Risiti za EFD zitaleta tatizo huko mbeleni

Mkata Mtaa

Senior Member
Jun 10, 2016
136
141
Nimejaribu kutafakari hili jambo naona litatuletea usumbufu baadae, kila unachonunua unabidi upewe risiti na mauzo unayofanya inabidi utoe risiti.

Mwisho wa mwaka kama unafanya hesabu unatakiwa kuangalia matumizi yako na mauzo yako ili kujua faida iko au hasara kwa ajiri ya biashara yako na TRA ili wakokotoe kujua kama umepata faida wakutoze kodi ya mapato.

Tatizo nililokuja kuligundua kwenye risiti karibu zote nilizonazo maandishi yake yanafutika baada ya muda, mfano nina risiti za petrol, Luku nk zote zimefutika kabisa.

Je mwisho wa mwaka nikitengeneza hesabu zangu kwamba haya ndio matumizi na mauzo yangu nikapeleka TRA itakuwaje?

Kwa uzoefu wangu TRA ukionyesha kwamba ukupata faida au kuwa ndogo mara nyingi uwa wanazikataa hesabu zako mpaka upeleleka ushahidi wa risiti au petty cash, lakini kwa sasa petty cash zitakuwa chache sana,
utapeleka risiti ambazo zitakuwa hazisomeki wakubaliane na mimi au ndio itakuwa vita either nifunge biashara au nilipe kodi watakavyotaka wao?

Hii kitu imenipa mashaka nikaona ngoja nisikilize mawazo toka kwa wenzangu.

Nakaribisha mjadala.
Mungu ibariki Tz.
 
mh.... mkuu mm ndo nimeomba, nimepewa barua nafkiri jumatatu ndo nitakwenda kuchkua kwa moja wa suppliers...
pia naskia hizi mashine zinakula hadi mtaji, ntaitaji kueleweshwa hapa inakula vp na jinsi gani kuizuia isitafune mitaji
tuko pamoja mkuu ngoja tuwasubiri wajuvi wa hizi ishu.
 
Nimejaribu kutafakari hili jambo naona litatuletea usumbufu baadae, kila unachonunua unabidi upewe risiti na mauzo unayofanya inabidi utoe risiti.

Mwisho wa mwaka kama unafanya hesabu unatakiwa kuangalia matumizi yako na mauzo yako ili kujua faida iko au hasara kwa ajiri ya biashara yako na TRA ili wakokotoe kujua kama umepata faida wakutoze kodi ya mapato.

Tatizo nililokuja kuligundua kwenye risiti karibu zote nilizonazo maandishi yake yanafutika baada ya muda, mfano nina risiti za petrol, Luku nk zote zimefutika kabisa.

Je mwisho wa mwaka nikitengeneza hesabu zangu kwamba haya ndio matumizi na mauzo yangu nikapeleka TRA itakuwaje?

Kwa uzoefu wangu TRA ukionyesha kwamba ukupata faida au kuwa ndogo mara nyingi uwa wanazikataa hesabu zako mpaka upeleleka ushahidi wa risiti au petty cash, lakini kwa sasa petty cash zitakuwa chache sana,
utapeleka risiti ambazo zitakuwa hazisomeki wakubaliane na mimi au ndio itakuwa vita either nifunge biashara au nilipe kodi watakavyotaka wao?

Hii kitu imenipa mashaka nikaona ngoja nisikilize mawazo toka kwa wenzangu.

Nakaribisha mjadala.
Mungu ibariki Tz.
Nimewahi kuambiwa na meneja wa TRA kuwa zipo karatasi feki na original, na kwamba zinazofutika ni feki.

Hata hivyo watu wanatoa kopi na kutunza kopi maana hazifutiki
 
Wakuu niza hovyosana alafu hazitaki msukosuko. Kwasisi wafanya biashara za shulba utata hautaisha nawatoza kodi yaani TRA. Mfano ukikosea kidogo ulikuwa unataka kuandika risiti ya 10,000 ukakosea ukaandika 100,000 yenyewe hairudi nyuma inakuwa tayari imesha record 100,000 nakodi itakokotolewa kutoka kwenye hiyo laki1 wakati umefanya biashara ya elfu10. Ili ujikomboe nahiyo, inabidi uandike barua haraka sana upeleke TRA ndani yasaa24, ikichelewa hapo imekula kwako. Sasa mtu utaandika barua ngapi maana kukosea nikawaida Kwa binadamu yeyote.
 
Kwani Anayebaki Na Risiti Ni Mteja Au Muuzaji? Unapofanya Transaction Kutumia Efd Hesabu Zinajirekodi Tra. Kingine Ni Kuwa Tra Hufanya Makadirio Na Wewe Unaanza Kulipa Instantly Kwa Awamu, Hivyo Mahesabu Yako Mwisho Wa Mwaka Yanakuja Kuoanishwa Na Makadirio.
 
Mkuu mimi hiyo kitu nilinunua toka 2013 nikatumia kama miezi mitatu hivi nikapadharura kidogo nikafunga duka muda kama wa miezi miwili nilivyorudi nikaiwasha inaletea ujumbe eror services contranct your distributor mpaka leo nimelitupa darini.
 
Unapofanya hesabu kwa mwaka lazima uonyeshe manunuzi na matumizi yako, kwa mauzo yako hayatakuwa na shida sababu record zako wanazo, tatizo linakuja je haya matumizi yako ni ya ukweli au umeyatengeneza tu. Kuna wakati uwa wanapenda kujiridhisha, uwa wanaomba risiti kama suporting documents sampling, sasa hizo suporting documents zinafutika, hapo ndipo mzozo utaanza kati ya TRA na mfanyabiashara.
 
Wafanya biashara mlikuwa mmezoea wafanyakazi wanawalipia kodi na wanawaendeshea nchi sasa na nyie mtaisoma No.

Unakuta mtu ana duka au Hosp analipa Tshs 3m/= kwa mwaka wakati mfanyakazi wa kawaida tu jumla atalipa kama Tshs 5M kwa mwaka.
 
KARATASI ZA MASHINE ZA EFD ZINATENGENEZWA NA KAMPUNI MBALIMBALI. ZIPO ZENYE NEMBO YA TRA. KAMA NDIZO HALISI, ZINA TATIZO LA HERUFI KUKAA JUU YA HERUFI ZINGINE. VEMA NEMBO IANDIKWE UPANDE WA NYUMA. DAWA TOA PHOTO KOPI.
 
Nimejaribu kutafakari hili jambo naona litatuletea usumbufu baadae, kila unachonunua unabidi upewe risiti na mauzo unayofanya inabidi utoe risiti.

Mwisho wa mwaka kama unafanya hesabu unatakiwa kuangalia matumizi yako na mauzo yako ili kujua faida iko au hasara kwa ajiri ya biashara yako na TRA ili wakokotoe kujua kama umepata faida wakutoze kodi ya mapato.

Tatizo nililokuja kuligundua kwenye risiti karibu zote nilizonazo maandishi yake yanafutika baada ya muda, mfano nina risiti za petrol, Luku nk zote zimefutika kabisa.

Je mwisho wa mwaka nikitengeneza hesabu zangu kwamba haya ndio matumizi na mauzo yangu nikapeleka TRA itakuwaje?

Kwa uzoefu wangu TRA ukionyesha kwamba ukupata faida au kuwa ndogo mara nyingi uwa wanazikataa hesabu zako mpaka upeleleka ushahidi wa risiti au petty cash, lakini kwa sasa petty cash zitakuwa chache sana,
utapeleka risiti ambazo zitakuwa hazisomeki wakubaliane na mimi au ndio itakuwa vita either nifunge biashara au nilipe kodi watakavyotaka wao?

Hii kitu imenipa mashaka nikaona ngoja nisikilize mawazo toka kwa wenzangu.

Nakaribisha mjadala.
Mungu ibariki Tz.

Sasa hata tatizo dogo na rahisi kama hilo unashindwa kutatua, huko Shuleni mlikwenda kufanya nini? Si ni bora mngebakia tu nyumbani?
 
Yote kwa yote kodi ilipwe regardless of party running the state!

Iwe CCM,Chausta ,Jahazi asilia ,CCK or Chadema
 
Wakuu niza hovyosana alafu hazitaki msukosuko. Kwasisi wafanya biashara za shulba utata hautaisha nawatoza kodi yaani TRA. Mfano ukikosea kidogo ulikuwa unataka kuandika risiti ya 10,000 ukakosea ukaandika 100,000 yenyewe hairudi nyuma inakuwa tayari imesha record 100,000 nakodi itakokotolewa kutoka kwenye hiyo laki1 wakati umefanya biashara ya elfu10. Ili ujikomboe nahiyo, inabidi uandike barua haraka sana upeleke TRA ndani yasaa24, ikichelewa hapo imekula kwako. Sasa mtu utaandika barua ngapi maana kukosea nikawaida Kwa binadamu yeyote.
Una cancel mkuu,jaoo wataifunga kutaka maelezo kwa nini uli cancel
 
Kama ulianza kukusanya hizo risiti una record kwenye vitabu halafu unatatumbukkza kwenye box bila kujua kama zinafutika? baada ya muda muda mrefu unakuja kugundua baadae utafanyaje? mimi ninazo za Luku, petrol nk zote zimefutika
 
Binafsi nanunua vitu kwenye maduka makubwa napewa risiti za EFD, kisha naenda kuwauzia watu juu kwa juu. Mfano nanunua kitu cha chenye thamani ya 120,000 kisha naenda kuuza kwa thamani ya 150,000 faida yangu 30,000, je EFD nikichukua ntamtolea risiti ya shs ngapi? Wakati mteja wangu katoa 150,000, ukizingatia nikimtolea risiti ya 150,000 basi faida yangu yote 30,000 inaenda TRA. Vat inakuwa elfu 27,000 inabaki elfu 3,000 nauli kila kitu muda nabaki sina kitu. Sio hapa kazi tu, bali hapa kukomoana tu. Maana asilimia kubwa ni wachuuzi kama mimi.
 
Kwanza zinaharibika ovyo na network zao ni jipu
ISP wao ni nani mkuu. Make shida ya nchi yetu mambo mengi huwa tunafanya kwa zima moto na kutanguliza 10%. Mkuu mimi naona tatizo ulilolisema haliko kwenye mashine ila karatasi. Yawezekana wakapata supplier wa karatasi wa hovyo anaye supply karatasi za kutolea risit zisizo na viwango. Na hawa jamaa huwa wana deal na supplier wahindi. Ushauri wangu ni wafanyabiashara ambao tayari mnatumia machine hizi na wote mna experience matatizo kama uliyoyasema, bora muungane ili mpeleke malalamiko yenu TRA mapema ili kuepusha usumbufu wa siku moja kulazimishwa kulipa zaidi.
 
Binafsi nanunua vitu kwenye maduka makubwa napewa risiti za EFD, kisha naenda kuwauzia watu juu kwa juu. Mfano nanunua kitu cha chenye thamani ya 120,000 kisha naenda kuuza kwa thamani ya 150,000 faida yangu 30,000, je EFD nikichukua ntamtolea risiti ya shs ngapi? Wakati mteja wangu katoa 150,000, ukizingatia nikimtolea risiti ya 150,000 basi faida yangu yote 30,000 inaenda TRA. Vat inakuwa elfu 27,000 inabaki elfu 3,000 nauli kila kitu muda nabaki sina kitu. Sio hapa kazi tu, bali hapa kukomoana tu. Maana asilimia kubwa ni wachuuzi kama mimi.
Nadhani wafanyabiashara aidha kwa kutumia wawakilishi wenu au nyie wenye mkaungana ili TRA wawape elimu katika maswala kama haya. Pia huwa kuna kitu kinaitwa tax return sina uhakika sheria za kodi Tanzania zinasemaje kuhusu tax return. Kwa sababu kulingana na hoja yako unatoa risiti hizo za EFD mwisho wa siku TRA lazima wafanye calculation kujua kama uliuza kwa faida ili ulipe kodi. Sina hukakika ni kiasi gani cha faida ambacho unapaswa uwe umefikia ili uweze kulipa kodi yao. Vitu kama hivyo huwa vipo, ila TRA mara nyingine wanatumia uelewa mdogo wa wafanyabiashara kuwatoza kodi hata kama kiliwalichotengeneza kwa kipindi hicho hakipaswi kulipiwa kodi. Mfano kwenye mishahara kuna kiwango ambacho kimesamehewa kodi. Hivyo hivyo kwenye biashara kuna kiwango cha faida utakachopata hakipaswi kulipiwa kodi. Jaribu kufuatilia upate elimu hii Mkuu. Make unaweza kusema ukwepe kwa hali ilivyo sasa wakaja kubeba kamtaji kako kote.
 
Back
Top Bottom