Risasi Zarindima Mwanza, 10 Wauwawa, 17 Wajeruhiwa, Majambazi 6 nayo yauwawa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Risasi Zarindima Mwanza, 10 Wauwawa, 17 Wajeruhiwa, Majambazi 6 nayo yauwawa.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pascal Mayalla, Jan 17, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Jan 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Kuna habari za kurindima kwa risasi mjini Mwanza ambapo watu 10 wameuwawa na majambazi, 17 Wajeruhiwa, Majambazi 6 nayo yauwawa na wananchi wenye hasira.
  habari hizi ni kwa mijibu wa 7:00 pm news ya Ch.10.

  Wenzetu wa Mwanza, tujulisheni zaidi
  Update 1.
  Waliokufa wafikia 14. Wengine wawili wamefariki wakiwa njia kupelekwa Hospital, na wawili zaidi wameuwawa kijijini.
  BBC Swahili imemkariri Kamanda polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow asubuhi hii amesema majeruhi 6 wamehamishiwa hospitali ya Bugando kwa helcopter ya polisi, wengine 11 bado wamelazwa hospitali ya wilaya ya Ukerewe.

  Update 2.

  Akizungumza asubuhi hii kwenye kipindi cha Nipashe cha Radio One akiwa bado Nansio Ukerewe, Kamanda Rwambo amefafanua, watu 7 walifariki on the spot, watatu kati yao ni majambazi.Baadhi ya washirika wa majambazi hao, wametiwa nguvuni.

  Naye Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongela, amesema ameshitushwa na tukio hilo, na leo atatarejea jimboni kwake Ukerewe kushirikiana na wapiga kura wake kwenye majonzi makubwa haya.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jan 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,611
  Trophy Points: 280
  Sunday January 17, 2010 Sunday News
  14 killed in Izinga island raid
  [​IMG]
  Map of

  ROSE ATHUMANI, 17th January 2010 @ 11:48,

  ARMED robbers shot and killed 14 people and fatally injured 17 others, in an attempted robbery in Izinga island in Ukerewe district, Mwanza region.

  Speaking to the 'Daily News' on his way to the scene of incident, Mwanza Regional Police Commander (RPC), Jamal Rwambow, said there was an attempted robbery yesterday night, that was foiled by the public before the shooting started.

  "There was an attempted robbery and the public foiled it when the robbers decided to open fire, killing 14 people and injuring the others," RPC Rwambow said.

  Several suspects have been apprehended, but RPC Rwambow could not divulge more details for security reasons.

  "We have suspects in custody but we cannot give more details on that for security reasons," he explained.

  The Mwanza RPC said six out of the seventeen injured have been air-lifted by police helicopter to Bugando hospital in Mwanza.

  The remaining 11 were receiving treatment at the Ukerewe District Hospital, RPC Rwambow said.

  It was not clear, however, what the suspects were trying to steal. Ukerewe Member of Parliament, Ms Getrude Mongella, said she was shocked by the news and she would be travelling to Izinga today.
   
 3. O

  Ogah JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Mkuu Bob salama huko lakini?........please say/write something please!
   
 4. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Thanks for this.
   
 5. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #5
  Jan 18, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Mauaji ya kutisha Mwanza
  Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 17th January 2010 @ 23:59 Imesomwa na watu: 155; Jumla ya maoni: 0

  WATU 14 akiwamo jambazi mmoja wameuawa katika shambulio la kutupiana risasi kati ya majambazi na wananchi usiku wa kuamkia jana katika kisiwa kidogo cha Izinga kilichoko wilayani Ukerewe Mkoa wa Mwanza.

  Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Jamal Rwambow alilithibitishia gazeti hili kwa simu jana jioni muda mfupi baada ya kutua Mwanza akitokea Ukerewe kwamba kulikuwa na vifo 14 na majeruhi 17.

  Kamanda Rwambow alisema kati ya waliokufa, mmoja ni jambazi na mwingine ambaye ni majeruhi, wanachunguza ushiriki wake katika tukio la uvamizi kwenye nyumba mbili za kulala wageni kisiwani Izinga, ambalo ndilo lililosababisha mauaji hayo ya kutisha mwanzoni mwa mwaka huu.

  Alisema kati ya majeruhi hao 17, sita wamehamishiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa ajili ya matibabu zaidi baada ya hali zao kuwa mbaya, wakati wengine 11 wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe mjini Nansio.

  Kamanda Rwambow hata hivyo hakuweza kutaja majina ya waliokufa na wale waliolazwa kwa matibabu, ingawa alisema tayari maiti tisa wametambuliwa wakati maiti wengine watano hawajatambuliwa.

  "Tukio hilo limetokea saa nane na saa tisa usiku wa kuamkia leo (jana) kwenye kisiwa kidogo cha Izinga wilayani Ukerewe, baada ya watu wanaodaiwa kuwa majambazi kuvamia guest house (nyumba za kulala wageni) mbili.

  "Inaaminika wakati huu ni msimu wa mavuno ya dagaa, kwa hiyo baada ya wananchi kugundua uvamizi huo, walijikusanya na kuzingira watu hao kwa nia ya kuwadhibiti, lakini majambazi hao walipogundua hilo, walifyatua risasi na kuwajeruhi watu hao na vifo kutokea," alisema Kamanda Rwambow.

  "Kwa hiyo, tunaendelea na uchunguzi na sasa tunamchunguza mmoja wa majeruhi wa tukio hilo tukimhusisha na majambazi hao," alifafanua Kamanda Rwambow.

  Naye Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mwalimu Queen Mlozi, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa manane kuamkia jana, na kama alivyoeleza Kamanda wa Polisi wa Mkoa, alisema watu hao walifika kisiwani huko na mtumbwi, na kwamba wananchi waliwazingira eneo la ziwani ili wasiondoke.

  "Unajua walikuja na mtumbwi, sasa walipobanwa, walikimbilia kwenye mtumbwi wao ili waondoke, na mwenzao mmoja alikuwa akiwapigia simu wawahi kupanda, ndipo walipoona hali ni mbaya, walifyatua risasi na kuwaua watu hao…kwa kweli hali ni ya kusikitisha," alisema DC Mlozi kwa simu jana jioni na kuongeza:

  "Lakini naushukuru uongozi wa Mkoa, umefika hapa na kusaidiana nasi…namshukuru Rais Kikwete kwa kutupa faraja na kutusaidia…majeruhi wetu wanaendelea vizuri ingawa sita wamepelekwa Bugando kwa sababu hali zao sio nzuri. Nawashukuru madaktari wa wilaya na polisi wetu wa wilaya."

  DC Mlozi alisema kutokana na hali ilivyokuwa jana, leo ndio watakwenda katika eneo la tukio ingawa tayari polisi wamekwisha kwenda huko na pia viongozi wa mikoa ya jirani wamearifiwa ili kuhakikisha wanadhibiti watu wote watakaotiwa shaka wakihusishwa na tukio hilo.
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  Tukio hili linauzunisha sana
  tutaendelea na mauaji ya namna hii mpaka lini jamani
  Mungu awape faraja wote waliopatwa na mkasa huu pia awafariji ndugu na jamaa wa marehemu wote
   
 7. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #7
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Haya matukio yamezidi sana tunaomba polisi waimarishe ulinzi kila sehemu ya nchi! Usikute hii midubwana (mijambazi) imetoka nchi za jirani
   
 8. O

  Omumura JF-Expert Member

  #8
  Jan 18, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Mwaka huu kweli kazi ipo, eti mbunge Gertrude mongela ataahirisha kikao chenye mahela leo ili aende ukerewe kwa wapiga kura wake, ama kweli na akifika tu wote anawaamkia shikamooni!
   
 9. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #9
  Jan 18, 2010
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  [FONT=&quot]Date::1/18/2010 [/FONT]
  [FONT=&quot]Majambazi wacharuka, waua watu 14 Ukerewe, waliteka kisiwa [/FONT]
  [FONT=&quot]
  [/FONT]​
  [FONT=&quot]Na Waandishi wa Mwananchi, Mwanza.[/FONT]
  [FONT=&quot]WIMBI la ujambazi linazidi kutikisa nchi baada ya watu 14 kuuawa na wengine 17 kujeruhiwa kwa risasi katika shambulio lililofanywa na kundi la majambazi kwenye kisiwa kidogo cha Izinga kilicho wilayani Ukerewe na wengine 17 kujeruhiwa kwa risasi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika salamu zake za Mwaka Mpya, Rais Jakaya Kikwete alilipongeza Jeshi la Polisi kwa kufanikiwa kupunguza wimbi la ujambazi, lakini siku chache baadaye kuliripotiwa matukio makubwa ya ujambazi, likiwemo la mkoani Ruvuma ambako askari polisi walinusurika kuuawa baada ya kushambuliwa na majambazi na kuporwa bunduki mbili.[/FONT]
  [FONT=&quot]Tukio jingine lilitokea mkoani Mwanza ambako jambazi mmoja aliuawa wakati polisi wakirushiana risasi na kundi la majambazi katika jaribio la uporaji kwenye mgahawa wa UTurn.[/FONT]
  [FONT=&quot]Hali imekuwa mbaya zaidi kwenye kisiwa cha Izinga kilicho Ziwa Victoria ambako majambazi hao walivamia majira ya saa 9:25 usiku.[/FONT]
  [FONT=&quot]Watu walioshuhudia tukio hilo waliiambia Mwananchi kuwa umati wa watu ulijitokeza kujaribu kupambana na majambazi hao baada ya kusikia kelele za kuomba msaada.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mashuhuda hao walisema baada ya wananchi kujitokeza, mmoja wa majambazi hao aliwafyutulia risasi na kasababisha majeruhi na vifo vya watu hao.[/FONT]
  [FONT=&quot]Waliongeza kuwa awali waliposikia mlio wa bunduki, walidhani ni baruti, lakini baada ya kelele hizo walijikusanya kwa ajili ya kuwakabili na wananchi wengine walienda kujaribu kuharibu mtumbwi wao ili wasiutumie kutoroka, ndipo majambazi hao wakamimina risasi na kuua watu zaidi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Walidai kuwa kundi la majambazi hao lilivamia kisiwa hicho usiku likitumia mitumbwi miwili ya injini, lakini wananchi walibaini kuingia kwao na kuwazingira. Baada ya kubaini kuwa wamezingira, walianza kufyatua risasi na kusababisha vifo vya wananchi saba.[/FONT]
  [FONT=&quot]Katika mashambulizi hayo wavamizi hao waliweza kujeruhi watu wengine 17 na wao wananchi kufanikiwa kuwaua wavamizi hao wawili.[/FONT]
  [FONT=&quot]Akizungumzia tukio hilo, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ukerewe, Queen Mwashinga Mlozi alisema kati ya watu hao waliokufa wawili wanasadikiwa kuwa ni majambazi.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mlozi ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Ukerewe alisema tayari taarifa ya tukio hilo ameifikisha kwa uongozi wa mkoa na kuongeza kuwa mkuu wa mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama walifika eneo la tukio ili kupata taarifa zaidi za tukio hilo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kaimu Mganga Mkuu wa wilaya ya Ukerewe, Dk Faustine Nkinga alisema hali za majeruhi bado ni mbaya na kwamba wanaendelea na kazi ya kunusuru maisha yao kwa sababu kati yao wanne walipoteza damu nyingi na wengine walifanyiwa upasuaji ili kuwaondoa risasi kwenye miili yao na wengine wamehamishiwa Hospitali ya Bugando.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mkuu wa mkoa, Abbas Kandoro, ofisa usalama wa mkoa, Jason Mutashongerwa na kamanda wa polisi mkoa, Jamal Rwambow waliondoka asubuhi jana kwenda eneo la tukio kujionea hali halisi ya uvamizi huo.[/FONT]
  [FONT=&quot]Kandoro alisema kuwa majeruhi wote 17 walihamishiwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando kwa ajili ya matibabu zaidi kutokana na hospitali ya Ukerewe kutomudu kuwahudumia wagonjwa hao.[/FONT]
  [FONT=&quot]Naye Kamanda Rwambow alisema kuwa watu waliothibitika kuuawa eneo la tukio kisiwani humo ni saba na watu wengine watano ambao walipelekwa wakiwa majeruhi kutibiwa walifariki wakati wakitibiwa. Habari zilizofika baadaye zilieleza kuwa watu wengine watatu walipoteza maisha.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Mpaka sasa niko na viongozi wengine wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa tukielekea eneo la tukio, lakini ninachoweza kukueleza ni kuwa tukio lipo na watu wamekufa na kati ya hao waliokufa wawili ni majambazi ambao waliuawa na wananchi. [/FONT]
  [FONT=&quot]Lakini taarifa kamili nitatoa baada ya uchunguzi kamili na kufika eneo la tukio," alieleza Kamanda Rwanbow kwa njia ya simu.[/FONT]
  [FONT=&quot]Mbunge wa Ukerewe, Getrude Mongella alisema kuwa Jeshi la Polisi linastahili lawama kutokana na tukio hilo kwa sababu wananchi wa visiwa vya wilayani Ukerewe walichanga Sh3 milioni ili wajengewe kituo, lakini hadi leo jeshi hilo limeshindwa kutoa maelekezo ya kufanikisha nia hiyo.[/FONT]
  [FONT=&quot]"Nimesikitishwa na tukio hili, lakini jeshi la polisi linastahili lawama kutokana na kuzembea kutoa maelekezo kwa wananchi ambao tayari wamechanga Sh3 milioni za kujengea vituo vya polisi katika visiwa vya uvuvi," alieleza Mongella.[/FONT]
  [FONT=&quot]Tukio hili linaufanya mkoa wa Mwanza kuwa miongoni mwa mikoa inayoongoza kwa matukio ya ujambazi. Wananchi wamekuwa wakivamia kila mara na kujeruhiwa kwa mapanga, nondo na silaha za moto na kuporwa mali na fedha.[/FONT]
  [FONT=&quot]Julai mwaka jana watu wanaosadikiwa kuwa majambazi walivamia na kuteka Kisiwa cha Ziragula na kujeruhi wananchi zaidi ya 13 na kupora mali na fedha. [/FONT]
  [FONT=&quot]Januari 14 mwaka huu majambazi pia walivamia eneo la uvuvi la Igombe na kupora Sh700,000 na kujeruhi wananchi watatu.[/FONT]
   
 10. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #10
  Jan 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Dah,wameona dar kimeo wanakimbilia mikoani.

  "Uhalifu haulipi"-Kamanda Kova
   
 11. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #11
  Jan 18, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,793
  Trophy Points: 280
  Sijawahi kusikia mauaji ya magnitude hii ndani ya eneo dogo Tanzania kama Ukerewe?!Kuna nini cha kuiba kwa hasira namna hiyo kule visiwani? Au ndio ile culture ya watu wachache kuua wenzao kama hawastaili kuishi maana hilo nalo ni tatizo kubwa lake Zone
   
 12. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #12
  Jan 18, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa namna yoyote ile mauaji kama haya hayakubaliki. Ila kuna kitu tunaki-miss hapa. Nacho ni kwa nini watu wanakuwa vibaka aua wahalifu?. Tunapoongelea amani na utulivu tunaongelea kwa waliopo kwenye nafasi nzuri za kujipatia mkate wao wa kila siku, Kama watu wapo tayari kufa ili kupora au kuzuia wasiporwe ujue hali si nzuri. Mwalimu aliisha wahi kusema kuwa "adui mbaya kabisa wa amani ni wananchi kukata tamaa ya kuishi" nayo hutokana na umasikini, ujinga na maradhi.

  Umefikia wakati sasa Serikali ijikite kwenye kuendeleza ajira kwa vijana na kukuza uchumi badala ya kujinufaisha watu wachache. Mambo ya mwenzetu tumpe cheo yaishe tuangalie wajasiriamali watakaokuwa na vision ya kuanzisha njia za kukuza ajira endelevu. Tuangalie utanzania sasa badala ya U-CCM katika kuteua watendaji wenye forward looking vision. Ni matumaini yangu kuwa uchaguzi huu wa 2010 utakuwa na agenda ya kuendeleza nchi zaidi ya masilahi ya kundi fulani. Vinginevyo tutarajie mauji mengi kama haya siku zijazo.
   
 13. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #13
  Jan 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  [/FONT]

  I hate politicians because of their hypocrisy. Huyu alikuwa wapi kufutilia ujenzi wa hicho kituo kabla yatukio hili??
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Hofstede, watu waliokata tamaa wako tayari kufanya chochote. Mapinduzi ya Bolshevick huko Urusi ya October 1917, wananchi masikini wa Urusi walikata tamaa kufuati gap kubwa kati ya wenye nacho na wasionacho, V.I.Lenin aliyekuwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi, aliwaorganize wafanyakazi walio wengi, kuwatimua matajiri wakati huo wakiitwa Craz, na kuitwaa ikulu ya nchi hiyo.

  Hapa nchini hii gap ya wenyenacho na wasionacho, inazidi kukua siku hadi siku, Waswahili Kariakoo wanahamishwa na kuingia matajiri, safari sasa inaelekea Ilala na Magomeni, vile vijumba vya mabati ya madebe vimeyeyuka na kuingia maghorofa ya haja.

  Atajatokea Lenin wa Kitanzania kuwaorganize walio wengi kuwa nchi hii ni mali yao, walioko ikulu yao wameuza nchi yao kwa wageni. Masikini hawa wakimarch hata bila silaha yoyote kuelekea Magogoni, patakuwa hapatoshi, wale wa maghorofani, watatunguliwa huku huko kama popo.

  Tunashukuru Mungu, Watanzania ni wapole, wapenda amani na utulivu, vitendo kama hivi vya ujambazi wa kutumia nguvu ni bad indicator kuwa things are not the same, sasa siku wapole hawa wakisema basi, imetosha na wakicharuka...patakuwa hapatoshi!.
   
Loading...