News Alert: Ripoti ya Uchunguzi wa Maabara: Mashine moja ilikuwa na hitilafu. Upimaji wa COVID19 umehamishiwa katika Maabara mpya iliyopo Mabibo

elvischirwa

JF-Expert Member
Jan 26, 2013
6,716
2,000

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kueleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na Kamati teule ya Uchunguzi

Amebainisha kuwa Kamati imegundua uwepo wa Mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19

Amesema "Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati"

Amesema "Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii"

"Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1,800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu"

Aidha, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo, DSM na kuzungumza na madereva wa malori na kuwahakikishia kupata majibu ya Covid-19 ndani ya masaa 24

Mila na desturi za kiafrika lazima zizingatiwe, baba hadanganyi.
 
field marshall1

JF-Expert Member
Sep 17, 2017
598
1,000
HAO NI MATAPELI, WANAJUA WANASEMA UONGO ILI KUHALALISHA ALICHOSEMA BABA YAO MAGUFULI. NCHI HII TUNA SAFARI NDEFU SANA KUFIKA TUNAKOTAKA KUFIKA. UONGO UMETAMALAKI SERIKALI HII....OOH MARA NDEGE YA WATALII IMEFIKA KILIMANJARO.....?

COMMON GUYS....NANI AJE TANZANIA AKAFE???? ACHENI UJINGA NINYI SERIKALI YA TANZANIA....HIYO NDEGE HAIJAWAHI KUPITA ANGA LA TANZANIA, HAIPO HATA KWENYE RATIBA YA KIA, NDEGE IPO UJERUMANI NA HAIKWENDA SEHEMU YOYOTE ZAIDI YA UGIRIKI. TUNAIJUA VIZURI UWANJA WA KIA ULIVYO MSITUDANGANYE NINY
I>
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
2,328
2,000
hapana imejengwa kuchukua vipimo vya covid 19.
soma paragraf ya mwisho wa hii thread inasema hivi,nanukuu:
"Aidha waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo,DSM na kuzungumza na madereva wa maroli na kuwa hakikishia kupata majibu ya Covid 19 ndani ya masaa 24"
mwisho wa kunukuu.
sjui umeelewa bwashee ?

Sent using Jamii Forums mobile app
kwa Tanzania covid-19 ime target madereva wa malori au
 
Wansambuki

Member
May 17, 2020
5
45

Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametoa ripoti ya Uchunguzi wa Maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii na kueleza mambo kadhaa yaliyogunduliwa na Kamati teule ya Uchunguzi

Amebainisha kuwa Kamati imegundua uwepo wa Mapungufu katika mfumo wa kimuundo, kiutendaji na uendeshaji wa kitaaluma katika upimaji wa vipimo, uhakiki wa ubora wa majibu na udhaifu katika uhifadhi wa vipimo vya COVID-19

Amesema "Mojawapo ya Mashine za kupima sampuli za Covid-19 ilikua na hitilafu bila Uongozi wa Maabara kuchukua hatua za kuifanyia matengenezo kwa wakati"

Amesema "Upimaji wa Sampuli zote za Covid-19 umehamishiwa katika maabara Mpya iliyokamilika kujengwa katika eneo la Mabibo Dar es Salaam ambayo kwa sasa ndiyo itakuwa maabara ya Taifa ya Afya ya Jamii"

"Maabara hii mpya ina uwezo wa kupima sampuli 1,800 za Ugonjwa wa Covid -19 ndani ya masaa 24 tofauti na ile ya awali ilokua na uwezo wa kupima sampuli 300 tu"

Aidha, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu ametembelea maabara mpya ya Taifa Mabibo, DSM na kuzungumza na madereva wa malori na kuwahakikishia kupata majibu ya Covid-19 ndani ya masaa 24

Buildings, machines, multitudes of people singing praises are all good; but the critical issue is showing people that our interventions are working. We need evidence of results, not ngojera. This we have seen, now folks: deliver results! That is the role of government to its people.
 
kababaa1

JF-Expert Member
Jul 26, 2013
488
500
Nimenote tu,, mapungufu ya kiutendaji, uendeshaji, na nn vile sijui...

Politics at fleek!
Aidha pongezi zote kwa kuwa na maabara mpya ya kisasa.
Go JPM go
 
Top Bottom