Risala ya kamati ya wanafunzi wa kamati ya vyuo vikuu na taasisi ya elimu ya juu

aleesha

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
776
1,121
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Mh. Maalim Seif Sharif Hamad,
Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, Mh. Nassor Ahmed Mazrui,
Mheshimiwa Makamo Mwenyekiti Mstaafu, Mh. Juma Duni Hajji,
Waheshimiwa Wakurugenzi wa Chama cha Wananchi CUF,
Waheshimiwa Viongozi wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa,
Waheshimiwa Wabunge,
Waheshimiwa Wawakilishi,
Waheshimiwa Viongozi wa Jumuiya zote za Chama cha Wananchi CUF,
Waheshimiwa Viongozi wa Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu,
Waheshimiwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu muliohudhuria hafla hii,
Waheshimiwa Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Assalaam alaykum.
Mh.Mgeni Rasmi,

Awali ya yote tunamshukuru M/Mungu kwa kutujaalia siku hii ya leo kuweza kukutana hapa katika muendelezo wa harakati za kulikwamua taifa letu tukiwa katika hali ya uzima wa Afya na wale wanaosumbuliwa na maradhi tunawaombea kwa M/Mungu awajaalie shufaa.

Shukrani zetu za kipekee na za dhati kabisa ziende kwako kwa kuacha majukumu yako yote na kuja kuungana nasi katika shuguli hii muhimu, pia tunakushukuru na kukupongeza wewe na Viongozi wenzako kwa kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ya Wazanzibari.

Mheshimiwa Mgeni Rasmi na wote mliohudhuria hafla hii,
Kwa niaba ya Kurugenzi na Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Zanzibar iliyo chini ya JUVICUF - Taifa, tunayo heshima na furaha kubwa kukukaribisheni ili mushiriki nasi katika hafla hii muhimu na ya kihistoria ya muendelezo wa harakati za kutetea haki zetu za msingi chini ya Chama cha Wananchi CUF.

Mh. Mgeni Rasmi,
Hafla hii iliyoandaliwa na Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu imetokana na ziara ya miezi mitatu nyuma ambapo Kamati ilianza kumtembelea Mh. Juma Duni Haji, Mzee Ali Haji Pandu, Mzee Machano Khamis Ali,Mh. Salim Bimani na leo tunamalizia kwako wewe Katibu Mkuu. Lengo la kuwatembelea Viongozi hao ni kutaka kufahamu maisha yao katika harakati za kupigania haki sawa kwa Wote ndani ya Chama cha Wananchi CUF, Changamoto walizokumbana nazo, mafaniko na hatima ya haki yetu.

Mh. Mgeni Rasmi,
Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu iliyo chini ya JUVICUF - Taifa ilianzishwa rasmi December 10, 2011 na Viongozi Watangulizi wa JUVICUF – Taifa ambao kwa wakati huo walikua ni Mh. Yussuf Kaiza Makame (mbunge wa chakechake), Mh. Pavu Abdalla (Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu), Hafidh Ali Hafidh (Afisa wa kitengo cha Mafuzo na Utafiti cha kamati), Biubwa Mselem, Juma Gora, Suleiman Salim na Khalifa Abdalla Ali (Mwakilishi wa Wawi). Kamati hii ilikuwa chini ya ulezi wa Mh. Salim Bimani (Mkurugenzi wa Habari).

Mh. Mgeni Rasmi,
Kamati hii ilitekeleza majukumu mbali mbali ya kichama katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa October 2015 kama vile; kushiriki katika mchakato wa kutafuta na kuhakiki wadhamini wa Mgombea Uraisi wa mwaka 2015 Mh. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhamasisha Vijana wa Vyuo kwenda kupiga kura katika maeneo yao hasa wakaazi wa Pemba, kuhamasisha Vijana wa Vyuo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwenye maeneo ya karibu ya Vyuo vyao kwa wale Wanaoishi katika Madahalia kama Sheria ya Uchaguzi inavyoelekeza, kushiriki katika kampeni za Uchaguzi wa October 2015 ambapo kupitia Katibu Mtendaji wa JUVICUF - Taifa Mh. Mahmoud Ali Mahinda na Uongozi wake tuliwafikia Vijana wa maeneo mbali mbali ya Kaskazini na Kusini na kuwashawishi katika kushiriki kupiga kura na kuwapatia kadi, kushiriki katika uangalizi wa Uchaguzi (Observers), kushiriki katika Uwakala wa Chama, kukisaidia Chama katika kukusanya matokeo ya Uchaguzi wa October 2015 (Data center). Pia Kamati hii hadi sasa inafanya kazi kwa karibu sana na Viongozi wa Jumuiya ya Vijana na Wakurugenzi mbali mbali wa Chama ili kukisaidia Chama. Vile vile Kamati hii inadhamiria kumpendekeza Mh. Katibu Mkuu na Rais wetu Maalim Seif Sharif Hamad, katika Nobel Prize ambapo hatua kadhaa zimeshakamilishwa.

Mh. Mgeni Rasmi,
Kutokana na ushiriki huo wa kuhakikisha kua Chama cha Wananchi CUF kinashinda Uchaguzi Mkuu wa October 2015, Utakumbuka kua tuliwahi kukufuata katika ofisi yako ya makao makuu ya Chama Mtendeni mjini Zanzibar kwa lengo la kutaka kujua khatma na mustakbali wa haki yetu ya kikatiba tuliyoihangaikia katikika Uchaguzi Mkuu wa 25,October 2015 ambayo madhalimu waliamua kuipora.

Hivyo, lengo hasa la ghafla hii ni kufanya mahojiano ya kina kati ya kundi la Vijana wa Vyuo Vikuu na wewe Mheshimiwa Katibu Mkuu juu ya khatma ya chama chetu pamoja na mustakbali wa maamuzi yetu ukizingatia leo nitarehe 23.09.2017,tukiwa na maana kwamba zimebakia siku tano (5) tu kutimia miezi mitatu uliyouahidi ulimwengu kwamba katika kipindi hicho haki ya Wazanzibari itakua imeshapatikana,uamuzi wetu huu wakukutana na wewe leo hautokani na uchache wa imani yetu kwako bali ni tathmini yetu ya kina juu ya mwenendo wa masuala ya siasa ya nchi yetu.

Mh. Mgeni Rasmi,
Mwisho kabisa, pamoja na mambo mengine, kupitia halfa hii tunaimani kubwa kwamba sisi na umma wa Kizanzibari na Tanzania kwa ujumla tutapata neno litakalotufanya tuondoke hapa na matumaini mapya ya kuiendea Zanzibar yenye Mamlaka kamili.

Ahsanteni sana.
Haki sawa kwa wote.
Samha Abdalla.
 
21992817_993867344086444_509815709750886205_o.jpg
 
Mheshimiwa Mgeni Rasmi, Mh. Maalim Seif Sharif Hamad,
Mheshimiwa Naibu Katibu Mkuu, Mh. Nassor Ahmed Mazrui,
Mheshimiwa Makamo Mwenyekiti Mstaafu, Mh. Juma Duni Hajji,
Waheshimiwa Wakurugenzi wa Chama cha Wananchi CUF,
Waheshimiwa Viongozi wa Baraza Kuu la Uongozi Taifa,
Waheshimiwa Wabunge,
Waheshimiwa Wawakilishi,
Waheshimiwa Viongozi wa Jumuiya zote za Chama cha Wananchi CUF,
Waheshimiwa Viongozi wa Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu,
Waheshimiwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu muliohudhuria hafla hii,
Waheshimiwa Waandishi wa Habari,
Mabibi na Mabwana.
Assalaam alaykum.
Mh.Mgeni Rasmi,
Awali ya yote tunamshukuru M/Mungu kwa kutujaalia siku hii ya leo kuweza kukutana hapa katika muendelezo wa harakati za kulikwamua taifa letu tukiwa katika hali ya uzima wa Afya na wale wanaosumbuliwa na maradhi tunawaombea kwa M/Mungu awajaalie shufaa. Shukrani zetu za kipekee na za dhati kabisa ziende kwako kwa kuacha majukumu yako yote na kuja kuungana nasi katika shuguli hii muhimu, pia tunakushukuru na kukupongeza wewe na Viongozi wenzako kwa kuwa mstari wa mbele katika kupigania haki ya Wazanzibari.
Mheshimiwa Mgeni Rasmi na wote mliohudhuria hafla hii,
Kwa niaba ya Kurugenzi na Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya juu Zanzibar iliyo chini ya JUVICUF - Taifa, tunayo heshima na furaha kubwa kukukaribisheni ili mushiriki nasi katika hafla hii muhimu na ya kihistoria ya muendelezo wa harakati za kutetea haki zetu za msingi chini ya Chama cha Wananchi CUF.
Mh. Mgeni Rasmi,
Hafla hii iliyoandaliwa na Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu imetokana na ziara ya miezi mitatu nyuma ambapo Kamati ilianza kumtembelea Mh. Juma Duni Haji, Mzee Ali Haji Pandu, Mzee Machano Khamis Ali,Mh. Salim Bimani na leo tunamalizia kwako wewe Katibu Mkuu. Lengo la kuwatembelea Viongozi hao ni kutaka kufahamu maisha yao katika harakati za kupigania haki sawa kwa Wote ndani ya Chama cha Wananchi CUF, Changamoto walizokumbana nazo, mafaniko na hatima ya haki yetu.
Mh. Mgeni Rasmi,
Kamati ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Taasisi za Elimu ya Juu iliyo chini ya JUVICUF - Taifa ilianzishwa rasmi December 10, 2011 na Viongozi Watangulizi wa JUVICUF – Taifa ambao kwa wakati huo walikua ni Mh. Yussuf Kaiza Makame (mbunge wa chakechake), Mh. Pavu Abdalla (Naibu Mkurugenzi wa Haki za Binadamu), Hafidh Ali Hafidh (Afisa wa kitengo cha Mafuzo na Utafiti cha kamati), Biubwa Mselem, Juma Gora, Suleiman Salim na Khalifa Abdalla Ali (Mwakilishi wa Wawi). Kamati hii ilikuwa chini ya ulezi wa Mh. Salim Bimani (Mkurugenzi wa Habari).
Mh. Mgeni Rasmi,
Kamati hii ilitekeleza majukumu mbali mbali ya kichama katika kipindi cha Uchaguzi Mkuu wa October 2015 kama vile; kushiriki katika mchakato wa kutafuta na kuhakiki wadhamini wa Mgombea Uraisi wa mwaka 2015 Mh. Maalim Seif Sharif Hamad, kuhamasisha Vijana wa Vyuo kwenda kupiga kura katika maeneo yao hasa wakaazi wa Pemba, kuhamasisha Vijana wa Vyuo kujiandikisha katika daftari la wapiga kura kwenye maeneo ya karibu ya Vyuo vyao kwa wale Wanaoishi katika Madahalia kama Sheria ya Uchaguzi inavyoelekeza, kushiriki katika kampeni za Uchaguzi wa October 2015 ambapo kupitia Katibu Mtendaji wa JUVICUF - Taifa Mh. Mahmoud Ali Mahinda na Uongozi wake tuliwafikia Vijana wa maeneo mbali mbali ya Kaskazini na Kusini na kuwashawishi katika kushiriki kupiga kura na kuwapatia kadi, kushiriki katika uangalizi wa Uchaguzi (Observers), kushiriki katika Uwakala wa Chama, kukisaidia Chama katika kukusanya matokeo ya Uchaguzi wa October 2015 (Data center). Pia Kamati hii hadi sasa inafanya kazi kwa karibu sana na Viongozi wa Jumuiya ya Vijana na Wakurugenzi mbali mbali wa Chama ili kukisaidia Chama. Vile vile Kamati hii inadhamiria kumpendekeza Mh. Katibu Mkuu na Rais wetu Maalim Seif Sharif Hamad, katika Nobel Prize ambapo hatua kadhaa zimeshakamilishwa.
Mh. Mgeni Rasmi,
Kutokana na ushiriki huo wa kuhakikisha kua Chama cha Wananchi CUF kinashinda Uchaguzi Mkuu wa October 2015, Utakumbuka kua tuliwahi kukufuata katika ofisi yako ya makao makuu ya Chama Mtendeni mjini Zanzibar kwa lengo la kutaka kujua khatma na mustakbali wa haki yetu ya kikatiba tuliyoihangaikia katikika Uchaguzi Mkuu wa 25,October 2015 ambayo madhalimu waliamua kuipora.
Hivyo, lengo hasa la ghafla hii ni kufanya mahojiano ya kina kati ya kundi la Vijana wa Vyuo Vikuu na wewe Mheshimiwa Katibu Mkuu juu ya khatma ya chama chetu pamoja na mustakbali wa maamuzi yetu ukizingatia leo nitarehe 23.09.2017,tukiwa na maana kwamba zimebakia siku tano (5) tu kutimia miezi mitatu uliyouahidi ulimwengu kwamba katika kipindi hicho haki ya Wazanzibari itakua imeshapatikana,uamuzi wetu huu wakukutana na wewe leo hautokani na uchache wa imani yetu kwako bali ni tathmini yetu ya kina juu ya mwenendo wa masuala ya siasa ya nchi yetu.
Mh. Mgeni Rasmi,
Mwisho kabisa, pamoja na mambo mengine, kupitia halfa hii tunaimani kubwa kwamba sisi na umma wa Kizanzibari na Tanzania kwa ujumla tutapata neno litakalotufanya tuondoke hapa na matumaini mapya ya kuiendea Zanzibar yenye Mamlaka kamili.
Ahsanteni sana.
Haki sawa kwa wote.
Samha Abdalla.
Safi sana vijana wetu ila subirini kwanza mtapata maelekezo hata sisi wakubwa tumechoka na dhulma
 
Back
Top Bottom