Risasi zasikika baada ya mwanamke mwengine mweusi kuuawa na polisi akiwa nyumbani kwake

Status
Not open for further replies.

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,566
Risasi zarindima Kentucky, US baada ya mwanamke mweusi kuuawa na polisi nyumbani

Risasi zarindima Kentucky, US baada ya mwanamke mweusi kuuawa na polisi nyumbani
Maaandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi yameshika kasi nchini Marekani baada ya polisi mzungu kumuua kwa kumpiga risasi mwanamke mweusi akiwa nyumbani kwake katika jimbo la Kentucky.

Milio ya risasi imesikika katika maandamano hayo yaliyozuka baada ya polisi wa Marekani kumuua mwanamke huyo mwenye asili ya Afrika, kwa jina la Breonna Taylor, akiwa ndani ya nyumba yake.

Mauaji hayo yamefanyika huku maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi nchini Marekani yakiendelea kushuhudiwa katika kona mbali mbali za nchi hiyo.

Mauaji ya mwanamke huyo wa Marekani mwenye asili ya Afrika yamechochea zaidi maandamano na ghasia za kupinga ubaguzi na ukatili wa polisi nchini Marekani zilizoanza baada ya polisi mwingine mzungu kumuua Mmarekani mweusi, George Floyd katika mji wa Minneapolisi jimboni Minnesota tarehe 25 Mei.

Siku chache baadaye, Rayshard Brooks, Mmarekani mwingine mweusi aliuawa kwa kupigwa risasi na polisi mzungu huko Atlanta.

Mauaji ya kikatili ya Floyd yaliyozusha maandamano ya kupinga ubaguzi Marekani
Makundi ya kiraia na mashirika ya kutetea haki za binadamu yamesema Wamarekani hawataacha maandamano na malalamiko yao hadi pale kilio chao kitakaposikilizwa na matakwa yao ya kufanyika marekebisho katika ngazi zote za jeshi la polisi yatakapotekelezwa.

Mbali na Marekani, maandamano hayo ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi yameshuhudiwa pia katika nchi mbali mbali duniani hususan za Ulaya.

4bva62dd97684c1nxjt_800C450.jpg

====
FACT CHECK: Tukio hili lilitokea 20/03/2020
 
Milio ya risasi imesikika katika maandamano hayo yaliyozuka baada ya polisi wa Marekani kumuua mwanamke huyo mwenye asili ya Afrika, kwa jina la Breonna Taylor, akiwa ndani ya nyumba yake.

Mauaji hayo yamefanyika huku maandamano ya kupinga ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi nchini Marekani yakiendelea kushuhudiwa katika kona mbali mbali za nchi hiyo.
Breonna Taylor aliuawa kabla ya George Floyd!
 
Hii habari haijakamilika kabisa. Polisi walienda hapo kwake kufanya nini?
 
Status
Not open for further replies.
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom