Ripoti ya Upambanaji wa rushwa na Ufisadi kimataifa - Tanzania yang'ara

Machawa kazini mama kuwa makini kwenye msafara wa mamba kenge pia wamo.
 
Eti mwananchi huru. Acha upumbavu wewe. Una uhuru gani mlamba viatu mkubwa wewe. Ameng'ara nini. Amezuia rushwa lini hadi atambulike? Mama yenu anahamasisha watu wale rushwa kwa urefu wa kamba zao halafu unaleta uharo wako hapa?
daaah
 
View attachment 2098543
=====
Taasisi inayojishughulisha na harakati za kusimamia uwazi na mapambano dhidi ya rushwa na Ufisadi duniani ya " Transparency International " tayari imetoa ripoti yake ya mwaka,

Taasisi hii iliyofanya kazi ya kuchunguza kiasi cha rushwa na Ufisadi kwenye nchi zipatazo 180 duniani kwa kutumia kipimo cha Corruption Perceptions Index ( CPI ) huku Tanzania nayo ikiwemo mwaka 2020|21.

Ripoti iliyotolewa na taasisi hiyo inayoheshimika zaidi duniani kwa kuwa na taarifa za kweli ya Transparency International inaonesha nchi ya Tanzania rushwa na Ufisadi vimepungua kwa kasi hasa kwenye Uongozi huu wa Rais Samia Suluhu Hassan,

Mtakumbuka Tanzania ilipata alama 36 kati ya alama 100 zilizotolewa na taasisi hiyo mwaka 2019|20 huku Tanzania tukishika nafasi ya 94 kati ya nchi 180 zilizochunguzwa mwaka huo,

Kwamujibu wa ripoti iliyotolewa hivi majuzi Tanzania imepanda kwa nafasi saba ( 7 ) toka ile ya 94/180 mwaka 2019|20 hadi kufikia nafasi ya 87/180 huku ikijizolea alama 39 kati ya alama 100 zilizotolewa,

Point to note,
Rushwa duniani kote inazuiwa kwa watu kuwa huru kupitia asasi mbalimbali za kiraia kuweza kupaza sauti kama ilivyo sasa,

Rushwa kamwe huwezi kuipinga kwa kutumia vitisho na tumbuatumbua kwenye hili hata Hayati Dkt John Joseph Pombe Magufuli alichemka sana,
Safi sana Mama Samia,
 
Mtu unaandika Kama vile hujawahi kufika Tanzania?
Tuulize sisi tukiozaliwa, kukulia na kuishi Tanzania.
Wewe unamuamini beberu anayekuja kukaa hapa tz siku tano Tena akiwa kwenye hoteli ya Bei mbaya akupe taarifa feki?
Tuulize tukujuze. Nchi inadidimia. Siku ukipata muda tembelea tanroads uone wachina wanavyonunua mainjinia.
 
Utafiti hupingwa kwa Utafiti,

Wewe unasemaje?
 
Ripoti iliyotolewa na taasisi hiyo inayoheshimika zaidi duniani kwa kuwa na taarifa za kweli ya Transparency International inaonesha nchi ya Tanzania rushwa na Ufisadi vimepungua kwa kasi hasa kwenye Uongozi huu wa Rais Samia Suluhu Hassan,
Wewe ni mwongo na chawa wa Samia tu. Data zilizotumika kutathmini hali ya rushwa nchini (2021) ni za miaka miwili nyuma (soma methodology). Hii ripoti inaakisi matokeo ya utawala wa mwendazake, siyo Hangaya.
Aidha, Tanzania imepanda nafasi moja tu kutoka ripoti ya 2020. Data hizi hapa:
TanzaniaTZASSA39 (2021)38 (2019)136 (2018)3
Hayo mambo ya uchawa acha!
 
Umeisoma hiyo ripoti vizuri?
 
Back
Top Bottom