Risiti za EFD yenye maneno Not Registered inakata VAT?

Mar 21, 2015
13
0
Habarini wana Jamvi?

Naomba kusaidiwa hapa, kama tunavyojua ili taifa liendelee kulipa kodi ni swala lisilopingika. Na ukizingatia hata Mhe Rais amekua akihimiza wananchi kudai au kutoa risiti pale manunizi au mauzo yanapofanyika

Mimi ni mmoja wa waumini wakubwa wa kodi, lakini napata tabu hasa pale napopewa risiti ya EFD baada ya muamala lakini nikiisoma kuona kiasi cha VAT iliyolipwa naona hamna. Na nikiangalia juu mwanzoni mwa risiti pale kwenye VRN naona neno "*Not Registered*" hii maana yake nini??

Je ina maanisha baadhi ya wafanya biashara hawalipi kodi hasa pale risiti wanazotoa kutokua wamesajili VRN?? Naomba msaada wa mawazo.
 
Ili Upate VRN ni lazima uwe na mauzo yasiyopungua Mil 50 kwa mwaka, lakini.kwa sheria mpya ya sasa ni lazima uwe na mauzo yasiyopungua Mil 100. Sasa kama ulipewa risiti hiyo basi ujue mfanyabiashara huyo bado hajafikia kiwango hicho au bado hana sifa za kuchaji VAT. So hakuna Tatizo.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom