RITA yapiga marufuku uvaaji wa mavazi yasiyofaa

Uchangiaji wa jazba kwa baadhi ya members!
Soma link niliyotoa hapo juu.
Nadhani inabidi tutoke hapa tulipo. Moderation ikiwa ni kufunga mijadala pale baadhi ya members wanapokuwa na jazba basi ni mijadala michache itaendelea. Nilidhani kama kuna tatizo la member au post yake basi ingetakiwa wadeal na huyo member au hizo post zake zisizofaa hapa jukwaani. Otherwise sioni ubaya wa kuendesha mjadala huu/ule. Labda kama suala lilikuwa sio aina ya uchangiaji bali ni authenticity mada yenyewe (ili kuwatendea haki RITA) - kama tangazo lenyewe hasa limetolewa na RITA kam inavyodaiwa ama la.
 
Mtu akienda kitovu nje hawatampa huduma? Kwa sheria gani ya nchi mtu hahudumiwi na serikali kisa maadili?

Hivi ni maadili gani hayo wanayozungumzia hao watu?

I'm so sick and tired of this maadili talk coz it's full of shit!
 
  • Thanks
Reactions: Tom
Mkuu lakini kuna mwananchi anadai ameenda pale kupata huduma akakataliwa kwa sababu alikuwa amevaa kaptula. Hatuwezi kulipuuzia kama kweli watu wanakataliwa huduma kutokana na mavazi yao. Soma hapa: MICHUZI: yale yaleeeee....

Tunapuuza kwa vile halijatukuta. Lakini serikali kunyima watu huduma kwa "makosa" yanayotokana na opinions tu ambazo zinakiuka katiba si haki hata kidogo
 
nakubaliana na wewe kabisaa.

Mtoa mada hakuliona hilo.

Lakin vile vile lazima ajue kuwa Tz kuna dressing code za kuingia kwenye taasisi zake zote.
Kwani RITA siku hizi ni private ompany?

Unaweza kutwekea hapa hizo regulations za dressing code ambao zinatumika tuu kwenye public sector lakini sio kwenye private sector? Huo si ubaguzi?
 
Tunapuuza kwa vile halijatukuta. Lakini serikali kunyima watu huduma kwa "makosa" yanayotokana na opinions tu ambazo zinakiuka katiba si haki hata kidogo

Hivi hao hapo kwenye picha wakitinga pale wakiwa wamevaa hivyo watakataliwa kuingia?

barack-obama-wearing-shorts.jpg
 
Kaptula hata wewe utaiafiki mtu aivae katika hadhara? Hoja kuu ni hiyo NIKABU!!

Kuna tatizo gani la kuvaa kaptula hadharani? Hivi mtu akienda kwenye duka la serikali linazouza vitabu kweli watakataa kumwuzia kwa sababu amevaa hayo mavazi? Kiongozi mkuuw a serikali akitinga hapo RITA amevaa hayo mavazi watamkatalia kuingia?
 
Hilo tangazo mwanzo mwisho ni aibu.

Umeona hizo space baina ya maneno?

Kaptula nayo umeiona?

Kininja jee?

Seriously! Duh

Public relation mbaya sana. Tumeyaona matangazo ya aina hii mengi tuu mpaka yale yanayotoka magogoni.
 
Kuna tatizo gani la kuvaa kaptula hadharani? Hivi mtu akienda kwenye duka la serikali linazouza vitabu kweli watakataa kumwuzia kwa sababu amevaa hayo mavazi? Kiongozi mkuuw a serikali akitinga hapo RITA amevaa hayo mavazi watamkatalia kuingia?

Okay......hatuna sera za mavazi kitaifa hata hivyo......ni imani au wehu wetu ndio vinatusukuma tuvae vipi
 
...hatutapendelea baadhi ya mavazi yasiyofaa na yasiyo na heshima kuvaliwa ofisi kama yafuatayo:-
  1. Mavazi yanayofunika uso wote - Kininja "Nikab"
Ngoja hasira za za kushindwa kuzuia mitihani ya Ndanda zihamie RITA !
 
Public relation mbaya sana. Tumeyaona matangazo ya aina hii mengi tuu mpaka yale yanayotoka magogoni.

Mimi siamini kuwa mtu mzima na akili timamu aloyefaulu hata darasa la saba anaweza kuandika vile.
 
Okay......hatuna sera za mavazi kitaifa hata hivyo......ni imani au wehu wetu ndio vinatusukuma tuvae vipi

Hili tangazo ni ubaguzi wa nje nje. Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote kuweka sharti lolote ambalo ni la ubaguzi ama wa dhahiri au kwa taathira yake. Ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa kazi au shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi.
 
Kuna tatizo gani la kuvaa kaptula hadharani? Hivi mtu akienda kwenye duka la serikali linazouza vitabu kweli watakataa kumwuzia kwa sababu amevaa hayo mavazi? Kiongozi mkuuw a serikali akitinga hapo RITA amevaa hayo mavazi watamkatalia kuingia?
Mwisho wa siku inategemea na mtazamo wa mtu., nilishawahi kuingia na pens ya timberland ofisi ya lecturer
chuo akagoma kunihudumia hadi nikavae kistaarab.
Af sitaki kuamini hl tangazo maana halina muhuri, sahihi wala logo na ni la 2011
 
Tunapuuza kwa vile halijatukuta. Lakini serikali kunyima watu huduma kwa "makosa" yanayotokana na opinions tu ambazo zinakiuka katiba si haki hata kidogo
Mimi yalinikuta tena hapo hapo RITA...askari aliniKimbilia nikiwa naelekea kwenye ofisi akaniambia nimevaa nguo imeacha mabega wazi kwa hiyo nitafute mtandio....
Niligoma kutoka na nilihudumiwa vile vile kwa sababu binafsi sikuona ubaya wowote wa nilichokua nimevaa, tena mabega si kwamba niliacha wazi kivile....
Inaudhi sana lakini, wanaacha kuangalia mambo ya msingi wanaangalia kaptula na milegezo na nikab.

Sehemu yenyewe wanyotolea huduma kwa mfano ya vyeti vya kuzaliwa ni nje kabisa na nadhani lilikuwa eneo maalum kwa ajili ya parking!? Sasa wanataka twende maegesho tumevaa suti?
 
Back
Top Bottom