Risasi zatembea, pesa zabebwa!

Maxence Melo

JF Founder
Feb 10, 2006
4,230
13,414
Ni dakika kama 10 zilizopita maeneo ya Pugu Road eneo la Jeti kwenye kona.

Kuna gari ndogo saloon type nyeusi imevamiwa na majambazi mchana huu na kupasuliwa vibaya vioo vyote huku ndani pakiachwa pametapakaa damu.

Kilikuwa kitendo cha haraka sana na risasi kama 6 hivi zimerindima.

Dereva kakimbizwa hospitali na furushi la hela ambayo inaelekea ilikuwa nyingi limebebwa na majambazi hapo hapo wakiwa na gari jeupe wametimka kuelekea maeneo ya TAZARA.

Zaidi tutafahamu kutoka kwa watu wengine ila tendo hili limefanyika mbele za macho yangu.

Mbaya zaidi watu wanaona balaa hili lakini wanakimbilia ndani ya gari kuangalia masalio ya hela badala ya kumwokoa dereva. Kweli wamefanikiwa kukuta fuko jingine na wahuni wakatokomea nalo mtaani.

Hatari!
 
Bongo imeanza kurudia tena ile hali ya 2004/5. Naona jamaa wajenga urafiki tena na makamanda wa Polisi. Kova ana kazi nzito.
 
Kuna kiwanda cha samaki eneo hili. Dereva alikuwa ni mhindi ametoka kiwandani kuelekea barabarani na amevamiwa baada ya kutoka kwenye geti la kiwanda hicho.

Alikuwa anavuja damu sana na amekimbizwa hospitali haraka
 
pole zao, ujambazi bado upo kumbe! huu ni wa kuotea au ni mchongo tu jamani.
 
Tatizo maisha ni magumu watu hawawezi hata kujikimu na mlo na wao wanaona mafurushi ya ela kila siku yanawapitia.
Mi nakwambia Huo ni ugaidi na mwanzo wa chuki mbaya.
Na majambazi wengi wamekuwa wakitumia mbinu za kijeshi...Wengi wao ni polisi ama wanajeshi na ama wakimbizi walio na uzoefu wa vita.
 
Polisi itoe ofa ya kusafirisha fedha kwa wanaohitaji kama kuelekea benki ama kupelekwa kwenye kampuni. Just Kampuni ipige simu kwenye idara maalum na kulipa kiasi fulani ili usalama wa fedha na wasindikizaji uwe salama.
 
duh.. Tanzania yetu hii! Ulifanikiwa kuona mwitikio wowote wa Polisi.. na kama Polisi wameshafika eneo la tukio (kama bado upo)
 
pole zao, ujambazi bado upo kumbe! huu ni wa kuotea au ni mchongo tu jamani.
Utakuwa mchongo tu, yani hawa jamaa (majambazi) walikuwa upande mwingine kama unaenda uwanja wa ndege lakini walikuwa wameegesha gari. Ghafla wakati hilo gari linatoka kiwandani wakachepuka upande wa pili na kulimiminia risasi mfululizo kisha kutoweka na kiroba kikubwa ambamo inadaiwa kulikuwa na pesa.

Kama si deal, basi ujambazi umerejea upya Dar. Mimi badala ya kukimbia nilibakia kuangalia nikiwa nimeduwaa...
 
pole, maana matukio mengine hasa kama hili sio la kushuhudia!
 
duh.. Tanzania yetu hii! Ulifanikiwa kuona mwitikio wowote wa Polisi.. na kama Polisi wameshafika eneo la tukio (kama bado upo)
YES,

Kuna polisi wamefika dakika kama 13 baada ya tukio toka kituo cha Airport. Ni eneo ambapo nilikuwa nimesimama nikijaribu kutafakari jambo, lakini baada ya hapo hata jambo lenyewe nikalisahau.

Mara ya kwanza naona jambo kama hili. Inatisha, mpaka naziogopa hela
 
pole zao, ujambazi bado upo kumbe! huu ni wa kuotea au ni mchongo tu jamani.

Ujambazi umerudi kwa kasi..nadhani hata jana usiku mawakili na Mkuu wa Kitengo cha Sheria UDSM wamevamiwa na armed thugs wakaibiwa pesa na simu
 
Ujambazi umerudi kwa kasi..nadhani hata jana usiku mawakili na Mkuu wa Kitengo cha Sheria UDSM wamevamiwa na armed thugs wakaibiwa pesa na simu
Basi kwa maelezo haya napata picha kuwa tunaelekea pabaya zaidi. Something must be done immediately!
 
Pole w0rM, hope ur nt goin to get nightmares, mimi pia nk karibu na eneo hilo, hopeful i wil get more info later, lakini kwanini mtu usafirishe pesa bila ulinzi wowote, mi nishashuhudia wafanyabiashara wa kihindi wanavyoleta miburungutu ya pesa benki bila ulinzi wowote.
 
hii nimchongo mtu huwezi eti subiri tu gari itoke ukalivamie si wangejikuta wanaishia na mapanki!!!
lazima wahusika wanatoka ndani ya kiwanda tu period.
 
Utakuwa mchongo tu, yani hawa jamaa (majambazi) walikuwa upande mwingine kama unaenda uwanja wa ndege lakini walikuwa wameegesha gari. Ghafla wakati hilo gari linatoka kiwandani wakachepuka upande wa pili na kulimiminia risasi mfululizo kisha kutoweka na kiroba kikubwa ambamo inadaiwa kulikuwa na pesa.

Kama si deal, basi ujambazi umerejea upya Dar. Mimi badala ya kukimbia nilibakia kuangalia nikiwa nimeduwaa...

Hii nadhani ni deal kwa kuwa watajuaje kuna mafuko ya pesa ya ndani ya gari?inaonekana walichora mtego siku nyingi.Mungu amsaidie dereva apone haraka majeraha yake
 
Ujambazi umerudi kwa kasi..nadhani hata jana usiku mawakili na Mkuu wa Kitengo cha Sheria UDSM wamevamiwa na armed thugs wakaibiwa pesa na simu

Duh, Jamaa walinyamaza ili kutunga mbinu mpya. Sasa wameibuka tena, hivi ujambazi ni profession au unasababishwa na uvivu au tamaa ya kupata bila kuvuja jasho?
 
Pole kwa wale waliopatwa na masahibu haya.

lakini kwa nini watu wasitumie mgari yale ya kusafirisha fedha nina hakika sio bei ghali na hata kama hao wa magari watachonga plan ni bora kuliko kupoteza maisha just for money. na kama mtu anaweza kuwa na mafurushi makubwa ya hela am sure they can afford to hire these vehicles
 
Duh, Jamaa walinyamaza ili kutunga mbinu mpya. Sasa wameibuka tena, hivi ujambazi ni professional au unasababishwa na uvivu au tamaa ya kupata bila kuvuja jasho?
unachangiwa na vitu vingi ila zaidi ni uvivu wa kufikiri, manake si kweli kwamba hawavuji jasho, kwahiyo physically si wavivu ila mentally ni wavivu, kwani na wao hujiangaisha ati, wakikimbizana na kupora watu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom