Ripoti za Mchanga wa Makanikia, Wahujumu uchumi wataguswa vipi? Sio siasa hizi?

MAHANJU

JF-Expert Member
Aug 26, 2014
5,039
2,000
Hivi hili suala kwa mtu makini kabisa ukifikiria kwa umakini wa dhati kabisa huwezi kuona kua hizi ni siasa tu? Ni nani atakayekubali kusulubiwa kwa sababu ya maagizo ya bosi wake? Kama haya mambo yalijadiliwa na baraza la mawaziri kwa maagizo ya wakulu, hawa mawaziri,wanasheria na maofisa wengine wa Serikali kipindi hicho waliotajwa walikua na maamuzi gani ya kutia saini kwenye mikataba bila ya kuagizwa? Ni nani alikua na maamuzi ya kufanya jambo la kitaifa bila baraka za bosi wa nchi?

Tunasema kwa Uchungu kabisa kua Walioliingiza taifa kwenye mikataba mibovu washughulikiwe huku tunasema tusiwataje mabosi wao wala kuwaingiza kwenye sakata hilo, hawa wanaotakiwa kuwajibika walikua na uwezo gani kuyakataa maagizo ya mabosi wao? Are we serious? Tunapata uchungu juu ya hili kivipi ilihali tunaziba njia za kuwashughulikia? Kwanini tusiziite kua ni siasa hizi?


Kuna mashaka makubwa juu ya utekelezwaji wa maagizo ya kamati, uthubutu utatoka wapi hapa? Kama suala ni katiba kuwalinda mabosi hao kwani amendment inatumia muda gani na kupata maazimio ya bunge?


Ni lini Serikali ya CCM ambayo ndio inalelewa na wahusika wakubwa waliolipoteza taifa ikawashughulikia? Inawezekanaje? Kwanini tusiite kua hizi ni siasa? Watanzania uelewa wetu unatupa shida sana!
 

Elli Mshana

Verified Member
Mar 17, 2008
38,489
2,000
Hahahahaa unataka kutoa mwiba kwenye kidole mguuni halafu hutaki kuugusa mguu, unataka ugusu kidole tu na maumivu yaishie kwenye kidole tu bila mguu kusikia maumivu. Maajabu ya CCM haya
 

Jambazi

JF-Expert Member
Jan 18, 2014
16,566
2,000
Ile ni siasa., kama ilivyo ishu ya madawa ya kulevya tuliambiwa wapo watu wazito, mawaziri, vigogo wa ccm... Mwisho wa picha kila mmoja anajua nin kilitokea
 

Ngushi

JF-Expert Member
Jul 8, 2016
9,097
2,000
Ukishaona mtu ukimdodosa kidogo tu anakuwa mkali anza kumshtukia!
Ukiliangalia vizuri hili swala hakuna trillion zitakazolipwa!
Ni Suala la muda tu
 

Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,691
2,000
Ulishaambiwa kuwa tutakaa na mwizi wetu kisha atulipe.Baadae akasema kuwa wote waliohusika wachunguzwe.Baadae akaua zaidi kwa kusema wazee wetu wastaafu WAACHENI wapumzike wamechoka na kulihudumia taifa kwa kujitoa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom