweli kweli, alisema kisha akakata simu, kabla Inspekta Jamila hajaongeza neno lolote, kwani alishambaini kuwa yule ni askari kanzu na wala hana mgonjwa!
Inspekta Jamila ilipokatwa ile simu, akamgeukia afande Dihenga, kama mtu aliekuwa anataka kuelezwa kitu!
Afande Dihenga, akiwa anavua vifaa vya mawasiliano masikioni mwake, alimnyooshea alama ya kidole gumba Inspekta Jamila.
Inspekta Jamila, kwa wahka mkubwa akamwambia afande Dihenga.
"Nipe uelekeo tafadhali."
"Tabata Segerea, Bs motel"
Afande Dihenga alijibu huku akitazama compyuta ilyokuwa mbele ya macho yake.
Bila ya kupoteza muda, Inspekta Jamila alimpa tano afande Dihenga, akatoka na afande Kubuta, wakiwa tayari kuelekea Tabata Segerea.
Askari wale wakiwa katika gari lenye namba za kiraia, mali ya Jeshi la Polisi gari aina ya Toyota Soluna walikuwa wanaitafuta Tabata Segerea.
Dakika arobaini baadae gari ile waliiegesha nje ya jengo la Hotel ya BS, pale eneo la Segerea.
Afande Kubuta na Inspekta Jamila wakateremka ndani ya gari ile wakionekana kama Bibi na Bwana wakajichoma ndani ya Hoteli ile.
Walipoingia tu pale ndani katika sehemu ya kupatia vinywaji, walikutana uso kwa uso na Dokta Masawe akiwa anapata kilevi.
Hali aliyokuwa nayo Dokta Masawe baada ya kumuona Inspekta Jamila, pombe yote ilimtumbukia nyongo!
Kwani alitahayari kama mtu aliyefumaniwa akiwa katika ugoni.
Inspekta Jamila na Afande Kubuta wakakaa katika viti vitupu vilivyokuwa katika meza ya Dokta Masawe na Inspekta Jamila akamsalimia Dokta Masawe.
"Habari ya safari ya Moshi Dokta vipi umerudi kwa concord?!"
Ilikuwa ni salamu ya uzushi na dharau kutoka kwa Inspekta Jamila.
Dokta Masawe hakuweza kusema chochote bali alikuwa amejiinania huku akiwa na wasiwasi na hofu.
Kitendo bila ya kuchelewa Afande Kubuta alitoa pingu akamfunga nazo mikononi Dokta Masawe.
"Kwa nini mnanifunga pingu hali sijakataa kwenda huko mnapotaka kunipeleka. Hii siyo sheria bwana, nitawashitaki kwa kitendo hiki cha kunidhalilisha!"
Dokta Masawe alikuwa anatatalika kama bisi kikaangoni.
Lakini wapi bwana alichukuliwa kituuteni hadi ndani ya gari na safari ya mjini ikaanza.
Dokta Masawe hakika alikuwa amepatikana kweli kweli, ikawa hana jinsi ila kuyakubali matokeo, akawa muumini mtiifu wa ule msemo usemao, kubali yaishe!
Wakati Afande Kubuta alikuwa anaendesha gari, Inpekta Jamila alikuwa anamchunga Dokta Masawe aliyekaa naye katika kiti cha nyuma ya gari ile, huku akiiperuzi simu ya Dokta Masawe.
Katika kupekua pekua kwake, akakutana na ujumbe uliomsisimua.
Ujumbe huo ulikuwa unasomeka hivi;


***DOKTA MASSAWE AMEPATIKANA…ametaharuki kupita kawaida naakili haifanyi kazi, ametiwa pingu…..
Katika simu yake umekutwa ujumbe…..ni ujumbe gani,….
JE UPELELEZI umekaribia kukamilika???


Jagarld Jullie Z Sangomwile Khantwe Mr Rocky Gunda66 Himidini VAN HEIST BPM ABUBAKAR SHEKAU NYIROmamsapkhan born again pagan princetx Ennie mcubic jonnie_vincy slim5 MAVUNO mp anold amoneyazan
 
RIWAYA: BARUA KUTOKA JELA
MTUNZI: IBRAHIM GAMA


SEHEMU YA KUMI NA NNE

Dokta Masawe hakuweza kusema chochote bali alikuwa amejiinania huku akiwa na wasiwasi na hofu.
Kitendo bila ya kuchelewa Afande Kubuta alitoa pingu akamfunga nazo mikononi Dokta Masawe.
"Kwa nini mnanifunga pingu hali sijakataa kwenda huko mnapotaka kunipeleka. Hii siyo sheria bwana, nitawashitaki kwa kitendo hiki cha kunidhalilisha!"
Dokta Masawe alikuwa anatatalika kama bisi kikaangoni.
Lakini wapi bwana alichukuliwa kituuteni hadi ndani ya gari na safari ya mjini ikaanza.
Dokta Masawe hakika alikuwa amepatikana kweli kweli, ikawa hana jinsi ila kuyakubali matokeo, akawa muumini mtiifu wa ule msemo usemao, kubali yaishe!
Wakati Afande Kubuta alikuwa anaendesha gari, Inpekta Jamila alikuwa anamchunga Dokta Masawe aliyekaa naye katika kiti cha nyuma ya gari ile, huku akiiperuzi simu ya Dokta Masawe.
Katika kupekua pekua kwake, akakutana na ujumbe uliomsisimua.
Ujumbe huo ulikuwa unasomeka hivi;
"Dokta kuwa makini na yule dada uliyekuwa unaongea naye pale friends corner Hotel, kaa naye mbali kwani yule dada ni shushushu. Hivyo kwa taarifa kamili tutaongea hiyo kesho saa tisa kama tulivyopanga tukikutana pale Baracuda, nikuandikiapo ujumbe huu tayari ameshawamaliza Juja na mwenzake Mwaky, hivyo kuwa makini sana hakikisha leo hulali nyumbani kwako"!
Inspekta Jamila alipoangalia namba iliyotuma ujumbe ule na muda, aliona jina lililotuma ujumbe ule limeandikwa MWAIPOPO.
Na ametuma ujumbe ule jana saa moja usiku.
Inspekta Jamila akamuuliza, Dokta Masawe, wakati huo gari yao ikiwa katika eneo la Sanene kule Tabata Segera wakirudi mjini.
"Huyu Mwaipopo ni yule Geradi Mwaipopo uliyekuwa naye jana mchana pale Friends Corner Hotel?"
Dokta Masawe hakujibu kitu alikaa kimya. Inspekta Jamila akamwambia.
"Bado muda wako Dokta Masawe, bali muda ukifika utatueleza kila kitu na wewe mwenyewe utatupeleka kwa hao jamaa zako."
Inspekta Jamila alizungumza kwa hasira, huku aiuma meno yake, na uendelea kumsimanga Dokta Masawe.
"Daktari kama wewe serikali inakuamini, lakini wewe umeshindwa kuibeba amana, yani wala huelekei kwani unalipwa pesa nyingi sana kwa kwenda kwako kazini siku ya Jumanne na Alhamisi, Yaani siku saba za wiki wewe unakwenda kazini siku mbili na bado una Zahanati yako bila shaka hata wale wagonjwa unawahamisha kutoka katika hospitali ya serikali na kuwapeleka katika Zahanati yako, kwa tamaa iliyokujaa ya pesa. Ukisikia Wachaga kwa kutafuta pesa wanaongoza, basi ndio utafute hata pesa za roho za watu?!"
Afande Kubuta aliendesha gari,na sasa alikuwa yupo katika maeneo ya Tabata Sigara wakienda ofisini kwao. Nusu saa baadae wakawa wanaingia katika jengo la Wizara ya mambo ya ndani ya nchi.
Dokta Masawe akateremshwa ndani ya gari ile, wakaingia nae ofisini kwao.
Walipofika ndani ya ofisi, Inspekta Jamila aliangalia saa ya ukutani iliyokuwa ofisini mle, nakuona ilishatimu saa saba na nusu za mchana, alitoa simu yake katika mfuko wa suruali aliyovaa ya kitambaa cha suti iliyomkaa vyema, ikimbana sehemu ya mapajani na kuonyesha hipsi zilivyotokeza, na makalio yalivyotuna kwa nyuma, na chini suruali ile ilimwaga katika mtindo wa Bwanga huku miguuni akiwa amevaa viatu vya ngozi vya kutumbukiza.
Alibonyeza namba kadhaa na baada ya muda simu ya upande wa pili ikawa hewani,na Inspekta Jamila akatoa maelekezo.
"Nendeni mkatege katika eneo la Baracuda Baa, pale katika kona yakwendea Tabata Chang'ombe na Vingunguti machinjion. Kwani mnamo majira ya saa tisa, yule mualifu tunaemtafuta, Jeradi Mwaipopo atakuwa maeneo yale."
Baada yakuongea maneno yale akakata simu.
"Hivi mnanikamata kwa kosa gani, mpaka mnanidhalilisha kiasi hiki?!"
"Dokta Masawe unajuwa tulilokukamatia, na kitu tunachotaka kutoka kwako"
Inspekta Jamila alimjibu Dokta Masawe alieanza kupata sauti baada ya kusikia na mwenzake akiwindwa!
"Sawa lakini huna ushahidi wowote kama mimi na wewe tuliwahi kupanga mpango wowote, lakini pia sijashiriki jambo lolote baya na wewe ukalishuhudia, basi kama hivyo ndivyo kosa langu lipo wapi?"
Dokta Masawe alijaribu kujitetea, na Inspekta Jamila hakumjibu kwa mdomo, alichofanya aliivua Flash Disc yake kutoka shingoni alipokuwa ameivaa, nakuipachika katika sehemu yake katika Computer iliyokuwa mle ndani ya ofisi,na kuifungua.
Baada ya sekunde zisizozidi ishirini, Computer ile ikaifungua ile Flash Disc na kuisoma.
picha za Video zenye sauti zikawa zinaonekana!
Dokta Masawe akajishuhudia toka alipokuwa anainuka katika meza aliyokuwa amekaa na wenzake hadi alipofika katika meza ya Inspekta Jamila.
Ngoma haikuishia hapo! Alionekana mzee wa kithethe alipoyaingilia maongezi yao, picha zikamalizia kwa wale jamaa zake waliokuwa wamekaa nae awali akiwemo Geradi Mwaipopo!
Ama kwa picha zile Dokta Masawe alifadhaika sana, kiasi alipoteza matumaini kabisa yakunusurika na kifungo pindi ushahidi ule ukifikishwa mahakamani, kwani atakuwa hana la maana atakalojitetea kwalo!
"Ndugu zangu naomba tuyamalize maswala haya hapahapa yasifike mbele!"
Dokta Masawe alianzisha mazungumzo yakupelekea kutoa hongo.
Afande Kubuta alitaka kusema neno, Inspekta Jamila alimzuia kwa ishara ya mkono kisha akamuuliza Dokta Masawe.
"Unataka tuyamalizeje sema tunakusikiliza"
"Mimi nipo tayari kutoa kiasi chochote cha pesa ili mambo haya yaishie hapahapa"
Dokta Masawe alikuwa anatafuta MLISI! Inspekta Jamila akamwambia.
"Sisi tupo tayari kukuachia bila ya kuchukua hata senti tano yako, lakini tunataka utupe ushirikiano ututajie wale wahusika wenzio majina yao na wanapokaa, lakini pia unafahamu nini kuhusu kifo cha Marehemu Bartazal na mkewe Hamida.ukitwambia hayo kwa ufasaha tutakuachia, kinyume na hivyo wewe utaozea jela uwaache wenzio walioshirikiana na wewe wawe wanapeta mitaani kwa kunywa Lager!"
Maneno yale yalimchoma sana Dokta Masawe na kwa kweli hakuwa tayari kwenda jela, hivyo akajikuta katika wakati mgumu, hatimae akaanza kutapika mambo ambayo Inspekta Jamila na Afande Kubuta yaliwaacha midomo wazi!
Dokta Masawe alianza kwa kusema.
"Mimi na Bwana Bartazal tulifahamiana kiasi miaka mitatu iliyopita, mara ya kwanza kuonana na Bwana Bartazal, ilikuwa pale kazini kwangu Muhimbili alipokuja kutibiwa mguu baada ya kuvunjika katika ajali ya gari. Nilipomfanyia upasuaji na kumuunga mguu wake alianza kuwa Karibu na mimi, kiasi yeye na mkewe walikuwa wakija katika Zahanati yangu mara kwa mara, Bwana Bartazal akiwa na hamu sana ya mtoto na mkewe alikuwa haonyeshi dalili ya ujauzito!
Bwana Bartazal siku moja akasema nikiwa mimi na yeye na mkewe. Dokta Masawe kama mke wangu akijaaliwa kupata ujauzito, mali zangu zote nitamuandikisha yeye! Kwani yeye ndiyo mimi na mimi ndiyo yeye pamoja na mtoto wetu mtarajiwa, kwani mimi binaadamu sina uhakika na mwisho wa maisha yangu, hivyo nachelea nisije kufa kisha mtoto na mke wangu wakaja kunyang'anywa mali na ndugu zangu, kama baadhi ya Jamii nyingine za Watanzania zinavyofanya!"
Dokta Masawe alisimama kidogo, kisha akaendelea.
"Baada ya kuniambia maneno yale, miezi miwili baadae Hamida alinijia peke yake akaniambia kwamba, nina mpango wangu nakuomba sana utilie baraka zako, kwani mume wangu wewe anakuamini sana, hivyo chochote utakacho mwambia wewe atakikubali! Mimi kuanzia sasa naweza kuachika katika ndoa, kwa sababu mume wangu anataka mtoto, na mimi sina uwezo wa kuzaa' kwani nilipokuwa shuleni nilipewa mimba na mwalimu wangu wa darasa, kisha akanipeleka kwa Daktari mmoja rafiki yake akanitoa mimba ile! Kumbe alinitoa vibaya akasababisha mfuko wa uzazi kuuharibu! Hivyo hata ningekutana na wanaume wa dunia nzima, Hamida mimi siwezi kupata ujauzito! Chondechonde nakuomba nistili na ndoa yangu."
Kama kulikuwa kuna mtu katika wakati ule alikuwa na huzuni na uchungu, basi alikuwa ni Inspekta Jamila.
Kwani alikamatika kusikiliza mkasa ule kwa shauku kubwa. Na Dokta Masawe akaendelea kusimulia mkasa ule mzito.
"Mimi nikamuuliza nawezaje kukusaia na kuiokoa ndoa yako?! Yeye akanambia, mimi nataka kujidanganya kuwa ninahisi mimba, hivyo kwa vyovyote vile mume wangu atanileta kwako ili uje kunithibitisha kama kweli nimenasa! Sasa ikitokezea tukaja kwako, usifanye makosa, nithibitishe kuwa ninayo mimba tena ya mtoto wa kiume!
Aliponiambia maneno hayo, nikamwambia itakuwa ngumu sana kufanya hivyo, kwanza itaniharibia CV yangu, lakini pia mumeo akishajua kwamba huna mimba bali ulikuwa ukimuongopea si ndipo utakapoachika? Akasema laa, yeye hatofika huko mpaka kujua kuwa anamuongopea, kwani atakapo mwambia kuwa ana mimba na mimi nikaithibitisha, Mumewe atamuandikisha mali zake zote!
Nae baada yakuandikishwa mali hizo, haitochukua muda mrefu atamuua mumewe, ili Dili lake lisibumbuluke!"
Alipofika hapa Inspekta Jamila alianza kumchukia Marehemu Hamida, nakumuona kuwa yeye ndiyo chanzo cha mambo yote haya kwa tamaa zake!
"Ehee baada ya hapo nini kikaendelea?"
Inspekta Jamila akamuimiza Dokta Masawe ili aendelee kwani alitaka kujua hatima ya jambo lile lilivyokuwa.
"Mimi nilikataa katakata, kwani sikuiona faida nitakayoipata katika jambo lile zaidi ya dhambi. Lakini Hamida alinihakikishia kuwa, kama nitakubali kushirikiana nae katika mpango wake huo, atanigawia Robo ya mali yake yote atakayoandikishiwa na mumewe! Nami Shetani akanitawala, nikashawishika nikajikuta nashiriki katika mpango huo!"
Dokta Masawe alizungumza huku machozi yakimtoka, akionyesha kujutia kitendo kile, lakini wapi Maji yakisha mwagika hayazoleki.
Dokta Masawe alifuta machozi kisha akaendelea.
"Nilipomkubalia alinipiga busu zito, akaniachia na pesa shilingi Elfu hamsini tasilimu, akaniaga nakutoka. Baada ya kama wiki tatu baadae Hamida alikuja na mumewe ili kuja kupima ujauzito, nami nikajua mchezo umeshaanza! Nilimchukua vipimo vya damu ya mshipa pamoja na mkojo wake nikajifungia navyo maabara, nilipotoka nilimpa Hongera Bwana Bartazal na atarajie mtoto wa kiume!
Kwa kweli Bwana Bartazal alionyesha furaha isiyo kifani, kwani alimkumbatia mkewe na kumbusu mbele yangu, huku akiniambia, Dokta niliwahi kuahidi mbele yako kuwa mke wangu akipata ujauzito, nitamuandikisha mali zangu zote, kwa kuwa hili limetimia, basi na mimi sina budi ila kutimiza ahadi yangu kwani Ahadi ni deni!"
"Bwana Bartazal alimuandikisha mali zake zote mkewe.
Ilipofika miezi mitatu Hamida akanijia nakuniambia, sasa umefika wakati wakupata Robo ya mali yangu, kama tulivyokubaliana, na ili jambo hilo litimie, bado juhudi zangu zinahitajika!
Nazo ni kumpa mbinu ya kumuuwa mume wake mpendwa Bwana Bartazal Halim.




******Siri inafichuka….
ITAENDELEAAA
 
Da! Dr Massawe anasema shetani alimpitia.. We shetani kama unasoma hapa, ujue we mbaya, tena sikupendi
^^
 
Ha ha ha! Kweli, Kwanza sidhani hata kama jamaa yupo au alishahamia mbele ya sayari ya Pluto!
^^

Himidini kabisa aise maana kuna watu wanakamatwa ugoni wanasingizia shetani mafisadi nao wanasingizia shetani yaani shetani huko aliko nafikiri anapata pressure kabisa kuona haya
 
Last edited by a moderator:
Himidini kabisa aise maana kuna watu wanakamatwa ugoni wanasingizia shetani mafisadi nao wanasingizia shetani yaani shetani huko aliko nafikiri anapata pressure kabisa kuona haya

Ha ha akijitokeza atakana wengi sana.. Kwenye dini huko wanakomkemea ndo usiombe, pamegeuka chaka la hirizi zinazopumua, mwamvuli wa wezi, kinga ya usaliti..
INATIA HASIRA SANA.. Yaani hulka na silka zetu kuzibatiza majina ya excuse!
^^
 
Last edited by a moderator:
Ha ha akijitokeza atakana wengi sana.. Kwenye dini huko wanakomkemea ndo usiombe, pamegeuka chaka la hirizi zinazopumua, mwamvuli wa wezi, kinga ya usaliti..
INATIA HASIRA SANA.. Yaani hulka na silka zetu kuzibatiza majina ya excuse!
^^


Mkuu Dini siku hizi ni biashara inayolipa sana na ukishajua mistari miwili mitatu wewe kaanzishe lako na jua kunena kwa lugha na kuomba kwa sauti na kupunguza sauti umepata waumini na wewe unakuwa ni mheshimiwa sana baba dr, nabii, mtume, mpakwa mafuta vyeo vyote jipe huku kwapani una hirizi au una sharti kutoka kwa mganga wako wa Nigeria
 
Mkuu Dini siku hizi ni biashara inayolipa sana na ukishajua mistari miwili mitatu wewe kaanzishe lako na jua kunena kwa lugha na kuomba kwa sauti na kupunguza sauti umepata waumini na wewe unakuwa ni mheshimiwa sana baba dr, nabii, mtume, mpakwa mafuta vyeo vyote jipe huku kwapani una hirizi au una sharti kutoka kwa mganga wako wa Nigeria

Bravo Mr Rocky Sayari yetu hii, PESA imeshika katikati ya ufahamu wa mwanadamu,sasa inasakwa kwa njia halali au haramu.
^^
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom