Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Burundi inawasaidia waasi wa NRC kuiangusha serikali ya Kagame

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Ripoti ya Umoja wa Mataifa: Burundi yamsaidia Jenerali muasi wa Rwanda
na RFI
000_Par3091045_0.jpg

Jenerali muasi katika jeshi la Rwanda (RDF) Faustin Kayumba Nyamwasa.

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imeonesha kuwa Jenerali wa zamani kwenye jeshi la Rwanda (RDF) anayeishi uhamishoni, Kayumba Nyamwasa anasajili wapiganaji na kupata silaha kutoka nchi za Burundi, Uganda na DRC.

Ripoti hiyo ya wataalamu ya tarehe 31 Desemba mwaka jana, imesema Jenerali Nyamwasa ambaye anaishi nchini Afrika Kusini kwa sasa, amesafiri mara kadhaa kwenda kwenye nchi za ukanda kuunda kundi jipya la uasi linalofahamika kama P5 ambalo liko chini ya kundi la waasi la Rwanda National Congress (RNC).

Kulingana na ripoti hiyo, kundi hilo jipya la waasi linaundwa na wapiganaji kutoka Burundi, waasi wa Kihutu wa FDLR na raia wa DRC kutoka jamii ya Wanyamulenge.

Hata hivyo Burundi imenyooshewa kidole cha lawama kwenye ripoti hiyo kwa kukusanya wapiganaji na kuwasafirisha mashariki mwa DRC katika maeneo ya Uvira. Wapiganaji wake wanadaiwa kutekeleza mashambulizi ya hivi karibuni kwenye maeneo ya mpaka wa nchi ya Rwanda.

Ripoti hiyo iliyowasilishwa kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Desemba 18, 2018 inabaini kuwa Burundi inasaidia kundi la waasi wa Rwanda, la Rwanda National Congress (RNC), lenye makao yake makuu katika mkoa wa Kivu Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), kundi ambalo linaoongozwa na Jenerali muasi Kayumba Nyamwasa, afisa wa zamani wa ngazi ya juu wa jeshi la Rwanda (RDF) ambaye anaendesha uasi wa kupindua serikali ya Kagame.

Kulingana na ushuhuda uliotolewa na wapiganaji wa zamani kutoka kundi hilo, hata wanaharakati wa mashirika ya kiraia kutoka DRC na jeshi la DRC (FARDC), makao makuu ya kundi la waasi wa Rwanda la RNC yanapatikana katikaeneo la Bijabo katika wilaya ya Fizi, kilomita chache na mji mkuu wa Burundi, Bujumbura.

"Msajili mkuu wa wapiganaji wa kundi hilo anapewa hifadhi mjini Bujumbura, Burundi chini ya ulinzi mkali. Mtu huyo anafahamika kwa jina la Rashid, pia anafahamika kwa majina ya Sunday Charles. Yeye ndio anahusika na kusafirisha wapiganaji kutoka Bujumbura hadi Bijabo wakipitia kwenye Ziwa Tanganyika kwa kutumia boti", wapiganaji wa zamani wa RNC wamewaambia wataalamu wa Umoja wa Mataifa.

Ripoti hii inaonyesha kuwa wapiganaji wanatoka katika nchi za Afrika ya Kati, Afrika Mashariki na kusini mwa Afrika, na hata katika ukanda wa Asia ya mashariki.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wapiganaji wengi wa zamani wanabaini kwamba walipewa silaha, risasi, buti, sare na chakula kutoka Burundi.
 
Vita vya nini wkt wenzake wote E/Africa Uchumi wao unakua kwa >5% yeye Burundi unakua kwa 0.0%.

Kinchi maskini hicho hakina uwezo wa kupigana vita,acha kijifie na njaa tu.
slim ana madudu yake lkn this time yeye ndo anachokozwa na nadhani burundi kuna sehemu inampa kiburi hicho

ila slim awe makini tu kama kayumba yupo on this game

Sent using Jamii Forums mobile app
 
slim ana madudu yake lkn this time yeye ndo anachokozwa na nadhani burundi kuna sehemu inampa kiburi hicho

ila slim awe makini tu kama kayumba yupo on this game

Sent using Jamii Forums mobile app
Kayumba?ana support ya Watusi wenzake?

Kwa watusi Kagame ni demi-God wao na ana full support kutoka kwao.

Kayumba anasapotiwa na nani?Wahutu au Burundi au mtasema sijui France/South Africa?Consipiracy stories.
 
tatizo sio support ya kabila lao kwanza ni wachache

apo kayumba lzm apate support ya pua nene kwanza kaungana na fdrl pia hutu watamsupport kwanza ili kumtoa slim then baadae ndio watamtazama kayumba kama mtuc

Sent using Jamii Forums mobile app
Hao wengi wana nini?ill equipmed army mpk UN imewapunguza 1000 huko kwny mission wanabaki kulia lia.

Hao wote unaowasema sijui pua nene+fdlr+nakadhalika hakuna kitu hapo.
 
Muda utaongea ila kagame naona kashaona maji ni mengi kuzidi unga alionao..Mr slim baada ya kujaza silaha na kuzifanyia upelelezi vya kutosha Tanzania,Uganda,DRC,Burundi akajiamini sana kiasi cha kuitukana Tanzania akiamini kuna mstari haitavuka kule drc,ila majibu aliopata ni tofauti kabisa na uhalisia vita ile ilipiganwa na JWTZ vs RDF wakiwa na sare halisi za rwanda.Kikwete alitaka kumuonesha uhalisia japo iliwekwa siri

UMENIKUMBUSHA MBALI SANA ILIKUWA HATARE
 
Hakika ww ni most great thinker

duh jw na rdf walipigana lini,wap na chanzo ilikuwa ni nini?

kama ni m-23 wale walikuwa ni waasi waliokuwa ndani ya jeshi la congo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom