Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,410
Siku 83 baada ya Serikali kuzuia usafirishaji wa mchanga wa madini kwenda nje ya nchi, bei ya hisa za Kampuni ya ACACIA imetetereka kwenye Soko la Hisa Uingereza (LSE) na Dar es Salaam (DSE).
Machi 3, Wizara ya Nishati na Madini ilitoa agizo la kuzuia uuzwaji wa makinikia na kuzitaka kampuni husika kujenga kinu cha kuchenjulia nchini.
ACACIA, kampuni kubwa ya uchimbaji dhahabu nchini na Afrika kwa ujumla, imeorodheshwa kwenye Soko la LSE na DSE, lakini tangu sakata la kutosafirisha mchanga lilipoibuka imeyumba sokoni.
Migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi inayomilikiwa na kampuni hiyo, iliathirika kutokana na kuzalisha kiwango kikubwa cha mchanga huo wenye dhahabu, shaba na fedha. Mgodi mwingine uliopo chini ya ACACIA ni North Mara.
Kwa kipindi chote hicho, ACACIA ilikuwa inasubiri kutenguliwa kwa agizo hilo lakini kamati iliyoundwa na Rais John Magufuli Machi 29, imefuta matumaini hayo na kulazimika kutoa taarifa kwa wawekezaji na wadau. Kabla ya Rais kukabidhiwa ripoti ya mchanga wa madini, ACACIA ilitoa taarifa yake kwa umma kuwajulisha kilichokuwa kikiendelea.
Chanzo: Mwananchi