RITES Matapeli-Said Amour Arfi(CHADEMA)

Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,130
44
MBUNGE wa Mpanda Kati, Said Amour Arfi (CHADEMA), ametaka mkataba wa ukodishaji wa Shirika la Reli nchini (TRC) kwa Kampuni ya RITES ya India uliosainiwa mwaka jana baina ya serikali na kampuni hiyo, uangaliwe upya, kwani hauonyeshi ufanisi, badala yake umelipunguzia taifa mapato.

Alitoa kauli hiyo jana mjini hapa, alipokuwa akiwasilisha hoja binafsi kuhusu uendeshaji usioridhisha wa TRC, unaofanywa na RITES, ambayo ilitarajiwa kuleta ufanisi katika sekta ya usafiri wa treni lakini matokeo yake imekuwa ni karaha kwa wasafiri na wafanyakazi wa kampuni hiyo.

Aidha, Arfi alitoa takwimu za kutofanya vizuri kwa kampuni hiyo kiasi cha kushuka kwa mapato yatokanayo na mizigo, ambapo kabla ya kuja kwa RITES, Reli ya Kati ilibeba mizigo ya tani 1,169,000 na kuingiza zaidi ya sh bilioni 62 mwaka 2005, lakini katika kipindi cha mwaka mmoja uwezo wake ulipungua kwa asilimia 33 na kusafirisha tani 775,281 tu zilizoiingizia kampuni hiyo sh bilioni 46.2.

“Kulingana na takwimu nilizozitoa hapo juu, ni dhahiri kuwa kampuni hii haina uwezo wa kufanya biashara husika na imekuwa mzigo mkubwa kwetu badala ya kuwa mkombozi na hivyo kuzidisha kero kwa wasafiri pamoja na watumishi wake,” alisema Arfi.

Kwa misingi hiyo, aliitaka serikali kuweka bayana mchakato mzima wa upatikanaji wa mzabuni ulioipa ushindi RITES na kujua nani aliyetoa ushauri wa kukodishwa kwa shirika hilo.

Aidha, alisema kuna minong’ono kuwa RITES walipewa jukumu la kushauri na kuangalia mali za TRC, matatizo, mafanikio na njia zinazofaa za kuliendesha shirika hilo na baada ya kazi hiyo kukamilika zilipatikana kampuni nne zilizotaka kupewa dhamana ya kuiendesha TRC, ikiwamo RITES.

Alisema kuna kampuni iliyokwenda mahakamani kupinga mchakato huo, lakini katika hali isiyoeleweka iliamua kuondoa kesi mahakamani.

Alisema kutokana na uwezo mdogo wa kampuni hiyo, ni wakati muafaka kwa wananchi na Bunge kujua mchakato mzima ulivyoendeshwa ili kuweka bayana baadhi ya mambo yanayosemwa tofauti na hali halisi ilivyokuwa.

“Serikali inamiliki asilimia 49 ya hisa, na mwekezaji anamiliki asilimia 51, ni vema sasa wananchi wakajua kila mwanahisa alitoa kiasi gani na vifaa gani katika kuendeleza biashara husika, ili tuondoe wingu la kuwa hawa jamaa wa RITES hawakuleta chochote,” alisema Arfi.

Mbali na hilo, Arfi alitaka wananchi wafahamu mtaji wa kuanzisha kampuni hiyo ni kiasi gani, kila mbia amelipa nini na za serikali zimelipwa kutoka katika vyanzo gani na iwapo ziliidhinishwa na Bunge.

Aidha, alisema wakurugenzi wa RITES ni wageni na hakuna hata Mtanzania aliyepewa dhamana ya kuongoza kitengo chochote katika kampuni hiyo, jambo linaloweza kuwa na hatari kwa taifa pamoja na usalama sambamba na kutojua nini faida wanayopata kwa kukosa uwakilishi.

Aidha, alisema kuna taarifa kuwa TRL imepata mkopo wa dola milioni 77 kwa dhamana na mwamvuli wa serikali, na dola milioni 33 kutoka Shirika la International Development Agency (IDA), na dola milioni 44 kutoka kwa Shirika la International Finance Corporation (IFC) na kwamba, serikali iliwahi kulijulisha Bunge kuwa RITES itajenga kilomita 645 za reli wakati wa mkataba wake.

Alisema kwa taarifa alizonazo zinaonyesha kuwa TRC kabla haijakodishwa kwa RITES, ilikuwa imeomba kutoka IDA na IFC dola milioni 77 kwa ajili ya ukarabati wa kilomita 645 za reli, ukarabati wa injini 90, mabehewa ya abiria 100 na ya mizigo 1,280 yaliyokuwa ya TRC na kwamba TRL wangetoa dola milioni 34 kufikia dola milioni 121 zilizokuwa zinahitajika kwa kazi zilizotajwa.

Alisema mambo yote yaliyofanywa na RITES, kwa kiasi kikubwa ndiyo ambayo yalishaanzwa kufanywa na TRC, hivyo RITES walikuja kudandia kile kilichofanywa na mtu mwingine hivyo kufanya dhana halisi ya uwekezaji wa RITES kukosekana.

“Serikali inaweza kutupa maelezo kuhusu nafasi ya RITES katika uwekezaji huu? Na kama wananchi wakisema wametapeliwa watakuwa wanakosea? Kwani hawa jamaa hawajaleta chochota hapa,” alisema Arfi.

Alisema kuna taarifa zinazokinzana kati ya watumishi na uongozi wa TRL kuhusu vipuri vilivyohamishwa kutoka Tanzania kupelekwa India na kutaka Bunge lithibitishiwe uhakika wa taarifa hizo na kama ni kweli, ni vifaa gani vilivyopelekwa India, vyenye thamani gani na kwa lengo gani.
 
Huu mkataba wa RITEs naona umekaa kama ni Management than of an investor, kama wa Net Group Solution, maana sioni contribution yao zaidi ya ufijaji in both sides, kwenye hiyo management wanaofanya na kwenye hiyo shares zao za sisi kuwapa 51%
 
Back
Top Bottom