Elections 2010 Ripoti ya waangalizi wa uchaguzi inaleta kichefuchefu...

'a' na 'b' ni kweli
hususani wasomi kwa 'a'
na 'b' chadema hawakufika vijijini hasa hasa mikoa ya kusini na zbr.

2015 mipango ianze sasa.
 
Kwanini tunapenda sana kuwashinikiza watu waandike au wajibu kile tunachikitaka sisi?? Tukuue ndiyo, usile leo sawa, sema ccm chama cha mafisadi sawa, nchi hii imeharibika sawa, chadema inataka kurithi a failed state sawa, Huo si ni umbumbu kupita maelezo kwa maana nyingine ni upumbavu kukubaliana kila jambo hata kama halina msingi.

Kama unataka kupinga matokeo ya kitafiti ya mwenzio nawe fanya utafiti wako kwa misingi inayofanana ili upate jibu linalopingana. Utafiti wa kisayansi siyo utafiti ya kisiasa ndugu. Sayansi ina base kenye facts siyo political truth na ndiyo maana methodology inayotumika inawekwa wazi ili kwa wale wanoupinga utafiti huo wapinge kisayansi ili kutoa mapungufu au uongo uliofanywa na taasisi au mtu fulani na hiyo inakubalika.

Kiutaratibu report ya waangalizi wa uchaguzi kama ambayo mimi nimeshawahifanya inapelekwa kwa wadau wote Tume ya Uchaguzi ya nchi husika, mkuu wa nchi, vyama vya siasa vilivyoshiriki uchaguzi, taasisi husika na vyombo vya habari maana siyo siri.

Tuache majungu ya kisiasa kama ni maswala ya kichama peleka kwenye blog ya chama na siyo JF kama mmiliki wa JF anashadadia hayo aandike chama flani JF iwe ya jamii ya chama hicho tu na siyo wote.
 
the truth ni kuwa wanajua JK ni bwana misifa, bora wampe taarifa ya uongo ili apumbazike, kwa sababu ikiwa uchaguzi ungekuwa huru na wa haki, isingewachukua miezi mitatu kuikamilisha kwa sababu kusingekuwa na dosari yo yote ya kuchakachua.
 
Sioni sababu ya kulalamika kwamba Report hiyo alikabdihiwa nani... kinachopaswa kujadiliwa ni ukweli na usahihi wa kile walichokishuhudia...kama kweli CCM ni chama imara... KAMA kweli TISS NA NEC hawakuhusika kwa namna mmoja ya uchakachuaji na kama kweli tofauti ya watu Millioni 12 wote walisema eti hawaendi kupiga kura kwa sababu CCM itashinda yaonesha kwamba hata hao waandaji wa report hiyo ni mbumbumbu wa mambo ya Tanzania... labda wangesema tu kwamba daftari lilichakachuriwa with the benefit of hindsite, au watanzania waligoma kupiga kura mpaka wangehakikishiwa kwamba wizi ambao mara nyingi hufanywa na CCM umepatiwa Dawa.... kwan nini wakapigie kura wakati wanajua kwamba hata wakipiga CCM NI WEZI tu wataziiba...
kunawatu wanajua kufikiri sijui kwanini nchi hii inaongozwa na VILAZA!
 
hakuna haja ya kujadili hili eti 1.ccm ni chama imara 2.TISS na NEC yao hawakuhusika na uchakajuaji wa matokeo 3.watu 12 ml walisema hawaendi kupiga kura sbb wanajua ccm itashinda......hawa jamaa uwa wanafanya kazi na kutoa ripoti zao kwa ku-base na matakwa ya walio watuma ambao ni nchi za magharibi i.e wakioona rais ni easy kumwendesha kama jk basi wanatoa +tive ripoti wakioona ni ngangari kama bagbo basi tegemea -ve riport ili aondoke----hawa jamaaa uuuuuuuuuuh!...puuuuuuuuuuuuuuuuuh!...the go to hell
 
Hamna lolote nyie chadema wanafiki tu. Mwenzenu lipumba aliyakubali mpeema matokeo nyie mnataka kuleta vurugu eeh tumewagundua.
 
Ripoti za ulaya hata mie si ziamini kwani huwa wana muangalizi mmoja kila mkoa sijuwi anaangalia nini? Afadhali redet walikuwa na waangalizi wengi takriban kila kituo.
 
Hata mi niliisikia kwa mbali. Eti kampeni zilitawaliwa na chama tawala..................wehu wakubwa!!!
 
SOURCE: ITV leo taarifa yahabari ya saa mbili usiku..........

Yaani nilichoona kimenishtua sana..........................waangalizi hawa hivi walikuwa nchi gani vile?

Wamedai yafuatayo:-

a) Wapigakura wengi hawakupiga kura kisa waliona CCM itashinda tu na hivyo kusababisha kura zilizohesabiwa kuwa kiduchu..........................ukweli ni kuwa TISS na NEC waliminya kura kibao..............................................

b) Walidai ya kuwa CCM bado ni chama imara wakati Chadema iliwaangusha ila kazi chafu ya TISS na NEC ndiyo inakiweka CCM madarakani......................

c) Hawakuongelea mahudhurio makubwa kwenye mikutano ya Dr. Slaa na kama hao wote yaani waliohudhuria walibaki majumbani hawakupiga kura......................................I just cannot take this boloney........................

d) mapoungufu ya NEC na TISS yamefumbiwa macho.........................................

la ajabu kuliko yote eti JK mchakachuaji in-chief ndie anayepewa hiyo taarifa.......................................kweli nimeamini hawa waangalizi na CCM lao ni moja kuhalalisha viongozi tusiyo wahitaji...........................hawa ndiyo walimhalalisha Hosni Mubarak ambaye leo kila mmoja amejua kumbe hachaguliki kabisa.,..........ni wizi wa kura tu ndiyo umemweka madarakani miaka 30..............

Umetupa source ya heading ya thread yako. Naomba utuwekee source ya mistari iliyowekea rangi nyekundu.

Kuna mstari nimeweka rangi ya kijani. Hapo nataka nikupe angalizo kuwa watu kujaa ktk mikutano ya mgombea haina maana kuwa watampigia kura. Mwaka 1995, Mhe A. L Mrema alikuwa anajaza watu vibaya lakini watu hao hawakumchagua. Mimi binafsi nilihudhuria mikutano yote ya wagombea urais mwaka 2010, je ina maana siku ya kupiga kura niliwachagua wote?

Kuhudhuria si kuchagua. Tunakwenda kusikiliza sera za mgombea na muda mwingine tunakwenda kushangaa helkopta na comedy kama watakuwepo. Hata kusikiliza muziki maana uwezo wa kuingi ktk kumbi za starehe hatuna
 
Kweli kuna watu wanafiki dunia hii, Hao jamaa wangesema Dr. Slaa alishinda ila akapokwa ushindi, wangesema kura ziliibwa, wangesema uchaguzi haukua wa huru na haki ungekuta wanashangiliwa mno ila tu kwa kuwa iko kinyume na mtakwa yao basi ooh siwaamini watu weupe ohh sijui unafiki gani. Hiyo ndiyo siasa ya maji machafu.
 
Back
Top Bottom