Risasi zarindima mtaa wa swahili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Risasi zarindima mtaa wa swahili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kisale, May 8, 2009.

 1. kisale

  kisale Senior Member

  #1
  May 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  HABARI TOKA MTAA WA MSIMBAZI JIJINI DAR SASA HIVI ZINASEMA KUNA MAPAMBANO MAKALI KATI YA POLISI NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI.
  wadau mliopo karibu na maeneo hayo tunaomba ripoti.
   
 2. kisale

  kisale Senior Member

  #2
  May 8, 2009
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 111
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Taarifa za hivi Punde zinadai mapambano yamemalizika na Polisi wamefanikiwa kuyatia nguvuni majambazi matano.matatu yamejeruhiwa vibaya sana.
   
 3. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #3
  May 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  jamani, wizi asubuhi asubuhi namna hii, Mungu tu ajalie wasiuliwe raia wasio na hatia kwani msongamano uliopo kariakoo mhh..
   
 4. Brooklyn

  Brooklyn JF-Expert Member

  #4
  May 8, 2009
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 1,453
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Jamani mbona kuna mdau amenipigia simu sasa hivi anasema mitaa yote ya kuingia kkoo imefungwa??? Sijui kama ka mradi kangu kamepona pale mtaa wa Nyarung'ombe!! Najaribu kuwatafuta wasaidizi wangu pale kkoo siwapati!!
   
 5. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #5
  May 8, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wamesema kova atatoa taarifa baadaye leo mchana
   
 6. Kinyau

  Kinyau JF-Expert Member

  #6
  May 8, 2009
  Joined: Nov 24, 2006
  Messages: 793
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 60
  tetesi zasema majambazi hawa walijaribu kupora Bereau de change moja karibu na nbc msimbazi. Polisi wamejitahidi sana kuwadhibiti na wamekamatwa.

  Lets wait for more updates.
   
 7. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #7
  May 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  inatisha kweli kweli
   
 8. J

  Jafar JF-Expert Member

  #8
  May 8, 2009
  Joined: Nov 3, 2006
  Messages: 1,138
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Naona leo ndio ilikuwa 40 zao.
   
 9. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #9
  May 8, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mbona hizi taarifa zinakuja in pieces? hakuna mtu mwenye data zilizokamilika wakuu......?
   
 10. DDT

  DDT Member

  #10
  May 8, 2009
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Next Level
  Si unajua tena, breaking news lazima ziji break into pieces? Natania tu
  Ila Tanzania tukicheza mambo yatakuwa mabaya zaidi, majambazi yanajijenga upya kwa ari, kasi na nguvu mpya
   
 11. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #11
  May 8, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  inabidi tuombee majeruhi wapone waweze kubana wawataje wenzao ktk mtandao...
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  May 8, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Polisi wakiamua kufanya kazi ya ukweli na ya kuaminika wanaifanya bila shida...
  Ishu kama hiyo imo ndani kabisa ya uwezo wao..... Tunawaaminia na kuwasupport.

  Taarifa kuja into pieces usiogope bwana NEXT LEVEL... kAMA ulivyosoma hapo, Kova atatupa full scandal badae.....Tulia
   
 13. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #13
  May 8, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Tuwapongeze vijana wetu polisi waliokuwa doria huko na kufanya kweli. Pia msamaria mwema aliyetia taarifa hizi maana mipango kama hiyo huwa inapangwa kwa muda, hivyo pia tumshukuru aliyezivujisha habari za mipango hiyo. Pia hii ni changamoto kwa Jeshi lote la polisi maana ujambazi umeanza kuibuka tena kwa kasi baada ya kutulia kwa kiasi mpaka wengine tumepata usingizi majumbani mwetu. Usingizi wetu huu usiwakumbe jeshi la polisi maana kila kukicha majambazi wanapanga mbinu mpya za ujambazi!! Kova please, jitahidi!! na tuko nyuma yako.

  Kwa sasa ujambazi umeanza kwa kasi Dar na Arusha!!
   
 14. M

  Msindima JF-Expert Member

  #14
  May 8, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Big up jeshi la Police.
   
 15. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #15
  May 8, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Ni kweli polisi wakiamua kazi wanaifanya vizuri hasa pale majambazi hao wanafanikiwa mara ya kwanza na badala ya kukata fungu kama walivyoahidiana wanayeyusha na kusema hawakupiga nyingi. Next time polisi wanakuwa na kisasi nao na kuamua kulipiza kisasi cha kunyimwa mgao wa mwanzo.

  Walininikamata hawa wenye difenda one day, na kutaka niwape laki tano kwa bahati nzuri akapita afande mmoja ananijua, akaniambia hao jamaa ni wabaya wanavisasi niwape hata hela ya soda vinginevyo wanaweza hata kunishambulia siku ingine kwa risasi wakiniita jambazi. Yaani hakuna kosa lolote zaidi ya kuendeshwa na mtu aliye na leseni changa gari ikatuzimikia barabarani si unajua manual, wakang'ang'ani tunafudishana, hawakutaka kuona leseni wala nini, ukawa ubishi mkubwa ila sikuwapa hata shillingi maana ilibidi watupeleke kituoni.

  Credit kwa baadhi:
  kuna baadhi ya polisi wazuri na wachapa kazi hasa na waaminifu ila wanavunjwa nguvu na wenzao wachache na maslahi duni wanayolipwa wakati wakiwaona wenzao wasio waaminifu wanajenga mahekalu na kununua magari ya kifahari kwa kushirikiana na majambazi.
   
 16. Babylon

  Babylon JF-Expert Member

  #16
  May 8, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 1,338
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Ni mambo ya kawaida hayo Hapa jijini DAr
   
 17. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #17
  May 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,187
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Hizi tetesi bwana.....
  Ngoja nisubiri taarifa kamili maana unaweza kuta sio majambazi yakawa kama mambo yanayomuandama Zombe!
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  May 8, 2009
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,319
  Likes Received: 22,164
  Trophy Points: 280
  Raia mwema mmoja aliyeiacha chai yake kwenda kuangalia risasi ameambulia hali ya u nusu mauti baada ya kuchabangwa risasi ya mbavuni.
  Amekimbizwa muhimbili ili kujaribu kuiunganisha roho yake na mwili, maana inaweeza kukatika kutoka mwilini muda wowote maana alikuwa ana breed sana.
   
 19. Himawari

  Himawari JF-Expert Member

  #19
  May 8, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 2,187
  Likes Received: 681
  Trophy Points: 280
  Mkuu zingatia matumizi ya r na l vinginevyo neno linapoteza maana halisi.
  Breed=Bleed?!
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  May 8, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Inajulikana wazi kuwa Kova ana usongo na majambazi na aliahidi mwanzoni kuwa ama zao ama zake na ndio tunaona juhudi zake kuwa,kila wanapokutana face to face watamkamata japo mmoja.
   
Loading...