Risasi mwaulanga kuongoza matembezi ya vijana 100 dar mpaka Moro

King Kong III

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
51,632
68,560
Balozi wa amani(Nd. Risasi Mwaulanga) kushirikiana na zitto kabwe wanatarajia kufanya matembezi kutoka dar mpaka moro kwa miguu,lengo ni kuhamasisha vijana wajikite kwenye kilimo,anasema tanzania ukimwita mtu mkulima ni kama unamkashifu wkt usa ukimwita mtu mkulima yani ni sifa kubwa sawa na kumlinganisha na 50 cent


Source:Times FM

Huyu Jamaa kaitwa kuzungumzia kilimo lakini anampigia promo jakaya
 
Mi nadhani badala ya kufanya matembezi ya Dar-Moro basi wangejikita kwanza kutafuta soko la mazao yanayozalishwa hapa Tanzania.
Kwa hali ilivyo sasa vijana na watu wengine hawahamasiki kulima kwasababu, baada ya kutoa jasho na kuangaika juani huku ukilima, mwisho serikali inakupangia bei au wafanya biashara wanakupangia bei ya kununua mazao yako. Mkulima anazuiwa asiuze nje hata kama kuna soko zuri, kwa nini? Tafakari chukua hatua. Tafuteni soko, ruhusuni watu walime na kuuza wanapotaka uone watu watakavyojikita kwenye kilimo.
Hii dhana ya kutueleza kuwa wakiruhusiwa watauza chakula chote then tubaki na njaa sioni kama ina mashiko.
 
Back
Top Bottom