Ripoti ya Uchunguzi wa Maabara: Mashine moja ilikuwa na hitilafu. Upimaji wa COVID19 umehamishiwa katika Maabara mpya iliyopo Mabibo

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,438
3,333


Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kueleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na Kamati teule ya Uchunguzi

Amebainisha kuwa Kamati imegundua uwepo wa Mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19

Amesema "Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati"

Amesema "Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii"

"Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1,800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu"

Aidha, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo, DSM na kuzungumza na madereva wa malori na kuwahakikishia kupata majibu ya Covid-19 ndani ya masaa 24

EYsnhTRWkAEKe-y.jpg


EYsnLgRXYAE1KKc.jpg
 
Maabara wamejengewa madereva?
hapana imejengwa kuchukua vipimo vya covid 19.

soma paragraf ya mwisho wa hii thread inasema hivi,nanukuu:

"Aidha waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo,DSM na kuzungumza na madereva wa maroli na kuwa hakikishia kupata majibu ya Covid 19 ndani ya masaa 24"
mwisho wa kunukuu.

sjui umeelewa bwashee ?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waanze sasa na kutupa Updates za huo ugonjwa ili tuendelee kwa nguvu zote kujikinga badala tu ya kutuambia tupige kelele kwa kisingizio eti hiyo Corona imekwiisha.
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom