Rita Mlaki hatarini kusimamishwa udiwani Dar

Kasheshe

JF-Expert Member
Jun 29, 2007
4,694
787
Kamati ya Fedha na Uongozi ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, imemtaka Meya Adam Kimbisa kukutana na mjumbe wa baraza hilo, Rita Mlaki kumshauri ahudhurie mikutano ya halmashauri hiyo kabla ya kuchukuliwa hatua za nidhamu.

Taarifa hiyo iliwasilishwa jana na Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, Salum Londa, mbele ya Naibu Meya wa Jiji hilo, Ahmed Mwilima, wakati baraza hilo lilipokutana kwa ajili ya kupitia na kupitisha taarifa za kamati za robo tatu ya mwaka 2007/2008.

Londa alisema hadi kufikia Februari 26, mwaka huu, Mlaki ambaye pia ni Mbunge wa Kawe, hakuhudhuria mikutano 17 ya baraza hilo na mikutano 25 ya Kamati ya Fedha na Uongozi, hali ambayo kwa mujibu wa kanuni, alipaswa kusimamishwa udiwani wa halmashauri ya jiji.

“Mheshimiwa Mlaki alikuwa akipelekewa taarifa ya wito wa vikao vya baraza hili tangu Februari mwaka 2006 pasipo kuhudhuria,” alisema Londa. Londa alisema katika taarifa hiyo kuwa kamati hiyo imeazimia kwamba Kimbisa akutane na mjumbe huyo ili kumshauri ahudhurie mikutano ya halmashauri kwa mujibu wa kanuni kabla ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu.

Mlaki alipopigiwa simu na gazeti hili kujua ni sababu zipi zilizomzuia kuhudhuria vikao hivyo kwa kipindi chote hicho, alikuwa mkali na kushutumu vikali gazeti hili kwa kuandika habari hiyo na kudai kuwa hawezi kujibu chochote kuhusiana na suala hilo.

“Nasema hivi mimi ndio Rita Mlaki, andika chochote unachotaka na sikujibu, ninyi gazeti la Serikali badala ya kuwaachia akina (alitaja jina la gazeti) waandike mambo kama haya, nyie ndio mnaandika, sasa sisemi kitu na ukaandike,” alisema mbunge huyo kwa hasira.
Halima Mlacha
Daily News; Thursday,July 03, 2008 @00:03

Pia Londa katika taarifa yake hiyo, alisema kamati hiyo imeazimia kuwa kesi ya Halmashauri ya Jiji dhidi ya Mamlaka ya Majisafi na Majitaka (Dawasa), juu ya umiliki wa jengo lililopo Mwananyamala, isifutwe kama ilivyoamriwa na uongozi wa ngazi za juu.

Alisema jengo hilo ambalo awali lilikuwa mali ya iliyokuwa Tume ya Jiji, lilipewa kwa Jiji na kupangishwa na Dawasa waliolitumia kama ofisi yao na kukubaliana kulipa kodi ya pango, jambo ambalo baadaye walikiuka kulipa kodi hiyo na kuifanya Jiji iishtaki Dawasa.

Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Mvumbo Dollah, akiwasilisha taarifa ya kamati yake, alisema mpaka sasa majengo ya biashara 6,191 yamekaguliwa katika manispaa zote tatu za Ilala, Temeke na Kinondoni ambako zilitolewa ilani 2,153 na kutekelezwa ilani 1,231 hivyo kuwafikisha mahakamani wamiliki 243 kwa kukaidi ilani hizo.

Source: Habari leo
 
Hii kali, kweli tuna shida. Kumbe kwa mujibu wake magazeti ya serikali yanatakiwa yafiche uozo? Hajui kwamba kila mtu sasa hataki kuoza na haoni kuwa wakiendelea kuficha uozo wataoza wao?
 
Mimi nimekuwa nikisema huku bodini kwa muda sasa: huyu Mama Rita Mlaki hafai kwenye siasa...HAFAI kabisa..huyu mama namjua miaka mingi mpaka alipoenda kusoma Masters ya mambo ya kemikali za plastic na baadaye kuwa General Manager wa Teggy Plastic...huo Ubunge wa Kawe ni kwa kifua cha Ben Mkapa (kupitia urafiki wake na Mama Mkapa) la sivyo asingeambulia kitu huko Kawe.

Kutokuhudhuria hivyo vikao ni dharau zake tu hana sababu yoyote ya maana...huyo mwandishi alipoteza dola zake kumpigia simu. Wamfukuze kabisa....

Wapinzani kaeni tayari hili jimbo la kawe ni rahisi sana kulichukua iwapo CCM watamuweka Rita Mlaki kama mgombea 2010 (kitu ambacho nitashangaa sana).
 
huyu mama anadharau sana, kawe hawamtaki wameshamshtukia na porojo zake zisizo nafaida kwao, aachane na ubunge arudi kwenye maplastick aliosomea.
 
hebu acheni mambo ya ajabu........! yaani amesomea kuokota kuokota vichupa vya maji ya uhai?
yaani wale tunaowaona wamebeba mifuko huku wakiokota masalia ya plastiki ndo fildi yake?
 
Mimi nimekuwa nikisema huku bodini kwa muda sasa: huyu Mama Rita Mlaki hafai kwenye siasa...HAFAI kabisa..huyu mama namjua miaka mingi mpaka alipoenda kusoma Masters ya mambo ya kemikali za plastic na baadaye kuwa General Manager wa Teggy Plastic...huo Ubunge wa Kawe ni kwa kifua cha Ben Mkapa (kupitia urafiki wake na Mama Mkapa) la sivyo asingeambulia kitu huko Kawe.

Kutokuhudhuria hivyo vikao ni dharau zake tu hana sababu yoyote ya maana...huyo mwandishi alipoteza dola zake kumpigia simu. Wamfukuze kabisa....

Wapinzani kaeni tayari hili jimbo la kawe ni rahisi sana kulichukua iwapo CCM watamuweka Rita Mlaki kama mgombea 2010 (kitu ambacho nitashangaa sana).

Sasa kwanini kikaoni hataki kwenda?
Ama kuna somethign going on?
Hayo mambo ya DAWASA Ni kwamba wameuziana ama ni rushwa?
Maana halitakuwa jambo la maana kuendelea kupoteza pesa za wananchi bila mpango.
Tunahitaji mabadiliko makubwa kwani TAIFA LIKO MIKONONI MWA MKOLONI NA VIBARAKA WAO...NA MASIKINI NDIO WATAWALIWA NA WENYE KUNYANYASWA KILA KUKICHA KWENYE ARDHI YAO...LICHA YA KWAMBA KODI ZAO NA MALI ZAO MAFISADI WALIZOUZA NA KUGAWANA NDIO KILICHOWAPA KIBURI!
WE WANT FREEDOM!
 
One by one kila mmoja anaonyesha mapungufu yake katika ulimwengu wa siasa za tz. Watu wanatakiwa wabadilike ndio njia tu la sivyo wataishia kusakamwa kila siku. Halafu kama mtu hauwezi kutekeleza majukumu yote hayo cha maana ni kujipunguzia mzigo.
 
aachane na ubunge arudi kwenye maplastick aliosomea.

Ndugu Majembe, hivi Ubunge, Uwaziri na Urais, unaweza ukavisomea na kuwa mtaaluma wavyo?
Kama huyu Mama atarudi kwenye maplastick aliyosomea, basi hata Rais wetu atarudi kwenye Uchumi (benki) aliosomea, na pia Wabunge wote watarudi kwenye fani zao walizosomea.

Hili umeliandika kama vile una Uhasama na huyu Mama.
 
Ilo sio tatizo ndugu
hiyo field ni nzuri na inalipa sana kwa sababu ya mazingira yetu, inategemea na msomaji anaitumia vipi.

Hapa tatizo ni kiburi cha huyu mama, na lingine ni hili la kuwa magazeti ya serikali kumbe kazi yake ni kuficha ukweli

Haya kila kitu kitajulikana tu mpaka kieleweke hapa

Mgosi Makamba(2008) alisema gazeti la mwanachi huwa haliwaandiki vizuri wana sisiem kwa hiyo hata matangazo yao wana magazeti maalum ya kuandika.
Haya Magazeti ya serikali bado yako kule enzi za SHIHATA ya akina BWM.
 
hebu acheni mambo ya ajabu........! yaani amesomea kuokota kuokota vichupa vya maji ya uhai?
yaani wale tunaowaona wamebeba mifuko huku wakiokota masalia ya plastiki ndo fildi yake?

Ndugu Mahesabu, ulivyokuwa unaaandika hii ulikuwa unamaanisha kutoka moyoni au ulikuwa unakejeli?
Kama Wewe Fani yako ni Mahesabu, Je unafundisha watu kuhesabu chembe za Mchanga?
Ndugu, Piga mahesabu yako vizuri.
 
Kama kavunja sheria na kanuni za Halimashsuri kwa nini asichukuliwe hatua?

Kuna haja ya kuwajibishana kwa mujibu wa sheria na sio vinginevyo.
 
Siasa za Bongo zinachekesha sana, yaani mtu hajahudhuria vikao kibao lakini bado anatumiwa mtu ili aende kumbembeleza na kumuuliza kwanini hajahudhuria badala ya kumchukulia hatua za kinidhamu kwa kufuata sheria na taratibu zilizopo.

Mtu asipotimiza wajibu wake anastahili haki yake .... kama alikuwa na sababu za kutohudhuria angetoa taarifa. Kitendo cha kukaa kimya ni dharau kwa Meya pamoja na Kamati husika. Bado Meya anaendelea kujidhalilisha kwa kutuma mtu na majibu ndo hayo sasa, sijui Londa anajisikiaje baada ya kusoma news kama hiyo iliyoandikwa na gazeti la serikali. News ingekuwa imeandikwa na magazeti mengine wangesingizia wapinzani wanatumika kuwavuruga na kumbe wao wenyewe ndio wana vurugana!
 
Ndio bongo hiyo tena wandugu.
 
..mara nyingine huyu Mama wanamshambulia kutokana na chuki dhidi ya kabila lake.

..sioni ajabu yoyote kwa yeye kushindwa kuhudhuria vikao vya madiwani. labda ametingwa na shughuli nyingine ambazo ni muhimu zaidi kwake.

..cha msingi hapa sheria na taratibu zifuatwe katika kushughulikia suala hili.

..zaidi, hivi Rita Mlaki ndiye diwani pekee nchi nzima,mkoa wa dsm,...asiyehudhuria vikao?
 
Si ndio zao hao nambari one kubebana hata kama mtu kachemka...inawezekana wanaogopa kumchukulia hatua huyo mama kwa kujua ni chichiemu mwenzao kumbe wanalea uozo tu. Na hao waliompa kura za ubunge walikosa pa kuzipeleka nini?? au ndio yale mambo ya ubwabwa kwa kanga za KTM....
 
hebu acheni mambo ya ajabu........! yaani amesomea kuokota kuokota vichupa vya maji ya uhai? yaani wale tunaowaona wamebeba mifuko huku wakiokota masalia ya plastiki ndo fildi yake?

Embu acheni kudhihaki elimu za watu, huyo mama kama kwenda shule amekwenda, tulalamikie vitendo vyake, lakini kudhihaki elimu ya mtu binafsi naona ni kuishiwa hoja.
 
..mara nyingine huyu Mama wanamshambulia kutokana na chuki dhidi ya kabila lake.

..sioni ajabu yoyote kwa yeye kushindwa kuhudhuria vikao vya madiwani. labda ametingwa na shughuli nyingine ambazo ni muhimu zaidi kwake.

..cha msingi hapa sheria na taratibu zifuatwe katika kushughulikia suala hili.

..zaidi, hivi Rita Mlaki ndiye diwani pekee nchi nzima,mkoa wa dsm,...asiyehudhuria vikao?

sijui nikuite nanga?
 
Back
Top Bottom