Rishi Sunak: Waziri Mkuu tajiri kuliko Mfalme Charles III

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,375
8,113
Waziri Mkuu mpya wa 79 wa Uingereza, Rishi Sunak ametajwa kuwa na utajiri kuliko wa Mfalme Charles III.

Sunak na mkewe, Akshata Murty wanaelezwa kuwa na utajiri wa Pauni 730 milioni, ambao ni mara mbili ya utajiri wa Mfalme Charles III wa Pauni 370 milioni.

Utajiri wa Sunak umeelezwa umetokana na mali za mkewe, Akshata zilizotokana na hisa alizonazo kwenye kampuni ya baba yake ya IT Infosys alikopewa hisa asilimia 0.91 zenye thamani ya Pauni 727 milioni.

Akshata na mumewe, Sunak wana nyumba nne, ikiwa ni pamoja na mali ya Pauni milioni saba huko Kensington, moja kwenye Barabara ya Old Brompton ya London, jumba la kifahari la Pauni milioni 1.5 katika eneo Bunge la North Yorkshire, na jumba la Santa Monica huko California, Marekani linalokadiriwa kuwa na thamani ya Pauni 5.5 milioni, wakati Mfalme Charles anaishi kwenye kasiri ya kifalme. Baba mkwe wa Sunak, Narayana Murthy anatajwa ni ‘Bill Gates’ wa India ambaye hivi karibuni ameshika nafasi ya sita kwa matajiri wa India na 654 kwa matajiri duniani. Sunak na mkewe pia wana uwekezaji mwingine mkubwa waliofanya nchini Mauritius.

Kuna wakati Sunak aliwahi kutangaza hadharani kuwa usafiri wa familia ni gari aina ya Volkswagen Golf, hata hivyo, vyanzo vingine vilisema wanamiliki Range Rover, Lexus na BMW.

Mfalme Charles amerithi kasri zikiwamo za Balmoral na Sandringham. Pia, Mfalme Charles anamiliki gari aina ya Jaguar XJ, Range na Aston Martin DB6 volante.

Utajiri wa mkewe

Akshata mbali ya kuwa ni mwanamke tajiri kushinda Malkia, pia ni binti wa ‘Bill Gates’ wa India.

Ulipotajwa utajiri wa Akshata ulikuwa ni wakati wa utawala wa Malkia Elizabeth II, aliyefariki dunia Septemba 8, 2022.

Pia, Sunak na Akshata waliwahi kuwa na ‘Green card’ walipokuwa wakiishi na kufanya kazi Marekani.

Walikuwa na kadi za hadhi hiyo hata walipohamia Uingereza kabla ya Sunak kuchaguliwa kuwa mbunge wa Richmond (Yorkshire) mwaka 2015.

Akshata (42) ni binti wa bilionea wa India Narayana Murthy, mmoja wa wafanyabiashara maarufu aliyepewa jina la ‘Bill Gates’ wa India.

Kuna wakati Sunak aliitwa mbunge tajiri ndani ya Bunge la Uingereza, na siyo kwa kazi zake za awali kama ile ya ofisa wa benki, bali ni kutokana na utajiri wa kurithi wa mkewe, Akshata.

Baba mzazi wa Akshata, Murthy na mkewe Sudha ndio waanzilishi wa kampuni ya IT Infosys. Ana utajiri wa Pauni 3.45 bilioni.

Akshata anamiliki biashara zake mwenyewe, lakini pia ana hisa asilimia 0.91 kwenye kampuni ya Infosys ambayo ndiyo inayotengeneza sehemu kubwa ya mali zake.

Pia, ana akiba ya Pauni milioni 500, na kumfanya kuwa mwanamke tajiri zaidi Uingereza kuliko Malkia.

Kuhusu kodi

Kuna wakati Sunak alihojiwa na wanahabari kuhusiana na hadhi ya mkewe kulipa kodi na yeye alitetea.

Alisema: “Kila senti moja ambayo anapata nchini Uingereza hulipa ushuru, bila shaka analipa. Na kila senti ambayo anapata kimataifa, kwa mfano nchini India, angelipa ushuru kamili.

“Hivyo ndivyo mfumo unavyofanya kazi kwa watu kama yeye ambao ni wa kimataifa waliohamia hapa. Kumpaka matope mke wangu ili anione ni balaa. Anaipenda nchi yake kama mimi ninavyoipenda yangu,” alisema Sunak.

Kumiliki ‘green card’

Sky News iliwahi kuripoti kwamba Sunak aliendelea kushikilia kadi ya kijani kwa angalau mwaka hata baada ya kuchaguliwa kuwa Kansela mwaka 2020.

Wamiliki wa kadi za kijani wanatakiwa kulipa kodi ya Marekani kwa mapato yao ya kimataifa na pia kujitolea kisheria “kuifanya Marekani kuwa makao yako ya kudumu”.

Wanatakiwa kuwasilisha marejesho ya kodi ya kila mwaka ya Marekani, na wanawajibika kuripoti mapato yao na kulipa kodi kwa mapato yoyote ya kigeni. Sunak hata hivyo, aliwahi kukiri kumiliki kadi ya kijani wakati akiwa Kansela, lakini alisema aliirejesha.

“Chini ya sheria za Marekani, hauchukuliwi kuwa mkazi wa Marekani kwa kushikilia tu kadi ya kijani. Zaidi ya hayo, kwa mtazamo wa uhamiaji wa Marekani, inachukuliwa ni hali ya mkazi wa kudumu, inaachwa baada ya mhusika kutokuwepo kwa muda mrefu nchini humo,” aliwahi kukaririwa msemaji wa Sunak kuhusu umiliki wa kadi hizo.
 
Hivi wahindu ni polygamists? Najaribu kuwaza tu kama mkewe atamruhusu kuongeza mke taamaa zake zikimtuma hivyo! Au inambidi awe mpole tu ale mema ya nchi kimya kimya na kwa adabu bila kumuudhi tycoon mkewe.
 
Kwa data zako hizo manaake mfalume wa uingereza hana uwezo hata wa kununua kirabu ya mpira kama Chelsea ilio uzwa $4bn......hata huyu waziri mkuu team ya Newcastle ni tajiri kuliko yeye kama kweli utajili wake haufiki hata £1bn
Bbc kuna wakati habari zao huwa wanajikoroga sana.
 
Back
Top Bottom