Risiti za Ushuru wa Maegesho za TARURA zinaweza kuvunja ndoa za watu

mandawa

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
732
1,062
Leo nimeamini TARURA laweza kuwa janga jipya hapa Dar. Leo tumepewa bill ya maegesho nikiwa na mwenza wangu, la ajabu katika bill, inaonyesha tarehe ambayo sote tulikuwa nyumbani mapumziko na la kushangaza zaidi bill inaonyesha gari lilipaki nje ya guest inayofahamika mitaa ya Sinza muda wa masaa manne.

Katika hali ya kawaida lazima mpate taharuki kila mtu anamuuliza mwenzie we ndio ulitoka na gari? Kucheki tarehe, tukacheka! Imagine kama isingekuwa hivyo, hapo ingebidi kila mtu ajitete kama sio kugombana.

Nashauri wasimamizi wa parking waweke sehemu ya jina signature/ saini ili mwenye gari ajue katozwa dio wakijisikia wanafoji tu bill.

Mi nimeapa silipi bill yao hadi wanipe kithibitisho cha gari yangu kuweko mahali hapo. Kinyume na hapo tutaebda sawa!

Pia soma:

Mimi bidada alikuja kwenye kioo Cha Gari ananibembeleza nilipe.
Ndo tukaanza kupiga story kumbe wanapewa kiwango Cha kukusanya kwa siku wasipo fikia Target wanakula mbokoo na sirikali
 
Hivi hizo taarifa ya kuwa unadaiwa unaijuaje, tueleweshane wakuu, maana tunaeteseka ni sisi.
Kuna app yao android , Gepg kama sikosei hapo kuna kila aina aina za kodi na tozo za serikali , na njia za kujua outstanding fines au balances , tarura pia ipo hapo
 
Download app ya termis

Mitaa ya sinza hata hawakimbizani na wewe utaenda kulipa mbele ya safari huko
Kuna mapungufu sana kwenye hili huko mbele itakuja kuleta utata!!
Parking huchajiwa kwa masaaa sasa kwa kuwa siku hizi hawatoi receipt yw kuwenka kwenye windscreen , waeza kujikita ndani ya saa moja umeandikiwa mara tatu , just because hukupaki sehemu moja .
 
Duh huo ni wizi wa kiwango cha sgr
Na kweli wengi wanalalamika sana
 
Hivi hizo taarifa ya kuwa unadaiwa unaijuaje, tueleweshane wakuu, maana tunaeteseka ni sisi.
Download hiyo app itakusaidia kulipa malipo yote ya serikali.
Screenshot_20211216-213902_One%20UI%20Home.jpg
 
Back
Top Bottom