Ripoti ya ukaguzi ya CAG yatua kwa JK leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya ukaguzi ya CAG yatua kwa JK leo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Mar 29, 2012.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo, Alhamisi, Machi 29, 2012, amepokea rasmi Ripoti ya Mwaka ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kutoka kwa Mkaguzi na Mthibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)Bwana Ludovic Utouh kwa mujibu wa mahitaji ya Kifungu 143 (4) cha Katiba yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Katika shughuli hiyo iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, Rais Kikwete kwa zaidi ya saambili amemsikiliza Bwana Utouh akiwasilisha Ripoti hiyo ya Mwaka wa Fedha wa 2010/2011 na ambayo zamu hii imepanuliwa kwa kiasi kikubwa kulingana na mahitaji ya sasa ya ukaguzi na ikilinganishwa na ripoti za miaka iliyopita.

  Bwana Utouh amewasilisha Ripoti yenye sehemu mbili kuu ambazo ni (1) Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali Kuu na (2) Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali za Mitaa.
  Mbali naripoti hizo mbili kuu, Bwana Utouh pia amewasilisha Ripoti ya Ukaguzi wa Mashirika ya Umma, Ripoti ya Ukaguzi wa Balozi wa Tanzania nje, Ripoti ya Miradi Mikubwa ya Maendeleo, Ripoti ya Ufanisi na Uchunguzi na Ripoti ya Ajali za Barabarani nchini.

  MY TAKE: Thereafter? What next?

   
 2. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #2
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi nipo interested na matumizi ya ile trillion 1.7 kama stimulus package. Tunataka tuone List ya makampuni yaliyofaidika na alichokisema CAG
   
 3. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #3
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  zitto aliipigia kelele sana hii, ngoja tuone nani atatajwa humo
   
 4. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #4
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii itakuwa "funika kombe mwanaharamu apite" kama ilivyokuwa EPA ndivyo CCM walivyochota pesa kwa gia ya STIMULUS PACKAGES
   
 5. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #5
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Nimezipata za juu juu kuwa kuna vigogo wengi sana walifaidika na hii stimulus package. Nadhani danadana zote za Mkulo kipindi kile bungeni, na zile kampuni 40 ambazo CAG alinyimwa nyaraka zake ilikuwa ni janja ya ku-buy time, ili watoto wa mjini waweze kucheza na files pale BRELA (ili kuficha wamiliki halisi).
  Lets wait and see, but orodha ile ikiwekwa hadharani sidhani kama atapona mtu
   
 6. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #6
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Tena mbaya zaidi walengwa wa fidia mpaka sasa wanadaiwa na mabenki.

   
 7. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #7
  Mar 29, 2012
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,173
  Likes Received: 1,175
  Trophy Points: 280
  Hakuna hatua itakayo chukuliwa hapo, ndo imetoka!
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Usikute JK ata hakuiangalia!
  Ivi kwa nini report ya CAG isiwe inaletwa bungeni na kuijadili maana nayo ni sehemu ya bajeti control
   
 9. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #9
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanaweza kufanya lolote walitakalo, hata kutoisoma kabisa hiyo ripoti, sembuse kuchukua hatua, lakini ipo siku isiyo na jina watavuna walichopanda.

   
 10. Michael Scofield

  Michael Scofield JF-Expert Member

  #10
  Mar 29, 2012
  Joined: Jul 30, 2011
  Messages: 1,218
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii hata wacheze BRELA ngoma ya kisauzi, hamna kitu hapo, kilichopo ni ukweli kwa kwenda mbele pindi wakiupindisha imekula kwao. makampuni yanayonunua pamba yanajulikana. mie hata kwa kichwa nakutajia na kiasi cha pamba walichonunua kwa mwaka 2008/2009

  Mbona wanalo hili wamerikoroga wasubiri kulinywa....!

   
 11. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #11
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Nadhani CAG ataipeleka pia bungeni wakati wa mkutano ujao mwezi wa nne. Lakini sidhani kama itajadiliwa kwenye mkutano huo maana hoja za kujadiliwa zinatakiwa kumfikia Katibu wa bunge kabla ya mkutano kuanza UNLESS iwe hoja ya dharula kama ileee ya mgomo wa madaktari
   
 12. Entrepreneur

  Entrepreneur JF-Expert Member

  #12
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 1,092
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tukiwa na watu waliokuwa informed kama wewe, nadhani tutafika sehemu tunayoitaka. Ngoja tuone watafanyaje, kwani hata waki-backdate data tutajua tu. Njia pekee wanayoweza kufanya ni kuficha ushahidi. Swali ni kwa gharama gani? Mimi sijui. Ingawa muda ni bidhaa ambayo hatuna kwa sasa, lakini ndio msemakweli pekee tunayemtegemea.

  Ngoja tusubiri, ila ni bora ikaeleweka mapema kuwa kashfa hii itakuwa kubwa kuliko ile kashfa ya EPA, kwani makampuni mengi yaliyopata hasara hayakufidiwa kile kinachostahili au hayakupewa gawio kabisa.Sasa kama hivi ndivyo, mgao huo walipewa kina nani? Mimi sijui,ila kwa sasa hatutoi macho kwenye zawadi.
  "EYES ON THE PRIZE"
   
 13. m

  matawi JF-Expert Member

  #13
  Mar 29, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huyu keng toka anibowe kwenye ripoti ya jairo namchukia mpaka basi yaani kama ningejua ni yeye nisingefungua hii thread. Jitu zima na kengelezake 2 hovyoooo
   
 14. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #14
  Mar 29, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  huyo cag hana jipya
   
 15. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2012
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Duh ila kwa jairo kweli aliingia choo cha kike
   
 16. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #16
  Mar 29, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu katiba inataka ipelekwe kwa Rais na Rais aipeleke Bungeni. Nadhani wazo lako ni zuri kwamba CAG awe ana present report Bungeni bila kupitia kwa Rais.
   
 17. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  CAG anaripoti kwa rais. Mwenye mandate ya kuamua iende bungeni ama la ni rais. Kwa mfumo wa sasa CAG haripoti bungeni. Mpaka katiba irekebishwe ili nafasi ya CAG iwe inashindaniwa na mshindi aridhiwe na bunge ndo atakuwa na mandate ya kuipeleka direct bungeni
   
 18. K

  Kacharimbe JF-Expert Member

  #18
  Mar 29, 2012
  Joined: Apr 2, 2011
  Messages: 204
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Kipi ambacho unadhani CAG haja cover? Problem ya wengi nadhani hawaelewi core function ya CAG. Kazi yake ni kutoa recomendations kwa ajili ya kuziba mianya ya upotevu wa fedha ama matumizi mabaya. Na anachotoa siyo certificate bali ni opinion yake bali through report yake vyombo vingine kama PCCB, bodi za wakurugenzi, madiwani, maafisa masuuli wanaweza ku act kama watakuwa na wasiwasi na maeneo fulani
   
 19. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #19
  Mar 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  CAG huyu hafai,kwanza 2nasubiri utekelezaji wa maamuzi ya bunge juu ya jairo saga...cag hajawajibishwa bado..ila kwa Jk hapa 2takaa sana.
   
 20. TUMBIRI

  TUMBIRI JF-Expert Member

  #20
  Mar 29, 2012
  Joined: May 7, 2011
  Messages: 1,934
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mi namshangaa Utouh, Sheria inasema once amewasilisha ripoti kwa Rais, hiyo ripoti inakuwa ni Public report. Sasa mimi nimeenda kwenye website ya Ofisi yake nashangaa nazikuta ripoti za mwaka jana! Simuelewi kabisa anamaanisha nini kumpa Kikwete huku akituacha kwenye mataaa sisi mabosi wa Kikwete! Au anatuprintia na sisi wananchi copy zetu?
   
Loading...