Ripoti ya Utetezi wa Bwawa la Stiegler - Ndiyo Hii? Nimeshindwa Kuisoma...

Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
19,476
2,000
Ni political abstact lazima iwe ndefu
P.
Hapana aisee inakosa maana. Walishindwa kutafuta maneno ya page moja ambayo yangetosha kubeba report nzima? Nimejaribu kusoma leo yaani hii report ipo kucrash zile report zilizopita. Yaani waandishi walienda na majibu yao tayari. Yaani haina hypothesis. Naona Objectives zilikuwa kwenda against na report ya WWF na UNESCO.
 
Mwalimu

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
1,543
2,000
Tumesikia na kusoma juu ya uzinduzi wa "ripoti ya wataalamu" wazalendo. Mimi binafsi naunga mkono ujenzi wa bwawa hili na nilikuwa miunngoni mwa watu waliofurahia sana kuwa hatimaye hili linafanyika... Lakini si kwa utetezi unaojaribiwa kwenye ripoti hii. Nimejaribu kusoma lakini sikufika mbali...

Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
Halafu ilivyopambwa kwa mbwembwe nyingi na maandishi font size kubwa ili ionekane ya "kitaalamu"!
 
Victoire

JF-Expert Member
Jul 4, 2008
19,476
2,000
Nitaisoma polepole, ila uandishi wake unanipa mimi pia wasiwasi na sifa za wataalamu walioindaika. Abstract yenye page nane na Figure mbili siyo abstract kabisa. Kuna aina mbili za abstracts: (a) Descriptive au limited abstract ambayo ni summary ya ripoti yote in straight line. halfu (b) Informative au complete abstract ambayo ni summary ya kuonyesha lengo kuu la la report, yaani inatoa background, purpose, methodology, results, and conclusions. Yote hayo yanatakiwa yawe katika paragraph moja au mbili tu. na isizidi nusu page.

Jambo la pili linalonikatisha tamaa na credibility yake ni lugha iliyotumika; ripoti imeandikwa kwa kiingereza chenye makosa mengi sana kiasi kuwa ni afadhali ingeandikwa kwa kiswahili tu.
View attachment 1161160

Ukiachilia makosa ya lugha na poor choice of words, hiyo ni paragaraph moja yenye sentesi moja tu, jambo ambalo halikubaliki kwenye technical writing. A paragraph is a series of sentences that are organized and coherent, and are all related to a single topic.

Sasa content ni kitu ambacho nitakichimba pole pole kwani report inapokuwa imeandikwa kwa lugha mbovu, basi pia inakuwa ni ngume ku-comprehend intent sawasawa
Ni Musiba kabisa hii report. Nami nitaisoma polepole. Mwalimu umeandika point kabisa.
 
Lombo

JF-Expert Member
Jan 21, 2011
4,537
2,000
Tumesikia na kusoma juu ya uzinduzi wa "ripoti ya wataalamu" wazalendo. Mimi binafsi naunga mkono ujenzi wa bwawa hili na nilikuwa miunngoni mwa watu waliofurahia sana kuwa hatimaye hili linafanyika... Lakini si kwa utetezi unaojaribiwa kwenye ripoti hii. Nimejaribu kusoma lakini sikufika mbali...

Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
Wewe unaunga mkono mradi huu kwa hoja zipi!
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,356
2,000
Tumesikia na kusoma juu ya uzinduzi wa "ripoti ya wataalamu" wazalendo. Mimi binafsi naunga mkono ujenzi wa bwawa hili na nilikuwa miunngoni mwa watu waliofurahia sana kuwa hatimaye hili linafanyika... Lakini si kwa utetezi unaojaribiwa kwenye ripoti hii. Nimejaribu kusoma lakini sikufika mbali...

Ila inaitwa ni ya "wataalamu"... seriously... Ningekuwa na kaudikteta kadogo tu Ningeagiza watalaamu hawa wote waende Butimba angalau kwa mwezi mmoja... Kama wangeita ni "utetezi wa kisiasa".. nisingekuwa na matatizo nayo hii ripoti... lakini kuiita ni ya "kitaalamu".. basi neno "utaalamu" limepoteza maana...
Mkuu utaalam ni nini? Unasema utetezi wa kisiasa sasa kama ni wataalam wa Social, Economic, Political and Environment Assessment utasemaje si ya kitaalam?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,894
2,000
It seems to me as a report iliyojikita kujibu hoja za wadau wanaopinga utekelezaji wa hiyo project, sioni kama imeandaliwa kwa ajili ya publication kwenye journal. Hata hivyo hiyo wanayoita abstract imejazwa mambo mengi, labda mambo mengi yangehamishiwa kwenye introduction, project rationale & justification
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,870
2,000
Ndugu hapo sio swala la ubora wa elimu tu! pia wataalam kutaka kumfurahisha mtawala maana aliepoa anataka kusikia anachopenda tu
Hili ni tatizo sana. Asiposikia anachopenda kusikia kutoka kwako, kibarua kinaota nyasi!

Namkumbuka yule mama wa Kagera, sijui DAS au DED ambaye hakuwa amekariri tarakimu za miradi. Hiyo ndiyo elimu tunayotaka tuitambue sasa - ujue kukariri tarakimu na kuzitapika unapotakiwa kufanya hivyo, hata kama tarakimu zenyewe hazina maana yoyote.
 
Swigho

Member
Jul 5, 2019
9
45
Tatizo la hii inch ni Siasa. Kila kitu ni siasa, hapo wataalamu wameweka Elimu mifukono wametanguliza siasa mbele
Kwel Kabisa inafika stage hata vtu ambavyo haviitaji Siasa vinaingiziwa Siasa at the end of the day yanafanyika mambo ya Ajabu kabisa
 
kiunzi

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
518
500
Umri umesogea sasa m/kijiji kama ya
Hali ya
maji yaliyokologeka! Ungeipitia.
 
newazz

JF-Expert Member
Mar 28, 2009
666
500
Oh noooo.. siwaamini kabisa... nawasoma kwa umakini na nauliza kila assumption wanayotoa. Binafsi nilitarajia ripoti hii isiwe ye kisiasa kabisa; ingedeal na facts na facts tupu. Na pale inapotoa mahitimisho basi yatolewe kutokana na facts zilizopo. Siasa waachiwe wanasiasa. Binafsi kama mtu ambaye naunga mkono ujenzi wa bwawa hili hoja za umuhimu, ulazima na uharaka wa kujenga bwawa hili zinasimama peke yake bila kuhangaika na kujibu hoja za watalaamu wa "Ulaya". Unajua kuwa 2 + 2 ni 4. Haijalishi anayejumlisha ni Mchina, Mtumbatu, au Mdigo. Tunaweza kutofautiana kwenye mbili za "nini" na mbili za "nini" zinajumlishwa.
Niliona wameanza kuchemsha kwa mwanzo wa maelezo yao.. Unaweka conclusion, kabla hujabuild cases factor.. Ni kama judge anatoa hukumu ya kesi, kabla ya hapajasikilizwa submission... Inachekesha, ni kama vile kubishana kijiweni, hakuna points wala nini ni mwenye kelele tu.
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
16,990
2,000
What do you expect when “wataalamu” were picked from garbage dumping area!?
Kuna makatibu wakuu wawili wastaafu. Kuna msitaafu wa NEMC. Wengine sina uhakika.
Ni njaa tu inawasumbua. Hakuna mwenye taaluma ya kuweka kujibu hoja za kitalaamu hata mmoja.
 
Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
8,870
2,000
LIcha ya hivyo, ningependa kujua competencies zao ni nini... kwa mfano, nimeona jina la Dkt. Kashililah.. ninadhania ni yule yule aliyekuwa Bungeni siyo? Hawa wataalamu wengine ni wabobezi wa maeneo gani ya kitaaluma?
Kwa kawaida, mtu anayeteuliwa kuandika au kutafiti jambo, kati ya mambo yanayotizamwa katika uteuzi huo ni eneo lake la ujuzi kama linaendana na kinachotafitiwa, ikiwa ni pamoja na uzoefu katika eneo hilo. Je, ana uzoefu kiasi gani. Kafanya tafiti na kuzichapisha?

Kwa vile mradi huu wa Stieglers umepigiwa kelele nyingi na watu wa Mazingira, lengo la hawa walioteuliwa bila shaka lilikuwa ni kupunguza au kuondoa mashaka yaliyotajwa na hao wanamazingira kwa kujibu hoja zinazowapa hofu kuhusu mradi wenyewe.

Ni vigumu kwa mtu kuwa na 'cometencies' katika eneo ambalo hana utaalam nalo. Pengine anaweza kuwa na 'competency' za kukusanya taaraifa na kuziweka pamoja katika ripoti, lakini hata hapa kundi hilo lingetakiwa angalau awepo mtu mwenye 'specific competencies' katika eneo la mazingira ili kumudu vizuri kujibu hoja zilizoibuliwa na wanamazingira walio na hofu na utekelezwaji wa mradi huo.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom