rrm72
JF-Expert Member
- Mar 10, 2015
- 508
- 300
Ndugu wana JF
Nilikutana na mtu kabeba bidhaa zake alizonunua, nikamuuliza umenunua shilingi ngapi, akanitajia. Nikauliza umechukua risiti ya EFD akasema ndiyo na bila kumuomba akaitoa kunioonyesha. Kusoma pesa iliyoandika ni robo ya pesa aliyonitajia. Nikamuuliza mbona hii pesa sio, akasema Jumla ya gharama nzima ilikuwa kubwa kuliko pesa niliyokuwa nayo, akanipunguzia kidogo naye akanikatia risiti hii ya EFD.
Nikajiuliza,
1. huyu serikali anapoteza pesa kiasi gani kwa kutoa mashine ambazo muuzaji wa bidhaa ama huduma anaamua aandike shilingi ngapi kwa mapatano na mnunuzi?
2. Huyu TRA hajaona huu ni udhaifu mkubwa unaotoa mwanya wa kukwepa mapato?
3. Ni technologia ngumu kiasi gani ambayo TRA hawajaweza kuwa nayo isaidie kuahakikisha hizi risiti za EFD zinabeba taarifa zote muhimu kama vile jina la bidhaa/huduma, kiasi kilichonunuliwa, bei ya kununulia na pesa iliyolipwa?
4. Hivi TRA wameona tarehe kutokea kwenye hii risiti ni bora kuliko taarifa muhimu za kusaidia kufuatilia kama kupata mlinganisho sawia?
KAMA KUNA MTU WA TRA HUMU TAFADHALI ANIJIBU MASWALI HAYA