Maxence Melo
JF Founder
- Feb 10, 2006
- 4,167
- 12,868
Ni dakika kama 10 zilizopita maeneo ya Pugu Road eneo la Jeti kwenye kona.
Kuna gari ndogo saloon type nyeusi imevamiwa na majambazi mchana huu na kupasuliwa vibaya vioo vyote huku ndani pakiachwa pametapakaa damu.
Kilikuwa kitendo cha haraka sana na risasi kama 6 hivi zimerindima.
Dereva kakimbizwa hospitali na furushi la hela ambayo inaelekea ilikuwa nyingi limebebwa na majambazi hapo hapo wakiwa na gari jeupe wametimka kuelekea maeneo ya TAZARA.
Zaidi tutafahamu kutoka kwa watu wengine ila tendo hili limefanyika mbele za macho yangu.
Mbaya zaidi watu wanaona balaa hili lakini wanakimbilia ndani ya gari kuangalia masalio ya hela badala ya kumwokoa dereva. Kweli wamefanikiwa kukuta fuko jingine na wahuni wakatokomea nalo mtaani.
Hatari!